Skip to main content

003-Aal-'Imraan: Aayah Na Mafunzo046-Aayah Na Mafunzo: Watoto Watatu Ambao Waliongea Wakiwa Wachanga

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Watoto Watatu Ambao Waliongea Wakiwa Wachanga

www.alhidaaya.com

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Atawasemesha watu katika utoto wake na utu uzima wake na ni miongoni mwa Swalihina.

Mafunzo:

Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hawakuongea watoto wachanga isipokuwa watatu; ‘Iysaa na (kisa cha Jurayj katika Baniy Israaiyl, na kisha cha farisi mzuri ambaye mama wa mtoto aliyeongea utotoni alitamani mwanawe awe kama yeye, lakini mtoto akatamka kukataa…” [Al-Bukhaariy (3436)].