Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy05 - Kitabu Cha Manaasik (Ibaada Za Hajj)

من كتاب المناسك

1-Mlangoباب من أراد الحج فليتعجلMlango Wa Anayetaka Kuhiji, Basi Na Afanye Haraka

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ عَمْرٍو الْفُقَيْمِيُّ، عَنْ مِهْرَانَ أَبِي صَفْوَانَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أَرَادَ الْحَجَّ فَلْيَتَعَجَّلْ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Abuw Mu'aawiyah, ametusimulia Al-Hasan bin 'Amr Al-Fuqaymiy, kutoka kwa Mihraan Abuw Swafwaan, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwenye kutaka (kwenda) Hajj, basi na afanye haraka."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1121
Hadiyth
1825

2-Mlangoباب من مات ولم يحجMlango Wa Aliyekufa Na Hakuhiji

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَابِطٍ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ لَمْ يَمْنَعْهُ عَنْ الْحَجِّ حَاجَةٌ ظَاهِرَةٌ، أَوْ سُلْطَانٌ جَائِرٌ، أَوْ مَرَضٌ حَابِسٌ، فَمَاتَ وَلَمْ يَحُجَّ، فَلْيَمُتْ إِنْ شَاءَ يَهُودِيًّا، وَإِنْ شَاءَ نَصْرَانِيًّا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Saabitw, kutoka kwa Abuw Umaamah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ambaye hakuzuiliwa kuhiji na haja iliyo dhahiri, au mtawala dhalimu, au ugonjwa unaomzuia, kisha akafa na hakuhiji, basi na afe akipenda (akiwa) Yahudi, na akipenda (akiwa) Mnaswara."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1122
Hadiyth
1826

3-Mlangoباب في حج النبي صلى الله عليه وسلم حجة واحدةMlango Wa Kuhusu Kuhiji
Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Hajj Moja

أَخْبَرَنَا مُجَاهِدُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ آدَمَ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، قَالَ: سَمِعْتُ زَيْدَ بْنَ أَرْقَمَ، يَقُولُ: "حَجَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعْدَ هِجْرَتِهِ حَجَّةً" قَالَ: وَقَالَ أَبُو إِسْحَاق: "حَجَّ قَبْلَ هِجْرَتِهِ حَجَّةً"

Ametukhabarisha Mujaahid bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Aadam, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuw Is-haaq, amesema: Nilimsikia Zayd bin Arqam (رضي الله عنه) akisema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alihiji baada ya Hijrah yake Hajj moja." Akasema: Na Abuw Is-haaq amesema: "Alihiji kabla ya Hijrah yake Hajj moja."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1123
Hadiyth
1827

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، قَالَ: قُلْتُ لِأَنَسٍ: كَمْ حَجَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ قَالَ: "حَجَّةً وَاحِدَةً، وَاعْتَمَرَ أَرْبَعًا: عُمْرَتُهُ الْأُولَى الَّتِي صَدَّهُ الْمُشْرِكُونَ عَنْ الْبَيْتِ، وَعُمْرَتُهُ الثَّانِيَةُ حِينَ صَالَحُوهُ فَرَجَعَ مِنْ الْعَامِ الْمُقْبِلِ، وَعُمْرَتُهُ مِنْ الْجِعْرَانَةِ حِينَ قَسَّمَ غَنِيمَةَ حُنَيْنٍ فِي ذِي الْقَعْدَةِ، وَعُمْرَتُهُ مَعَ حَجَّتِهِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Qataadah, amesema: Nilimwambia Anas (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alihiji mara ngapi? Akasema: "Hajj moja, na alifanya 'Umrah (Hija ndogo) nne: 'Umrah yake ya kwanza ambayo washirikina walimzuia (kufika) Al-Bayt (Al-Ka'bah); na 'Umrah yake ya pili, walipofanya suluhu naye, akarejea (kuifanya) mwaka uliofuata; na 'Umrah yake kutoka Al-Ji'raanah, alipogawa ngawira ya Hunayn katika (mwezi wa) Dhul-Qa'dah; na 'Umrah yake pamoja na Hajj yake."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1123
Hadiyth
1828

4-Mlangoباب كيف وجوب الحجMlango Wa Namna Ya Uwajibu Wa Hajj

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سِنَانٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كُتِبَ عَلَيْكُمْ الْحَجُّ". فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ فِي كُلِّ عَامٍ؟ قَالَ: "لَا، وَلَوْ قُلْتُهَا لَوَجَبَتْ، الْحَجُّ مَرَّةٌ فَمَا زَادَ فَهُوَ تَطَوُّعٌ".

Ametusimulia Muhammad bin Kathiyr, ametusimulia Sulaymaan bin Kathiyr, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sinaan, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmeandikiwa (kufaradhishiwa) Hajj." Pakasemwa: Yaa Rasula-Allaah, (je, ni) katika kila mwaka? Akasema: "Hapana; na lau ningelisema (hilo), ingekuwa wajibu. Hajj ni mara moja; basi kilichozidi, hicho ni cha kujitolea (kwa hiari)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1124
Hadiyth
1829

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ سِمَاكٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwa namna inayokaribiana nayo.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1125
Hadiyth
1830

5-Mlangoباب المواقيت في الحجMlango Wa Miyqaat (Mipaka Ya Kuhirimia) Katika Hajj

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "وَقَّتَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ ذَا الْحُلَيْفَةِ، وَلِأَهْلِ الشَّامِ الْجُحْفَةَ، وَلِأَهْلِ نَجْدٍ قَرْنًا". قَالَ: قَالَ ابْنُ عُمَرَ: أَمَّا هَذِهِ الثَّلَاثُ فَإِنِّي سَمِعْتُهُنَّ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَبَلَغَنِي أَنَّهُ وَقَّتَ لِأَهْلِ الْيَمَنِ يَلَمْلَمَ.

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwawekea watu wa Madiynah miyqaat (mahali pa kuanzia Ihraam) ya Dhul-Hulayfah, na watu wa Shaam Al-Juhfah, na watu wa Najd Qarn." Akasema: Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: Ama hizi tatu, hakika mimi nilizisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); na imenifikia (khabari) kwamba aliwawekea watu wa Yemen Yalamlam.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1125
Hadiyth
1831

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارَ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، مِثْلَهُ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1126
Hadiyth
1832

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "وَقَّتَ لِأَهْلِ الْمَدِينَةِ ذَا الْحُلَيْفَةِ، وَلِأَهْلِ الشَّامِ الْجُحْفَةَ، وَلِأَهْلِ نَجْدٍ قَرْنَ الْمَنَازِلِ، وَلِأَهْلِ الْيَمَنِ يَلَمْلَمَ، هُنَّ لِأَهْلِهِنَّ، وَلِكُلِّ آتٍ أَتَى عَلَيْهِنَّ مِنْ غَيْرِهِنَّ مِمَّنْ أَرَادَ الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ، وَمَنْ كَانَ دُونَ ذَلِكَ فَمِنْ حَيْثُ أَنْشَأَ، حَتَّى أَهْلُ مَكَّةَ مِنْ مَكَّةَ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliwawekea watu wa Madiynah miyqaat (mahali pa kuanzia Ihraam) ya Dhul-Hulayfah, na watu wa Shaam Al-Juhfah, na watu wa Najd Qarnul-Manaazil, na watu wa Yemen Yalamlam. Hizo ni kwa ajili ya watu wake, na kwa kila anayezifikia asiyekuwa miongoni mwa watu wake, miongoni mwa wanaokusudia Hajj na 'Umrah (Hija ndogo). Na aliye ndani ya hapo, basi (ahirimie) kutoka pale alipoanzia (safari yake); mpaka watu wa Makkah (huhirimia) kutoka Makkah."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1126
Hadiyth
1833

6-Mlangoباب في الاغتسال في الإحرامMlango Wa Kuhusu Kuoga
Katika Ihraam (Hali Ya Kuhirimia Hajj Au 'Umrah)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ حُنَيْنٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: امْتَرَى الْمِسْوَرُ بْنُ مَخْرَمَةَ، وَابْنُ عَبَّاسٍ فِي غَسْلِ الْمُحْرِمِ رَأْسَهُ، فَأَرْسَلُونِي إِلَى أَبِي أَيُّوبَ الْأَنْصَارِيّ: كَيْفَ رَأَيْتَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَغْسِلُ رَأْسَهُ وَهُوَ مُحْرِمٌ؟ فَأَتَيْتُ أَبَا أَيُّوبَ وَهُوَ بَيْنَ قَرْنَيْ الْبِئْرِ وَقَدْ سُتِرَ عَلَيْهِ بِثَوْبٍ، فَسَلَّمْتُ عَلَيْهِ فَضَمَّ الثَّوْبَ إِلَيْهِ، فَقُلْتُ: أَرْسَلَنِي إِلَيْكَ ابْنُ أَخِيكَ ابْنُ عَبَّاسٍ: كَيْفَ رَأَيْتَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَغْسِلُ رَأْسَهُ؟ "فَأَمَرَّ يَدَيْهِ عَلَى رَأْسِهِ مُقْبِلًا وَمُدْبِرًا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa Ibraahiym bin 'Abdi-Allaah bin Hunayn, kutoka kwa baba yake, amesema: Al-Miswar bin Makhramah na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) walibishana kuhusu mwenye Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) kuosha kichwa chake. Wakanituma kwa Abuw Ayyuwb Al-Answaariy (رضي الله عنه) (nimuulize): Ulimwonaje Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiosha kichwa chake naye akiwa katika Ihraam? Nikamwendea Abuw Ayyuwb (رضي الله عنه) naye akiwa baina ya nguzo mbili za kisima, na amesitiriwa kwa nguo. Nikamsalimia, akaikusanya nguo kwake. Nikasema: Amenituma kwako mtoto wa ndugu yako, Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), (akuulize): Ulimwonaje Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiosha kichwa chake? "Akapitisha mikono yake miwili juu ya kichwa chake, akiipeleka mbele na kuirudisha nyuma."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1127
Hadiyth
1834

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي زِيَادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَعْقُوبَ الْمَدَنِيُّ، عَنْ ابْنِ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ خَارِجَةَ بْنِ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "تَجَرَّدَ لِلْإِهْلَالِ وَاغْتَسَلَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Abiy Ziyaad, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Ya'quwb Al-Madaniy, kutoka kwa Ibn Abiz-Zinaad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Khaarijah bin Zayd bin Thaabit, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alivua nguo zake kwa ajili ya kuhirimia, na akaoga."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1128
Hadiyth
1835

7-Mlangoباب في فضل الحج والعمرةMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Hajj Na 'Umrah (Hija Ndogo)

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سُمَيٍّ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "حَجَّةٌ مَبْرُورَةٌ لَيْسَ لَهَا ثَوَابٌ إِلَّا الْجَنَّةُ، وَعُمْرَتَانِ تُكَفِّرَانِ مَا بَيْنَهُمَا مِنْ الذُّنُوبِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Sumayy, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hajj iliyokubaliwa haina malipo isipokuwa Jannah (Pepo); na 'Umrah (Hija ndogo) mbili zinafuta madhambi yaliyo baina ya hizo mbili."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1129
Hadiyth
1836

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنِي مَنْصُورٌ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا حَازِمٍ يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: "مَنْ حَجَّ الْبَيْتَ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ، رَجَعَ كَمَا وَلَدَتْهُ أُمُّهُ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, amenisimulia Manswuwr, amesema: Nilimsikia Abuw Haazim akisimulia kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Mwenye kuihiji Nyumba (Al-Ka'bah), asifanye tendo la ndoa wala ufasiki, atarejea kama siku aliyozaliwa na mama yake."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1129
Hadiyth
1837

8-Mlangoباب أي الحج أفضلMlango Wa Ni Hajj Ipi Iliyo Bora Zaidi

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْمَاعِيل بْنِ أَبِي فُدَيْكٍ، عَنْ الضَّحَّاكِ بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَرْبُوعٍ، عَنْ أَبِي بَكْرٍ، قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الْحَجِّ أَفْضَلُ؟ قَالَ: "الْعَجُّ وَالثَّجُّ". الْعَجُّ يَعْنِي: التَّلْبِيَةَ، وَالثَّجُّ يَعْنِي: إِهْرَاقَ الدَّمِ

Ametusimulia Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Muhammad bin Ismaa'iyl bin Abiy Fudayk, kutoka kwa Adhw-Dhwahhaak bin 'Uthmaan, kutoka kwa Muhammad bin Al-Munkadir, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yarbuw', kutoka kwa Abuw Bakr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa: Ni Hajj ipi iliyo bora zaidi? Akasema: "Al-'ajj na ath-thajj." Al-'ajj maana yake ni: Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah); na ath-thajj maana yake ni: kumwaga damu (ya wanyama wa kuchinjwa).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1131
Hadiyth
1838

9-Mlangoباب ما يلبس المحرم من الثيابMlango Wa Nguo Anazovaa
Mwenye Ihraam (Hali Ya Kuhirimia Hajj Au 'Umrah)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى هُوَ ابْنُ سَعِيدٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ نَافِعٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: مَا نَلْبَسُ مِنْ الثِّيَابِ إِذَا أَحْرَمْنَا؟ قَالَ: "لَا تَلْبَسُوا الْقُمُصَ، وَلَا السَّرَاوِيلَاتِ، وَلَا الْعَمَائِمَ، وَلَا الْبَرَانِسَ، وَلَا الْخِفَافَ، إِلَّا أَنْ يَكُونَ أَحَدٌ لَيْسَتْ لَهُ نَعْلَانِ، فَلْيَلْبَسْ الْخُفَّيْنِ وَلْيَجْعَلْهُمَا أَسْفَلَ مِنْ الْكَعْبَيْنِ، وَلَا تَلْبَسُوا مِنْ الثِّيَابِ شَيْئًا مَسَّهُ وَرْسٌ وَلَا زَعْفَرَانٌ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa — naye ni Ibn Sa'iyd —, kutoka kwa 'Umar bin Naafi', kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Tuvae nguo gani tunapohirimia? Akasema: "Msivae kanzu, wala suruali, wala vilemba, wala majoho yenye kofia, wala khuff (soksi za ngozi), isipokuwa mtu asiye na viatu viwili; basi avae khuff mbili, na azifanye chini ya vifundo viwili vya miguu. Wala msivae nguo yoyote iliyoguswa na wars (mmea unaotia rangi ya manjano) wala zafarani."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1133
Hadiyth
1839

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ أَبِي الشَّعْثَاءِ، أَخْبَرَنِي ابْنُ عَبَّاسٍ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ لَمْ يَجِدْ إِزَارًا، فَلْيَلْبَسْ سَرَاوِيلَ، وَمَنْ لَمْ يَجِدْ نَعْلَيْنِ، فَلْيَلْبَسْ خُفَّيْنِ". قَالَ: قُلْتُ أَوْ قِيلَ: أَيَقْطَعُهُمَا؟ قَالَ: "لَا"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Abush-Sha'thaa, amenikhabarisha Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Asiyepata izaar (shuka ya chini), basi avae suruali; na asiyepata viatu viwili, basi avae khuff (soksi za ngozi) mbili." Akasema: Nikasema — au: ilisemwa —: Je, azikate? Akasema: "Hapana."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1133
Hadiyth
1840

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَمَّا يَلْبَسُ الْمُحْرِمُ، قَالَ: "لَا يَلْبَسُ الْقُمُصَ، وَلَا الْعَمَائِمَ، وَلَا السَّرَاوِيلَاتِ، وَلَا الْبَرَانِسَ، وَلَا الْخِفَافَ، إِلَّا أَنْ لَا يَجِدَ نَعْلَيْنِ، فَيَلْبَسُ خُفَّيْنِ وَلْيَقْطَعْهُمَا أَسْفَلَ مِنْ الْكَعْبَيْنِ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu anachovaa mwenye Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah). Akasema: "Asivae kanzu, wala vilemba, wala suruali, wala majoho yenye kofia, wala khuff (soksi za ngozi), isipokuwa asipopata viatu viwili; basi atavaa khuff mbili, na azikate chini ya vifundo viwili vya miguu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1134
Hadiyth
1841

10-Mlangoباب الطيب عند الإحرامMlango Wa Manukato Wakati Wa Kuhirimia

أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّهَا قَالَتْ: "كُنْتُ أُطَيِّبُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَبْلَ أَنْ يُحْرِمَ بِأَطْيَبِ الطِّيبِ"، قَالَ: وَكَانَ عُرْوَةُ يَقُولُ لَنَا: "تَطَيَّبُوا قَبْلَ أَنْ تُحْرِمُوا وَقَبْلَ أَنْ تُفِيضُوا يَوْمَ النَّحْرِ"

Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba alisema: "Nilikuwa nikimtia manukato Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla ya kuhirimia kwa manukato mazuri kabisa." Akasema: Na 'Urwah alikuwa akituambia: "Jitieni manukato kabla ya kuhirimia, na kabla ya kufanya Ifaadhwah (kuondoka kwenda Makkah kutufu) Siku ya Kuchinja."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1136
Hadiyth
1842

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "لَقَدْ كُنْتُ أُطَيِّبُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ إِحْرَامِهِ بِأَطْيَبِ مَا أَجِدُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Urwah, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Hakika nilikuwa nikimtia manukato Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati wa kuhirimia kwake kwa manukato mazuri kabisa ninayoyapata."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1137
Hadiyth
1843

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، وَجَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الْقَاسِمِ أَخْبَرَهُ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَمِعْتُ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، تَقُولُ: "طَيَّبْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِحُرْمِهِ، وَطَيَّبْتُهُ بِمِنًى قَبْلَ أَنْ يُفِيضَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn na Ja'far bin 'Awn, wamesema: Ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim alimkhabarisha kutoka kwa baba yake, amesema: Nilimsikia 'Aaishah (رضي الله عنها) akisema: "Nilimtia manukato Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa ajili ya kuhirimia kwake, na nilimtia manukato huko Minaa kabla ya kufanya Ifaadhwah (kuondoka kwenda Makkah kutufu)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1137
Hadiyth
1844

11-Mlangoباب في النفساء والحائض إذا أرادتا الحج وبلغتا الميقاتMlango Wa Kuhusu Mwanamke Mwenye Nifaas (Damu Ya Uzazi)
Na Mwenye Hedhi Wanapotaka Hajj
Na Wakafika Miyqaat (Mahali Pa Kuanzia Ihraam)

حَدَّثَنِي عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدَةُ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: " نُفِسَتْ أَسْمَاءُ بِمُحَمَّدِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ بِالشَّجَرَةِ فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا بَكْرٍ أَنْ" تَغْتَسِلَ وَتُهِلَّ "

Amenisimulia 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia 'Abdah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Asmaa (رضي الله عنها) alijifungua Muhammad bin Abiy Bakr huko Ash-Shajarah; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha Abuw Bakr (رضي الله عنه) kwamba (Asmaa) aoge na ahirimie."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1138
Hadiyth
1845

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَابِرٍ، فِي حَدِيثِ أَسْمَاءَ بِنْتِ عُمَيْسٍ، حِينَ نُفِسَتْ بِذِي الْحُلَيْفَةِ، فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَبَا بَكْرٍ أَنْ يَأْمُرَهَا أَنْ "تَغْتَسِلَ وَتُهِلَّ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), katika Hadiyth ya Asmaa bint 'Umays (رضي الله عنها) alipojifungua huko Dhul-Hulayfah: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha Abuw Bakr (رضي الله عنه) amwamrishe "aoge na ahirimie."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1139
Hadiyth
1846

12-Mlangoباب في أي وقت يستحب الإحرامMlango Wa Kuhusu Ni Wakati Gani Inapendekezwa Kuhirimia

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ السَّلَامِ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ خُصَيْفٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَحْرَمَ دُبُرَ الصَّلَاةِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari 'Abdus-Salaam bin Harb, kutoka kwa Khuswayf, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alihirimia baada ya Swalaah."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1139
Hadiyth
1847

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، قَالَ: أَخْبَرَنَا النَّضْرُ هُوَ ابْنُ شُمَيْلٍ، أَنْبَأَنَا أَشْعَثُ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَحْرَمَ وَأَهَلَّ فِي دُبُرِ الصَّلَاةِ"

Ametukhabarisha Is-haaq, amesema: Ametukhabarisha An-Nadhwr — naye ni Ibn Shumayl —, ametupa khabari Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alihirimia, na akaleta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah) kwa sauti baada ya Swalaah."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1140
Hadiyth
1848

13-Mlangoباب في التلبيةMlango Wa Kuhusu Talbiyah (Kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى يَعْنِي ابْنَ سَعِيدٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا لَبَّى، قَالَ: "لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ" قَالَ يَحْيَى: وَذَكَرَ نَافِعٌ أَنَّ ابْنَ عُمَرَ كَانَ يَزِيدُ هَؤُلَاءِ الْكَلِمَاتِ: "لَبَّيْكَ وَالرَّغْبَاءُ إِلَيْكَ وَالْعَمَلُ، لَبَّيْكَ لَبَّيْكَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa — yaani Ibn Sa'iyd —, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoleta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah), husema:

لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ، إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ

Nimekuitikia, Yaa Allaah, nimekuitikia. Nimekuitikia, huna mshirika, nimekuitikia. Hakika Himdi na Neema ni Zako, na Ufalme (ni Wako); huna mshirika.

Yahyaa amesema: Na Naafi' alitaja kwamba Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akiongeza maneno haya:

لَبَّيْكَ وَالرَّغْبَاءُ إِلَيْكَ وَالْعَمَلُ، لَبَّيْكَ لَبَّيْكَ

Nimekuitikia; na matarajio ni Kwako, na amali (ni kwa ajili Yako). Nimekuitikia, nimekuitikia.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1140
Hadiyth
1849

14-Mlangoباب في رفع الصوت بالتلبيةMlango Wa Kuhusu Kupaza Sauti
Kwa Talbiyah (Kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبِي بَكْرِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ خَلَّادِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَتَانِي جِبْرِيلُ، فَقَالَ: مُرْ أَصْحَابَكَ أَوْ مَنْ مَعَكَ أَنْ يَرْفَعُوا أَصْوَاتَهُمْ بِالتَّلْبِيَةِ أَوْ بِالْإِهْلَالِ".

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Abiy Bakr bin Al-Haarith, kutoka kwa Khallaad bin As-Saaib, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Jibriyl (عليه السلام) alinijia, akasema: Waamrishe Swahaba zako (رضي الله عنهم) — au: walio pamoja nawe — wapaze sauti zao kwa Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah), au kwa Ihlaal (kupaza sauti kwa Talbiyah wakati wa kuhirimia)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1142
Hadiyth
1850

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، بِإِسْنَادِهِ نَحْوَهُ

Ametusimulia 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) yake, kwa namna inayokaribiana nayo.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1142
Hadiyth
1851

15-Mlangoباب الاشتراط في الحجMlango Wa Kuweka Sharti Katika Hajj

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا هِلَالُ بْنُ خَبَّابٍ، قَالَ: فَحَدَّثْتُ عِكْرِمَةَ فَحَدَّثَنِي، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ ضُبَاعَةَ بِنْتَ الزُّبَيْرِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أَحُجَّ، فَكَيْفَ أَقُولُ؟ قَالَ: "قُولِي: لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ وَمَحِلِّي حَيْثُ تَحْبِسُنِي، فَإِنَّ لَكِ عَلَى رَبِّكِ مَا اسْتَثْنَيْتِ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Thaabit bin Yaziyd, ametusimulia Hilaal bin Khabbaab, amesema: Nikamsimulia 'Ikrimah, naye akanisimulia kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Dhwubaa'ah bint Az-Zubayr bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنها) alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi ninataka kuhiji; basi niseme vipi? Akasema: "Sema:

لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ وَمَحِلِّي حَيْثُ تَحْبِسُنِي

Nimekuitikia, Yaa Allaah, nimekuitikia. Nimekuitikia; na mahali pangu pa kutoka katika Ihraam ni pale Utakaponizuia.

Kwani hakika wewe una kwa Rabb wako kile ulichokiwekea sharti."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1142
Hadiyth
1852

16-Mlangoباب في إفراد الحجMlango Wa Kuhusu Ifraad (Kuhirimia Hajj Peke Yake)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ تَعَالَى عَنْهَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَفْرَدَ الْحَجَّ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alifanya Ifraad (kuhirimia Hajj peke yake) ya Hajj."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1143
Hadiyth
1853

17-Mlangoباب في القرانMlango Wa Kuhusu Qiraan (Kuunganisha Hajj
Na 'Umrah Katika Ihraam Moja)

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، أَخْبَرَنَا أَبُو هِلَالٍ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ مُطَرِّفٍ، قَالَ: قَالَ عِمْرَانُ بْنُ حُصَيْنٍ: إِنِّي مُحَدِّثُكَ بِحَدِيثٍ لَعَلَّ اللَّهَ أَنْ يَنْفَعَكَ بِهِ بَعْدُ، إِنَّهُ كَانَ يُسَلَّمُ عَلَيَّ وَإِنَّ ابْنَ زِيَادٍ أَمَرَنِي فَاكْتَوَيْتُ، فَاحْتُبِسَ عَنِّي حَتَّى ذَهَبَ أَثَرُ الْمَكَاوِي، وَاعْلَمْ أَنَّ "الْمُتْعَةَ حَلَالٌ فِي كِتَابِ اللَّهِ، لَمْ يَنْهَ عَنْهَا نَبِيٌّ، وَلَمْ يَنْزِلْ فِيهَا كِتَابٌ"، قَالَ رَجُلٌ بِرَأْيِهِ مَا بَدَا لَهُ

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametukhabarisha Abuw Hilaal, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Mutwarrif, amesema: 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه) amesema: Hakika mimi nitakusimulia Hadiyth, huenda Allaah Akakunufaisha kwayo baadaye: Hakika nilikuwa nikisalimiwa [na Malaika (عليهم السلام)]; na kwamba Ibn Ziyaad aliniamrisha, nikajitibu kwa kujichoma moto, (salaam hiyo) ikazuiliwa kwangu mpaka athari ya vyuma vya kuchomea ilipoondoka. Na ujue kwamba "Mut'ah (kuhirimia 'Umrah kisha Hajj katika msimu mmoja) ni halaal katika Kitabu cha Allaah; hakuna Nabiy yeyote (عليه السلام) aliyeikataza, wala hakikuteremka kuhusu hiyo Kitabu (cha kuiharamisha)." Mtu mmoja alisema kwa rai yake alichoona.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1143
Hadiyth
1854

18-Mlangoباب في التمتعMlango Wa Kuhusu Tamattu' (Kuhirimia 'Umrah Kisha Hajj
Katika Msimu Mmoja)

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نَوْفَلٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَامَ حَجَّ مُعَاوِيَةُ يَسْأَلُ سَعْدَ بْنَ مَالِكٍ: "كَيْفَ تَقُولُ بِالتَّمَتُّعِ بِالْعُمْرَةِ إِلَى الْحَجِّ؟ قَالَ: حَسَنَةٌ جَمِيلَةٌ". فَقَالَ: قَدْ كَانَ عُمَرُ يَنْهَى عَنْهَا، فَأَنْتَ خَيْرٌ مِنْ عُمَرَ؟ قَالَ: عُمَرُ خَيْرٌ مِنِّي، وَقَدْ فَعَلَ ذَلِكَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ خَيْرٌ مِنْ عُمَرَ

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdi-Allaah bin Nawfal, amesema: Nilimsikia — mwaka ambao Mu'aawiyah (رضي الله عنه) alihiji — akimuuliza Sa'd bin Maalik (رضي الله عنه): "Unasemaje kuhusu Tamattu' (kuhirimia 'Umrah kisha Hajj katika msimu mmoja) kwa 'Umrah (Hija ndogo) hadi Hajj? Akasema: Ni jambo jema, zuri." Akasema: Hakika 'Umar (رضي الله عنه) alikuwa akiikataza; je, wewe ni bora kuliko 'Umar (رضي الله عنه)? Akasema: 'Umar (رضي الله عنه) ni bora kuliko mimi; na hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya hivyo, naye ni bora kuliko 'Umar (رضي الله عنه).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1144
Hadiyth
1855

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا قَيْسُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ طَارِقٍ، عَنْ أَبِي مُوسَى، قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ حَجَّ وَهُوَ مُنِيخٌ بِالْبَطْحَاءِ، فَقَالَ لِي: "أَحَجَجْتَ؟" قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: "كَيْفَ أَهْلَلْتَ؟". قَالَ: قُلْتُ: لَبَّيْكَ بِإِهْلَالٍ كَإِهْلَالِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. قَالَ: "أَحْسَنْتَ، اذْهَبْ فَطُفْ بِالْبَيْتِ، وَبِالصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، ثُمَّ حِلَّ". قَالَ: فَطُفْتُ بِالْبَيْتِ، وَبِالصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، ثُمَّ أَتَيْتُ امْرَأَةً مِنْ نِسَاءِ بَنِي قَيْسٍ فَجَعَلَتْ تَفْلِي رَأْسِي، فَجَعَلْتُ أُفْتِي النَّاسَ بِذَلِكَ، فَقَالَ لِي رَجُلٌ: يَا عَبْدَ اللَّهِ بْنَ قَيْسٍ، رُوَيْدًا بَعْضَ فُتْيَاكَ، فَإِنَّكَ لَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَ أَمِيرُ الْمُؤْمِنِينَ فِي النُّسُكِ بَعْدَكَ. فَقُلْتُ: يَا أَيُّهَا النَّاسُ، مَنْ كُنَّا أَفْتَيْنَاهُ فُتْيَا، فَلْيَتَّئِدْ، فَإِنَّ أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ قَادِمٌ عَلَيْكُمْ فَبِهِ فَأْتَمُّوا. فَلَمَّا قَدِمَ أَتَيْتُهُ فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: إِنْ نَأْخُذْ بِكِتَابِ اللَّهِ، فَإِنَّ كِتَابَ اللَّهِ يَأْمُرُ بِالتَّمَامِ، وَإِنْ نَأْخُذْ بِسُنَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمْ يَحِلَّ حَتَّى بَلَغَ الْهَدْيُ مَحِلَّهُ

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Qays bin Muslim, kutoka kwa Twaariq, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), amesema: Nilimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipohiji, naye amemkalisha ngamia wake huko Al-Batwhaa (bonde la Makkah). Akaniambia: "Je, umehiji?" Nikasema: Ndiyo. Akasema: "Umehirimia vipi?" Akasema: Nikasema: Nimekuitikia kwa uhirimiaji kama uhirimiaji wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: "Umefanya vizuri. Nenda ukatufu Al-Bayt (Al-Ka'bah), na [ukafanye Sa'yi (kwenda na kurudi) baina ya] Asw-Swafaa na Al-Marwah, kisha utoke katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)." Akasema: Nikatufu Al-Bayt, na [nikafanya Sa'yi baina ya] Asw-Swafaa na Al-Marwah, kisha nikamwendea mwanamke mmoja miongoni mwa wanawake wa Banuw Qays, akawa ananitoa chawa kichwani mwangu. Nikawa nikiwapa watu fatwa kwa hilo. Mtu mmoja akaniambia: Yaa 'Abda-Allaah bin Qays, punguza kasi katika baadhi ya fatwa zako; kwani hujui Amiri wa Waumini amefanya nini kipya katika ibaada (ya Hajj) baada yako. Nikasema: Enyi watu! Ambaye tulimpa fatwa yoyote, basi asubiri (asiharakishe); kwani Amiri wa Waumini anakuja kwenu, basi mfuateni yeye. Alipowasili, nilimwendea, nikamtajia hilo. Akasema: Tukishika Kitabu cha Allaah, basi hakika Kitabu cha Allaah kinaamrisha kutimiza; na tukishika Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakutoka katika Ihraam mpaka Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) alipofikia machinjoni pake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1145
Hadiyth
1856

19-Mlangoباب ما يقتل المحرم في إحرامهMlango Wa Anaowaua Mwenye Ihraam (Hali Ya Kuhirimia Hajj
Au 'Umrah) Katika Ihraam Yake

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "خَمْسٌ لَا جُنَاحَ فِي قَتْلِ مَنْ قُتِلَ مِنْهُنَّ: الْغُرَابُ، وَالْفَأْرَةُ، وَالْحِدَأَةُ، وَالْعَقْرَبُ، وَالْكَلْبُ الْعَقُورُ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "(Wanyama) watano, hakuna dhambi katika kumuua yeyote atakayeuawa miongoni mwao: kunguru, na panya, na mwewe, na nge, na mbwa mwenye kuuma."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1146
Hadiyth
1857

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، أَنْبَأَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، حَدَّثَنَا مَعْمَرٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: "أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَتْلِ خَمْسِ فَوَاسِقَ فِي الْحِلِّ وَالْحَرَمِ: الْحِدَأَةِ، وَالْغُرَابِ، وَالْفَأْرَةِ، وَالْعَقْرَبِ، وَالْكَلْبِ الْعَقُورِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: الْكَلْبُ الْعَقُورُ، وَقَالَ بَعْضُهُمْ: الْأَسْوَدُ.

Ametukhabarisha Is-haaq, ametupa khabari 'Abdur-Razzaaq, ametusimulia Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrisha kuuawa (wanyama) watano waovu nje ya Haram (eneo tukufu) na ndani ya Haram: mwewe, na kunguru, na panya, na nge, na mbwa mwenye kuuma."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: "Mbwa mwenye kuuma"; na baadhi yao wamesema: (Mbwa) mweusi.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1146
Hadiyth
1858

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، قَالَ بَعْضُ أَصْحَابِنَا: إِنَّ مَعْمَرًا كَانَ يَذْكُرُهُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، وَعَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Ametukhabarisha 'Abdur-Razzaaq: Baadhi ya wenzetu wamesema: Hakika Ma'mar alikuwa akiitaja (Hadiyth hii) kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)]; na kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1146
Hadiyth
1859

20-Mlangoباب الحجامة للمحرمMlango Wa Kuumikwa
Kwa Mwenye Ihraam (Hali Ya Kuhirimia Hajj Au 'Umrah)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "احْتَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ مُحْرِمٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Uthmaan, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliumikwa naye akiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1148
Hadiyth
1860

حَدَّثَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ بِلَالٍ، حَدَّثَنَا عَلْقَمَةُ بْنُ أَبِي عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْأَعْرَجِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابْنِ بُحَيْنَةَ، قَالَ: "احْتَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلَحْيِ جَمَلٍ، وَهُوَ مُحْرِمٌ"

Ametusimulia Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Sulaymaan bin Bilaal, ametusimulia 'Alqamah bin Abiy 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan Al-A'raj, kutoka kwa 'Abdu-Allaah Ibn Buhaynah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliumikwa huko Lahyu Jamal (mahali katika njia ya Makkah), naye akiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1148
Hadiyth
1861

حَدَّثَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ عَطَاءٍ، وَطَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "احْتَجَمَ وَهُوَ مُحْرِمٌ". قَالَ إِسْحَاق: قَالَ سُفْيَانُ مَرَّةً: عَنْ عَطَاءٍ، وَمَرَّةً، عَنْ طَاوُسٍ، وَجَمَعَهُمَا مَرَّةً

Ametusimulia Is-haaq, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa 'Atwaa na Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliumikwa naye akiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)." Is-haaq amesema: Sufyaan alisema mara moja: kutoka kwa 'Atwaa; na mara (nyingine): kutoka kwa Twaawuws; na mara (nyingine) aliwakusanya wote wawili.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1148
Hadiyth
1862

21-Mlangoباب في تزويج المحرمMlango Wa Kuhusu Kuoa Kwa Muhrim (Aliye
Katika Hali Ya Kuhirimia Hajj Au 'Umrah)

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "تَزَوَّجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ مُحْرِمٌ"

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Jaabir bin Zayd, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alioa naye akiwa muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1149
Hadiyth
1863

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ نُبَيْهِ بْنِ وَهْبٍ: أَنَّ رَجُلًا مِنْ قُرَيْشٍ خَطَبَ إِلَى أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ وَهُوَ أَمِيرُ الْمَوْسِمِ، فَقَالَ أَبَانُ: لَا أُرَاهُ إِلا عِرَاقِيًّا جَافِيًا، "إِنَّ الْمُحْرِمَ لَا يَنْكِحُ وَلَا يُنْكِحُ". أَخْبَرَنَا بِذَلِكَ عُثْمَانُ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. سُئِلَ أَبُو مُحَمَّد: تَقُولُ بِهَذَا؟ قَالَ: نَعَمْ

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Nubayh bin Wahb: Kwamba mtu mmoja wa Quraysh alipeleka posa kwa Abaan bin 'Uthmaan, naye alikuwa ndiye amiri wa msimu (wa Hajj). Abaan akasema: Simwoni (mtu huyu) isipokuwa ni mtu wa 'Iraaq mjeuri (asiyejua adabu): "Hakika muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) haoi wala haozeshi." Ametukhabarisha hilo 'Uthmaan (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unasema kwa (kauli) hii? Akasema: "Ndiyo."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1149
Hadiyth
1864

حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ الشَّهِيدِ، عَنْ مَيْمُونِ بْنِ مِهْرَانَ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ الْأَصَمِّ، أَنَّ مَيْمُونَةَ، قَالَتْ: "تَزَوَّجَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ حَلَالَانِ بَعْدَمَا رَجَعَ مِنْ مَكَّةَ بِسَرِفَ"

Ametusimulia 'Amr bin 'Aaswim, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Habiyb bin Ash-Shahiyd, kutoka kwa Maymuwn bin Mihraan, kutoka kwa Yaziyd bin Al-Asamm, kwamba Maymuwnah (رضي الله عنها) amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinioa nasi wawili tukiwa hatuko katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), baada ya kurejea kutoka Makkah, huko Sarif."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1151
Hadiyth
1865

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ مَطَرٍ الْوَرَّاقِ، عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي رَافِعٍ، قَالَ: "تَزَوَّجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَيْمُونَةَ حَلَالًا، وَبَنَى بِهَا حَلَالًا، وَكُنْتُ الرَّسُولَ بَيْنَهُمَا"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Matwar Al-Warraaq, kutoka kwa Rabiy'ah bin Abiy 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Raafi' (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwoa Maymuwnah (رضي الله عنها) akiwa hayuko katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), na akaingia naye nyumbani akiwa hayuko katika Ihraam; nami nilikuwa mjumbe baina yao wawili."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1151
Hadiyth
1866

22-Mlangoباب في أكل لحم الصيد للمحرم إذا لم يصد هوMlango Wa Kuhusu Muhrim (Aliye
Katika Hali Ya Kuhirimia Hajj Au 'Umrah) Kula Nyama Ya Windo
Ikiwa Hakuwinda Yeye Mwenyewe

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ الدَّسْتَوَائِيُّ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: انْطَلَقَ أَبِي مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَامَ الْحُدَيْبِيَةِ، فَأَحْرَمَ أَصْحَابُهُ وَلَمْ يُحْرِمْ أَبُو قَتَادَةَ، فَأَصَابَ حِمَارَ وَحْشٍ، فَطَعَنَهُ وَأَكَلَ مِنْ لَحْمِهِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أَصَبْتُ حِمَارَ وَحْشٍ، فَطَعَنْتُهُ، فَقَالَ لِلْقَوْمِ: "كُلُوا" وَهُمْ مُحْرِمُونَ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Hishaam Ad-Dastuwaaiy, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, amesema: Baba yangu (رضي الله عنه) alikwenda pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mwaka wa Al-Hudaybiyah. Swahaba zake (رضي الله عنهم) wakahirimia, na Abuw Qataadah (رضي الله عنه) hakuhirimia. Akampata punda mwitu, akamchoma (kwa mkuki), na akala katika nyama yake. Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nimempata punda mwitu, nikamchoma. Akawaambia watu: "Kuleni", nao wakiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1152
Hadiyth
1867

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَوْهَبٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: بَيْنَمَا نَحْنُ نَسِيرُ وَهُمْ مُحْرِمُونَ، وَأَبُو قَتَادَةَ حَلَالٌ، إِذْ رَأَيْتُ حِمَارًا، فَرَكِبْتُ فَرَسًا، فَأَصَبْتُهُ، فَأَكَلُوا مِنْ لَحْمِهِ وَهُمْ مُحْرِمُونَ وَلَمْ آكُلْ، فَأَتَوْا النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَسَأَلُوهُ، فَقَالَ: "أَشَرْتُمْ، قَتَلْتُمْ؟ أَوْ قَالَ: ضَرَبْتُمْ؟ قَالُوا: لَا، قَالَ: فَكُلُوا"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Abdi-Allaah bin Mawhab, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Wakati sisi tukienda — nao wakiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), na Abuw Qataadah (رضي الله عنه) hakuwa katika Ihraam —, ghafla nilimwona punda (mwitu). Nikapanda farasi, nikampata. Wakala katika nyama yake nao wakiwa katika Ihraam, na mimi sikula. Wakamwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakamuuliza. Akasema: "Je, mliashiria (kumwonyesha)? Mliua?" — au alisema: "Mlipiga?" — Wakasema: Hapana. Akasema: "Basi kuleni."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1152
Hadiyth
1869

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ صَالِحِ بْنِ كَيْسَانَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ الصَّعْبِ بْنِ جَثَّامَةَ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِلَحْمِ حِمَارِ وَحْشٍ، فَرَدَّهُ وَقَالَ: "إِنَّا حُرُمٌ لَا نَأْكُلُ الصَّيْدَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Asw-Swa'b bin Jaththaamah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa nyama ya punda mwitu, akairudisha, na akasema: "Hakika sisi tuko katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah); hatuli mawindo."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1152
Hadiyth
1870

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ ابْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ مُعَاذِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كُنَّا مَعَ طَلْحَةَ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ فِي سَفَرٍ، فَأُهْدِيَ لَهُ طَيْرٌ وَهُمْ مُحْرِمُونَ، وَهُوَ رَاقِدٌ، فَمِنَّا مَنْ أَكَلَ، وَمِنَّا مَنْ تَوَرَّعَ، فَاسْتَيْقَظَ طَلْحَةُ فَأَخْبَرُوهُ، فَوَافَقَ مَنْ أَكَلَهُ، وَقَالَ: "أَكَلْنَاهُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibn Al-Munkadir, kutoka kwa Mu'aadh bin 'Abdir-Rahmaan bin 'Uthmaan At-Taymiy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Tulikuwa pamoja na Twalhah bin 'Ubaydi-Allaah (رضي الله عنه) safarini. Akapewa zawadi ya ndege — nao wakiwa katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) —, naye akiwa amelala. Miongoni mwetu kuna aliyekula, na miongoni mwetu kuna aliyejizuia (kwa kuchelea). Twalhah (رضي الله عنه) akaamka, wakamkhabarisha; akamwafiki aliyekula, na akasema: "Tulimla pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1152
Hadiyth
1871

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي الصَّعْبُ بْنُ جَثَّامَةَ، قَالَ: مَرَّ بِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا بِالْأَبْوَاءِ أَوْ بِوَدَّانَ، وَأَهْدَيْتُ لَهُ لَحْمَ حِمَارِ وَحْشٍ، فَرَدَّهُ عَلَيَّ، فَلَمَّا رَأَى فِي وَجْهِي الْكَرَاهِيَةَ، قَالَ: "إِنَّهُ لَيْسَ بِنَا رَدٌّ عَلَيْكَ، وَلَكِنَّا حُرُمٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Amenisimulia Asw-Swa'b bin Jaththaamah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinipitia nami nikiwa Al-Abwaa — au Waddaan —, na nikampa zawadi nyama ya punda mwitu; akanirudishia. Alipoona katika uso wangu kuchukia (kwa kurudishiwa), akasema: "Hakika hatuna (sababu ya) kukurudishia, lakini sisi tuko katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1153
Hadiyth
1872

23-Mlangoباب في الحج عن الحيMlango Wa Kuhusu Kumhijia Aliye Hai

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ الْفَضْلِ بْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّهُ كَانَ رَدِيفَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ، جَاءَتْ امْرَأَةٌ مِنْ خَثْعَمَ، فَقَالَتْ: إِنَّ فَرِيضَةَ اللَّهِ فِي الْحَجِّ عَلَى عِبَادِهِ أَدْرَكَتْ أَبِي شَيْخًا كَبِيرًا لَا يَسْتَمْسِكُ عَلَى رَاحِلَتِهِ، وَلَمْ يَحُجَّ، أَفَأَحُجُّ عَنْهُ، قَالَ: "نَعَمْ". سُئِلَ أَبُو مُحَمَّد: تَقُولُ بِهَذَا؟ قَالَ: نَعَمْ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Al-Fadhwl bin 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba yeye alikuwa amepandishwa nyuma ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hajj ya Kuaga. Akaja mwanamke mmoja wa (kabila la) Khath'am, akasema: Hakika faradhi ya Allaah juu ya waja Wake katika Hajj imemkuta baba yangu akiwa mzee mkongwe, hawezi kuthibiti juu ya kipando chake, na hajahiji; je, nimhijie? Akasema: "Ndiyo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: "Je, unasema kwa (kauli) hii?" Akasema: "Ndiyo."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1154
Hadiyth
1873

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ الْفَضْلِ هُوَ ابْنُ عَبَّاسٍ، أَنَّ امْرَأَةً سَأَلَتْ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: إِنَّ أَبِي شَيْخٌ لَا يَسْتَوِي عَلَى الْبَعِيرِ أَدْرَكَتْهُ فَرِيضَةُ اللَّهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "حُجِّي عَنْهُ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Al-Fadhwl (رضي الله عنهما) — naye ni Ibn 'Abbaas —, kwamba mwanamke mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika baba yangu ni mzee, hawezi kukaa sawasawa juu ya ngamia; faradhi ya Allaah imemkuta. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mhijie."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1155
Hadiyth
1874

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ امْرَأَةً مِنْ خَثْعَمَ اسْتَفْتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ، وَالْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ رَدِيفُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ فَرِيضَةَ اللَّهِ عَلَى عِبَادِهِ أَدْرَكَتْ أَبِي شَيْخًا كَبِيرًا، لَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَسْتَوِيَ عَلَى الرَّاحِلَةِ، فَهَلْ يَقْضِي أَنْ أَحُجَّ عَنْهُ؟ قَالَ: "نَعَمْ".

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba mwanamke mmoja wa (kabila la) Khath'am alimuomba fatwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hajj ya Kuaga — na Al-Fadhwl bin 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa amepandishwa nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika faradhi ya Allaah juu ya waja Wake imemkuta baba yangu akiwa mzee mkongwe, hawezi kukaa sawasawa juu ya kipando; je, itamlipia (faradhi hiyo) nikimhijia? Akasema: "Ndiyo."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1155
Hadiyth
1875

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوًا مِنْ حَدِيثِ الْأَوْزَاعِيِّ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa namna inayokaribiana na Hadiyth ya Al-Awzaa'iy.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1155
Hadiyth
1876

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، أَخْبَرَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، حَدَّثَنِي الْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ أَوْ عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ الْعَبَّاسِ، أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أَبِي أَوْ أُمِّي عَجُوزٌ كَبِيرٌ، إِنْ أَنَا حَمَلْتُهَا لَمْ تَسْتَمْسِكْ، وَإِنْ رَبَطْتُهَا، خَشِيتُ أَنْ أَقْتُلَهَا. قَالَ: "أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ عَلَى أَبِيكَ أَوْ أُمِّكَ دَيْنٌ، أَكُنْتَ تَقْضِيهِ؟". قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: "فَحُجَّ عَنْ أَبِيكَ، أَوْ أُمِّكَ"

Ametusimulia Musaddad, ametukhabarisha Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Is-haaq, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, amenisimulia Al-Fadhwl bin 'Abbaas (رضي الله عنهما) — au 'Ubaydu-Allaah bin Al-'Abbaas (رضي الله عنهما) —, kwamba mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika baba yangu — au mama yangu — ni mzee mkongwe; nikimbeba (juu ya kipando) hawezi kujishikilia, na nikimfunga (kwa kamba) nachelea nisije kumuua. Akasema: "Unaonaje lau baba yako — au mama yako — angekuwa na deni, je, ungelilipa?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Basi mhijie baba yako, au mama yako."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1156
Hadiyth
1877

24-Mlangoباب الحج عن الميتMlango Wa Kumhijia Maiti

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ الزُّبَيْرِ مَوْلًى لِآلِ الْزُّبَيْرِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الزُّبَيْرِ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ مِنْ خَثْعَمَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: إِنَّ أَبِي أَدْرَكَهُ الْإِسْلَامُ وَهُوَ شَيْخٌ كَبِيرٌ لَا يَسْتَطِيعُ رُكُوبَ الرَّحْلِ، وَالْحَجُّ مَكْتُوبٌ عَلَيْهِ، أَفَأَحُجُّ عَنْهُ؟ قَالَ: "أَنْتَ أَكْبَرُ وَلَدِهِ؟". قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "أَرَأَيْتَ لَوْ كَانَ عَلَى أَبِيكَ دَيْنٌ فَقَضَيْتَهُ عَنْهُ، أَكَانَ ذَلِكَ يُجْزِئُ عَنْهُ؟". قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "فَاحْجُجْ عَنْهُ"

Ametusimulia Muhammad bin Humayd, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Yuwsuf bin Az-Zubayr, mawlaa (mwachwa huru) wa familia ya Az-Zubayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Az-Zubayr (رضي الله عنهما), amesema: Mtu mmoja wa (kabila la) Khath'am alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika baba yangu Islaam imemkuta naye ni mzee mkongwe, hawezi kupanda juu ya tandiko (la ngamia), na Hajj imeandikwa (kuwa faradhi) juu yake; je, nimhijie? Akasema: "Wewe ndiye mkubwa wa wanawe?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Unaonaje lau baba yako angekuwa na deni, ukamlipia, je, hilo lingemtosheleza?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Basi mhijie."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1157
Hadiyth
1878

أَخْبَرَنَا صَالِحُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ هُوَ ابْنُ عَبْدِ الصَّمَدِ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ مَوْلَى ابْنِ الزُّبَيْرِ، يُقَالُ لَهُ: يُوسُفُ بْنُ الزُّبَيْرِ أَوْ الزُّبَيْرُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سَوْدَةَ بِنْتِ زَمْعَةَ، قَالَتْ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: إِنَّ أَبِي شَيْخٌ كَبِيرٌ لَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَحُجَّ. قَالَ: "أَرَأَيْتَ لَوْ كَانَ عَلَى أَبِيكَ دَيْنٌ فَقَضَيْتَهُ عَنْهُ، قُبِلَ مِنْهُ؟". قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "اللَّهُ أَرْحَمُ، حُجَّ عَنْ أَبِيكَ"

Ametukhabarisha Swaalih bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz — naye ni Ibn 'Abdisw-Swamad —, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa mawlaa (mwachwa huru) wa Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما) aitwaye Yuwsuf bin Az-Zubayr — au Az-Zubayr bin Yuwsuf —, kutoka kwa Sawdah bint Zam'ah (رضي الله عنها), amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika baba yangu ni mzee mkongwe, hawezi kuhiji. Akasema: "Unaonaje lau baba yako angekuwa na deni, ukamlipia, je, lingekubaliwa kutoka kwake?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Allaah Ni Mwingi wa Rehma zaidi. Mhijie baba yako."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1158
Hadiyth
1879

25-Mlangoباب في استلام الحجرMlango Wa Kuhusu Kuligusa Al-Hajar (Jiwe Jeusi)

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "مَا تَرَكْتُ اسْتِلَامَ هَذَيْنِ الرُّكْنَيْنِ فِي شِدَّةٍ وَلَا رَخَاءٍ مُنْذُ رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتَلِمُهُمَا". قُلْتُ لِنَافِعٍ: أَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَمْشِي بَيْنَ الرُّكْنَيْنِ؟ قَالَ: إِنَّمَا كَانَ يَمْشِي لِيَكُونَ أَيْسَرَ لِاسْتِلَامِهِ

Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Sijaacha kuzigusa pembe hizi mbili (za Al-Ka'bah), katika dhiki wala katika wepesi, tangu nilipomwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akizigusa." Nikamwambia Naafi': Je, Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akitembea (kwa mwendo wa kawaida) baina ya pembe mbili hizo? Akasema: Hakika alikuwa akitembea tu ili iwe wepesi zaidi kwake kuigusa (pembe).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1159
Hadiyth
1880

26-Mlangoباب الفضل في استلام الحجرMlango Wa Fadhila Ya Kuligusa Al-Hajar (Jiwe Jeusi)

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، وَسُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُثْمَانَ بْنِ خُثَيْمٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَيَبْعَثَنَّ اللَّهُ الْحَجَرَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَهُ عَيْنَانِ يُبْصِرُ بِهِمَا، وَلِسَانٌ يَنْطِقُ بِهِ، يَشْهَدُ عَلَى مَنْ اسْتَلَمَهُ بِحَقٍّ". قَالَ سُلَيْمَانُ: لِمَنْ اسْتَلَمَهُ

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal na Sulaymaan bin Harb, wamesema: Ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Uthmaan bin Khuthaym, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kwa hakika Allaah Atalifufua Jiwe (Jeusi) Siku ya Qiyaamah, nalo lina macho mawili linayoonea, na ulimi linaotamkia, likimshuhudia aliyeligusa kwa haki." Sulaymaan amesema: "Kwa ajili ya aliyeligusa."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1160
Hadiyth
1881

27-Mlangoباب من رمل ثلاثا ومشى أربعاMlango Wa Aliyefanya Ramal (Mwendo Wa Haraka
Kwa Hatua Fupi) Mizunguko Mitatu Na Akatembea Minne

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "رَمَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ الْحَجَرِ إِلَى الْحَجَرِ ثَلَاثَةَ أَشْوَاطٍ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Maalik bin Anas, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya ramal (mwendo wa haraka kwa hatua fupi) kutoka kwenye Jiwe (Jeusi) mpaka kwenye Jiwe, mizunguko mitatu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1160
Hadiyth
1882

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، حَدَّثَنِي نَافِعٌ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "إِذَا طَافَ بِالْبَيْتِ الطَّوَافَ الْأَوَّلَ، خَبَّ ثَلَاثَةً، وَمَشَى أَرْبَعَةً، وَكَانَ يَسْعَى بِبَطْنِ الْمَسِيلِ إِذَا سَعَى بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ". فَقُلْتُ لِنَافِعٍ: أَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ يَمْشِي إِذَا بَلَغَ الرُّكْنَ الْيَمَانِيَ؟ قَالَ: لَا، إِلَّا أَنْ يُزَاحَمَ عَلَى الرُّكْنِ، فَإِنَّهُ كَانَ لَا يَدَعُهُ حَتَّى يَسْتَلِمَهُ

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, amenisimulia Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikuwa anapoitufu Al-Bayt (Al-Ka'bah) Twawaaf ya kwanza, hutembea kwa haraka (mizunguko) mitatu, na hutembea (kwa kawaida) minne; na alikuwa akienda mbio katika tumbo la mkondo (wa bonde) anapofanya Sa'yi (kwenda na kurudi) baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah." Nikamwambia Naafi': Je, 'Abdu-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما) alikuwa akitembea (kwa kawaida) anapofika Ar-Rukn Al-Yamaaniy (pembe ya upande wa Yemen)? Akasema: Hapana, isipokuwa anaposongwa kwenye pembe hiyo; kwani alikuwa haiachi mpaka aiguse.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1160
Hadiyth
1883

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ بْنِ أَبَانَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "رَمَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ الْحَجَرِ إِلَى الْحَجَرِ ثَلَاثًا، وَمَشَى أَرْبَعًا"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Umar bin Abaan, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, ametupa khabari 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya ramal (mwendo wa haraka kwa hatua fupi) kutoka kwenye Jiwe (Jeusi) mpaka kwenye Jiwe (mizunguko) mitatu, na akatembea minne."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1160
Hadiyth
1884

28-Mlangoباب الاضطباع في الرملMlango Wa Al-Idhwtwibaa' (Kupitisha
Shuka Chini Ya Kwapa La Kulia
Na Kuzitupa Ncha Zake Juu Ya Bega La Kushoto)
Katika Ramal (Mwendo Wa Haraka Kwa Hatua Fupi)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ هُوَ ابْنُ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ يَعْلَى، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، "أَنَّهُ طَافَ مُضْطَبِعًا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Abdul-Hamiyd — naye ni Ibn Jubayr —, kutoka kwa Ibn Ya'laa, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): "Kwamba yeye alitufu akiwa amefanya idhwtwibaa' (kupitisha shuka chini ya kwapa la kulia na kuzitupa ncha zake juu ya bega la kushoto)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1162
Hadiyth
1885

29-Mlangoباب طواف القارنMlango Wa Twawaaf Ya Mwenye Kufanya
Qiraan (Kuunganisha Hajj Na 'Umrah)

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَنْ أَهَلَّ بِالْحَجِّ وَالْعُمْرَةِ، كَفَاهُ لَهُمَا طَوَافٌ وَاحِدٌ، وَلَا يَحِلُّ حَتَّى يَحِلَّ مِنْهُمَا"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayehirimia Hajj na 'Umrah (Hija ndogo), inamtosha kwa ajili ya zote mbili Twawaaf moja, na hatatoka katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) mpaka atoke katika zote mbili."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1163
Hadiyth
1886

30-Mlangoباب الطواف على الراحلةMlango Wa Kutufu Juu Ya Kipando

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "طَافَ بِالْبَيْتِ عَلَى بَعِيرٍ، كُلَّمَا أَتَى عَلَى الرُّكْنِ، أَشَارَ إِلَيْهِ بِشَيْءٍ فِي يَدِهِ، وَكَبَّرَ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliitufu Al-Bayt (Al-Ka'bah) juu ya ngamia; kila alipoifikia Ar-Rukn (pembe ya Al-Ka'bah yenye Jiwe Jeusi), aliiashiria kwa kitu kilichokuwa mkononi mwake, na akamtukuza (Allaah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1164
Hadiyth
1887

31-Mlangoباب ما تصنع الحاجة إذا كانت حائضاMlango Wa Anachofanya Mwanamke Anayehiji Akiwa Na Hedhi

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: قَدِمْتُ مَكَّةَ وَأَنَا حَائِضٌ، وَلَمْ أَطُفْ بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، فَشَكَوْتُ ذَلِكَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "افْعَلِي مَا يَفْعَلُ الْحَاجُّ، غَيْرَ أَنْ لَا تَطُوفِي بِالْبَيْتِ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Niliwasili Makkah nami nikiwa na hedhi, na sikutufu baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah. Nikamshtakia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hilo, akasema: "Fanya anayofanya mwenye kuhiji, isipokuwa usitufu Al-Bayt (Al-Ka'bah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1164
Hadiyth
1888

32-Mlangoباب الكلام في الطوافMlango Wa Kuzungumza Katika Twawaaf

أَخْبَرَنَا الْحُمَيْدِيُّ، حَدَّثَنَا الْفُضَيْلُ بْنُ عِيَاضٍ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الطَّوَافُ بِالْبَيْتِ صَلَاةٌ، إِلَّا أَنَّ اللَّهَ أَبَاحَ فِيهِ الْمَنْطِقَ، فَمَنْ نَطَقَ فِيهِ، فَلَا يَنْطِقْ إِلَّا بِخَيْرٍ".

Ametukhabarisha Al-Humaydiy, ametusimulia Al-Fudhwayl bin 'Iyaadhw, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Twawaaf kuizunguka Al-Bayt (Al-Ka'bah) ni Swalaah, isipokuwa Allaah Ameruhusu ndani yake kuzungumza; basi atakayezungumza ndani yake, asizungumze isipokuwa kheri."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1165
Hadiyth
1889

أَخْبَرَنَا عَلِيُّ بْنُ مَعْبَدٍ، عَنْ مُوسَى بْنِ أَعْيَنَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha 'Aliy bin Ma'bad, kutoka kwa Muwsaa bin A'yan, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1166
Hadiyth
1890

33-Mlangoباب الصلاة خلف المقامMlango Wa Kuswali
Nyuma Ya Al-Maqaam [Maqaamu Ibraahiym (عليه السلام) ]

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ: وَافَقْتُ رَبِّي فِي ثَلَاثٍ، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، "لَوْ اتَّخَذْتَ مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: {وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى}"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه) amesema: "Nilimwafiki Rabb wangu katika (mambo) matatu. Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, lau ungefanya mahali pa kusimama Ibraahiym (عليه السلام) kuwa ni pahala pa kuswalia." Allaah Akateremsha:

وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia [Al-Baqarah (2:125)]

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1166
Hadiyth
1891

34-Mlangoباب في سنة الحاجMlango Wa Kuhusu Sunnah Ya Mwenye Kuhiji

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا حَاتِمُ بْنُ إِسْمَاعِيلَ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضِيَ اللهِ عَنْهُمَا، قَالَ أَبُو جَعْفَرٍ: دَخَلْنَا عَلَى جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، فَسَأَلَ عَنْ الْقَوْمِ حَتَّى انْتَهَى إِلَيَّ، فَقُلْتُ أَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَلِيِّ بْنِ الْحُسَيْنِ بْنِ عَلِيٍّ، فَأَهْوَى بِيَدِهِ إِلَى زِرِّيَ الْأَعْلَى وَزِرِّيَ الْأَسْفَلِ، ثُمَّ وَضَعَ فَمَهُ بَيْنَ ثَدْيَيَّ، وَأَنَا يَوْمَئِذٍ غُلَامٌ شَابٌّ، فَقَالَ: مَرْحَبًا بِكَ يَا ابْنَ أَخِي، سَلْ عَمَّا شِئْتَ. فَسَأَلْتُهُ، وَهُوَ أَعْمَى، وَجَاءَ وَقْتُ الصَّلَاةِ، فَقَامَ فِي نِسَاجَةٍ مُلْتَحِفًا بِهَا، كُلَّمَا وَضَعَهَا عَلَى مَنْكِبَيْهِ، رَجَعَ طَرَفُهَا إِلَيْهِ مِنْ صِغَرِهَا، وَرِدَاؤُهُ إِلَى جَنْبِهِ عَلَى الْمِشْجَبِ، فَصَلَّى، فَقُلْتُ: أَخْبِرْنِي عَنْ حَجَّةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَقَالَ بِيَدِهِ فَعَقَدَ تِسْعًا، فَقَالَ: مَكَثَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تِسْعَ سِنِينَ لَمْ يَحُجَّ، ثُمَّ أُذِّنَ فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ فِي الْعَاشِرَةِ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَاجٌّ، فَقَدِمَ الْمَدِينَةَ بَشَرٌ كَثِيرٌ كُلُّهُمْ يَلْتَمِسُ أَنْ يَأْتَمَّ بِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَيَعْمَلَ مِثْلَ عَمَلِهِ، فَخَرَجْنَا مَعَهُ حَتَّى أَتَيْنَا ذَا الْحُلَيْفَةِ، فَوَلَدَتْ أَسْمَاءُ بِنْتُ عُمَيْسٍ مُحَمَّدَ بْنَ أَبِي بَكْرٍ رَضِيَ اللهِ عَنْهُمْ، فَأَرْسَلَتْ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: كَيْفَ أَصْنَعُ؟ فَقَالَ: "اغْتَسِلِي وَاسْتَثْفِرِي بِثَوْبٍ وَأَحْرِمِي". فَصَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْمَسْجِدِ، ثُمَّ رَكِبَ الْقَصْوَاءَ حَتَّى اسْتَوَتْ بِهِ نَاقَتُهُ عَلَى الْبَيْدَاءِ، فَنَظَرْتُ إِلَى مَدِّ بَصَرِي مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ مِنْ رَاكِبٍ وَمَاشٍ، وَعَنْ يَمِينِهِ مِثْلُ ذَلِكَ، وَعَنْ يَسَارِهِ مِثْلُ ذَلِكَ، وَخَلْفَهُ مِثْلُ ذَلِكَ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَيْنَ أَظْهُرِنَا، وَعَلَيْهِ يُنْزَلُ الْقُرْآنُ وَهُوَ يَعْرِفُ تَأْوِيلَهُ، فَأَهَلَّ بِالتَّوْحِيدِ: "لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ". فَأَهَلَّ النَّاسُ بِهَذَا الَّذِي يُهِلُّونَ بِهِ، فَلَمْ يَرُدَّ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ شَيْئًا، وَلَبَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَلْبِيَتَهُ حَتَّى إِذَا أَتَيْنَا الْبَيْتَ مَعَهُ. قَالَ جَابِرٌ: لَسْنَا نَنْوِي إِلَّا الْحَجَّ، لَسْنَا نَعْرِفُ الْعُمْرَةَ، حَتَّى إِذَا أَتَيْنَا الْبَيْتَ مَعَهُ، اسْتَلَمَ الرُّكْنَ فَرَمَلَ ثَلَاثًا، وَمَشَى أَرْبَعًا، ثُمَّ تَقَدَّمَ إِلَى مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ فَصَلَّى، فَقَرَأَ {وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى}، فَجَعَلَ الْمَقَامَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ الْبَيْتِ، وَكَانَ أَبِي يَقُولُ: وَلَا أَعْلَمُهُ ذَكَرَهُ إِلَّا عَنْ جَابِرٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: كَانَ يَقْرَأُ فِي الرَّكْعَتَيْنِ: قُلْ هُوَ اللَّهُ أَحَدٌ وَقُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ، ثُمَّ رَجَعَ إِلَى الرُّكْنِ فَاسْتَلَمَهُ، ثُمَّ خَرَجَ مِنْ الْبَاب إِلَى الصَّفَا، فَلَمَّا أَتَى الصَّفَا، قَرَأَ: {إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ}، "أَبْدَأُ بِمَا بَدَأَ اللَّهُ بِهِ". فَبَدَأَ بِالصَّفَا فَرَقِيَ عَلَيْهِ حَتَّى رَأَى الْبَيْتَ، فَوَحَّدَ اللَّهَ وَكَبَّرَهُ، وَقَالَ: "لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ، لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ، أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَهَزَمَ الْأَحْزَابَ وَحْدَهُ". ثُمَّ دَعَا بَيْنَ ذَلِكَ، فَقَالَ مِثْلَ هَذَا ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ نَزَلَ إِلَى الْمَرْوَةِ، حَتَّى إِذَا انْصَبَّتْ قَدَمَاهُ فِي بَطْنِ الْوَادِي، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الدَّارِمِيُّ: يَعْنِي: فَرَمَلَ، حَتَّى إِذَا صَعِدْنَا مَشَى، حَتَّى إِذَا أَتَيْنَا الْمَرْوَةَ، فَفَعَلَ عَلَى الْمَرْوَةِ كَمَا فَعَلَ عَلَى الصَّفَا، حَتَّى إِذَا كَانَ آخِرَ طَوَافٍ عَلَى الْمَرْوَةِ، قَالَ: "إِنِّي لَوْ اسْتَقْبَلْتُ مِنْ أَمْرِي مَا اسْتَدْبَرْتُ، لَمْ أَسُقْ الْهَدْيَ وَجَعَلْتُهَا عُمْرَةً، فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ لَيْسَ مَعَهُ هَدْيٌ، فَلْيُحِلَّ وَلْيَجْعَلْهَا عُمْرَةً". فَقَامَ سُرَاقَةُ بْنُ مَالِكِ بْنِ جُعْشُمٍ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلِعَامِنَا هَذَا أَمْ لِأَبَدِ؟ فَشَبَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَصَابِعَهُ فِي الْأُخْرَى، فَقَالَ: "دَخَلَتِ الْعُمْرَةُ فِي الْحَجِّ"، هَكَذَا مَرَّتَيْنِ "لَا، بَلْ لِأَبَدِ أَبَدٍ، لَا بَلْ لِأَبَدِ أَبَدٍ". وَقَدِمَ عَلِيٌّ بِبُدْنٍ مِنْ الْيَمَنِ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَوَجَدَ فَاطِمَةَ مِمَّنْ حَلَّ، وَلَبِسَتْ ثِيَابَ صَبِيغٍ، وَاكْتَحَلَتْ، فَأَنْكَرَ عَلِيٌّ ذَلِكَ عَلَيْهَا، فَقَالَتْ: أَبِي أَمَرَنِي، فَكَانَ عَلِيٌّ يَقُولُ: ذَهَبْتُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُحَرِّشُهُ عَلَى فَاطِمَةَ فِي الَّذِي صَنَعَتْ، مُسْتَفْتِيًا لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا ذَكَرَتْ، فَأَنْكَرْتُ ذَلِكَ عَلَيْهَا، فَقَالَ: "صَدَقَتْ، مَا فَعَلْتَ حِينَ فَرَضْتَ الْحَجَّ؟". قَالَ: قُلْتُ: اللَّهُمَّ إِنِّي أُهِلُّ بِمَا أَهَلَّ بِهِ رَسُولُكَ. قَالَ: "فَإِنَّ مَعِيَ الْهَدْيَ فَلَا تَحْلِلْ". قَالَ: فَكَانَ جَمَاعَةُ الْهَدْيِ الَّذِي قَدِمَ بِهِ عَلِيٌّ مِنْ الْيَمَنِ، وَالَّذِي أَتَى بِهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِئَةَ بَدَنَةٍ، فَحَلَّ النَّاسُ كُلُّهُمْ وَقَصَّرُوا إِلَّا النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَنْ كَانَ مَعَهُ هَدْيٌ، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ التَّرْوِيَةِ، وَجَّهَ إِلَى مِنًى، فَأَهْلَلْنَا بِالْحَجِّ، وَرَكِبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَصَلَّى بِنَا الظُّهْرَ، وَالْعَصْرَ، وَالْمَغْرِبَ، وَالْعِشَاءَ، وَالصُّبْحَ، ثُمَّ مَكَثَ قَلِيلًا حَتَّى إِذَا طَلَعَتْ الشَّمْسُ، أَمَرَ بِقُبَّةٍ مِنْ شَعْرٍ تُضْرَبُ لَهُ بِنَمِرَةَ، ثُمَّ رَكِبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَسَارَ لَا تَشُكُّ قُرَيْشٌ إِلَّا أَنَّهُ وَاقِفٌ عِنْدَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ، كَمَا كَانَتْ قُرَيْشٌ تَصْنَعُ فِي الْجَاهِلِيَّةِ فِي الْمُزْدَلِفَةِ، فَسَارَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى أَتَى عَرَفَةَ، فَوَجَدَ الْقُبَّةَ قَدْ ضُرِبَتْ بِنَمِرَةَ، فَنَزَلَهَا حَتَّى إِذَا زَاغَتِ يَعْنِي الشَّمْسَ، أَمَرَ بِالْقَصْوَاءِ فَرُحِّلَتْ لَهُ، فَأَتَى بَطْنَ الْوَادِي، فَخَطَبَ النَّاسَ وَقَالَ: "إِنَّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ حَرَامٌ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، فِي شَهْرِكُمْ هَذَا، فِي بَلَدِكُمْ هَذَا، أَلَا إِنَّ كُلَّ شَيْءٍ مِنْ أَمْرِ الْجَاهِلِيَّةِ تَحْتَ قَدَمَيَّ مَوْضُوعٌ، وَدِمَاءُ الْجَاهِلِيَّةِ مَوْضُوعَةٌ وَأَوَّلُ دَمٍ وُضِعَ دِمَاؤُنَا: دَمُ رَبِيعَةَ بْنِ الْحَارِثِ، كَانَ مُسْتَرْضَعًا فِي بَنِي سَعْدٍ، فَقَتَلَتْهُ هُذَيْلٌ. وَرِبَا الْجَاهِلِيَّةِ مَوْضُوعٌ، وَأَوَّلُ رِبًا أَضَعُهُ رِبَا عَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَإِنَّهُ مَوْضُوعٌ كُلُّهُ، فَاتَّقُوا اللَّهَ فِي النِّسَاءِ، فَإِنَّمَا أَخَذْتُمُوهُنَّ بِأَمَانَةِ اللَّهِ، وَاسْتَحْلَلْتُمْ فُرُوجَهُنَّ بِكَلِمَةِ اللَّهِ، وَإِنَّ لَكُمْ عَلَيْهِنَّ أَنْ لَا يُوطِئْنَ فُرُشَكُمْ أَحَدًا تَكْرَهُونَهُ، فَإِنْ فَعَلْنَ ذَلِكَ، فَاضْرِبُوهُنَّ ضَرْبًا غَيْرَ مُبَرِّحٍ، وَلَهُنَّ عَلَيْكُمْ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ. وَأَنْتُمْ مَسْئولونَ عَنِّي فَمَا أَنْتُمْ قَائِلُونَ؟" قَالُوا: نَشْهَدُ أَنَّكَ قَدْ بَلَّغْتَ وَأَدَّيْتَ وَنَصَحْتَ. فَقَالَ بِأُصْبُعِهِ السَّبَّابَةِ فَرَفَعَهَا إِلَى السَّمَاءِ، وَيَنْكُتُهَا إِلَى النَّاسِ: "اللَّهُمَّ اشْهَدْ، اللَّهُمَّ اشْهَدْ، اللَّهُمَّ اشْهَدْ". ثُمَّ أَذَّنَ بِلَالٌ بِنِدَاءٍ وَاحِدٍ وَإِقَامَةٍ، فَصَلَّى الظُّهْرَ، ثُمَّ أَقَامَ فَصَلَّى الْعَصْرَ، لَمْ يُصَلِّ بَيْنَهُمَا شَيْئًا، ثُمَّ رَكِبَ حَتَّى وَقَفَ، فَجَعَلَ بَطْنَ نَاقَتِهِ الْقَصْوَاءِ إِلَى الصُّخَيْرَاتِ، وَقَالَ إِسْمَاعِيل: إِلَى الشُّجَيْرَاتِ، وَجَعَلَ حَبْلَ الْمُشَاةِ بَيْنَ يَدَيْهِ، ثُمَّ اسْتَقْبَلَ الْقِبْلَةَ، فَلَمْ يَزَلْ وَاقِفًا حَتَّى غَرَبَتْ الشَّمْسُ وَذَهَبَتْ الصُّفْرَةُ، حَتَّى غَابَ الْقُرْصُ، فَأَرْدَفَ أُسَامَةَ خَلْفَهُ، ثُمَّ دَفَعَ، وَقَدْ شَنَقَ لِلْقَصْوَاءِ الزِّمَامَ، حَتَّى إِنَّهُ لَيُصِيبُ رَأْسُهَا مَوْرِكَ رَحْلِهِ، وَيَقُولُ بِيَدِهِ الْيُمْنَى: "السَّكِينَةَ السَّكِينَةَ". كُلَّمَا أَتَى حَبْلًا مِنْ الْحِبَالِ، أَرْخَى لَهَا قَلِيلًا حَتَّى تَصْعَدَ، حَتَّى أَتَى الْمُزْدَلِفَةَ، فَصَلَّى بِهَا الْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ بِأَذَانٍ وَإِقَامَتَيْنِ، ثُمَّ اضْطَجَعَ حَتَّى إِذَا طَلَعَ الْفَجْرُ، صَلَّى الْفَجْرَ، بِأَذَانٍ وَإِقَامَةٍ، ثُمَّ رَكِبَ الْقَصْوَاءَ حَتَّى وَقَفَ عَلَى الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ، وَاسْتَقْبَلَ الْقِبْلَةَ، فَدَعَا اللَّهَ وَكَبَّرَهُ وَهَلَّلَهُ وَوَحَّدَهُ حَتَّى أَسْفَرَ جِدًا، ثُمَّ دَفَعَ قَبْلَ أَنْ تَطْلُعَ الشَّمْسُ، وَأَرْدَفَ الْفَضْلَ بْنَ الْعَبَّاسِ، وَكَانَ رَجُلًا حَسَنَ الشَّعْرِ، أَبْيَضَ، وَسِيمًا، فَلَمَّا دَفَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، مَرَّ بِالظُّعُنِ يَجْرِينَ، فَطَفِقَ الْفَضْلُ يَنْظُرُ إِلَيْهِنَّ، فَأَخَذَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ فَوَضَعَهَا عَلَى وَجْهِ الْفَضْلِ، فَحَوَّلَ الْفَضْلُ رَأْسَهُ مِنْ الشِّقِّ الْآخَرِ، فَوَضَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ مِنْ الشِّقِّ الْآخَرِ حَتَّى إِذَا أَتَى مُحَسِّرَ، حَرَّكَ قَلِيلًا، ثُمَّ سَلَكَ الطَّرِيقَ الْوُسْطَى الَّتِي تُخْرِجُكَ إِلَى الْجَمْرَةِ الْكُبْرَى، حَتَّى إِذَا أَتَى الْجَمْرَةَ الَّتِي عِنْدَهَا الشَّجَرَةُ، فَرَمَى بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ حَصَاةٍ مِنْ حَصَى الْخَذْفِ، ثُمَّ رَمَى مِنْ بَطْنِ الْوَادِي، ثُمَّ انْصَرَفَ إِلَى الْمَنْحَرِ، فَنَحَرَ ثَلَاثًا وَسِتِّينَ بَدَنَةً بِيَدِهِ، ثُمَّ أَعْطَى عَلِيًّا فَنَحَرَ مَا غَبَرَ، وَأَشْرَكَهُ فِي بُدْنِهِ، ثُمَّ أَمَرَ مِنْ كُلِّ بَدَنَةٍ بِبَضْعَةٍ، فَجُعِلَتْ فِي قِدْرٍ، فَطُبِخَتْ فَأَكَلَا مِنْ لُحُومِهَا، وَشَرِبَا مِنْ مَرَقِهَا، ثُمَّ رَكِبَ فَأَفَاضَ إِلَى الْبَيْتِ، فَأَتَى الْبَيْتَ فَصَلَّى الظُّهْرَ بِمَكَّةَ، وَأَتَى بَنِي عَبْدِ الْمُطَّلِبِ وَهُمْ يَسْتَقُونَ عَلَى زَمْزَمَ، فَقَالَ: "انْزِعُوا بَنِي عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَلَوْلَا يَغْلِبُكُمُ النَّاسُ عَلَى سِقَايَتِكُمْ، لَنَزَعْتُ مَعَكُمْ". فَنَاوَلُوهُ دَلْوًا فَشَرِبَ.

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Haatim bin Ismaa'iyl, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما): Abuw Ja'far amesema: Tuliingia kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), akauliza kuhusu watu (tulioingia) mpaka akanifikia mimi. Nikasema: Mimi ni Muhammad bin 'Aliy bin Al-Husayn bin 'Aliy. Akanyoosha mkono wake kwenye kifungo changu cha juu na kifungo changu cha chini, kisha akaweka mdomo wake baina ya matiti yangu — nami siku hiyo nilikuwa kijana mdogo —, akasema: Karibu sana, yaa mwana wa ndugu yangu! Uliza unalotaka. Nikamuuliza — naye alikuwa kipofu. Wakati wa Swalaah ukafika, akasimama katika shuka dogo lililofumwa akiwa amejifunika nalo; kila alipoliweka juu ya mabega yake, ncha yake ilimrudia kwa sababu ya udogo wake, na joho lake liko kando yake juu ya kiango cha nguo. Akaswali. Nikasema: Nikhabarishe kuhusu Hajj ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akaashiria kwa mkono wake, akakunja (vidole) tisa, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikaa miaka tisa bila kuhiji. Kisha ikatangazwa kwa watu kuhusu Hajj katika mwaka wa kumi kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) anahiji. Watu wengi wakawasili Madiynah, kila mmoja wao akitaka kumfuata Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na kufanya mfano wa amali yake. Tukatoka pamoja naye mpaka tukafika Dhul-Hulayfah. Asmaa bint 'Umays akamzaa Muhammad bin Abiy Bakr (رضي الله عنهم). Akatuma (ujumbe) kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Nifanyeje? Akasema: "Oga, na ujifunge kitambaa (cha damu) kwa nguo, na uhirimie." Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaswali Msikitini, kisha akapanda Al-Qaswwaa (ngamia wake) mpaka ngamia wake aliposimama naye wima juu ya Al-Baydaa. Nikatazama upeo wa macho yangu mbele yake: (watu) waliopanda na waendao kwa miguu; na kuliani kwake mfano wa hivyo, na kushotoni kwake mfano wa hivyo, na nyuma yake mfano wa hivyo. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) yuko kati yetu, naye ndiye anayeteremshiwa Qur-aan, na yeye anajua maana yake (na utekelezaji wake). Akahirimia kwa Tawhiyd:

لَبَّيْكَ اللَّهُمَّ لَبَّيْكَ، لَبَّيْكَ لَا شَرِيكَ لَكَ لَبَّيْكَ إِنَّ الْحَمْدَ وَالنِّعْمَةَ لَكَ وَالْمُلْكَ، لَا شَرِيكَ لَكَ

Nimekuitikia, Yaa Allaah, nimekuitikia. Nimekuitikia, huna mshirika, nimekuitikia. Hakika Himdi na Neema ni Zako, na Ufalme (ni Wako); huna mshirika.

Watu wakahirimia kwa haya wanayohirimia nayo, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwakatalia chochote; na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaleta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah) yake mpaka tulipoifikia Al-Bayt (Al-Ka'bah) pamoja naye. Jaabir (رضي الله عنه) amesema: Hatukuwa tukinuia isipokuwa Hajj; hatukuwa tukiijua 'Umrah (Hija ndogo). Mpaka tulipoifikia Al-Bayt pamoja naye, aliigusa Ar-Rukn (pembe ya Al-Ka'bah yenye Jiwe Jeusi), akafanya ramal (mwendo wa haraka kwa hatua fupi) (mizunguko) mitatu, na akatembea minne. Kisha akasonga mbele kwenda Maqaamu Ibraahiym (عليه السلام), akaswali, akasoma:

وَاتَّخِذُوا مِنْ مَقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

na fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni pahala pa kuswalia [Al-Baqarah (2:125)]

Akaweka Al-Maqaam baina yake na Al-Bayt. [Ja'far amesema:] Na baba yangu alikuwa akisema — na sijui kwamba aliitaja isipokuwa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) —: Alikuwa akisoma katika Rakaa mbili Suwrah Al-Ikhlaasw (112) na Suwrah Al-Kaafiruwn (109). Kisha akarudi kwenye Ar-Rukn akaigusa. Kisha akatoka kupitia mlango kwenda Asw-Swafaa. Alipoifikia Asw-Swafaa, alisoma:

إِنَّ الصَّفَا وَالْمَرْوَةَ مِنْ شَعَائِرِ اللَّهِ

Hakika Swafaa na Marwah ni katika Alama za Allaah [Al-Baqarah (2:158)]

"Ninaanza kwa Alichoanza nacho Allaah." Akaanza kwa Asw-Swafaa, akapanda juu yake mpaka akaiona Al-Bayt. Akampwekesha Allaah na akamtukuza, na akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ، لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، يُحْيِي وَيُمِيتُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ، أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَهَزَمَ الْأَحْزَابَ وَحْدَهُ

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, Hana mshirika; ni Wake ufalme, na ni Zake Himdi, Anahuisha na Anafisha, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake; Ametimiza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi (vya maadui) Peke Yake.

Kisha akaomba Du'aa baina ya hayo; akasema mfano wa haya mara tatu. Kisha akashuka kwenda Al-Marwah, mpaka nyayo zake zilipoteremka katika tumbo la bonde — 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan Ad-Daarimiy amesema: Yaani: akafanya ramal —, mpaka tulipopanda, akatembea; mpaka tulipoifikia Al-Marwah, akafanya juu ya Al-Marwah kama alivyofanya juu ya Asw-Swafaa. Mpaka ulipokuwa mzunguko wa mwisho juu ya Al-Marwah, akasema: "Hakika mimi lau ningelijua mapema jambo langu nililolijua baadaye, nisingeliiswaga Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram), na ningeifanya kuwa 'Umrah. Basi aliye miongoni mwenu asiyekuwa na Hadyu, atoke katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), na aifanye kuwa 'Umrah." Suraaqah bin Maalik bin Ju'shum (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Yaa Rasula-Allaah, je, ni kwa mwaka wetu huu au ni kwa milele? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaviingiza vidole vyake (vya mkono mmoja) ndani ya (vidole vya mkono) mwingine, akasema: "'Umrah imeingia ndani ya Hajj" — hivi mara mbili — "Hapana, bali ni kwa milele na milele; hapana, bali ni kwa milele na milele." 'Aliy (رضي الله عنه) akawasili kutoka Yemen na ngamia wa kuchinjwa kwa ajili ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akamkuta Faatwimah (رضي الله عنها) miongoni mwa waliotoka katika Ihraam; amevaa nguo za rangi, na amejitia wanja. 'Aliy (رضي الله عنه) akamkemea kwa hilo. Akasema: Baba yangu ndiye aliyeniamrisha. 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa akisema: Nilikwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nikimchochea juu ya Faatwimah (رضي الله عنها) kwa lile alilolifanya, nikimuuliza fatwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu aliyoyataja, na kwamba mimi nilimkemea kwa hilo. Akasema: "Amesema kweli. Ulifanya nini ulipoilazimisha Hajj (juu ya nafsi yako)?" Akasema: Nilisema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أُهِلُّ بِمَا أَهَلَّ بِهِ رَسُولُكَ

Yaa Allaah, hakika mimi ninahirimia kwa aliyohirimia nayo Rasuli Wako.

Akasema: "Basi hakika mimi nina Hadyu, kwa hiyo usitoke katika Ihraam." Akasema: Jumla ya Hadyu aliyokuja nayo 'Aliy (رضي الله عنه) kutoka Yemen, na aliyokuja nayo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), ilikuwa ngamia mia moja. Watu wote wakatoka katika Ihraam na wakapunguza (nywele), isipokuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na aliyekuwa na Hadyu. Ilipokuwa Siku ya Tarwiyah (tarehe nane Dhul-Hijjah), akaelekea Minaa, tukahirimia Hajj. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapanda (kipando chake), akatuswalisha Adhuhuri, na Alasiri, na Magharibi, na Ishaa, na Alfajiri. Kisha akakaa kidogo mpaka jua lilipochomoza, akaamrisha hema la manyoya lisimikwe kwa ajili yake huko Namirah. Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akapanda, akaenda, na Maquraysh hawakuwa na shaka isipokuwa kwamba yeye atasimama kwenye Al-Mash'aril-Haraam, kama walivyokuwa Maquraysh wakifanya katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) huko Al-Muzdalifah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaenda mpaka akaifikia 'Arafah, akakuta hema limekwisha simikwa huko Namirah, akashukia hapo. Mpaka lilipopinduka — yaani: jua —, akaamrisha Al-Qaswwaa atandikwe kwa ajili yake. Akaenda katika tumbo la bonde, akawakhutubia watu, na akasema: "Hakika damu zenu na mali zenu ni haraam, kama utukufu wa siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika nchi yenu hii. Tanabahini! Kila kitu katika mambo ya Jaahiliyyah kiko chini ya nyayo zangu, kimefutwa; na damu za Jaahiliyyah zimefutwa. Na damu ya kwanza iliyofutwa ni damu zetu: damu ya Rabiy'ah bin Al-Haarith — alikuwa akinyonyeshwa kwa Banuw Sa'd, (kabila la) Hudhayl likamuua. Na riba ya Jaahiliyyah imefutwa; na riba ya kwanza ninayoifuta ni riba ya 'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه), kwani hakika hiyo imefutwa yote. Basi mcheni Allaah kuhusu wanawake; kwani hakika nyinyi mmewachukua kwa Amana ya Allaah, na mmehalalisha tupu zao kwa Neno la Allaah. Na haki yenu juu yao ni kwamba wasimkalishe kwenye matandiko yenu yeyote mnayemchukia. Wakifanya hivyo, basi wapigeni kipigo kisichoumiza. Na haki yao juu yenu ni riziki yao na mavazi yao kwa wema. Na nyinyi mtaulizwa kuhusu mimi; basi mtasema nini?" Wakasema: Tunashuhudia kwamba wewe umefikisha (ujumbe), na umetekeleza (amana), na umetoa nasaha. Akasema kwa kidole chake cha shahada — akikiinua kuelekea mbinguni, na akikielekeza kwa watu —:

اللَّهُمَّ اشْهَدْ، اللَّهُمَّ اشْهَدْ، اللَّهُمَّ اشْهَدْ

Yaa Allaah, Shuhudia! Yaa Allaah, Shuhudia! Yaa Allaah, Shuhudia!

Kisha Bilaal (رضي الله عنه) akaadhini kwa wito mmoja, na Iqaamah; akaswali Adhuhuri. Kisha akakimu, akaswali Alasiri; hakuswali chochote baina ya hizo mbili. Kisha akapanda mpaka akasimama (mahali pa kusimama); akaliweka tumbo la ngamia wake Al-Qaswwaa kuelekea Asw-Swukhayraat (majabali madogo) — na Ismaa'iyl amesema: kuelekea Ash-Shujayraat (miti midogo) —, na akaifanya njia ya waendao kwa miguu mbele yake. Kisha akaelekea Qiblah. Hakuacha kusimama mpaka jua lilipozama na manjano (ya machweo) yakaondoka, mpaka duara (la jua) likatoweka. Akampandisha Usaamah (رضي الله عنه) nyuma yake, kisha akaondoka, naye amemvutia Al-Qaswwaa hatamu kwa nguvu, mpaka hakika kichwa chake kinagusa mahali pa kuwekea mguu pa tandiko lake; naye akisema kwa (kuashiria kwa) mkono wake wa kulia: "Utulivu! Utulivu!" Kila alipofika kwenye kilima cha mchanga, alimlegezea kidogo mpaka apande. Mpaka akaifikia Al-Muzdalifah, akaswali huko Magharibi na Ishaa kwa Adhaan moja na Iqaamah mbili. Kisha akajinyoosha (kulala) mpaka Alfajiri ilipochomoza, akaswali Alfajiri kwa Adhaan na Iqaamah. Kisha akampanda Al-Qaswwaa mpaka akasimama kwenye Al-Mash'aril-Haraam, akaelekea Qiblah, akamwomba Allaah, na akamtukuza, na akaleta Tahliyl (kusema: Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah), na akampwekesha, mpaka kukawa na mwangaza sana. Kisha akaondoka kabla ya jua kuchomoza, na akampandisha nyuma yake Al-Fadhwl bin Al-'Abbaas (رضي الله عنهما) — naye alikuwa mtu mwenye nywele nzuri, mweupe, mwenye uso mzuri. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoondoka, alipita karibu na wanawake waliopanda ngamia wakienda mbio. Al-Fadhwl (رضي الله عنه) akaanza kuwatazama. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaushika mkono wake, akauweka juu ya uso wa Al-Fadhwl (رضي الله عنه). Al-Fadhwl (رضي الله عنه) akageuza kichwa chake upande mwingine; Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaweka mkono wake kutoka upande ule mwingine; mpaka alipofika Muhassir, akamwendesha (ngamia) kidogo kwa kasi. Kisha akashika njia ya katikati inayokutoa kwenye Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) kubwa, mpaka alipoifikia Jamrah iliyo karibu na mti, akaipiga kwa vijiwe saba, akimtukuza (Allaah) kwa kila kijiwe — (vijiwe) mfano wa vijiwe vya khadhf (vidogo vya kurusha kwa vidole) —; akapiga kutoka katika tumbo la bonde. Kisha akaondoka kwenda mahali pa kuchinjia, akachinja ngamia sitini na watatu kwa mkono wake. Kisha akampa 'Aliy (رضي الله عنه), akachinja waliobaki, na akamshirikisha katika ngamia wake wa kuchinjwa. Kisha akaamrisha kipande (cha nyama) kutoka kwa kila ngamia, vikatiwa katika chungu, vikapikwa; wakala (wote wawili) katika nyama yake, na wakanywa katika mchuzi wake. Kisha akapanda, akamiminika kwenda kwenye Al-Bayt; akaifikia Al-Bayt, akaswali Adhuhuri Makkah. Akawaendea Banuw 'Abdil-Muttwalib nao wakiteka maji kwenye Zamzam, akasema: "Tekeni maji, enyi Baniy 'Abdil-Muttwalib! Lau kama si kwamba watu watakushindeni katika (haki yenu ya) kunywesha, ningeteka pamoja nanyi." Wakampa ndoo, akanywa.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1167
Hadiyth
1892

أخبرنا محمد بن سعيد الأصبهاني، أخبرنا حاتم بن إسماعيل، عن جعفر، عن أبيه، عن جابر بهذا

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd Al-Aswbahaaniy, ametukhabarisha Haatim bin Ismaa'iyl, kutoka kwa Ja'far, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwa (Hadiyth) hii.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1173
Hadiyth
1893

35-Mlangoباب في المحرم إذا مات ما يصنع بهMlango Wa Kuhusu Mwenye Ihraam (Hali Ya Kuhirimia Hajj
Au 'Umrah) Anapofariki, Afanyiwe Nini

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ هُوَ ابْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَجُلٌ وَاقِفٌ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِعَرَفَةَ، فَوَقَعَ عَنْ رَاحِلَتِهِ أَوْ قَالَ: فَأَقْعَصَتْهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اغْسِلُوهُ بِمَاءٍ وَسِدْرٍ، وَكَفِّنُوهُ فِي ثَوْبَيْنِ، وَلَا تُحَنِّطُوهُ، وَلَا تُخَمِّرُوا رَأْسَهُ، فَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَبْعَثُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مُلَبِّيًا"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad — naye ni Ibn Zayd —, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Mtu mmoja alipokuwa amesimama pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) huko 'Arafah, alianguka kutoka kwa mnyama wake wa kupanda — au alisema: (mnyama huyo) akamuua papo hapo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Muosheni kwa maji na mkunazi, na mkafinini katika nguo mbili, wala msimtie manukato (ya maiti), wala msikifunike kichwa chake; kwani hakika Allaah (تعالى) Atamfufua Siku ya Qiyaamah akileta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1174
Hadiyth
1894

36-Mlangoباب الذكر في الطواف والسعي بين الصفا والمروةMlango Wa Kumdhukuru Allaah
Katika Twawaaf (Kuzunguka Al-Ka'bah) Na Sa'yi (Kwenda
Mara Saba) Baina Ya Asw-Swafaa Na Al-Marwah

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ الْقَاسِمِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "إِنَّمَا جُعِلَ الطَّوَافُ بِالْبَيْتِ، وَرَمْيُ الْجِمَارِ، وَالسَّعْيُ بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، لِإِقَامَةِ ذِكْرِ اللَّهِ". قَالَ أَبُو عَاصِمٍ: كَانَ يَرْفَعُهُ.

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Hakika Twawaaf (kuzunguka Al-Ka'bah) ya Al-Bayt, na kurusha vijiwe katika Jamaraat (nguzo za kurushia vijiwe), na Sa'yi (kwenda mara saba) baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah, vimewekwa tu kwa ajili ya kusimamisha kumdhukuru Allaah." Abuw 'Aaswim amesema: Alikuwa akiipandisha [kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)].

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1174
Hadiyth
1895

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، وَمُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ الْقَاسِمِ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym na Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1176
Hadiyth
1896

37-Mlangoباب في فسخ الحجMlango Wa Kuhusu Kuivunja Hajj (Kuifanya 'Umrah)

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ رَبِيعَةَ بْنِ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ بِلَالِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ: فَسْخُ الْحَجِّ أَلَنَا خَاصَّةً، أَمْ لِمَنْ بَعْدَنَا؟ قَالَ: "بَلْ لَنَا خَاصَّةً"

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa Rabiy'ah bin Abiy 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Al-Haarith bin Bilaal bin Al-Haarith, kutoka kwa baba yake [Bilaal bin Al-Haarith (رضي الله عنه)], amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, kuivunja Hajj (kuifanya 'Umrah) — je, ni kwetu sisi peke yetu, au ni kwa wale watakaokuja baada yetu? Akasema: "Bali ni kwetu sisi peke yetu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1177
Hadiyth
1897

38-Mlangoباب من اعتمر في أشهر الحجMlango Wa Aliyefanya 'Umrah (Hija Ndogo) Katika Miezi Ya Hajj

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "هَذِهِ عُمْرَةٌ اسْتَمْتَعْنَا بِهَا، فَمَنْ لَمْ يَكُنْ مَعَهُ هَدْيٌ فَلْيَحِلَّ الْحِلَّ كُلَّهُ، فَقَدْ دَخَلَتِ الْعُمْرَةُ فِي الْحَجِّ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ"

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hii ni 'Umrah (Hija ndogo) tuliyostarehe nayo; basi ambaye hana Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) pamoja naye, atoke katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) kikamilifu; kwani 'Umrah imeingia ndani ya Hajj mpaka Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1178
Hadiyth
1898

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ رَبِيعِ بْنِ سَبْرَةَ، أَنَّ أَبَاهُ حَدَّثَهُ: أَنَّهُمْ سَارُوا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى بَلَغُوا عُسْفَانَ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ مِنْ بَنِي مُدْلِجٍ يُقَالُ لَهُ مَالِكُ بْنُ سُرَاقَةَ أَوْ سُرَاقَةُ بْنُ مَالِكٍ: اقْضِ لَنَا قَضَاءَ قَوْمٍ وُلِدُوا الْيَوْمَ. قَالَ: "إِنَّ اللَّهَ قَدْ أَدْخَلَ عَلَيْكُمْ فِي حَجِّكُمْ هَذَا عُمْرَةً، فَإِذَا أَنْتُمْ قَدِمْتُمْ فَمَنْ تَطَوَّفَ بِالْبَيْتِ وَبِالصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، فَقَدْ حَلَّ إِلَّا مَنْ كَانَ مَعَهُ هَدْيٌ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz, kutoka kwa Rabiy' bin Sabrah, kwamba baba yake [Sabrah (رضي الله عنه)] alimsimulia: kwamba wao walikwenda pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mpaka walipofika 'Usfaan. Mtu mmoja wa Banuw Mudlij, anayeitwa Maalik bin Suraaqah au Suraaqah bin Maalik (رضي الله عنه), akamwambia: Tuhukumie hukmu (iliyo wazi kama) ya watu waliozaliwa leo. Akasema: "Hakika Allaah Amewaingizieni katika Hajj yenu hii 'Umrah (Hija ndogo). Basi mtakapofika (Makkah), atakayetufu Al-Bayt na Asw-Swafaa na Al-Marwah, amekwisha toka katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), isipokuwa ambaye ana Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) pamoja naye."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1178
Hadiyth
1899

39-Mlangoباب كم اعتمر النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Alifanya 'Umrah (Hija Ndogo) Mara Ngapi

أَخْبَرَنَا شِهَابُ بْنُ عَبَّادٍ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ اعْتَمَرَ أَرْبَعَ عُمَرٍ: عُمْرَةَ الْحُدَيْبِيَةِ، وَعُمْرَةَ الْقَضَاءِ أَوْ قَالَ: عُمْرَةَ الْقِصَاصِ، شَكَّ شِهَابُ بْنُ عَبَّادٍ مِنْ قَابِلٍ، وَالثَّالِثَةَ مِنْ الْجِعْرَانَةِ، وَالرَّابِعَةَ الَّتِي مَعَ حَجَّتِهِ "

Ametukhabarisha Shihaab bin 'Abbaad, ametusimulia Daawuwd bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya 'Umrah (Hija ndogo) nne: 'Umrah ya Al-Hudaybiyah; na 'Umratul-Qadhwaa ('Umrah ya kulipa) — au alisema: 'Umratul-Qiswaasw ('Umrah ya kulipiza); Shihaab bin 'Abbaad ametia shaka — mwaka uliofuata; na ya tatu kutoka Al-Ji'raanah; na ya nne ni ile iliyokuwa pamoja na Hajj yake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1179
Hadiyth
1900

40-Mlangoباب فضل العمرة في رمضانMlango Wa Fadhila Ya 'Umrah (Hija Ndogo) Katika Ramadhwaan

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ لِامْرَأَةٍ: "اعْتَمِرِي فِي رَمَضَانَ، فَإِنَّ عُمْرَةً فِي رَمَضَانَ تَعْدِلُ حَجَّةً"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia mwanamke mmoja: "Fanya 'Umrah (Hija ndogo) katika Ramadhwaan; kwani 'Umrah katika Ramadhwaan ni sawa na Hajj."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1180
Hadiyth
1901

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ عِيسَى بْنِ مَعْقِلِ بْنِ أَبِي مَعْقَلٍ الْأَسَدِيِّ أَسَدُ خُزَيْمَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي يُوسُفُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلَامٍ، عَنْ جَدَّتِهِ أُمِّ مَعْقَلٍ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عُمْرَةٌ فِي رَمَضَانَ تَعْدِلُ حَجَّةً"

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa 'Iysaa bin Ma'qil bin Abiy Ma'qal Al-Asadiy — (yaani) Asad wa Khuzaymah —, amesema: Amenisimulia Yuwsuf bin 'Abdi-Allaah bin Salaam, kutoka kwa bibi yake Ummu Ma'qal (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "'Umrah (Hija ndogo) katika Ramadhwaan ni sawa na Hajj."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1180
Hadiyth
1902

41-Mlangoباب الميقات في العمرةMlango Wa Miyqaat (Mahali Pa Kuanzia Ihraam)
Katika 'Umrah (Hija Ndogo)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْبَزَّازُ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ زَكَرِيَّا، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَنِي مُزَاحِمُ بْنُ أَبِي مُزَاحِمٍ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ مُحَرِّشٍ الْكَعْبِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "خَرَجَ مِنْ الْجِعْرَانَةِ حِينَ أَنْشَأَ مُعْتَمِرًا، فَدَخَلَ مَكَّةَ لَيْلًا، فَقَضَى عُمْرَتَهُ ثُمَّ خَرَجَ مِنْ تَحْتِ لَيْلَتِهِ، فَأَصْبَحَ بِالْجِعْرَانَةِ كَبَائِتٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Al-Bazzaaz, ametusimulia Yahyaa bin Zakariyyaa, ametusimulia Ibn Jurayj, amenikhabarisha Muzaahim bin Abiy Muzaahim, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Muharrish Al-Ka'biy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka Al-Ji'raanah alipoanza (safari) akiwa katika 'Umrah (Hija ndogo); akaingia Makkah usiku, akamaliza 'Umrah yake. Kisha akatoka (Makkah) usiku huo huo, akapambaukiwa Al-Ji'raanah kama aliyelala hapo usiku.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1182
Hadiyth
1903

حَدَّثَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَمْرٍو، سَمِعَ عَمْرَو بْنَ أَوْسٍ يَقُولُ: أَخْبَرَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ يَقُولُ: "أَمَرَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ أُرْدِفَ عَائِشَةَ فَأُعْمِرَهَا مِنْ التَّنْعِيمِ". قَالَ سُفْيَانُ: كَانَ شُعْبَةُ يُعْجِبُهُ مِثْلَ هَذَا الْإِسْنَادِ

Ametusimulia Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Amr, alimsikia 'Amr bin Aws akisema: Amenikhabarisha 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr (رضي الله عنهما), akisema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniamrisha nimpandishe 'Aaishah (رضي الله عنها) nyuma yangu (juu ya kipando), nimfanyishe 'Umrah (Hija ndogo) kutoka At-Tan'iym." Sufyaan amesema: Shu'bah alikuwa akipendezwa na Isnaad (mlolongo wa wapokezi) mfano wa huu.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1183
Hadiyth
1904

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ الْعَطَّارُ، عَنْ ابْنِ خُثَيْمٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، عَنْ حَفْصَةَ بِنْتِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ، عَنْ أَبِيهَا، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لِعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ: "أَرْدِفْ أُخْتَكَ يَعْنِي: عَائِشَةَ وَأَعْمِرْهَا مِنْ التَّنْعِيمِ، فَإِذَا هَبَطْتَ مِنْ الْأَكَمَةِ، فَمُرْهَا فَلْتُحْرِمْ، فَإِنَّهَا عُمْرَةٌ مُتَقَبَّلَةٌ"

Ametusimulia Ahmad bin Yuwnus, ametusimulia Daawuwd Al-'Atwtwaar, kutoka kwa Ibn Khuthaym, kutoka kwa Yuwsuf bin Maahak, kutoka kwa Hafswah bint 'Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr Asw-Swiddiyq, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakr (رضي الله عنهما): "Mpandishe dada yako nyuma yako (juu ya kipando) — yaani: 'Aaishah (رضي الله عنها) — na umfanyishe 'Umrah (Hija ndogo) kutoka At-Tan'iym. Utakaposhuka kutoka kwenye kilima, basi mwamrishe ahirimie; kwani hiyo ni 'Umrah yenye kukubaliwa."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1183
Hadiyth
1905

42-Mlangoباب في تقبيل الحجرMlango Wa Kuhusu Kulibusu Al-Hajar (Jiwe Jeusi)

أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ عُمَرَ قَالَ: "إِنِّي لَأُقَبِّلُكَ، وَإِنِّي لَأَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ، وَلَكِنِّي رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقَبِّلُكَ"

Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba 'Umar (رضي الله عنه) alisema [akiliambia Al-Hajar (Jiwe Jeusi)]: "Hakika mimi ninakubusu, nami hakika najua kwamba wewe ni jiwe; lakini nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikubusu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1184
Hadiyth
1906

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُثْمَانَ، قَالَ: رَأَيْتُ مُحَمَّدَ بْنَ عَبَّادِ بْنِ جَعْفَرٍ "يَسْتَلِمُ الْحَجَرَ، ثُمَّ يُقَبِّلُهُ وَيَسْجُدُ عَلَيْهِ"، فَقُلْتُ لَهُ: مَا هَذَا؟ فَقَالَ: رَأَيْتُ خَالَكَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ يَفْعَلُهُ، ثُمَّ قَالَ: رَأَيْتُ عُمَرَ فَعَلَهُ، ثُمَّ قَالَ: إِنِّي لَأَعْلَمُ أَنَّكَ حَجَرٌ، وَلَكِنِّي رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَفْعَلُ هَذَا

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ja'far bin 'Abdi-Allaah bin 'Uthmaan, amesema: Nilimwona Muhammad bin 'Abbaad bin Ja'far akiligusa Al-Hajar (Jiwe Jeusi), kisha akilibusu na kusujudu juu yake. Nikamwambia: Ni nini hiki? Akasema: Nilimwona mjomba wako 'Abdu-Allaah bin 'Abbaas (رضوان الله عليه) akilifanya. Kisha akasema: Nilimwona 'Umar (رضي الله عنه) akilifanya; kisha akasema: Hakika mimi najua kwamba wewe ni jiwe; lakini nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akifanya hivi.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1185
Hadiyth
1907

43-Mlangoباب الصلاة في الكعبةMlango Wa Kuswali Ndani Ya Al-Ka'bah

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: دَخَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَكَّةَ وَرَدِيفُهُ أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، فَأَنَاخَ فِي أَصْلِ الْكَعْبَةِ، فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: وَسَعَى النَّاسُ، فَدَخَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَبِلَالٌ وَأُسَامَةُ، فَقُلْتُ لِبِلَالٍ مِنْ وَرَاءِ الْبَاب: "أَيْنَ صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَقَالَ: بَيْنَ السَّارِيَتَيْنِ".

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Makkah, na aliyekuwa amepanda nyuma yake ni Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما); akamkalisha (ngamia wake) kando ya msingi wa Al-Ka'bah. Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akasema: Na watu wakaja mbio. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingia (ndani ya Al-Ka'bah), na Bilaal na Usaamah (رضي الله عنهما). Nikamwambia Bilaal (رضي الله عنه) kutoka nyuma ya mlango: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali wapi? Akasema: Baina ya nguzo mbili."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1187
Hadiyth
1908

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا لَيْثٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، أَنَّهُ قَالَ: دَخَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْبَيْتَ هُوَ وَأُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ، وَبِلَالٌ، وَعُثْمَانُ بْنُ طَلْحَةَ الْحَجَبِيُّ، فَذَكَرَ نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Layth, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما), kwamba alisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Al-Bayt, yeye na Usaamah bin Zayd, na Bilaal, na 'Uthmaan bin Twalhah Al-Hajabiy (رضي الله عنهم); akataja mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1187
Hadiyth
1909

44-Mlangoباب الحجر من البيتMlango Wa Al-Hijr (Sehemu Iliyozungushiwa Ukuta Mfupi
Nje Ya Jengo La Al-Ka'bah) Ni Sehemu Ya Al-Bayt

حَدَّثَنِي فَرْوَةُ بْنُ أَبِي الْمَغْرَاءِ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْلَا حَدَاثَةُ عَهْدِ قَوْمِكِ بِالْكُفْرِ، لَنَقَضْتُ الْكَعْبَةَ ثُمَّ لَبَنَيْتُهَا عَلَى أُسِّ إِبْرَاهِيمَ، فَإِنَّ قُرَيْشًا حِينَ بَنَتْ اسْتَقْصَرَتْ، ثُمَّ جَعَلْتُ لَهَا خَلْفًا"

Amenisimulia Farwah bin Abil-Maghraa, ametusimulia 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: "Lau si kaumu yako kuwa karibuni tu wametoka katika ukafiri, ningeibomoa Al-Ka'bah, kisha ningeijenga juu ya msingi wa Ibraahiym (عليه السلام); kwani Quraysh walipoijenga waliipunguza. Kisha ningeiwekea mlango wa nyuma."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1188
Hadiyth
1910

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَحْوَصِ، عَنْ الْأَشْعَثِ بْنِ سُلَيْمٍ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْحِجْرِ: أَمِنَ الْبَيْتِ هُوَ؟. قَالَ: نَعَمْ. قُلْتُ: فَمَا لَهُمْ لَمْ يُدْخِلُوهُ فِي الْبَيْتِ؟ فَقَالَ: "إِنَّ قَوْمَكِ قَصَّرَتْ بِهِمْ النَّفَقَةُ". قُلْتُ: فَمَا شَأْنُ بَابِهِ مُرْتَفِعًا؟ قَالَ: "فَعَلَ ذَلِكَ قَوْمُكِ لِيُدْخِلُوا مَنْ شَاءُوا وَيَمْنَعُوا مَنْ شَاءُوا، وَلَوْلَا أَنَّ قَوْمَكِ حَدِيثُ عَهْدٍ بِجَاهِلِيَّةٍ فَأَخَافُ أَنْ تُنْكِرَ قُلُوبُهُمْ، لَعَمَدْتُ إِلَى الْحِجْرِ فَجَعَلْتُهُ فِي الْبَيْتِ وَأَلْزَقْتُ بَابَهُ بِالْأَرْضِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Abul-Ahwasw, kutoka kwa Al-Ash'ath bin Sulaym, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu Al-Hijr (sehemu iliyozungushiwa ukuta mfupi nje ya jengo la Al-Ka'bah): Je, ni sehemu ya Al-Bayt? Akasema: "Ndiyo." Nikasema: Basi wana nini hawakuuingiza katika Al-Bayt? Akasema: "Hakika kaumu yako iliwapungukia gharama." Nikasema: Basi ni nini jambo la mlango wake kuwa juu? Akasema: "Kaumu yako walifanya hivyo ili wamwingize wanayemtaka na wamzuie wanayemtaka. Na lau si kwamba kaumu yako ni karibuni tu (wametoka) katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam), nikahofia nyoyo zao zitakataa, ningeuendea Al-Hijr nikauingiza katika Al-Bayt, na ningeugandamiza mlango wake na ardhi."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1188
Hadiyth
1911

45-Mlangoباب في التحصيبMlango Wa Kuhusu At-Tahswiyb (Kushuka
Al-Muhaswswab, Bonde La Makkah)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، يَقُولُ: "التَّحْصِيبُ لَيْسَ بِشَيْءٍ، إِنَّمَا هُوَ مَنْزِلٌ نَزَلَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: التَّحْصِيبُ مَوْضِعٌ بِمَكَّةَ، وَهُوَ مَوْضِعٌ بِبَطْحَاءَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: Nilimsikia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akisema: "At-Tahswiyb (kushuka Al-Muhaswswab, bonde la Makkah) si kitu (katika ibaada za Hajj); hakika ni mahali pa kushukia tu alipofikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: At-Tahswiyb ni mahali huko Makkah, nalo ni mahali katika Batwhaa (bonde la Makkah).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1189
Hadiyth
1912

46-Mlangoباب كم صلاة يصلى بمنى حتى يغدو إلى عرفاتMlango Wa Swalaah Ngapi Zinaswaliwa Minaa
Mpaka Aondoke Asubuhi Kwenda 'Arafaat

أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا أَبُو كُدَيْنَةَ هُوَ يَحْيَى بْنُ الْمُهَلَّبِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ مِقْسَمٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمِنًى خَمْسَ صَلَوَاتٍ"

Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Abuw Kudaynah — naye ni Yahyaa bin Al-Muhallab —, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Miqsam, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Minaa Swalaah tano."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1190
Hadiyth
1913

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، وَأَحْمَدُ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ حَنْبَلٍ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ الثَّوْرِيُّ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ رُفَيْعٍ، قَالَ: قُلْتُ لِأَنَسِ بْنِ مَالِكٍ: حَدِّثْنِي بِشَيْءٍ عَقَلْتَهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيْنَ صَلَّى الظُّهْرَ يَوْمَ التَّرْوِيَةِ؟ قَالَ: بِمِنًى. قَالَ: قُلْتُ: فَأَيْنَ صَلَّى الْعَصْرَ يَوْمَ النَّفْرِ؟ قَالَ: بِالْأَبْطَحِ، ثُمَّ قَالَ: "اصْنَعْ مَا يَصْنَعُ أُمَرَاؤُكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad na Ahmad bin Muhammad bin Hanbal, kutoka kwa Is-haaq bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan Ath-Thawriy, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Rufay', amesema: Nilimwambia Anas bin Maalik (رضي الله عنه): Nisimulie kitu ulichokihifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Aliswali wapi Adhuhuri Siku ya Tarwiyah (tarehe nane Dhul-Hijjah)? Akasema: Minaa. Akasema: Nikasema: Basi aliswali wapi Alasiri siku ya An-Nafr (kuondoka Minaa)? Akasema: Al-Abtwah (bonde lililo karibu na Makkah). Kisha akasema: "Fanya wanavyofanya viongozi wako."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1190
Hadiyth
1914

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، قَالَ: حَدَّثَنِي خَالِدٌ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِلَالٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ أَنَّهُ حَدَّثَهُ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "صَلَّى الظُّهْرَ وَالْعَصْرَ وَالْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ، وَرَقَدَ رَقْدَةً بِمِنًى، ثُمَّ رَكِبَ إِلَى الْبَيْتِ فَطَافَ بِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amesema: Amenisimulia Khaalid, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Hilaal, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba alimsimulia: kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliswali Adhuhuri na Alasiri na Magharibi na Ishaa, na akalala usingizi mfupi huko Minaa; kisha akapanda (kipando chake) kwenda Al-Bayt, akaitufu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1191
Hadiyth
1915

47-Mlangoباب قصر الصلاة بمنىMlango Wa Kufupisha Swalaah Minaa

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، عَنْ مَنْصُورِ بْنِ أَبِي الْأَسْوَدِ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ وَصَلَّى مَعَ عُثْمَانَ بِمِنًى أَرْبَعَ رَكَعَاتٍ: "لَقَدْ صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي هَذَا الْمَكَانِ رَكْعَتَيْنِ رَكْعَتَيْنِ، وَمَعَ أَبِي بَكْرٍ رَكْعَتَيْنِ رَكْعَتَيْنِ، وَمَعَ عُمَرَ رَكْعَتَيْنِ رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ تَفَرَّقَتْ بِكُمْ الطُّرُقُ، فَلَيْتَ حَظِّي مِنْ أَرْبَعِ رَكَعَاتٍ رَكْعَتَانِ مُتَقَبَّلَتَانِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, kutoka kwa Manswuwr bin Abil-Aswad, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) alisema — naye alikuwa ameswali pamoja na 'Uthmaan (رضي الله عنه) huko Minaa Rakaa nne —: "Hakika niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mahali hapa Rakaa mbili mbili, na pamoja na Abuw Bakr (رضي الله عنه) Rakaa mbili mbili, na pamoja na 'Umar (رضي الله عنه) Rakaa mbili mbili. Kisha njia zikakutawanyeni. Basi laiti fungu langu katika Rakaa nne lingekuwa Rakaa mbili zenye kukubaliwa."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1192
Hadiyth
1916

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "صَلَّى بِمِنًى رَكْعَتَيْنِ، وَأَبَا بَكْرٍ رَكْعَتَيْنِ، وَعُمَرَ رَكْعَتَيْنِ، وَعُثْمَانَ رَكْعَتَيْنِ صَدْرًا مِنْ إِمَارَتِهِ، ثُمَّ أَتَمَّهَا بَعْدُ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliswali Minaa Rakaa mbili, na Abuw Bakr (رضي الله عنه) (aliswali) Rakaa mbili, na 'Umar (رضي الله عنه) Rakaa mbili, na 'Uthmaan (رضي الله عنه) Rakaa mbili mwanzoni mwa uongozi wake; kisha akaitimiza (Rakaa nne) baadaye."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1192
Hadiyth
1917

48-Mlangoباب كيف العمل في القدوم من منى إلى عرفةMlango Wa Namna Ya Amali Katika Kwenda
Kutoka Minaa Mpaka 'Arafah

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي سَلَمَةَ الْمَاجِشُونِ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ مِنًى، فَمِنَّا مَنْ يُكَبِّرُ وَمِنَّا مَنْ يُلَبِّي"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Salamah Al-Maajishuwn, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kutoka Minaa; basi miongoni mwetu kuna aliyekuwa akimtukuza Allaah, na miongoni mwetu kuna aliyekuwa akileta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1193
Hadiyth
1918

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ أَبِي بَكْرٍ الثَّقَفِيُّ، قَالَ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ وَنَحْنُ غَادِيَانِ مِنْ مِنًى إِلَى عَرَفَاتٍ عَنْ التَّلْبِيَةِ: كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ قَالَ: "كَانَ يُلَبِّي الْمُلَبِّي فَلَا يُنْكَرُ عَلَيْهِ، وَيُكَبِّرُ الْمُكَبِّرُ فَلَا يُنْكَرُ عَلَيْهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Maalik, amenisimulia Muhammad bin Abiy Bakr Ath-Thaqafiy, amesema: Nilimuuliza Anas bin Maalik (رضي الله عنه) — nasi wawili tukiwa tunakwenda asubuhi kutoka Minaa kwenda 'Arafaat — kuhusu Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah): Mlikuwa mkifanya vipi pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: "Mwenye kuleta Talbiyah alikuwa akileta Talbiyah, wala hakemewi; na mwenye kumtukuza Allaah alikuwa akimtukuza, wala hakemewi."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1193
Hadiyth
1919

49-Mlangoباب الوقوف بعرفةMlango Wa Kusimama 'Arafah

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ دِينَارٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، قَالَ: قَالَ جُبَيْرٌ: أَضْلَلْتُ بَعِيرًا لِي فَذَهَبْتُ أَطْلُبُهُ، فَرَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "وَاقِفًا مَعَ النَّاسِ بِعَرَفَةَ"، فَقُلْتُ: وَاللَّهِ إِنَّ هَذَا لَمِنْ الْحُمْسِ، فَمَا شَأْنُهُ هَا هُنَا

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, amenisimulia 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Muhammad bin Jubayr bin Mutw'im, amesema: Jubayr (رضي الله عنه) amesema: Nilipoteza ngamia wangu, nikaenda kumtafuta. "Nikamwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesimama pamoja na watu huko 'Arafah." Nikasema: Wa-Allaahi, hakika huyu ni miongoni mwa Al-Hums (Maquraysh na wafuasi wao, waliokuwa wakisimama Al-Muzdalifah badala ya 'Arafah); basi ana nini hapa?

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1194
Hadiyth
1920

50-Mlangoباب عرفة كلها موقفMlango Wa 'Arafah Yote Ni Mahali Pa Kusimama

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ جَابِرٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَمَى، ثُمَّ قَعَدَ لِلنَّاسِ، فَجَاءَهُ رَجُلٌ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي حَلَقْتُ قَبْلَ أَنْ أَنْحَرَ؟ قَالَ: "لَا حَرَجَ" ثُمَّ جَاءَهُ آخَرُ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، طُفْتُ قَبْلَ أَنْ أَرْمِيَ؟ قَالَ: "لَا حَرَجَ". قَالَ: فَمَا سُئِلَ عَنْ شَيْءٍ إِلَّا قَالَ: "لَا حَرَجَ" ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كُلُّ عَرَفَةَ مَوْقِفٌ، وَكُلُّ مُزْدَلِفَةَ مَوْقِفٌ، وَمِنًى كُلُّهَا مَنْحَرٌ، وَكُلُّ فِجَاجِ مَكَّةَ طَرِيقٌ وَمَنْحَرٌ"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alirusha (vijiwe), kisha akawakalia watu. Mtu mmoja akamjia, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nimenyoa kabla ya kuchinja. Akasema: "Hakuna ubaya." Kisha akamjia mwingine, akasema: Yaa Rasula-Allaah, nimetufu kabla ya kurusha (vijiwe). Akasema: "Hakuna ubaya." Akasema: Basi hakuulizwa kuhusu kitu chochote isipokuwa alisema: "Hakuna ubaya." Kisha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "'Arafah yote ni mahali pa kusimama, na Muzdalifah yote ni mahali pa kusimama, na Minaa yote ni mahali pa kuchinjia, na kila njia pana ya Makkah ni njia na mahali pa kuchinjia."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1195
Hadiyth
1921

51-Mlangoباب كيف السير في الإفاضة من عرفةMlango Wa Namna Ya Mwendo
Katika Kumiminika Kutoka 'Arafah

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، أَنَّهُ كَانَ رَدِيفَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَأَفَاضَ مِنْ عَرَفَةَ، وَكَانَ يَسِيرُ الْعَنَقَ، فَإِذَا أَتَى عَلَى فَجْوَةٍ، نَصَّ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), kwamba alikuwa amepanda nyuma ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); "akamiminika kutoka 'Arafah, na alikuwa akienda mwendo wa 'anaq (mwendo wa haraka kiasi); na anapofika kwenye nafasi wazi, huenda naswsw (mwendo wa kasi zaidi)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1196
Hadiyth
1922

52-Mlangoباب الجمع بين الصلاتين بجمعMlango Wa Kujumuisha Baina Ya Swalaah
Mbili Huko Jam' (Al-Muzdalifah)

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ عُقْبَةَ، قَالَ: أَخْبَرَنِي كُرَيْبٌ أَنَّهُ: سَأَلَ أُسَامَةَ بْنَ زَيْدٍ، قَالَ: أَخْبِرْنِي عَشِيَّةَ رَدِفْتَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: كَيْفَ فَعَلْتُمْ أَوْ صَنَعْتُمْ؟ قَالَ: "جِئْنَا الشِّعْبَ الَّذِي يُنِيخُ النَّاسُ فِيهِ لِلْمُعَرَّسِ، فَأَنَاخَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَاقَتَهُ، ثُمَّ بَالَ وَمَا قَالَ: أَهْرَاقَ الْمَاءَ، ثُمَّ دَعَا بِالْوَضُوءِ فَتَوَضَّأَ وُضُوءًا لَيْسَ بِالسَّابِغِ جِدًّا، ثُمَّ قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، الصَّلَاةَ؟ قَالَ: الصَّلَاةُ أَمَامَكَ. قَالَ: فَرَكِبَ حَتَّى قَدِمْنَا الْمُزْدَلِفَةَ، فَأَقَامَ الْمَغْرِبَ، ثُمَّ أَنَاخَ وَالنَّاسُ فِي مَنَازِلِهِمْ، فَلَمْ يَحِلُّوا حَتَّى أَقَامَ الْعِشَاءَ الْآخِرَةَ، فَصَلَّى، ثُمَّ حَلَّ النَّاسُ". قَالَ: قُلْتُ: أَخْبِرْنِي كَيْفَ فَعَلْتُمْ حِينَ أَصْبَحْتُمْ؟. قَالَ: رَدِفَهُ الْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ، فَانْطَلَقْتُ أَنَا فِي سُبَّاقِ قُرَيْشٍ عَلَى رِجْلَيَّ.

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Ibraahiym bin 'Uqbah, amesema: Amenikhabarisha Kurayb kwamba alimuuliza Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), akasema: Nikhabarishe jioni ile ulipopanda nyuma ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): mlifanya vipi — au: mlitenda vipi? Akasema: "Tulikuja kwenye bonde jembamba ambalo watu huwakalisha ngamia wao humo kwa ajili ya kushuka kupumzika. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamkalisha ngamia wake jike, kisha akakojoa — na hakusema: alimwaga maji —, kisha akaagiza maji ya Wudhuu, akatawadha Wudhuu usio kamili sana. Kisha nikasema: Yaa Rasula-Allaah, Swalaah? Akasema: 'Swalaah iko mbele yako.' Akasema: Akapanda mpaka tukafika Al-Muzdalifah, akakimu (Swalaah ya) Magharibi. Kisha akamkalisha (ngamia wake), na watu wakiwa katika vituo vyao; hawakufungua (mizigo) mpaka alipokimu Ishaa ya mwisho, akaswali. Kisha watu wakafungua (mizigo)." Akasema: Nikasema: Nikhabarishe mlifanya vipi mlipoamka asubuhi? Akasema: Al-Fadhwl bin 'Abbaas (رضي الله عنهما) alipanda nyuma yake, na mimi nikaenda kwa miguu yangu pamoja na watangulizi wa Quraysh.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1196
Hadiyth
1923

أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ عُقْبَةَ، عَنْ كُرَيْبِ بْنِ أَبِي مُسْلِمٍ، عَنْ أُسَامَةَ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad, ametusimulia Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Kurayb bin Abiy Muslim, kutoka kwa Usaamah (رضي الله عنه), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1198
Hadiyth
1924

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ عَدِيُّ بْنُ ثَابِتٍ: أَنْبَأَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ يَزِيدَ، عَنْ أَبِي أَيُّوبَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "جَمَعَ بَيْنَ الْمَغْرِبِ وَالْعِشَاءِ" يَعْنِي: بِجَمْعٍ

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, amesema: 'Adiyy bin Thaabit — amenipa khabari —, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd (رضي الله عنه), kutoka kwa Abuw Ayyuwb (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alijumuisha baina ya Magharibi na Ishaa" — yaani: huko Jam' (Al-Muzdalifah).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1198
Hadiyth
1925

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "صَلَّى الْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ بِالْمُزْدَلِفَةِ، لَمْ يُنَادِ فِي وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا إِلَّا بِالْإِقَامَةِ، وَلَمْ يُسَبِّحْ بَيْنَهُمَا، وَلَا عَلَى إِثْرِ وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)], kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliswali Magharibi na Ishaa huko Al-Muzdalifah; hakuita (kwa Swalaah) katika yoyote kati ya hizo mbili isipokuwa kwa Iqaamah, wala hakuswali Sunnah baina yake, wala baada ya yoyote kati yake."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1198
Hadiyth
1926

53-Mlangoباب الرخصة في النفر من جمع بليلMlango Wa Ruhusa Ya Kuondoka Jam' (Al-Muzdalifah) Usiku

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ شَوَّالٍ: أَخْبَرَهُ أَنَّ أُمَّ حَبِيبَةَ أَخْبَرَتْهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَمَرَهَا أَنْ تَنْفِرَ مِنْ جَمْعٍ بِلَيْلٍ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn Shawwaal — alimkhabarisha —, kwamba Ummu Habiybah (رضي الله عنها) alimkhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alimwamrisha aondoke kutoka Jam' (Al-Muzdalifah) usiku."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1199
Hadiyth
1927

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا أَفْلَحُ، قَالَ: سَمِعْتُ الْقَاسِمَ بْنَ مُحَمَّدٍ يُحَدِّثُ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "اسْتَأْذَنَتْ سَوْدَةُ بِنْتُ زَمْعَةَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَأْذَنَ لَهَا فَتَدْفَعَ قَبْلَ أَنْ يَدْفَعَ، فَأَذِنَ لَهَا". قَالَ الْقَاسِمُ: وَكَانَتْ امْرَأَةً ثَبِطَةً وَقَالَ الْقَاسِمُ: الثَّبِطَةُ: الثَّقِيلَةُ، فَدَفَعَتْ وَحُبِسْنَا مَعَهُ حَتَّى دَفَعْنَا بِدَفْعِهِ قَالَتْ عَائِشَةُ: "فَلَأَنْ أَكُونَ اسْتَأْذَنْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا اسْتَأْذَنَتْ سَوْدَةُ، فَأَدْفَعَ قَبْلَ النَّاسِ، أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ مَفْرُوحٍ بِهِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Aflah, amesema: Nilimsikia Al-Qaasim bin Muhammad akihadithia kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Sawdah bint Zam'ah (رضي الله عنها) alimwomba idhini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ampe idhini aondoke (Al-Muzdalifah) kabla yeye hajaondoka; akampa idhini." Al-Qaasim amesema: Na alikuwa mwanamke thabitwah — na Al-Qaasim amesema: Ath-thabitwah ni mzito —. Akaondoka, na sisi tukazuiliwa pamoja naye mpaka tukaondoka kwa kuondoka kwake. 'Aaishah (رضي الله عنها) akasema: "Kwamba ningekuwa nimemwomba idhini Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama alivyomwomba idhini Sawdah (رضي الله عنها), nikaondoka kabla ya watu, ni jambo linalopendeza zaidi kwangu kuliko kitu chochote cha kufurahisha."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1199
Hadiyth
1928

54-Mlangoباب بما يتم الحجMlango Wa Kile Ambacho Kwacho Hajj Hutimia

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا بُكَيْرُ بْنُ عَطَاءٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَعْمُرَ الدِّيلِيَّ يَقُولُ: سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْحَجِّ، فَقَالَ: "الْحَجُّ عَرَفَاتٌ أَوْ قَالَ: عَرَفَةَ، وَمَنْ أَدْرَكَ لَيْلَةَ جَمْعٍ قَبْلَ صَلَاةِ الصُّبْحِ، فَقَدْ أَدْرَكَ" وَقَالَ: "أَيَّامُ مِنًى ثَلَاثَةُ أَيَّامٍ {فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ}"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Bukayr bin 'Atwaa, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Ya'mur Ad-Diyliy (رضي الله عنه) akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu Hajj, akasema: "Hajj ni 'Arafaat — au alisema: 'Arafah —; na atakayeudiriki usiku wa Jam' (Al-Muzdalifah) kabla ya Swalaah ya Swubhi (Alfajiri), basi ameidiriki (Hajj)." Na akasema: "Siku za Minaa ni siku tatu."

فَمَنْ تَعَجَّلَ فِي يَوْمَيْنِ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ وَمَنْ تَأَخَّرَ فَلا إِثْمَ عَلَيْهِ

Atakayeharakisha kuondoka katika siku mbili basi hakuna dhambi juu yake, na atakayeakhirisha, basi hakuna dhambi juu yake [Al-Baqarah (2:203)]

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1200
Hadiyth
1929

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ مُضَرِّسٍ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالْمَوْقِفِ عَلَى رُءُوسِ النَّاسِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، جِئْتُ مِنْ جَبَلِ طَيِّىءٍ، أَكْلَلْتُ مَطِيَّتِي: وَأَتْعَبْتُ نَفْسِي، وَاللَّهِ إِنْ بَقِيَ جَبَلٌ إِلَّا وَقَفْتُ عَلَيْهِ، فَهَلْ لِي حَجٌّ؟ قَالَ: "مَنْ شَهِدَ مَعَنَا هَذِهِ الصَّلَاةَ، وَقَدْ أَتَى عَرَفَاتٍ قَبْلَ ذَلِكَ لَيْلًا أَوْ نَهَارًا، فَقَدْ قَضَى تَفَثَهُ، وَتَمَّ حَجُّهُ".

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Ismaa'iyl, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Urwah bin Mudhwarris (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mahali pa kusimama (Al-Mawqif), mbele ya watu, akasema: Yaa Rasula-Allaah, nimekuja kutoka mlima wa (kabila la) Twayyi'; nimemchosha mnyama wangu wa kupanda, na nimeichosha nafsi yangu. Wa-Allaahi, hakuna mlima uliobaki isipokuwa nilisimama juu yake; je, nina Hajj? Akasema: "Atakayehudhuria pamoja nasi Swalaah hii, naye alikuwa amefika 'Arafaat kabla ya hapo, usiku au mchana, basi amemaliza tafath (taka za mwili kama kunyoa nywele na kukata kucha) yake, na Hajj yake imetimia."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1201
Hadiyth
1930

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي السَّفَرِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ مُضَرِّسِ بْنِ حَارِثَةَ بْنِ لَامٍ، قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَذَكَرَ نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abis-Safar, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Urwah bin Mudhwarris bin Haarithah bin Laam (رضي الله عنه), amesema: Nilimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); akataja mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1201
Hadiyth
1931

55-Mlangoباب وقت الدفع من المزدلفةMlango Wa Wakati Wa Kuondoka Kutoka Al-Muzdalifah

أَخْبَرَنَا أَبُو غَسَّانَ مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عَمْرِو بْنِ مَيْمُونٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ، قَالَ: كَانَ أَهْلُ الْجَاهِلِيَّةِ يُفِيضُونَ مِنْ جَمْعٍ بَعْدَ طُلُوعِ الشَّمْسِ، وَكَانُوا يَقُولُونَ: أَشْرِقْ ثَبِيرُ لَعَلَّنَا نُغِيرُ، وَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَالَفَهُمْ "فَدَفَعَ قَبْلَ طُلُوعِ الشَّمْسِ بِقَدْرِ صَلَاةِ الْمُسْفِرِينَ أَوْ قَالَ: الْمُشْرِقِينَ بِصَلَاةِ الْغَدَاةِ"

Ametukhabarisha Abuw Ghassaan Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Amr bin Maymuwn, kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه), amesema: Watu wa Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) walikuwa wakiondoka kutoka Jam' (Al-Muzdalifah) baada ya kuchomoza jua, na walikuwa wakisema: Ingia katika mwangaza wa jua, yaa Thabiyr (mlima wa Al-Muzdalifah), ili tupate kuondoka (upesi)! Na hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwakhalifu, akaondoka kabla ya kuchomoza jua kwa kiasi cha (muda wa) Swalaah ya wanaoswali katika mwangaza wa asubuhi — au alisema: wanaoingia katika mwangaza wa jua — kwa Swalaah ya Al-Ghadaah (Alfajiri).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1202
Hadiyth
1932

56-Mlangoباب الوضع في وادي محسرMlango Wa Kuongeza Mwendo Katika Bonde La Muhassir

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا عِيسَى بْنُ يُونُسَ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ: أَنَّ أَبَا مَعْبَدٍ مَوْلَى ابْنِ عَبَّاسٍ أَخْبَرَهُ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ الْفَضْلِ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ فِي عَشِيَّةِ عَرَفَةَ وَغَدَاةِ جَمْعٍ حِينَ دَفَعُوا: "عَلَيْكُمْ السَّكِينَةَ"، وَهُوَ كَافٌّ نَاقَتَهُ، حَتَّى إِذَا دَخَلَ وَادِي مُحَسِّرٍ، أَوْضَعَ.

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametupa khabari 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha Abuz-Zubayr kwamba Abuw Ma'bad, mawlaa (mwachwa huru) wa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), alimkhabarisha, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Al-Fadhwl [bin 'Abbaas] (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema jioni ya 'Arafah na asubuhi ya Jam' (Al-Muzdalifah) walipoondoka: "Lazimianeni na utulivu," naye akimzuia ngamia wake jike; mpaka alipoingia bonde la Muhassir, akaongeza mwendo (wa ngamia wake).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1203
Hadiyth
1933

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا لَيْثٌ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، بِإِسْنَادِهِ نَحْوَهُ. قَالَ عَبْد اللَّهِ: الْإِيضَاعُ لِلْإِبِلِ، وَالْإِيجَافُ لِلْخَيْلِ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Layth, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) yake, mfano wake.

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Al-iydhwaa' (kuongeza mwendo) ni kwa ngamia, na al-iyjaaf (kukimbiza mbio) ni kwa farasi.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1203
Hadiyth
1934

57-Mlangoباب في المحصر بعدوMlango Wa Kuhusu Aliyezuiliwa Na Adui

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، وَسَالِمًا كَلَّمَا ابْنَ عُمَرَ لَيَالِيَ نَزَلَ الْحَجَّاجُ بِابْنِ الزُّبَيْرِ، قَبْلَ أَنْ يُقْتَلَ، فَقَالَا: لَا يَضُرُّكَ أَنْ لَا تَحُجَّ الْعَامَ، نَخَافُ أَنْ يُحَالَ بَيْنَكَ وَبَيْنَ الْبَيْتِ. فَقَالَ: "قَدْ خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُعْتَمِرِينَ، فَحَالَ كُفَّارُ قُرَيْشٍ دُونَ الْبَيْتِ، فَنَحَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ هَدْيَهُ، وَحَلَقَ رَأْسَهُ، ثُمَّ رَجَعَ، فَأُشْهِدُكُمْ أَنِّي قَدْ أَوْجَبْتُ عُمْرَةً، فَإِنْ خُلِّيَ بَيْنِي وَبَيْنَ الْبَيْتِ، طُفْتُ، وَإِنْ حِيلَ بَيْنِي وَبَيْنَهُ، فَعَلْتُ كَمَا كَانَ فَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا مَعَهُ، فَأَهَلَّ بِالْعُمْرَةِ مِنْ ذِي الْحُلَيْفَةِ، ثُمَّ سَارَ، فَقَالَ: إِنَّمَا شَأْنُهُمَا وَاحِدٌ، أُشْهِدُكُمْ أَنِّي قَدْ أَوْجَبْتُ حَجًّا مَعَ عُمْرَتِي. قَالَ نَافِعٌ: فَطَافَ لَهُمَا طَوَافًا وَاحِدًا، وَسَعَى لَهُمَا سَعْيًا وَاحِدًا، ثُمَّ لَمْ يَحِلَّ حَتَّى جَاءَ يَوْمَ النَّحْرِ فَأَهْدَى، وَكَانَ يَقُولُ: مَنْ جَمَعَ الْعُمْرَةَ وَالْحَجَّ فَأَهَلَّ بِهُمَا جَمِيعًا، فَلَا يَحِلَّ حَتَّى يَحِلَّ مِنْهُمَا جَمِيعًا يَوْمَ النَّحْرِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kwamba 'Abdu-Allaah bin 'Abdi-Allaah na Saalim walizungumza na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) katika masiku ambayo Al-Hajjaaj alipiga kambi dhidi ya Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما), kabla hajauawa; wakasema: Haitakudhuru usipohiji mwaka huu; tunahofia kwamba utazuiliwa baina yako na Al-Bayt (Al-Ka'bah). Akasema: "Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukiwa katika 'Umrah (Hija ndogo), makafiri wa Quraysh wakazuia (tusifike) Al-Bayt; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akachinja Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) wake, na akanyoa kichwa chake, kisha akarejea. Basi nakushuhudisheni kwamba hakika mimi nimejilazimisha 'Umrah; ikiwa nitaachiwa njia baina yangu na Al-Bayt, nitatufu; na ikiwa nitazuiliwa baina yangu na Al-Bayt, nitafanya kama alivyofanya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nami nilikuwa pamoja naye." Akahirimia 'Umrah kutoka Dhul-Hulayfah, kisha akaenda; akasema: "Hakika jambo la viwili hivi (Hajj na 'Umrah) ni moja; nakushuhudisheni kwamba hakika mimi nimejilazimisha Hajj pamoja na 'Umrah yangu." Naafi' amesema: Akatufu kwa ajili ya viwili hivyo Twawaaf moja, na akafanya Sa'yi (kwenda mara saba baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah) kwa ajili ya viwili hivyo Sa'yi moja; kisha hakutoka katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) mpaka ilipofika Siku ya Kuchinja, akatoa Hadyu. Na alikuwa akisema: "Atakayejumuisha 'Umrah na Hajj, akazihirimia zote mbili pamoja, basi asitoke katika Ihraam mpaka atoke katika zote mbili pamoja Siku ya Kuchinja."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1204
Hadiyth
1935

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ حَجَّاجٍ الصَّوَّافِ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ الْحَجَّاجِ بْنِ عَمْرٍو الْأَنْصَارِيِّ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ كُسِرَ، أَوْ عُرِجَ، فَقَدْ حَلَّ، وَعَلَيْهِ حَجَّةٌ أُخْرَى". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: رَوَاهُ مُعَاوِيَةُ بْنُ سَلَّامٍ، وَمَعْمَرٌ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ رَافِعٍ، عَنْ الْحَجَّاجِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Hajjaaj Asw-Swawwaaf, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Al-Hajjaaj bin 'Amr Al-Answaariy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Aliyevunjika (kiungo) au akachechemea, basi amekwisha kutoka katika Ihraam (hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah), na juu yake ni Hajj nyingine."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Wameipokea Mu'aawiyah bin Sallaam na Ma'mar, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Raafi', kutoka kwa Al-Hajjaaj bin 'Amr (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1205
Hadiyth
1936

58-Mlangoباب في جمرة العقبة أي ساعة ترمىMlango Wa Kuhusu Jamrah Ya Al-'Aqabah: Inapigwa Saa Gani

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، أَنْبَأَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "رَمَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْجَمْرَةَ يَوْمَ النَّحْرِ: الضُّحَى، وَبَعْدَ ذَلِكَ عِنْدَ زَوَالِ الشَّمْسِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, ametupa khabari Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) Siku ya Kuchinja wakati wa Dhwuhaa (asubuhi baada ya jua kupanda), na baada ya hapo (alipiga) wakati wa kupinduka jua."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1206
Hadiyth
1937

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ أَبِي الْبَدَّاحِ بْنِ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَرْخَصَ لِرِعَاءِ الْإِبِلِ أَنْ يَرْمُوا يَوْمَ النَّحْرِ، ثُمَّ يَرْمُوا الْغَدَ أَوْ مِنْ بَعْدِ الْغَدِ لِيَوْمَيْنِ، ثُمَّ يَرْمُوا يَوْمَ النَّفْرِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: مِنْهُمْ مَنْ يَقُولُ: عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي الْبَدَّاحِ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa Abul-Baddaah bin 'Aaswim, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaruhusu wachungaji wa ngamia wapige [Jamaraat (nguzo za kurushia vijiwe)] Siku ya Kuchinja, kisha wapige kesho yake au baada ya kesho, kwa ajili ya siku mbili, kisha wapige Siku ya An-Nafr (kuondoka Minaa).

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Miongoni mwao wapo wanaosema: 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abul-Baddaah.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1206
Hadiyth
1938

59-Mlangoباب في الرمي بمثل حصى الخذفMlango Wa Kuhusu Kupiga (Jamaraat)
Kwa Mfano Wa Vijiwe Vya Kutupia Kwa Vidole

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ التَّيْمِيِّ، قَالَ: "أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ أَنْ نَرْمِيَ الْجَمْرَةَ بِمِثْلِ حَصَى الْخَذْفِ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia 'Uthmaan bin Murrah, kutoka kwa Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin 'Uthmaan At-Taymiy (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha katika Hajj ya kuaga tupige Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) kwa (vijiwe) mfano wa vijiwe vya kutupia kwa vidole."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1207
Hadiyth
1939

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "أَمَرَهُمْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَرَمَوْا بِمِثْلِ حَصَى الْخَذْفِ، وَأَوْضَعَ فِي وَادِي مُحَسِّرٍ، وَقَالَ: عَلَيْكُمْ السَّكِينَةَ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaamrisha, wakapiga kwa (vijiwe) mfano wa vijiwe vya kutupia kwa vidole; na akaongeza mwendo (wa ngamia wake) katika bonde la Muhassir, na akasema: "Lazimianeni na utulivu."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1207
Hadiyth
1940

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدٌ، عَنْ حُمَيْدٍ الْأَعْرَجِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مُعَاذٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَأْمُرُنَا أَنْ "نَرْمِيَ الْجِمَارَ بِمِثْلِ حَصَى الْخَذْفِ". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مُعَاذٍ لَهُ صُحْبَةٌ؟ قَالَ: نَعَمْ

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid, kutoka kwa Humayd Al-A'raj, kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Mu'aadh (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akituamrisha tupige Jamaraat (nguzo za kurushia vijiwe) kwa (vijiwe) mfano wa vijiwe vya kutupia kwa vidole.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, 'Abdur-Rahmaan bin Mu'aadh (رضي الله عنه) ni Swahaba? Akasema: Ndiyo.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1207
Hadiyth
1941

60-Mlangoباب في رمي الجمار يرميها راكباMlango Wa Kuhusu Kupiga Jamaraat:
Mtu Anazipiga Akiwa Amepanda

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، وَالْمُؤَمَّلُ، وَأَبُو نُعَيْمٍ، عَنْ أَيْمَنَ بْنِ نَابِلٍ، عَنْ قُدَامَةَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمَّارٍ الْكِلَابِيِّ، قَالَ: "رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْمِي الْجِمَارَ عَلَى نَاقَةٍ صَهْبَاءَ لَيْسَ ثَمَّ ضَرْبٌ، وَلَا طَرْدٌ، وَلَا إِلَيْكَ إِلَيْكَ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, na Al-Muammal, na Abuw Nu'aym, kutoka kwa Ayman bin Naabil, kutoka kwa Qudaamah bin 'Abdi-Allaah bin 'Ammaar Al-Kilaabiy (رضي الله عنه), amesema: "Nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akipiga Jamaraat (nguzo za kurushia vijiwe) juu ya ngamia jike mwenye rangi nyeupe iliyochanganyika na wekundu; hapakuwa na kupiga (watu), wala kufukuza, wala (kuambiwa): Pisha! Pisha!"

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1209
Hadiyth
1942

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الْكَرِيمِ هُوَ الْجَزَرِيُّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ الْفَضْلِ، قَالَ: كُنْتُ رِدْفَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَلَمْ يَزَلْ يُلَبِّي حَتَّى رَمَى الْجَمْرَةَ"

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr, kutoka kwa 'Abdul-Kariym — naye ni Al-Jazariy —, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Al-Fadhwl [bin 'Abbaas] (رضي الله عنهما), amesema: "Nilikuwa nimepanda nyuma ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); hakuacha kuleta Talbiyah (kusema: Nimekuitikia, Yaa Allaah) mpaka alipopiga Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1209
Hadiyth
1943

61-Mlangoباب الرمي من بطن الوادي والتكبير مع كل حصاةMlango Wa Kupiga (Jamaraat) Kutoka Tumbo La Bonde
Na Takbiyr Pamoja Na Kila Kijiwe

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا يُونُسُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "إِذَا رَمَى الْجَمْرَةَ الَّتِي تَلِي الْمَسْجِدَ مَسْجِدَ مِنًى، يَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ يُكَبِّرُ مَعَ كُلِّ حَصَاةٍ، ثُمَّ تَقَدَّمَ أَمَامَهَا فَوَقَفَ مُسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةِ رَافِعًا يَدَيْهِ، وَكَانَ يُطِيلُ الْوُقُوفَ، ثُمَّ يَأْتِي الْجَمْرَةَ الثَّانِيَةَ فَيَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ، ثُمَّ يَنْحَدِرُ ذَاتَ الْيَسَارِ مِمَّا يَلِي الْوَادِي رَافِعًا يَدَيْهِ يَدْعُو، ثُمَّ يَأْتِي الْجَمْرَةَ الَّتِي عِنْدَ الْعَقَبَةِ، فَيَرْمِيهَا بِسَبْعِ حَصَيَاتٍ، يُكَبِّرُ كُلَّمَا رَمَى بِحَصَاةٍ، ثُمَّ يَنْصَرِفُ وَلَا يَقِفُ عِنْدَهَا". قَالَ الزُّهْرِيُّ: سَمِعْتُ سَالِمَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ يُحَدِّثُ بِهَذَا الْحَدِيثِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَفْعَلُهُ

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapopiga Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) iliyo karibu na Msikiti — Msikiti wa Minaa —, huipiga kwa vijiwe saba, akimtukuza Allaah pamoja na kila kijiwe; kisha husogea mbele yake, akasimama akielekea Qiblah, hali ameinua mikono yake (miwili); na alikuwa akirefusha kusimama. Kisha huiendea Jamrah ya pili, akaipiga kwa vijiwe saba, akimtukuza Allaah kila anapopiga kijiwe; kisha huteremka upande wa kushoto unaopakana na bonde, hali ameinua mikono yake akiomba Du'aa. Kisha huiendea Jamrah iliyo karibu na Al-'Aqabah, akaipiga kwa vijiwe saba, akimtukuza Allaah kila anapopiga kijiwe; kisha huondoka, wala hasimami kwake. Az-Zuhriy amesema: Nilimsikia Saalim bin 'Abdi-Allaah akisimulia Hadiyth hii kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)], kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Amesema: Na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akiifanya.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1210
Hadiyth
1944

62-Mlangoباب البقرة تجزئ عن البدنةMlango Wa Ng'ombe Kutosheleza Badala Ya Ngamia Wa Hadyu

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ هُوَ الْمَاجِشُونُ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ هُوَ ابْنُ الْقَاسِمِ، عَنْ الْقَاسِمِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: خَرَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَا نَذْكُرُ إِلَّا الْحَجَّ، فَلَمَّا جِئْنَا سَرِفَ، طَمِثْتُ، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ النَّحْرِ، طَهُرْتُ، فَأَرْسَلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَفَضْتُ، فَأُتِيَ بِلَحْمِ بَقَرٍ، فَقُلْتُ: مَا هَذَا؟ قَالُوا: "أَهْدَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نِسَائِهِ الْبَقَرَةَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz — naye ni Al-Maajishuwn —, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan — naye ni Ibn Al-Qaasim —, kutoka kwa Al-Qaasim, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Tulitoka pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), hatutaji (chochote) isipokuwa Hajj. Tulipofika Sarif, nikapata hedhi. Ilipokuwa Siku ya Kuchinja, nikatwahirika; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanituma, nikafanya Ifaadhwah (kuondoka kwenda Makkah kutufu). Kisha ikaletwa nyama ya ng'ombe; nikasema: Hii ni nini? Wakasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ametoa ng'ombe kuwa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) kwa niaba ya wake zake (رضي الله عنهن)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1211
Hadiyth
1945

63-Mlangoباب من قال: ليس على النساء حلقMlango Wa Aliyesema: Hakuna Kunyoa Juu Ya Wanawake

أَخْبَرَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الْمَدِينِيُّ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَنِي عَبْدُ الْحَمِيدِ بْنُ جُبَيْرٍ، عَنْ صَفِيَّةَ بِنْتِ شَيْبَةَ، قَالَتْ: أَخْبَرَتْنِي أُمُّ عُثْمَانَ بِنْتُ أَبِي سُفْيَانَ، أَنَّ ابْنَ عَبَّاسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَيْسَ عَلَى النِّسَاءِ حَلْقٌ، إِنَّمَا عَلَى النِّسَاءِ التَّقْصِيرُ"

Ametukhabarisha 'Aliy bin 'Abdi-Allaah Al-Madiyniy, ametusimulia Hishaam bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn Jurayj, amenikhabarisha 'Abdul-Hamiyd bin Jubayr, kutoka kwa Swafiyyah bint Shaybah, amesema: Amenikhabarisha Ummu 'Uthmaan bint Abiy Sufyaan (رضي الله عنها) kwamba Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna kunyoa juu ya wanawake; hakika juu ya wanawake ni kupunguza (nywele)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1212
Hadiyth
1946

64-Mlangoباب فضل الحلق على التقصيرMlango Wa Ubora Wa Kunyoa Kuliko Kupunguza

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّهُ قَالَ: "رَحِمَ اللَّهُ الْمُحَلِّقِينَ". قِيلَ: وَالْمُقَصِّرِينَ؟ قَالَ: "رَحِمَ اللَّهُ الْمُحَلِّقِينَ". قَالَ فِي الرَّابِعَةِ: "وَالْمُقَصِّرِينَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Allaah Awarehemu walionyoa." Ikasemwa: Na waliopunguza? Akasema: "Allaah Awarehemu walionyoa." Akasema katika (mara ya) nne: "Na waliopunguza."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1213
Hadiyth
1947

65-Mlangoباب فيمن قدم نسكه شيئا قبل شيءMlango Wa Kuhusu Aliyetanguliza Kitu
Katika Ibaada Zake (Za Hajj) Kabla Ya Kitu (Kingine)

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ هُوَ ابْنُ أَبِي سَلَمَةَ الْمَاجِشُونُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عِيسَى بْنِ طَلْحَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ الْجَمْرَةِ وَهُوَ يُسْأَلُ، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نَحَرْتُ قَبْلَ أَنْ أَرْمِيَ؟ قَالَ: "ارْمِ وَلَا حَرَجَ" قَالَ آخَرُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، حَلَقْتُ قَبْلَ أَنْ أَنْحَرَ؟ قَالَ: "انْحَرْ وَلَا حَرَجَ". قَالَ: فَمَا سُئِلَ عَنْ شَيْءٍ قُدِّمَ وَلَا أُخِّرَ إِلَّا قَالَ: "افْعَلْ وَلَا حَرَجَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz — naye ni Ibn Abiy Salamah Al-Maajishuwn —, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Iysaa bin Twalhah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) karibu na Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe) naye akiulizwa. Mtu mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, nimechinja kabla sijapiga (Jamrah)? Akasema: "Piga, na hakuna ubaya." Mwingine akasema: Yaa Rasula-Allaah, nimenyoa kabla sijachinja? Akasema: "Chinja, na hakuna ubaya." Amesema: Basi hakuulizwa kuhusu jambo lolote lililotangulizwa wala lililoakhirishwa isipokuwa alisema: "Fanya, na hakuna ubaya."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1214
Hadiyth
1948

أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، حَدَّثَنَا الزُّهْرِيُّ، عَنْ عِيسَى بْنِ طَلْحَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَقَفَ لِلنَّاسِ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، حَلَقْتُ قَبْلَ أَنْ أَذْبَحَ؟ قَالَ: "لَا حَرَجَ" قَالَ: لَمْ أَشْعُرْ، ذَبَحْتُ قَبْلَ أَنْ أَرْمِيَ؟ قَالَ: "لَا حَرَجَ". فَلَمْ يُسْأَلْ يَوْمَئِذٍ عَنْ شَيْءٍ قُدِّمَ أَوْ أُخِّرَ إِلَّا قَالَ: "لَا حَرَجَ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: أَنَا أَقُولُ بِهَذَا، وَأَهْلُ الْكُوفَةِ يُشَدِّدُونَ

Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Yahyaa, ametusimulia Maalik bin Anas, ametusimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Iysaa bin Twalhah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwasimamia watu katika Hajj ya kuaga. Mtu mmoja akamwambia: Yaa Rasula-Allaah, nimenyoa kabla sijachinja? Akasema: "Hakuna ubaya." Akasema: Sikutambua; nimechinja kabla sijapiga [Jamrah (nguzo ya kurushia vijiwe)]? Akasema: "Hakuna ubaya." Basi hakuulizwa siku hiyo kuhusu jambo lolote lililotangulizwa au lililoakhirishwa isipokuwa alisema: "Hakuna ubaya."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Mimi ninasema kwa (kauli) hii, na watu wa Kuwfah wanatia ukali (katika hilo).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1214
Hadiyth
1949

66-Mlangoباب سنة البدنة إذا عطبتMlango Wa Sunnah Ya Ngamia
Wa Hadyu Anapokaribia Kuangamia

أَخْبَرَنَا عَبْدُ الْوَهَّابِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ نَاجِيَةَ الْأَسْلَمِيِّ صَاحِبِ هَدْيِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: كَيْفَ أَصْنَعُ بِمَا عَطِبَ مِنْ الْهَدْيِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كُلُّ بَدَنَةٍ عَطِبَتْ فَانْحَرْهَا، ثُمَّ أَلْقِ نَعْلَهَا فِي دَمِهَا، ثُمَّ خَلِّ بَيْنَهَا وَبَيْنَ النَّاسِ فَلْيَأْكُلُوهَا".

Ametukhabarisha 'Abdul-Wahhaab bin Sa'iyd, ametusimulia Shu'ayb bin Is-haaq, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Naajiyah Al-Aslamiy (رضي الله عنه), msimamizi wa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Nifanye nini kwa (mnyama) atakayekaribia kuangamia (njiani) katika Hadyu? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Kila ngamia (wa Hadyu) atakayekaribia kuangamia, basi mchinje, kisha tupa kiatu chake (alichovishwa kishada) katika damu yake, kisha mwache baina yake na watu, ili wamle."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1215
Hadiyth
1950

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ نَاجِيَةَ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Naajiyah (رضي الله عنه), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1215
Hadiyth
1951

67-Mlangoباب من قال: الشاة تجزئ في الهديMlango Wa Aliyesema: Mbuzi Anatosheleza Katika Hadyu

أَخْبَرَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، وَأَبُو نُعَيْمٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "أَهْدَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّةً غَنَمًا"

Ametukhabarisha Ya'laa bin 'Ubayd na Abuw Nu'aym, wamesema: Ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) mara moja mbuzi na kondoo."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1216
Hadiyth
1952

68-Mlangoباب في الإشعار كيف يشعرMlango Wa Kuhusu Kumtia Alama
Mnyama Wa Hadyu: Atiwe Alama Vipi

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا حَسَّانَ يُحَدِّثُ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "صَلَّى الظُّهْرَ بِذِي الْحُلَيْفَةِ، ثُمَّ دَعَا بِبَدَنَةٍ فَأَشْعَرَهَا مِنْ صَفْحَةِ سَنَامِهَا الْأَيْمَنِ، ثُمَّ سَلَتَ الدَّمَ عَنْهَا وَقَلَّدَهَا نَعْلَيْنِ، ثُمَّ أُتِيَ بِرَاحِلَتِهِ، فَلَمَّا قَعَدَ عَلَيْهَا وَاسْتَوَتْ عَلَى الْبَيْدَاءِ، أَهَلَّ بِالْحَجِّ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, amesema: Nilimsikia Abuw Hassaan akisimulia kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali Adhuhuri huko Dhul-Hulayfah, kisha akaagiza aletewe ngamia wa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram), akamtia alama (kwa kumchanja) upande wa kulia wa nundu yake, kisha akaipangusa damu kutoka kwake, na akamvisha kishada cha viatu viwili. Kisha akaletewa mnyama wake wa kupanda; alipokaa juu yake na (mnyama) akasimama sawasawa naye juu ya Al-Baydaa, alihirimia Hajj.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1216
Hadiyth
1953

69-Mlangoباب في ركوب البدنةMlango Wa Kuhusu Kumpanda Ngamia Wa Hadyu

أَخْبَرَنَا أَبُو النَّضْرِ هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: قَتَادَةُ أَخْبَرَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ أَنَسًا يُحَدِّثُ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ انْتَهَى إِلَى رَجُلٍ يَسُوقُ بَدَنَةً، قَالَ: "ارْكَبْهَا". فَقَالَ: إِنَّهَا بَدَنَةٌ. قَالَ: "ارْكَبْهَا". قَالَ: إِنَّهَا بَدَنَةٌ، قَالَ: "ارْكَبْهَا وَيْحَكَ!"

Ametukhabarisha Abun-Nadhwr Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, amesema: Qataadah amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia Anas (رضي الله عنه) akisimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alimfikia mtu mmoja akimswaga ngamia wa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram), akasema: "Mpande." Akasema: Hakika yeye ni ngamia wa Hadyu. Akasema: "Mpande." Akasema: Hakika yeye ni ngamia wa Hadyu. Akasema: "Mpande, ole wako!"

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1217
Hadiyth
1954

70-Mlangoباب في نحر البدن قياماMlango Wa Kuhusu Kuchinja
Ngamia Wa Hadyu Wakiwa Wamesimama

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يُونُسَ بْنِ عُبَيْدٍ، عَنْ زِيَادِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّهُ رَأَى رَجُلًا قَدْ أَنَاخَ بَدَنَةً، فَقَالَ: "ابْعَثْهَا قِيَامًا مُقَيَّدَةً، سُنَّةَ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus bin 'Ubayd, kutoka kwa Ziyaad bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba alimwona mtu mmoja aliyekwisha kumpigisha magoti ngamia wa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram), akasema: "Mwinue akiwa amesimama, amefungwa — (kwa kufuata) Sunnah ya Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1217
Hadiyth
1955

71-Mlangoباب في خطبة الموسمMlango Wa Kuhusu Khutbah Ya Msimu [Wa Hajj]

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَرَأْتُ عَلَى أَبِي قُرَّةَ مُوسَى بْنُ طَارِقٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُثْمَانَ بْنِ خُثَيْمٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ رَجَعَ مِنْ عُمْرَةِ الْجِعْرَانَةِ، بَعَثَ أَبَا بَكْرٍ عَلَى الْحَجِّ، فَأَقْبَلْنَا مَعَهُ حَتَّى إِذَا كُنَّا بِالْعَرْجِ ثُوِّبَ بِالصُّبْحِ، فَلَمَّا اسْتَوَى لِيُكَبِّرَ، سَمِعَ الرَّغْوَةَ خَلْفَ ظَهْرِهِ، فَوَقَفَ عَنْ التَّكْبِيرِ، فَقَالَ: هَذِهِ رَغْوَةُ نَاقَةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْجَدْعَاءِ، لَقَدْ بَدَا لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْحَجِّ، فَلَعَلَّهُ أَنْ يَكُونَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَنُصَلِّيَ مَعَهُ، فَإِذَا عَلِيٌّ عَلَيْهَا، فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: أَمِيرٌ أَمْ رَسُولٌ؟ قَالَ: لَا، بَلْ رَسُولٌ، "أَرْسَلَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِبَرَاءَةٌ أَقْرَؤُهَا عَلَى النَّاسِ فِي مَوَاقِفِ الْحَجِّ". فَقَدِمْنَا مَكَّةَ، فَلَمَّا كَانَ قَبْلَ التَّرْوِيَةِ بِيَوْمٍ، قَامَ أَبُو بَكْرٍ فَخَطَبَ النَّاسَ، فَحَدَّثَهُمْ عَنْ مَنَاسِكِهِمْ حَتَّى إِذَا فَرَغَ، قَامَ عَلِيٌّ فَقَرَأَ عَلَى النَّاسِ بَرَاءَةٌ حَتَّى خَتَمَهَا. ثُمَّ خَرَجْنَا مَعَهُ حَتَّى إِذَا كَانَ يَوْمُ عَرَفَةَ، قَامَ أَبُو بَكْرٍ فَخَطَبَ النَّاسَ، فَحَدَّثَهُمْ عَنْ مَنَاسِكِهِمْ، حَتَّى إِذَا فَرَغَ، قَامَ عَلِيٌّ فَقَرَأَ عَلَى النَّاسِ بَرَاءَةٌ حَتَّى خَتَمَهَا. ثُمَّ كَانَ يَوْمُ النَّحْرِ فَأَفَضْنَا، فَلَمَّا رَجَعَ أَبُو بَكْرٍ خَطَبَ النَّاسَ، فَحَدَّثَهُمْ عَنْ إِفَاضَتِهِمْ، وَعَنْ نَحْرِهِمْ، وَعَنْ مَنَاسِكِهِمْ، فَلَمَّا فَرَغَ، قَامَ عَلِيٌّ فَقَرَأَ عَلَى النَّاسِ بَرَاءَةٌ حَتَّى خَتَمَهَا، فَلَمَّا كَانَ يَوْمُ النَّفْرِ الْأَوَّلُ، قَامَ أَبُو بَكْرٍ فَخَطَبَ النَّاسَ، فَحَدَّثَهُمْ كَيْفَ يَنْفِرُونَ، وَكَيْفَ يَرْمُونَ، فَعَلَّمَهُمْ مَنَاسِكَهُمْ، فَلَمَّا فَرَغَ، قَامَ عَلِيٌّ فَقَرَأَ بَرَاءَةٌ عَلَى النَّاسِ حَتَّى خَتَمَهَا

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, amesema: Nilimsomea Abuw Qurrah Muwsaa bin Twaariq, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenisimulia 'Abdu-Allaah bin 'Uthmaan bin Khuthaym, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliporejea kutoka 'Umrah (Hija ndogo) ya Al-Ji'raanah, alimtuma Abuw Bakr (رضي الله عنه) (kuwa kiongozi) wa Hajj. Tukaenda pamoja naye, mpaka tulipokuwa Al-'Arj, Iqaamah ya Swalaah ya Swubhi (Alfajiri) ilikimiwa. Aliposimama sawasawa ili alete Takbiyr (ya kuanza Swalaah), akasikia mlio wa ngamia nyuma ya mgongo wake, akasita kuleta Takbiyr, akasema: Huu ni mlio wa ngamia jike wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), Al-Jad'aa. Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amepata rai (nyingine) kuhusu Hajj; basi huenda akawa ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nasi tuswali pamoja naye. Ghafla 'Aliy (رضي الله عنه) yuko juu yake. Abuw Bakr (رضي الله عنه) akasema: (Umekuja ukiwa) kiongozi au mjumbe? Akasema: Hapana, bali ni mjumbe; "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amenituma na (Suwrah) Baraa-ah (9) niisome kwa watu katika visimamo vya Hajj." Tukawasili Makkah. Ilipokuwa siku moja kabla ya (Siku ya) Tarwiyah (tarehe nane Dhul-Hijjah), Abuw Bakr (رضي الله عنه) alisimama, akawakhutubia watu, akawasimulia kuhusu ibaada zao za Hajj; mpaka alipomaliza, 'Aliy (رضي الله عنه) alisimama, akawasomea watu Baraa-ah mpaka akaimaliza. Kisha tukatoka pamoja naye, mpaka ilipokuwa Siku ya 'Arafah, Abuw Bakr (رضي الله عنه) alisimama, akawakhutubia watu, akawasimulia kuhusu ibaada zao za Hajj; mpaka alipomaliza, 'Aliy (رضي الله عنه) alisimama, akawasomea watu Baraa-ah mpaka akaimaliza. Kisha ikawa Siku ya Kuchinja, tukafanya Ifaadhwah (kuondoka kwenda Makkah kutufu). Aliporejea Abuw Bakr (رضي الله عنه), aliwakhutubia watu, akawasimulia kuhusu Ifaadhwah yao, na kuhusu uchinjaji wao, na kuhusu ibaada zao za Hajj. Alipomaliza, 'Aliy (رضي الله عنه) alisimama, akawasomea watu Baraa-ah mpaka akaimaliza. Ilipokuwa Siku ya An-Nafr ya kwanza (siku ya kwanza ya kuondoka Minaa), Abuw Bakr (رضي الله عنه) alisimama, akawakhutubia watu, akawasimulia namna watakavyoondoka na namna watakavyopiga [Jamaraat (nguzo za kurushia vijiwe)], akawafundisha ibaada zao za Hajj. Alipomaliza, 'Aliy (رضي الله عنه) alisimama, akawasomea watu Baraa-ah mpaka akaimaliza.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1218
Hadiyth
1956

72-Mlangoباب في الخطبة يوم النحرMlango Wa Kuhusu Khutbah Siku Ya Kuchinja

أَخْبَرَنَا أَبُو حَاتِمٍ أَشْهَلُ بْنُ حَاتِمٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَمَّا كَانَ ذَلِكَ الْيَوْمُ، قَعَدَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى بَعِيرٍ لَا أَدْرِي جَمَلٌ أَوْ نَاقَةٌ، وَأَخَذَ إِنْسَانٌ بِخِطَامِهِ أَوْ قَالَ: بِزِمَامِهِ، فَقَالَ: "أَيُّ يَوْمٍ هَذَا؟" قَالَ: فَسَكَتْنَا حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّهُ سَيُسَمِّيهِ سِوَى اسْمِهِ، فَقَالَ: "أَلَيْسَ يَوْمَ النَّحْرِ؟" قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: "فَأَيُّ شَهْرٍ هَذَا؟" قَالَ: فَسَكَتْنَا حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّهُ سَيُسَمِّيهِ سِوَى اسْمِهِ، فَقَالَ: "أَلَيْسَ ذَا الْحِجَّةِ؟". قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: "فَأَيُّ بَلَدٍ هَذَا؟". قَالَ: فَسَكَتْنَا حَتَّى ظَنَنَّا أَنَّهُ سَيُسَمِّيهِ سِوَى اسْمِهِ، فَقَالَ: "أَلَيْسَ الْبَلْدَةَ؟". قُلْنَا: بَلَى. قَالَ: "فَإِنَّ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ بَيْنَكُمْ حَرَامٌ كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا، فِي شَهْرِكُمْ هَذَا، فِي بَلَدِكُمْ هَذَا، أَلَا لِيُبَلِّغْ الشَّاهِدُ الْغَائِبَ، فَإِنَّ الشَّاهِدَ عَسَى أَنْ يُبَلِّغَ مَنْ هُوَ أَوْعَى مِنْهُ"

Ametukhabarisha Abuw Haatim Ash-hal bin Haatim, ametusimulia Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn], kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Ilipokuwa siku ile, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikaa juu ya ngamia — sijui ni dume au jike —, na mtu mmoja akashika hatamu yake — au alisema: kamba yake ya kuongozea —, akasema: "Hii ni siku gani?" Akasema: Tukanyamaza mpaka tukadhani kwamba ataiita jina lisilokuwa jina lake. Akasema: "Je, si Siku ya Kuchinja?" Tukasema: Bila shaka. Akasema: "Basi huu ni mwezi gani?" Akasema: Tukanyamaza mpaka tukadhani kwamba atauita jina lisilokuwa jina lake. Akasema: "Je, si Dhul-Hijjah?" Tukasema: Bila shaka. Akasema: "Basi huu ni mji gani?" Akasema: Tukanyamaza mpaka tukadhani kwamba atauita jina lisilokuwa jina lake. Akasema: "Je, si Al-Baldah (mji mtukufu wa Makkah)?" Tukasema: Bila shaka. Akasema: "Basi hakika damu zenu, na mali zenu, na heshima zenu baina yenu ni haraam, kama utukufu wa siku yenu hii, katika mwezi wenu huu, katika mji wenu huu. Tanabahini! Aliyehudhuria amfikishie asiyekuwepo; kwani huenda aliyehudhuria akamfikishia ambaye ni mwenye kuhifadhi zaidi kuliko yeye."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1220
Hadiyth
1957

73-Mlangoباب المرأة تحيض بعد الزيارةMlango Wa Mwanamke Anayepata Hedhi
Baada Ya Az-Ziyaarah (Twawaaf Ya Ifaadhwah)

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: حَاضَتْ صَفِيَّةُ، فَلَمَّا كَانَتْ لَيْلَةُ النَّفْرِ، قَالَتْ: أَيْ حَلْقَى، أَيْ عَقْرَى! بِلُغَةٍ لَهُمْ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَلَسْتِ قَدْ طُفْتِ يَوْمَ النَّحْرِ؟" قَالَتْ: بَلَى. قَالَ: "فَارْكَبِي".

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Swafiyyah (رضي الله عنها) alipata hedhi. Ilipokuwa usiku wa An-Nafr (kuondoka Minaa), akasema: «أَيْ حَلْقَى، أَيْ عَقْرَى» (neno la mshangao kwa Waarabu lisilokusudiwa maana yake halisi), kwa lugha yao. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, hukuwa umeshatufu (Al-Ka'bah) Siku ya Kuchinja?" Akasema: Bila shaka. Akasema: "Basi panda (kipando chako)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1221
Hadiyth
1958

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَائِشَةَ، بِنَحْوِهِ

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwa (Hadiyth) mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1222
Hadiyth
1959

74-Mlangoباب لا يطوف بالبيت عريانMlango Wa Asiitufu Al-Bayt Aliye Uchi

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْبَزَّازُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ زَيْدِ بْنِ يُثَيْعٍ، قَالَ: سَأَلْنَا عَلِيًّا: بِأَيِّ شَيْءٍ بُعِثْتَ؟. قَالَ: "بُعِثْتُ بِأَرْبَعٍ: لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ إِلَّا نَفْسٌ مُؤْمِنَةٌ، وَلَا يَطُوفُ بِالْبَيْتِ عُرْيَانٌ، وَلَا يَجْتَمِعُ مُسْلِمٌ وَكَافِرٌ فِي الْحَجِّ بَعْدَ عَامِهِمْ هَذَا، وَمَنْ كَانَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَهْدٌ، فَعَهْدُهُ إِلَى مُدَّتِهِ، وَمَنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ عَهْدٌ، فَهِيَ أَرْبَعَةُ أَشْهُرٍ. يَقُولُ بَعْدَ يَوْمِ النَّحْرِ أَجَلُهُمْ عِشْرِينَ مِنْ ذِي الْحِجَّةِ، فَاقْتُلُوهُمْ بَعْدَ الْأَرْبَعَةِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Al-Bazzaaz, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Zayd bin Yuthay', amesema: Tulimuuliza 'Aliy (رضي الله عنه): Ulitumwa na kitu gani? Akasema: "Nilitumwa na (mambo) manne: Haingii Jannah (Pepo) isipokuwa nafsi iliyoamini; wala asiitufu Al-Bayt (Al-Ka'bah) aliye uchi; wala wasikusanyike Muislamu na kafiri katika Hajj baada ya mwaka wao huu; na aliyekuwa na ahadi baina yake na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), basi ahadi yake ni mpaka muda wake (umalizike); na asiyekuwa na ahadi, basi (muda wake) ni miezi minne. Anasema: Baada ya Siku ya Kuchinja, muda wao ni (siku) ishirini za Dhul-Hijjah; basi waueni baada ya (miezi) minne."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1222
Hadiyth
1960

75-Mlangoباب إذا ودع البيت لا يرفع يديهMlango Wa Anapoiaga Al-Bayt Hanyanyui Mikono Yake

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ الْحَنَفِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي أَبُو قَزَعَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ مُهَاجِرًا يَقُولُ: سُئِلَ جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ عَنْ رَفْعِ الْأَيْدِي عِنْدَ الْبَيْتِ، فَقَالَ: "إِنَّمَا كَانَ يَصْنَعُ ذَلِكَ الْيَهُودُ، حَجَجْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَفَصَنَعْنَا ذَلِكَ؟"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd Al-Hanafiy, ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha Abuw Qaza'ah, amesema: Nilimsikia Muhaajir akisema: Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) aliulizwa kuhusu kunyanyua mikono mbele ya Al-Bayt (Al-Ka'bah). Akasema: "Hakika walikuwa wakifanya hivyo Mayahudi. Tulihiji pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); je, tulifanya hivyo?"

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1223
Hadiyth
1961

76-Mlangoباب في حرمة المسلمMlango Wa Kuhusu Utukufu Wa Muislamu

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، وَحَجَّاجٌ، قَالَا: حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي عَلِيُّ بْنُ مُدْرِكٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا زُرْعَةَ يُحَدِّثُ، عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "اسْتَنْصَتَ النَّاسَ"، فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ، ثُمَّ قَالَ: "لَا تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفَّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd na Hajjaaj, wamesema: Ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha 'Aliy bin Mudrik, amesema: Nilimsikia Abuw Zur'ah akisimulia kutoka kwa Jariyr bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: "Wanyamazishe watu (wasikilize)" — katika Hajj ya Kuaga —, kisha akasema: "Msirudi baada yangu kuwa makafiri, baadhi yenu wakizipiga shingo za wengine."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1224
Hadiyth
1962

77-Mlangoباب في السعي بين الصفا والمروةMlango Wa Kuhusu Sa'yi Baina Ya Asw-Swafaa Na Al-Marwah

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبِي خَالِدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ أَبِي أَوْفَى يَقُولُ: "سَعَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَيْنَ الصَّفَا وَالْمَرْوَةِ، وَنَحْنُ نَسْتُرُهُ مِنْ أَهْلِ مَكَّةَ أَنْ يُصِيبَهُ أَحَدٌ بِحَجَرٍ أَوْ بِرَمْيَةٍ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametusimulia Ismaa'iyl bin Abiy Khaalid, amesema: Nilimsikia Ibn Abiy Awfaa (رضي الله عنهما) akisema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifanya Sa'yi (kwenda mara saba) baina ya Asw-Swafaa na Al-Marwah, nasi tukimsitiri kutokana na watu wa Makkah, asije yeyote akampiga kwa jiwe au kwa kurusha (kitu)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1225
Hadiyth
1963

78-Mlangoباب في القرانMlango Wa Kuhusu Qiraan (Kuunganisha Hajj Na 'Umrah)

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ الْحُسَيْنِ، عَنْ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، أَنَّهُ شَهِدَ عَلِيًّا وَعُثْمَانَ بَيْنَ مَكَّةَ وَالْمَدِينَةِ، وَعُثْمَانُ يَنْهَى عَنْ الْمُتْعَةِ، فَلَمَّا رَأَى ذَلِكَ عَلِيٌّ، "أَهَلَّ بِهِمَا جَمِيعًا، فَقَالَ: لَبَّيْكَ بِحَجَّةٍ وَعُمْرَةٍ مَعًا". فَقَالَ: تَرَانِي أَنْهَى عَنْهُ وَتَفْعَلُهُ؟ فَقَالَ: لَمْ أَكُنْ لِأَدَعَ سُنَّةَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَوْلِ أَحَدٍ مِنْ النَّاسِ

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa 'Aliy bin Al-Husayn, kutoka kwa Marwaan bin Al-Hakam, kwamba alimshuhudia 'Aliy na 'Uthmaan (رضي الله عنهما) baina ya Makkah na Madiynah, na 'Uthmaan (رضي الله عنه) alikuwa akikataza Mut'ah (Tamattu' — kuhirimia 'Umrah katika miezi ya Hajj, kisha kuhirimia Hajj mwaka huo huo). 'Aliy (رضي الله عنه) alipoona hilo, alihirimia kwa [Hajj na 'Umrah (Hija ndogo)] zote mbili kwa pamoja, akasema:

لَبَّيْكَ بِحَجَّةٍ وَعُمْرَةٍ مَعًا

Nimekuitikia kwa Hajj na 'Umrah kwa pamoja.

Akasema: Unaniona ninalikataza nawe unalifanya? Akasema: Sikuwa mtu wa kuiacha Sunnah ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa sababu ya kauli ya yeyote miongoni mwa watu.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1226
Hadiyth
1964

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَبَّيْكَ بِعُمْرَةٍ وَحَجٍّ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema:

لَبَّيْكَ بِعُمْرَةٍ وَحَجٍّ

Nimekuitikia kwa 'Umrah na Hajj.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1226
Hadiyth
1965

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ الشَّهِيدِ، عَنْ بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَنَسٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَهَلَّ بِهِمَا جَمِيعًا"، فَلَقِيتُ ابْنَ عُمَرَ فَأَخْبَرْتُهُ بِقَوْلِ أَنَسٍ، فَقَالَ: إِنَّمَا أَهَلَّ بِالْحَجِّ، فَرَجَعْتُ إِلَى أَنَسٍ فَأَخْبَرْتُهُ بِقَوْلِ ابْنِ عُمَرَ، فَقَالَ: مَا يَعُدُّونَنَا إِلَّا صِبْيَانًا

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Habiyb bin Ash-Shahiyd, kutoka kwa Bakr bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), "kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alihirimia kwa [Hajj na 'Umrah (Hija ndogo)] zote mbili kwa pamoja." Nikakutana na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), nikamkhabarisha kauli ya Anas (رضي الله عنه); akasema: "Hakika alihirimia Hajj tu." Nikarudi kwa Anas (رضي الله عنه), nikamkhabarisha kauli ya Ibn 'Umar (رضي الله عنهما); akasema: Hawatuhesabu isipokuwa kuwa ni watoto wadogo.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1226
Hadiyth
1966

79-Mlangoباب الطواف في غير وقت الصلاةMlango Wa Twawaaf Katika Wakati Usiokuwa Wa Swalaah

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ بَابَاهُ، عَنْ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ، إِنْ وَلِيتُمْ هَذَا الْأَمْرَ، فَلَا تَمْنَعُوا أَحَدًا طَافَ أَوْ صَلَّى أَيَّ سَاعَةٍ شَاءَ مِنْ لَيْلٍ أَوْ نَهَارٍ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Baabaah, kutoka kwa Jubayr bin Mutw'im (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yaa Baniy 'Abdi Manaaf! Mkilitawalia jambo hili, basi msimzuie yeyote aliyetufu au aliyeswali saa yoyote anayotaka, ya usiku au ya mchana."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1227
Hadiyth
1967

80-Mlangoباب في دخول البيت نهاراMlango Wa Kuhusu Kuingia Al-Bayt Mchana

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، أَخْبَرَنِي نَافِعٌ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "بَاتَ بِذِي طُوًى حَتَّى أَصْبَحَ، ثُمَّ دَخَلَ مَكَّةَ"، وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يَفْعَلُهُ

Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, amenikhabarisha Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), "kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala usiku Dhuw Twuwaa (bonde lililo karibu na Makkah) mpaka asubuhi, kisha akaingia Makkah." Na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akilifanya hilo.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1227
Hadiyth
1968

81-Mlangoباب في أي طريق يدخل مكةMlango Wa Kuhusu Ni Kupitia Njia Gani Aingie Makkah

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنِي نَافِعٌ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "كَانَ يَدْخُلُ مَكَّةَ مِنْ الثَّنِيَّةِ الْعُلْيَا، وَيَخْرُجُ مِنْ الثَّنِيَّةِ السُّفْلَى"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, amenisimulia Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), "kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiingia Makkah kupitia Ath-Thaniyyah Al-'Ulyaa (njia ya mlima ya juu), na akitoka kupitia Ath-Thaniyyah As-Suflaa (njia ya mlima ya chini)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1228
Hadiyth
1969

82-Mlangoباب متى يهل الرجلMlango Wa Ni Wakati Gani Mtu Ahirimie

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "إِذَا أَدْخَلَ رِجْلَهُ فِي الْغَرْزِ وَاسْتَوَتْ بِهِ نَاقَتُهُ، أَهَلَّ مِنْ مَسْجِدِ ذِي الْحُلَيْفَةِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa, "anapoingiza mguu wake katika kikuku cha kupandia, na ngamia wake jike akasimama wima naye, huhirimia kutoka Msikiti wa Dhul-Hulayfah (mahali pa kuhirimia kwa watu wa Madiynah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1229
Hadiyth
1970

83-Mlangoباب ما يصنع المحرم إذا اشتكى عينيهMlango Wa Anachofanya Muhrim (Aliye
Katika Hali Ya Kuhirimia Hajj
Au 'Umrah) Anapoumwa Macho Yake

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي شَيْبَةَ، وَمُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ مُوسَى، عَنْ نُبَيْهِ بْنِ وَهْبٍ، عَنْ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ أَبِيهِ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ فِي الْمُحْرِمِ إِذَا اشْتَكَى عَيْنَيْهِ: "يَضْمِدُهَا بِالصَّبِرِ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad bin Abiy Shaybah na Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, wamesema: Ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ayyuwb bin Muwsaa, kutoka kwa Nubayh bin Wahb, kutoka kwa Abaan bin 'Uthmaan, kutoka kwa baba yake ['Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه)], kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema kuhusu muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) anapoumwa macho yake: "Ayafunge kwa shubiri."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1229
Hadiyth
1971

84-Mlangoباب أين يصلي الرجل بعد الطوافMlango Wa Mahali Anaposwali Mtu Baada Ya Twawaaf

أَخْبَرَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ، يَقُولُ: "قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَطَافَ بِالْبَيْتِ وَصَلَّى عِنْدَ الْمَقَامِ رَكْعَتَيْنِ، ثُمَّ خَرَجَ إِلَى الصَّفَا".

Ametukhabarisha Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, amesema: Nilimsikia Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akisema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwasili (Makkah), akatufu Al-Bayt (Al-Ka'bah), na akaswali Rakaa mbili kwenye Al-Maqaam [Maqaam ya Ibraahiym (عليه السلام)], kisha akatoka kwenda Asw-Swafaa."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1230
Hadiyth
1972

قَالَ شُعْبَةُ: فَحَدَّثَنِي أَيُّوبُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: هِيَ السُّنَّةُ

Shu'bah amesema: Na akanisimulia Ayyuwb, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Hiyo ndiyo Sunnah.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1230
Hadiyth
1973

85-Mlangoباب في طواف الوداعMlango Wa Kuhusu Twawaaful-Widaa'i (Twawaaf Ya Kuaga)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ ابْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ الْأَحْوَلِ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: كَانَ النَّاسُ يَنْصَرِفُونَ فِي كُلِّ وَجْهٍ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَنْفِرَنَّ أَحَدٌ حَتَّى يَكُونَ آخِرُ عَهْدِهِ بِالْبَيْتِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Sulaymaan Al-Ahwal, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Watu walikuwa wakiondoka (baada ya Hajj) kila upande. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Asiondoke kabisa yeyote mpaka kiwe kitu chake cha mwisho ni (Twawaaf ya) Al-Bayt (Al-Ka'bah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1230
Hadiyth
1974

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "رُخِّصَ لِلْحَائِضِ أَنْ تَنْفِرَ إِذَا أَفَاضَتْ".

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Imeruhusiwa kwa mwanamke mwenye hedhi kuondoka (Makkah) anapokuwa ameshafanya Twawaaf ya Ifaadhwah (Twawaaf ya nguzo ya Hajj)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1231
Hadiyth
1975

قَالَ: وَسَمِعْتُ ابْنَ عُمَرَ عَامَ الْأَوَّلِ: أَنَّهَا لَا تَنْفِرُ، ثُمَّ سَمِعْتُهُ، يَقُولُ: تَنْفِرُ، إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَخَّصَ لَهُنَّ

Amesema: Na nilimsikia Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) mwaka uliotangulia (akisema) kwamba yeye (mwanamke mwenye hedhi) haondoki; kisha nikamsikia akisema: Anaondoka; "hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaruhusu wao (wanawake)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1231
Hadiyth
1976

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، يَقُولُ: حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي عُقَيْلٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي طَاوُسٌ الْيَمَانِيُّ، أَنَّهُ سَمِعَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُمَرَ وَهُوَ يُسْأَلُ عَنْ حَبْسِ النِّسَاءِ عَنْ الطَّوَافِ بِالْبَيْتِ إِذَا حِضْنَ قَبْلَ النَّفْرِ، وَقَدْ أَفَضْنَ يَوْمَ النَّحْرِ، فَقَالَ: "إِنَّ عَائِشَةَ كَانَتْ تَذْكُرُ رُخْصَةً لِلنِّسَاءِ". وَذَلِكَ قَبْلَ مَوْتِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بِعَامٍ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, anasema: Amenisimulia Al-Layth, amenisimulia 'Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: Amenikhabarisha Twaawuws Al-Yamaaniy kwamba alimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), naye akiulizwa kuhusu kuwazuia wanawake (wasiondoke) kwa ajili ya Twawaaf ya Al-Bayt (Al-Ka'bah) wanapopata hedhi kabla ya An-Nafr (kuondoka Minaa), nao wameshafanya Twawaaf ya Ifaadhwah (Twawaaf ya nguzo ya Hajj) Siku ya Kuchinja. Akasema: "Hakika 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa akitaja ruhusa kwa wanawake." Na hilo lilikuwa mwaka mmoja kabla ya kufariki 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1231
Hadiyth
1977

86-Mlangoباب في الذي يبعث هديه وهو يقيم في بلدهMlango Wa Kuhusu Anayepeleka Hadyu (Mnyama Wa Kuchinjwa
Haram) Yake Naye Akabaki Katika Mji Wake

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل يَعْنِي ابْنَ أَبِي خَالِدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، أَنَّهُ قَالَ لِعَائِشَةَ: يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، إِنَّ رِجَالًا يَبْعَثُ أَحَدُهُمْ بِالْهَدْيِ مَعَ الرَّجُلِ، فَيَقُولُ: إِذَا بَلَغْتَ مَكَانَ كَذَا وَكَذَا، فَقَلِّدْهُ، فَإِذَا بَلَغَ ذَلِكَ الْمَكَانَ، لَمْ يَزَلْ مُحْرِمًا حَتَّى يَحِلَّ النَّاسُ. قَالَ: فَسَمِعْتُ صَفْقَتَهَا بِيَدِهَا مِنْ وَرَاءِ الْحِجَابِ، وَقَالَتْ: "لَقَدْ كُنْتُ أَفْتِلُ الْقَلَائِدَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَيَبْعَثُ بِالْهَدْيِ إِلَى الْكَعْبَةِ، مَا يَحْرُمُ عَلَيْهِ شَيْءٌ مِمَّا يَحِلُّ لِلرَّجُلِ مِنْ أَهْلِهِ حَتَّى يَرْجِعَ النَّاسُ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Ismaa'iyl — yaani Ibn Abiy Khaalid —, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Masruwq, kwamba alimwambia 'Aaishah (رضي الله عنها): Yaa Ummal-Muuminiyn, hakika kuna wanaume ambao mmoja wao hupeleka Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) pamoja na mtu, akamwambia: Utakapofika mahali fulani na fulani, mvishe kigwe. Basi (Hadyu) inapofika mahali hapo, (mwenye kuipeleka) huendelea kuwa muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah) mpaka watu watoke katika Ihraam. Amesema: Nikasikia kupiga kwake makofi kwa mkono wake nyuma ya pazia, na akasema: "Kwa hakika nilikuwa nikisokota vigwe kwa ajili ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), naye anapeleka Hadyu kwenye Al-Ka'bah, wala hakuharamikii kitu chochote katika yale yaliyo halaal kwa mwanamume kutoka kwa ahli yake, mpaka watu warudi."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1232
Hadiyth
1978

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ بْنُ الزُّبَيْرِ، وَعَمْرَةُ بِنْتُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ عَائِشَةَ قَالَتْ: "كُنْتُ أَفْتِلُ قَلَائِدَ هَدْيِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَيَبْعَثُ بِهَدْيِهِ مُقَلَّدَةً، وَيُقِيمُ بِالْمَدِينَةِ وَلَا يَجْتَنِبُ شَيْئًا حَتَّى يُنْحَرَ هَدْيُهُ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha 'Urwah bin Az-Zubayr na 'Amrah bint 'Abdir-Rahmaan, kwamba 'Aaishah (رضي الله عنها) alisema: "Nilikuwa nikisokota vigwe vya Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram) ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), naye anapeleka Hadyu yake ikiwa imevishwa vigwe, na anabaki Madiynah, wala haepuki chochote mpaka Hadyu yake ichinjwe."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1232
Hadiyth
1979

87-Mlangoباب كراهية البنيان بمنىMlango Wa Karaha Ya Kujenga Majengo Minaa

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مُهَاجِرٍ، عَنْ يُوسُفَ بْنِ مَاهَكَ، عَنْ أُمِّهِ مُسَيْكَةَ وَأَثْنَى عَلَيْهَا خَيْرًا، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَلَا نَبْنِي لَكَ بِمِنًى بِنَاءً يُظِلُّكَ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا، مِنًى مُنَاخُ مَنْ سَبَقَ"

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Wakiy', ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Ibraahiym bin Muhaajir, kutoka kwa Yuwsuf bin Maahak, kutoka kwa mama yake Musaykah — naye akamsifu kwa kheri —, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, je, tusikujengee huko Minaa jengo litakalokupa kivuli? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hapana; Minaa ni mahali pa kupiga kambi kwa aliyetangulia (kufika)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1233
Hadiyth
1980

88-Mlangoباب في دخول مكة بغير إحرام حج ولا عمرةMlango Wa Kuhusu Kuingia Makkah
Bila Ihraam Ya Hajj Wala 'Umrah

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ مَكَّةَ عَامَ الْفَتْحِ وَعَلَى رَأْسِهِ مِغْفَرٌ، فَلَمَّا نَزَعَهُ جَاءَهُ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذَا ابْنُ خَطَلٍ مُتَعَلِّقٌ بِأَسْتَارِ الْكَعْبَةِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اقْتُلُوهُ". قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَالِدٍ: وَقُرِئَ عَلَى مَالِكٍ: قَالَ: قَالَ ابْنُ شِهَابٍ: وَلَمْ يَكُنْ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَئِذٍ مُحْرِمًا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Khaalid, ametusimulia Maalik bin Anas, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Makkah mwaka wa Ufunguzi (wa Makkah), na juu ya kichwa chake kuna kofia ya chuma. Alipoivua, alimjia mtu mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, huyu Ibn Khatwal amejishikiza na mapazia ya Al-Ka'bah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Muueni." 'Abdu-Allaah bin Khaalid amesema: Na (Hadiyth hii) ilisomwa kwa Maalik, akasema: Ibn Shihaab amesema: Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa siku hiyo muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah).

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1233
Hadiyth
1981

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ عَمَّارٍ الدُّهْنِيُّ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "دَخَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَكَّةَ حِينَ افْتَتَحَهَا وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاءُ بِغَيْرِ إِحْرَامٍ". قَالَ إِسْمَاعِيل: سَمِعَهُ مِنْ أَبِي الزُّبَيْرِ. كَانَ مَعَ أَبِيهِ

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Abaan, ametusimulia Mu'aawiyah bin 'Ammaar Ad-Duhniy, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia Makkah alipoifungua, na juu yake kuna kilemba cheusi, bila Ihraam." Ismaa'iyl amesema: Aliisikia kutoka kwa Abuz-Zubayr; alikuwa pamoja na baba yake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1234
Hadiyth
1982

89-Mlangoباب لا يعطى الجازر من البدن شيئاMlango Wa Mchinjaji Hapewi Chochote
Katika Ngamia Wa Hadyu (Mnyama Wa Kuchinjwa Haram)

أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي الْحَسَنُ بْنُ مُسْلِمٍ، وَعَبْدُ الْكَرِيمِ الْجَزَرِيُّ، أَنَّ مُجَاهِدًا أَخْبَرَهُمَا، أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ أَبِي لَيْلَى أَخْبَرَهُ، أَنَّ عَلِيًّا أَخْبَرَهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَمَرَهُ أَنْ يَقُومَ عَلَى بُدْنِهِ، وَأَنْ يَقْسِمَ بُدْنَهُ كُلَّهَا: لُحُومَهَا وَجُلُودَهَا وَجِلَالَهَا، وَلَا يُعْطِيَ فِي جِزَارَتِهَا مِنْهَا شَيْئًا"

Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha Al-Hasan bin Muslim na 'Abdul-Kariym Al-Jazariy, kwamba Mujaahid aliwakhabarisha, kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa alimkhabarisha, kwamba 'Aliy (رضي الله عنه) alimkhabarisha, "kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuamrisha asimamie ngamia wake wa Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram), na agawe ngamia wake wote — nyama zao, na ngozi zao, na nguo zao za kufunikwa —, wala asitoe chochote katika hao kwa ujira wa kuwachinja."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1234
Hadiyth
1983

90-Mlangoباب في جزاء الضبعMlango Wa Kuhusu Fidia Ya Fisi

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي عَمَّارٍ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الضَّبُعِ، فَقَالَ: "هُوَ صَيْدٌ وَفِيهِ كَبْشٌ إِذَا أَصَابَهُ الْمُحْرِمُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Jariyr bin Haazim, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Ubayd bin 'Umayr, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy 'Ammaar, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu fisi, akasema: "Yeye ni windo, na ndani yake kuna (fidia ya) kondoo dume, anapomuua muhrim (aliye katika hali ya kuhirimia Hajj au 'Umrah)."

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1235
Hadiyth
1984

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي عَمَّارٍ، قَالَ: سَأَلْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ عَنْ الضَّبُعِ آكُلُهُ؟ قَالَ: نَعَمْ، قُلْتُ: هُوَ صَيْدٌ؟ قَالَ: نَعَمْ ". قُلْتُ: سَمِعْتَهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ قَالَ: نَعَمْ. قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: مَا تَقُولُ فِي الضَّبُعِ تَأْكُلُهُ؟ قَالَ: أَنَا أَكْرَهُ أَكْلَهُ

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Ubayd bin 'Umayr, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin 'Abdi-Allaah bin Abiy 'Ammaar, amesema: Nilimuuliza Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) kuhusu fisi: Je, nimle? Akasema: Ndiyo. Nikasema: Je, ni windo? Akasema: Ndiyo. Nikasema: Je, ulilisikia hilo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Ndiyo.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Unasemaje kuhusu fisi, je, unamla? Akasema: Mimi nachukia kumla.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1235
Hadiyth
1985

91-Mlangoباب فيمن يبيت بمكة ليالي منى من علةMlango Wa Kuhusu Anayelala Usiku Makkah
Katika Siku Za Minaa Kwa Sababu Ya Udhuru

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ: أَنَّ الْعَّبَاسَ بْنَ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ اسْتَأْذَنَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِيَبِيتَ بِمَكَّةَ لَيَالِيَ مِنًى مِنْ أَجْلِ سِقَايَتِهِ. فَأَذِنَ لَهُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه) alimuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) idhini ya kulala Makkah usiku wa (siku za) Minaa kwa ajili ya kazi yake ya kunywesha (Mahujaji); naye akampa idhini.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1236
Hadiyth
1986

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ عِيسَى بْنِ يُونُسَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، نَحْوَهُ

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, (Hadiyth) mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
5
Ukurasa
1237
Hadiyth
1987