Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy00 - Muqaddimah (Utangulizi)

[المقدمة]

أخبرنا الشيخ المسند أبو الوقت عبد الأول بن عيسى بن شعيب السجزي الهروي قراءة عليه، أخبرنا الشيخ أبو الحسن عبد الرحمن بن محمد بن المظفر الداوودي قراءة عليه في جمادى الآخرة سنة خمس وستين وأربعمائة، أخبرنا أبو محمد عبد الله بن أحمد بن حمويه السرخسي قراءة عليه سنة إحدى وثمانين وثلاثمائة، أخبرنا أبو عمران عيسى بن عمر بن العباس السمرقندي، أخبرنا أبو محمد عبد الله بن عبد الرحمن الدارمي السمرقندي رحمه الله قال:

Ametukhabarisha Ash-Shaykh, Al-Musnid (mpokezi wa Hadiyth kwa Isnaad zake), Abul-Waqt 'Abdul-Awwal bin 'Iysaa bin Shu'ayb As-Sijziy Al-Harawiy, kwa kusomewa yeye; ametukhabarisha Ash-Shaykh Abul-Hasan 'Abdur-Rahmaan bin Muhammad bin Al-Mudhwaffar Ad-Daawuwdiy, kwa kusomewa yeye katika (mwezi wa) Jumaadaa Al-Aakhirah, mwaka wa mia nne na sitini na tano; ametukhabarisha Abuw Muhammad 'Abdu-Allaah bin Ahmad bin Hammuwyah As-Sarakhsiy, kwa kusomewa yeye mwaka wa mia tatu na themanini na moja; ametukhabarisha Abuw 'Imraan 'Iysaa bin 'Umar bin Al-'Abbaas As-Samarqandiy; ametukhabarisha Abuw Muhammad 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan Ad-Daarimiy As-Samarqandiy (رحمه الله), amesema:

1-Mlangoباب ما كان عليه الناس قبل مبعث النبي صلى الله عليه وسلم من الجهل والضلالةMlango Wa Yale Waliyokuwa Nayo Watu
Kabla Ya Kutumwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Katika Ujinga Na Upotofu

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُؤَاخَذُ الرَّجُلُ بِمَا عَمِلَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ؟، قَالَ: "مَنْ أَحْسَنَ فِي الْإِسْلَامِ لَمْ يُؤَاخَذْ بِمَا كَانَ عَمِلَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَمَنْ أَسَاءَ فِي الْإِسْلَامِ، أُخِذَ بِالْأَوَّلِ وَالْآخِرِ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, je, mtu atahesabiwa kwa yale aliyoyatenda katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam)? Akasema: "Atakayefanya wema katika Islaam, hatahesabiwa kwa yale aliyokuwa ameyatenda katika Jaahiliyyah; na atakayefanya ubaya katika Islaam, atahesabiwa kwa (amali za) mwanzo na za mwisho."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
153
Hadiyth
1

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ النَّضْرِ الرَّمْلِيُّ، عَنْ مَسَرَّةَ بْنِ مَعْبَدٍ مِنْ بَنِي الْحَارِثِ بْنِ أَبِي الْحَرَامِ مِنْ لَخْمٍ، عَنْ الْوَضِينِ، أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا كُنَّا أَهْلَ جَاهِلِيَّةٍ وَعِبَادَةِ أَوْثَانٍ، فَكُنَّا نَقْتُلُ الْأَوْلَادَ، وَكَانَتْ عِنْدِي بِنْتٌ لِي فَلَمَّا أَجَابَتْ، وَكَانَتْ مَسْرُورَةً بِدُعَائِي إِذَا دَعَوْتُهَا، فَدَعَوْتُهَا يَوْمًا، فَاتَّبَعَتْنِي فَمَرَرْتُ حَتَّى أَتَيْتُ بِئْرًا مِنْ أَهْلِي غَيْرَ بَعِيدٍ، فَأَخَذْتُ بِيَدِهَا فَرَدَّيْتُ بِهَا فِي الْبِئْرِ، وَكَانَ آخِرَ عَهْدِي بِهَا أَنْ تَقُولَ: يَا أَبَتَاهُ! يَا أَبَتَاهُ! فَبَكَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى وَكَفَ دَمْعُ عَيْنَيْهِ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ مِنْ جُلَسَاءِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَحْزَنْتَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ لَهُ: "كُفَّ فَإِنَّهُ يَسْأَلُ عَمَّا أَهَمَّهُ"، ثُمَّ قَالَ لَهُ: "أَعِدْ عَلَيَّ حَدِيثَكَ" فَأَعَادَهُ، فَبَكَى حَتَّى وَكَفَ الدَّمْعُ مِنْ عَيْنَيْهِ عَلَى لِحْيَتِهِ، ثُمَّ قَالَ لَهُ: "إِنَّ اللَّهَ قَدْ وَضَعَ عَنْ الْجَاهِلِيَّةِ مَا عَمِلُوا، فَاسْتَأْنِفْ عَمَلَكَ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin An-Nadhwr Ar-Ramliy, kutoka kwa Masarrah bin Ma'bad — miongoni mwa Banuw Al-Haarith bin Abil-Haraam, wa (kabila la) Lakhm —, kutoka kwa Al-Wadhwiyn, kwamba mtu mmoja alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tulikuwa watu wa Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) na wa kuabudu masanamu; tulikuwa tukiwaua watoto. Nami nilikuwa na binti yangu; alipofikia (umri wa) kuitikia, na alikuwa akifurahi ninapomwita, siku moja nilimwita, akanifuata. Nikapita mpaka nikafika kwenye kisima kisichokuwa mbali na watu wangu; nikamshika mkono wake, nikamtumbukiza ndani ya kisima. Na kitu cha mwisho nilichokisikia kutoka kwake kilikuwa ni kusema kwake: Yaa baba yangu! Yaa baba yangu! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akalia mpaka machozi ya macho yake yakatiririka. Mtu mmoja miongoni mwa waliokuwa wakikaa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Umemhuzunisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). (Nabiy) akamwambia: "Acha, kwani yeye anauliza kuhusu jambo linalomhangaisha." Kisha akamwambia (yule mwenye kisa): "Nirudie khabari yako." Akamrudia. Akalia mpaka machozi yakatiririka kutoka machoni mwake juu ya ndevu zake. Kisha akamwambia: "Hakika Allaah Amewaondolea (watu wa) Jaahiliyyah yale waliyoyatenda; basi anza upya amali yako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
153
Hadiyth
2

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ سُلَيْمَانَ الْمُؤَدِّبِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي مَوْلَايَ: "أَنَّ أَهْلَهُ بَعَثُوا مَعَهُ بِقَدَحٍ فِيهِ زُبْدٌ وَلَبَنٌ إِلَى آلِهَتِهِمْ، قَالَ: فَمَنَعَنِي أَنْ آكُلَ الزُّبْدَ لِمَخَافَتِهَا، قَالَ: فَجَاءَ كَلْبٌ فَأَكَلَ الزُّبْدَ وَشَرِبَ اللَّبَنَ، ثُمَّ بَالَ عَلَى الصَّنَمِ وَهُوَ: إِسَافٌ، وَنَائِلَةُ، قَالَ هَارُونُ: كَانَ الرَّجُلُ فِي الْجَاهِلِيَّةِ إِذَا سَافَرَ، حَمَلَ مَعَهُ أَرْبَعَةَ أَحْجَارٍ: ثَلَاثَةً لِقِدْرِهِ وَالرَّابِعَ يَعْبُدُهُ وَيُرَبِّي كَلْبَهُ، وَيَقْتُلُ وَلَدَهُ"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Ibraahiym bin Sulaymaan Al-Muaddib, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Mujaahid, amesema: Amenisimulia bwana wangu (aliyeniacha huru): "Kwamba watu wake walimtuma pamoja na bakuli lenye siagi na maziwa kwa miungu yao. Akasema: Kuiogopa (miungu hiyo) kukanizuia kula siagi. Akasema: Akaja mbwa, akala siagi na akanywa maziwa, kisha akakojolea sanamu, nalo ni: Isaaf na Naailah." Haaruwn amesema: Mtu katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) alikuwa anaposafiri, hubeba pamoja naye mawe manne: matatu kwa ajili ya chungu chake (cha kupikia), na la nne analiabudu; na humlea mbwa wake, na humuua mtoto wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
154
Hadiyth
3

حَدَّثَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا رَيْحَانُ هُوَ ابْنُ سَعِيدٍ السَّامِيُّ، حَدَّثَنَا عَبَّادٌ هُوَ ابْنُ مَنْصُورٍ، عَنْ أَبِي الرَّجَاءِ، قَالَ: "كُنَّا فِي الْجَاهِلِيَّةِ إِذَا أَصَبْنَا حَجَرًا حَسَنًا، عَبَدْنَاهُ، وَإِنْ لَمْ نُصِبْ حَجَرًا، جَمَعْنَا كُثْبَةً مِنْ رَمْلٍ، ثُمَّ جِئْنَا بِالنَّاقَةِ الصَّفِيِّ فَتَفَاجَّ عَلَيْهَا، فَنَحْلُبُهَا عَلَى الْكُثْبَةِ حَتَّى نَرْوِيَهَا، ثُمَّ نَعْبُدُ تِلْكَ الْكُثْبَةَ مَا أَقَمْنَا بِذَلِكَ الْمَكَانِ"، قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: الصَّفِيُّ: الْكَثِيرَةُ الْأَلْبَانِ، فَتَفَاجَّ يَعْنِي: النَّاقَةَ إِذَا فَرَّجَتْ بَيْنَ رِجْلَيْهَا لِلْحَلْبِ، وَالْفَجُّ: الطَّرِيقُ الْوَاسِعُ، وَجَمْعُهُ: فِجَاجٌ

Ametusimulia Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia Rayhaan — naye ni Ibn Sa'iyd As-Saamiy —, ametusimulia 'Abbaad — naye ni Ibn Manswuwr —, kutoka kwa Abur-Rajaa, amesema: "Tulikuwa katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam), tunapopata jiwe zuri, tunaliabudu; na tusipopata jiwe, tunakusanya rundo la mchanga, kisha tunamleta ngamia jike mwenye maziwa mengi, naye hutanua miguu yake juu yake (ili akamuliwe), tunamkamua juu ya rundo hilo mpaka tulilowanishe; kisha tunaliabudu rundo hilo muda wote tuliokaa mahali hapo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Asw-Swafiyy: (ngamia jike) mwenye maziwa mengi. Na fatafaajja maana yake ni: ngamia jike anapotanua kati ya miguu yake kwa ajili ya kukamuliwa. Na al-fajj: njia pana, na wingi wake ni fijaaj.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
155
Hadiyth
4

2-Mlangoباب صفة النبي صلى الله عليه وسلم في الكتب قبل مبعثهMlango Wa Sifa Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Katika Vitabu Kabla Ya Kutumwa Kwake

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَحْوَصِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، قَالَ: قَالَ كَعْبٌ: نَجِدُهُ مَكْتُوبًا: "مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَا فَظًّا، وَلَا غَلِيظًا، وَلَا صَخَّابًا بِالْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ، وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَغْفِرُ، وَأُمَّتُهُ الْحَمَّادُونَ يُكَبِّرُونَ اللَّهَ عز وجل عَلَى كُلِّ نَجْدٍ، وَيَحْمَدُونَهُ فِي كُلِّ مَنْزِلَةٍ، يَتَأَزَّرُونَ عَلَى أَنْصَافِهِمْ، وَيَتَوَضَّئُونَ عَلَى أَطْرَافِهِمْ، مُنَادِيهِمْ يُنَادِي فِي جَوِّ السَّمَاءِ صَفُّهُمْ فِي الْقِتَالِ، وَصَفُّهُمْ فِي الصَّلَاةِ سَوَاءٌ، لَهُمْ بِاللَّيْلِ دَوِيٌّ كَدَوِيِّ النَّحْلِ، مَوْلِدُهُ بِمَكَّةَ، وَمُهَاجِرُهُ بِطَيْبَةَ، وَمُلْكُهُ بِالشَّامِ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Ar-Rabiy', ametusimulia Abul-Ahwasw, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, amesema: Ka'b amesema: Tunamkuta ameandikwa (hivi): "Muhammad Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): si mwenye maneno makali, wala si mwenye moyo mgumu, wala si mpiga kelele masokoni, wala halipi ubaya kwa ubaya, lakini husamehe na hughufiria. Na Ummah wake ni wenye kumhimidi (Allaah) sana: wanamtukuza Allaah (عز وجل) juu ya kila mwinuko, na wanamhimidi katika kila kituo; wanajifunga izari zao mpaka nusu (ya miundi) yao, na wanatawadha viungo vyao; mwenye kuwaita (kwa Adhaan) huita katika anga la mbingu; safu yao katika vita na safu yao katika Swalaah ni sawa; wana mvumo usiku kama mvumo wa nyuki. Mahali pa kuzaliwa kwake ni Makkah, na mahali pa kuhamia kwake ni Twaybah (Madiynah), na ufalme wake uko Shaam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
156
Hadiyth
5

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي خَالِدٌ هُوَ ابْنُ يَزِيدَ، عَنْ سَعِيدٍ هُوَ ابْنُ أَبِي هِلَالٍ، عَنْ هِلَالِ بْنِ أُسَامَةَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ ابْنِ سَلَامٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "إِنَّا لَنَجِدُ صِفَةَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: إِنَّا أَرْسَلْنَاكَ شَاهِدًا وَمُبَشِّرًا وَنَذِيرًا، وَحِرْزًا، لِلْأُمِّيِّينَ، أَنْتَ عَبْدِي وَرَسُولِي، سَمَّيْتُهُ الْمُتَوَكِّلَ، لَيْسَ بِفَظٍّ، وَلَا غَلِيظٍ، وَلَا صَخَّابٍ بِالْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ مِثْلَهَا، وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَتَجَاوَزُ، وَلَنْ أَقْبِضَهُ حَتَّى يُقِيمَ الْمِلَّةَ الْمُتَعَوِّجَةَ بِأَنْ يَشْهَدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، نَفْتَحُ بِهِ أَعْيُنًا عُمْيًا وَآذَانًا صُمًا، وَقُلُوبًا غُلْفًا"، قَالَ عَطَاءُ بْنُ يَسَارٍ: وَأَخْبَرَنِي أَبُو وَاقِدٍ اللَّيْثِيُّ: أَنَّهُ سَمِعَ كَعْبًا يَقُولُ مِثْلَ مَا قَالَ ابْنُ سَلَامٍ

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Khaalid — naye ni Ibn Yaziyd —, kutoka kwa Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Hilaal —, kutoka kwa Hilaal bin Usaamah, kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar, kutoka kwa Ibn Salaam (رضي الله عنه), kwamba alikuwa akisema: "Hakika sisi tunaikuta sifa ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (hivi): Hakika Sisi Tumekutuma ukiwa ni shahidi, mwenye kubashiri na mwonyaji, na kinga kwa watu wasiojua kusoma na kuandika. Wewe ni Mja Wangu na Rasuli Wangu; Nimemwita Al-Mutawakkil (mwenye kutawakali kwa Allaah). Si mwenye maneno makali, wala si mwenye moyo mgumu, wala si mpiga kelele masokoni, wala halipi ubaya kwa mfano wake, lakini husamehe na hupuuza (makosa). Na Sitamfisha mpaka aisimamishe mila iliyopinda, kwa kushuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah. Tunafungua kupitia kwake macho yaliyo vipofu, na masikio yaliyo viziwi, na nyoyo zilizofunikwa." 'Atwaa bin Yasaar amesema: Na amenikhabarisha Abuw Waaqid Al-Laythiy (رضي الله عنه) kwamba alimsikia Ka'b akisema mfano wa aliyoyasema Ibn Salaam (رضي الله عنه).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
156
Hadiyth
6

أَخْبَرَنَا زَيْدُ بْنُ عَوْفٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ ذَكْوَانَ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ كَعْبٍ: "فِي السَّطْرِ الْأَوَّلِ: مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ، عَبْدِي الْمُخْتَارُ، لَا فَظًّا، وَلَا غَلِيظًا، وَلَا صَخَّابًا فِي الْأَسْوَاقِ، وَلَا يَجْزِي بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ، وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَغْفِرُ، مَوْلِدُهُ بِمَكَّةَ، وَهِجْرَتُهُ بِطَيْبَةَ، وَمُلْكُهُ بِالشَّامِ، وَفِي السَّطْرِ الثَّانِي: مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ، أُمَّتُهُ الْحَمَّادُونَ يَحْمَدُونَ اللَّهَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ، يَحْمَدُونَ اللَّهَ فِي كُلِّ مَنْزِلَةٍ، وَيُكَبِّرُونَه عَلَى كُلِّ شَرَفٍ، رُعَاةُ الشَّمْسِ يُصَلُّونَ الصَّلَاةَ إِذَا جَاءَ وَقْتُهَا وَلَوْ كَانُوا عَلَى رَأْسِ كُنَاسَةٍ، وَيَأْتَزِرُونَ عَلَى أَوْسَاطِهِمْ، وَيُوَضِّئُونَ أَطْرَافَهُمْ، وَأَصْوَاتُهُمْ بِاللَّيْلِ فِي جَوِّ السَّمَاءِ كَأَصْوَاتِ النَّحْلِ"

Ametukhabarisha Zayd bin 'Awf, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Dhakwaan Abuw Swaalih, kutoka kwa Ka'b: "Katika mstari wa kwanza: Muhammad Rasuli wa Allaah, Mja Wangu Mteule; si mwenye maneno makali, wala si mwenye moyo mgumu, wala si mpiga kelele masokoni, wala halipi ubaya kwa ubaya, lakini husamehe na hughufiria. Mahali pa kuzaliwa kwake ni Makkah, na Hijrah yake ni Twaybah (Madiynah), na ufalme wake uko Shaam. Na katika mstari wa pili: Muhammad Rasuli wa Allaah; Ummah wake ni wenye kumhimidi (Allaah) sana: wanamhimidi Allaah katika hali ya wasaa na katika hali ya shida, wanamhimidi Allaah katika kila kituo, na wanamtukuza juu ya kila mwinuko. Ni wachungaji wa jua (wanaofuatilia mwenendo wake kwa ajili ya nyakati za Swalaah): wanaswali Swalaah inapofika wakati wake, hata wakiwa juu ya jaa la taka. Na wanajifunga izari kwenye viuno vyao, na wanatawadha viungo vyao; na sauti zao usiku katika anga la mbingu ni kama sauti za nyuki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
156
Hadiyth
7

أَخْبَرَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا مَعْنُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ أَبِي فَرْوَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنَّهُ سَأَلَ كَعْبَ الْأَحْبَارِ: كَيْفَ تَجِدُ نَعْتَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي التَّوْرَاةِ؟، فَقَالَ كَعْبٌ: "نَجِدْهُ مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ يُولَدُ بِمَكَّةَ، وَيُهَاجِرُ إِلَى طَابَةَ، وَيَكُونُ مُلْكُهُ بِالشَّامِ، وَلَيْسَ بِفَحَّاشٍ، وَلَا صَخَّابٍ فِي الْأَسْوَاقِ، وَلَا يُكَافِئُ بِالسَّيِّئَةِ السَّيِّئَةَ، وَلَكِنْ يَعْفُو وَيَغْفِرُ، أُمَّتُهُ الْحَمَّادُونَ، يَحْمَدُونَ اللَّهَ فِي كُلِّ سَرَّاءَ، وَيُكَبِّرُونَ اللَّهَ عَلَى كُلِّ نَجْدٍ، يُوَضِّئُونَ أَطْرَافَهُمْ، وَيَأْتَزِرُونَ فِي أَوْسَاطِهِمْ، يُصَفُّونَ فِي صَلاتِهِمْ كَمَا يُصَفُّونَ فِي قِتَالِهِمْ، دَوِيُّهُمْ فِي مَسَاجِدِهِمْ كَدَوِيِّ النَّحْلِ، يُسْتَمَعُ مُنَادِيهِمْ فِي جَوِّ السَّمَاءِ"

Ametukhabarisha Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia Ma'n bin 'Iysaa, ametusimulia Mu'aawiyah bin Swaalih, kutoka kwa Abuw Farwah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba alimuuliza Ka'b Al-Ahbaar: Unaikutaje sifa ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Tawraat? Ka'b akasema: "Tunamkuta: Muhammad bin 'Abdi-Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), atazaliwa Makkah, na atahamia Twaabah (Madiynah), na ufalme wake utakuwa Shaam. Si mwenye maneno machafu, wala si mpiga kelele masokoni, wala halipizi ubaya kwa ubaya, lakini husamehe na hughufiria. Ummah wake ni wenye kumhimidi (Allaah) sana: wanamhimidi Allaah katika kila hali ya wasaa, na wanamtukuza Allaah juu ya kila mwinuko; wanatawadha viungo vyao, na wanajifunga izari kwenye viuno vyao; wanapanga safu katika Swalaah zao kama wanavyopanga safu katika vita vyao; mvumo wao katika Misikiti yao ni kama mvumo wa nyuki; mwenye kuwaita (kwa Adhaan) husikilizwa katika anga la mbingu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
158
Hadiyth
8

أَخْبَرَنَا حَيْوَةُ بْنُ شُرَيْحٍ، حَدَّثَنَا بَقِيَّةُ بْنُ الْوَلِيدِ الْمِيثَمِيُّ، حَدَّثَنَا بَحِيرُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ، عَنْ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ الْحَضْرَمِيِّ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ إِلَيْكُمْ لَيْسَ بِوَهِنٍ، وَلَا كَسِلٍ، لِيُحْيِيَ قُلُوبًا غُلْفًا، وَيَفْتَحَ أَعْيُنًا عُمْيًا، وَيُسْمِعَ آذَانًا صُمًّا، وَيُقِيمَ السُّنَّةَ العَوْجَاءَ، حَتَّى يُقَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ"

Ametukhabarisha Haywah bin Shurayh, ametusimulia Baqiyyah bin Al-Waliyd Al-Miythamiy, ametusimulia Bahiyr bin Sa'd, kutoka kwa Khaalid bin Ma'daan, kutoka kwa Jubayr bin Nufayr Al-Hadhwramiy, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika amekujieni Rasuli, si dhaifu wala si mvivu, ili azihuishe nyoyo zilizofunikwa, na ayafungue macho yaliyo vipofu, na ayasikilizishe masikio yaliyo viziwi, na aisimamishe njia iliyopinda, mpaka isemwe: Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
159
Hadiyth
9

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ: كَانَ رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَهُ إِلَيْهِ حَاجَةٌ، فَمَشَى مَعَهُ حَتَّى دَخَلَ، قَالَ: فَإِحْدَى رِجْلَيْهِ فِي الْبَيْتِ وَالْأُخْرَى خَارِجَة كَأَنَّهُ يُنَاجِي، فَالْتَفَتَ، فَقَالَ: "أَتَدْرِي مَنْ كُنْتُ أُكَلِّمُ؟ إِنَّ هَذَا مَلَكٌ لَمْ أَرَهُ قَطُّ قَبْلَ يَوْمِي هَذَا، اسْتَأْذَنَ رَبَّهُ أَنْ يُسَلِّمَ عَلَيَّ، قَالَ: إِنَّا آتَيْنَاكَ أَوْ أَنْزَلْنَا الْقُرْآنَ فَصْلًا، وَالسَّكِينَةَ صَبْرًا، وَالْفُرْقَانَ وَصْلًا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Al-Hizaamiy, ametusimulia Is-haaq bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Amr bin Abiy Qays, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa 'Aamir, amesema: Mtu mmoja miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa na haja kwake; akatembea pamoja naye mpaka (Nabiy) akaingia (nyumbani). Akasema: Mguu wake mmoja ukawa ndani ya nyumba na mwingine nje, kama kwamba anazungumza kwa siri (na mtu). Kisha akageuka, akasema: "Je, unajua nilikuwa nikizungumza na nani? Hakika huyu ni Malaika (عليه السلام) ambaye sijapata kumuona kabla ya siku yangu hii; amemuomba Rabb wake idhini ili anisalimie. Akasema: Hakika Sisi Tumekupa — au: Tumeteremsha — Qur-aan ikiwa ni upambanuzi, na utulivu ukiwa ni subira, na pambanuo (la haki na baatwil) likiwa ni kiungo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
159
Hadiyth
10

أَخْبَرَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا رَيْحَانُ هُوَ ابْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَبَّادٌ هُوَ ابْنُ مَنْصُورٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ عَطِيَّةَ، أَنَّهُ سَمِعَ رَبِيعَةَ الْجُرَشِيَّ، يَقُولُ: أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقِيلَ لَهُ: لِتَنَمْ عَيْنُكَ، وَلْتَسْمَعْ أُذُنُكَ، وَلْيَعْقِلْ قَلْبُكَ، قَالَ: "فَنَامَتْ عَيْنَايَ، وَسَمِعَتْ أُذُنَايَ، وَعَقَلَ قَلْبِي"، قَالَ: فَقِيلَ لِي: سَيِّدٌ بَنَى دَارًا فَصَنَعَ مَأْدُبَةً، وَأَرْسَلَ دَاعِيًا، فَمَنْ أَجَابَ الدَّاعِيَ، دَخَلَ الدَّارَ، وَأَكَلَ مِنْ الْمَأْدُبَةِ، وَرَضِيَ عَنْهُ السَّيِّدُ، وَمَنْ لَمْ يُجِبْ الدَّاعِيَ، لَمْ يَدْخُلْ الدَّارَ، وَلَمْ يَطْعَمْ مِنْ الْمَأْدُبَةِ، وَسَخِطَ عَلَيْهِ السَّيِّدُ، قَالَ: "فَاللَّهُ: السَّيِّدُ، وَمُحَمَّدٌ: الدَّاعِي، وَالدَّارُ: الْإِسْلَامُ، وَالْمَأْدُبَةُ: الْجَنَّةُ"

Ametukhabarisha Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia Rayhaan — naye ni Ibn Sa'iyd —, ametusimulia 'Abbaad — naye ni Ibn Manswuwr —, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa 'Atwiyyah, kwamba alimsikia Rabiy'ah Al-Jurashiy akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijiwa, akaambiwa: Jicho lako lilale, na sikio lako lisikie, na moyo wako uelewe. Akasema: "Basi macho yangu yakalala, na masikio yangu yakasikia, na moyo wangu ukaelewa." Akasema: "Kisha nikaambiwa: Bwana mmoja amejenga nyumba, akaandaa karamu, na akamtuma mwitaji. Basi atakayemuitikia mwitaji, ataingia nyumbani, na atakula katika karamu, na bwana atamridhia; na asiyemuitikia mwitaji, hataingia nyumbani, wala hatakula katika karamu, na bwana atamkasirikia." Akasema: "Basi Allaah Ndiye Bwana, na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ndiye mwitaji, na nyumba ni Islaam, na karamu ni Jannah (Pepo)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
160
Hadiyth
11

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مَيْمُونٍ التَّمِيمِيِّ، عَنْ أَبِي عُثْمَانَ النَّهْدِيِّ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ إِلَى الْبَطْحَاءِ، وَمَعَهُ ابْنُ مَسْعُودٍ، فَأَقْعَدَهُ وَخَطَّ عَلَيْهِ خَطًّا، ثُمَّ قَالَ: "لَا تَبْرَحَنَّ فَإِنَّهُ سَيَنْتَهِي إِلَيْكَ رِجَالٌ فَلَا تُكَلِّمْهُمْ، فَإِنَّهُمْ لَنْ يُكَلِّمُوكَ"، فَمَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَيْثُ أَرَادَ، ثُمَّ جَعَلُوا يَنْتَهُونَ إِلَى الْخَطِّ لَا يُجَاوِزُونَهُ، ثُمَّ يَصْدُرُونَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى إِذَا كَانَ مِنْ آخِرِ اللَّيْلِ، جَاءَ إِلَيَّ فَتَوَسَّدَ فَخِذِي، وَكَانَ إِذَا نَامَ، نَفَخَ فِي النَّوْمِ، نَفْخًا فَبَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُتَوَسِّدٌ فَخِذِي، رَاقِدٌ، إِذْ أَتَانِي رِجَالٌ كَأَنَّهُمْ الْجِمَالُ عَلَيْهِمْ ثِيَابٌ بِيضٌ اللَّهُ أَعْلَمُ مَا بِهِمْ مِنْ الْجَمَالِ حَتَّى قَعَدَ طَائِفَةٌ مِنْهُمْ عِنْدَ رَأْسِهِ، وَطَائِفَةٌ مِنْهُمْ عِنْدَ رِجْلَيْهِ، فَقَالُوا بَيْنَهُمْ: مَا رَأَيْنَا عَبْدًا أُوتِيَ مِثْلَ مَا أُوتِيَ هَذَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: إِنَّ عَيْنَيْهِ لَتَنَامَانِ، وَإِنَّ قَلْبَهُ لَيَقْظَانُ، اضْرِبُوا لَهُ مَثَلًا: سَيِّدٌ بَنَى قَصْرًا ثُمَّ جَعَلَ مَأْدُبَةً فَدَعَا النَّاسَ إِلَى طَعَامِهِ وَشَرَابِهِ، ثُمَّ ارْتَفَعُوا، وَاسْتَيْقَظَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ، فَقَالَ: "أَتَدْرِي مَنْ هَؤُلَاءِ؟"، قُلْتُ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: "هُمْ الْمَلَائِكَةُ"، قَالَ: "وَهَلْ تَدْرِي مَا الْمَثَلُ الَّذِي ضَرَبُوهُ؟"، قُلْتُ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: "الرَّحْمَنُ بَنَى الْجَنَّةَ فَدَعَا إِلَيْهَا عِبَادَهُ، فَمَنْ أَجَابَهُ، دَخَلَ جَنَّتَهُ، وَمَنْ لَمْ يُجِبْ، عَاقَبَهُ وَعَذَّبَهُ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin 'Aliy, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Ja'far bin Maymuwn At-Tamiymiy, kutoka kwa Abuw 'Uthmaan An-Nahdiy, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka kwenda Al-Batwhaa (bonde la Makkah), na pamoja naye alikuwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه). Akamketisha, na akampigia mstari kumzunguka, kisha akasema: "Usiondoke kabisa (mahali hapa), kwani watakufikia wanaume; basi usiwasemeshe, kwani wao hawatakusemesha." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaenda alikotaka. Kisha (wale wanaume) wakawa wanafika kwenye ule mstari bila kuuvuka, kisha wanarudi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mpaka ilipokuwa mwishoni mwa usiku, (Nabiy) alinijia akalaza kichwa chake juu ya paja langu; na alikuwa anapolala, hupuliza (pumzi) katika usingizi. Basi wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amelaza kichwa chake juu ya paja langu, amelala, ghafla wakanijia wanaume kama kwamba ni ngamia, wamevaa nguo nyeupe — Allaah Ndiye Mjuzi zaidi wa uzuri waliokuwa nao —, mpaka kundi moja miongoni mwao likaketi karibu na kichwa chake, na kundi (jingine) miongoni mwao karibu na miguu yake. Wakasemezana wao kwa wao: Hatujapata kumuona mja aliyepewa mfano wa aliyopewa Nabiy huyu (صلى الله عليه وآله وسلم): hakika macho yake yanalala, na moyo wake uko macho. Mpigieni mfano: Bwana mmoja amejenga kasri, kisha akaandaa karamu, akawaita watu kwenye chakula chake na kinywaji chake. Kisha wakapanda juu. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamka wakati huo, akasema: "Je, unajua hawa ni akina nani?" Nikasema: Allaah na Rasuli Wake ndio wajuzi zaidi. Akasema: "Wao ni Malaika (عليهم السلام)." Akasema: "Na je, unajua ni mfano gani waliopiga?" Nikasema: Allaah na Rasuli Wake ndio wajuzi zaidi. Akasema: "Ar-Rahmaan Amejenga Jannah (Pepo), Akawaita Waja Wake kuiendea; basi atakayemuitikia, ataingia Jannah Yake, na asiyeitikia, Atamlipa (ubaya wake) na Atamuadhibu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
161
Hadiyth
12

3-Mlangoباب كيف كان أول شأن النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Ulikuwaje
Mwanzo Wa Jambo La Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ بَحِيرٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَمْرٍو السُّلَمِيُّ، عَنْ عُتْبَةَ بْنِ عَبْدٍ السُّلَمِيِّ، أَنَّهُ حَدَّثَهُمْ وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ لَهُ رَجُلٌ: كَيْفَ كَانَ أَوَّلُ شَأْنِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟، قَالَ: "كَانَتْ حَاضِنَتِي مِنْ بَنِي سَعْدِ بْنِ بَكْرٍ، فَانْطَلَقْتُ أَنَا، وَابْنٌ لَهَا فِي بَهْمٍ لَنَا وَلَمْ نَأْخُذْ مَعَنَا زَادًا، فَقُلْتُ: يَا أَخِي، اذْهَبْ فَأْتِنَا بِزَادٍ مِنْ عِنْدِ أُمِّنَا، فَانْطَلَقَ أَخِي وَمَكَثْتُ عِنْدَ الْبَهْمِ، فَأَقْبَلَ طَائِرَانِ أَبْيَضَانِ كَأَنَّهُمَا نَسْرَانِ، فَقَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: أَهُوَ هُوَ؟، قَالَ الْآخَرُ: نَعَمْ، فَأَقْبَلَا يَبْتَدِرَانِي فَأَخَذَانِي فَبَطَحَانِي لِلْقَفَا فَشَقَّا بَطْنِي ثُمَّ اسْتَخْرَجَا قَلْبِي فَشَقَّاهُ، فَأَخْرَجَا مِنْهُ عَلَقَتَيْنِ سَوْدَاوَيْنِ، فَقَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: ائْتِنِي بِمَاءِ ثَلْجٍ، فَغَسَلَ بِهِ جَوْفِي، ثُمَّ قَالَ: ائْتِنِي بِمَاءِ بَرَدٍ، فَغَسَلَ بِهِ قَلْبِي، ثُمَّ قَالَ: ائْتِنِي بِالسَّكِينَةِ فَذَرَّهُ فِي قَلْبِي، ثُمَّ قَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: حُصْهُ، فَحَاصَهُ وَخَتَمَ عَلَيْهِ بِخَاتَمِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ قَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: اجْعَلْهُ فِي كِفَّةٍ وَاجْعَلْ أَلْفًا مِنْ أُمَّتِهِ فِي كِفَّةٍ"، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَإِذَا أَنَا أَنْظُرُ إِلَى الْأَلْفِ فَوْقِي أُشْفِقُ أَنْ يَخِرَّ عَلَيَّ بَعْضُهُمْ، فَقَالَ: لَوْ أَنَّ أُمَّتَهُ وُزِنَتْ بِهِ لَمَالَ بِهِمْ، ثُمَّ انْطَلَقَا وَتَرَكَانِي"، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "وَفَرِقْتُ فَرَقًا شَدِيدًا، ثُمَّ انْطَلَقْتُ إِلَى أُمِّي فَأَخْبَرْتُهَا بِالَّذِي لَقِيتُ، فَأَشْفَقَتْ أَنْ يَكُونَ قَدْ الْتَبَسَ بِي، فَقَالَتْ: أُعِيذُكَ بِاللَّهِ، فَرَحَلَتْ بَعِيرًا لَهَا، فَجَعَلَتْنِي عَلَى الرَّحْلِ وَرَكِبَتْ خَلْفِي حَتَّى بُلَغْنَا إِلَى أُمِّي، فَقَالَتْ: أَدَّيْتُ أَمَانَتِي وَذِمَّتِي، وَحَدَّثَتْهَا بِالَّذِي لَقِيتُ، فَلَمْ يَرُعْهَا ذَلِكَ، وَقَالَتْ: إِنِّي رَأَيْتُ حِينَ خَرَجَ مِنِّي شَيْئًا، يَعْنِي: نُورًا أَضَاءَتْ مِنْهُ قُصُورُ الشَّامِ"

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia Baqiyyah, kutoka kwa Bahiyr, kutoka kwa Khaalid bin Ma'daan, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr As-Sulamiy, kutoka kwa 'Utbah bin 'Abd As-Sulamiy (رضي الله عنه), kwamba aliwasimulia — naye alikuwa miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —: Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), mtu mmoja alimwambia: Ulikuwaje mwanzo wa jambo lako, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Mlezi wangu (aliyenilea) alikuwa ni kutoka kwa Banuw Sa'd bin Bakr. Nikaenda mimi na mwanawe mmoja kwa wanyama wetu wadogo (wana-kondoo na wana-mbuzi), wala hatukuchukua pamoja nasi chakula. Nikasema: Yaa ndugu yangu, nenda ukatuletee chakula kutoka kwa mama yetu. Ndugu yangu akaenda, nami nikabakia kwa wale wanyama wadogo. Wakaja ndege wawili weupe kama kwamba ni tai wawili. Mmoja wao akamwambia mwenzake: Je, ndiye huyu? Mwingine akasema: Ndiyo. Wakanijia mbio, wakanichukua, wakanilaza chali, wakapasua tumbo langu, kisha wakautoa moyo wangu wakaupasua, wakatoa ndani yake mabonge mawili ya damu meusi. Mmoja wao akamwambia mwenzake: Niletee maji ya theluji. Akaosha kwayo ndani ya tumbo langu. Kisha akasema: Niletee maji ya barafu (ya mvua ya mawe). Akaosha kwayo moyo wangu. Kisha akasema: Niletee utulivu. Akaunyunyiza ndani ya moyo wangu. Kisha mmoja wao akamwambia mwenzake: Ushone. Akaushona, na akaupiga muhuri kwa muhuri wa Unabii. Kisha mmoja wao akamwambia mwenzake: Mweke katika kitanga kimoja (cha mizani), na uweke watu elfu moja katika Ummah wake katika kitanga (kingine)." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Basi ghafla nikawa ninaitazama ile elfu juu yangu, nikihofia baadhi yao wasije kuniangukia. Akasema (mmoja wao): Lau Ummah wake ungepimwa naye, angeuzidi uzito. Kisha wakaondoka na wakaniacha." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Nikaogopa hofu kubwa sana. Kisha nikaenda kwa mama yangu (mlezi), nikamkhabarisha yale yaliyonikuta. Akahofia kwamba huenda nimepatwa na kitu (cha majini). Akasema: Nakukinga kwa Allaah. Akamtandikia ngamia wake tandiko, akaniweka juu ya tandiko, na akapanda nyuma yangu, mpaka tukamfikia mama yangu. Akasema: Nimetekeleza amana yangu na dhamana yangu; na akamsimulia yale yaliyonikuta. Hilo halikumshtua, na akasema: Hakika mimi niliona, alipotoka ndani yangu, kitu — yaani: nuru — ambacho majumba ya Shaam yaling'aa kutokana nacho."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
163
Hadiyth
13

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ، حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عُثْمَانَ الْقُرَشِيُّ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ الْغِفَارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، كَيْفَ عَلِمْتَ أَنَّكَ نَبِيٌّ حَتَّى اسْتَيْقَنْتَ؟، فَقَالَ: "يَا أَبَا ذَرٍّ، أَتَانِي مَلَكَانِ وَأَنَا بِبَعْضِ بَطْحَاءِ مَكَّةَ فَوَقَعَ أَحَدُهُمَا عَلَي الْأَرْضِ، وَكَانَ الْآخَرُ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، فَقَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: أَهُوَ هُوَ؟، قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: زِنْهُ بِرَجُلٍ، فَوُزِنْتُ بِهِ فَوَزَنْتُهُ، ثُمَّ قَالَ: فَزِنْهُ بِعَشَرَةٍ، فَوُزِنْتُ بِهِمْ فَرَجَحْتُهُمْ، ثُمَّ قَالَ: زِنْهُ بِمِئَةٍ، فَوُزِنْتُ بِهِمْ فَرَجَحْتُهُمْ، ثُمَّ قَالَ: زِنْهُ بِأَلْفٍ، فَوُزِنْتُ بِهِمْ فَرَجَحْتُهُمْ كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَيْهِمْ يَنْتَثِرُونَ عَلَيَّ مِنْ خِفَّةِ الْمِيزَانِ، قَالَ: فَقَالَ أَحَدُهُمَا لِصَاحِبِهِ: لَوْ وَزَنْتَهُ بِأُمَّتِهِ لَرَجَحَهَا"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Abuw Daawuwd, ametusimulia Ja'far bin 'Uthmaan Al-Qurashiy, kutoka kwa 'Umar bin 'Urwah bin Az-Zubayr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Dharr Al-Ghifaariy (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, ulijuaje kwamba wewe ni Nabiy mpaka ukawa na yakini? Akasema: "Yaa Abaa Dharr, walinijia Malaika wawili (عليهما السلام) nami nikiwa katika sehemu ya Batwhaa (bonde) ya Makkah. Mmoja wao akatua ardhini, na mwingine alikuwa kati ya mbingu na ardhi. Mmoja wao akamwambia mwenzake: Je, ndiye huyu? Akasema: Ndiyo. Akasema: Mpime (katika mizani) na mtu mmoja. Nikapimwa naye, nikamzidi uzito. Kisha akasema: Mpime na watu kumi. Nikapimwa nao, nikawazidi uzito. Kisha akasema: Mpime na watu mia. Nikapimwa nao, nikawazidi uzito. Kisha akasema: Mpime na watu elfu. Nikapimwa nao, nikawazidi uzito, kama kwamba ninawatazama wakinitawanyikia kutokana na wepesi wa mizani (yao). Akasema: Mmoja wao akamwambia mwenzake: Lau ungempima na Ummah wake, angeuzidi uzito."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
164
Hadiyth
14

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيلُ بْنُ خَلِيلٍ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُسْهِرٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُنَادِيهِمْ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّمَا أَنَا رَحْمَةٌ مُهْدَاةٌ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Khaliyl, ametusimulia 'Aliy bin Mus-hir, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiwaita (watu): "Enyi watu! Hakika mimi ni Rehma iliyotolewa zawadi (kwenu)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
165
Hadiyth
15

4-Mlangoباب ما أكرم الله تعالى به نبيه صلى الله عليه وسلم
من إيمان الشجر به، والبهائم، والجن
Mlango Wa Yale Ambayo Allaah (تعالى)
Amemkirimu Kwayo Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)
Ya Kuaminiwa Kwake Na Miti, Wanyama Na Majini

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ طَرِيفٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ فُضَيْلٍ، حَدَّثَنَا أَبُو حَيَّانَ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فِي سَفَرٍ فَأَقْبَلَ أَعْرَابِيٌّ فَلَمَّا دَنَا مِنْهُ، قَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَيْنَ تُرِيدُ؟"، قَالَ: إِلَى أَهْلِي، قَالَ: "هَلْ لَكَ فِي خَيْرٍ؟"، قَالَ: وَمَا هُوَ؟، قَالَ: "تَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ"، فَقَالَ: وَمَنْ يَشْهَدُ عَلَى مَا تَقُولُ؟، قَالَ: "هَذِهِ السَّلَمَةُ"، فَدَعَاهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهِيَ بِشَاطِئِ الْوَادِي فَأَقْبَلَتْ تَخُدُّ الْأَرْضَ خَدًّا حَتَّى قَامَتْ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَاسْتَشْهَدَهَا ثَلَاثًا، فَشَهِدَتْ ثَلَاثًا أَنَّهُ كَمَا قَالَ، ثُمَّ رَجَعَتْ إِلَى مَنْبَتِهَا، وَرَجَعَ الْأَعْرَابِيُّ إِلَى قَوْمِهِ، وَقَالَ: إِنْ اتَّبَعُونِي أَتَيْتُكَ بِهِمْ، وَإِلَّا رَجَعْتُ، فَكُنْتُ مَعَكَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Twariyf, ametusimulia Muhammad bin Fudhwayl, ametusimulia Abuw Hayyaan, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini. Akaja Bedui mmoja; alipomkaribia, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Unakwenda wapi?" Akasema: Kwa jamaa zangu. Akasema: "Je, unataka kheri?" Akasema: Ni ipi hiyo? Akasema: "Ushuhudie kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, hana mshirika, na kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Mja Wake na Rasuli Wake." Akasema: Na nani atashuhudia juu ya unayoyasema? Akasema: "Mti huu wa salamah (aina ya mti wa miiba)." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauita, nao ulikuwa ukingoni mwa bonde. Ukaja ukiipasua ardhi mpaka ukasimama mbele yake. Akautaka ushuhudie mara tatu, ukashuhudia mara tatu kwamba yeye ni kama alivyosema. Kisha ukarudi mahali ulipoota; na yule Bedui akarudi kwa watu wake, na akasema: Wakinifuata, nitakujia nao; na wasiponifuata, nitarudi, niwe pamoja nawe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
166
Hadiyth
16

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ عَبْدِ الْمَلِكِ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: خَرَجْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، وَكَانَ لَا يَأْتِي الْبَرَازَ حَتَّى يَتَغَيَّبَ فَلَا يُرَى، فَنَزَلْنَا بِفَلَاةٍ مِنْ الْأَرْضِ لَيْسَ فِيهَا شَجَرةٌ، وَلَا عَلَمٌ، فَقَالَ: "يَا جَابِرُ، اجْعَلْ فِي إِدَاوَتِكَ مَاءً ثُمَّ انْطَلِقْ بِنَا"، قَالَ: فَانْطَلَقْنَا حَتَّى لَا نُرَى، فَإِذَا هُوَ بِشَجَرَتَيْنِ بَيْنَهُمَا أَرْبَعُ أَذْرُعٍ، فَقَالَ: "يَا جَابِرُ، انْطَلِقْ إِلَى هَذِهِ الشَّجَرَةِ، فَقُلْ: يُقُولُ لَكِ رَسولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: الْحَقِي بِصَاحِبَتِكِ حَتَّى أَجْلِسَ خَلْفَكُمَا"، قَالَ: فَفَعَلْتُ، فَرَجَعَتْ إِلَيْهَا، فَجَلَسَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَلْفَهُمَا، ثُمَّ رَجَعَتَا إِلَى مَكَانِهِمَا، فَرَكِبْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَسُولُ اللَّهِ بَيْنَنَا كَأَنَّمَا عَلَيْنَا الطَّيْرُ تُظِلُّنَا، فَعَرَضَتْ لَهُ امْرَأَةٌ مَعَهَا صَبِيٌّ لَهَا، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ ابْنِي هَذَا يَأْخُذُهُ الشَّيْطَانُ كُلَّ يَوْمٍ ثَلَاثَ مِرَارٍ، قَالَ: فَتَنَاوَلَ الصَّبِيَّ فَجَعَلَهُ بَيْنَهُ وَبَيْنَ مُقَدَّمِ الرَّحْلِ، ثُمَّ قَالَ: "اخْسَأْ عَدُوَّ اللَّهِ، أَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، اخْسَأْ عَدُوَّ اللَّهِ أَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلَاثًا"، ثُمَّ دَفَعَهُ إِلَيْهَا، فَلَمَّا قَضَيْنَا سَفَرَنَا، مَرَرْنَا بِذَلِكَ الْمَكَانِ فَعَرَضَتْ لَنَا الْمَرْأَةُ مَعَهَا صَبِيُّهَا، وَمَعَهَا كَبْشَانِ تَسُوقُهُمَا، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ اقْبَلْ مِنِّي هَدِيَّتِي، فَوَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ مَا عَادَ إِلَيْهِ بَعْدُ، فَقَالَ: "خُذُوا مِنْهَا وَاحِدًا وَرُدُّوا عَلَيْهَا الْآخَرَ"، قَالَ: ثُمَّ سِرْنَا وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَيْنَنَا كَأَنَّمَا عَلَيْنَا الطَّيْرُ تُظِلُّنَا، فَإِذَا جَمَلٌ نَادٌّ حَتَّى إِذَا كَانَ بَيْنَ سِمَاطَيْنِ خَرَّ سَاجِدًا، فَجَلَسَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَالَ عَلَيَّ النَّاسَ: "مَنْ صَاحِبُ الْجَمَلِ؟" فَإِذَا فِتْيَةٌ مِنْ الْأَنْصَارِ، قَالُوا: هُوَ لَنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: "فَمَا شَأْنُهُ"؟، قَالُوا: اسْتَنَيْنَا عَلَيْهِ مُنْذُ عِشْرِينَ سَنَةً وَكَانَتْ بِهِ شُحَيْمَةٌ فَأَرَدْنَا أَنْ نَنْحَرَهُ فَنَقْسِمَهُ بَيْنَ غِلْمَانِنَا، فَانْفَلَتَ مِنَّا، قَالَ: "بِيعُونِيهِ"، قَالُوا: لَا، بَلْ هُوَ لَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: "أَمَّا لا، فَأَحْسِنُوا إِلَيْهِ حَتَّى يَأْتِيَهُ أَجَلُهُ"، قَالَ الْمُسْلِمُونَ عِنْدَ ذَلِكَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَحْنُ أَحَقُّ بِالسُّجُودِ لَكَ مِنْ الْبَهَائِمِ، قَالَ: "لَا يَنْبَغِي لِشَيْءٍ أَنْ يَسْجُدَ لِشَيْءٍ وَلَوْ كَانَ ذَلِكَ، كَانَ النِّسَاءُ لِأَزْوَاجِهِنَّ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Ismaa'iyl bin 'Abdil-Malik, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Nilitoka pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika safari; na alikuwa haendi kujisaidia mpaka ajifiche asionekane. Tukashuka katika jangwa lisilokuwa na mti wala alama yoyote. Akasema: "Yaa Jaabir, tia maji katika chombo chako, kisha twende." Akasema: Tukaenda mpaka tusionekane. Ghafla akakuta miti miwili ambayo baina yake kuna dhiraa nne. Akasema: "Yaa Jaabir, nenda kwa mti huu, useme: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anakuambia: Ungana na mwenzako, ili nikae nyuma yenu (miwili)." Akasema: Nikafanya (hivyo); ukarudi kwa (mwenzake). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akakaa nyuma ya miti hiyo miwili, kisha ikarudi mahali pao. Tukapanda (vipando vyetu) pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na Rasuli wa Allaah akiwa baina yetu, kama kwamba ndege wako juu yetu wakitufunika kivuli. Mwanamke mmoja akamjia akiwa na mtoto wake mchanga, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika huyu mwanangu shaytwaan humshika kila siku mara tatu. Akasema: Akamchukua yule mtoto akamweka kati yake na mbele ya tandiko, kisha akasema: "Hizika, adui wa Allaah! Mimi ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Hizika, adui wa Allaah! Mimi ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)" — mara tatu. Kisha akamrudishia (mtoto). Tulipomaliza safari yetu, tulipita mahali pale; yule mwanamke akatujia pamoja na mtoto wake, na pamoja naye kondoo dume wawili akiwaswaga. Akasema: Yaa Rasula-Allaah, pokea kwangu zawadi yangu; naapa kwa Ambaye Amekutuma kwa haki, (shaytwaan) hakumrudia baada ya hapo. Akasema: "Chukueni kwake mmoja, na mrudishieni mwingine." Akasema: Kisha tukaenda, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa baina yetu, kama kwamba ndege wako juu yetu wakitufunika kivuli. Ghafla (tukamkuta) ngamia aliyekimbia (akajitenga); alipokuwa kati ya safu mbili (za watu), akaanguka akisujudu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akakaa, na akasema: "Niletee watu! Ni nani mwenye ngamia huyu?" Ghafla wakawa ni vijana wa Answaar (رضي الله عنهم); wakasema: Ni wetu, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Ana nini?" Wakasema: Tumekuwa tukimtumia kutekea maji tangu miaka ishirini, na alikuwa na mafuta kidogo, tukataka kumchinja tumgawe kwa vijana wetu; akatukimbia. Akasema: "Niuzieni." Wakasema: Hapana, bali ni wako, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Ama ikiwa (hamtaki) hivyo, basi mfanyieni wema mpaka ajali yake imfikie." Waislamu (رضي الله عنهم) wakasema wakati huo: Yaa Rasula-Allaah, sisi tunastahiki zaidi kukusujudia kuliko wanyama. Akasema: "Haifai kwa kitu chochote kumsujudia kitu (kingine); na lau hilo lingekuwa (linafaa), wanawake wangewasujudia waume zao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
167
Hadiyth
17

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَجْلَحُ، عَنْ الذَّيَّالِ بْنِ حَرْمَلَةَ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: أَقْبَلْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى دُفِعْنَا إِلَى حَائِطٍ فِي بَنِي النَّجَّارِ، فَإِذَا فِيهِ جَمَلٌ لَا يَدْخُلُ الْحَائِطَ أَحَدٌ إِلَّا شَدَّ عَلَيْهِ، فَذَكَرُوا ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَاهُ، فَدَعَاهُ فَجَاءَ وَاضِعًا مِشْفَرَهُ عَلَى الْأَرْضِ حَتَّى بَرَكَ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَقَالَ: "هَاتُوا خِطَامًا"، فَخَطَمَهُ وَدَفَعَهُ إِلَى صَاحِبِهِ، ثُمَّ الْتَفَتَ، فَقَالَ: "مَا بَيْنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ أَحَدٌ إِلَّا يَعْلَمُ أَنِّي رَسُولُ اللَّهِ، إِلَّا عَاصِيَ الْجِنِّ وَالْإِنْسِ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Al-Ajlah, kutoka kwa Adh-Dhayyaal bin Harmalah, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Tulikuja pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka tukafika kwenye bustani (iliyozungushiwa ukuta) ya Banuw An-Najjaar. Ghafla ndani yake kuna ngamia; hakuna mtu anayeingia bustanini ila humshambulia. Wakamtajia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hilo. Akamwendea, akamwita; akaja ameweka mdomo wake ardhini mpaka akapiga magoti mbele yake. Akasema: "Leteni hatamu." Akamfunga hatamu, na akampa mwenyewe. Kisha akageuka akasema: "Hakuna yeyote aliye baina ya mbingu na ardhi ila anajua kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa waasi miongoni mwa majini na wanaadam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
169
Hadiyth
18

أَخْبَرَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ فَرْقَدٍ السَّبَخِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، إِنَّ امْرَأَةً جَاءَتْ بِابْنٍ لَهَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ ابْنِي بِهِ جُنُونٌ، وَإِنَّهُ يَأْخُذُهُ عِنْدَ غَدَائِنَا وَعَشَائِنَا فَيُخَبَّثُ عَلَيْنَا، "فَمَسَحَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَدْرَهُ، وَدَعَا فَثَعَّ ثَعَّةً، وَخَرَجَ مِنْ جَوْفِهِ مِثْلُ الْجِرْوِ الْأَسْوَدِ، فَسَعَى"

Ametukhabarisha Al-Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Farqad As-Sabakhiy, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba mwanamke mmoja alikuja na mwanawe kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mwanangu ana wazimu, na (wazimu huo) humshika wakati wa chakula chetu cha mchana na cha jioni, akatuharibia (chakula chetu). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akampangusa kifua chake na akaomba Du'aa; (mtoto) akatapika mara moja, na kikatoka tumboni mwake (kitu) mfano wa mtoto wa mbwa mweusi, kikaenda mbio.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
169
Hadiyth
19

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ الْعَبْدِيُّ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ طَهْمَانَ، عَنْ سِمَاكٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنِّي لَأَعْرِفُ حَجَرًا بِمَكَّةَ كَانَ يُسَلِّمُ عَلَيَّ قَبْلَ أَنْ أُبْعَثَ إِنِّي لَأَعْرِفُهُ الْآنَ"

Ametusimulia Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari Yahyaa bin Abiy Bukayr Al-'Abdiy, kutoka kwa Ibraahiym bin Twahmaan, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mimi nalijua jiwe moja huko Makkah ambalo lilikuwa likinisalimia kabla sijatumwa; hakika mimi nalijua hivi sasa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
169
Hadiyth
20

حَدَّثَنَا فَرْوَةُ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ أَبِي ثَوْرٍ الْهَمْدَانِيُّ، عَنْ إِسْمَاعِيل السُّدِّيِّ، عَنْ عَبَّادٍ أَبِي يَزِيدَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ، قَالَ: "كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَكَّةَ فَخَرَجْنَا مَعَهُ فِي بَعْضِ نَوَاحِيهَا، فَمَرَرْنَا بَيْنَ الْجِبَالِ وَالشَّجَرِ، فَلَمْ نَمُرَّ بِشَجَرَةٍ وَلَا جَبَلٍ إِلَّا قَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ"

Ametusimulia Farwah, ametusimulia Al-Waliyd bin Abiy Thawr Al-Hamdaaniy, kutoka kwa Ismaa'iyl As-Suddiy, kutoka kwa 'Abbaad Abuw Yaziyd, kutoka kwa 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضوان الله عليه), amesema: "Tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) huko Makkah; tukatoka pamoja naye kwenda katika baadhi ya viunga vyake. Tukapita kati ya milima na miti; hatukupita kwa mti wala mlima ila ulisema: Amani iwe juu yako, yaa Rasula-Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
169
Hadiyth
21

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ شِمْرِ بْنِ عَطِيَّةَ، عَنْ رَجُلٍ مِنْ مُزَيْنَةَ، أَوْ جُهَيْنَةَ، قَالَ: صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْفَجْرَ فَإِذَا هُوَ بِقَرِيبٍ مِنْ مِئَةِ ذِئْبٍ قَدْ أَقْعَيْنَ وُفُودُ الذِّئَابِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تَرْضَخُونَ لَهُمْ شَيْئًا مِنْ طَعَامِكُمْ وَتَأْمَنُونَ عَلَى مَا سِوَى ذَلِكَ؟"، فَشَكَوْا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْحَاجَةَ، قَالَ: "فَآذِنُوهُنَّ"، قَالَ: فَآذَنُوهُنَّ فَخَرَجْنَ وَلَهُنَّ عُوَاءٌ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Shimr bin 'Atwiyyah, kutoka kwa mtu mmoja wa (kabila la) Muzaynah au Juhaynah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Alfajiri; ghafla (akakuta) karibu mbwa mwitu mia moja wamekaa kwa matako yao — ujumbe wa mbwa mwitu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia (watu): "Je, mtawapa kitu kidogo katika chakula chenu, na mkawa salama juu ya (mali yenu) isiyokuwa hiyo?" Wakamshtakia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) uhitaji (wao). Akasema: "Basi waarifuni (wajue kwamba hawana kitu)." Akasema: Wakawaarifu; wakatoka (mbwa mwitu) huku wakilia kwa sauti ndefu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
171
Hadiyth
22

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: جَاءَ جِبْرِيلُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ جَالِسٌ حَزِينٌ، وَقَدْ تَخَضَّبَ بِالدَّمِ مِنْ فِعْلِ أَهْلِ مَكَّةَ مِنْ قُرَيْشٍ، فَقَالَ جِبْرِيلُ عَلَيْهِ السَّلامُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلْ تُحِبُّ أَنْ أُرِيَكَ آيَةً؟، قَالَ: "نَعَمْ، فَنَظَرَ إِلَى شَجَرَةٍ مِنْ وَرَائِهِ"، فَقَالَ: ادْعُ بِهَا، فَدَعَا بِهَا، فَجَاءَتْ وَقَامَتْ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَقَالَ: مُرْهَا فَلْتَرْجِعْ، فَأَمَرَهَا فَرَجَعَتْ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "حَسْبِي حَسْبِي"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia Abuw Mu'aawiyah, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Jibriyl (عليه السلام) alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akiwa amekaa, ana huzuni, na ametapakaa damu kutokana na kitendo cha watu wa Makkah miongoni mwa Quraysh. Jibriyl (عليه السلام) akasema: Yaa Rasula-Allaah, je, unapenda nikuonyeshe ishara (muujiza)? Akasema: "Ndiyo." [Jibriyl (عليه السلام)] akatazama mti ulio nyuma yake, akasema: Uite. Akauita; ukaja ukasimama mbele yake. Akasema: Uamrishe urudi. Akauamrisha, ukarudi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yanitosha, yanitosha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
172
Hadiyth
23

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، وَأَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي ظَبْيَانَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: أَتَى رَجُلٌ مِنْ بَنِي عَامِرٍ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَلَا أُرِيكَ آيَةً؟"، قَالَ: بَلَى، قَالَ: "فَاذْهَبْ فَادْعُ تِلْكَ النَّخْلَةَ"، فَدَعَاهَا فَجَاءَتْ تَنْقُزُ بَيْنَ يَدَيْهِ، قَالَ: قُلْ لَهَا تَرْجِعْ، قَالَ لَهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ارْجِعِي"، فَرَجَعَتْ حَتَّى عَادَتْ إِلَى مَكَانِهَا، فَقَالَ: يَا بَنِي عَامِرٍ، مَا رَأَيْتُ رَجُلًا كَالْيَوْمِ أَسْحَرَ مِنْهُ!

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia Jariyr na Abuw Mu'aawiyah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Dhwabyaan, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Mtu mmoja wa Banuw 'Aamir alimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, nisikuonyeshe ishara (muujiza)?" Akasema: Bila shaka. Akasema: "Basi nenda ukauite mtende ule." Akauita; ukaja ukiruka-ruka mbele yake. (Yule mtu) akasema: Uambie urudi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauambia: "Rudi." Ukarudi mpaka ukarejea mahali pake. (Yule mtu) akasema: Yaa Baniy 'Aamir! Sijapata kuona kama leo mtu aliye mchawi zaidi kuliko yeye!

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
172
Hadiyth
24

5-Mlangoباب ما أكرم الله النبي صلى الله عليه وسلم من تفجير الماء من بين أصابعهMlango Wa Yale Ambayo Allaah
Amemkirimu Kwayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ya Kububujisha
Maji Kutoka Baina Ya Vidole Vyake

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا شُعَيْبُ بْنُ صَفْوَانَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ أَبِي الضُّحَى، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: دَعَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلَالًا، فَطَلَبَ بِلَالٌ الْمَاءَ ثُمَّ جَاءَ، فَقَالَ: لَا وَاللَّهِ مَا وَجَدْتُ الْمَاءَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَهَلْ مِنْ شَنٍّ؟" فَأَتَاهُ بِشَنٍّ، فَبَسَطَ كَفَّيْهِ فِيهِ فَانْبَعَثَتْ تَحْتَ يَدَيْهِ عَيْنٌ، قَالَ: فَكَانَ ابْنُ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ يَشْرَبُ، وَغَيْرُهُ يَتَوَضَّأُ

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Ibraahiym, ametusimulia Shu'ayb bin Swafwaan, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Abudh-Dhwuhaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwita Bilaal (رضي الله عنه). Bilaal (رضي الله عنه) akatafuta maji, kisha akaja, akasema: Hapana, Wa-Allaahi, sikupata maji. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Basi je, kuna kiriba kikuukuu?" Akamletea kiriba kikuukuu; akakunjua viganja vyake ndani yake, ikabubujika chemchemi chini ya mikono yake. Akasema: Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) akawa anakunywa, na wengine wakitawadha.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
173
Hadiyth
25

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانَ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ الْأَسْوَدِ بْنِ قَيْسٍ، عَنْ نُبَيْحٍ الْعَنَزِيِّ، قَالَ: قَالَ جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: غَزَوْنَا أَوْ سَافَرْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ يَوْمَئِذٍ بِضْعَةَ عَشَرَ وَمِائَتَانِ فَحَضَرَتْ الصَّلَاةُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هَلْ فِي الْقَوْمِ مِنْ طَهُورٍ؟"، فَجَاءَ رَجُلٌ يَسْعَى، بِإِدَاوَةٍ فِيهَا شَيْءٌ مِنْ مَاءٍ، لَيْسَ فِي الْقَوْمِ مَاءٌ غَيْرُهُ، "فَصَبَّهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي قَدَحٍ، ثُمَّ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ، ثُمَّ انْصَرَفَ وَتَرَكَ الْقَدَحَ"، فَرَكِبَ النَّاسُ ذَلِكَ الْقَدَحَ، وَقَالُوا: تَمَسَّحُوا تَمَسَّحُوا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَلَى رِسْلِكُمْ" حِينَ سَمِعَهُمْ يَقُولُونَ ذَلِكَ، "فَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَفَّهُ فِي الْمَاءِ وَالْقَدَحِ"، وَقَالَ: "بِسْمِ اللَّهِ"، ثُمَّ قَالَ: "أَسْبِغُوا الطُّهُورَ"، فَوَالَّذِي هُوَ ابْتَلَانِي بِبَصَرِي لَقَدْ رَأَيْتُ الْعُيُونَ، عُيُونَ الْمَاءِ تَخْرُجُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِهِ فَلَمْ يَرْفَعْهَا حَتَّى تَوَضَّئُوا أَجْمَعُونَ

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-Aswad bin Qays, kutoka kwa Nubayh Al-'Anaziy, amesema: Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) amesema: Tulipigana vita — au: tulisafiri — pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nasi siku hiyo tulikuwa mia mbili na kumi na kitu (kati ya kumi na tatu na kumi na tisa). Wakati wa Swalaah ukafika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, kuna (maji ya) twahara katika watu?" Mtu mmoja akaja mbio na chombo kidogo cha ngozi (cha maji) chenye maji kidogo ndani yake; hapakuwa katika watu maji mengine isipokuwa hayo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akayamimina katika bakuli, kisha akatawadha akaufanya Wudhuu wake vizuri, kisha akaondoka na akaliacha bakuli. Watu wakalivamia bakuli hilo, na wakasema: Jipanguseni (kwa maji yake), jipanguseni! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Tulieni (kwa utaratibu wenu)!" — aliposikia wakisema hivyo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka kiganja chake ndani ya maji na bakuli, na akasema:

بِسْمِ اللَّهِ

Kwa Jina la Allaah.

Kisha akasema: "Kamilisheni twahara." Basi naapa kwa Ambaye Yeye Ndiye Aliyenitia mtihani katika macho yangu, hakika niliona chemchemi — chemchemi za maji — zikitoka kati ya vidole vyake; na hakukiinua (kiganja chake) mpaka wakatawadha wote.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
174
Hadiyth
26

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، وَسَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، قَالَا: حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، وَحُصَيْنٍ، سَمِعَا سَالِمَ بْنَ أَبِي الْجَعْدِ، يَقُولُ: سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: أَصَابَنَا عَطَشٌ فَجَهَشْنَا، فَانْتَهَيْنَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، "فَوَضَعَ يَدَهُ فِي تَوْرٍ، فَجَعَلَ يَفُورُ كَأَنَّهُ عُيُونٌ، مِنْ خَلَلِ أَصَابِعِهِ"، وَقَالَ: "اذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ"، فَشَرِبْنَا حَتَّى وَسِعَنَا وَكَفَانَا، وَفِي حَدِيثِ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ: فَقُلْنَا لِجَابِرٍ: كَمْ كُنْتُمْ؟، قَالَ: كُنَّا أَلْفًا وَخَمْسَ مِئَةٍ وَلَوْ كُنَّا مِئَةَ أَلْفٍ لَكَفَانَا

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy na Sa'iyd bin Ar-Rabiy', wamesema: Ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah na Huswayn, wote wawili walimsikia Saalim bin Abil-Ja'd akisema: Nilimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Tulipatwa na kiu, tukafadhaika (tukakaribia kulia), tukafika kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akaweka mkono wake ndani ya chombo (kidogo cha maji); (maji) yakaanza kufoka kama kwamba ni chemchemi kutoka kati ya mapengo ya vidole vyake, na akasema: "Litajeni Jina la Allaah." Tukanywa mpaka yakatutosha na yakatukifu. Na katika Hadiyth ya 'Amr bin Murrah: Tukamwambia Jaabir (رضي الله عنه): Mlikuwa wangapi? Akasema: Tulikuwa elfu moja na mia tano; na lau tungekuwa elfu mia moja, yangetutosha.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
175
Hadiyth
27

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، حَدَّثَنَا الْجَعْدُ أَبُو عُثْمَانَ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، حَدَّثَنَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: شَكَا أَصْحَابُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْعَطَشَ، "فَدَعَا بِعُسٍّ، فَصُبَّ فِيهِ مَاءٌ، وَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ فِيهِ"، قَالَ: فَجَعَلْتُ أَنْظُرُ إِلَى الْمَاءِ يَنْبُعُ عُيُونًا مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَالنَّاسُ يَسْتَقُونَ حَتَّى اسْتَقَى النَّاسُ كُلُّهُمْ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Ja'far bin Sulaymaan, ametusimulia Al-Ja'd Abuw 'Uthmaan, ametusimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه), ametusimulia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walimshtakia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kiu. Akaagiza bakuli kubwa, likamiminiwa maji ndani yake, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake ndani yake. Akasema: Nikawa natazama maji yakibubujika kama chemchemi kutoka kati ya vidole vya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na watu wakichota maji mpaka watu wote wakachota.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
175
Hadiyth
28

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: سَمِعَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ بِخَسْفٍ، فَقَالَ: كُنَّا أَصْحَابَ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَعُدُّ الْآيَاتِ بَرَكَةً، وَأَنْتُمْ تَعُدُّونَهَا تَخْوِيفًا، إِنَّا بَيْنَمَا نَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْسَ مَعَنَا مَاءٌ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اطْلُبُوا مَنْ مَعَهُ فَضْلُ مَاءٍ"، "فَأُتِيَ بِمَاءٍ، فَصَبَّهُ فِي الْإِنَاءِ، ثُمَّ وَضَعَ كَفَّهُ فِيهِ، فَجَعَلَ الْمَاءُ يَخْرُجُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِهِ"، ثُمَّ قَالَ: "حَيَّ عَلَى الطَّهُورِ الْمُبَارَكِ، وَالْبَرَكَةُ مِنْ اللَّهِ تَعَالَى"، فَشَرِبْنَا، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: كُنَّا نَسْمَعُ تَسْبِيحَ الطَّعَامِ وَهُوَ يُؤْكَلُ

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) alisikia (khabari ya) kupatwa (kwa jua au mwezi), akasema: Sisi Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) tulikuwa tukizihesabu ishara (miujiza) kuwa ni baraka, nanyi mnazihesabu kuwa ni vitisho. Hakika sisi, wakati tulipokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), hatukuwa na maji. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Tafuteni mwenye maji ya ziada." Akaletewa maji, akayamimina katika chombo, kisha akaweka kiganja chake ndani yake; maji yakaanza kutoka kati ya vidole vyake. Kisha akasema: "Njooni kwenye twahara iliyobarikiwa, na baraka ni kutoka kwa Allaah (تعالى)." Tukanywa. 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) amesema: Tulikuwa tukisikia Tasbiyh (kumtakasa Allaah) ya chakula nacho kikiliwa.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
175
Hadiyth
29

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نُمَيْرٍ، حَدَّثَنَا أَبُو الْجَوَّابِ، عَنْ عَمَّارِ بْنِ رُزَيْقٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: زُلْزِلَتْ الْأَرْضُ عَلَى عَهْدِ عَبْدِ اللَّهِ، فَأُخْبِرَ بِذَلِكَ، فَقَالَ: إِنَّا كُنَّا أَصْحَابَ مُحَمَّدٍ صلى الله عليه وسلم نَرَى الْآيَاتِ بَرَكَاتٍ، وَأَنْتُمْ تَرَوْنَهَا تَخْوِيفًا، بَيْنَا نَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ إِذْ حَضَرَتْ الصَّلَاةُ وَلَيْسَ مَعَنَا مَاءٌ إِلَّا يَسِيرٌ، "فَدَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَاءٍ فِي صَحْفَةٍ، وَوَضَعَ كَفَّهُ فِيهِ، فَجَعَلَ الْمَاءُ يَنْبَجِسُ مِنْ بَيْنِ أَصَابِعِهِ"، ثُمَّ نَادَى: "حَيَّ عَلَى أَهْلِ الْوَضُوءِ، وَالْبَرَكَةُ مِنْ اللَّهِ"، قالَ: فَأَقْبَلَ النَّاسُ فَتَوَضَّئُوا، وَجَعَلْتُ لَا هَمَّ لِي إِلَّا مَا أُدْخِلُهُ بَطْنِي لِقَوْلِهِ: "وَالْبَرَكَةُ مِنْ اللَّهِ"، فَحَدَّثْتُ بِهِ سَالِمَ بْنَ أَبِي الْجَعْدِ، فَقَالَ: كَانُوا خَمْسَ عَشْرَةَ مِئَةٍ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah bin Numayr, ametusimulia Abul-Jawwaab, kutoka kwa 'Ammaar bin Ruzayq, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Ardhi ilitetemeka katika zama za 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه), akakhabarishwa hilo. Akasema: "Hakika sisi Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) tulikuwa tukiziona ishara (miujiza) kuwa ni baraka, nanyi mnaziona kuwa ni vitisho." Wakati tulipokuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini, Swalaah ilifika, na hatukuwa na maji isipokuwa kidogo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaagiza maji katika sahani kubwa, na akaweka kiganja chake ndani yake; maji yakaanza kububujika kutoka kati ya vidole vyake. Kisha akaita: "Njooni kwa watu wa Wudhuu, na baraka ni kutoka kwa Allaah." Akasema: Watu wakaja wakatawadha; nami nikawa sina hamu isipokuwa (maji) ninayoyaingiza tumboni mwangu, kwa sababu ya kauli yake: "Na baraka ni kutoka kwa Allaah." Nikamsimulia hayo Saalim bin Abil-Ja'd, akasema: Walikuwa mia kumi na tano.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
175
Hadiyth
30

6-Mlangoباب ما أكرم النبي صلى الله عليه وسلم من حنين المنبرMlango Wa Yale Aliyokirimiwa
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Ya Kilio Cha Shauku Cha Mimbari
[Ya Shina La Mtende]

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا مُعَاذُ بْنُ الْعَلَاءِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "يَخْطُبُ إِلَى جِذْعٍ، فَلَمَّا اتَّخَذَ الْمِنْبَرَ حَنَّ الْجِذْعُ حَتَّى أَتَاهُ، فَمَسَحَهُ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Mu'aadh bin Al-'Alaa, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikhutubu akiegemea shina la mtende. Alipoichukua mimbari, shina likalia kwa shauku mpaka akalijia, akalipangusa.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
177
Hadiyth
31

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا تَمِيمُ بْنُ عَبْدِ الْمُؤْمِنِ، حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ حَيَّانَ، حَدَّثَنِي ابْنُ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا خَطَبَ قَامَ فَأَطَالَ الْقِيامَ، فَكَانَ يَشُقُّ عَلَيْهِ قِيَامُهُ، فَأُتِيَ بِجِذْعِ نَخْلَةٍ فَحُفِرَ لَهُ وَأُقِيمَ إِلَى جَنْبِهِ قَائِمًا لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا خَطَبَ فَطَالَ الْقِيَامُ عَلَيْهِ، اسْتَنَدَ إِلَيْهِ فَاتَّكَأَ عَلَيْهِ فَبَصُرَ بِهِ رَجُلٌ كَانَ وَرَدَ الْمَدِينَةَ، فَرَآهُ قَائِمًا إِلَى جَنْبِ ذَلِكَ الْجِذْعِ، فَقَالَ: لِمَنْ يَلِيهِ مِنْ النَّاسِ: لَوْ أَعْلَمُ أَنَّ مُحَمَّدًا يَحْمَدُنِي فِي شَيْءٍ يَرْفُقُ بِهِ، لَصَنَعْتُ لَهُ مَجْلِسًا يَقُومُ عَلَيْهِ، فَإِنْ شَاءَ، جَلَسَ مَا شَاءَ، وَإِنْ شَاءَ، قَامَ، فَبَلَغَ ذَلِكَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "ائْتُونِي بِهِ"، فَأَتَوْهُ بِهِ، فَأُمِرَهُ أَنْ يَصْنَعَ لَهُ هَذِهِ الْمَرَاقِيَ الثَّلَاثَ، أَوْ الْأَرْبَعَ هِيَ الْآنَ فِي مِنْبَرِ الْمَدِينَةِ، فَوَجَدَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي ذَلِكَ رَاحَةً، فَلَمَّا فَارَقَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْجِذْعَ وَعَمَدَ إِلَى هَذِهِ الَّتِي صُنِعَتْ لَهُ، جَزِعَ الْجِذْعُ فَحَنَّ كَمَا تَحِنُّ النَّاقَةُ حِينَ فَارَقَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَزَعَمَ ابْنُ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ سَمِعَ حَنِينَ الْجِذْعِ، رَجَعَ إِلَيْهِ فَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهِ وَقَالَ: "اخْتَرْ أَنْ أَغْرِسَكَ فِي الْمَكَانِ الَّذِي كُنْتَ فِيهِ، فَتَكُونَ كَمَا كُنْتَ، وَإِنْ شِئْتَ أَنْ أَغْرِسَكَ فِي الْجَنَّةِ فَتَشْرَبَ مِنْ أَنْهَارِهَا وَعُيُونِهَا فَيَحْسُنُ نَبْتُكَ، وَتُثْمِرُ فَيَأْكُلَ أَوْلِيَاءُ اللَّهِ مِنْ ثَمَرَتِكَ وَنَخْلِكَ فَعَلْتُ" فَزَعَمَ أَنَّهُ سَمِعَ مِنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَقُولُ لَهُ: "نَعَمْ قَدْ فَعَلْتُ مَرَّتَيْنِ"، فَسُأَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "اخْتَارَ أَنْ أَغْرِسَهُ فِي الْجَنَّةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Tamiym bin 'Abdil-Muumin, ametusimulia Swaalih bin Hayyaan, amenisimulia Ibn Buraydah, kutoka kwa baba yake [Buraydah (رضي الله عنه)], amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapokhutubu husimama, akarefusha kusimama, na kusimama kwake kukawa kunamtaabisha. Akaletewa shina la mtende, likachimbiwa (shimo), na likasimamishwa kando yake likiwa limesimama kwa ajili ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawa anapokhutubu na kusimama kukamrefukia, huliegemea, akajiegemeza juu yake. Mtu mmoja aliyekuwa amefika Madiynah akamwona, akamwona amesimama kando ya shina hilo. Akawaambia watu waliokuwa karibu naye: Lau ningejua kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) angenishukuru kwa kitu kinachomrahisishia, ningemtengenezea kiti cha kusimama juu yake; akitaka, angekaa kadiri atakavyo, na akitaka, angesimama. Hilo likamfikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Nileteeni." Wakamleta kwake; akamwamrisha amtengenezee vidaraja hivi vitatu — au vinne — ambavyo sasa viko katika mimbari ya Madiynah. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akapata faraja katika hilo. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoliacha shina na akaiendea hii aliyotengenezewa, shina likahuzunika, likalia kwa shauku kama ngamia jike anavyolia kwa shauku, wakati Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoliacha. Ibn Buraydah akadai kutoka kwa baba yake [Buraydah (رضي الله عنه)] kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposikia kilio cha shauku cha shina, alirudi kwake, akaweka mkono wake juu yake, na akasema: "Chagua: nikupande mahali ulipokuwa, uwe kama ulivyokuwa; na ukitaka nikupande Jannah (Pepo), unywe kutoka katika mito yake na chemchemi zake, uote vizuri, na uzae matunda, wale vipenzi vya Allaah kutoka katika matunda yako na mitende yako, nitafanya." [Buraydah (رضي الله عنه)] akadai kwamba alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiliambia: "Ndiyo, nimefanya" — mara mbili. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaulizwa (kuhusu hilo), akasema: "Limechagua nilipande Jannah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
177
Hadiyth
32

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ كَثِيرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَقُومُ إِلَى جِذْعٍ قَبْلَ أَنْ يُجْعَلَ الْمِنْبَرُ، فَلَمَّا جُعِلَ الْمِنْبَرُ حَنَّ ذَلِكَ الْجِذْعُ حَتَّى سَمِعْنَا حَنِينَهُ، فَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ عَلَيْهِ فَسَكَنَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Sulaymaan bin Kathiyr, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah Al-Answaariy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisimama akiegemea shina la mtende kabla ya kuwekwa mimbari. Mimbari ilipowekwa, shina hilo likalia kwa shauku mpaka tukasikia kilio chake; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake juu yake, likatulia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
178
Hadiyth
33

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ حَفْصِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ إِلَى خَشَبَةٍ، فَلَمَّا صُنِعَ الْمِنْبَرُ فَجَلَسَ عَلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، حَنَّتْ حَنِينَ الْعِشَارِ حَتَّى وَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ عَلَيْهَا فَسَكَنَتْ"

Ametusimulia Muhammad bin Kathiyr, ametusimulia Sulaymaan bin Kathiyr, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Hafsw bin 'Ubaydi-Allaah, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikhutubu akiegemea gogo. Mimbari ilipotengenezwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaketi juu yake, (gogo hilo) lililia kwa shauku kama kilio cha ngamia wenye mimba (iliyotimiza miezi kumi), mpaka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake juu yake, likatulia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
178
Hadiyth
34

أَخْبَرَنَا فَرْوَةُ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ زَكَرِيَّا، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي كَرِبٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "حَنَّتْ الْخَشَبَةُ حَنِينَ النَّاقَةِ الْخَلُوجِ"

Ametukhabarisha Farwah, ametusimulia Yahyaa bin Zakariyyaa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Karib, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), amesema: "Gogo lililia kwa shauku kama kilio cha ngamia jike aliyetenganishwa na mtoto wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
178
Hadiyth
35

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَقِيلٍ، عَنْ الطُّفَيْلِ بْنِ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: يُصَلِّي إِلَى جِذْعٍ وَيَخْطُبُ إِلَيْهِ إِذْ كَانَ الْمَسْجِدُ عَرِيشًا، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِهِ: أَلَا نَجْعَلُ لَكَ عَرِيشًا تَقُومُ عَلَيْهِ يَرَاكَ النَّاسُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، وَتُسْمِعُ مِنْ خُطْبَتِكَ؟، قَالَ: "نَعَمْ"، فَصُنِعَ لَهُ الثَّلَاثَ دَرَجَاتٍ، هُنَّ اللَّوَاتِي عَلَى الْمِنْبَرِ، فَلَمَّا صُنِعَ الْمِنْبَرُ وَوُضِعَ فِي مَوْضِعِهِ الَّذِي وَضَعَهُ فِيهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَلَمَّا جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُرِيدُ الْمِنْبَرَ مَرَّ عَلَيْهِ، فَلَمَّا جَاوَزَهُ، خَارَ الْجِذْعُ حَتَّى تَصَدَّعَ وَانْشَقَّ، فَرَجَعَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَسَحَهُ بِيَدِهِ حَتَّى سَكَنَ، ثُمَّ رَجَعَ إِلَى الْمِنْبَرِ، قَالَ: فَكَانَ إِذَا صَلَّى، صَلَّى إِلَيْهِ فَلَمَّا هُدِمَ الْمَسْجِدُ أَخَذَ ذَلِكَ الْجِذْعَ أُبَيُّ بْنُ كَعْبٍ فَلَمْ يَزَلْ عِنْدَهُ حَتَّى بَلِيَ فَأَكَلَتْهُ الْأَرَضَةُ وَعَادَ رُفَاتًا

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Muhammad bin 'Aqiyl, kutoka kwa Atw-Twufayl bin Ubayy bin Ka'b, kutoka kwa baba yake [Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiswali akielekea shina la mtende, na akikhutubu akiliegemea, wakati Msikiti ulipokuwa kibanda (cha makuti). Mtu mmoja miongoni mwa Swahaba zake (رضي الله عنهم) akamwambia: Je, tusikutengenezee kibanda (jukwaa) cha kusimama juu yake, watu wakuone siku ya Ijumaa, na uwasikilizishe khutbah (hotuba) yako? Akasema: "Ndiyo." Akatengenezewa vile vidaraja vitatu, ambavyo ndivyo vilivyoko kwenye mimbari. Mimbari ilipotengenezwa na ikawekwa mahali pake ambapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliiweka, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuja akiikusudia mimbari, alilipita (shina hilo); alipolivuka, shina likatoa mlio mpaka likapasuka na likachanika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akarudi kwake, akalipangusa kwa mkono wake mpaka likatulia, kisha akarudi kwenye mimbari. Akasema: Akawa anaposwali, huswali akilielekea. Msikiti ulipobomolewa, Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه) alilichukua shina hilo; likaendelea kuwa kwake mpaka likachakaa, mchwa wakalila, na likawa vipande vilivyosagika.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
180
Hadiyth
36

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ مُجَالِدٍ، عَنْ أَبِي الْوَدَّاكِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَخْطُبُ إِلَى لِزْقِ جِذْعٍ فَأَتَاهُ رَجُلٌ رُومِيٌّ، فَقَالَ: أَصْنَعُ لَكَ مِنْبَرًا تَخْطُبُ عَلَيْهِ، فَصَنَعَ لَهُ مِنْبَرًا هَذَا الَّذِي تَرَوْنَ، قَالَ: فَلَمَّا قَامَ عَلَيْهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ، حَنَّ الْجِذْعُ حَنِينَ النَّاقَةِ إِلَى وَلَدِهَا، فَنَزَلَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَضَمَّهُ إِلَيْهِ فَسَكَنَ، فَأَمَرَ بِهِ أَنْ يُحْفَرَ لَهُ وَيُدْفَنَ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Mujaalid, kutoka kwa Abul-Waddaak, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikhutubu kando ya shina la mtende. Mtu mmoja Mrumi akamjia, akasema: Nikutengenezee mimbari ukikhutubu juu yake? Akamtengenezea mimbari — hii mnayoiona. Akasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliposimama juu yake akikhutubu, shina likalia kwa shauku kama kilio cha ngamia jike kwa mtoto wake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akashuka kulijia, akalikumbatia, likatulia. Akaamrisha kuhusu (shina) hilo lichimbiwe (shimo) na lizikwe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
181
Hadiyth
37

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا الصَّعْقُ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ، يَقُولُ: لَمَّا أَنْ قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ جَعَلَ "يُسْنِدُ ظَهْرَهُ إِلَى خَشَبَةٍ وَيُحَدِّثُ النَّاسَ"، فَكَثُرُوا حَوْلَهُ، فَأَرَادَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُسْمِعَهُمْ، فَقَالَ: "ابْنُوا لِي شَيْئًا أَرْتَفِعُ عَلَيْهِ"، قَالُوا: كَيْفَ يَا نَبِيَّ اللَّهِ؟، قَالَ: "عَرِيشٌ كَعَرِيشِ مُوسَى"، فَلَمَّا أَنْ بَنَوْا لَهُ، قَالَ الْحَسَنُ: حَنَّتْ وَاللَّهِ الْخَشَبَةُ، قَالَ الْحَسَنُ: سُبْحَانَ اللَّهِ! هَلْ تُبْتَغَى قُلُوبُ قَوْمٍ سَمِعُوا؟ قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: يَعْنِي هَذَا

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Asw-Swa'q, amesema: Nilimsikia Al-Hasan akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofika Madiynah, alikuwa akiegemeza mgongo wake kwenye gogo na kuzungumza na watu. Wakawa wengi kumzunguka, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akataka kuwasikilizisha. Akasema: "Nijengeeni kitu nipande juu yake." Wakasema: Vipi, yaa Nabiyya-Allaah? Akasema: "Kibanda kama kibanda cha Muwsaa (عليه السلام)." Walipomjengea, — Al-Hasan amesema: — Wa-Allaahi, gogo lililia kwa shauku! Al-Hasan amesema: Subhaana-Allaah! Je, nyoyo za watu waliosikia (hayo) zinatafutwa?

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Anakusudia hili.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
181
Hadiyth
38

أَخْبَرَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَمَّارِ بْنِ أَبِي عَمَّارٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ: يَخْطُبُ إِلَى جِذْعٍ قَبْلَ أَنْ يَتَّخِذَ الْمِنْبَرَ، فَلَمَّا اتَّخَذَ الْمِنْبَرَ وَتَحَوَّلَ إِلَيْهِ، حَنَّ الْجِذْعُ، فَاحْتَضَنَهُ، فَسَكَنَ "، وَقَالَ:" لَوْ لَمْ أَحْتَضِنْهُ، لَحَنَّ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ "،

Ametukhabarisha Al-Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Ammaar bin Abiy 'Ammaar, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikhutubu akiegemea shina la mtende kabla ya kuchukua mimbari. Alipoichukua mimbari na akahamia kwake, shina likalia kwa shauku; akalikumbatia, likatulia. Na akasema: "Lau nisingelikumbatia, lingeendelea kulia kwa shauku mpaka Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
182
Hadiyth
39

أَخْبَرَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، بِمِثْلِهِ

Ametukhabarisha Al-Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), mfano wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
183
Hadiyth
40

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: حَنَّتِ الْخَشَبَةُ الَّتِي كَانَ يَقُومُ عِنْدَهَا، "فَقَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهَا، وَوَضَعَ يَدَهُ عَلَيْهَا"، فَسَكَنَتْ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), amesema: Gogo ambalo (Nabiy) alikuwa akisimama karibu nalo lililia kwa shauku. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama kulielekea, na akaweka mkono wake juu yake; likatulia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
183
Hadiyth
41

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا عِكْرِمَةُ بْنُ عَمَّارٍ، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ أَبِي طَلْحَةَ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ: يَقُومُ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَيُسْنِدُ ظَهْرَهُ إِلَى جِذْعٍ فِي الْمَسْجِدِ فَيَخْطُبُ النَّاسَ، فَجَاءَهُ رُومِيٌّ، فَقَالَ: أَلَا أَصْنَعُ لَكَ شَيْئًا تَقْعُدُ عَلَيْهِ وَكَأَنَّكَ قَائِمٌ؟ فَصَنَعَ لَهُ مِنْبَرًا لَهُ دَرَجَتَانِ، وَيَقْعُدُ عَلَى الثَّالِثَةِ، فَلَمَّا قَعَدَ نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى ذَلِكَ الْمِنْبَرِ، خَارَ الْجِذْعُ كَخُوَارِ الثَّوْرِ حَتَّى ارْتَجَّ الْمَسْجِدُ حُزْنًا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَنَزَلَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ الْمِنْبَرِ، فَالْتَزَمَهُ وَهُوَ يَخُورُ، فَلَمَّا الْتَزَمَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، سَكَنَ، ثُمَّ قَالَ: "أَمَا وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَوْ لَمْ أَلْتَزِمْهُ، لَمَا زَالَ هَكَذَا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ حُزْنًا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"، فَأَمَرَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَدُفِنَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia 'Umar bin Yuwnus, ametusimulia 'Ikrimah bin 'Ammaar, ametusimulia Is-haaq bin Abiy Twalhah, ametusimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisimama siku ya Ijumaa, akiegemeza mgongo wake kwenye shina la mtende ndani ya Msikiti, akiwakhutubia watu. Mrumi mmoja akamjia, akasema: Je, nisikutengenezee kitu ukae juu yake, nawe uwe kama uliyesimama? Akamtengenezea mimbari yenye vidaraja viwili, naye akawa anakaa juu ya cha tatu. Nabiy wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoketi juu ya mimbari hiyo, shina likatoa mlio kama mlio wa ng'ombe dume, mpaka Msikiti ukatikisika, kwa huzuni juu ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akashuka kulijia kutoka kwenye mimbari, akalikumbatia, nalo likitoa mlio. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipolikumbatia, likatulia. Kisha akasema: "Tambueni! Naapa kwa Ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake! Lau nisingelikumbatia, lisingeacha kuwa hivi mpaka Siku ya Qiyaamah, kwa huzuni juu ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha kuhusu (shina) hilo, likazikwa.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
183
Hadiyth
42

7-Mlangoباب ما أكرم به النبي صلى الله عليه وسلم في بركة طعامهMlango Wa Yale Aliyokirimiwa Kwayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Katika Baraka Ya Chakula Chake

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ بْنِ أَبَانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مُحَمَّدٍ الْمُحَارِبِيُّ، عَنْ عَبْدِ الْوَاحِدِ بْنِ أَيْمَنَ الْمَكِّيِّ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قُلْتُ لِجَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: حَدِّثْنِي بِحَدِيثٍ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَمِعْتَهُ مِنْهُ أَرْوِيهِ عَنْكَ، فَقَالَ جَابِرٌ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ نَحْفُرُهُ، فَلَبِثْنَا ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ لَا نَطْعَمُ طَعَامًا، وَلَا نَقْدِرُ عَلَيْهِ، فَعَرَضَتْ فِي الْخَنْدَقِ كُدْيَةٌ فَجِئْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذِهِ كُدْيَةٌ قَدْ عَرَضَتْ، فِي الْخَنْدَقِ فَرَشَشْنَا عَلَيْهَا الْمَاءَ، فَقَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبَطْنُهُ مَعْصُوبٌ بِحَجَرٍ، فَأَخَذَ الْمِعْوَلَ، أَوْ الْمِسْحَاةَ، ثُمَّ سَمَّى ثَلَاثًا، ثُمَّ ضَرَبَ فَعَادَتْ كَثِيبًا أَهْيَلَ، فَلَمَّا رَأَيْتُ ذَلِكَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، ائْذَنْ لِي، قَالَ: فَأَذِنَ لِي، فَجِئْتُ امْرَأَتِي، فَقُلْتُ: ثَكِلَتْكِ أُمُّكِ قَدْ رَأَيْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا لَا صَبْرَ لِي عَلَيْهِ، فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَيْءٍ؟، فَقَالَتْ: عِنْدِي صَاعٌ مِنْ شَعِيرٍ، وَعَنَاقٌ، قَالَ: فَطَحَنَّا الشَّعِيرَ، وَذَبَحْنَا الْعَنَاقَ، وَسَلَخْتُهَا، وَجَعَلْتُهَا، فِي الْبُرْمَةِ وَعَجَنْتُ الشَّعِيرَ، قَالَ: ثُمَّ رَجَعْتُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَبِثْتُ سَاعَةً، ثُمَّ اسْتَأْذَنْتُهُ الثَّانِيَةَ فَأَذِنَ لِي، فَجِئْتُ، فَإِذَا الْعَجِينُ قَدْ أَمْكَنَ، فَأَمَرْتُهَا بِالْخَبْزِ وَجَعَلْتُ الْقِدْرَ عَلَى الْأَثَاثِي، قَالَ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ: إِنَّمَا هِيَ الْأَثَافِيُّ وَلَكِنْ كَذَا قَالَ: ثُمَّ جِئْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: إِنَّ عِنْدَنَا طُعَيِّمًا لَنَا، فَإِنْ رَأَيْتَ أَنْ تَقُومَ مَعِي أَنْتَ وَرَجُلٌ أَوْ رَجُلَانِ مَعَكَ، فَقَالَ: "وَكَمْ هُوَ؟"، قُلْتُ: صَاعٌ مِنْ شَعِيرٍ، وَعَنَاقٌ، فَقَالَ: "ارْجِعْ إِلَى أَهْلِكَ وَقُلْ لَهَا لَا تَنْزِعْ الْقِدْرَ مِنْ الْأَثَافِيِّ، وَلَا تُخْرِجْ الْخُبْزَ مِنْ التَّنُّورِ حَتَّى آتِيَ"، ثُمَّ قَالَ لِلنَّاسِ: "قُومُوا إِلَى بَيْتِ جَابِرٍ"، قَالَ: فَاسْتَحْيَيْتُ حَيَاءً لَا يَعْلَمُهُ إِلَّا اللَّهُ، فَقُلْتُ لِامْرَأَتِي: ثَكِلَتْكِ أُمُّكِ، قَدْ جَاءَكِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِأَصْحَابِهِ أَجْمَعِينَ، فَقَالَتْ: أَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَأَلَكَ: كَمْ الطَّعَامُ؟، فَقُلْتُ: نَعَمْ، قَالَتْ: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَدْ أَخْبَرْتَهُ بِمَا كَانَ عِنْدَنَا، قَالَ: فَذَهَبَ عَنِّي بَعْضُ مَا كُنْتُ أَجِدُ، وَقُلْتُ: لَقَدْ صَدَقْتِ، فَجَاءَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَدَخَلَ، ثُمَّ قَالَ لِأَصْحَابِهِ: "لَا تَضَاغَطُوا"، "ثُمَّ بَرَّكَ عَلَى التَّنُّورِ وَعَلَى الْبُرْمَةِ"، قَالَ: فَجَعَلْنَا نَأْخُذُ مِنْ التَّنُّورِ الْخُبْزَ، وَنَأْخُذُ اللَّحْمَ مِنْ الْبُرْمَةِ، فَنُثَرِّدُ وَنَغْرِفُ لَهُمْ، وَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لِيَجْلِسْ عَلَى الصَّحْفَةِ سَبْعَةٌ أَوْ ثَمَانِيَةٌ"، فَإِذَا أَكَلُوا كَشَفْنَا عَنْ التَّنُّورِ، وَكَشَفْنَا عَنْ الْبُرْمَةِ، فَإِذَا هُمَا أَمْلَأُ مِمَّا كَانَا، فَلَمْ نَزَلْ نَفْعَلُ ذَلِكَ كُلَّمَا فَتَحْنَا التَّنُّورَ وَكَشَفْنَا عَنْ الْبُرْمَةِ، وَجَدْنَاهُمَا أَمْلَأَ مَا كَانَا حَتَّى شَبِعَ الْمُسْلِمُونَ كُلُّهُمْ، وَبَقِيَ طَائِفَةٌ مِنْ الطَّعَامِ، فَقَالَ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ النَّاسَ قَدْ أَصَابَتْهُمْ مَخْمَصَةٌ، فَكُلُوا وَأَطْعِمُوا"، فَلَمْ نَزَلْ يَوْمَنَا نَأْكُلُ وَنُطْعِمُ، قَالَ: وَأَخْبَرَنِي أَنَّهُمْ كَانُوا ثَمَانِمِئَةٍ، أَوْ قَالَ: ثَلَاثَمِئَةٍ، قَالَ أَيْمَنُ: لَا أَدْرِي أَيُّهُمَا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Umar bin Abaan, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Muhammad Al-Muhaaribiy, kutoka kwa 'Abdul-Waahid bin Ayman Al-Makkiy, kutoka kwa baba yake, amesema: Nilimwambia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما): Nisimulie Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) uliyoisikia kutoka kwake, niipokee kutoka kwako. Jaabir (رضي الله عنه) akasema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya (vita vya) Al-Khandaq (Handaki) tukilichimba. Tukakaa siku tatu hatuli chakula, wala hatukipati. Likajitokeza katika handaki jabali gumu. Nikaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hili ni jabali gumu limejitokeza katika handaki, na tumelinyunyizia maji. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama, na tumbo lake limefungwa jiwe, akachukua sururu — au sepetu —, kisha akataja Jina la Allaah mara tatu, kisha akapiga, (jabali) likawa rundo la mchanga linalomwagika. Nilipoona hilo kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Yaa Rasula-Allaah, nipe idhini (niende). Akasema: Akanipa idhini. Nikamjia mke wangu, nikasema: Mama yako akufiwe! Hakika nimeona kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) jambo ambalo siwezi kulivumilia; je, una kitu chochote? Akasema: Nina Swaa' (pishi) moja ya shayiri na mwana-mbuzi jike. Akasema: Tukasaga shayiri, na tukamchinja yule mwana-mbuzi; nikamchuna na nikamweka ndani ya chungu, na nikaukanda (unga wa) shayiri. Akasema: Kisha nikarudi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), nikakaa muda, kisha nikamwomba idhini mara ya pili, akanipa idhini. Nikaja, na kumbe unga uliokandwa umeshakuwa tayari. Nikamwamrisha aoke mikate, na nikakiweka chungu juu ya al-athaathiy (mafiga) — Abuw 'Abdir-Rahmaan amesema: Hakika ni al-athaafiy (mafiga), lakini hivyo ndivyo alivyosema —. Kisha nikamjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Hakika tuna chakula kidogo chetu; basi ukiona (vyema) usimame pamoja nami, wewe na mtu mmoja au wawili pamoja nawe. Akasema: "Na ni kiasi gani?" Nikasema: Swaa' moja ya shayiri na mwana-mbuzi jike. Akasema: "Rudi kwa mkeo, umwambie asikiteremshe chungu kutoka kwenye mafiga, wala asiitoe mikate kutoka kwenye tanuri mpaka nije." Kisha akawaambia watu: "Simameni (twende) nyumbani kwa Jaabir (رضي الله عنه)." Akasema: Nikaona haya sana, haya ambayo hakuna anayeijua ila Allaah. Nikamwambia mke wangu: Mama yako akufiwe! Amekujia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pamoja na Swahaba zake (رضي الله عنهم) wote. Akasema: Je, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuuliza: Chakula ni kiasi gani? Nikasema: Ndiyo. Akasema: Allaah na Rasuli Wake ndio wajuzi zaidi; hakika umeshamkhabarisha tulichokuwa nacho. Akasema: Baadhi ya (wasiwasi) niliokuwa nao ukaniondokea, na nikasema: Hakika umesema kweli. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaja akaingia, kisha akawaambia Swahaba zake (رضي الله عنهم): "Msisongamane." Kisha akaomba baraka juu ya tanuri na juu ya chungu. Akasema: Tukawa tunachukua mikate kutoka kwenye tanuri, na tunachukua nyama kutoka kwenye chungu, tunaandaa thariyd (mkate uliovunjwa katika mchuzi) na tunawapakulia. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Wakae kwenye sahani kubwa watu saba au wanane." Walipokwisha kula, tukafunua tanuri na tukafunua chungu, kumbe vyote viwili vimejaa zaidi kuliko vilivyokuwa. Hatukuacha kufanya hivyo; kila tulipofungua tanuri na tukafunua chungu, tuliviona vimejaa zaidi kuliko vilivyokuwa, mpaka Waislamu (رضي الله عنهم) wote wakashiba, na kikabaki kiasi cha chakula. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatuambia: "Hakika watu wamepatwa na njaa kali; basi kuleni na lisheni (wengine)." Tukaendelea siku yetu tukila na tukilisha. Akasema: Na akanikhabarisha kwamba walikuwa mia nane, au alisema: mia tatu. Ayman amesema: Sijui ni ipi kati ya hizo mbili.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
184
Hadiyth
43

قَالَ: أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ هُوَ ابْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: أَمَرَ أَبُو طَلْحَةَ أُمَّ سُلَيْمٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا، أَنْ تَجْعَلَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَعَامًا يَأْكُلُ مِنْهُ، قَالَ: ثُمَّ بَعَثَنِي أَبُو طَلْحَةَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَيْتُهُ، فَقُلْتُ: بَعَثَنِي إِلَيْكَ أَبُو طَلْحَةَ، فَقَالَ لِلْقَوْمِ: "قُومُوا"، فَانْطَلَقَ وَانْطَلَقَ الْقَوْمُ مَعَهُ، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّمَا صَنَعْتُ طَعَامًا لِنَفْسِكَ خَاصَّةً؟، فَقَالَ: "لَا عَلَيْكَ انْطَلِقْ"، قَالَ: فَانْطَلَقَ وَانْطَلَقَ الْقَوْمُ، قَالَ: فَجِيءَ بِالطَّعَامِ، "فَوَضَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ وَسَمَّى عَلَيْهِ"، ثُمَّ قَالَ: "ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ"، قَالَ: فَأَذِنَ لَهُمْ، فَقَالَ: "كُلُوا بِاسْمِ اللَّهِ"، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا، ثُمَّ قَامُوا، "ثُمَّ وَضَعَ يَدَهُ كَمَا صَنَعَ فِي الْمَرَّةِ الْأُولَى وَسَمَّى عَلَيْهِ"، ثُمَّ قَالَ: "ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ"، فَأَذِنَ لَهُمْ، فَقَالَ: "كُلُوا، بِاسْمِ اللَّهِ" فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا، ثُمَّ قَامُوا حَتَّى فَعَلَ ذَلِكَ بِثَمَانِينَ رَجُلًا، قَالَ: "وَأَكَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَهْلُ الْبَيْتِ وَتَرَكُوا سُؤْرًا"

Amesema: Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah — naye ni Ibn 'Amr —, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Abuw Twalhah (رضي الله عنه) alimwamrisha Ummu Sulaym (رضي الله عنها) amtengenezee Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) chakula ale kutoka kwacho. Akasema: Kisha Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akanituma kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); nikamjia, nikasema: Abuw Twalhah (رضي الله عنه) amenituma kwako. Akawaambia watu: "Simameni." Akaondoka, na watu wakaondoka pamoja naye. Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika nimetengeneza chakula kwa ajili yako peke yako! Akasema: "Usijali; nenda." Akasema: Akaondoka, na watu wakaondoka. Akasema: Chakula kikaletwa; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake na akataja Jina la Allaah juu yake, kisha akasema: "Wape idhini watu kumi." Akasema: Akawapa idhini. Akasema: "Kuleni kwa Jina la Allaah." Wakala mpaka wakashiba, kisha wakasimama. Kisha akaweka mkono wake kama alivyofanya mara ya kwanza, na akataja Jina la Allaah juu yake, kisha akasema: "Wape idhini watu kumi." Akawapa idhini. Akasema: "Kuleni kwa Jina la Allaah." Wakala mpaka wakashiba, kisha wakasimama; mpaka akafanya hivyo kwa wanaume themanini. Akasema: Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akala, pamoja na watu wa nyumba, na wakaacha mabaki.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
187
Hadiyth
44

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا أَبَانُ هُوَ الْعَطَّارُ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، عَنْ أَبِي عُبَيْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، أَنَّهُ طَبَخَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قِدْرًا، فَقَالَ لَهُ: "نَاوِلْنِي ذِرَاعَهَا"، وَكَانَ يُعْجِبُهُ الذِّرَاعُ، فَنَاوَلَهُ الذِّرَاعَ، ثُمَّ قَالَ: "نَاوِلْنِي الذِّرَاعَ"، فَنَاوَلَهُ ذِرَاعًا، ثُمَّ قَالَ: "نَاوِلْنِي الذِّرَاعَ"، فَقُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، وَكَمْ لِلشَّاةِ مِنْ ذِرَاعٍ؟ فَقَالَ: "وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ أَنْ لَوْ سَكَتَّ لَأُعْطَيْتَ أَذْرُعًا مَا دَعَوْتُ بِهِ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Abaan — naye ni Al-'Attwaar —, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, kutoka kwa Abuw 'Ubayd (رضي الله عنه), kwamba alimpikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) chungu (cha nyama). (Nabiy) akamwambia: "Nipe mkono wake (wa mbele)." Na alikuwa akipendezwa na mkono (wa mbele). Akampa mkono, kisha akasema: "Nipe mkono." Akampa mkono (mwingine). Kisha akasema: "Nipe mkono." Nikasema: Yaa Nabiyya-Allaah, na mbuzi ana mikono mingapi? Akasema: "Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Lau ungenyamaza, ungepewa mikono maadamu ningeiomba."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
188
Hadiyth
45

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَان، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ نُبَيْحٍ الْعَنَزِيِّ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْمُشْرِكِينَ لِيُقَاتِلَهُمْ، فَقَالَ أَبِي عَبْدُ اللَّهِ: يَا جَابِرُ، لَا عَلَيْكَ أَنْ تَكُونَ، فِي نَظَّارِي أَهْلِ الْمَدِينَةِ حَتَّى تَعْلَمَ إِلَى مَا يَصِيرُ أَمْرُنَا، فَإِنِّي وَاللَّهِ لَوْلَا أَنِّي أَتْرُكُ بَنَاتٍ لِي بَعْدِي، لَأَحْبَبْتُ أَنْ تُقْتَلَ بَيْنَ يَدَيَّ، قَالَ: فَبَيْنَمَا أَنَا فِي النَّظَّارِينَ إِذْ جَاءَتْ عَمَّتِي بِأَبِي وَخَالِي لِتَدْفُنَهُمَا فِي مَقَابِرِنَا، فَلَحِقَ رَجُلٌ يُنَادِي، إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَأْمُرُكُمْ أَنْ تَرُدُّوا الْقَتْلَى فَتَدْفُنُوهَا فِي مَضَاجِعَهَا حَيْثُ قُتِلَتْ، فَرَدَدْنَاهُمَا، فَدَفَنَّاهُمَا فِي مَضْجَعِهِمَا حَيْثُ قُتِلَا: فَبَيْنَا أَنَا فِي خِلَافَةِ مُعَاوِيَةَ بْنِ أَبِي سُفْيَانَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، إِذْ جَاءَنِي رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، لَقَدْ أَثَارَ أَبَاكَ عُمَّالُ مُعَاوِيَةَ، فَبَدَا، فَخَرَجَ طَائِفَةٌ مِنْهُمْ، فَانْطَلَقْتُ إِلَيْهِ فَوَجَدْتُهُ عَلَى النَّحْوِ الَّذِي دَفَنْتُهُ لَمْ يَتَغَيَّرْ إِلَّا مَا لَمْ يَدَعِ الْقَتِيلَ، قَالَ: فَوَارَيْتُهُ، وَتَرَكَ أَبِي عَلَيْهِ دَيْنًا مِنْ التَّمْرِ فَاشْتَدَّ عَلَيَّ بَعْضُ غُرَمَائِهِ، فِي التَّقَاضِي، فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أَبِي أُصِيبَ يَوْمَ كَذَا وَكَذَا، وَإِنَّهُ تَرَكَ عَلَيْهِ دَيْنًا مِنَ التَّمْرِ، وَإِنَّهُ قَدْ اشْتَدَّ عَلَيَّ بَعْضُ غُرَمَائِهِ فِي الطَّلَبِ، فَأُحِبُّ أَنْ تُعِينَنِي عَلَيْهِ لَعَلَّهُ أَنْ يُنْظِرَنِي طَائِفَةً مِنْ تَمْرِهِ إِلَى هَذَا الصِّرَامِ الْمُقْبِلِ، قَالَ:" نَعَمْ آتِيكَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ قَرِيبًا مِنْ وَسَطِ النَّهَارِ "، قَالَ: فَجَاءَ وَمَعَهُ حَوَارِيُّوهُ، قَالَ: فَجَلَسُوا فِي الظِّلِّ وَسَلَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَاسْتَأْذَنَ ثُمَّ دَخَلَ عَلَيْنَا، قَالَ: وَقَدْ قُلْتُ لِامْرَأَتِي: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَاءَنِي الْيَوْمَ وَسَطَ النَّهَارِ، فَلَا يَرَيَنَّكِ وَلَا تُؤْذِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْتِي بِشَيْءٍ وَلَا تُكَلِّمِيهِ، فَفَرَشَتْ فِرَاشًا وَوِسَادَةً فَوَضَعَ رَأْسَهُ، فَنَامَ، فَقُلْتُ لِمَوْلًى لِي: اذْبَحْ هَذِهِ الْعَنَاقَ، وَهِيَ دَاجِنٌ سَمِينَة، فَالْوَحَا وَالْعَجْلَ افْرَغْ مِنْهَا قَبْلَ أَنْ يَسْتَيْقِظَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا مَعَكَ، فَلَمْ نَزَلْ فِيهَا حَتَّى فَرَغْنَا مِنْهَا، وَهُوَ نَائِمٌ، فَقُلْتُ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ يَسْتَيْقِظُ يَدْعُو بِطَهُورِهِ، وَأَنَا أَخَافُ إِذَا فَرَغَ أَنْ يَقُومَ، فَلَا يَفْرَغْ مِنْ طُهُورِهِ حَتَّى يُوضَعَ الْعَنَاقُ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَلَمَّا اسْتَيْقَظَ، قَالَ: " يَا جَابِرُ ائْتِنِي بِطَهُورٍ "، قَالَ: نَعَمْ، فَلَمْ يَفْرَغْ مِنْ وُضُوئِهِ حَتَّى وُضِعَتِ الْعَنَاقُ بَيْنَ يَدَيْهِ، قَالَ: فَنَظَرَ إِلَيَّ، فَقَالَ: " كَأَنَّكَ قَدْ عَلِمْتَ حُبَّنَا اللَّحْمَ، ادْعُ أَبَا بَكْر "، ثُمَّ دَعَا حَوَارِيِّيهِ، قَالَ: فَجِيءَ بِالطَّعَامِ فَوُضِعَ، قَالَ: فَوَضَعَ يَدَهُ، وَقَالَ: " بِسْمِ اللَّهِ كُلُوا "، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا وَفَضَلَ مِنْهَا لَحْمٌ كَثِيرٌ، وَقَالَ: وَاللَّهِ إِنَّ مَجْلِسَ بَنِي سَلِمَةَ لَيَنْظُرُونَ إِلَيْهِمْ، هُوَ أَحَبُّ إِلَيْهِمْ مِنْ أَعْيُنِهِمْ، مَا يَقْرَبُونَهُ مَخَافَةَ أَنْ يُؤْذُوهُ، ثُمَّ قَامَ، وَقَامَ أَصْحَابُهُ، فَخَرَجُوا بَيْنَ يَدَيْهِ، وَكَانَ يَقُولُ: " خَلُّوا ظَهْرِي لِلْمَلَائِكَةِ "، قَالَ: فَاتَّبَعْتُهُمْ حَتَّى بَلَغْتُ أُسْكُفَّةَ الْبَابِ، فَأَخْرَجَتِ امْرَأَتِي صَدْرَهَا وَكَانَتْ سَتِّيرَةً، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، صَلِّ عَلَيَّ وَعَلَى زَوْجِي، قَالَ: " صَلَّى اللَّهُ عَلَيْكِ وَعَلَى زَوْجِكِ "، ثُمَّ قَالَ: " ادْعُوا لِي فُلَانًا لِلْغَرِيمِ الَّذِي اشْتَدَّ عَلَيَّ فِي الطَّلَبِ، فَقَالَ: " أَنْسِئْ جَابِرًا طَائِفَةً مِنْ دَيْنِكَ الَّذِي عَلَى أَبِيهِ إِلَى هَذَا الصِّرَامِ الْمُقْبِلِ "، قَالَ: مَا أَنَا بِفَاعِلٍ، قَالَ: وَاعْتَلَّ وَقَالَ: إِنَّمَا هُوَ مَالُ يَتَامَى، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " أَيْنَ جَابِرٌ؟ " قَالَ: قُلْتُ: أَنَا ذَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: " كِلْ لَهُ، فَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى سَوْفَ يُوَفِّيهِ "، فَرَفَعَ رَأْسَهُ إِلَى السَّمَاءِ، فَإِذَا الشَّمْسُ قَدْ دَلَكَتْ، قَالَ: " الصَّلَاةُ يَا أَبَا بَكْرٍ "، فَانْدَفَعُوا إِلَى الْمَسْجِدِ، فَقُلْتُ لِغَرِيمِي: قَرِّبْ أَوْعِيَتَكَ، فَكِلْتُ لَهُ مِنْ الْعَجْوَةِ فَوَفَّاهُ اللَّهُ وَفَضُلَ لَنَا مِنْ التَّمْرِ كَذَا وَكَذَا، قَالَ: فَجِئْتُ أَسْعَى إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَسْجِدِهِ كَأَنِّي شَرَارَةٌ، فَوَجَدْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ صَلَّى، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنِّي قَدْ كِلْتُ لِغَرِيمِي تَمْرَهُ فَوَفَّاهُ اللَّهُ وَفَضُلَ لَنَا مِنْ التَّمْرِ كَذَا وَكَذَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " أَيْنَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ؟ "، قَالَ: فَجَاءَ يُهَرْوِلُ، قَالَ: " سَلْ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ عَنْ غَرِيمِهِ وَتَمْرِهِ "، قَالَ: مَا أَنَا بِسَائِلِهِ، قَدْ عَلِمْتُ أَنَّ اللَّهَ سَوْفَ يُوَفِّيهِ إِذْ أَخْبَرْتَ أَنَّ اللَّهَ سَوْفَ يُوَفِّيهِ فَرَدَّدَ عَلَيْهِ، وَرَدَّدَ عَلَيْهِ هَذِهِ الْكَلِمَةَ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، كُلُّ ذَلِكَ يَقُولُ: مَا أَنَا بِسَائِلِهِ، وَكَانَ لَا يُرَاجَعُ بَعْدَ الْمَرَّةِ الثَّالِثَةِ، فَقَالَ: مَا فَعَلَ غَرِيمُكَ وَتَمْرُكَ؟، قَالَ: قُلْتُ: وَفَّاهُ اللَّهُ وَفَضُلَ لَنَا مِنْ التَّمْرِ كَذَا وَكَذَا، قالَ: فَرَجَعْتُ إِلَى امْرَأَتِي، فَقُلْتُ: أَلَمْ أَكُنْ نَهَيْتُكِ أَنْ تُكَلِّمِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْتِي؟، فَقَالَتْ: تَظُنُّ أَنَّ اللَّهَ تَعَالَى يُورِدُ نَبِيَّهُ فِي بَيْتِي ثُمَّ يَخْرُجُ وَلَا أَسْأَلُهُ الصَّلَاةَ عَلَيَّ وَعَلَى زَوْجِي

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa Nubayh Al-'Anaziy, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka kwenda kwa washirikina ili apigane nao. Baba yangu 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) akasema: Yaa Jaabir, si vibaya kwako kuwa miongoni mwa watazamaji (walinzi) wa watu wa Madiynah mpaka ujue jambo letu litaishia wapi; kwani mimi, Wa-Allaahi, lau si kwamba ninawaacha mabinti zangu baada yangu, ningependa uuawe mbele yangu. Akasema: Basi nilipokuwa miongoni mwa watazamaji, ghafla shangazi yangu akaja na baba yangu (رضي الله عنه) na mjomba wangu (wakiwa wameuawa) ili awazike katika makaburi yetu. Mtu mmoja akaja nyuma (akatufikia) akinadi: Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) anakuamrisheni muwarudishe waliouawa, muwazike mahali walipoangukia pale walipouawa. Tukawarudisha wawili hao, tukawazika mahali walipoangukia pale walipouawa. Basi nilipokuwa katika (zama za) Ukhalifa wa Mu'aawiyah bin Abiy Sufyaan (رضي الله عنه), ghafla mtu mmoja akanijia, akasema: Yaa Jaabir bin 'Abdi-Allaah, wafanyakazi wa Mu'aawiyah wamemfukua baba yako (رضي الله عنه), akadhihirika, na baadhi yao (waliozikwa) wakatokeza nje. Nikaenda kwake, nikamkuta katika hali ile ile niliyomzika nayo; hakubadilika isipokuwa kile ambacho aliyeuawa hakiachi. Akasema: Nikamfukia (tena). Na baba yangu (رضي الله عنه) aliacha deni la tende juu yake; baadhi ya wadai wake wakanibana katika kudai. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika baba yangu (رضي الله عنه) alipatwa (aliuawa) siku kadhaa wa kadhaa, na kwamba aliacha deni la tende juu yake, na kwamba baadhi ya wadai wake wamenibana katika kudai; basi napenda unisaidie kwake, huenda akanipa muhula wa sehemu ya tende zake mpaka mavuno haya (ya tende) yajayo. Akasema: "Ndiyo, nitakujia, Akipenda Allaah, karibu na katikati ya mchana." Akasema: Akaja pamoja na wafuasi wake watiifu (رضي الله عنهم). Akasema: Wakaketi kivulini; na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoa Salaam, akaomba idhini, kisha akaingia kwetu. Akasema: Na nilikuwa nimemwambia mke wangu: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anakuja kwangu leo katikati ya mchana; basi asikuone, wala usimuudhi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nyumbani mwangu kwa chochote, wala usimsemeshe. Akatandika tandiko na mto; akaweka kichwa chake akalala. Nikamwambia mwachwa huru wangu mmoja: Mchinje mwana-mbuzi huyu — naye alikuwa ni wa kufugwa nyumbani, mnono — haraka haraka, upesi upesi! Mmalize kabla Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hajaamka, nami niko pamoja nawe. Hatukuacha kushughulika naye mpaka tukammaliza, naye (Nabiy) akiwa amelala. Nikasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anapoamka huagiza maji yake ya kujitwaharishia, nami nahofia akimaliza atasimama (aondoke); basi asimalize kujitwaharisha kwake mpaka mwana-mbuzi awekwe mbele yake. Alipoamka, akasema: "Yaa Jaabir, niletee maji ya kujitwaharishia." Akasema: Ndiyo. Hakumaliza Wudhuu wake mpaka mwana-mbuzi akawekwa mbele yake. Akasema: Akanitazama, akasema: "Kama kwamba umejua kupenda kwetu nyama. Mwite Abuw Bakr (رضي الله عنه)." Kisha akawaita wafuasi wake watiifu (رضي الله عنهم). Akasema: Chakula kikaletwa, kikawekwa. Akasema: Akaweka mkono wake, na akasema: "Bismi-Allaah (Kwa Jina la Allaah), kuleni." Wakala mpaka wakashiba, na ikabaki nyama nyingi. Na akasema: Wa-Allaahi, hakika baraza la Banuw Salimah walikuwa wakiwatazama; yeye (Nabiy) ni kipenzi zaidi kwao kuliko macho yao; hawamkaribii kwa kuogopa kumuudhi. Kisha akasimama, na Swahaba zake (رضي الله عنهم) wakasimama, wakatoka mbele yake; na alikuwa akisema: "Uachieni mgongo wangu Malaika (عليهم السلام)." Akasema: Nikawafuata mpaka nikafika kizingitini mwa mlango. Mke wangu akatokeza kifua chake — naye alikuwa mwenye kujisitiri sana — akasema: Yaa Rasula-Allaah, niombee Allaah Aniswalie mimi na mume wangu. Akasema: "Allaah Akuswalie wewe na mume wako." Kisha akasema: "Niitieni fulani" — (yaani) yule mdai aliyenibana katika kudai. Akasema: "Mpe Jaabir (رضي الله عنه) muhula wa sehemu ya deni lako lililo juu ya baba yake (رضي الله عنه) mpaka mavuno haya yajayo." Akasema: Mimi sitafanya. Akasema: Akatoa udhuru, na akasema: Hakika hayo ni mali ya mayatima. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yuko wapi Jaabir (رضي الله عنه)?" Akasema: Nikasema: Mimi huyu hapa, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Mpimie, kwani Allaah (تعالى) Atamtimizia." Akainua kichwa chake mbinguni, kumbe jua limekwisha pinduka. Akasema: "Swalaah, yaa Abaa Bakr!" Wakaondoka kwa haraka kwenda Msikitini. Nikamwambia mdai wangu: Sogeza karibu vyombo vyako. Nikampimia katika tende za 'ajwah (aina bora ya tende za Madiynah); Allaah Akamtimizia, na zikatubakia tende kiasi kadhaa wa kadhaa. Akasema: Nikaja mbio kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Msikiti wake kama kwamba mimi ni cheche ya moto; nikamkuta Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekwisha swali. Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nimempimia mdai wangu tende zake, na Allaah Amemtimizia, na zimetubakia tende kiasi kadhaa wa kadhaa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yuko wapi 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه)?" Akasema: Akaja akienda mbio-mbio. Akasema: "Muulize Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) kuhusu mdai wake na tende zake." ('Umar) akasema: Mimi sitamuuliza; nimekwisha jua kwamba Allaah Atamtimizia, kwa kuwa wewe ulikhabarisha kwamba Allaah Atamtimizia. (Nabiy) akamrudia, na akamrudia neno hilo mara tatu; kila mara ('Umar) anasema: Mimi sitamuuliza. Na (Nabiy) alikuwa harejewi (katika jambo) baada ya mara ya tatu. Basi ('Umar) akasema: Amefanya nini mdai wako na tende zako? Akasema: Nikasema: Allaah Amemtimizia, na zimetubakia tende kiasi kadhaa wa kadhaa. Akasema: Nikarudi kwa mke wangu, nikasema: Je, sikuwa nimekukataza kumsemesha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nyumbani mwangu? Akasema: Je, unadhani kwamba Allaah (تعالى) Atamleta Nabiy Wake nyumbani mwangu, kisha atoke bila mimi kumuomba aniombee Allaah Aniswalie mimi na mume wangu?

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
189
Hadiyth
46

8-Mlangoباب ما أعطي النبي صلى الله عليه وسلم من الفضلMlango Wa Fadhila Alizopewa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا إِسْحَاقُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا يَزِيدُ بْنُ أَبِي حَكِيمٍ، حَدَّثَنِي الْحَكَمُ بْنُ أَبَانَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "إِنَّ اللَّهَ فَضَّلَ مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم عَلَى الْأَنْبِيَاءِ عَلَيْهِمْ السَّلامُ وَعَلَى أَهْلِ السَّمَاءِ، فَقَالُوا: يَا ابْنَ عَبَّاسٍ، بِمَ فَضَّلَهُ عَلَى أَهْلِ السَّمَاءِ؟، قَالَ: إِنَّ اللَّهَ قَالَ لِأَهْلِ السَّمَاءِ {وَمَنْ يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَهٌ مِنْ دُونِهِ فَذَلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ كَذَلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ}، الْآيَةَ، وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى لِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ}، قَالُوا: فَمَا فَضْلُهُ عَلَى الْأَنْبِيَاءِ عَلَيْهِمْ السَّلامُ؟ قَالَ: قَالَ اللَّهُ عز وجل: {وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ}، الْآيَةَ، وَقَالَ اللَّهُ عز وجل لِمُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلا كَافَّةً لِلنَّاسِ}، فَأَرْسَلَهُ إِلَى الْجِنِّ وَالْإِنْسِ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametupa khabari Yaziyd bin Abiy Hakiym, amenisimulia Al-Hakam bin Abaan, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Hakika Allaah Amemfadhilisha Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) juu ya Manabii (عليهم السلام) na juu ya watu wa mbinguni. Wakasema: Yaa Ibna 'Abbaas, kwa kitu gani Amemfadhilisha juu ya watu wa mbinguni? Akasema: Hakika Allaah Amewaambia watu wa mbinguni:

وَمَنْ يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَهٌ مِنْ دُونِهِ فَذَلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ كَذَلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ

Na yeyote yule miongoni mwao atakayesema: Mimi ni mwabudiwa badala Yake, basi huyo Tutamlipa Jahannam. Hivyo ndivyo Tunavyolipa madhalimu. [Al-Anbiyaa (21:29)]

mpaka mwisho wa Aayah. Na Allaah (تعالى) Akamwambia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ

Hakika Tumekupa ushindi, ushindi bayana. Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia [Al-Fat-h (48:1-2)]

Wakasema: Basi ni ipi fadhila yake juu ya Manabii (عليهم السلام)? Akasema: Allaah (عز وجل) Amesema:

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ

Na Hatukutuma Rasuli yeyote isipokuwa kwa lugha ya kaumu yake ili awabainishie (Risala). [Ibraahiym (14:4)]

mpaka mwisho wa Aayah. Na Allaah (عز وجل) Akamwambia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلا كَافَّةً لِلنَّاسِ

Na Hatukukutuma isipokuwa kwa watu wote [Saba-a (34:28)]

Basi Akamtuma kwa majini na wanaadam.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
193
Hadiyth
47

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا زَمْعَةُ، عَنْ سَلَمَةَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: جَلَسَ نَاسٌ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْتَظِرُونَهُ فَخَرَجَ حَتَّى إِذَا دَنَا مِنْهُمْ، سَمِعَهُمْ يَتَذَاكَرُونَ، فَتَسَمَّعَ حَدِيثَهُمْ، فَإِذَا بَعْضُهُمْ، يَقُولُ: عَجَبًا إِنَّ اللَّهَ اتَّخَذَ مِنْ خَلْقِهِ خَلِيلًا، فَإِبْرَاهِيمُ خَلِيلُهُ، وَقَالَ آخَرُ: مَاذَا بِأَعْجَبَ مِنْ: {وَكَلَّمَ اللَّهُ مُوسَى تَكْلِيمًا}، وَقَالَ آخَرُ: فَعِيسَى كَلِمَةُ اللَّهِ وَرُوحُهُ، وَقَالَ آخَرُ: وَآدَمُ اصْطَفَاهُ اللَّه، فَخَرَجَ عَلَيْهِمْ فَسَلَّمَ، وَقَالَ: "قَدْ سَمِعْتُ كَلَامَكُمْ وَعَجَبَكُمْ، إِنَّ إِبْرَاهِيمَ خَلِيلُ اللَّهِ، وَهُوَ كَذَلِكَ، وَمُوسَى نَجِيُّهُ، وَهُوَ كَذَلِكَ، وَعِيسَى رُوحُهُ وَكَلِمَتُهُ، وَهُوَ كَذَلِكَ، وَآدَمُ اصْطَفَاهُ اللَّهُ تَعَالَى، وَهُوَ كَذَلِكَ، أَلَا وَأَنَا حَبِيبُ اللَّهِ، وَلَا فَخْرَ، وَأَنَا حَامِلُ لِوَاءِ الْحَمْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَلَا فَخْرُ وَأَنَا أَوَّلُ شَافِعٍ، وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ يُحَرِّكُ بِحَلَقِ الْجَنَّةِ وَلَا فَخْرُ، فَيَفْتَحُ اللَّهُ فَيُدْخِلُنِيهَا وَمَعِي فُقَرَاءُ الْمُؤْمِنِينَ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا أَكْرَمُ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ عَلَى اللَّهِ، وَلَا فَخْرُ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Zam'ah, kutoka kwa Salamah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Watu miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) waliketi wakimsubiri. Akatoka, mpaka alipowakaribia akawasikia wakizungumza (wakikumbushana), akasikiliza mazungumzo yao. Kumbe baadhi yao anasema: Ajabu! Hakika Allaah Amejifanyia katika viumbe Vyake Khaliyl (kipenzi mwandani): basi Ibraahiym (عليه السلام) ni Khaliyl Wake. Na mwingine akasema: Ni kipi cha ajabu zaidi kuliko (Kauli Yake):

وَكَلَّمَ اللَّهُ مُوسَى تَكْلِيمًا

Na bila shaka Allaah Alimsemesha Muwsaa maneno moja kwa moja [An-Nisaa (4:164)]

Na mwingine akasema: Na 'Iysaa (عليه السلام) ni Neno la Allaah na roho Yake (Aliyoiumba). Na mwingine akasema: Na Aadam (عليه السلام), Allaah Amemkhitari. Akawatokea, akatoa Salaam, na akasema: "Nimesikia maneno yenu na kustaajabu kwenu: hakika Ibraahiym (عليه السلام) ni Khaliyl wa Allaah, naye ni hivyo; na Muwsaa (عليه السلام) ni msiri Wake (Aliyezungumza naye kwa siri), naye ni hivyo; na 'Iysaa (عليه السلام) ni roho Yake na Neno Lake, naye ni hivyo; na Aadam (عليه السلام), Allaah (تعالى) Amemkhitari, naye ni hivyo. Tanabahini! Na mimi ni kipenzi wa Allaah, wala si kujifakhiri; na mimi ni mbebaji wa bendera ya Himdi Siku ya Qiyaamah, wala si kujifakhiri; na mimi ni wa kwanza mwenye kuombea, na wa kwanza mwenye kukubaliwa uombezi Siku ya Qiyaamah, wala si kujifakhiri; na mimi ni wa kwanza atakayetikisa vipete vya (mlango wa) Jannah (Pepo), wala si kujifakhiri; Allaah Atafungua, Aniingize humo, na pamoja nami mafakiri wa Waumini, wala si kujifakhiri; na mimi ni mtukufu zaidi wa wa mwanzo na wa mwisho mbele ya Allaah, wala si kujifakhiri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
194
Hadiyth
48

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ مَنْصُورِ بْنِ أَبِي الْأَسْوَدِ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ الرَّبِيعِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَا أَوَّلُهُمْ خُرُوجًا، وَأَنَا قَائِدُهُمْ إِذَا وَفَدُوا، وَأَنَا خَطِيبُهُمْ إِذَا أَنْصَتُوا، وَأَنَا مُسْتَشْفِعُهُمْ إِذَا حُبِسُوا، وَأَنَا مُبَشِّرُهُمْ إِذَا أَيِسُوا، الْكَرَامَةُ وَالْمَفَاتِيحُ يَوْمَئِذٍ بِيَدِي، وَأَنَا أَكْرَمُ وَلَدِ آدَمَ عَلَى رَبِّي، يَطُوفُ عَلَيَّ أَلْفُ خَادِمٍ كَأَنَّهُمْ بَيْضٌ مَكْنُونٌ، أَوْ لُؤْلُؤٌ مَنْثُورٌ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Manswuwr bin Abil-Aswad, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Ar-Rabiy' bin Anas, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi ni wa kwanza wao kutoka (makaburini), na mimi ni kiongozi wao watakapokwenda kama ujumbe, na mimi ni khatibu wao watakaponyamaza, na mimi ni mwenye kuwaombea uombezi watakapozuiliwa, na mimi ni mbashiriaji wao watakapokata tamaa. Utukufu na funguo siku hiyo zitakuwa mkononi mwangu. Na mimi ni mtukufu zaidi wa wana wa Aadam (عليه السلام) kwa Rabb wangu. Watanizungukia watumishi elfu moja, kama kwamba wao ni mayai yaliyohifadhiwa, au lulu zilizotawanywa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
195
Hadiyth
49

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْحَكَمِ الْمِصْرِيُّ، حَدَّثَنَا بَكْرُ بْنُ مُضَرَ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ رَبِيعَةَ، عَنْ صَالِحٍ هُوَ ابْنُ عَطَاءِ بْنِ خَبَّابٍ مَوْلَى بَنِي الدُّئِلِ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "أَنَا قَائِدُ الْمُرْسَلِينَ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا خَاتَمُ النَّبِيِّينَ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا أَوَّلُ شَافِعٍ وَأَوَّلُ مُشَفَّعٍ وَلَا فَخْرُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Abdil-Hakam Al-Miswriy, ametusimulia Bakr bin Mudhwar, kutoka kwa Ja'far bin Rabiy'ah, kutoka kwa Swaalih — naye ni Ibn 'Atwaa bin Khabbaab, mwachwa huru wa Banuw Ad-Duil —, kutoka kwa 'Atwaa bin Abiy Rabaah, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi ni kiongozi wa Rusuli (عليهم السلام), wala si kujifakhiri; na mimi ni mwisho wa Manabii (عليهم السلام), wala si kujifakhiri; na mimi ni wa kwanza mwenye kuombea, na wa kwanza mwenye kukubaliwa uombezi, wala si kujifakhiri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
196
Hadiyth
50

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبَّادٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ هُوَ ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ ابْنِ جُدْعَانَ، عَنْ أَنَسٍ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "أَنَا أَوَّلُ مَنْ يَأْخُذُ بِحَلْقَةِ بَابِ الْجَنَّةِ فَأُقَعْقِعُهَا"، قَالَ أَنَسٌ: كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَى يَدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُحَرِّكُهَا، وَصَفَ لَنَا سُفْيَانُ كَذَا، وَجَمَعَ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ أَصَابِعَهُ وَحَرَّكَهَا، قَالَ: وَقَالَ لَهُ ثَابِتٌ: مَسَسْتَ يَدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِكَ؟، قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: فَأَعْطِنِيهَا أُقَبِّلْهَا

Ametusimulia Muhammad bin 'Abbaad, ametusimulia Sufyaan — naye ni Ibn 'Uyaynah —, kutoka kwa Ibn Jud'aan, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi ni wa kwanza atakayeshika kipete cha mlango wa Jannah (Pepo), nikigonge (kitoe sauti)." Anas (رضي الله عنه) akasema: Kama kwamba ninautazama mkono wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikitikisa. Sufyaan alitusifia hivi — na Abuw 'Abdi-Allaah akakusanya vidole vyake na akavitikisa. Akasema: Na Thaabit akamwambia: Je, uliugusa mkono wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa mkono wako? Akasema: Ndiyo. Akasema: Basi nipe (mkono huo) niubusu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
197
Hadiyth
51

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا حُسَيْنُ بْنُ عَلِيٍّ، عَنْ زَائِدَةَ، عَنْ الْمُخْتَارِ بْنِ فُلْفُلٍ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَا أَوَّلُ شَفِيعٍ فِي الْجَنَّةِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Husayn bin 'Aliy, kutoka kwa Zaaidah, kutoka kwa Al-Mukhtaar bin Fulful, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi ni muombezi wa kwanza katika Jannah (Pepo)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
197
Hadiyth
52

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ هُوَ ابْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْهَادِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي عَمْرٍو، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "إِنِّي لَأَوَّلُ النَّاسِ تَنْشَقُّ الْأَرْضُ عَنْ جُمْجُمَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا فَخْرُ، وَأُعْطَى لِوَاءَ الْحَمْدِ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا سَيِّدُ النَّاسِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا فَخْرُ، وَأَنَا أَوَّلُ مَنْ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا فَخْرُ، وَآتِي بَابَ الْجَنَّةِ فَآخُذُ بِحَلْقَتِهَا فَيَقُولُونَ: مَنْ هَذَا؟، فَأَقُولُ أَنَا مُحَمَّدٌ، فَيَفْتَحُونَ لِي فَأَدْخُلُ فَأَجِدُ الْجَبَّارَ مُسْتَقْبِلِي، فَأَسْجُدُ لَهُ، فَيَقُولُ: ارْفَعْ رَأْسَكَ يَا مُحَمَّدُ وَتَكَلَّمْ، يُسْمَعْ مِنْكَ، وَقُلْ، يُقْبَلْ مِنْكَ، وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ، فَأَرْفَعُ رَأْسِي، فَأَقُولُ: أُمَّتِي أُمَّتِي يَا رَبّ، فَيَقُولُ: اذْهَبْ إِلَى أُمَّتِكَ، فَمَنْ وَجَدْتَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِنْ شَعِيرٍ مِنْ الْإِيمَانِ، فَأَدْخِلْهُ الْجَنَّةَ، فَأَذْهَبُ، فَمَنْ وَجَدْتُ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالَ ذَلِكَ أَدْخَلْتُهُمْ الْجَنَّةَ، فَأَجِدُ الْجَبَّارَ مُسْتَقْبِلِي فَأَسْجُدُ لَهُ، فَيَقُولُ: ارْفَعْ رَأْسَكَ يَا مُحَمَّدُ وَتَكَلَّمْ، يُسْمَعْ مِنْكَ، وَقُلْ: يُقْبَلْ مِنْكَ، وَاشْفَعْ تُشَفَّعْ، فَأَرْفَعُ رَأْسِي فَأَقُولُ: أُمَّتِي أُمَّتِي يَا رَبِّ، فَيَقُولُ: اذْهَبْ إِلَى أُمَّتِكَ، فَمَنْ وَجَدْتَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِنْ خَرْدَلٍ مِنْ الْإِيمَانِ فَأَدْخِلْهُ الْجَنَّةَ، فَأَذْهَبُ، فَمَنْ وَجَدْتُ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالَ ذَلِكَ أَدْخَلْتُهُمْ الْجَنَّةَ، وَفُرِغَ مِنْ حِسَابِ النَّاسِ وَأُدْخِلَ مَنْ بَقِيَ مِنْ أُمَّتِي فِي النَّارِ مَعَ أَهْلِ النَّارِ، فَيَقُولُ أَهْلُ النَّارِ: مَا أَغْنَى عَنْكُمْ أَنَّكُمْ كُنْتُمْ تَعْبُدُونَ اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُونَ بِهِ شَيْئًا، فَيَقُولُ الْجَبَّارُ: فَبِعِزَّتِي لَأَعْتِقَنَّهُمْ مِنْ النَّارِ، فَيُرْسِلُ إِلَيْهِمْ، فَيَخْرُجُونَ مِنْ النَّارِ وَقَدْ امْتُحِشُوا، فَيُدْخَلُونَ فِي نَهَرِ الْحَيَاةِ، فَيَنْبُتُونَ فِيهِ كَمَا تَنْبُتُ الْحِبَّةُ فِي غُثَاءِ السَّيْلِ وَيُكْتَبُ بَيْنَ أَعْيُنِهِمْ هَؤُلَاءِ عُتَقَاءُ اللَّهِ، فَيُذْهَبُ بِهِمْ فَيَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ، فَيَقُولُ لَهُمْ أَهْلُ الْجَنَّةِ: هَؤُلَاءِ الْجَهَنَّمِيُّونَ، فَيَقُولُ الْجَبَّار: بَلْ هَؤُلَاءِ عُتَقَاءُ الْجَبَّارِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yaziyd — naye ni Ibn 'Abdi-Allaah bin Al-Haad —, kutoka kwa 'Amr bin Abiy 'Amr, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika mimi ni wa kwanza wa watu ambaye ardhi itapasuka kutoka kwenye fuvu langu la kichwa Siku ya Qiyaamah, wala si kujifakhiri; na nitapewa bendera ya Himdi, wala si kujifakhiri; na mimi ni bwana wa watu Siku ya Qiyaamah, wala si kujifakhiri; na mimi ni wa kwanza atakayeingia Jannah (Pepo) Siku ya Qiyaamah, wala si kujifakhiri. Nitaujia mlango wa Jannah, nikishike kipete chake; waseme: Ni nani huyu? Nitasema: Mimi ni Muhammad. Wanifungulie, niingie, nimkute Al-Jabbaar (Jabari Asiyeshindwa kufanya Atakalo) Akinielekea, nimsujudie. Aseme: Inua kichwa chako, yaa Muhammad, na zungumza, utasikilizwa; na sema, utakubaliwa; na ombea, utakubaliwa uombezi. Niinue kichwa changu, niseme: Ummah wangu! Ummah wangu! Yaa Rabbi! Aseme: Nenda kwa Ummah wako; utakayemkuta moyoni mwake kuna uzito wa punje ya shayiri ya imaan, mwingize Jannah. Niende; niliyemkuta moyoni mwake kuna uzito wa hicho, nimewaingiza Jannah. Kisha nimkute Al-Jabbaar Akinielekea, nimsujudie. Aseme: Inua kichwa chako, yaa Muhammad, na zungumza, utasikilizwa; na sema, utakubaliwa; na ombea, utakubaliwa uombezi. Niinue kichwa changu, niseme: Ummah wangu! Ummah wangu! Yaa Rabbi! Aseme: Nenda kwa Ummah wako; utakayemkuta moyoni mwake kuna uzito wa punje ya haradali ya imaan, mwingize Jannah. Niende; niliyemkuta moyoni mwake kuna uzito wa hicho, nimewaingiza Jannah. Na hesabu ya watu itakuwa imekwisha, na wale waliobakia katika Ummah wangu wataingizwa motoni pamoja na watu wa motoni. Watu wa motoni waseme: Haikukufaeni kitu kwamba mlikuwa mkimwabudu Allaah na hammshirikishi na chochote! Al-Jabbaar Aseme: Basi Naapa kwa Utukufu Wangu, hakika Nitawaacha huru kutoka motoni. Atume kwao, watoke motoni nao wamekwisha ungua; waingizwe katika mto wa uhai, waote humo kama inavyoota mbegu katika takataka zinazochukuliwa na mafuriko; na kuandikwe baina ya macho yao: Hawa ni walioachwa huru na Allaah. Wapelekwe, waingie Jannah. Watu wa Jannah wawaambie: Hawa ni watu wa Jahannam! Al-Jabbaar Aseme: Bali hawa ni walioachwa huru na Al-Jabbaar."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
198
Hadiyth
53

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي مُعَاوِيَةُ، عَنْ يُونُسَ بْنِ مَيْسَرَةَ، عَنْ أَبِي إِدْرِيسَ الْخَوْلَانِيِّ، عَنْ ابْنِ غَنْمٍ، قَالَ: "نَزَلَ جِبْرِيلُ عَلَيْهِ السَّلامُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَشَقَّ بَطْنَهُ، ثُمَّ قَالَ جِبْرِيلُ: قَلْبٌ وَكِيعٌ فِيهِ أُذُنَانِ سَمِيعَتَانِ وَعَيْنَانِ بَصِيرَتَانِ مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ الْمُقَفِّي، الْحَاشِرُ، خُلُقُكَ قَيِّمٌ، وَلِسَانُكَ صَادِقٌ، وَنَفْسُكَ مُطْمَئِنَّةٌ"، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: وَكِيعٌ يَعْنِي: شَدِيدًا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Mu'aawiyah, kutoka kwa Yuwnus bin Maysarah, kutoka kwa Abuw Idriys Al-Khawlaaniy, kutoka kwa Ibn Ghanm, amesema: "Jibriyl (عليه السلام) aliteremka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akapasua tumbo lake. Kisha Jibriyl (عليه السلام) akasema: Moyo madhubuti, ndani yake kuna masikio mawili yenye kusikia, na macho mawili yenye kuona. Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Rasuli wa Allaah, Al-Muqaffiy (aliyekuja kufuatia Manabii), Al-Haashir (Mkusanyaji): tabia yako ni iliyonyooka, na ulimi wako ni wa kweli, na nafsi yako ni iliyotua."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Wakiy' maana yake ni: madhubuti.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
199
Hadiyth
54

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي مُعَاوِيَةُ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ رُوَيْمٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ قَيْسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِنَّ اللَّهَ أَدْرَكَ بِيَ الْأَجَلَ الْمَرْحُومَ وَاخْتَصَرَ لِيَ اخْتِصَارًا فَنَحْنُ الْآخِرُونَ، وَنَحْنُ السَّابِقُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَإِنِّي قَائِلٌ قَوْلًا غَيْرَ فَخْرٍ: إِبْرَاهِيمُ خَلِيلُ اللَّهِ، وَمُوسَى صَفِيُّ اللَّهِ، وَأَنَا حَبِيبُ اللَّهِ، وَمَعِي لِوَاءُ الْحَمْدِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَإِنَّ اللَّهَ عز وجل وَعَدَنِي فِي أُمَّتِي وَأَجَارَهُمْ مِنْ ثَلَاثٍ: لَا يَعُمُّهُمْ بِسَنَةٍ، وَلَا يَسْتَأْصِلُهُمْ عَدُوٌّ، وَلَا يَجْمَعُهُمْ عَلَى ضَلَالَةٍ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Mu'aawiyah, kutoka kwa 'Urwah bin Ruwaym, kutoka kwa 'Amr bin Qays, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Amenifikishia muda uliorehemewa, na Amenifupishia ufupisho; basi sisi ndio wa mwisho, na sisi ndio watangulizi Siku ya Qiyaamah. Na hakika mimi ninasema kauli isiyo ya kujifakhiri: Ibraahiym (عليه السلام) ni Khaliyl (kipenzi mwandani) wa Allaah, na Muwsaa (عليه السلام) ni mteule wa Allaah, na mimi ni kipenzi wa Allaah; na pamoja nami iko bendera ya Himdi Siku ya Qiyaamah. Na hakika Allaah (عز وجل) Ameniahidi kuhusu Ummah wangu, na Amewalinda na mambo matatu: Hatawaenea (wote) kwa mwaka wa ukame, wala adui hatawang'oa (wote), wala Hatawakusanya juu ya upotofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
200
Hadiyth
55

9-Mlangoباب ما أكرم النبي صلى الله عليه وسلم بنزول الطعام من السماءMlango Wa Yale Aliyokirimiwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kwa Kuteremshiwa Chakula Kutoka Mbinguni

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا أَرْطَاةُ بْنُ الْمُنْذِرِ، عَنْ ضَمْرَةَ بْنِ حَبِيبٍ، قَالَ: سَمِعْتُ مَسْلَمَةَ السَّكُونِيَّ، وَقَالَ غَيْرُ مُحَمَّدٍ: سَلَمَةَ السَّكُونِيَّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذْ قَالَ قَائِلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلْ أُتِيتَ بِطَعَامٍ مِنْ السَّمَاءِ؟، قَالَ: "نَعَمْ أُتِيتُ بِطَعَامٍ"، قَالَ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، هَلْ كَانَ فِيهِ مِنْ فَضْلٍ؟، قَالَ: "نَعَمْ"، قَالَ: فَمَا فُعِلَ بِهِ؟، قَالِ: "رُفِعَ إِلَى السَّمَاءِ، وَقَدْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنِّي غَيْرُ لَابِثٍ فِيكُمْ إِلَّا قَلِيلًا، ثُمَّ تَلْبَثُونَ، حَتَّى تَقُولُوا: مَتَى مَتَى؟ ثُمَّ تَأْتُونِي أَفْنَادًا يُفْنِي بَعْضُكُمْ بَعْضًا، بَيْنَ يَدَيْ السَّاعَةِ مُوتَانٌ شَدِيدٌ، وَبَعْدَهُ سَنَوَاتُ الزَّلَازِلِ"

Ametusimulia Muhammad bin Al-Mubaarak, ametusimulia Mu'aawiyah bin Yahyaa, ametusimulia Artwaah bin Al-Mundhir, kutoka kwa Dhwamrah bin Habiyb, amesema: Nilimsikia Maslamah As-Sakuwniy (رضي الله عنه) — na asiyekuwa Muhammad amesema: Salamah As-Sakuwniy (رضي الله عنه) —, amesema: Tulipokuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ghafla msemaji mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, je, umeletewa chakula kutoka mbinguni? Akasema: "Ndiyo, nimeletewa chakula." Akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, je, kulikuwa na ziada ndani yake? Akasema: "Ndiyo." Akasema: Basi ilifanywa nini? Akasema: "Ilipandishwa mbinguni. Na nimefunuliwa Wahyi kwamba mimi sitakaa nanyi isipokuwa kidogo, kisha mtakaa mpaka mseme: Lini? Lini? Kisha mtanijia makundi makundi, mkiangamizana nyinyi kwa nyinyi. Kabla ya Saa (ya Qiyaamah) kutakuwa na vifo vingi vikali, na baada yake miaka ya matetemeko ya ardhi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
200
Hadiyth
56

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَخْبَرنَا سُلَيْمَانُ التَّيْمِيُّ، عَنْ أَبِي الْعَلَاءِ، عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أُتِيَ بِقَصْعَةٍ مِنْ ثَرِيدٍ"، فَوُضِعَتْ بَيْنَ يَدَيْ الْقَوْمِ، فَتَعَاقَبُوهَا إِلَى الظُّهْرِ مِنْ غُدْوَةٍ، يَقُومُ قَوْمٌ وَيَجْلِسُ آخَرُونَ، فَقَالَ رَجُلٌ لِسَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ: أَمَا كَانَتْ تُمَدُّ؟، فَقَالَ سَمُرَةُ: مِنْ أَيِّ شَيْءٍ تَعْجَبُ؟ مَا كَانَتْ تُمَدُّ إِلَّا مِنْ هَاهُنَا، وَأَشَارَ بِيَدِهِ إِلَى السَّمَاءِ

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametukhabarisha Sulaymaan At-Taymiy, kutoka kwa Abul-'Alaa, kutoka kwa Samurah bin Jundub (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliletewa bakuli kubwa la thariyd (mkate uliovunjwa ndani ya mchuzi), likawekwa mbele ya watu; wakawa wakipokezana (kula) kutoka asubuhi mpaka Adhuhuri: watu wanasimama na wengine wanaketi." Mtu mmoja akamwambia Samurah bin Jundub (رضي الله عنه): Je, (bakuli hilo) halikuwa likiongezewa (chakula)? Samurah (رضي الله عنه) akasema: "Kwa kitu gani unastaajabu? Halikuwa likiongezewa isipokuwa kutoka hapa," na akaashiria kwa mkono wake mbinguni.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
201
Hadiyth
57

10-Mlangoباب في حسن النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Uzuri Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَشْعَثَ بْنِ سَوَّارٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي لَيْلَةٍ إِضْحِيَانٍ، وَعَلَيْهِ حُلَّةٌ حَمْرَاءُ، فَجَعَلْتُ أَنْظُرُ إِلَيْهِ وَإِلَى الْقَمَرِ، قَالَ: فَلَهُوَ كَانَ أَحْسَنَ فِي عَيْنِي مِنْ الْقَمَرِ"

Ametusimulia Muhammad bin Sa'iyd, ametukhabarisha 'Abdur-Rahmaan bin Muhammad, kutoka kwa Ash'ath bin Sawwaar, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Jaabir bin Samurah (رضي الله عنهما), amesema: "Nilimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika usiku wenye mbalamwezi angavu, naye amevaa vazi jekundu (la vipande viwili). Nikawa ninamtazama yeye na ninautazama mwezi. Akasema: Basi hakika yeye alikuwa mzuri zaidi machoni mwangu kuliko mwezi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
202
Hadiyth
58

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ أَبِي ثَابِتٍ الزُّهْرِيُّ، حَدَّثَنِي إِسْمَاعِيلُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ ابْنُ أَخِي مُوسَى، عَنْ عَمِّهِ مُوسَى بْنِ عُقْبَةَ، عَنْ كُرَيْبٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَفْلَجَ الثَّنِيَّتَيْنِ، إِذَا تَكَلَّمَ رُئِيَ كَالنُّورِ يَخْرُجُ مِنْ بَيْنِ ثَنَايَاهُ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Abiy Thaabit Az-Zuhriy, amenisimulia Ismaa'iyl bin Ibraahiym, mtoto wa ndugu yake Muwsaa, kutoka kwa ami yake Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Kurayb, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa na mwanya kati ya meno yake mawili ya mbele; anapozungumza, huonekana kama nuru inayotoka kati ya meno yake ya mbele."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
203
Hadiyth
59

أَخْبَرَنَا مَحْمُودُ بْنُ غَيْلَانَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مِسْعَرٌ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: "مَا رَأَيْتُ أَحَدًا أَنْجَدَ، وَلَا أَجْوَدَ، وَلَا أَشْجَعَ، وَلَا أَضْوَأَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Mahmuwd bin Ghaylaan, ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Mis'ar, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, amesema: Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: "Sijapata kumuona yeyote aliye hodari zaidi (wa kusaidia), wala mkarimu zaidi, wala shujaa zaidi, wala mwenye kung'aa zaidi kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
203
Hadiyth
60

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمَّارِ بْنِ يَاسِرٍ، قَالَ: قُلْتُ: لِلرُّبَيِّعِ بِنْتِ مُعَوِّذِ ابْنِ عَفْرَاءَ: صِفِي لَنَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا بُنَيَّ "لَوْ رَأَيْتَهُ، رَأَيْتَ الشَّمْسَ طَالِعَةً"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir Al-Hizaamiy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, ametusimulia Usaamah bin Zayd, kutoka kwa Abuw 'Ubaydah bin Muhammad bin 'Ammaar bin Yaasir, amesema: Nilimwambia Ar-Rubayyi' bint Mu'awwidh bin 'Afraa (رضي الله عنها): Tueleze sifa za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Yaa mwanangu! "Lau ungemuona, ungeliona jua likichomoza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
203
Hadiyth
61

أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا ثَابِتٌ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَزْهَرَ اللَّوْنِ كَأَنَّ عَرَقَهُ اللُّؤْلُؤُ، إِذَا مَشَى تَكَفَّأَ، وَمَا مَسِسْتُ حَرِيرَةً وَلَا دِيبَاجَةً أَلْيَنَ مِنْ كَفِّهِ، وَلَا شَمِمْتُ رَائِحَةً قَطُّ أَطْيَبُ مِنْ رَائِحَتِهِ: مِسْكَةً وَلَا غَيْرَهَا"

Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa "mwenye rangi nyeupe ing'aayo; jasho lake kama lulu. Anapotembea, huinamia mbele (kwa nguvu). Na sijawahi kugusa hariri nyepesi wala hariri nzito iliyo laini zaidi kuliko kiganja chake; wala sijawahi kunusa harufu yoyote kamwe iliyo nzuri zaidi kuliko harufu yake": (si) miski wala (kitu) kingine.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
203
Hadiyth
62

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، أَنْبَأَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "خَدَمْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَا قَالَ لِي: أُفٍّ قَطُّ، وَلَا قَالَ لِي لِشَيْءٍ صَنَعْتُهُ: لِمَ صَنَعْتَ كَذَا وَكَذَا أَوْ هَلَّا صَنَعْتَ كَذَا وَكَذَا، وَقَالَ: لَا وَاللَّهِ مَا مَسِسْتُ بِيَدِي دِيبَاجًا، وَلَا حَرِيرًا أَلْيَنَ مِنْ يَدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَا وَجَدْتُ رِيحًا قَطُّ أَوْ عَرْفًا كَانَ أَطْيَبَ مِنْ عَرْفِ أَوْ رِيحِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametupa khabari Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: "Nilimtumikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); hakuwahi kuniambia: Uff (neno la kuchukizwa) kamwe; wala hakuniambia kwa jambo nililolifanya: Kwa nini umefanya hivi na hivi? au: Kwa nini hukufanya hivi na hivi? Na akasema: Hapana, Wa-Allaahi! Sijawahi kugusa kwa mkono wangu hariri nzito wala hariri nyepesi iliyo laini zaidi kuliko mkono wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); wala sijawahi kupata harufu yoyote kamwe — au: harufu nzuri — iliyokuwa nzuri zaidi kuliko harufu nzuri — au: harufu — ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
203
Hadiyth
63

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الرِّفَاعِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ خُدْرَةَ، حَدَّثَنِي رَجُلٌ مِنْ بَنِي حُرَيْشٍ، قَالَ: كُنْتُ مَعَ أَبِي حِينَ رَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَاعِزَ بْنَ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَلَمَّا أَخَذَتْهُ الْحِجَارَةُ أُرْعِبْتُ، "فَضَمَّنِي إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَسَالَ عَلَيَّ مِنْ عَرَقِ إِبْطِهِ مِثْلُ رِيحِ الْمِسْكِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Ar-Rifaa'iy, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Habiyb bin Khudrah, amenisimulia mtu mmoja wa Banuw Huraysh (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa pamoja na baba yangu wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipompiga mawe Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه). Mawe yalipoanza kumpata, nilitishika. "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanikumbatia kwake, na kukatiririka juu yangu katika jasho la kwapa lake (kitu) mfano wa harufu ya miski."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
205
Hadiyth
64

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْبَرَاءِ، قَالَ: سَأَلَهُ رَجُلٌ: أَرَأَيْتَ كَانَ وَجْهُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِثْلَ السَّيْفِ؟، قَالَ: "لَا، مِثْلَ الْقَمَرِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Baraa (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alimuuliza (Al-Baraa): Je, unaonaje, uso wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ulikuwa mfano wa upanga? Akasema: "Hapana, (bali) mfano wa mwezi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
205
Hadiyth
65

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يُعْرَفُ بِاللَّيْلِ بِرِيحِ الطِّيبِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitambulikana usiku kwa harufu ya manukato."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
205
Hadiyth
66

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ الْفَضْلِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْهَاشِمِيُّ، أَنْبَأَنَا الْمُغِيرَةُ بْنُ عَطِيَّةَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَمْ يَسْلُكْ طَرِيقًا أَوْ لَا يَسْلُكُ طَرِيقًا، فَيَتْبَعُهُ أَحَدٌ إِلَّا عَرَفَ أَنَّهُ قَدْ سَلَكَهُ مِنْ طِيبِ عَرْفِهِ"، أَوْ قَالَ: مِنْ رِيحِ عَرَقِهِ

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Is-haaq bin Al-Fadhwl bin 'Abdir-Rahmaan Al-Haashimiy, ametupa khabari Al-Mughiyrah bin 'Atwiyyah, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنهما): "Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupita njia yoyote — au: hapiti njia yoyote — kisha mtu akamfuata, ila hutambua kwamba yeye amepita hapo kutokana na uzuri wa harufu yake," au alisema: "kutokana na harufu ya jasho lake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
205
Hadiyth
67

11-Mlangoباب ما أكرم الله عز وجل به نبيه صلى الله عليه وسلم من كلام الموتىMlango Wa Yale
Ambayo Allaah (عز وجل) Amemkirimu Kwayo Nabiy
Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) Ya Kusemeshwa Na Vilivyokufa

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو اللَّيْثِيُّ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: يَأْكُلُ الْهَدِيَّةَ، وَلَا يَقْبَلُ الصَّدَقَةَ، فَأَهْدَتْ لَهُ امْرَأَةٌ مِنْ يَهُودِ خَيْبَرَ شَاةً مَصْلِيَّةً، فَتَنَاوَلَ مِنْهَا، وَتَنَاوَلَ مِنْهَا بِشْرُ بْنُ الْبَرَاءِ، ثُمَّ رَفَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّ هَذِهِ تُخْبِرُنِي أَنَّهَا مَسْمُومَةٌ"، فَمَاتَ بِشْرُ بْنُ الْبَرَاءِ فَأَرْسَلَ إِلَيْهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا حَمَلَكِ عَلَى مَا صَنَعْتِ؟"، فَقَالَتْ: إِنْ كُنْتَ نَبِيًّا لَمْ يَضُرَّكَ شَيْءٌ، وَإِنْ كُنْتَ مَلِكًا، أَرَحْتُ النَّاسَ مِنْكَ، فَقَالَ: فِي مَرَضِهِ: "مَا زِلْتُ مِنْ الْأَكْلَةِ الَّتِي أَكَلْتُ بِخَيْبَرَ، فَهَذَا أَوَانُ انْقِطَاعِ أَبْهَرِي"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr Al-Laythiy, kutoka kwa Abuw Salamah, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akila zawadi, na hakubali swadaka. Mwanamke mmoja miongoni mwa Mayahudi wa Khaybar akampa zawadi ya mbuzi aliyechomwa. Akala kidogo katika (nyama) yake, na Bishr bin Al-Baraa (رضي الله عنه) akala kidogo katika (nyama) yake. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akainua mkono wake, kisha akasema: "Hakika huyu (mbuzi) ananikhabarisha kwamba ametiwa sumu." Bishr bin Al-Baraa (رضي الله عنه) akafa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamtumia (mjumbe) yule mwanamke (akamuuliza): "Ni nini kilichokupelekea kufanya uliyoyafanya?" Akasema: Ikiwa wewe ni Nabiy, hakitakudhuru kitu; na ikiwa wewe ni mfalme, nitakuwa nimewapumzisha watu kutokana nawe. Akasema katika ugonjwa wake: "Sijaacha (kuhisi maumivu) kutokana na tonge nililolila Khaybar; basi huu ndio wakati wa kukatika kwa mshipa mkuu wa moyo wangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
207
Hadiyth
68

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبُ بْنُ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: كَانَ جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا يُحَدِّثُ، أَنَّ يَهُودِيَّةً مِنْ أَهْلِ خَيْبَرَ سَمَّتْ شَاةً مَصْلِيَّةً، ثُمَّ أَهْدَتْهَا إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَخَذَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الذِّرَاعَ فَأَكَلَ مِنْهَا، وَأَكَلَ الرَّهْطُ مِنْ أَصْحَابِهِ مَعَهُ، ثُمَّ قَالَ لَهُمْ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ارْفَعُوا أَيْدِيَكُمْ"، وَأَرْسَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْيَهُودِيَّةِ فَدَعَاهَا، فَقَالَ لَهَا: "أَسَمَمْتِ هَذِهِ الشَّاةَ؟"، فَقَالَتْ: نَعَمْ، وَمَنْ أَخْبَرَكَ؟، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَخْبَرَتْنِي هَذِهِ فِي يَدِيَ: لِلذِّرَاعِ"، فَقَالَتْ: نَعَمْ، قَالَ: "فَمَاذَا أَرَدْتِ إِلَى ذَلِكَ؟"، قَالَتْ: قُلْتُ: إِنْ كَانَ نَبِيًّا لَمْ يَضُرَّهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ نَبِيًّا، اسْتَرَحْنَا مِنْهُ، "فَعَفَا عَنْهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَمْ يُعَاقِبْهَا"، وَتُوُفِّيَ بَعْضُ أَصْحَابِهِ الَّذِينَ أَكَلُوا مِنْ الشَّاةِ، "وَاحْتَجَمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى كَاهِلِهِ مِنْ أَجْلِ الَّذِي أَكَلَ مِنْ الشَّاةِ"، حَجَمَهُ أَبُو هِنْدٍ مَوْلَى بَنِي بَيَاضَةَ، بِالْقَرْنِ وَالشَّفْرَةِ، وَهُوَ مِنْ بَنِي ثُمَامَةَ، وَهُمْ حَيٌّ مِنْ الْأَنْصَارِ

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) alikuwa akisimulia kwamba mwanamke mmoja Myahudi miongoni mwa watu wa Khaybar alimtia sumu mbuzi aliyechomwa, kisha akampa zawadi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akachukua mkono (wa mbele wa mbuzi), akala kutoka humo, na kikundi cha Swahaba (رضي الله عنهم) wake wakala pamoja naye. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Inueni mikono yenu." Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamtumia (mjumbe) yule mwanamke Myahudi, akamwita, akamwambia: "Je, umemtia sumu mbuzi huyu?" Akasema: Ndiyo; na ni nani aliyekukhabarisha? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Amenikhabarisha huu ulioko mkononi mwangu" — (akiashiria) mkono (wa mbuzi). Akasema: Ndiyo. Akasema: "Basi ulikusudia nini kwa hilo?" Akasema: Nilisema: Ikiwa ni Nabiy, haitamdhuru; na ikiwa si Nabiy, tutapumzika kutokana naye. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamsamehe, na hakumuadhibu. Na baadhi ya Swahaba (رضي الله عنهم) wake waliokula katika mbuzi yule wakafariki. Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaumikwa (akatolewa damu kwa chuku) juu ya sehemu ya juu ya mgongo wake kati ya mabega kwa sababu ya alichokula katika mbuzi yule. Aliyemuumika ni Abuw Hind (رضي الله عنه), mwachwa huru wa Banuw Bayaadhwah, kwa pembe na wembe; naye ni wa Banuw Thumaamah, nao ni ukoo miongoni mwa Answaar (رضي الله عنهم).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
208
Hadiyth
69

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي سَعِيدُ بْنُ أَبِي سَعِيدٍ الْمَقْبُرِيُّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: لَمَّا فُتِحَتْ خَيْبَرَ، أُهْدِيَتْ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَاةٌ فِيهَا سُمٌّ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اجْمَعُوا لِي مَنْ كَانَ هَاهُنَا مِنْ الْيَهُودِ"، فَجُمِعُوا لَهُ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنِّي سَائِلُكُمْ عَنْ شَيْءٍ فَهَلْ أَنْتُمْ صَادِقِيَّ عَنْهُ؟"، قَالُوا: نَعَمْ، يَا أَبَا الْقَاسِمِ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أَبُوكُمْ؟"، قَالُوا: أَبُونَا فُلَانٌ، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كَذَبْتُمْ، بَلْ أَبُوكُمْ فُلَانٌ"، قَالُوا: صَدَقْتَ وَبَرَرْتَ، فَقَالَ لَهُمْ: "هَلْ أَنْتُمْ صَادِقِيَّ عَنْ شَيْءٍ إِنْ سَأَلْتُكُمْ عَنْهُ؟"، فَقَالُوا: نَعَمْ، وَإِنْ كَذَبْنَاكَ، عَرَفْتَ كَذِبَنَا كَمَا عَرَفْتَهُ فِي أَبِينَا، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَمَنْ أَهْلُ النَّارِ؟"، فَقَالُوا: نَكُونُ فِيهَا يَسِيرًا ثُمَّ تَخْلِفُونَنَا فِيهَا، فَقَالَ لَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اخْسَؤُوا فِيهَا، وَاللَّهِ لَا نَخْلِفُكُمْ فِيهَا أَبَدًا"، ثُمَّ قَالَ لَهُمْ: "هَلْ أَنْتُمْ صَادِقِيَّ عَنْ شَيْءٍ إِنْ سَأَلْتُكُمْ عَنْهُ؟"، قَالُوا: نَعَمْ، قَالَ: "هَلْ جَعَلْتُمْ فِي هَذِهِ الشَّاةِ سُمًّا؟"، قَالُوا: نَعَمْ، قَالَ: "مَا حَمَلَكُمْ عَلَى ذَلِكَ؟"، قَالُوا: أَرَدْنَا إِنْ كُنْتَ كَاذِبًا أَنْ نَسْتَرِيحَ مِنْكَ، وَإِنْ كُنْتَ نَبِيًّا لَمْ يَضُرَّكَ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd Al-Maqburiy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Khaybar ilipofunguliwa (kwa ushindi), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipewa zawadi ya mbuzi ambaye ndani yake mna sumu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Nikusanyieni waliokuwa hapa miongoni mwa Mayahudi." Wakakusanywa kwake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Hakika mimi nitawauliza kuhusu jambo; je, mtanieleza ukweli kuhusu hilo?" Wakasema: Ndiyo, yaa Abal-Qaasim. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Baba yenu ni nani?" Wakasema: Baba yetu ni fulani. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Mmesema uongo; bali baba yenu ni fulani." Wakasema: Umesema kweli na umetenda wema. Akawaambia: "Je, mtanieleza ukweli kuhusu jambo nikiwauliza kuhusu hilo?" Wakasema: Ndiyo; na tukikuambia uongo, utautambua uongo wetu kama ulivyoutambua kuhusu baba yetu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Basi ni nani watu wa motoni?" Wakasema: Tutakuwa humo kwa muda mfupi, kisha mtatufuatia (mtakaa mahali petu) humo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Hizikeni humo! Wa-Allaahi, hatutakufuatieni humo kamwe." Kisha akawaambia: "Je, mtanieleza ukweli kuhusu jambo nikiwauliza kuhusu hilo?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Je, mmetia sumu katika mbuzi huyu?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Ni nini kilichowapelekea kufanya hivyo?" Wakasema: Tulitaka, ikiwa wewe ni muongo, tupumzike kutokana nawe; na ikiwa wewe ni Nabiy, haitakudhuru.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
209
Hadiyth
70

12-Mlangoباب في سخاء النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Ukarimu Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ ابْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "مَا سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا قَطُّ، فَقَالَ: لَا"، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: قَالَ ابْنُ عُيَيْنَةَ: إِذَا لَمْ يَكُنْ عِنْدَهُ وَعَدَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ibn Al-Munkadir, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuombwa kitu chochote kamwe, akasema: Hapana."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ibn 'Uyaynah amesema: Asipokuwa nacho, huahidi.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
211
Hadiyth
71

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ الطَّيَالِسِيُّ، عَنْ زَمْعَةَ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ، قَالَ: "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَيِيًّا، لَا يُسْأَلُ شَيْئًا إِلَّا أَعْطَاهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Abuw Daawuwd Atw-Twayaalisiy, kutoka kwa Zam'ah, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mwenye haya sana; haombwi kitu chochote ila hukitoa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
211
Hadiyth
72

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، قالَ: حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ رَجُلٍ مِنْ الْعَرَبِ، قَالَ: زَحَمْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ حُنَيْنٍ وَفِي رِجْلِي نَعْلٌ كَثِيفَةٌ، فَوَطِئْتُ بِهَا عَلَى رِجْلِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَنَفَحَنِي نَفْحَةً بِسَوْطٍ فِي يَدِهِ، وَقَالَ: "بِسْمِ اللَّهِ أَوْجَعْتَنِي"، قَالَ: فَبِتُّ لِنَفْسِي لَائِمًا، أَقُولُ: أَوْجَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَبِتُّ بِلَيْلَةٍ كَمَا يَعْلَمُ اللَّهُ، فَلَمَّا أَصْبَحْنَا، إِذَا رَجُلٌ يَقُولُ: أَيْنَ فُلَانٌ؟، قَالَ: قُلْتُ: هَذَا وَاللَّهِ الَّذِي كَانَ مِنِّي بِالْأَمْسِ، قَالَ: فَانْطَلَقْتُ وَأَنَا مُتَخَوِّفٌ، فَقَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّكَ وَطِئْتَ بِنَعْلِكَ عَلَى رِجْلِي بِالْأَمْسِ فَأَوْجَعْتَنِي، فَنَفَحْتُكَ نَفْحَةً بِالسَّوْطِ، فَهَذِهِ ثَمَانُونَ نَعْجَةً، فَخُذْهَا بِهَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Muhammad, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, amesema: Amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa mtu mmoja miongoni mwa Waarabu (رضي الله عنه), amesema: Nilisongamana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya (vita vya) Hunayn, na mguuni mwangu kulikuwa na kiatu kizito. Nikamkanyaga kwacho Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mguuni mwake. Akanipiga pigo (jepesi) kwa mjeledi uliokuwa mkononi mwake, na akasema: "Bismi-Allaah (Kwa Jina la Allaah)! Umeniumiza." Akasema: Nikalala usiku huo nikijilaumu, nikisema: Nimemuumiza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Nikalala usiku ambao Allaah Anajua (ulivyokuwa). Tulipoamka asubuhi, ghafla mtu mmoja akawa anasema: Yuko wapi fulani? Akasema: Nikasema: Hili, Wa-Allaahi, ni kwa sababu ya lile lililotokea kwangu jana. Akasema: Nikaenda nami nikiwa na hofu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaniambia: "Hakika wewe ulinikanyaga kwa kiatu chako mguuni mwangu jana ukaniumiza, nami nikakupiga pigo kwa mjeledi; basi hawa ni kondoo jike themanini, wachukue kwa ajili ya (pigo) hilo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
211
Hadiyth
73

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ ابْنِ أَخِي الزُّهْرِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: إِنَّ جِبْرِيلَ، قَالَ: "مَا فِي الْأَرْضِ أَهْلُ عَشَرَةِ أَبْيَاتٍ إِلَّا قَلَّبْتُهُمْ، فَمَا وَجَدْتُ أَحَدًا أَشَدَّ إِنْفَاقًا لِهَذَا الْمَالِ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Humayd, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa mtoto wa ndugu yake Az-Zuhriy, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Hakika Jibriyl (عليه السلام) amesema: "Hakuna katika ardhi watu wa nyumba kumi ila nimewageuza-geuza (nimewachunguza), na sikumkuta yeyote mwenye kutoa zaidi mali hii kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
212
Hadiyth
74

13-Mlangoباب في تواضع النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Unyenyekevu Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا الْفَضْلُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ وَاقِدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عُقَيْلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ الذِّكْرَ، وَيُقِلُّ اللَّغْوَ، وَيُطِيلُ الصَّلَاةَ، وَيُقْصِرُ الْخُطْبَةَ، وَلَا يَأْنَفُ وَلَا يَسْتَنْكِفُ أَنْ يَمْشِيَ مَعَ الْأَرْمَلَةِ وَالْمِسْكِينِ فَيَقْضِيَ لَهُمَا حَاجَتَهُمَا"

Ametusimulia Muhammad bin Humayd, ametusimulia Al-Fadhwl bin Muwsaa, ametusimulia Al-Husayn bin Waaqid, kutoka kwa Yahyaa bin 'Uqayl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Awfaa (رضي الله عنهما), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikithirisha kumdhukuru (Allaah), na akipunguza maneno yasiyo na faida, na akirefusha Swalaah, na akifupisha khutbah, na hakuwa akiona kinyongo wala akijiona mkubwa kutembea pamoja na mjane na masikini, akawatimizia haja yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
213
Hadiyth
75

14-Mlangoباب في وفاة النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Kufariki Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، أَنْبَأَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ: قَالَ الْعَبَّاسُ رِضْوَانُ اللَّهُ عَلَيْهِ: لَأَعْلَمَنَّ مَا بَقَاءُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِينَا؟، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أَرَاهُمْ قَدْ آذَوْكَ وَآذَاكَ غُبَارُهُمْ، فَلَوِ اتَّخَذْتَ عَرِيشًا تُكَلِّمُهُمْ مِنْهُ؟، فَقَالَ: "لَا أَزَالُ بَيْنَ أَظْهُرِهِمْ يَطَؤُونَ عَقِبِي، وَيُنَازِعُونِي رِدَائِي حَتَّى يَكُونَ اللَّهُ هُوَ الَّذِي يُرِيحُنِي مِنْهُمْ"، قَالَ: فَعَلِمْتُ أَنَّ بَقَاءَهُ فِينَا قَلِيلٌ

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametupa khabari Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa 'Ikrimah, amesema: Al-'Abbaas (رضوان الله عليه) amesema: Kwa hakika nitajua ni kwa muda gani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) atabaki pamoja nasi. Akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi ninawaona (watu) wamekuudhi, na vumbi lao limekuudhi; basi lau ungejitengenezea kibanda (cha kivuli) ukawa unawasemesha kutoka humo? Akasema: "Sitaacha kuwa kati yao, wakikanyaga visigino vyangu, na wakinivuta shuka yangu, mpaka Allaah Awe Ndiye Atakayenipumzisha kutokana nao." Akasema: Basi nikajua kwamba kubaki kwake pamoja nasi ni (kwa muda) mchache.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
213
Hadiyth
76

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ عَلِيٍّ، قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلَا نَحْجُبُكَ؟، فَقَالَ: "لَا، دَعُوهُمْ يَطَؤُونَ عَقِبِي وَأَطَأُ أَعْقَابَهُمْ حَتَّى يُرِيحَنِيَ اللَّهُ مِنْهُمْ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Daawuwd bin 'Aliy, amesema: Ilisemwa: Yaa Rasula-Allaah, je, tusikuwekee kizuizi (cha kukuzuilia watu)? Akasema: "Hapana; waacheni wakanyage visigino vyangu, nami nikanyage visigino vyao, mpaka Allaah Anipumzishe kutokana nao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
214
Hadiyth
77

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا حَاتِمُ بْنُ إِسْمَاعِيل، عَنْ أُنَيْسِ بْنِ أَبِي يَحْيَى، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: خَرَجَ عَلَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَرَضِهِ الَّذِي مَاتَ فِيهِ، وَنَحْنُ فِي الْمَسْجِدِ عَاصِبًا رَأْسَهُ بِخِرْقَةٍ حَتَّى أَهْوَى نَحْوَ الْمِنْبَرِ، فَاسْتَوَى عَلَيْهِ وَاتَّبَعْنَاهُ، قَالَ: "وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنِّي لَأَنْظُرُ إِلَى الْحَوْضِ مِنْ مَقَامِي هَذَا"، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّ عَبْدًا عُرِضَتْ عَلَيْهِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا، فَاخْتَارَ الْآخِرَةَ"، قَالَ: فَلَمْ يَفْطِنْ لَهَا أَحَدٌ غَيْرُ أَبِي بَكْرٍ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ فَذَرَفَتْ عَيْنَاهُ، فَبَكَى، ثُمَّ قَالَ: بَلْ نَفْدِيكَ بِآبَائِنَا وَأُمَّهَاتِنَا وَأَنْفُسِنَا وَأَمْوَالِنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: ثُمَّ هَبَطَ فَمَا قَامَ عَلَيْهِ حَتَّى السَّاعَةِ

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia Haatim bin Ismaa'iyl, kutoka kwa Unays bin Abiy Yahyaa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutokea katika ugonjwa wake ambao alifariki ndani yake, nasi tukiwa Msikitini, naye amefunga kichwa chake kwa kitambaa, mpaka akaelekea upande wa mimbari, akapanda juu yake na kutulia, nasi tukamfuata. Akasema: "Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Hakika mimi ninaliona Hawdhw (Hodhi lake la Siku ya Qiyaamah, linalopata maji kutoka mto wa Al-Kawthar) nikiwa mahali pangu hapa." Kisha akasema: "Hakika mja mmoja amehudhurishiwa dunia na mapambo yake, akachagua Aakhirah." Akasema: Hakuna yeyote aliyetambua (maana ya) hilo isipokuwa Abuw Bakr (رضوان الله عليه); macho yake yakatiririka machozi, akalia, kisha akasema: Bali tutakufidia kwa baba zetu, na mama zetu, na nafsi zetu, na mali zetu, yaa Rasula-Allaah. Akasema: Kisha akashuka, na hakusimama juu yake (tena) mpaka saa hii.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
215
Hadiyth
78

أَخْبَرَنَا خَلِيفَةُ بْنُ خَيَّاطٍ، حَدَّثَنَا بَكْرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ بْنِ عَلِيِّ بْنِ عَدِيٍّ، عَنْ عُبَيْدٍ مَوْلَى الْحَكَمِ بْنِ أَبِي الْعَاصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي مُوَيْهِبَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنِّي قَدْ أُمِرْتُ أَنْ أَسْتَغْفِرَ لِأَهْلِ الْبَقِيعِ، فَانْطَلِقْ مَعِي" فَانْطَلَقْتُ مَعَهُ فِي جَوْفِ اللَّيْلِ فَلَمَّا وَقَفَ عَلَيْهِمْ، قَالَ: "السَّلَامُ عَلَيْكُمْ يَا أَهْلَ الْمَقَابِرِ، لِيُهْنِكُمْ مَا أَصْبَحْتُمْ فِيهِ مِمَّا أَصْبَحَ فِيهِ النَّاسُ، لَوْ تَعْلَمُونَ مَا نَجَّاكُمُ اللَّهُ مِنْهُ، أَقْبَلَتْ الْفِتَنُ كَقِطْعِ اللَّيْلِ الْمُظْلِمِ يَتْبَعُ آخِرُهَا أَوَّلَهَا: الْآخِرَةُ أَشَرُّ مِنْ الْأُولَى"، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيَّ، فَقَالَ: "يَا أَبَا مُوَيْهِبَةَ إِنِّي قَدْ أُوتِيتُ بِمَفَاتِيحِ خَزَائِنِ الدُّنْيَا وَالْخُلْدَ فِيهَا، ثُمَّ الْجَنَّةُ، فَخُيِّرْتُ بَيْنَ ذَلِكَ وَبَيْنَ لِقَاءِ رَبِّي"، قُلْتُ: بِأَبِي أَنْتَ وَأُمِّي، خُذْ مَفَاتِيحَ خَزَائِنِ الدُّنْيَا وَالْخُلْدَ فِيهَا، ثُمَّ الْجَنَّةَ، قَالَ: "لَا وَاللَّهِ يَا أَبَا مُوَيْهِبَةَ لَقَدْ اخْتَرْتُ لِقَاءَ رَبِّي"، ثُمَّ اسْتَغْفَرَ لِأَهْلِ الْبَقِيعِ، ثُمَّ انْصَرَفَ، فَبُدِئَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِوَجَعِهِ الَّذِي مَاتَ فِيهِ

Ametukhabarisha Khaliyfah bin Khayyaatw, ametusimulia Bakr bin Sulaymaan, ametusimulia Ibn Is-haaq, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin 'Umar bin 'Aliy bin 'Adiyy, kutoka kwa 'Ubayd, mwachwa huru wa Al-Hakam bin Abil-'Aasw, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Abuw Muwayhibah (رضي الله عنه), mwachwa huru wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: "Hakika mimi nimeamrishwa niwaombee Maghfirah watu wa Al-Baqiy' (makaburi ya Madiynah); basi ondoka pamoja nami." Nikaondoka pamoja naye katikati ya usiku. Aliposimama kwao, akasema: "Amani iwe juu yenu, enyi watu wa makaburi! Iwe hongera kwenu hali mliyoamkia ndani yake kulinganisha na hali waliyoamkia ndani yake watu. Lau mngelijua yale Aliyokuokoeni nayo Allaah! Fitna zimekuja kama vipande vya usiku wenye giza, mwisho wake ukifuata mwanzo wake; ya mwisho ni shari zaidi kuliko ya kwanza." Kisha akanigeukia, akasema: "Yaa Abaa Muwayhibah, hakika mimi nimeletewa funguo za hazina za dunia na kudumu milele humo, kisha Jannah (Pepo); nikapewa khiyari kati ya hilo na kati ya kukutana na Rabb wangu." Nikasema: Baba yangu na mama yangu wawe fidia kwako! Chukua funguo za hazina za dunia na kudumu milele humo, kisha Jannah. Akasema: "Hapana, Wa-Allaahi, yaa Abaa Muwayhibah; hakika nimechagua kukutana na Rabb wangu." Kisha akawaombea Maghfirah watu wa Al-Baqiy', kisha akaondoka. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanzwa na maumivu yake ambayo alifariki ndani yake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
215
Hadiyth
79

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَبَّادِ بْنِ الْعَوَّامِ، عَنْ هِلَالِ بْنِ خَبَّابٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ ( إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ ) دَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاطِمَةَ، فَقَالَ: "قَدْ نُعِيَتْ إِلَيَّ نَفْسِي"، فَبَكَتْ، فَقَالَ: "لَا تَبْكِي، فَإِنَّكِ أَوَّلُ أَهْلِي لِحَاقًا بِي"، فَضَحِكَتْ، فَرَآهَا بَعْضُ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقُلْنَ: يَا فَاطِمَةُ، رَأَيْنَاكِ بَكَيْتِ ثُمَّ ضَحِكْتِ؟، قَالَتْ: إِنَّهُ أَخْبَرَنِي أَنَّهُ قَدْ نُعِيَتْ إِلَيْهِ نَفْسُهُ فَبَكَيْتُ، فَقَالَ لِي: "لَا تَبْكِي فَإِنَّكِ أَوَّلُ أَهْلِي لَاحِقٌ بِي"، فَضَحِكْتُ، وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ، وَجَاءَ أَهْلُ الْيَمَنِ"، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا أَهْلُ الْيَمَنِ؟ فَقَالَ: "هُمْ أَرَقُّ أَفْئِدَةً، وَالْإِيمَانُ يَمَانٍ، وَالْحِكْمَةُ يَمَانِيَةٌ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Abbaad bin Al-'Awwaam, kutoka kwa Hilaal bin Khabbaab, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Ilipoteremka:

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ

Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi. [An-Naswr (110:1)]

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwita Faatwimah (رضي الله عنها), akasema: "Nimetangaziwa kifo changu." Akalia. Akasema: "Usilie, kwani wewe ni wa kwanza katika watu wa nyumbani kwangu kunifuata." Akacheka. Baadhi ya wake (رضي الله عنهن) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwona, wakasema: Yaa Faatwimah, tumekuona ukilia kisha ukacheka? Akasema: Hakika yeye alinikhabarisha kwamba ametangaziwa kifo chake, nikalia; akaniambia: "Usilie, kwani wewe ni wa kwanza katika watu wa nyumbani kwangu atakayenifuata," nikacheka. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Imekuja Nusura ya Allaah na ushindi, na wamekuja watu wa Yemen." Mtu mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, na ni nani watu wa Yemen? Akasema: "Wao ni walio laini zaidi wa nyoyo; na Imaan ni ya Yemen, na hekima ni ya Yemen."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
216
Hadiyth
80

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ابْنِ إِسْحَاق، عَنْ يَعْقُوبَ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: رَجَعَ إِلَيَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ يَوْمٍ مِنْ جَنَازَةٍ مِنْ الْبَقِيعِ، فَوَجَدَنِي وَأَنَا أَجِدُ صُدَاعًا وَأَنَا أَقُولُ: وَا رَأْسَاهُ!، قَالَ: "بَلْ أَنَا يَا عَائِشَةُ وَا رَأْسَاهُ"، قَالَ: "وَمَا ضَرَّكِ لَوْ مِتِّ قَبْلِي فَغَسَّلْتُكِ وَكَفَّنْتُكِ وَصَلَّيْتُ عَلَيْكِ وَدَفَنْتُكِ؟"، فَقُلْتُ: لَكَأَنِّي بِكَ وَاللَّهِ لَوْ فَعَلْتُ ذَلِكَ لَرَجَعْتَ إِلَى بَيْتِي فَأَعْرَسْتَ فِيهِ بِبَعْضِ نِسَائِكَ، قَالَتْ: "فَتَبَسَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ثُمَّ بُدِئَ فِي وَجَعِهِ الَّذِي مَاتَ فِيهِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Muhammad bin Salamah, kutoka kwa Ibn Is-haaq, kutoka kwa Ya'quwb bin 'Utbah, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alirudi kwangu siku moja kutoka kwenye jeneza (huko) Al-Baqiy' (makaburi ya Madiynah), akanikuta nami nina maumivu ya kichwa, nami nikisema: Ole kichwa changu! Akasema: "Bali ni mimi, yaa 'Aaishah, ole kichwa changu!" Akasema: "Na ingekudhuru nini lau ungekufa kabla yangu, nikakuosha, na nikakukafini, na nikakuswalia, na nikakuzika?" Nikasema: Wa-Allaahi, ni kama kwamba ninakuona: lau ungefanya hivyo, ungerudi nyumbani kwangu ukafanya harusi humo na baadhi ya wake zako. Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatabasamu, kisha akaanzwa na maumivu yake ambayo alifariki ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
217
Hadiyth
81

أَخْبَرَنَا فَرْوَةُ بْنُ أَبِي الْمَغْرَاءِ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُخْتَارٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا، قَالَتْ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مَرَضِهِ: "صُبُّوا عَلَيَّ سَبْعَ قِرَبٍ مِنْ سَبْعِ آبَارٍ شَتَّى حَتَّى أَخْرُجَ إِلَى النَّاسِ فَأَعْهَدَ إِلَيْهِمْ"، قَالَ: فَأَقْعَدْنَاهُ فِي مِخْضَبٍ لِحَفْصَةَ فَصَبَبْنَا عَلَيْهِ الْمَاءَ صَبًّا أَوْ شَنَنَّا عَلَيْهِ شَنًّا، الشَّكُّ مِنْ قِبَلِ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، فَوَجَدَ رَاحَةً، فَخَرَجَ فَصَعِدَ الْمِنْبَرَ، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ وَاسْتَغْفَرَ لِلشُّهَدَاءِ مِنْ أَصْحَابِ أُحُدٍ، وَدَعَا لَهُمْ، ثُمَّ قَالَ: "أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ الْأَنْصَارَ عَيْبَتِي الَّتِي أَوَيْتُ إِلَيْهَا، فَأَكْرِمُوا كَرِيمَهُمْ، وَتَجَاوَزُوا عَنْ مُسِيئِهِمْ إِلَّا فِي حَدٍّ، أَلَا إِنَّ عَبْدًا مِنْ عِبَادِ اللَّهِ قَدْ خُيِّرَ بَيْنَ الدُّنْيَا وَبَيْنَ مَا عِنْدَ اللَّهِ، فَاخْتَارَ مَا عِنْدَ اللَّهِ"، فَبَكَى أَبُو بَكْرٍ، وَظَنَّ أَنَّهُ يَعْنِي نَفْسَهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَلَى رِسْلِكَ يَا أَبَا بَكْرٍ، سُدُّوا هَذِهِ الْأَبْوَابَ الشَّوَارِعَ إِلَى الْمَسْجِدِ إِلَّا بَابَ أَبِي بَكْرٍ، فَإِنِّي لَا أَعْلَمُ امْرَأً أَفْضَلَ عِنْدِي يَدًا فِي الصُّحْبَةِ مِنْ أَبِي بَكْرٍ"

Ametukhabarisha Farwah bin Abil-Maghraa, ametusimulia Ibraahiym bin Mukhtaar, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Muhammad bin Ka'b, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema katika ugonjwa wake: "Nimiminieni viriba saba (vya maji) kutoka visima saba tofauti, ili nitoke kwa watu niwausie." Akasema: Tukamketisha katika beseni la Hafswah (رضي الله عنها), tukammiminia maji kwa kumimina — au: tukammwagia kwa kunyunyiza; shaka ni kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq —, akapata nafuu. Akatoka, akapanda mimbari, akamhimidi Allaah na akamsifu, na akawaombea Maghfirah mashahidi miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa (vita vya) Uhud, na akawaombea Du'aa. Kisha akasema: "Ama baada ya hayo: Hakika Answaar ni wahifadhi wa siri zangu ambao nimekimbilia kwao; basi wakirimuni mtukufu wao, na mpuuzieni mkosaji wao, isipokuwa katika hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah). Tanabahini! Hakika mja mmoja miongoni mwa waja wa Allaah amepewa khiyari kati ya dunia na kati ya yaliyoko kwa Allaah, akachagua yaliyoko kwa Allaah." Abuw Bakr (رضي الله عنه) akalia, na akadhani kwamba anaikusudia nafsi yake. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Taratibu, yaa Abaa Bakr! Zibeni milango hii inayofunguka kuelekea Msikitini, isipokuwa mlango wa Abuw Bakr; kwani mimi simjui mtu aliye na fadhila zaidi kwangu katika usuhuba kuliko Abuw Bakr."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
218
Hadiyth
82

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا فُلَيْحُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: أُوذِنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالصَّلَاةِ فِي مَرَضِهِ، فَقَالَ: "مُرُوا أَبَا بَكْرٍ يُصَلِّي بِالنَّاسِ"، ثُمَّ أُغْمِيَ عَلَيْهِ، فَلَمَّا سُرِّيَ عَنْهُ، قَالَ: "هَلْ أَمَرْتُنَّ أَبَا بَكْرٍ يُصَلِّي بِالنَّاسِ؟"، فَقُلْتُ: إِنَّ أَبَا بَكْرٍ رَجُلٌ رَقِيقٌ، فَلَوْ أَمَرْتَ عُمَرَ، فَقَالَ: "أَنْتُنَّ صَوَاحِبُ يُوسُفَ مُرُوا أَبَا بَكْرٍ يُصَلِّي بِالنَّاسِ، فَرُبَّ قَائِلٍ مُتَمَنٍّ وَيَأْبَى اللَّهُ وَالْمُؤْمِنُونَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia Fulayh bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan, kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alijulishwa (kuwadia kwa) Swalaah katika ugonjwa wake. Akasema: "Mwamrisheni Abuw Bakr awaswalishe watu." Kisha akazimia. Alipozinduka, akasema: "Je, mmemwamrisha Abuw Bakr awaswalishe watu?" Nikasema: Hakika Abuw Bakr (رضي الله عنه) ni mtu mwenye moyo laini; lau ungemwamrisha 'Umar (رضي الله عنه)! Akasema: "Nyinyi ni (kama) wanawake wenzake Yuwsuf (عليه السلام)! Mwamrisheni Abuw Bakr awaswalishe watu; kwani huenda msemaji akawa ni mwenye kutamani, na Allaah na Waumini Wanakataa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
219
Hadiyth
83

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ: "تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ الِاثْنَيْنِ، فَحُبِسَ بَقِيَّةَ يَوْمِهِ وَلَيْلَتَهُ وَالْغَدَ حَتَّى دُفِنَ لَيْلَةَ الْأَرْبِعَاءِ، وَقَالُوا: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَمُتْ، وَلَكِنْ عُرِجَ بِرُوحِهِ كَمَا عُرِجَ بِرُوحِ مُوسَى، فَقَامَ عُمَرُ، فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَمُتْ، وَلَكِنْ عُرِجَ بِرُوحِهِ كَمَا عُرِجَ بِرُوحِ مُوسَى، وَاللَّهِ لَا يَمُوتُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى يَقْطَعَ أَيْدِيَ أَقْوَامٍ وَأَلْسِنَتَهُمْ، فَلَمْ يَزَلْ عُمَرُ يَتَكَلَّمُ حَتَّى أَزْبَدَ شِدْقَاهُ مِمَّا يُوعِدُ وَيَقُولُ، فَقَامَ الْعَبَّاسُ، فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ مَاتَ، وَإِنَّهُ لَبَشَرٌ وَإِنَّهُ يَأْسَنُ كَمَا يَأْسَنُ الْبَشَرُ، أَيْ قَوْمِ فَادْفِنُوا صَاحِبَكُمْ، فَإِنَّهُ أَكْرَمُ عَلَى اللَّهِ مِنْ أَنْ يُمِيتَهُ إِمَاتَتَيْنِ، أَيُمِيتُ أَحَدَكُمْ إِمَاتَةً وَيُمِيتُهُ إِمَاتَتَيْنِ وَهُوَ أَكْرَمُ عَلَى اللَّهِ مِنْ ذَلِكَ؟، أَيْ قَوْمِ، فَادْفِنُوا صَاحِبَكُمْ، فَإِنْ يَكُ كَمَا تَقُولُونَ فَلَيْسَ بِعَزِيزٍ عَلَى اللَّهِ أَنْ يَبْحَثَ عَنْهُ التُّرَابَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَاللَّهِ مَا مَاتَ حَتَّى تَرَكَ السَّبِيلَ نَهْجًا وَاضِحًا، فَأَحَلَّ الْحَلَالَ، وَحَرَّمَ الْحَرَامَ، وَنَكَحَ وَطَلَّقَ، وَحَارَبَ وَسَالَمَ، مَا كَانَ رَاعِي غَنَمٍ يَتَّبِعُ بِهَا صَاحِبُهَا رُءُوسَ الْجِبَالِ يَخْبِطُ عَلَيْهَا الْعِضَاهَ بِمِخْبَطِهِ وَيَمْدُرُ حَوْضَهَا بِيَدِهِ بِأَنْصَبَ وَلَا أَدْأَبَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، كَانَ فِيكُمْ، أَيْ قَوْمِ فَادْفِنُوا صَاحِبَكُمْ، قَالَ: وَجَعَلَتْ أُمُّ أَيْمَنَ تَبْكِي، فَقِيلَ لَهَا: يَا أُمَّ أَيْمَنَ تَبْكِينَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، قَالَتْ: إِنِّي وَاللَّهِ مَا أَبْكِي عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ لا أَكُونَ أَعْلَمُ أَنَّهُ قَدْ ذَهَبَ إِلَى مَا هُوَ خَيْرٌ لَهُ مِنْ الدُّنْيَا، وَلَكِنِّي أَبْكِي عَلَى خَبَرِ السَّمَاءِ انْقَطَعَ، قَالَ حَمَّادٌ: خَنَقَتِ الْعَبْرَةُ أَيُّوبَ حِينَ بَلَغَ هَاهُنَا"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa 'Ikrimah, amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki siku ya Jumatatu; akabakishwa (bila kuzikwa) muda uliobaki wa siku yake, na usiku wake, na kesho yake, mpaka akazikwa usiku wa (kuamkia) Jumatano." Na (watu) wakasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufariki, lakini roho yake imepandishwa kama ilivyopandishwa roho ya Muwsaa (عليه السلام). 'Umar (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufariki, lakini roho yake imepandishwa kama ilivyopandishwa roho ya Muwsaa (عليه السلام). Wa-Allaahi, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hatafariki mpaka akate mikono ya watu (fulani) na ndimi zao. 'Umar (رضي الله عنه) hakuacha kuzungumza mpaka pembe za mdomo wake zikatoa povu, kutokana na anayoyatishia na anayoyasema. Al-'Abbaas (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amefariki; na hakika yeye ni mwanaadam, na hakika (mwili wake) hubadilika kama wanavyobadilika wanaadam. Enyi watu! Basi mzikeni mwenzenu; kwani yeye ni mtukufu zaidi kwa Allaah kuliko Amfishe mara mbili. Je, Atamfisha mmoja wenu mara moja, na Amfishe yeye mara mbili, naye ni mtukufu zaidi kwa Allaah kuliko hivyo? Enyi watu! Basi mzikeni mwenzenu. Na ikiwa ni kama mnavyosema, basi si jambo zito kwa Allaah kumfukulia udongo. Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Wa-Allaahi, hakufariki mpaka alipoiacha njia (ya Dini) ikiwa wazi na bayana: alihalalisha halaal, na akaharamisha haraam, na akaoa na akataliki, na akapigana vita na akafanya amani. Hakuna mchungaji wa mbuzi na kondoo, ambaye mwenye nao huwapeleka vilele vya milima, akiwaangushia majani ya miti ya miiba kwa fimbo yake, na akilisiliba birika lao kwa mkono wake, aliyekuwa na taabu zaidi wala mwenye kudumu zaidi katika kazi kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa kati yenu. Enyi watu! Basi mzikeni mwenzenu. Akasema: Na Ummu Ayman (رضي الله عنها) akawa analia. Akaambiwa: Yaa Umma Ayman, unamlilia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Hakika mimi, Wa-Allaahi, simlilii Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa kuwa sijui kwamba ameenda kwenye kilicho bora zaidi kwake kuliko dunia; lakini ninalilia khabari ya mbinguni (Wahyi) iliyokatika. Hammaad amesema: Kilio kilimkaba Ayyuwb alipofika hapa.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
220
Hadiyth
84

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ بْنُ سَعِيدٍ الدِّمَشْقِيُّ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، وَحَدَّثَنِي يَعِيشُ بْنُ الْوَلِيدِ، حَدَّثَنِي مَكْحُولٌ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِذَا أَصَابَ أَحَدَكُمْ مُصِيبَةٌ فَلْيَذْكُرْ مُصِيبَتَهُ بِي فَإِنَّهَا مِنْ أَعْظَمِ الْمَصَائِبِ"

Ametukhabarisha 'Abdul-Wahhaab bin Sa'iyd Ad-Dimashqiy, ametusimulia Shu'ayb — naye ni Ibn Is-haaq —, ametusimulia Al-Awzaa'iy, na amenisimulia Ya'iysh bin Al-Waliyd, amenisimulia Mak-huwl, kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakapopatwa mmoja wenu na msiba, basi aukumbuke msiba wake kwangu, kwani huo ni miongoni mwa misiba mikubwa kabisa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
222
Hadiyth
85

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا فِطْرٌ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا أَصَابَ أَحَدَكُمْ مُصِيبَةٌ، فَلْيَذْكُرْ مُصَابَهُ بِي، فَإِنَّهَا مِنْ أَعْظَمِ الْمَصَائِبِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Fitwr, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakapopatwa mmoja wenu na msiba, basi aukumbuke msiba alioupata kwangu, kwani huo ni miongoni mwa misiba mikubwa kabisa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
222
Hadiyth
86

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عُمَرَ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "مَا سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ يَذْكُرُ النَّبِيَّ قَطُّ إِلَّا بَكَى"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Umar bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, amesema: "Sijapata kumsikia Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akimtaja Nabiy kamwe ila hulia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
222
Hadiyth
87

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ فَاطِمَةَ، قَالَتْ: يَا أَنَسُ "كَيْفَ طَابَتْ أَنْفُسُكُمْ أَنْ تَحْثُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ التُّرَابَ؟، وَقَالَتْ: يَا أَبَتَاهْ، مِنْ رَبِّهِ مَا أَدْنَاهْ، وَا أَبَتَاهْ جَنَّةُ الْفِرْدَوْسِ مَأْوَاهْ، وَا أَبَتَاهْ إِلَى جِبْرِيلَ نَنْعَاهْ، وَا أَبَتَاهْ أَجَابَ رَبًّا دَعَاهْ، قَالَ حَمَّادٌ: حِينَ حَدَّثَ ثَابِتٌ بَكَى، وَقَالَ ثَابِتٌ: حِينَ حَدَّثَ بِهِ أَنَسٌ بَكَى"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه): "Kwamba Faatwimah (رضي الله عنها) alisema: Yaa Anas, vipi nafsi zenu zimeridhika kummwagia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) udongo? Na akasema: Yaa baba yangu! Jinsi alivyo karibu na Rabb wake! Yaa baba yangu! Jannah (Pepo) ya Al-Firdaws ndio makazi yake! Yaa baba yangu! Kwa Jibriyl (عليه السلام) tunamtangazia kifo chake! Yaa baba yangu! Amemuitikia Rabb Aliyemwita!" Hammaad amesema: Thaabit aliposimulia, alilia. Na Thaabit amesema: Anas (رضي الله عنه) alipoisimulia, alilia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
223
Hadiyth
88

حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، وَذَكَرَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "شَهِدْتُهُ يَوْمَ دَخَلَ الْمَدِينَةَ فَمَا رَأَيْتُ يَوْمًا قَطُّ، كَانَ أَحْسَنَ وَلَا أَضْوَأَ مِنْ يَوْمٍ دَخَلَ عَلَيْنَا فِيهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَشَهِدْتُهُ يَوْمَ مَوْتِهِ، فَمَا رَأَيْتُ يَوْمًا كَانَ أَقْبَحَ، وَلَا أَظْلَمَ مِنْ يَوْمٍ مَاتَ فِيهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), naye alimtaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Nilimshuhudia siku alipoingia Madiynah; sikuwahi kuona siku yoyote kamwe iliyokuwa nzuri zaidi wala yenye mwangaza zaidi kuliko siku aliyoingia kwetu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Na nilimshuhudia siku ya kufariki kwake; sikuwahi kuona siku iliyokuwa mbaya zaidi wala yenye giza zaidi kuliko siku aliyofariki Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
223
Hadiyth
89

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُطِيعٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ أَبِي عَبْدِ الْجَلِيلِ، عَنْ أَبِي حَرِيزٍ الْأَزْدِيِّ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَلَامٍ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا نَجِدُكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ قَائِمًا عِنْدَ رَبِّكَ وَأَنْتَ مُحْمَارَّةٌ وَجْنَتَاكَ مُسْتَحْيٍ مِنْ رَبِّكَ مِمَّا أَحْدَثَتْ أُمَّتُكَ مِنْ بَعْدِكَ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Mutwiy', ametusimulia Hushaym, kutoka kwa Abuw 'Abdil-Jaliyl, kutoka kwa Abuw Hariyz Al-Azdiy, amesema: 'Abdu-Allaah bin Salaam (رضي الله عنه) alimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): "Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tunakukuta Siku ya Qiyaamah ukiwa umesimama kwa Rabb wako, nawe mashavu yako yamekuwa mekundu, ukimuonea haya Rabb wako kwa yale ambayo Ummah wako umeyazusha baada yako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
223
Hadiyth
90

أَخْبَرَنَا الْقَاسِمُ بْنُ كَثِيرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ شُرَيْحٍ يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِي الْأَسْوَدِ الْقُرَشِيِّ، عَنْ أَبِي قُرَّةَ مَوْلَى أَبِي جَهْلٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ هَذِهِ السُّورَةَ لَمَّا أُنْزِلَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ {إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا}، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَيَخْرُجُنَّ مِنْهُ أَفْوَاجًا كَمَا دَخَلُوهُ أَفْوَاجًا"

Ametukhabarisha Al-Qaasim bin Kathiyr, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Shurayh akisimulia, kutoka kwa Abul-Aswad Al-Qurashiy, kutoka kwa Abuw Qurrah, mwachwa huru wa Abuw Jahl, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kwamba Suwrah hii ilipoteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم):

إِذَا جَاءَ نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا

Itakapokuja Nusura ya Allaah na ushindi. Na ukawaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah makundi makundi. [An-Naswr (110:1-2)]

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: "Kwa hakika watatoka humo makundi makundi kama walivyoingia humo makundi makundi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
223
Hadiyth
91

أَخْبَرَنِي أَبُو بَكْرٍ الْمِصْرِيُّ، عَنْ سُلَيْمَانَ أَبِي أَيُّوبَ الْخُزَاعِيِّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ الْأُمَوِيِّ، عَنْ مَعْرُوفِ بْنِ خَرَّبُوذَ الْمَكِّيِّ، عَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ، قَالَ: "دَخَلَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْأَهْتَمِ عَلَى عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ مَعَ الْعَامَّةِ فَلَمْ يُفْجَأْ عُمَرُ إِلَّا وَهُوَ بَيْنَ يَدَيْهِ يَتَكَلَّمُ، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: أَمَّا بَعْدُ، فَإِنَّ اللَّهَ خَلَقَ الْخَلْقَ غَنِيًّا عَنْ طَاعَتِهِمْ، آمِنًا لِمَعْصِيَتِهِمْ، وَالنَّاسُ يَوْمَئِذٍ فِي الْمَنَازِلِ وَالرَّأْيِ مُخْتَلِفُونَ، فَالْعَرَبُ بِشَرِّ تِلْكَ الْمَنَازِلِ: أَهْلُ الْحَجَرِ، وَأَهْلُ الْوَبَرِ، وَأَهْلُ الدَّبَرِ، تُجْتَازُ دُونَهُمْ طَيِّبَاتُ الدُّنْيَا وَرَخَاءُ عَيْشِهَا، لَا يَسْأَلُونَ اللَّهَ جَمَاعَةً، وَلَا يَتْلُونَ لَهُ كِتَابًا، مَيِّتُهُمْ فِي النَّارِ، وَحَيُّهُمْ أَعْمَى نَجِسٌ مَعَ مَا لَا يُحْصَى مِنْ الْمَرْغُوبِ عَنْهُ، وَالْمَزْهُودِ فِيهِ، فَلَمَّا أَرَادَ اللَّهُ أَنْ يَنْشُرَ عَلَيْهِمْ رَحْمَتَهُ، بَعَثَ إِلَيْهِمْ رَسُولًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ، وَعَلَيْهِ السَّلَامُ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، فَلَمْ يَمْنَعْهُمْ ذَلِكَ أَنْ جَرَحُوهُ فِي جِسْمِهِ وَلَقَّبُوهُ فِي اسْمِهِ، وَمَعَهُ كِتَابٌ مِنْ اللَّهِ نَاطِقٌ، لَا يُقُومُ إِلَّا بِأَمْرِهِ، وَلَا يُرْحَلُ إِلَّا بِإِذْنِهِ، فَلَمَّا أُمِرَ بِالْعَزْمَةِ، وَحُمِلَ عَلَى الْجِهَادِ، انْبَسَطَ لِأَمْرِ اللَّهِ لَوْثُهُ، فَأَفْلَجَ اللَّهُ حُجَّتَهُ، وَأَجَازَ كَلِمَتَهُ، وَأَظْهَرَ دَعْوَتَهُ، وَفَارَقَ الدُّنْيَا تَقِيًّا نَقِيًّا، ثُمَّ قَامَ بَعْدَهُ أَبُو بَكْرٍ فَسَلَكَ سُنَّتَهُ، وَأَخَذَ سَبِيلَهُ، وَارْتَدَّتْ الْعَرَبُ أَوْ مَنْ فَعَلَ ذَلِكَ مِنْهُمْ، فَأَبَى أَنْ يَقْبَلَ مِنْهُمْ بَعْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا الَّذِي كَانَ قَابِلًا، انْتَزَعَ السُّيُوفَ مِنْ أَغْمَادِهَا، وَأَوْقَدَ النِّيرَانَ فِي شُعُلِهَا، ثُمَّ نَكِبَ بِأَهْلِ الْحَقِّ أَهْلَ الْبَاطِلِ، فَلَمْ يَبْرَحْ يُقَطِّعُ أَوْصَالَهُمْ، وَيَسْقِي الْأَرْضَ دِمَاءَهُمْ، حَتَّى أَدْخَلَهُمْ فِي الَّذِي خَرَجُوا مِنْهُ، وَقَرَّرَهُمْ بِالَّذِي نَفَرُوا عَنْهُ، وَقَدْ كَانَ أَصَابَ مِنْ مَالِ اللَّهِ بَكْرًا، يَرْتَوِي عَلَيْهِ، وَحَبَشِيَّةً أَرْضَعَتْ وَلَدًا لَهُ، فَرَأَى ذَلِكَ عِنْدَ مَوْتِهِ غُصَّةً فِي حَلْقِهِ، فَأَدَّى ذَلِكَ إِلَى الْخَلِيفَةِ مِنْ بَعْدِهِ، وَفَارَقَ الدُّنْيَا تَقِيًّا نَقِيًّا عَلَى مِنْهَاجِ صَاحِبِهِ، ثُمَّ قَامَ بَعْدَهُ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ، فَمَصَّرَ الْأَمْصَارَ، وَخَلَطَ الشِّدَّةَ بِاللِّينِ، وَحَسَرَ عَنْ ذِرَاعَيْهِ، وَشَمَّرَ عَنْ سَاقَيْهِ وَعَدَّ لِلْأُمُورِ أَقْرَانَهَا، وَلِلْحَرْبِ آلَتَهَا، فَلَمَّا أَصَابَهُ فَتَي الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، أَمَرَ ابْنَ عَبَّاسٍ يَسْأَلُ النَّاسَ: هَلْ يُثْبِتُونَ قَاتِلَهُ: فَلَمَّا قِيلَ: فَتَي الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، اسْتَهَلَّ يَحْمَدُ رَبَّهُ أَنْ لَا يَكُونَ أَصَابَهُ ذُو حَقٍّ فِي الْفَيْءِ فَيَحْتَجَّ عَلَيْهِ بِأَنَّهُ إِنَّمَا اسْتَحَلَّ دَمَهُ بِمَا اسْتَحَلَّ مِنْ حَقِّهِ، وَقَدْ كَانَ أَصَابَ مِنْ مَالِ اللَّهِ بِضْعَةً وَثَمَانِينَ أَلْفًا، فَكَسَرَ لَهَا رِبَاعَهُ وَكَرِهَ بِهَا كَفَالَةَ أَوْلَادِهِ، فَأَدَّاهَا إِلَى الْخَلِيفَةِ مِنْ بَعْدِهِ، وَفَارَقَ الدُّنْيَا تَقِيًّا نَقِيًّا عَلَى مِنْهَاجِ صَاحِبَيْهِ، ثُمَّ إِنَّكَ يَا عُمَرُ بُنَيُّ الدُّنْيَا وَلَّدَتْكَ مُلُوكُهَا، وَأَلْقَمَتْكَ ثَدْيَيْهَا، وَنَبَتَّ فِيهَا تَلْتَمِسُهَا مَظَانَّهَا، فَلَمَّا وُلِيتَهَا أَلْقَيْتَهَا حَيْثُ أَلْقَاهَا اللَّهُ، هَجَرْتَهَا وَجَفَوْتَهَا، وَقَذِرْتَهَا إِلَّا مَا تَزَوَّدْتَ مِنْهَا، فَالْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي جَلَا بِكَ حَوْبَتَنَا وَكَشَفَ بِكَ كُرْبَتَنَا، فَامْضِ وَلَا تَلْتَفِتْ، فَإِنَّهُ لَا يَعِزُّ عَلَى الْحَقِّ شَيْءٌ، وَلَا يَذِلُّ عَلَى الْبَاطِلِ شَيْءٌ، أَقُولُ قَوْلِي هَذَا، وَأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ لِي وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ"، قَالَ أَبُو أَيُّوبَ: فَكَانَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، يَقُولُ فِي الشَّيْءِ: قَالَ لِيَ ابْنُ الْأَهْتَمِ: امْضِ وَلَا تَلْتَفِتْ

Amenikhabarisha Abuw Bakr Al-Miswriy, kutoka kwa Sulaymaan Abuw Ayyuwb Al-Khuzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd Al-Umawiy, kutoka kwa Ma'ruwf bin Kharrabuwdh Al-Makkiy, kutoka kwa Khaalid bin Ma'daan, amesema: "'Abdu-Allaah bin Al-Ahtam aliingia kwa 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz pamoja na watu wa kawaida; 'Umar hakushtukia ila (kumwona) yuko mbele yake akizungumza. Akamhimidi Allaah na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo: Hakika Allaah Ameumba viumbe Akiwa Hahitaji utiifu wao, na Akiwa Hana khofu kutokana na maasi yao. Na watu siku hizo walikuwa wametofautiana katika daraja zao na katika rai zao; na Waarabu walikuwa katika daraja ovu kabisa kati ya hizo: watu wa (makazi ya) mawe, na watu wa (mahema ya) manyoya ya ngamia, na watu wa ad-dabar (vidonda vya migongo ya ngamia); mazuri ya dunia na raha ya maisha yake yanapita mbali nao (bila kuwafikia). Hawamuombi Allaah wakiwa jamaa moja, wala hawamsomei kitabu chochote; maiti wao yuko motoni, na aliye hai miongoni mwao ni kipofu, najisi; pamoja na yasiyohesabika miongoni mwa mambo ya kuchukiza na ya kudharauliwa. Allaah Alipotaka Kuwaenezea Rehma Yake, Aliwatumia Rasuli anayetokana na wao wenyewe, yanamtia mashaka (na huzuni) yanayokutaabisheni, anakujalini, kwa Waumini ni mwenye huruma mno, mwenye rehma (صلى الله عليه وآله وسلم), na juu yake iwe amani na Rehma ya Allaah na Baraka Zake. Hilo halikuwazuia kumjeruhi mwilini mwake na kumbandikia majina mabaya katika jina lake. Na pamoja naye kulikuwa na Kitabu kutoka kwa Allaah kinachotamka; hasimami ila kwa Amri Yake, wala haondoki ila kwa Idhini Yake. Alipoamrishwa kuazimia (kupigana), na akabebeshwa jihaad, nguvu zake zikakunjuka kwa ajili ya Amri ya Allaah; Allaah Akaipa ushindi hoja yake, na Akalipitisha neno lake, na Akaidhihirisha da'wah yake; na akaiacha dunia akiwa mwenye kumkhofu Allaah, msafi. Kisha akasimama baada yake Abuw Bakr (رضي الله عنه); akaifuata Sunnah yake, na akashika njia yake. Na Waarabu wakaritadi — au wale waliofanya hivyo miongoni mwao —; akakataa kukubali kutoka kwao, baada ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), isipokuwa yale aliyokuwa (Rasuli) akiyakubali. Akazichomoa panga kutoka kwenye ala zake, na akaiwasha mioto katika mienge yake; kisha akawapiga watu wa batili kwa watu wa haki. Hakuacha kukata viungo vyao, na kuinywesha ardhi damu zao, mpaka akawaingiza katika yale waliyotoka, na akawathibitisha juu ya yale waliyoyakimbia. Na alikuwa amepata kutoka katika mali ya Allaah ngamia mchanga aliyekuwa akitekea maji kwake, na mjakazi wa Kihabeshi aliyemnyonyesha mtoto wake; akaliona hilo wakati wa kufariki kwake kama donge kooni mwake, akalirudisha hilo kwa khalifa wa baada yake. Na akaiacha dunia akiwa mwenye kumkhofu Allaah, msafi, juu ya njia ya sahibu yake. Kisha akasimama baada yake 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه); akaianzisha miji mikubwa, na akachanganya ukali na ulaini, na akapandisha (mikono ya nguo) kutoka kwenye mikono yake, na akapandisha (nguo) kutoka kwenye miundi yake, na akayaandalia mambo yanayolingana nayo, na vita zana zake. Alipopigwa na kijana wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه), alimwamrisha Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) awaulize watu: Je, wanamtambua muuaji wake? Ilipoambiwa: Ni kijana wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah, alianza kumhimidi Rabb wake kwamba aliyempiga hakuwa mtu mwenye haki katika Fay-u (mali inayopatikana bila ya vita), ambaye angemtolea hoja kwamba yeye amehalalisha damu yake kwa sababu tu ('Umar) aliihalalisha haki yake. Na alikuwa amepata kutoka katika mali ya Allaah (dirham) elfu themanini na kitu; akauza nyumba zake kwa ajili yake, na akachukia kuwatwika watoto wake dhamana yake; akaitoa kwa khalifa wa baada yake. Na akaiacha dunia akiwa mwenye kumkhofu Allaah, msafi, juu ya njia ya sahibu zake wawili. Kisha wewe, yaa 'Umar, ni mwana mdogo wa dunia: wafalme wake ndio waliokuzaa, na imekunyonyesha matiti yake mawili, na umekulia ndani yake ukiitafuta mahali inapotarajiwa kupatikana. Ulipopewa utawala wake, uliitupa pale ambapo Allaah Ameitupa; ukaihama, ukaiepuka, na ukaiona chafu, isipokuwa kile ulichojichukulia kama masurufu kutoka humo. Basi Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ameondoa kupitia kwako dhambi yetu, na Ameondoa kupitia kwako dhiki yetu. Basi endelea mbele wala usigeuke (nyuma); kwani hakika hakuna kitu kilicho kigumu kwa haki, wala hakuna kitu kinachodhalilika kwa batili. Nasema kauli yangu hii, na ninamuomba Allaah Maghfirah kwa ajili yangu na kwa ajili ya Waumini wanaume na Waumini wanawake." Abuw Ayyuwb amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz alikuwa akisema kuhusu jambo (fulani): Ibn Al-Ahtam aliniambia: Endelea mbele wala usigeuke.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
225
Hadiyth
92

15-Mlangoباب ما أكرم الله تعالى نبيه صلى الله عليه وسلم بعد موتهMlango Wa Yale Ambayo Allaah (تعالى)
Amemkirimu Kwayo Nabiy Wake (صلى الله عليه وآله وسلم)
Baada Ya Kufariki Kwake

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ مَالِكٍ النُّكْرِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو الْجَوْزَاءِ أَوْسُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "قَحَطَ أَهْلُ الْمَدِينَةِ قَحْطًا شَدِيدًا، فَشَكَوْا إِلَى عَائِشَةَ، فَقَالَتْ: انْظُرُوا قَبْرَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَاجْعَلُوا مِنْهُ كُوًى إِلَى السَّمَاءِ حَتَّى لَا يَكُونَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ السَّمَاءِ سَقْفٌ، قَالَ: فَفَعَلُوا، فَمُطِرْنَا مَطَرًا حَتَّى نَبَتَ الْعُشْبُ، وَسَمِنَتِ الْإِبِلُ حَتَّى تَفَتَّقَتْ مِنْ الشَّحْمِ، فَسُمِّيَ عَامَ الْفَتْقِ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Sa'iyd bin Zayd, ametusimulia 'Amr bin Maalik An-Nukriy, ametusimulia Abul-Jawzaa Aws bin 'Abdi-Allaah, amesema: Watu wa Madiynah walipatwa na ukame mkali; wakamshtakia 'Aaishah (رضي الله عنها). Akasema: "Litazameni kaburi la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mlitobolee matundu kuelekea mbinguni, mpaka pasiwe kati yake na mbingu dari." Akasema: Wakafanya (hivyo); tukanyeshewa mvua mpaka majani yakaota, na ngamia wakanenepa mpaka wakapasuka kwa mafuta; ukaitwa mwaka wa Al-Fatq (kupasuka).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
227
Hadiyth
93

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ، قَالَ: "لَمَّا كَانَ أَيَّامُ الْحَرَّةِ لَمْ يُؤَذَّنْ فِي مَسْجِدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلَاثًا، وَلَمْ يُقَمْ وَلَمْ يَبْرَحْ سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ الْمَسْجِدِ، وَكَانَ لَا يَعْرِفُ وَقْتَ الصَّلَاةِ إِلَّا بِهَمْهَمَةٍ يَسْمَعُهَا مِنْ قَبْرِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"، فَذَكَرَ مَعْنَاهُ

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, kutoka kwa Sa'iyd bin 'Abdil-'Aziyz, amesema: "Zilipokuwa siku za Al-Harrah (vita vilivyopiganwa Madiynah), haikuadhiniwa katika Msikiti wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (siku) tatu, wala haikukimiwa (Iqaamah); na Sa'iyd bin Al-Musayyib hakuondoka Msikitini, na alikuwa hajui wakati wa Swalaah ila kwa sauti ya chini aliyokuwa akiisikia kutoka kaburi la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)." Kisha akataja maana yake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
227
Hadiyth
94

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي خَالِدٌ هُوَ ابْنُ يَزِيدَ، عَنْ سَعِيدٍ هُوَ ابْنُ أَبِي هِلَالٍ، عَنْ نُبَيْهِ بْنِ وَهْبٍ، أَنَّ كَعْبًا دَخَلَ عَلَى عَائِشَةَ، فَذَكَرُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ كَعْبٌ: "مَا مِنْ يَوْمٍ يَطْلُعُ إِلَّا نَزَلَ سَبْعُونَ أَلْفًا مِنْ الْمَلَائِكَةِ، حَتَّى يَحُفُّوا بِقَبْرِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَضْرِبُونَ بِأَجْنِحَتِهِمْ، وَيُصَلُّونَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى إِذَا أَمْسَوْا، عَرَجُوا وَهَبَطَ مِثْلُهُمْ، فَصَنَعُوا مِثْلَ ذَلِكَ حَتَّى إِذَا انْشَقَّتْ عَنْهُ الْأَرْضُ، خَرَجَ فِي سَبْعِينَ أَلْفًا مِنْ الْمَلَائِكَةِ يَزِفُّونَهُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Khaalid — naye ni Ibn Yaziyd —, kutoka kwa Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Hilaal —, kutoka kwa Nubayh bin Wahb, kwamba Ka'b aliingia kwa 'Aaishah (رضي الله عنها); wakamtaja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Ka'b akasema: "Hakuna siku inayochomoza ila huteremka Malaika (عليهم السلام) elfu sabini mpaka wanalizunguka kaburi la Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakipiga mbawa zao, na wakimswalia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); mpaka wanapoingia jioni hupanda juu, na hushuka mfano wao, nao hufanya mfano wa hayo. Mpaka ardhi itakapopasuka kutoka kwake, atatoka katika (msafara wa) Malaika (عليهم السلام) elfu sabini wakimsindikiza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
228
Hadiyth
95

16-Mlangoباب اتباع السنةMlango Wa Kuifuata Sunnah

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، أَنْبَأَنَا ثَوْرُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنِي خَالِدُ بْنُ مَعْدَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ عِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الْفَجْرِ، ثُمَّ وَعَظَنَا مَوْعِظَةً بَلِيغَةً ذَرَفَتْ مِنْهَا الْعُيُونُ، وَوَجِلَتْ مِنْهَا الْقُلُوبُ، فَقَالَ قَائِلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ؟ فَأَوْصِنَا، فَقَالَ: "أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإِنْ كَانَ عَبْدًا حَبَشِيًّا، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافًا كَثِيرًا، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسَنَّةِ الْخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ الْمَهْدِيِّينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ وَإِيَّاكُمْ وَالْمُحْدَثَاتِ، فَإِنَّ كُلَّ مُحْدَثَةٍ بِدْعَةٌ"، وقَالَ أَبُو عَاصِمٍ مَرَّةً: "وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الْأُمُورِ، فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, ametupa khabari Thawr bin Yaziyd, amenisimulia Khaalid bin Ma'daan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr, kutoka kwa 'Irbaadhw bin Saariyah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha Swalaah ya Alfajiri, kisha akatupa mawaidha fasaha ambayo macho yalitokwa machozi kwayo, na nyoyo zikaogopa kwayo. Mtu mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, kama kwamba ni mawaidha ya mwenye kuaga! Basi tuusie. Akasema: "Nakuusieni taqwa ya Allaah, na kusikiliza na kutii, hata kama (kiongozi) ni mtumwa wa Kihabeshi. Kwani hakika atakayeishi miongoni mwenu baada yangu, ataona ikhtilafu nyingi. Basi shikamaneni na Sunnah yangu na Sunnah ya Makhalifa waongofu walioongoka; iumeni kwa magego. Na tahadharini na mambo yaliyozushwa, kwani hakika kila kilichozushwa ni bid'ah (uzushi katika Dini)." Na Abuw 'Aaswim amesema mara moja: "Na tahadharini na mambo yaliyozushwa, kwani hakika kila bid'ah ni upotofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
228
Hadiyth
96

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يُونُسَ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: كَانَ مَنْ مَضَى مِنْ عُلَمَائِنَا يَقُولُونَ: "الِاعْتِصَامُ بِالسُّنَّةِ نَجَاةٌ، وَالْعِلْمُ يُقْبَضُ قَبْضًا سَرِيعًا، فَنَعْشُ الْعِلْمِ ثَبَاتُ الدِّينِ وَالدُّنْيَا، وَفِي ذَهَابِ الْعِلْمِ ذَهَابُ ذَلِكَ كُلِّهِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yuwnus bin Yaziyd, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Waliotangulia miongoni mwa 'Ulamaa (Wanazuoni) wetu walikuwa wakisema: "Kushikamana na Sunnah ni uokovu; na ilimu inachukuliwa kwa haraka. Basi kuiinua ilimu ni uthabiti wa Dini na dunia, na katika kuondoka kwa ilimu kuna kuondoka kwa hayo yote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
229
Hadiyth
97

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي عَمْرٍو السَّيْبَانِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الدَّيْلَمِيِّ، قَالَ: "بَلَغَنِي أَنَّ أَوَّلَ ذَهَابِ الدِّينِ تَرْكُ السُّنَّةُ، يَذْهَبُ الدِّينُ سُنَّةً سُنَّةً، كَمَا يَذْهَبُ الْحَبْلُ قُوَّةً قُوَّةً"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy 'Amr As-Saybaaniy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ad-Daylamiy, amesema: "Imenifikia (khabari) kwamba mwanzo wa kuondoka kwa Dini ni kuacha Sunnah. Dini inaondoka Sunnah moja baada ya nyingine, kama kamba inavyoondoka uzi mmoja baada ya mwingine."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
229
Hadiyth
98

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ حَسَّانَ، قَالَ: "مَا ابْتَدَعَ قَوْمٌ بِدْعَةً فِي دِينِهِمْ إِلَّا نَزَعَ اللَّهُ مِنْ سُنَّتِهِمْ مِثْلَهَا، ثُمَّ لَا يُعِيدُهَا إِلَيْهِمْ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Hassaan, amesema: "Watu hawazushi bid'ah (uzushi katika Dini) katika Dini yao ila Allaah Huwaondolea katika Sunnah yao mfano wake, kisha Hairudishi kwao mpaka Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
229
Hadiyth
99

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: "مَا ابْتَدَعَ رَجُلٌ بِدْعَةً إِلَّا اسْتَحَلَّ السَّيْفَ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: "Hakuna mtu anayezusha bid'ah (uzushi katika Dini) ila huhalalisha upanga."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
229
Hadiyth
100

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: "إِنَّ أَهْلَ الْأَهْوَاءِ أَهْلُ الضَّلَالَةِ، وَلَا أَرَى مَصِيرَهُمْ إِلَّا إِلَى النَّارِ، فَجَرِّبْهُمْ فَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْهُمْ يَنْتَحِلُ قَوْلًا أَوْ قَالَ: حَدِيثًا فَيَتَنَاهَى بِهِ الْأَمْرُ دُونَ السَّيْفِ، وَإِنَّ النِّفَاقَ كَانَ ضُرُوبًا، ثُمَّ تَلَا: {وَمِنْهُمْ مَنْ عَاهَدَ اللَّهَ لَئِنْ آتَانَا مِنْ فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ}، {وَمِنْهُمْ مَنْ يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِنْ لَمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ}، {وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَكُمْ} فَاخْتَلَفَ قَوْلُهُمْ وَاجْتَمَعُوا، فِي الشَّكِّ وَالتَّكْذِيبِ، وَإِنَّ هَؤُلَاءِ اخْتَلَفَ قَوْلُهُمْ وَاجْتَمَعُوا فِي السَّيْفِ، وَلَا أَرَى مَصِيرَهُمْ إِلَّا إِلَى النَّارِ"، قَالَ حَمَّادٌ: ثُمَّ قَالَ أَيُّوبُ عِنْدَ ذَا الْحَدِيثِ أَوْ عِنْدَ الْأَوَّلِ: وَكَانَ وَاللَّهِ مِنْ الْفُقَهَاءِ ذَوِي الْأَلْبَابِ: يَعْنِي أَبَا قِلَابَةَ

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: "Hakika watu wa matamanio ni watu wa upotofu, na sioni mwisho wao ila ni motoni. Basi wajaribu: hakuna yeyote miongoni mwao anayejinasibisha na kauli — au amesema: Hadiyth — kisha jambo likaishia kwake kabla ya (kufikia) upanga. Na hakika unafiki ulikuwa wa aina mbalimbali. Kisha akasoma:

وَمِنْهُمْ مَنْ عَاهَدَ اللَّهَ لَئِنْ آتَانَا مِنْ فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ

Na miongoni mwao wako waliomuahidi Allaah (kuwa): Akitupa katika Fadhila Zake, bila shaka tutatoa swadaqa, na bila shaka tutakuwa miongoni mwa wema. [At-Tawbah (9:75)]

وَمِنْهُمْ مَنْ يَلْمِزُكَ فِي الصَّدَقَاتِ فَإِنْ أُعْطُوا مِنْهَا رَضُوا وَإِنْ لَمْ يُعْطَوْا مِنْهَا إِذَا هُمْ يَسْخَطُونَ

Na miongoni mwao wako wanaokukosoa katika (ugawaji wa) swadaqa. Wakipewa fungu wanaridhika, na wasipopewa fungu tahamaki wao wanaghadhibika. [At-Tawbah (9:58)]

وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَكُمْ

Na miongoni mwao wako wale wanaomuudhi Nabiy, na wanasema: Yeye ni mtegaji sikio tu. Sema: Sikio la kheri kwenu [At-Tawbah (9:61)]

Kauli zao zikatofautiana, na wakakusanyika katika shaka na ukadhibishaji. Na hakika hawa (watu wa matamanio) kauli zao zimetofautiana, na wamekusanyika katika upanga; na sioni mwisho wao ila ni motoni." Hammaad amesema: Kisha Ayyuwb akasema katika Hadiyth hii — au katika ile ya kwanza —: Na alikuwa, Wa-Allaahi, miongoni mwa Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wenye akili — yaani Abuw Qilaabah.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
231
Hadiyth
101

17-Mlangoباب التورع عن الجواب فيما ليس فيه كتاب ولا سنةMlango Wa Kujiepusha Na Kujibu Kuhusu Yale
Ambayo Hayana Kitabu Wala Sunnah

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، وَحُذَيْفَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّهُمَا كَانَا جَالِسَيْنِ فَجَاءَ رَجُلٌ فَسَأَلَهُمَا عَنْ شَيْءٍ، فَقَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ لِحُذَيْفَةَ: "لِأَيِّ شَيْءٍ تَرَى يَسْأَلُونِي عَنْ هَذَا؟، قَالَ: يَعْلَمُونَهُ ثُمَّ يَتْرُكُونَهُ، فَأَقْبَلَ إِلَيْهِ ابْنُ مَسْعُودٍ، فَقَالَ: مَا سَأَلْتُمُونَا عَنْ شَيْءٍ مِنْ كِتَابِ اللَّهِ تَعَالَى نَعْلَمُهُ، أَخْبَرْنَاكُمْ بِهِ، أَوْ سُنَّةٍ مِنْ نَبِيِّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخْبَرْنَاكُمْ بِهِ، وَلَا طَاقَةَ لَنَا بِمَا أَحْدَثْتُمْ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Ibn Mas'uwd na Hudhayfah (رضي الله عنهما), kwamba wao wawili walikuwa wamekaa; akaja mtu mmoja akawauliza kuhusu jambo fulani. Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) akamwambia Hudhayfah (رضي الله عنه): "Unaona ni kwa sababu gani wananiuliza kuhusu hili? Akasema: Wanalijua, kisha wanaliacha. Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) akamwelekea (yule mtu), akasema: Lolote mlilotuuliza katika Kitabu cha Allaah (تعالى) tunalolijua, tumekukhabarisheni; au Sunnah kutoka kwa Nabiy wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), tumekukhabarisheni; wala hatuna uwezo na yale mliyoyazusha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
232
Hadiyth
102

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ مَيْسَرَةَ، عَنْ النَّزَّالِ بْنِ سَبْرَةَ، قَالَ: "مَا خَطَبَ عَبْدُ اللَّهِ خُطْبَةً بِالْكُوفَةِ إِلَّا شَهِدْتُهَا، فَسَمِعْتُهُ يَوْمًا، وَسُئِلَ عَنْ رَجُلٍ يُطَلِّقُ امْرَأَتَهُ ثَمَانِيَةً وَأَشْبَاهِ ذَلِكَ، قَالَ: هُوَ كَمَا، قَالَ، ثُمَّ قَالَ: إِنَّ اللَّهَ أَنْزَلَ كِتَابَهُ وَبَيَّنَ بَيَانَهُ، فَمَنْ أَتَى الْأَمْرَ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ فَقَدْ بُيِّنَ لَهُ، وَمَنْ خَالَفَ فَوَاللَّهِ مَا نُطِيقُ خِلَافَكُمْ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Maysarah, kutoka kwa An-Nazzaal bin Sabrah, amesema: "'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) hakutoa khutbah yoyote huko Al-Kuwfah ila niliihudhuria. Basi nilimsikia siku moja, naye ameulizwa kuhusu mtu anayemtaliki mkewe talaka nane na mfano wa hayo, akasema: Ni kama alivyosema. Kisha akasema: Hakika Allaah Ameteremsha Kitabu Chake, na Amebainisha ubainifu Wake. Basi mwenye kulijia jambo kwa upande wake wa mbele, amekwisha bainishiwa; na mwenye kwenda kinyume — Wa-Allaahi, hatuwezi kustahimili kwenda kinyume kwenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
233
Hadiyth
103

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي عَبْدُ الْمَلِكِ بْنُ مَيْسَرَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّزَّالَ بْنَ سَبْرَةَ، قَالَ: "شَهِدْتُ عَبْدَ اللَّهِ وَأَتَاهُ رَجُلٌ وَامْرَأَةٌ فِي تَحْرِيمٍ، فَقَالَ: إِنَّ اللَّهَ قَدْ بَيَّنَ، فَمَنْ أَتَى الْأَمْرَ مِنْ قِبَلِ وَجْهِهِ، فَقَدْ بُيِّنَ، وَمَنْ خَالَفَ، فَوَاللَّهِ مَا نُطِيقُ خِلَافَكُمْ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha 'Abdul-Malik bin Maysarah, amesema: Nilimsikia An-Nazzaal bin Sabrah, amesema: "Nilimshuhudia 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), na wakamjia mwanamume na mwanamke katika (suala la) kuharamisha. Akasema: Hakika Allaah Amekwisha bainisha; basi mwenye kulijia jambo kwa upande wake wa mbele, amekwisha bainishiwa; na mwenye kwenda kinyume — Wa-Allaahi, hatuwezi kustahimili kwenda kinyume kwenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
233
Hadiyth
104

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا حَفْصٌ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ: "أَنَّهُ كَانَ لَا يَقُولُ بِرَأْيِهِ إِلَّا شَيْئًا سَمِعَهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Hafsw, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn: "Kwamba yeye alikuwa hasemi kwa rai yake isipokuwa kitu alichokisikia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
234
Hadiyth
105

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَثَّامٌ وَالِدُ عَلِيِّ بْنِ عَثَّامٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: "مَا سَمِعْتُ إِبْرَاهِيمَ يَقُولُ بِرَأْيِهِ فِي شَيْءٍ قَطُّ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Aththaam — baba yake 'Aliy bin 'Aththaam —, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: "Sijapata kamwe kumsikia Ibraahiym akisema kwa rai yake katika jambo lolote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
234
Hadiyth
106

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: "مَا قُلْتُ بِرَأْيِي مُنْذُ ثَلَاثِينَ سَنَةً"، قَالَ أَبُو هِلَالٍ: "مُنْذُ أَرْبَعِينَ سَنَةً"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Qataadah, amesema: "Sijasema kwa rai yangu tangu miaka thelathini." Abuw Hilaal amesema: "Tangu miaka arobaini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
234
Hadiyth
107

حَدَّثَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، ثَنَا حَكَّامُ بْنُ سَلْمٍ، عَنْ أَبِي خَيْثَمَةَ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ رُفَيْعٍ، قَالَ: سُئِلَ عَطَاءٌ عَنْ شَيْءٍ فَقَالَ: لَا أَدْرِي، قَالَ: قِيلَ لَهُ: أَلَا تَقُولُ فِيهَا بِرَأْيِكَ؟، قَالَ: "إِنِّي أَسْتَحْيِي مِنْ اللَّهِ عز وجل أَنْ يُدَانَ فِي الْأَرْضِ بِرَأْيِي"

Ametusimulia Makhlad bin Maalik, ametusimulia Hakkaam bin Salm, kutoka kwa Abuw Khaythamah, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Rufay', amesema: 'Atwaa aliulizwa kuhusu jambo fulani, akasema: Sijui. Akasema: Akaambiwa: Je, husemi kuhusu hilo kwa rai yako? Akasema: "Hakika mimi naona haya kwa Allaah (عز وجل) kwamba (watu) waifuate Dini katika ardhi kwa rai yangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
234
Hadiyth
108

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، أَخْبَرَنِي حَاتِمٌ هُوَ ابْنُ إِسْمَاعِيل، عَنْ عِيسَى، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: جَاءَهُ رَجُلٌ يَسْأَلُهُ عَنْ شَيْءٍ، فَقَالَ: "كَانَ ابْنُ مَسْعُودٍ يَقُولُ فِيهِ كَذَا وَكَذَا، قَالَ: أَخْبِرْنِي أَنْتَ بِرَأْيِكَ، فَقَالَ: أَلَا تَعْجَبُونَ مِنْ هَذَا؟ أَخْبَرْتُهُ عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، وَيَسْأَلُنِي عَنْ رَأْيِي، وَدِينِي عِنْدِي آثَرُ مِنْ ذَلِكَ، وَاللَّهِ لَأَنْ أَتَعَنَّى بِعَنِيَّةٍ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أُخْبِرَكَ بِرَأْيِي"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, amenikhabarisha Haatim — naye ni Ibn Ismaa'iyl —, kutoka kwa 'Iysaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Alimjia mtu akimuuliza kuhusu jambo fulani. Akasema: "Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa akisema kuhusu hilo kadha wa kadha. (Yule mtu) akasema: Nikhabarishe wewe kwa rai yako. Akasema: Je, hamshangai na huyu? Nimemkhabarisha kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), naye ananiuliza kuhusu rai yangu! Na Dini yangu kwangu ni yenye kupendelewa zaidi kuliko hilo. Wa-Allaahi, kujipaka 'aniyyah (mchanganyiko unaonuka wa kuwapaka ngamia wenye upele) ni jambo ninalolipenda zaidi kuliko kukukhabarisha rai yangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
235
Hadiyth
109

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا حَاتِمٌ هُوَ ابْنُ إِسْمَاعِيل، عَنْ عِيسَى، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "إِيَّاكُمْ وَالْمُقَايَسَةَ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَئِنْ أَخَذْتُمْ بِالْمُقَايَسَةِ لَتُحِلُّنَّ الْحَرَامَ وَلَتُحَرِّمُنَّ الْحَلَالَ، وَلَكِنْ مَا بَلَغَكُمْ عَمَّنْ حَفِظَ مِنْ أَصْحَابِ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاعْمَلُوا بِهِ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Haatim — naye ni Ibn Ismaa'iyl —, kutoka kwa 'Iysaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Tahadharini na kulinganisha (mambo kwa rai). Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, mkichukua kwa kulinganisha, bila shaka mtahalalisha haraam na mtaharamisha halaal. Lakini kile kinachokufikieni kutoka kwa aliyehifadhi miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), basi kifanyieni kazi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
235
Hadiyth
110

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ، فَقَالَ: إِنَّهُ طَلَّقَ امْرَأَتَهُ الْبَارِحَةَ ثَمَانِيًا، قَالَ: بِكَلَامٍ وَاحِدٍ؟، قَالَ: بِكَلَامٍ وَاحِدٍ، قَالَ: فَيُرِيدُونَ أَنْ يُبِينُوا مِنْكَ امْرَأَتَكَ؟ قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: وَجَاءَهُ رَجُلٌ، فَقَالَ: إِنَّهُ طَلَّقَ امْرَأَتَهُ مِائَةَ طَلْقَةٍ قَالَ: بِكَلَامٍ وَاحِدٍ؟، قَالَ: بِكَلَامٍ وَاحِدٍ، قَالَ: فَيُرِيدُونَ أَنْ يُبِينُوا مِنْكَ امْرَأَتَكَ؟، قَالَ: نَعَمْ، فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "مَنْ طَلَّقَ كَمَا أَمَرَ اللَّهُ، فَقَدْ بَيَّنَ اللَّهُ الطَّلَاقَ وَمَنْ لَبَّسَ عَلَى نَفْسِهِ، وَكَّلْنَا بِهِ لَبْسَهُ وَاللَّهِ لَا تُلَبِّسُونَ عَلَى أَنْفُسِكُمْ وَنَتَحَمَّلُهُ نَحْنُ، هُوَ كَمَا تَقُولُونَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa 'Alqamah, amesema: Mtu mmoja alikuja kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), akasema: Hakika yeye amemtaliki mkewe jana usiku talaka nane. Akasema: Kwa tamko moja? Akasema: Kwa tamko moja. Akasema: Basi wanataka kumtenganisha mkeo nawe? Akasema: Ndiyo. Akasema: Na akamjia mtu (mwingine), akasema: Hakika yeye amemtaliki mkewe talaka mia. Akasema: Kwa tamko moja? Akasema: Kwa tamko moja. Akasema: Basi wanataka kumtenganisha mkeo nawe? Akasema: Ndiyo. 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) akasema: "Mwenye kutaliki kama Alivyoamrisha Allaah, basi Allaah Amekwisha bainisha talaka; na mwenye kujitatanishia nafsi yake, tunamwachia utatanishi wake. Wa-Allaahi, hamtajitatanishia nafsi zenu kisha sisi ndio tuubebe! Ni kama mnavyosema."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
235
Hadiyth
111

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ الْقَاسِمِ، قَالَ: "لَأَنْ يَعِيشَ الرَّجُلُ جَاهِلًا بَعْدَ أَنْ يَعْلَمَ حَقَّ اللَّهِ عَلَيْهِ خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَقُولَ مَا لَا يَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Al-Qaasim, amesema: "Mtu kuishi akiwa jahili baada ya kujua Haki ya Allaah juu yake, ni bora kwake kuliko kusema asiyoyajua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
236
Hadiyth
112

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، قَالَ: سَمِعْتُ الْقَاسِمَ سُئِلَ، قَالَ: "إِنَّا وَاللَّهِ مَا نَعْلَمُ كُلَّ مَا تَسْأَلُونَ عَنْهُ، وَلَوْ عَلِمْنَا مَا كَتَمْنَاكُمْ، وَلَا حَلَّ لَنَا أَنْ نَكْتُمَكُمْ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, amesema: Nilimsikia Al-Qaasim — alipoulizwa — akasema: "Hakika sisi, Wa-Allaahi, hatujui kila mnalouliza; na lau tungelijua, tusingekuficheni; wala si halaal kwetu kukuficheni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
237
Hadiyth
113

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: سُئِلَ الْقَاسِمُ عَنْ شَيْءٍ قَدْ سَمَّاهُ، فَقَالَ: "مَا أَضْطَرُّ إِلَى مَشُورَةٍ، وَمَا أَنَا مِنْ ذِي فِي شَيْءٍ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema: Al-Qaasim aliulizwa kuhusu jambo fulani ambalo (Ibn 'Awn) alilitaja kwa jina, akasema: "Silazimiki kutoa shauri, wala mimi si mtu wa hili katika chochote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
237
Hadiyth
114

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ يَحْيَى، قَالَ: قُلْتُ لِلْقَاسِمِ: مَا أَشَدَّ عَلَيَّ أَنْ تُسْأَلَ عَنْ الشَّيْءِ لَا يَكُونُ عِنْدَكَ وَقَدْ كَانَ أَبُوكَ إِمَامًا، قَالَ: "إِنَّ أَشَدَّ مِنْ ذَلِكَ عِنْدَ اللَّهِ وَعِنْدَ مَنْ عَقَلَ عَنْ اللَّهِ أَنْ أُفْتِيَ بِغَيْرِ عِلْمٍ، أَوْ أَرْوِيَ عَنْ غَيْرِ ثِقَةٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Yahyaa, amesema: Nilimwambia Al-Qaasim: Ni jambo zito kiasi gani kwangu kwamba uulizwe kuhusu jambo ambalo huna (ilimu yake), na hali baba yako alikuwa Imaam! Akasema: "Hakika lililo zito zaidi kuliko hilo mbele ya Allaah, na mbele ya aliyepata ufahamu kutoka kwa Allaah, ni mimi kutoa Fatwa bila ilimu, au kupokea kutoka kwa asiyeaminika."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
237
Hadiyth
115

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ الْعَوَّامِ، عَنْ الْمُسَيَّبِ بْنِ رَافِعٍ، قَالَ: "كَانُوا إِذَا نَزَلَتْ بِهِمْ قَضِيَّةٌ لَيْسَ فِيهَا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَثَرٌ، اجْتَمَعُوا لَهَا وَأَجْمَعُوا، فَالْحَقُّ فِيمَا رَأَوْا، فَالْحَقُّ فِيمَا رَأَوْا"،

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Hushaym, kutoka kwa Al-'Awwaam, kutoka kwa Al-Musayyab bin Raafi', amesema: "Walikuwa wanapofikwa na kesi isiyokuwa na mapokezi yoyote kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), walikusanyika kwa ajili yake na wakakubaliana kwa pamoja; basi haki ni katika yale waliyoyaona, basi haki ni katika yale waliyoyaona."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
238
Hadiyth
116

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، أَنْبَأَنَا يَزِيدُ، عَنْ الْعَوَّامِ بِهَذَا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah, ametupa khabari Yaziyd, kutoka kwa Al-'Awwaam, kwa (Hadiyth) hii.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
238
Hadiyth
117

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، وَمُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، قَالَا: حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو سَلَمَةَ الْحِمْصِيُّ، أَنَّ وَهْبَ بْنَ عَمْرٍو الْجُمَحِيَّ حَدَّثَهُ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا تَعْجَلُوا بِالْبَلِيَّةِ قَبْلَ نُزُولِهَا، فَإِنَّكُمْ إِنْ لَا تَعْجَلُوهَا قَبْلَ نُزُولِهَا، لَا يَنْفَكُّ الْمُسْلِمُونَ وَفِيهِمْ إِذَا هِيَ نَزَلَتْ مَنْ إِذَا قَالَ، وُفِّقَ وَسُدِّدَ، وَإِنَّكُمْ إِنْ تَعْجَلُوهَا، تَخْتَلِفْ بِكُمْ الْأَهْوَاءُ، فَتَأْخُذُوا هَكَذَا وَهَكَذَا، وَأَشَارَ بَيْنَ يَدَيْهِ وَعَنْ يَمِينِهِ وَعَنْ شِمَالِهِ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan na Muhammad bin Al-Mubaarak, wamesema: Ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, ametusimulia Abuw Salamah Al-Himswiy, kwamba Wahb bin 'Amr Al-Jumahiy alimsimulia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiiharakishe balaa kabla ya kuteremka kwake; kwani hakika nyinyi msipoiharakisha kabla ya kuteremka kwake, Waislamu hawataacha kuwa miongoni mwao — itakapoteremka — yupo ambaye akisema, huwafikishwa na huelekezwa sawasawa. Na hakika nyinyi mkiiharakisha, matamanio yatatofautiana nanyi, mkachukua hivi na hivi" — na akaashiria mbele yake, na kuliani kwake na kushotoni kwake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
238
Hadiyth
118

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، حَدَّثَنِي أَبُو سَلَمَةَ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ الْأَمْرِ يَحْدُثُ لَيْسَ فِي كِتَابٍ وَلَا سُنَّةٍ، قَالَ: "يَنْظُرُ فِيهِ الْعَابِدُونَ مِنْ الْمُؤْمِنِينَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, amenisimulia Abuw Salamah, kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu jambo linalotokea lisilokuwemo katika Kitabu wala Sunnah, akasema: "Wataliangalia wenye kuabudu miongoni mwa Waumini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
239
Hadiyth
119

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ مُعَاذٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: قَالَ الْقَاسِمُ: "إِنَّكُمْ لَتَسْأَلُونَا عَنْ أَشْيَاءَ مَا كُنَّا نَسْأَلُ عَنْهَا، وَتُنَقِّرُونَ عَنْ أَشْيَاءَ مَا كُنَّا نُنَقِّرُ عَنْهَا، وَتَسْأَلُونَ عَنْ أَشْيَاءَ مَا أَدْرِي مَا هِيَ، وَلَوْ عَلِمْنَاهَا مَا حَلَّ لَنَا أَنْ نَكْتُمُكُمُوهَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Mu'aadh bin Mu'aadh, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema: Al-Qaasim amesema: "Hakika nyinyi mnatuuliza kuhusu mambo ambayo hatukuwa tukiuliza kuhusu hayo, na mnachimbua mambo ambayo hatukuwa tukiyachimbua, na mnauliza kuhusu mambo ambayo sijui ni nini; na lau tungeyajua, isingekuwa halaal kwetu kukuficheni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
239
Hadiyth
120

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ ابْنُ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ الْأَشَجِّ، أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِنَّهُ سَيَأْتِي نَاسٌ يُجَادِلُونَكُمْ بِشُبُهَاتِ الْقُرْآنِ، فَخُذُوهُمْ بِالسُّنَنِ، فَإِنَّ أَصْحَابَ السُّنَنِ أَعْلَمُ بِكِتَابِ اللَّهِ عز وجل"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa 'Umar bin Al-Ashajj, kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: "Hakika watakuja watu watakaobishana nanyi kwa mambo yenye kutatiza ya Qur-aan; basi wakamateni kwa Sunnah, kwani hakika watu wa Sunnah ndio wajuzi zaidi wa Kitabu cha Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
240
Hadiyth
121

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا عَلِيٌّ هُوَ ابْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ هِشَامٍ هُوَ ابْنُ عُرْوَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ نَوْفَلٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، قَالَ: "مَا زَالَ أَمْرُ بَنِي إِسْرَائِيلَ مُعْتَدِلًا لَيْسَ فِيهِ شَيْءٌ حَتَّى نَشَأَ فِيهِمْ الْمُوَلَّدُونَ، أَبْنَاءُ سَبَايَا الْأُمَمِ، أَبْنَاءُ النِّسَاءِ الَّتِي سَبَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ مِنْ غَيْرِهِمْ، فَقَالُوا فِيهِمْ: بِالرَّأْيِ فَأَضَلُّوهُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, ametusimulia 'Aliy — naye ni Ibn Mus-hir —, kutoka kwa Hishaam — naye ni Ibn 'Urwah —, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Nawfal, kutoka kwa 'Urwah bin Az-Zubayr, amesema: "Jambo la Banuw Israaiyl liliendelea kuwa sawasawa, halina kitu (cha kasoro) ndani yake, mpaka walipozuka miongoni mwao wazaliwa wa mchanganyiko — watoto wa mateka wa mataifa (mengine), watoto wa wanawake ambao Banuw Israaiyl waliwateka kutoka kwa wasiokuwa wao —; wakasema miongoni mwao kwa rai, wakawapoteza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
241
Hadiyth
122

18-Mlangoباب كراهية الفتياMlango Wa Kuchukia Kutoa Fatwa

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ يَزِيدَ الْمِنْقَرِيُّ، حَدَّثَنِي أَبِي، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ يَوْمًا إِلَى ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، فَسَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ لَا أَدْرِي مَا هُوَ، فَقَالَ لَهُ ابْنُ عُمَرَ: "لَا تَسْأَلْ عَمَّا لَمْ يَكُنْ، فَإِنِّي سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ يَلْعَنُ مَنْ سَأَلَ عَمَّا لَمْ يَكُنْ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Hammaad bin Yaziyd Al-Minqariy, amenisimulia baba yangu, amesema: Mtu mmoja alikuja siku moja kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), akamuuliza kuhusu kitu ambacho sijui ni kitu gani. Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akamwambia: "Usiulize kuhusu (jambo) ambalo halijatokea, kwani mimi nilimsikia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه) akimlaani anayeuliza kuhusu (jambo) ambalo halijatokea."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
242
Hadiyth
123

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: بَلَغَنَا أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيَّ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ كَانَ يَقُولُ إِذَا سُئِلَ عَنْ الْأَمْرِ: "أَكَانَ هَذَا؟ فَإِنْ قَالُوا: نَعَمْ، قَدْ كَانَ، حَدَّثَ فِيهِ بِالَّذِي يَعْلَمُ وَالَّذِي يَرَى، وَإِنْ قَالُوا: لَمْ يَكُنْ، قَالَ: فَذَرُوهُ حَتَّى يَكُونَ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Imetufikia kwamba Zayd bin Thaabit Al-Answaariy (رضوان الله عليه) alikuwa akisema anapoulizwa kuhusu jambo: "Je, hili limetokea? Wakisema: Ndiyo, limekwisha tokea, husimulia kuhusu hilo kwa yale anayoyajua na anayoyaona (kwa rai yake). Na wakisema: Halijatokea, husema: Basi liacheni mpaka litokee."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
242
Hadiyth
124

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا أَبُو هِشَامٍ الْمَخْزُومِيُّ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ: سُئِلَ عَمَّارُ بْنُ يَاسِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ مَسْأَلَةٍ، فَقَالَ: "هَلْ كَانَ هَذَا بَعْدُ؟، قَالُوا: لَا، قَالَ: دَعُونَا حَتَّى يَكُونَ، فَإِذَا كَانَ، تَجَشَّمْنَاهَا لَكُمْ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametupa khabari Abuw Hishaam Al-Makhzuwmiy, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Daawuwd, kutoka kwa 'Aamir, amesema: 'Ammaar bin Yaasir (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu suala moja, akasema: "Je, hili limekwisha tokea? Wakasema: Hapana. Akasema: Tuacheni mpaka litokee; litakapotokea, tutajikalifu nalo kwa ajili yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
243
Hadiyth
125

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ عَلَى الْمِنْبَرِ: "أُحَرِّجُ بِاللَّهِ عَلَى رَجُلٍ سَأَلَ عَمَّا لَمْ يَكُنْ، فَإِنَّ اللَّهَ قَدْ بَيَّنَ مَا هُوَ كَائِنٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa Twaawus, amesema: 'Umar (رضوان الله عليه) alisema juu ya mimbari: "Ninamuapia kwa Allaah (kuwa ni dhambi) mtu anayeuliza kuhusu (jambo) ambalo halijatokea; kwani Allaah Amekwisha kubainisha yale yatakayokuwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
244
Hadiyth
126

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي شَيْبَةَ، ، حَدَّثَنَا ابْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مَا رَأَيْتُ قَوْمًا كَانُوا خَيْرًا مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، مَا سَأَلُوهُ إِلَّا عَنْ ثَلَاثَ عَشْرَةَ مَسْأَلَةً حَتَّى قُبِضَ، كُلُّهُنَّ، فِي الْقُرْآنِ مِنْهُنَّ، {يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ}، وَ {وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ}، قَالَ: مَا كَانُوا يَسْأَلُونَ إِلَّا عَمَّا يَنْفَعُهُمْ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah, ametusimulia Ibn Fudhwayl, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Sijaona watu waliokuwa bora kuliko Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): hawakumuuliza ila masuala kumi na matatu mpaka alipofariki, yote hayo yamo katika Qur-aan; miongoni mwake:

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ

Wanakuuliza kuhusu mwezi mtukufu [Al-Baqarah (2:217)]

na:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ

Na wanakuuliza kuhusu hedhi [Al-Baqarah (2:222)]

Akasema: Hawakuwa wakiuliza ila yale yanayowanufaisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
244
Hadiyth
127

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ عُمَيْرِ بْنِ إِسْحَاق، قَالَ: "لَمَنْ أَدْرَكْتُ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْثَرُ مِمَّنْ سَبَقَنِي مِنْهُمْ، فَمَا رَأَيْتُ قَوْمًا أَيْسَرَ سِيرَةً، وَلَا أَقَلَّ تَشْدِيدًا مِنْهُمْ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Ibn 'Awn, kutoka kwa 'Umayr bin Is-haaq, amesema: "Kwa hakika wale niliowadiriki miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni wengi zaidi kuliko wale walionitangulia miongoni mwao. Na sijaona watu wenye mwenendo mwepesi zaidi, wala wenye ukali mdogo zaidi, kuliko wao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
245
Hadiyth
128

أَخْبَرَنِي الْعَبَّاسُ بْنُ سُفْيَانَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ حُبَابٍ، أَخْبَرَنِي رَجَاءُ بْنُ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ عُبَادَةَ بْنَ نُسَيٍّ الْكِنْدِيَّ، وَسُئِلَ عَنْ امْرَأَةٍ مَاتَتْ مَعَ قَوْمٍ لَيْسَ لَهَا وَلِيٌّ، فَقَالَ: "أَدْرَكْتُ أَقْوَامًا مَا كَانُوا يُشَدِّدُونَ تَشْدِيدَكُمْ، وَلَا يَسْأَلُونَ مَسَائِلَكُمْ"

Amenikhabarisha Al-'Abbaas bin Sufyaan, kutoka kwa Zayd bin Hubaab, amenikhabarisha Rajaa bin Abiy Salamah, amesema: Nilimsikia 'Ubaadah bin Nusayy Al-Kindiy — naye aliulizwa kuhusu mwanamke aliyefariki akiwa pamoja na watu, hana walii (msimamizi) — akasema: "Nimewadiriki watu waliokuwa hawakazi (mambo) kama mnavyokaza nyinyi, wala hawaulizi masuala kama yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
245
Hadiyth
129

أَخْبَرَنَا الْعَبَّاسُ بْنُ سُفْيَانَ، أَنْبَأَنَا زَيْدُ بْنُ حُبَابٍ، أَخْبَرَنِي رَجَاءُ بْنُ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي خَالِدُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ مُسْلِمٍ الْقُرَشِيِّ، قَالَ: كُنْتُ مَعَ ابْنِ مُحَيْرِيزٍ، بِمَرْجِ الدِّيبَاجِ فَرَأَيْتُ مِنْهُ خَلْوَةً، فَسَأَلْتُهُ عَنْ مَسْأَلَةٍ، فَقَالَ لِي: مَا تَصْنَعُ بِالْمَسَائِلِ؟، قُلْتُ: " لَوْلَا الْمَسَائِلُ، لَذَهَبَ الْعِلْمُ، قَالَ:" لَا تَقُلْ ذَهَبَ الْعِلْمُ، إِنَّهُ لَا يَذْهَبُ الْعِلْمُ مَا قُرِئَ الْقُرْآنُ، وَلَكِنْ لَوْ قُلْتَ: يَذْهَبُ الْفِقْهُ "

Ametukhabarisha Al-'Abbaas bin Sufyaan, ametupa khabari Zayd bin Hubaab, amenikhabarisha Rajaa bin Abiy Salamah, amesema: Amenisimulia Khaalid bin Haazim, kutoka kwa Hishaam bin Muslim Al-Qurashiy, amesema: Nilikuwa pamoja na Ibn Muhayriyz huko Marj Ad-Diybaaj, nikamwona yuko faragha, nikamuuliza kuhusu suala moja. Akaniambia: Unafanya nini na masuala? Nikasema: Lau si masuala, ilimu ingeondoka. Akasema: "Usiseme: Ilimu imeondoka; hakika ilimu haiondoki maadamu Qur-aan inasomwa. Lakini lau ungesema: Fiqh (ufahamu wa Dini) inaondoka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
246
Hadiyth
130

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، أَنَّ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّا لَا نَدْرِي، "لَعَلَّنَا نَأْمُرُكُمْ بِأَشْيَاءَ لَا تَحِلُّ لَكُمْ، وَلَعَلَّنَا نُحَرِّمُ عَلَيْكُمْ أَشْيَاءَ هِيَ لَكُمْ حَلَالٌ، إِنَّ آخِرَ مَا نَزَلَ مِنْ الْقُرْآنِ آيَةُ الرِّبَا، وَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يُبَيِّنْهَا لَنَا حَتَّى مَاتَ، فَدَعُوا مَا يَرِيبُكُمْ إِلَى مَا لَا يَرِيبُكُمْ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba 'Umar (رضي الله عنه) alisema: Enyi watu! Hakika sisi hatujui; "huenda tunakuamrisheni mambo yasiyokuhalalikieni, na huenda tunakuharamishieni mambo ambayo ni halaal kwenu. Hakika (Aayah) ya mwisho iliyoteremka katika Qur-aan ni Aayah ya riba, na hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutubainishia mpaka alipofariki. Basi acheni kinachokutieni shaka, mwende kwa kisichokutieni shaka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
246
Hadiyth
131

19-Mlangoباب من هاب الفتيا وكره التنطع والتبدعMlango Wa Aliyeiogopa Fatwa
Na Akachukia Kupindukia Mipaka Na Uzushi

أَخْبَرَنَا سَلْمُ بْنُ جُنَادَةَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ عَمِّهِ، قَالَ: "خَرَجْتُ مِنْ عِنْدِ إِبْرَاهِيمَ، فَاسْتَقْبَلَنِي حَمَّادٌ، فَحَمَّلَنِي ثَمَانِيَةَ أَبْوَابٍ، مَسَائِلَ، فَسَأَلْتُهُ، فَأَجَابَنِي عَنْ أَرْبَعٍ وَتَرَكَ أَرْبَعًا"

Ametukhabarisha Salm bin Junaadah, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa ami yake, amesema: "Nilitoka kwa Ibraahiym, Hammaad akanipokea, akanibebesha milango minane ya masuala. Nikamuuliza, akanijibu (masuala) manne na akaacha manne."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
247
Hadiyth
132

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبْجَرَ، عَنْ زُبَيْدٍ، قَالَ: "مَا سَأَلْتُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ شَيْءٍ إِلَّا عَرَفْتُ الْكَرَاهِيَةَ فِي وَجْهِهِ"

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametukhabarisha Sufyaan, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Abjar, kutoka kwa Zubayd, amesema: "Sikumuuliza Ibraahiym kuhusu kitu chochote ila nilitambua kuchukia usoni mwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
247
Hadiyth
133

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ مَنْصُورٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ أَبِي زَائِدَةَ، قَالَ: "مَا رَأَيْتُ أَحَدًا أَكْثَرَ أَنْ يَقُولَ إِذَا سُئِلَ عَنْ شَيْءٍ: لَا عِلْمَ لِي بِهِ مِنْ الشَّعْبِيِّ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Is-haaq bin Manswuwr, kutoka kwa 'Umar bin Abiy Zaaidah, amesema: "Sijaona yeyote anayekithirisha zaidi kusema anapoulizwa kuhusu kitu: Sina ilimu nacho, kuliko Ash-Sha'biy."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
247
Hadiyth
134

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: سَمِعْتُهُ يَذْكُرُ، قَالَ: كَانَ الشَّعْبِيُّ إِذَا جَاءَهُ شَيْءٌ اتَّقَى، وَكَانَ إِبْرَاهِيمُ يَقُولُ، وَيَقُولُ، وَيَقُولُ، قَالَ أَبُو عَاصِمٍ: "كَانَ الشَّعْبِيُّ فِي هَذَا أَحْسَنَ حَالًا عِنْدَ ابْنِ عَوْنٍ مِنْ إِبْرَاهِيمَ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema — nilimsikia akitaja, amesema —: Ash-Sha'biy alikuwa anapojiwa na jambo hujihadhari; na Ibraahiym alikuwa husema, na husema, na husema. Abuw 'Aaswim amesema: "Ash-Sha'biy alikuwa katika hili na hali nzuri zaidi mbele ya Ibn 'Awn kuliko Ibraahiym."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
247
Hadiyth
135

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا أَحْمَدُ بْنُ بَشِيرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ إِيَاسٍ، قَالَ: قُلْتُ لِسَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ: مَا لَكَ لَا تَقُولُ فِي الطَّلَاقِ شَيْئًا؟، قَالَ: "مَا مِنْهُ شَيْءٌ إِلَّا قَدْ سَأَلْتُ عَنْهُ، وَلَكِنِّي أَكْرَهُ أَنْ أُحِلَّ حَرَامًا، أَوْ أُحَرِّمَ حَلَالًا"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametupa khabari Ahmad bin Bashiyr, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ja'far bin Iyaas, amesema: Nilimwambia Sa'iyd bin Jubayr: Una nini husemi lolote kuhusu talaka? Akasema: "Hakuna lolote katika hilo ila nimekwisha kuliuliza; lakini mimi nachukia kuhalalisha haraam, au kuharamisha halaal."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
247
Hadiyth
136

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ أَبِي لَيْلَى، يَقُولُ: "لَقَدْ أَدْرَكْتُ فِي هَذَا الْمَسْجِدِ عِشْرِينَ وَمِائَةً مِنْ الْأَنْصَارِ، وَمَا مِنْهُمْ مِنْ أَحَدٍ يُحَدِّثُ بِحَدِيثٍ إِلَّا وَدَّ أَنَّ أَخَاهُ كَفَاهُ الْحَدِيثَ، وَلَا يُسْأَلُ عَنْ فُتْيَا إِلَّا وَدَّ أَنَّ أَخَاهُ كَفَاهُ الْفُتْيَا"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa akisema: "Kwa hakika nimewadiriki katika Msikiti huu mia moja na ishirini miongoni mwa Answaar (رضي الله عنهم); hakuna yeyote miongoni mwao anayesimulia Hadiyth ila alipenda kwamba ndugu yake angemtosheleza (kusimulia) Hadiyth hiyo, wala haulizwi Fatwa ila alipenda kwamba ndugu yake angemtosheleza Fatwa hiyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
248
Hadiyth
137

حَدَّثَنَا يُوسُفُ بْنُ يَعْقُوبَ الصَّفَّارُ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ دَاوُدَ، قَالَ: سَأَلْتُ الشَّعْبِيَّ، كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ إِذَا سُئِلْتُمْ؟، قَالَ: "عَلَى الْخَبِيرِ وَقَعْتَ، كَانَ إِذَا سُئِلَ الرَّجُلُ، قَالَ لِصَاحِبِهِ: أَفْتِهِمْ، فَلَا يَزَالُ حَتَّى يَرْجِعَ إِلَى الْأَوَّلِ"

Ametusimulia Yuwsuf bin Ya'quwb Asw-Swaffaar, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Daawuwd, amesema: Nilimuuliza Ash-Sha'biy: Mlikuwa mkifanya nini mnapoulizwa? Akasema: "Umemwangukia mjuzi (wa jambo hili). Mtu alikuwa anapoulizwa, humwambia mwenzake: Wape Fatwa; basi (suala) huendelea hivyo mpaka hurudi kwa yule wa kwanza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
249
Hadiyth
138

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ الْحَجَّاجِ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ، عَنْ ابْنِ الْمُنْكَدِرِ، قَالَ: "إِنَّ الْعَالِمَ يَدْخُلُ فِيمَا بَيْنَ اللَّهِ وَبَيْنَ عِبَادِهِ، فَلْيَطْلُبْ لِنَفْسِهِ الْمَخْرَجَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Al-Hajjaaj, amesema: Nilimsikia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Al-Munkadir, amesema: "Hakika 'Aalim (Mwanazuoni) huingia kati ya Allaah na waja Wake; basi ajitafutie njia ya kutokea."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
249
Hadiyth
139

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ قُدَامَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ مِسْعَرٍ، قَالَ: أَخْرَجَ إِلَيَّ مَعْنُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ كِتَابًا، فَحَلَفَ لِي بِاللَّهِ أَنَّهُ خَطُّ أَبِيه، فَإِذَا فِيهِ: قَال عَبْدُ اللَّهِ: "وَالَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ مَا رَأَيْتُ أَحَدًا كَانَ أَشَدَّ عَلَى الْمُتَنَطِّعِينَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَمَا رَأَيْتُ أَحَدًا كَانَ أَشَدَّ عَلَيْهِمْ مِنْ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، وَإِنِّي لَأَرَى عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ كَانَ أَشَدَّ خَوْفًا عَلَيْهِمْ أَوْ لَهُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Qudaamah, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Mis'ar, amesema: Ma'n bin 'Abdir-Rahmaan alinitolea kitabu, akaniapia kwa Allaah kwamba ni hati ya mkono wa baba yake; kumbe ndani yake mna: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Naapa kwa Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, sijaona yeyote aliyekuwa mkali zaidi juu ya wenye kupindukia mipaka kuliko Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); wala sijaona yeyote aliyekuwa mkali zaidi juu yao kuliko Abuw Bakr (رضي الله عنه); na hakika mimi namwona 'Umar (رضي الله عنه) kwamba alikuwa na hofu kubwa zaidi juu yao — au: kwa ajili yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
249
Hadiyth
140

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَمْعَةُ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ حَاضِرٍ الْأَزْدِيِّ، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، فَقُلْتُ: أَوْصِنِي، فَقَالَ: نَعَمْ، "عَلَيْكَ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالِاسْتِقَامَةِ، اتَّبِعْ وَلَا تَبْتَدِعْ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zam'ah bin Swaalih, kutoka kwa 'Uthmaan bin Haadhwir Al-Azdiy, amesema: Niliingia kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), nikasema: Niusie. Akasema: Ndiyo; "shikamana na taqwa ya Allaah na kuwa na msimamo imara; fuata wala usizushe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
250
Hadiyth
141

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ بن جابر، أَنْبَأَنَا النَّضْرُ بْنُ شُمَيْلٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "كَانُوا يَرَوْنَ أَنَّهُ عَلَى الطَّرِيقِ مَا كَانَ عَلَى الْأَثَرِ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik bin Jaabir, ametupa khabari An-Nadhwr bin Shumayl, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Walikuwa wakiona kwamba (mtu) yuko juu ya njia (iliyonyooka) maadamu yuko juu ya athar (mapokezi ya waliotangulia)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
250
Hadiyth
142

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا أَزْهَرُ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "مَا دَامَ عَلَى الْأَثَرِ، فَهُوَ عَلَى الطَّرِيقِ"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametusimulia Az-har, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Maadamu (mtu) yuko juu ya athar (mapokezi ya waliotangulia), basi yeye yuko juu ya njia (iliyonyooka)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
250
Hadiyth
143

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ قَبْلَ أَنْ يُقْبَضَ، وَقَبْضُهُ أَنْ يَذْهَبَ أَهْلُهُ، أَلَا وَإِيَّاكُمْ، وَالتَّنَطُّعَ، وَالتَّعَمُّقَ، وَالْبِدَعَ، وَعَلَيْكُمْ بِالْعَتِيقِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni ilimu kabla haijachukuliwa; na kuchukuliwa kwake ni kuondoka watu wake. Zindukeni! Tahadharini na kupindukia mipaka, na kujikalifu kuzama (katika mambo), na bid'ah (uzushi katika Dini); na shikamaneni na (jambo) la zamani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
250
Hadiyth
144

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، وَأَبُو النُّعْمَانِ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: قَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "عَلَيْكُمْ بِالْعِلْمِ قَبْلَ أَنْ يُقْبَضَ، وَقَبْضُهُ أَنْ يُذْهَبَ بِأَصْحَابِهِ، عَلَيْكُمْ بِالْعِلْمِ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَا يَدْرِي مَتَى يُفْتَقَرُ إِلَيْهِ أَوْ يُفْتَقَرُ إِلَى مَا عِنْدَهُ، إِنَّكُمْ سَتَجِدُونَ أَقْوَامًا يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ يَدْعُونَكُمْ إِلَى كِتَابِ اللَّهِ وَقَدْ نَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ، فَعَلَيْكُمْ بِالْعِلْمِ، وَإِيَّاكُمْ وَالتَّبَدُّعَ، وَإِيَّاكُمْ وَالتَّنَطُّعَ، وَإِيَّاكُمْ وَالتَّعَمُّقَ، وَعَلَيْكُمْ بِالْعَتِيقِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb na Abun-Nu'maan, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Shikamaneni na ilimu kabla haijachukuliwa; na kuchukuliwa kwake ni kuondoshwa kwa wenye nayo. Shikamaneni na ilimu, kwani mmoja wenu hajui ni lini atahitajiwa, au yatahitajiwa yaliyo kwake. Hakika nyinyi mtawakuta watu wanaodai kwamba wanakuiteni kwenye Kitabu cha Allaah, ilhali wamekitupa nyuma ya migongo yao. Basi shikamaneni na ilimu; na tahadharini na kuzusha bid'ah (uzushi katika Dini), na tahadharini na kupindukia mipaka, na tahadharini na kujikalifu kuzama (katika mambo); na shikamaneni na (jambo) la zamani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
251
Hadiyth
145

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، أَنَّ رَجُلًا يُقَالُ لَهُ: صَبِيغٌ قَدِمَ الْمَدِينَةَ فَجَعَلَ يَسْأَلُ عَنْ مُتَشَابِهِ الْقُرْآنِ، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ عُمَرُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ وَقَدْ أَعَدَّ لَهُ عَرَاجِينَ النَّخْلِ، فَقَالَ: "مَنْ أَنْتَ؟، قَالَ: أَنَا عَبْدُ اللَّهِ صَبِيغٌ، فَأَخَذَ عُمَرُ عُرْجُونًا مِنْ تِلْكَ الْعَرَاجِينِ، فَضَرَبَهُ وَقَالَ: أَنَا عَبْدُ اللَّهِ عُمَرُ فَجَعَلَ لَهُ ضَرْبًا حَتَّى دَمِيَ رَأْسُهُ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، حَسْبُكَ، قَدْ ذَهَبَ الَّذِي كُنْتُ أَجِدُ فِي رَأْسِي"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Yaziyd bin Haazim, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kwamba mtu mmoja aitwaye Swabiygh alikuja Madiynah, akawa anauliza kuhusu (Aayah) zisizokuwa wazi maana zake katika Qur-aan. 'Umar (رضي الله عنه) akamtumia (mjumbe), naye amekwisha kumwandalia mashina ya vishada vya tende. Akasema: "Wewe ni nani? Akasema: Mimi ni mja wa Allaah, Swabiygh. 'Umar (رضي الله عنه) akachukua shina moja katika mashina hayo, akampiga, na akasema: Mimi ni mja wa Allaah, 'Umar (رضي الله عنه). Akaendelea kumpiga mpaka kichwa chake kikatoka damu. Akasema: Yaa Amiri wa Waumini, inakutosha; kimekwisha ondoka kile nilichokuwa nakihisi kichwani mwangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
252
Hadiyth
146

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، وَيَزِيدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ، عَنْ الْقَاسِمِ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا، قَالَتْ: تَلَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ} فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا رَأَيْتُمْ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ، فَاحْذَرُوهُمْ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaad bin Salamah na Yaziyd bin Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Mulaykah, kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisoma:

هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ

Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu. Humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake [Aal-‘Imraan (3:7)]

Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mtakapowaona wale wanaofuata zile zisizokuwa wazi maana zake miongoni mwake, basi tahadharini nao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
253
Hadiyth
147

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا حَفْصٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ شَقِيقٍ، قَالَ: سُئِلَ عَبْدُ اللَّه عَنْ شَيْءٍ، فَقَالَ: "إِنِّي لَأَكْرَهُ أَنْ أُحِلَّ لَكَ شَيْئًا حَرَّمَهُ اللَّهُ عَلَيْكَ، أَوْ أُحَرِّمَ مَا أَحَلَّهُ اللَّهُ لَكَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Hafsw, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Shaqiyq, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu kitu, akasema: "Hakika mimi nachukia kukuhalalishia kitu ambacho Allaah Amekuharamishia, au kuharamisha kile ambacho Allaah Amekuhalalishia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
253
Hadiyth
148

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ: "لَأَنْ أَرُدَّهُ بِعِيِّهِ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَتَكَلَّفَ لَهُ مَا لَا أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Humayd bin 'Abdir-Rahmaan, amesema: "Kumrudisha (muulizaji) pamoja na kutojua kwake kunapendeza zaidi kwangu kuliko kujikalifu kumwambia nisiyoyajua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
253
Hadiyth
149

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، أَخْبَرَنِي ابْنُ عَجْلَانَ، عَنْ نَافِعٍ مَوْلَى عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ صَبِيغًا الْعِرَاقِيَّ، جَعَلَ يَسْأَلُ عَنْ أَشْيَاءَ مِنْ الْقُرْآنِ فِي أَجْنَادِ الْمُسْلِمِينَ حَتَّى قَدِمَ مِصْرَ، فَبَعَثَ بِهِ عَمْرُو بْنُ الْعَاصِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ إِلَى عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَلَمَّا أَتَاهُ الرَّسُولُ بِالْكِتَابِ فَقَرَأَهُ، فَقَالَ: أَيْنَ الرَّجُلُ؟، فَقَالَ: فِي الرَّحْلِ، قَالَ عُمَرُ: "أَبْصِرْ أَنْ يَكُونُ ذَهَبَ فَتُصِيبَكَ مِنِّي بِهِ الْعُقُوبَةُ الْمُوجِعَةُ، فَأَتَاهُ بِهِ، فَقَالَ عُمَرُ: تَسْأَلُ مُحْدَثَةً، فَأَرْسَلَ عُمَرُ إِلَى رَطَائِبَ مِنْ جَرِيدٍ، فَضَرَبَهُ بِهَا حَتَّى تَرَكَ ظَهْرَهُ دَبِرَةً، ثُمَّ تَرَكَهُ حَتَّى بَرَأَ، ثُمَّ عَادَ لَهُ، ثُمَّ تَرَكَهُ حَتَّى بَرَأَ، فَدَعَا بِهِ لِيَعُودَ لَهُ، قَالَ: فَقَالَ صَبِيغٌ: إِنْ كُنْتَ تُرِيدُ قَتْلِي، فَاقْتُلْنِي قَتْلًا جَمِيلًا، وَإِنْ كُنْتَ تُرِيدُ أَنْ تُدَاوِيَنِي، فَقَدْ وَاللَّهِ بَرَأْتُ، فَأَذِنَ لَهُ إِلَى أَرْضِهِ، وَكَتَبَ إِلَى أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنْ لَا يُجَالِسَهُ أَحَدٌ مِنْ الْمُسْلِمِينَ، فَاشْتَدَّ ذَلِكَ عَلَى الرَّجُلِ، فَكَتَبَ أَبُو مُوسَى إِلَى عُمَرَ: أَنْ قَدْ حَسُنَتْ تَوْبَتُهُ، فَكَتَبَ عُمَرُ: أَنْ ائْذَنْ لِلنَّاسِ بِمُجَالَسَتِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenikhabarisha Ibn 'Ajlaan, kutoka kwa Naafi' mawlaa (mwachwa huru) wa 'Abdi-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما), kwamba Swabiygh Al-'Iraaqiy alianza kuuliza kuhusu mambo ya Qur-aan katika majeshi ya Waislamu mpaka akafika Misri. 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنه) akampeleka kwa 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه). Mjumbe alipomfikia na barua, akaisoma, akasema: Yuko wapi mtu huyo? Akasema: Yuko kwenye mizigo (ya msafara). 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Angalia (asije) akawa ameondoka, ikakupata kutoka kwangu kwa sababu yake adhabu yenye kuumiza." Akamleta kwake. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Unauliza (mambo) yaliyozushwa?" 'Umar (رضي الله عنه) akatuma (mtu) kuleta makuti mabichi ya mtende, akampiga kwayo mpaka akaliacha mgongo wake na majeraha. Kisha akamwacha mpaka akapona, kisha akamrudia (kumpiga), kisha akamwacha mpaka akapona. Kisha akamwita ili amrudie (kumpiga). Akasema: Swabiygh akasema: Ikiwa unataka kuniua, basi niue kwa kuua kuzuri; na ikiwa unataka kunitibu, basi Wa-Allaahi nimekwisha pona. Akampa idhini (ya kurudi) katika nchi yake, na akamwandikia Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه) kwamba asikae naye yeyote miongoni mwa Waislamu. Hilo likawa zito kwa yule mtu. Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) akamwandikia 'Umar (رضي الله عنه): Kwamba tawbah yake imekuwa nzuri. 'Umar (رضي الله عنه) akamwandikia: Kwamba waruhusu watu kukaa naye.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
254
Hadiyth
150

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبِي خَالِدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَامِرًا، يَقُولُ: اسْتَفْتَى رَجُلٌ أُبَيَّ بْنَ كَعْبٍ، فَقَالَ: يَا أَبَا الْمُنْذِرِ، مَا تَقُولُ فِي كَذَا وَكَذَا؟، قَالَ: يَا بُنَيَّ، أَكَانَ الَّذِي سَأَلْتَنِي عَنْهُ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: "أَمَّا لَا، فَأَجِّلْنِي حَتَّى يَكُونَ، فَنُعَالِجَ أَنْفُسَنَا حَتَّى نُخْبِرَكَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Zuhayr, ametusimulia Ismaa'iyl bin Abiy Khaalid, amesema: Nilimsikia 'Aamir akisema: Mtu mmoja alimwomba Fatwa Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه), akasema: Yaa Abal-Mundhir, unasemaje kuhusu kadhaa na kadhaa? Akasema: Yaa mwanangu, je, limetokea lile uliloniuliza? Akasema: Hapana. Akasema: "Ama ikiwa sivyo, basi niakhirishie mpaka litokee, tuzitaabishe nafsi zetu (kulifanyia kazi) mpaka tukukhabarishe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
255
Hadiyth
151

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، أَخْبَرَنَا أَبُو عَوَانَةَ، قَالَ: أَخْبَرَنَا عَنْ فِرَاسٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ: كُنْتُ أَمْشِي مَعَ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَقَالَ فَتًى: مَا تَقُولُ يَا عَمَّاهُ كَذَا وَكَذَا؟، قَالَ: يَا ابْنَ أَخِي، أَكَانَ هَذَا؟، قَالَ: لَا، قَالَ: "فَأَعْفِنَا حَتَّى يَكُونَ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametukhabarisha Abuw 'Awaanah, amesema: Ametukhabarisha, kutoka kwa Firaas, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Masruwq, amesema: Nilikuwa natembea pamoja na Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه); kijana mmoja akasema: Unasemaje, yaa ami yangu, kadhaa na kadhaa? Akasema: Yaa mwana wa ndugu yangu, je, hili limetokea? Akasema: Hapana. Akasema: "Basi tuachilie mpaka litokee."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
255
Hadiyth
152

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: "كَانَ إِبْرَاهِيمُ إِذَا سُئِلَ عَنْ شَيْءٍ لَمْ يُجِبْ فِيهِ إِلَّا جَوَابَ الَّذِي سُئِلَ عَنْهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: "Ibraahiym alikuwa anapoulizwa kuhusu kitu, hajibu ndani yake ila jawabu la kile alichoulizwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
256
Hadiyth
153

أَخْبَرَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ الْوَلِيدِ، عَنْ وُهَيْبٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ "أَنَّهُ كَانَ لَا يُفْتِي فِي الْفَرْجِ بِشَيْءٍ فِيهِ اخْتِلَافٌ"

Ametukhabarisha Al-Husayn bin Manswuwr, ametusimulia Al-Husayn bin Al-Waliyd, kutoka kwa Wuhayb, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn: "Kwamba yeye alikuwa hatoi Fatwa kuhusu (mambo ya) tupu kwa kitu chochote chenye khitilafu ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
256
Hadiyth
154

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا الصَّلْتُ بْنُ رَاشِدٍ، قَالَ: سَأَلْتُ طَاوُسًا عَنْ مَسْأَلَةٍ، فَقَالَ لِي: كَانَ هَذَا؟، قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: آللَّهِ، قُلْتُ: آللَّهِ، ثُمّ قَالَ: إِنَّ أَصْحَابَنَا أَخْبَرُونَا عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ قَالَ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، لَا تَعْجَلُوا بِالْبَلَاءِ قَبْلَ نُزُولِهِ، فَيُذْهَبُ بِكُمْ هَاهُنَا وَهَاهُنَا، فَإِنَّكُمْ إِنْ لَمْ تَعْجَلُوا بِالْبَلَاءِ قَبْلَ نُزُولِهِ، لَمْ يَنْفَكَّ الْمُسْلِمُونَ أَنْ يَكُونَ فِيهِمْ مَنْ إِذَا سُئِلَ، سُدَّدَ، وَإِذَا قَالَ، وُفِّقَ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Asw-Swalt bin Raashid, amesema: Nilimuuliza Twaawus kuhusu suala moja, akaniambia: Je, hili limetokea? Nikasema: Ndiyo. Akasema: (Unaapa) kwa Allaah? Nikasema: (Naapa) kwa Allaah. Kisha akasema: Hakika wenzetu walitukhabarisha kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) kwamba alisema: "Enyi watu! Msiiharakishe balaa kabla ya kushuka kwake, mkapelekwa huku na huko. Kwani nyinyi msipoiharakisha balaa kabla ya kushuka kwake, Waislamu hawataacha kuwa miongoni mwao yupo ambaye akiulizwa huelekezwa kwenye usahihi, na akisema huwafikishwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
256
Hadiyth
155

حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مَيْمُونٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، - سَأَلْتُهُ عَنْ رَجُلٍ أَدْرَكَهُ رَمَضَانَانِ - فَقَالَ: أَكَانَ أَوْ لَمْ يَكُنْ؟، قَالَ: لَمْ يَكُنْ بَعْدُ، قَالَ: اتْرُكْ بَلِيَّتَهُ حَتَّى تَنْزِلَ، قَالَ: فَدَلَسْنَا لَهُ رَجُلًا، فَقَالَ: قَدْ كَانَ، فَقَالَ "يُطْعِمُ عَنْ الْأَوَّلِ مِنْهُمَا ثَلَاثِينَ مِسْكِينًا، لِكُلِّ يَوْمٍ مِسْكِينٌ"

Ametusimulia Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa 'Amr bin Maymuwn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) — nilimuuliza kuhusu mtu aliyefikiwa na Ramadhwaan mbili —, akasema: Je, limetokea au halijatokea? Akasema: Halijatokea bado. Akasema: "Iache balaa yake mpaka ishuke." Akasema: Tukampenyezea mtu (kwa hila), akasema: Limekwisha tokea. Akasema: Atalisha kwa ajili ya ile ya kwanza kati ya hizo mbili masikini thelathini; kwa kila siku masikini mmoja.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
257
Hadiyth
156

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ سُلَيْمَانَ، حَدَّثَنَا الْعُمَرِيُّ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: كُنْتُ أَجْلِسُ بِمَكَّةَ إِلَى ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ يَوْمًا، وَإِلَى ابْنِ عَبَّاس رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا يَوْمًا، فَمَا يَقُولُ ابْنُ عُمَرَ فِيمَا يُسْأَلُ "لَا عِلْمَ لِي، أَكْثَرُ مِمَّا يُفْتِي بِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Is-haaq bin Sulaymaan, ametusimulia Al-'Umariy, kutoka kwa 'Ubayd bin Jurayj, amesema: Nilikuwa nikikaa Makkah kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) siku moja, na kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) siku (nyingine). Basi kauli ya Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) katika anayoulizwa: "Sina ilimu," ilikuwa nyingi zaidi kuliko anayoyatolea Fatwa.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
257
Hadiyth
157

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "تَعَلَّمُوا، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَا يَدْرِي مَتَى يُخْتَلفُ إِلَيْهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni, kwani mmoja wenu hajui ni lini (watu) watamwendea (kumuuliza)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
257
Hadiyth
158

20-Mlangoباب الفتيا وما فيه من الشدةMlango Wa Kutoa Fatwa Na Uzito Uliomo Ndani Yake

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي أَيُّوبَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي جَعْفَرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَجْرَؤُكُمْ عَلَى الْفُتْيَا، أَجْرَؤُكُمْ عَلَى النَّارِ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Muwsaa, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Ayyuwb, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Ja'far, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwenye ujasiri zaidi kati yenu juu ya kutoa Fatwa ndiye mwenye ujasiri zaidi kati yenu juu ya moto."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
258
Hadiyth
159

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ عَبْدَةَ بْنِ أَبِي لُبَابَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مَنْ أَحْدَثَ رَأْيًا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ، وَلَمْ تَمْضِ بِهِ سُنَّةٌ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، لَمْ يَدْرِ عَلَى مَا هُوَ مِنْهُ إِذَا لَقِيَ اللَّهَ عز وجل"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa 'Abdah bin Abiy Lubaabah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Atakayezusha rai isiyokuwemo katika Kitabu cha Allaah, wala haikupita kwayo Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), hatajua yuko katika hali gani kuhusu hilo atakapokutana na Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
259
Hadiyth
160

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي أَيُّوبَ، حَدَّثَنِي بَكْرُ بْنُ عَمْرٍو الْمَعَافِرِيُّ، عَنْ أَبِي عُثْمَانَ مُسْلِمِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أُفْتِيَ بِفُتْيَا مِنْ غَيْرِ ثَبْتٍ فَإِنَّمَا إِثْمُهُ عَلَى مَنْ أَفْتَاهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd bin Abiy Ayyuwb, amenisimulia Bakr bin 'Amr Al-Ma'aafiriy, kutoka kwa Abuw 'Uthmaan Muslim bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): "Atakayepewa Fatwa bila ya uthibitisho, basi dhambi yake ni juu ya aliyempa Fatwa hiyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
259
Hadiyth
161

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي سِنَانٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "مَنْ أَفْتَى بِفُتْيَا يُعَمَّى عَنْهَا، فَإِثْمُهَا عَلَيْه"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Sinaan, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Atakayetoa Fatwa ambayo yeye mwenyewe hana uoni nayo (haijui hakika yake), basi dhambi yake ni juu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
259
Hadiyth
162

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ بُرْقَانَ، حَدَّثَنَا مَيْمُونُ بْنُ مِهْرَانَ، قَالَ: كَانَ أَبُو بَكْرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، إِذَا وَرَدَ عَلَيْهِ الْخَصْمُ نَظَرَ فِي كِتَابِ اللَّهِ، فَإِنْ وَجَدَ فِيهِ مَا يَقْضِي بَيْنَهُمْ، قَضَى بِهِ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي الْكِتَابِ، وَعَلِمَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي ذَلِكَ الْأَمْرِ سُنَّةً، قَضَى بِهِ، فَإِنْ أَعْيَاهُ، خَرَجَ فَسَأَلَ الْمُسْلِمِينَ، وَقَالَ: أَتَانِي كَذَا وَكَذَا، فَهَلْ عَلِمْتُمْ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَضَى فِي ذَلِكَ بِقَضَاءٍ؟ فَرُبَّمَا اجْتَمَعَ إِلَيْهِ النَّفَرُ كُلُّهُمْ يَذْكُرُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهِ قَضَاءً، فَيَقُولُ أَبُو بَكْرٍ: "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي جَعَلَ فِينَا مَنْ يَحْفَظُ عَلَى نَبِيِّنَا صلى الله عليه وسلم فَإِنْ أَعْيَاهُ أَنْ يَجِدَ فِيهِ سُنَّةً مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، جَمَعَ رُءُوسَ النَّاسِ وَخِيَارَهُمْ فَاسْتَشَارَهُمْ، فَإِذَا اجْتَمَعَ رَأْيُهُمْ عَلَى أَمْرٍ، قَضَى بِهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Ja'far bin Burqaan, ametusimulia Maymuwn bin Mihraan, amesema: Abuw Bakr (رضي الله عنه) alikuwa wanapomjia wenye kesi, hutazama katika Kitabu cha Allaah; akikuta ndani yake cha kuhukumu baina yao, huhukumu kwacho. Na kama hakimo katika Kitabu, naye akajua Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika jambo hilo, huhukumu kwayo. Likimshinda, hutoka akawauliza Waislamu, na husema: "Nimejiwa na kadhaa na kadhaa; je, mnajua kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu katika hilo hukmu (fulani)?" Huenda wakakusanyika kwake kundi la watu, kila mmoja wao akitaja hukmu ndani yake kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Basi Abuw Bakr (رضي الله عنه) husema: "Himdi ni ya Allaah Ambaye Amejaalia miongoni mwetu mwenye kuhifadhi (Sunnah) kutoka kwa Nabiy wetu (صلى الله عليه وآله وسلم)." Na likimshinda kupata ndani yake Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), huwakusanya wakuu wa watu na wabora wao, akawashauri. Rai yao ikikubaliana juu ya jambo, huhukumu kwalo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
259
Hadiyth
163

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، وَعَمْرُو بْنُ زُرَارة، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِي سُهَيْلٍ، قَالَ: كَانَ عَلَى امْرَأَتِي اعْتِكَافُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ، فَسَأَلْتُ عُمَرَ بْنَ عَبْدِ الْعَزِيزِ، وَعِنْدَهُ ابْنُ شِهَابٍ، قَالَ: قُلْتُ عَلَيْهَا صِيَامٌ، قَالَ ابْنُ شِهَابٍ: لَا يَكُونُ اعْتِكَافٌ إِلَّا بِصِيَامٍ، فَقَالَ لَهُ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ: أَعَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: فَعَنْ أَبِي بَكْرٍ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: فَعَنْ عُمَرَ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: فَعَنْ عُثْمَانَ؟، قَالَ: لَا، قَالَ عُمَرُ: مَا أَرَى عَلَيْهَا صِيَامًا، فَخَرَجْتُ فَوَجَدْتُ طَاوُسًا، وَعَطَاءَ بْنَ أَبِي رَبَاحٍ، فَسَأَلْتُهُمَا، فَقَالَ طَاوُسٌ: كَانَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، "لَا يَرَى عَلَيْهَا صِيَامًا إِلَّا أَنْ تَجْعَلَهُ عَلَى نَفْسِهَا"، قَالَ: وَقَالَ عَطَاءٌ: ذَلِكَ رَأْيِي

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Muwsaa na 'Amr bin Zuraarah, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa Abuw Suhayl, amesema: Mke wangu alikuwa na (nadhiri ya) i'tikaaf (kukaa Msikitini kwa ajili ya ibaada) ya siku tatu katika Al-Masjid Al-Haraam. Nikamuuliza 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz, na kwake alikuwepo Ibn Shihaab. Amesema: Nikasema: Je, ni juu yake Swiyaam? Ibn Shihaab akasema: Hakuna i'tikaaf ila kwa Swiyaam. 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz akamwambia: Je, ni kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Hapana. Akasema: Basi ni kutoka kwa Abuw Bakr (رضي الله عنه)? Akasema: Hapana. Akasema: Basi ni kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه)? Akasema: Hapana. Akasema: Basi ni kutoka kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه)? Akasema: Hapana. 'Umar [bin 'Abdil-'Aziyz] akasema: Sioni kuwa ni juu yake Swiyaam. Nikatoka nikawakuta Twaawus na 'Atwaa bin Abiy Rabaah, nikawauliza. Twaawus akasema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) "alikuwa haoni kuwa ni juu yake Swiyaam isipokuwa akiijaalia juu ya nafsi yake." Akasema: Na 'Atwaa akasema: Hiyo ndiyo rai yangu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
262
Hadiyth
164

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا أَبُو عَقِيلٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، قَالَ: لَمَّا قَدِمَ أَبُو سَلَمَةَ الْبَصْرَةَ، أَتَيْتُهُ أَنَا، وَالْحَسَنُ، "فَقَالَ لِلْحَسَنِ: أَنْتَ الْحَسَنُ؟ مَا كَانَ أَحَدٌ بِالْبَصْرَةِ أَحَبَّ إِلَيَّ لِقَاءً مِنْكَ، وَذَلِكَ أَنَّهُ بَلَغَنِي أَنَّكَ تُفْتِي بِرَأْيِكَ، فَلَا تُفْتِ بِرَأْيِكَ إِلَّا أَنْ تَكُونَ سُنَّةٌ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَوْ كِتَابٌ مُنْزَلٌ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Abuw 'Aqiyl, ametusimulia Sa'iyd Al-Jurayriy, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, amesema: Abuw Salamah alipokuja Al-Baswrah, nilimwendea mimi na Al-Hasan. "Akamwambia Al-Hasan: Wewe ndiye Al-Hasan? Hakuwepo yeyote katika Al-Baswrah niliyependa zaidi kukutana naye kuliko wewe; na hiyo ni kwa sababu imenifikia kwamba wewe unatoa Fatwa kwa rai yako. Basi usitoe Fatwa kwa rai yako isipokuwa iwe kuna Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), au Kitabu kilichoteremshwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
263
Hadiyth
165

أَخْبَرَنَا عِصْمَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ الْحُبَابِ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ عُقْبَةَ، حَدَّثَنَا الضَّحَّاكُ، عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ، أَنَّ ابْنَ عُمَرَ لَقِيَهُ فِي الطَّوَافِ، فَقَالَ لَهُ: "يَا أَبَا الشَّعْثَاءِ إِنَّكَ مِنْ فُقَهَاءِ الْبَصْرَةِ فَلَا تُفْتِ إِلَّا بِقُرْآنٍ نَاطِقٍ، أَوْ سُنَّةٍ مَاضِيَةٍ، فَإِنَّكَ إِنْ فَعَلْتَ غَيْرَ ذَلِكَ، هَلَكْتَ وَأَهْلَكْتَ"

Ametukhabarisha 'Iswmah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Zayd bin Al-Hubaab, kutoka kwa Yaziyd bin 'Uqbah, ametusimulia Adhw-Dhwahhaak, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kwamba Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikutana naye katika Twawaaf, akamwambia: "Yaa Abash-Sha'thaa, hakika wewe ni miongoni mwa Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wa Al-Baswrah; basi usitoe Fatwa ila kwa Qur-aan inayotamka (wazi), au Sunnah iliyothibiti. Kwani ukifanya kinyume na hivyo, utaangamia na utaangamiza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
263
Hadiyth
166

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ حُرَيْثِ بْنِ ظُهَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "أَتَى عَلَيْنَا زَمَانٌ لَسْنَا نَقْضِي وَلَسْنَا هُنَالِكَ، وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ قَدَّرَ مِنْ الْأَمْرِ أَنْ قَدْ بَلَغْنَا مَا تَرَوْنَ، فَمَنْ عَرَضَ لَهُ قَضَاءٌ بَعْدَ الْيَوْمِ، فَلْيَقْضِ فِيهِ بِمَا فِي كِتَابِ اللَّهِ عز وجل فَإِنْ جَاءَهُ مَا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ، فَلْيَقْضِ بِمَا قَضَى بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَإِنْ جَاءَهُ مَا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ، وَلَمْ يَقْضِ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلْيَقْضِ بِمَا قَضَى بِهِ الصَّالِحُونَ، وَلَا يَقُلْ إِنِّي أَخَافُ، وَإِنِّي أُرَى، فَإِنَّ الْحَرَامَ بَيِّنٌ، وَالْحَلَالَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَ ذَلِكَ أُمُورٌ مُشْتَبِهَةٌ، فَدَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لَا يَرِيبُكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa 'Umaarah bin 'Umayr, kutoka kwa Hurayth bin Dhwuhayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Kumetupitia zama ambazo hatukuwa tukihukumu, wala hatukuwa huko (katika daraja hiyo). Na hakika Allaah Amekadiria katika jambo hili kwamba tumefikia (hali) mnayoiona. Basi atakayekabiliwa na kesi baada ya leo, ahukumu ndani yake kwa yaliyomo katika Kitabu cha Allaah (عز وجل). Likimjia lisilokuwemo katika Kitabu cha Allaah, ahukumu kwa aliyohukumu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Likimjia lisilokuwemo katika Kitabu cha Allaah, wala hakulihukumu Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ahukumu kwa waliyohukumu watu wema. Wala asiseme: Hakika mimi naogopa, na hakika mimi naona. Kwani haraam iko wazi, na halaal iko wazi, na baina ya hayo kuna mambo yenye kutatanisha. Basi acha kinachokutia shaka, uende kwa kisichokutia shaka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
263
Hadiyth
167

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي يَزِيدَ، قَالَ: كَانَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا "إِذَا سُئِلَ عَنْ الْأَمْرِ فَكَانَ فِي الْقُرْآنِ، أَخْبَرَ بِهِ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي الْقُرْآنِ وَكَانَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَخْبَرَ بِهِ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ، فَعَنْ أَبِي بَكْرٍ، وَعُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فَإِنْ لَمْ يَكُنْ، قَالَ فِيهِ بِرَأْيِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Yaziyd, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) "alikuwa anapoulizwa kuhusu jambo, likiwa limo katika Qur-aan, hulikhabarisha; na kama halimo katika Qur-aan, na likawa (limepokewa) kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), hulikhabarisha; na kama halikuwa (hivyo), basi (huchukua) kutoka kwa Abuw Bakr na 'Umar (رضي الله عنهما); na kama halikuwa (hivyo), husema ndani yake kwa rai yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
263
Hadiyth
168

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ شُرَيْحٍ: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ كَتَبَ إِلَيْهِ: "إِنْ جَاءَكَ شَيْءٌ فِي كِتَابِ اللَّهِ، فَاقْضِ بِهِ وَلَا تَلْفِتْكَ عَنْهُ الرِّجَالُ، فَإِنْ جَاءَكَ مَا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ فَانْظُرْ سُنَّةَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَاقْضِ بِهَا، فَإِنْ جَاءَكَ مَا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ وَلَمْ يَكُنْ فِيهِ سُنَّةٌ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَانْظُرْ مَا اجْتَمَعَ عَلَيْهِ النَّاسُ فَخُذْ بِهِ، فَإِنْ جَاءَكَ مَا لَيْسَ فِي كِتَابِ اللَّهِ وَلَمْ يَكُنْ فِي سُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَمْ يَتَكَلَّمْ فِيهِ أَحَدٌ قَبْلَكَ، فَاخْتَرْ أَيَّ الْأَمْرَيْنِ شِئْتَ: إِنْ شِئْتَ أَنْ تَجْتَهِدَ بِرَأْيَكَ ثُمَّ تُقَدَّمَ فَتَقَدَّمْ، وَإِنْ شِئْتَ أَنْ تَتَأَخَّرَ، فَتَأَخَّرْ، وَلَا أَرَى التَّأَخُّرَ إِلَّا خَيْرًا لَكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Shurayh, kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) alimwandikia: "Likikujia jambo lililomo katika Kitabu cha Allaah, basi hukumu kwalo, wala wasikugeuze watu kutoka kwalo. Likikujia lisilokuwemo katika Kitabu cha Allaah, basi tazama Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), uhukumu kwayo. Likikujia lisilokuwemo katika Kitabu cha Allaah, wala halikuwa na Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi tazama yale waliyokubaliana watu, uyachukue. Likikujia lisilokuwemo katika Kitabu cha Allaah, wala halikuwa katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), wala hakulizungumza yeyote kabla yako, basi chagua lolote ulitakalo kati ya mambo mawili: ukitaka kujitahidi kwa rai yako kisha usonge mbele, basi songa mbele; na ukitaka kurudi nyuma, basi rudi nyuma; na sioni kurudi nyuma ila ni kheri kwako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
265
Hadiyth
169

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ الثَّقَفِيِّ، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ عَمْرِو ابْنِ أَخِي الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، عَنْ نَاسٍ مِنْ أَهْلِ حِمْصٍ مِنْ أَصْحَابِ مُعَاذٍ، عَنْ مُعَاذٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا بَعَثَهُ إِلَى الْيَمَنِ، قَالَ: "أَرَأَيْتَ إِنْ عَرَضَ لَكَ قَضَاءٌ كَيْفَ تَقْضِي؟"، قَالَ: أَقْضِي بِكِتَابِ اللَّهِ، قَالَ: "فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي كِتَابِ اللَّهِ؟"، قَالَ: فَبِسُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِي سُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ؟"، قَالَ: أَجْتَهِدُ رَأْيِي وَلَا آلُو، قَالَ: فَضَرَبَ صَدْرَهُ، ثُمَّ قَالَ: "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي وَفَّقَ رَسُولَ رَسُولِ اللَّهِ لِمَا يُرْضِي رَسُولَ اللَّهِ"

Ametusimulia Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muhammad bin 'Ubaydi-Allaah Ath-Thaqafiy, kutoka kwa Al-Haarith bin 'Amr, mwana wa ndugu yake Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه), kutoka kwa watu wa Himsw miongoni mwa wanafunzi wa Mu'aadh, kutoka kwa Mu'aadh (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Yemen, alisema: "Waonaje ikikukabili kesi, utahukumu vipi?" Akasema: Nitahukumu kwa Kitabu cha Allaah. Akasema: "Na ikiwa haimo katika Kitabu cha Allaah?" Akasema: Basi kwa Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: "Na ikiwa haimo katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah?" Akasema: Nitajitahidi kwa rai yangu, wala sitafanya taksiri. Akasema: Akampiga kifuani mwake, kisha akasema: "Himdi ni ya Allaah Ambaye Amemwafikisha mjumbe wa Rasuli wa Allaah kwa yale yanayomridhisha Rasuli wa Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
266
Hadiyth
170

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ حُرَيْثِ بْنِ ظُهَيْرٍ، قَالَ: أَحْسَبُ أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "قَدْ أَتَى عَلَيْنَا زَمَانٌ وَمَا نُسْأَلُ، وَمَا نَحْنُ هُنَاكَ، وَإِنَّ اللَّهَ قَدَّرَ أَنْ بَلَغْتُ مَا تَرَوْنَ، فَإِذَا سُئِلْتُمْ عَنْ شَيْءٍ، فَانْظُرُوا فِي كِتَابِ اللَّهِ، فَإِنْ لَمْ تَجِدُوهُ فِي كِتَابِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ فَفِي سُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ، فَإِنْ لَمْ تَجِدُوهُ فِي سُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ، فَمَا أَجْمَعَ عَلَيْهِ الْمُسْلِمُونَ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيمَا أَجْمَعَ عَلَيْهِ الْمُسْلِمُونَ، فَاجْتَهِدْ رَأْيَكَ، وَلَا تَقُلْ: إِنِّي أَخَافُ وَأَخْشَى، فَإِنَّ الْحَلَالَ بَيِّنٌ، وَالْحَرَامَ بَيِّنٌ، وَبَيْنَ ذَلِكَ أُمُورٌ مُشْتَبِهَةٌ، فَدَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لَا يَرِيبُكَ"،

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa 'Umaarah bin 'Umayr, kutoka kwa Hurayth bin Dhwuhayr, amesema: Nadhani kwamba 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) alisema: "Kwa hakika kumetupitia zama tulizokuwa hatuulizwi, wala hatukuwa huko (katika daraja hiyo). Na hakika Allaah Amekadiria kwamba nimefikia (hali) mnayoiona. Basi mtakapoulizwa kuhusu jambo, tazameni katika Kitabu cha Allaah; msipolikuta katika Kitabu cha Allaah (عز وجل), basi (tazameni) katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah; msipolikuta katika Sunnah ya Rasuli wa Allaah, basi (tazameni) yale waliyoyakubali kwa pamoja Waislamu; na kama halimo katika yale waliyoyakubali kwa pamoja Waislamu, basi jitahidi kwa rai yako, wala usiseme: Hakika mimi naogopa na nakhofu. Kwani halaal iko wazi, na haraam iko wazi, na baina ya hayo kuna mambo yenye kutatanisha. Basi acha kinachokutia shaka, uende kwa kisichokutia shaka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
269
Hadiyth
171

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ أَبِي عَوَانَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَن عَبْدِ اللَّهِ، نَحْوَهُ،

Ametusimulia Yahyaa bin Hammaad, kutoka kwa Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa 'Umaarah bin 'Umayr, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), mfano wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
270
Hadiyth
172

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَن عَبْدِ اللَّهِ، بِنَحْوِهِ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Al-Qaasim bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kwa mfano wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
270
Hadiyth
173

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّكُمْ سَتُحْدِثُونَ وَيُحْدَثُ لَكُمْ، فَإِذَا رَأَيْتُمْ مُحْدَثَةً فَعَلَيْكُمْ بِالْأَمْرِ الْأَوَّلِ"، قَالَ حَفْصٌ: كُنْتُ أُسْنِدُ، عَنْ حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، ثُمَّ دَخَلَنِي مِنْهُ شَكٌّ

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Hafsw bin Ghiyaath, ametusimulia Al-A'mash, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Enyi watu! Hakika nyinyi mtazusha (mambo mapya), na mtazushiwa (mambo mapya). Basi mtakapoona jambo lililozushwa, shikamaneni na jambo la mwanzo." Hafsw amesema: Nilikuwa nikiitaja kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa Abuw 'Abdir-Rahmaan; kisha shaka ikaniingia kuhusu hilo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
270
Hadiyth
174

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ لِابْنِ مَسْعُودٍ: "أَلَمْ أُنْبَأْ أَوْ أُنْبِئْتُ أَنَّكَ تُفْتِي وَلَسْتَ بِأَمِيرٍ؟ وَلِّ حَارَّهَا مَنْ تَوَلَّى قَارَّهَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) alimwambia Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه): "Je, sikukhabarishwa — au: nimekhabarishwa — kwamba wewe unatoa Fatwa na hali wewe si amiri? Mwachie joto lake yule aliyeshika ubaridi wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
270
Hadiyth
175

21-MlangoبابMlango Wa [Kuhusu Anayeulizwa
Asiyoyajua, Na Kusema: Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi]

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: "إِنَّ الَّذِي يُفْتِي النَّاسَ فِي كُلِّ مَا يُسْتَفْتَى لَمَجْنُونٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Hakika yule anayewapa watu Fatwa katika kila jambo analoombwa Fatwa, kwa yakini ni mwendawazimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
272
Hadiyth
176

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ حُذَيْفَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِنَّمَا يُفْتِي النَّاسَ ثَلَاثَةٌ: رَجُلٌ إِمَامٌ أَوْ وَالٍ، وَرَجُلٌ يَعْلَمُ نَاسِخَ الْقُرْآنِ مِنْ الْمَنْسُوخِ"، قَالُوا: يَا حُذَيْفَةُ، مَنْ ذَاكَ؟، قَالَ: "عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ، أَوْ أَحْمَقُ مُتَكَلِّفٌ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه), amesema: "Hakika wanaowapa watu Fatwa ni watatu tu: mtu ambaye ni Imaam au mtawala; na mtu anayejua kinachofuta (hukmu) katika Qur-aan na kilichofutwa" — wakasema: Yaa Hudhayfah, ni nani huyo? Akasema: "'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه)" — "au mpumbavu mwenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
272
Hadiyth
177

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ حَسَّانَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ بْنِ حُذَيْفَةَ، قَالَ: قَالَ حُذَيْفَةُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "إِنَّمَا يُفْتِي النَّاسَ أَحَدُ ثَلَاثَةٍ: رَجُلٌ عَلِمَ نَاسِخَ الْقُرْآنِ مِنْ مَنْسُوخِهِ"، قَالُوا: وَمَنْ ذَاكَ؟، قَالَ: "عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ، قَالَ: وَأَمِيرٌ لَا يَجِدُ بُدًّا، أَوْ أَحْمَقُ مُتَكَلِّفٌ"، ثُمَّ قَالَ مُحَمَّدٌ: فَلَسْتُ بِوَاحِدٍ مِنْ هَذَيْنِ، وَأَرْجُو أَنْ لَا أَكُونَ الثَّالِثَ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametupa khabari Abuw Usaamah, kutoka kwa Hishaam bin Hassaan, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa Abuw 'Ubaydah bin Hudhayfah, amesema: Hudhayfah (رضي الله عنه) amesema: "Hakika anayewapa watu Fatwa ni mmoja wa watatu: mtu anayejua kinachofuta (hukmu) katika Qur-aan na kilichofutwa katika hiyo." Wakasema: Na ni nani huyo? Akasema: "'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه)." Akasema: "Na amiri asiyepata budi (ila kutoa Fatwa), au mpumbavu mwenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu." Kisha Muhammad akasema: Basi mimi si mmoja wa hawa wawili, na ninatumaini nisiwe wa tatu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
272
Hadiyth
178

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "مَنْ عَلِمَ مِنْكُمْ عِلْمًا، فَلْيَقُلْ بِهِ، وَمَنْ لَمْ يَعْلَمْ، فَلْيَقُلْ لِمَا لَا يَعْلَمُ: اللَّهُ أَعْلَمُ، فَإِنَّ: الْعَالِمَ إِذَا سُئِلَ عَمَّا لَا يَعْلَمُ، قَالَ: اللَّهُ عز وجل أَعْلَمُ، وَقَدْ قَالَ اللَّهُ لِرَسُولِهِ: {قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ}"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Yeyote miongoni mwenu anayejua ilimu, basi aiseme; na asiyejua, basi aseme kuhusu asichokijua: Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. Kwani 'Aalim (Mwanazuoni) anapoulizwa asichokijua, husema: Allaah (عز وجل) Ndiye Mjuzi zaidi." [Akasema]: Na kwa hakika Allaah Amemwambia Rasuli Wake:

قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُتَكَلِّفِينَ

Sema: Sikuombeni ujira wowote juu ya hili, na wala mimi si miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu. [Swaad (38:86)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
179

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَبِي رَجَاءٍ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ، أَنَّ أَبَا مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ فِي خُطْبَتِهِ: "مَنْ عَلِمَ عِلْمًا، فَلْيُعَلِّمْهُ النَّاسَ، وَإِيَّاهُ أَنْ يَقُولَ مَا لَا عِلْمَ لَهُ بِهِ فَيَمْرُقَ مِنْ الدِّينِ وَيَكُونَ مِنْ الْمُتَكَلِّفِينَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Humayd, kutoka kwa Abuw Rajaa, kutoka kwa Abul-Muhallab, kwamba Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) alisema katika khutbah (hotuba) yake: "Mwenye kujua ilimu, basi awafundishe watu; na ajiepushe kusema asilokuwa na ilimu nalo, akatoka katika Dini, na akawa miongoni mwa wenye kujidai kuzusha chochote kisichohusu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
180

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ أَبِي الْبَخْتَرِيِّ، وَزَاذَانَ، قَالَا: قَالَ عَلِيٌّ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ: "وَا بَرْدَهَا عَلَى الْكَبِدِ إِذَا سُئِلْتُ عَمَّا لَا أَعْلَمُ، أَنْ أَقُولَ: اللَّهُ أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Abul-Bakhtariy na Zaadhaan, wamesema: 'Aliy (رضوان الله عليه) amesema: "Lo! Ubaridi ulioje juu ya ini, ninapoulizwa nisiyoyajua, kusema: Allaah Ndiye Mjuzi zaidi!"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
181

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ أَبِي الْبَخْتَرِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ، قَالَ: "يَا بَرْدَهَا عَلَى الْكَبِدِ أَنْ تَقُولَ لِمَا لَا تَعْلَمُ: اللَّهُ أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Abul-Bakhtariy, kutoka kwa 'Aliy (رضوان الله عليه), amesema: "Lo! Ubaridi ulioje juu ya ini, kusema kuhusu usiyoyajua: Allaah Ndiye Mjuzi zaidi!"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
182

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا عُمَيْرُ بْنُ عَرْفَجَةَ، حَدَّثَنَا رَزِينٌ أَبُو النُّعْمَانِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِذَا سُئِلْتُمْ عَمَّا لَا تَعْلَمُونَ، فَاهْرُبُوا"، قَالَ: وَكَيْفَ الْهَرَبُ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ؟، قَالَ: "تَقُولُونَ: اللَّهُ أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia 'Umayr bin 'Arfajah, ametusimulia Raziyn Abun-Nu'maan, kutoka kwa 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه), amesema: "Mtakapoulizwa msiyoyajua, basi kimbieni." (Mtu mmoja) akasema: Na vipi kukimbia, yaa Amiri wa Waumini? Akasema: "Mseme: Allaah Ndiye Mjuzi zaidi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
183

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُسْلِمٍ الْبَطِينِ، عَنْ عَزْرَةَ التَّمِيمِيِّ، قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "وَا بَرْدَهَا عَلَى الْكَبِدِ، ثَلَاثَ مَرَّاتٍ"، قَالُوا: وَمَا ذَلِكَ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ؟، قَالَ: "أَنْ يُسْأَلَ الرَّجُلُ عَمَّا لَا يَعْلَمُ، فَيَقُولُ: اللَّهُ أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Muslim Al-Batwiyn, kutoka kwa 'Azrah At-Tamiymiy, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Lo! Ubaridi ulioje juu ya ini" — mara tatu. Wakasema: Ni nini hicho, yaa Amiri wa Waumini? Akasema: "Mtu kuulizwa asiyoyajua, naye akasema: Allaah Ndiye Mjuzi zaidi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
184

أَخْبَرَنَا فَرْوَةُ بْنُ أَبِي الْمَغْرَاءِ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَجُلًا سَأَلَهُ عَنْ مَسْأَلَةٍ فَقَالَ: لَا عِلْمَ لِي بِهَا، فَلَمَّا أَدْبَرَ الرَّجُلُ، قَالَ ابْنُ عُمَرَ: "نِعْمَ مَا قَالَ ابْنُ عُمَرَ، سُئِلَ عَمَّا لَا يَعْلَمُ، فَقَالَ: لَا عِلْمَ لِي بِهِ"

Ametukhabarisha Farwah bin Abil-Maghraa, ametusimulia 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba mtu mmoja alimuuliza kuhusu suala fulani, akasema: Sina ilimu nalo. Yule mtu alipogeuka kuondoka, Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akasema: "Ni vizuri alivyosema Ibn 'Umar! Aliulizwa asilolijua, akasema: Sina ilimu nalo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
185

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "لَا أَدْرِي نِصْفُ الْعِلْمِ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "(Kusema:) Sijui, ni nusu ya ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
186

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ الْعُمَرِيُّ، عَنْ نَافِعٍ، أَنَّ رَجُلًا أَتَى ابْنَ عُمَرَ يَسْأَلُهُ عَنْ شَيْءٍ، فَقَالَ: "لَا عِلْمَ لِي، ثُمَّ الْتَفَتَ بَعْدَ أَنْ قَفَّي الرَّجُلُ، فَقَالَ: نِعْمَ مَا قَالَ ابْنُ عُمَرَ! يُسْأَلُ عَمَّا لَا يَعْلَمُ، فَقَالَ: لَا عِلْمَ لِي"، يَعْنِي: ابْنُ عُمَرَ نَفْسَهُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia 'Abdu-Allaah Al-'Umariy, kutoka kwa Naafi', kwamba mtu mmoja alimjia Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akimuuliza kuhusu jambo fulani, akasema: "Sina ilimu (nalo). Kisha akageuka (kutazama) baada ya yule mtu kuondoka, akasema: Ni vizuri alivyosema Ibn 'Umar! Anaulizwa asilolijua, akasema: Sina ilimu (nalo)" — yaani: Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) mwenyewe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
187

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، ثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مُغِيرَةَ، قَالَ: "كَانَ عَامِرٌ إِذَا سُئِلَ عَنْ شَيْءٍ، يَقُولُ: لَا أَدْرِي، فَإِنْ رُدُّوا عَلَيْهِ، قَالَ: إِنِّي حَلَفْتُ لَكَ بِاللَّهِ إِنْ كَانَ لِي بِهِ عِلْمٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Mughiyrah, amesema: "'Aamir alikuwa anapoulizwa jambo, husema: Sijui. Na wakimrudia (kwa kuuliza tena), husema: Hakika mimi nimekuapia kwa Allaah kwamba sina ilimu nalo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
188

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَفْصٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "مَا أُبَالِي سُئِلْتُ عَمَّا أَعْلَمُ أَوْ مَا لَا أَعْلَمُ، لِأَنِّي إِذَا سُئِلْتُ عَمَّا أَعْلَمُ، قُلْتُ مَا أَعْلَمُ، وَإِذَا سُئِلْتُ عَمَّا لَا أَعْلَمُ قُلْتُ: لَا أَعْلَمُ"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Hafsw, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Sijali kuulizwa ninachokijua au nisichokijua; kwa sababu ninapoulizwa ninachokijua, nasema ninachokijua; na ninapoulizwa nisichokijua, nasema: Sijui."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
189

أَخْبَرَنَا هَارُونُ، عَنْ حَفْصٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: "مَا سَمِعْتُ إِبْرَاهِيمَ يَقُولُ قَطُّ: حَلَالٌ وَلَا حَرَامٌ، إِنَّمَا كَانَ يَقُولُ: كَانُوا يَتَكْرَهُونَ، وَكَانُوا يَسْتَحِبُّونَ"

Ametukhabarisha Haaruwn, kutoka kwa Hafsw, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: "Sijapata kabisa kumsikia Ibraahiym akisema: (Hili ni) halaal, wala (hili ni) haraam. Hakika alikuwa akisema tu: Walikuwa wakilichukia (jambo hili), na walikuwa wakilipenda (jambo hili)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
273
Hadiyth
190

22-Mlangoباب تغير الزمان وما يحدث فيهMlango Wa Kubadilika Kwa Zama Na Yanayozuka Ndani Yake

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ شَقِيقٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "كَيْفَ أَنْتُمْ إِذَا لَبِسَتْكُمْ فِتْنَةٌ يَهْرَمُ فِيهَا الْكَبِيرُ وَيَرْبُو فِيهَا الصَّغِيرُ، وَيَتَّخِذُهَا النَّاسُ سُنَّةً، فَإِذَا غُيِّرَتْ، قَالُوا: غُيِّرَتْ السُّنَّةُ"، قَالُوا: وَمَتَى ذَلِكَ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ؟، قَالَ: "إِذَا كَثُرَتْ قُرَّاؤُكُمْ، وَقَلَّتْ فُقَهَاؤُكُمْ، وَكَثُرَتْ أُمَرَاؤُكُمْ، وَقَلَّتْ أُمَنَاؤُكُمْ، وَالْتُمِسَتِ الدُّنْيَا بِعَمَلِ الْآخِرَةِ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Shaqiyq, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Itakuwaje kwenu itakapowafunika fitna ambayo mkubwa atazeeka ndani yake, na mdogo atakua ndani yake, na watu wakaichukua kuwa ni Sunnah; na itakapobadilishwa, watasema: Sunnah imebadilishwa!" Wakasema: Na hilo litakuwa lini, yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan? Akasema: "Watakapokuwa wengi wasomaji wenu (wa Qur-aan), na wakawa wachache Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wenu, na wakawa wengi viongozi wenu, na wakawa wachache waaminifu wenu, na dunia ikatafutwa kwa amali ya Aakhirah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
278
Hadiyth
191

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "كَيْفَ أَنْتُمْ إِذَا لَبِسَتْكُمْ فِتْنَةٌ يَهْرَمُ فِيهَا الْكَبِيرُ وَيَرْبُو فِيهَا الصَّغِيرُ، إِذَا تُرِكَ مِنْهَا شَيْءٌ، قِيلَ: تُرِكَتْ السُّنَّةُ"، قَالُوا: وَمَتَى ذَلِكَ؟، قَالَ: "إِذَا ذَهَبَتْ عُلَمَاؤُكُمْ، وَكَثُرَتْ جُهَلَاؤُكُمْ، وَكَثُرَتْ قُرَّاؤُكُمْ، وَقَلَّتْ فُقَهَاؤُكُمْ، وَكَثُرَتْ أُمَرَاؤُكُمْ، وَقَلَّتْ أُمَنَاؤُكُمْ، وَالْتُمِسَتْ الدُّنْيَا بِعَمَلِ الْآخِرَةِ، وَتُفُقِّهَ لِغَيْرِ الدِّينِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Itakuwaje kwenu itakapowafunika fitna ambayo mkubwa atazeeka ndani yake, na mdogo atakua ndani yake; kikiachwa kitu chochote katika hiyo, husemwa: Sunnah imeachwa!" Wakasema: Na hilo litakuwa lini? Akasema: "Watakapoondoka 'Ulamaa (Wanazuoni) wenu, na wakawa wengi wajinga wenu, na wakawa wengi wasomaji wenu (wa Qur-aan), na wakawa wachache Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wenu, na wakawa wengi viongozi wenu, na wakawa wachache waaminifu wenu, na dunia ikatafutwa kwa amali ya Aakhirah, na ufahamu wa Dini ukatafutwa kwa ajili ya (lengo) lisilokuwa la Dini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
278
Hadiyth
192

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، قَالَ: أُنْبِئْتُ أَنَّهُ كَانَ يُقَالُ: "وَيْلٌ لِلْمُتَفَقِّهِينَ لِغَيْرِ الْعِبَادَةِ، وَالْمُسْتَحِلِّينَ الْحُرُمَاتِ بِالشُّبُهَاتِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amesema: Nimepewa khabari kwamba ilikuwa ikisemwa: "Ole wao wanaotafuta ufahamu wa Dini kwa ajili ya (lengo) lisilokuwa la ibaada, na wanaohalalisha yaliyoharamishwa kwa (hila za) mambo yenye utata!"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
279
Hadiyth
193

حَدَّثَنَا صَالِحُ بْنُ سُهَيْلٍ مَوْلَى يَحْيَى بْنِ أَبِي زَائِدَةَ، ثَنَا يَحْيَى، عَنْ مُجَالِدٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا يَأْتِي عَلَيْكُمْ عَامٌ إِلَّا وَهُوَ شَرٌّ مِنْ الَّذِي كَانَ قَبْلَهُ، أَمَا إِنِّي لَسْتُ أَعْنِي عَامًا أَخْصَبَ مِنْ عَامٍ، وَلَا أَمِيرًا خَيْرًا مِنْ أَمِيرٍ، وَلَكِنْ عُلَمَاؤُكُمْ وَخِيَارُكُمْ وَفُقَهَاؤُكُمْ يَذْهَبُونَ، ثُمَّ لَا تَجِدُونَ مِنْهُمْ خَلَفًا، وَيَجِيءُ قَوْمٌ يَقِيسُونَ الْأُمُورَ بِرَأْيِهِمْ"

Ametusimulia Swaalih bin Suhayl, mwachwa huru wa Yahyaa bin Abiy Zaaidah, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Mujaalid, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Hautawajia mwaka wowote ila utakuwa mbaya zaidi kuliko ule uliokuwa kabla yake. Ama mimi, sikusudii mwaka wenye rutuba zaidi kuliko mwaka (mwingine), wala amiri bora kuliko amiri (mwingine); lakini 'Ulamaa (Wanazuoni) wenu, na wabora wenu, na Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wenu wataondoka, kisha hamtapata miongoni mwao wa kushika nafasi yao; na watakuja watu watakaoyapima mambo kwa rai zao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
279
Hadiyth
194

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سُلَيْمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ دَاوُدَ بْنَ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "أَوَّلُ مَنْ قَاسَ إِبْلِيسُ، وَمَا عُبِدَتْ الشَّمْسُ وَالْقَمَرُ إِلَّا بِالْمَقَايِيسِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Yahyaa bin Sulaym, amesema: Nilimsikia Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Wa kwanza aliyefanya qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai) ni Ibliys; na jua na mwezi havikuabudiwa ila kwa sababu ya vipimo hivyo vya qiyaas."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
195

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ ابْنِ شَوْذَبٍ، عَنْ مَطَرٍ، عَنْ الْحَسَنِ أَنَّهُ تَلَا هَذِهِ الْآيَةَ: {خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ} قَالَ: "قَاسَ إِبْلِيسُ وَهُوَ أَوَّلُ مَنْ قَاسَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Ibn Shawdhab, kutoka kwa Matwar, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba aliisoma Aayah hii:

خَلَقْتَنِي مِنْ نَارٍ وَخَلَقْتَهُ مِنْ طِينٍ

Umeniumba kwa moto, na yeye Umemuumba kwa udongo [Al-A’raaf (7:12)]

Akasema: "Ibliys alifanya qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai), naye ndiye wa kwanza aliyefanya qiyaas."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
196

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ أَبِي خَالِدٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ مَسْرُوقٍ، أَنَّهُ قَالَ: "إِنِّي أَخَافُ، أَوْ أَخْشَى أَنْ أَقِيسَ، فَتَزِلَّ قَدَمِي"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Abiy Khaalid, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Masruwq, kwamba alisema: "Hakika mimi ninaogopa — au: ninahofia — kufanya qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai), mguu wangu ukateleza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
197

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا أَبُو خَالِدٍ الْأَحْمَرُ، عَنْ إِسْمَاعِيل، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "وَاللَّهِ لَئِنْ أَخَذْتُمْ بِالْمَقَايِيسِ، لَتُحَرِّمُنَّ الْحَلَالَ، وَلَتُحِلُّنَّ الْحَرَامَ"

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Abuw Khaalid Al-Ahmar, kutoka kwa Ismaa'iyl, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Wa-Allaahi, mkishika vipimo vya qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai), bila shaka mtaharamisha halaal, na bila shaka mtahalalisha haraam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
198

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ بِشْرٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ إِسْمَاعِيل، عَنْ عَامِرٍ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "مَا أَبْغَضَ إِلَيَّ أَرَأَيْتَ، أَرَأَيْتَ يَسْأَلُ الرَّجُلُ صَاحِبَهُ فَيَقُولُ: أَرَأَيْتَ وَكَانَ لَا يُقَايِسُ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Bishr, ametusimulia baba yangu, kutoka kwa Ismaa'iyl, kutoka kwa 'Aamir, kwamba alikuwa akisema: "Hakuna kitu ninachokichukia zaidi kuliko (kusema): Unaonaje? Unaonaje? — mtu anamuuliza mwenzake, akasema: Unaonaje (lau ingekuwa hivi)? Na alikuwa hafanyi qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
199

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ الزِّبْرِقَانِ، قَالَ: "نَهَانِي أَبُو وَائِلٍ أَنْ أُجَالِسَ أَصْحَابَ أَرَأَيْتَ"

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Az-Zibriqaan, amesema: "Abuw Waail alinikataza nisikae pamoja na watu wa (kusema): Unaonaje?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
200

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، أَنْبَأَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ إِسْمَاعِيل، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "لَوْ أَنَّ هَؤُلَاءِ كَانُوا عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَنَزَلَتْ عَامَّةُ الْقُرْآنِ يَسْأَلُونَكَ، يَسْأَلُونَكَ"

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametupa khabari Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Ismaa'iyl, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Lau hawa wangekuwa katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), bila shaka sehemu kubwa ya Qur-aan ingeteremka (kwa maneno): Wanakuuliza, Wanakuuliza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
201

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، أَخْبَرَنِي مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ طَلْحَةَ، عَنْ مَيْمُونٍ أَبِي حَمْزَةَ، قَالَ: قَالَ لِي إِبْرَاهِيمُ: "يَا أَبَا حَمْزَةَ، وَاللَّهِ لَقَدْ تَكَلَّمْتُ، وَلَوْ وَجَدْتُ بُدًّا مَا تَكَلَّمْتُ، وَإِنَّ زَمَانًا أَكُونُ فِيهِ فَقِيهَ أَهْلِ الْكُوفَةِ زَمَانُ سُوءٍ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, amenikhabarisha Muhammad — naye ni Ibn Twalhah —, kutoka kwa Maymuwn Abuw Hamzah, amesema: Ibraahiym aliniambia: "Yaa Abaa Hamzah, Wa-Allaahi, kwa hakika nimezungumza (kutoa Fatwa); na lau ningepata budi (njia nyingine), nisingezungumza. Na hakika zama ambazo mimi ninakuwa ndani yake Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh) wa watu wa Al-Kuwfah ni zama mbaya."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
280
Hadiyth
202

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "إِيَّايَ وَالْمُكَايَلَةَ"، يَعْنِي: فِي الْكَلَامِ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Najitahadharisha na mukaayalah (kulipizana kipimo kwa kipimo)" — yaani: katika maneno.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
282
Hadiyth
203

أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ الْبَصْرِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ الْهُذَلِيُّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "شَهِدْتُ شُرَيْحًا، وَجَاءَهُ رَجُلٌ مِنْ مُرَادٍ، فَقَالَ: يَا أَبَا أُمَيَّةَ، مَا دِيَةُ الْأَصَابِعِ؟، قَالَ: عَشْرٌ عَشْرٌ، قَالَ: يَا سُبْحَانَ اللَّهِ، أَسَوَاءٌ هَاتَانِ؟ جَمَعَ بَيْنَ الْخِنْصِرِ وَالْإِبْهَامِ، فَقَالَ شُرَيْحٌ: يَا سُبْحَانَ اللَّهِ، أَسَوَاءٌ أُذُنُكَ وَيَدُكَ؟ فَإِنَّ الْأُذُنَ يُوَارِيهَا الشَّعْرُ، وَالْكُمَّةُ وَالْعِمَامَةُ فِيهَا نِصْفُ الدِّيَةِ، وَفِي الْيَدِ نِصْفُ الدِّيَةِ، وَيْحَكَ: إِنَّ السُّنَّةَ سَبَقَتْ قِيَاسَكُمْ فَاتَّبِعْ وَلَا تَبْتَدِعْ، فَإِنَّكَ لَنْ تَضِلَّ مَا أَخَذْتَ بِالْأَثَرِ، قَالَ أَبُو بَكْرٍ: فَقَالَ لِي الشَّعْبِيُّ: يَا هُذَلِيُّ، لَوْ أَنَّ أَحْنَفَكُمْ قُتِلَ وَهَذَا الصَّبِيُّ فِي مَهْدِهِ أَكَانَ دِيَتُهُمَا سَوَاءً؟، قُلْتُ: نَعَمْ، قَالَ: فَأَيْنَ الْقِيَاسُ؟"

Ametukhabarisha Hajjaaj Al-Baswriy, ametusimulia Abuw Bakr Al-Hudhaliy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Nilikuwepo kwa Shurayh, na akamjia mtu mmoja wa (kabila la) Muraad, akasema: Yaa Abaa Umayyah, ni ipi diyah (fidia ya damu) ya vidole? Akasema: Kumi kumi (ngamia kumi kwa kila kidole). Akasema: Yaa Subhaana-Allaah! Je, hivi viwili ni sawa? — akaunganisha baina ya kidole kidogo na kidole gumba. Shurayh akasema: Yaa Subhaana-Allaah! Je, sikio lako na mkono wako ni sawa? Kwani sikio hufunikwa na nywele, na kofia, na kilemba, (na) ndani yake kuna nusu ya diyah; na katika mkono kuna nusu ya diyah. Ole wako! Hakika Sunnah imeitangulia qiyaas (kulinganisha jambo na jingine kwa rai) yenu; basi fuata, wala usizushe; kwani hakika wewe hutapotea muda wote utakaposhika athar (mapokezi ya waliotangulia). Abuw Bakr amesema: Ash-Sha'biy akaniambia: Yaa Hudhaliy, lau Ahnaf wenu angeuawa, na mtoto huyu (angeuawa) akiwa katika susu lake, je, diyah yao ingekuwa sawa? Nikasema: Ndiyo. Akasema: Basi qiyaas iko wapi?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
283
Hadiyth
204

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ، عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: قَالَ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "يُفْتَحُ الْقُرْآنُ عَلَى النَّاسِ حَتَّى يَقْرَأَهُ الْمَرْأَةُ وَالصَّبِيُّ وَالرَّجُلُ، فَيَقُولُ الرَّجُلُ: قَدْ قَرَأْتُ الْقُرْآنَ فَلَمْ أُتَّبَعُ، وَاللَّهِ لَأَقُومَنَّ بِهِ فِيهِمْ لَعَلِّي أُتَّبَعُ، فَيَقُومُ بِهِ فِيهِمْ فَلَا يُتَّبَعُ، فَيَقُولُ: قَدْ قَرَأْتُ الْقُرْآنَ فَلَمْ أُتَّبَعْ، وَقَدْ قُمْتُ بِهِ فِيهِمْ، فَلَمْ أُتَّبَعْ، لأَحْتَظِرْنَّ فِي بَيْتِي مَسْجِدًا لَعَلِّي أُتَّبَعْ، فَيَحْتَظِرُ فِي بَيْتِهِ مَسْجِدًا فَلَا يُتَّبَعُ، فَيَقُولُ: قَدْ قَرَأْتُ الْقُرْآنَ فَلَمْ أُتَّبَعْ، وَقُمْتُ بِهِ فِيهِمْ فَلَمْ أُتَّبَعْ، وَقَدْ احْتَظَرْتُ فِي بَيْتِي مَسْجِدًا، فَلَمْ أُتَّبَعْ، وَاللَّهِ لَآتِيَنَّهُمْ بِحَدِيثٍ لَا يَجِدُونَهُ فِي كِتَابِ اللَّهِ جَلَّ وَعَلَا وَلَمْ يَسْمَعُوهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَعَلِّي أُتَّبَعُ، قَالَ مُعَاذٌ: فَإِيَّاكُمْ وَمَا جَاءَ بِهِ فَإِنَّ مَا جَاءَ بِهِ ضَلَالَةٌ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sa'iyd, kutoka kwa Rabiy'ah bin Yaziyd, amesema: Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) amesema: "Qur-aan itafunguliwa kwa watu mpaka aisome mwanamke, na mtoto, na mwanamume. Basi mtu atasema: Nimeisoma Qur-aan, lakini sifuatwi; Wa-Allaahi, nitasimama nayo kati yao, huenda nikafuatwa. Atasimama nayo kati yao, lakini hafuatwi. Atasema: Nimeisoma Qur-aan, sikufuatwa; na nimesimama nayo kati yao, sikufuatwa; nitajizungushia Msikiti ndani ya nyumba yangu, huenda nikafuatwa. Atajizungushia Msikiti ndani ya nyumba yake, lakini hafuatwi. Atasema: Nimeisoma Qur-aan, sikufuatwa; na nimesimama nayo kati yao, sikufuatwa; na nimejizungushia Msikiti ndani ya nyumba yangu, sikufuatwa; Wa-Allaahi, nitawaletea maneno wasiyoyakuta katika Kitabu cha Allaah (جل وعلا), wala hawakuyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), huenda nikafuatwa." Mu'aadh (رضي الله عنه) akasema: "Basi tahadharini na aliyoyaleta, kwani hakika aliyoyaleta ni upotofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
283
Hadiyth
205

23-Mlangoباب في كراهية أخذ الرأيMlango Wa Kuhusu Kuchukiwa Kwa Kuchukua Rai

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ هُوَ ابْنُ مِغْوَلٍ قَالَ: قَالَ لِي الشَّعْبِيُّ: "مَا حَدَّثُوكَ هَؤُلَاءِ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَخُذْ بِهِ، وَمَا قَالُوهُ بِرَأْيِهِمْ، فَأَلْقِهِ فِي الْحُشِّ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Maalik — naye ni Ibn Mighwal —, amesema: Ash-Sha'biy aliniambia: "Walichokusimulia hawa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi kichukue; na walichokisema kwa rai zao, basi kitupe chooni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
284
Hadiyth
206

أَخْبَرَنَا الْعَبَّاسُ بْنُ سُفْيَانَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ حُبَابٍ، أَخْبَرَنِي رَجَاءُ بْنُ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَةَ بْنَ أَبِي لُبَابَةَ، يَقُولُ: "قَدْ رَضِيتُ مِنْ أَهْلِ زَمَانِي هَؤُلَاءِ أَنْ لَا يَسْأَلُونِي وَلَا أَسْأَلُهُمْ، إِنَّمَا يَقُولُ أَحَدُهُمْ أَرَأَيْتَ، أَرَأَيْتَ؟"

Ametukhabarisha Al-'Abbaas bin Sufyaan, kutoka kwa Zayd bin Hubaab, amenikhabarisha Rajaa bin Abiy Salamah, amesema: Nilimsikia 'Abdah bin Abiy Lubaabah akisema: "Kwa hakika nimeridhika na watu wa zama zangu hawa wasiniulize wala nisiwaulize; hakika mmoja wao husema tu: Unaonaje? Unaonaje?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
285
Hadiyth
207

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا عَاصِمُ ابْنُ بَهْدَلَةَ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: خَطَّ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا خَطًّا، ثُمَّ قَالَ: "هَذَا سَبِيلُ اللَّهِ"، ثُمَّ خَطَّ خُطُوطًا عَنْ يَمِينِهِ، وَعَنْ شِمَالِهِ، ثُمَّ قَالَ: "هَذِهِ سُبُلٌ عَلَى كُلِّ سَبِيلٍ مِنْهَا شَيْطَانٌ يَدْعُو إِلَيْهِ، ثُمَّ تَلَا: {وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ}"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia 'Aaswim bin Bahdalah, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituchorea siku moja mstari, kisha akasema: "Hii ni Njia ya Allaah." Kisha akachora mistari kuliani mwake na kushotoni mwake, kisha akasema: "Hizi ni njia (nyingine); juu ya kila njia miongoni mwazo yuko shaytwaan anayeilingania." Kisha akasoma:

وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ

Na kwamba hii ndiyo njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake [Al-An’aam (6:153)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
285
Hadiyth
208

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا وَرْقَاءُ، عَنْ ابْنِ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ: {وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ}، قَالَ: "الْبِدَعَ وَالشُّبُهَاتِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Warqaa, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, (kuhusu Kauli ya Allaah):

وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ

Na wala msifuate njia nyinginezo [Al-An’aam (6:153)]

Akasema: "(Ni) bid'ah (uzushi katika Dini) na mambo yenye utata."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
285
Hadiyth
209

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا عَمْرُو بْنُ يَحْيَى، قَالَ: سَمِعْتُ أَبِي يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كُنَّا نَجْلِسُ عَلَى بَابِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَبْلَ صَلَاةِ الْغَدَاةِ، فَإِذَا خَرَجَ، مَشَيْنَا مَعَهُ إِلَى الْمَسْجِدِ، فَجَاءَنَا أَبُو مُوسَى الْأَشْعَرِيُّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَقَالَ: أَخَرَجَ إِلَيْكُمْ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ؟ قُلْنَا: لَا، بَعْدُ. فَجَلَسَ مَعَنَا حَتَّى خَرَجَ، فَلَمَّا خَرَجَ، قُمْنَا إِلَيْهِ جَمِيعًا، فَقَالَ لَهُ أَبُو مُوسَى: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ، إِنِّي رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ آنِفًا أَمْرًا أَنْكَرْتُهُ وَلَمْ أَرَ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ إِلَّا خَيْرًا، قَالَ: فَمَا هُوَ؟، فَقَالَ: إِنْ عِشْتَ فَسَتَرَاهُ، قَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ قَوْمًا حِلَقًا جُلُوسًا يَنْتَظِرُونَ الصَّلَاةَ فِي كُلِّ حَلْقَةٍ رَجُلٌ، وَفِي أَيْدِيهِمْ حَصَا، فَيَقُولُ: كَبِّرُوا مِائَةً، فَيُكَبِّرُونَ مِائَةً، فَيَقُولُ: هَلِّلُوا مِائَةً، فَيُهَلِّلُونَ مِائَةً، وَيَقُولُ: سَبِّحُوا مِائَةً، فَيُسَبِّحُونَ مِائَةً، قَالَ: فَمَاذَا قُلْتَ لَهُمْ؟، قَالَ: مَا قُلْتُ لَهُمْ شَيْئًا انْتِظَارَ رَأْيِكَ أَوِ انْتِظَارَ أَمْرِكَ، قَالَ: أَفَلَا أَمَرْتَهُمْ أَنْ يَعُدُّوا سَيِّئَاتِهِمْ، وَضَمِنْتَ لَهُمْ أَنْ لَا يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِهِمْ؟ ثُمَّ مَضَى وَمَضَيْنَا مَعَهُ حَتَّى أَتَى حَلْقَةً مِنْ تِلْكَ الْحِلَقِ، فَوَقَفَ عَلَيْهِمْ، فَقَالَ: مَا هَذَا الَّذِي أَرَاكُمْ تَصْنَعُونَ؟، قَالُوا: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ حَصًا نَعُدُّ بِهِ التَّكْبِيرَ، وَالتَّهْلِيلَ، وَالتَّسْبِيحَ، قَالَ: "فَعُدُّوا سَيِّئَاتِكُمْ، فَأَنَا ضَامِنٌ أَنْ لَا يَضِيعَ مِنْ حَسَنَاتِكُمْ شَيْءٌ، وَيْحَكُمْ يَا أُمَّةَ مُحَمَّدٍ، مَا أَسْرَعَ هَلَكَتَكُمْ! هَؤُلَاءِ صَحَابَةُ نَبِيِّكُمْ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُتَوَافِرُونَ، وَهَذِهِ ثِيَابُهُ لَمْ تَبْلَ، وَآنِيَتُهُ لَمْ تُكْسَرْ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنَّكُمْ لَعَلَى مِلَّةٍ هِيَ أَهْدَى مِنْ مِلَّةِ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَوْ مُفْتَتِحُو بَابِ ضَلَالَةٍ"، قَالُوا: وَاللَّهِ يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ، مَا أَرَدْنَا إِلَّا الْخَيْرَ، قَالَ: "وَكَمْ مِنْ مُرِيدٍ لِلْخَيْرِ لَنْ يُصِيبَهُ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدَّثَنَا أَنَّ قَوْمًا يَقْرَءُونَ الْقُرْآنَ لَا يُجَاوِزُ تَرَاقِيَهُمْ، وَايْمُ اللَّهِ مَا أَدْرِي لَعَلَّ أَكْثَرَهُمْ مِنْكُمْ"، ثُمَّ تَوَلَّى عَنْهُمْ، فَقَالَ عَمْرُو بْنُ سَلَمَةَ: رَأَيْنَا عَامَّةَ أُولَئِكَ الْحِلَقِ يُطَاعِنُونَا يَوْمَ النَّهْرَوَانِ مَعَ الْخَوَارِجِ

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari 'Amr bin Yahyaa, amesema: Nilimsikia baba yangu akisimulia kutoka kwa baba yake, amesema: Tulikuwa tukikaa mlangoni kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) kabla ya Swalaah ya asubuhi (Alfajiri); anapotoka, tunatembea pamoja naye kwenda Msikitini. Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه) akatujia, akasema: Je, Abuw 'Abdir-Rahmaan (رضي الله عنه) ameshatoka kwenu? Tukasema: Hapana, bado. Akakaa pamoja nasi mpaka akatoka. Alipotoka, tukasimama sote kumwendea. Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) akamwambia: Yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan, hakika mimi nimeona Msikitini punde hivi jambo nililolikana, na sikuona — Al-Hamdu li-Allaah — ila kheri. Akasema: Basi ni nini? Akasema: Ukiishi, utaliona. Akasema: Nimeona Msikitini watu wamekaa katika duara wakingojea Swalaah; katika kila duara kuna mtu mmoja, na mikononi mwao kuna vijiwe. Basi (mtu huyo) husema: Mtukuzeni (Allaah) mara mia; nao humtukuza mara mia. Kisha husema: Mpwekesheni (Allaah) mara mia; nao humpwekesha mara mia. Na husema: Msabbihini (Allaah) mara mia; nao humsabbih mara mia. Akasema: Basi uliwaambia nini? Akasema: Sikuwaambia kitu chochote, nikingojea rai yako — au: nikingojea amri yako. Akasema: "Kwa nini usiwaamrishe wahesabu maovu yao, na ukawadhamini kwamba hakitapotea chochote katika mema yao?" Kisha akaenda, nasi tukaenda pamoja naye, mpaka akafika kwenye duara moja miongoni mwa duara hizo, akasimama juu yao, akasema: "Ni nini hiki ninachowaona mnakifanya?" Wakasema: Yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan, ni vijiwe tunavyohesabia Takbiyr (kusema: Allaah Ni Mkubwa zaidi), na Tahliyl (kusema: Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah), na Tasbiyh (kusema: Subhaana-Allaah). Akasema: "Basi hesabuni maovu yenu, nami ni mdhamini kwamba hakitapotea chochote katika mema yenu. Ole wenu, yaa Ummah wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)! Ni haraka ilioje maangamizi yenu! Hawa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy wenu (صلى الله عليه وآله وسلم) bado wako wengi, na hizi ni nguo zake hazijachakaa, na vyombo vyake havijavunjika. Naapa kwa Yule ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Hakika nyinyi mko juu ya mila iliyoongoka zaidi kuliko mila ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), au ni wenye kufungua mlango wa upotofu." Wakasema: Wa-Allaahi, yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan, hatukutaka ila kheri. Akasema: "Na ni wangapi wanaotaka kheri wasiipate! Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitusimulia kwamba watu fulani wanasoma Qur-aan, haivuki mitulinga yao (ya koo). Na naapa kwa Allaah, sijui; huenda wengi wao ni miongoni mwenu." Kisha akawaacha. 'Amr bin Salamah akasema: Tuliwaona wengi wa watu wa duara hizo wakitushambulia kwa mikuki siku ya An-Nahrawaan pamoja na Khawaarij (waliojitoa katika utiifu wa Waislamu na kuwakufurisha).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
286
Hadiyth
210

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "اتَّبِعُوا، وَلَا تَبْتَدِعُوا، فَقَدْ كُفِيتُمْ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Habiyb, kutoka kwa Abuw 'Abdir-Rahmaan, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Fuateni, wala msizushe; kwani kwa hakika mmeshatoshelezwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
287
Hadiyth
211

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سُلَيْمٍ، حَدَّثَنِي جَعْفَرُ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْأَنْصَارِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَحَمِدَ اللَّهَ، وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّ أَفْضَلَ الْهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَشَرَّ الْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Yahyaa bin Sulaym, amenisimulia Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah Al-Answaariy (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituhutubia; akamhimidi Allaah na akamsifu, kisha akasema: "Hakika uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na mambo mabaya kabisa ni yale yaliyozushwa, na kila bid'ah (uzushi katika Dini) ni upotofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
287
Hadiyth
212

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ أَسْلَمَ الْمِنْقَرِيِّ، عَنْ بِلَادِ بْنِ عِصْمَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: وَكَانَ إِذَا كَانَ عَشِيَّةَ الْخَمِيسِ لَيْلَةِ الْجُمُعَةِ، قَامَ فَقَالَ: "إِنَّ أَصْدَقَ الْقَوْلِ قَوْلُ اللَّهِ عز وجل وَإِنَّ أَحْسَنَ الْهَدْيِ هَدْيُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَالشَّقِيُّ مَنْ شَقِيَ فِي بَطْنِ أُمِّهِ، وَإِنَّ شَرَّ الرَّوَايَا رَوَايَا الْكَذِبِ، وَشَرَّ الْأُمُورِ مُحْدَثَاتُهَا، وَكُلَّ مَا هُوَ آتٍ قَرِيبٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Aslam Al-Minqariy, kutoka kwa Bilaad bin 'Iswmah, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) akisema — na alikuwa inapofika jioni ya Alkhamisi, usiku wa kuamkia Ijumaa, husimama akasema —: "Hakika kauli ya kweli kabisa ni Kauli ya Allaah (عز وجل), na hakika uongofu bora kabisa ni uongofu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Na mwovu ni yule aliyekuwa mwovu katika tumbo la mama yake. Na hakika masimulizi mabaya kabisa ni masimulizi ya uongo, na mambo mabaya kabisa ni yale yaliyozushwa; na kila kitakachokuja kiko karibu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
287
Hadiyth
213

أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "مَا أَخَذَ رَجُلٌ بِبِدْعَةٍ فَرَاجَعَ سُنَّةً"

Amenikhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Hakuna mtu aliyeshika bid'ah (uzushi katika Dini), kisha akarejea kwenye Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
287
Hadiyth
214

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي أَسْمَاءَ، عَنْ ثَوْبَانَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: "إِنَّمَا أَخَافُ عَلَى أُمَّتِي الْأَئِمَّةَ الْمُضِلِّينَ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abuw Asmaa, kutoka kwa Thawbaan (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Hakika ninachokiogopea Ummah wangu ni Imaam wapotoshaji tu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
287
Hadiyth
215

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ أَبُو الْوَلِيدِ الْهَرَوِيُّ، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ مُعَاذٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي زُرْعَةَ بْنِ عَمْرِو بْنِ جَرِيرٍ، عَنْ حَيَّةَ بِنْتِ أَبِي حَيَّةَ، قَالَتْ: دَخَلَ عَلَيْنَا رَجُلٌ بِالظَّهِيرَةِ، فَقُلْتُ: يَا عَبْدَ اللَّهِ، مِنْ أَيْنَ أَقْبَلْتَ؟، قَالَ: أَقْبَلْتُ أَنَا وَصَاحِبٌ لِي فِي بُغَاءٍ لَنَا، فَانْطَلَقَ صَاحِبِي يَبْغِي، وَدَخَلْتُ أَنَا أَسْتَظِلُّ بِالظِّلِّ، وَأَشْرَبُ مِنْ الشَّرَابِ، فَقُمْتُ إِلَى لُبَيْنَةٍ حَامِضَةٍ، ورُبَّمَا قَالَتْ: فَقُمْتُ إِلَى ضَيْحَةٍ حَامِضَةٍ، فَسَقَيْتُهُ مِنْهَا، فَشَرِبَ، وَشَرِبْتُ، قَالَتْ: وَتَوَسَّمْتُهُ فَقُلْتُ: يَا عَبْدَ اللَّهِ مَنْ أَنْتَ؟، فَقَالَ أَنَا أَبُو بَكْرٍ، قُلْتُ: أَنْتَ أَبُو بَكْرٍ صَاحِبُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّذِي سَمِعْتُ بِهِ؟، قَالَ: نَعَمْ، قَالَتْ: فَذَكَرْتُ غَزْوَنَا خَثْعَمًا، وَغَزْوَةَ بَعْضِنَا بَعْضًا فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَمَا جَاءَ اللَّهُ بِهِ مِنْ الْأُلْفَةِ وَأَطْنَابِ الْفَسَاطِيطِ وَشَبَّكَ ابْنُ عَوْنٍ أَصَابِعَهُ، وَوَصَفَهُ لَنَا مُعَاذٌ، وَشَبَّكَ أَحْمَدُ، فَقُلْتُ: يَا عَبْدَ اللَّهِ، حَتَّى مَتَى تَرَى أَمْرَ النَّاسِ هَذَا؟، قَالَ: "مَا اسْتَقَامَتْ الْأَئِمَّةُ"، قُلْتُ: مَا الْأَئِمَّةُ؟، قَالَ: "أَمَا رَأَيْتِ السَّيِّدَ يَكُونُ فِي الْحِوَاءِ فَيَتَّبِعُونَهُ، وَيُطِيعُونَهُ؟ فَمَا اسْتَقَامَ أُولَئِكَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah Abul-Waliyd Al-Harawiy, ametusimulia Mu'aadh bin Mu'aadh, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa 'Amr bin Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Zur'ah bin 'Amr bin Jariyr, kutoka kwa Hayyah bint Abiy Hayyah, amesema: Mtu mmoja aliingia kwetu wakati wa jua kali la mchana. Nikasema: Yaa 'Abda-Allaah, umetokea wapi? Akasema: Nimekuja mimi na sahibu yangu tukimtafuta (mnyama) wetu (aliyepotea); sahibu yangu akaenda kutafuta, nami nikaingia ili nijikinge kivulini, na ninywe kinywaji. Nikasimama (nikaendea) maziwa machache yaliyochachuka — na huenda alisema: Nikasimama (nikaendea) maziwa yaliyochanganywa na maji, yaliyochachuka —, nikamnywesha katika hayo, akanywa, nami nikanywa. Akasema: Nikamtazama kwa makini, nikasema: Yaa 'Abda-Allaah, wewe ni nani? Akasema: Mimi ni Abuw Bakr (رضي الله عنه). Nikasema: Wewe ni Abuw Bakr (رضي الله عنه), sahibu wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ambaye nimesikia khabari zake? Akasema: Ndiyo. Akasema: Nikataja vita vyetu dhidi ya (kabila la) Khath'am, na kushambuliana sisi kwa sisi katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam), na yale Aliyoyaleta Allaah ya kuzoeana na (kuungana kama) kamba za mahema — na Ibn 'Awn akafumanisha vidole vyake, na Mu'aadh akatuelezea hilo, na Ahmad akafumanisha (vidole vyake) —. Nikasema: Yaa 'Abda-Allaah, mpaka lini unaona jambo hili la watu (litadumu)? Akasema: "Muda wote ambao Imaam watanyooka." Nikasema: Imaam ni nini? Akasema: "Je, hukumwona bwana (wa watu) anayekuwa katika kambi ya mahema, nao wakamfuata na wakamtii? Basi (litadumu) muda wote ambao hao watanyooka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
292
Hadiyth
216

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَخٍ لِعَدِيِّ بْنِ أَرْطَاةَ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ أَخْوَفُ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ الْأَئِمَّةَ الْمُضِلِّينَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Ibraahiym bin Sa'd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ndugu mmoja wa 'Adiyy bin Artwaah, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni Imaam wapotoshaji."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
293
Hadiyth
217

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ بَيَانٍ بْنِ بِشْرٍ، عَنْ قَيْسِ بْنِ أَبِي حَازِمٍ، قَالَ: دَخَلَ أَبُو بَكْرٍ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ عَلَى امْرَأَةٍ مِنْ أَحْمَسَ يُقَالُ لَهَا زَيْنَبُ، قَالَ: فَرَآهَا لَا تَتَكَلَّمُ، فَقَالَ: "مَا لَهَا لَا تَتَكَلَّمُ؟"، قَالُوا: نَوَتْ حَجَّةً مُصْمِتَةً، فَقَالَ لَهَا: "تَكَلَّمِي، فَإِنَّ هَذَا لَا يَحِلُّ، هَذَا مِنْ عَمَلِ الْجَاهِلِيَّةِ"، قَالَ: فَتَكَلَّمَتْ، فَقَالَتْ: مَنْ أَنْتَ، قَالَ: أَنَا امْرُؤٌ مِنْ الْمُهَاجِرِينَ، قَالَتْ: مِنْ أَيِّ الْمُهَاجِرِينَ؟، قَالَ: مِنْ قُرَيْشٍ، قَالَتْ: فَمِنْ أَيِّ قُرَيْشٍ أَنْتَ؟، قَالَ: إِنَّكِ لَسَئُولٌ، أَنَا أَبُو بَكْرٍ، قَالَتْ: مَا بَقَاؤُنَا عَلَى هَذَا الْأَمْرِ الصَّالِحِ الَّذِي جَاءَ اللَّهُ بِهِ بَعْدَ الْجَاهِلِيَّةِ؟، فَقَالَ: بَقَاؤُكُمْ عَلَيْهِ مَا اسْتَقَامَتْ بِكُمْ أَئِمَّتُكُمْ، قَالَتْ: وَمَا الْأَئِمَّةُ؟، قَالَ: أَمَا كَانَ لِقَوْمِكِ رُؤَسَاءُ وَأَشْرَافٌ، يَأْمُرُونَهُمْ فَيُطِيعُونَهُمْ؟، قَالَتْ: بَلَى، قَالَ: فَهُمْ مِثْلُ أُولَئِكَ عَلَى النَّاسِ

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Bayaan bin Bishr, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, amesema: Abuw Bakr (رضوان الله عليه) aliingia kwa mwanamke mmoja wa (kabila la) Ahmas anayeitwa Zaynab. Akasema: Akamwona hasemi, akasema: "Ana nini, hasemi?" Wakasema: Ameweka niya ya Hajj ya kunyamaza. Akamwambia: "Sema, kwani hili si halaal; hili ni katika amali za Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam)." Akasema: Basi (yule mwanamke) akazungumza, akasema: Wewe ni nani? Akasema: Mimi ni mtu miongoni mwa Muhaajiruwn (waliohajiri kwenda Madiynah) (رضي الله عنهم). Akasema: Muhaajiruwn (رضي الله عنهم) wapi? Akasema: Wa Quraysh. Akasema: Basi wewe ni wa Quraysh wapi? Akasema: Hakika wewe ni mwingi wa kuuliza! Mimi ni Abuw Bakr (رضي الله عنه). Akasema: Tutabakia mpaka lini juu ya jambo hili jema Aliloleta Allaah baada ya Jaahiliyyah? Akasema: Mtabakia juu yake muda wote ambao Imaam wenu watawanyooshea (mambo). Akasema: Na Imaam ni nini? Akasema: Je, kaumu yako haikuwa na wakuu na watukufu wanaowaamrisha, nao wakawatii? Akasema: Bila shaka. Akasema: Basi hao (Imaam) ni mfano wa hao juu ya watu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
293
Hadiyth
218

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَهْدِيٍّ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ وَاصِلٍ، عَنْ امْرَأَةٍ يُقَالُ لَهَا عَائِذَةُ، قَالَتْ: رَأَيْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ يُوصِي الرِّجَالَ وَالنِّسَاءَ، وَيَقُولُ: "مَنْ أَدْرَكَ مِنْكُمْ مِنْ امْرَأَةٍ، أَوْ رَجُلٍ، فَالسَّمْتَ الْأَوَّلَ السَّمْتَ الْأَوَّلَ، فَإِنَّكُمْ عَلَى الْفِطْرَةِ"، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: السَّمْتُ الطَّرِيقُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Waaswil, kutoka kwa mwanamke mmoja anayeitwa 'Aaidhah, amesema: Nilimwona Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) akiwausia wanaume na wanawake, na akisema: "Yeyote kati yenu atakayefikia (zama hizo), mwanamke au mwanamume, basi (ashike) as-samt (mwenendo) wa kwanza, as-samt wa kwanza; kwani hakika nyinyi mko juu ya Fitwrah (maumbile ya asili)." 'Abdu-Allaah amesema: As-samt ni njia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
294
Hadiyth
219

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، أَنْبَأَنَا عَلِيٌّ هُوَ ابْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ زِيَادِ بْنِ حُدَيْرٍ، قَالَ: قَالَ لِي عُمَرُ: هَلْ تَعْرِفُ مَا يَهْدِمُ الْإِسْلَامَ؟، قَالَ: قُلْتُ: لَا، قَالَ: "يَهْدِمُهُ زَلَّةُ الْعَالِمِ، وَجِدَالُ الْمُنَافِقِ بِالْكِتَابِ، وَحُكْمُ الْأَئِمَّةِ الْمُضِلِّينَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, ametupa khabari 'Aliy — naye ni Ibn Mus-hir —, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Ziyaad bin Hudayr, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) aliniambia: "Je, unajua kinachoibomoa Islaam?" Akasema: Nikasema: Hapana. Akasema: "Inabomolewa na kuteleza kwa 'Aalim (Mwanazuoni), na mabishano ya mnafiki kwa (kutumia) Kitabu, na hukmu ya Imaam wapotoshaji."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
295
Hadiyth
220

أَخْبَرَنَا هَارُونُ، عَنْ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَلِيٍّ، قَالَ: "لَا تُجَالِسُوا أَصْحَابَ الْخُصُومَاتِ، فَإِنَّهُمْ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ"

Ametukhabarisha Haaruwn, kutoka kwa Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Muhammad bin 'Aliy, amesema: "Msikae pamoja na watu wa mabishano, kwani wao hushughulika kuzisakama Aayaat za Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
295
Hadiyth
221

أَخْبَرَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ شريك، عَنْ الْمُبَارَكِ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "سُنَّتُكُمْ وَاللَّهِ الَّذِي لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ بَيْنَهُمَا: بَيْنَ الْغَالِي وَالْجَافِي، فَاصْبِرُوا عَلَيْهَا رَحِمَكُمْ اللَّهُ، فَإِنَّ أَهْلَ السُّنَّةِ كَانُوا أَقَلَّ النَّاسِ فِيمَا مَضَى، وَهُمْ أَقَلُّ النَّاسِ فِيمَا بَقِيَ: الَّذِينَ لَمْ يَذْهَبُوا مَعَ أَهْلِ الْإِتْرَافِ فِي إِتْرَافِهِمْ، وَلَا مَعَ أَهْلِ الْبِدَعِ فِي بِدَعِهِمْ، وَصَبَرُوا عَلَى سُنَّتِهِمْ حَتَّى لَقُوا رَبَّهُمْ، فَكَذَاكُمْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ فَكُونُوا"

Ametukhabarisha Al-Husayn bin Manswuwr, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Al-Mubaarak, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Sunnah yenu — Wa-Allaahi, Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye — iko kati ya hao wawili: kati ya mwenye kuchupa mipaka na mwenye kuzembea. Basi isubirieni — Allaah Awarehemu —, kwani watu wa Sunnah walikuwa wachache zaidi ya watu katika (zama) zilizopita, na wao ni wachache zaidi ya watu katika (zama) zilizobaki: wale ambao hawakwenda pamoja na watu wa anasa katika anasa zao, wala pamoja na watu wa bid'ah (uzushi katika Dini) katika bid'ah zao, na wakasubiri juu ya Sunnah yao mpaka wakakutana na Rabb wao. Basi kuweni hivyo hivyo — Akipenda Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
295
Hadiyth
222

أَخْبَرَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا عِيسَى بْنُ يُونُسَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ عُمَارَةَ، وَمَالِكِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "الْقَصْدُ فِي السُّنَّةِ خَيْرٌ مِنْ الِاجْتِهَادِ فِي الْبِدْعَةِ"

Ametukhabarisha Muwsaa bin Khaalid, ametusimulia 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa 'Umaarah na Maalik bin Al-Haarith, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Kuwa wastani katika Sunnah ni bora kuliko kujitahidi katika bid'ah (uzushi katika Dini)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
295
Hadiyth
223

24-Mlangoباب الاقتداء بالعلماءMlango Wa Kufuata Mwenendo Wa 'Ulamaa (Wanazuoni)

أَخْبَرَنَا مَنْصُورُ بْنُ سَلَمَةَ الْخُزَاعِيُّ، عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَقَدْ أَدْرَكْتُ أَقْوَامًا لَوْ لَمْ يُجَاوِزْ أَحَدُهُمْ ظِفْرًا، لَمَا جَاوَزْتُهُ، كَفَى إِزْرَاءً عَلَى قَوْمٍ أَنْ تُخَالَفَ أَفْعَالُهُمْ"

Ametukhabarisha Manswuwr bin Salamah Al-Khuzaa'iy, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Abuw Hamzah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Hakika nimewadiriki watu ambao lau mmoja wao asingevuka (mpaka wa) ukucha, nami nisingeuvuka. Inatosha kuwa ni kuwadharau watu kwamba vitendo vyao vikhalifiwe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
297
Hadiyth
224

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءٍ: {أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الأَمْرِ مِنْكُمْ}، قَالَ: "أُولُو الْعِلْمِ وَالْفِقْهِ، وَطَاعَةُ الرَّسُولِ: اتِّبَاعُ الْكِتَابِ وَالسُّنَّةِ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa:

أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الأَمْرِ مِنْكُمْ

Mtiini Allaah na mtiini Rasuli na wenye madaraka katika nyinyi [An-Nisaa (4:59)]

Amesema: "(Wenye madaraka ni) wenye ilimu na Fiqh (ufahamu wa Dini); na kumtii Rasuli ni kufuata Kitabu na Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
297
Hadiyth
225

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ أَدْهَمَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ شُبْرُمَةَ عَنْ شَيْءٍ، وَكَانَتْ عِنْدِي مَسْأَلَةٌ شَدِيدَةٌ، فَقُلْتُ: رَحِمَكَ اللَّهُ، انْظُرْ فِيهَا، قَالَ: "إِذَا وَضَحَ لِيَ الطَّرِيقُ، وَوَجَدْتُ الْأَثَرَ، لَمْ أَحْبَسْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibraahiym bin Ad-ham, amesema: Nilimuuliza Ibn Shubrumah kuhusu jambo fulani, na nilikuwa na suala zito. Nikasema: Allaah Akurehemu, litazame (suala hili). Akasema: "Njia inaponibainikia, na nikapata mapokezi (ya waliotangulia), sisiti."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
297
Hadiyth
226

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ الْهَيْثَمِ، حَدَّثَنَا عَوْفٌ، عَنْ رَجُلٍ يُقَالُ لَهُ سُلَيْمَانُ بْنُ جَابِرٍ مِنْ أَهْلِ هَجَرَ، قَالَ: قَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ، قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ وَعَلِّمُوهُ النَّاسَ، تَعَلَّمُوا الْفَرَائِضَ وَعَلِّمُوهَا النَّاسَ، تَعَلَّمُوا الْقُرْآنَ وَعَلِّمُوهُ النَّاسَ، فَإِنِّي امْرُؤٌ مَقْبُوضٌ، وَالْعِلْمُ سَيُنْقَصُ وَتَظْهَرُ الْفِتَنُ حَتَّى يَخْتَلِفَ اثْنَانِ فِي فَرِيضَةٍ لَا يَجِدَانِ أَحَدًا يَفْصِلُ بَيْنَهُمَا"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Al-Haytham, ametusimulia 'Awf, kutoka kwa mtu mmoja anayeitwa Sulaymaan bin Jaabir, miongoni mwa watu wa Hajar, amesema: Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: "Jifunzeni ilimu na wafundisheni watu; jifunzeni Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi) na wafundisheni watu; jifunzeni Qur-aan na wafundisheni watu. Kwani mimi ni mtu atakayefishwa, na ilimu itapunguzwa, na fitna zitadhihiri, mpaka watu wawili watatofautiana katika fungu moja (la mirathi), wasimpate yeyote wa kuamua baina yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
297
Hadiyth
227

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ أَبِي خَلِيفَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ زِيَادَ بْنَ مِخْرَاقٍ ذَكَرَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: أَرْسَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُعَاذَ بْنَ جَبَلٍ، وَأَبَا مُوسَى إِلَى الْيَمَنِ، قَالَ: "تَسَانَدَا وَتَطَاوَعَا، وَيَسِّرَا وَلَا تُنَفِّرَا"، فَقَدِمَا الْيَمَنَ، فَخَطَبَ النَّاسَ مُعَاذٌ فَحَضَّهُمْ عَلَى الْإِسْلَامِ، وَأَمَرَهُمْ بِالتَّفَقُّهِ فِي الْقُرْآنِ، وَقَالَ: إِذَا فَعَلْتُمْ ذَلِكَ، فَاسْأَلُونِي أُخْبِرْكُمْ عَنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَمَكَثُوا مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَمْكُثُوا، فَقَالُوا لِمُعَاذٍ: قَدْ كُنْتَ أَمَرْتَنَا إِذَا نَحْنُ تَفَقَّهْنَا وَقَرَأْنَا أَنْ نَسْأَلَكَ فَتُخْبِرَنَا بِأَهْلِ الْجَنَّةِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَقَالَ لَهُمْ مُعَاذٌ: إِذَا ذُكِرَ الرَّجُلُ بِخَيْرٍ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَإِذَا ذُكِرَ بِشَرٍّ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia 'Umar bin Abiy Khaliyfah, amesema: Nilimsikia Ziyaad bin Mikhraaq akitaja kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwatuma Mu'aadh bin Jabal na Abuw Muwsaa (رضي الله عنهما) kwenda Yemen, akasema: "Saidianeni, na mtiiane, na sahilisheni wala msiwakimbize (watu)." Wakafika Yemen. Mu'aadh (رضي الله عنه) akawakhutubia watu, akawahimiza juu ya Islaam, na akawaamrisha kujifunza kwa kina (maana ya) Qur-aan. Na akasema: Mtakapofanya hivyo, basi niulizeni, nitawakhabarisha kuhusu watu wa Jannah (Pepo) miongoni mwa watu wa moto. Wakakaa muda Aliotaka Allaah wakae. Kisha wakamwambia Mu'aadh (رضي الله عنه): Ulikuwa umetuamrisha kwamba tutakapojifunza kwa kina na tukasoma, tukuulize, nawe utukhabarishe kuhusu watu wa Jannah miongoni mwa watu wa moto. Mu'aadh (رضي الله عنه) akawaambia: Mtu anapotajwa kwa kheri, basi yeye ni miongoni mwa watu wa Jannah; na anapotajwa kwa shari, basi yeye ni miongoni mwa watu wa moto.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
297
Hadiyth
228

حَدَّثَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْقَطَّانُ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ أَبِي سَعِيدٍ يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُّ النَّاسِ أَكْرَمُ؟، قَالَ: "أَتْقَاهُمْ"، قَالُوا: لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ، قَالَ: "فَيُوسُفُ بْنُ يَعْقُوبَ نَبِيُّ اللَّهِ ابْنُ نَبِيِّ اللَّهِ ابْنِ خَلِيلِ اللَّهِ"، قَالُوا: لَيْسَ عَنْ هَذَا نَسْأَلُكَ، قَالَ: "فَعَنْ مَعَادِنِ الْعَرَبِ تَسْأَلُونِي؟ خِيَارُهُمْ فِي الْجَاهِلِيَّةِ خِيَارُهُمْ فِي الْإِسْلَامِ إِذَا فَقُهُوا"

Ametusimulia Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd Al-Qatwtwaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd akisimulia kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Pakasemwa: Yaa Rasula-Allaah, ni nani mtukufu zaidi wa watu? Akasema: "Mchaji Allaah zaidi wao." Wakasema: Si kuhusu hili tunakuuliza. Akasema: "Basi ni Yuwsuf mwana wa Ya'quwb, Nabiy wa Allaah, mwana wa Nabiy wa Allaah, mwana wa Khaliyl (kipenzi) wa Allaah (عليهم السلام)." Wakasema: Si kuhusu hili tunakuuliza. Akasema: "Basi mnaniuliza kuhusu asili (koo) za Waarabu? Walio bora wao katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) ndio walio bora wao katika Islaam, watakapopata ufahamu (wa Dini)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
299
Hadiyth
229

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ هُوَ ابْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أُسَامَةَ بْنِ الْهَادِ، عَنْ عَبْدِ الْوَهَّابِ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ مُعَاوِيَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ يُرِدْ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah — naye ni Ibn Swaalih —, amenisimulia Al-Layth, kutoka kwa Yaziyd bin 'Abdi-Allaah bin Usaamah bin Al-Haad, kutoka kwa 'Abdul-Wahhaab, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Humayd bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Mu'aawiyah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayemtakia Allaah kheri, Humfahamisha Dini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
300
Hadiyth
230

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ جَعْفَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ يُرِدْ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Ja'far, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd bin Abiy Hind, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayemtakia Allaah kheri, Humfahamisha Dini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
300
Hadiyth
231

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ جَبَلَةَ بْنِ عَطِيَّةَ، عَنْ ابْنِ مُحَيْرِيزٍ، عَنْ مُعَاوِيَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ يُرِدْ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Jabalah bin 'Atwiyyah, kutoka kwa Ibn Muhayriyz, kutoka kwa Mu'aawiyah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayemtakia Allaah kheri, Humfahamisha Dini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
300
Hadiyth
232

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ الزَّهْرَانِيُّ، أَنْبَأَنَا إِسْمَاعِيلُ هُوَ ابْنُ جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ أَبِي عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْحُوَيْرِثِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، عَنْ أَبِيهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ شَهِدَ خُطْبَةَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي يَوْمِ عَرَفَةَ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ: "أَيُّهَا النَّاسُ، إِنِّي وَاللَّهِ لَا أَدْرِي لَعَلِّي لَا أَلْقَاكُمْ بَعْدَ يَوْمِي هَذَا بِمَكَانِي هَذَا، فَرَحِمَ اللَّهُ مَنْ سَمِعَ مَقَالَتِي الْيَوْمَ فَوَعَاهَا، فَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ وَلَا فِقْهَ لَهُ، وَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ إِلَى مَنْ هُوَ أَفْقَهُ مِنْهُ، وَاعْلَمُوا أَنَّ أَمْوَالَكُمْ وَدِمَاءَكُمْ حَرَامٌ عَلَيْكُمْ كَحُرْمَةِ هَذَا الْيَوْمِ، فِي هَذَا الشَّهْرِ، فِي هَذَا الْبَلَدِ، وَاعْلَمُوا أَنَّ الْقُلُوبَ لَا تُغِلُّ عَلَى ثَلَاثٍ: إِخْلَاصِ الْعَمَلِ لِلَّهِ، وَمُنَاصَحَةِ أُولِي الْأَمْرِ، وَعَلَى لُزُومِ جَمَاعَةِ الْمُسْلِمِينَ، فَإِنَّ دَعْوَتَهُمْ تُحِيطُ مِنْ وَرَائِهِمْ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Daawuwd Az-Zahraaniy, ametupa khabari Ismaa'iyl — naye ni Ibn Ja'far —, ametusimulia 'Amr bin Abiy 'Amr, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Huwayrith, kutoka kwa Muhammad bin Jubayr bin Mutw'im, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba alihudhuria hotuba ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) siku ya 'Arafah katika Hijjah ya kuaga: "Enyi watu! Hakika mimi — Wa-Allaahi — sijui; huenda nisikutane nanyi baada ya siku yangu hii mahali pangu hapa. Basi Allaah Amrehemu aliyesikia maneno yangu leo akayahifadhi. Kwani huenda mbebaji wa Fiqh (ufahamu wa Dini) hana Fiqh, na huenda mbebaji wa Fiqh akaifikisha kwa aliye na Fiqh zaidi kuliko yeye. Na jueni kwamba mali zenu na damu zenu ni haraam juu yenu kama utukufu wa siku hii, katika mwezi huu, katika mji huu. Na jueni kwamba nyoyo haziingiwi na chuki (wala khiyana) katika (mambo) matatu: kumtakasia Allaah amali, na kuwanasihi wenye madaraka, na kushikamana na jamaa ya Waislamu; kwani Du'aa yao inawazunguka (walio) nyuma yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
300
Hadiyth
233

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالْخَيْفِ مِنْ مِنًى، فَقَالَ: "نَضَّرَ اللَّهُ عَبْدًا سَمِعَ مَقَالَتِي فَوَعَاهَا، ثُمَّ أَدَّاهَا إِلَى مَنْ لَمْ يَسْمَعْهَا، فَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ لَا فِقْهَ لَهُ، وَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ إِلَى مَنْ هُوَ أَفْقَهُ مِنْهُ ثَلَاثٌ لَا يُغِلُّ عَلَيْهِنَّ قَلْبُ الْمُؤْمِنِ: إِخْلَاصُ الْعَمَلِ لِلَّهِ، وَطَاعَةُ ذَوِي الْأَمْرِ، وَلُزُومُ الْجَمَاعَةِ، فَإِنَّ دَعْوَتَهُمْ تَكُونُ مِنْ وَرَائِهِمْ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Muhammad bin Jubayr bin Mutw'im, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama huko Al-Khayf katika Minaa, akasema: "Allaah Amng'arishe (uso) mja aliyesikia maneno yangu akayahifadhi, kisha akayafikisha kwa ambaye hakuyasikia. Kwani huenda mbebaji wa Fiqh (ufahamu wa Dini) hana Fiqh, na huenda mbebaji wa Fiqh akaifikisha kwa aliye na Fiqh zaidi kuliko yeye. (Mambo) matatu ambayo moyo wa Muumini hauingiwi na chuki (wala khiyana) juu yake: kumtakasia Allaah amali, na kuwatii wenye madaraka, na kushikamana na jamaa; kwani Du'aa yao iko nyuma yao (ikiwazunguka)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
301
Hadiyth
234

أَخْبَرَنَا عِصْمَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا حَرَمِيُّ بْنُ عُمَارَةَ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عُمَرَ بْنِ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: خَرَجَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، مِنْ عِنْدِ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، بِنِصْفِ النَّهَارِ، قَالَ: فَقُلْتُ مَا خَرَجَ هَذِهِ السَّاعَةَ مِنْ عِنْدِ مَرْوَانَ إِلَّا وَقَدْ سَأَلَهُ عَنْ شَيْءٍ، فَأَتَيْتُهُ، فَسَأَلْتُهُ، قَالَ: نَعَمْ، سَأَلَنِي عَنْ حَدِيثٍ سَمِعْتُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:" نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا حَدِيثًا فَحَفِظَهُ، فَأَدَّاهُ إِلَى مَنْ هُوَ أَحْفَظُ مِنْهُ، فَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ لَيْسَ بِفَقِيهٍ، وَرُبَّ حَامِلِ فِقْهٍ إِلَى مَنْ هُوَ أَفْقَهُ مِنْهُ، لَا يَعْتَقِدُ قَلْبُ مُسْلِمٍ عَلَى ثَلَاثِ خِصَالٍ إِلَّا دَخَلَ الْجَنَّةَ "، قَالَ: قُلْتُ: مَا هُنَّ؟، قَالَ: إِخْلَاصُ الْعَمَلِ، وَالنَّصِيحَةُ لِوُلَاةِ الْأَمْرِ، وَلُزُومُ الْجَمَاعَةِ، فَإِنَّ دَعْوَتَهُمْ تُحِيطُ مِنْ وَرَاءِهِمْ، وَمَنْ كَانَتْ الْآخِرَةُ نِيَّتَهُ، جَعَلَ اللَّهُ غِنَاهُ فِي قَلْبِهِ، وَجَمَعَ لَهُ شَمْلَهُ، وَأَتَتْهُ الدُّنْيَا وَهِيَ رَاغِمَةٌ، وَمَنْ كَانَتْ الدُّنْيَا نِيَّتَهُ، فَرَّقَ اللَّهُ عَلَيْهِ شَمْلَهُ، وَجَعَلَ فَقْرَهُ بَيْنَ عَيْنَيْهِ، وَلَمْ يَأْتِهِ مِنْ الدُّنْيَا إِلَّا مَا قُدِّرَ لَهُ "، قَالَ: وَسَأَلْتُهُ عَنْ صَلَاةِ الْوُسْطَى، قَالَ: هِيَ الظُّهْرُ

Ametukhabarisha 'Iswmah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Haramiy bin 'Umaarah, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Umar bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abaan bin 'Uthmaan, kutoka kwa baba yake, amesema: Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) alitoka kwa Marwaan bin Al-Hakam katikati ya mchana. Akasema: Nikasema (moyoni): Hakutoka saa hii kwa Marwaan ila amemuuliza kuhusu jambo fulani. Nikamwendea, nikamuuliza. Akasema: Ndiyo; aliniuliza kuhusu Hadiyth niliyoisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Allaah Amng'arishe (uso) mtu aliyesikia kutoka kwetu Hadiyth akaihifadhi, kisha akaifikisha kwa aliye mhifadhi zaidi kuliko yeye. Kwani huenda mbebaji wa Fiqh (ufahamu wa Dini) si mwenye Fiqh, na huenda mbebaji wa Fiqh akaifikisha kwa aliye na Fiqh zaidi kuliko yeye. Moyo wa Muislamu haushikamani na sifa tatu ila ataingia Jannah (Pepo)." Akasema: Nikasema: Ni zipi hizo? Akasema: "Kuitakasa amali, na kuwanasihi wenye mamlaka, na kushikamana na jamaa; kwani Du'aa yao inawazunguka (walio) nyuma yao. Na ambaye Aakhirah ni niya yake, Allaah Atajaalia utajiri wake moyoni mwake, na Atamkusanyia mambo yake yaliyotawanyika, na dunia itamjia ilhali imenyenyekea. Na ambaye dunia ni niya yake, Allaah Atamtawanyia mambo yake, na Atajaalia ufakiri wake kati ya macho yake mawili, wala hatajiwa na (chochote cha) dunia ila kile alichokadiriwa." Akasema: Na nikamuuliza kuhusu Swalaah ya katikati, akasema: "Ni Adhuhuri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
302
Hadiyth
235

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ مُحَمَّدٍ الْقُرَشِيُّ، أَنْبَأَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ زُبَيْدٍ الْيَامِيِّ، عَنْ أَبِي الْعَجْلَانِ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "نَضَّرَ اللَّهُ امْرَءًا سَمِعَ مِنَّا حَدِيثًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَهُ، فَرُبَّ مُبَلَّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ، ثَلَاثٌ لَا يَغِلُّ عَلَيْهِنَّ قَلْبُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ: إِخْلَاصُ الْعَمَلِ لِلَّهِ، وَالنَّصِيحَةُ لِكُلِّ مُسْلِمٍ، وَلُزُومُ جَمَاعَةِ الْمُسْلِمِينَ، فَإِنَّ دُعَاءَهُمْ مُحِيطٌ مِنْ وَرَائِهِمْ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Muwsaa, ametusimulia 'Amr bin Muhammad Al-Qurashiy, ametupa khabari Israaiyl, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Zubayd Al-Yaamiy, kutoka kwa Abul-'Ajlaan, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitukhutubia, akasema: "Allaah Amng'arishe (uso) mtu aliyesikia kutoka kwetu Hadiyth akaifikisha kama alivyoisikia; kwani huenda aliyefikishiwa akawa mwenye kuhifadhi zaidi kuliko aliyesikia. (Mambo) matatu ambayo moyo wa mtu Muislamu hauingiwi na chuki (wala khiyana) juu yake: kumtakasia Allaah amali, na kumnasihi kila Muislamu, na kushikamana na jamaa ya Waislamu; kwani Du'aa yao inawazunguka (walio) nyuma yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
303
Hadiyth
236

25-Mlangoباب اتقاء الحديث عن النبي صلى الله عليه وسلم، والتثبت فيهMlango Wa Kujihadhari Katika Kusimulia Hadiyth Kutoka
Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Kuhakikisha Usahihi Wake

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَنْبَأَنَا أَبُو الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hushaym, ametupa khabari Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
303
Hadiyth
237

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ عَبْدِ الْأَعْلَى، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa 'Abdul-A'laa, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
238

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ الزُّبَيْرِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ حَدَّثَ عَنِّي كَذِبًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yaziyd bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Umar bin 'Abdi-Allaah bin 'Urwah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Urwah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Az-Zubayr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Az-Zubayr (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayesimulia kutoka kwangu uongo, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
239

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنِي الصَّبَّاحُ بْنُ مُحَارِبٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَعْلَى بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, amenisimulia Asw-Swabbaah bin Muhaarib, kutoka kwa 'Umar bin 'Abdi-Allaah bin Ya'laa bin Murrah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake [Ya'laa bin Murrah (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
240

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَتَّابٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: لَوْلَا أَنِّي أَخْشَى أَنْ أُخْطِئَ لَحَدَّثْتُكُمْ بِأَشْيَاءَ سَمِعْتُهَا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَوْ قَالَهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَذَاكَ أَنِّي سَمِعْتُهُ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Attaab, amesema: Nilimsikia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) akisema: Lau si kwamba ninaogopa kukosea, ningekusimulieni mambo niliyoyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) — au: aliyoyasema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —; na hilo ni kwa sababu nilimsikia [Nabiy] (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
241

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنْبَأَنَا أَبُو دَاوُدَ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ، وَعَنْ حَمَّادِ بْنِ أَبِي سُلَيْمَانَ، وَعَنْ التَّيْمِيِّ، وَعَنْ عَتَّابٍ مَوْلَى ابْنِ هُرْمُزَ، سَمِعُوا أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah, ametupa khabari Abuw Daawuwd, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz, na kutoka kwa Hammaad bin Abiy Sulaymaan, na kutoka kwa At-Taymiy, na kutoka kwa 'Attaab mwachwa huru wa Ibn Hurmuz: (wote) walimsikia Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
242

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ مَعْبَدِ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ عَلَى الْمِنْبَرِ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِيَّاكُمْ وَكَثْرَةَ الْحَدِيثِ عَنِّي، فَمَنْ قَالَ عَلَيَّ، فَلَا يَقُلْ إِلَّا حَقًّا أَوْ إِلَّا صِدْقًا، وَمَنْ قَالَ عَلَيَّ مَا لَمْ أَقُلْ، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Ma'bad bin Ka'b, kutoka kwa Abuw Qataadah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema juu ya mimbari: "Enyi watu! Tahadharini na wingi wa (kusimulia) Hadiyth kutoka kwangu. Basi atakayesema (jambo) kwa kuninasibishia, asiseme ila haki — au: ila kweli —; na atakayeninasibishia nisiyoyasema, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
243

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَاصِمٍ الْأَحْوَلِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ بِشْرٍ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Ibraahiym bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Aaswim Al-Ahwal, kutoka kwa Muhammad bin Bishr, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
304
Hadiyth
244

26-Mlangoباب في ذهاب العلمMlango Wa Kuhusu Kuondoka Kwa Ilimu

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامٌ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ لَا يَقْبِضُ الْعِلْمَ انْتِزَاعًا يَنْتَزِعُهُ مِنْ النَّاسِ، وَلَكِنْ: قَبْضُ الْعِلْمِ قَبْضُ الْعُلَمَاءِ، فَإِذَا لَمْ يُبْقِ عَالِمًا، اتَّخَذَ النَّاسُ رُءُوسًا جُهَّالًا، فَسُئِلُوا، فَأَفْتَوْا بِغَيْرِ عِلْمٍ، فَضَلُّوا وَأَضَلُّوا"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Haichukui ilimu kwa kuinyakua, Akiinyakua kutoka kwa watu; lakini kuchukuliwa kwa ilimu ni kuchukuliwa kwa 'Ulamaa (Wanazuoni). Basi Asipobakisha 'Aalim (Mwanazuoni), watu watawafanya wajinga kuwa viongozi; wataulizwa, nao watatoa Fatwa bila ilimu; basi watapotea na watapoteza (wengine)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
308
Hadiyth
245

أَخْبَرَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، أَنْبَأَنَا مُعْتَمِرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ الْحَجَّاجِ، عَنِ الْوَلِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي مَالِكٍ، عَنْ الْقَاسِمِ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ مَوْلَى عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: "خُذُوا الْعِلْمَ قَبْلَ أَنْ يَذْهَبَ"، قَالُوا: وَكَيْفَ يَذْهَبُ الْعِلْمُ يَا نَبِيَّ اللَّهِ، وَفِينَا كِتَابُ اللَّهِ؟، قَالَ: فَغَضِبَ، ثُمَّ قَالَ: "ثَكِلَتْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ، أَوَلَمْ تَكُنِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنْجِيلُ فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ، فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمْ شَيْئًا؟ إِنَّ ذَهَابَ الْعِلْمِ أَنْ يَذْهَبَ حَمَلَتُهُ، إِنَّ ذَهَابَ الْعِلْمِ أَنْ يَذْهَبَ حَمَلَتُهُ"

Ametukhabarisha Muwsaa bin Khaalid, ametupa khabari Mu'tamir bin Sulaymaan, kutoka kwa Al-Hajjaaj, kutoka kwa Al-Waliyd bin 'Abdir-Rahmaan bin Abiy Maalik, kutoka kwa Al-Qaasim Abuw 'Abdir-Rahmaan, mwachwa huru wa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa Abuw Umaamah (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba amesema: "Ichukueni ilimu kabla haijaondoka." Wakasema: Na vipi ilimu itaondoka, yaa Nabiyya-Allaah, na kwetu kuna Kitabu cha Allaah? Akasema (Abuw Umaamah): Akaghadhibika, kisha akasema: "Mama zenu wawafiwe! Je, kwani Tawraat na Injiyl hazikuwa kwa Wana wa Israaiyl, nazo hazikuwafaa kitu? Hakika kuondoka kwa ilimu ni kuondoka wabebaji wake; hakika kuondoka kwa ilimu ni kuondoka wabebaji wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
308
Hadiyth
246

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا هِلَالٌ هُوَ ابْنُ خَبَّابٍ، قَالَ: سَأَلْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ، قُلْتُ: يَا أَبَا عَبْدِ اللَّهِ، مَا عَلَامَةُ هَلَاكِ النَّاسِ؟، قَالَ: "إِذَا هَلَكَ عُلَمَاؤُهُمْ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Thaabit bin Yaziyd, ametusimulia Hilaal — naye ni Ibn Khabbaab —, amesema: Nilimuuliza Sa'iyd bin Jubayr; nilisema: Yaa Abaa 'Abdi-Allaah, ni ipi alama ya kuangamia kwa watu? Akasema: "Wanapoangamia 'Ulamaa (Wanazuoni) wao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
309
Hadiyth
247

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا مَسْعُودُ بْنُ سَعْدٍ الْجُعْفِيُّ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ رُبَيِّعَةَ، عَنْ سَلْمَانَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا بَقِيَ الْأَوَّلُ حَتَّى يَتَعَلَّمَ أَوْ يُعَلِّمَ الْآخِرَ، فَإِذَا هَلَكَ الْأَوَّلُ قَبْلَ أَنْ يُعَلِّمَ أَوْ يَتَعَلَّمَ الْآخِرُ، هَلَكَ النَّاسُ"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Mas'uwd bin Sa'd Al-Ju'fiy, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Rubayyi'ah, kutoka kwa Salmaan (رضي الله عنه), amesema: "Watu hawataacha kuwa katika kheri maadamu wa mwanzo angali yupo, mpaka wa mwisho ajifunze — au: amfundishe wa mwisho —. Basi wa mwanzo atakapoangamia kabla ya kumfundisha — au: kabla ya kujifunza — wa mwisho, watu wataangamia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
309
Hadiyth
248

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا أَبُو كُدَيْنَةَ، عَنْ قَابُوسَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "هَلْ تَدْرُونَ مَا ذَهَابُ الْعِلْمِ؟، قُلْنَا: لَا، قَالَ: ذَهَابُ الْعُلَمَاءِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Abuw Kudaynah, kutoka kwa Qaabuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Je, mnajua kuondoka kwa ilimu ni nini?" Tukasema: Hapana. Akasema: "Ni kuondoka kwa 'Ulamaa (Wanazuoni)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
309
Hadiyth
249

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَسْعَدَ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، قَالَ: قَالَ حُذَيْفَةُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَتَدْرِي كَيْفَ يُنْقَصُ الْعِلْمُ؟، قَالَ: قُلْتُ: كَمَا يُنْفَضُ الثَّوْبُ، وَكَمَا يَقْسُو الدِّرْهَمُ، قَالَ: "لَا، وَإِنَّ ذَلِكَ لَمِنْهُ، قَبْضُ الْعِلْمِ: قَبْضُ الْعُلَمَاءِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin As'ad, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Waail, amesema: Hudhayfah (رضي الله عنه) alisema: Je, unajua vipi ilimu itapunguzwa? Akasema (Abuw Waail): Nikasema: Kama nguo inavyochakaa (ikapoteza rangi yake), na kama dirhamu inavyokuwa ngumu (ikapoteza thamani yake). Akasema: "Hapana, ingawa hilo ni sehemu yake; kuchukuliwa kwa ilimu ni kuchukuliwa kwa 'Ulamaa (Wanazuoni)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
309
Hadiyth
250

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، عَنْ مَنْصُورِ بْنِ أَبِي الْأَسْوَدِ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "مَا لِي أَرَى عُلَمَاءَكُمْ يَذْهَبُونَ وَجُهَّالَكُمْ لَا يَتَعَلَّمُونَ؟ تَعَلَّمُوا قَبْلَ أَنْ يُرْفَعَ الْعِلْمُ، فَإِنَّ رَفْعَ الْعِلْمِ ذَهَابُ الْعُلَمَاءِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, kutoka kwa Manswuwr bin Abil-Aswad, kutoka kwa Huswayn, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: "Nina nini, ninawaona 'Ulamaa (Wanazuoni) wenu wanaondoka, na wajinga wenu hawajifunzi? Jifunzeni kabla ilimu haijainuliwa; kwani kuinuliwa kwa ilimu ni kuondoka kwa 'Ulamaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
311
Hadiyth
251

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ أَسَدٍ أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا عَبْثَرٌ، عَنْ بُرْد، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "النَّاسُ عَالِمٌ وَمُتَعَلِّمٌ، وَلَا خَيْرَ فِيمَا بَعْدَ ذَلِكَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Asad Abuw 'Aaswim, ametusimulia 'Abthar, kutoka kwa Burd, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: "Watu ni 'Aalim (Mwanazuoni) na mwenye kujifunza, na hakuna kheri katika wanaobaki baada ya hao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
312
Hadiyth
252

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ أَسَدٍ أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا عَبْثَرٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "مُعَلِّمُ الْخَيْرِ، وَالْمُتَعَلِّمُ فِي الْأَجْرِ سَوَاءٌ، وَلَيْسَ لِسَائِرِ النَّاسِ بَعْدُ خَيْرٌ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Asad Abuw 'Aaswim, ametusimulia 'Abthar, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: "Mwenye kufundisha kheri na mwenye kujifunza ni sawa katika ujira; na hakuna kheri kwa watu wengine waliobaki baada (ya hao)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
312
Hadiyth
253

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، أَنْبَأَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "اغْدُ عَالِمًا أَوْ مُتَعَلِّمًا أَوْ مُسْتَمِعًا، وَلَا تَكُنِ الرَّابِعَ فَتَهْلِكَ"

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametupa khabari Sufyaan, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Amka asubuhi ukiwa 'Aalim (Mwanazuoni), au mwenye kujifunza, au msikilizaji; wala usiwe wa nne, ukaangamia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
312
Hadiyth
254

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدٌ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ رُبَيِّعَةَ، قَالَ: قَالَ سَلْمَانُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "لَا يَزَالُ النَّاسُ بِخَيْرٍ مَا بَقِيَ الْأَوَّلُ حَتَّى يَتَعَلَّمَ الْآخِرُ، فَإِذَا هَلَكَ الْأَوَّلُ قَبْلَ أَنْ يَتَعَلَّمَ الْآخِرُ، هَلَكَ النَّاسُ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Rubayyi'ah, amesema: Salmaan (رضي الله عنه) amesema: "Watu hawataacha kuwa katika kheri maadamu wa mwanzo angali yupo, mpaka wa mwisho ajifunze. Basi wa mwanzo atakapoangamia kabla wa mwisho hajajifunza, watu wataangamia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
312
Hadiyth
255

أَخْبَرَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، وَعُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، قَالَا: أَنْبَأَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ الْأَحْنَفِ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "تَفَقَّهُوا قَبْلَ أَنْ تُسَوَّدُوا"

Ametukhabarisha Wahb bin Jariyr na 'Uthmaan bin 'Umar, wamesema: Ametupa khabari Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa Al-Ahnaf, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni Fiqh (ufahamu wa Dini) kabla hamjafanywa mabwana (viongozi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
314
Hadiyth
256

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا بَقِيَّةُ، حَدَّثَنِي صَفْوَانُ بْنُ رُسْتُمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَيْسَرَةَ، عَنْ تَمِيمٍ الدَّارِيِّ، رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: تَطَاوَلَ النَّاسُ فِي الْبِنَاءِ فِي زَمَنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَقَالَ عُمَرُ: "يَا مَعْشَرَ الْعُرَيْبِ، الْأَرْضَ الْأَرْضَ، إِنَّهُ لَا إِسْلَامَ إِلَّا بِجَمَاعَةٍ، وَلَا جَمَاعَةَ إِلَّا بِإِمَارَةٍ، وَلَا إِمَارَةَ إِلَّا بِطَاعَةٍ، فَمَنْ سَوَّدَهُ قَوْمُهُ عَلَى الْفِقْهِ، كَانَ حَيَاةً لَهُ وَلَهُمْ، وَمَنْ سَوَّدَهُ قَوْمُهُ عَلَى غَيْرِ فِقْهٍ، كَانَ هَلَاكًا لَهُ وَلَهُمْ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Baqiyyah, amenisimulia Swafwaan bin Rustum, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Maysarah, kutoka kwa Tamiym Ad-Daariy (رضي الله عنه), amesema: Watu walishindana katika kurefusha majengo katika zama za 'Umar (رضي الله عنه). 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Enyi jamii ya Waarabu! Ardhi! Ardhi! (Shikamaneni na ardhi.) Hakika hakuna Islaam ila kwa jamaa, wala hakuna jamaa ila kwa uongozi, wala hakuna uongozi ila kwa utiifu. Basi ambaye watu wake wamemfanya bwana (kiongozi) juu ya msingi wa Fiqh (ufahamu wa Dini), itakuwa ni uhai kwake na kwao; na ambaye watu wake wamemfanya bwana bila Fiqh, itakuwa ni maangamizi kwake na kwao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
315
Hadiyth
257

27-Mlangoباب العمل بالعلم وحسن النية فيهMlango Wa Kuitendea Kazi Ilimu Na Uzuri Wa Niya Ndani Yake

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا بَقِيَّةُ، حَدَّثَنَا صَدَقَةُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّ الْمُهَاصِرَ بْنَ حَبِيبٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: "إِنِّي لَسْتُ كُلَّ كَلَامِ الْحَكِيمِ أَتَقَبَّلُ، وَلَكِنِّي أَتَقَبَّلُ هَمَّهُ وَهَوَاهُ، فَإِنْ كَانَ هَمُّهُ وَهَوَاهُ فِي طَاعَتِي، جَعَلْتُ صَمْتَهُ حَمْدًا لِي وَوَقَارًا، وَإِنْ لَمْ يَتَكَلَّمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Baqiyyah, ametusimulia Swadaqah bin 'Abdi-Allaah, kwamba Al-Muhaasir bin Habiyb amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Allaah (تعالى) Amesema: Hakika Mimi Sikubali kila neno la mwenye hekima, lakini Nakubali hamu yake na matamanio yake. Basi ikiwa hamu yake na matamanio yake yako katika kunitii Mimi, Naufanya ukimya wake kuwa ni kunihimidi Mimi na ni utulivu, hata kama hakuzungumza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
258

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، عَنْ حَجَّاجِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ لَيْثِ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ صَالِحٍ، عَنْ أَبِي الزَّاهِرِيَّةِ، يَرْفَعُ الْحَدِيثَ، أَنَّ اللَّهَ قَالَ: "أَبُثُّ الْعِلْمَ فِي آخِرِ الزَّمَانِ حَتَّى يَعْلَمَهُ الرَّجُلُ وَالْمَرْأَةُ، وَالْعَبْدُ وَالْحُرُّ، وَالصَّغِيرُ وَالْكَبِيرُ، فَإِذَا فَعَلْتُ ذَلِكَ بِهِمْ، أَخَذْتُهُمْ بِحَقِّي عَلَيْهِمْ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, kutoka kwa Hajjaaj bin Muhammad, kutoka kwa Layth bin Sa'd, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Swaalih, kutoka kwa Abuz-Zaahiriyyah — akiipandisha Hadiyth [kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)] —, kwamba Allaah Amesema: "Nitaieneza ilimu katika zama za mwisho, mpaka aijue mwanamume na mwanamke, na mtumwa na muungwana, na mdogo na mkubwa. Nitakapowafanyia hilo, Nitawashika (Nitawahesabu) kwa Haki Yangu juu yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
259

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا مَخْلَدُ بْنُ حُسَيْنٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "مَنْ طَلَبَ شَيْئًا مِنْ هَذَا الْعِلْمِ، فَأَرَادَ بِهِ مَا عِنْدَ اللَّهِ، يُدْرِكْ إِنْ شَاءَ اللَّهُ، وَمَنْ أَرَادَ بِهِ الدُّنْيَا، فَذَاكَ وَاللَّهِ حَظُّهُ مِنْهُ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Makhlad bin Husayn, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Atakayetafuta kitu katika ilimu hii, akakusudia kwacho yaliyo kwa Allaah, atayapata, Akipenda Allaah. Na atakayekusudia kwacho dunia, basi hiyo — Wa-Allaahi — ndiyo fungu lake katika (ilimu) hiyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
260

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ عِيسَى، قَالَ: قَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ: "لَا تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ لِثَلَاثٍ: لِتُمَارُوا بِهِ السُّفَهَاءَ، وَتُجَادِلُوا بِهِ الْعُلَمَاءَ، وَلِتَصْرِفُوا بِهِ وُجُوهَ النَّاسِ إِلَيْكُمْ، وَابْتَغُوا بِقَوْلِكُمْ مَا عِنْدَ اللَّهِ، فَإِنَّهُ يَدُومُ وَيَبْقَى، وَيَنْفَدُ مَا سِوَاهُ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Muhammad bin 'Awn, kutoka kwa Ibraahiym bin 'Iysaa, amesema: Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Msijifunze ilimu kwa (sababu) tatu: ili mbishane kwayo na wapumbavu, na mjadiliane kwayo na 'Ulamaa (Wanazuoni), na ili mgeuze kwayo nyuso za watu kuelekea kwenu. Na tafuteni kwa kauli zenu yaliyo kwa Allaah, kwani hayo yanadumu na yanabaki, na yanamalizika yasiyokuwa hayo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
261

وَبِهَذَا الْإِسْنَادِ، قَالَ: "كُونُوا يَنَابِيعَ الْعِلْمِ، مَصَابِيحَ الْهُدَى، أَحْلَاسَ الْبُيُوتِ، سُرُجَ اللَّيْلِ، جُدُدَ الْقُلُوبِ، خُلْقَانَ الثِّيَابِ، تُعْرَفُونَ فِي أَهْلِ السَّمَاءِ، وَتَخْفَوْنَ عَلَى أَهْلِ الْأَرْضِ"

Na kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) hii hii, amesema [Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه)]: "Kuweni chemchemi za ilimu, taa za uongofu, matandiko ya nyumba (msiotoka majumbani mwenu), mienge ya usiku, wenye nyoyo mpya, wenye nguo kuukuu; mtajulikana kwa watu wa mbinguni, na mtafichikana kwa watu wa ardhini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
262

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُمَارَةَ بْنِ حَزْمٍ، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَطْلُبُ هَذَا الْعِلْمَ أَحَدٌ لَا يُرِيدُ بِهِ إِلَّا الدُّنْيَا، إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ عَرْفَ الْجَنَّةِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, ametusimulia Muhammad bin 'Umaarah bin Hazm, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hatafuti ilimu hii yeyote asiyekusudia kwayo ila dunia, isipokuwa Allaah Atamharamishia harufu ya Jannah (Pepo) Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
263

أَخْبَرَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ نُمَيْرٍ، عَنْ مَالِكِ بْنِ مِغْوَلٍ، قَالَ: قَالَ رَجُلٌ لِلشَّعْبِيِّ: أَفْتِنِي أَيُّهَا الْعَالِمُ، فَقَالَ: "الْعَالِمُ مَنْ يَخَافُ اللَّهَ عز وجل"

Ametukhabarisha Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Numayr, kutoka kwa Maalik bin Mighwal, amesema: Mtu mmoja alimwambia Ash-Sha'biy: Nipe Fatwa, yaa 'Aalim (Mwanazuoni). Akasema: "'Aalim ni yule anayemkhofu Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
316
Hadiyth
264

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ مَزْيَدٍ، عَنْ أَوْفَى بْنِ دَلْهَمٍ أَنَّهُ بَلَغَهُ، عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ، تُعْرَفُوا بِهِ، وَاعْمَلُوا بِهِ، تَكُونُوا مِنْ أَهْلِهِ، فَإِنَّهُ سَيَأْتِي بَعْدَ هَذَا زَمَانٌ لَا يَعْرِفُ فِيهِ تِسْعَةُ عُشَرَائِهِمْ الْمَعْرُوفَ، وَلَا يَنْجُو مِنْهُ إِلَّا كُلُّ نُوَمَةٍ، فَأُولَئِكَ أَئِمَّةُ الْهُدَى وَمَصَابِيحُ الْعِلْمِ، لَيْسُوا بِالْمَسَايِيحِ، وَلَا الْمَذَايِيعِ الْبُذُرِ"، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: نُوَمَةٌ: غَافِلٌ عَنْ الشَّرِّ، الْمَذَايِيعُ: كَثِيرُ الْكَلَامِ، وَالْبُذْرِ: النَّمَّامُونَ

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia 'Umar bin Mazyad, kutoka kwa Awfaa bin Dalham, kwamba ilimfikia kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Jifunzeni ilimu, mtajulikana kwayo; na itendeeni kazi, mtakuwa miongoni mwa watu wake. Kwani hakika zitakuja baada ya hili zama ambazo sehemu tisa kati ya kumi zao hawatayajua mema ndani yake, wala hataokoka humo ila kila mwenye kughafilika (na shari). Basi hao ndio Imaam wa uongofu na taa za ilimu; wao si wenye kueneza (maovu), wala si wenye kutangaza (siri), wenye kupayuka."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Nuwamah: mwenye kughafilika na shari; al-madhaayiy': mwingi wa maneno; na al-budhur: wafitinishaji (wenye kupeleka maneno).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
318
Hadiyth
265

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ بَعْدَ أَنْ تَعْلَمُوا، فَلَنْ يَأْجُرَكُمْ اللَّهُ تَعَاليَ بِالْعِلْمِ حَتَّى تَعْمَلُوا"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sa'iyd bin 'Abdil-'Aziyz, kutoka kwa Yaziyd bin Jaabir, amesema: Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) amesema: "Tendeni mtakalo baada ya kujua; kwani Allaah (تعالى) Hatakulipeni ujira kwa ilimu mpaka mtende."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
266

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَالِدِ بْنِ حَازِمٍ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مَزْيَدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ بْنِ جَابِرٍ يُحَدِّثُ، عَنْ سَعْدٍ، أَنَّهُ أَتَى ابْنَ مُنَبِّهٍ فَسَأَلَهُ عَنْ الْحَسَنِ، وَقَالَ لَهُ: كَيْفَ عَقْلُهُ؟ فَأَخْبَرَهُ، ثُمَّ قَالَ: إِنَّا لَنَتَحَدَّثُ، أَوْ نَجِدُ فِي الْكُتُبِ أَنَّهُ: "مَا آتَى اللَّهُ سًبْحَانَه عَبْدًا عِلْمًا فَعَمِلَ بِهِ عَلَى سَبِيلِ الْهُدَى، فَيَسْلُبَهُ عَقْلَهُ حَتَّى يَقْبِضَهُ اللَّهُ إِلَيْهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Khaalid bin Haazim, ametusimulia Al-Waliyd bin Mazyad, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir akisimulia, kutoka kwa Sa'd, kwamba alimjia Ibn Munabbih, akamuuliza kuhusu Al-Hasan, na akamwambia: Akili yake ikoje? Akamkhabarisha. Kisha akasema: Hakika sisi tunazungumza — au: tunakuta katika vitabu — kwamba: "Allaah (سبحانه) Hampi mja ilimu, naye akaitendea kazi juu ya njia ya uongofu, kisha (Allaah) Amnyang'anye akili yake, mpaka Allaah Amchukue (Amfishe) Kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
267

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ ابْنِ الْقَاسِمِ بْنِ قَيْسٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي يُونُسُ بْنُ سَيْفٍ الْحِمْصِيُّ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو كَبْشَةَ السَّلُولِيُّ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: "إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللَّهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ، عَالِمٌ لَا يَنْتَفِعُ بِعِلْمِهِ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Ibn Al-Qaasim bin Qays, amesema: Amenisimulia Yuwnus bin Sayf Al-Himswiy, amesema: Amenisimulia Abuw Kabshah As-Saluwliy, amesema: Nilimsikia Abud-Dardaa (رضي الله عنه) akisema: "Hakika miongoni mwa watu waovu kabisa mbele ya Allaah kwa daraja Siku ya Qiyaamah ni 'Aalim (Mwanazuoni) asiyenufaika na ilimu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
268

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو قُدَامَةَ، عَنْ مَالِكِ بْنِ دِينَارٍ، قَالَ: قَالَ أَبُو الدَّرْدَاءِ: "مَنْ يَزْدَدْ عِلْمًا، يَزْدَدْ وَجَعًا"،

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Abuw Qudaamah, kutoka kwa Maalik bin Diynaar, amesema: Abud-Dardaa (رضي الله عنه) amesema: "Atakayezidi ilimu, atazidi maumivu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
269

أخْبَرَنَا وَقَالَ أَبُو الدَّرْدَاءِ: "مَا أَخَافُ عَلَى نَفْسِي أَنْ يُقَالَ لِي: مَا عَلِمْتَ، وَلَكِنْ أَخَافُ أَنْ يُقَالَ لِي: مَاذَا عَمِلْتَ"

Ametukhabarisha, na Abud-Dardaa (رضي الله عنه) amesema: "Siogopi juu ya nafsi yangu kuambiwa: Ulijua nini? Lakini naogopa kuambiwa: Ulitenda nini?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
270

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ جُرَيْجٍ يَذْكُرُ عَمَّنْ حَدَّثَهُ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "تَدَارُسُ الْعِلْمِ سَاعَةً مِنْ اللَّيْلِ، خَيْرٌ مِنْ إِحْيَائِهَا"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Hafsw bin Ghiyaath, amesema: Nilimsikia Ibn Jurayj akitaja kutoka kwa aliyemsimulia, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Kudurusiana ilimu saa moja ya usiku ni bora kuliko kuuhuisha (usiku huo kwa ibaada)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
271

أَخْبَرَنَا وقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "إِنِّي لَأُجَزِّئُ اللَّيْلَ ثَلَاثَةَ أَجْزَاءٍ: فَثُلُثٌ أَنَامُ، وَثُلُثٌ أَقُومُ، وَثُلُثٌ أَتَذَكَّرُ أَحَادِيثَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha, na Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: "Hakika mimi naugawa usiku sehemu tatu: theluthi moja nalala, na theluthi nasimama (kuswali), na theluthi nazikumbuka Hadiyth za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
272

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَرَفَةَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "مَنْ ابْتَغَى شَيْئًا مِنْ الْعِلْمِ يَبْتَغِي بِهِ وَجْهَ اللَّهِ سُبْحَانَهُ، آتَاهُ اللَّهُ مِنْهُ مَا يَكْفِيهِ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin 'Arafah, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Al-Hasan bin 'Amr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Atakayetafuta kitu katika ilimu, akikusudia kwacho Wajihi wa Allaah (سبحانه), Allaah Atampa katika (ilimu) hiyo kinachomtosheleza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
319
Hadiyth
273

28-Mlangoباب من هاب الفتيا مخافة السقطMlango Wa Aliyeiogopa Fatwa Kwa Kuhofia Kukosea

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ، قَالَ: سَأَلْتُ الشَّعْبِيَّ عَنْ حَدِيثٍ، فَحَدَّثَنِيهِ، فَقُلْتُ: إِنَّهُ يُرْفَعُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "لَا، عَلَى مَنْ دُونَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحَبُّ إِلَيْنَا، فَإِنْ كَانَ فِيهِ زِيَادَةٌ أَوْ نُقْصَانٌ، كَانَ عَلَى مَنْ دُونَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Thaabit bin Yaziyd, ametusimulia 'Aaswim, amesema: Nilimuuliza Ash-Sha'biy kuhusu Hadiyth moja, akanisimulia. Nikasema: Hakika hiyo inapandishwa mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: "Hapana; (kuisimamisha) kwa aliye chini ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kunapendeza zaidi kwetu; kwani ikiwa ndani yake kuna ziada au upungufu, (hilo) litakuwa juu ya aliye chini ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
323
Hadiyth
274

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَبِي هَاشِمٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْمُحَاقَلَةِ وَالْمُزَابَنَةِ"، فَقِيلَ لَهُ: أَمَا تَحْفَظُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدِيثًا غَيْرَ هَذَا؟، قَالَ: بَلَى، وَلَكِنْ أَقُولُ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: قَالَ عَلْقَمَةُ، أَحَبُّ إِلَيَّ

Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Abuw Haashim, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza muhaaqalah (kuuza mimea ya nafaka iliyo shambani kwa nafaka kwa kipimo) na muzaabanah (kuuza tende zilizo mtini kwa tende kavu kwa kipimo)." Akaambiwa: Je, huhifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Hadiyth nyingine isiyokuwa hii? Akasema: Bila shaka; lakini kusema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema, 'Alqamah amesema, kunapendeza zaidi kwangu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
323
Hadiyth
275

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ، قَالَ: كَانَ أَبُو الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، إِذَا حَدَّثَ بِحَدِيثٍ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "هَذَا أَوْ نَحْوَهُ، أَوْ شِبْهَهُ، أَوْ شَكْلَهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Ismaa'iyl bin 'Ubaydi-Allaah, amesema: Abud-Dardaa (رضي الله عنه) alikuwa anaposimulia Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), husema: "(Ni) hivi, au karibu na hivi, au kinachofanana nacho, au cha namna yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
324
Hadiyth
276

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ، عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: كَانَ أَبُو الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، إِذَا حَدَّثَ حَدِيثًا، قَالَ: "اللَّهُمَّ إِلَّا هَكَذَا، أَوْ كَشَكْلِهِ"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Mu'aawiyah, kutoka kwa Rabiy'ah bin Yaziyd, amesema: Abud-Dardaa (رضي الله عنه) alikuwa anaposimulia Hadiyth, husema: "Yaa Allaah, (si vinginevyo) isipokuwa hivi, au kama namna yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
324
Hadiyth
277

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُسْلِمٍ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مَيْمُونٍ، قَالَ: "كُنْتُ لَا تَفُوتُنِي عَشِيَّةُ خَمِيسٍ إِلَّا وَآتِي فِيهَا عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَمَا سَمِعْتُهُ يَقُولُ لِشَيْءٍ، قَطُّ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ، حَتَّى كَانَتْ ذَاتَ عَشِيَّةٍ، فَقَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَاغْرَوْرَقَتْ عَيْنَاهُ وَانْتَفَخَتْ أَوْدَاجُه، فَأَنَا رَأَيْتُهُ مَحْلُولَةً أَزْرَارُهُ، وَقَالَ: أَوْ مِثْلُهُ، أَوْ نَحْوُهُ، أَوْ شَبِيهٌ بِهِ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Ibn 'Awn, kutoka kwa Muslim Abuw 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibraahiym At-Taymiy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Amr bin Maymuwn, amesema: "Ilikuwa hainipiti jioni ya Alkhamisi ila ninamjia ndani yake 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه). Sikupata kumsikia kamwe akisema kwa kitu chochote: Rasuli wa Allaah amesema; mpaka ilipokuwa jioni moja, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema. Akasema: Macho yake yakajaa machozi, na mishipa ya shingo yake ikavimba. Basi mimi nilimwona vifungo vyake (vya kanzu) vikiwa vimefunguliwa; na akasema: Au mfano wake, au karibu na hivyo, au kinachofanana nacho."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
324
Hadiyth
278

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، وَابْنِ سِيرِينَ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، كَانَ إِذَا حَدَّثَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْأَيَّامِ، تَرَبَّدَ وَجْهُهُ، وَقَالَ: "هَكَذَا أَوْ نَحْوَهُ، هَكَذَا أَوْ نَحْوَهُ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy na Ibn Siyriyn, kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa anaposimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika siku (fulani), uso wake hubadilika rangi, na husema: "Hivi au karibu na hivi, hivi au karibu na hivi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
325
Hadiyth
279

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا تَوْبَةُ الْعَنْبَرِيُّ، قَالَ: قَالَ لِي الشَّعْبِيُّ: "أَرَأَيْتَ فُلَانًا الَّذِي يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ؟ قَعَدْتُ مَعَ ابْنِ عُمَرَ سَنَتَيْنِ، أَوْ سَنَةً وَنِصْفًا، فَمَا سَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا، إِلَّا هَذَا الْحَدِيثَ"

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Tawbah Al-'Anbariy, amesema: Ash-Sha'biy aliniambia: "Je, unamwona fulani ambaye husema: Rasuli wa Allaah amesema, Rasuli wa Allaah amesema? Nilikaa pamoja na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) miaka miwili, au mwaka mmoja na nusu, sikumsikia akisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kitu chochote, isipokuwa Hadiyth hii."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
326
Hadiyth
280

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي السَّفَرِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "جَالَسْتُ ابْنَ عُمَرَ سَنَةً، فَلَمْ أَسْمَعْهُ يَذْكُرُ حَدِيثًا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Abis-Safar, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Nilikaa pamoja na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) mwaka mmoja, sikumsikia akitaja Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
326
Hadiyth
281

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ أَبِي حَصِينٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ ثَابِتِ بْنِ قُطْبَةَ الْأَنْصَارِيِّ، قَالَ: كَانَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، "يُحَدِّثُنَا فِي الشَّهْرِ بِالْحَدِيثَيْنِ، أَوْ الثَّلَاثَةِ"

Ametukhabarisha 'Aaswim bin Yuwsuf, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Abuw Haswiyn, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Thaabit bin Qutwbah Al-Answaariy, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) "alikuwa akitusimulia katika mwezi (mmoja) Hadiyth mbili, au tatu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
326
Hadiyth
282

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا يُونُسُ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُبَيْدٍ، قَالَ: مَرَّ بِنَا أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ، فَقُلْنَا حَدِّثْنَا بِبَعْضِ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، فَقَالَ: "وَأَتَحَلَّلُ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Yuwnus, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Ubayd, amesema: Anas bin Maalik (رضي الله عنه) alipita kwetu, tukasema: Tusimulie baadhi ya yale uliyoyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: "Na (hapo) nijitoe (katika dhima ya kukosea)?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
326
Hadiyth
283

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَ: ثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: كَانَ أَنَسٌ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَلِيلَ الْحَدِيثِ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ إِذَا حَدَّثَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَوْ كَمَا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, amesema: Ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad, amesema: Anas (رضي الله عنه) alikuwa mchache wa (kusimulia) Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); na alikuwa anaposimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), husema: "Au kama alivyosema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
326
Hadiyth
284

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: كَانَ أَنَسٌ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِذَا حَدَّثَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدِيثًا، قَالَ: "أَوْ كَمَا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Ismaa'iyl, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Muhammad, amesema: Anas (رضي الله عنه) alikuwa anaposimulia Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), husema: "Au kama alivyosema Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
327
Hadiyth
285

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي السَّائِبُ بْنُ يَزِيدَ، قَالَ: خَرَجْتُ مَعَ سَعْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، إِلَى مَكَّةَ، "فَمَا سَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ حَدِيثًا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، حَتَّى رَجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, amesema: Amenisimulia As-Saaib bin Yaziyd (رضي الله عنه), amesema: Nilitoka pamoja na Sa'd [bin Abiy Waqqaasw] (رضي الله عنه) kwenda Makkah, "sikumsikia akisimulia Hadiyth yoyote kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka tukarudi Madiynah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
328
Hadiyth
286

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا بَيَانٌ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ قَرَظَةَ بْنِ كَعْبٍ: أَنَّ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، شَيَّعَ الْأَنْصَارَ حِينَ خَرَجُوا مِنْ الْمَدِينَةِ، فَقَالَ: "أَتَدْرُونَ لِمَ شَيَّعْتُكُمْ؟ قُلْنَا: لِحَقِّ الْأَنْصَارِ، قَالَ: إِنَّكُمْ تَأْتُونَ قَوْمًا تَهْتَزُّ أَلْسِنَتُهُمْ بِالْقُرْآنِ اهْتِزَازَ النَّخْلِ، فَلَا تَصُدُّوهُمْ بِالْحَدِيثِ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَنَا شَرِيكُكُمْ"، قَالَ: فَمَا حَدَّثْتُ بِشَيْءٍ، وَقَدْ سَمِعْتُ كَمَا سَمِعَ أَصْحَابِي

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Bayaan, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Qaradhwah bin Ka'b (رضي الله عنه): kwamba 'Umar (رضي الله عنه) aliwasindikiza Answaar (رضي الله عنهم) walipotoka Madiynah, akasema: "Je, mnajua kwa nini nimekusindikizeni? Tukasema: Kwa ajili ya haki ya Answaar (رضي الله عنهم). Akasema: Hakika nyinyi mnakwenda kwa watu ambao ndimi zao zinatikisika kwa Qur-aan kama kutikisika kwa mitende; basi msiwazuie kwa (kuwasimulia) Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nami ni mshirika wenu." Akasema (Qaradhwah): Basi sikusimulia kitu chochote, ilhali nimesikia kama walivyosikia wenzangu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
328
Hadiyth
287

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَشْعَثُ بْنُ سَوَّارٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ قُرَظَةَ بْنِ كَعْبٍ، قَالَ: بَعَثَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، رَهْطًا مِنْ الْأَنْصَارِ إِلَى الْكُوفَةِ، فَبَعَثَنِي مَعَهُمْ، فَجَعَلَ يَمْشِي مَعَنَا حَتَّى أَتَى صِرَارَ وَصِرَارٌ: مَاءٌ فِي طَرِيقِ الْمَدِينَةِ فَجَعَلَ يَنْفُضُ التُّرَابَ عَنْ رِجْلَيْهِ، ثُمّ قَالَ: "إِنَّكُمْ تَأْتُونَ الْكُوفَةَ، فَتَأْتُونَ قَوْمًا لَهُمْ أَزِيزٌ بِالْقُرْآنِ فَيَأْتُونَكُمْ، فَيَقُولُونَ: قَدِمَ أَصْحَابُ مُحَمَّدٍ! قَدِمَ أَصْحَابُ مُحَمَّدٍ! فَيَأْتُونَكُمْ فَيَسْأَلُونَكُمْ عَنْ الْحَدِيثِ، فَاعْلَمُوا أَنَّ أَسْبَغَ الْوُضُوءِ ثَلَاثٌ، وَثِنْتَانِ تُجْزِيَانِ، ثُمَّ قَالَ: إِنَّكُمْ تَأْتُونَ الْكُوفَةَ، فَتَأْتُونَ قَوْمًا لَهُمْ أَزِيزٌ بِالْقُرْآنِ، فَيَقُولُونَ: قَدِمَ أَصْحَابُ مُحَمَّدٍ! قَدِمَ أَصْحَابُ مُحَمَّدٍ! فَيَأْتُونَكُمْ فَيَسْأَلُونَكُمْ عَنْ الْحَدِيثِ، فَأَقِلُّوا الرِّوَايَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَنَا شَرِيكُكُمْ فِيهِ"، قَالَ قَرَظَةُ: وَإِنْ كُنْتُ لَأَجْلِسُ فِي الْقَوْمِ، فَيَذْكُرُونَ الْحَدِيثَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَإِنِّي لَمِنْ أَحْفَظِهِمْ لَهُ، فَإِذَا ذَكَرْتُ وَصِيَّةَ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، سَكَتُّ، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: مَعْنَاهُ عِنْدِي: الْحَدِيثُ عَنْ أَيَّامِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، لَيْسَ السُّنَنَ وَالْفَرَائِضَ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ash'ath bin Sawwaar, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Qaradhwah bin Ka'b (رضي الله عنه), amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) alituma kikundi cha Answaar (رضي الله عنهم) kwenda Al-Kuwfah, akanituma pamoja nao. Akawa anatembea pamoja nasi mpaka akafika Swiraar — na Swiraar ni (mahali pa) maji katika njia ya Madiynah —; akawa anakung'uta mchanga kutoka miguuni mwake, kisha akasema: "Hakika nyinyi mnakwenda Al-Kuwfah, mtawafikia watu wenye mvumo (wa kisomo) wa Qur-aan; watakujieni waseme: Wamekuja Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)! Wamekuja Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)! Watakujieni wakuulizeni kuhusu Hadiyth. Basi jueni kwamba Wudhuu uliokamilika zaidi ni (mara) tatu, na mbili zinatosheleza." Kisha akasema: "Hakika nyinyi mnakwenda Al-Kuwfah, mtawafikia watu wenye mvumo (wa kisomo) wa Qur-aan; waseme: Wamekuja Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)! Wamekuja Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)! Watakujieni wakuulizeni kuhusu Hadiyth. Basi punguzeni kusimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nami ni mshirika wenu katika hilo." Qaradhwah (رضي الله عنه) amesema: Na hakika nilikuwa nikikaa katika watu, wakitaja Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nami nikiwa miongoni mwa wanaoihifadhi zaidi; ninapokumbuka wasia wa 'Umar (رضي الله عنه), ninanyamaza.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Maana yake kwangu ni: Hadiyth kuhusu siku (za vita na matukio) za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), si Sunnah na faradhi.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
329
Hadiyth
288

أَخْبَرَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ نُمَيْرٍ، عَنْ مَالِكِ بْنِ مِغْوَلٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلْقَمَةَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ثُمَّ ارْتَعَدَ، ثُمَّ قَالَ: نَحْوَ ذَلِكَ أَوْ فَوْقَ ذَاكَ"

Ametukhabarisha Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia Ibn Numayr, kutoka kwa Maalik bin Mighwal, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Alqamah, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema — kisha akatetemeka, kisha akasema: Karibu na hivyo, au zaidi ya hivyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
330
Hadiyth
289

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: صَحِبْتُ ابْنَ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ إِلَى الْمَدِينَةِ، فَلَمْ أَسْمَعْهُ يُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِحَدِيثٍ، إِلَّا أَنَّهُ قَالَ: كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأُتِيَ بِجُمَّارٍ، فَقَالَ: "إِنَّ مِنْ الشَّجَرِ شَجَرًا مِثْلَ الرَّجُلِ الْمُسْلِمِ"، فَأَرَدْتُ أَنْ أَقُولَ: هِيَ النَّخْلَةُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا أَنَا أَصْغَرُ الْقَوْمِ، فَسَكَتُّ، قَالَ عُمَرُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: وَدِدْتُ أَنَّكَ قُلْتَ، وَعَلَيَّ كَذَا

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa Mujaahid, amesema: Nilifuatana na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) mpaka Madiynah, sikumsikia akisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Hadiyth yoyote, isipokuwa kwamba alisema: Nilikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akaletewa kiini cha mtende; akasema: "Hakika miongoni mwa miti kuna mti mfano wa mtu Muislamu." Nikataka kusema: Ni mtende. Nikatazama, kumbe mimi ni mdogo kuliko wote katika watu; nikanyamaza. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: Ningependa kwamba ungelisema, na juu yangu (ningelitoa) kadhaa (kwa furaha ya hilo).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
330
Hadiyth
290

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ يَزِيدَ الْهَدَادِيُّ، حَدَّثَنَا صَالِحٌ الدَّهَّانُ، قَالَ: مَا سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ زَيْدٍ يَقُولُ قَطُّ: "قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِعْظَامًا وَاتِّقَاءً أَنْ يَكْذِبَ عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia Khaalid bin Yaziyd Al-Hadaadiy, ametusimulia Swaalih Ad-Dahhaan, amesema: Sijapata kumsikia Jaabir bin Zayd akisema kamwe: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema", kwa kumtukuza na kuogopa kumsemea uongo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
331
Hadiyth
291

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، أَنْبَأَنَا رَوْحٌ، عَنْ كَهْمَسِ بْنِ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ شَقِيقٍ، قَالَ: جَاءَ أَبُو هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِلَى كَعْبٍ يَسْأَلُ عَنْهُ، وَكَعْبٌ فِي الْقَوْمِ، فَقَالَ كَعْبٌ: مَا تُرِيدُ مِنْهُ؟ فَقَالَ: أَمَا إِنِّي لَا أَعْرِفُ لِأَحَدٍ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَكُونَ أَحْفَظَ لِحَدِيثِهِ مِنِّي، فَقَالَ كَعْبٌ: "أَمَا إِنَّكَ لَنْ تَجِدَ طَالِبَ شَيْءٍ إِلَّا سَيَشْبَعُ مِنْهُ يَوْمًا مِنْ الدَّهْرِ، إِلَّا طَالِبَ عِلْمٍ أَوْ طَالِبَ دُنْيَا"، فَقَالَ: أَنْتَ كَعْبٌ؟، قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: لِمِثْلِ هَذَا جِئْتُ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah, ametupa khabari Rawh, kutoka kwa Kahmas bin Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Shaqiyq, amesema: Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) alikuja kwa Ka'b akiuliza kuhusu yeye, na Ka'b alikuwa katika watu. Ka'b akasema: Unataka nini kwake? Akasema: Ama mimi, sijui yeyote miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anayehifadhi zaidi Hadiyth zake kuliko mimi. Ka'b akasema: "Ama wewe, hutampata mtafutaji wa kitu chochote ila atashiba nacho siku moja katika zama, isipokuwa mtafutaji wa ilimu au mtafutaji wa dunia." Akasema: Wewe ni Ka'b? Akasema: Ndiyo. Akasema: Kwa ajili ya mfano wa hili nimekuja.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
331
Hadiyth
292

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا شِبْلٌ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُّ النَّاسِ أَعْلَمُ؟، قَالَ: "مَنْ جَمَعَ عِلْمَ النَّاسِ إِلَى عِلْمِهِ، وَكُلُّ طَالِبِ عِلْمٍ غَرْثَانُ إِلَى عِلْمٍ"

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Bukayr, ametusimulia Shibl, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Twaawuws, amesema: Iliulizwa: Yaa Rasula-Allaah, ni nani mjuzi zaidi katika watu? Akasema: "Ni yule anayekusanya ilimu ya watu pamoja na ilimu yake. Na kila mtafutaji wa ilimu ana njaa ya ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
332
Hadiyth
293

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ الْخَلِيلِ بْنِ مُرَّةَ، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ قُرَّةَ، قَالَ: "كُنْتُ فِي حَلْقَةٍ فِيهَا الْمَشْيَخَةُ وَهُمْ يَتَرَاجَعُونَ، فِيهِمْ عَابِدُ بْنُ عَمْرٍو، فَقَالَ شَابٌّ فِي نَاحِيَةِ الْقَوْمِ: أَفِيضُوا فِي ذِكْرِ اللَّهِ، بَارَكَ اللَّهُ فِيكُمْ، فَنَظَرَ الْقَوْمُ بَعْضُهُمْ إِلَى بَعْضٍ، فِي أَيِّ شَيْءٍ رَآنَا؟ ثُمَّ قَالَ بَعْضُهُمْ: مَنْ أَمَرَكَ بِهَذَا؟ فَمُرَّ، لَئِنْ عُدْتَ، لَنَفْعَلَنَّ وَلَنَفْعَلَنَّ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Al-Khaliyl bin Murrah, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Qurrah, amesema: "Nilikuwa katika duara (la watu wa ilimu) ambalo ndani yake walikuwemo wazee, nao wakirudiana (maneno ya ilimu); miongoni mwao alikuwa 'Aabid bin 'Amr (رضي الله عنه). Kijana mmoja aliyekuwa pembeni mwa watu akasema: Zameni katika kumdhukuru Allaah, Allaah Akubarikini. Watu wakatazamana wao kwa wao: Ametuona (tuko) katika kitu gani? Kisha baadhi yao wakasema: Nani amekuamrisha hili? Basi ondoka; ukirudia, hakika tutakufanya (hivi) na tutakufanya (vile)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
332
Hadiyth
294

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، أَنْبَأَنَا أَبُو عَامِرٍ، أَنْبَأَنَا قُرَّةُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّه: "نِعْمَ الْمَجْلِسُ مَجْلِسٌ تُنْشَرُ فِيهِ الْحِكْمَةُ، وَتُرْجَى فِيهِ الرَّحْمَةُ"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametupa khabari Abuw 'Aamir, ametupa khabari Qurrah bin Khaalid, kutoka kwa 'Awn bin 'Abdi-Allaah, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Kikao kizuri ni kikao ambacho ndani yake inaenezwa hekima, na inatarajiwa ndani yake Rehma."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
332
Hadiyth
295

29-Mlangoباب من قال: العلم: الخشية وتقوى اللهMlango Wa Waliosema: Ilimu Ni Khofu Na Taqwa Ya Allaah

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي مُعَاوِيَةُ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ، عَنْ أَبِيهِ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَشَخَصَ بِبَصَرِهِ إِلَى السَّمَاءِ، ثُمَّ قَالَ: "هَذَا أَوَانُ يُخْتَلَسُ الْعِلْمُ مِنْ النَّاسِ، حَتَّى لَا يَقْدِرُوا مِنْهُ عَلَى شَيْءٍ، فَقَالَ زِيَادُ بْنُ لَبِيدٍ الْأَنْصَارِيُّ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَكَيْفَ يُخْتَلَسُ مِنَّا وَقَدْ قَرَأْنَا الْقُرْآنَ؟ فَوَاللَّهِ لَنَقْرَأَنَّهُ، وَلَنُقْرِئَنَّهُ نِسَاءَنَا وَأَبْنَاءَنَا، فَقَالَ: ثَكِلَتْكَ أُمُّكَ يَا زِيَادُ، إِنْ كُنْتُ لَأَعُدُّكَ مِنْ فُقَهَاءِ أَهْلِ الْمَدِينَةِ، هَذِهِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنْجِيلُ عِنْدَ الْيَهُودِ، وَالنَّصَارَى، فَمَاذَا يُغْنِي عَنْهُمْ؟"، قَالَ جُبَيْرٌ: فَلَقِيتُ عُبَادَةَ بْنَ الصَّامِتِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قُلْتُ أَلَا تَسْمَعُ مَا يَقُولُ أَخُوكَ أَبُو الدَّرْدَاءِ؟ فَأَخْبَرْتُهُ بِالَّذِي قَالَ، قَالَ: صَدَقَ أَبُو الدَّرْدَاءِ، إِنْ شِئْتَ لَأُحَدِّثَنَّكَ بِأَوَّلِ عِلْمٍ يُرْفَعُ مِنْ النَّاسِ: الْخُشُوعُ يُوشِكُ أَنْ تَدْخُلَ مَسْجِدَ الْجَمَاعَةِ، فَلَا تَرَى فِيهِ رَجُلًا خَاشِعًا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Mu'aawiyah, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa baba yake Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akakodoa macho yake kuelekea mbinguni, kisha akasema: "Huu ni wakati ambao ilimu inanyakuliwa kutoka kwa watu, mpaka wasiweze kupata chochote katika hiyo." Ziyaad bin Labiyd Al-Answaariy (رضي الله عنه) akasema: Yaa Rasula-Allaah, itanyakuliwa vipi kutoka kwetu na hali tumeisoma Qur-aan? Wa-Allaahi, hakika tutaisoma, na hakika tutawasomesha wake zetu na watoto wetu. Akasema: "Mama yako akufiwe, yaa Ziyaad! Hakika nilikuwa nikikuhesabu miongoni mwa Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wa watu wa Madiynah. Hii hapa Tawraat na Injiyl ziko kwa Mayahudi na Manaswara; basi zinawafaa nini?" Jubayr amesema: Nikakutana na 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه); amesema: Nikasema: Je, husikii anayoyasema ndugu yako Abud-Dardaa (رضي الله عنه)? Nikamkhabarisha yale aliyoyasema. Akasema: Amesema kweli Abud-Dardaa (رضي الله عنه). Ukitaka, hakika nitakusimulia ilimu ya kwanza itakayoondolewa kutoka kwa watu: unyenyekevu. Inakaribia uingie Msikiti wa jamaa, usimwone ndani yake mtu yeyote mwenye unyenyekevu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
333
Hadiyth
296

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ جَمِيلٍ الْكِنَانِيُّ، حَدَّثَنَا مَكْحُولٌ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:" فَضْلُ الْعَالِمِ عَلَى الْعَابِدِ كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُمْ "، ثُمَّ تَلَا هَذِهِ الْآيَةَ {إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ}، ثُمَّ قَالَ إِنَّ اللَّهَ وَمَلَائِكَتَهُ وَأَهْلَ سَمَاوَاتِهِ وَأَرَضِيهِ، وَالنُّونَ فِي الْبَحْرِ يُصَلُّونَ عَلَى الَّذِينَ يُعَلِّمُونَ النَّاسَ الْخَيْرَ "

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Waliyd bin Jamiyl Al-Kinaaniy, ametusimulia Makhuwl, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Fadhila ya 'Aalim (Mwanazuoni) juu ya mfanya ibaada ni kama fadhila yangu juu ya wa chini kabisa kati yenu." Kisha akasoma Aayah hii:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

Hakika wanaomkhofu Allaah katika Waja Wake ni ‘Ulamaa [Faatwir (35:28)]

Kisha akasema: "Hakika Allaah na Malaika Wake (عليهم السلام), na watu wa mbingu Zake na ardhi Zake, na samaki ndani ya bahari, wanawaswalia wale wanaowafundisha watu kheri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
334
Hadiyth
297

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ أَسَدٍ أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ يَمَانٍ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ رَجُلٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "لَا يَكُونُ الرَّجُلُ عَالِمًا حَتَّى لَا يَحْسُدَ مَنْ فَوْقَهُ، وَلَا يَحْقِرَ مَنْ دُونَهُ، وَلَا يَبْتَغِيَ بِعِلْمِهِ ثَمَنًا"

Ametukhabarisha Ahmad bin Asad Abuw 'Aaswim, ametusimulia Yahyaa bin Yamaan, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Mtu hawi 'Aalim (Mwanazuoni) mpaka asimhusudu aliye juu yake, wala asimdharau aliye chini yake, wala asitafute thamani kwa ilimu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
334
Hadiyth
298

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ أَبِي أُسَامَةَ، عَنْ مِسْعَرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الْأَعْلَى التَّيْمِيَّ، يَقُولُ: "مَنْ أُوتِيَ مِنْ الْعِلْمِ مَا لَا يُبْكِيهِ، لَخَلِيقٌ أَنْ لَا يَكُونَ أُوتِيَ عِلْمًا يَنْفَعُهُ، لِأَنَّ اللَّهَ تَعَالَى نَعَتَ الْعُلَمَاءَ، ثُمَّ قَرَأ: {إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ إِلَى قَوْلِهِ يَبْكُونَ}"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Abuw Usaamah, kutoka kwa Mis'ar, amesema: Nilimsikia 'Abdul-A'laa At-Taymiy akisema: "Aliyepewa katika ilimu kisichomliza, inastahiki kwamba hakupewa ilimu yenye kumnufaisha; kwa sababu Allaah (تعالى) Amewasifu 'Ulamaa (Wanazuoni)," kisha akasoma:

إِنَّ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ

Hakika wale waliopewa ilimu [Al-Israa (17:107)]

mpaka Kauli Yake:

يَبْكُونَ

huku wanalia [Al-Israa (17:109)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
335
Hadiyth
299

أَخْبَرَنَا عِصْمَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ حُبَابٍ، عَنْ مُبَارَكِ بْنِ فَضَالَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ الْعُمَرِيِّ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، قَالَ: "لَا تَكُونُ عَالِمًا حَتَّى يَكُونَ فِيكَ ثَلَاثُ خِصَالٍ: لَا تَبْغِي عَلَى مَنْ فَوْقَكَ، وَلَا تَحْقِرُ مَنْ دُونَكَ، وَلَا تَأْخُذُ عَلَى عِلْمِكَ دُنْيَا"

Ametukhabarisha 'Iswmah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Zayd bin Hubaab, kutoka kwa Mubaarak bin Fadhwaalah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar Al-'Umariy, kutoka kwa Abuw Haazim, amesema: "Huwi 'Aalim (Mwanazuoni) mpaka ndani yako ziwe na sifa tatu: usimfanyie jeuri aliye juu yako, wala usimdharau aliye chini yako, wala usichukue dunia kwa ilimu yako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
336
Hadiyth
300

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا عَبْثَرٌ، عَنْ بُرْدِ بْنِ سِنَانٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى الدِّمَشْقِيِّ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا تَكُونُ عَالِمًا حَتَّى تَكُونَ مُتَعَلِّمًا، وَلَا تَكُونُ بِالْعِلْمِ عَالِمًا حَتَّى تَكُونَ بِهِ عَامِلًا، وَكَفَى بِكَ إِثْمًا أَنْ لَا تَزَالَ مُخَاصِمًا، وَكَفَى بِكَ إِثْمًا أَنْ لَا تَزَالَ مُمَارِيًا، وَكَفَى بِكَ كَاذِبًا أَنْ لَا تَزَالَ مُحَدِّثًا فِي غَيْرِ ذَاتِ اللَّهِ عز وجل"

Ametukhabarisha Ahmad bin Asad, ametusimulia 'Abthar, kutoka kwa Burd bin Sinaan, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa Ad-Dimashqiy, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: "Huwi 'Aalim (Mwanazuoni) mpaka uwe mwanafunzi, wala huwi 'Aalim wa ilimu mpaka uwe mwenye kuitendea kazi. Na yatosha kuwa ni dhambi kwako kwamba usiache kuwa mwenye kugombana; na yatosha kuwa ni dhambi kwako kwamba usiache kuwa mwenye kubishana; na yatosha kuwa ni mwongo kwako kwamba usiache kuwa mwenye kusimulia katika yasiyokuwa kwa ajili ya Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
336
Hadiyth
301

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَرَفَةَ، حَدَّثَنَا الْمُبَارَكُ بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ أَخِيهِ سُفْيَانَ الثَّوْرِيِّ، عَنْ عِمْرَانَ الْمِنْقَرِيِّ، قَالَ: قُلْتُ لِلْحَسَنِ يَوْمًا فِي شَيْءٍ، قَالَهُ: يَا أَبَا سَعِيدٍ، لَيْسَ هَكَذَا يَقُولُ الْفُقَهَاءُ، فَقَالَ: "وَيْحَكَ! وَرَأَيْتَ أَنْتَ فَقِيهًا قَطُّ، إِنَّمَا الْفَقِيهُ الزَّاهِدُ فِي الدُّنْيَا، الرَّاغِبُ فِي الْآخِرَةِ، الْبَصِيرُ بِأَمْرِ دِينِهِ، الْمُدَاوِمُ عَلَى عِبَادَةِ رَبِّهِ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin 'Arafah, ametusimulia Al-Mubaarak bin Sa'iyd, kutoka kwa ndugu yake Sufyaan Ath-Thawriy, kutoka kwa 'Imraan Al-Minqariy, amesema: Nilimwambia Al-Hasan siku moja kuhusu jambo alilolisema: Yaa Abaa Sa'iyd, sivyo hivi wanavyosema Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh). Akasema: "Ole wako! Je, umewahi wewe kumwona Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh) hata mara moja? Hakika Faqiyh ni yule asiyeipupia dunia, mwenye kuitamani Aakhirah, mwenye kuona sawasawa katika jambo la Dini yake, mwenye kudumu katika ibaada ya Rabb wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
337
Hadiyth
302

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَرَفَةَ، حَدَّثَنَا النَّضْرُ بْنُ إِسْمَاعِيل الْبَجَلِيُّ، عَنْ مِسْعَرٍ، عَنْ سَعْدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قِيلَ لَهُ: مَنْ أَفْقَهُ أَهْلِ الْمَدِينَةِ؟، قَالَ: "أَتْقَاهُمْ لِرَبِّهِ عز وجل"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin 'Arafah, ametusimulia An-Nadhwr bin Ismaa'iyl Al-Bajaliy, kutoka kwa Mis'ar, kutoka kwa Sa'd bin Ibraahiym, amesema: Aliulizwa: Ni nani mjuzi zaidi wa Fiqh kati ya watu wa Madiynah? Akasema: "Ni yule mwenye taqwa zaidi kwa Rabb wake (عز وجل) kati yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
337
Hadiyth
303

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَرَفَةَ، حَدَّثَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ عَلِيٍّ، عَنْ لَيْثِ بْنِ أَبِي سُلَيْمٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: "إِنَّمَا الْفَقِيهُ مَنْ يَخَافُ اللَّهَ تَعَالَى"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin 'Arafah, ametusimulia Al-Husayn bin 'Aliy, kutoka kwa Layth bin Abiy Sulaym, kutoka kwa Mujaahid, amesema: "Hakika Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh) ni yule anayemkhofu Allaah (تعالى)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
304

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ يَعْقُوبَ الْقُمِّيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي لَيْثُ بْنُ أَبِي سُلَيْمٍ، عَنْ يَحْيَى هُوَ ابْنُ عَبَّادٍ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِنَّ الْفَقِيهَ حَقَّ الْفَقِيهِ، مَنْ لَمْ يُقَنِّطْ النَّاسَ مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ، وَلَمْ يُرَخِّصْ لَهُمْ فِي مَعَاصِي اللَّهِ، وَلَمْ يُؤَمِّنْهُمْ مِنْ عَذَابِ اللَّهِ، وَلَمْ يَدَعْ الْقُرْآنَ رَغْبَةً عَنْهُ إِلَى غَيْرِهِ، إِنَّهُ لَا خَيْرَ فِي عِبَادَةٍ لَا عِلْمَ فِيهَا، وَلَا عِلْمٍ لَا فَهْمَ فِيهِ، وَلَا قِرَاءَةٍ لَا تَدَبُّرَ فِيهَا"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Ya'quwb Al-Qummiy, amesema: Amenisimulia Layth bin Abiy Sulaym, kutoka kwa Yahyaa — naye ni Ibn 'Abbaad —, kutoka kwa 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه), amesema: "Hakika Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh), Faqiyh wa kweli, ni yule asiyewakatisha watu tamaa ya Rehma ya Allaah, wala asiyewapa ruhusa katika maasi ya Allaah, wala asiyewaaminisha na Adhabu ya Allaah, wala asiyeiacha Qur-aan kwa kuipa mgongo na kuelekea kisichokuwa hiyo. Hakika hakuna kheri katika ibaada isiyokuwa na ilimu ndani yake, wala katika ilimu isiyokuwa na ufahamu ndani yake, wala katika kisomo kisichokuwa na kuzingatia ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
305

حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَرَفَةَ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَبَّادٍ، قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ: "الْفَقِيهُ حَقُّ الْفَقِيهِ الَّذِي لَا يُقَنِّطُ النَّاسَ مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ، وَلَا يُؤَمِّنُهُمْ مِنْ عَذَابِ اللَّهِ، وَلَا يُرَخِّصُ لَهُمْ فِي مَعَاصِي اللَّهِ، إِنَّهُ لَا خَيْرَ فِي عِبَادَةٍ لَا عِلْمَ فِيهَا، وَلَا خَيْرَ فِي عِلْمٍ لَا فَهْمَ فِيهِ، وَلَا خَيْرَ فِي قِرَاءَةٍ لَا تَدَبُّرَ فِيهَا"

Ametusimulia Al-Hasan bin 'Arafah, ametusimulia Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Yahyaa bin 'Abbaad, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh), Faqiyh wa kweli, ni yule ambaye hawakatishi watu tamaa ya Rehma ya Allaah, wala hawaaminishi na Adhabu ya Allaah, wala hawapi ruhusa katika maasi ya Allaah. Hakika hakuna kheri katika ibaada isiyokuwa na ilimu ndani yake, wala hakuna kheri katika ilimu isiyokuwa na ufahamu ndani yake, wala hakuna kheri katika kisomo kisichokuwa na kuzingatia ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
306

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ حَازِمٍ، حَدَّثَنِي عَمِّي جَرِيرُ بْنُ زَيْدٍ، أَنَّهُ سَمِعَ تُبَيْعًا يُحَدِّثُ، عَنْ كَعْبٍ، قَالَ: "إِنِّي لَأَجِدُ نَعْتَ قَوْمٍ يَتَعَلَّمُونَ لِغَيْرِ الْعَمَلِ، وَيَتَفَقَّهُونَ لِغَيْرِ الْعِبَادَةِ، وَيَطْلُبُونَ الدُّنْيَا بِعَمَلِ الْآخِرَةِ، وَيَلْبَسُونَ جُلُودَ الضَّأْنِ، وَقُلُوبُهُمْ أَمَرُّ مِنْ الصَّبْرِ، فَبِي يَغْتَرُّونَ، أَوْ إِيَّايَ يُخَادِعُونَ؟ فَحَلَفْتُ بِي لَأُتِيحَنَّ لَهُمْ فِتْنَةً تَتْرُكُ الْحَلِيمَ فِيهَا حَيْرَانَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yaziyd bin Haazim, amenisimulia ammi yangu Jariyr bin Zayd, kwamba alimsikia Tubay' akisimulia kutoka kwa Ka'b, amesema: "Hakika mimi ninaikuta sifa ya watu wanaojifunza (ilimu) kwa ajili ya kisichokuwa kuitendea kazi, na wanajifunza Fiqh kwa ajili ya kisichokuwa ibaada, na wanaitafuta dunia kwa amali ya Aakhirah, na wanavaa ngozi za kondoo, na nyoyo zao ni chungu zaidi kuliko shubiri. (Allaah Anasema:) Je, ni Mimi wanayedanganyika Naye, au ni Mimi wanayemhadaa? Basi Nimeapa kwa Mimi Mwenyewe: hakika Nitawaletea fitna itakayomwacha mpole (mwenye busara) ndani yake akiwa ameduwaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
307

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عَبْدِ الصَّمَدِ الْعَمِّيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو عِمْرَانَ الْجَوْنِيُّ، عَنْ هَرِمِ بْنِ حَيَّانَ، أَنَّهُ قَالَ: "إِيَّاكُمْ وَالْعَالِمَ الْفَاسِقَ، فَبَلَغَ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَكَتَبَ إِلَيْهِ وَأَشْفَقَ مِنْهَا، مَا الْعَالِمُ الْفَاسِقُ؟، قَالَ: فَكَتَبَ إِلَيْهِ هَرِمٌ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، وَاللَّهِ مَا أَرَدْتُ بِهِ إِلَّا الْخَيْرَ: يَكُونُ إِمَامٌ يَتَكَلَّمُ بِالْعِلْمِ، وَيَعْمَلُ بِالْفِسْقِ، فَيُشَبِّهُ عَلَى النَّاسِ، فَيَضِلُّوا"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin 'Abdis-Swamad Al-'Ammiy, ametusimulia Abuw 'Imraan Al-Jawniy, kutoka kwa Harim bin Hayyaan, kwamba alisema: "Jihadharini na 'Aalim (Mwanazuoni) fasiki." Hilo likamfikia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) — akamwandikia — naye akaliogopa (neno) hilo: 'Aalim fasiki ni nani? Akasema: Harim akamwandikia: Yaa Amiri wa Waumini, Wa-Allaahi, sikukusudia kwalo isipokuwa kheri: anakuwepo Imaam (kiongozi) anayezungumza kwa ilimu na anatenda kwa ufasiki, basi anawababaishia watu, wakapotea.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
308

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ مُطَرِّفٍ، وَعَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ إِسْمَاعِيل بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي الْمُهَاجِرِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: "مَنْ أَرَادَ أَنْ يُكْرَمَ دِينُهُ، فَلَا يَدْخُلْ عَلَى السُّلْطَانِ، وَلَا يَخْلُوَنَّ بِالنِّسْوَانِ، وَلَا يُخَاصِمَنَّ أَصْحَابَ الْأَهْوَاءِ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, ametusimulia Al-Waliyd bin Muslim, kutoka kwa Muhammad bin Mutwarrif na 'Abdul-'Aziyz bin Ismaa'iyl bin 'Ubaydi-Allaah bin Abil-Muhaajir, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Anayetaka Dini yake iheshimiwe, basi asiingie kwa mtawala, wala asikae faragha kabisa na wanawake, wala asibishane kabisa na watu wa matamanio."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
309

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ يُونُسَ، قَالَ: كَتَبَ إِلَيَّ مَيْمُونُ بْنُ مِهْرَانَ: "إِيَّاكَ وَالْخُصُومَةَ وَالْجِدَالَ فِي الدِّينِ، وَلَا تُجَادِلَنَّ عَالِمًا، وَلَا جَاهِلًا، أَمَّا الْعَالِمُ، فَإِنَّهُ يَخْزَنُ عَنْكَ عِلْمَهُ، وَلَا يُبَالِي مَا صَنَعْتَ، وَأَمَّا الْجَاهِلُ، فَإِنَّهُ يُخَشِّنُ بِصَدْرِكَ وَلَا يُطِيعُكَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Yuwnus, amesema: Maymuwn bin Mihraan aliniandikia: "Jihadhari na ugomvi na mabishano katika Dini; wala usibishane kabisa na 'Aalim (Mwanazuoni) wala mjinga. Ama 'Aalim, yeye atakuzuilia ilimu yake, wala hajali ulichokifanya; na ama mjinga, yeye atakutia ukali kifuani mwako, wala hatakutii."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
338
Hadiyth
310

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، قَالَ: قَالَ سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ عَلَيْهِ السَّلَام لِابْنِهِ: "دَعِ الْمِرَاءَ، فَإِنَّ نَفْعَهُ قَلِيلٌ، وَهُوَ يُهَيِّجُ الْعَدَاوَةَ بَيْنَ الْإِخْوَانِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, amesema: Sulaymaan bin Daawuwd (عليهما السلام) alimwambia mwanawe: "Acha mabishano, kwani manufaa yake ni machache, nayo huchochea uadui baina ya ndugu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
341
Hadiyth
311

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ أَبِي حَكِيمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ عَبْدِ الْعَزِيزِ، يَقُولُ: "مَنْ جَعَلَ دِينَهُ غَرَضًا لِلْخُصُومَاتِ، أَكْثَرَ التَّنَقُّلَ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Idriys, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Abiy Hakiym, amesema: Nilimsikia 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz akisema: "Anayeifanya Dini yake kuwa shabaha ya magomvi, hukithirisha kugeuka-geuka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
342
Hadiyth
312

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، قَالَ: كَتَبَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ إِلَى أَهْلِ الْمَدِينَةِ: "أَنَّهُ مَنْ تَعَبَّدَ بِغَيْرِ عِلْمٍ، كَانَ مَا يُفْسِدُ أَكْثَرَ مِمَّا يُصْلِحُ، وَمَنْ عَدَّ كَلَامَهُ مِنْ عَمَلِهِ، قَلَّ كَلَامُهُ إِلَّا فِيمَا يَعْنِيهِ، وَمَنْ جَعَلَ دِينَهُ غَرَضًا لِلْخُصُومَاتِ، كَثُرَ تَنَقُّلُهُ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sa'iyd bin 'Abdil-'Aziyz, amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz aliwaandikia watu wa Madiynah: "Kwamba anayefanya ibaada bila ya ilimu, anachokiharibu huwa ni zaidi kuliko anachokitengeneza; na anayehesabu maneno yake kuwa ni katika amali zake, maneno yake huwa machache isipokuwa katika yale yanayomhusu; na anayeifanya Dini yake kuwa shabaha ya magomvi, kugeuka-geuka kwake hukithiri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
342
Hadiyth
313

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ بُرْقَانَ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ، قَالَ: سَأَلَهُ رَجُلٌ عَنْ شَيْءٍ مِنْ الْأَهْوَاءِ، فَقَالَ: "عَلَيْكَ بِدِينِ الْأَعْرَابِيِّ، وَالْغُلَامِ فِي الْكُتَّابِ، وَالْهَ عَمَّا سِوَى ذَلِكَ"، قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: كَثُرَ تَنَقُّلُهُ، أَيْ: يَنْتَقِلُ مِنْ رَأْيٍ إِلَى رَأْيٍ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ja'far bin Burqaan, kutoka kwa 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz, amesema: Mtu mmoja alimuuliza kuhusu jambo katika matamanio (ya uzushi). Akasema: "Shikamana na Dini ya Bedui, na ya kijana aliye chuoni (anayejifunza kusoma), na achana na yasiyokuwa hayo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: "Kugeuka-geuka kwake hukithiri" maana yake ni: anahama kutoka rai moja kwenda rai nyingine.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
342
Hadiyth
314

30-Mlangoباب في اجتناب الأهواءMlango Wa Kuhusu Kujiepusha Na Matamanio

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ: "إِذَا رَأَيْتَ قَوْمًا يُنْتِجُونَ بِأَمْرٍ دُونَ عَامَّتِهِمْ، فَهُمْ عَلَى تَأْسِيسِ الضَّلَالَةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz amesema: "Ukiwaona watu wanaonong'onezana kwa siri juu ya jambo bila ya watu wao wengine, basi wao wako katika kuasisi upotofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
343
Hadiyth
315

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: "قَالَ إِبْلِيسُ لِأَوْلِيَائِهِ: مِنْ أَيِّ شَيْءٍ تَأْتُونَ بَنِي آدَمَ؟، فَقَالُوا: مِنْ كُلِّ شَيْءٍ، قَالَ: فَهَلْ تَأْتُونَهُمْ مِنْ قِبَلِ الِاسْتِغْفَارِ؟، فَقَالُوا: هَيْهَاتَ! ذَاكَ شَيْءٌ قُرِنَ بِالتَّوْحِيدِ، قَالَ: لَأَبُثَّنَّ فِيهِمْ شَيْئًا لَا يَسْتَغْفِرُونَ اللَّهَ مِنْهُ، قَالَ: فَبَثَّ فِيهِمْ الْأَهْوَاءَ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Is-haaq, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: "Ibliys aliwaambia vipenzi vyake: Mnawajia wanaadam kupitia kitu gani? Wakasema: Kupitia kila kitu. Akasema: Je, mnawajia kupitia upande wa istighfaar (kuomba Maghfirah)? Wakasema: Wapi! Hilo ni jambo lililofungamanishwa na Tawhiyd. Akasema: Hakika nitaeneza kati yao kitu ambacho hawatamuomba Allaah Maghfirah kutokana nacho. Akasema: Basi akaeneza kati yao matamanio (ya uzushi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
344
Hadiyth
316

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ الْمُحَارِبِيِّ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: "مَا أَدْرِي أَيُّ النِّعْمَتَيْنِ عَلَيَّ أَعْظَمُ: أَنْ هَدَانِي لِلْإِسْلَامِ، أَوْ عَافَانِي مِنْ هَذِهِ الْأَهْوَاءِ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Is-haaq, kutoka kwa Al-Muhaaribiy, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Mujaahid, amesema: "Sijui ni ipi kati ya Neema mbili juu yangu iliyo kubwa zaidi: kwamba Ameniongoza kwenye Islaam, au Ameniepusha na matamanio haya."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
344
Hadiyth
317

أَخْبَرَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا عِيسَى بْنُ يُونُسَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ الْأَعْوَرِ، عَنْ حَبَّةَ بْنِ جُوَيْنٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَلِيًّا، أَوْ قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "لَوْ أَنَّ رَجُلًا صَامَ الدَّهْرَ كُلَّهُ، وَقَامَ الدَّهْرَ كُلَّهُ، ثُمَّ قُتِلَ بَيْنَ الرُّكْنِ وَالْمَقَامِ، لَحَشَرَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ مَنْ يَرَى أَنَّهُ كَانَ عَلَى هُدًى"

Ametukhabarisha Muwsaa bin Khaalid, ametusimulia 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim Al-A'war, kutoka kwa Habbah bin Juwayn, amesema: Nilimsikia 'Aliy (رضي الله عنه) — au alisema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema —: "Lau mtu angefunga Swawm dahari yote, na akasimama (kuswali usiku) dahari yote, kisha akauawa baina ya Ar-Rukn (pembe ya Jiwe Jeusi) na Al-Maqaam [mahali pa kisimamo cha Ibraahiym (عليه السلام)], Allaah Angemkusanya Siku ya Qiyaamah pamoja na yule anayeona kwamba alikuwa juu ya uongofu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
344
Hadiyth
318

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، عَنْ هَارُونَ هُوَ ابْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ شُعَيْبٍ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، عَنْ أَبِي صَادِقٍ، قَالَ: قَالَ سَلْمَانُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "لَوْ وَضَعَ رَجُلٌ رَأْسَهُ عَلَى الْحَجَرِ الْأَسْوَدِ، فَصَامَ النَّهَارَ، وَقَامَ اللَّيْلَ، لَبَعَثَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ هَوَاهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, kutoka kwa Haaruwn — naye ni Ibn Al-Mughiyrah —, kutoka kwa Shu'ayb, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa Abuw Swaadiq, amesema: Salmaan (رضي الله عنه) amesema: "Lau mtu angeweka kichwa chake juu ya Jiwe Jeusi, akafunga Swawm mchana, na akasimama (kuswali) usiku, Allaah Angemfufua Siku ya Qiyaamah pamoja na matamanio yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
344
Hadiyth
319

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا مَنْصُورٌ هُوَ ابْنُ أَبِي الْأَسْوَدِ، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ حَصِيرَةَ، عَنْ أَبِي صَادِقٍ الْأَزْدِيِّ، عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ نَاجِذٍ، قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "كُونُوا فِي النَّاسِ كَالنَّحْلَةِ فِي الطَّيْرِ: إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ الطَّيْرِ شَيْءٌ إِلَّا وَهُوَ يَسْتَضْعِفُهَا، وَلَوْ يَعْلَمُ الطَّيْرُ مَا فِي أَجْوَافِهَا مِنْ الْبَرَكَةِ، لَمْ يَفْعَلُوا ذَلِكَ بِهَا، خَالِطُوا النَّاسَ بِأَلْسِنَتِكُمْ وَأَجْسَادِكُمْ، وَزَايِلُوهُمْ بِأَعْمَالِكُمْ وَقُلُوبِكُمْ، فَإِنَّ لِلْمَرْءِ مَا اكْتَسَبَ، وَهُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ مَنْ أَحَبَّ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Manswuwr — naye ni Ibn Abil-Aswad —, kutoka kwa Al-Haarith bin Haswiyrah, kutoka kwa Abuw Swaadiq Al-Azdiy, kutoka kwa Rabiy'ah bin Naajidh, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Kuweni kati ya watu kama nyuki kati ya ndege: hakika hakuna yeyote katika ndege ila anamwona kuwa dhaifu; na lau ndege wangejua baraka iliyomo ndani ya matumbo yake, wasingemfanyia hivyo. Changamaneni na watu kwa ndimi zenu na miili yenu, na tengananeni nao kwa amali zenu na nyoyo zenu; kwani mtu atapata alichokichuma, naye Siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na anayempenda."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
345
Hadiyth
320

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنِي بَقِيَّةُ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "نِعْمَ وَزِيرُ الْعِلْمِ الرَّأْيُ الْحَسَنُ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', amenisimulia Baqiyyah, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Ni msaidizi bora ulioje wa ilimu: rai nzuri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
346
Hadiyth
321

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ: "كَفَى بِالْمَرْءِ عِلْمًا أَنْ يَخْشَى اللَّهَ، وَكَفَى بِالْمَرْءِ جَهْلًا أَنْ يُعْجَبَ بِعِلْمِهِ"،

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Masruwq, amesema: "Yatosha kwa mtu kuwa ni ilimu kwamba amkhofu Allaah; na yatosha kwa mtu kuwa ni ujinga kwamba ajione ajabu kwa ilimu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
346
Hadiyth
322

قَالَ: وقَالَ مَسْرُوقٌ: "الْمَرْءُ حَقِيقٌ أَنْ يَكُونَ لَهُ مَجَالِسُ يَخْلُو فِيهَا، فَيَذْكُرُ ذُنُوبَهُ، فَيَسْتَغْفِرُ اللَّهَ تَعَالَى مِنْهَا"

Amesema: Na Masruwq amesema: "Mtu anastahiki kuwa na vikao ambavyo anakaa faragha humo, akakumbuka madhambi yake, na akamuomba Allaah (تعالى) Maghfirah kutokana nayo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
346
Hadiyth
323

31-Mlangoباب من رخص في الحديث إذا أصاب المعنىMlango Wa Aliyetoa Ruhusa
Katika [Kusimulia] Hadiyth Anapoipatia Maana

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنِي مَعْنٌ، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ صَالِحٍ، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ مَكْحُولٍ، عَنْ وَاثِلَةَ بْنِ الْأَسْقَعِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِذَا حَدَّثْنَاكُمْ بِالْحَدِيثِ عَلَى مَعْنَاهُ، فَحَسْبُكُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, amenisimulia Ma'n, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Swaalih, kutoka kwa Al-'Alaa bin Al-Haarith, kutoka kwa Makhuwl, kutoka kwa Waathilah bin Al-Asqa' (رضي الله عنه), amesema: "Tunapokusimulieni Hadiyth kwa maana yake, basi inakutosheni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
324

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا فُضَيْلُ بْنُ عِيَاضٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ: "أَنَّهُ كَانَ إِذَا حَدَّثَ، لَمْ يُقَدِّمْ وَلَمْ يُؤَخِّرْ، وَكَانَ الْحَسَنُ إِذَا حَدَّثَ، قَدَّمَ وَأَخَّرَ"

Ametukhabarisha 'Aaswim bin Yuwsuf, ametusimulia Fudhwayl bin 'Iyaadhw, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Ibn Siyriyn: "Kwamba yeye alikuwa anaposimulia, hatangulizi wala haakhirishi (neno); na Al-Hasan alikuwa anaposimulia, hutanguliza na huakhirisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
325

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَخْبَرَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، قَالَ: "كَانَ الْحَسَنُ يُحَدِّثُ بِالْحَدِيثِ الْأَصْلُ وَاحِدٌ، وَالْكَلَامُ مُخْتَلِفٌ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametukhabarisha Jariyr bin Haazim, amesema: "Al-Hasan alikuwa akisimulia Hadiyth: asili ni moja, na maneno yanatofautiana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
326

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سُوقَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَلِيِّ بْنِ الْحُسَيْنِ، قَالَ: حَدَّثَ عُبَيْدُ بْنُ عُمَيْرٍ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَثَلُ الْمُنَافِقِ مَثَلُ الشَّاةِ بَيْنَ الرَّبَضَيْنِ أَوْ بَيْنَ الْغَنَمَيْنِ"، فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: لَا، إِنَّمَا قَالَ كَذَا، وَكَذَا، قَالَ: وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ إِذَا سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَزِدْ فِيهِ، وَلَمْ يُنْقِصْ مِنْهُ، وَلَمْ يُجَاوِزْهُ، وَلَمْ يُقَصِّرْ عَنْهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Muhammad bin Suwqah, kutoka kwa Muhammad bin 'Aliy bin Al-Husayn, amesema: 'Ubayd bin 'Umayr alimsimulia 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mfano wa mnafiki ni kama mfano wa mbuzi aliye kati ya mazizi mawili, au kati ya makundi mawili ya mbuzi na kondoo." Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akasema: Hapana; hakika alisema hivi na hivi. Akasema: Na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa anapomsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), haongezi ndani yake, wala hapunguzi kutoka kwake, wala haivuki, wala hapungukiwi nayo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
327

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُلَيَّةَ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: كَانَ الشَّعْبِيُّ، وَالنَّخَعِيُّ، وَالْحَسَنُ يُحَدِّثُونَ بِالْحَدِيثِ مَرَّةً هَكَذَا، وَمَرَّةً هَكَذَا، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِمُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، فَقَالَ: "أَمَا إِنَّهُمْ لَوْ حَدَّثُوا بِهِ كَمَا سَمِعُوهُ، كَانَ خَيْرًا لَهُمْ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Ibn 'Ulayyah, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema: Ash-Sha'biy, na An-Nakha'iy, na Al-Hasan walikuwa wakisimulia Hadiyth mara hivi na mara hivi. Nikamtajia hilo Muhammad bin Siyriyn, akasema: "Ama wao, lau wangeisimulia kama walivyoisikia, ingekuwa ni bora kwao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
328

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا عَثَّامٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، قَالَ: "إِنِّي لَأَسْمَعُ الْحَدِيثَ لَحْنًا، فَأَلْحَنُ اتِّبَاعًا لِمَا سَمِعْتُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia 'Aththaam, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa 'Umaarah bin 'Umayr, kutoka kwa Abuw Ma'mar, amesema: "Hakika mimi huisikia Hadiyth ikiwa na kosa la lugha (la i'raab), nami hukosea (vivyo hivyo) kwa kufuata nilichokisikia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
347
Hadiyth
329

32-Mlangoباب في فضل العلم والعالمMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Ilimu Na 'Aalim (Mwanazuoni)

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مَيْسَرَةَ، قَالَ: رَأَى مُجَاهِدٌ طَاوُوسًا فِي الْمَنَامِ، كَأَنَّهُ فِي الْكَعْبَةِ يُصَلِّي مُتَقَنِّعًا، وَالنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى بَابِ الْكَعْبَةِ، فَقَالَ لَهُ: "يَا عَبْدَ اللَّهِ، اكْشِفْ قِنَاعَكَ وَأَظْهِرْ قِرَاءَتَكَ"، قَالَ: فَكَأَنَّهُ عَبَّرَهُ عَلَى الْعِلْمِ، فَانْبَسَطَ بَعْدَ ذَلِكَ فِي الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibraahiym bin Maysarah, amesema: Mujaahid alimwona Twaawuws usingizini (katika ndoto), kama kwamba yuko ndani ya Al-Ka'bah akiswali amejifunika kichwa, na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) yuko mlangoni mwa Al-Ka'bah. Akamwambia: "Yaa 'Abda-Allaah, funua kitambaa chako, na dhihirisha kisomo chako." Akasema: Basi ni kama kwamba aliifasiri (ndoto hiyo) kuwa ni ilimu; akawa mkunjufu baada ya hapo katika (kusimulia) Hadiyth.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
349
Hadiyth
330

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ يَمَانٍ، عَنْ ابْنِ ثَوْبَانَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ ضَمْرَةَ، عَنْ كَعْبٍ، قَالَ: "الدُّنْيَا مَلْعُونَةٌ، مَلْعُونٌ مَا فِيهَا، إِلَّا مُتَعَلِّمَ خَيْرٍ، أَوْ مُعَلِّمَهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Ibn Yamaan, kutoka kwa Ibn Thawbaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Dhwamrah, kutoka kwa Ka'b, amesema: "Dunia imelaaniwa, kimelaaniwa kilichomo ndani yake, isipokuwa mwenye kujifunza kheri au mwenye kuifundisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
350
Hadiyth
331

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ بَحِيرِ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ، قَالَ: "النَّاسُ عَالِمٌ وَمُتَعَلِّمٌ، وَمَا بَيْنَ ذَلِكَ هَمَجٌ لَا خَيْرَ فِيهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Bahiyr bin Sa'd, kutoka kwa Khaalid bin Ma'daan, amesema: "Watu ni 'Aalim (Mwanazuoni) na mwanafunzi; na walio kati ya hao ni watu duni wasio na thamani, hakuna kheri ndani yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
350
Hadiyth
332

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ رَجَاءٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: كَانُوا يَقُولُونَ: "مَوْتُ الْعَالِمِ ثُلْمَةٌ فِي الْإِسْلَامِ، لَا يَسُدُّهَا شَيْءٌ مَا اخْتَلَفَ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Rajaa, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: Walikuwa wakisema: "Kifo cha 'Aalim (Mwanazuoni) ni pengo katika Islaam, hakuna kitu kinachoweza kuliziba maadamu usiku na mchana vinapishana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
350
Hadiyth
333

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْحَسَنِ الصَّنْعَانِيُّ، حَدَّثَنَا مُنْذِرٌ هُوَ ابْنُ النُّعْمَانِ، عَنْ وَهْبِ بْنِ مُنَبِّهٍ، قَالَ: "مَجْلِسٌ يُتَنَازَعُ فِيهِ الْعِلْمُ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ قَدْرِهِ صَلَاةً، لَعَلَّ أَحَدَهُمْ يَسْمَعُ الْكَلِمَةَ فَيَنْتَفِعُ بِهَا سَنَةً، أَوْ مَا بَقِيَ مِنْ عُمُرِهِ"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametusimulia Ibraahiym bin Muwsaa, ametupa khabari Muhammad bin Al-Hasan Asw-Swan'aaniy, ametusimulia Mundhir — naye ni Ibn An-Nu'maan —, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, amesema: "Kikao ambacho ilimu inapokezanwa (inajadiliwa) ndani yake ni kipenzi zaidi kwangu kuliko (kuswali) Swalaah kwa kiasi cha muda wake; huenda mmoja wao akasikia neno, akanufaika nalo mwaka mzima, au (muda) uliobakia wa umri wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
350
Hadiyth
334

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا وَكِيعٌ، قَالَ: قَالَ سُفْيَانُ: "مَا أَعْلَمُ عَمَلًا أَفْضَلَ مِنْ طَلَبِ الْعِلْمِ وَحِفْظِهِ لِمَنْ أَرَادَ اللَّهُ تَعَالَى بِهِ خَيْرًا"،

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametupa khabari Wakiy', amesema: Sufyaan amesema: "Sijui amali iliyo bora zaidi kuliko kutafuta ilimu na kuihifadhi, kwa yule ambaye Allaah (تعالى) Amemtakia kheri kwayo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
350
Hadiyth
335

وَقَالَ: قَالَ الْحَسَنُ بْنُ صَالِحٍ: "إِنَّ النَّاسَ لَيَحْتَاجُونَ إِلَى هَذَا الْعِلْمِ فِي دِينِهِمْ، كَمَا يَحْتَاجُونَ إِلَى الطَّعَامِ وَالشَّرَابِ فِي دُنْيَاهُمْ"

Na amesema: Al-Hasan bin Swaalih amesema: "Hakika watu wanaihitaji ilimu hii katika Dini yao, kama wanavyohitaji chakula na kinywaji katika dunia yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
352
Hadiyth
336

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، وَجَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا مِسْعَرٌ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، قَالَ: قَالَ أَبُو الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "تَعَلَّمُوا قَبْلَ أَنْ يُقْبَضَ الْعِلْمُ، فَإِنَّ قَبْضَ الْعِلْمِ قَبْضُ الْعُلَمَاءِ، وَإِنَّ الْعَالِمَ وَالْمُتَعَلِّمَ فِي الْأَجْرِ سَوَاءٌ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym na Ja'far bin 'Awn, wamesema: Ametusimulia Mis'ar, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, amesema: Abud-Dardaa (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni kabla ilimu haijachukuliwa; kwani kuchukuliwa kwa ilimu ni kuchukuliwa kwa 'Ulamaa (Wanazuoni). Na hakika 'Aalim (Mwanazuoni) na mwanafunzi ni sawa katika malipo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
337

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ الْخُرَاسَانِيِّ، عَنْ الضَّحَّاكِ: {وَلَكِنْ كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنْتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ}، قَالَ: "حَقٌّ عَلَى كُلِّ مَنْ قَرَأَ الْقُرْآنَ أَنْ يَكُونَ فَقِيهًا"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa Abuw 'Abdi-Allaah Al-Khuraasaaniy, kutoka kwa Adh-Dhwahhaak, (kuhusu Kauli Yake):

وَلَكِنْ كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنْتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ

bali (atawaambia): Kuweni Rabbaaniyyuwn (Marabi) kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu [Aal-‘Imraan (3:79)]

amesema: "Ni haki juu ya kila aliyesoma Qur-aan kwamba awe Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
338

أَخْبَرَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَفْصٍ، عَنْ أَشْعَثَ بْنِ سَوَّارٍ، عَنْ الْحَسَنِ: {لَوْلا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالأَحْبَارُ}، قَالَ: "الْحُكَمَاءُ الْعُلَمَاءُ"

Ametukhabarisha Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Hafsw, kutoka kwa Ash'ath bin Sawwaar, kutoka kwa Al-Hasan, (kuhusu Kauli Yake):

لَوْلا يَنْهَاهُمُ الرَّبَّانِيُّونَ وَالأَحْبَارُ

Basi mbona Ar-Rabbaaniyyuwn (Marabi) na Al-Ahbaar (Mafuqahaa wa Kiyahudi) hawawakatazi [Al-Maaidah (5:63)]

amesema: "(Hao ni) wenye hekima, 'Ulamaa (Wanazuoni)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
339

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: {كُونُوا رَبَّانِيِّينَ}، قَالَ: "عُلَمَاءُ فُقَهَاءُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: (kuhusu Kauli Yake):

كُونُوا رَبَّانِيِّينَ

Kuweni Rabbaaniyyuwn (Marabi) [Aal-‘Imraan (3:79)]

amesema: "'Ulamaa (Wanazuoni), Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
340

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ بْنَ عُيَيْنَةَ، يَقُولُ: "يُرَادُ لِلْعِلْمِ الْحِفْظُ، وَالْعَمَلُ، وَالِاسْتِمَاعُ، وَالْإِنْصَاتُ، وَالنَّشْرُ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Sa'iyd, amesema: Nilimsikia Sufyaan bin 'Uyaynah akisema: "Ilimu inahitaji kuhifadhiwa, na kutendewa kazi, na kusikilizwa, na kunyamaziwa kimya (kwa makini), na kuenezwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
341

قَالَ: وَأَخْبَرَنِي مُحَمَّدٌ أَبُو عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، قَالَ: "أَجْهَلُ النَّاسِ مَنْ تَرَكَ مَا يَعْلَمُ، وَأَعْلَمُ النَّاسِ مَنْ عَمِلَ بِمَا يَعْلَمُ، وَأَفْضَلُ النَّاسِ أَخْشَعَهُمْ لِلَّهِ عز وجل"

Amesema: Na amenikhabarisha Muhammad Abuw 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, amesema: "Mjinga zaidi wa watu ni yule anayeacha anachokijua; na mjuzi zaidi wa watu ni yule anayetenda kwa anachokijua; na bora zaidi wa watu ni yule mwenye kumnyenyekea zaidi Allaah (عز وجل) kati yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
342

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ جَعْفَرٍ الرَّقِّيُّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ زَيْدٍ هُوَ ابْنُ أَبِي أُنَيْسَةَ، عَنْ سَيَّارٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "مَنْهُومَانِ لَا يَشْبَعَانِ: مَنْهُومٌ فِي الْعِلْمِ لَا يَشْبَعُ مِنْهُ، وَمَنْهُومٌ فِي الدُّنْيَا لَا يَشْبَعُ مِنْهَا، فَمَنْ تَكُنِ الْآخِرَةُ هَمَّهُ، وَبَثَّهُ، وَسَدَمَهُ، يَكْفِي اللَّهُ ضَيْعَتَهُ، وَيَجْعَلُ غِنَاهُ فِي قَلْبِهِ، وَمَنْ تَكُنِ الدُّنْيَا هَمَّهُ، وَبَثَّهُ، وَسَدَمَهُ، يُفْشِي اللَّهُ عَلَيْهِ ضَيْعَتَهُ، وَيَجْعَلُ فَقْرَهُ بَيْنَ عَيْنَيْهِ، ثُمَّ لَا يُصْبِحُ إِلَّا فَقِيرًا، وَلَا يُمْسِي إِلَّا فَقِيرًا"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Ja'far Ar-Raqqiy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr, kutoka kwa Zayd — naye ni Ibn Abiy Unaysah —, kutoka kwa Sayyaar, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Wenye uchu wawili hawashibi: mwenye uchu wa ilimu, hashibi nayo; na mwenye uchu wa dunia, hashibi nayo. Basi ambaye Aakhirah imekuwa ndiyo hamu yake, na huzuni yake, na shauku yake kubwa, Allaah Atamtosheleza mambo yake ya maisha, na Ataujaalia utajiri wake ndani ya moyo wake. Na ambaye dunia imekuwa ndiyo hamu yake, na huzuni yake, na shauku yake kubwa, Allaah Atamtawanyishia mambo yake ya maisha, na Ataujaalia ufakiri wake baina ya macho yake; kisha hapambaukiwi ila akiwa fakiri, wala hakuchwi ila akiwa fakiri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
353
Hadiyth
343

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عُمَيْسٍ، عَنْ عَوْنٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "مَنْهُومَانِ لَا يَشْبَعَانِ: صَاحِبُ الْعِلْمِ، وَصَاحِبُ الدُّنْيَا، وَلَا يَسْتَوِيَانِ، أَمَّا صَاحِبُ الْعِلْمِ، فَيَزْدَادُ رِضًا لِلرَّحْمَنِ، وَأَمَّا صَاحِبُ الدُّنْيَا، فَيَتَمَادَى فِي الطُّغْيَانِ"، ثُمَّ قَرَأَ عَبْدُ اللَّهِ: {كَلَّا إِنَّ الإِنْسَانَ لَيَطْغَى أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَى}، قَالَ: وَقَالَ الْآخَرُ: {إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ}

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Abuw 'Umays, kutoka kwa 'Awn, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Wenye uchu wawili hawashibi: mwenye ilimu na mwenye dunia; na hawalingani. Ama mwenye ilimu, yeye huzidi katika kumridhisha Ar-Rahmaan; na ama mwenye dunia, yeye huendelea zaidi katika kupindukia mipaka." Kisha 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) akasoma:

كَلَّا إِنَّ الإِنْسَانَ لَيَطْغَى أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَى

Laa hasha! Hakika binaadam bila shaka hupindukia mipaka kuasi. Anapojiona kuwa amejitosheleza. [Al-‘Alaq (96:6-7)]

Akasema: Na mwingine akasema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

Hakika wanaomkhofu Allaah katika Waja Wake ni ‘Ulamaa [Faatwir (35:28)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
355
Hadiyth
344

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُخْتَارٍ، حَدَّثَنَا عَنْبَسَةُ بْنُ الْأَزْهَرِ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: {إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ}، قَالَ: "مَنْ خَشِيَ اللَّهَ فَهُوَ عَالِمٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Ibraahiym bin Mukhtaar, ametusimulia 'Anbasah bin Al-Azhar, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), (kuhusu Kauli Yake):

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

Hakika wanaomkhofu Allaah katika Waja Wake ni ‘Ulamaa [Faatwir (35:28)]

amesema: "Mwenye kumkhofu Allaah, basi yeye ni 'Aalim (Mwanazuoni)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
356
Hadiyth
345

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَال: "مَنْهُومَانِ لَا يَشْبَعَانِ: طَالِبُ عِلْمٍ، وَطَالِبُ دُنْيَا"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Idriys, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Wenye uchu wawili hawashibi: mtafutaji wa ilimu na mtafutaji wa dunia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
357
Hadiyth
346

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ رَبِيعَةَ الصَّنْعَانِيُّ، حَدَّثَنَا رَبِيعَةُ بْنُ يَزِيدَ، قَالَ: سَمِعْتُ وَاثِلَةَ بْنَ الْأَسْقَعِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ طَلَبَ الْعِلْمَ فَأَدْرَكَهُ، كَانَ لَهُ كِفْلَانِ مِنْ الْأَجْرِ، فَإِنْ لَمْ يُدْرِكْهُ، كَانَ لَهُ كِفْلٌ مِنْ الْأَجْرِ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Yaziyd bin Rabiy'ah Asw-Swan'aaniy, ametusimulia Rabiy'ah bin Yaziyd, amesema: Nilimsikia Waathilah bin Al-Asqa' (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayetafuta ilimu akaipata, atakuwa na mafungu mawili ya malipo; na asipoipata, atakuwa na fungu moja la malipo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
357
Hadiyth
347

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ عَوْفٍ، عَنْ عَبَّاسٍ الْعَمِّيِّ، قَالَ: بَلَغَنِي أَنَّ دَاوُدَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ فِي دُعَائِهِ: "سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ، أَنْتَ رَبِّي تَعَالَيْتَ فَوْقَ عَرْشِكَ، وَجَعَلْتَ خَشْيَتَكَ عَلَى مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، فَأَقْرَبُ خَلْقِكَ مِنْكَ مَنْزِلَةً أَشَدُّهُمْ لَكَ خَشْيَةً، وَمَا عِلْمُ مَنْ لَمْ يَخْشَكَ؟ وَمَا حِكْمَةُ مَنْ لَمْ يُطِعْ أَمْرَكَ؟!"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah, ametusimulia Marwaan bin Mu'aawiyah, kutoka kwa 'Awf, kutoka kwa 'Abbaas Al-'Ammiy, amesema: Imenifikia kwamba Nabiy Daawuwd (عليه السلام) alikuwa akisema katika Du'aa yake:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ، أَنْتَ رَبِّي تَعَالَيْتَ فَوْقَ عَرْشِكَ، وَجَعَلْتَ خَشْيَتَكَ عَلَى مَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، فَأَقْرَبُ خَلْقِكَ مِنْكَ مَنْزِلَةً أَشَدُّهُمْ لَكَ خَشْيَةً، وَمَا عِلْمُ مَنْ لَمْ يَخْشَكَ؟ وَمَا حِكْمَةُ مَنْ لَمْ يُطِعْ أَمْرَكَ؟

Utakasifu ni Wako, Yaa Allaah! Wewe Ndiye Rabb wangu; Umetukuka juu ya 'Arsh Yako, na Umeijaalia khofu Yako iwe juu ya walioko mbinguni na ardhini. Basi aliye karibu zaidi Kwako kwa daraja kati ya viumbe Vyako ni yule mwenye kukukhofu zaidi kati yao. Na ni ilimu gani ya asiyekukhofu? Na ni hekima gani ya asiyetii Amri Yako?

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
358
Hadiyth
348

أَخْبَرَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا سَلَّامٌ هُوَ ابْنُ أَبِي مُطِيعٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا الْهَزْهَازِ يُحَدِّثُ، عَنْ الضَّحَّاكِ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "اغْدُ عَالِمًا، أَوْ مُتَعَلِّمًا، وَلَا خَيْرَ فِيمَا سِوَاهُمَا"

Ametukhabarisha Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia Sallaam — naye ni Ibn Abiy Mutwiy' —, amesema: Nilimsikia Abul-Hazhaaz akisimulia kutoka kwa Adh-Dhwahhaak, amesema: 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Toka asubuhi ukiwa 'Aalim (Mwanazuoni) au mwanafunzi, wala hakuna kheri katika wasiokuwa hao wawili."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
359
Hadiyth
349

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، أَنْبَأَنَا الْوَلِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ الْقَاسِمِ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "سَتَكُونُ فِتَنٌ يُصْبِحُ الرَّجُلُ فِيهَا مُؤْمِنًا، وَيُمْسِي كَافِرًا، إِلَّا مَنْ أَحْيَاهُ اللَّهُ بِالْعِلْمِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Al-Waliyd bin Muslim, ametupa khabari Al-Waliyd bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Aliy bin Yaziyd, kutoka kwa Al-Qaasim Abuw 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abuw Umaamah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kutakuwa na fitna ambazo mtu atapambaukiwa ndani yake akiwa Muumini, na ataingiliwa na jioni akiwa kafiri, isipokuwa yule ambaye Allaah Amemhuisha kwa ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
359
Hadiyth
350

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي هَارُونُ بْنُ رِئَابٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "اغْدُ عَالِمًا أَوْ مُتَعَلِّمًا، وَلَا تَغْدُ فِيمَا بَيْنَ ذَلِكَ، فَإِنَّ مَا بَيْنَ ذَلِكَ جَاهِلٌ، وَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ تَبْسُطُ أَجْنِحَتَهَا لِلرَّجُلِ غَدَا يَبْتَغِي الْعِلْمَ مِنْ الرِّضَا بِمَا يَصْنَعُ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Haaruwn bin Ri-aab, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), kwamba alikuwa akisema: "Toka asubuhi ukiwa 'Aalim (Mwanazuoni) au mwanafunzi, wala usitoke asubuhi (ukiwa) kati ya hayo; kwani aliye kati ya hayo ni mjinga. Na hakika Malaika (عليهم السلام) hutandaza mbawa zao kwa mtu aliyetoka asubuhi akitafuta ilimu, kwa kuridhika na anachokifanya."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
359
Hadiyth
351

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، عَنْ رَجُلَيْنِ كَانَا فِي بَنِي إِسْرَائِيلَ: أَحَدُهُمَا كَانَ عَالِمًا يُصَلِّي الْمَكْتُوبَةَ، ثُمَّ يَجْلِسُ فَيُعَلِّمُ النَّاسَ الْخَيْرَ، وَالْآخَرُ يَصُومُ النَّهَارَ وَيَقُومُ اللَّيْلَ، أَيُّهُمَا أَفْضَلُ؟، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَضْلُ هَذَا الْعَالِمِ الَّذِي يُصَلِّي الْمَكْتُوبَةَ ثُمَّ يَجْلِسُ فَيُعَلِّمُ النَّاسَ الْخَيْرَ، عَلَى الْعَابِدِ الَّذِي يَصُومُ النَّهَارَ وَيَقُومُ اللَّيْلَ، كَفَضْلِي عَلَى أَدْنَاكُمْ رَجُلًا"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu watu wawili waliokuwa katika Banuw Israaiyl: mmoja wao alikuwa 'Aalim (Mwanazuoni) anaswali Swalaah ya faradhi, kisha anakaa akiwafundisha watu kheri; na mwingine anafunga Swawm mchana na anasimama (kuswali) usiku: ni yupi kati yao aliye bora zaidi? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Fadhila ya 'Aalim huyu ambaye anaswali Swalaah ya faradhi, kisha anakaa akiwafundisha watu kheri, juu ya mfanya ibaada ambaye anafunga Swawm mchana na anasimama (kuswali) usiku, ni kama fadhila yangu juu ya mtu wa chini kabisa kati yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
359
Hadiyth
352

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ الرَّبِيعِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ ذَكْوَانَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "دَخَلْتُ الْمَسْجِدَ، فَإِذَا الْأَسْوَدُ بْنُ سَرِيعٍ يَقُصُّ، وَحُمَيْدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ يَذْكُرُ الْعِلْمَ فِي نَاحِيَةِ الْمَسْجِدِ، فَمَيَّلْتُ إِلَى أَيِّهِمَا أَجْلِسُ، فَنَعَسْتُ، فَأَتَانِي آتٍ، فَقَالَ: مَيَّلْتَ إِلَى أَيِّهِمَا تَجْلِسُ؟ إِنْ شِئْتَ أَرَيْتُكَ مَكَانَ جِبْرَائِيلَ عَلَيْهِ السَّلامُ مِنْ حُمَيْدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Ar-Rabiy', kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Ubaydi-Allaah, kutoka kwa Al-Hasan bin Dhakwaan, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Niliingia Msikitini; ghafla Al-Aswad bin Sariy' (رضي الله عنه) anasimulia visa (vya mawaidha), na Humayd bin 'Abdir-Rahmaan anataja ilimu katika upande wa Msikiti. Nikasitasita ni kwa yupi kati yao nikae; nikasinzia. Akanijia mjaji, akasema: Unasitasita ni kwa yupi kati yao ukae? Ukitaka nitakuonyesha mahali pa Jibriyl (عليه السلام) kwa Humayd bin 'Abdir-Rahmaan."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
359
Hadiyth
353

أَخْبَرَنَا نَصْرُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دَاوُدَ، عَنْ عَاصِمِ بْنِ رَجَاءِ بْنِ حَيْوَةَ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ جَمِيلٍ، عَنْ كَثِيرِ بْنِ قَيْسٍ، قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا مَعَ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ فِي مَسْجِدِ دِمَشْقَ، فَأَتَاهُ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا أَبَا الدَّرْدَاءِ، إِنِّي أَتَيْتُكَ مِنْ الْمَدِينَةِ، مَدِينَةِ الرَّسُولِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِحَدِيثٍ بَلَغَنِي عَنْكَ أَنَّكَ تُحَدِّثُهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَمَا جَاءَ بِكَ تِجَارَةٌ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: وَلَا جَاءَ بِكَ غَيْرُهُ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَلْتَمِسُ بِهِ عِلْمًا، سَهَّلَ اللَّهُ بِهِ طَرِيقًا مِنْ طُرُقِ الْجَنَّةِ، وَإِنَّ الْمَلَائِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا رِضًا لِطَالِبِ الْعِلْمِ، وَإِنَّ طَالِبَ الْعِلْمِ، لَيَسْتَغْفِرُ لَهُ مَنْ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ حَتَّى الْحِيتَانُ فِي الْمَاءِ، وَإِنَّ فَضْلَ الْعَالِمِ عَلَى الْعَابِدِ كَفَضْلِ الْقَمَرِ عَلَى سَائِرِ النُّجُومِ، إِنَّ الْعُلَمَاءَ هُمْ وَرَثَةُ الْأَنْبِيَاءِ، إِنَّ الْأَنْبِيَاءَ لَمْ يُوَرِّثُوا دِينَارًا، وَلَا دِرْهَمًا، وَإِنَّمَا وَرَّثُوا الْعِلْمَ، فَمَنْ أَخَذَ بِهِ أَخَذَ بِحَظِّهِ، أَوْ بِحَظٍّ وَافِرٍ"

Ametukhabarisha Naswr bin 'Aliy, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Daawuwd, kutoka kwa 'Aaswim bin Rajaa bin Haywah, kutoka kwa Daawuwd bin Jamiyl, kutoka kwa Kathiyr bin Qays, amesema: Nilikuwa nimeketi pamoja na Abud-Dardaa (رضي الله عنه) katika Msikiti wa Dimashq. Mtu mmoja akamjia, akasema: Yaa Abad-Dardaa, hakika mimi nimekujia kutoka Madiynah, mji wa Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa ajili ya Hadiyth iliyonifikia kutoka kwako, kwamba unaisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Je, hukuja kwa sababu ya biashara? Akasema: Hapana. Akasema: Wala hukuja kwa sababu ya jambo jingine? Akasema: Hapana. Akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayeshika njia akitafuta ilimu ndani yake, Allaah Atamsahilishia kwayo njia miongoni mwa njia za Jannah (Pepo). Na hakika Malaika (عليهم السلام) huweka mbawa zao kwa kumridhia mtafutaji wa ilimu. Na hakika mtafutaji wa ilimu huombewa Maghfirah na walioko mbinguni na ardhini, hata samaki ndani ya maji. Na hakika fadhila ya 'Aalim (Mwanazuoni) juu ya mfanya ibaada ni kama fadhila ya mwezi juu ya nyota nyinginezo zote. Hakika 'Ulamaa (Wanazuoni) ndio warithi wa Manabii (عليهم السلام). Hakika Manabii (عليهم السلام) hawakurithisha dinari wala dirhamu, bali walirithisha ilimu; basi atakayeichukua, amechukua fungu lake — au: fungu kamili —."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
361
Hadiyth
354

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ شِمْرِ بْنِ عَطِيَّةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مُعَلِّمُ الْخَيْرِ يَسْتَغْفِرُ لَهُ كُلُّ شَيْءٍ، حَتَّى الْحُوتُ فِي الْبَحْرِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Shimr bin 'Atwiyyah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Mwenye kufundisha kheri, kila kitu kinamuombea Maghfirah, hata samaki baharini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
355

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا مِنْ رَجُلٍ يَسْلُكُ طَرِيقًا يَطْلُبُ فِيهِ عِلْمًا، إِلَّا سَهَّلَ اللَّهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَنْ أَبْطَأَ بِهِ عَمَلُهُ، لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna mtu yeyote anayefuata njia akitafuta ilimu ndani yake, ila Allaah Atamsahilishia kwa hilo njia ya kwenda Jannah (Pepo). Na ambaye amali yake imemchelewesha, nasaba yake haitamharakisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
356

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ يَعْقُوبَ هُوَ الْقُّمِّيُّ، عَنْ هَارُونَ بْنِ عَنْتَرَةَ عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مَا سَلَكَ رَجُلٌ طَرِيقًا يَبْتَغِي فِيهِ الْعِلْمَ، إِلَّا سَهَّلَ اللَّهُ لَهُ بِهِ طَرِيقًا إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَنْ يُبْطِئْ بِهِ عَمَلُهُ، لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Ya'quwb — naye ni Al-Qummiy —, kutoka kwa Haaruwn bin 'Antarah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Hakuna mtu aliyefuata njia akitafuta ilimu ndani yake, ila Allaah Atamsahilishia kwa hilo njia ya kwenda Jannah (Pepo). Na ambaye amali yake inamchelewesha, nasaba yake haitamharakisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
357

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ ابْنِ شَوْذَبٍ، عَنْ مُطَر: {وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ}، قَالَ: "هَلْ مِنْ طَالِبِ خَيْرٍ فَيُعَانَ عَلَيْهِ؟"،

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Ibn Shawdhab, kutoka kwa Matwar, (kuhusu Kauli ya Allaah):

وَلَقَدْ يَسَّرْنَا الْقُرْآنَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِنْ مُدَّكِرٍ

Na kwa yakini Tumeiwepesisha Qur-aan ili ipate kusomwa, kuhifadhiwa na kufahamika. Basi je, yuko yeyote mwenye kuwaidhika? [Al-Qamar (54:17)]

Amesema: "Je, yuko mwenye kutafuta kheri, ili asaidiwe juu yake?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
358

وأَخْبَرَنَا مَرْوَانُ، عَنْ ضَمْرَةَ، قَالَ: "طَالِبُ عِلْمٍ"

Na ametukhabarisha Marwaan, kutoka kwa Dhwamrah, amesema: "(Ni) mwenye kutafuta ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
359

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا يَعْقُوبُ هُوَ الْقُمِّيُّ، عَنْ عَامِرِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: كَانَ أَبُو الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ إِذَا رَأَى طَلَبَةَ الْعِلْمِ، قَالَ: "مَرْحَبًا بِطَلَبَةِ الْعِلْمِ، وَكَانَ يَقُولُ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَوْصَى بِكُمْ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Ya'quwb — naye ni Al-Qummiy —, kutoka kwa 'Aamir bin Ibraahiym, amesema: Abud-Dardaa (رضي الله عنه) alikuwa anapowaona wanaotafuta ilimu, husema: "Karibuni, wanaotafuta ilimu. Na alikuwa akisema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameusia kuhusu nyinyi (mtendewe wema)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
362
Hadiyth
360

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ زِيَادِ بْنِ أَنْعُمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ رَافِعٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، مَرَّ بِمَجْلِسَيْنِ فِي مَسْجِدِهِ، فَقَالَ: "كِلَاهُمَا عَلَى خَيْرٍ، وَأَحَدُهُمَا أَفْضَلُ مِنْ صَاحِبِهِ، أَمَّا هَؤُلَاءِ فَيَدْعُونَ اللَّهَ، وَيَرْغَبُونَ إِلَيْهِ، فَإِنْ شَاءَ أَعْطَاهُمْ، وَإِنْ شَاءَ مَنَعَهُمْ، وَأَمَّا هَؤُلَاءِ فَيَتَعَلَّمُونَ الْفِقْهَ وَالْعِلْمَ، وَيُعَلِّمُونَ الْجَاهِلَ، فَهُمْ أَفْضَلُ، وَإِنَّمَا بُعِثْتُ مُعَلِّمًا"، قَالَ: ثُمَّ جَلَسَ فِيهِمْ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Ziyaad bin An'um, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Raafi', kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipita kwenye vikao viwili katika Msikiti wake, akasema: "Vyote viwili viko juu ya kheri, na kimoja chao ni bora kuliko mwenzake. Ama hawa, wanamuomba Allaah na wanaelekea Kwake kwa shauku; basi Akipenda Atawapa, na Akipenda Atawanyima. Na ama hawa, wanajifunza Fiqh (ufahamu wa Dini) na ilimu, na wanamfundisha asiyejua; basi wao ni bora zaidi. Na hakika mimi nimetumwa nikiwa mwalimu." Akasema: Kisha akaketi pamoja nao.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
365
Hadiyth
361

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ مُطَرِّفِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الشِّخِّيرِ، أَنَّهُ قَالَ لِابْنِهِ: "يَا بُنَيَّ، إِنَّ الْعِلْمَ خَيْرٌ مِنْ الْعَمَلِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa 'Awn bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Mutwarrif bin 'Abdi-Allaah bin Ash-Shikhkhiyr, kwamba alimwambia mwanawe: "Yaa mwanangu, hakika ilimu ni bora kuliko amali."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
362

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، أَخْبَرَنَا شُرَحْبِيلُ بْنُ شَرِيكٍ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْحُبُلِيَّ، يَقُولُ: "لَيْسَ هَدِيَّةٌ أَفْضَلَ مِنْ كَلِمَةِ حِكْمَةٍ، تُهْدِيهَا لِأَخِيكَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, ametukhabarisha Shurahbiyl bin Shariyk, kwamba alimsikia Abuw 'Abdir-Rahmaan Al-Hubuliy akisema: "Hakuna zawadi iliyo bora kuliko neno la hekima unalompa ndugu yako zawadi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
363

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ يَمَانٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَجْلَانَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "فَضْلُ الْعَالِمِ عَلَى الْمُجْتَهِدِ مِئَةُ دَرَجَةٍ، مَا بَيْنَ الدَّرَجَتَيْنِ خَمْسُ مِئَةِ سَنَةٍ، حُضْرِ الْفَرَسِ الْمُضَمَّرِ السَّرِيعِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Yahyaa bin Yamaan, ametusimulia Muhammad bin 'Ajlaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Ubora wa 'Aalim (Mwanazuoni) juu ya mwenye kujitahidi (katika ibaada) ni daraja mia; baina ya daraja mbili ni (mwendo wa) miaka mia tano, kwa mbio za farasi aliyekondeshwa (kwa ajili ya mashindano), mwepesi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
364

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، قَالَ: أَخْبَرَنِي السَّكَنُ بْنُ أَبِي كَرِيمَةَ، عَنْ عِكْرِمَةَ مَوْلَى ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: {يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ}، قَالَ: "يَرْفَعُ اللَّهُ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا بِدَرَجَاتٍ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, amesema: Amenikhabarisha As-Sakan bin Abiy Kariymah, kutoka kwa 'Ikrimah, mwachwa huru wa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), (kuhusu Kauli ya Allaah):

يَرْفَعِ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ

Allaah Atawainua wale walioamini miongoni mwenu, na waliopewa ilimu wana daraja nyingi [Al-Mujaadalah (58:11)]

Amesema: "Allaah Anawainua wale waliopewa ilimu juu ya wale walioamini kwa daraja (nyingi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
365

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ ثَابِتٍ الْبَزَّارُ، حَدَّثَنَا نَصْرُ بْنُ الْقَاسِمِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْمَاعِيل، عَنْ عَمْرِو بْنِ كَثِيرٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ جَاءَهُ الْمَوْتُ وَهُوَ يَطْلُبُ الْعِلْمَ لِيُحْيِيَ بِهِ الْإِسْلَامَ، فَبَيْنَهُ وَبَيْنَ النَّبِيِّينَ دَرَجَةٌ وَاحِدَةٌ فِي الْجَنَّةِ"

Ametukhabarisha Bishr bin Thaabit Al-Bazzaar, ametusimulia Naswr bin Al-Qaasim, kutoka kwa Muhammad bin Ismaa'iyl, kutoka kwa 'Amr bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yeyote ambaye mauti yamemjia naye anatafuta ilimu ili aihuishe kwayo Islaam, basi baina yake na Manabii (عليهم السلام) kuna daraja moja katika Jannah (Pepo)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
366

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مِهْرَانُ، حَدَّثَنَا أَبُو سِنَانٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عَمْرِو بْنِ مَيْمُونٍ، قَالَ: "ذَهَبَ عُمَرُ بِثُلُثَيْ الْعِلْمِ"، قَالَ: فَذَكَرْتُ لِإِبْرَاهِيمَ، فَقَالَ: "ذَهَبَ عُمَرُ بِتِسْعَةِ أَعْشَارِ الْعِلْمِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Mihraan, ametusimulia Abuw Sinaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Amr bin Maymuwn, amesema: "'Umar (رضي الله عنه) ameondoka na theluthi mbili za ilimu." Akasema: Nikamtajia Ibraahiym (hilo), akasema: "'Umar (رضي الله عنه) ameondoka na sehemu tisa kati ya kumi za ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
366
Hadiyth
367

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ ثَابِتٍ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ يَزِيدَ أَبِي خَالِدٍ، عَنْ هَارُونَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مَا اجْتَمَعَ قَوْمٌ فِي بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللَّهِ، يَتَذَاكَرُونَ كِتَابَ اللَّهِ وَيَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إِلَّا أَظَلَّتْهُمْ الْمَلَائِكَةُ بِأَجْنِحَتِهَا، حَتَّى يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ، وَمَنْ سَلَكَ طَرِيقًا يَبْتَغِي بِهِ الْعِلْمَ، سَهَّلَ اللَّهُ طَرِيقَهُ إِلَى الْجَنَّةِ، وَمَنْ أَبْطَأَ بِهِ عَمَلُهُ، لَمْ يُسْرِعْ بِهِ نَسَبُهُ"

Ametukhabarisha Bishr bin Thaabit, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Yaziyd Abuw Khaalid, kutoka kwa Haaruwn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Hawakukusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah, wakikumbushana Kitabu cha Allaah na wakikidurusu baina yao, ila Malaika (عليهم السلام) huwafunika kivuli kwa mbawa zao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Na atakayefuata njia akitafuta kwayo ilimu, Allaah Atamsahilishia njia yake ya kwenda Jannah (Pepo). Na ambaye amali yake imemchelewesha, nasaba yake haitamharakisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
369
Hadiyth
368

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ هُوَ ابْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ زرٍّ، قَالَ: غَدَوْتُ عَلَى صَفْوَانَ بْنِ عَسَّالٍ الْمُرَادِيِّ، وَأَنَا أُرِيدُ أَنْ أَسْأَلَهُ عَنْ الْمَسْحِ عَلَى الْخُفَّيْنِ، فَقَالَ: مَا جَاءَ بِكَ؟، قُلْتُ: ابْتِغَاءُ الْعِلْمِ، قَالَ: أَلَا أُبَشِّرُكَ؟، قُلْتُ: بَلَى، فَقَالَ: رَفَعَ الْحَدِيثَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَالَ: "إِنَّ الْمَلَائِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ الْعِلْمِ، رِضًا بِمَا يَطْلُبُ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Aaswim, ametusimulia Hammaad — naye ni Ibn Salamah —, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Zirr, amesema: Nilikwenda asubuhi kwa Swafwaan bin 'Assaal Al-Muraadiy (رضي الله عنه), nami nikitaka kumuuliza kuhusu kupangusa juu ya khuff (soksi za ngozi) mbili. Akasema: Ni nini kilichokuleta? Nikasema: Kutafuta ilimu. Akasema: Je, nisikubashirie? Nikasema: Bila shaka. Akasema — aliipandisha Hadiyth mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) —, na akasema: "Hakika Malaika (عليهم السلام) huweka mbawa zao kwa ajili ya mwenye kutafuta ilimu, kwa kuridhia anachokitafuta."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
370
Hadiyth
369

33-Mlangoباب من طلب العلم بغير نية فرده العلم إلى النيةMlango Wa Aliyetafuta Ilimu Bila Ya Niya
Na Ilimu Ikamrudisha Kwenye Niya

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ يَمَانٍ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ مُنْذُ أَرْبَعِينَ سَنَةً، قَالَ: "مَا كَانَ طَلَبُ الْحَدِيثِ أَفْضَلَ مِنْهُ الْيَوْمَ، قَالُوا لِسُفْيَانَ: إِنَّهُمْ يَطْلُبُونَهُ بِغَيْرِ نِيَّةٍ؟، قَالَ: طَلَبُهُمْ إِيَّاهُ نِيَّةٌ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Yahyaa bin Yamaan, amesema: Nilimsikia Sufyaan tangu miaka arobaini (iliyopita), amesema: "Kutafuta Hadiyth hakukuwa bora zaidi kuliko kulivyo leo. Wakamwambia Sufyaan: Hakika wao wanaitafuta bila ya niya? Akasema: Kuitafuta kwao ni niya."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
370
Hadiyth
370

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْأَجْلَحِ، حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: "طَلَبْنَا هَذَا الْعِلْمَ وَمَا لَنَا فِيهِ كَبِيرُ نِيَّةٍ، ثُمَّ رَزَقَ اللَّهُ بَعْدُ فِيهِ النِّيَّةَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Ajlah, amenisimulia baba yangu, kutoka kwa Mujaahid, amesema: "Tuliitafuta ilimu hii na hatukuwa na niya kubwa ndani yake; kisha baadaye Allaah Akaturuzuku niya ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
371
Hadiyth
371

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ ثَابِتٍ الْبَزَّارُ، حَدَّثَنَا حَسَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ يُونُسَ بْنِ عُبَيْدٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "لَقَدْ طَلَبَ أَقْوَامٌ الْعِلْمَ، مَا أَرَادُوا بِهِ اللَّهَ تعَالَيَ وَلَا مَا عِنْدَهُ، قَالَ: فَمَا زَالَ بِهِمْ الْعِلْمُ، حَتَّى أَرَادُوا بِهِ اللَّهَ وَمَا عِنْدَهُ"

Ametukhabarisha Bishr bin Thaabit Al-Bazzaar, ametusimulia Hassaan bin Muslim, kutoka kwa Yuwnus bin 'Ubayd, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Kwa hakika watu walitafuta ilimu, hawakumkusudia kwayo Allaah (تعالى) wala yale yaliyoko Kwake. Akasema: Basi ilimu haikuacha kuwa nao, mpaka wakamkusudia kwayo Allaah na yale yaliyoko Kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
371
Hadiyth
372

34-Mlangoباب: التوبيخ لمن يطلب العلم لغير اللهMlango Wa Karipio Kwa Anayetafuta Ilimu
Kwa Ajili Ya Asiyekuwa Allaah

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: قَالَ أَبُو مُسْلِمٍ الْخَوْلَانِيُّ: "الْعُلَمَاءُ ثَلَاثَةٌ: فَرَجُلٌ عَاشَ فِي عِلْمِهِ وَعَاشَ مَعَهُ النَّاسُ فِيهِ، وَرَجُلٌ عَاشَ فِي عِلْمِهِ وَلَمْ يَعِشْ مَعَهُ فِيهِ أَحَدٌ، وَرَجُلٌ عَاشَ النَّاسُ فِي عِلْمِهِ وَكَانَ وَبَالًا عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: Abuw Muslim Al-Khawlaaniy amesema: "'Ulamaa (Wanazuoni) ni watatu: mtu aliyeishi katika ilimu yake, na watu wakaishi pamoja naye ndani yake; na mtu aliyeishi katika ilimu yake, na hakuishi pamoja naye ndani yake yeyote; na mtu ambaye watu waliishi katika ilimu yake, nayo ikawa ni balaa juu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
372
Hadiyth
373

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: قَالَ مُوسَى عَلَيْهِ السَّلامُ: "يَا رَبِّ، أَيُّ عِبَادِكَ أَحْكَمُ؟، قَالَ: الَّذِي يَحْكُمُ لِلنَّاسِ كَمَا يَحْكُمُ لِنَفْسِهِ، قَالَ: يَا رَبِّ، أَيُّ عِبَادِكَ أَغْنَى؟، قَالَ: أَرْضَاهُمْ بِمَا قَسَمْتُ لَهُ، قَالَ: يَا رَبِّ، أَيُّ عِبَادِكَ أَخْشَى لَكَ؟، قَالَ: أَعْلَمُهُمْ بِي"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa 'Uthmaan bin Al-Aswad, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: Muwsaa (عليه السلام) amesema: "Yaa Rabbi, ni yupi miongoni mwa Waja Wako mwenye kuhukumu kwa hekima zaidi? Akasema: Ni yule anayewahukumia watu kama anavyojihukumia nafsi yake. Akasema: Yaa Rabbi, ni yupi miongoni mwa Waja Wako aliye mkwasi zaidi? Akasema: Ni aliye radhi zaidi miongoni mwao kwa kile Nilichomgawia. Akasema: Yaa Rabbi, ni yupi miongoni mwa Waja Wako anayekukhofu zaidi? Akasema: Ni aliye mjuzi zaidi miongoni mwao wa (kunijua) Mimi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
372
Hadiyth
374

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، قَالَ: "كَانَ يُقَالُ الْعُلَمَاءُ ثَلَاثَةٌ: عَالِمٌ بِاللَّهِ يَخْشَى اللَّهَ لَيْسَ بِعَالِمٍ بِأَمْرِ اللَّهِ، وَعَالِمٌ بِاللَّهِ عَالِمٌ بِأَمْرِ اللَّهِ يَخْشَى اللَّهَ، فَذَاكَ الْعَالِمُ الْكَامِلُ، وَعَالِمٌ بِأَمْرِ اللَّهِ لَيْسَ بِعَالِمٍ بِاللَّهِ لَا يَخْشَى اللَّهَ، فَذَلِكَ الْعَالِمُ الْفَاجِرُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, amesema: "Ilikuwa ikisemwa: 'Ulamaa (Wanazuoni) ni watatu: 'Aalim (Mwanazuoni) anayemjua Allaah, anamkhofu Allaah, (lakini) si mjuzi wa Amri ya Allaah; na 'Aalim anayemjua Allaah, mjuzi wa Amri ya Allaah, anamkhofu Allaah — huyo ndiye 'Aalim kamili; na 'Aalim wa Amri ya Allaah, asiyemjua Allaah, asiyemkhofu Allaah — huyo ndiye 'Aalim muovu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
372
Hadiyth
375

أَخْبَرَنَا مَكِّيُّ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "الْعِلْمُ عِلْمَانِ: فَعِلْمٌ فِي الْقَلْبِ فَذَلِكَ الْعِلْمُ النَّافِعُ، وَعِلْمٌ عَلَى اللِّسَانِ فَذَلِكَ حُجَّةُ اللَّهِ عَلَى ابْنِ آدَمَ"،

Ametukhabarisha Makkiyy bin Ibraahiym, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Ilimu ni ilimu mbili: ilimu iliyo moyoni, hiyo ndiyo ilimu yenye manufaa; na ilimu iliyo juu ya ulimi, hiyo ni Hoja ya Allaah juu ya mwanaadam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
373
Hadiyth
376

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ فُضَيْلِ بْنِ عِيَاضٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، مِثْلَ ذَلِكَ

Ametukhabarisha 'Aaswim bin Yuwsuf, kutoka kwa Fudhwayl bin 'Iyaadhw, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wa hayo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
374
Hadiyth
377

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "تَعَلَّمُوا، تَعَلَّمُوا، فَإِذَا عَلِمْتُمْ، فَاعْمَلُوا"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Jifunzeni, jifunzeni; na mtakapojua, basi tendeni (kwa mujibu wake)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
374
Hadiyth
378

أَخْبَرَنَا أَبُو عُبَيْدٍ الْقَاسِمُ بْنُ سَلَّامٍ، حَدَّثَنَا أَبُو إِسْمَاعِيل هُوَ إِبْرَاهِيمُ بْنُ سُلَيْمَانَ الْمُؤَدِّبُ، عَنْ عَاصِمٍ الْأَحْوَلِ، عَنْ مَنْ حَدَّثَهُ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "مَنْ طَلَبَ الْعِلْمَ لِأَرْبَعٍ، دَخَلَ النَّارَ أَوْ نَحْوَ هَذِهِ الْكَلِمَةِ: لِيُبَاهِيَ بِهِ الْعُلَمَاءَ، أَوْ لِيُمَارِيَ بِهِ السُّفَهَاءَ، أَوْ لِيَصْرِفَ بِهِ وُجُوهَ النَّاسِ إِلَيْهِ، أَوْ لِيَأْخُذَ بِهِ مِنْ الْأُمَرَاءِ"

Ametukhabarisha Abuw 'Ubayd Al-Qaasim bin Sallaam, ametusimulia Abuw Ismaa'iyl — naye ni Ibraahiym bin Sulaymaan Al-Muaddib —, kutoka kwa 'Aaswim Al-Ahwal, kutoka kwa aliyemsimulia, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Atakayetafuta ilimu kwa ajili ya (mambo) manne, ataingia motoni — au mfano wa neno hili —: ili ajifakhirishe kwayo mbele ya 'Ulamaa (Wanazuoni), au ili abishane kwayo na wapumbavu, au ili azigeuze kwayo nyuso za watu kumwelekea yeye, au ili achukue kwayo (mali) kutoka kwa watawala."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
374
Hadiyth
379

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هِشَامٍ صَاحِبِ الدَّسْتَوَائِيِّ، قَالَ: قَرَأْتُ فِي كِتَابٍ بَلَغَنِي أَنَّهُ مِنْ كَلَامِ عِيسَى عَلَيْهِ السَّلامُ: "تَعْمَلُونَ لِلدُّنْيَا، وَأَنْتُمْ تُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ عَمَلٍ، وَلَا تَعْمَلُونَ لِلْآخِرَةِ، وَأَنْتُمْ لَا تُرْزَقُونَ فِيهَا إِلَّا بِالْعَمَلِ، ويْلَكُمْ عُلَمَاءَ السَّوْءِ: الْأَجْرَ تَأْخُذُونَ، وَالْعَمَلَ تُضَيِّعُونَ، يُوشِكُ رَبُّ الْعَمَلِ أَنْ يَطْلُبَ عَمَلَهُ، وَتُوشِكُونَ أَنْ تَخْرُجُوا مِنْ الدُّنْيَا الْعَرِيضَةِ إِلَى ظُلْمَةِ الْقَبْرِ وَضِيقِهِ، اللَّهُ يَنْهَاكُمْ عَنْ الْخَطَايَا، كَمَا أَمَرَكُمْ بِالصَّلَاةِ وَالصِّيَامِ، كَيْفَ يَكُونُ مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ مَنْ سَخِطَ رِزْقَهُ، وَاحْتَقَرَ مَنْزِلَتَهُ، وَقَدْ عَلِمَ أَنَّ ذَلِكَ مِنْ عِلْمِ اللَّهِ وَقُدْرَتِهِ؟ كَيْفَ يَكُونُ مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ مَنْ اتَّهَمَ اللَّهَ فِيمَا قَضَى لَهُ، فَلَيْسَ يَرْضَى شَيْئًا أَصَابَهُ؟ كَيْفَ يَكُونُ مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ مَنْ دُنْيَاهُ آثَرُ عِنْدَهُ مِنْ آخِرَتِهِ، وَهُوَ فِي الدُّنْيَا أَفْضَلُ رَغْبَةً؟ كَيْفَ يَكُونُ مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ مَنْ مَصِيرُهُ إِلَى آخِرَتِهِ، وَهُوَ مُقْبِلٌ عَلَى دُنْيَاهُ، وَمَا يَضُرُّهُ أَشْهَى إِلَيْهِ، أَوْ قَالَ: أَحَبُّ إِلَيْهِ مِمَّا يَنْفَعُهُ؟ كَيْفَ يَكُونُ مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ مَنْ يَطْلُبُ الْكَلَامَ لِيُخْبِرَ بِهِ، وَلَا يَطْلُبُهُ لِيَعْمَلَ بِهِ؟"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hishaam sahibu wa Ad-Dastawaaiy, amesema: Nilisoma katika kitabu ambacho imenifikia kwamba ni katika maneno ya 'Iysaa (عليه السلام): "Mnaifanyia kazi dunia, nanyi mnaruzukiwa humo bila ya kufanya kazi; wala hamuifanyii kazi Aakhirah, nanyi hamtaruzukiwa humo ila kwa amali. Ole wenu, enyi 'Ulamaa (Wanazuoni) waovu! Ujira mnauchukua, na kazi mnaipoteza. Yu karibu mwenye kazi kuitaka kazi yake, na mko karibu kutoka katika dunia hii pana kwenda kwenye giza la kaburi na dhiki yake. Allaah Anakukatazeni makosa kama Alivyokuamrisheni Swalaah na Swiyaam. Vipi atakuwa miongoni mwa watu wa ilimu yule aliyeichukia riziki yake, na akaidharau daraja yake, ilhali anajua kwamba hilo ni katika Ilimu ya Allaah na Uwezo Wake? Vipi atakuwa miongoni mwa watu wa ilimu yule aliyemtuhumu Allaah katika yale Aliyomkadiria, basi haridhii kitu kilichomsibu? Vipi atakuwa miongoni mwa watu wa ilimu yule ambaye dunia yake inapendelewa zaidi kwake kuliko Aakhirah yake, naye katika dunia ana shauku kubwa zaidi? Vipi atakuwa miongoni mwa watu wa ilimu yule ambaye marejeo yake ni Aakhirah yake, naye anaielekea dunia yake, na kinachomdhuru kinatamanika zaidi kwake — au alisema: kinapendeza zaidi kwake — kuliko kinachomnufaisha? Vipi atakuwa miongoni mwa watu wa ilimu yule anayetafuta maneno ili ayakhabarishe, wala hayatafuti ili ayatendee kazi?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
375
Hadiyth
380

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا حَرِيزٌ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ عُبَيْدٍ، قَالَ: كَانَ يُقَالُ: "تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ وَانْتَفِعُوا بِهِ، وَلَا تَعَلَّمُوهُ لِتَتَجَمَّلُوا بِهِ، فَإِنَّهُ يُوشِكُ إِنْ طَالَ بِكُمْ عُمُرٌ، أَنْ يَتَجَمَّلَ ذُو الْعِلْمِ بِعِلْمِهِ، كَمَا يَتَجَمَّلُ ذُو الْبِزَّةِ بِبِزَّتِهِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Hariyz, kutoka kwa Habiyb bin 'Ubayd, amesema: Ilikuwa ikisemwa: "Jifunzeni ilimu na mnufaike nayo, wala msiijifunze ili mjipambe nayo; kwani huenda, umri ukirefuka kwenu, mwenye ilimu akajipamba kwa ilimu yake kama anavyojipamba mwenye mavazi mazuri kwa mavazi yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
376
Hadiyth
381

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ الْأَحْوَصِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الشَّرِّ، فَقَالَ:" لَا تَسْأَلُونِي عَنْ الشَّرِّ، وَاسْأَلُونِي عَنْ الْخَيْرِ، يَقُولُهَا ثَلَاثًا، ثُمَّ قَالَ: " أَلَا إِنَّ شَرَّ الشَّرِّ شِرَارُ الْعُلَمَاءِ، وَإِنَّ خَيْرَ الْخَيْرِ خِيَارُ الْعُلَمَاءِ "

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia Baqiyyah, kutoka kwa Al-Ahwasw bin Hakiym, kutoka kwa baba yake, amesema: Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu shari, akasema: "Msiniulize kuhusu shari, na niulizeni kuhusu kheri" — akiyasema mara tatu —, kisha akasema: "Tanabahini! Hakika shari ya shari ni waovu wa 'Ulamaa (Wanazuoni), na hakika kheri ya kheri ni wabora wa 'Ulamaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
376
Hadiyth
382

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا حُمَيْدُ بْنُ الْأَسْوَدِ، عَنْ عِيسَى، قَالَ: سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ: "إِنَّمَا كَانَ يَطْلُبُ هَذَا الْعِلْمَ مَنْ اجْتَمَعَتْ فِيهِ خَصْلَتَانِ: الْعَقْلُ وَالنُّسُكُ، فَإِنْ كَانَ نَاسِكًا، وَلَمْ يَكُنْ عَاقِلًا، قَالَ: هَذَا أَمْرٌ لَا يَنَالُهُ إِلَّا الْعُقَلَاءُ، فَلَمْ يَطْلُبْهُ، وَإِنْ كَانَ عَاقِلًا وَلَمْ يَكُنْ نَاسِكًا، قَالَ: هَذَا أَمْرٌ لَا يَنَالُهُ إِلَّا النُّسَّاكُ، فَلَمْ يَطْلُبْهُ، فَقَالَ الشَّعْبِيُّ: وَلَقَدْ رَهِبْتُ أَنْ يَكُونَ يَطْلُبُهُ الْيَوْمَ مَنْ لَيْسَتْ فِيهِ وَاحِدَةٌ مِنْهُمَا: لَا عَقْلٌ وَلَا نُسُكٌ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, ametusimulia Humayd bin Al-Aswad, kutoka kwa 'Iysaa, amesema: Nilimsikia Ash-Sha'biy akisema: "Hakika aliyekuwa akiitafuta ilimu hii ni yule tu ambaye zimekusanyika ndani yake sifa mbili: akili na ibaada. Akiwa ni mfanya ibaada na hakuwa mwenye akili, husema: Hili ni jambo ambalo halipatwi ila na wenye akili; basi haliitafuti. Na akiwa ni mwenye akili na hakuwa mfanya ibaada, husema: Hili ni jambo ambalo halipatwi ila na wafanya ibaada; basi haliitafuti. Ash-Sha'biy akasema: Na kwa hakika nimehofia kwamba leo anaitafuta yule ambaye hamna ndani yake hata moja kati ya hizo mbili: si akili wala ibaada."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
376
Hadiyth
383

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، قَالَ: زَعَمَ لِي سُفْيَانُ، قَالَ: "كَانَ الرَّجُلُ لَا يَطْلُبُ الْعِلْمَ حَتَّى يَتَعَبَّدَ قَبْلَ ذَلِكَ أَرْبَعِينَ سَنَةً"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, amesema: Sufyaan aliniambia, amesema: "Mtu alikuwa haitafuti ilimu mpaka afanye ibaada kabla ya hapo miaka arobaini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
377
Hadiyth
384

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ بُرْدِ بْنِ سِنَانٍ أَبِي الْعَلَاءِ، عَنْ مَكْحُولٍ، قَالَ: "مَنْ طَلَبَ الْعِلْمَ لِيُمَارِيَ بِهِ السُّفَهَاءَ، وَلِيُبَاهِيَ بِهِ الْعُلَمَاءَ، أَوْ لِيَصْرِفَ بِهِ وُجُوهَ النَّاسِ إِلَيْهِ، فَهُوَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Burd bin Sinaan Abul-'Alaa, kutoka kwa Makhuwl, amesema: "Atakayetafuta ilimu ili abishane kwayo na wapumbavu, na ili ajifakhirishe kwayo mbele ya 'Ulamaa (Wanazuoni), au ili azigeuze kwayo nyuso za watu kumwelekea yeye, basi yeye yumo katika moto wa Jahannam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
378
Hadiyth
385

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ بِسْطَامَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ حَمْزَةَ، حَدَّثَنِي النُّعْمَانُ، عَنْ مَكْحُولٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ طَلَبَ الْعِلْمَ لِيُبَاهِيَ بِهِ الْعُلَمَاءَ، أَوْ لِيُمَارِيَ بِهِ السُّفَهَاءَ، أَوْ يُرِيدُ أَنْ يُقْبِلَ بِوُجُوهِ النَّاسِ إِلَيْهِ، أَدْخَلَهُ اللَّهُ جَهَنَّمَ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Bistwaam, kutoka kwa Yahyaa bin Hamzah, amenisimulia An-Nu'maan, kutoka kwa Makhuwl, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayetafuta ilimu ili ajifakhirishe kwayo mbele ya 'Ulamaa (Wanazuoni), au ili abishane kwayo na wapumbavu, au anataka kuzielekeza nyuso za watu kwake, Allaah Atamuingiza Jahannam."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
378
Hadiyth
386

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ يَمَانٍ، عَنْ الْمِنْهَالِ بْنِ خَلِيفَةَ، عَنْ مَطَرٍ الْوَرَّاقِ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "إِنَّمَا يُحْفَظُ حَدِيثُ الرَّجُلِ عَلَى قَدْرِ نِيَّتِهِ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Yahyaa bin Yamaan, kutoka kwa Al-Minhaal bin Khaliyfah, kutoka kwa Matwar Al-Warraaq, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Hakika Hadiyth ya mtu huhifadhiwa kulingana na kiasi cha niya yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
378
Hadiyth
387

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ الْقَاسِمِ، قَالَ: قَالَ لِي عَبْدُ اللَّهِ: "إِنِّي لَأَحْسَبُ الرَّجُلَ يَنْسَى الْعِلْمَ كَانَ يَعْلَمُهُ لِلْخَطِيئَةِ كَانَ يَعْمَلُهَا"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa Al-Qaasim, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) aliniambia: "Hakika mimi nadhani mtu huisahau ilimu aliyokuwa akiijua kwa sababu ya kosa alilokuwa akilitenda."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
378
Hadiyth
388

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبُ بْنُ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ ابْنِ أَبِي حُسَيْنٍ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، قَالَ: بَلَغَنِي أَنَّ لُقْمَانَ الْحَكِيمَ كَانَ يَقُولُ لِابْنِهِ: "يَا بُنَيَّ، لَا تَعَلَّمْ الْعِلْمَ لِتُبَاهِيَ بِهِ الْعُلَمَاءَ، أَوْ لِتُمَارِيَ بِهِ السُّفَهَاءَ، أَوْ تُرَائِيَ بِهِ فِي الْمَجَالِسِ، وَلَا تَتْرُكْ الْعِلْمَ زُهْدًا فِيهِ وَرَغْبَةً فِي الْجَهَالَةِ، يَا بُنَيَّ، اخْتَرْ الْمَجَالِسَ عَلَى عَيْنِكَ، وَإِذَا رَأَيْتَ قَوْمًا يَذْكُرُونَ اللَّهَ، فَاجْلِسْ مَعَهُمْ، فَإِنَّكَ إِنْ تَكُنْ عَالِمًا يَنْفَعْكَ عِلْمُكَ، وَإِنْ تَكُنْ جَاهِلًا يُعَلِّمُوكَ، وَلَعَلَّ اللَّهَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِمْ بِرَحْمَتِهِ فَيُصِيبَكَ بِهَا مَعَهُمْ، وَإِذَا رَأَيْتَ قَوْمًا لَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ، فَلَا تَجْلِسْ مَعَهُمْ، فَإِنَّكَ إِنْ تَكُنْ عَالِمًا لَا يَنْفَعْكَ عِلْمُكَ، وَإِنْ تَكُنْ جَاهِلًا زَادُوكَ غَيًّا، وَلَعَلَّ اللَّهَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِمْ بِعَذَابٍ فَيُصِيبَكَ مَعَهُمْ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametukhabarisha Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Ibn Abiy Husayn, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, amesema: Imenifikia kwamba Luqmaan Al-Hakiym (mwenye hekima) alikuwa akimwambia mwanawe: "Yaa mwanangu, usijifunze ilimu ili ujifakhirishe kwayo mbele ya 'Ulamaa (Wanazuoni), au ili ubishane kwayo na wapumbavu, au ujionyeshe kwayo katika vikao; wala usiiache ilimu kwa kutoipenda na kupenda ujinga. Yaa mwanangu, chagua vikao kwa jicho lako (kwa uangalifu). Na ukiwaona watu wanamdhukuru Allaah, basi kaa pamoja nao; kwani ukiwa ni 'Aalim (Mwanazuoni), ilimu yako itakunufaisha, na ukiwa ni mjinga, watakufundisha; na huenda Allaah Akawaangalia kwa Rehma Yake, Akakusibu nayo pamoja nao. Na ukiwaona watu hawamdhukuru Allaah, basi usikae pamoja nao; kwani ukiwa ni 'Aalim, ilimu yako haitakunufaisha, na ukiwa ni mjinga, watakuzidishia upotofu; na huenda Allaah Akawaangalia kwa adhabu, Akakusibu pamoja nao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
379
Hadiyth
389

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ سُلَيْمَانَ، حَدَّثَنَا حَرِيزٌ، عَنْ سَلْمَانَ بْنِ سُمَيْرٍ، عَنْ كَثِيرِ بْنِ مُرَّةَ، قَالَ: "لَا تُحَدِّثْ الْبَاطِلَ الْحُكَمَاءَ فَيَمْقُتُوكَ، وَلَا تُحَدِّثْ الْحِكْمَةَ لِلسُّفَهَاءِ فَيُكَذِّبُوكَ، وَلَا تَمْنَعْ الْعِلْمَ أَهْلَهُ فَتَأْثَمَ، وَلَا تَضَعْهُ فِي غَيْرِ أَهْلِهِ فَتُجَهَّلَ، إِنَّ عَلَيْكَ فِي عِلْمِكَ حَقًّا كَمَا أَنَّ عَلَيْكَ فِي مَالِكَ حَقًّا"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametusimulia Is-haaq bin Sulaymaan, ametusimulia Hariyz, kutoka kwa Salmaan bin Sumayr, kutoka kwa Kathiyr bin Murrah, amesema: "Usiwasimulie wenye hekima batili, wakakuchukia; wala usiwasimulie wapumbavu hekima, wakakukadhibisha; wala usiizuie ilimu kwa wanaostahiki, ukapata dhambi; wala usiiweke kwa wasiostahiki, ukahesabiwa mjinga. Hakika juu yako katika ilimu yako kuna haki, kama ambavyo juu yako katika mali yako kuna haki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
380
Hadiyth
390

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي مُعَاوِيَةُ، أَنَّ أَبَا فَرْوَةَ حَدَّثَهُ، أَنَّ عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ عَلَيْهِ السَّلامُ، كَانَ يَقُولُ: "لَا تَمْنَعْ الْعِلْمَ مِنْ أَهْلِهِ فَتَأْثَمَ، وَلَا تَنْشُرْهُ عِنْدَ غَيْرِ أَهْلِهِ فَتُجَهَّلَ، وَكُنْ طَبِيبًا رَفِيقًا يَضَعُ دَوَاءَهُ حَيْثُ يَعْلَمُ أَنَّهُ يَنْفَعُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Mu'aawiyah, kwamba Abuw Farwah alimsimulia kwamba 'Iysaa bin Maryam (عليه السلام) alikuwa akisema: "Usiizuie ilimu kwa wanaostahiki, ukapata dhambi; wala usiieneze kwa wasiostahiki, ukahesabiwa mjinga. Na kuwa tabibu mpole, anayeweka dawa yake pale anapojua kwamba itanufaisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
380
Hadiyth
391

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا مَهْدِيٌّ، عَنْ غَيْلَانَ، عَنْ مُطَرِّفٍ، قَالَ: "لَا تُطْعِمْ طَعَامَكَ مَنْ لَا يَشْتَهِيهِ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Mahdiyy, kutoka kwa Ghaylaan, kutoka kwa Mutwarrif, amesema: "Usimlishe chakula chako asiyekitamani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
380
Hadiyth
392

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ شَابُورَ، سَمِعَ شَهْرَ بْنَ حَوْشَبٍ، يَقُولُ: قَالَ لُقْمَانُ لِابْنِهِ: "يَا بُنَيَّ، لَا تَعَلَّمْ الْعِلْمَ لِتُبَاهِيَ بِهِ الْعُلَمَاءَ، وَتُمَارِيَ بِهِ السُّفَهَاءَ، وَتُرَائِيَ بِهِ فِي الْمَجَالِسِ، وَلَا تَتْرُكْ الْعِلْمَ زَهَادَةً فِيهِ، وَرَغْبَةً فِي الْجَهَالَةِ، وَإِذَا رَأَيْتَ قَوْمًا يَذْكُرُونَ اللَّهَ، فَاجْلِسْ مَعَهُمْ، إِنْ تَكُ عَالِمًا يَنْفَعْكَ عِلْمُكَ، وَإِنْ تَكُ جَاهِلًا عَلَّمُوكَ، وَلَعَلَّ اللَّهَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِمْ بِرَحْمَتِهِ فَيُصِيبَكَ بِهَا مَعَهُمْ، وَإِذَا رَأَيْتَ قَوْمًا لَا يَذْكُرُونَ اللَّهَ فَلَا تَجْلِسْ مَعَهُمْ، إِنْ تَكُ عَالِمًا لَمْ يَنْفَعْكَ عِلْمُكَ، وَإِنْ تَكُ جَاهِلًا زَادُوكَ غَيًّا أَوْ عِيًّا وَلَعَلَّ اللَّهَ أَنْ يَطَّلِعَ عَلَيْهِمْ بِسَخَطٍ فَيُصِيبَكَ بِهِ مَعَهُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Daawuwd bin Shaabuwr, (kwamba) alimsikia Shahr bin Hawshab akisema: Luqmaan alimwambia mwanawe: "Yaa mwanangu, usijifunze ilimu ili ujifakhirishe kwayo mbele ya 'Ulamaa (Wanazuoni), na ubishane kwayo na wapumbavu, na ujionyeshe kwayo katika vikao; wala usiiache ilimu kwa kutoipenda na kupenda ujinga. Na ukiwaona watu wanamdhukuru Allaah, basi kaa pamoja nao: ukiwa ni 'Aalim (Mwanazuoni), ilimu yako itakunufaisha, na ukiwa ni mjinga, watakufundisha; na huenda Allaah Akawaangalia kwa Rehma Yake, Akakusibu nayo pamoja nao. Na ukiwaona watu hawamdhukuru Allaah, basi usikae pamoja nao: ukiwa ni 'Aalim, ilimu yako haitakunufaisha, na ukiwa ni mjinga, watakuzidishia upotofu — au: kushindwa (kujieleza) —; na huenda Allaah Akawaangalia kwa Machukizo, Akakusibu nayo pamoja nao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
381
Hadiyth
393

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ بِشْرٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ ثُوَيْرٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ جَعْدَةَ، عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "يَا حَمَلَةَ الْعِلْمِ، اعْمَلُوا بِهِ، فَإِنَّمَا الْعَالِمُ مَنْ عَمِلَ بِمَا عَلِمَ وَوَافَقَ عِلْمُهُ عَمَلَهُ، وَسَيَكُونُ أَقْوَامٌ يَحْمِلُونَ الْعِلْمَ لَا يُجَاوِزُ تَرَاقِيَهُمْ، يُخَالِفُ عَمَلُهُمْ عِلْمَهُمْ، وَتُخَالِفُ سَرِيرَتُهُمْ عَلَانِيَتَهُمْ، يَجْلِسُونَ حِلَقًا فَيُبَاهِيَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا، حَتَّى إِنَّ الرَّجُلَ لَيَغْضَبُ عَلَى جَلِيسِهِ أَنْ يَجْلِسَ إِلَى غَيْرِهِ وَيَدَعَهُ، أُولَئِكَ لَا تَصْعَدُ أَعْمَالُهُمْ فِي مَجَالِسِهِمْ تِلْكَ إِلَى اللَّهِ تعَالَيَ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Bishr, amesema: Amenisimulia baba yangu, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Thuwayr, kutoka kwa Yahyaa bin Ja'dah, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Enyi wabebaji wa ilimu! Itendeeni kazi; kwani hakika 'Aalim (Mwanazuoni) ni yule aliyetenda kwa aliyoyajua, na ilimu yake ikaafikiana na amali yake. Na watakuja watu wanaobeba ilimu, (ambayo) haivuki mitulinga (ya koo) yao; amali zao zinapingana na ilimu yao, na siri zao zinapingana na dhahiri yao; wanakaa katika duara, wakijifakhirisha wao kwa wao, hata mtu humkasirikia mwenzake wa kikao kwa kuketi kwa mwingine na kumwacha. Hao amali zao hazipandi kwa Allaah (تعالى) katika vikao vyao hivyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
382
Hadiyth
394

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ: "كَفَى بِالْمَرْءِ عِلْمًا أَنْ يَخْشَى اللَّهَ، وَكَفَى بِالْمَرْءِ جَهْلًا أَنْ يُعْجَبَ بِعِلْمِهِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Masruwq, amesema: "Inatosha kuwa ni ilimu kwa mtu kumkhofu Allaah, na inatosha kuwa ni ujinga kwa mtu kujiona kwa sababu ya ilimu yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
383
Hadiyth
395

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُجَيْرٍ، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ قُرَّةَ، قَالَ: "لَوْ أَنَّ أَدْنَى هَذِهِ الْأُمَّةِ عِلْمًا أَخَذَتْ أُمَّةٌ مِنْ الْأُمَمِ بِعِلْمِهِ، لَرَشَدَتْ تِلْكَ الْأُمَّةُ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Bujayr, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Qurrah, amesema: "Lau mtu wa chini kabisa kwa ilimu katika Ummah huu, Ummah miongoni mwa Ummah (zingine) ungeichukua ilimu yake, basi Ummah huo ungeongoka."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
383
Hadiyth
396

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "إِنْ كَانَ الرَّجُلُ لَيُصِيبُ الْبَابَ مِنْ الْعِلْمِ فَيَعْمَلُ بِهِ، فَيَكُونُ خَيْرًا لَهُ مِنْ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا، لَوْ كَانَتْ لَهُ فَجَعَلَهَا فِي الْآخِرَةِ"،

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Hakika mtu alikuwa akipata mlango wa ilimu akautendea kazi, ukawa bora kwake kuliko dunia na vilivyomo, lau angekuwa nayo akaifanya (yote) kwa ajili ya Aakhirah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
383
Hadiyth
397

قَالَ: قَالَ الْحَسَنُ: "كَانَ الرَّجُلُ إِذَا طَلَبَ الْعِلْمَ لَمْ يَلْبَثْ أَنْ يُرَى ذَلِكَ فِي بَصَرِهِ، وَتَخَشُّعِهِ، وَلِسَانِهِ، وَيَدِهِ، وَصِلاتِهِ، وَزُهْدِهِ"،

Amesema: Al-Hasan amesema: "Mtu alikuwa anapotafuta ilimu, haukupita muda ila (athari ya) hilo huonekana katika macho yake, na unyenyekevu wake, na ulimi wake, na mkono wake, na mawasiliano yake mema (na watu), na kuipa kwake dunia mgongo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
383
Hadiyth
398

قَالَ: وقَالَ مُحَمَّدٌ: "انْظُرُوا عَمَّنْ تَأْخُذُونَ هَذَا الْحَدِيثَ، فَإِنَّمَا هُوَ دِينُكُمْ"

Amesema: Na Muhammad [bin Siyriyn] amesema: "Angalieni ni kutoka kwa nani mnaichukua Hadiyth hii, kwani hakika hiyo ni Dini yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
384
Hadiyth
399

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ، يَقُولُ: "مَا ازْدَادَ عَبْدٌ عِلْمًا، فَازْدَادَ فِي الدُّنْيَا رَغْبَةً، إِلَّا ازْدَادَ مِنْ اللَّهِ بُعْدًا"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, amesema: Nilimsikia Sufyaan akisema: "Mja hakuzidi ilimu, kisha akazidi shauku katika dunia, ila alizidi kuwa mbali na Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
384
Hadiyth
400

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ حَسَّانَ، قَالَ: "مَا ازْدَادَ عَبْدٌ بِاللَّهِ عِلْمًا، إِلَّا ازْدَادَ النَّاسُ مِنْهُ قُرْبًا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ"،

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Hassaan, amesema: "Mja hakuzidi ilimu ya (kumjua) Allaah, ila watu walizidi kumkaribia, (ukaribu utokanao) na Rehma ya Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
384
Hadiyth
401

وَقَالَ فِي حَدِيثٍ آخَرَ: "مَا ازْدَادَ عَبْدٌ عِلْمًا، إِلَّا ازْدَادَ قَصْدًا، وَلَا قَلَّدَ اللَّهُ عَبْدًا قِلَادَةً خَيْرًا مِنْ سَكِينَةٍ"

Na akasema katika Hadiyth nyingine: "Mja hakuzidi ilimu ila alizidi kuwa na wastani (katika mambo yake); wala Allaah Hakumvisha mja kidani bora kuliko utulivu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
384
Hadiyth
402

أَخْبَرَنَا الْقَاسِمُ بْنُ كَثِيرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ شُرَيْحٍ يُحَدِّثُ، عَنْ عَمِيرَةَ أَنَّهُ سَمِعَهُ، يَقُولُ: إِنَّ رَجُلًا قَالَ لِابْنِهِ: "اذْهَبْ فَاطْلُبْ الْعِلْمَ، فَخَرَجَ فَغَابَ عَنْهُ مَا غَابَ، ثُمَّ جَاءَ فَحَدَّثَهُ بِأَحَادِيثَ، فَقَالَ لَهُ أَبُوهُ: يَا بُنَيَّ، اذْهَبْ فَاطْلُبْ الْعِلْمَ، فَغَابَ عَنْهُ أَيْضًا زَمَانًا، ثُمَّ جَاءَ بِقَرَاطِيسَ فِيهَا مِنْ كُتُبٍ، فَقَرَأَهَا عَلَيْهِ، فَقَالَ لَهُ: هَذَا سَوَادٌ فِي بَيَاضٍ، فَاذْهَبْ فَاطْلُبْ الْعِلْمَ، فَخَرَجَ فَغَابَ عَنْهُ مَا غَابَ، ثُمَّ جَاءَ، فَقَالَ لِأَبِيهِ: سَلْنِي عَمَّا بَدَا لَكَ، فَقَالَ لَهُ أَبُوهُ: أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّكَ مَرَرْتَ بِرَجُلٍ يَمْدَحُكَ، وَمَرَرْتَ بِآخَرَ يَعِيبُكَ؟، قَالَ: إِذًا لَمْ أَلُمْ الَّذِي يَعِيبُنِي، وَلَمْ أَحْمَدْ الَّذِي يَمْدَحُنِي، فَقَالَ: أَرَأَيْتَ لَوْ مَرَرْتَ بِصَفِيحَةٍ؟، قَالَ أَبُو شُرَيْحٍ: لَا أَدْرِي أَمِنْ ذَهَبٍ أَوْ وَرِقٍ، فَقَالَ: إِذًا لَمْ أُهَيِّجْهَا وَلَمْ أَقْرَبْهَا، فَقَالَ: اذْهَبْ فَقَدْ عَلِمْتَ"

Ametukhabarisha Al-Qaasim bin Kathiyr, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Shurayh akisimulia kutoka kwa 'Amiyrah, kwamba alimsikia akisema: Hakika mtu mmoja alimwambia mwanawe: "Nenda ukatafute ilimu. Akatoka, akawa mbali naye muda aliokuwa mbali, kisha akaja, akamsimulia Hadiyth (kadhaa). Baba yake akamwambia: Yaa mwanangu, nenda ukatafute ilimu. Akawa mbali naye pia kwa muda, kisha akaja na karatasi zenye maandishi fulani, akamsomea. Akamwambia: Huu ni weusi juu ya weupe; basi nenda ukatafute ilimu. Akatoka, akawa mbali naye muda aliokuwa mbali, kisha akaja, akamwambia baba yake: Niulize unalotaka. Baba yake akamwambia: Waonaje lau ungempita mtu anayekusifu, na ukampita mwingine anayekuaibisha? Akasema: Basi nisingemlaumu anayeniaibisha, wala nisingemsifu anayenisifu. Akasema: Waonaje lau ungepita kwenye bamba (la madini)?" Abuw Shurayh amesema: Sijui (kama alisema) la dhahabu au la fedha. "Akasema: Basi nisingelitikisa wala nisingelikaribia. Akasema: Nenda, kwani umekwisha kujua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
385
Hadiyth
402

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ السَّكَنِ بْنِ عُمَيْرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ وَهْبَ بْنَ مُنَبِّهٍ، يَقُولُ: "يَا بُنَيَّ، عَلَيْكَ بِالْحِكْمَةِ، فَإِنَّ الْخَيْرَ فِي الْحِكْمَةِ كُلَّهُ، وَتُشَرِّفُ الصَّغِيرَ عَلَى الْكَبِيرِ، وَالْعَبْدَ عَلَى الْحُرِّ، وَتُزِيدُ السَّيِّدَ سُؤْدُدًا، وَتُجْلِسُ الْفَقِيرَ مَجَالِسَ الْمُلُوكِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Baqiyyah, kutoka kwa As-Sakan bin 'Umayr, amesema: Nilimsikia Wahb bin Munabbih akisema: "Yaa mwanangu, shikamana na hekima, kwani kheri yote imo katika hekima; nayo humtukuza mdogo juu ya mkubwa, na mtumwa juu ya muungwana, na humzidishia bwana utukufu, na humketisha fakiri katika vikao vya wafalme."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
386
Hadiyth
403

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، قَالَ: أَخْبَرَنِي بَقِيَّةُ، سَمِعْتُ عُتْبَةَ بْنَ أَبِي حَكِيمٍ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "وَمَا نَحْنُ لَوْلَا كَلِمَاتُ الْعُلَمَاءِ؟"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, amesema: Amenikhabarisha Baqiyyah: Nilimsikia 'Utbah bin Abiy Hakiym, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: "Na sisi tungekuwa nini lau si maneno ya 'Ulamaa (Wanazuoni)?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
386
Hadiyth
404

35-Mlangoباب اجتناب أهل الأهواء، والبدع، والخصومةMlango Wa Kujiepusha
Na Watu Wa Matamanio, Na Uzushi, Na Mabishano

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، قَالَ: قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: "لَا تُجَالِسُوا أَهْلَ الْأَهْوَاءِ وَلَا تُجَادِلُوهُمْ، فَإِنِّي لَا آمَنُ أَنْ يَغْمِسُوكُمْ فِي ضَلَالَتِهِمْ، أَوْ يَلْبِسُوا عَلَيْكُمْ مَا كُنْتُمْ تَعْرِفُونَ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, amesema: Abuw Qilaabah amesema: "Msikae pamoja na watu wa matamanio, wala msibishane nao; kwani mimi sina amani kwamba hawatakuzamisheni katika upotofu wao, au hawatakutatanishieni yale mliyokuwa mkiyajua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
405

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، قَالَ: رَآنِي سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ جَلَسْتُ إِلَى طَلْقِ بْنِ حَبِيبٍ، فَقَالَ لِي: "أَلَمْ أَرَكَ جَلَسْتَ إِلَى طَلْقِ بْنِ حَبِيبٍ؟ لَا تُجَالِسَنَّهُ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, amesema: Sa'iyd bin Jubayr aliniona nimekaa kwa Twalq bin Habiyb, akaniambia: "Je, sikukuona umekaa kwa Twalq bin Habiyb? Usikae naye kabisa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
406

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، أَنْبَأَنَا حَيْوَةُ بْنُ شُرَيْحٍ، حَدَّثَنِي أَبُو صَخْرٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ جَاءَهُ رَجُلٌ فَقَالَ: إِنَّ فُلَانًا يَقْرَأُ عَلَيْكَ السَّلَامَ، قَالَ: "بَلَغَنِي أَنَّهُ قَدْ أَحْدَثَ، فَإِنْ كَانَ قَدْ أَحْدَثَ، فَلَا تَقْرَأْ عَلَيْهِ السَّلَامَ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, ametupa khabari Haywah bin Shurayh, amenisimulia Abuw Swakhr, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba mtu mmoja alimjia akasema: Hakika fulani anakusomea salaam. Akasema: "Imenifikia (khabari) kwamba yeye amezusha (jambo katika Dini). Basi ikiwa amezusha, usimsomee salaam (kutoka kwangu)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
407

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَغْرَاءَ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، قَالَ: "كَانَ إِبْرَاهِيمُ لَا يَرَى غِيبَةً لِلْمُبْتَدِعِ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Maghraa, ametusimulia Al-A'mash, amesema: "Ibraahiym alikuwa haoni kuwa (kumsema) mzushi (katika Dini) ni usengenyaji."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
408

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ ابْنِ شُبْرُمَةَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "إِنَّمَا سُمِّيَ الْهَوَى لِأَنَّهُ يَهْوِي بِصَاحِبِهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Ibn Shubrumah, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Hakika hawaa (matamanio ya nafsi) imeitwa (hivyo) kwa sababu inamporomosha mwenye nayo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
409

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ وَاسِعٍ، قَالَ: كَانَ مُسْلِمُ بْنُ يَسَارٍ، يَقُولُ: "إِيَّاكُمْ وَالْمِرَاءَ، فَإِنَّهَا سَاعَةُ جَهْلِ الْعَالِمِ، وَبِهَا يَبْتَغِي الشَّيْطَانُ زَلَّتَهُ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Muhammad bin Waasi', amesema: Muslim bin Yasaar alikuwa akisema: "Tahadharini na mabishano, kwani hiyo ni saa ya ujinga wa 'Aalim (Mwanazuoni), na kupitia hayo shaytwaan hutafuta kuteleza kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
387
Hadiyth
410

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ أَسْمَاءَ بْنِ عُبَيْدٍ، قَالَ: دَخَلَ رَجُلَانِ مِنْ أَصْحَابِ الْأَهْوَاءِ عَلَى ابْنِ سِيرِينَ، فَقَالَا: يَا أَبَا بَكْرٍ، نُحَدِّثُكَ بِحَدِيثٍ؟، قَالَ: لَا، قَالَا: فَنَقْرَأُ عَلَيْكَ آيَةً مِنْ كِتَابِ اللَّهِ؟، قَالَ: لَا، لِتَقُومَانِ عَنِّي أَوْ لَأَقُومَنَّ، قَالَ: فَخَرَجَا، فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ: يَا أَبَا بَكْرٍ، وَمَا كَانَ عَلَيْكَ أَنْ يَقْرَآ عَلَيْكَ آيَةً مِنْ كِتَابِ اللَّهِ تعَالَى قَالَ: "إِنِّي خَشِيتُ أَنْ يَقْرَآ عَلَيَّ آيَةً فَيُحَرِّفَانِهَا، فَيَقِرُّ ذَلِكَ فِي قَلْبِي"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Asmaa bin 'Ubayd, amesema: Watu wawili miongoni mwa watu wa matamanio waliingia kwa Ibn Siyriyn, wakasema: Yaa Abaa Bakr, tukusimulie Hadiyth? Akasema: "Hapana." Wakasema: Basi tukusomee Aayah kutoka katika Kitabu cha Allaah? Akasema: "Hapana. Ama mtaondoka kwangu, au nitaondoka mimi." Akasema (Asmaa): Wakatoka. Baadhi ya watu wakasema: Yaa Abaa Bakr, kungekuwa na ubaya gani kwako lau wangekusomea Aayah kutoka katika Kitabu cha Allaah (تعالى)? Akasema: "Hakika mimi niliogopa wasije wakanisomea Aayah, wakaipotosha, na hilo likatulia moyoni mwangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
389
Hadiyth
411

أَخْبَرَنَا سَعِيدٌ، عَنْ سَلَّامِ بْنِ أَبِي مُطِيعٍ، أَنَّ رَجُلًا مِنْ أَهْلِ الْأَهْوَاءِ، قَالَ لِأَيُّوبَ: يَا أَبَا بَكْرٍ، أَسْأَلُكَ عَنْ كَلِمَةٍ؟، قَالَ: "فَوَلَّى وَهُوَ يُشِيرُ بِأُصْبُعِهِ وَلَا نِصْفَ كَلِمَةٍ"، وَأَشَارَ لَنَا سَعِيدٌ بِخِنْصِرِهِ الْيُمْنَى

Ametukhabarisha Sa'iyd, kutoka kwa Sallaam bin Abiy Mutwiy', kwamba mtu mmoja miongoni mwa watu wa matamanio alimwambia Ayyuwb: Yaa Abaa Bakr, nikuulize kuhusu neno moja? Akasema (Sallaam): "Akageuka (akaondoka), huku akiashiria kwa kidole chake: Wala nusu ya neno!" Na Sa'iyd akatuashiria kwa kidole chake kidogo cha (mkono wa) kulia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
390
Hadiyth
412

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ كُلْثُومِ بْنِ جَبْرٍ، أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ عَنْ شَيْءٍ، فَلَمْ يُجِبْهُ، فَقِيلَ لَهُ، فَقَالَ: "أَزِيشَانْ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Kulthuwm bin Jabr, kwamba mtu mmoja alimuuliza Sa'iyd bin Jubayr kuhusu jambo fulani, hakumjibu. Akaambiwa (kuhusu hilo), akasema: "Aziyshaan (neno la Kifursi: ni miongoni mwao)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
390
Hadiyth
413

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا فُضَيْلٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ أَبِي جَعْفَرٍ مُحَمَّدِ بْنِ عَلِيٍّ، قَالَ: "لَا تُجَالِسُوا أَصْحَابَ الْخُصُومَاتِ، فَإِنَّهُمْ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِ اللَّهِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Fudhwayl, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Abuw Ja'far Muhammad bin 'Aliy, amesema: "Msikae pamoja na watu wa mabishano, kwani wao ndio wale wanaoshughulika kuzisakama Aayaat za Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
390
Hadiyth
414

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، وَابْنِ سِيرِينَ، أنهما قَالَا: "لَا تُجَالِسُوا أَصْحَابَ الْأَهْوَاءِ، وَلَا تُجَادِلُوهُمْ، وَلَا تَسْمَعُوا مِنْهُمْ"

Ametukhabarisha Ahmad, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan na Ibn Siyriyn, kwamba wao wawili walisema: "Msikae pamoja na watu wa matamanio, wala msibishane nao, wala msisikilize kutoka kwao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
390
Hadiyth
415

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ أُمَيٍّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "إِنَّمَا سُمُّوا أَصْحَابَ الْأَهْوَاءِ، لِأَنَّهُمْ يَهْوُونَ فِي النَّارِ"

Ametukhabarisha Ahmad, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Umayy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Hakika wameitwa watu wa hawaa (matamanio ya nafsi) kwa sababu wao wanaporomoka motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
390
Hadiyth
416

36-Mlangoباب التسوية في العلمMlango Wa Kuwaweka [Watu] Sawa Katika Ilimu

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ مَيْسَرَةَ، قَالَ: "مَا رَأَيْتُ أَحَدًا مِنْ النَّاسِ الشَّرِيفُ وَالْوَضِيعُ عِنْدَهُ سَوَاءٌ غَيْرَ طَاوُسٍ وَهُوَ يَحْلِفُ عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Maysarah, amesema: "Sijapata kumuona yeyote miongoni mwa watu ambaye mtukufu na duni ni sawa kwake, isipokuwa Twaawuws" — naye akiapia hilo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
392
Hadiyth
417

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "كُنَّا نَكْرَهُ كِتَابَةَ الْعِلْمِ حَتَّى أَكْرَهَنَا عَلَيْهِ السُّلْطَانُ فَكَرِهْنَا أَنْ نَمْنَعَهُ أَحَدًا"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Tulikuwa tukichukia kuandika ilimu, mpaka mtawala alipotulazimisha (kuiandika); basi tukachukia kumzuilia yeyote (asiipate)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
392
Hadiyth
418

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ مُعَاذٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، قَالَ: كَلَّمُوا مُحَمَّدًا فِي رَجُلٍ يَعْنِي: يُحَدِّثُهُ فَقَالَ: "لَوْ كَانَ رَجُلًا مِنْ الزِّنْجِ، لَكَانَ عِنْدِي، وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ فِي هَذَا سَوَاءً"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametusimulia Mu'aadh bin Mu'aadh, ametusimulia Ibn 'Awn, amesema: Walimsemesha Muhammad [bin Siyriyn] kuhusu mtu mmoja — yaani: amsimulie (Hadiyth) — akasema: "Lau angekuwa mtu miongoni mwa Zanj (watu weusi wa pwani ya Afrika ya Mashariki), basi kwangu yeye na 'Abdu-Allaah bin Muhammad wangekuwa sawa katika hili."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
392
Hadiyth
419

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ الصَّلْتِ بْنِ رَاشِدٍ، قَالَ: سَأَلَ سَلْمُ بْنُ قُتَيْبَةَ طَاوُوسًا عَنْ مَسْأَلَةٍ فَلَمْ يُجِبْهُ، فَقِيلَ لَهُ: هَذَا سَلْمُ بْنُ قُتَيْبَةَ، قَالَ: "ذَلِكَ أَهْوَنُ لَهُ عَلَيَّ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, kutoka kwa Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Asw-Swalt bin Raashid, amesema: Salm bin Qutaybah alimuuliza Twaawuws kuhusu suala fulani, hakumjibu. Akaambiwa: Huyu ni Salm bin Qutaybah! Akasema: "Hilo linamfanya kuwa duni zaidi kwangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
392
Hadiyth
420

37-Mlangoباب في توقير العلماءMlango Wa Kuhusu Kuwaheshimu 'Ulamaa (Wanazuoni)

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ بَقِيَّةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي حَبِيبُ بْنُ صَالِحٍ، قَالَ: "مَا خِفْتُ أَحَدًا مِنْ النَّاسِ مَخَافَتِي خَالِدِ بْنِ مَعْدَانَ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Is-haaq, kutoka kwa Baqiyyah, amesema: Amenisimulia Habiyb bin Swaalih, amesema: "Sijapata kumwogopa yeyote miongoni mwa watu kama nilivyomwogopa Khaalid bin Ma'daan."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
421

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مُغِيرَةَ، قَالَ: "كُنَّا نَهَابُ إِبْرَاهِيمَ هَيْبَةَ الْأَمِيرِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Mughiyrah, amesema: "Tulikuwa tukimwonea Ibraahiym haiba kama haiba ya Amiri (kiongozi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
422

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، قَالَ: حَدَّثَ سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ يَوْمًا بِحَدِيثٍ فَقُمْتُ إِلَيْهِ فَاسْتَعَدْتُهُ، فَقَالَ: "مَا كُلَّ سَاعَةٍ أَحْلُبُ فَأُشْرَبُ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, amesema: Sa'iyd bin Jubayr alisimulia siku moja Hadiyth fulani; nikasimama nikamwendea, nikamwomba aniirudie. Akasema: "Si kila saa ninakamua (maziwa) nikanywa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
423

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا هَارُونُ هُوَ ابْنُ الْمُغِيرَةِ، وَيَحْيَى بْنُ ضُرَيْسٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ عَطَاءٍ "أَنَّ أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ كَرِهَ الْحَدِيثَ فِي الطَّرِيقِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Haaruwn — naye ni Ibn Al-Mughiyrah — na Yahyaa bin Dhwurays, kutoka kwa 'Amr bin Abiy Qays, kutoka kwa 'Atwaa: "Kwamba Abuw 'Abdir-Rahmaan alichukia (kusimulia) Hadiyth njiani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
424

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ ضُرَيْسٍ، حَدَّثَنَا أَبُو سِنَانٍ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ أَبِي ثَابِتٍ، قَالَ: كُنَّا عِنْدَ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ فَحَدَّثَ بِحَدِيثٍ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: مَنْ حَدَّثَكَ هَذَا أَوْ مِمَّنْ سَمِعْتَ هَذَا؟ "فَغَضِبَ وَمَنَعَنَا حَدِيثَهُ حَتَّى قَامَ؟"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Yahyaa bin Dhwurays, ametusimulia Abuw Sinaan, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, amesema: Tulikuwa kwa Sa'iyd bin Jubayr, akasimulia Hadiyth fulani. Mtu mmoja akamwambia: Nani amekusimulia hii? — au: Umeisikia hii kutoka kwa nani? — "Akakasirika, na akatunyima Hadiyth zake mpaka akasimama (akaondoka)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
425

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: "لَوْ رَفَقْتُ بِابْنِ عَبَّاسٍ لَأَصَبْتُ مِنْهُ عِلْمًا كَثِيرًا"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Salamah, amesema: "Lau ningemfanyia upole Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), ningepata kutoka kwake ilimu nyingi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
426

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ أُمِّ عَبْدِ اللَّهِ بِنْتِ خَالِدٍ، قَالَتْ: "مَا رَأَيْتُ أَحَدًا أَكْرَمَ لِلْعِلْمِ مِنْ أَبِي"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Baqiyyah, kutoka kwa Ummu 'Abdi-Allaah bint Khaalid, amesema: "Sijapata kumuona yeyote anayeiheshimu ilimu zaidi kuliko baba yangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
393
Hadiyth
427

38-Mlangoباب في الحديث عن الثقاتMlango Wa Kuhusu Kusimulia Hadiyth
Kutoka Kwa Wapokezi Waaminifu

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ عِيسَى بْنِ يُونُسَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى، قَالَ: قُلْتُ لِطَاوُسٍ: إِنَّ فُلَانًا حَدَّثَنِي بِكَذَا وَكَذَا، قَالَ: "إِنْ كَانَ صَاحِبُكَ مَلِيًّا، فَخُذْ عَنْهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, kutoka kwa 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa, amesema: Nilimwambia Twaawuws: Hakika fulani amenisimulia kadhaa wa kadhaa. Akasema: "Ikiwa sahibu yako ni mwaminifu (anayetegemewa), basi chukua kutoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
395
Hadiyth
428

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مِسْعَرٍ، قَالَ: قَالَ سَعْدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ: "لَا يُحَدِّثْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا الثِّقَاتُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Mis'ar, amesema: Sa'd bin Ibraahiym amesema: "Asisimulie kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa wapokezi waaminifu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
395
Hadiyth
429

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "كَانُوا لَا يَسْأَلُونَ عَنْ الْإِسْنَادِ، ثُمَّ سَأَلُوا بَعْدُ لِيَعْرِفُوا مَنْ كَانَ صَاحِبَ سُنَّةٍ أَخَذُوا عَنْهُ، وَمَنْ لَمْ يَكُنْ صَاحِبَ سُنَّةٍ، لَمْ يَأْخُذُوا عَنْهُ"، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: مَا أَظُنُّهُ سَمِعَهُ مِنْ عَاصِمٍ

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Walikuwa hawaulizi kuhusu Isnaad (mlolongo wa wapokezi); kisha baadaye wakawa wanauliza, ili wamjue aliyekuwa mtu wa Sunnah wachukue kutoka kwake, na asiyekuwa mtu wa Sunnah wasichukue kutoka kwake."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Sidhani kuwa aliisikia kutoka kwa 'Aaswim.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
395
Hadiyth
430

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ عَاصِمٍ، قَالَ: قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ سِيرِينَ: "مَا حَدَّثْتَنِي، فَلَا تُحَدِّثْنِي عَنْ رَجُلَيْنِ، فَإِنَّهُمَا لَا يُبَالِيَانِ عَمَّنْ أَخَذَا حَدِيثَهُمَا"، قَالَ أَبُو مُحَمَّد عَبْدُ اللَّهِ: لَا أَظُنُّهُ سَمِعَهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa 'Aaswim, amesema: Muhammad bin Siyriyn amesema: "Chochote utakachonisimulia, basi usinisimulie kutoka kwa watu wawili, kwani wao hawajali wamechukua Hadiyth zao kutoka kwa nani."

Abuw Muhammad 'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Sidhani kuwa aliisikia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
396
Hadiyth
431

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ الْقَعْقَاعِ، قَالَ: قَالَ إِبْرَاهِيمُ: "إِذَا حَدَّثْتَنِي، فَحَدِّثْنِي، عَنْ أَبِي زُرْعَةَ، فَإِنَّهُ حَدَّثَنِي بِحَدِيثٍ ثُمَّ سَأَلْتُهُ بَعْدَ ذَلِكَ بِسَنَةٍ فَمَا خَرَمَ مِنْهَا حَرْفًا"

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa 'Umaarah bin Al-Qa'qaa', amesema: Ibraahiym amesema: "Ukinisimulia, basi nisimulie kutoka kwa Abuw Zur'ah, kwani yeye alinisimulia Hadiyth fulani, kisha nikamuuliza (kuhusu hiyo) mwaka mmoja baada ya hapo, hakupunguza humo hata herufi moja."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
432

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: "إِنَّ هَذَا الْعِلْمَ دِينٌ فَلْيَنْظُرْ الرَّجُلُ عَمَّنْ يَأْخُذُ دِينَهُ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn], amesema: "Hakika ilimu hii ni Dini, basi mtu na atazame anachukua Dini yake kutoka kwa nani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
433

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "كَانُوا إِذَا أَتَوْا الرَّجُلَ لِيَأْخُذُوا عَنْهُ، نَظَرُوا إِلَى صَلَاتِهِ، وَإِلَى سَمْتِهِ، وَإِلَى هَيْئَتِهِ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Hushaym, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Walikuwa wanapomwendea mtu ili wachukue (ilimu) kutoka kwake, huitazama Swalaah yake, na mwenendo wake, na muonekano wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
434

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ زُرَارَةَ، أَنْبَأَنَا هُشَيْمٌ، أَنْبَأَنَا مُغِيرَةُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "كَانُوا إِذَا أَتَوْا الرَّجُلَ يَأْخُذُونَ عَنْهُ الْعِلْمَ، نَظَرُوا إِلَى صَلَاتِهِ، وَإِلَى سَمْتِهِ، وَإِلَى هَيْئَتِهِ، ثُمَّ يَأْخُذُونَ عَنْهُ"،

Ametukhabarisha 'Amr bin Zuraarah, ametupa khabari Hushaym, ametupa khabari Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Walikuwa wanapomwendea mtu wakichukua ilimu kutoka kwake, huitazama Swalaah yake, na mwenendo wake, na muonekano wake; kisha (ndipo) huchukua kutoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
435

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ رَوْحٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، نَحْوَ حَدِيثِ إِبْرَاهِيمَ

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Rawh, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan, mfano wa Hadiyth ya Ibraahiym.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
436

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي جَعْفَرٍ الرَّازِيُّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الرَّبِيعِ، عَنْ أَبِي الْعَالِيَةِ، قَالَ: "كُنَّا نَأْتِي الرَّجُلَ لِنَأْخُذَ عَنْهُ، فَنَنْظُرُ إِذَا صَلَّى، فَإِنْ أَحْسَنَهَا، جَلَسْنَا إِلَيْهِ وَقُلْنَا: هُوَ لِغَيْرِهَا أَحْسَنُ، وَإِنْ أَسَاءَهَا، قُمْنَا عَنْهُ وَقُلْنَا: هُوَ لِغَيْرِهَا أَسْوَأُ"، قَالَ أَبُو مَعْمَرٍ: لَفْظُهُ نَحْوُ هَذَا

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, ametupa khabari 'Abdu-Allaah bin Abiy Ja'far Ar-Raaziy, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ar-Rabiy', kutoka kwa Abul-'Aaliyah, amesema: "Tulikuwa tukimwendea mtu ili tuchukue (ilimu) kutoka kwake; basi tunatazama anaposwali: akiiswali vizuri, tunakaa kwake na tunasema: Yeye kwa (amali) nyinginezo ni mzuri zaidi. Na akiiswali vibaya, tunaondoka kwake na tunasema: Yeye kwa nyinginezo ni mbaya zaidi." Abuw Ma'mar amesema: Tamshi lake ni mfano wa haya.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
397
Hadiyth
437

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، قَالَ: لَا أَدْرِي سَمِعْتُهُ مِنْهُ، أَوْ لَابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ "إِنَّ هَذَا الْعِلْمَ دِينٌ، فَانْظُرُوا عَمَّنْ تَأْخُذُونَ دِينَكُمْ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, amesema: Sijui kama niliisikia kutoka kwake au la — Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn]: "Hakika ilimu hii ni Dini, basi tazameni mnachukua Dini yenu kutoka kwa nani."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
398
Hadiyth
438

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى، قَالَ: قُلْتُ لِطَاوُسٍ: إِنَّ فُلَانًا حَدَّثَنِي بِكَذَا وَكَذَا، قَالَ: "فَإِنْ كَانَ صَاحِبُكَ مَلِيًّا، فَخُذْ عَنْهُ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sa'iyd bin 'Abdil-'Aziyz, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa, amesema: Nilimwambia Twaawuws: Hakika fulani amenisimulia kadhaa wa kadhaa. Akasema: "Basi ikiwa sahibu yako ni mwaminifu (anayetegemewa), chukua kutoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
399
Hadiyth
439

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ هِشَامِ بْنِ حُجَيْرٍ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: جَاءَ بُشَيْرُ بْنُ كَعْبٍ إِلَى ابْنِ عَبَّاسٍ فَجَعَلَ يُحَدِّثُهُ، فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: أَعِدْ عَلَيَّ الْحَدِيثَ الْأَوَّلَ، قَالَ لَهُ بُشَيْرٌ: مَا أَدْرِي عَرَفْتَ حَدِيثِي كُلَّهُ وَأَنْكَرْتَ هَذَا، أَوْ عَرَفْتَ هَذَا وَأَنْكَرْتَ حَدِيثِي كُلَّهُ؟، فَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: "إِنَّا كُنَّا نُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذْ لَمْ يَكُنْ يُكْذَبُ عَلَيْهِ، فَلَمَّا رَكِبَ النَّاسُ الصَّعْبَ وَالذَّلُولَ تَرَكْنَا الْحَدِيثَ عَنْهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hishaam bin Hujayr, kutoka kwa Twaawuws, amesema: Bushayr bin Ka'b alikuja kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), akaanza kumsimulia. Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: "Nirudie Hadiyth ya kwanza." Bushayr akamwambia: Sijui, je, umezitambua Hadiyth zangu zote ukaikataa hii, au umeitambua hii ukazikataa Hadiyth zangu zote? Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: "Hakika sisi tulikuwa tukisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) pale ambapo hakuwa akisingiziwa uongo. Watu walipopanda (ngamia) mkaidi na mpole (yaani: walipoanza kusimulia kila kitu bila kuchagua), tuliacha kusimulia kutoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
399
Hadiyth
440

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، قَالَ: حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "كُنَّا نَحْفَظُ الْحَدِيثَ، وَالْحَدِيثُ يُحْفَظُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى رَكِبْتُمْ الصَّعْبَة وَالذَّلُولَ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, amesema: Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Tulikuwa tukihifadhi Hadiyth, na Hadiyth ilikuwa ikihifadhiwa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), mpaka mlipopanda (ngamia) mkaidi na mpole (yaani: mlipoanza kusimulia kila kitu bila kuchagua)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
399
Hadiyth
441

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "يُوشِكُ أَنْ يَظْهَرَ شَيَاطِينُ قَدْ أَوْثَقَهَا سُلَيْمَانُ عَلَيْهِ السَّلامُ يُفَقِّهُونَ النَّاسَ فِي الدِّينِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: "Wanakaribia kudhihiri mashaytwaan ambao Sulaymaan (عليه السلام) aliwafunga, wakiwafahamisha watu Dini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
400
Hadiyth
442

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: "انْظُرُوا عَمَّنْ تَأْخُذُونَ هَذَا الْحَدِيثَ، فَإِنَّهُ دِينُكُمْ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn], amesema: "Tazameni mnachukua Hadiyth hii kutoka kwa nani, kwani hiyo ni Dini yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
400
Hadiyth
443

39-Mlangoباب ما يتقى من تفسير حديث النبي صلى الله عليه وسلم،
وقول غيره عند قوله صلى الله عليه وسلم
Mlango Wa Yanayopasa Kujihadhari Nayo Katika Kufasiri
Hadiyth Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) , Na Kauli Ya Mwingine
Mbele Ya Kauli Yake (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "لِيُتَّقَى مِنْ تَفْسِيرِ حَدِيثِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا يُتَّقَى مِنْ تَفْسِيرِ الْقُرْآنِ"

Ametukhabarisha Muwsaa bin Khaalid, ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa baba yake, amesema: "Na itahadhariwe katika kufasiri Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama inavyotahadhariwa katika kufasiri Qur-aan."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
401
Hadiyth
444

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: "أَمَا تَخَافُونَ أَنْ تُعَذَّبُوا، أَوْ يُخْسَفَ بِكُمْ أَنْ تَقُولُوا: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَالَ فُلَانٌ؟"

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa baba yake, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Je, hamuogopi kuadhibiwa, au kudidimizwa ardhini, kwa kusema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema, na fulani amesema?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
401
Hadiyth
445

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ بِشْرٍ، حَدَّثَنَا الْمُعَافَى، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: كَتَبَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ رَحِمَهُ الله تَعالَيَ: "إِنَّهُ لَا رَأْيَ لِأَحَدٍ فِي كِتَابِ اللَّهِ، وَإِنَّمَا رَأْيُ الْأَئِمَّةِ فِيمَا لَمْ يَنْزِلْ فِيهِ كِتَابٌ، وَلَمْ تَمْضِ بِهِ سُنَّةٌ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَا رَأْيَ لِأَحَدٍ فِي سُنَّةٍ سَنَّهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Bishr, ametusimulia Al-Mu'aafaa, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz (رحمه الله تعالى) aliandika: "Hakika hakuna rai kwa yeyote katika Kitabu cha Allaah. Na hakika rai ya Imaam (viongozi wa Waislamu) ni katika yale ambayo hakikuteremka Kitabu kuhusu hayo, wala haikupita Sunnah kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hayo. Na hakuna rai kwa yeyote katika Sunnah aliyoiweka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
401
Hadiyth
446

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، أَنَّ عُمَرَ بْنَ عَبْدِ الْعَزِيزِ رَحِمَهُ الله خَطَبَ، فَقَالَ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللَّهَ لَمْ يَبْعَثْ بَعْدَ نَبِيِّكُمْ نَبِيًّا، وَلَمْ يُنْزِلْ بَعْدَ هَذَا الْكِتَابِ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْهِ كِتَابًا، فَمَا أَحَلَّ اللَّهُ عَلَى لِسَانِ نَبِيِّهِ فَهُوَ حَلَالٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ، وَمَا حَرَّمَ عَلَى لِسَانِ نَبِيِّهِ فَهُوَ حَرَامٌ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ، أَلَا وَإِنِّي لَسْتُ بِقَاضٍ وَلَكِنِّي مُنَفِّذٌ، وَلَسْتُ بِمُبْتَدِعٍ وَلَكِنِّي مُتَّبِعٌ، وَلَسْتُ بِخَيْرٍ مِنْكُمْ، غَيْرَ أَنِّي أَثْقَلُكُمْ حِمْلًا، أَلَا وَإِنَّهُ لَيْسَ لِأَحَدٍ مِنْ خَلْقِ اللَّهِ أَنْ يُطَاعَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ، أَلَا هَلْ أَسْمَعْتُ؟"

Ametusimulia Muwsaa bin Khaalid, ametusimulia Mu'tamir bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kwamba 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz (رحمه الله) alikhutubu, akasema: "Enyi watu! Hakika Allaah Hakumtuma Nabiy baada ya Nabiy wenu, wala Hakuteremsha Kitabu baada ya Kitabu hiki Alichokiteremsha kwake. Basi Alichokihalalisha Allaah kwa ulimi wa Nabiy Wake, ni halaal mpaka Siku ya Qiyaamah; na Alichokiharamisha kwa ulimi wa Nabiy Wake, ni haraam mpaka Siku ya Qiyaamah. Tanabahini! Hakika mimi si mwamuzi (wa kujitungia hukmu), bali mimi ni mtekelezaji; na mimi si mzushi, bali mimi ni mfuataji; na mimi si bora kuliko nyinyi, isipokuwa mimi ndiye mwenye mzigo mzito zaidi kuliko nyinyi. Tanabahini! Hakika haifai kwa yeyote katika viumbe vya Allaah kutiiwa katika kumuasi Allaah. Tanabahini! Je, nimewasikilizisha?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
401
Hadiyth
447

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ حُجَيْرٍ، قَالَ: كَانَ طَاوُوسٌ يُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ بَعْدَ الْعَصْرِ، فَقَالَ لَهُ ابْنُ عَبَّاسٍ: "اتْرُكْهُمَا قَالَ: إِنَّمَا نُهِيَ عَنْهَا أَنْ تُتَّخَذُ سُلَّمًا، قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: فَإِنَّهُ قَدْ نُهِيَ عَنْ صَلَاةٍ بَعْدَ الْعَصْرِ، فَلَا أَدْرِي أَتُعَذَّبُ عَلَيْهَا أَمْ تُؤْجَرُ، لِأَنَّ اللَّهَ يَقُولُ: {وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلالا مُبِينًا}"، قَالَ سُفْيَانُ: "تُتَّخَذَ سُلَّمًا، يَقُولُ: يُصَلِّي بَعْدَ الْعَصْرِ إِلَى اللَّيْلِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Hishaam bin Hujayr, amesema: Twaawuws alikuwa akiswali Rakaa mbili baada ya Alasiri. Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akamwambia: "Ziache." Akasema: "Hakika imekatazwa (Swalaah hiyo) isije ikafanywa ngazi." Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Hakika imekatazwa Swalaah baada ya Alasiri; basi sijui kama utaadhibiwa kwa ajili yake au utalipwa (thawabu), kwa sababu Allaah Anasema:

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَنْ يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَنْ يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلالا مُبِينًا

Na haiwi kwa Muumini mwanamume wala kwa Muumini mwanamke, Anapohukumu Allaah na Rasuli Wake jambo lolote, iwe wana khiari katika jambo lao. Na anayemuasi Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amepotoka upotofu bayana. [Al-Ahzaab (33:36)]

Sufyaan amesema: "Isije ikafanywa ngazi" — anamaanisha: (mtu) aswali baada ya Alasiri mpaka usiku.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
402
Hadiyth
448

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا ابْنُ نُمَيْرٍ، عَنْ مُجَالِدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِنُسْخَةٍ مِنْ التَّوْرَاةِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذِهِ نُسْخَةٌ مِنْ التَّوْرَاةِ، فَسَكَتَ، فَجَعَلَ يَقْرَأُ وَوَجْهُ رَسُولِ اللَّهِ يَتَغَيَّرُ، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ رَحْمَةُ اللَّهِ عَلَيهِ: ثَكِلَتْكَ الثَّوَاكِلُ، مَا تَرَى بِوَجْهِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَنَظَرَ عُمَرُ إِلَى وَجْهِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ غَضَبِ اللَّهِ وَغَضَبِ رَسُولِهِ، رَضِينَا بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: رَضِينَا بِاللَّهِ رَبًّا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ، لَوْ بَدَا لَكُمْ مُوسَى فَاتَّبَعْتُمُوهُ وَتَرَكْتُمُونِي، لَضَلَلْتُمْ عَنْ سَوَاءِ السَّبِيلِ، وَلَوْ كَانَ حَيًّا وَأَدْرَكَ نُبُوَّتِي لَاتَّبَعَنِي"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Ibn Numayr, kutoka kwa Mujaalid, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه) alimletea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nakala ya Tawraat, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hii ni nakala ya Tawraat. Akanyamaza. ['Umar (رضي الله عنه)] akaanza kuisoma, na uso wa Rasuli wa Allaah ukawa unabadilika. Abuw Bakr (رضي الله عنه) akasema: Wakulilie wanawake wafiwa! Huoni kilichoko usoni mwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? 'Umar (رضي الله عنه) akautazama uso wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Najikinga kwa Allaah kutokana na Ghadhabu ya Allaah na ghadhabu ya Rasuli Wake. Tumeridhika na Allaah kuwa ni Rabb, na Islaam kuwa ni Dini, na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Nabiy. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Tumeridhika na Allaah kuwa ni Rabb, na Islaam kuwa ni Dini, na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni Nabiy." Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Naapa kwa Yule ambaye nafsi ya Muhammad iko Mkononi Mwake! Lau Muwsaa (عليه السلام) angewadhihirikia, mkamfuata na mkaniacha, mngelipotea njia iliyo sawa. Na lau angekuwa hai, na akaudiriki Unabii wangu, angelinifuata."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
403
Hadiyth
449

حَدَّثَنَا قَبِيصَةُ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي رَبَاحٍ شَيْخٌ مِنْ آلِ عُمَرَ، قَالَ: رَأَى سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ رَجُلًا يُصَلِّي بَعْدَ الْعَصْرِ الرَّكْعَتَيْنِ يُكَبِّرُ، فَقَالَ لَهُ: يَا أَبَا مُحَمَّدٍ، أَيُعَذِّبُنِي اللَّهُ عَلَى الصَّلَاةِ؟، قَالَ: "لَا، وَلَكِنْ يُعَذِّبُكَ اللَّهُ بِخِلَافِ السُّنَّةِ"

Ametusimulia Qabiyswah, ametukhabarisha Sufyaan, kutoka kwa Abuw Rabaah — shaykh (mzee) mmoja wa familia ya 'Umar —, amesema: Sa'iyd bin Al-Musayyib alimuona mtu akiswali baada ya Alasiri Rakaa mbili, akimtukuza (Allaah). (Yule mtu) akamwambia: Yaa Abaa Muhammad, je, Allaah Ataniadhibu kwa sababu ya Swalaah? Akasema: "Hapana, lakini Allaah Atakuadhibu kwa sababu ya kuikhalifu Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
403
Hadiyth
450

40-Mlangoباب تعجيل عقوبة من بلغه عن النبي
صلى الله عليه وسلم حديث فلم يعظمه ولم يوقره
Mlango Wa Kuharakishwa Adhabu Ya Ambaye Imemfikia Hadiyth
Kutoka Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kisha Asiitukuze Wala Asiiheshimu

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي ابْنُ عَجْلَانَ، عَنْ الْعَجْلَانِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "بَيْنَمَا رَجُلٌ يَتَبَخْتَرُ فِي بُرْدَيْنِ، خَسَفَ اللَّهُ بِهِ الْأَرْضَ، فَهُوَ يَتَجَلْجَلُ فِيهَا إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ"، فَقَالَ لَهُ فَتًى قَدْ سَمَّاهُ وَهُوَ فِي حُلَّةٍ لَهُ: يَا أَبَا هُرَيْرَةَ، أَهَكَذَا كَانَ يَمْشِي ذَلِكَ الْفَتَى الَّذِي خُسِفَ بِهِ؟ ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدِهِ، فَعَثَرَ عَثْرَةً كَادَ يَتَكَسَّرُ مِنْهَا، فَقَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ لِلْمَنْخَرَيْنِ وَلِلْفَمِ: {إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ}

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Ibn 'Ajlaan, kutoka kwa Al-'Ajlaan, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Wakati mtu mmoja akitembea kwa maringo katika mashuka yake mawili, Allaah Akaididimiza ardhi pamoja naye; basi yeye anazama ndani yake huku akitikisika mpaka Siku ya Qiyaamah." Kijana mmoja — (mpokezi) alimtaja jina — akamwambia, naye akiwa amevaa vazi lake kamili (la nguo mbili): Yaa Abaa Hurayrah, je, hivi ndivyo alivyokuwa akitembea kijana yule aliyedidimizwa? Kisha akapiga kwa mkono wake, akajikwaa mkwao ambao nusura avunjike kwa huo. Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akasema: (Uanguke) kwa pua na kwa mdomo!

إِنَّا كَفَيْنَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ

Hakika Sisi Tunakutosheleza dhidi ya wafanyao istihzai [Al-Hijr (15:95)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
404
Hadiyth
451

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا هَارُونُ هُوَ ابْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ الزُّبَيْرِ بْنِ عَدِيٍّ، عَنْ خِرَاشِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَسْجِدِ فَتًى يَخْذِفُ، فَقَالَ لَهُ شَيْخٌ: لَا تَخْذِفْ، فَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ الْخَذْفِ"، فَغَفَلَ الْفَتَى وَظَنَّ أَنَّ الشَّيْخَ لَا يَفْطِنُ لَهُ، فَخَذَفَ، فَقَالَ لَهُ الشَّيْخُ: أُحَدِّثُكَ أَنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "يَنْهَى عَنْ الْخَذْفِ" ثُمَّ تَخْذِفُ؟ وَاللَّهِ لَا أَشْهَدُ لَكَ جَنَازَةً، وَلَا أَعُودُكَ فِي مَرَضٍ، وَلَا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا، فَقُلْتُ لِصَاحِبٍ لِي يُقَالُ لَهُ مُهَاجِرٌ: انْطَلِقْ إِلَى خِرَاشٍ فَاسْأَلْهُ، فَأَتَاهُ، فَسَأَلَهُ عَنْهُ فَحَدَّثَهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Haaruwn — naye ni Ibn Al-Mughiyrah —, kutoka kwa 'Amr bin Abiy Qays, kutoka kwa Az-Zubayr bin 'Adiyy, kutoka kwa Khiraash bin Jubayr, amesema: Nilimuona kijana mmoja Msikitini akirusha vijiwe kwa vidole. Mzee mmoja (رضي الله عنه) akamwambia: Usirushe vijiwe kwa vidole, kwani mimi nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza khadhf (kurusha vijiwe kwa vidole). Kijana akaghafilika, na akadhani kwamba mzee hamtambui, akarusha. Mzee akamwambia: Ninakusimulia kwamba nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza khadhf, kisha unarusha? Wa-Allaahi, sitahudhuria jeneza lako, wala sitakutembelea katika ugonjwa, wala sitakusemesha kamwe. Nikamwambia sahibu yangu mmoja aitwaye Muhaajir: Nenda kwa Khiraash umuulize. Akamwendea, akamuuliza kuhusu hilo, naye akamsimulia.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
452

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "عَنْ الْخَذْفِ" وَقَالَ: "إِنَّهَا لَا تَصْطَادُ صَيْدًا، وَلَا تَنْكِأُ عَدُوًّا، وَلَكِنَّهَا تَكْسِرُ السِّنَّ، وَتَفْقَأُ الْعَيْنَ"، فَرَفَعَ رَجُلٌ بَيْنَهُ وَبَيْنَ سَعِيدٍ قَرَابَةٌ شَيْئًا مِنْ الْأَرْضِ، فَقَالَ: هَذِهِ؟ وَمَا تَكُونُ هَذِهِ؟، فَقَالَ سَعِيدٌ: أَلَا أُرَانِي أُحَدِّثُكَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ثُمَّ تَهَاوَنُ بِهِ، لَا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza khadhf (kurusha vijiwe kwa vidole), na akasema: "Hakika (kijiwe kinachorushwa) hakiwindi mnyama, wala hakimuumizi adui, lakini kinavunja jino na kinatoboa jicho." Mtu mmoja ambaye kati yake na Sa'iyd kulikuwa na ujamaa akainua kitu kutoka ardhini, akasema: Hiki? Na hiki kitakuwa nini? Sa'iyd akasema: Hivi mimi ninakusimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha wewe unalidharau? Sitakusemesha kamwe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
453

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا كَهْمَسُ بْنُ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ، قَالَ: رَأَى عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُغَفَّلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ رَجُلًا مِنْ أَصْحَابِهِ يَخْذِفُ، فَقَالَ: لَا تَخْذِفْ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كَانَ يَنْهَى عَنْ الْخَذْفِ أَوْ كَانَ يَكْرَه الْخَذْفَ"، وَقَالَ: "إِنَّهُ لَا يُنْكَأُ بِهِ عَدُوٌّ، وَلَا يُصَادُ بِهِ صَيْدٌ، وَلَكِنَّهُ قَدْ يَفْقَأُ الْعَيْنَ، وَيَكْسِرُ السِّنَّ"، ثُمَّ رَآهُ بَعْدَ ذَلِكَ يَخْذِفُ، فَقَالَ لَهُ: أَلَمْ أُخْبِرْكَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَنْهَى عَنْهُ، ثُمَّ أَرَاكَ تَخْذِفُ، وَاللَّهِ لَا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Kahmas bin Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Buraydah, amesema: 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه) alimuona mtu mmoja miongoni mwa wenzake akirusha vijiwe kwa vidole. Akasema: Usirushe vijiwe kwa vidole, kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikataza khadhf (kurusha vijiwe kwa vidole) — au: alikuwa akichukia khadhf — na akasema: "Hakika kwa huo (urushaji) adui haumizwi, wala mnyama hawindwi; lakini huenda ukatoboa jicho, na ukavunja jino." Kisha akamuona baada ya hapo akirusha vijiwe kwa vidole, akamwambia: Je, sikukukhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akikataza hilo, kisha nakuona unarusha vijiwe kwa vidole? Wa-Allaahi, sitakusemesha kamwe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
454

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ بَشِيرٍ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: حَدَّثَ ابْنُ سِيرِينَ رَجُلًا بِحَدِيثٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ رَجُلٌ: قَالَ فُلَانٌ: كَذَا وَكَذَا، فَقَالَ ابْنُ سِيرِينَ: "أُحَدِّثُكَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَتَقُولُ: قَالَ فُلَانٌ وَفُلَانٌ: كَذَا وَكذَا، لَا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sa'iyd bin Bashiyr, kutoka kwa Qataadah, amesema: Ibn Siyriyn alimsimulia mtu mmoja Hadiyth kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mtu mmoja akasema: Fulani amesema kadhaa wa kadhaa. Ibn Siyriyn akasema: "Ninakusimulia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), nawe unasema: Fulani na fulani wamesema kadhaa wa kadhaa! Sitakusemesha kamwe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
455

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِذَا اسْتَأْذَنَتْ أَحَدَكُمْ امْرَأَتُهُ إِلَى الْمَسْجِدِ، فَلَا يَمْنَعْهَا"، فَقَالَ فُلَانُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ: إِذًا وَاللَّهِ أَمْنَعُهَا، فَأَقْبَلَ عَلَيْهِ ابْنُ عُمَرَ فَشَتَمَهُ شَتْمَةً لَمْ أَرَهُ شَتَمَهَا أَحَدًا قَبْلَهُ، ثُمَّ قَالَ: أُحَدِّثُكَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَتَقُولُ: إِذًا وَاللَّهِ أَمْنَعُهَا!!

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mke wa mmoja wenu akimwomba idhini (ya kwenda) Msikitini, basi asimzuie." Fulani bin 'Abdi-Allaah akasema: Basi, Wa-Allaahi, nitamzuia. Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akamwelekea, akamtukana tusi ambalo sijamuona akimtukana nalo yeyote kabla yake. Kisha akasema: Ninakusimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nawe unasema: Basi, Wa-Allaahi, nitamzuia!

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
456

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا هَارُونُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ مَعْرُوفٍ، عَنْ أَبِي الْمُخَارِقِ، قَالَ: ذَكَرَ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "نَهَى عَنْ دِرْهَمَيْنِ بِدِرْهَمٍ"، فَقَالَ فُلَانٌ: مَا أَرَى بِهَذَا بَأْسًا، يَدًا بِيَدٍ، فَقَالَ عُبَادَةُ: أَقُولُ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَتَقُولُ: لَا أَرَى بِهِ بَأْسًا، وَاللَّهِ لَا يُظِلُّنِي وَإِيَّاكَ سَقْفٌ أَبَدًا

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Haaruwn bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ma'ruwf, kutoka kwa Abul-Mukhaariq, amesema: 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه) alitaja kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza (kuuza) dirhamu mbili kwa dirhamu moja. Fulani akasema: Sioni ubaya wowote katika hili, (ikiwa ni) mkono kwa mkono. 'Ubaadah (رضي الله عنه) akasema: Ninasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema, nawe unasema: Sioni ubaya katika hilo! Wa-Allaahi, paa halitanifunika mimi na wewe (pamoja) kamwe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
457

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الرِّفَاعِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو عَامِرٍ الْعَقَدِيُّ، عَنْ زَمْعَةَ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ وَهْرَامٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا تَطْرُقُوا النِّسَاءَ لَيْلًا"، قَالَ: وَأَقْبَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَافِلًا، فَانْسَلَّ رَجُلَانِ إِلَى أَهْلَيْهِمَا، فَكِلَاهُمَا وَجَدَ مَعَ امْرَأَتِهِ رَجُلًا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Ar-Rifaa'iy, ametusimulia Abuw 'Aamir Al-'Aqadiy, kutoka kwa Zam'ah, kutoka kwa Salamah bin Wahraam, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Msiwajie wanawake (wenu) usiku (kwa ghafla, mnaporudi safarini)." Akasema: Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akarejea (kutoka safarini); watu wawili wakaondoka kwa kunyemelea kwenda kwa ahali zao, na kila mmoja wao akamkuta mwanamume pamoja na mkewe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
458

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ حَرْمَلَةَ الْأَسْلَمِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَدِمَ مِنْ سَفَرٍ نَزَلَ الْمُعَرَّسَ، ثُمَّ قَالَ: "لَا تَطْرُقُوا النِّسَاءَ لَيْلًا"، فَخَرَجَ رَجُلَانِ مِمَّنْ سَمِعَ مَقَالَتَهُ، فَطَرَقَا أَهْلَهُمَا فَوَجَدَ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مَعَ امْرَأَتِهِ رَجُلًا

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Harmalah Al-Aslamiy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaporudi kutoka safarini, hushuka Al-Mu'arras (mahali pa kupumzika usiku huko Dhul-Hulayfah), kisha akasema: "Msiwajie wanawake (wenu) usiku (kwa ghafla)." Watu wawili miongoni mwa walioisikia kauli yake wakatoka, wakawajia ahali zao usiku; kila mmoja wao akamkuta mwanamume pamoja na mkewe.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
459

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ حَرْمَلَةَ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ يُوَدِّعُهُ بِحَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ، فَقَالَ لَهُ: لَا تَبْرَحْ حَتَّى تُصَلِّيَ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا يَخْرُجُ بَعْدَ النِّدَاءِ مِنْ الْمَسْجِدِ إِلَّا مُنَافِقٌ، إِلَّا رَجُلٌ أَخْرَجَتْهُ حَاجَهٌ وَهُوَ يُرِيدُ الرَّجْعَةَ إِلَى الْمَسْجِدِ"، فَقَالَ: إِنَّ أَصْحَابِي بِالْحَرَّةِ، قَالَ: فَخَرَجَ قَالَ: فَلَمْ يَزَلْ سَعِيدٌ يَوْلَعُ بِذِكْرِهِ حَتَّى أُخْبِرَ أَنَّهُ وَقَعَ مِنْ رَاحِلَتِهِ فَانْكَسَرَتْ فَخِذُهُ

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Harmalah, amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib kumuaga (akienda) Hajj au 'Umrah. Akamwambia: Usiondoke mpaka uswali, kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hatoki Msikitini baada ya Adhaan isipokuwa mnafiki, isipokuwa mtu ambaye haja imemtoa, naye anataka kurejea Msikitini." Akasema: Hakika wenzangu wako Al-Harrah (ardhi ya mawe meusi huko Madiynah). Akasema ('Abdur-Rahmaan): Akatoka. Akasema: Sa'iyd hakuacha kumtaja mara kwa mara, mpaka akakhabarishwa kwamba alianguka kutoka kwenye kipando chake, paja lake likavunjika.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
405
Hadiyth
460

41-Mlangoباب من كره أن يمل الناسMlango Wa Aliyechukia Kuwachosha Watu

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الصَّمَدِ بْنُ عَبْدِ الْوَارِثِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي الْأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا تُمِلُّوا النَّاسَ"

Ametukhabarisha 'Abdusw-Swamad bin 'Abdil-Waarith, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Msiwachoshe watu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
411
Hadiyth
461

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَشْعَثُ، عَنْ كُرْدُوسٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِنَّ لِلْقُلُوبِ لَنَشَاطًا وَإِقْبَالًا، وَإِنَّ لَهَا تَوْلِيَةً وَإِدْبَارًا، فَحَدِّثُوا النَّاسَ مَا أَقْبَلُوا عَلَيْكُمْ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ash'ath, kutoka kwa Kurduws, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Hakika nyoyo zina uchangamfu na kuelekea (kwa hamu), na hakika zina kugeuka na kupa mgongo; basi wasimulieni watu maadamu wanakuelekeeni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
411
Hadiyth
462

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا أَبُو هِلَالٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ يَقُولُ: كَانَ يُقَالُ: "حَدِّثْ الْقَوْمَ مَا أَقْبَلُوا عَلَيْكَ بِوُجُوهِهِمْ، فَإِذَا الْتَفَتُوا، فَاعْلَمْ أَنَّ لَهُمْ حَاجَاتٍ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Abuw Hilaal, amesema: Nilimsikia Al-Hasan akisema: Ilikuwa ikisemwa: "Wasimulie watu maadamu wanakuelekea kwa nyuso zao; wanapogeuka (pembeni), basi jua kwamba wana haja (zao)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
411
Hadiyth
463

42-Mlangoباب من لم ير كتابة الحديثMlango Wa Wasioona [Kufaa] Kuandika Hadiyth

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا هَمَّامٌ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا تَكْتُبُوا عَنِّي شَيْئًا إِلَّا الْقُرْآنَ، فَمَنْ كَتَبَ عَنِّي شَيْئًا غَيْرَ الْقُرْآنِ، فَلْيَمْحُهُ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Hammaam, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiandike kutoka kwangu chochote isipokuwa Qur-aan; na aliyeandika kutoka kwangu chochote kisichokuwa Qur-aan, basi akifute."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
412
Hadiyth
464

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، قَالَ: حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ أَسْلَمَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّهُمُ اسْتَأْذَنُوا النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أَنْ يَكْتُبُوا عَنْهُ "فَلَمْ يَأْذَنْ لَهُمْ"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, amesema: Ametusimulia Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه): Kwamba wao walimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) idhini ya kuandika kutoka kwake, "naye hakuwapa idhini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
412
Hadiyth
465

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ ابْنِ شُبْرُمَةَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "يَا شِبَاكُ، أَرُدُّ عَلَيْكَ، يَعْنِي: الْحَدِيثَ؟ مَا أَرَدْتُ أَنْ يُرَدَّ عَلَيَّ حَدِيثٌ قَطُّ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Ibn Shubrumah, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba alikuwa akisema: "Yaa Shibaak, nikurudie — yaani: Hadiyth? Sijapata kamwe kutaka nirudiwe Hadiyth yoyote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
412
Hadiyth
466

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ مَهْدِيٍّ، يَقُولُ: سَمِعْتُ مَالِكَ بْنَ أَنَسٍ، يَقُولُ: جَاءَ الزُّهْرِيُّ بِحَدِيثٍ فَلَقِيتُهُ فِي بَعْضِ الطَّرِيقِ، فَأَخَذْتُ بِلِجَامِهِ، فَقُلْتُ: يَا أَبَا بَكْرٍ، أَعِدْ عَلَيَّ الْحَدِيثَ الَّذِي حَدَّثْتَنَا بِهِ، قَالَ: "وَتَسْتَعِيدُ الْحَدِيثَ؟، قَالَ: قُلْتُ: وَمَا كُنْتَ تَسْتَعِيدُ الْحَدِيثَ؟، قَالَ: لَا، قُلْتُ: وَلَا تَكْتُبُ؟، قَالَ: لَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy akisema: Nilimsikia Maalik bin Anas akisema: Az-Zuhriy alikuja na Hadiyth moja; nikakutana naye katika baadhi ya njia, nikashika hatamu (ya kipando) chake, nikasema: Yaa Abaa Bakr, nirudie Hadiyth uliyotusimulia. Akasema: "Na wewe unataka kurudiwa Hadiyth? Akasema: Nikasema: Je, wewe hukuwa ukitaka kurudiwa Hadiyth? Akasema: Hapana. Nikasema: Wala huandiki? Akasema: Hapana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
413
Hadiyth
467

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: "كَانَ قَتَادَةُ يَكْرَهُ الْكِتَابَةَ، فَإِذَا سَمِعَ وَقْعَ الْكِتَابِ، أَنْكَرَهُ وَالْتَمَسَهُ بِيَدِهِ"،

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: "Qataadah alikuwa akichukia kuandika; alipokuwa akisikia sauti ya kuandika, aliikataa na akikitafuta (kinachoandikwa) kwa mkono wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
414
Hadiyth
468

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، قَالَ: "كَانَ الْأَوْزَاعِيُّ يَكْرَهُهُ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, amesema: "Al-Awzaa'iy alikuwa akikuchukia (kuandika)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
414
Hadiyth
469

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مَنْصُورٍ "أَنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ يَكْرَهُ الْكِتَابَ"، يَعْنِي: الْعِلْمَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr: "Kwamba Ibraahiym alikuwa akichukia kuandika," yaani: ilimu.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
414
Hadiyth
470

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، أَنْبَأَنَا أَزْهَرُ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "لَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا كِتَابًا، لَاتَّخَذْتُ رَسَائِلَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametupa khabari Azhar, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Lau ningekuwa mwenye kujichukulia kitabu, ningejichukulia barua za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
414
Hadiyth
471

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: "رَأَيْتُ حَمَّادًا يَكْتُبُ عِنْدَ إِبْرَاهِيمَ، فَقَالَ لَهُ إِبْرَاهِيمُ: أَلَمْ أَنْهَكَ؟، قَالَ: إِنَّمَا هِيَ أَطْرَافٌ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema: "Nilimuona Hammaad akiandika mbele ya Ibraahiym; Ibraahiym akamwambia: Je, sikukukataza? Akasema: Hakika hizi ni ncha (za Hadiyth) tu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
415
Hadiyth
472

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ لِي عَبِيدَةُ: "لَا تُخَلِّدَنَّ بِي كِتَابًا"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Abiydah aliniambia: "Usibakishe kamwe kitabu (cha maandishi) kinachonihusu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
415
Hadiyth
473

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هِشَامٍ، قَالَ: "مَا كَتَبْتُ عَنْ مُحَمَّدٍ إِلَّا حَدِيثَ الْأَعْمَاقِ، فَلَمَّا حَفِظْتُهُ، مَحَوْتُهُ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hishaam, amesema: "Sikuandika kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn] isipokuwa Hadiyth ya Al-A'maaq (mahali huko Shaam patakapotokea vita vikubwa kabla ya Qiyaamah); nilipoihifadhi, niliifuta."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
415
Hadiyth
474

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ عَبْدِ الْعَزِيزِ، يَقُولُ: "مَا كَتَبْتُ حَدِيثًا قَطُّ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin 'Abdil-'Aziyz akisema: "Sijapata kamwe kuandika Hadiyth yoyote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
415
Hadiyth
475

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْمُغِيرَةِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "مَا كَتَبْتُ شَيْئًا قَطُّ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Abuw Daawuwd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Sijapata kamwe kuandika kitu chochote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
416
Hadiyth
476

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ رَجَاءٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: سَأَلْتُ عَبِيدَةَ قِطْعَةَ جِلْدٍ أَكْتُبُ فِيهِ، فَقَالَ: "يَا إِبْرَاهِيمُ، لَا تُخَلِّدَنَّ عَنِّي كِتَابًا"،

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Abuw Daawuwd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Rajaa, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: Nilimuomba 'Abiydah kipande cha ngozi niandike ndani yake; akasema: "Yaa Ibraahiym, usibakishe kamwe kitabu (cha maandishi) kutoka kwangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
417
Hadiyth
477

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبِيدَةَ، مِثْلَهُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah [bin 'Imraan], ametusimulia Abuw Daawuwd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abiydah, mfano wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
417
Hadiyth
478

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ أَبِي عَتِيكٍ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: "أَنَّهُ كَانَ يَكْرَهُ أَنْ يُكْتَبَ الْحَدِيثُ فِي الْكَرَارِيسِ، وَيَقُولُ: يُشَبَّهُ بِالْمَصَاحِفِ"،

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Sulaymaan bin Abiy 'Atiyk, kutoka kwa Abuw Ma'shar, kutoka kwa Ibraahiym: "Kwamba alikuwa akichukia Hadiyth kuandikwa katika madaftari, na akisema: (Hilo) linafananishwa na Miswahafu (nakala za Qur-aan zilizoandikwa)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
417
Hadiyth
479

قَالَ يَحْيَى: وَوَجَدْتُ فِي كِتَابِي، عَنْ زِيَادٍ الْكَاتِبِ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، "فَاكْتُبْ كَيْفَ شِئْتَ"

Yahyaa amesema: Na nilikuta katika kitabu changu, kutoka kwa Ziyaad Al-Kaatib, kutoka kwa Abuw Ma'shar: "Basi andika upendavyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
480

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، وَعُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ نُعْمَانَ بْنِ قَيْسٍ، أَنَّ عَبِيدَةَ دَعَا بِكُتُبِهِ فَمَحَاهَا عِنْدَ الْمَوْتِ، وَقَالَ: "إِنِّي أَخَافُ أَنْ يَلِيَهَا قَوْمٌ، فَلَا يَضَعُونَهَا مَوَاضِعَهَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf na 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Nu'maan bin Qays, kwamba 'Abiydah aliagiza vitabu vyake akavifuta wakati wa kufa (kwake), na akasema: "Hakika mimi nahofia visimamiwe na watu wasioviweka mahali pake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
481

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، وَزَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، عَنْ عَبْدِ الْوَاحِدِ بْنِ زِيَادٍ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، "أَنَّهُ كَرِهَ أَنْ يُكْتَبَ الْعِلْمُ فِي الْكَرَارِيسِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak na Zakariyyaa bin 'Adiyy, kutoka kwa 'Abdul-Waahid bin Ziyaad, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid: "Kwamba alichukia ilimu kuandikwa katika madaftari."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
482

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: "مَا زَالَ هَذَا الْعِلْمُ عَزِيزًا يَتَلَقَّاهُ الرِّجَالُ حَتَّى وَقَعَ فِي الصُّحُفِ، فَحَمَلَهُ، أَوْ دَخَلَ فِيهِ غَيْرُ أَهْلِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdur-Rahmaan bin Swaalih, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: "Ilimu hii iliendelea kuwa tukufu (yenye thamani), watu wakiipokea (mmoja kutoka kwa mwingine), mpaka ilipoingia katika kurasa (za maandishi); basi wakaibeba — au: wakaingia ndani yake — wasiokuwa watu wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
483

أَخْبَرَنَا يُوسُفُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ يُونُسَ، قَالَ: "كَانَ الْحَسَنُ يَكْتُبُ وَيُكْتِبُ، وَكَانَ ابْنُ سِيرِينَ لَا يَكْتُبُ وَلَا يُكْتِبُ"

Ametukhabarisha Yuwsuf bin Muwsaa, ametusimulia Abuw Daawuwd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Yuwnus, amesema: "Al-Hasan alikuwa akiandika na akiwaandikisha (wengine), na Ibn Siyriyn alikuwa haandiki wala haandikishi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
484

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ، أَنْبَأَنَا الْعَوَّامُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، قَالَ: بَلَغَ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ عِنْدَ نَاسٍ كِتَابًا يُعْجَبُونَ بِهِ، فَلَمْ يَزَلْ بِهِمْ حَتَّى أَتَوْهُ بِهِ، فَمَحَاهُ، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّمَا هَلَكَ أَهْلُ الْكِتَابِ قَبْلَكُمْ: أَنَّهُمْ أَقْبَلُوا عَلَى كُتُبِ عُلَمَائِهِمْ، وَتَرَكُوا كِتَابَ رَبِّهِمْ"

Ametukhabarisha Yaziyd, ametupa khabari Al-'Awwaam, kutoka kwa Ibraahiym At-Taymiy, amesema: Ilimfikia Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) (khabari) kwamba watu fulani wana kitabu wanachokistaajabia. Hakuacha kuwashughulikia mpaka wakamletea; akakifuta, kisha akasema: "Hakika Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu: Mayahudi na Manaswara) waliokuwa kabla yenu waliangamia tu kwa kuwa walivielekea vitabu vya 'Ulamaa (Wanazuoni) wao, na wakakiacha Kitabu cha Rabb wao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
485

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ قَالَ: قُلْتُ لِعَبِيدَةَ: "أَكْتُبُ مَا أَسْمَعُ مِنْكَ، قَالَ: لَا، قُلْتُ: فَإِنْ وَجَدْتُ كِتَابًا أَقْرَؤُهُ؟، قَالَ: لَا"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn], amesema: Nilimwambia 'Abiydah: "Niandike ninayoyasikia kutoka kwako? Akasema: Hapana. Nikasema: Basi nikikuta kitabu, nikisome? Akasema: Hapana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
486

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، قَالَ: قُلْتُ لِأَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَلَا تُكْتِبُنَا، فَإِنَّا لَا نَحْفَظُ؟، فَقَالَ: "لَا، إِنَّا لَنْ نُكْتِبَكُمْ، وَلَنْ نَجْعَلَهُ قُرْآنًا، وَلَكِنْ احْفَظُوا عَنَّا كَمَا حَفِظْنَا نَحْنُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Jurayriy, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, amesema: Nilimwambia Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه): Je, hutuandikishi, kwani sisi hatuhifadhi? Akasema: "Hapana, hatutakuandikisheni kamwe, wala hatutaifanya (Hadiyth) kuwa Qur-aan; lakini hifadhini kutoka kwetu kama tulivyohifadhi sisi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
487

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا كَثِيرٍ، يَقُولُ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: "إِنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ لَا يَكْتُبُ، وَلَا يُكْتِبُ"

Ametusimulia Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: Nilimsikia Abuw Kathiyr akisema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: "Hakika Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) haandiki wala haandikishi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
488

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي مُوسَى، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ هِلَالٍ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ: "أَنَّهُ كَانَ يَكْتُبُ حَدِيثَ أَبِيهِ، فَرَآهُ أَبُو مُوسَى، فَمَحَاهُ"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abuw Muwsaa, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa Abuw Burdah: "Kwamba alikuwa akiandika Hadiyth za baba yake; Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) akamuona, akazifuta."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
489

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنِي قُرَيْشُ بْنُ أَنَسٍ، قَالَ: قَالَ لِي ابْنُ عَوْنٍ: "وَاللَّهِ مَا كَتَبْتُ حَدِيثًا قَطُّ"، قَالَ: وَقَالَ ابْنُ سِيرِينَ: "لَا وَاللَّهِ مَا كَتَبْتُ حَدِيثًا قَطُّ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', amenisimulia Quraysh bin Anas, amesema: Ibn 'Awn aliniambia: "Wa-Allaahi, sijapata kamwe kuandika Hadiyth yoyote." Akasema: Na Ibn Siyriyn amesema: "Hapana, Wa-Allaahi, sijapata kamwe kuandika Hadiyth yoyote."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
490

قَالَ ابْنُ عَوْنٍ: قَالَ لِي ابْنُ سِيرِينَ: عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَرَادَنِي مَرْوَانُ بْنُ الْحَكَمِ وَهُوَ أَمِيرٌ عَلَى الْمَدِينَةِ أَنْ أُكْتِبَهُ شَيْئًا، قَالَ: فَلَمْ أَفْعَلْ، قَالَ: فَجَعَلَ سِتْرًا بَيْنَ مَجْلِسِهِ وَبَيْنَ بَقِيَّةِ دَارِهِ، قَالَ: فَكَانَ أَصْحَابُهُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِ، وَيَتَحَدَّثُونَ فِي ذَلِكَ الْمَوْضِعِ، فَأَقْبَلَ مَرْوَانُ عَلَى أَصْحَابِهِ، فَقَالَ: مَا أُرَانَا إِلَّا قَدْ خُنَّاهُ، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيَّ، قَالَ: قُلْتُ وَمَا ذَاكَ؟، قَالَ: مَا أُرَانَا إِلَّا قَدْ خُنَّاكَ، قَالَ: قُلْتُ: وَمَا ذَاكَ؟، قَالَ: "إِنَّا أَمَرْنَا رَجُلًا يَقْعُدُ خَلْفَ هَذَا السِّتْرِ، فَيَكْتُبُ مَا تُفْتِي هَؤُلَاءِ وَمَا تَقُولُ"

Ibn 'Awn amesema: Ibn Siyriyn aliniambia, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه): Marwaan bin Al-Hakam — naye alikuwa amiri wa Madiynah — alinitaka nimwandikishe kitu; akasema: Sikufanya. Akasema: Basi akaweka pazia kati ya baraza lake na sehemu iliyobaki ya nyumba yake. Akasema: Wenzake walikuwa wakiingia kwake na wakizungumza mahali pale. Marwaan akawaelekea wenzake, akasema: Sioni ila tumemfanyia khiyana. Kisha akanielekea; akasema: Nikasema: Ni nini hicho? Akasema: Sioni ila tumekufanyia khiyana. Akasema: Nikasema: Ni nini hicho? Akasema: "Hakika sisi tulimuamrisha mtu akae nyuma ya pazia hili, aandike unayowapa Fatwa hawa na unayoyasema."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
491

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْقَطَّانُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، قَالَ: قُلْتُ لِإِبْرَاهِيمَ: إِنَّ سَالِمًا أَتَمُّ مِنْكَ حَدِيثًا؟ قَالَ: "إِنَّ سَالِمًا كَانَ يَكْتُبُ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd Al-Qatwtwaan, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, amesema: Nilimwambia Ibraahiym: Hakika Saalim ni mkamilifu zaidi kuliko wewe katika Hadiyth? Akasema: "Hakika Saalim alikuwa akiandika."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
418
Hadiyth
492

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ هِشَامٍ، حَدَّثَنَا الْحَارِثُ بْنُ يَزِيدَ الْحِمْصِيُّ، عَنْ عَمْرِو بْنِ قَيْسٍ، قَالَ: وَفَدْتُ مَعَ أَبِي إِلَى يَزِيدَ بْنِ مُعَاوِيَةَ بِحُوَّارَيْنَ حِينَ تُوُفِّيَ مُعَاوِيَةُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ نُعَزِّيهِ، وَنُهَنِّيهِ بِالْخِلَافَةِ، فَإِذَا رَجُلٌ فِي مَسْجِدِهَا، يَقُولُ: "أَلَا إِنَّ مِنْ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ أَنْ يُرْفَعَ الْأَشْرَارُ، ويُوضَعُ الْأَخْيَارُ، أَلَا إِنَّ مِنْ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ أَنْ يَظْهَرَ الْقَوْلُ وَيُخْزَنَ الْعَمَلُ، أَلَا إِنَّ مِنْ أَشْرَاطِ السَّاعَةِ أَنْ تُتْلَى الْمَثْنَاةُ، فَلَا يُوجَدُ مَنْ يُغَيِّرُهَا، قِيلَ لَهُ: وَمَا الْمَثْنَاةُ؟، قَالَ: مَا اسْتُكْتِبَ مِنْ كِتَابٍ غَيْرِ الْقُرْآنِ، فَعَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَبِهِ هُدِيتُمْ، وَبِهِ تُجْزَوْنَ، وَعَنْهُ تُسْأَلُونَ"، فَلَمْ أَدْرِ مَنْ الرَّجُلُ، فَحَدَّثْتُ هذَا الْحَدِيثِ بَعْدَ ذَلِكَ بِحِمْصَ، فَقَالَ لِي رَجُلٌ مِنْ الْقَوْمِ: أَوَ مَا تَعْرِفُهُ؟، قُلْتُ: لَا، قَالَ: ذَلِكَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Hishaam, ametusimulia Al-Haarith bin Yaziyd Al-Himswiy, kutoka kwa 'Amr bin Qays, amesema: Nilikwenda kama mjumbe pamoja na baba yangu kwa Yaziyd bin Mu'aawiyah huko Huwwaariyn (mji huko Shaam), wakati Mu'aawiyah (رضي الله عنه) alipofariki, ili tumpe pole na tumpongeze kwa ukhalifa. Ghafla (tukamkuta) mtu mmoja katika Msikiti wake (mji huo) akisema: "Fahamuni! Hakika miongoni mwa alama za Saa (Qiyaamah) ni waovu kunyanyuliwa, na wema kushushwa. Fahamuni! Hakika miongoni mwa alama za Saa ni kauli kudhihirika na amali kufichwa (isitendwe). Fahamuni! Hakika miongoni mwa alama za Saa ni kusomwa Al-Mathnaah (maandishi yanayosomwa kando ya Qur-aan), wala asipatikane wa kuibadilisha. Akaulizwa: Al-Mathnaah ni nini? Akasema: Ni kile kilichoombwa kuandikwa katika kitabu kisichokuwa Qur-aan. Basi shikamaneni na Qur-aan, kwani kwayo mmeongozwa, na kwayo mtalipwa, na kuhusu hiyo mtaulizwa." Sikujua yule mtu ni nani. Baada ya hapo nikaisimulia Hadiyth hii huko Himsw; mtu mmoja katika watu akaniambia: Je, humjui? Nikasema: Hapana. Akasema: Huyo ni 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
423
Hadiyth
493

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا أَبُو زُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا حُصَيْنٌ، عَنْ مُرَّةَ الْهَمْدَانِيِّ، قَالَ: جَاءَ أَبُو قُرَّةَ الْكِنْدِيُّ بِكِتَابٍ مِنْ الشَّامِ، فَحَمَلَهُ، فَدَفَعَهُ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَنَظَرَ فِيهِ، فَدَعَا بِطَسْتٍ، ثُمَّ دَعَا بِمَاءٍ، فَمَرَسَهُ فِيهِ، وَقَالَ: "إِنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِاتِّبَاعِهِمْ الْكُتُبَ وَتَرْكِهِمْ كِتَابَهُمْ"، قَالَ حُصَيْنٌ: فَقَالَ مُرَّةُ: "أَمَا إِنَّهُ لَوْ كَانَ مِنْ الْقُرْآنِ، أَوْ السُّنَّةِ لَمْ يَمْحُهُ، وَلَكِنْ كَانَ مِنْ كُتُبِ أَهْلِ الْكِتَابِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Abuw Zubayd, ametusimulia Huswayn, kutoka kwa Murrah Al-Hamdaaniy, amesema: Abuw Qurrah Al-Kindiy alikuja na kitabu kutoka Shaam; akakibeba, akampa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه). Akakitazama, kisha akaagiza beseni, kisha akaagiza maji, akakisugua ndani yake, na akasema: "Hakika walioangamia kabla yenu waliangamia tu kwa kufuata kwao vitabu na kuacha kwao Kitabu chao." Huswayn amesema: Murrah akasema: "Ama hakika lau kingekuwa ni katika Qur-aan au Sunnah, asingekifuta; lakini kilikuwa ni katika vitabu vya Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu: Mayahudi na Manaswara)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
424
Hadiyth
494

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ يَحْيَى بْنِ جَعْدَةَ، قَالَ: أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَتِفٍ فِيهِ كِتَابٌ، فَقَالَ: "كَفَى بِقَوْمٍ ضَلَالًا أَنْ يَرْغَبُوا عَمَّا جَاءَ بِهِ نَبِيُّهُمْ إِلَى مَا جَاءَ بِهِ نَبِيٌّ غَيْرُ نَبِيِّهِمْ، أَوْ كِتَابٌ غَيْرُ كِتَابِهِمْ"، فَأَنْزَلَ اللَّهُ عز وجل: {أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنْزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَى عَلَيْهِمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَى لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ}

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa Yahyaa bin Ja'dah, amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa mfupa wa bega (wa mnyama) ulio na maandishi; akasema: "Inawatosha watu kuwa ni upotofu kwamba wayapuuze yale aliyokuja nayo Nabiy wao (na waelekee) yale aliyokuja nayo Nabiy asiyekuwa Nabiy wao, au kitabu kisichokuwa kitabu chao." Basi Allaah (عز وجل) Akateremsha:

أَوَلَمْ يَكْفِهِمْ أَنَّا أَنْزَلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ يُتْلَى عَلَيْهِمْ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَرَحْمَةً وَذِكْرَى لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Je, haikuwatosheleza kwamba hakika Sisi Tumekuteremshia Kitabu (Qur-aan) wanachosomewa? Hakika katika hayo bila shaka kuna rehma na ukumbusho (na mawaidha) kwa watu wanaoamini. [Al-‘Ankabuwt (29:51)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
425
Hadiyth
495

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْأَشْعَثِ، عَنْ أَبِيهِ، وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: رَأَيْتُ مَعَ رَجُلٍ صَحِيفَةً فِيهَا: سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، فَقُلْتُ لَهً: أَنْسِخْنِيهَا، فَكَأَنَّهُ بَخِلَ بِهَا، ثُمَّ وَعَدَنِي أَنْ يُعْطِيَنِيهَا، فَأَتَيْتُ عَبْدَ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ فَإِذَا هِيَ بَيْنَ يَدَيْهِ، فَقَالَ: "إِنَّ مَا فِي هَذَا الْكِتَابِ بِدْعَةٌ، وَفِتْنَةٌ، وَضَلَالَةٌ، وَإِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ هَذَا وَأَشْبَاهُ هَذَا، إِنَّهُمْ كَتَبُوهَا، فَاسْتَلَذَّتْهَا أَلْسِنَتُهُمْ، وَأُشْرِبَتْهَا قُلُوبُهُمْ، فَأَعْزِمُ عَلَى كُلِّ امْرِئٍ يَعْلَمُ مَكَانَ كِتَابٍ إِلَّا دَلَّ عَلَيْهِ، وَأُقْسِمُ بِاللَّهِ، قَالَ شُعْبَةُ: فَأَقْسَمَ بِاللَّهِ؟، قَالَ: أَحْسَبُهُ أَقْسَمَ: لَوْ أَنَّهَا ذُكِرَتْ لَهُ بِدَيْرٍ لِهِنْدٍ نَرَاهُ يَعْنِي مَكَانًا بِالْكُوفَةِ بَعِيدًا، لآَتَيْتُهُ وَلَوْ مَشْيًا"

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Ash'ath, kutoka kwa baba yake — naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) —, amesema: Nilimuona mtu mmoja akiwa na karatasi ambayo ndani yake (imeandikwa):

سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ

Utakasifu ni wa Allaah, na Himdi zote ni za Allaah, na hapana mungu apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na Allaah ni Mkubwa.

Nikamwambia: Niandikie nakala yake. Akawa kama kwamba ameifanyia ubakhili, kisha akaniahidi kwamba atanipa. Nikamwendea 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه), mara ghafla (ile karatasi) iko mbele yake. Akasema: "Hakika yaliyomo katika kitabu hiki ni bid'ah (uzushi katika Dini), na fitna, na upotofu. Na hakika kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni hiki na mfano wa hiki: hakika wao waliviandika, ndimi zao zikaviona vitamu, na nyoyo zao zikanyweshwa (mapenzi yake). Basi namtaka kwa msisitizo kila mtu anayejua mahali kilipo kitabu (cha namna hii) ila akionyeshe. Na naapa kwa Allaah —" Shu'bah amesema: "Je, aliapa kwa Allaah?" Akasema: "Nadhani aliapa —: lau (kitabu hicho) kingetajwa kwake kuwa kiko katika nyumba ya watawa ya Hind — tunaiona — yaani: mahali mbali huko Al-Kuwfah —, ningekiendea hata kwa kutembea kwa miguu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
425
Hadiyth
496

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ هُوَ ابْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "أَنَّ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَتَبُوا كِتَابًا، فَتَبِعُوهُ وَتَرَكُوا التَّوْرَاةَ"

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah — naye ni Ibn 'Amr —, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه): "Kwamba Banuw Israaiyl waliandika kitabu, wakakifuata na wakaiacha Tawraat."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
425
Hadiyth
497

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ أَبِي الْمُغِيرَةِ، عَنْ عَفَّاقٍ الْمُحَارِبِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: "إِنَّ نَاسًا يَسْمَعُونَ كَلَامِي، ثُمَّ يَنْطَلِقُونَ فَيَكْتُبُونَهُ، وَإِنِّي لَا أُحِلُّ لِأَحَدٍ أَنْ يَكْتُبَ إِلَّا كِتَابَ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa 'Uthmaan bin Abil-Mughiyrah, kutoka kwa 'Affaaq Al-Muhaaribiy, kutoka kwa baba yake, amesema: Nilimsikia Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) akisema: "Hakika watu (fulani) wanasikia maneno yangu, kisha wanaondoka wakayaandika; na hakika mimi simhalalishii yeyote kuandika isipokuwa Kitabu cha Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
425
Hadiyth
498

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ ابْنِ شُبْرُمَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، يَقُولُ: "مَا كَتَبْتُ سَوْدَاءَ فِي بَيْضَاءَ، وَلَا اسْتَعَدْتُ حَدِيثًا مِنْ إِنْسَانٍ"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Muhammad bin Fudhwayl, kutoka kwa Ibn Shubrumah, amesema: Nilimsikia Ash-Sha'biy akisema: "Sijapata kuandika cheusi juu ya cheupe, wala sijapata kumtaka mtu yeyote anirudie Hadiyth."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
425
Hadiyth
499

43-Mlangoباب من رخص في كتابة العلمMlango Wa Waliotoa Ruhusa Ya Kuandika Ilimu

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ وَهْبِ بْنِ مُنَبِّهٍ، عَنْ أَخِيهِ، سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، يَقُولُ: "لَيْسَ أَحَدٌ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَكْثَرَ حَدِيثًا عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنِّي، إِلَّا مَا كَانَ مِنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، فَإِنَّهُ كَانَ يَكْتُبُ، وَلَا أَكْتُبُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, kutoka kwa ndugu yake [Hammaam bin Munabbih], (kwamba) alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: "Hakuna yeyote miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliye na Hadiyth nyingi zaidi kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko mimi, isipokuwa yale yaliyokuwa kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما); kwani yeye alikuwa akiandika, nami siandiki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
428
Hadiyth
500

أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ الْأَخْنَسِ، قَالَ: حَدَّثَنِي الْوَلِيدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: كُنْتُ أَكْتُبُ كُلَّ شَيْءٍ أَسْمَعُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُرِيدُ حِفْظَهُ، فَنَهَتْنِي قُرَيْشٌ، وَقَالُوا: تَكْتُبُ كُلَّ شَيْءٍ سَمِعْتَهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَشَرٌ يَتَكَلَّمُ فِي الْغَضَبِ وَالرِّضَا؟ فَأَمْسَكْتُ عَنْ الْكِتَابِ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَوْمَأَ بِإِصْبَعِهِ إِلَى فِيهِ، وَقَالَ: "اكْتُبْ، فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، مَا خَرَجَ مِنْهُ إِلَّا حَقٌّ"

Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Al-Akhnas, amesema: Amenisimulia Al-Waliyd bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Yuwsuf bin Maahak, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Nilikuwa nikiandika kila kitu ninachokisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikitaka kukihifadhi. Quraysh wakanikataza, na wakasema: Unaandika kila kitu ulichokisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na hali Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ni binaadam anayezungumza katika hasira na katika ridhaa? Nikaacha kuandika; nikamtajia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akaashiria kwa kidole chake kinywani mwake, na akasema: "Andika; kwani naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hakikutoka humo isipokuwa haki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
428
Hadiyth
501

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي خَالِدُ بْنُ يَزِيدَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلَالٍ، عَنْ عَبْدِ الْوَاحِدِ بْنِ قَيْسٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي مُخْبِرٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، أَنَّهُ أَتَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أَرْوِيَ مِنْ حَدِيثِكَ، فَأَرَدْتُ أَنْ أَسْتَعِينَ بِكِتَابِ يَدِي مَعَ قَلْبِي إِنْ رَأَيْتَ ذَلِكَ؟، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِنْ كَانَ قَالَهُ: "عِ حَدِيثِي، ثُمَّ اسْتَعِنْ بِيَدِكَ مَعَ قَلْبِكَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Khaalid bin Yaziyd, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Hilaal, kutoka kwa 'Abdul-Waahid bin Qays, amesema: Amenikhabarisha mkhabarishaji (mmoja), kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kwamba yeye alimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nataka kupokea (na kusimulia) katika Hadiyth zako; basi nimetaka kujisaidia kwa maandishi ya mkono wangu pamoja na moyo wangu, ikiwa utaona hilo (linafaa)? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema — ikiwa alilisema —: "Zihifadhi Hadiyth zangu, kisha jisaidie kwa mkono wako pamoja na moyo wako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
429
Hadiyth
502

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قَبِيلٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ حَوْلَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَكْتُبُ إِذْ سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الْمَدِينَتَيْنِ تُفْتَحُ أَوَّلًا: قُسْطَنْطِينِيَّةُ، أَوْ رُومِيَّةُ؟، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا، بَلْ مَدِينَةُ هِرَقْلَ أَوَّلًا"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Yahyaa bin Is-haaq, ametusimulia Yahyaa bin Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qabiyl, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما) akisema: Wakati sisi tukiwa tumemzunguka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukiandika, ghafla Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa: Ni mji upi kati ya miji miwili utakaofunguliwa kwanza: Qustwantwiyniyyah (Konstantinopoli) au Ruwmiyyah (Roma)? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hapana, bali mji wa Hiraql (mfalme wa Warumi) ndio wa kwanza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
430
Hadiyth
503

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ أَبِي ضَمْرَةَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، قَالَ: كَتَبَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ رَحِمَهُ الله إِلَى أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ: "أَنْ اكْتُبْ إِلَيَّ بِمَا ثَبَتَ عِنْدَكَ مِنْ الْحَدِيثِ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَبِحَدِيثِ عَمْرَةَ فَإِنِّي قَدْ خَشِيتُ دُرُوسَ الْعِلْمِ وَذَهَابَهُ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Ibraahiym Abuw Ma'mar, kutoka kwa Abuw Dhwamrah, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz (رحمه الله) alimwandikia Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm: "Niandikie yale yaliyothibiti kwako katika Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na Hadiyth ya 'Amrah; kwani hakika mimi nimehofia kufutika kwa ilimu na kuondoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
430
Hadiyth
504

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، قَالَ: كَتَبَ عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ إِلَى أَهْلِ الْمَدِينَةِ: "أَنْ انْظُرُوا حَدِيثَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاكْتُبُوهُ، فَإِنِّي قَدْ خِفْتُ دُرُوسَ الْعِلْمِ وَذَهَابَ أَهْلِهِ"

Ametusimulia Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muslim, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz aliwaandikia watu wa Madiynah: "Itazameni Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha iandikeni; kwani hakika mimi nimeogopa kufutika kwa ilimu na kuondoka kwa watu wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
505

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي الْمَلِيحِ، قَالَ: "يَعِيبُونَ عَلَيْنَا الْكِتَابَ، وَقَدْ قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: {عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي فِي كِتَابٍ}"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abul-Maliyh, amesema: Wanatuaibisha kwa kuandika, na hali Allaah (تعالى) Amesema:

عِلْمُهَا عِنْدَ رَبِّي فِي كِتَابٍ

Ujuzi wake uko kwa Rabb wangu katika Kitabu [Twaaha (20:52)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
506

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا سَوَادَةُ بْنُ حَيَّانَ، قَالَ: سَمِعْتُ مُعَاوِيَةَ بْنَ قُرَّةَ أَبَا إِيَاسٍ، يَقُولُ: كَانَ يُقَالُ: "مَنْ لَمْ يَكْتُبْ عِلْمَهُ، لَمْ يُعَدَّ عِلْمُهُ عِلْمًا"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Sawaadah bin Hayyaan, amesema: Nilimsikia Mu'aawiyah bin Qurrah Abuw Iyaas akisema: Ilikuwa ikisemwa: "Asiyeiandika ilimu yake, ilimu yake haihesabiwi kuwa ni ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
507

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُثَنَّى، حَدَّثَنِي ثُمَامَةُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَنَسٍ: أَنَّ أَنَسًا رَضِيَ اللهُ عَنْهُ كَانَ يَقُولُ لِبَنِيهِ: "يَا بَنِيَّ قَيِّدُوا هَذَا الْعِلْمَ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Muthannaa, amenisimulia Thumaamah bin 'Abdi-Allaah bin Anas: Kwamba Anas (رضي الله عنه) alikuwa akiwaambia wanawe: "Yaa wanangu, ifungeni ilimu hii (kwa maandishi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
508

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ مَهْدِيِّ بْنِ مَيْمُونٍ، عَنْ سَلْمٍ الْعَلَوِيِّ، قَالَ: "رَأَيْتُ أَبَانَ يَكْتُبُ عِنْدَ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ فِي سَبُّورَةٍ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa Mahdiy bin Maymuwn, kutoka kwa Salm Al-'Alawiy, amesema: "Nilimuona Abaan akiandika mbele ya Anas (رضي الله عنه) katika ubao (wa kuandikia)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
509

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، عَنْ مُعَاوِيَةَ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ جَابِرٍ، أَنَّهُ سَأَلَ أَبَا أُمَامَةَ الْبَاهِلِيَّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ كِتَابِ الْعِلْمِ، فَقَالَ: "لَا بَأْسَ بِذَلِكَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Iysaa, ametusimulia Ibn Wahb, kutoka kwa Mu'aawiyah, kutoka kwa Al-Hasan bin Jaabir, kwamba alimuuliza Abuw Umaamah Al-Baahiliy (رضي الله عنه) kuhusu kuandika ilimu; akasema: "Hakuna ubaya kwa hilo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
510

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا مُعَاذٌ، حَدَّثَنَا عِمْرَانُ بْنُ حُدَيْرٍ، عَنْ أَبِي مِجْلَزٍ، عَنْ بَشِيرِ بْنِ نَهِيكٍ، قَالَ: كُنْتُ أَكْتُبُ مَا أَسْمَعُ مِنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَلَمَّا أَرَدْتُ أَنْ أُفَارِقَهُ، "أَتَيْتُهُ بِكِتَابِهِ، فَقَرَأْتُهُ عَلَيْهِ، وَقُلْتُ لَهُ: هَذَا سَمِعْتُ مِنْكَ؟، قَالَ: نَعَمْ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Mu'aadh, ametusimulia 'Imraan bin Hudayr, kutoka kwa Abuw Mijlaz, kutoka kwa Bashiyr bin Nahiyk, amesema: Nilikuwa nikiandika ninayoyasikia kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه). Nilipotaka kuachana naye, "nilimjia na kitabu chake, nikakisoma kwake, na nikamwambia: Haya nimeyasikia kutoka kwako? Akasema: Ndiyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
511

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ طَارِقِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: كُنْتُ أَسْمَعُ مِنْ ابْنِ عُمَرَ، وَابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا "الْحَدِيثَ بِاللَّيْلِ فَأَكْتُبُهُ فِي وَاسِطَةِ الرَّحْلِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Twaariq bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: "Nilikuwa nikisikia kutoka kwa Ibn 'Umar na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) Hadiyth usiku, nikaiandika katika ubao wa katikati wa tandiko (la ngamia)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
431
Hadiyth
512

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "مَا يُرَغِّبُنِي فِي الْحَيَاةِ إِلَّا الصَّادِقَةُ وَالْوَهْطُ، فَأَمَّا الصَّادِقَةُ، فَصَحِيفَةٌ كَتَبْتُهَا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَمَّا الْوَهْطُ، فَأَرْضٌ تَصَدَّقَ بِهَا عَمْرُو بْنُ الْعَاصِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ كَانَ يَقُومُ عَلَيْهَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: "Hakuna kinachonivutia katika maisha isipokuwa As-Swaadiqah (iliyo ya kweli) na Al-Wahtw (ardhi huko Twaaif). Ama As-Swaadiqah, ni karatasi niliyoiandika kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); na ama Al-Wahtw, ni ardhi aliyoitoa swadaka 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنه), alikuwa akiisimamia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
436
Hadiyth
513

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، أَخْبَرَنِي ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ عَمِّهْ عَمْرِو بْنِ أَبِي سُفْيَانَ، أَنَّهُ سَمِعَ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ، يَقُولُ: "قَيِّدُوا الْعِلْمَ بِالْكِتَابِ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, amenikhabarisha Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Sufyaan, kutoka kwa ammi yake 'Amr bin Abiy Sufyaan, kwamba alimsikia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه) akisema: "Ifungeni ilimu kwa maandishi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
437
Hadiyth
514

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عَبْدُ الْمَلِكِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي سُفْيَانَ الثَّقَفِيُّ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا أَنَّهُ، قَالَ: "قَيِّدُوا هَذَا الْعِلْمَ بِالْكِتَابِ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, ametusimulia Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha 'Abdul-Malik bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Sufyaan Ath-Thaqafiy, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba yeye amesema: "Ifungeni ilimu hii kwa maandishi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
437
Hadiyth
515

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ، حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ حَكِيمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ، يَقُولُ: "كُنْتُ أَسِيرُ مَعَ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ فِي طَرِيقِ مَكَّةَ لَيْلًا، وَكَانَ يُحَدِّثُنِي بِالْحَدِيثِ فَأَكْتُبُهُ فِي وَاسِطَةِ الرَّحْلِ حَتَّى أُصْبِحَ فَأَكْتُبَهُ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia 'Abdul-Waahid, ametusimulia 'Uthmaan bin Hakiym, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin Jubayr akisema: "Nilikuwa nikienda pamoja na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) katika njia ya Makkah usiku, naye alikuwa akinisimulia Hadiyth, nami nikiiandika katika ubao wa katikati wa tandiko (la ngamia), mpaka kunapopambazuka, nikaiandika (upya)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
516

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ يَعْقُوبَ الْقُمِّيِّ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ أَبِي الْمُغِيرَةِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: "كُنْتُ أَكْتُبُ عِنْدَ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي صَحِيفَةٍ، وَأَكْتُبُ فِي نَعْلَيَّ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Ya'quwb Al-Qummiy, kutoka kwa Ja'far bin Abil-Mughiyrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: "Nilikuwa nikiandika mbele ya Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) katika karatasi, na nikiandika katika viatu vyangu viwili."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
517

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا مَنْدَلُ بْنُ عَلِيٍّ الْعَنَزِيُّ، حَدَّثَنِي جَعْفَرُ بْنُ أَبِي الْمُغِيرَةِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: "كُنْتُ أَجْلِسُ إِلَى ابْنِ عَبَّاسٍ فَأَكْتُبُ فِي الصَّحِيفَةِ حَتَّى تَمْتَلِئَ، ثُمَّ أَقْلِبُ نَعْلَيَّ فَأَكْتُبُ فِي ظُهُورِهِمَا"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Mandal bin 'Aliy Al-'Anaziy, amenisimulia Ja'far bin Abil-Mughiyrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: "Nilikuwa nikiketi kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), nikaandika katika karatasi mpaka ijae; kisha nikageuza viatu vyangu viwili, nikaandika juu ya migongo yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
518

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا فُضَيْلٌ، عَنْ عُبَيْدٍ الْمُكْتِبِ، قَالَ: "رَأَيْتُهُمْ يَكْتُبُونَ التَّفْسِيرَ عِنْدَ مُجَاهِدٍ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Fudhwayl, kutoka kwa 'Ubayd Al-Muktib, amesema: "Niliwaona wakiandika Tafsiyr (ufafanuzi wa Qur-aan) mbele ya Mujaahid."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
519

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا وَكِيعٌ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ حَنَشٍ، قَالَ: "رَأَيْتُهُمْ يَكْتُبُونَ عِنْدَ الْبَرَاءِ بِأَطْرَافِ الْقَصَبِ عَلَى أَكُفِّهِمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari Wakiy', ametusimulia baba yangu, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Hanash, amesema: "Niliwaona wakiandika mbele ya Al-Baraa (رضي الله عنه) kwa ncha za mianzi juu ya viganja vyao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
520

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ ابْنِ إِدْرِيسَ، عَنْ هَارُونَ بْنِ عَنْتَرَةَ، عَنْ أَبِيهِ، حَدَّثَنِي ابْنُ عَبَّاسٍ بِحَدِيثٍ، فَقُلْتُ: أَكْتُبُهُ عَنْكَ؟، قَالَ: "فَرَخَّصَ لِي وَلَمْ يَكَدْ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Ibn Idriys, kutoka kwa Haaruwn bin 'Antarah, kutoka kwa baba yake, (amesema): Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alinisimulia Hadiyth; nikasema: Niiandike kutoka kwako? Akasema: "Akaniruhusu, na nusura asiniruhusu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
521

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ شُعَيْبِ بْنِ شَابُورٍ، أَنْبَأَنَا الْوَلِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ بْنِ أَبِي السَّائِبِ، عَنْ رَجَاءِ بْنِ حَيْوَةَ، أَنَّهُ حَدَّثَهُ، قَالَ: كَتَبَ هِشَامُ بْنُ عَبْدِ الْمَلِكِ إِلَى عَامِلِهِ أَنْ يَسْأَلَنِي عَنْ حَدِيثٍ، قَالَ رَجَاءٌ: "فَكُنْتُ قَدْ نَسِيتُهُ لَوْلَا أَنَّهُ كَانَ عِنْدِي مَكْتُوبًا"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', amenisimulia Muhammad bin Shu'ayb bin Shaabuwr, ametupa khabari Al-Waliyd bin Sulaymaan bin Abis-Saaib, kutoka kwa Rajaa bin Haywah, kwamba alimsimulia, amesema: Hishaam bin 'Abdil-Malik alimwandikia liwali wake kwamba aniulize kuhusu Hadiyth moja. Rajaa amesema: "Ningekuwa nimeisahau, lau isingekuwa kwamba ilikuwa kwangu imeandikwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
522

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ شُعَيْبٍ، أَخْبَرَنَا هِشَامُ بْنُ الْغَازِ، قَالَ: "كَانَ يُسْأَلُ عَطَاءُ بْنُ أَبِي رَبَاحٍ، وَيُكْتَبُ مَا يُجِيبَ فِيهِ بَيْنَ يَدَيْهِ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', amenikhabarisha Muhammad bin Shu'ayb, ametukhabarisha Hishaam bin Al-Ghaaz, amesema: "'Atwaa bin Abiy Rabaah alikuwa akiulizwa, na yakiandikwa mbele yake yale anayoyajibu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
523

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ شُعَيْبِ بْنِ شَابُورٍ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ بْنِ أَبِي السَّائِبِ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى "أَنَّهُ رَأَى نَافِعًا مَوْلَى ابْنِ عُمَرَ، يُمْلِي عِلْمَهُ، وَيُكْتَبُ بَيْنَ يَدَيْهِ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', ametukhabarisha Muhammad bin Shu'ayb bin Shaabuwr, ametusimulia Al-Waliyd bin Sulaymaan bin Abis-Saaib, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa: "Kwamba yeye alimuona Naafi', mawlaa (mwachwa huru) wa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), akiisomea (watu) ilimu yake (waiandike), na ikiandikwa mbele yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
524

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنَا الْمُبَارَكُ بْنُ سَعِيدٍ، قَالَ: "كَانَ سُفْيَانُ يَكْتُبُ الْحَدِيثَ بِاللَّيْلِ فِي الْحَائِطِ، فَإِذَا أَصْبَحَ نَسَخَهُ ثُمَّ حَكَّهُ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', ametusimulia Al-Mubaarak bin Sa'iyd, amesema: "Sufyaan alikuwa akiandika Hadiyth usiku ukutani; asubuhi ilipofika, aliiandika nakala yake, kisha akaikwangua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
438
Hadiyth
525

أَخْبَرَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو غِفَارٍ الْمُثَنَّى بْنُ سَعْدٍ الطَّائِيُّ، حَدَّثَنِي عَوْنُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قُلْتُ لِعُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ: حَدَّثَنِي فُلَانٌ رَجُلٌ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَعَرَفَهُ عُمَرُ، قُلْتُ: حَدَّثَنِي أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِنَّ الْحَيَاءَ وَالْعَفَافَ وَالْعِيَّ عِيَّ اللِّسَانِ لَا عِيَّ الْقَلْبِ وَالْفِقْهَ مِنْ الْإِيمَانِ، وَهُنَّ مِمَّا يَزِدْنَ فِي الْآخِرَةِ، وَيُنْقِصْنَ مِنْ الدُّنْيَا، وَمَا يَزِدْنَ فِي الْآخِرَةِ أَكْثَرُ، وَإِنَّ الْبَذَاءَ وَالْجَفَاءَ وَالشُّحَّ مِنْ النِّفَاقِ، وَهُنَّ مِمَّا يَزِدْنَ فِي الدُّنْيَا، وَيُنْقِصْنَ فِي الْآخِرَةِ، وَمَا يُنْقِصْنَ فِي الْآخِرَةِ أَكْثَرُ"،

Ametukhabarisha Al-Husayn bin Manswuwr, ametusimulia Abuw Usaamah, ametusimulia Abuw Ghifaar Al-Muthannaa bin Sa'd Atw-Twaaiy, amenisimulia 'Awn bin 'Abdi-Allaah, amesema: Nilimwambia 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz: Amenisimulia fulani (رضي الله عنه) — mtu mmoja miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, na 'Umar akamjua. Nikasema: Alinisimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika hayaa, na kujizuia (na yasiyofaa), na kushindwa kusema — kushindwa kwa ulimi, si kushindwa kwa moyo —, na Fiqh (ufahamu wa Dini) ni katika imaan. Na hayo ni miongoni mwa yanayozidisha katika Aakhirah na kupunguza katika dunia; na yanayozidisha katika Aakhirah ni mengi zaidi. Na hakika maneno machafu, na ukavu (wa tabia), na ubakhili ni katika unafiki. Na hayo ni miongoni mwa yanayozidisha katika dunia na kupunguza katika Aakhirah; na yanayopunguza katika Aakhirah ni mengi zaidi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
441
Hadiyth
526

أَخْبَرَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، حَدَّثَنِي سُلَيْمَانُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، قَالَ: قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: خَرَجَ عَلَيْنَا عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ لِصَلَاةِ الظُّهْرِ، وَمَعَهُ قِرْطَاسٌ ثُمَّ خَرَجَ عَلَيْنَا لِصَلَاةِ الْعَصْرِ، وَهُوَ مَعَهُ، فَقُلْتُ لَهُ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، مَا هَذَا الْكِتَابُ؟، قَالَ: "هَذَا حَدِيثٌ حَدَّثَنِي بِهِ عَوْنُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، فَأَعْجَبَنِي فَكَتَبْتُهُ"، فَإِذَا فِيهِ هَذَا الْحَدِيثُ

Ametukhabarisha Al-Husayn bin Manswuwr, ametusimulia Abuw Usaamah, amenisimulia Sulaymaan bin Al-Mughiyrah, amesema: Abuw Qilaabah amesema: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz alitutokea kwa ajili ya Swalaah ya Adhuhuri, akiwa na karatasi; kisha akatutokea kwa ajili ya Swalaah ya Alasiri, nayo ikiwa pamoja naye. Nikamwambia: Yaa Amiri wa Waumini, ni maandishi gani haya? Akasema: "Hii ni Hadiyth aliyonisimulia 'Awn bin 'Abdi-Allaah; ikanipendeza, nikaiandika." Na ghafla ndani yake imo Hadiyth hii.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
442
Hadiyth
527

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا مَسْعُودٌ، عَنْ يُونُسَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي فَرْوَةَ، عَنْ شُرَحْبِيلَ أَبِي سَعْدٍ، قَالَ: دَعَا الْحَسَنُ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ بَنِيهِ وَبَنِي أَخِيهِ، فَقَالَ: "يَا بَنِيَّ وَبَنِي أَخِي، إِنَّكُمْ صِغَارُ قَوْمٍ يُوشِكُ أَنْ تَكُونُوا كِبَارَ آخَرِينَ، فَتَعَلَّمُوا الْعِلْمَ، فَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ مِنْكُمْ أَنْ يَرْوِيَهُ، أَوْ قَالَ: يَحْفَظَهُ فَلْيَكْتُبْهُ، وَلْيَضَعْهُ فِي بَيْتِهِ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Mas'uwd, kutoka kwa Yuwnus bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Farwah, kutoka kwa Shurahbiyl Abuw Sa'd, amesema: Al-Hasan [bin 'Aliy] (رضي الله عنه) aliwaita wanawe na wana wa ndugu yake, akasema: "Yaa wanangu na wana wa ndugu yangu, hakika nyinyi ni wadogo wa kaumu (moja), mnakaribia kuwa wakubwa wa (kaumu) nyingine; basi jifunzeni ilimu. Na yeyote miongoni mwenu asiyeweza kuipokea (na kuisimulia) — au alisema: kuihifadhi —, basi aiandike na aiweke nyumbani kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
443
Hadiyth
528

44-Mlangoباب من سن سنة حسنة أو سيئةMlango Wa Aliyeanzisha Desturi Nzuri Au Mbaya

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ، عَنْ شَقِيقٍ، عَنْ جَرِيرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ سَنَّ سُنَّةً حَسَنَةً عُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ، كَانَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يُنْقَصَ مِنْ أَجْرِهِ شَيْءٌ، وَمَنْ سَنَّ سُنَّةً سَيِّئَةً، كَانَ عَلَيْهِ مِثْلُ وِزْرِ مَنْ يَعْمَلُ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يُنْقَصَ مِنْ أَوْزَارِهِمْ شَيْءٌ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, ametusimulia 'Aaswim, kutoka kwa Shaqiyq, kutoka kwa Jariyr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeanzisha desturi nzuri, ikafanywa baada yake, atapata mfano wa ujira wa atakayeifanya, bila kupungua chochote katika ujira wake (mfanyaji huyo). Na atakayeanzisha desturi mbaya, atakuwa na mfano wa mzigo wa dhambi wa atakayeifanya, bila kupungua chochote katika mizigo yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
443
Hadiyth
529

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ جَعْفَرٍ، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَعْقُوبَ مَوْلَى الْحُرَقَةِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى، كَانَ لَهُ مِنْ الْأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ اتَّبَعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلَالَةٍ، كَانَ عَلَيْهِ مِنْ الْإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئًا"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', ametusimulia Ismaa'iyl bin Ja'far, kutoka kwa Al-'Alaa bin 'Abdir-Rahmaan bin Ya'quwb, mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Huraqah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayelingania kwenye uongofu, atapata ujira mfano wa ujira wa wale waliomfuata; hilo halipunguzi chochote katika ujira wao. Na atakayelingania kwenye upotofu, atakuwa na dhambi mfano wa dhambi za wale waliomfuata; hilo halipunguzi chochote katika dhambi zao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
443
Hadiyth
530

أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ بْنُ شُجَاعٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ مُسْلِمٍ يَعْنِي ابْنَ صُبَيْحٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ هِلَالٍ الْعَبْسِيِّ، عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَحَثَّ النَّاسَ عَلَى الصَّدَقَةِ، فَأَبْطَئُوا حَتَّى بَانَ فِي وَجْهِهِ الْغَضَبُ"، ثُمَّ إِنَّ رَجُلًا مِنْ الْأَنْصَارِ جَاءَ بِصُرَّةٍ، فَتَتَابَعَ النَّاسُ حَتَّى رُئِيَ فِي وَجْهِهِ السُّرُورُ، فَقَالَ: "مَنْ سَنَّ سُنَّةً حَسَنَةً، كَانَ لَهُ أَجْرُهُ، وَمِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يُنْقَصَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ، وَمَنْ سَنَّ سُنَّةً سَيِّئَةً، كَانَ عَلَيْهِ وِزْرُهُ، وَمِثْلُ وِزْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا مِنْ غَيْرِ أَنْ يُنْقَصَ مِنْ أَوْزَارِهِمْ شَيْءٌ"

Ametukhabarisha Al-Waliyd bin Shujaa', ametusimulia Abuw Mu'aawiyah, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Muslim — yaani Ibn Swubayh —, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Hilaal Al-'Absiy, kutoka kwa Jariyr bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitukhutubia, akawahimiza watu kutoa swadaka; wakachelewa, mpaka ghadhabu ikadhihirika usoni mwake. Kisha mtu mmoja wa Answaar (رضي الله عنهم) akaja na kifuko (cha mali), na watu wakafuatana (kutoa), mpaka furaha ikaonekana usoni mwake. Akasema: "Atakayeanzisha desturi nzuri, atapata ujira wake, na mfano wa ujira wa atakayeifanya, bila kupungua chochote katika ujira wao. Na atakayeanzisha desturi mbaya, atakuwa na mzigo wake wa dhambi, na mfano wa mzigo wa dhambi wa atakayeifanya, bila kupungua chochote katika mizigo yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
444
Hadiyth
531

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي حَسَّانُ بْنُ عَطِيَّةَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "أَنَا أَعْظَمُكُمْ أَجْرًا يَوْمَ الْقِيَامَةِ، لِأَنَّ لِي أَجْرِي وَمِثْلَ أَجْرِ مَنْ اتَّبَعَنِي"

Ametukhabarisha 'Abdul-Wahhaab bin Sa'iyd, ametusimulia Shu'ayb — naye ni Ibn Is-haaq —, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Hassaan bin 'Atwiyyah, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mimi ni mwenye ujira mkubwa zaidi kuliko nyinyi Siku ya Qiyaamah, kwa sababu mimi nina ujira wangu, na mfano wa ujira wa aliyenifuata."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
445
Hadiyth
532

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا عَبْدُ السَّلَامِ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ بِشْرٍ، عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ دَعَا إِلَى أَمْرٍ وَلَوْ دَعَا رَجُلٌ رَجُلًا، كَانَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَوْقُوفًا بِهِ، لَازِمًا بِغَارِبِهِ، ثُمَّ قَرَأَ: {وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ}"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia 'Abdus-Salaam, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Bishr, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayelingania kwenye jambo — hata kama ni mtu aliyemlingania mtu (mmoja) —, atakuwa Siku ya Qiyaamah amesimamishwa pamoja naye, akiwa amemganda (ameshikilia) bega lake." Kisha akasoma:

وَقِفُوهُمْ إِنَّهُمْ مَسْئُولُونَ

Wasimamisheni. Hakika wao wataulizwa. [Asw-Swaaffaat (37:24)]

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
445
Hadiyth
533

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "أَرْبَعٌ يُعْطَاهَا الرَّجُلُ بَعْدَ مَوْتِهِ: ثُلُثُ مَالِهِ إِذَا كَانَ فِيهِ قَبْلَ ذَلِكَ لِلَّهِ مُطِيعًا، وَالْوَلَدُ الصَّالِحُ يَدْعُو لَهُ مِنْ بَعْدِ مَوْتِهِ، وَالسُّنَّةُ الْحَسَنَةُ يَسُنُّهَا الرَّجُلُ فَيُعْمَلُ بِهَا بَعْدَ مَوْتِهِ، وَالْمِائَةُ إِذَا شَفَعُوا لِلرَّجُلِ شُفِّعُوا فِيهِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Aaswim, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Mambo manne mtu hupewa baada ya kufa kwake: theluthi ya mali yake, ikiwa kabla ya hapo alikuwa mtiifu kwa Allaah katika (mali) hiyo; na mtoto mwema anayemuombea Du'aa baada ya kufa kwake; na desturi nzuri anayoianzisha mtu, kisha ikafanywa baada ya kufa kwake; na (watu) mia, wanapomuombea mtu, hukubaliwa maombezi yao kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
445
Hadiyth
534

45-Mlangoباب من كره الشهرة والمعرفةMlango Wa Aliyechukia Umaarufu Na Kujulikana

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ الْحَجَّاجِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: "جَهَدْنَا بِإِبْرَاهِيمَ أَنْ نُجْلِسَهُ إِلَى سَارِيَةٍ، فَأَبَى"

Ametukhabarisha Ahmad bin Al-Hajjaaj, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: "Tulijitahidi sana kwa Ibraahiym tumketishe kwenye nguzo (ya Msikiti, awafundishe watu), akakataa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
446
Hadiyth
535

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ "أَنَّهُ كَانَ يَكْرَهُ أَنْ يَسْتَنِدَ إِلَى السَّارِيَةِ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, kwamba yeye alikuwa "akichukia kuegemea nguzo (ya Msikiti)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
446
Hadiyth
536

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، قَالَ: "كَانَ إِبْرَاهِيمُ لَا يَبْتَدِئُ الْحَدِيثَ حَتَّى يُسْأَلَ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, amesema: "Ibraahiym alikuwa haanzi kusimulia Hadiyth mpaka aulizwe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
446
Hadiyth
537

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ خَيْثَمَةَ، قَالَ: كَانَ الْحَارِثُ بْنُ قَيْسٍ الْجُعْفِيُّ وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ عَبْدِ اللَّهِ، وَكَانُوا مُعْجَبِينَ بِهِ، "فَكَانَ يَجْلِسُ إِلَيْهِ الرَّجُلُ وَالرَّجُلَانِ فَيُحَدِّثُهُمَا، فَإِذَا كَثُرُوا، قَامَ وَتَرَكَهُمْ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Yuwnus bin Bukayr, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Khaythamah, amesema: "Al-Haarith bin Qays Al-Ju'fiy — naye alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), na walikuwa wakipendezwa naye —, alikuwa anapokaa kwake mtu mmoja au watu wawili, huwasimulia; na wanapokuwa wengi, husimama na kuwaacha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
446
Hadiyth
538

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، قَالَ: قِيلَ لَهُ حِينَ مَاتَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: لَوْ قَعَدْتَ فَعَلَّمْتَ النَّاسَ السُّنَّةَ؟، فَقَالَ: "أَتُرِيدُونَ أَنْ يُوطَأَ عَقِبِي؟"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, amesema: Aliambiwa, alipofariki 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه): Lau ungekaa ukawafundisha watu Sunnah? Akasema: "Je, mnataka nyayo zangu zikanyagwe (kwa kufuatwa nyuma na watu)?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
447
Hadiyth
539

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، قَالَ: سَمِعْتُ هَارُونَ بْنَ عَنْتَرَةَ، عَنْ سُلَيْمِ بْنِ حَنْظَلَةَ، قَالَ: أَتَيْنَا أُبَيَّ بْنَ كَعْبٍ لِنَتَحَدَّثَ إِلَيْهِ، فَلَمَّا قَامَ قُمْنَا، وَنَحْنُ نَمْشِي خَلْفَهُ، فَرَهَقَنَا عُمَرُ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ، فَتَبِعَهُ فَضَرَبَهُ عُمَرُ بِالدِّرَّةِ، قَالَ: فَاتَّقَاهُ بِذِرَاعَيْهِ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، مَا نَصْنَعُ؟، قَالَ: "أَوَ مَا تَرَى؟ فِتْنَةً لِلْمَتْبُوعِ، مَذَلَّةً لِلتَّابِعِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Ibn Idriys, amesema: Nilimsikia Haaruwn bin 'Antarah, kutoka kwa Sulaym bin Handhwalah, amesema: Tulimwendea Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه) ili tuzungumze naye. Aliposimama, tukasimama, nasi tukitembea nyuma yake. 'Umar (رضوان الله عليه) akatufikia, akamfuata, na 'Umar (رضي الله عنه) akampiga kwa mjeledi. Akasema: (Ubayy) akajikinga nao kwa mikono yake miwili, akasema: Yaa Amiri wa Waumini, tunafanya nini? Akasema: "Au huoni? (Hii ni) fitna kwa anayefuatwa, na udhalili kwa mfuataji."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
540

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ قَالَ: "كَانُوا يَكْرَهُونَ أَنْ تُوطَأَ أَعْقَابُهُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Walikuwa wakichukia nyayo zao zikanyagwe (kwa kufuatwa nyuma na watu)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
541

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ بِسْطَامِ بْنِ مُسْلِمٍ، قَالَ: كَانَ مُحَمَّدُ بْنُ سِيرِينَ إِذَا مَشَى مَعَهُ الرَّجُلُ قَامَ، فَقَالَ: "أَلَكَ حَاجَةٌ؟ فَإِنْ كَانَتْ لَهُ حَاجَةٌ، قَضَاهَا، وَإِنْ عَادَ يَمْشِي مَعَهُ قَامَ، فَقَالَ: أَلَكَ حَاجَةٌ؟"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Bistwaam bin Muslim, amesema: Muhammad bin Siyriyn alikuwa anapotembea pamoja naye mtu, husimama, akasema: "Je, una haja? Ikiwa ana haja, huitimiza; na akirudi kutembea pamoja naye, husimama, akasema: Je, una haja?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
542

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنُ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "إِيَّاكُمْ أَنْ تُوطَأَ أَعْقَابُكُمْ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan bin Swaalih, kutoka kwa Abuw Hamzah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Tahadharini nyayo zenu zisikanyagwe (kwa kufuatwa nyuma na watu)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
543

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْهَيْثَمِ، عَنْ عَاصِمِ بْنِ ضَمْرَةَ أَنَّهُ رَأَى أُنَاسًا يَتْبَعُونَ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْر، قَالَ: فَأُرَاهُ قَالَ: نَهَاهُمْ، وَقَالَ: "إِنَّ صَنِيعَكُمْ هَذَا أَوْ مَشْيَكُمْ هَذَا مَذَلَّةٌ لِلتَّابِعِ، وَفِتْنَةٌ لِلْمَتْبُوعِ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Hajjaaj bin Muhammad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Haytham, kutoka kwa 'Aaswim bin Dhwamrah, kwamba yeye aliwaona watu wakimfuata Sa'iyd bin Jubayr. Akasema (mpokezi): Nadhani alisema: Akawakataza, na akasema: "Hakika kitendo chenu hiki — au: kutembea kwenu huku — ni udhalili kwa mfuataji, na fitna kwa anayefuatwa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
544

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا حُمَيْدُ بْنُ أَسْوَدَ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، قَالَ: "شَاوَرْتُ مُحَمَّدًا فِي بِنَاءٍ أَرَدْتُ أَنْ أَبْنِيَهُ فِي الْكَلَّاءِ، قَالَ: فَأَشَارَ عَلَيَّ، وَقَالَ: إِذَا أَرَدْتَ أَسَاسَ الْبِنَاءِ فَآذِنِّي حَتَّى أَجِيءَ مَعَكَ، قَالَ: فَأَتَيْتُهُ، قَالَ: فَبَيْنَمَا نَحْنُ نَمْشِي إِذْ جَاءَ رَجُلٌ فَمَشَى مَعَهُ، فَقَامَ، فَقَالَ: أَلَكَ حَاجَةٌ؟، قَالَ: لَا، قَالَ: أَمَّا لَا، فَاذْهَبْ، ثُمَّ أَقْبَلَ عَلَيَّ، فَقَالَ: أَنْتَ أَيْضًا فَاذْهَبْ، قَالَ: فَذَهَبْتُ حَتَّى خَالَفْتُ الطَّرِيقَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, ametusimulia Humayd bin Aswad, kutoka kwa Ibn 'Awn, amesema: "Nilimtaka shauri Muhammad [bin Siyriyn] kuhusu jengo nililotaka kulijenga huko Al-Kallaa (mahali katika Al-Baswrah). Akasema: Akanipa shauri, na akasema: Utakapotaka (kuweka) msingi wa jengo, nijulishe ili nije pamoja nawe. Akasema: Nikamwendea. Akasema: Basi tulipokuwa tukitembea, ghafla akaja mtu, akatembea pamoja naye. Akasimama, akasema: Je, una haja? Akasema: Hapana. Akasema: Ama ikiwa hapana, basi nenda. Kisha akanielekea, akasema: Na wewe pia nenda. Akasema: Nikaenda mpaka nikashika njia nyingine."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
545

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ الْحَجَّاجِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَهْدِيٍّ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ نُسَيْرٍ، أَنَّ الرَّبِيعَ كَانَ إِذَا أَتَوْهُ، يَقُولُ: "أَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ شَرِّكُمْ"، يَعْنِي: أَصْحَابَهُ

Ametukhabarisha Ahmad bin Al-Hajjaaj, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Nusayr, kwamba Ar-Rabiy' alikuwa wanapomjia, husema: "Najikinga kwa Allaah kutokana na shari yenu" — yaani: wanafunzi wake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
546

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ رَجَاءٍ الْأَنْصَارِيِّ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ بِشْرٍ، قَالَ: كُنَّا عِنْدَ خَبَّابِ بْنِ الْأَرَتِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَاجْتَمَعَ إِلَيْهِ أَصْحَابُهُ وَهُوَ سَاكِتٌ، فَقِيلَ لَهُ: أَلَا تُحَدِّثُ أَصْحَابَكَ؟، قَالَ: "أَخَافُ أَنْ أَقُولَ لَهُمْ مَا لَا أَفْعَلُ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Rajaa Al-Answaariy, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Bishr, amesema: Tulikuwa kwa Khabbaab bin Al-Aratt (رضي الله عنه); wenzake wakakusanyika kwake, naye akiwa kimya. Akaambiwa: Je, huwasimulii wenzako? Akasema: "Ninaogopa kuwaambia yale nisiyoyafanya."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
547

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ صَالِحٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الشَّعْبِيَّ، قَالَ: "وَدِدْتُ أَنِّي نَجَوْتُ مِنْ عَمَلِي كَفَافًا لَا لِي وَلَا عَلَيَّ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Swaalih, amesema: Nilimsikia Ash-Sha'biy akisema: "Natamani lau ningeokoka katika amali yangu kwa kulingana sawa: si (thawabu) kwangu, wala si (dhambi) juu yangu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
548

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ الْحَسَنِ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ كَانَ يَمْشِي وَنَاسٌ يَطَئُونَ عَقِبَهُ، فَقَالَ: "لَا تَطَئُوا عَقِبِي، فَوَاللَّهِ لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أُغْلِقُ عَلَيْهِ بَابِي، مَا تَبِعَنِي رَجُلٌ مِنْكُمْ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Ibn 'Awn, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa akitembea na watu wakikanyaga nyayo zake (wakimfuata nyuma). Akasema: "Msikanyage nyayo zangu; kwani Wa-Allaahi, lau mngejua ninayoyafungia mlango wangu, asingenifuata mtu yeyote miongoni mwenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
549

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: "فِتْنَةٌ لِلْمَتْبُوعِ، مَذَلَّةٌ لِلتَّابِعِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: "(Kufuatwa nyuma ni) fitna kwa anayefuatwa, na udhalili kwa mfuataji."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
550

أَخْبَرَنَا شِهَابُ بْنُ عَبَّادٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أُمَيٍّ، قَالَ: مَشَوْا خَلْفَ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، فَقَالَ: "عَنِّي خَفْقَ نِعَالِكُمْ، فَإِنَّهَا مُفْسِدَةٌ لِقُلُوبِ نَوْكَى الرِّجَالِ"

Ametukhabarisha Shihaab bin 'Abbaad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Umayy, amesema: Walitembea nyuma ya 'Aliy (رضي الله عنه); akasema: "Niondoleeni mlio wa viatu vyenu, kwani huo unaharibu nyoyo za wapumbavu miongoni mwa wanaume."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
551

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ، يَقُولُ: "إِنَّ خَفْقَ النِّعَالِ خَلْفَ الرِّجَالِ قَلَّ مَا يُلَبِّثُ الْحَمْقَى"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yaziyd bin Haazim, amesema: Nilimsikia Al-Hasan akisema: "Hakika mlio wa viatu nyuma ya watu, ni nadra kuwaacha wapumbavu (wakabaki katika hali yao)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
552

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حَاتِمٍ الْمُكْتِبُ، حَدَّثَنَا قَاسِمُ هُوَ ابْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا لَيْثٌ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: "كَانَ إِذَا جَلَسَ إِلَيْهِ الرَّجُلُ أَوْ الرَّجُلَانِ، قَامَ فَتَنَحَّى"

Ametukhabarisha Muhammad bin Haatim Al-Muktib, ametusimulia Qaasim — naye ni Ibn Maalik —, ametusimulia Layth, kutoka kwa Twaawuws, amesema: "Alikuwa anapokaa kwake mtu mmoja au watu wawili, husimama na kujitenga."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
448
Hadiyth
553

أَخْبَرَنَا أَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الْأَسْلَمِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ عُمُرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ، وَعَنْ عِلْمِهِ مَا فَعَلَ بِهِ، وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ وَفِيمَا أَنْفَقَهُ، وَعَنْ جِسْمِهِ فِيمَا أَبْلَاهُ"

Ametukhabarisha Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Sa'iyd bin 'Abdi-Allaah bin Jurayj, kutoka kwa Abuw Barzah Al-Aslamiy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Miguu miwili ya mja haitaondoka (mahali pake) Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe kuhusu umri wake, ameumaliza katika nini; na kuhusu ilimu yake, ameifanyia nini; na kuhusu mali yake, ameichuma wapi, na ameitumia katika nini; na kuhusu mwili wake, ameuchakaza katika nini."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
452
Hadiyth
554

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ غَزِيَّةَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ رَاشِدٍ، حَدَّثَنِي فُلَانٌ الْعُرَنِيُّ، عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا يَدَعُ اللَّهُ الْعِبَادَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ حَتَّى يَسْأَلَهُمْ عَنْ أَرْبَعٍ: عَمَّا أَفْنَوْا فِيهِ أَعْمَارَهُمْ، وَعَمَّا أَبْلَوْا فِيهِ أَجْسَادَهُمْ، وَعَمَّا كَسَبُوا وفِيمَا أَنْفَقُوا، وَعَمَّا عَمِلُوا فِيمَا عَلِمُوا"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa 'Umaarah bin Ghaziyyah, kutoka kwa Yahyaa bin Raashid, amenisimulia fulani Al-'Uraniy, kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه), amesema: "Allaah Hatawaacha waja Siku ya Qiyaamah — Siku watakayosimama watu kwa Rabb wa walimwengu — mpaka Awaulize kuhusu (mambo) manne: kuhusu nini wameumaliza umri wao; na kuhusu nini wameichakaza miili yao; na kuhusu walichokichuma, na katika nini wamekitumia; na kuhusu waliyoyafanya katika waliyoyajua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
453
Hadiyth
555

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ عَدِيٍّ، عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ الصُّنَابِحِيِّ، عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "لَا تَزُولُ قَدَمَا عَبْدٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ حَتَّى يُسْأَلَ عَنْ أَرْبَعٍ: عَنْ عُمُرِهِ فِيمَا أَفْنَاهُ، وَعَنْ جَسَدِهِ فِيمَا أَبْلَاهُ، وَعَنْ مَالِهِ مِنْ أَيْنَ اكْتَسَبَهُ، وَفِيمَا وَضَعَهُ، وَعَنْ عِلْمِهِ مَاذَا عَمِلَ فِيهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa 'Adiyy bin 'Adiyy, kutoka kwa Abuw 'Abdi-Allaah Asw-Swunaabihiy, kutoka kwa Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه), amesema: "Miguu miwili ya mja haitaondoka (mahali pake) Siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe kuhusu (mambo) manne: kuhusu umri wake, ameumaliza katika nini; na kuhusu mwili wake, ameuchakaza katika nini; na kuhusu mali yake, ameichuma wapi, na ameiweka katika nini; na kuhusu ilimu yake, amefanya nini kwayo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
453
Hadiyth
556

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ لَيْثٍ، قَالَ: قَالَ لِي طَاوُسٌ: "مَا تَعَلَّمْتَ، فَتَعَلَّمْ لِنَفْسِكَ، فَإِنَّ النَّاسَ قَدْ ذَهَبَتْ مِنْهُمْ الْأَمَانَةُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Layth, amesema: Twaawuws aliniambia: "Ulichojifunza, basi jifunze kwa ajili ya nafsi yako; kwani watu, amana imekwisha kuondoka kwao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
454
Hadiyth
557

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ مِهْرَانَ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "أَدْرَكْتُ النَّاسَ وَالنَّاسِكُ إِذَا نَسَكَ لَمْ يُعْرَفْ مِنْ قِبَلِ مَنْطِقِهِ، وَلَكِنْ يُعْرَفُ مِنْ قِبَلِ عَمَلِهِ، فَذَلِكَ الْعِلْمُ النَّافِعُ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa 'Umaarah bin Mihraan, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Niliwadiriki watu (wakiwa katika hali ambayo) mwenye kujitolea kwa ibaada, anapojitolea kwa ibaada, hajulikani kwa upande wa maneno yake, lakini hujulikana kwa upande wa amali yake. Basi hiyo ndiyo ilimu yenye manufaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
454
Hadiyth
558

46-Mlangoباب البلاغ عن رسول الله صلى الله عليه وسلم، وتعليم السننMlango Wa Kufikisha Kutoka
Kwa Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)
, Na Kufundisha Sunnah

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ حَسَّانَ، عَنْ أَبِي كَبْشَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرٍو رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً، وَحَدِّثُوا عَنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا حَرَجَ، وَمَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Hassaan, kutoka kwa Abuw Kabshah, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Fikisheni kutoka kwangu hata kama ni Aayah moja; na simulieni kutoka kwa Wana wa Israaiyl wala hakuna ubaya; na atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
559

أَخْبَرَنَا عَلِيُّ بْنُ حُجْرٍ السَّعْدِيُّ، أَنْبَأَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْعَوَّامُ بْنُ حَوْشَبٍ أَبُو عِيسَى الشَّيْبَانِيُّ، حَدَّثَنَا الْقَاسِمُ بْنُ عَوْفٍ الشَّيْبَانِيُّ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَنْ لَا يَغْلِبُونَا عَلَى ثَلَاثٍ: أَنْ نَأْمُرَ بِالْمَعْرُوفِ، وَنَنْهَى عَنْ الْمُنْكَرِ، وَنُعَلِّمَ النَّاسَ السُّنَنَ"

Ametukhabarisha 'Aliy bin Hujr As-Sa'diy, ametupa khabari Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-'Awwaam bin Hawshab Abuw 'Iysaa Ash-Shaybaaniy, ametusimulia Al-Qaasim bin 'Awf Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha (kwamba watu) wasitushinde katika mambo matatu: tuamrishe mema, na tukataze maovu, na tuwafundishe watu Sunnah.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
560

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا صَفْوَانُ، حَدَّثَنِي سُلَيْمُ بْنُ عَامِرٍ، قَالَ: كَانَ أَبُو أُمَامَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ إِذَا قَعَدْنَا إِلَيْهِ يَجِيئُنَا مِنْ الْحَدِيثِ بِأَمْرٍ عَظِيمٍ، وَيَقُولُ: "لَنَا اسْمَعُوا وَاعْقِلُوا، وَبَلِّغُوا عَنَّا مَا تَسْمَعُونَ"، قَالَ سُلَيْمٌ: "بِمَنْزِلَةِ الَّذِي يُشْهِدُ عَلَى مَا عَلِمَ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Swafwaan, amenisimulia Sulaym bin 'Aamir, amesema: Abuw Umaamah (رضي الله عنه) alikuwa tunapokaa kwake, hutuletea katika Hadiyth jambo kubwa, na hutuambia: "Sikilizeni na fahamuni, na fikisheni kutoka kwetu mnayoyasikia." Sulaym amesema: "(Hayo ni) kama mfano wa yule anayewashuhudisha (wengine) juu ya alichokijua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
561

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي أَبُو كَثِيرٍ، حَدَّثَنِي أَبِي، قَالَ: أَتَيْتُ أَبَا ذَرٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ وَهُوَ جَالِسٌ عِنْدَ الْجَمْرَةِ الْوُسْطَى، وَقَدْ اجْتَمَعَ النَّاسُ عَلَيْهِ يَسْتَفْتُونَهُ، فَأَتَاهُ رَجُلٌ فَوَقَفَ عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: أَلَمْ تُنْهَ عَنْ الْفُتْيَا؟ فَرَفَعَ رَأْسَهُ إِلَيْهِ، فَقَالَ: "أَرَقِيبٌ أَنْتَ عَلَيَّ؟ لَوْ وَضَعْتُمْ الصَّمْصَامَةَ عَلَى هَذِهِ وَأَشَارَ إِلَى قَفَاهُ، ثُمَّ ظَنَنْتُ أَنِّي أُنْفِذُ كَلِمَةً سَمِعْتُهَا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَبْلَ أَنْ تُجِيزُوا عَلَيَّ لَأَنْفَذْتُهَا"

Ametukhabarisha 'Abdul-Wahhaab bin Sa'iyd, ametusimulia Shu'ayb — naye ni Ibn Is-haaq —, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Abuw Kathiyr, amenisimulia baba yangu, amesema: Nilimwendea Abuw Dharr (رضي الله عنه) naye akiwa amekaa kwenye Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) ya katikati, na watu walikuwa wamekusanyika kwake wakimuuliza Fatwa. Mtu mmoja akamjia, akasimama mbele yake, kisha akasema: Je, hukukatazwa kutoa Fatwa? Akainua kichwa chake kumtazama, akasema: "Je, wewe ni mlinzi juu yangu? Lau mngeweka upanga mkali juu ya hii — na akaashiria kisogo chake —, kisha nikadhani kwamba nitaweza kulifikisha neno moja nililolisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla hamjanimaliza, basi ningelifikisha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
562

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبَّادٌ هُوَ ابْنُ الْعَوَّامِ، عَنْ عَوْفٍ، عَنْ أَبِي الْعَالِيَةِ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا عَنْ شَيْءٍ، فَقَالَ: يَا أَبَا الْعَالِيَةِ، أَتُرِيدُ أَنْ تَكُونَ مُفْتِيًا؟، فَقُلْتُ: "لَا، وَلَكِنْ لَا آمَنُ أَنْ تَذْهَبُوا وَنَبْقَى"، فَقَالَ: "صَدَقَ أَبُو الْعَالِيَةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abbaad — naye ni Ibn Al-'Awwaam —, kutoka kwa 'Awf, kutoka kwa Abul-'Aaliyah, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu jambo fulani. Akasema: Yaa Abal-'Aaliyah, je, unataka kuwa mtoa Fatwa? Nikasema: "Hapana, lakini siamini kwamba mtaondoka (mtafariki), nasi tubakie (bila ilimu)." Akasema: "Amesema kweli Abul-'Aaliyah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
563

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبَّادٌ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "كَانَ عَبِيدَةُ يَأْتِي عَبْدَ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ كُلَّ خَمِيسٍ، فَيَسْأَلُهُ عَنْ أَشْيَاءَ غَابَ عَنْهَا، فَكَانَ عَامَّةُ مَا يُحْفَظُ عَنْ عَبْدِ اللَّهِ مِمَّا يَسْأَلُهُ عَبِيدَةُ عَنْهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abbaad, kutoka kwa Huswayn, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "'Abiydah alikuwa akimwendea 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) kila Alkhamisi, akamuuliza kuhusu mambo yaliyompita (hakuwepo). Basi mengi ya yanayohifadhiwa kutoka kwa 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) ni katika yale aliyokuwa 'Abiydah akimuuliza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
564

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا غَسَّانُ هُوَ ابْنُ مُضَرَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: سَمِعْتُ عِكْرِمَةَ، يَقُولُ: "مَا لَكُمْ لَا تَسْأَلُونِي، أَفْلَسْتُمْ؟"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Ghassaan — naye ni Ibn Mudhwar —, kutoka kwa Sa'iyd bin Yaziyd, amesema: Nilimsikia 'Ikrimah akisema: "Mna nini hamniulizi? Je, mmefilisika?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
565

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حَاتِمٍ الْمُكْتِبُ، حَدَّثَنَا عَامِرُ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ: "الْعِلْمُ خَزَائِنُ، وَتَفْتَحُهَا الْمَسْأَلَةُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Haatim Al-Muktib, ametusimulia 'Aamir bin Swaalih, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: "Ilimu ni hazina, na kinachozifungua ni kuuliza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
566

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ جَرِيرٍ، قَالَ: قَالَ إِبْرَاهِيمُ: "مَنْ رَقَّ وَجْهُهُ، رَقَّ عِلْمُهُ"،

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Is-haaq, kutoka kwa Jariyr, amesema: Ibraahiym amesema: "Ambaye uso wake una haya (ya kuuliza), ilimu yake huwa haba."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
455
Hadiyth
567

أَخْبَرَنَا وَكِيعٌ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "مَنْ رَقَّ وَجْهُهُ، رَقَّ عِلْمُهُ"،

Ametukhabarisha Wakiy', kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Ambaye uso wake una haya (ya kuuliza), ilimu yake huwa haba."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
458
Hadiyth
568

وَعَنْ ضَمْرَةَ، عَنْ حَفْصِ بْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "مَنْ رَقَّ وَجْهُهُ، رَقَّ عِلْمُهُ"

Na kutoka kwa Dhwamrah, kutoka kwa Hafsw bin 'Umar, amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: "Ambaye uso wake una haya (ya kuuliza), ilimu yake huwa haba."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
459
Hadiyth
569

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ جَرِيرٍ، عَنْ رَجُلٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: "لَا يَتَعَلَّمُ مَنْ اسْتَحْيَى وَاسْتَكْبَرَ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Is-haaq, kutoka kwa Jariyr, kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwa Mujaahid, amesema: "Hajifunzi (ilimu) mwenye kuona haya, na mwenye kutakabari."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
459
Hadiyth
570

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ عِيَاضٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ كَانَ يَجْمَعُ بَنِيهِ، فَيَقُولُ: "يَا بَنِيَّ، تَعَلَّمُوا، فَإِنْ تَكُونُوا صِغَارَ قَوْمٍ، فَعَسَى أَنْ تَكُونُوا كِبَارَ آخَرِينَ، وَمَا أَقْبَحَ عَلَى شَيْخٍ يُسْأَلُ لَيْسَ عِنْدَهُ عِلْمٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Anas bin 'Iyaadhw, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kwamba yeye alikuwa akiwakusanya wanawe, akisema: "Yaa wanangu, jifunzeni (ilimu); kwani ikiwa nyinyi ni wadogo wa watu (fulani), huenda mkawa wakubwa wa (watu) wengine. Na ni ubaya ulioje kwa mzee anayeulizwa (jambo), naye hana ilimu!"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
459
Hadiyth
571

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ الزُّبَيْرِ بْنِ الْخِرِّيتِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ: كَانَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا "يَضَعُ فِي رِجْلَيَّ الْكَبْلَ، وَيُعَلِّمُنِي الْقُرْآنَ وَالسُّنَنَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Az-Zubayr bin Al-Khirriyt, kutoka kwa 'Ikrimah, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa "akiniwekea pingu miguuni mwangu, na akinifundisha Qur-aan na Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
460
Hadiyth
572

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ الضُّرَيْسِ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ، يَقُولُ: "مَنْ تَرَأَّسَ سَرِيعًا، أَضَرَّ بِكَثِيرٍ مِنْ الْعِلْمِ، وَمَنْ لَمْ يَتَرَأَّسْ، طَلَبَ وَطَلَبَ حَتَّى يَبْلُغَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Yahyaa bin Adhw-Dhwurays, amesema: Nilimsikia Sufyaan akisema: "Mwenye kujifanya kiongozi haraka, huidhuru sehemu kubwa ya ilimu; na asiyejifanya kiongozi, hutafuta na kutafuta mpaka afikie (daraja)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
460
Hadiyth
573

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ صَالِحِ بْنِ خَبَّابٍ، عَنْ حُصَيْنِ بْنِ عُقْبَةَ، عَنْ سَلْمَانَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَهُ: "عِلْمٌ لَا يُقَالُ بِهِ، كَكَنْزٍ لَا يُنْفَقُ مِنْهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Swaalih bin Khabbaab, kutoka kwa Huswayn bin 'Uqbah, kutoka kwa Salmaan (رضي الله عنه), ameyasema (maneno haya): "Ilimu isiyozungumzwa ni kama hazina isiyotolewa (matumizi) kutoka kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
460
Hadiyth
574

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، حَدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ، عَنْ أَبِي عِيَاضٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَثَلُ عِلْمٍ لَا يُنْتَفَعُ بِهِ، كَمَثَلِ كَنْزٍ لَا يُنْفَقُ مِنْهُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, amenisimulia Ibraahiym, kutoka kwa Abuw 'Iyaadhw, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mfano wa ilimu isiyonufaikiwa nayo, ni kama mfano wa hazina isiyotolewa kutoka kwake (chochote) katika Njia ya Allaah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
460
Hadiyth
575

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ مُوسَى بْنِ يَسَارٍ عَمِّهِ، قَالَ: بَلَغَنِي أَنَّ سَلْمَانَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، كَتَبَ إِلَى أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "إِنَّ الْعِلْمَ كَالْيَنَابِيعِ يَغْشَاهُنَّ النَّاسُ، فَيَخْتَلِجُهُ هَذَا وَهَذَا، فَيَنْفَعُ اللَّهُ بِهِ غَيْرَ وَاحِدٍ، وَإِنَّ حِكْمَةً لَا يُتَكَلَّمُ بِهَا كَجَسَدٍ لَا رُوحَ فِيهِ، وَإِنَّ عِلْمًا لَا يُخْرَجُ كَكَنْزٍ لَا يُنْفَقُ مِنْهُ، وَإِنَّمَا مَثَلُ الْعَالِمِ كَمَثَلِ رَجُلٍ حَمَلَ سِرَاجًا فِي طَرِيقٍ مُظْلِمٍ يَسْتَضِيءُ بِهِ مَنْ مَرَّ بِهِ، وَكُلٌّ يَدْعُو لَهُ بِالْخَيْرِ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Muwsaa bin Yasaar, ami yake, amesema: Imenifikia kwamba Salmaan (رضي الله عنه) alimwandikia Abud-Dardaa (رضي الله عنه): "Hakika ilimu ni kama chemchemi ambazo watu huzijia; huyu na huyu wakaichota, na Allaah Akawanufaisha nayo zaidi ya mmoja. Na hakika hekima isiyozungumzwa ni kama mwili usio na roho ndani yake. Na hakika ilimu isiyotolewa (kwa watu) ni kama hazina isiyotolewa (matumizi) kutoka kwake. Na hakika mfano wa 'Aalim (Mwanazuoni) ni kama mfano wa mtu aliyebeba taa katika njia yenye giza; anapata mwangaza kwayo kila anayempita, na kila mmoja anamuombea kheri."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
461
Hadiyth
576

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا مَنْصُورُ بْنُ أَبِي الْأَسْوَدِ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ حَمَّادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "يَتْبَعُ الرَّجُلَ بَعْدَ مَوْتِهِ ثَلَاثُ خِلَالٍ: صَدَقَةٌ تَجْرِي بَعْدَهُ، وَصَلَاةُ وَلَدِهِ عَلَيْهِ، وَعِلْمٌ أَفْشَاهُ يُعْمَلُ بِهِ بَعْدَهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Manswuwr bin Abil-Aswad, kutoka kwa Abuw Is-haaq Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mambo matatu humfuata mtu baada ya kufa kwake: swadaka inayoendelea baada yake, na Swalaah ya mwanawe juu yake (kumuombea), na ilimu aliyoieneza inayofanyiwa kazi baada yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
462
Hadiyth
577

حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنِي إِسْمَاعِيل بْنُ جَعْفَرٍ الْمَدَنِيُّ، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِذَا مَاتَ الْإِنْسَانُ انْقَطَعَ عَمَلُهُ إِلَّا مِنْ ثَلَاثٍ: عِلْمٍ يُنْتَفَعُ بِهِ، أَوْ صَدَقَةٍ تَجْرِي لَهُ، أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو لَهُ"

Ametusimulia Muwsaa bin Ismaa'iyl, amenisimulia Ismaa'iyl bin Ja'far Al-Madaniy, kutoka kwa Al-'Alaa bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mtu anapokufa, amali yake hukatika isipokuwa kutoka katika (mambo) matatu: ilimu inayonufaisha, au swadaka inayoendelea kwa ajili yake, au mtoto mwema anayemuombea Du'aa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
462
Hadiyth
578

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ بْنُ يَعِيشَ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ صَالِحِ بْنِ رُسْتُمَ الْمُزَنِيِّ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، أَنَّهُ قَالَ حِينَ قَدِمَ الْبَصْرَةَ: "بَعَثَنِي إِلَيْكُمْ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ أُعَلِّمُكُمْ كِتَابَ رَبِّكُمْ، وَسُنَّتَكُمْ، وَأُنَظِّفُ طُرُقَكُمْ"

Ametukhabarisha 'Ubayd bin Ya'iysh, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Swaalih bin Rustum Al-Muzaniy, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), kwamba alisema alipofika Al-Baswrah: "Amenituma kwenu 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه) niwafundishe Kitabu cha Rabb wenu, na Sunnah yenu, na nisafishe njia zenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
462
Hadiyth
579

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُعَلَّى، حَدَّثَنَا زِيَادُ بْنُ خَيْثَمَةَ، عَنْ أَبِي دَاوُدَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَخْبَرَةَ، عَنْ سَخْبَرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ طَلَبَ الْعِلْمَ، كَانَ كَفَّارَةً لِمَا مَضَى"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Muhammad bin Al-Mu'allaa, ametusimulia Ziyaad bin Khaythamah, kutoka kwa Abuw Daawuwd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Sakhbarah, kutoka kwa Sakhbarah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayetafuta ilimu, (kutafuta huko) kunakuwa kafara ya (madhambi) yaliyopita."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
462
Hadiyth
580

47-Mlangoباب الرحلة في طلب العلم، واحتمال العناء فيهMlango Wa Kusafiri
Kwa Ajili Ya Kutafuta Ilimu, Na Kustahamili Taabu Katika Hilo

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: "لَقَدْ أَقَمْتُ بِالْمَدِينَةِ ثَلَاثًا مَا لِي حَاجَةٌ إِلَّا وَقَدْ فَرَغْتُ مِنْهَا، إِلَّا أَنَّ رَجُلًا كَانُوا يَتَوَقَّعُونَهُ، كَانَ يَرْوِي حَدِيثًا، فَأَقَمْتُ حَتَّى قَدِمَ فَسَأَلْتُهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: "Hakika nilikaa Madiynah siku tatu, sina haja yoyote ila nilikuwa nimekwisha kuimaliza, isipokuwa mtu mmoja ambaye walikuwa wakimtarajia (kufika); alikuwa akisimulia Hadiyth (fulani). Basi nikakaa mpaka alipofika, nikamuuliza."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
464
Hadiyth
581

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بنْ مُسِلمٍ، عَنْ عَبْدَ الرَّحْمَنَ بِنْ يزيدٍ بْنِ جَابِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ بُسْرَ بْنَ عُبَيْدِ اللَّهِ، يَقُولُ: "إِنْ كُنْتُ لَأَرْكَبُ إِلَى الْمِصْرِ مِنْ الْأَمْصَارِ فِي الْحَدِيثِ الْوَاحِدِ لِأَسْمَعَهُ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Al-Waliyd bin Muslim, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir, amesema: Nilimsikia Busr bin 'Ubaydi-Allaah akisema: "Hakika nilikuwa nikipanda (kipando) kwenda mji mmoja miongoni mwa miji kwa ajili ya Hadiyth moja, ili niisikie."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
464
Hadiyth
582

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ زُرَارَةَ، أَنْبَأَنَا أَبُو قَطَنٍ عَمْرُو بْنُ الْهَيْثَمِ، عَنْ أَبِي خَلْدَةَ، عَنْ أَبِي الْعَالِيَةِ، قَالَ: "إِنْ كُنَّا نَسْمَعُ الرِّوَايَةَ بِالْبَصْرَةِ عَنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَمْ نَرْضَ حَتَّى رَكِبْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ، فَسَمِعْنَاهَا مِنْ أَفْوَاهِهِمْ"

Ametukhabarisha 'Amr bin Zuraarah, ametupa khabari Abuw Qatwan 'Amr bin Al-Haytham, kutoka kwa Abuw Khaldah, kutoka kwa Abul-'Aaliyah, amesema: "Hakika tulikuwa tukisikia Riwaayah (upokezi) huko Al-Baswrah kutoka kwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), lakini hatukuridhika mpaka tulipopanda (vipando) kwenda Madiynah, tukaisikia kutoka vinywani mwao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
464
Hadiyth
583

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ التُّسْتَرِيِّ، قَالَ: قَالَ دَاوُدُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "قُلْ لِصَاحِبِ الْعِلْمِ يَتَّخِذْ عَصًا مِنْ حَدِيدٍ، وَنَعْلَيْنِ مِنْ حَدِيدٍ، وَيَطْلُبْ الْعِلْمَ، حَتَّى تَنْكَسِرَ الْعَصَا وَتَنْخَرِقَ النَّعْلَانِ"

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia Baqiyyah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan At-Tustariy, amesema: Nabiy Daawuwd (عليه السلام) amesema: "Mwambie mwenye ilimu ajichukulie fimbo ya chuma na viatu viwili vya chuma, na aitafute ilimu mpaka fimbo ivunjike na viatu viwili vitoboke."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
465
Hadiyth
584

أَخْبَرَنَا مَخْلَدُ بْنُ مَالِكٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ الْأُمَوِيُّ، حَدَّثَنَا الْحَجَّاجُ، عَنْ حُصَيْنِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ مِنْ آلِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: "طَلَبْتُ الْعِلْمَ فَلَمْ أَجِدْهُ أَكْثَرَ مِنْهُ فِي الْأَنْصَارِ، فَكُنْتُ آتِي الرَّجُلَ فَأَسْأَلُ عَنْهُ، فَيُقَالُ لِي: نَائِمٌ فَأَتَوَسَّدُ رِدَائِي، ثُمَّ أَضْطَجِعُ حَتَّى يَخْرُجَ إِلَى الظُّهْرِ، فَيَقُولُ: مَتَى كُنْتَ هَاهُنَا يَا ابْنَ عَمِّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، فَأَقُولُ: مُنْذُ طَوِيلٍ، فَيَقُولُ: بِئْسَ مَا صَنَعْتَ، هَلَّا أَعْلَمْتَنِي؟، فَأَقُولُ: أَرَدْتُ أَنْ تَخْرُجَ إِلَيَّ وَقَدْ قَضَيْتَ حَاجَتَكَ"

Ametukhabarisha Makhlad bin Maalik, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd Al-Umawiy, ametusimulia Al-Hajjaaj, kutoka kwa Huswayn bin 'Abdir-Rahmaan — miongoni mwa ukoo wa Sa'd bin Mu'aadh (رضي الله عنه) —, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Niliitafuta ilimu, sikuikuta (mahali) ikiwa nyingi zaidi kuliko kwa Answaar (رضي الله عنهم). Nilikuwa nikimjia mtu, nikamuulizia, nikaambiwa: Amelala. Basi ninaifanya shuka yangu kuwa mto, kisha ninajilaza mpaka anatoka kwenda (Swalaah ya) Adhuhuri. Naye anasema: Ulikuwa hapa tangu lini, yaa mwana wa ami ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Nami ninasema: Tangu muda mrefu. Naye anasema: Ni ubaya ulioje ulioufanya! Kwa nini hukunijulisha? Nami ninasema: Nilitaka unitokee nawe ukiwa umekwisha kumaliza haja yako."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
465
Hadiyth
585

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "وُجِدَ أَكْثَرُ حَدِيثِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ هَذَا الْحَيِّ مِنْ الْأَنْصَارِ، وَاللَّهِ إِنْ كُنْتُ لَآتِي الرَّجُلَ مِنْهُمْ، فَيُقَالُ: هُوَ نَائِمٌ، فَلَوْ شِئْتُ أَنْ يُوقَظَ لِي، فَأَدَعُهُ حَتَّى يَخْرُجَ لِأَسْتَطِيبَ بِذَلِكَ حَدِيثَهُ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Hadiyth nyingi zaidi za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zilipatikana kwa kabila hili la Answaar (رضي الله عنهم). Wa-Allaahi, hakika nilikuwa nikimjia mtu miongoni mwao, nikaambiwa: Amelala. Na lau ningetaka aamshwe kwa ajili yangu, (angeamshwa); lakini ninamwacha mpaka atoke, ili kwa hilo nipate Hadiyth yake (akiwa katika hali nzuri ya moyo)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
466
Hadiyth
586

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: "لَوْ رَفَقْتُ بِابْنِ عَبَّاسٍ، لَأَصَبْتُ مِنْهُ عِلْمًا كَثِيرًا"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Salamah, amesema: "Lau ningemfanyia upole Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), ningepata kutoka kwake ilimu nyingi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
466
Hadiyth
587

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، حَدَّثَنَا مَعْمَرٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "كُنْتُ آتِي بَابَ عُرْوَةَ، فَأَجْلِسُ بِالْبَابِ، وَلَوْ شِئْتُ أَنْ أَدْخُلَ لَدَخَلْتُ، وَلَكِنْ إِجْلَالًا لَهُ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdur-Razzaaq, ametusimulia Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Nilikuwa nikiujia mlango wa 'Urwah, nikakaa mlangoni; na lau ningetaka kuingia, ningeingia; lakini (sikuingia) kwa kumheshimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
467
Hadiyth
588

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنْ يَعْلَى بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "لَمَّا تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قُلْتُ لِرَجُلٍ مِنْ الْأَنْصَارِ: يَا فُلَانُ، هَلُمَّ فَلْنَسْأَلْ أَصْحَابَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَإِنَّهُمْ الْيَوْمَ كَثِيرٌ، فَقَالَ: وَاعَجَبًا لَكَ يَا ابْنَ عَبَّاسٍ، أَتَرَى النَّاسَ يَحْتَاجُونَ إِلَيْكَ وَفِي النَّاسِ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَنْ تَرَى؟ فَتَرَكَ ذَلِكَ، وَأَقْبَلْتُ عَلَى الْمَسْأَلَةِ، فَإِنْ كَانَ لَيَبْلُغُنِي الْحَدِيثُ عَنْ الرَّجُلِ فَآتِيهِ، وَهُوَ قَائِلٌ، فَأَتَوَسَّدُ رِدَائِي عَلَى بَابِهِ، فَتَسْفِي الرِّيحُ عَلَى وَجْهِي التُّرَابَ، فَيَخْرُجُ، فَيَرَانِي، فَيَقُولُ: يَا ابْنَ عَمِّ رَسُولِ اللَّهِ، مَا جَاءَ بِكَ؟ أَلَا أَرْسَلْتَ إِلَيَّ فَآتِيَكَ؟، فَأَقُولُ: لَا، أَنَا أَحَقُّ أَنْ آتِيَكَ، فَأَسْأَلُهُ عَنْ الْحَدِيثِ، قَالَ: فَبَقِيَ الرَّجُلُ حَتَّى رَآنِي وَقَدْ اجْتَمَعَ النَّاسُ عَلَيَّ، فَقَالَ: كَانَ هَذَا الْفَتَى أَعْقَلَ مِنِّي"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Jariyr bin Haazim, kutoka kwa Ya'laa bin Hakiym, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofariki, nilimwambia mtu mmoja wa Answaar: Yaa fulani, njoo tuwaulize Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwani wao leo ni wengi. Akasema: Ni ajabu iliyoje kwako, yaa Ibna 'Abbaas! Je, unaona kwamba watu watakuhitajia wewe, na miongoni mwa watu kuna Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) unaowaona? Basi akaliacha hilo, nami nikaelekea katika kuuliza. Na hakika ilikuwa inanifikia Hadiyth kutoka kwa mtu, nikamjia naye akiwa amelala (usingizi wa) mchana; nikaifanya shuka yangu kuwa mto mlangoni pake, na upepo ukinipeperushia mavumbi usoni mwangu. Kisha anatoka, ananiona, na anasema: Yaa mwana wa ami ya Rasuli wa Allaah, kilichokuleta ni nini? Kwa nini hukunitumia (mtu), nikakujia? Nami ninasema: Hapana, mimi nina haki zaidi ya kukujia. Kisha ninamuuliza kuhusu Hadiyth. Akasema: Yule mtu (wa Answaar) akabaki mpaka aliponiona, na watu wamekusanyika kwangu; akasema: Kijana huyu alikuwa na akili zaidi kuliko mimi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
467
Hadiyth
590

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بُرَيْدَةَ، "أَنَّ رَجُلًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَحَلَ إِلَى فَضَالَةَ بْنِ عُبَيْدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، وَهُوَ بِمِصْرَ، فَقَدِمَ عَلَيْهِ وَهُوَ يَمُدُّ لِنَاقَةٍ لَهُ، فَقَالَ: مَرْحَبًا، قَالَ: أَمَا إِنِّي لَمْ آتِكَ زَائِرًا، وَلَكِنْ سَمِعْتُ أَنَا وَأَنْتَ حَدِيثًا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، رَجَوْتُ أَنْ يَكُونَ عِنْدَكَ مِنْهُ عِلْمٌ، قَالَ: كَذَا وَكَذَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Jurayriy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Buraydah: "Kwamba mtu mmoja miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisafiri kwenda kwa Fadhwaalah bin 'Ubayd (رضي الله عنه), naye akiwa Misri. Akamfikia naye akiwa anampa lishe ngamia wake jike. Akasema: Karibu! (Yule mtu) akasema: Ama mimi sikukujia kwa ajili ya kukutembelea, lakini mimi na wewe tulisikia Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); nikataraji kwamba utakuwa na ilimu kuhusu hiyo. Akasema: (Ni) hivi na hivi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
468
Hadiyth
591

48-Mlangoباب صيانة العلمMlango Wa Kuilinda Ilimu

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ السَّلَامِ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ عَبْدِ الْأَعْلَى، عَنْ الْحَسَنِ، أَنَّهُ دَخَلَ السُّوقَ فَسَاوَمَ رَجُلًا بِثَوْبٍ، فَقَالَ: "هُوَ لَكَ بِكَذَا وَكَذَا، وَاللَّهِ لَوْ كَانَ غَيْرَكَ مَا أَعْطَيْتُهُ، فَقَالَ: فَعَلْتُمُوهَا، فَمَا رُئِيَ بَعْدَهَا مُشْتَرِيًا مِنْ السُّوقِ، وَلَا بَائِعًا حَتَّى لَحِقَ بِاللَّهِ عز وجل"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia 'Abdus-Salaam bin Harb, kutoka kwa 'Abdul-A'laa, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba aliingia sokoni, akapatana bei ya nguo na mtu mmoja. (Yule mtu) akasema: "Ni yako kwa kiasi fulani na fulani; Wa-Allaahi, lau angekuwa mwingine si wewe, nisingempa. Akasema (Al-Hasan): Mmeifanya! Basi hakuonekana baada ya hapo akinunua sokoni wala akiuza, mpaka alipokutana na Allaah (عز وجل)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
468
Hadiyth
592

أَخْبَرَنَا الْهَيْثَمُ بْنُ جَمِيلٍ، عَنْ حُسَامٍ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، أَنَّهُ كَانَ "لَا يَشْتَرِي مِمَّنْ يَعْرِفُهُ"

Ametukhabarisha Al-Haytham bin Jamiyl, kutoka kwa Husaam, kutoka kwa Abuw Ma'shar, kutoka kwa Ibraahiym, kwamba yeye alikuwa "hanunui kutoka kwa anayemjua."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
469
Hadiyth
593

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ السَّلَامِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْوَلِيدِ الْمُزَنِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ الْحَسَنِ، قَالَ: قَسَمَ مُصْعَبُ بْنُ الزُّبَيْرِ مَالًا فِي قُرَّاءِ أَهْلِ الْكُوفَةِ حِينَ دَخَلَ شَهْرُ رَمَضَانَ، فَبَعَثَ إِلَى عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَعْقِلٍ بِأَلْفَيْ دِرْهَمٍ، فَقَالَ لَهُ: اسْتَعِنْ بِهَا فِي شَهْرِكَ هَذَا، فَرَدَّهَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَعْقِلٍ وَقَالَ: "لَمْ نَقْرَأْ الْقُرْآنَ لِهَذَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari 'Abdus-Salaam, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Al-Waliyd Al-Muzaniy, kutoka kwa 'Ubayd bin Al-Hasan, amesema: Musw'ab bin Az-Zubayr aligawa mali kwa Qurraa (wasomaji wa Qur-aan) wa watu wa Al-Kuwfah ulipoingia mwezi wa Ramadhwaan; akampelekea 'Abdur-Rahmaan bin Ma'qil dirhamu elfu mbili, akamwambia: Jisaidie kwazo katika mwezi wako huu. 'Abdur-Rahmaan bin Ma'qil akazirudisha, na akasema: "Hatukusoma Qur-aan kwa ajili ya hili."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
469
Hadiyth
594

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ عِيَاضٍ، حَدَّثَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ، أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ عَلَيْه رضْوَانُ اللَّهِ تَعَالَى، قَالَ لِعَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلَامٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "مَنْ أَرْبَابُ الْعِلْمِ؟"، قَالَ: "الَّذِينَ يَعْمَلُونَ بِمَا يَعْلَمُونَ، قَالَ: فَمَا يَنْفِي الْعِلْمَ مِنْ صُدُورِ الرِّجَالِ؟، قَالَ: الطَّمَعُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Anas bin 'Iyaadhw, amenisimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (عليه رضوان الله تعالى) alimwambia 'Abdu-Allaah bin Salaam (رضي الله عنه): "Ni nani wenye kumiliki ilimu?" Akasema: "Ni wale wanaotenda kwa yale wanayoyajua. Akasema: Basi ni nini kinachoiondoa ilimu kutoka vifuani mwa watu? Akasema: Tamaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
469
Hadiyth
595

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ زَيْدٍ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: "مَا أَوَى شَيْءٌ إِلَى شَيْءٍ أَزْيَنَ مِنْ حِلْمٍ إِلَى عِلْمٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Zayd, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: "Hakuna kitu kilichojiunga na kitu (kingine) kikawa kizuri zaidi kuliko upole uliojiunga na ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
470
Hadiyth
596

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا عَاصِمٌ الْأَحْوَلُ، عَنْ عَامِرٍ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "زَيْنُ الْعِلْمِ حِلْمُ أَهْلِهِ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari 'Aaswim Al-Ahwal, kutoka kwa 'Aamir Ash-Sha'biy, amesema: "Pambo la ilimu ni upole wa watu wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
470
Hadiyth
597

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ، حَدَّثَنَا زَمْعَةُ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ وَهْرَامٍ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: "مَا حُمِلَ الْعِلْمُ فِي مِثْلِ جِرَابِ حِلْمٍ"

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan, ametusimulia Zam'ah bin Swaalih, kutoka kwa Salamah bin Wahraam, kutoka kwa Twaawuws, amesema: "Ilimu haijabebwa katika (chombo) mfano wa mfuko wa upole."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
470
Hadiyth
598

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ ابْنِ شُبْرُمَةَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "زَيْنُ الْعِلْمِ حِلْمُ أَهْلِهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Ibn Shubrumah, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Pambo la ilimu ni upole wa watu wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
470
Hadiyth
599

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا مُطَرِّفُ بْنُ مَازِنٍ، عَنْ يَعْلَى بْنِ مِقْسَمٍ، عَنْ وَهْبِ بْنِ مُنَبِّهٍ، قَالَ: "إِنَّ الْحِكْمَةَ تَسْكُنُ الْقَلْبَ الْوَادِعَ السَّاكِنَ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Mutwarrif bin Maazin, kutoka kwa Ya'laa bin Miqsam, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, amesema: "Hakika hekima hukaa katika moyo mpole, uliotulia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
471
Hadiyth
600

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ، يَقُولُ: قَالَ عُبَيْدُ اللَّهِ: "شِنْتُمْ الْعِلْمَ وَأَذْهَبْتُمْ نُورَهُ، وَلَوْ أَدْرَكَنِي وَإِيَّاكُمْ عُمَرُ رِضْوَانُ الله عَلَيْهِ لَأَوْجَعَنَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, amesema: Nilimsikia Sufyaan akisema: 'Ubaydu-Allaah amesema: "Mmeitia ilimu aibu, na mmeiondoa nuru yake. Na lau 'Umar (رضوان الله عليه) angenidiriki mimi na nyinyi, angetuumiza (kwa kipigo)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
471
Hadiyth
601

أَخْبَرَنَا شِهَابُ بْنُ عَبَّادٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أُمَيٍّ الْمُرَادِيِّ، قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ: "تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ، فَإِذَا عَلِمْتُمُوهُ، فَاكْظِمُوا عَلَيْهِ وَلَا تَشُوبُوهُ بِضَحِكٍ، وَلَا بِلَعِبٍ فَتَمُجَّهُ الْقُلُوبُ"

Ametukhabarisha Shihaab bin 'Abbaad, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Umayy Al-Muraadiy, amesema: 'Aliy (رضوان الله عليه) amesema: "Jifunzeni ilimu; na mtakapoijua, basi ishikeni kwa utulivu, wala msiichanganye na kicheko wala mchezo, nyoyo zikaitema."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
471
Hadiyth
602

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ الْفُضَيْلِ بْنِ غَزْوَانَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ حُسَيْنٍ رَحِمَةُ اللَّهِ عَلَيْهِ، قَالَ: "مَنْ ضَحِكَ ضَحْكَةً مَجَّ مَجَّةً مِنْ الْعِلْمِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Al-Fudhwayl bin Ghazwaan, kutoka kwa 'Aliy bin Husayn (رحمة الله عليه), amesema: "Atakayecheka kicheko kimoja, ametema mtemo mmoja wa ilimu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
471
Hadiyth
603

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، أَنَّ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ لِكَعْبٍ: "مَنْ أَرْبَابُ الْعِلْمِ؟، قَالَ: الَّذِينَ يَعْمَلُونَ بِمَا يَعْلَمُونَ، قَالَ: فَمَا أَخْرَجَ الْعِلْمَ مِنْ قُلُوبِ الْعُلَمَاءِ؟، قَالَ: الطَّمَعُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kwamba 'Umar (رضي الله عنه) alimwambia Ka'b: "Ni nani wenye kumiliki ilimu? Akasema: Ni wale wanaotenda kwa yale wanayoyajua. Akasema: Basi ni nini kilichoitoa ilimu kutoka nyoyoni mwa 'Ulamaa (Wanazuoni)? Akasema: Tamaa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
471
Hadiyth
604

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بِشْرٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْوَلِيدِ، عَنْ عُمَرَ بْنِ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي إِيَاسٍ، قَالَ: كُنْتُ نَازِلًا عَلَى عَمْرِو بْنِ النُّعْمَانِ فَأَتَاهُ رَسُولُ مُصْعَبِ بْنِ الزُّبَيْرِ حِينَ حَضَرَهُ رَمَضَانُ بِأَلْفَيْ دِرْهَمٍ، فَقَالَ: إِنَّ الْأَمِيرَ يُقْرِئُكَ السَّلَامَ، وَقَالَ: إِنَّا لَمْ نَدَعْ قَارِئًا شَرِيفًا إِلَّا وَقَدْ وَصَلَ إِلَيْهِ مِنَّا مَعْرُوفٌ، فَاسْتَعِنْ بِهَذَيْنِ عَلَى نَفَقَةِ شَهْرِكَ هَذَا، فَقَالَ: أَقْرِئْ الْأَمِيرَ السَّلَامَ، وَقُلْ لَهُ: "إِنَّا وَاللَّهِ مَا قَرَأْنَا الْقُرْآنَ نُرِيدُ بِهِ الدُّنْيَا وَدِرْهَمَهَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin Humayd, ametusimulia Muhammad bin Bishr, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Waliyd, kutoka kwa 'Umar bin Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Iyaas, amesema: Nilikuwa nimefikia kwa 'Amr bin An-Nu'maan; mjumbe wa Musw'ab bin Az-Zubayr akamjia, ulipowadia (mwezi wa) Ramadhwaan, na dirhamu elfu mbili. Akasema: Hakika Amiri anakutolea Salaam, na amesema: Hakika sisi hatukumwacha msomaji (wa Qur-aan) mtukufu yeyote isipokuwa wema kutoka kwetu umemfikia; basi jisaidie kwa hizi (elfu) mbili kwa matumizi ya mwezi wako huu. Akasema: Mfikishie Amiri Salaam, na umwambie: "Hakika sisi — Wa-Allaahi — hatukusoma Qur-aan tukikusudia kwayo dunia na dirhamu zake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
472
Hadiyth
605

49-Mlangoباب: السنة قاضية على كتاب الله تعالىMlango Wa Sunnah Ni Mwamuzi Juu Ya Kitabu Cha Allaah (تعالى)

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ جَابِرٍ، عَنْ الْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِ يكَرِبَ الْكِنْدِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "حَرَّمَ أَشْيَاءَ يَوْمَ خَيْبَرَ: الْحِمَارَ وَغَيْرَهُ"، ثُمَّ قَالَ: "لَيُوشِكُ ِالرَّجُل مُتَّكِئًا عَلَى أَرِيكَتِهِ، يُحَدَّثُ بِحَدِيثِي فَيَقُولُ: بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ كِتَابُ اللَّهِ، مَا وَجَدْنَا فِيهِ مِنْ حَلَالٍ، اسْتَحْلَلْنَاهُ، وَمَا وَجَدْنَا فِيهِ مِنْ حَرَامٍ، حَرَّمْنَاهُ، أَلَا وَإِنَّ مَا حَرَّمَ رَسُولُ اللَّهِ، فَهُوَ مِثْلُ مَا حَرَّمَ اللَّهُ تَعَالَى"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Mu'aawiyah, ametusimulia Al-Hasan bin Jaabir, kutoka kwa Al-Miqdaam bin Ma'diykarib Al-Kindiy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliharamisha vitu (kadhaa) siku ya Khaybar: punda na vinginevyo. Kisha akasema: "Hivi karibuni mtu ataegemea juu ya kitanda chake cha kifahari, akasimuliwa Hadiyth yangu, naye aseme: Baina yetu na baina yenu ni Kitabu cha Allaah; tulichokikuta ndani yake cha halaal, tutakihalalisha, na tulichokikuta ndani yake cha haraam, tutakiharamisha. Tanabahini! Na hakika alichokiharamisha Rasuli wa Allaah, basi ni mfano wa Alichokiharamisha Allaah (تعالى)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
473
Hadiyth
606

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، قَالَ: "السُّنَّةُ قَاضِيَةٌ عَلَى الْقُرْآنِ وَلَيْسَ الْقُرْآنُ بِقَاضٍ عَلَى السُّنَّةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, amesema: "Sunnah ni mwamuzi juu ya Qur-aan, wala Qur-aan si mwamuzi juu ya Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
473
Hadiyth
607

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ حَسَّانَ، قَالَ: "كَانَ جِبْرِيلُ يَنْزِلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالسُّنَّةِ كَمَا يَنْزِلُ عَلَيْهِ بِالْقُرْآنِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Hassaan, amesema: "Jibriyl (عليه السلام) alikuwa akimteremkia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na Sunnah, kama anavyomteremkia na Qur-aan."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
473
Hadiyth
608

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ مَكْحُولٍ، قَالَ: "السُّنَّةُ سُنَّتَانِ: سُنَّةٌ الْأَخْذُ بِهَا فَرِيضَةٌ، وَتَرْكُهَا كُفْرٌ، وَسُنَّةٌ الْأَخْذُ بِهَا فَضِيلَةٌ، وَتَرْكُهَا إِلَى غَيْرِ حَرَجٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Makhuwl, amesema: "Sunnah ni (aina) mbili: Sunnah ambayo kuishika ni faradhi, na kuiacha ni ukafiri; na Sunnah ambayo kuishika ni fadhila, na kuiacha hakuna uzito (wa dhambi)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
473
Hadiyth
609

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ يَعْلَى بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ "أَنَّهُ حَدَّثَ يَوْمًا بِحَدِيثٍ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ رَجُلٌ: فِي كِتَابِ اللَّهِ مَا يُخَالِفُ هَذَا؟، قَالَ: لَا أُرَانِي أُحَدِّثُكَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَتُعَرِّضُ فِيهِ بِكِتَابِ اللَّهِ، كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَعْلَمَ بِكِتَابِ اللَّهِ تَعَالَى مِنْكَ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ya'laa bin Hakiym, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr: "Kwamba siku moja alisimulia Hadiyth kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Mtu mmoja akasema: Katika Kitabu cha Allaah kuna kinachokhalifu hii? Akasema: Sioni (inafaa) nikikusimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nawe ukaipinga kwa Kitabu cha Allaah! Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa mjuzi zaidi wa Kitabu cha Allaah (تعالى) kuliko wewe."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
473
Hadiyth
610

50-Mlangoباب تأويل حديث رسول الله صلى الله عليه وسلمMlango Wa Ufafanuzi Wa Hadiyth
Ya Rasuli Wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ ابْنِ عَجْلَانَ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ، قَالَ: "إِذَا حُدِّثْتُمْ بِالْحَدِيثِ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَظُنُّوا بِهِ الَّذِي هُوَ أَهْيَأُ، وَالَّذِي هُوَ أَهْدَى، وَالَّذِي هُوَ أَتْقَى"

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa Ibn 'Ajlaan, kutoka kwa 'Awn bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), kwamba amesema: "Mtakaposimuliwa Hadiyth kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi idhanieni (maana) ile iliyo ya kufaa zaidi, na ile iliyo ya uongofu zaidi, na ile iliyo ya taqwa zaidi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
476
Hadiyth
611

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا مِسْعَرٌ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي الْبَخْتَرِيِّ، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ السُّلَمِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "إِذَا حُدِّثْتُمْ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَظُنُّوا بِهِ الَّذِي هُوَ أَهْدَى، وَالَّذِي هُوَ أَتْقَى، وَالَّذِي هُوَ أَهْيَأُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Mis'ar, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa Abul-Bakhtariy, kutoka kwa Abuw 'Abdir-Rahmaan As-Sulamiy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Mtakaposimuliwa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi idhanieni (maana) ile iliyo ya uongofu zaidi, na ile iliyo ya taqwa zaidi, na ile iliyo ya kufaa zaidi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
476
Hadiyth
612

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيل بْنُ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ صَالِحِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ عَاصِمِ بْنِ كُلَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: كَانَ إِذَا حَدَّثَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا، فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنْ النَّارِ"،

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Swaalih bin 'Umar, kutoka kwa 'Aaswim bin Kulayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Alikuwa anaposimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), husema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenizulia uongo kwa makusudi, basi ajiandalie makazi yake motoni."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
476
Hadiyth
613

فَكَانَ ابْنُ عَبَّاسٍ إِذَا حَدَّثَ قَالَ: إِذَا سَمِعْتُمُونِي أُحَدِّثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمْ تَجِدُوهُ فِي كِتَابِ اللَّهِ، أَوْ حَسَنًا عِنْدَ النَّاسِ، فَاعْلَمُوا أَنِّي قَدْ كَذَبْتُ عَلَيْهِ

Na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa anaposimulia, husema: Mtakaponisikia nikisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kisha msiikute katika Kitabu cha Allaah, au (msiikute) kuwa ni nzuri mbele ya watu, basi jueni kwamba nimemzulia uongo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
477
Hadiyth
614

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عِمْرَانَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ الْأَحْوَلِ،

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin 'Imraan, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Sulaymaan Al-Ahwal,

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
477
Hadiyth
615

عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ: "إِنَّ أَزْهَدَ النَّاسِ فِي عَالِمٍ أَهْلُهُ"

kutoka kwa 'Ikrimah, amesema: "Hakika watu wasiomjali zaidi 'Aalim (Mwanazuoni) ni watu wa nyumbani kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
477
Hadiyth
616

51-Mlangoباب مذاكرة العلمMlango Wa Kukumbushana Ilimu

أَخْبَرَنَا أَسَدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْجُرَيْرِيِّ، وَأَبِي مَسْلَمَةَ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: "تَذَاكَرُوا الْحَدِيثَ، فَإِنَّ الْحَدِيثَ يُهَيِّجُ الْحَدِيثَ"

Ametukhabarisha Asad bin Muwsaa, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Jurayriy na Abuw Maslamah, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Kumbushaneni Hadiyth, kwani Hadiyth huchochea Hadiyth (nyingine)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
477
Hadiyth
617

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "تَذَاكَرُوا الْحَدِيثَ، فَإِنَّ الْحَدِيثَ يُهَيِّجُ الْحَدِيثَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Kumbushaneni Hadiyth, kwani Hadiyth huchochea Hadiyth (nyingine)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
478
Hadiyth
618

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ هُشَيْمٍ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْريَّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "تَذَاكَرُوا الْحَدِيثَ، فَإِنَّ الْحَدِيثَ يُهَيِّجُ الْحَدِيثَ"،

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar, kutoka kwa Hushaym, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Kumbushaneni Hadiyth, kwani Hadiyth huchochea Hadiyth (nyingine)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
478
Hadiyth
619

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ أَبِي مُعَاوِيَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَن أَبِي سَعِيدٍ،

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar, kutoka kwa Abuw Mu'aawiyah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه),

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
478
Hadiyth
620

وَابْنِ عُلَيَّةَ، عَنْ الْجُرَيْرِيِّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَن أَبِي سَعِيدٍ،

na Ibn 'Ulayyah, kutoka kwa Al-Jurayriy, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه),

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
621

أَخْبَرَنَا أَبُو مَسْلَمَةَ يُعْنِي، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَن أَبي سَعيدٍ، وَفِيهِ كَلَامٌ أَكْثَرُ مِنْ هَذَا

Ametukhabarisha Abuw Maslamah — yaani —, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه); na ndani yake kuna maneno mengi zaidi kuliko haya.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
622

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو، قَالَ: قَالَ لِي طَاوُسٌ: "اذْهَبْ بِنَا نُجَالِسْ النَّاسَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr, amesema: Twaawuws aliniambia: "Twende pamoja tukakae na watu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
623

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا يَعْقُوبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الْقُمِّيُّ، حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ أَبِي الْمُغِيرَةِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "تَذَاكَرُوا هَذَا الْحَدِيثَ لَا يَنْفَلِتْ مِنْكُمْ، فَإِنَّهُ لَيْسَ مِثْلَ الْقُرْآنِ مَجْمُوعٌ مَحْفُوظٌ، وَإِنَّكُمْ إِنْ لَمْ تَذَاكَرُوا هَذَا الْحَدِيثَ يَنْفَلِتْ مِنْكُمْ، وَلَا يَقُولَنَّ أَحَدُكُمْ حَدَّثْتُ أَمْسِ فَلَا أُحَدِّثُ الْيَوْمَ، بَلْ حَدِّثْ أَمْسِ، وَلْتُحَدِّثْ الْيَوْمَ، وَلْتُحَدِّثْ غَدًا"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Ya'quwb bin 'Abdi-Allaah Al-Qummiy, ametusimulia Ja'far bin Abil-Mughiyrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Kumbushaneni Hadiyth hii isiwaponyoke; kwani hiyo si kama Qur-aan iliyokusanywa, iliyohifadhiwa. Na hakika nyinyi msipokumbushana Hadiyth hii, itawaponyoka. Wala mmoja wenu asiseme: Nilisimulia jana, kwa hiyo sisimulii leo. Bali simulia jana, na usimulie leo, na usimulie kesho."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
624

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا مِنْدَلُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنِي جَعْفَرُ بْنُ أَبِي الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنِي سَعِيدُ بْنُ جُبَيْرٍ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: "رُدُّوا الْحَدِيثَ وَاسْتَذْكِرُوهُ، فَإِنَّهُ إِنْ لَمْ تَذْكُرُوهُ، ذَهَبَ، وَلَا يَقُولَنَّ رَجُلٌ لِحَدِيثٍ قَدْ حَدَّثَهُ قَدْ حَدَّثْتُهُ مَرَّةً، فَإِنَّهُ مَنْ كَانَ سَمِعَهُ يَزْدَادُ بِهِ عِلْمًا، وَيَسْمَعُ مَنْ لَمْ يَسْمَعْ"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Mandal bin 'Aliy, amenisimulia Ja'far bin Abil-Mughiyrah, amenisimulia Sa'iyd bin Jubayr, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Irudieni Hadiyth na mjikumbushe; kwani msipoikumbuka, itaondoka. Wala mtu asiseme kuhusu Hadiyth aliyokwisha kuisimulia: Nimekwisha kuisimulia mara moja. Kwani aliyekuwa ameisikia, huzidi kwayo ilimu; na asiyekuwa ameisikia, huisikia."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
625

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، قَالَ: "تَذَاكَرُوا، فَإِنَّ إِحْيَاءَ الْحَدِيثِ مُذَاكَرَتُهُ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, amesema: "Kumbushaneni, kwani kuihuisha Hadiyth ni kuikumbushana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
626

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، وَمُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، قَالَا: حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، قَالَ: "تَذَاكَرُوا الْحَدِيثَ، فَإِنَّ ذِكْرَهُ حَيَاتُهُ"

Ametukhabarisha Qabiyswah na Muhammad bin Yuwsuf, wamesema: Ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, amesema: "Kumbushaneni Hadiyth, kwani kuitaja ndio uhai wake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
627

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ قُدَامَةَ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ زِيَادِ بْنِ سَعْدٍ، قَالَ: "كَانَ ابْنُ شِهَابٍ يُحَدِّثُ الْأَعْرَابَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Qudaamah, kutoka kwa Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Ziyaad bin Sa'd, amesema: "Ibn Shihaab alikuwa akiwasimulia Mabedui."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
628

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: "كَانَ إِسْمَاعِيل بْنُ رَجَاءٍ يَجْمَعُ صِبْيَانَ الْكُتَّابِ يُحَدِّثُهُمْ يَتَحَفَّظُ بِذَلِكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametupa khabari Muhammad bin Fudhwayl, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: "Ismaa'iyl bin Rajaa alikuwa akiwakusanya watoto wa chuo (cha kusomea), akiwasimulia, akijihifadhia (Hadiyth) kwa hilo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
629

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَبِي عَبْدِ اللَّهِ الشَّقَرِيِّ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "حَدِّثْ حَدِيثَكَ مَنْ يَشْتَهِيهِ، وَمَنْ لَا يَشْتَهِيهِ، فَإِنَّهُ يَصِيرُ عِنْدَكَ كَأَنَّهُ إِمَامٌ تَقْرَؤُهُ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Abuw 'Abdi-Allaah Ash-Shaqariy, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Simulia Hadiyth yako kwa anayeitamani na asiyeitamani, kwani inakuwa kwako kama kwamba ni daftari unalolisoma."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
630

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، وَمُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ السَّلَامِ، عَنْ حَجَّاجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "إِذَا سَمِعْتُمْ مِنَّا حَدِيثًا، فَتَذَاكَرُوهُ بَيْنَكُمْ"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar na Muhammad bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Abdus-Salaam, kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Mtakaposikia kutoka kwetu Hadiyth, basi ikumbushaneni baina yenu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
631

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ هُشَيْمٍ، أَخْبَرَنَا يُونُسُ، قَالَ: "كُنَّا نَأْتِي الْحَسَنَ، فَإِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِهِ، تَذَاكَرْنَا بَيْنَنَا"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar, kutoka kwa Hushaym, ametukhabarisha Yuwnus, amesema: "Tulikuwa tukimjia Al-Hasan; tunapotoka kwake, tunakumbushana baina yetu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
479
Hadiyth
632

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ وَهْبٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ حُنَيْنِ بْنِ أَبِي حَكِيمٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، قَالَ: "إِذَا أَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يَرْوِيَ حَدِيثًا، فَلْيُرَدِّدْهُ ثَلَاثًا"

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Wahb, kutoka kwa 'Amr bin Al-Haarith, kutoka kwa Hunayn bin Abiy Hakiym, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Mmoja wenu anapotaka kusimulia Hadiyth, basi aikariri mara tatu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
482
Hadiyth
633

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ يَزِيدَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، قَالَ: "إِحْيَاءُ الْحَدِيثِ مُذَاكَرَتُهُ"، فَقَالَ لَهُ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ شَدَّادٍ: "يَرْحَمُكَ اللَّهُ، كَمْ مِنْ حَدِيثٍ أَحْيَيْتَهُ فِي صَدْرِي كَانَ قَدْ مَاتَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia Muhammad bin Fudhwayl, kutoka kwa Yaziyd, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, amesema: "Kuihuisha Hadiyth ni kuikumbushana." 'Abdu-Allaah bin Shaddaad akamwambia: "Allaah Akurehemu! Ni Hadiyth ngapi umezihuisha kifuani mwangu, ambazo zilikuwa zimekwisha kufa!"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
483
Hadiyth
634

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "كَانَ الْحَارِثُ بْنُ يَزِيدَ الْعُكْلِيُّ، وَابْنُ شُبْرُمَةَ، وَالْقَعْقَاعُ بْنُ يَزِيدَ، وَمُغِيرَةُ إِذَا صَلَّوْا الْعِشَاءَ الْآخِرَةَ، جَلَسُوا فِي الْفِقْهِ، فَلَمْ يُفَرِّقْ بَيْنَهُمْ إِلَّا أَذَانُ الصُّبْحِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Muhammad bin Fudhwayl, kutoka kwa baba yake, amesema: "Al-Haarith bin Yaziyd Al-'Ukliy, na Ibn Shubrumah, na Al-Qa'qaa' bin Yaziyd, na Mughiyrah, walikuwa wanaposwali Ishaa ya mwisho, hukaa (kujadiliana) katika Fiqh (ufahamu wa Dini); na hakuna kilichowatenganisha isipokuwa Adhaan ya Swubhi (Alfajiri)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
483
Hadiyth
635

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، قَالَ: سَمِعْتُ شَرِيكًا ذَكَرَ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ عَطَاءٍ، وَطَاوُسٍ، وَمُجَاهِدٍ، قَالَ: عَنْ اثْنَيْنِ مِنْهُمْ "لَا بَأْسَ بِالسَّمَرِ فِي الْفِقْهِ"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, amesema: Nilimsikia Shariyk akitaja kutoka kwa Layth, kutoka kwa 'Atwaa, na Twaawuws, na Mujaahid — amesema: kutoka kwa wawili miongoni mwao —: "Hakuna ubaya kukesha usiku (kwa mazungumzo) katika Fiqh (ufahamu wa Dini)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
483
Hadiyth
636

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ السَّلَامِ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، قَالَ: "لَا بَأْسَ بِالسَّمَرِ فِي الْفِقْهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia 'Abdus-Salaam, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid, amesema: "Hakuna ubaya kukesha usiku (kwa mazungumzo) katika Fiqh (ufahamu wa Dini)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
483
Hadiyth
637

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، ثَنَا حَفْصٌ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا: "تَدَارُسُ الْعِلْمِ سَاعَةً مِنْ اللَّيْلِ، خَيْرٌ مِنْ إِحْيَائِهَا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia Hafsw, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Kudurusu ilimu saa moja ya usiku ni bora kuliko kuuhuisha (usiku mzima kwa ibaada)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
483
Hadiyth
638

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، وَمُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، عَنْ هُشَيْمٍ، أَنْبَأَنَا حَجَّاجٌ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: "كُنَّا نَأْتِي جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا، فَإِذَا خَرَجْنَا مِنْ عِنْدِهِ تَذَاكَرْنَا، فَكَانَ أَبُو الزُّبَيْرِ أَحْفَظَنَا لِحَدِيثِهِ"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar na Muhammad bin 'Iysaa, kutoka kwa Hushaym, ametupa khabari Hajjaaj, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: "Tulikuwa tukimjia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما); tunapotoka kwake, tunakumbushana. Na Abuz-Zubayr alikuwa ndiye mwenye kuhifadhi zaidi Hadiyth zake miongoni mwetu."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
484
Hadiyth
639

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ اللَّيْثَ بْنَ سَعْدٍ، يَقُولُ: "تَذَكَّرَ ابْنُ شِهَابٍ لَيْلَةً بَعْدَ الْعِشَاءِ حَدِيثًا وَهُوَ جَالِسٌ مُتَوَضِّئًا، قَالَ: فَمَا زَالَ ذَلِكَ مَجْلِسَهُ حَتَّى أَصْبَحَ"، قَالَ مَرْوَانُ: "جَعَلَ يَتَذَاكَرُ الْحَدِيثَ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, amesema: Nilimsikia Al-Layth bin Sa'd akisema: "Ibn Shihaab aliikumbuka Hadiyth (fulani) usiku mmoja baada ya Ishaa, naye akiwa amekaa, ametawadha. Akasema: Basi hapo hapakuacha kuwa ndipo kikao chake mpaka akapambaukiwa." Marwaan amesema: "Akawa anakumbushana Hadiyth."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
485
Hadiyth
640

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "كُنْتُ إِذَا لَقِيتُ عُبَيْدَ اللَّهِ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، فَكَأَنَّمَا أَفْجُرُ بِهِ بَحْرًا"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Nilikuwa ninapokutana na 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, ni kama kwamba ninabubujisha bahari kupitia kwake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
485
Hadiyth
641

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "كَانَ الْحَارِثُ الْعُكْلِيُّ وَأَصْحَابُهُ يَتَجَالَسُونَ بِاللَّيْلِ، وَيَذْكُرُونَ الْفِقْهَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Abdi-Allaah, amesema: "Al-Haarith Al-'Ukliy na wenzake walikuwa wakikaa pamoja usiku, na wakiitaja (kuijadili) Fiqh (ufahamu wa Dini)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
485
Hadiyth
642

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، ثَنَا أَبُو إِسْرَائِيلَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ أَبِيهِ، رَوَى عَنْ أَبِي الْأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ: "تَذَاكَرُوا هَذَا الْحَدِيثَ، فَإِنَّ حَيَاتَهُ مُذَاكَرَتُهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Abuw Israaiyl, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa baba yake — amepokea kutoka kwa Abul-Ahwasw —, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Kumbushaneni Hadiyth hii, kwani uhai wake ni kuikumbushana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
485
Hadiyth
643

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ عَوْنٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ لِأَصْحَابِهِ حِينَ قَدِمُوا عَلَيْهِ: هَلْ تَجَالَسُونَ؟، قَالُوا: لَيْسَ نُتْرَكُ ذَاكَ، قَالَ: فَهَلْ تَزَاوَرُونَ؟، قَالُوا: نَعَمْ، يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ، إِنَّ الرَّجُلَ مِنَّا لَيَفْقِدُ أَخَاهُ، فَيَمْشِي فِي طَلَبِهِ إِلَى أَقْصَى الْكُوفَةِ حَتَّى يَلْقَاهُ، قَالَ: "فَإِنَّكُمْ لَنْ تَزَالُوا بِخَيْرٍ مَا فَعَلْتُمْ ذَلِكَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa 'Awn, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) aliwaambia wanafunzi wake walipomjia: Je, mnakaa pamoja? Wakasema: Hatuliachi hilo. Akasema: Basi je, mnatembeleana? Wakasema: Ndiyo, yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan; hakika mtu miongoni mwetu humkosa ndugu yake, basi hutembea kumtafuta mpaka mwisho wa Al-Kuwfah ili akutane naye. Akasema: "Basi hakika nyinyi hamtaacha kuwa katika kheri madamu mnafanya hivyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
486
Hadiyth
644

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "آفَةُ الْعِلْمِ النِّسْيَانُ، وَتَرْكُ الْمُذَاكَرَةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, ametusimulia Al-Waliyd, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Afa ya ilimu ni kusahau na kuacha kukumbushana."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
645

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عُمَيْسٍ، عَنْ الْقَاسِمِ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: "آفَةُ الْحَدِيثِ النِّسْيَانُ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Abuw 'Umays, kutoka kwa Al-Qaasim, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Afa ya Hadiyth ni kusahau."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
646

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ طَارِقٍ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "إِنَّ لِكُلِّ شَيْءٍ آفَةً، وَآفَةُ الْعِلْمِ النِّسْيَانُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Twaariq, kutoka kwa Hakiym bin Jaabir, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Hakika kila kitu kina afa yake, na afa ya ilimu ni kusahau."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
647

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "آفَةُ الْعِلْمِ النِّسْيَانُ، وَإِضَاعَتُهُ أَنْ تُحَدِّثَ بِهِ غَيْرَ أَهْلِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Afa ya ilimu ni kusahau, na kuipoteza kwake ni kuisimulia kwa wasiostahiki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
648

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا أَبُو حَمْزَةَ التَّمَّارُ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "غَائِلَةُ الْعِلْمِ النِّسْيَانُ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Abuw Hamzah At-Tammaar, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Kinachoiangamiza ilimu ni kusahau."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
649

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا كَهْمَسٌ، عَنْ ابْنِ بُرَيْدَةَ، قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ: "تَذَاكَرُوا هَذَا الْحَدِيثَ، وَتَزَاوَرُوا، فَإِنَّكُمْ إِنْ لَا تَفْعَلُوا يَدْرُسْ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Kahmas, kutoka kwa Ibn Buraydah, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Kumbushaneni Hadiyth hii, na mtembeleane; kwani msipofanya (hivyo), itafutika."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
650

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، قَالَ: سَمِعْتُ سُفْيَانَ، يَقُولُ: قَالَ الزُّهْرِيُّ: "كُنْتُ أَحْسَبُ بِأَنِّي أَصَبْتُ مِنْ الْعِلْمِ، فَجَالَسْتُ عُبَيْدَ اللَّهِ، فَكَأَنِّي كُنْتُ فِي شِعْبٍ مِنْ الشِّعَابِ"

Ametukhabarisha Bishr bin Al-Hakam, amesema: Nilimsikia Sufyaan akisema: Az-Zuhriy amesema: "Nilikuwa nikidhani kwamba nimepata (kitu) katika ilimu; kisha nikakaa na 'Ubaydu-Allaah, nikawa kama kwamba nilikuwa katika bonde moja miongoni mwa mabonde."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
487
Hadiyth
651

52-Mlangoباب اختلاف الفقهاءMlango Wa Kutofautiana Kwa Fuqahaa (Wanazuoni Wa Fiqh)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ حُمَيْدٍ، قَالَ: قُلْتُ لِعُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ رَحِمَهُ الله تَعَالَي: لَوْ جَمَعْتَ النَّاسَ عَلَى شَيْءٍ؟، فَقَالَ: "مَا يَسُرُّنِي أَنَّهُمْ لَمْ يَخْتَلِفُوا، قَالَ: ثُمَّ كَتَبَ إِلَى الْآفَاقِ وَإِلَى الْأَمْصَارِ، لِيَقْضِ كُلُّ قَوْمٍ بِمَا اجْتَمَعَ عَلَيْهِ فُقَهَاؤُهُمْ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Humayd, amesema: Nilimwambia 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz (رحمه الله تعالى): Lau ungewakusanya watu juu ya jambo moja? Akasema: "Hainifurahishi kwamba wao wasingetofautiana." Akasema: Kisha akaandika kwa pande (zote za nchi) na kwa miji mikuu: Watu wa kila jamii wahukumu kwa yale ambayo Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh) wao wamekubaliana juu yake.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
489
Hadiyth
652

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ، عَنْ الْمَسْعُودِيِّ، عَنْ عَوْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "مَا أُحِبُّ أَنَّ أَصْحَابَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَخْتَلِفُوا، فَإِنَّهُمْ لَوْ اجْتَمَعُوا عَلَى شَيْءٍ، فَتَرَكَهُ رَجُلٌ، تَرَكَ السُّنَّةَ، وَلَوْ اخْتَلَفُوا، فَأَخَذَ رَجُلٌ بِقَوْلِ أَحَدٍ، أَخَذَ بِالسُّنَّةِ"

Ametukhabarisha Yaziyd, kutoka kwa Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa 'Awn bin 'Abdi-Allaah, amesema: "Sipendi kwamba Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wasingetofautiana. Kwani lau wangekubaliana juu ya jambo, kisha mtu mmoja akaliacha, angekuwa ameiacha Sunnah. Na lau wangetofautiana, kisha mtu akachukua kauli ya yeyote (miongoni mwao), angekuwa ameichukua Sunnah."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
489
Hadiyth
653

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: "رُبَّمَا رَأَى ابْنُ عَبَّاسٍ الرَّأْيَ، ثُمَّ تَرَكَهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, amesema: "Mara nyingine Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa akiona rai (fulani), kisha akaiacha."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
489
Hadiyth
654

أَخْبَرَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ الْمِنْهَالِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، قَالَ: قَالَ لِي عُثْمَانُ بْنُ عَفَّانَ: إِنَّ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ، قَالَ لِي: إِنِّي قَدْ رَأَيْتُ فِي الْجَدِّ رَأْيًا، فَإِنْ رَأَيْتُمْ أَنْ تَتَّبِعُوهُ فَاتَّبِعُوهُ، قَالَ عُثْمَانُ: "إِنْ نَتَّبِعْ رَأْيَكَ، فَإِنَّهُ رَشَدٌ، وَإِنْ نَتَّبِعْ رَأْيَ الشَّيْخِ قَبْلَكَ فَنِعْمَ ذُو الرَّأْيِ كَانَ"، قَالَ: وَكَانَ أَبُو بَكْرٍ يَجْعَلُهُ أَبًا

Ametukhabarisha Al-Hajjaaj bin Al-Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa Marwaan bin Al-Hakam, amesema: 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) aliniambia: Hakika 'Umar (رضي الله عنه) aliniambia: Hakika mimi nimeona rai (fulani) kuhusu (mirathi ya) babu; basi mkiona kuifuata, ifuateni. 'Uthmaan (رضي الله عنه) akasema: "Tukifuata rai yako, basi hiyo ni uongofu; na tukifuata rai ya mzee (aliyekuwa) kabla yako, basi alikuwa mwenye rai bora kabisa!" Akasema: Na Abuw Bakr (رضي الله عنه) alikuwa akimfanya (babu) kuwa (ni sawa na) baba.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
490
Hadiyth
655

53-Mlangoباب في العرضMlango Wa Kuhusu Kumsomea Mwalimu (Hadiyth)

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ الْأَحْوَلُ، قَالَ: "عَرَضْتُ عَلَى الشَّعْبِيِّ أَحَادِيثَ الْفِقْهِ، فَأَجَازَهَا لِي"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir Al-Hizaamiy, ametusimulia Marwaan bin Mu'aawiyah, ametusimulia 'Aaswim Al-Ahwal, amesema: "Nilimsomea Ash-Sha'biy Hadiyth za Fiqh (ufahamu wa Dini), akaniruhusu (kuzisimulia kutoka kwake)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
656

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، قَالَ: قُلْتُ لِعَمْرِو بْنِ دِينَارٍ: أَسَمِعْتَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِرَجُلٍ مَرَّ فِي الْمَسْجِدِ بِسِهَامٍ: "أَمْسِكْ بِنِصَالِهَا"؟، قَالَ: نَعَمْ

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, amesema: Nilimwambia 'Amr bin Diynaar: Je, ulimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia mtu aliyepita Msikitini akiwa na mishale: "Shika ncha zake"? Akasema: Ndiyo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
657

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ: قُلْتُ لِعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ: أَسَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ، عَنْ عَائِشَةَ أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "يُقَبِّلُهَا وَهُوَ صَائِمٌ"؟، قَالَ: نَعَمْ

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir, ametusimulia Sufyaan, amesema: Nilimwambia 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim: Je, ulimsikia baba yako akisimulia kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa "akimbusu naye amefunga (Swawm)"? Akasema: Ndiyo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
658

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا مِسْكِينُ بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: كَتَبَ إِلَيَّ مَنْصُورٌ بِحَدِيثٍ فَلَقِيتُهُ، فَقُلْتُ: أُحَدِّثُ بِهِ عَنْكَ؟، قَالَ: "أَوَ لَيْسَ إِذَا كَتَبْتُ إِلَيْكَ فَقَدْ حَدَّثْتُكَ؟"،

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Ahmad, ametusimulia Miskiyn bin Bukayr, ametusimulia Shu'bah, amesema: Manswuwr aliniandikia Hadiyth moja; kisha nikakutana naye, nikasema: Je, niisimulie kutoka kwako? Akasema: "Je, si kwamba nikikuandikia, basi nimekwisha kukusimulia?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
659

قَالَ: وَسَأَلْتُ أَيُّوبَ السَّخْتِيَانِيَّ، فَقَالَ: مِثْلَ ذَلِكَ

Akasema: Na nilimuuliza Ayyuwb As-Sakhtiyaaniy, akasema mfano wa hivyo.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
660

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: عَرَضْتُ عَلَيْهِ كِتَابًا فَقُلْتُ: أَرْوِيهِ عَنْكَ؟، قَالَ: "وَمَنْ حَدَّثَكَ بِهِ غَيْرِي"

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametupa khabari 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Nilimsomea (Az-Zuhriy) kitabu (fulani), nikasema: Je, nikisimulie kutoka kwako? Akasema: "Na ni nani mwingine aliyekusimulia hicho isipokuwa mimi?"

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
661

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ بْنُ عَطَاءٍ مَوْلَى الْمُزَنِيِّينَ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "عَرْضُ الْكِتَابِ وَالْحَدِيثُ سَوَاءٌ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir Al-Hizaamiy, ametusimulia Daawuwd bin 'Atwaa, mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Muzaniyyiyn, ametusimulia Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, amesema: "Kumsomea (mwalimu) kitabu na (yeye) kusimulia ni sawa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
662

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ بْنُ عَطَاءٍ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "عَرْضُ الْكِتَابِ وَالْحَدِيثُ سَوَاءٌ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir, ametusimulia Daawuwd bin 'Atwaa, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, amesema: "Kumsomea (mwalimu) kitabu na (yeye) kusimulia ni sawa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
663

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ بْنُ عَطَاءٍ، قَالَ: "كَانَ زَيْدُ بْنُ أَسْلَمَ يَرَى عَرْضَ الْكِتَابِ وَالْحَدِيثَ سَوَاءً، وَكَانَ ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ يَرَى ذَلِكَ"

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir, ametusimulia Daawuwd bin 'Atwaa, amesema: "Zayd bin Aslam alikuwa akiona kwamba kumsomea (mwalimu) kitabu na (yeye) kusimulia ni sawa; na Ibn Abiy Dhi'b alikuwa akiona hivyo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
664

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ، حَدَّثَنَا مُطَرِّفٌ، عَنْ مَالِكِ بْنِ أَنَسٍ "أَنَّهُ كَانَ يَرَى الْعَرْضَ وَالْحَدِيثَ سَوَاءً"

Ametukhabarisha Ibraahiym, ametusimulia Mutwarrif, kutoka kwa Maalik bin Anas, kwamba yeye alikuwa "akiona kwamba kumsomea (mwalimu) na (yeye) kusimulia ni sawa."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
491
Hadiyth
665

54-Mlangoباب الرجل يفتي بشيء، ثم يبلغه عن النبي
صلى الله عليه وسلم، فيرجع إلى قول النبي صلى الله عليه وسلم
Mlango Wa Mtu Anayetoa Fatwa
Kuhusu Jambo, Kisha Ikamfikia (Khabari)
Kutoka Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) , Akarejea
Kwenye Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، قَالَ: كَانَ إِبْرَاهِيمُ، يَقُولُ: يَقُومُ عَنْ يَسَارِهِ، فَحَدَّثْتُهُ عَن سُمَيْعٍ الزَّيَّاتِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَقَامَهُ عَنْ يَمِينِهِ"، فَأَخَذَ بِهِ

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, amesema: Ibraahiym alikuwa akisema: (Maamuma mmoja) husimama upande wa kushoto wa (Imaam). Nikamsimulia kutoka kwa Sumay' Az-Zayyaat, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alimsimamisha upande wake wa kulia." Akalichukua (hilo).

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
494
Hadiyth
666

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا هَارُونُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ عَنْبَسَةَ بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ زَيْدٍ الْأَنْصَارِيِّ، عَنْ عَقَّارِ بْنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، عَنْ أَبِيهِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، قَالَ: نَشَدَ عُمَرُ النَّاسَ: أَسَمِعَ مِنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَحَدٌ مِنْكُمْ فِي الْجَنِينِ؟ فَقَامَ الْمُغِيرَةُ بْنُ شُعْبَةَ، فَقَالَ: قَضَى فِيهِ عَبْدًا أَوْ أَمَةً، فَنَشَدَ النَّاسَ أَيْضًا: فَقَامَ الْمَقْضِيُّ لَهُ، فَقَالَ: "قَضَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِي بِهِ عَبْدًا أَوْ أَمَةً" فَنَشَدَ النَّاسَ أَيْضًا: فَقَامَ الْمَقْضِيُّ عَلَيْهِ، فَقَالَ: قَضَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "عَلَيَّ غُرَّةً عَبْدًا أَوْ أَمَةً"، فَقُلْتُ: أَتَقْضِي عَلَيَّ فِيهِ فِيمَا لَا أَكَلَ، وَلَا شَرِبَ، وَلَا اسْتَهَلَّ، وَلَا نَطَقَ؟ أَنْ تُطِلَّهُ فَهُوَ أَحَقُّ مَا يُطَلُّ "فَهَوَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهِ بِشَيْءٍ مَعَهُ"، فَقَالَ: "أَشِعْرٌ؟"، فَقَالَ عُمَرُ: لَوْلَا مَا بَلَغَنِي مِنْ قَضَاءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَجَعَلْتُهُ دِيَةً بَيْنَ دِيَتَيْنِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Humayd, ametusimulia Haaruwn bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa 'Anbasah bin Sa'iyd, kutoka kwa Khaalid bin Zayd Al-Answaariy, kutoka kwa 'Aqqaar bin Al-Mughiyrah bin Shu'bah, kutoka kwa baba yake, Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه), amesema: 'Umar (رضي الله عنه) aliwaapisha watu (kwa Allaah): Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliyesikia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (hukmu) kuhusu kijusi (mtoto aliye tumboni)? Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Aliamua kuhusu hilo mtumwa mwanamume au mjakazi. Akawaapisha watu tena; akasimama yule aliyeamuliwa kwa faida yake, akasema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniamulia kwa ajili yake mtumwa mwanamume au mjakazi." Akawaapisha watu tena; akasimama yule aliyeamuliwa dhidi yake, akasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamua "juu yangu ghurrah (fidia ya mimba iliyoharibika): mtumwa mwanamume au mjakazi." Nikasema: Je, unaniamulia kulipa kuhusu (kiumbe) ambacho hakikula, wala hakikunywa, wala hakikupiga ukelele (kilipozaliwa), wala hakikutamka? Ukiiacha (damu yake) bure, basi ndiyo inayostahiki zaidi kuachwa bure. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwelekezea kitu alichokuwa nacho, akasema: "Je, ni shairi?" 'Umar (رضي الله عنه) akasema: Lau si yale yaliyonifikia ya hukmu ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ningeifanya (fidia yake) kuwa diyah (fidia ya damu) iliyo kati ya diyah mbili.

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
494
Hadiyth
668

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، قَالَ: كَانَ سَلَّامٌ يَذْكُرُ، عَنْ أَيُّوبَ، قَالَ: "إِذَا أَرَدْتَ أَنْ تَعْرِفَ خَطَأَ مُعَلِّمِكَ، فَجَالِسْ غَيْرَهُ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, amesema: Sallaam alikuwa akitaja kutoka kwa Ayyuwb, amesema: "Ukitaka kujua makosa ya mwalimu wako, basi kaa na (mwalimu) mwingine."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
494
Hadiyth
669

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، قَالَ: "تَذَاكَرْنَا بِمَكَّةَ الرَّجُلَ يَمُوتُ، فَقُلْتُ: عِدَّتُهَا مِنْ يَوْمِ يَأْتِيهَا الْخَبَرُ، لِقَوْلِ الْحَسَنِ، وَقَتَادَةَ، وَأَصْحَابِنَا، قَالَ: فَلَقِيَنِي طَلْقُ بْنُ حَبِيبٍ الْعَنَزِيُّ، فَقَالَ: إِنَّكَ عَلَيَّ كَرِيمٌ، وَإِنَّكَ مِنْ أَهْلِ بَلَدٍ الْعَيْنُ إِلَيْهِمْ سَرِيعَةٌ، وَإِنِّي لَسْتُ آمَنُ عَلَيْكَ، قَالَ: وَإِنَّكَ قُلْتَ قَوْلًا هَاهُنَا خِلَافَ قَوْلِ أَهْلِ الْبَلَدِ وَلَسْتُ آمَنُ، فَقُلْتُ: وَفِي ذَا اخْتِلَافٌ؟، قَالَ: نَعَمْ، عِدَّتُهَا مِنْ يَوْمِ يَمُوتُ، فَلَقِيتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ فَسَأَلْتُهُ، فَقَالَ: عِدَّتُهَا مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، وَسَأَلْتُ مُجَاهِدًا، فَقَالَ: عِدَّتُهَا مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، وَسَأَلْتُ عَطَاءَ بْنَ أَبِي رَبَاحٍ، فَقَالَ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، وَسَأَلْتُ أَبَا قِلَابَةَ، فَقَالَ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، وَسَأَلْتُ مُحَمَّدَ بْنَ سِيرِينَ، فَقَالَ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، قَالَ: وَحَدَّثَنِي نَافِعٌ: أَنَّ ابْنَ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، وسَمِعْت عِكْرِمَةَ، يَقُولُ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، قَالَ: وَقَالَ جَابِرُ بْنُ زَيْدٍ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، قَالَ: وَكَانَ ابْنُ عَبَّاسٍ، يَقُولُ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، قَالَ حَمَّادٌ: وَسَمِعْتُ لَيْثًا يُحَدِّثُ، عَنْ الْحَكَمِ أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مَسْعُودٍ، قَالَ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ، قَالَ: وَقَالَ عَلِيٌّ: مِنْ يَوْمِ يَأْتِيهَا الْخَبَرُ، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ: أَقُولُ: مِنْ يَوْمِ تُوُفِّيَ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Ayyuwb, amesema: Tulikumbushana huko Makkah (kuhusu) mtu anayefariki (mkewe akiwa mbali naye). Nikasema: "Eda yake (mke) inaanzia siku inapomfikia khabari," kwa kauli ya Al-Hasan, na Qataadah, na wenzetu. Akasema: Kisha Twalq bin Habiyb Al-'Anaziy akakutana nami, akasema: Hakika wewe ni mtukufu kwangu, na hakika wewe ni miongoni mwa watu wa mji ambao jicho (la watu) huwaelekea upesi, nami sina amani juu yako. Akasema: Na hakika wewe umesema hapa kauli iliyo kinyume na kauli ya watu wa mji (huu), nami sina amani (juu yako). Nikasema: Je, katika hili kuna ikhtilafu? Akasema: "Ndiyo; eda yake ni kuanzia siku anayofariki (mumewe)." Nikakutana na Sa'iyd bin Jubayr nikamuuliza, akasema: "Eda yake ni kuanzia siku aliyofariki." Na nikamuuliza Mujaahid, akasema: "Eda yake ni kuanzia siku aliyofariki." Na nikamuuliza 'Atwaa bin Abiy Rabaah, akasema: "Kuanzia siku aliyofariki." Na nikamuuliza Abuw Qilaabah, akasema: "Kuanzia siku aliyofariki." Na nikamuuliza Muhammad bin Siyriyn, akasema: "Kuanzia siku aliyofariki." Akasema: Na amenisimulia Naafi' kwamba Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: "Kuanzia siku aliyofariki." Na nilimsikia 'Ikrimah akisema: "Kuanzia siku aliyofariki." Akasema: Na Jaabir bin Zayd amesema: "Kuanzia siku aliyofariki." Akasema: Na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa akisema: "Kuanzia siku aliyofariki." Hammaad amesema: Na nilimsikia Layth akisimulia kutoka kwa Al-Hakam kwamba 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Kuanzia siku aliyofariki." Akasema: Na 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Kuanzia siku inapomfikia khabari."

'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan [Ad-Daarimiy] amesema: Mimi nasema: "Kuanzia siku aliyofariki."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
494
Hadiyth
670

55-Mlangoباب الرجل يفتي بالشيء ثم يرى غيرهMlango Wa Mtu Anayetoa Fatwa
Kuhusu Jambo, Kisha Akaona (Rai) Nyingine

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ الْفَضْلِ، عَنْ وَهْبِ بْنِ مُنَبِّهٍ، عَنْ الْحَكَمِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: أَتَيْنَا عُمَرَ فِي الْمُشَرَّكَةِ فَلَمْ يُشَرِّكْ، ثُمَّ أَتَيْنَاهُ الْعَامَ الْمُقْبِلَ فَشَرَّكَ، فَقُلْنَا لَهُ: فَقَالَ: "تِلْكَ عَلَى مَا قَضَيْنَاهُ، وَهَذِهِ عَلَى مَا قَضَيْنَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin Humayd, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Simaak bin Al-Fadhwl, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, kutoka kwa Al-Hakam bin Mas'uwd, amesema: Tulimjia 'Umar (رضي الله عنه) kuhusu (mas-ala ya) Al-Musharrakah (mirathi ambayo ndugu wa baba na mama hushirikishwa na ndugu wa mama katika theluthi), hakushirikisha. Kisha tukamjia mwaka uliofuata, akashirikisha. Tukamwambia (kuhusu hilo); akasema: "Ile ni kwa mujibu wa tulivyoihukumu (wakati ule), na hii ni kwa mujibu wa tulivyohukumu (sasa)."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
497
Hadiyth
671

56-Mlangoباب: في إعظام العلمMlango Wa Kuhusu Kuitukuza Ilimu

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا رَوْحٌ، حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ الْأَسْوَدُ، قَالَ: قَالَ ابْنُ مُنَبِّهٍ: "كَانَ أَهْلُ الْعِلْمِ فِيمَا مَضَى يَضَنُّونَ بِعِلْمِهِمْ عَنْ أَهْلِ الدُّنْيَا، فَيَرْغَبُ أَهْلُ الدُّنْيَا فِي عِلْمِهِمْ، فَيَبْذُلُونَ لَهُمْ دُنْيَاهُمْ، وَإِنَّ أَهْلَ الْعِلْمِ الْيَوْمَ بَذَلُوا عِلْمَهُمْ لِأَهْلِ الدُّنْيَا، فَزَهِدَ أَهْلُ الدُّنْيَا فِي عِلْمِهِمْ، فَضَنُّوا عَلَيْهِمْ بِدُنْيَاهُمْ"

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia Rawh, ametusimulia Hajjaaj Al-Aswad, amesema: Ibn Munabbih amesema: "Watu wa ilimu katika zama zilizopita walikuwa wakiifanyia ubakhili ilimu yao kwa watu wa dunia; basi watu wa dunia wakaitamani ilimu yao, wakawatolea dunia yao. Na hakika watu wa ilimu leo wamewatolea watu wa dunia ilimu yao; basi watu wa dunia wakaipuuza ilimu yao, na wakawafanyia ubakhili dunia yao."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
499
Hadiyth
672

أَخْبَرَنَا يَعْقُوبُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُمَرَ بْنِ الْكُمَيْتِ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ وَهْبٍ الْهَمْدَانِيُّ، حَدَّثَنَا الضَّحَّاكُ بْنُ مُوسَى، قَالَ: "مَرَّ سُلَيْمَانُ بْنُ عَبْدِ الْمَلِكِ بِالْمَدِينَةِ وَهُوَ يُرِيدُ مَكَّةَ، فَأَقَامَ بِهَا أَيَّامًا، فَقَالَ: هَلْ بِالْمَدِينَةِ أَحَدٌ أَدْرَكَ أَحَدًا مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، فَقَالُوا لَهُ: أَبُو حَازِمٍ، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ، فَلَمَّا دَخَلَ عَلَيْهِ، قَالَ لَهُ: يَا أَبَا حَازِمٍ، مَا هَذَا الْجَفَاءُ؟، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، وَأَيُّ جَفَاءٍ رَأَيْتَ مِنِّي؟، قَالَ: أَتَانِي وُجُوهُ أَهْلِ الْمَدِينَةِ وَلَمْ تَأْتِنِي، قَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، أُعِيذُكَ بِاللَّهِ أَنْ تَقُولَ مَا لَمْ يَكُنْ، مَا عَرَفْتَنِي قَبْلَ هَذَا الْيَوْمِ، وَلَا أَنَا رَأَيْتُكَ، قَالَ: فَالْتَفَتَ سُلَيْمَانُ إِلَى مُحَمَّدِ بْنِ شِهَابٍ الزُّهْرِيِّ، فَقَالَ أَصَابَ الشَّيْخُ: وَأَخْطَأْتُ، قَالَ سُلَيْمَانُ: يَا أَبَا حَازِمٍ، مَا لَنَا نَكْرَهُ الْمَوْتَ؟، قَالَ: لِأَنَّكُمْ أَخْرَبْتُمْ الْآخِرَةَ، وَعَمَّرْتُمْ الدُّنْيَا، فَكَرِهْتُمْ أَنْ تَنْتَقِلُوا مِنْ الْعُمْرَانِ إِلَى الْخَرَابِ، قَالَ: أَصَبْتَ يَا أَبَا حَازِمٍ، فَكَيْفَ الْقُدُومُ غَدًا عَلَى اللَّهِ؟، قَالَ: أَمَّا الْمُحْسِنُ، فَكَالْغَائِبِ يَقْدُمُ عَلَى أَهْلِهِ، وَأَمَّا الْمُسِيءُ، فَكَالْآبِقِ يَقْدُمُ عَلَى مَوْلَاهُ، فَبَكَى سُلَيْمَانُ، وَقَالَ: لَيْتَ شِعْرِي مَا لَنَا عِنْدَ اللَّهِ؟، قَالَ: اعْرِضْ عَمَلَكَ عَلَى كِتَابِ اللَّهِ، قَالَ: وَأَيُّ مَكَانٍ أَجِدُهُ؟، قَالَ: {إِنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ}، قَالَ سُلَيْمَانُ: فَأَيْنَ رَحْمَةُ اللَّهِ يَا أَبَا حَازِمٍ؟، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: رَحْمَةَ اللَّهِ قَرِيبٌ مِنْ الْمُحْسِنِينَ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: يَا أَبَا حَازِمٍ، فَأَيُّ عِبَادِ اللَّهِ أَكْرَمُ؟، قَالَ: أُولُو الْمُرُوءَةِ وَالنُّهَى، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: يَا أَبَا حَازِمٍ، فَأَيُّ الْأَعْمَالِ أَفْضَلُ؟، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: أَدَاءُ الْفَرَائِضِ مَعَ اجْتِنَابِ الْمَحَارِمِ، قَالَ سُلَيْمَانُ: فَأَيُّ الدُّعَاءِ أَسْمَعُ؟، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: دُعَاءُ الْمُحْسَنِ إِلَيْهِ لِلْمُحْسِنِ، قَالَ: فَأَيُّ الصَّدَقَةِ أَفْضَلُ؟، قَالَ: لِلسَّائِلِ الْبَائِسِ، وَجُهْدُ الْمُقِلِّ لَيْسَ فِيهَا مَنٌّ وَلَا أَذًى، قَالَ: فَأَيُّ الْقَوْلِ أَعْدَلُ؟، قَالَ: قَوْلُ الْحَقِّ عِنْدَ مَنْ تَخَافُهُ أَوْ تَرْجُوهُ، قَالَ: فَأَيُّ الْمُؤْمِنِينَ أَكْيَسُ؟، قَالَ: رَجُلٌ عَمِلَ بِطَاعَةِ اللَّهِ وَدَلَّ النَّاسَ عَلَيْهَا، قَالَ: فَأَيُّ الْمُؤْمِنِينَ أَحْمَقُ؟، قَالَ: رَجُلٌ انْحَطَّ فِي هَوَى أَخِيهِ وَهُوَ ظَالِمٌ، فَبَاعَ آخِرَتَهُ بِدُنْيَا غَيْرِهِ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: أَصَبْتَ، فَمَا تَقُولُ فِيمَا نَحْنُ فِيهِ؟، قَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، أَوَ تُعْفِينِي؟، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: لَا، وَلَكِنْ نَصِيحَةٌ تُلْقِيهَا إِلَيَّ، قَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، إِنَّ آبَاءَكَ قَهَرُوا النَّاسَ بِالسَّيْفِ، وَأَخَذُوا هَذَا الْمُلْكَ عَنْوَةً عَلَى غَيْرِ مَشُورَةٍ مِنْ الْمُسْلِمِينَ، وَلَا رِضًا لَهُمْ حَتَّى قَتَلُوا مِنْهُمْ مَقْتَلَةً عَظِيمَةً، فَقَدْ ارْتَحَلُوا عَنْهَا، فَلَوْ شَعَرْتَ مَا قَالُوهُ، وَمَا قِيلَ لَهُمْ؟، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ مِنْ جُلَسَائِهِ: بِئْسَ مَا قُلْتَ يَا أَبَا حَازِمٍ، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: كَذَبْتَ، إِنَّ اللَّهَ أَخَذَ مِيثَاقَ الْعُلَمَاءِ لَيُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا يَكْتُمُونَهُ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: فَكَيْفَ لَنَا أَنْ نُصْلِحَ؟، قَالَ: تَدَعُونَ الصَّلَفَ، وَتَمَسَّكُونَ بِالْمُرُوءَةِ، وَتَقْسِمُونَ بِالسَّوِيَّةِ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: كَيْفَ لَنَا بِالْمَأْخَذِ بِهِ؟، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: تَأْخُذُهُ مِنْ حِلِّهِ، وَتَضَعُهُ فِي أَهْلِهِ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: هَلْ لَكَ يَا أَبَا حَازِمٍ أَنْ تَصْحَبَنَا فَتُصِيبَ مِنَّا وَنُصِيبَ مِنْكَ؟ قَالَ: أَعُوذُ بِاللَّهِ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: وَلِمَ ذَاكَ؟، قَالَ: أَخْشَى أَنْ أَرْكَنَ إِلَيْكُمْ شَيْئًا قَلِيلًا فَيُذِيقَنِي اللَّهُ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: ارْفَعْ إِلَيْنَا حَوَائِجَكَ؟، قَالَ: تُنْجِينِي مِنْ النَّارِ وَتُدْخِلُنِي الْجَنَّةَ، قَالَ سُلَيْمَانُ: لَيْسَ ذَاكَ إِلَيَّ، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: فَمَا لِي إِلَيْكَ حَاجَةٌ غَيْرُهَا، قَالَ: فَادْعُ لِي، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: اللَّهُمَّ إِنْ كَانَ سُلَيْمَانُ وَلِيَّكَ، فَيَسِّرْهُ لِخَيْرِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَإِنْ كَانَ عَدُوَّكَ، فَخُذْ بِنَاصِيَتِهِ إِلَى مَا تُحِبُّ وَتَرْضَى، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: قَطُّ، قَالَ أَبُو حَازِمٍ: قَدْ أَوْجَزْتُ وَأَكْثَرْتُ إِنْ كُنْتَ مِنْ أَهْلِهِ، وَإِنْ لَمْ تَكُنْ مِنْ أَهْلِهِ فَمَا يَنْفَعُنِي أَنْ أَرْمِيَ عَنْ قَوْسٍ لَيْسَ لَهَا وَتَرٌ؟، قَالَ لَهُ سُلَيْمَانُ: أَوْصِنِي، قَالَ: سَأُوصِيكَ وَأُوجِزُ: عَظِّمْ رَبَّكَ وَنَزِّهْهُ أَنْ يَرَاكَ حَيْثُ نَهَاكَ، أَوْ يَفْقِدَكَ حَيْثُ أَمَرَكَ، فَلَمَّا خَرَجَ مِنْ عِنْدِهِ، بَعَثَ إِلَيْهِ بِمِائَةِ دِينَارٍ، وَكَتَبَ إِلَيْهِ: أَنْ أَنْفِقْهَا وَلَكَ عِنْدِي مِثْلُهَا كَثِيرٌ، قَالَ: فَرَدَّهَا عَلَيْهِ وَكَتَبَ إِلَيْهِ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، أُعِيذُكَ بِاللَّهِ أَنْ يَكُونَ سُؤَالُكَ إِيَّايَ هَزْلًا، أَوْ رَدِّي عَلَيْكَ بَذْلًا وَمَا أَرْضَاهَا لَكَ، فَكَيْفَ أَرْضَاهَا لِنَفْسِي؟ وَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ مُوسَى بْنَ عِمْرَانَ لَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ، وَجَدَ عَلَيْهَا رِعَاءً يَسْقُونَ، وَوَجَدَ مِنْ دُونِهِمْ جَارِيَتَيْنِ تَذُودَانِ، فَسَأَلَهُمَا، فَقَالَتَا: {لا نَسْقِي حَتَّى يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ فَسَقَى لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّى إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنْزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ}، وَذَلِكَ أَنَّهُ كَانَ جَائِعًا خَائِفًا لَا يَأْمَنُ، فَسَأَلَ رَبَّهُ وَلَمْ يَسْأَلْ النَّاسَ، فَلَمْ يَفْطِنْ الرِّعَاءُ وَفَطِنَتْ الْجَارِيتَانِ، فَلَمَّا رَجَعَتَا إِلَى أَبِيهِمَا، أَخْبَرَتَاهُ بِالْقِصَّةِ وَبِقَوْلِهِ، فَقَالَ أَبُوهُمَا وَهُوَ شُعَيْبٌ: هَذَا رَجُلٌ جَائِعٌ، فَقَالَ لِإِحْدَاهُمَا: اذْهَبِي فَادْعِيهِ، فَلَمَّا أَتَتْهُ، عَظَّمَتْهُ وَغَطَّتْ وَجْهَهَا، وَقَالَتْ: {إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا} فَشَقَّ عَلَى مُوسَى حِينَ ذَكَرَتْ: أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا، وَلَمْ يَجِدْ بُدًّا مِنْ أَنْ يَتْبَعَهَا، إِنَّهُ كَانَ بَيْنَ الْجِبَالِ جَائِعًا مُسْتَوْحِشًا، فَلَمَّا تَبِعَهَا، هَبَّتْ الرِّيحُ فَجَعَلَتْ تَصْفِقُ ثِيَابَهَا عَلَى ظَهْرِهَا فَتَصِفُ لَهُ عَجِيزَتَهَا، وَكَانَتْ ذَاتَ عَجُزٍ، وَجَعَلَ مُوسَى يُعْرِضُ مَرَّةً، وَيَغُضُّ أُخْرَى، فَلَمَّا عِيلَ صَبْرُهُ، نَادَاهَا: يَا أَمَةَ اللَّهِ، كُونِي خَلْفِي وَأَرِينِي السَّمْتَ بِقَوْلِكِ، فَلَمَّا دَخَلَ عَلَى شُعَيْبٍ إِذْ هُوَ بِالْعَشَاءِ مُهَيَّأً، فَقَالَ لَهُ شُعَيْبٌ: اجْلِسْ يَا شَابُّ فَتَعَشَّ، فَقَالَ لَهُ مُوسَى: أَعُوذُ بِاللَّهِ، فَقَالَ لَهُ شُعَيْبٌ: لِمَ؟ أَمَا أَنْتَ جَائِعٌ؟، قَالَ: بَلَى، وَلَكِنِّي أَخَافُ أَنْ يَكُونَ هَذَا عِوَضًا لِمَا سَقَيْتُ لَهُمَا، وَإِنَّا مِنْ أَهْلِ بَيْتٍ لَا نَبِيعُ شَيْئًا مِنْ دِينِنَا بِمِلْءِ الْأَرْضِ ذَهَبًا، فَقَالَ لَهُ شُعَيْبٌ: لَا يَا شَابُّ، وَلَكِنَّهَا عَادَتِي وَعَادَةُ آبَائِي نُقْرِي الضَّيْفَ، وَنُطْعِمُ الطَّعَامَ، فَجَلَسَ مُوسَى، فَأَكَلَ، فَإِنْ كَانَتْ هَذِهِ الْمِائَةُ دِينَارٍ عِوَضًا لِمَا حَدَّثْتُ، فَالْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنْزِيرِ فِي حَالِ الِاضْطِرَارِ أَحَلُّ مِنْ هَذِهِ، وَإِنْ كَانَ لِحَقٍّ فِي بَيْتِ الْمَالِ، فَلِي فِيهَا نُظَرَاءُ، فَإِنْ سَاوَيْتَ بَيْنَنَا، وَإِلَّا فَلَيْسَ لِي فِيهَا حَاجَةٌ"

Ametukhabarisha Ya'quwb bin Ibraahiym, ametusimulia Muhammad bin 'Umar bin Al-Kumayt, ametusimulia 'Aliy bin Wahb Al-Hamdaaniy, ametusimulia Adhw-Dhwahhaak bin Muwsaa, amesema: Sulaymaan bin 'Abdil-Malik alipita Madiynah akiwa anakusudia (kwenda) Makkah, akakaa humo siku kadhaa. Akasema: Je, yuko Madiynah mtu yeyote aliyemdiriki mmoja wa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)? Wakamwambia: Abuw Haazim. Akamtumia (mjumbe). Alipoingia kwake, akamwambia: Yaa Abaa Haazim, ni kujitenga gani huku? Abuw Haazim akasema: Yaa Amiri wa Waumini, ni kujitenga gani umekuona kwangu? Akasema: Wamenijia watu mashuhuri wa Madiynah, nawe hukunijia. Akasema: Yaa Amiri wa Waumini, nakukinga kwa Allaah usije ukasema jambo ambalo halikuwa. Hukunijua kabla ya siku hii, wala mimi sikuwahi kukuona. Akasema: Sulaymaan akamgeukia Muhammad bin Shihaab Az-Zuhriy, akasema: Mzee amepatia, nami nimekosea. Sulaymaan akasema: Yaa Abaa Haazim, kwa nini sisi tunachukia mauti? Akasema: "Kwa sababu nyinyi mmeiharibu Aakhirah, na mmeistawisha dunia; kwa hiyo mnachukia kuhama kutoka kwenye ustawi kwenda kwenye uharibifu." Akasema: Umepatia, yaa Abaa Haazim. Basi kufika kesho kwa Allaah kutakuwaje? Akasema: "Ama mtenda wema, ni kama aliyekuwa safarini anayefika kwa ahli zake; na ama mtenda ubaya, ni kama mtumwa aliyetoroka anayefika kwa bwana wake." Sulaymaan akalia, na akasema: Laiti ningejua: tuna nini mbele ya Allaah? Akasema: "Ilinganishe amali yako na Kitabu cha Allaah." Akasema: Na ni mahali gani nitakapoipata? Akasema:

إِنَّ الأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ

Hakika Al-Abraar (watendao khayraat kwa wingi) bila shaka watakuwa katika neema (taanasa, furaha n.k). Na hakika watendao dhambi bila shaka watakuwa katika moto wa Jahiym (uwakao vikali mno). [Al-Infitwaar (82:13-14)]

Sulaymaan akasema: Basi iko wapi Rehma ya Allaah, yaa Abaa Haazim? Abuw Haazim akasema: "Rehma ya Allaah iko karibu na wafanyao ihsaan." Sulaymaan akamwambia: Yaa Abaa Haazim, basi ni waja gani wa Allaah walio watukufu zaidi? Akasema: "Wenye utu na akili." Sulaymaan akamwambia: Yaa Abaa Haazim, basi ni amali gani iliyo bora zaidi? Abuw Haazim akasema: "Kutekeleza faradhi pamoja na kujiepusha na yaliyoharamishwa." Sulaymaan akasema: Basi ni Du'aa gani inayosikilizwa zaidi? Abuw Haazim akasema: "Du'aa ya aliyefanyiwa wema kwa aliyemfanyia wema." Akasema: Basi ni swadaka gani iliyo bora zaidi? Akasema: "(Ile inayotolewa) kwa muombaji aliye katika dhiki, na juhudi ya mwenye kidogo, isiyokuwa na masimbulizi wala udhia ndani yake." Akasema: Basi ni kauli gani iliyo ya uadilifu zaidi? Akasema: "Kauli ya haki mbele ya unayemuogopa au unayemtaraji." Akasema: Basi ni Muumini gani aliye mwerevu zaidi? Akasema: "Mtu aliyetenda kwa kumtii Allaah, na akawaongoza watu kwenye (utiifu) huo." Akasema: Basi ni Muumini gani aliye mpumbavu zaidi? Akasema: "Mtu aliyeporomoka katika matamanio ya nduguye naye (nduguye) ni dhalimu, akauza Aakhirah yake kwa dunia ya mwingine." Sulaymaan akamwambia: Umepatia. Basi unasemaje kuhusu haya tuliyomo? Akasema: Yaa Amiri wa Waumini, je, utaniachilia (nisiseme)? Sulaymaan akamwambia: Hapana, lakini ni nasiha unayonipa. Akasema: Yaa Amiri wa Waumini, "Hakika baba zako waliwashinda watu kwa upanga, na wakauchukua ufalme huu kwa nguvu bila ushauri wa Waislamu wala ridhaa yao, mpaka wakaua miongoni mwao mauaji makubwa; na wamekwisha kuiondokea (dunia). Basi lau ungejua waliyoyasema, na waliyoambiwa?" Mtu mmoja miongoni mwa waliokuwa wakikaa naye akamwambia: Ni ubaya ulioje uliyoyasema, yaa Abaa Haazim! Abuw Haazim akasema: "Umesema uongo! Hakika Allaah Amechukua ahadi ya nguvu ya 'Ulamaa (Wanazuoni) kwamba bila shaka wataibainisha kwa watu na wala hawatoificha." Sulaymaan akamwambia: Basi tutawezaje kutengeneza (hali yetu)? Akasema: "Mtaacha majivuno, na mtashikamana na utu, na mtagawa kwa usawa." Sulaymaan akamwambia: Tutawezaje kuichukua (mali)? Abuw Haazim akasema: "Uichukue kutoka mahali pake pa halaal, na uiweke kwa wanaoistahiki." Sulaymaan akamwambia: Je, uko tayari, yaa Abaa Haazim, kuandamana nasi, ukapata kutoka kwetu, nasi tukapata kutoka kwako? Akasema: "Najikinga kwa Allaah." Sulaymaan akamwambia: Na kwa nini hivyo? Akasema: "Naogopa nisije nikaelemea kwenu kidogo, kisha Allaah Akanionjesha (adhabu) maradufu ya uhai na (adhabu) maradufu ya mauti." Sulaymaan akamwambia: Tuletee haja zako. Akasema: "Uniokoe na moto, na uniingize Jannah (Peponi)." Sulaymaan akasema: Hilo si langu (kulimiliki). Abuw Haazim akasema: "Basi sina haja nyingine kwako isipokuwa hiyo." Akasema: Basi niombee Du'aa. Abuw Haazim akasema:

اللَّهُمَّ إِنْ كَانَ سُلَيْمَانُ وَلِيَّكَ، فَيَسِّرْهُ لِخَيْرِ الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَإِنْ كَانَ عَدُوَّكَ، فَخُذْ بِنَاصِيَتِهِ إِلَى مَا تُحِبُّ وَتَرْضَى

Yaa Allaah, ikiwa Sulaymaan ni walii Wako, basi Mwepesishie kheri ya dunia na Aakhirah; na ikiwa ni adui Wako, basi Shika hatamu za paji lake, Umpeleke kwenye Unayoyapenda na Unayoyaridhia.

Sulaymaan akamwambia: Inatosha. Abuw Haazim akasema: "Nimekwisha kufupisha na nimekwisha kukithirisha, ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wake (wa kheri hiyo); na ikiwa wewe si miongoni mwa watu wake, basi kunifaa nini mimi kurusha (mshale) kwa upinde usio na kamba?" Sulaymaan akamwambia: Niusie. Akasema: "Nitakuusia na nitafupisha: Mtukuze Rabb wako, na Mtakase asije Akakuona mahali Alipokukataza, au Akakukosa mahali Alipokuamrisha." Alipotoka kwake, (Sulaymaan) akampelekea dinari mia moja, na akamwandikia: Zitumie, nawe una kwangu mfano wake mwingi. Akasema: Akazirudisha kwake, na akamwandikia: "Yaa Amiri wa Waumini, nakukinga kwa Allaah kwamba kuniuliza kwako kuwe ni mzaha, au kukujibu kwangu kuwe ni kutoa (ilimu kwa malipo); na sizikubali hizo kwa ajili yako, basi vipi nitazikubali kwa ajili ya nafsi yangu?" Na akamwandikia: "Hakika Muwsaa bin 'Imraan (عليه السلام) alipofika kwenye maji ya Madyan, alikuta kwenye (maji) hayo wachungaji wakinywesha (wanyama wao), na akakuta kando yao wasichana wawili wakiwazuia (wanyama wao). Akawauliza, wakasema:

لا نَسْقِي حَتَّى يُصْدِرَ الرِّعَاءُ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ فَسَقَى لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّى إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا أَنْزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ

Hatunyweshi mpaka waondoke wachungaji, na baba yetu ni mtu mzima sana. Basi akawanyweshea, kisha akageuka kwenda kivulini, akasema: Rabb wangu! Hakika mimi ni mhitajia wa kheri yoyote Utakayoniteremshia. [Al-Qaswasw (28:23-24)]

Na hilo ni kwa kuwa alikuwa na njaa, mwenye khofu, asiye na amani; akamuomba Rabb wake, wala hakuwaomba watu. Wachungaji hawakutambua, lakini wale wasichana wawili walitambua. Waliporudi kwa baba yao, wakamkhabarisha kisa (hicho) na kauli yake. Baba yao — naye ni Shu'ayb (عليه السلام) — akasema: Huyu ni mtu mwenye njaa. Akamwambia mmoja wao: Nenda ukamwite. Alipomfikia, alimheshimu na akafunika uso wake, na akasema:

إِنَّ أَبِي يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا

Baba yangu anakwita ili akulipe ujira wa kutunyweshea. [Al-Qaswasw (28:25)]

Ikawa uzito kwa Muwsaa (عليه السلام) pale alipotaja: ujira wa kutunyweshea; lakini hakupata budi ila kumfuata, kwa kuwa alikuwa kati ya milima akiwa na njaa na upweke. Alipomfuata, upepo ukavuma, ukaanza kuzipiga nguo zake (msichana) juu ya mgongo wake, zikamdhihirishia umbo la makalio yake, naye alikuwa na makalio makubwa. Muwsaa (عليه السلام) akawa mara anageuza uso, na mara nyingine anainamisha macho. Subira yake ilipomwishia, alimwita: Yaa mja wa kike wa Allaah, kuwa nyuma yangu, na unionyeshe njia kwa kauli yako. Alipoingia kwa Shu'ayb (عليه السلام), ghafla (alikuta) chakula cha usiku kiko tayari. Shu'ayb (عليه السلام) akamwambia: Keti, yaa kijana, ule chakula cha usiku. Muwsaa (عليه السلام) akamwambia: Najikinga kwa Allaah. Shu'ayb (عليه السلام) akamwambia: Kwa nini? Je, huna njaa? Akasema: Bila shaka (ninayo), lakini naogopa kwamba hiki kitakuwa ni malipo ya kuwanyweshea (wanyama wao); nami ni miongoni mwa watu wa nyumba ambao hatuuzi chochote katika Dini yetu (hata) kwa dhahabu ya kujaza ardhi. Shu'ayb (عليه السلام) akamwambia: Hapana, yaa kijana, lakini hii ni ada yangu na ada ya baba zangu: tunawakirimu wageni na tunalisha chakula. Muwsaa (عليه السلام) akaketi, akala. Basi ikiwa dinari hizi mia ni malipo ya yale niliyosimulia, basi mzoga, na damu, na nyama ya nguruwe, katika hali ya dharura, ni halaal zaidi kuliko hizi. Na ikiwa ni kwa haki (yangu) katika Baytul-Maal (hazina ya Waislamu), basi nina walio mfano wangu katika hizo; ukitusawazisha baina yetu, (sawa), la sivyo, sina haja nazo."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
499
Hadiyth
673

أَخْبَرَنَا أَبُو عُثْمَانَ الْبَصْرِيُّ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ مُسْلِمٍ الْقَسْمَلِيِّ، أَنْبَأَنَا زَيْدٌ الْعَمِّيُّ، عَنْ بَعْضِ الْفُقَهَاءِ أَنَّهُ، قَالَ: "يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، اعْمَلْ بِعِلْمِكَ، وَأَعْطِ فَضْلَ مَالِكَ، وَاحْبِسْ الْفَضْلَ مِنْ قَوْلِكَ إِلَّا بِشَيْءٍ مِنْ الْحَدِيثِ يَنْفَعُكَ عِنْدَ رَبِّكَ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ إِنَّ الَّذِي عَلِمْتَ ثُمَّ لَمْ تَعْمَلْ بِهِ قَاطِعٌ حُجَّتَكَ وَمَعْذِرَتَكَ عِنْدِ رَبِّكَ إِذَا لَقِيتَهُ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، إِنَّ الَّذِي أُمِرْتَ بِهِ مِنْ طَاعَةِ اللَّهِ لَيَشْغَلُكَ عَمَّا نُهِيتَ عَنْهُ مِنْ مَعْصِيَةِ اللَّهِ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، لَا تَكُونَنَّ قَوِيًّا فِي عَمَلِ غَيْرِكَ، ضَعِيفًا فِي عَمَلِ نَفْسِكَ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، لَا يَشْغَلَنَّكَ الَّذِي لِغَيْرِكَ عَنْ الَّذِي لَكَ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، عَظِّمْ الْعُلَمَاءَ، وَزَاحِمْهُمْ وَاسْتَمِعْ مِنْهُمْ، وَدَعْ مُنَازَعَتَهُمْ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، عَظِّمْ الْعُلَمَاءَ لِعِلْمِهِمْ، وَصَغِّرْ الْجُهَّالَ لِجَهْلِهِمْ، وَلَا تُبَاعِدْهُمْ، وَقَرِّبْهُمْ وَعَلِّمْهُمْ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، لَا تُحَدِّثْ بِحَدِيثٍ فِي مَجْلِسٍ حَتَّى تَفْهَمَهُ، وَلَا تُجِبْ امْرَأً فِي قَوْلِهِ حَتَّى تَعْلَمَ مَا قَالَ لَكَ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، لَا تَغْتَرَّ بِاللَّهِ، وَلَا تَغْتَرَّ بِالنَّاسِ، فَإِنَّ الْغِرَّةَ بِاللَّهِ تَرْكُ أَمْرِهِ، وَالْغِرَّةَ بِالنَّاسِ اتِّبَاعُ أَهْوَائِهِمْ، وَاحْذَرْ مِنْ اللَّهِ مَا حَذَّرَكَ مِنْ نَفْسِهِ، وَاحْذَرْ مِنْ النَّاسِ فِتْنَتَهُمْ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، إِنَّهُ لَا يَكْمُلُ ضَوْءُ النَّهَارِ إِلَّا بِالشَّمْسِ، كَذَلِكَ لَا تَكْمُلُ الْحِكْمَةُ إِلَّا بِطَاعَةِ اللَّهِ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، إِنَّهُ لَا يَصْلُحُ الزَّرْعُ إِلَّا بِالْمَاءِ وَالتُّرَابِ، كَذَلِكَ لَا يَصْلُحُ الْإِيمَانُ إِلَّا بِالْعِلْمِ وَالْعَمَلِ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، كُلُّ مُسَافِرٍ مُتَزَوِّدٌ، وَسَيَجِدُ إِذَا احْتَاجَ إِلَى زَادٍ مَا تَزَوَّدَ، وَكَذَلِكَ سَيَجِدُ كُلُّ عَامِلٍ إِذَا مَا احْتَاجَ إِلَى عَمَلِهِ فِي الْآخِرَةِ مَا عَمِلَ فِي الدُّنْيَا، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، إِذَا أَرَادَ اللَّهُ أَنْ يَحُضَّكَ عَلَى عِبَادَتِهِ، فَاعْلَمْ أَنَّهُ إِنَّمَا أَرَادَ أَنْ يُبَيِّنَ لَكَ كَرَامَتَكَ عَلَيْهِ، فَلَا تَحَوَّلَنَّ إِلَى غَيْرِهِ، فَتَرْجِعَ مِنْ كَرَامَتِهِ إِلَى هَوَانِهِ، يَا صَاحِبَ الْعِلْمِ، إِنَّكَ إِنْ تَنْقُلْ الْحِجَارَةَ وَالْحَدِيدَ أَهْوَنُ عَلَيْكَ مِنْ أَنْ تُحَدِّثَ مَنْ لَا يَعْقِلُ حَدِيثَكَ، وَمَثَلُ الَّذِي يُحَدِّثُ مَنْ لَا يَعْقِلُ حَدِيثَهُ كَمَثَلِ الَّذِي يُنَادِي الْمَيِّتَ وَيَضَعُ الْمَائِدَةَ لِأَهْلِ الْقُبُورِ"

Ametukhabarisha Abuw 'Uthmaan Al-Baswriy, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Muslim Al-Qasmaliy, ametupa khabari Zayd Al-'Ammiy, kutoka kwa baadhi ya Fuqahaa (Wanazuoni wa Fiqh), kwamba alisema: "Yaa mwenye ilimu! Tenda kwa ilimu yako, na toa ziada ya mali yako, na zuia ziada ya maneno yako, isipokuwa kitu katika Hadiyth kitakachokunufaisha mbele ya Rabb wako. Yaa mwenye ilimu! Hakika ulichokijua kisha usikifanyie kazi kinakata hoja yako na udhuru wako mbele ya Rabb wako utakapokutana Naye. Yaa mwenye ilimu! Hakika yale uliyoamrishwa katika kumtii Allaah yatakushughulisha mbali na yale uliyokatazwa katika kumuasi Allaah. Yaa mwenye ilimu! Usiwe kabisa mwenye nguvu katika amali ya mwingine, dhaifu katika amali ya nafsi yako. Yaa mwenye ilimu! Kisikushughulishe kabisa kilicho cha mwingine, ukaacha kilicho chako. Yaa mwenye ilimu! Watukuze 'Ulamaa (Wanazuoni), na usongamane nao, na usikilize kutoka kwao, na uache kuzozana nao. Yaa mwenye ilimu! Watukuze 'Ulamaa kwa sababu ya ilimu yao, na uwadunishe wajinga kwa sababu ya ujinga wao, wala usiwaweke mbali, bali wakaribishe na uwafundishe. Yaa mwenye ilimu! Usisimulie Hadiyth katika kikao mpaka uielewe, wala usimjibu mtu katika kauli yake mpaka ujue amekuambia nini. Yaa mwenye ilimu! Usidanganyike kuhusu Allaah, wala usidanganyike na watu; kwani kudanganyika kuhusu Allaah ni kuacha Amri Yake, na kudanganyika na watu ni kufuata matamanio yao. Na jihadhari na Allaah kwa yale Aliyokutahadharisha kuhusu Nafsi Yake, na jihadhari na watu (na) fitna yao. Yaa mwenye ilimu! Hakika mwangaza wa mchana haukamiliki ila kwa jua; vivyo hivyo hekima haikamiliki ila kwa kumtii Allaah. Yaa mwenye ilimu! Hakika mimea haitengemai ila kwa maji na udongo; vivyo hivyo imaan haitengemai ila kwa ilimu na amali. Yaa mwenye ilimu! Kila msafiri hujichukulia masurufu, na atakuta, atakapohitajia masurufu, yale aliyojichukulia; na vivyo hivyo kila mtendaji atakuta, atakapohitajia amali yake katika Aakhirah, yale aliyoyatenda duniani. Yaa mwenye ilimu! Allaah Anapotaka kukuhimiza kwenye ibaada Yake, basi jua kwamba Hakutaka ila Akubainishie utukufu wako mbele Yake; basi usigeuke kabisa kwenda kwa mwingine (asiyekuwa Yeye), ukarudi kutoka kwenye kukirimiwa Naye kwenda kwenye kudunishwa Naye. Yaa mwenye ilimu! Hakika wewe kubeba mawe na chuma ni wepesi zaidi kwako kuliko kumsimulia asiyeielewa Hadiyth yako; na mfano wa anayemsimulia asiyeielewa Hadiyth yake ni kama mfano wa anayemwita maiti, na anayeweka meza (ya chakula) kwa watu wa makaburi."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
504
Hadiyth
674

57-Mlangoرسالة عباد بن عباد الخواص الشاميMlango Wa Barua Ya 'Abbaad
Bin 'Abbaad Al-Khawwaasw Ash-Shaamiy

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ بْنُ سُلَيْمَانَ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْأِنْطَاكِيُّ، عَنْ عَبَّادِ بْنِ عَبَّادٍ الْخَوَّاصِ الشَّامِيِّ أَبِي عُتْبَةَ، قَالَ: "أَمَّا بَعْدُ، اعْقِلُوا وَالْعَقْلُ نِعْمَةٌ، فَرُبَّ ذِي عَقْلٍ قَدْ شُغِلَ قَلْبُهُ بِالتَّعَمُّقِ فِيمَا هُوَ عَلَيْهِ ضَرَرٌ، عَنْ الِانْتِفَاعِ بِمَا يَحْتَاجُ إِلَيْهِ حَتَّى صَارَ عَنْ ذَلِكَ سَاهِيًا، وَمِنْ فَضْلِ عَقْلِ الْمَرْءِ تَرْكُ النَّظَرِ فِيمَا لَا نَظَرَ فِيهِ حَتَّى لَا يَكُونَ فَضْلُ عَقْلِهِ وَبَالًا عَلَيْهِ فِي تَرْكِ مُنَافَسَةِ مَنْ هُوَ دُونَهُ فِي الْأَعْمَالِ الصَّالِحَةِ، أَوْ رَجُلٍ شُغِلَ قَلْبُهُ بِبِدْعَةٍ قَلَّدَ فِيهَا دِينَهُ رِجَالًا دُونَ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَوْ اكْتَفَى بِرَأْيِهِ فِيمَا لَا يَرَى الْهُدَى إِلَّا فِيهَا، وَلَا يَرَى الضَّلَالَةَ إِلَّا بِتَرْكِهَا، يَزْعُمُ أَنَّهُ أَخَذَهَا مِنْ الْقُرْآنِ وَهُوَ يَدْعُو إِلَى فِرَاقِ الْقُرْآنِ، أَفَمَا كَانَ لِلْقُرْآنِ حَمَلَةٌ قَبْلَهُ وَقَبْلَ أَصْحَابِهِ يَعْمَلُونَ بِمُحْكَمِهِ، وَيُؤْمِنُونَ بِمُتَشَابِهِهِ؟ وَكَانُوا مِنْهُ عَلَى مَنَارٍ لِوَضَحِ الطَّرِيقِ، وَكَانَ الْقُرْآنُ إِمَامَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِمَامًا لِأَصْحَابِهِ، وَكَانَ أَصْحَابُهُ أَئِمَّةً لِمَنْ بَعْدَهُمْ رِجَالٌ مَعْرُوفُونَ مَنْسُوبُونَ فِي الْبُلْدَانِ، مُتَّفِقُونَ فِي الرَّدِّ عَلَى أَصْحَابِ الْأَهْوَاءِ مَعَ مَا كَانَ بَيْنَهُمْ مِنْ الِاخْتِلَافِ، وَتَسَكَّعَ أَصْحَابُ الْأَهْوَاءِ بِرَأْيِهِمْ فِي سُبُلٍ مُخْتَلِفَةٍ جَائِرَةٍ عَنْ الْقَصْدِ، مُفَارِقَةٍ لِلصِّرَاطِ الْمُسْتَقِيمِ، فَتَوَّهَتْ بِهِمْ أَدِلَّاؤُهُمْ فِي مَهَامِهَ مُضِلَّةٍ، فَأَمْعَنُوا فِيهَا مُتَعَسِّفِينَ فِي تِيهِهِمْ، كُلَّمَا أَحْدَثَ لَهُمْ الشَّيْطَانُ بِدْعَةً فِي ضَلَالَتِهِمْ، انْتَقَلُوا مِنْهَا إِلَى غَيْرِهَا، لِأَنَّهُمْ لَمْ يَطْلُبُوا أَثَرَ السَّابِقِينَ، وَلَمْ يَقْتَدُوا بِالْمُهَاجِرِينَ، وَقَدْ ذُكِرَ عَنْ عُمَرَ أَنَّهُ قَالَ لِزِيَادٍ: هَلْ تَدْرِي مَا يَهْدِمُ الْإِسْلَامَ؟ زَلَّةُ عَالِمٍ، وَجِدَالُ مُنَافِقٍ بِالْقُرْآنِ، وَأَئِمَّةٌ مُضِلُّونَ، اتَّقُوا اللَّهَ وَمَا حَدَثَ فِي قُرَّائِكُمْ وَأَهْلِ مَسَاجِدِكُمْ مِنْ الْغِيبَةِ، وَالنَّمِيمَةِ، وَالْمَشْيِ بَيْنَ النَّاسِ بِوَجْهَيْنِ وَلِسَانَيْنِ، وَقَدْ ذُكِرَ أَنَّ مَنْ كَانَ ذَا وَجْهَيْنِ فِي الدُّنْيَا، كَانَ ذَا وَجْهَيْنِ فِي النَّارِ، يَلْقَاكَ صَاحِبُ الْغِيبَةِ فَيَغْتَابُ عِنْدَكَ مَنْ يَرَى أَنَّكَ تُحِبُّ غِيبَتَهُ، وَيُخَالِفُكَ إِلَى صَاحِبِكَ فَيَأْتِيهِ عَنْكَ بِمِثْلِهِ، فَإِذَا هُوَ قَدْ أَصَابَ عِنْدَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْكُمَا حَاجَتَهُ، وَخَفِيَ عَلَى كُلِّ وَاحِدٍ مِنْكُمَا مَا أُتِيَ بِهِ عِنْدَ صَاحِبِهِ، حُضُورُهُ عِنْدَ مَنْ حَضَرَهُ حُضُورُ الْإِخْوَانِ، وَغَيْبَتُهُ عَنْ مَنْ غَابَ عَنْهُ غَيْبَةُ الْأَعْدَاءِ، مَنْ حَضَرَ مِنْهُمْ كَانَتْ لَهُ الْأَثَرَةُ، وَمَنْ غَابَ مِنْهُمْ لَمْ تَكُنْ لَهُ حُرْمَةٌ، يَفْتِنُ مَنْ حَضَرَهُ بِالتَّزْكِيَةِ، وَيَغْتَابُ مَنْ غَابَ عَنْهُ بِالْغِيبَةِ، فَيَا لَعِبَادَ اللَّهِ أَمَا فِي الْقَوْمِ مِنْ رَشِيدٍ وَلَا مُصْلِحٍ بِهِ يَقْمَعُ هَذَا عَنْ مَكِيدَتِهِ، وَيَرُدُّهُ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ الْمُسْلِمِ؟ بَلْ عَرَفَ هَوَاهُمْ فِيمَا مَشَى بِهِ إِلَيْهِمْ، فَاسْتَمْكَنَ مِنْهُمْ وَأَمْكَنُوهُ مِنْ حَاجَتِهِ، فَأَكَلَ بِدِينِهِ مَعَ أَدْيَانِهِمْ، فَاللَّهَ اللَّهَ، ذُبُّوا عَنْ حُرَمِ أَعْيَانِكُمْ، وَكُفُّوا أَلْسِنَتَكُمْ عَنْهُمْ إِلَّا مِنْ خَيْرٍ، وَنَاصِحُوا اللَّهَ فِي أُمَّتِكُمْ إِذْ كُنْتُمْ حَمَلَةَ الْكِتَابِ وَالسُّنَّةِ، فَإِنَّ الْكِتَابَ لَا يَنْطِقُ حَتَّى يُنْطَقَ بِهِ، وَإِنَّ السُّنَّةَ لَا تَعْمَلُ حَتَّى يُعْمَلَ بِهَا، فَمَتَى يَتَعَلَّمُ الْجَاهِلُ إِذَا سَكَتَ الْعَالِمُ، فَلَمْ يُنْكِرْ مَا ظَهَرَ، وَلَمْ يَأْمُرْ بِمَا تُرِكَ؟ وَقَدْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ، اتَّقُوا اللَّهَ فَإِنَّكُمْ فِي زَمَانٍ رَقَّ فِيهِ الْوَرَعُ، وَقَلَّ فِيهِ الْخُشُوعُ، وَحَمَلَ الْعِلْمَ مُفْسِدُوهُ، فَأَحَبُّوا أَنْ يُعْرَفُوا بِحَمْلِهِ، وَكَرِهُوا أَنْ يُعْرَفُوا بِإِضَاعَتِهِ، فَنَطَقُوا فِيهِ بِالْهَوَى لَمَّا أَدْخَلُوا فِيهِ مِنْ الْخَطَإِ، وَحَرَّفُوا الْكَلِمَ عَمَّا تَرَكُوا مِنْ الْحَقِّ إِلَى مَا عَمِلُوا بِهِ مِنْ بَاطِلٍ، فَذُنُوبُهُمْ ذُنُوبٌ لَا يُسْتَغْفَرُ مِنْهَا، وَتَقْصِيرُهُمْ تَقْصِيرٌ لَا يُعْتَرَفُ بِهِ، كَيْفَ يَهْتَدِي الْمُسْتَدِلُّ الْمُسْتَرْشِدُ إِذَا كَانَ الدَّلِيلُ حَائِرًا؟ أَحَبُّوا الدُّنْيَا، وَكَرِهُوا مَنْزِلَةَ أَهْلِهَا، فَشَارَكُوهُمْ فِي الْعَيْشِ، وَزَايَلُوهُمْ بِالْقَوْلِ، وَدَافَعُوا بِالْقَوْلِ عَنْ أَنْفُسِهِمْ أَنْ يُنْسَبُوا إِلَى عَمَلِهِمْ، فَلَمْ يَتَبَرَّءُوا مِمَّا انْتَفَوْا مِنْهُ، وَلَمْ يَدْخُلُوا فِيمَا نَسَبُوا إِلَيْهِ أَنْفُسَهُمْ، لِأَنَّ الْعَامِلَ بِالْحَقِّ مُتَكَلِّمٌ وَإِنْ سَكَتَ، وَقَدْ ذُكِرَ أَنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَقُولُ: إِنِّي لَسْتُ كُلَّ كَلَامِ الْحَكِيمِ أَتَقَبَّلُ: وَلَكِنِّي أَنْظُرُ إِلَى هَمِّهِ وَهَوَاهُ، فَإِنْ كَانَ هَمُّهُ وَهَوَاهُ لِي، جَعَلْتُ صَمْتَهُ حَمْدًا وَوَقَارًا، وَإِنْ لَمْ يَتَكَلَّمْ، وَقَالَ اللَّهُ تَعَالَى: {مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا}: كُتُبًا، وَقَالَ: {خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ}، قَالَ: الْعَمَلُ بِمَا فِيهِ، وَلَا تَكْتَفُوا مِنْ السُّنَّةِ بِانْتِحَالِهَا بِالْقَوْلِ دُونَ الْعَمَلِ بِهَا، فَإِنَّ انْتِحَالَ السُّنَّةِ دُونَ الْعَمَلِ بِهَا كَذِبٌ بِالْقَوْلِ مَعَ إِضَاعَةِ الْعِلْمِ، وَلَا تَعِيبُوا بِالْبِدَعِ تَزَيُّنًا بِعَيْبِهَا، فَإِنَّ فَسَادَ أَهْلِ الْبِدَعِ لَيْسَ بِزَائِدٍ فِي صَلَاحِكُمْ، وَلَا تَعِيبُوهَا بَغْيًا عَلَى أَهْلِهَا، فَإِنَّ الْبَغْيَ مِنْ فَسَادِ أَنْفُسِكُمْ، وَلَيْسَ يَنْبَغِي لِلطَّبِيبِ أَنْ يُدَاوِيَ الْمَرْضَى بِمَا يُبَرِّئُهُمْ وَيُمْرِضُهُ، فَإِنَّهُ إِذَا مَرِضَ، اشْتَغَلَ بِمَرَضِهِ عَنْ مُدَاوَاتِهِمْ، وَلَكِنْ يَنْبَغِي أَنْ يَلْتَمِسَ لِنَفْسِهِ الصِّحَّةَ لِيَقْوَى بِهِ عَلَى عِلَاجِ الْمَرْضَى، فَلْيَكُنْ أَمْرُكُمْ فِيمَا تُنْكِرُونَ عَلَى إِخْوَانِكُمْ نَظَرًا مِنْكُمْ لِأَنْفُسِكُمْ وَنَصِيحَةً مِنْكُمْ لِرَبِّكُمْ، وَشَفَقَةً مِنْكُمْ عَلَى إِخْوَانِكُمْ، وَأَنْ تَكُونُوا مَعَ ذَلِكَ بِعُيُوبِ أَنْفُسِكُمْ أَعْنَى مِنْكُمْ بِعُيُوبِ غَيْرِكُمْ، وَأَنْ يَسْتَفْطِمَ بَعْضُكُمْ بَعْضًا النَّصِيحَةَ، وَأَنْ يَحْظَى عِنْدَكُمْ مَنْ بَذَلَهَا لَكُمْ وَقَبِلَهَا مِنْكُمْ، وَقَدْ قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ رَحِمَ اللَّهُ مَنْ أَهْدَى إِلَيَّ عُيُوبِي، تُحِبُّونَ أَنْ تَقُولُوا فَيُحْتَمَلَ لَكُمْ، وَإِنْ قِيلَ مِثْلُ الَّذِي قُلْتُمْ، غَضِبْتُمْ، تَجِدُونَ عَلَى النَّاسِ فِيمَا تُنْكِرُونَ مِنْ أُمُورِهِمْ، وَتَأْتُونَ مِثْلَ ذَلِكَ أَفَلَا تُحِبُّونَ أَنْ يُؤْخَذَ عَلَيْكُمْ؟ اتَّهِمُوا رَأْيَكُمْ وَرَأْيَ أَهْلِ زَمَانِكُمْ، وَتَثَبَّتُوا قَبْلَ أَنْ تَكَلَّمُوا، وَتَعَلَّمُوا قَبْلَ أَنْ تَعْمَلُوا، فَإِنَّهُ يَأْتِي زَمَانٌ يَشْتَبِهُ فِيهِ الْحَقُّ وَالْبَاطِلُ، وَيَكُونُ الْمَعْرُوفُ فِيهِ مُنْكَرًا، وَالْمُنْكَرُ فِيهِ مَعْرُوفًا، فَكَمْ مِنْ مُقْتَرِبٍ إِلَى اللَّهِ بِمَا يُبَاعِدُهُ، وَمُتَحَبِّبٍ إِلَيْهِ بِمَا يُبْغِضُهُ عَلَيْهِ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: {أَفَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا}، الْآيَةَ، فَعَلَيْكُمْ بِالْوُقُوفِ عِنْدَ الشُّبُهَاتِ حَتَّى يَبْرُزَ لَكُمْ وَاضِحُ الْحَقِّ بِالْبَيِّنَةِ، فَإِنَّ الدَّاخِلَ فِيمَا لَا يَعْلَمُ بِغَيْرِ عِلْمٍ آثِمٌ، وَمَنْ نَظَرَ لِلَّهِ، نَظَرَ اللَّهُ لَهُ، عَلَيْكُمْ بِالْقُرْآنِ فَأْتَمُّوا بِهِ، وَأُمُّوا بِهِ، وَعَلَيْكُمْ بِطَلَبِ أَثَرِ الْمَاضِينَ، فِيهِ، وَلَوْ أَنَّ الْأَحْبَارَ وَالرُّهْبَانَ لَمْ يَتَّقُوا زَوَالَ مَرَاتِبِهِمْ، وَفَسَادَ مَنْزِلَتِهِمْ بِإِقَامَةِ الْكِتَابِ بأَعْمَالِهِمُ، وَتِبْيَانِهِ مَا حَرَّفُوهُ وَلَا كَتَمُوهُ، وَلَكِنَّهُمْ لَمَّا خَالَفُوا الْكِتَابَ بِأَعْمَالِهِمْ، الْتَمَسُوا أَنْ يَخْدَعُوا قَوْمَهُمْ عَمَّا صَنَعُوا مَخَافَةَ أَنْ يُفْسِدُوا مَنَازِلَهُمْ، وَأَنْ يَتَبَيَّنَ لِلنَّاسِ فَسَادُهُمْ فَحَرَّفُوا الْكِتَابَ بِالتَّفْسِيرِ، وَمَا لَمْ يَسْتَطِيعُوا تَحْرِيفَهُ، كَتَمُوهُ، فَسَكَتُوا عَنْ صَنِيعِ أَنْفُسِهِمْ إِبْقَاءً عَلَى مَنَازِلِهِمْ، وَسَكَتُوا عَمَّا صَنَعَ قَوْمُهُمْ مُصَانَعَةً لَهُمْ، وَقَدْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ، بَلْ مَالَئوا عَلَيْهِ وَرَفَقُوا لَهُمْ فِيهِ"

Ametukhabarisha 'Abdul-Malik bin Sulaymaan Abuw 'Abdir-Rahmaan Al-Antwaakiy, kutoka kwa 'Abbaad bin 'Abbaad Al-Khawwaasw Ash-Shaamiy Abuw 'Utbah, amesema: "Ammaa ba'd (Ama baada ya hayo): Tumieni akili, na akili ni Neema. Kwani huenda mwenye akili moyo wake ukashughulishwa na kuzama kwa kina katika yale yaliyo madhara juu yake, (ukaachana) na kunufaika na yale anayoyahitajia, mpaka akawa ameyaghafilikia. Na katika ziada ya akili ya mtu ni kuacha kutazama katika yale yasiyostahiki kutazamwa, ili ziada ya akili yake isiwe balaa juu yake kwa kuacha kushindana na aliye chini yake katika amali njema. Au mtu ambaye moyo wake umeshughulishwa na bid'ah (uzushi katika Dini), ambayo katika hiyo amewafuata kibubusa katika Dini yake watu badala ya Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); au ametosheka na rai yake katika (bid'ah) ambayo haoni uongofu isipokuwa ndani yake, wala haoni upotofu isipokuwa kwa kuiacha; anadai kwamba ameichukua kutoka katika Qur-aan, na hali yeye analingania kujitenga na Qur-aan. Je, kwani Qur-aan haikuwa na wabebaji wake kabla yake na kabla ya wenzake, wanaotenda kwa (Aayaat) zake zenye maana wazi, na wanaziamini zile zisizokuwa wazi maana zake? Na walikuwa, kutokana nayo, juu ya mnara (wa alama) kwa ajili ya uwazi wa njia. Na Qur-aan ilikuwa ndiyo kiongozi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa kiongozi wa Swahaba wake (رضي الله عنهم), na Swahaba wake (رضي الله عنهم) walikuwa viongozi wa waliokuja baada yao — watu wanaojulikana, wanaonasibishwa na miji (yao), walioafikiana katika kuwaraddi watu wa hawaa (matamanio ya nafsi), pamoja na tofauti zilizokuwa baina yao. Na watu wa hawaa wakatangatanga kwa rai zao katika njia mbali mbali zilizopotoka mbali na njia (ya haki), zilizofarikiana na njia iliyonyooka. Viongozi wao wa njia wakawapoteza katika majangwa yanayopotosha, nao wakazama ndani yake wakitangatanga ovyo katika upotevu wao. Kila mara shaytwaan anapowazushia bid'ah katika upotofu wao, huihama kwenda kwenye nyingine; kwa sababu wao hawakutafuta nyayo za waliotangulia, wala hawakuwaiga Muhaajiruwn (waliohajiri kwenda Madiynah) (رضي الله عنهم). Na imetajwa kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه) kwamba alimwambia Ziyaad: Je, unajua kinachoibomoa Islaam? Kuteleza kwa 'Aalim (Mwanazuoni), na mabishano ya mnafiki kwa (kutumia) Qur-aan, na Imaam wapotoshaji. Mcheni Allaah, na (jihadharini na) yaliyozuka kwa wasomaji wenu wa Qur-aan na watu wa Misikiti yenu, ya kusengenya, na kufitinisha, na kutembea baina ya watu kwa nyuso mbili na ndimi mbili. Na imetajwa kwamba aliyekuwa mwenye nyuso mbili duniani, atakuwa mwenye nyuso mbili motoni. Mwenye kusengenya hukutana nawe, akamsengenya mbele yako yule ambaye anaona kwamba wewe unapenda asengenywe; kisha anakwenda kinyume chako kwa mwenzako, akamletea kutoka kwako mfano wa hayo. Basi hapo yeye amekwisha kupata kwa kila mmoja wenu wawili haja yake, na kila mmoja wenu wawili amefichikiwa na yale aliyoyaleta kwa mwenzake. Kuhudhuria kwake kwa aliye mbele yake ni kuhudhuria kwa ndugu, na kutokuwepo kwake kwa asiyekuwepo ni kutokuwepo kwa maadui. Aliyehudhuria miongoni mwao ana upendeleo, na asiyekuwepo miongoni mwao hana heshima. Anamfitini aliye mbele yake kwa kumsifu, na anamsengenya asiyekuwepo kwa usengenyaji. Enyi waja wa Allaah! Je, hakuna miongoni mwa watu mwongofu, wala mtengenezaji ambaye kwa (juhudi) yake angemzuia huyu na hila zake, na angemrudisha mbali na heshima ya ndugu yake Muislamu? Bali ameijua hawaa yao katika yale aliyoyapeleka kwao, akapata nafasi juu yao, nao wakampa uwezo wa (kupata) haja yake; basi akala kwa Dini yake pamoja na Dini zao. Basi (mcheni) Allaah, (mcheni) Allaah! Ziteteeni heshima za watu wenu mashuhuri, na zizuieni ndimi zenu kwao isipokuwa kwa kheri. Na mfanyieni Allaah nasaha katika Ummah wenu, kwa kuwa nyinyi ni wabebaji wa Kitabu na Sunnah. Kwani Kitabu hakitamki mpaka kitamkwe, na Sunnah haitendi mpaka itendewe kazi. Basi ni lini mjinga atajifunza ikiwa 'Aalim amenyamaza, asikatae (maovu) yaliyodhihiri, wala asiamrishe (mema) yaliyoachwa? Na hakika Allaah Amechukua ahadi ya nguvu ya wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Mcheni Allaah, kwani nyinyi mko katika zama ambazo wara' (kujiepusha na yenye shaka) umepungua ndani yake, na unyenyekevu umekuwa mchache ndani yake, na ilimu wameibeba wenye kuiharibu. Wakapenda wajulikane kwa kuibeba, na wakachukia wajulikane kwa kuipoteza. Basi wakatamka ndani yake kwa hawaa, kwa sababu ya makosa waliyoyaingiza ndani yake; na wakabadilisha maneno kutoka katika yale waliyoyaacha ya haki, kuyapeleka kwenye yale waliyoyatenda ya baatwil. Basi madhambi yao ni madhambi yasiyoombewa Maghfirah, na upungufu wao ni upungufu usiokiriwa. Vipi atahidika mwenye kutafuta mwelekezaji, mwenye kutaka kuongozwa, ikiwa mwelekezaji mwenyewe amechanganyikiwa? Wameipenda dunia, na wakachukia daraja ya watu wake; basi wakashirikiana nao katika maisha, na wakajitenga nao kwa kauli; na wakajitetea kwa kauli wasinasibishwe na amali yao. Basi hawakujitoa katika yale waliyojikana nayo, wala hawakuingia katika yale waliyozinasibisha nafsi zao nayo; kwa sababu mwenye kuitenda haki ni mzungumzaji hata akinyamaza. Na imetajwa kwamba Allaah (تعالى) Anasema: Hakika Mimi Sipokei kila neno la mwenye hekima, lakini Ninatazama hima yake na matakwa yake. Basi ikiwa hima yake na matakwa yake ni kwa ajili Yangu, Nitaufanya ukimya wake kuwa himdi na utulivu (wa heshima), hata kama hakusema. Na Allaah (تعالى) Amesema:

مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا

Mfano wa wale waliobebeshwa Tawraat, kisha wasiibebe ni kama mfano wa punda abebaye mijalada ya vitabu [Al-Jumu’ah (62:5)]

(Yaani): vitabu. Na Amesema:

خُذُوا مَا آتَيْنَاكُمْ بِقُوَّةٍ

Shikilieni Tuliyokupeni kwa nguvu [Al-Baqarah (2:63)]

Amesema: (Maana yake ni) kutenda kwa yaliyomo ndani yake. Na msitosheke katika Sunnah kwa kujidai nayo kwa kauli bila ya kuitendea kazi; kwani kujidai Sunnah bila ya kuitendea kazi ni uongo kwa kauli pamoja na kuipoteza ilimu. Wala msizikosoe bid'ah kwa ajili ya kujipamba kwa kuzikosoa, kwani uharibifu wa watu wa bid'ah hauzidishi chochote katika wema wenu; wala msizikosoe kwa kuwafanyia jeuri watu wake, kwani jeuri ni katika uharibifu wa nafsi zenu. Na haimpasi tabibu kuwatibu wagonjwa kwa kitu kinachowaponya na kumtia yeye ugonjwa; kwani akiugua, atashughulika na ugonjwa wake, akaacha kuwatibu. Lakini inampasa ajitafutie nafsi yake afya, ili kwayo apate nguvu ya kuwatibu wagonjwa. Basi jambo lenu katika yale mnayowakemea ndugu zenu liwe ni kuziangalia nafsi zenu, na nasaha kutoka kwenu kwa Rabb wenu, na huruma kutoka kwenu kwa ndugu zenu; na pamoja na hayo, muwe wenye kujishughulisha zaidi na aibu za nafsi zenu kuliko aibu za wengine; na mtakiane nasaha nyinyi kwa nyinyi; na apate hadhi kwenu yule anayewapa (nasaha) na anayeipokea kutoka kwenu. Na hakika 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: Allaah Amrehemu mtu aliyenizawadia aibu zangu. Mnapenda kusema mkavumiliwa, na ikisemwa mfano wa yale mliyoyasema, mnakasirika. Mnawakasirikia watu kwa yale mnayoyakemea katika mambo yao, na nyinyi mnafanya mfano wa hayo; je, basi hampendi kwamba mchukuliwe hatua juu yenu? Itilieni shaka rai yenu na rai ya watu wa zama zenu; na hakikisheni kabla ya kusema, na jifunzeni kabla ya kutenda. Kwani zitakuja zama ambazo haki na baatwil zitatatanishwa ndani yake, na mema yatakuwa ndani yake ni maovu, na maovu yatakuwa ndani yake ni mema. Basi ni wangapi wanaojikurubisha kwa Allaah kwa kile kinachowaweka mbali (Naye), na wanaojipendekeza Kwake kwa kile kinachomfanya Awachukie! Allaah (تعالى) Amesema:

أَفَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ فَرَآهُ حَسَنًا

Je, yule aliyepambiwa uovu wa amali yake akaiona ni nzuri (je, ni sawa na aliyehidika?) [Faatwir (35:8)]

mpaka mwisho wa Aayah. Basi shikamaneni na kusimama penye mambo yenye utata, mpaka iwadhihirikie haki iliyo wazi kwa hoja bayana; kwani mwenye kuingia katika asiyoyajua bila ya ilimu ni mwenye dhambi. Na mwenye kuangalia kwa ajili ya Allaah, Allaah Atamwangalia. Shikamaneni na Qur-aan; basi ifanyeni kuwa kiongozi wenu, na waongozeni (wengine) kwayo. Na shikamaneni na kutafuta nyayo za waliopita katika hilo. Na lau Al-Ahbaar (Mafuqahaa wa Kiyahudi) na Ar-Ruhbaan (Monaki wa Kinaswara) wasingeogopa kuondoka kwa vyeo vyao na kuharibika kwa hadhi yao kwa kukisimamisha Kitabu kwa amali zao na kukibainisha, wasingekipotoa wala wasingekificha. Lakini walipokikhalifu Kitabu kwa amali zao, walitafuta kuwadanganya watu wao kuhusu yale waliyoyafanya, kwa kuogopa wasije wakaziharibu hadhi zao, na uharibifu wao ukabainika kwa watu. Basi wakakipotoa Kitabu kwa kukifasiri, na kile ambacho hawakuweza kukipotoa, wakakificha. Wakanyamazia matendo ya nafsi zao ili kuzihifadhi hadhi zao, na wakanyamazia yale waliyoyafanya watu wao kwa kuwabembeleza. Na hakika Allaah Amechukua ahadi ya nguvu ya wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Bali walishirikiana (na watu wao) juu ya hilo, na wakawalainikia ndani yake."

Mjalada
1
Kitabu
Muqaddimah
Ukurasa
506
Hadiyth
675