Skip to main content

007-Al-A'Raaf: Aayah Na Mafunzo181-Aayah Na Mafunzo: Kundi Katika Ummah Huu Watabakia Katika Haki Mpaka Siku Ya Qiyaamah

Aayah Na Mafunzo

www.alhidaaya.com

Al-A’raaf 181

181-Kundi Katika Ummah Huu Watabakia Katika Haki Mpaka Siku Ya Qiyaamah

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمِمَّنْ خَلَقْنَا أُمَّةٌ يَهْدُونَ بِالْحَقِّ وَبِهِ يَعْدِلُونَ ﴿١٨١﴾

Na katika Tuliowaumba, wako ummah wanaoongoza kwa haki na kwayo wanahukumu kiadilifu. [Al-A'raaf: 181]

Mafunzo:

Amesimulia Mu’aawiyah bin Abiy Sufyaan (رضي الله عنه) : Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Kutakuweko kundi katika Ummah wangu litaendelea kuwa juu ya haki likiwa na nguvu, hawezi kuwadhuru yeyote aliyekwenda nao kinyume au aliyesaliti mpaka Siku ya Qiyaamah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]