Skip to main content

Fataawaa: Yanayobatilisha Na Yasiyobatilisha Swawm07-Imaam Ibn ‘Uthyamiyn: Akimeza Maji Bila Kukusudia Kutokana Na Kusukutua Swawm Yake Inabatilika?

Akimeza Maji Bila Kukusudia Kutokana Na Kusukutua Swawm Yake Inabatilika?

Imaam Ibn ‘Uthyamiyn (Rahimahu Allaah)

www.alhidaaya.com

SWALI:

Je, Swawm ya mfungaji inabatilika ikiwa atasukutua kinywa au pua na kwa bahati mbaya akameza maji?

JIBU:

Aliyekuwa katika swawm akaukutua kinywa au pua na maji yakamuingia, Swawm yake haibatiliki, kwa kuwa hakukusudia hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

وَلَـٰكِن مَّا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ

lakini isipokuwa katika yale yaliyoyakusudia nyoyo zenu  [Al-Ahzaab 33;5]

[Imaam Muhammad  Swaalih Ibn 'Uthaymiyn -  Fiqhul-'Ibaadat, uk. 253]