Vitumbua Vya Kuku

Vitumbua Vya Kuku

Vipimo

Kuku - 3 Lb

Mayai - 6

Baking Powder - 1 kijiko cha chai

Pilipili boga - Robo kipande

Kitunguu maji - 1 kidogo

Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai

Kitunguu saumu(thomu) na Tangawizi - 1 kijiko cha supu

Chumvi - ½ kijiko cha chai

Mafuta ya kuchomea

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Chemsha kuku  mpaka awive. hakikisha umemchemsha na viungo vyote. baada ya kuwiva,  toa mifupa kwa kunyambua mnofu vipande vidogo vidogo.
  2. Kata kitunguu  vipande vidogo vidogo
  3. Kata pilipili boga (la kijani) vipande vidogo
  4. Tia vitu vyote hivyo katika mashine  la kusagia (Blender)
  5. Tia mayai, hakikisha mayai yanafunika mchanganyiko.
  6. Saga kwa muda mfupi tu.
  7. Weka mchanganyiko  uliosagika vizuri kwenye bakuli.
  8. Tia chumvi, pilipili manga na baking powder.
  9. Tayarisha chuma  cha kuchomea vitumbua kwenye jiko.
  10. Weka mafuta kidogo.
  11. Choma kama unavyochoma vitumbua vya mchele.

 

 

 

 

Share