118-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unaposimama Katika Mlima Wa Swafaa Na Wa Marwah

Hiswnul-Muslim

118-Du’aa  Unaposimama Katika Mlima Wa Swafaa Na Wa Marwah

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 [236]

Amesema Jaabir (رضي الله عنه)  katika Hadiyth ndefu aliyoielezea Hijah ya  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) kwamba alipokurubia Swafaa alisoma:

 

 إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِن شَعَائِرِ اللَّـهِ ۖ

Hakika Swafaa na Mar-wah ni katika alama za (Dini ya) Allaah[1] 

 

أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اللهُ بِهِ

Abdau bimaa Badaa-Allaahu bih

 

Ninaanza kwa alichoanza Allaah

 

… Akaanza Swafaa akapanda mpaka akaiona Al-Ka’bah kisha akaielekea na kusema:

 

اللهُ أكْبَرُ، اللهُ أكْبَرُ، اللهُ أكْبَرُ

Allaahu Akbar, Allaahu Akbar, Allaahu Akbar

 

Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa, Allaah ni Mkubwa.

 

… kisha atasema yafuatayo mara tatu akiomba du’aa (yoyote apendayo) baada ya kila mara:

 

لا إِلهَ إلاَّ  اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

 

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul  Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu,  wa hazzamal ahzaaba Wahdah

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na ni Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muwezahapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake.

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alisoma hivi mara tatu na baina yake akiomba du’aa, kisha akafanya alipokuwa Marwah kama alivyofanya alipokuwa Swafaa[2]

 

 

 

[1]Al-Baqarah (2: 158)

 

[2]Muslim (2/888) [1218].

 

 

Share