Saladi
Saladi Ya Bilingani Tango, Vitunguu Vyeupe Na Parsley
Vipimo na Namna ya Kutayarisha
Bilingani ndogo ndogo freshi Osha, katakata vipande vya mraba (cubes) - 5
Majani ya saladi (lettuce) Osha, katakata - 2 majani
Tango Osha, katakata - 2
Vitunguu vyepe Menya, katakata - 2
Nyanya/tungule Osha, katakata - 1
Parsley majani Osha, chuja maji, katakata - 1 mshikano (bunch)
Siki - 2 vijiko vya supu
Chumvi – Kisia
Pilipili nyekundu ya unga - ½ kijiko cha chai
Mafuta ya kukaangia bilingani - kiasi
Namna Ya Kutayarisha:
- Weka mafuta kiasi katika karai, wash moto.
- Kaanga bilingani katika mafuta yamoto, zikiiva na kugeuka rangi epua weka katika chujio zichuje mafuta.
- Katika bakuli, tia vitu vyote isipokuwa chumvi na siki.
- Karibu na kula, changanya vitu vyote utie chumvi na siki, uchanganye vizuri.
Majani ya parsley: