من كتاب الأضاحي
1-Mlangoباب السنة في الأضحيةMlango Wa Sunnah
Katika Udhwhiyah (Wanyama Wa Kuchinjwa Siku Ya 'Iyd)
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: "ضَحَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ، وَيُسَمِّي وَيُكَبِّرُ، لَقَدْ رَأَيْتُهُ يَذْبَحُهُمَا بِيَدِهِ وَاضِعًا عَلَى صِفَاحِهِمَا قَدَمَهُ"، قُلْتُ: أَنْتَ سَمِعْتَهُ؟ قَالَ: نَعَمْ
Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alichinja kuwa udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) kondoo dume wawili weupe waliochanganyika na weusi, wenye pembe, huku akitaja Jina la Allaah na akimtukuza (Allaah). Hakika nilimuona akiwachinja kwa mkono wake, akiwa ameweka mguu wake juu ya ubavu wa shingo zao." (Shu'bah amesema:) Nikasema (kumuuliza Qataadah): Je, wewe ulimsikia [Anas (رضي الله عنه)]? Akasema: Ndiyo.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1239
- Hadiyth
- 1988
أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي عَيَّاشٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: ضَحَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ فِي يَوْمِ الْعِيدِ، فَقَالَ حِينَ وَجَّهَهُمَا: "إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا وَمَا أَنَا مِنْ الْمُشْرِكِينَ. إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا شَرِيكَ لَهُ، وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ. اللَّهُمَّ إِنَّ هَذَا مِنْكَ وَلَكَ، عَنْ مُحَمَّدٍ وَأُمَّتِهِ"، ثُمَّ سَمَّى اللَّهَ وَكَبَّرَ وَذَبَحَ
Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Abuw 'Ayyaash, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alichinja kuwa udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) kondoo dume wawili siku ya 'Iyd. Akasema alipowaelekeza (Qiblah):
إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا وَمَا أَنَا مِنْ الْمُشْرِكِينَ. إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ، لَا شَرِيكَ لَهُ، وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ. اللَّهُمَّ إِنَّ هَذَا مِنْكَ وَلَكَ، عَنْ مُحَمَّدٍ وَأُمَّتِهِ
Hakika mimi nimeelekeza uso wangu kwa Ambaye Ameanzisha mbingu na ardhi, nikijitenga na itikadi potofu na kuelemea haki, nami si katika washirikina. Hakika Swalaah yangu, na ibaada yangu ya kuchinja, na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee Rabb wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza. Yaa Allaah! Hakika huyu (mnyama) ni kutoka Kwako na ni kwa ajili Yako, kwa niaba ya Muhammad na Ummah wake.
Kisha akataja Jina la Allaah, na akamtukuza (Allaah), na akachinja.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1239
- Hadiyth
- 1989
2-Mlangoباب ما يستدل من حديث النبي صلى الله عليه وسلم أن الأضحية ليس بواجبMlango Wa Yanayotolewa Dalili Kutokana
Na Hadiyth Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kwamba Udhwhiyah
(Wanyama Wa Kuchinjwa Siku Ya 'Iyd) Si Wajibu
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي خَالِدٌ يَعْنِي: ابْنَ يَزِيدَ، حَدَّثَنِي سَعِيدٌ يَعْنِي: ابْنَ أَبِي هِلَالٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُسْلِمٍ قَالَ: أَخْبَرَنِي ابْنُ الْمُسَيَّبِ، أَنَّ أُمَّ سَلَمَةَ أَخْبَرَتْهُ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ، قَالَ: "مَنْ أَرَادَ أَنْ يُضَحِّيَ، فَلَا يُقَلِّمْ أَظْفَارَهُ، وَلَا يَحْلِقْ شَيْئًا مِنْ شَعْرِهِ فِي الْعَشْرِ الْأُوَلِ مِنْ ذِي الْحِجَّةِ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Khaalid — yaani: Ibn Yaziyd —, amenisimulia Sa'iyd — yaani: Ibn Abiy Hilaal —, kutoka kwa 'Amr bin Muslim, amesema: Amenikhabarisha Ibn Al-Musayyib, kwamba Ummu Salamah (رضي الله عنها) alimkhabarisha, kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba amesema: "Anayetaka kuchinja udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd), basi asikate kucha zake, wala asinyoe chochote katika nywele zake katika (siku) kumi za mwanzo za (mwezi wa) Dhul-Hijjah."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1240
- Hadiyth
- 1990
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنِي عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ حُمَيْدٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِذَا دَخَلَتْ الْعَشْرُ، وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ، فَلَا يَمَسَّ مِنْ شَعْرِهِ وَلَا أَظْفَارِهِ شَيْئًا"
Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, amenisimulia 'Abdur-Rahmaan bin Humayd, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Ummu Salamah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Zinapoingia (siku) kumi (za Dhul-Hijjah), na mmoja wenu akataka kuchinja udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd), basi asiguse chochote katika nywele zake wala kucha zake."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1240
- Hadiyth
- 1991
3-Mlangoباب ما لا يجوز في الأضاحيMlango Wa Wasiofaa Miongoni Mwa Udhwhiyah
(Wanyama Wa Kuchinjwa Siku Ya 'Iyd)
أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ فَيْرُوزَ، عَنْ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، قَالَ: سُئِلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا يُتَّقَى مِنْ الضَّحَايَا؟ قَالَ: "الْعَوْرَاءُ الْبَيِّنُ عَوَرُهَا، وَالْعَرْجَاءُ الْبَيِّنُ ظَلْعُهَا، وَالْمَرِيضَةُ الْبَيِّنُ مَرَضُهَا، وَالْعَجْفَاءُ الَّتِي لَا تُنْقِي"
Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Amr bin Al-Haarith, kutoka kwa 'Ubayd bin Fayruwz, kutoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa: Ni (wanyama) gani wanaoepukwa katika udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd)? Akasema: "Chongo aliye wazi uchongo wake, na kiguru aliye wazi kuchechemea kwake, na mgonjwa aliye wazi ugonjwa wake, na aliyekonda asiye na uboho (mifupani mwake)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1241
- Hadiyth
- 1992
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ فَيْرُوزَ، قَالَ: سَأَلْتُ الْبَرَاءَ عَمَّا نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ الْأَضَاحِيِّ، فَقَالَ: "أَرْبَعٌ لَا يُجْزِئْنَ: الْعَوْرَاءُ الْبَيِّنُ عَوَرُهَا، وَالْعَرْجَاءُ الْبَيِّنُ ظَلْعُهَا، وَالْمَرِيضَةُ الْبَيِّنُ مَرَضُهَا، وَالْكَسِيرُ الَّتِي لَا تُنْقِي". قَالَ: قُلْتُ لِلْبَرَاءِ: فَإِنِّي أَكْرَهُ أَنْ يَكُونَ فِي السِّنِّ نَقْصٌ، وَفِي الْأُذُنِ نَقْصٌ، وَفِي الْقَرْنِ نَقْصٌ، قَالَ: فَمَا كَرِهْتَ فَدَعْهُ، وَلَا تُحَرِّمْهُ عَلَى أَحَدٍ
Ametusimulia Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Sulaymaan bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Ubayd bin Fayruwz, amesema: Nilimuuliza Al-Baraa (رضي الله عنه) kuhusu (wanyama) aliowakataza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd). Akasema: "Wanne hawatoshelezi: chongo aliye wazi uchongo wake, na kiguru aliye wazi kuchechemea kwake, na mgonjwa aliye wazi ugonjwa wake, na aliyevunjika (mguu) asiye na uboho (mifupani mwake)." Akasema: Nikamwambia Al-Baraa (رضي الله عنه): Hakika mimi nachukia kuwe na upungufu katika meno, na upungufu katika sikio, na upungufu katika pembe. Akasema: Basi unachokichukia, kiache, wala usikiharamishe kwa yeyote.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1241
- Hadiyth
- 1993
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، قَالَ: سَمِعْتُ حُجَيَّةَ بْنَ عَدِيٍّ، قَالَ: سَمِعْتُ عَلِيًّا وَسَأَلَهُ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، الْبَقَرَةُ؟ قَالَ: عَنْ سَبْعَةٍ، قُلْتُ: الْقَرْنُ؟ قَالَ: لَا يَضُرُّكَ. قَالَ: قُلْتُ: الْعَرَجُ؟ قَالَ: إِذَا بَلَغَتْ الْمَنْسَكَ. ثُمَّ قَالَ: "أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ نَسْتَشْرِفَ الْعَيْنَ وَالْأُذُنَ"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, amesema: Nilimsikia Hujayyah bin 'Adiyy, amesema: Nilimsikia 'Aliy (رضي الله عنه), na mtu mmoja alikuwa amemuuliza, akasema: Yaa Amiyral-Muuminiyn (Kiongozi wa Waumini), ng'ombe (anatosha kwa wangapi)? Akasema: Kwa (watu) saba. Nikasema: (Kasoro ya) pembe? Akasema: Haikudhuru. Akasema: Nikasema: Kuchechemea? Akasema: Akiweza kufika mahali pa kuchinjia (kwa miguu yake, hakudhuru). Kisha akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha tuyachunguze kwa makini macho na masikio (ya mnyama wa kuchinjwa)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1242
- Hadiyth
- 1994
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ شُرَيْحِ بْنِ النُّعْمَانِ الصَّائِدِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: "أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ نَسْتَشْرِفَ الْعَيْنَ وَالْأُذُنَ، وَأَنْ لَا نُضَحِّيَ بِمُقَابَلَةٍ وَلَا مُدَابَرَةٍ وَلَا خَرْقَاءَ، وَلَا شَرْقَاءَ"، فَالْمُقَابَلَةُ: مَا قُطِعَ طَرَفُ أُذُنِهَا، وَالْمُدَابَرَةُ: مَا قُطِعَ مِنْ جَانِبِ الْأُذُنِ، وَالْخَرْقَاءُ: الْمَثْقُوبَةُ، وَالشَّرْقَاءُ: الْمَشْقُوقَةُ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Shurayh bin An-Nu'maan Asw-Swaaidiy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha tuyachunguze kwa makini macho na masikio, na tusichinje kuwa udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) muqaabalah, wala mudaabarah, wala kharqaa, wala sharqaa." Basi muqaabalah: ni (mnyama) aliyekatwa ncha ya sikio lake; na mudaabarah: ni aliyekatwa (kipande) upande wa (nyuma wa) sikio; na kharqaa: ni aliyetobolewa (sikio); na sharqaa: ni aliyepasuliwa (sikio).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1242
- Hadiyth
- 1995
4-Mlangoباب ما يجزئ من الضحاياMlango Wa Wanaotosheleza Miongoni Mwa Udhwhiyah
(Wanyama Wa Kuchinjwa Siku Ya 'Iyd)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ بَعْجَةَ الْجُهَنِيِّ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ، قَالَ: قَسَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ضَحَايَا بَيْنَ أَصْحَابِهِ فَأَصَابَنِي جَذَعٌ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّهَا صَارَتْ لِي جَذَعَةً، فَقَالَ: "ضَحِّ بِهَا"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Ba'jah Al-Juhaniy, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aligawa udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) baina ya Swahaba zake (رضي الله عنهم); mimi nikapata jadha' (mnyama mchanga wa umri wa karibu mwaka mmoja). Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika imenifikia jadha'ah. Akasema: "Ichinje kuwa udhwhiyah."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1243
- Hadiyth
- 1996
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ بْنُ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي الْخَيْرِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: أَعْطَانِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَنَمًا أَقْسِمُهَا عَلَى أَصْحَابِهِ، فَقَسَمْتُهَا وَبَقِيَ مِنْهَا عَتُودٌ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "ضَحِّ بِهِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: الْعَتُودُ: الْجَذَعُ مِنْ الْمَعْزِ
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Al-Layth, amenisimulia Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Abul-Khayr, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinipa mbuzi na kondoo niwagawe kwa Swahaba zake (رضي الله عنهم). Nikawagawa, na akabakia miongoni mwao 'atuwd. Nikamtajia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hilo, akasema: "Mchinje kuwa udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd)."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Al-'atuwd: ni jadha' (mnyama mchanga wa umri wa karibu mwaka mmoja) katika mbuzi.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1243
- Hadiyth
- 1997
5-Mlangoباب البدنة عن سبعة والبقرة عن سبعةMlango Wa Badanah (Ngamia Wa Kuchinjwa) Ni
Kwa Ajili Ya (Watu) Saba, Na Ng'ombe Ni
Kwa Ajili Ya (Watu) Saba
أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: نَحَرْنَا يَوْمَ الْحُدَيْبِيَةِ سَبْعِينَ بَدَنَةً، الْبَدَنَةُ عَنْ سَبْعَةٍ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اشْتَرِكُوا فِي الْهَدْيِ"
Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Tulichinja siku ya Al-Hudaybiyah badanah (ngamia wa kuchinjwa) sabini; badanah moja kwa ajili ya (watu) saba. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Shirikianeni katika Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1244
- Hadiyth
- 1998
أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "نَحَرْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْبَقَرَةَ عَنْ سَبْعَةٍ". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: تَقُولُ بِهِ؟ قَالَ: نَعَمْ
Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: "Tulichinja pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ng'ombe kwa ajili ya (watu) saba."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unasema kwa (kauli) hii? Akasema: Ndiyo.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1244
- Hadiyth
- 1999
6-Mlangoباب في لحوم الأضاحيMlango Wa Kuhusu Nyama Za Udhwhiyah
(Wanyama Wa Kuchinjwa Siku Ya 'Iyd)
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ لُحُومِ الْأَضَاحِيِّ، أَوْ قَالَ: "لَا تَأْكُلُوا لُحُومَ الْأَضَاحِيِّ بَعْدَ ثَلَاثٍ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza (kula) nyama za udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd), au alisema: "Msile nyama za udhwhiyah baada ya (siku) tatu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1245
- Hadiyth
- 2000
أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدٍ هُوَ ابْنُ عَبْدِ اللَّهِ الطَّحَّانُ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمَلِيحِ، عَنْ نُبَيْشَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِنَّا كُنَّا نَهَيْنَاكُمْ عَنْ لُحُومِ الْأَضَاحِيِّ أَنْ تَأْكُلُوهَا فَوْقَ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ كَيْ تَسَعَكُمْ، فَقَدْ جَاءَ اللَّهُ بِالسَّعَةِ، فَكُلُوا، وَادَّخِرُوا، وَائْتَجِرُوا". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: ائْتَجِرُوا: اطْلُبُوا فِيهِ الْأَجْرَ
Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid — naye ni Ibn 'Abdi-Allaah Atw-Twahhaan —, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Maliyh, kutoka kwa Nubayshah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika sisi tulikuwa tumekukatazeni nyama za udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) kuzila zaidi ya siku tatu ili zikutosheni (nyote). Basi Allaah Ameleta wasaa; kwa hiyo kuleni, na wekeni akiba, na tafuteni ujira."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: "I'tajiruw" (tafuteni ujira) maana yake ni: tafuteni ujira (wa Allaah) kwa (nyama) hiyo.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1245
- Hadiyth
- 2001
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَمْرَةَ بِنْتِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ نَهَى عَنْ لُحُومِ الْأَضَاحِيِّ بَعْدَ ثَلَاثٍ، فَلَمَّا كَانَ الْعَامُ الْقَابِلُ وَضَحَّى النَّاسُ، قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنْ كَانَتْ هَذِهِ الْأَضَاحِيُّ لَتَرْفُقُ بِالنَّاسِ، كَانُوا يَدَّخِرُونَ مِنْ لُحُومِهَا وَوَدَكِهَا. قَالَ: "فَمَا يَمْنَعُهُمْ مِنْ ذَلِكَ الْيَوْمَ؟" قُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، أَوَ لَمْ تَنْهَهُمْ عَامَ أَوَّلَ عَنْ أَنْ يَأْكُلُوا لُحُومَهَا فَوْقَ ثَلَاثٍ؟ فَقَالَ: "إِنَّمَا نَهَيْتُ عَنْ ذَلِكَ لِلْحَاضِرَةِ الَّتِي حَضَرَتْهُمْ مِنْ أَهْلِ الْبَادِيَةِ لِيَنُثُّوا لُحُومَهَا فِيهِمْ، فَأَمَّا الْآنَ، فَلْيَأْكُلُوا وَلْيَدَّخِرُوا"
Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa 'Amrah bint 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa amekataza (kula) nyama za udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) baada ya (siku) tatu. Ulipofika mwaka uliofuata, na watu wakachinja udhwhiyah, nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika udhwhiyah hizi zilikuwa zikiwafaa watu (sana); walikuwa wakiweka akiba katika nyama zake na mafuta yake. Akasema: "Basi ni nini kinachowazuia kufanya hivyo leo?" Nikasema: Yaa Nabiyya-Allaah, je, hukuwakataza mwaka uliopita kula nyama zake zaidi ya (siku) tatu? Akasema: "Hakika nilikataza hilo kwa ajili ya kundi la watu wa jangwani lililowafikia (Madiynah), ili wawagawie nyama zake; ama sasa, basi na wale na waweke akiba."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1246
- Hadiyth
- 2002
أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ الْوَلِيدِ الزَّبِيدِيُّ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ، حَدَّثَنِي أَبِي، أَنَّهُ سَمِعَ ثَوْبَانَ مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَنَحْنُ بِمِنًى: "أَصْلِحْ لَنَا مِنْ هَذَا اللَّحْمِ" فَأَصْلَحْتُ لَهُ مِنْهُ، فَلَمْ يَزَلْ يَأْكُلُ مِنْهُ حَتَّى بَلَغْنَا الْمَدِينَةَ
Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, amenisimulia Muhammad bin Al-Waliyd Az-Zubaydiy, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Jubayr bin Nufayr, amenisimulia baba yangu, kwamba alimsikia Thawbaan (رضي الله عنه) mawlaa (mwachwa huru) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia, nasi tukiwa Minaa: "Tutayarishie (kwa kuhifadhi) katika nyama hii." Nikamtayarishia katika nyama hiyo; hakuacha kuila mpaka tukafika Madiynah.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1246
- Hadiyth
- 2003
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَطَاءً، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرًا، يَقُولُ: "إِنْ كُنَّا لَنَتَزَوَّدُ مِنْ مَكَّةَ إِلَى الْمَدِينَةِ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: يَعْنِي: لُحُومَ الْأَضَاحِيِّ
Ametukhabarisha Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, amesema: Nilimsikia 'Atwaa, amesema: Nilimsikia Jaabir (رضي الله عنه) akisema: "Hakika tulikuwa tukichukua masurufu (ya safari) kutoka Makkah hadi Madiynah katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yaani: nyama za udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1247
- Hadiyth
- 2004
7-Mlangoباب في الذبح قبل الإمامMlango Wa Kuhusu Kuchinja Kabla Ya Imaam
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، وَزُبَيْدٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، أَنَّ أَبَا بُرْدَةَ بْنَ نِيَارٍ ضَحَّى قَبْلَ أَنْ يُصَلِّيَ، فَلَمَّا صَلَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، دَعَاهُ فَذَكَرَ لَهُ مَا فَعَلَ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّمَا شَاتُكَ شَاةُ لَحْمٍ". فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، عِنْدِي عَنَاقٌ جَذَعَةٌ مِنْ الْمَعْزِ هِيَ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ شَاتَيْنِ. قَالَ: "فَضَحِّ بِهَا، وَلَا تُجْزِئُ عَنْ أَحَدٍ بَعْدَكَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: قُرِئَ عَلَى مُحَمَّدٍ، عَنْ سُفْيَانَ: وَمَنْ ذَبَحَ بَعْدَ الصَّلَاةِ وَالْإِمَامُ يَخْطُبُ أَجْزَأَهُ
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr na Zubayd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib (رضي الله عنهما), kwamba Abuw Burdah bin Niyaar (رضي الله عنه) alichinja udhwhiyah (wanyama wa kuchinjwa siku ya 'Iyd) yake kabla ya kuswali (Swalaah ya 'Iyd). Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomaliza kuswali, alimwita; akamtajia aliyoyafanya. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Hakika mbuzi wako ni mbuzi wa nyama (tu)." Akasema: Yaa Rasula-Allaah, nina mwana-mbuzi jike aliye jadha'ah (mnyama mchanga wa umri wa karibu mwaka mmoja) katika mbuzi, naye ninampenda zaidi kuliko mbuzi wawili. Akasema: "Basi mchinje kuwa udhwhiyah; wala hatamtosheleza yeyote baada yako."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ilisomwa mbele ya Muhammad [bin Yuwsuf], kutoka kwa Sufyaan: "Na aliyechinja baada ya Swalaah na Imaam anakhutubu, (udhwhiyah yake) imemtosheleza."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1248
- Hadiyth
- 2005
حَدَّثَنَا أَبُو عَلِيٍّ الْحَنَفِيُّ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ بُشَيْرِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ نِيَارٍ، أَنَّ رَجُلًا ذَبَحَ قَبْلَ أَنْ يَنْصَرِفَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَأَمَرَهُ أَنْ يُعِيدَ"
Ametusimulia Abuw 'Aliy Al-Hanafiy, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Bushayr bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Burdah bin Niyaar (رضي الله عنه), kwamba mtu mmoja alichinja kabla Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hajaondoka (kutoka katika Swalaah), "akamwamrisha arudie (kuchinja)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1248
- Hadiyth
- 2006
8-Mlangoباب في الفرع والعتيرةMlango Wa Kuhusu Al-Fara' (Mzao Wa Kwanza Wa Ngamia
Uliokuwa Ukichinjwa Kwa Ajili Ya Masanamu) Na Al-'Atiyrah
(Mnyama Aliyekuwa Akichinjwa Katika Mwezi Wa Rajab)
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا فَرَعَ وَلَا عَتِيرَةَ"
Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna fara' (mzao wa kwanza wa ngamia uliokuwa ukichinjwa kwa ajili ya masanamu) wala 'atiyrah (mnyama aliyekuwa akichinjwa katika mwezi wa Rajab)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1249
- Hadiyth
- 2007
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ يَعْلَى بْنِ عَطَاءٍ، عَنْ وَكِيعِ بْنِ حُدُسٍ، عَنْ أَبِي رَزِينٍ الْعُقَيْلِيِّ: لَقِيطِ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا كُنَّا نَذْبَحُ فِي رَجَبٍ فَمَا تَرَى؟ قَالَ: "لَا بَأْسَ بِذَلِكَ". قَالَ وَكِيعٌ: لَا أَدَعُهُ أَبَدًا
Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Ya'laa bin 'Atwaa, kutoka kwa Wakiy' bin Hudus, kutoka kwa Abuw Raziyn Al-'Uqayliy, Laqiytw bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tulikuwa tukichinja katika (mwezi wa) Rajab; basi unaonaje? Akasema: "Hakuna ubaya kwa hilo." Wakiy' amesema: Sitaliacha kamwe.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1249
- Hadiyth
- 2008
9-Mlangoباب السنة في العقيقةMlango Wa Sunnah Katika 'Aqiyqah (Mnyama Anayechinjwa
Kwa Ajili Ya Mtoto Aliyezaliwa)
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عَطَاءٌ، عَنْ حَبِيبَةَ بِنْتِ مَيْسَرَةَ بْنِ أَبِي خُثَيْمٍ، عَنْ أُمِّ كُرْزٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ فِي الْعَقِيقَةِ: "عَنْ الْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ، وَعَنْ الْجَارِيَةِ شَاةٌ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha 'Atwaa, kutoka kwa Habiybah bint Maysarah bin Abiy Khuthaym, kutoka kwa Ummu Kurz (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema kuhusu 'aqiyqah (mnyama anayechinjwa kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa): "Kwa mtoto wa kiume ni mbuzi wawili wanaolingana, na kwa mtoto wa kike ni mbuzi mmoja."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1250
- Hadiyth
- 2009
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ حَفْصَةَ بِنْتِ سِيرِينَ، عَنْ سَلْمَانَ بْنِ عَامِرٍ الضَّبِّيِّ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "مَعَ الْغُلَامِ عَقِيقَةٌ، فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا، وَأَمِيطُوا عَنْهُ الْأَذَى"
Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Hafswah bint Siyriyn, kutoka kwa Salmaan bin 'Aamir Adhw-Dhwabbiy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Pamoja na mtoto wa kiume kuna 'aqiyqah (mnyama anayechinjwa kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa); basi mwagieni damu kwa ajili yake (kwa kuchinja), na mwondosheeni udhia."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1250
- Hadiyth
- 2010
حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي يَزِيدَ، عَنْ سِبَاعِ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ أُمِّ كُرْزٍ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَنْ الْغُلَامِ شَاتَانِ مِثْلَانِ، وَعَنْ الْجَارِيَةِ شَاةٌ"
Ametusimulia 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa Sibaa' bin Thaabit, kutoka kwa Ummu Kurz (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kwa mtoto wa kiume ni mbuzi wawili walio sawa, na kwa mtoto wa kike ni mbuzi mmoja."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1250
- Hadiyth
- 2011
أَخْبَرَنَا عَفَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَمُرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "كُلُّ غُلَامٍ رَهِينَةٌ بِعَقِيقَتِهِ يُذْبَحُ عَنْهُ يَوْمَ سَابِعِهِ، وَيُحْلَقُ وَيُدَمَّى". وَكَانَ قَتَادَةُ يَصِفُ الدَّمَ، فَيَقُولُ: إِذَا ذُبِحَتْ الْعَقِيقَةُ، تُؤْخَذُ صُوفَةٌ فَيُسْتَقْبَلُ بِهَا أَوْدَاجُ الذَّبِيحَةِ، ثُمَّ تُوضَعُ عَلَى يَافُوخِ الصَّبِيِّ حَتَّى إِذَا سَالَ شَبَهُ الْخَيْطِ، غُسِلَ رَأْسُهُ، ثُمَّ حُلِقَ بَعْدُ. قَالَ عَفَّانُ: حَدَّثَنَا أَبَانُ، بِهَذَا الْحَدِيثِ، قَالَ: وَيُسَمَّى. قَالَ عَبْد اللَّهِ: وَلَا أُرَاهُ وَاجِبًا
Ametukhabarisha 'Affaan bin Muslim, ametusimulia Hammaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Samurah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kila mtoto wa kiume ni rehani kwa 'aqiyqah (mnyama anayechinjwa kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa) yake: huchinjiwa siku yake ya saba, na hunyolewa, na hupakwa damu." Na Qataadah alikuwa akieleza (namna ya kupaka) damu, akisema: Inapochinjwa 'aqiyqah, huchukuliwa kipande cha sufi, kikaelekezwa kwenye mishipa ya shingo ya mnyama aliyechinjwa, kisha kikawekwa juu ya utosi wa mtoto, mpaka (damu) ikitiririka mfano wa uzi, kichwa chake huoshwa, kisha hunyolewa baada ya hapo. 'Affaan amesema: Ametusimulia Abaan Hadiyth hii, na akasema (mahali pa "hupakwa damu"): "na hupewa jina."
'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Wala sioni kuwa ni wajibu.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1251
- Hadiyth
- 2012
10-Mlangoباب في حسن الذبيحةMlango Wa Kuhusu Kuchinja Vizuri
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْأَشْعَثِ الصَّنْعَانِيِّ، عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ، قَالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ اثْنَتَيْنِ: قَالَ: "إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ عَلَيْكُمُ الْإِحْسَانَ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ، فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، ثُمَّ لِيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Ash'ath Asw-Swan'aaniy, kutoka kwa Shaddaad bin Aws (رضي الله عنه), amesema: Nimehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) mambo mawili; amesema: "Hakika Allaah Ameandika juu yenu ihsaan (kufanya kila jambo kwa ubora); basi mnapoua, uweni kwa namna nzuri, na mnapochinja, chinjeni kwa namna nzuri; na mmoja wenu na anoe kisu chake, kisha amstareheshe mnyama wake wa kuchinjwa."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1254
- Hadiyth
- 2013
11-Mlangoباب ما يجوز به الذبحMlango Wa Kinachofaa Kuchinjia
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ: أَنَّ امْرَأَةً كَانَتْ تَرْعَى لِآلِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ غَنَمًا بِسَلْعٍ، فَخَافَتْ عَلَى شَاةٍ مِنْهَا أَنْ تَمُوتَ، فَأَخَذَتْ حَجَرًا فَذَبَحَتْهَا بِهِ، وَإِنَّ ذَلِكَ ذُكِرَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَأَمَرَهُمْ بِأَكْلِهَا"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba mwanamke mmoja alikuwa akiwachunga mbuzi na kondoo wa jamaa wa Ka'b bin Maalik (رضي الله عنه) huko Sal' (mlima ulio Madiynah). Akahofia mbuzi mmoja miongoni mwao asije akafa; akachukua jiwe, akamchinja kwalo. Na hilo likatajwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), "akawaamrisha wamle."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1255
- Hadiyth
- 2014
12-Mlangoباب في ذبيحة المتردي في البئرMlango Wa Kuhusu Kumchinja (Mnyama) Aliyeanguka Kisimani
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، وَعُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، وَعَفَّانُ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي الْعُشَرَاءِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَمَا تَكُونُ الذَّكَاةُ إِلَّا فِي الْحَلْقِ وَاللَّبَّةِ؟ فَقَالَ: "لَوْ طَعَنْتَ فِي فَخِذِهَا، لَأَجْزَأَ عَنْكَ". قَالَ حَمَّادٌ: حَمَلْنَاهُ عَلَى الْمُتَرَدِّي
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, na 'Uthmaan bin 'Umar, na 'Affaan, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Abul-'Usharaa, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, je, kuchinja (kisheria) hakuwi isipokuwa katika koo na sehemu ya juu ya kifua? Akasema: "Lau ungemchoma katika paja lake, ingekutosheleza." Hammaad amesema: Tumelichukulia (hilo) kuwa ni kwa (mnyama) aliyeanguka (kisimani).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1256
- Hadiyth
- 2015
13-Mlangoباب النهي عن مثلة الحيوانMlango Wa Katazo La Kumtesa Mnyama Kwa Kumkatakata Viungo
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنِي الْمِنْهَالُ بْنُ عَمْرٍو، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ، يَقُولُ: خَرَجْتُ مَعَ ابْنِ عُمَرَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ، فَإِذَا بِغِلْمَةٍ يَرْمُونَ دَجَاجَةً، فَقَالَ ابْنُ عُمَرَ: مَنْ فَعَلَ هَذَا؟ فَتَفَرَّقُوا. فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "لَعَنَ مَنْ مَثَّلَ بِالْحَيَوَانِ"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, amenisimulia Al-Minhaal bin 'Amr, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin Jubayr akisema: Nilitoka pamoja na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) katika njia moja miongoni mwa njia za Madiynah; ghafla tukawakuta vijana wakimtupia (mishale) kuku. Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akasema: Ni nani aliyefanya hivi? Wakatawanyika. Akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alimlaani mwenye kumtesa mnyama kwa kumkatakata viungo."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1257
- Hadiyth
- 2016
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ جَعْفَرٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ بُكَيْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْأَشَجِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ تِعْلَى، عَنْ أَبِي أَيُّوبَ الْأَنْصَارِيِّ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ صَبْرِ الدَّابَّةِ". قَالَ أَبُو أَيُّوبَ: لَوْ كَانَتْ دَجَاجَةً مَا صَبَرْتُهَا
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa 'Abdul-Hamiyd bin Ja'far, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Bukayr bin 'Abdi-Allaah bin Al-Ashajj, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Ubayd bin Ti'laa, kutoka kwa Abuw Ayyuwb Al-Answaariy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kumzuia mnyama akiwa hai ili alengwe (mpaka afe)." Abuw Ayyuwb (رضي الله عنه) amesema: Lau angekuwa ni kuku, nisingemzuia (hivyo).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1257
- Hadiyth
- 2017
حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ "نَهَى عَنْ الْمُجَثَّمَةِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: الْمُجَثَّمَةُ: الْمَصْبُورَةُ
Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaad, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah "alikataza al-mujath-thamah (mnyama aliyefungwa akalengwa mpaka afe)."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Al-mujath-thamah ni (mnyama) aliyezuiwa akiwa hai (ili alengwe).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1258
- Hadiyth
- 2018
14-Mlangoباب اللحم يوجد فلا يدرى أذكر اسم الله عليه أم لاMlango Wa Nyama Inayopatikana Na Haijulikani
Kama Limetajwa Jina La Allaah Juu Yake Au Hapana
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحِيمِ هُوَ ابْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ الْمُؤْمِنِينَ، أَنَّ قَوْمًا قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ قَوْمًا يَأْتُونَا بِاللَّحْمِ لَا نَدْرِي أَذُكِرَ اسْمُ اللَّهِ عَلَيْهِ أَمْ لَا؟ فَقَالَ: "سَمُّوا أَنْتُمْ وَكُلُوا" وَكَانُوا حَدِيثَ عَهْدٍ بِجَاهِلِيَّةٍ
Ametukhabarisha Muhammad bin Sa'iyd, ametusimulia 'Abdur-Rahiym — naye ni Ibn Sulaymaan —, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah Mama wa Waumini (رضي الله عنها), kwamba watu fulani walisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika watu fulani wanatuletea nyama, hatujui kama limetajwa Jina la Allaah juu yake au hapana? Akasema: "Litajeni nyinyi (Jina la Allaah), na kuleni." Na walikuwa wapya katika kuachana na Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam).
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1258
- Hadiyth
- 2019
15-Mlangoباب في البهيمة إذا ندتMlango Wa Kuhusu Mnyama Anapokimbia (Akashindikana)
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبَايَةَ بْنِ رِفَاعَةَ بْنِ رَافِعٍ، عَنْ جَدِّهِ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ: أَنَّ بَعِيرًا نَدَّ وَلَيْسَ فِي الْقَوْمِ إِلَّا خَيْلٌ يَسِيرَةٌ، فَرَمَاهُ رَجُلٌ بِسَهْمٍ، فَحَبَسَهُ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ لِهَذِهِ الْبَهَائِمِ أَوَابِدَ كَأَوَابِدِ الْوَحْشِ، فَمَا غَلَبَكُمْ مِنْهَا، فَاصْنَعُوا بِهِ هَكَذَا"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abaayah bin Rifaa'ah bin Raafi', kutoka kwa babu yake Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), kwamba ngamia mmoja alikimbia, na watu hawakuwa na farasi isipokuwa wachache. Mtu mmoja akampiga mshale, akamzuia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Hakika wanyama hawa wana (tabia ya) kukimbia na kuwa pori kama kukimbia kwa wanyama wa mwituni; basi yeyote atakayewashinda miongoni mwao, mfanyieni hivi."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1259
- Hadiyth
- 2020
16-Mlangoباب من قتل شيئا من الدواب عبثاMlango Wa Aliyeua Kitu Katika Wanyama Kwa Mchezo
حَدَّثَنَا أَبُو مَعْمَرٍ إِسْمَاعِيلُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو هُوَ ابْنُ دِينَارٍ، عَنْ صُهَيْبٍ مَوْلَى ابْنِ عَامِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرٍو، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ قَتَلَ عُصْفُورًا بِغَيْرِ حَقِّهِ، سَأَلَهُ اللَّهُ عَنْهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ". قِيلَ: وَمَا حَقُّهُ؟ قَالَ: "أَنْ تَذْبَحَهُ فَتَأْكُلَهُ"
Ametusimulia Abuw Ma'mar Ismaa'iyl bin Ibraahiym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr — naye ni Ibn Diynaar —, kutoka kwa Swuhayb mawlaa (mwachwa huru) wa Ibn 'Aamir, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayemuua shomoro bila haki yake, Allaah Atamuuliza kuhusu yeye Siku ya Qiyaamah." Ikasemwa: Na ni ipi haki yake? Akasema: "Umchinje, kisha umle."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1259
- Hadiyth
- 2021
17-Mlangoباب في ذكاة الجنين ذكاة أمهMlango Wa Kuhusu Kwamba Kuchinjwa
Kwa Kijusi Ni Kuchinjwa Kwa Mama Yake
أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَتَّابُ بْنُ بَشِيرٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي زِيَادٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "ذَكَاةُ الْجَنِينِ ذَكَاةُ أُمِّهِ". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: يُؤْكَلُ؟ قَالَ: نَعَمْ
Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia 'Attaab bin Bashiyr, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Ziyaad, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kuchinjwa kwa kijusi (kilichomo tumboni) ni kuchinjwa kwa mama yake."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, (kijusi hicho) huliwa? Akasema: Ndiyo.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1260
- Hadiyth
- 2022
18-Mlangoباب ما لا يؤكل من السباعMlango Wa Wasioliwa Miongoni Mwa Wanyama Mwitu
أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ أَبِي إِدْرِيسَ الْخَوْلَانِيِّ، عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الْخُشَنِيِّ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْلِ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنَ السَّبُعِ"
Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abuw Idriys Al-Khawlaaniy, kutoka kwa Abuw Tha'labah Al-Khushaniy (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kula kila mwenye chonge miongoni mwa wanyama mwitu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1260
- Hadiyth
- 2023
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو أُوَيْسٍ ابْنُ عَمِّ مَالِكِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي إِدْرِيسَ الْخَوْلَانِيِّ، عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الْخُشَنِيِّ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْخَطْفَةِ، وَالْمُجَثَّمَةِ، وَالنُّهْبَةِ، وَعَنْ أَكْلِ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنْ السِّبَاعِ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Abuw Uways, mwana wa ami yake Maalik bin Anas, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Idriys Al-Khawlaaniy, kutoka kwa Abuw Tha'labah Al-Khushaniy (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza al-khatwfah (kiungo kinachonyakuliwa na mnyama mwitu kutoka kwa mnyama aliye hai), na al-mujath-thamah (mnyama anayefungwa akalengwa kwa mishale mpaka afe), na kunyang'anya nyara, na kula kila mwenye chonge miongoni mwa wanyama mwitu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1261
- Hadiyth
- 2024
أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ مَيْمُونِ بْنِ مِهْرَانَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْلِ كُلِّ ذِي نَابٍ مِنْ السِّبَاعِ، وَكُلِّ ذِي مِخْلَبٍ مِنْ الطَّيْرِ"
Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Maymuwn bin Mihraan, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kula kila mwenye chonge miongoni mwa wanyama mwitu, na kila mwenye makucha miongoni mwa ndege."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1261
- Hadiyth
- 2025
19-Mlangoباب النهي عن لبس جلود السباعMlango Wa Katazo La Kuvaa Ngozi Za Wanyama Mwitu
أَخْبَرَنَا يَعْمَرُ بْنُ بِشْرٍ، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَبِي الْمَلِيحِ، عَنْ أَبِيهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ جُلُودِ السِّبَاعِ أَنْ تُفْتَرَشَ".
Ametukhabarisha Ya'mar bin Bishr, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Abul-Maliyh, kutoka kwa baba yake [Usaamah bin 'Umayr (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza ngozi za wanyama mwitu kutandikwa."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1262
- Hadiyth
- 2026
أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَبِي الْمَلِيحِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَهُ
Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Abul-Maliyh, kutoka kwa baba yake [Usaamah bin 'Umayr (رضي الله عنه)], kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1263
- Hadiyth
- 2027
20-Mlangoباب الاستمتاع بجلود الميتةMlango Wa Kunufaika Na Ngozi Za Nyamafu
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ وَعْلَةَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ عَنْ الْأَسْقِيَةِ، فَقَالَ: مَا أَدْرِي مَا أَقُولُ لَكَ، غَيْرَ أَنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "أَيُّمَا إِهَابٍ دُبِغَ فَقَدْ طَهُرَ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Wa'lah, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu viriba (vya ngozi), akasema: Sijui nikuambie nini, isipokuwa mimi nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Ngozi yoyote ikisindikwa, basi imetwaharika."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1263
- Hadiyth
- 2028
حَدَّثَنَا يَعْلَى، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ الْقَعْقَاعِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ وَعْلَةَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ عَنْ جُلُودِ الْمَيْتَةِ، فَقَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "دِبَاغُهَا طَهُورُهَا". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ: تَقُولُ بِهَذَا؟ قَالَ: نَعَمْ، إِذَا كَانَ يُؤْكَلُ لَحْمُهُ
Ametusimulia Ya'laa, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Al-Qa'qaa' bin Hakiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Wa'lah, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu ngozi za nyamafu, akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kusindikwa kwake ndiko kutwaharika kwake."
Abuw Muhammad 'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unashika kauli hii? Akasema: Ndiyo, ikiwa (mnyama huyo) nyama yake inaliwa.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1263
- Hadiyth
- 2029
حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ قُسَيْطٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ ثَوْبَانَ، عَنْ أُمِّهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُسْتَمْتَعَ بِجُلُودِ الْمَيْتَةِ إِذَا دُبِغَتْ"
Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Yaziyd bin Qusayt, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Thawbaan, kutoka kwa mama yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrisha kunufaika na ngozi za nyamafu zinaposindikwa."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1263
- Hadiyth
- 2030
حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: مَاتَتْ شَاةٌ لِمَيْمُونَةَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْ اسْتَمْتَعْتُمْ بِإِهَابِهَا؟" قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّهَا مَيْتَةٌ، قَالَ: "إِنَّمَا حُرِّمَ أَكْلُهَا".
Ametusimulia Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Mbuzi wa Maymuwnah (رضي الله عنها) alikufa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Lau mngenufaika na ngozi yake?" Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika yeye ni nyamafu. Akasema: "Hakika kilichoharamishwa ni kuliwa kwake tu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1264
- Hadiyth
- 2031
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُصَفَّى، حَدَّثَنَا بَقِيَّةُ، عَنْ الزُّبَيْدِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَ هَذَا الْحَدِيثِ. قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: مَا تَقُولُ فِي الثَّعَالِبِ إِذَا دُبِغَتْ؟ قَالَ: أَكْرَهُهَا
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Muswaffaa, ametusimulia Baqiyyah, kutoka kwa Az-Zubaydiy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wa Hadiyth hii.
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Unasemaje kuhusu (ngozi za) mbweha zinaposindikwa? Akasema: Ninazichukia.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1265
- Hadiyth
- 2032
21-Mlangoباب في لحوم الحمر الأهليةMlango Wa Kuhusu Nyama Za Punda Wa Kufugwa
أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ الْحَسَنِ، وَعَبْدِ اللَّهِ ابْنَيْ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِمَا، عَنْ عَلِيٍّ، أَنَّ عَلِيًّا قَالَ لِابْنِ عَبَّاسٍ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ مُتْعَةِ النِّسَاءِ يَوْمَ خَيْبَرَ، وَعَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الْإِنْسِيَّةِ"
Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Al-Hasan na 'Abdu-Allaah, wana wawili wa Muhammad, kutoka kwa baba yao, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba 'Aliy (رضي الله عنه) alimwambia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mut'ah (ndoa ya muda) ya wanawake siku ya Khaybar, na nyama za punda wa kufugwa."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1265
- Hadiyth
- 2033
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: قَامَ رَجُلٌ يَوْمَ خَيْبَرَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أُكِلَتْ الْحُمُرُ أَوْ أُفْنِيَتِ الْحُمُرُ، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أُفْنِيَتِ الْحُمُرُ أَوْ أُكِلَتْ الْحُمُرُ، "فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا فَنَادَى إِنَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ يَنْهَيَانِكُمْ عَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ، فَإِنَّهَا رِجْسٌ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alisimama siku ya Khaybar, akasema: Yaa Rasula-Allaah, punda wameliwa — au: punda wamemalizwa —. Kisha akasema: Yaa Rasula-Allaah, punda wamemalizwa — au: punda wameliwa —. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha mtu mmoja, akanadi: "Hakika Allaah na Rasuli Wake wanakukatazeni nyama za punda, kwani hizo ni vichafu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1265
- Hadiyth
- 2034
22-Mlangoباب في أكل لحوم الخيلMlango Wa Kuhusu Kula Nyama Za Farasi
حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ فَاطِمَةَ بِنْتِ الْمُنْذِرِ، عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ أَبِي بَكْرٍ، قَالَتْ: "أَكَلْنَا لَحْمَ فَرَسٍ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالْمَدِينَةِ"
Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa Faatwimah bint Al-Mundhir, kutoka kwa Asmaa bint Abiy Bakr (رضي الله عنها), amesema: "Tulikula nyama ya farasi katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) huko Madiynah."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1267
- Hadiyth
- 2035
أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَلِيٍّ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمَ خَيْبَرَ عَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الْأَهْلِيَّةِ، وَأَذِنَ فِي لُحُومِ الْخَيْلِ"
Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Muhammad bin 'Aliy, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza siku ya Khaybar nyama za punda wa kufugwa, na akatoa idhini kuhusu nyama za farasi."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1267
- Hadiyth
- 2036
23-Mlangoباب النهي عن النهبةMlango Wa Katazo La Kunyang'anya Nyara
أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَأَبِي سَلَمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا يَنْتَهِبُ نُهْبَةً ذَاتَ شَرَفٍ يَرْفَعُ الْمُؤْمِنُونَ فِيهَا أَبْصَارَهُمْ وَهُوَ حِينَ يَنْتَهِبُهَا مُؤْمِنٌ"
Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "(Mtu) hanyang'anyi nyara yenye thamani kubwa ambayo Waumini wanainulia macho yao kuitazama, naye wakati anapoinyang'anya ni Muumini."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1267
- Hadiyth
- 2037
حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرِ بْنِ حَازِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ يَعْلَى بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِي لَبِيدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ النُّهْبَةِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: هَذَا فِي الْغَزْوِ إِذَا غَنِمُوا قَبْلَ أَنْ يُقْسَمَ
Ametusimulia Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia Wahb bin Jariyr bin Haazim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ya'laa bin Hakiym, kutoka kwa Abuw Labiyd, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Samurah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kunyang'anya nyara."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Hili ni katika vita, wanapopata ngawira kabla haijagawanywa.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1268
- Hadiyth
- 2038
24-Mlangoباب في أكل الميتة للمضطرMlango Wa Kuhusu Kula Nyamafu Kwa Aliyefikwa Na Dharura
حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ حَسَّانَ بْنِ عَطِيَّةَ، عَنْ أَبِي وَاقِدٍ، قَالَ: قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا بِأَرْضٍ تَكُونُ بِهَا الْمَخْمَصَةُ، فَمَا يَحِلُّ لَنَا مِنْ الْمَيْتَةِ؟ قَالَ: "إِذَا لَمْ تَصْطَبِحُوا، وَلَمْ تَغْتَبِقُوا، وَلَمْ تَخْتَفِئُوا بَقْلًا فَشَأْنُكُمْ بِهَا". قَالَ: النَّاسُ يَقُولُونَ بِالْحَاءِ، وَهَذَا قَالَ بِالْخَاءِ
Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Hassaan bin 'Atwiyyah, kutoka kwa Abuw Waaqid (رضي الله عنه), amesema: Tulisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tuko katika ardhi ambayo njaa kali hutokea humo; basi ni kipi kinachotuhalalikia katika nyamafu? Akasema: "Msipopata kinywaji cha asubuhi, wala msipopata kinywaji cha jioni, wala msipong'oa mboga, basi ni shauri lenu nayo." Akasema: Watu husema (neno hilo) kwa herufi ح, na huyu amesema kwa herufi خ.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1269
- Hadiyth
- 2039
25-Mlangoباب في الحالب يجهد الحلبMlango Wa Kuhusu Mkamaji Anayejitahidi Sana Katika Kukama
أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ يَعْقُوبَ بْنِ بَحِيرٍ، عَنْ ضِرَارِ بْنِ الْأَزْوَرِ، قَالَ: أَهْدَيْتُ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِقْحَةً، فَأَمَرَنِي أَنْ أَحْلُبَهَا، فَحَلَبْتُهَا، فَجَهَدْتُ فِي حَلْبِهَا، فَقَالَ "دَعْ دَاعِيَ اللَّبَنِ"
Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ya'quwb bin Bahiyr, kutoka kwa Dhwiraar bin Al-Azwar (رضي الله عنه), amesema: Nilimpa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zawadi ya ngamia jike mwenye maziwa. Akaniamrisha nimkame; nikamkama, nikajitahidi sana katika kumkama. Akasema: "Acha kinachoita maziwa (baki kidogo kiweleni)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1270
- Hadiyth
- 2040
26-Mlangoباب النهي عن قتل الضفدع والنحلةMlango Wa Katazo La Kuua Chura Na Nyuki
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ خَالِدٍ الْقَارِظِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ قَتْلِ الضِّفْدَعِ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Sa'iyd bin Khaalid Al-Qaaridhwiy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin 'Uthmaan (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kumuua chura."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1270
- Hadiyth
- 2041
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّزَّاقِ، أَنْبَأَنَا مَعْمَرٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ قَتْلِ أَرْبَعَةٍ مِنْ الدَّوَابِّ: النَّمْلَةِ، وَالنَّحْلَةِ، وَالْهُدْهُدِ، وَالصُّرَدِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yahyaa, ametusimulia 'Abdur-Razzaaq, ametupa khabari Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuua (aina) nne za wanyama: sisimizi, na nyuki, na al-hud-hud (ndege hudihudi), na asw-swurad (aina ya ndege mwenye kichwa kikubwa anayewinda wadudu na ndege wadogo)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1270
- Hadiyth
- 2042
27-Mlangoباب في قتل الوزغMlango Wa Kuhusu Kuua Mjusi
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ شَيْبَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ عَنْ أُمِّ شَرِيكٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "أَمَرَ بِقَتْلِ الْأَوْزَاغِ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Abdul-Hamiyd bin Jubayr bin Shaybah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Ummu Shariyk (رضي الله عنها), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "aliamrisha kuuawa mijusi."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1271
- Hadiyth
- 2043
28-Mlangoباب في الجلالة وما جاء فيه من النهيMlango Wa Kuhusu Al-Jallaalah (Mnyama Anayekula Kinyesi)
Na Katazo Lililopokewa Juu Yake
حَدَّثَنَا أَبُو زَيْدٍ: سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ الدَّسْتَوَائِيُّ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ الْمُجَثَّمَةِ، وَعَنْ لَبَنِ الْجَلَّالَةِ، وَأَنْ يُشْرَبَ مِنْ فِي السِّقَاءِ"
Ametusimulia Abuw Zayd Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Hishaam Ad-Dastuwaaiy, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza al-mujath-thamah (mnyama anayefungwa akalengwa kwa mishale mpaka afe), na maziwa ya al-jallaalah (mnyama anayekula kinyesi), na kunywa kutoka mdomoni mwa kiriba."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 6
- Ukurasa
- 1272
- Hadiyth
- 2044