060-Asbaabun-Nuzuwl: An-Nisaa Aayah 060: أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa 060-Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii pamoja na mbili zinazofuatia (4:60-62) zimeteremka kama alivyohadithia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  kuwa Abuu Barzah Al-Aslamiyy alikuwa ni Kuhani akitoa hukumu kuhusu magomvi yanayotokea baina ya Mayahudi. Siku moja baadhi ya watu katika washirikina walileta magomvi kwake, kisha Allaah Akateremsha Aayah hii:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ  

60. Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)  

 

[Abuu Haatim Atw-Twabaraaniy, na Ibn Hajar Al-‘Asqalaaniy (4/19) ambaye amesema isnaad yake ni nzuri]  

Sababun-Nuzuwl:

 

Pia Sababun-Nuzuwl nyingine ya Aayah hii ni kwamba waligombana mtu kutoka Answaar na Myahudi kisha Myahudi akasema: “Twende kwa Muhammad akatuhukumu.” Na yule Answaar akasema: “Twende kwa Ka’ab bin Al-Ashraf.” Imesemwa pia kuwa miongoni mwa wanafiki waliokuwa wakijidai kuwa ni Waislamu, lakini huku wakitafuta hukmu za kijaahiliyyah. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]  

 

Pia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما)  amesema: “Abuu Barzah Aslamiyy alikuwa mtabiri na akihukumu magomvi ya Mayahudi. Baadhi ya Waislamu walipomwendea kutaka awahukumu, Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَن يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلَالًا بَعِيدًا ﴿٦٠﴾

Je, huoni wale wanaodai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na yale yaliyoteremshwa kabla yako; wanataka wahukumiane kwa twaghuti (ubatilifu) na hali wameamrishwa wakanushe hayo. Na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali.

 

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا ﴿٦١﴾

Na wanapoambiwa: Njooni kwenye yale Aliyoyateremsha Allaah na kwa Rasuli, utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.

 

 

فَكَيْفَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ثُمَّ جَاءُوكَ يَحْلِفُونَ بِاللَّـهِ إِنْ أَرَدْنَا إِلَّا إِحْسَانًا وَتَوْفِيقًا ﴿٦٢﴾

Basi itakuwaje utakapowafika msiba kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yao? Kisha wakakujia wakiapa Wa-Allaahi hatukutaka ila mazuri na mapatano.  [(4:60-62) - Atw-Twabaraaniy]  

 

 

 

 

Share