Skip to main content

Mukhtasari Wa 'Aqiydah Ya Muislamu: Maswali Na Majibu26-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Je, Inajuzu kuswali na kaburi liko mbele yako?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

26-Je, Inajuzu kuswali na kaburi liko mbele yako?

Hapana! Haijuzu kuswali kulielekea kaburi.

فَوَلِّ وَجْهَكَ شَطْرَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِۚ

Basi elekeza uso wako upande wa Al-Masjidil-Haraam [Al-Baqarah: 144]

Yaani: Qiblah

((لا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ وَلا تُصَلُّوا إِلَيْهَا)) رواه مسلم

((Msikalie makaburi wala msiswali kuyaelekea)) [Muslim]