Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy03 - Kitabu Cha Zakaah

من كتاب الزكاة

1-Mlangoباب في فرض الزكاةMlango Wa Kuhusu Ufaradhi Wa Zakaah

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ زَكَرِيَّا بْنِ إِسْحَقَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ صَيْفِيٍّ، عَنْ أَبِي مَعْبَدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ، قَالَ: "إِنَّكَ تَأْتِي قَوْمًا أَهْلَ كِتَابٍ، فَادْعُهُمْ إِلَى أَنْ يَشْهَدُوا أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، فَإِنْ أَطَاعُوا لَكَ فِي ذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ فَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ فِي ذَلِكَ، فَأَخْبِرْهُمْ أَنَّ اللَّهَ فَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً فِي أَمْوَالِهِمْ، تُؤْخَذُ مِنْ أَغْنِيَائِهِمْ وَتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لَكَ فِي ذَلِكَ، فَإِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ، وَإِيَّاكَ وَدَعْوَةَ الْمَظْلُومِ، فَإِنَّهُ لَيْسَ لَهَا مِنْ دُونِ اللَّهِ حِجَابٌ"

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Zakariyyaa bin Is-haaq, kutoka kwa Yahyaa bin 'Abdi-Allaah bin Swayfiyy, kutoka kwa Abuw Ma'bad, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Mu'aadh (رضي الله عنه) Yemen, alisema: "Hakika wewe unawaendea watu ambao ni Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu). Basi walinganie kushuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni Rasuli wa Allaah. Wakikutii katika hilo, wakhabarishe kwamba Allaah Amewafaradhishia Swalaah tano katika kila mchana na usiku. Wakikutii katika hilo, wakhabarishe kwamba Allaah Amewafaradhishia swadaka (Zakaah) katika mali zao, inayochukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kurudishwa kwa mafakiri wao. Wakikutii katika hilo, basi tahadhari na (kuchukua) mali zao bora kabisa; na tahadhari na Du'aa ya aliyedhulumiwa, kwani hakika hiyo haina kizuizi chochote mbele ya Allaah."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1005
Hadiyth
1655

2-Mlangoباب المسكين الذي يتصدق عليهMlango Wa Masikini Anayepewa Swadaka

أَخْبَرَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ زِيَادٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ يُحَدِّثُ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: "لَيْسَ الْمِسْكِينُ الَّذِي تَرُدُّهُ اللُّقْمَةُ وَاللُّقْمَتَانِ، وَالْكِسْرَةُ وَالْكِسْرَتَانِ، وَالتَّمْرَةُ وَالتَّمْرَتَانِ، وَلَكِنْ الْمِسْكِينُ الَّذِي لَيْسَ لَهُ غِنًى يُغْنِيهِ، يَسْتَحْيِي أَنْ يَسْأَلَ النَّاسَ إِلْحَافًا، أَوْ لَا يَسْأَلُ النَّاسَ إِلْحَافًا"

Ametukhabarisha Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisimulia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Masikini si yule ambaye tonge moja na matonge mawili, na kipande (cha mkate) kimoja na vipande viwili, na tende moja na tende mbili humrudisha (akaondoka); lakini masikini ni yule asiye na utajiri unaomtosheleza, anaona haya kuwaomba watu kwa ung'ang'anizi — au: hawaombi watu kwa ung'ang'anizi."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1006
Hadiyth
1656

3-Mlangoباب من لم يؤد زكاة الإبل والبقر والغنمMlango Wa Asiyetoa Zakaah Ya Ngamia, Ng'ombe
Na Mbuzi Na Kondoo

أَخْبَرَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا مِنْ صَاحِبِ إِبِلٍ وَلَا بَقَرٍ وَلَا غَنَمٍ لَا يُؤَدِّي حَقَّهَا، إِلَّا أُقْعِدَ لَهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِقَاعٍ قَرْقَرٍ تَطَؤُهُ ذَاتُ الظِّلْفِ بِظِلْفِهَا، وَتَنْطَحُهُ ذَاتُ الْقَرْنِ بِقَرْنِهَا، لَيْسَ فِيهَا يَوْمَئِذٍ جَمَّاءُ وَلَا مَكْسُورَةُ الْقَرْنِ". قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا حَقُّهَا؟ قَالَ: "إِطْرَاقُ فَحْلِهَا، وَإِعَارَةُ دَلْوِهَا، وَمِنْحَتُهَا، وَحَلَبُهَا عَلَى الْمَاءِ، وَحَمْلٌ عَلَيْهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ"

Ametukhabarisha Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna mwenye ngamia, wala ng'ombe, wala mbuzi na kondoo asiyetoa haki yao, isipokuwa atakalishwa kwa ajili yao Siku ya Qiyaamah katika uwanda tambarare mpana; mwenye kwato atamkanyaga kwa kwato zake, na mwenye pembe atampiga kumbo kwa pembe yake; hakuna miongoni mwao siku hiyo asiye na pembe wala aliyevunjika pembe." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, na ni ipi haki yao? Akasema: "Kuazima dume lao kwa kupandisha, na kuazima ndoo yao, na kumuazima mtu (mnyama) wa kukamwa maziwa, na kuwakama karibu na maji, na kubeba juu yao katika Njia ya Allaah."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1006
Hadiyth
1657

حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَخْبَرَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَا مِنْ صَاحِبِ إِبِلٍ لَا يَفْعَلُ فِيهَا حَقَّهَا، إِلَّا جَاءَتْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَكْثَرُ مَا كَانَتْ قَطُّ، وَأُقْعِدَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ تَسْتَنُّ عَلَيْهِ بِقَوَائِمِهَا وَأَخْفَافِهَا، وَلَا صَاحِبِ بَقَرٍ لَا يَفْعَلُ فِيهَا حَقَّهَا، إِلَّا جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَكْثَرُ مَا كَانَتْ قَطُّ، وَأُقْعِدَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ، تَنْطَحُهُ بِقُرُونِهَا وَتَطَؤُهُ بِقَوَائِمِهَا، وَلَا صَاحِبِ غَنَمٍ لَا يَفْعَلُ فِيهَا حَقَّهَا، إِلَّا جَاءَتْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَكْثَرُ مَا كَانَتْ، وَأُقْعِدَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ، تَنْطَحُهُ بِقُرُونِهَا وَتَطَؤُهُ بِأَظْلَافِهَا، لَيْسَ فِيهَا جَمَّاءُ وَلَا مَكْسُورَةٌ قَرْنُهَا، وَلَا صَاحِبِ كَنْزٍ لَا يَفْعَلُ فِيهِ حَقَّهُ، إِلَّا جَاءَ كَنْزُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ شُجَاعًا أَقْرَعَ يَتْبَعُهُ فَاتِحًا فَاهُ، فَإِذَا أَتَاهُ، فَرَّ مِنْهُ، فَيُنَادِيهِ: خُذْ كَنْزَكَ الَّذِي خَبَّأْتَهُ. قَالَ: فَأَنَا عَنْهُ غَنِيٌّ، فَإِذَا رَأَى أَنَّهُ لَا بُدَّ مِنْهُ، سَلَكَ يَدَهُ فِي فَمِهِ فَيَقْضِمُهَا قَضْمَ الْفَحْلِ". قَالَ: قَالَ أَبُو الزُّبَيْرِ: سَمِعْتُ عُبَيْدَ بْنَ عُمَيْرٍ، يَقُولُ هَذَا الْقَوْلَ، ثُمَّ سَأَلْنَا جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، فَقَالَ مِثْلَ قَوْلِ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ. قَالَ: وَقَالَ أَبُو الزُّبَيْرِ: سَمِعْتُ عُبَيْدَ بْنَ عُمَيْرٍ يَقُولُ: قَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا حَقُّ الْإِبِلِ؟ قَالَ: "حَلَبُهَا عَلَى الْمَاءِ، وَإِعَارَةُ دَلْوِهَا، وَإِعَارَةُ فَحْلِهَا، وَمَنْحُهَا، وَحَمْلٌ عَلَيْهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ"

Ametusimulia Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdur-Razzaaq, ametukhabarisha Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha Abuz-Zubayr kwamba alimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna mwenye ngamia asiyetekeleza haki yao kwao, isipokuwa watakuja Siku ya Qiyaamah wakiwa wengi kabisa kuliko walivyopata kuwa, naye atakalishwa kwa ajili yao katika uwanda tambarare mpana; watamkanyaga mbiombio kwa miguu yao na nyayo zao. Wala mwenye ng'ombe asiyetekeleza haki yao kwao, isipokuwa watakuja Siku ya Qiyaamah wakiwa wengi kabisa kuliko walivyopata kuwa, naye atakalishwa kwa ajili yao katika uwanda tambarare mpana; watampiga kumbo kwa pembe zao na kumkanyaga kwa miguu yao. Wala mwenye mbuzi na kondoo asiyetekeleza haki yao kwao, isipokuwa watakuja Siku ya Qiyaamah wakiwa wengi kabisa kuliko walivyokuwa, naye atakalishwa kwa ajili yao katika uwanda tambarare mpana; watampiga kumbo kwa pembe zao na kumkanyaga kwa kwato zao; hakuna miongoni mwao asiye na pembe wala aliyevunjika pembe yake. Wala mwenye hazina asiyetekeleza haki yake ndani yake, isipokuwa hazina yake itakuja Siku ya Qiyaamah ikiwa nyoka mkubwa mwenye upara, akimfuata huku amefungua kinywa chake. Atakapomfikia, (mwenyewe) atamkimbia; naye (nyoka) atamwita: Chukua hazina yako uliyoificha! Akasema: Basi mimi sina haja nayo. Atakapoona kwamba hana budi naye, ataingiza mkono wake kinywani mwake, naye (nyoka) atautafuna kama anavyotafuna ngamia dume." Akasema: Abuz-Zubayr amesema: Nilimsikia 'Ubayd bin 'Umayr akisema kauli hii; kisha tukamuuliza Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), akasema mfano wa kauli ya 'Ubayd bin 'Umayr. Akasema: Na Abuz-Zubayr amesema: Nilimsikia 'Ubayd bin 'Umayr akisema: Mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, ni ipi haki ya ngamia? Akasema: "Kuwakama karibu na maji, na kuazima ndoo yao, na kuazima dume lao, na kuazima (ngamia jike) wa kukamwa maziwa, na kubeba juu yao katika Njia ya Allaah."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1007
Hadiyth
1658

أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَحْوَصِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ الْمَعْرُورِ بْنِ سُوَيْدٍ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِبَعْضِ هَذَا الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Al-Hasan bin Ar-Rabiy', ametusimulia Abul-Ahwasw, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Al-Ma'ruwr bin Suwayd, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa baadhi ya Hadiyth hii.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1009
Hadiyth
1659

4-Mlangoباب في زكاة الغنمMlango Wa Kuhusu Zakaah Ya Mbuzi Na Kondoo

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا عَبَّادُ بْنُ الْعَوَّامِ، وَإِبْرَاهِيمُ بْنُ صَدَقَةَ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "كَتَبَ الصَّدَقَةَ، وَكَانَ فِي الْغَنَمِ فِي كُلِّ أَرْبَعِينَ سَائِمَةً شَاةٌ إِلَى الْعِشْرِينَ وَمِئَةٍ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا شَاتَانِ إِلَى مِائَتَيْنِ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا ثَلَاثُ شِيَاهٍ إِلَى ثَلَاثِ مِئَةٍ، فَإِذَا زَادَتْ شَاةً، لَمْ يَجِبْ فِيهَا إِلَّا ثَلَاثُ شِيَاهٍ حَتَّى تَبْلُغَ أَرْبَعَ مِئَةٍ، فَإِذَا بَلَغَتْ أَرْبَعَ مِئَةِ شَاةٍ، فَفِي كُلِّ مِئَةٍ شَاةٌ، وَلَا تُؤْخَذُ فِي الصَّدَقَةِ هَرِمَةٌ، وَلَا ذَاتُ عَوَارٍ، وَلَا ذَاتُ عَيْبٍ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia 'Abbaad bin Al-'Awwaam na Ibraahiym bin Swadaqah, kutoka kwa Sufyaan bin Husayn, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliandika (maandiko ya) swadaka (Zakaah); na ilikuwa katika mbuzi na kondoo: katika kila arobaini wanaochunga malishoni, mbuzi mmoja, mpaka mia moja na ishirini. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) mbuzi wawili, mpaka mia mbili. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) mbuzi watatu, mpaka mia tatu. Wakizidi mbuzi mmoja, haiwajibiki ndani yao isipokuwa mbuzi watatu, mpaka wafikie mia nne. Wakifikia mbuzi mia nne, basi katika kila mia (kuna) mbuzi mmoja. Wala hachukuliwi katika swadaka (mbuzi) aliyezeeka sana, wala mwenye kasoro, wala mwenye dosari."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1009
Hadiyth
1660

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ الْخَوْلَانِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ مَعَ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ: "بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ، مِنْ مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ إِلَى شُرَحْبِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَالْحَارِثِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَنُعَيْمِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، فِي أَرْبَعِينَ شَاةً شَاةٌ إِلَى أَنْ تَبْلُغَ عِشْرِينَ وَمِئَةٍ، فَإِذَا زَادَتْ عَلَى عِشْرِينَ وَمِئَةٍ وَاحِدَةً، فَفِيهَا شَاتَانِ إِلَى أَنْ تَبْلُغَ مِائَتَيْنِ، فَإِذَا زَادَتْ وَاحِدَةً فَفِيهَا ثَلَاثَةٌ إِلَى أَنْ تَبْلُغَ ثَلَاثَ مِئَةٍ، فَمَا زَادَ، فَفِي كُلِّ مِئَةِ شَاةٍ شَاةٌ".

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd Al-Khawlaaniy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen (barua) pamoja na 'Amr bin Hazm (رضي الله عنه):

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu)

"Kutoka kwa Muhammad Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenda kwa Shurahbiyl bin 'Abdi Kulaal, na Al-Haarith bin 'Abdi Kulaal, na Nu'aym bin 'Abdi Kulaal: Katika mbuzi arobaini, (kuna) mbuzi mmoja, mpaka wafikie mia moja na ishirini. Wakizidi juu ya mia moja na ishirini mmoja, basi ndani yao (kuna) mbuzi wawili, mpaka wafikie mia mbili. Wakizidi mmoja, basi ndani yao (kuna) watatu, mpaka wafikie mia tatu. Na kilichozidi, basi katika kila mbuzi mia, (kuna) mbuzi mmoja."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1009
Hadiyth
1661

حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْحَكَمِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَنْبَأَنَا مَعْمَرٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ لَهُمْ كِتَابًا، فَذَكَرَ نَحْوَهُ

Ametusimulia Bishr bin Al-Hakam, ametusimulia 'Abdur-Razzaaq, ametupa khabari Ma'mar, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake, kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia maandiko; akataja mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1010
Hadiyth
1662

5-Mlangoباب زكاة البقرMlango Wa Zakaah Ya Ng'ombe

حَدَّثَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ شَقِيقٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، وَالْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَا: قَالَ مُعَاذٌ: "بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْيَمَنِ فَأَمَرَنِي أَنْ آخُذَ مِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ بَقَرَةً، مُسِنَّةً، وَمِنْ كُلِّ ثَلَاثِينَ تَبِيعًا أَوْ تَبِيعَةً"

Ametusimulia Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Shaqiyq, kutoka kwa Masruwq; na Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym; (wote wawili) wamesema: Mu'aadh (رضي الله عنه) amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinituma Yemen, akaniamrisha nichukue katika kila ng'ombe arobaini, musinnah (ng'ombe jike aliyetimiza miaka miwili); na katika kila (ng'ombe) thelathini, tabiy' (ndama wa mwaka mmoja) — au: tabiy'ah (ndama jike wa mwaka mmoja)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1010
Hadiyth
1663

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ يُوسُف، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ عَيَّاشٍ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ مُعَاذٍ، قَالَ: "بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْيَمَنِ، فَأَمَرَنِي أَنْ آخُذَ مِنْ الْبَقَرِ مِنْ ثَلَاثِينَ تَبِيعًا حَوْلِيًّا، وَمِنْ أَرْبَعِينَ بَقَرَةً مُسِنَّةً".

Ametukhabarisha 'Aaswim bin Yuwsuf, ametusimulia Abuw Bakr bin 'Ayyaash, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa Mu'aadh (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinituma Yemen, akaniamrisha nichukue katika ng'ombe: katika thelathini, tabiy' (ndama wa mwaka mmoja) aliyetimiza mwaka mzima; na katika arobaini, musinnah (ng'ombe jike aliyetimiza miaka miwili)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1011
Hadiyth
1664

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَيَّاشٍ، بِنَحْوِهِ

Ametusimulia Ahmad bin Yuwnus, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Ayyaash, mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1011
Hadiyth
1665

6-Mlangoباب زكاة الإبلMlango Wa Zakaah Ya Ngamia

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا عَبَّادُ بْنُ الْعَوَّامِ، وَإِبْرَاهِيمُ بْنُ صَدَقَةَ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ الصَّدَقَةَ، فَلَمْ تُخْرَجْ إِلَى عُمَّالِهِ حَتَّى قُبِضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا قُبِضَ أَخَذَهَا أَبُو بَكْرٍ، فَعَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِهِ، فَلَمَّا قُبِضَ أَبُو بَكْرٍ، أَخَذَهَا عُمَرُ فَعَمِلَ بِهَا مِنْ بَعْدِهِمَا، وَلَقَدْ قُتِلَ عُمَرُ وَإِنَّهَا لَمَقْرُونَةٌ بِسَيْفِهِ أَوْ بِوَصِيَّتِهِ، وَكَانَ فِي "صَدَقَةِ الْإِبِلِ: فِي كُلِّ خَمْسٍ شَاةٌ إِلَى خَمْسٍ وَعِشْرِينَ، فَإِذَا بَلَغَتْ خَمْسًا وَعِشْرِينَ، فَفِيهَا بِنْتُ مَخَاضٍ إِلَى خَمْسٍ وَثَلَاثِينَ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ بِنْتُ مَخَاضٍ، فَابْنُ لَبُونٍ ذَكَرٌ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا بِنْتُ لَبُونٍ إِلَى خَمْسٍ وَأَرْبَعِينَ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا حِقَّةٌ إِلَى سِتِّينَ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا جَذَعَةٌ إِلَى خَمْسٍ وَسَبْعِينَ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا بِنْتَا لَبُونٍ إِلَى تِسْعِينَ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا حِقَّتَانِ إِلَى عِشْرِينَ وَمِئَةٍ، فَإِذَا زَادَتْ، فَفِيهَا فِي كُلِّ خَمْسِينَ حِقَّةٌ، وَفِي كُلِّ أَرْبَعِينَ بِنْتُ لَبُونٍ".

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia 'Abbaad bin Al-'Awwaam na Ibraahiym bin Swadaqah, kutoka kwa Sufyaan bin Husayn, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliandika (maandiko ya) swadaka (Zakaah), lakini hayakutolewa kwa watumishi wake (wakusanyaji wa Zakaah) mpaka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipofariki. Alipofariki, Abuw Bakr (رضي الله عنه) akayachukua, akayafanyia kazi baada yake. Abuw Bakr (رضي الله عنه) alipofariki, 'Umar (رضي الله عنه) akayachukua, akayafanyia kazi baada yao wawili. Na hakika 'Umar (رضي الله عنه) aliuawa, nayo (maandiko hayo) yakiwa yameambatanishwa na upanga wake — au: na wasia wake. Na ilikuwa katika "swadaka (Zakaah) ya ngamia: katika kila (ngamia) watano, mbuzi mmoja, mpaka ishirini na watano. Wakifikia ishirini na watano, basi ndani yao (kuna) bintu makhaadhw (ngamia jike aliyetimiza mwaka mmoja), mpaka thelathini na watano. Ikiwa hakuna bintu makhaadhw, basi ibn labuun (ngamia dume aliyetimiza miaka miwili), dume. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) bintu labuun (ngamia jike aliyetimiza miaka miwili), mpaka arobaini na watano. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) hiqqah (ngamia jike aliyetimiza miaka mitatu), mpaka sitini. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) jadha'ah (ngamia jike aliyetimiza miaka minne), mpaka sabini na watano. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) bintu labuun wawili, mpaka tisini. Wakizidi, basi ndani yao (kuna) hiqqah wawili, mpaka mia moja na ishirini. Wakizidi, basi ndani yao: katika kila khamsini, hiqqah mmoja; na katika kila arobaini, bintu labuun mmoja."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1011
Hadiyth
1666

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَهُ

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Sufyaan bin Husayn, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1012
Hadiyth
1667

7-Mlangoباب في زكاة الورقMlango Wa Kuhusu Zakaah Ya Fedha

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ الْخَوْلَانِيِّ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ مَعَ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ إِلَى شُرَحْبِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَالْحَارِثِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَنُعَيْمِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ: "إِنَّ فِي كُلِّ خَمْسِ أَوَاقٍ مِنْ الْوَرِقِ خَمْسَةَ دَرَاهِمَ، فَمَا زَادَ، فَفِي كُلِّ أَرْبَعِينَ دِرْهَمًا دِرْهَمٌ، وَلَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ شَيْءٌ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd Al-Khawlaaniy, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliandika (barua) pamoja na 'Amr bin Hazm (رضي الله عنه) kwenda kwa Shurahbiyl bin 'Abdi Kulaal, na Al-Haarith bin 'Abdi Kulaal, na Nu'aym bin 'Abdi Kulaal: "Hakika katika kila uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) tano za fedha, (kuna) dirhamu tano. Na kilichozidi, basi katika kila dirhamu arobaini, (kuna) dirhamu moja. Na hakuna kitu katika kilicho chini ya uwqiyyah tano."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1013
Hadiyth
1668

أَخْبَرَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عَاصِمِ بْنِ ضَمْرَةَ، عَنْ عَلِيٍّ، رَفَعَهُ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "عَفَوْتُ عَنْ صَدَقَةِ الْخَيْلِ وَالرَّقِيقِ، هَاتُوا صَدَقَةَ الرِّقَةِ مِنْ كُلِّ أَرْبَعِينَ دِرْهَمًا دِرْهَمٌ، وَلَيْسَ فِي تِسْعِينَ وَمِئَةٍ شَيْءٌ حَتَّى تَبْلُغَ مِائَتَيْنِ"

Ametukhabarisha Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Aaswim bin Dhwamrah, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), ameipandisha (Hadiyth hii) mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Nimesamehe swadaka (Zakaah) ya farasi na ya watumwa. Leteni swadaka ya fedha: katika kila dirhamu arobaini, dirhamu moja. Wala hakuna kitu katika (dirhamu) mia moja na tisini mpaka zifikie mia mbili."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1013
Hadiyth
1669

8-Mlangoباب النهي عن الفرق بين المجتمع والجمع بين المتفرقMlango Wa Katazo La Kutenganisha (Mifugo) Iliyokusanyika
Na Kukusanya (Mifugo) Iliyotengana

أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ عُثْمَانَ الثَّقَفِيِّ، عَنْ أَبِي لَيْلَى هُوَ الْكِنْدِيُّ، عَنْ سُوَيْدِ بْنِ غَفَلَةَ، قَالَ: أَتَانَا مُصَدِّقُ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَخَذْتُ بِيَدِهِ، فَقَرَأْتُ فِي عَهْدِهِ: "أَنْ لَا يُجْمَعَ بَيْنَ مُتَفَرِّقٍ، وَلَا يُفَرَّقَ بَيْنَ مُجْتَمِعٍ خَشْيَةَ الصَّدَقَةِ"

Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa 'Uthmaan Ath-Thaqafiy, kutoka kwa Abuw Laylaa — naye ni Al-Kindiy —, kutoka kwa Suwayd bin Ghafalah, amesema: Mkusanyaji wa Zakaah wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitujia; nikamshika mkono wake, nikasoma katika maandiko ya agizo lake: "Kwamba isikusanywe (mifugo) iliyotengana, wala isitenganishwe (mifugo) iliyokusanyika, kwa kuogopa swadaka (Zakaah)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1014
Hadiyth
1670

9-Mlangoباب النهي عن أخذ الصدقة من كرائم أموال الناسMlango Wa Katazo La Kuchukua Swadaka
Kutoka Katika Mali Bora Kabisa Za Watu

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ زَكَرِيَّا، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ صَيْفِيٍّ، عَنْ أَبِي مَعْبَدٍ مَوْلَى ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا بَعَثَ مُعَاذًا إِلَى الْيَمَنِ، قَالَ: "إِيَّاكَ وَكَرَائِمَ أَمْوَالِهِمْ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Zakariyyaa, kutoka kwa Yahyaa bin 'Abdi-Allaah bin Swayfiyy, kutoka kwa Abuw Ma'bad mawlaa (mwachwa huru) wa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomtuma Mu'aadh (رضي الله عنه) Yemen, alisema: "Tahadhari na (kuchukua) mali zao bora kabisa."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1015
Hadiyth
1671

10-Mlangoباب ما لا تجب فيه الصدقة من الحيوانMlango Wa Kile Ambacho Swadaka Haiwajibiki
Ndani Yake Katika Wanyama

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ قَالَ: عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دِينَارٍ أَخْبَرَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ سُلَيْمَانَ بْنَ يَسَارٍ يُحَدِّثُ، عَنْ عِرَاكِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَيْسَ عَلَى فَرَسِ الْمُسْلِمِ وَلَا عَلَى غُلَامِهِ صَدَقَةٌ"

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, amesema: 'Abdu-Allaah bin Diynaar amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia Sulaymaan bin Yasaar akisimulia kutoka kwa 'Iraak bin Maalik, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakuna swadaka (Zakaah) juu ya Muislamu katika farasi wake wala katika mtumwa wake."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1015
Hadiyth
1672

11-Mlangoباب ما لا يجب فيه الصدقة من الحبوب والورق والذهبMlango Wa Kile Ambacho Swadaka Haiwajibiki
Ndani Yake Katika Nafaka, Fedha Na Dhahabu

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ يَحْيَى، أَخْبَرَنِي أَبِي عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسُقٍ صَدَقَةٌ، وَلَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ صَدَقَةٌ، وَلَا فِيمَا دُونَ خَمْسِ ذَوْدٍ صَدَقَةٌ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: الْوَسْقُ: سِتُّونَ صَاعًا، وَالصَّاعُ: مَنَوَانِ وَنِصْفٌ فِي قَوْلِ أَهْلِ الْحِجَازِ، وَأَرْبَعَةُ أَمْنَاءٍ فِي قَوْلِ أَهْلِ الْعِرَاقِ

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Amr bin Yahyaa, amenikhabarisha baba yangu, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakuna swadaka (Zakaah) katika kilicho chini ya wasq (kipimo cha ujazo cha pishi sitini) tano; wala hakuna swadaka katika kilicho chini ya uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) tano; wala (hakuna swadaka) katika kilicho chini ya ngamia watano."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Al-wasq ni swaa' (pishi) sitini; na swaa' ni manaa (kipimo cha uzito sawa na ratli mbili) mbili na nusu kwa kauli ya watu wa Hijaaz, na manaa nne kwa kauli ya watu wa 'Iraaq.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1016
Hadiyth
1673

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ أُمَيَّةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عُمَارَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسُقٍ صَدَقَةٌ مِنْ حَبٍّ وَلَا تَمْرٍ، وَلَا فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ صَدَقَةٌ، وَلَا فِيمَا دُونَ خَمْسِ ذَوْدٍ صَدَقَةٌ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Umayyah, kutoka kwa Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa Yahyaa bin 'Umaarah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna swadaka (Zakaah) katika kilicho chini ya wasq (kipimo cha ujazo cha pishi sitini) tano za nafaka wala za tende; wala hakuna swadaka katika kilicho chini ya uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) tano; wala hakuna swadaka katika kilicho chini ya ngamia watano."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1017
Hadiyth
1674

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ الْخَوْلَانِيِّ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ مَعَ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ إِلَى شُرَحْبِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَالْحَارِثِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَنُعَيْمِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ: "إِنَّ فِي كُلِّ خَمْسِ أَوَاقٍ مِنْ الْوَرِقِ خَمْسَةَ دَرَاهِمَ فَمَا زَادَ، فَفِي كُلِّ أَرْبَعِينَ دِرْهَمًا دِرْهَمٌ، وَلَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ شَيْءٌ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd Al-Khawlaaniy, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliandika (barua) pamoja na 'Amr bin Hazm (رضي الله عنه) kwenda kwa Shurahbiyl bin 'Abdi Kulaal, na Al-Haarith bin 'Abdi Kulaal, na Nu'aym bin 'Abdi Kulaal: "Hakika katika kila uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) tano za fedha, (kuna) dirhamu tano. Na kilichozidi, basi katika kila dirhamu arobaini, (kuna) dirhamu moja. Na hakuna kitu katika kilicho chini ya uwqiyyah tano."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1017
Hadiyth
1675

12-Mlangoباب في تعجيل الزكاةMlango Wa Kuhusu Kuharakisha Zakaah

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ زَكَرِيَّا، عَنْ الْحَجَّاجِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ الْحَكَمِ بْنِ عُتَيْبَةَ، عَنْ حُجَيَّةَ بْنِ عَدِيٍّ، عَنْ عَلِيٍّ: أَنَّ الْعَبَّاسَ "سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ تَعْجِيلِ صَدَقَتِهِ قَبْلَ أَنْ تَحِلَّ، فَرَخَّصَ لَهُ فِي ذَلِكَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: آخُذُ بِهِ، وَلَا أَرَى فِي تَعْجِيلِ الزَّكَاةِ بَأْسًا

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia Ismaa'iyl bin Zakariyyaa, kutoka kwa Al-Hajjaaj bin Diynaar, kutoka kwa Al-Hakam bin 'Utaybah, kutoka kwa Hujayyah bin 'Adiyy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba Al-'Abbaas (رضي الله عنه) "alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kuharakisha (kutoa) swadaka (Zakaah) yake kabla ya kuwajibika kwake, akamruhusu katika hilo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ninaifuata (Hadiyth) hii, na sioni ubaya wowote katika kuharakisha Zakaah.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1017
Hadiyth
1676

13-Mlangoباب ما يجب في مال سوى الزكاةMlango Wa Kinachowajibika Katika Mali Kisichokuwa Zakaah

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الطُّفَيْلِ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ فَاطِمَةَ بِنْتِ قَيْسٍ، قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ حَقًّا سِوَى الزَّكَاةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Atw-Twufayl, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Abuw Hamzah, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Faatwimah bint Qays (رضي الله عنها), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika katika mali zenu kuna haki isiyokuwa Zakaah."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1019
Hadiyth
1677

14-Mlangoباب فيمن يتصدق على غنيMlango Wa Kuhusu Anayempa Swadaka Tajiri

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، حَدَّثَنَا أَبُو الْجُوَيْرِيَةِ الْجَرْمِيُّ، أَنَّ مَعْنَ بْنَ يَزِيدَ حَدَّثَهُ، قَالَ: بَايَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ أَنَا وَأَبِي وَجَدِّي، وَخَطَبَ عَلَيَّ فَأَنْكَحَنِي، وَخَاصَمْتُ إِلَيْهِ، وَكَانَ أَبِي يَزِيدُ أَخْرَجَ دَنَانِيرَ يَتَصَدَّقُ بِهَا فَوَضَعَهَا عِنْدَ رَجُلٍ فِي الْمَسْجِدِ، فَجِئْتُ فَأَخَذْتُهَا، فَأَتَيْتُهُ بِهَا، فَقَالَ: وَاللَّهِ مَا إِيَّاكَ أَرَدْتُ بِهَا، فَخَاصَمْتُهُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "لَكَ مَا نَوَيْتَ يَا يَزِيدُ، وَلَكَ يَا مَعْنُ مَا أَخَذْتَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Israaiyl, ametusimulia Abul-Juwayriyah Al-Jarmiy, kwamba Ma'n bin Yaziyd (رضي الله عنهما) alimsimulia, amesema: Nilimpa bay'ah (ahadi ya utiifu) Rasuli wa Allaah, mimi na baba yangu na babu yangu (رضي الله عنهما); na akaniposea (mke), akanioza; na nilipeleka shauri (langu) kwake. Baba yangu Yaziyd (رضي الله عنه) alikuwa ametoa dinari (kadhaa) ili azitoe swadaka, akaziweka kwa mtu mmoja Msikitini. Nikaja nikazichukua, nikamjia nazo. Akasema: Wa-Allaahi, si wewe niliyekukusudia kwazo. Nikashtakiana naye kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Wewe una ulichokinuia, yaa Yaziyd; na wewe, yaa Ma'n, una ulichokichukua."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1020
Hadiyth
1678

15-Mlangoباب من تحل له الصدقةMlango Wa Anayehalalikiwa Na Swadaka

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، وَأَبُو نُعَيْمٍ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سَعْدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ رَيْحَانَ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَحِلُّ الصَّدَقَةُ لِغَنِيٍّ وَلَا لِذِي مِرَّةٍ سَوِيٍّ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: يَعْنِي: قَوِيٍّ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf na Abuw Nu'aym, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Sa'd bin Ibraahiym, kutoka kwa Rayhaan bin Yaziyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Swadaka haimhalalikii tajiri, wala mwenye nguvu aliye mzima wa viungo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yaani: mwenye nguvu.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1020
Hadiyth
1679

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ سَأَلَ عَنْ ظَهْرِ غِنًى، جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَفِي وَجْهِهِ خُمُوشٌ أَوْ كُدُوحٌ أَوْ خُدُوشٌ". قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَمَا الْغِنَى؟ قَالَ: "خَمْسُونَ دِرْهَمًا أَوْ قِيمَتُهَا مِنْ الذَّهَبِ".

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Hakiym bin Jubayr, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeomba na hali ana kinachomtosheleza, atakuja Siku ya Qiyaamah na usoni mwake kuna mikwaruzo — au: michubuko, au: majeraha ya kukwaruzwa." Pakasemwa: Yaa Rasula-Allaah, na ni kipi kinachomtosheleza? Akasema: "Dirhamu khamsini, au thamani yake katika dhahabu."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1022
Hadiyth
1680

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، وَمُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، بِنَحْوِهِ

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim na Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Hakiym bin Jubayr, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1023
Hadiyth
1681

16-Mlangoباب الصدقة لا تحل للنبي صلى الله عليه وسلم ولا لأهل بيتهMlango Wa Swadaka Haimhalalikii
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Wala Watu Wa Nyumbani Kwake

أَخْبَرَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ زِيَادٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ قَالَ: أَخَذَ الْحَسَنُ تَمْرَةً مِنْ تَمْرِ الصَّدَقَةِ، فَجَعَلَهَا فِي فِيهِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كِخْ كِخْ أَلْقِهَا، أَمَا شَعَرْتَ أَنَّا لَا نَأْكُلُ الصَّدَقَةَ؟"

Ametukhabarisha Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Al-Hasan (رضي الله عنه) alichukua tende moja katika tende za swadaka, akaitia kinywani mwake. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Acha! Acha! Itupe! Je, hukutambua kwamba sisi hatuli swadaka?"

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1023
Hadiyth
1682

أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عِيسَى، عَنْ عِيسَى، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ أَبِي لَيْلَى، قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعِنْدَهُ الْحَسَنُ بْنُ عَلِيٍّ، فَأَخَذَ تَمْرَةً مِنْ تَمْرِ الصَّدَقَةِ فَانْتَزَعَهَا مِنْهُ، وَقَالَ: "أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ لَا تَحِلُّ لَنَا الصَّدَقَةُ"

Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Iysaa, kutoka kwa 'Iysaa, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Abuw Laylaa (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na kwake alikuwepo Al-Hasan bin 'Aliy (رضي الله عنهما). Akachukua tende moja katika tende za swadaka; (Nabiy) akainyang'anya kutoka kwake, na akasema: "Je, hujui kwamba swadaka haituhalalikii sisi?"

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1023
Hadiyth
1683

17-Mlangoباب التشديد على من يسأل وهو غنيMlango Wa Onyo Kali
Kwa Anayeomba Naye Ni Mwenye Kujitosheleza

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ وَهْبِ بْنِ مُنَبِّهٍ، عَنْ أَخِيهِ، عَنْ مُعَاوِيَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تُلْحِفُوا بِي فِي الْمَسْأَلَةِ فَوَاللَّهِ لَا يَسْأَلُنِي أَحَدٌ شَيْئًا فَأُعْطِيَهُ وَأَنَا كَارِهٌ، فَيُبَارَكَ لَهُ فِيهِ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Wahb bin Munabbih, kutoka kwa ndugu yake [Hammaam bin Munabbih], kutoka kwa Mu'aawiyah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msinisisitizie kwa ung'ang'anizi katika kuomba; kwani Wa-Allaahi, hakuna yeyote anayeniomba kitu, nikampa nami nikiwa sipendi, kisha akabarikiwa ndani yake."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1024
Hadiyth
1684

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ هُوَ ابْنُ زُرَيْعٍ، أَخْبَرَنَا سَعِيدٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ مَعْدَانَ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ ثَوْبَانَ مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ سَأَلَ النَّاسَ مَسْأَلَةً وَهُوَ عَنْهَا غَنِيٌّ، كَانَتْ شَيْنًا فِي وَجْهِهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd — naye ni Ibn Zuray' —, ametukhabarisha Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa Ma'daan bin Abiy Twalhah, kutoka kwa Thawbaan (رضي الله عنه), mawlaa (mwachwa huru) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayewaomba watu ombi lolote naye amejitosheleza nalo (hana haja nalo), litakuwa ni aibu usoni mwake."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1024
Hadiyth
1685

18-Mlangoباب في الاستعفاف عن المسألةMlango Wa Kuhusu Kujizuia Na Kuomba

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَزِيدَ اللَّيْثِيِّ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، أَنَّ نَاسًا مِنْ الْأَنْصَارِ سَأَلُوا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَعْطَاهُمْ، ثُمَّ سَأَلُوا فَأَعْطَاهُمْ، حَتَّى إِذَا نَفِدَ مَا عِنْدَهُ، فَقَالَ: "مَا يَكُونُ عِنْدِي مِنْ خَيْرٍ، فَلَنْ أَدَّخِرَهُ عَنْكُمْ، وَمَنْ يَسْتَعْفِفْ، يُعِفَّهُ اللَّهُ، وَمَنْ يَسْتَغْنِ، يُغْنِهِ اللَّهُ، وَمَنْ يَتَصَبَّرْ، يُصَبِّرْهُ اللَّهُ، وَمَا أُعْطِيَ أَحَدٌ عَطَاءً هُوَ خَيْرٌ وَأَوْسَعُ مِنْ الصَّبْرِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Atwaa bin Yaziyd Al-Laythiy, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba watu katika Answaar (رضي الله عنهم) walimuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akawapa; kisha wakaomba, akawapa; mpaka kilipomalizika alichokuwa nacho, akasema: "Kheri yoyote nitakayokuwa nayo, sitaiweka akiba nikakunyimeni. Na atakayejitahidi kujizuia (kuomba), Allaah Atamzuia; na atakayejitosheleza, Allaah Atamtosheleza; na atakayejitahidi kusubiri, Allaah Atampa subira. Na hakuna yeyote aliyepewa kipawa bora na kipana zaidi kuliko subira."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1025
Hadiyth
1686

19-Mlangoباب النهي عن رد الهديةMlango Wa Katazo La Kurudisha Zawadi

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَالِمٍ، أَنَّهُ قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ، يَقُولُ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْطِينِي الْعَطَاءَ فَأَقُولُ: أَعْطِهِ مَنْ هُوَ أَفْقَرُ إِلَيْهِ مِنِّي. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "خُذْهُ، وَمَا آتَاكَ اللَّهُ مِنْ هَذَا الْمَالِ وَأَنْتَ غَيْرُ مُشْرِفٍ وَلَا سَائِلٍ، فَخُذْهُ، وَمَا لَا، فَلَا تُتْبِعْهُ نَفْسَكَ".

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amesema: Amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Saalim, kwamba alisema: 'Abdu-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما) amesema: Nilimsikia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akinipa kipawa, nami husema: Mpe aliye mhitaji zaidi kuliko mimi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ichukue. Na kinachokujia katika mali hii nawe huna tamaa nacho wala hukukiomba, basi kichukue; na kisichokuwa hivyo, usiifanye nafsi yako ikifuate."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1025
Hadiyth
1687

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، حَدَّثَنِي السَّائِبُ بْنُ يَزِيدَ، أَنَّ حُوَيْطِبَ بْنَ عَبْدِ الْعُزَّى أَخْبَرَهُ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ السَّعْدِيِّ أَخْبَرَهُ، عَنْ عُمَرَ، بِنَحْوِهِ.

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenisimulia As-Saaib bin Yaziyd (رضي الله عنه), kwamba Huwaytwib bin 'Abdil-'Uzzaa (رضي الله عنه) alimkhabarisha, kwamba 'Abdu-Allaah bin As-Sa'diy (رضي الله عنه) alimkhabarisha, kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه), kwa mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1026
Hadiyth
1688

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ بُكَيْرٍ، عَنْ بُسْرِ بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ ابْنِ السَّعْدِيِّ، قَالَ: اسْتَعْمَلَنِي عُمَرُ، فَذَكَرَ نَحْوًا مِنْهُ

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Al-Layth, kutoka kwa Bukayr, kutoka kwa Busr bin Sa'iyd, kutoka kwa Ibn As-Sa'diy (رضي الله عنه), amesema: 'Umar (رضي الله عنه) alinipa kazi; akataja mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1026
Hadiyth
1689

20-Mlangoباب النهي عن المسألةMlango Wa Katazo La Kuomba

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَعُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، أَنَّ حَكِيمَ بْنَ حِزَامٍ قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ، فَقَالَ: "يَا حَكِيمُ، إِنَّ هَذَا الْمَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ، فَمَنْ أَخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفْسٍ، بُورِكَ لَهُ فِيهِ، وَمَنْ أَخَذَهُ بِإِشْرَافِ نَفْسٍ لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأْكُلُ وَلَا يَشْبَعُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na 'Urwah bin Az-Zubayr, kwamba Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنه) amesema: Nilimuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akanipa; kisha nikamuomba, akanipa; kisha nikamuomba, akanipa; kisha nikamuomba, akasema: "Yaa Hakiym! Hakika mali hii ni ya kijani kibichi, tamu. Basi atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, atabarikiwa ndani yake; na atakayeichukua kwa tamaa ya nafsi, hatabarikiwa ndani yake, na atakuwa kama anayekula wala hashibi."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1027
Hadiyth
1690

21-Mlangoباب متى تستحب للرجل الصدقة؟Mlango Wa Ni Lini Swadaka Inapendekezwa Kwa Mtu

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي هِشَامٌ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "خَيْرُ الصَّدَقَةِ مَا تُصُدِّقَ بِهِ عَنْ ظَهْرِ غِنًى، وَلْيَبْدَأْ أَحَدُكُمْ بِمَنْ يَعُولُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Hishaam, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Swadaka bora ni ile inayotolewa kutoka katika ziada (baada ya kujitosheleza); na aanze mmoja wenu kwa anaowakimu."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1027
Hadiyth
1691

22-Mlangoباب في فضل اليد العلياMlango Wa Kuhusu Fadhila Za Mkono Wa Juu

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "الْيَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنْ الْيَدِ السُّفْلَى، قَالَ: وَالْيَدُ الْعُلْيَا يَدُ الْمُعْطِي، وَالْيَدُ السُّفْلَى يَدُ السَّائِلِ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini. Akasema: Na mkono wa juu ni mkono wa mtoaji, na mkono wa chini ni mkono wa mwombaji."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1028
Hadiyth
1692

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عُثْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ مُوسَى بْنَ طَلْحَةَ يَذْكُرُ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "خَيْرُ الصَّدَقَةِ عَنْ ظَهْرِ غِنًى، وَالْيَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنْ الْيَدِ السُّفْلَى، وَابْدَأْ بِمَنْ تَعُولُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Amr bin 'Uthmaan, amesema: Nilimsikia Muwsaa bin Twalhah akitaja, kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Swadaka bora ni (ile inayotolewa) kutoka katika ziada (baada ya kujitosheleza). Na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini; na anza kwa unaowakimu."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1028
Hadiyth
1693

23-Mlangoباب أي الصدقة أفضل؟Mlango Wa Swadaka Ipi Ni Bora Zaidi

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: سُلَيْمَانُ أَخْبَرَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا وَائِلٍ يُحَدِّثُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ زَيْنَبَ امْرَأَةِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّهَا قَالَتْ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ، تَصَدَّقْنَ وَلَوْ مِنْ حُلِيِّكُنَّ" وَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ خَفِيفَ ذَاتِ الْيَدِ، فَجِئْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَسْأَلُهُ، فَوَافَقَتْ زَيْنَبَ، امْرَأَةٌ مِنْ الْأَنْصَارِ، تَسْأَلُ عَمَّا أَسْأَلُ عَنْهُ، فَقُلْتُ لِبِلَالٍ: سَلْ لِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَيْنَ أَضَعُ صَدَقَتِي؟: عَلَى عَبْدِ اللَّهِ، أَوْ فِي قَرَابَتِي؟ فَسَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: أَيُّ الزَّيَانِبِ؟ فَقَالَ: امْرَأَةُ عَبْدِ اللَّهِ، فَقَالَ: "لَهَا أَجْرَانِ، أَجْرُ الْقَرَابَةِ، وَأَجْرُ الصَّدَقَةِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, amesema: Sulaymaan amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia Abuw Waail akisimulia, kutoka kwa 'Amr bin Al-Haarith, kutoka kwa Zaynab (رضي الله عنها), mke wa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kwamba alisema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Enyi kundi la wanawake! Toeni swadaka hata kama ni kutoka katika mapambo yenu." Na 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) alikuwa mwenye mkono mwepesi (wa mali). Nikaenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kumuuliza; mwanamke mmoja wa Answaar (رضي الله عنهم) akakutana na Zaynab (رضي الله عنها), akiuliza kuhusu kile ninachokiuliza. Nikamwambia Bilaal (رضي الله عنه): Niulizie Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Niiweke wapi swadaka yangu: kwa 'Abdu-Allaah, au kwa jamaa zangu wa karibu? Akamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Zaynab yupi?" Akasema: Mke wa 'Abdu-Allaah. Akasema: "Yeye ana malipo mawili: malipo ya ujamaa, na malipo ya swadaka."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1029
Hadiyth
1694

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: كَانَ أَبُو طَلْحَةَ أَكْثَرَ أَنْصَارِيٍّ بِالْمَدِينَةِ مَالًا نَخْلًا، وَكَانَتْ أَحَبَّ أَمْوَالِهِ إِلَيْهِ بَيْرُحَاءُ، وَكَانَتْ مُسْتَقْبِلَةَ الْمَسْجِدِ، وَكَانَ يَدْخُلُهَا وَيَشْرَبُ مِنْ مَائِهَا طَيِّبٌ. فَقَالَ أَنَسٌ: فَلَمَّا أُنْزِلَتْ هَذِهِ الْآيَةُ: {لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ}، قَالَ: إِنَّ أَحَبَّ أَمْوَالِي إِلَيَّ بَيْرُحَاءُ، وَإِنَّهَا صَدَقَةٌ للَّهِ أَرْجُو بِرَّهَا وَذُخْرَهَا عِنْدَ اللَّهِ، فَضَعْهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ حَيْثُ شِئْتَ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "بَخٍ ذَلِكَ مَالٌ رَابِحٌ أَوْ رَائِحٌ، وَقَدْ سَمِعْتُ مَا قُلْتَ فِيهِ، وَإِنِّي أَرَى أَنْ تَجْعَلَهُ فِي الْأَقْرَبِينَ". فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ: أَفْعَلُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَقَسَّمَهُ أَبُو طَلْحَةَ فِي قَرَابَةِ بَنِي عَمِّهِ

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Is-haaq bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Twalhah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Abuw Twalhah (رضي الله عنه) alikuwa Mwanswaari mwenye mali nyingi zaidi Madiynah, (mali yake ikiwa ni) mitende; na mali yake aliyoipenda zaidi ilikuwa (bustani ya) Bayruhaa, nayo ilikuwa inaelekeana na Msikiti; na [Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)] alikuwa akiiingia na kunywa maji yake mazuri. Anas (رضي الله عنه) amesema: Ilipoteremshwa Aayah hii:

لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ

Hamtoweza kuufikia wema uliokunjuka mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. [Aal-‘Imraan (3:92)]

[Abuw Twalhah (رضي الله عنه)] alisema: Hakika mali yangu ninayoipenda zaidi ni Bayruhaa, nayo ni swadaka kwa ajili ya Allaah; ninataraji wema wake na akiba yake kwa Allaah. Basi iweke, yaa Rasula-Allaah, popote utakapo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hongera! Hiyo ni mali yenye faida — au: yenye kurudi (thawabu zake) —; na nimesikia uliyosema kuhusu hiyo, nami naona kwamba uifanye kwa jamaa wa karibu." Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akasema: Nitafanya, yaa Rasula-Allaah. Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akaigawa kwa jamaa zake wa karibu, wana wa ami yake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1029
Hadiyth
1695

24-Mlangoباب الحث على الصدقةMlango Wa Kuhimiza Swadaka

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ هَيَّاجِ بْنِ عِمْرَانَ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ: "مَا خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا أَمَرَنَا فِيهَا بِالصَّدَقَةِ، وَنَهَانَا عَنْ الْمُثْلَةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Bashshaar, ametusimulia Mu'aadh bin Hishaam, ametusimulia baba yangu, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Hayyaaj bin 'Imraan, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutuhutubia (khutbah yoyote) ila alituamrisha ndani yake kutoa swadaka, na alitukataza kukatakata viungo (vya aliyeuawa)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1031
Hadiyth
1697

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي عَمْرُو بْنُ مُرَّةَ، قَالَ: سَمِعْتُ خَيْثَمَةَ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ، قَالَ: "اتَّقُوا النَّارَ وَلَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ، فَإِنْ لَمْ تَجِدُوا، فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَةٍ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha 'Amr bin Murrah, amesema: Nilimsikia Khaythamah, kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Jikingeni na moto hata kwa nusu ya tende; msipopata, basi (jikingeni) kwa neno zuri."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1031
Hadiyth
1698

25-Mlangoباب النهي عن الصدقة بجميع ما عند الرجلMlango Wa Katazo La Kutoa Swadaka Kwa Kila Alichonacho Mtu

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ إِبْرَاهِيمَ الدِّمَشْقِيُّ دُحَيْمٌ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مَسْلَمَةَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ أُمَيَّةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لُبَابَةَ، أَنَّ أَبَا لُبَابَةَ أَخْبَرَهُ، أَنَّهُ لَمَّا رَضِيَ عَنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ مِنْ تَوْبَتِي أَنْ أَهْجُرَ دَارَ قَوْمِي، وَأُسَاكِنَكَ، وَأَنْخَلِعَ مِنْ مَالِي صَدَقَةً لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يُجْزِي عَنْكَ الثُّلُثُ"

Ametukhabarisha 'Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym Ad-Dimashqiy Duhaym, ametusimulia Sa'iyd bin Maslamah, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Umayyah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Lubaabah, kwamba Abuw Lubaabah (رضي الله عنه) alimkhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomridhia, alisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika katika (kukamilika kwa) tawbah yangu ni kuhama nyumba ya watu wangu, na nikae karibu nawe, na nijivue na mali yangu (yote) iwe swadaka kwa ajili ya Allaah na Rasuli Wake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Inakutosheleza theluthi moja."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1031
Hadiyth
1699

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، وَأَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ عَاصِمِ بْنِ عُمَرَ بْنِ قَتَادَةَ، عَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذْ جَاءَهُ رَجُلٌ بِمِثْلِ الْبَيْضَةِ مِنْ ذَهَبٍ أَصَابَهَا فِي بَعْضِ الْمَغَازِي، قَالَ أَحْمَدُ: فِي بَعْضِ الْمَعَادِنِ، وَهُوَ الصَّوَابُ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، خُذْهَا مِنِّي صَدَقَةً، فَوَاللَّهِ مَا لِي مَالٌ غَيْرَهَا، فَأَعْرَضَ عَنْهُ، ثُمَّ جَاءَهُ عَنْ رُكْنِهِ الْأَيْسَرِ، فَقَالَ مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ جَاءَهُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ، فَقَالَ مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ قَالَ: "هَاتِهَا"، مُغْضَبًا، فَحَذَفَهُ بِهَا حَذْفَةً لَوْ أَصَابَهُ لَأَوْجَعَهُ أَوْ عَقَرَهُ ثُمَّ، قَالَ: "يَعْمِدُ أَحَدُكُمْ إِلَى مَالِهِ لَا يَمْلِكُ غَيْرَهُ فَيَتَصَدَّقُ بِهِ، ثُمَّ يَقْعُدُ يَتَكَفَّفُ النَّاسَ، إِنَّمَا الصَّدَقَةُ عَنْ ظَهْرِ غِنًى، خُذْ الَّذِي لَكَ لَا حَاجَةَ لَنَا بِهِ". فَأَخَذَ الرَّجُلُ مَالَهُ وَذَهَبَ. قَالَ أَبُو مُحَمَّد: كَانَ مَالِكٌ يَقُولُ: إِذَا جَعَلَ الرَّجُلُ مَالَهُ فِي الْمَسَاكِينِ يَتَصَدَّقُ بِثُلُثِ مَالِهِ

Ametukhabarisha Ya'laa na Ahmad bin Khaalid, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa 'Aaswim bin 'Umar bin Qataadah, kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Wakati tulipokuwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ghafla mtu mmoja akamjia na (kipande cha) dhahabu mfano wa yai, alichokipata katika baadhi ya vita — Ahmad amesema: katika baadhi ya machimbo (ya madini), nayo ndiyo sahihi —, akasema: Yaa Rasula-Allaah, ichukue kutoka kwangu iwe swadaka; kwani Wa-Allaahi, sina mali isipokuwa hiyo. (Nabiy) akampa mgongo. Kisha akamjia kutoka upande wake wa kushoto, akasema mfano wa hivyo. Kisha akamjia kutoka mbele yake, akasema mfano wa hivyo. Kisha akasema: "Ilete" — huku amekasirika —; akamtupia kwayo mtupo ambao lau ungempata, ungemuumiza au ungemjeruhi. Kisha akasema: "Mmoja wenu anaiendea mali yake asiyemiliki nyingine isipokuwa hiyo, akaitoa swadaka, kisha anakaa akiwaomba watu kwa viganja vyake! Hakika swadaka ni (ile inayotolewa) kutoka katika ziada (baada ya kujitosheleza). Chukua kilicho chako, hatuna haja nacho." Yule mtu akachukua mali yake akaenda.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Maalik alikuwa akisema: Mtu anapoifanya mali yake (yote) kwa ajili ya masikini, atatoa swadaka theluthi ya mali yake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1032
Hadiyth
1700

26-Mlangoباب الرجل يتصدق بجميع ما عندهMlango Wa Mtu Anayetoa Swadaka Kwa Kila Alichonacho

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ سَمِعْتُ عُمَرَ، قَالَ: أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ نَتَصَدَّقَ، فَوَافَقَ ذَلِكَ مَالًا عِنْدِي، فَقُلْتُ: الْيَوْمَ أَسْبِقُ أَبَا بَكْرٍ إِنْ سَبَقْتُهُ يَوْمًا. قَالَ: فَجِئْتُ بِنِصْفِ مَالِي، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا أَبْقَيْتَ لِأَهْلِكَ؟" قُلْتُ: مِثْلَهُ، قَالَ: فَأَتَى أَبُو بَكْرٍ بِكُلِّ مَا عِنْدَهُ، فَقَالَ: "يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا أَبْقَيْتَ لِأَهْلِكَ؟". فَقَالَ: أَبْقَيْتُ لَهُمْ اللَّهَ وَرَسُولَهُ. فَقُلْتُ: لَا أُسَابِقُكَ إِلَى شَيْءٍ أَبَدًا

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hishaam bin Sa'd, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa baba yake, amesema: Nilimsikia 'Umar (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha tutoe swadaka; na hilo likawa wakati nina mali. Nikasema: Leo nitamtangulia Abuw Bakr (رضي الله عنه), ikiwa nitamtangulia siku yoyote. Akasema: Nikaja na nusu ya mali yangu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Umewabakishia nini ahli zako?" Nikasema: Mfano wake. Akasema: Abuw Bakr (رضي الله عنه) akaja na kila kitu alichokuwa nacho. (Nabiy) akasema: "Yaa Abaa Bakr, umewabakishia nini ahli zako?" Akasema: Nimewabakishia Allaah na Rasuli Wake. Nikasema: Sitashindana nawe katika jambo lolote kamwe.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1033
Hadiyth
1701

27-Mlangoباب في زكاة الفطرMlango Wa Kuhusu Zakaatul-Fitwr

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، قَالَ: "فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْرِ مِنْ رَمَضَانَ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ أَوْ صَاعًا، مِنْ شَعِيرٍ عَلَى كُلِّ حُرٍّ وَعَبْدٍ، ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَى، مِنْ الْمُسْلِمِينَ". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: تَقُولُ بِهِ؟ قَالَ: مَالِكٌ كَانَ يَقُولُ بِهِ

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifaradhisha Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya kufungua Swawm) ya Ramadhwaan: Swaa' (pishi) moja ya tende, au Swaa' moja ya shayiri, juu ya kila muungwana na mtumwa, mwanamume au mwanamke, miongoni mwa Waislamu."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unashika (kauli) hiyo? Akasema: Maalik alikuwa akiishika.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1034
Hadiyth
1702

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِزَكَاةِ الْفِطْرِ عَنْ كُلِّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ، حُرٍّ أَوْ عَبْدٍ، صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ". قَالَ ابْنُ عُمَرَ: فَعَدَلَهُ النَّاسُ بِمُدَّيْنِ مِنْ بُرٍّ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrisha Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya kufungua Swawm) kwa ajili ya kila mdogo na mkubwa, muungwana au mtumwa: Swaa' (pishi) moja ya shayiri, au Swaa' moja ya tende." Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: "Watu wakaisawazisha (Swaa' hiyo) na mudd (kipimo cha ujazo wa konzi mbili za mikono) mbili za ngano."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1034
Hadiyth
1703

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ بْنُ قَيْسٍ، عَنْ عِيَاضِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: "كُنَّا نُخْرِجُ زَكَاةَ الْفِطْرِ إِذْ كَانَ فِينَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ كُلِّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ، حُرٍّ وَمَمْلُوكٍ، صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ، فَلَمْ يَزَلْ ذَلِكَ كَذَلِكَ حَتَّى قَدِمَ عَلَيْنَا مُعَاوِيَةُ الْمَدِينَةَ حَاجًّا، أَوْ مُعْتَمِرًا، فَقَالَ: إِنِّي أَرَى مُدَّيْنِ مِنْ سَمْرَاءِ الشَّامِ يَعْدِلُ صَاعًا مِنْ التَّمْرِ، فَأَخَذَ النَّاسُ بِذَلِكَ". قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: أَمَّا أَنَا، فَلَا أَزَالُ أُخْرِجُهُ كَمَا كُنْتُ أُخْرِجُهُ. قَالَ أَبُو مُحَمَّد: أَرَى صَاعًا مِنْ كُلِّ شَيْءٍ

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Daawuwd bin Qays, kutoka kwa 'Iyaadhw bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Tulikuwa tukitoa Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya kufungua Swawm) wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa pamoja nasi, kwa ajili ya kila mdogo na mkubwa, muungwana na mmilikiwa: Swaa' (pishi) moja ya chakula, au Swaa' moja ya tende, au Swaa' moja ya shayiri, au Swaa' moja ya maziwa yaliyokaushwa, au Swaa' moja ya zabibu kavu. Hilo halikuacha kuwa hivyo mpaka Mu'aawiyah (رضي الله عنه) alipotujia Madiynah akiwa anahiji au anafanya 'Umrah (Hija ndogo); akasema: Hakika mimi naona kwamba mudd (kipimo cha ujazo wa konzi mbili za mikono) mbili za ngano ya kahawia ya Shaam zinalingana na Swaa' moja ya tende. Watu wakachukua hilo." Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه) amesema: Ama mimi, sitaacha kuitoa kama nilivyokuwa nikiitoa.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Naona (itolewe) Swaa' moja kutoka katika kila kitu.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1034
Hadiyth
1704

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عِيَاضِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَعْدِ بْنِ أَبِي سَرْحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: "كُنَّا نُخْرِجُ زَكَاةَ الْفِطْرِ مِنْ رَمَضَانَ صَاعًا مِنْ طَعَامٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ تَمْرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ زَبِيبٍ، أَوْ صَاعًا مِنْ أَقِطٍ".

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Iyaadhw bin 'Abdi-Allaah bin Sa'd bin Abiy Sarh, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Tulikuwa tukitoa Zakaatul-Fitwr (Zakaah ya kufungua Swawm) ya Ramadhwaan: Swaa' (pishi) moja ya chakula, au Swaa' moja ya tende, au Swaa' moja ya shayiri, au Swaa' moja ya zabibu kavu, au Swaa' moja ya maziwa yaliyokaushwa."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1035
Hadiyth
1705

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عِيَاضِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: كُنَّا نُعْطِي عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَذَكَرَ نَحْوَهُ

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Iyaadhw bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), amesema: Tulikuwa tukitoa katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); akataja mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1035
Hadiyth
1706

28-Mlangoباب كراهية أن يكون الرجل عشاراMlango Wa Kuchukiza Mtu Kuwa Mtoza Ushuru

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ شِمَاسَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ عُقْبَةَ بْنَ عَامِرٍ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ صَاحِبُ مَكْسٍ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: يَعْنِي: عَشَّارًا

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Shumaasah, amesema: Nilimsikia 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hataingia Jannah (Pepo) mwenye maks (ushuru unaotozwa kwa dhulma)."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yaani: 'ashshaar (mtoza ushuru wa sehemu ya kumi).

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1036
Hadiyth
1708

29-Mlangoباب العشر فيما سقت السماء وفيما سقي بالنضحMlango Wa Sehemu Ya Kumi Katika Yaliyonyweshwa
Na Mvua Na Katika Yaliyonyweshwa Kwa Kumwagiliwa

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ مُعَاذٍ، قَالَ: "بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْيَمَنِ، فَأَمَرَنِي أَنْ آخُذَ مِنْ الثِّمَارِ مَا يُسْقَى بَعْلًا الْعُشْرَ، وَمَا سُقِيَ بِالسَّانِيَةِ، فَنِصْفَ الْعُشْرِ"

Ametukhabarisha 'Aaswim bin Yuwsuf, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa Mu'aadh (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinituma Yemen, akaniamrisha nichukue katika matunda: yale yanayonyweshwa ba'l (yanayonywea maji kwa mizizi yake bila kumwagiliwa), sehemu ya kumi; na yale yaliyonyweshwa kwa ngamia wa kuvuta maji, nusu ya sehemu ya kumi."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1037
Hadiyth
1709

30-Mlangoباب في الركازMlango Wa Kuhusu Rikaaz (Mali Iliyozikwa
Ardhini Tangu Zama Za Kabla Ya Islaam)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَأَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "جُرْحُ الْعَجْمَاءِ جُبَارٌ، وَالْبِئْرُ جُبَارٌ، وَالْمَعْدِنُ جُبَارٌ، وَفِي الرِّكَازِ الْخُمُسُ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Jeraha la mnyama ni hadar (halina fidia); na kisima ni hadar; na machimbo (ya madini) ni hadar; na katika rikaaz (mali iliyozikwa ardhini tangu zama za kabla ya Islaam) kuna khumsi (sehemu ya tano)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1037
Hadiyth
1710

31-Mlangoباب ما يهدى لعمال الصدقة لمن هوMlango Wa Zawadi Wanayopewa
Wakusanyaji Wa Swadaka Ni Ya Nani

أَخْبَرَنَا أَبُو الْيَمَانِ الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، حَدَّثَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ الْأَنْصَارِيِّ ثُمَّ السَّاعِدِيّ أَنَّهُ أَخْبَرَهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ اسْتَعْمَلَ عَامِلًا عَلَى الصَّدَقَةِ، فَجَاءَهُ الْعَامِلُ حِينَ فَرَغَ مِنْ عَمَلِهِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذَا الَّذِي لَكُمْ، وَهَذَا أُهْدِيَ لِي. فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: " فَهَلَّا قَعَدْتَ فِي بَيْتِ أَبِيكَ وَأُمِّكَ، فَنَظَرْتَ أَيُهْدَى لَكَ أَمْ لَا؟ ثُمَّ قَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشِيَّةً بَعْدَ الصَّلَاةِ عَلَى الْمِنْبَرِ، فَتَشَهَّدَ وَأَثْنَى عَلَى اللَّهِ بِمَا هُوَ أَهْلُهُ، ثُمَّ قَالَ: " أَمَّا بَعْدُ مَا بَالُ الْعَامِلِ نَسْتَعْمِلُهُ فَيَأْتِينَا فَيَقُولُ: هَذَا مِنْ عَمَلِكُمْ وَهَذَا أُهْدِيَ لِي؟! فَهَلَّا قَعَدَ فِي بَيْتِ أَبِيهِ وَأُمِّهِ فَيَنْظُرَ هَلْ يُهْدَى لَهُ أَمْ لَا؟ وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَا يَغُلُّ أَحَدُكُمْ مِنْهَا شَيْئًا، إِلَّا جَاءَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يَحْمِلُهُ عَلَى عُنُقِهِ: إِنْ كَانَ بَعِيرًا، جَاءَ بِهِ لَهُ رُغَاءٌ، وَإِنْ كَانَتْ بَقَرَةً، جَاءَ بِهَا لَهَا خُوَارٌ، وَإِنْ كَانَتْ شَاةً، جَاءَ بِهَا تَيْعَرُ، فَقَدْ بَلَّغْتُ ". قَالَ أَبُو حُمَيْدٍ: ثُمَّ رَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَيْهِ حَتَّى إِنَّا لَنَنْظُرُ إِلَى عُفْرَةِ إِبْطَيْهِ. قَالَ أَبُو حُمَيْدٍ: وَقَدْ سَمِعَ ذَلِكَ مَعِي مِنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ، فَسَلُوهُ

Ametukhabarisha Abul-Yamaan Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenisimulia 'Urwah bin Az-Zubayr, kutoka kwa Abuw Humayd Al-Answaariy kisha As-Saa'idiy (رضي الله عنه), kwamba alimkhabarisha kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimweka mtendaji mmoja kusimamia swadaka. Mtendaji huyo akamjia alipomaliza kazi yake, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hiki ni chenu, na hiki nimepewa zawadi. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Kwa nini hukukaa katika nyumba ya baba yako na mama yako, ukatazama je, utapewa zawadi au hapana?" Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama jioni baada ya Swalaah juu ya Minbar, akasoma Tashahhud (ya khutbah), na akamsifu Allaah kwa yale Anayostahiki, kisha akasema: "Ammaa ba'd (Ama baada ya hayo): Ana nini mtendaji tunayemtumia kazi, kisha anatujia akisema: Hiki ni katika kazi yenu, na hiki nimepewa zawadi?! Kwa nini hakukaa katika nyumba ya baba yake na mama yake, akatazama je, atapewa zawadi au hapana? Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hatafanya khiyana yeyote miongoni mwenu kwa kuchukua kitu chochote katika hiyo (swadaka), isipokuwa atakuja nacho Siku ya Qiyaamah akikibeba shingoni mwake: ikiwa ni ngamia, atakuja naye akiwa na sauti ya kulia (ya ngamia); na ikiwa ni ng'ombe, atakuja naye akiwa na sauti ya kulia (ya ng'ombe); na ikiwa ni mbuzi, atakuja naye akilia (kwa sauti ya mbuzi). Hakika nimefikisha." Abuw Humayd (رضي الله عنه) amesema: Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akainua mikono yake mpaka hakika sisi tukaona weupe wa kwapa zake. Abuw Humayd (رضي الله عنه) amesema: Na hakika Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) alisikia hilo pamoja nami kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); basi muulizeni.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1038
Hadiyth
1711

32-Mlangoباب ليرجع المصدق عنكم وهو راضMlango Wa Mkusanyaji Wa Zakaah Arudi
Kutoka Kwenu Naye Ameridhika

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ دَاوُدَ، وَمُجَالِدٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ جَرِيرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا جَاءَكُمْ الْمُصَدِّقُ، فَلَا يَصْدُرَنَّ عَنْكُمْ إِلَّا وَهُوَ رَاضٍ".

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Hushaym, kutoka kwa Daawuwd na Mujaalid, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Jariyr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mkusanyaji wa Zakaah atakapokujieni, basi asiondoke kwenu ila naye ameridhika."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1039
Hadiyth
1712

حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق الْفَزَارِيِّ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ جَرِيرٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَحْوَهُ

Amenisimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq Al-Fazaariy, kutoka kwa Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Jariyr (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1040
Hadiyth
1713

33-Mlangoباب كراهية رد السائل بغير شيءMlango Wa Kuchukiza Kumrudisha Mwombaji Bila Kitu

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا مَالِكٌ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُعَاذٍ الْأَشْهَلِيِّ، عَنْ جَدَّتِهِ يُقَالُ لَهَا حَوَّاءُ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا نِسَاءَ الْمُسْلِمَاتِ، لَا تَحْقِرَنَّ إِحْدَاكُنَّ لِجَارَتِهَا، وَلَوْ كُرَاعُ شَاةٍ مُحَرَّقٌ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Maalik, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Amr bin Mu'aadh Al-Ash-haliy, kutoka kwa bibi yake anayeitwa Hawwaa (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yaa wanawake wa Kiislamu! Asidharau mmoja wenu (kumpa) jirani yake (kitu), hata kama ni kwato ya mbuzi iliyochomwa."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1040
Hadiyth
1714

34-Mlangoباب من أسلم على شيءMlango Wa Aliyesilimu Akiwa Na Kitu

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبَانُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الْبَجَلِيُّ، حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ صَخْرِ بْنِ الْعَيْلَةِ، قَالَ: أُخِذَتْ عَمَّةُ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، فَقَدِمَتْ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَسَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَمَّتَهُ، فَقَالَ: "يَا صَخْرُ، إِنَّ الْقَوْمَ إِذَا أَسْلَمُوا، أَحْرَزُوا أَمْوَالَهُمْ وَدِمَاءَهُمْ، فَادْفَعْهَا إِلَيْهِمْ". وَكَانَ مَاءٌ لِبَنِي سُلَيْمٍ، فَأَسْلَمُوا، فَسَأَلُوهُ ذَلِكَ فَدَعَانِي، فَقَالَ: "يَا صَخْرُ، إِنَّ الْقَوْمَ إِذَا أَسْلَمُوا، أَحْرَزُوا أَمْوَالَهُمْ وَدِمَاءَهُمْ، فَادْفَعْهَا إِلَيْهِمْ" فَدَفَعْتُهَا.

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Abaan bin 'Abdi-Allaah Al-Bajaliy, ametusimulia 'Uthmaan bin Abiy Haazim, kutoka kwa Swakhr bin Al-'Aylah (رضي الله عنه), amesema: Shangazi wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه) alichukuliwa (mateka); akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). (Al-Mughiyrah) akamuomba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) (amrudishie) shangazi yake. (Nabiy) akasema: "Yaa Swakhr, hakika watu wanaposilimu, huhifadhi mali zao na damu zao; basi mkabidhi kwao." Na kulikuwa na maji (chemchemi) ya Banuw Sulaym; wakasilimu, wakamuomba hayo. Akaniita, akasema: "Yaa Swakhr, hakika watu wanaposilimu, huhifadhi mali zao na damu zao; basi yakabidhi kwao." Nikayakabidhi.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1040
Hadiyth
1715

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا أَبَانُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنِي عُثْمَانُ بْنُ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ صَخْرٍ، أَطْوَلَ مِنْ حَدِيثِ أَبِي نُعَيْمٍ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Abaan bin 'Abdi-Allaah, amenisimulia 'Uthmaan bin Abiy Haazim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake Swakhr (رضي الله عنه) — (Hadiyth) ndefu zaidi kuliko Hadiyth ya Abuw Nu'aym.

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1042
Hadiyth
1716

35-Mlangoباب في فضل الصدقةMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Swadaka

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ عِيسَى بْنِ يُونُسَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا تَصَدَّقَ امْرُؤٌ بِصَدَقَةٍ مِنْ كَسْبٍ طَيِّبٍ، وَلَا يَقْبَلُ اللَّهُ إِلَّا طَيِّبًا، إِلَّا وَضَعَهَا حِينَ يَضَعُهَا فِي كَفِّ الرَّحْمَنِ، وَإِنَّ اللَّهَ لَيُرَبِّي لِأَحَدِكُمْ التَّمْرَةَ كَمَا يُرَبِّي أَحَدُكُمْ فَلُوَّهُ أَوْ فَصِيلَهُ حَتَّى تَكُونَ مِثْلَ أُحُدٍ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Sa'iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna mtu anayetoa swadaka kutoka katika chumo zuri — na Allaah Hakubali isipokuwa kilicho kizuri — isipokuwa anaiweka, wakati anapoiweka, katika Kiganja cha Ar-Rahmaan. Na hakika Allaah Humlelea mmoja wenu tende moja kama mmoja wenu anavyomlea mwana farasi wake au mtoto wa ngamia wake, mpaka inakuwa mfano wa (mlima) Uhud."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1042
Hadiyth
1717

حَدَّثَنَا أَبُو الرَّبِيعِ الزَّهْرَانِيُّ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ جَعْفَرٍ، عَنْ الْعَلَاءِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللَّهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلَّهِ، إِلَّا رَفَعَهُ اللَّهُ"

Ametusimulia Abur-Rabiy' Az-Zahraaniy, ametusimulia Ismaa'iyl bin Ja'far, kutoka kwa Al-'Alaa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Swadaka haipunguzi mali. Na Allaah Hamzidishii mja kwa kusamehe isipokuwa utukufu. Na hakuna yeyote anayenyenyekea kwa ajili ya Allaah isipokuwa Allaah Humpandisha."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1042
Hadiyth
1718

36-Mlangoباب ليس في عوامل الإبل صدقةMlango Wa Hakuna Swadaka
Katika Ngamia Wanaotumikishwa Kazi

أَخْبَرَنَا النَّضْرُ بْنُ شُمَيْلٍ، حَدَّثَنَا بَهْزُ بْنُ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدَّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "فِي كُلِّ إِبِلٍ سَائِمَةٍ فِي كُلِّ أَرْبَعِينَ بِنْتُ لَبُونٍ، لَا تُفَرَّقُ إِبِلٌ عَنْ حِسَابِهَا، مَنْ أَعْطَاهَا مُؤْتَجِرًا بِهَا، فَلَهُ أَجْرُهَا، وَمَنْ مَنَعَهَا، فَإِنَّا آخِذُوهَا وَشَطْرَ مَالِهِ عَزْمَةٌ مِنْ عَزَمَاتِ اللَّهِ، لَا يَحِلُّ لِآلِ مُحَمَّدٍ مِنْهَا شَيْءٌ"

Ametukhabarisha An-Nadhwr bin Shumayl, ametusimulia Bahz bin Hakiym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake [Mu'aawiyah bin Haydah (رضي الله عنه)], amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Katika kila ngamia wanaochungwa (malishoni), katika kila (ngamia) arobaini (kuna) bintu labuun (ngamia jike aliyetimiza miaka miwili). Ngamia hawatenganishwi na hesabu yao. Atakayeitoa (Zakaah) akitaraji ujira kwayo, basi atapata ujira wake; na atakayeizuia, basi hakika sisi tutaichukua (Zakaah hiyo) pamoja na nusu ya mali yake — ni azimio miongoni mwa maazimio ya Allaah. Haihalaliki kwa ahli wa Muhammad chochote katika hiyo."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1043
Hadiyth
1719

37-Mlangoباب من تحل له الصدقةMlango Wa Anayehalalikiwa Na Swadaka

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، وَأَبُو نُعَيْمٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ هَارُونَ بْنِ رِئَابٍ، حَدَّثَنِي كِنَانَةُ بْنُ نُعَيْمٍ، عَنْ قَبِيصَةَ بْنِ مُخَارِقٍ الْهِلَالِيِّ، قَالَ: تَحَمَّلْتُ بِحَمَالَةٍ فَأَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَسْأَلُهُ فِيهَا، فَقَالَ: "أَقِمْ يَا قَبِيصَةُ حَتَّى تَأْتِيَنَا الصَّدَقَةُ، فَنَأْمُرَ لَكَ بِهَا"، ثُمَّ قَالَ: "يَا قَبِيصَةُ إِنَّ الْمَسْأَلَةَ لَا تَحِلُّ إِلَّا لِأَحَدِ ثَلَاثَةٍ: رَجُلٍ تَحَمَّلَ حَمَالَةً فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ، فَسَأَلَ حَتَّى يُصِيبَهَا، ثُمَّ يُمْسِكَ. وَرَجُلٍ أَصَابَتْهُ جَائِحَةٌ فَاجْتَاحَتْ مَالَهُ، فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ، فَسَأَلَ حَتَّى يُصِيبَ قِوَامًا مِنْ عَيْشٍ أَوْ قَالَ: سِدَادًا مِنْ عَيْشٍ. وَرَجُلٍ أَصَابَتْهُ فَاقَةٌ حَتَّى يَقُولَ ثَلَاثَةٌ مِنْ ذَوِي الْحِجَى مِنْ قَوْمِهِ: قَدْ أَصَابَ فُلَانًا الْفَاقَةُ، فَحَلَّتْ لَهُ الْمَسْأَلَةُ، فَسَأَلَ حَتَّى يُصِيبَ قِوَامًا مِنْ عَيْشٍ، أَوْ سِدَادًا مِنْ عَيْشٍ، ثُمَّ يُمْسِكَ، وَمَا سِوَاهُنَّ مِنْ الْمَسْأَلَةِ سُحْتٌ يَا قَبِيصَةُ يَأْكُلُهَا صَاحِبُهَا سُحْتًا"

Ametusimulia Musaddad na Abuw Nu'aym, wamesema: Ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Haaruwn bin Riyaab, amenisimulia Kinaanah bin Nu'aym, kutoka kwa Qabiyswah bin Mukhaariq Al-Hilaaliy (رضي الله عنه), amesema: Nilijitwika dhamana (ya kulipa deni au fidia kwa ajili ya kusuluhisha baina ya watu), nikamwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumuomba (msaada) kuhusu hiyo. Akasema: "Baki, yaa Qabiyswah, mpaka itujie swadaka (Zakaah), tukuamrishie upewe katika hiyo." Kisha akasema: "Yaa Qabiyswah, hakika kuomba hakuhalaliki isipokuwa kwa mmoja wa watu watatu: mtu aliyejitwika dhamana, ikamhalalikia kuomba; akaomba mpaka aipate, kisha ajizuie. Na mtu aliyefikwa na msiba ulioangamiza mali yake, ikamhalalikia kuomba; akaomba mpaka apate kinachomsimamisha maishani — au alisema: kinachomtosha maishani —. Na mtu aliyefikwa na ufukara mpaka waseme watu watatu wenye akili miongoni mwa watu wake: Kwa yakini fulani amefikwa na ufukara; ikamhalalikia kuomba; akaomba mpaka apate kinachomsimamisha maishani, au kinachomtosha maishani, kisha ajizuie. Na kisichokuwa hivyo katika kuomba ni haraam, yaa Qabiyswah; mwenyewe anaila kuwa ni haraam."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1044
Hadiyth
1720

38-Mlangoباب الصدقة على القرابةMlango Wa Swadaka Kwa Jamaa Wa Karibu

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَبَّادِ بْنِ الْعَوَّامِ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ بَشِيرٍ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ، أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الصَّدَقَاتِ أَيُّهَا أَفْضَلُ؟ قَالَ: "عَلَى ذِي الرَّحِمِ الْكَاشِحِ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Abbaad bin Al-'Awwaam, kutoka kwa Sufyaan bin Husayn, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Ayyuwb bin Bashiyr, kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنه), kwamba mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu swadaka: ipi kati yake ni bora zaidi? Akasema: "(Ni ile inayotolewa) kwa ndugu wa damu mwenye kuficha uadui (moyoni mwake)."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1045
Hadiyth
1721

أَخْبَرَنَا أَبُو حَاتِمٍ الْبَصْرِيُّ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ حَفْصَةَ بِنْتِ سِيرِينَ، عَنْ أُمِّ الرَّائِحِ بِنْتِ صُلَيْعٍ، عَنْ سَلْمَانَ بْنِ عَامِرٍ الضَّبِّيِّ، ذَكَرَ أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ الصَّدَقَةَ عَلَى الْمِسْكِينِ صَدَقَةٌ، وَإِنَّهَا عَلَى ذِي الرَّحِمِ اثْنَتَانِ، صَدَقَةٌ وَصِلَةٌ"

Ametukhabarisha Abuw Haatim Al-Baswriy, ametusimulia Ibn 'Awn, kutoka kwa Hafswah bint Siyriyn, kutoka kwa Ummur-Raaih bint Swulay', kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir Adhw-Dhwabbiy (رضي الله عنه), alitaja kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika swadaka kwa masikini ni swadaka; na hiyo kwa ndugu wa damu ni (swadaka) mbili: swadaka na kuunga udugu."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1045
Hadiyth
1722

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ ابْنِ عُيَيْنَةَ، قَالَ: وَقَدْ سَمِعْتُهُ مِنَ الثَّوْرِيِّ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ حَفْصَةَ بِنْتِ سِيرِينَ، عَنْ الرَّبَابِ، عَنْ سَلْمَانَ بْنِ عَامِرٍ الضَّبِّيِّ يَرْفَعُهُ، قَالَ: "الصَّدَقَةُ عَلَى الْمِسْكِينِ صَدَقَةٌ، وَهِيَ عَلَى ذِي الرَّحِمِ اثْنَتَانِ: صَدَقَةٌ وَصِلَةٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Ibn 'Uyaynah — amesema: Na kwa hakika nimeisikia kutoka kwa Ath-Thawriy —, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Hafswah bint Siyriyn, kutoka kwa Ar-Rabaab, kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir Adhw-Dhwabbiy (رضي الله عنه) — akiipandisha [Hadiyth hii mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)] —, amesema: "Swadaka kwa masikini ni swadaka; nayo kwa ndugu wa damu ni (swadaka) mbili: swadaka na kuunga udugu."

Mjalada
2
Kitabu
3
Ukurasa
1045
Hadiyth
1723