Shaykh Fawzaan: Amali Njema Za Kumfanyia Aliyefariki

 

 

'Amali Njema Za Kumfanyia Aliyefariki

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Vitendo gani vyema ambavyo aliye hai anaweza kumfanyia maiti?

 

 

JIBU:

 

 

Maiti anaweza kunufaika kwa vitendo vya walio hai ambavyo vinatokana na dalili sahihi inayodhihirisha kuruhusiwa kama; kumuombea du'aa, kumuombea maghfirah, kumfanyia swadaqah kumfanyia Hajj na 'Umrah, kumlipia madeni yake na kumtekelezea mirathi yake ya Kiislam. Vitendo vyote hivyo vimethibiti kishariy’ah.

 

Na baadhi ya ‘Ulamaa wameunganisha na hayo pia vitendo vyote vingine vya ‘ibaadah ambavyo Muislamu hutenda kwa ajili ya Muislamu mwengine ambaye yu hai au amefariki.

Lakini, iliyo sahihi ni kujiweka katika mipaka ya yale yaliyoruhusiwa yakiwa na dalili sahihi, kwani hivyo itakuwa ni kutokana na maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anaposema:

 

 وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ ﴿٣٩﴾

Na kwamba insani hatopata (jazaa) isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi. [An-Najm: 39]

 

 

[Shaykh Fawzaan - Al-Muntaqaa Min Fataawa Shaykh Ibn Fawzaan – Mj. 2, Uk. 161, Fatwa Namba 139] 

 

 

Share