Skip to main content

Fataawaa: Maasi Katika Ramadhwaan03-Shaykh 'Abdul-'Aziyz Aal Ash-Shaykh: Kupiga Punyeto Mchana Wa Mwezi Wa Ramadhwaan

Kupiga Punyeto Mchana Wa Mwezi Wa Ramadhwaan 



Shaykh 'Abdul-'Aziyz Aal Ash-Shaykh (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Muuliza kutoka Canada anauliza, nimetoa Manii (punyeto) mchana wa Ramadhwaan hali ya kuwa nimefunga. Nifanye nini? 



JIBU:



(Alichofanya ni haraam) na ni juu yake alipe siku hio. Kwa kuwa kutoa manii kwa makusudi haijuzu. Allaah Anasema: "Mwenye kufunga anatakiwa kuacha chakula chake, kinywaji chake na matamanio yake kwa ajili Yangu".