Biriyani Ya Kuku (kavu)

Biriyani Ya Kuku (kavu)

 

 

 

 

 

Vipimo

Mrowanishe kuku na viungo hivi kwa muda mdogo tu

Kuku (Mkate kate Vipande) - 4  LB

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 2  Vijiko vya supu

Chumvi - kiasi

Pilipili nyekundu ya unga - 1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano (Haldi au Tumeric) - 1 Kijiko cha chai

Bizari ya pilau ya powder (Jeera) - 1 Kijiko cha chai

Gilgilani powder (Dania) - 1 Kijiko cha chai

Ndimu - 1 Kijiko cha supu

 

Mchele na vitu vya Masala: 

Mchele (Basmati mzuri) (rowanisha) - 7 cups

Mafuta ya kupikia - kiasi

Vitunguu Vilivyokatwa - 8

Nyanya iliyokatwa katwa - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 1 Kijiko cha supu

Garam Masala -1 Kijiko cha supu

Hiliki powder - ½ Kijiko cha chai

Tomatoe paste - 1 Kijiko cha supu

Pilipili mbichi zipasue katikati - 4

Chumvi - kiasi

Mtindi - 4 Vijiko vya supu

Kotmiri iliokatwa (Chopped) - ½ Kikombe

Mafuta ya kunyunyuzia katika wali - 3 Vijiko vya supu

Zaafarani au rangi ya biriani - kiasi

 

Namna Ya Kutaarisha Na Kupika

Weka kuku aliyerowanishwa na viungo vyake katika Foil tray au chombo chocote utakachomwagia wali humo humo na kupikia biriani, kisha mchome (Bake)  mpaka awive na awe mkavu kiasi.

Wakati kuku anapikika, kaanga vitunguu katika karai au sufuria mpaka viwe brown na epua nusu yake weka kando.

Punguza mafuta yabakie kiasi tu, ongeza Thomu na tangawizi, na viungo vyote vya hapo juu isipokuwa Mtindi na kotmiri, endelea kukaanga hadi tomatoe zilainike. 

Ongeza chumvi, malizia mwisho kwa kutia mtindi, kotmiri na vile vitunguu ulivyoweka kando.  Masala yako tayari.

Mwagia masala juu ya kuku uliyekwishmpika changanya vizuri.

Chemsha Mchele uwive nusu, chuja na mwagia juu ya masala.

Nyunyiza mafuta kidogo juu ya mchele na zaafarani au rangi ya biriani.

 Bake katika moto wa 350 – 400 kwa muda wa 15 – 20 minutes.  Biriyani imekuwa tayari kuliwa.

 

Mtindi wa kutolea Biriyani:

Mtindi - 1 kikombe

Pilipili mbichi - 1 ndogo

Kitunguu saumu(/galic) thomu - chembe mbili

Nanaa - kiasi

Chumvi - chembe tu

Weka kwenye Blender na uchanganye, kisha mimina katika bakuli

 

 

 

Share