042-Aayah Na Mafunzo: Wanawake Wanne Walio Bora Kabisa

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Wanawake Wanne Walio Bora Kabisa

www.alhidaaya.com

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢﴾

42. Na pale waliposema Malaika: “Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.”

 

Mafunzo:

 

Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanaume wengi wamekamilika, na hawakukamilika katika wanawake  ila  Aasiyah mke wa Fir’awn, na Maryam bint ‘Imraan. Na hakika ubora wa ‘Aaishah kwa wanawake ni kama ubora wa thariyd katika chakula.” [Aswhaabus-Sunan isipokuwa Abuu Daawuwd].

 

Thariyd ni mikate mikavu iliyokatwa katwa na kumwagiwa supu ya nyama chakula kimojawapo alichokuwa akikipenda sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).  

 

 

Kufadhilishwa ‘Aaishah (Radhwiya Alllaahu ‘anhaa) juu ya wanawake wengine

 

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( كَمَلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ، وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلاَّ مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ، وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَفَضْلُ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ ))‏

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Fir'awn, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwa wanawake wengine ni kama mfano wa ubora wa thariydkwa vyakula vingine.” [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

Share