067-Asbaabun-Nuzuwl: Al-Maaidah Aayah 067: وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

 

Al-Maaidah    067-Na Allaah Atakuhifadhi na watu

 

 

يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ ۚ وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ ﴿٦٧﴾

Ee Rasuli! Balighisha yale yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Rabb wako. Na usipofanya, basi utakuwa hukubalighisha ujumbe Wake. Na Allaah Atakuhifadhi na watu. Hakika Allaah Haongoi watu makafiri. [Al-Maaidah (5:67)]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ

Na Allaah Atakuhifadhi na watu. (5:67).

 

Imeteremka pale Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposhuka chini ya kivuli cha mti na akalitundika panga lake juu ya huo mti kisha akasinzia. Bedui mmoja akamjia akiwa katika hali ya usingizi, akalikamata panga la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kisha akamuamsha, akamwambia huku amelishika panga lake juu: Nani ana uwezo wa kunizuia nisikuue? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamjibu yule bedui: “Allaah Ndiye mwenye uwezo wa kukuzuia.” Hapo ikateremka Kauli hii ya Allaah (سبحانه وتعالى):

وَاللَّـهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ

Na Allaah Atakuhifadhi na watu. (5:67).

 [Amehadithia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) ,    imepokelewa na Ibn Hibbaan]

 

 

Share