08-Imaam Ibn ‘Uthaymiyn: Kipulizio Cha Kusaidia Upungufu Wa Pumzi Hakibatilishi Swawm

Kipulizio Cha Kusaidia Upungufu Wa Pumzi Hakibatilishi Swawm

Imaam Ibn ‘Uthaymiyn  (Rahimahu-Allaah)

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya kutumia kipulizio kwa ajili ya kusaidia matatizo ya upungufu wa pumzi?

 

JIBU:

 

Kipulizio ni mvuke na haufikii tumboni. Kwa hiyo tunasema kwamba hakuna ubaya kutumia mtu anapokuwa katika swawm na haitabatilisha swawm yako kwa sababu kama tulivyosema hakuna kitu kitakachoingia tumboni. Kwa vile ni kitu kinachovutwa na kutoka mvuke kisha unapotea, basi hakuna kinachofika tumboni kwa hiyo inarushusiwa kutumia wakati una swawm na swawm haibatiliki kwayo.

 

[Imaam Ibn ‘Uthaymiyn Fataawaa Arkanul-Islaam Darus-salaam Mjalada 2 Uk. 658]

 

 

Share