Taqabbala Allaahu Minnaa Wa Minkum – Iydul-Adhw-haa Al-Mubaarak

 

Taqabbala Allaahu Minnaa Wa Minkum – Iydul-Adhw-haa Al-Mubaarak

 

 

 

Kwa Munaasabah huu wa furaha wa siku tukufu ya ‘Iyd Al-Adhw-haa tunapenda kuwawasilishia salaam zetu na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu Wa Ta'alaa) Atughufurie dhambi zetu na Atuwache huru kutokana na Moto na Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd).

 

Kadhaalika, tunamuomba Yeye Allaah ('Azza wa Jalla) kwa Majina Yake mazuri, na Sifa Zake tukufu, Awataqabalie Hujaji Hijjah yao, Atujaalie sote furaha, amani, mapenzi, siha na iymaan pamoja na thabaat katika masiku yote ya uhai wetu, na Atutakabalie du'aa zetu.

 

Msisahau kuendeleza Takbira mpaka tarehe 13 Dhul-Hijjah Kwa maelezo zaida tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo:

 

Katazo La Swiyaam (Funga) Ayyaamut-Tashriyq: 11, 12, 13 Dhul-Hijjah Na Amali Za Kutenda

 

 

Ukumbusho Wa Takbiyr Katika Masiku Kumi Na Tatu Ya Dhul-Hijjah: Tarehe 1–13 Dhul-Hijjah

 

Bonyeza bango upate Takbira:

 

 

 

 

 

Share