Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

Wali Wa Nyanya Wa Kukaanga

 

Vipimo

Mchele basmati, pishori - 3 vikombe

Vitunguu katakata - 2

Nyanya/tungule katakata - 5 takriban

Viazi/mbatata menya katakata - 3 kiasi

Thomu (saumu/garlic) ilosagwa - 1 kijiko cha supu

Bizari mchanganyiko - 1 kijiko cha kulia

Hiliki ya unga - ½  kijiko cha chai

Kidonge cha supu - 2

Chumvi - kisia

Mafuta  -  ½ kikombe

Maji ya moto au supu - 5  takriban

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika   

  1. Osha na roweka mchele
  2. Katika sufuria weka mafuta yashike moto, tia viazi, vitunguu ukaange.
  3. Vikianza tu kugeuka rangi tia thomu na bizari, hiliki, endelea kukaanga kidogo.
  4. Tia nyanya kaanga lakini usiache zikavurugika sana.
  5. Tia mchele ukaange chini ya dakika moja.
  6. Tia maji ya moto, na kidonge cha supu au supu yoyote kiasi cha kufunika mchele yazidi kidogo.
  7. Koroga vichanganyike vitu, kisha funika upike kama pilau.
  8. Pakua ikiwa tayari, tolea kwa samaki wa kukaanga au kitoweo chochote kile. Bonyeza kiungo kifuatacho:

Samaki Wa Changu Wa Kukaanga

 

Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)

 

Share