054-Aayah Na Mafunzo: Allaah Hana Sifa Ya Makri Isipokuwa Ni Kulipiza

Aayah Na Mafunzo

Aal-‘Imraan

Allaah Hana Sifa Ya Makri Isipokuwa Ni Kulipiza

www.alhidaaya.com

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu makafiri: 

 

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾

54. Na wakapanga makri lakini Allaah Akapanga kulipiza makri. Na Allaah ni Mbora wa kulipiza mipango ya makri.

 

 

Mafunzo:

 

Sifa ya makri (njama) huthibitishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa njia ya muqaabalah (yaani, ukipanga mabaya, Naye Ataamiliana nawe kwa ubaya, na ubaya utakurudia mwenyewe. Na ukipanga mazuri, Naye Ataamiliana nawe kwa uzuri, Atakusaidia na kukulipa mema). Na Sifa hii kama zilivyo zingine, huthibitishwa kwa Allaah kwa maana inayoendana na kulaikiana na Allaah (عزّ وجلّ). Kwa hiyo, Allaah Anamfanyia makri (njama) yule anayestahiki na pia yule ambaye anawafanyia makri waja Wake.

 

Hali kadhaalika kumfanyia Allaah (عزّ وجلّ) au waja Wake istihzai, kudhihaki na aina yoyote ya shutuma kama kudai kwamba Mkono wa Allaah umefumbwa (5:64) na mengineyo, basi Allaah Naye Huwarudishia shutuma zao.

 

 

Share