ومن كتاب الصيد
1-Mlangoباب التسمية عند إرسال الكلب، وصيد الكلابMlango Wa Kutaja Jina La Allaah
Wakati Wa Kumtuma Mbwa, Na Mawindo Ya Mbwa
أَخْبَرَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، ثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ، قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ صَيْدِ الْكَلْبِ، فَقَالَ: "مَا أَمْسَكَ عَلَيْكَ كَلْبِكَ فَكُلْ، فَإِنَّ أَخْذَهُ ذَكَاتُهُ، وَإِنْ وَجَدْتَ مَعَهُ كَلْبًا فَخَشِيتَ أَنْ يَكُونَ قَدْ أَخَذَهُ مَعَهُ، وَقَدْ قَتَلَهُ، فَلَا تَأْكُلْهُ، فَإِنَّكَ إِنَّمَا ذَكَرْتَ اسْمَ اللَّهِ عَلَى كَلْبِكَ، وَلَمْ تَذْكُرْهُ عَلَى غَيْرِهِ".
Ametukhabarisha Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه), amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mawindo ya mbwa. Akasema: "Alichokukamatia mbwa wako, basi kula; kwani kukamata kwake ndiko kuchinjwa kwake kihalali. Na ukimkuta pamoja naye mbwa (mwingine), ukahofia kwamba huenda (mbwa huyo) amemkamata pamoja naye, na amemuua, basi usimle; kwani hakika wewe umetaja Jina la Allaah juu ya mbwa wako tu, wala hukulitaja juu ya (mbwa) mwingine."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1273
- Hadiyth
- 2045
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ حَاتِمٍ، قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ صَيْدِ الْمِعْرَاضِ، فَذَكَرَ مِثْلَهُ
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه), amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mawindo ya mi'raadh (fimbo nzito au mshale usio na manyoya, unaopiga kwa ncha yake au kwa ubapa wake); akataja mfano wake.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1273
- Hadiyth
- 2046
2-Mlangoباب في اقتناء كلب الصيد، والماشيةMlango Wa Kuhusu Kufuga Mbwa Wa Kuwinda Na Wa Mifugo
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ اقْتَنَى كَلْبًا إِلَّا كَلْبَ صَيْدٍ أَوْ مَاشِيَةٍ، نَقَصَ مِنْ عَمَلِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطَانِ"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayefuga mbwa, isipokuwa mbwa wa kuwinda au wa (kulinda) mifugo, hupunguka katika amali yake kila siku qiyraatw (kipimo cha malipo) mbili."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1274
- Hadiyth
- 2047
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ خُصَيْفَةَ، عَنْ السَّائِبِ بْنِ يَزِيدَ، أَنَّهُ سَمِعَ سُفْيَانَ بْنَ أَبِي زُهَيْرٍ يُحَدِّثُ نَاسًا مَعَهُ عِنْدَ بَاب الْمَسْجِدِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "مَنْ اقْتَنَى كَلْبًا لَا يُغْنِي عَنْهُ زَرْعًا وَلَا ضَرْعًا، نَقَصَ مِنْ عَمَلِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطٌ". قَالُوا: أَنْتَ سَمِعْتَ هَذَا مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ قَالَ: إِي وَرَبِّ هَذَا الْمَسْجِدِ
Ametusimulia Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Yaziyd bin Khuswayfah, kutoka kwa As-Saaib bin Yaziyd (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Sufyaan bin Abiy Zuhayr (رضي الله عنه) akiwasimulia watu waliokuwa pamoja naye kwenye mlango wa Msikiti, amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayefuga mbwa asiyemfaa kwa (kulinda) mimea wala (kulinda) wanyama wa maziwa, hupunguka katika amali yake kila siku qiyraatw (kipimo cha malipo) moja." Wakasema: Je, wewe umesikia haya kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Ndiyo, naapa kwa Rabb wa Msikiti huu.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1274
- Hadiyth
- 2048
أَخْبَرَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي التَّيَّاحِ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِقَتْلِ الْكِلَابِ، ثُمَّ قَالَ: "مَالِي وَلِلْكِلَابِ؟"، ثُمَّ رَخَّصَ فِي كَلْبِ الزَّرْعِ وَكَلْبِ الصَّيْدِ
Ametukhabarisha Wahb bin Jariyr, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abut-Tayyaah, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrisha mbwa wauawe, kisha akasema: "Nina nini mimi na mbwa?" Kisha akaruhusu (kufuga) mbwa wa (kulinda) mimea na mbwa wa kuwinda.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1275
- Hadiyth
- 2049
3-Mlangoباب في قتل الكلابMlango Wa Kuhusu Kuua Mbwa
أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَتْلِ الْكِلَابِ"
Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamrisha mbwa wauawe."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1276
- Hadiyth
- 2050
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا عَوْفٌ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْلَا أَنَّ الْكِلَابَ أُمَّةٌ مِنْ الْأُمَمِ، لَأَمَرْتُ بِقَتْلِهَا كُلِّهَا، وَلَكِنْ اقْتُلُوا مِنْهَا كُلَّ أَسْوَدَ بَهِيمٍ". قَالَ سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ: الْبَهِيمُ: الْأَسْوَدُ كُلُّهُ
Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, ametusimulia 'Awf, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Lau si kwamba mbwa ni umati miongoni mwa nyumati, ningeamrisha wauawe wote; lakini ueni miongoni mwao kila mweusi bahiym (mweusi mtupu)." Sa'iyd bin 'Aamir amesema: Al-bahiym ni: aliye mweusi mwili wote.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1276
- Hadiyth
- 2051
4-Mlangoباب في صيد المعراضMlango Wa Kuhusu Mawindo Ya Mi'raadh
أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي السَّفَرِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ، قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْمِعْرَاضِ، فَقَالَ: "إِذَا أَصَابَ بِحَدِّهِ، فَكُلْ، وَإِذَا أَصَابَ بِعَرْضِهِ فَقَتَلَ، فَإِنَّهُ وَقِيذٌ، فَلَا تَأْكُلْ"
Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abis-Safar, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Nilimsikia 'Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) akisema: Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mi'raadh (fimbo nzito au mshale usio na manyoya, unaopiga kwa ncha yake au kwa ubapa wake). Akasema: "Ukimpata (mnyama) kwa ncha yake, basi kula; na ukimpata kwa ubapa wake ukamuua, basi hakika yeye ni (mnyama) aliyepigwa akafa, basi usile."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1277
- Hadiyth
- 2052
5-Mlangoباب في أكل الجرادMlango Wa Kuhusu Kula Nzige
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِي يَعْفُورٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى، قَالَ: "غَزَوْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَبْعَ غَزَوَاتٍ نَأْكُلُ الْجَرَادَ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuw Ya'fuwr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Awfaa (رضي الله عنهما), amesema: "Tulipigana vita pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) vita saba, tukila nzige."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1277
- Hadiyth
- 2053
6-Mlangoباب في صيد البحرMlango Wa Kuhusu Mawindo Ya Bahari
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، قِرَاءَةً، عَنْ مَالِكٍ، عَنْ صَفْوَانَ بْنِ سُلَيْمٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ سَلَمَةَ مِنْ آلِ الْأَزْرَقِ، أَنَّ الْمُغِيرَةَ بْنَ أَبِي بُرْدَةَ وَهُوَ رَجُلٌ مِنْ بَنِي عَبْدِ الدَّارِ أَخْبَرَهُ أَنَّهُ، سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: إِنَّا نَرْكَبُ الْبَحْرَ وَنَحْمِلُ مَعَنَا الْقَلِيلَ مِنْ الْمَاءِ، فَإِنْ تَوَضَّأْنَا بِهِ، عَطِشْنَا، أَفَنَتَوَضَّأُ مِنْ مَاءِ الْبَحْرِ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هُوَ الطَّهُورُ مَاؤُهُ، الْحِلُّ مَيْتَتُهُ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak — kwa kusomewa (yeye) —, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Swafwaan bin Sulaym, kutoka kwa Sa'iyd bin Salamah — wa jamaa wa Al-Azraq —, kwamba Al-Mughiyrah bin Abiy Burdah — naye ni mtu wa Banuw 'Abdid-Daar — alimkhabarisha kwamba yeye alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika sisi tunapanda bahari (kusafiri), na tunabeba pamoja nasi maji kidogo; tukitawadha kwayo tunapata kiu. Je, tutawadhe kwa maji ya bahari? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hiyo (bahari) maji yake ni twahara yenye kutwaharisha, mfu wake (kiumbe chake kilichokufa) ni halaal."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1278
- Hadiyth
- 2054
أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَمْرٍو يَعْنِي: ابْنَ دِينَارٍ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "بَعَثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي ثَلَاثِ مِئَةٍ، فَأَصَابَنَا جُوعٌ حَتَّى أَتَيْنَا الْبَحْرَ وَقَدْ قَذَفَ دَابَّةً، فَأَكَلْنَا مِنْهَا حَتَّى ثَابَتْ أَجْسَامُنَا، فَأَخَذَ أَبُو عُبَيْدَةَ ضِلْعًا مِنْ أَضْلَاعِهَا فَوَضَعَهُ، ثُمَّ حَمَلَ أَطْوَلَ رَجُلٍ فِي الْجَيْشِ عَلَى أَعْظَمِ بَعِيرٍ فِي الْجَيْشِ فَمَرَّ تَحْتَهُ، هَذَا مَعْنَاهُ"
Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Amr — yaani: Ibn Diynaar —, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitutuma (tukiwa watu) mia tatu. Tukapatwa na njaa mpaka tukaifikia bahari, nayo ilikuwa imetupa (pwani) mnyama. Tukala katika (nyama ya) mnyama huyo mpaka miili yetu ikarejea (katika hali yake). Kisha Abuw 'Ubaydah (رضي الله عنه) akachukua ubavu mmoja katika mbavu zake akauweka, kisha akampandisha mtu mrefu zaidi katika jeshi juu ya ngamia mkubwa zaidi katika jeshi, naye akapita chini yake. Hii ndiyo maana yake."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1278
- Hadiyth
- 2055
7-Mlangoباب في أكل الأرنبMlango Wa Kuhusu Kula Sungura
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: هِشَامُ بْنُ زَيْدِ بْنِ أَنَسٍ أَخْبَرَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ، يَقُولُ: أَنْفَجْنَا أَرْنَبًا وَنَحْنُ بِمَرِّ الظَّهْرَانِ، فَسَعَى الْقَوْمُ فَلَغِبُوا، فَأَخَذْتُهَا وَجِئْتُ بِهَا إِلَى أَبِي طَلْحَةَ، فَذَبَحَهَا وَبَعَثَ بِوَرِكَيْهَا أَوْ فَخِذَيْهَا، شَكَّ شُعْبَةُ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَقَبِلَهَا"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, amesema: Hishaam bin Zayd bin Anas amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia Anas bin Maalik (رضي الله عنه) akisema: Tulimshtua sungura (akatoka mafichoni mwake) nasi tukiwa Marr Adhw-Dhwahraan. Watu wakamkimbiza mpaka wakachoka. Nikamkamata, nikaja naye kwa Abuw Twalhah (رضي الله عنه); akamchinja, na akapeleka viuno vyake viwili — au mapaja yake mawili; Shu'bah ametia shaka — kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), "akaikubali (zawadi hiyo)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1279
- Hadiyth
- 2056
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا دَاوُدُ بْنُ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ صَفْوَانَ، أَنَّهُ مَرَّ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِأَرْنَبَيْنِ مُعَلِّقُهُمَا، فَقَالَ: " يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي دَخَلْتُ غَنَمَ أَهْلِي فَاصْطَدْتُ هَذَيْنِ الْأَرْنَبَيْنِ، فَلَمْ أَجِدْ حَدِيدَةً أُذَكِّيهِمَا بِهَا، فَذَكَّيْتُهُمَا بِمَرْوَةٍ، أَفَآكُلُ؟ قَالَ: " نَعَمْ "
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Muhammad bin Swafwaan (رضي الله عنه), kwamba alipita kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiwa amewaning'iniza sungura wawili, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi niliingia kwa mbuzi na kondoo wa jamaa zangu, nikawawinda sungura hawa wawili, nikakosa chuma cha kuwachinja kihalali, nikawachinja kwa jiwe lenye makali. Je, nile? Akasema: "Ndiyo."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1280
- Hadiyth
- 2057
8-Mlangoباب في أكل الضبMlango Wa Kuhusu Kula Dhwabb
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الضَّبِّ، فَقَالَ: "لَسْتُ بِآكِلِهِ وَلَا مُحَرِّمِهِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu dhwabb (mnyama wa jangwani anayefanana na kenge). Akasema: "Mimi si mwenye kumla, wala si mwenye kumharamisha."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1281
- Hadiyth
- 2058
أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا الْحَكَمُ، قَالَ: سَمِعْتُ زَيْدَ بْنَ وَهْبٍ يُحَدِّثُ، عَنْ الْبَرَاءِ بْنِ عَازِبٍ، عَنْ ثَابِتِ بْنِ وَدِيعَةَ، قَالَ: أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِضَبٍّ، فَقَالَ: "أُمَّةٌ مُسِخَتْ وَاللَّهُ أَعْلَمُ"
Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Al-Hakam, amesema: Nilimsikia Zayd bin Wahb akisimulia kutoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib (رضي الله عنهما), kutoka kwa Thaabit bin Wadiy'ah (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa dhwabb (mnyama wa jangwani anayefanana na kenge), akasema: "Ni umati uliogeuzwa umbo; na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1281
- Hadiyth
- 2059
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، أَنَّهُ قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو أُمَامَةَ بْنُ سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ الْأَنْصَارِيُّ، أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَبَّاسٍ أَخْبَرَهُ، أَنَّ خَالِدَ بْنَ الْوَلِيدِ الَّذِي يُقَالُ لَهُ سَيْفُ اللَّهِ أَخْبَرَهُ، أَنَّهُ دَخَلَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى مَيْمُونَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهِيَ خَالَتُهُ وَخَالَةُ ابْنِ عَبَّاسٍ، فَوَجَدَ عِنْدَهَا ضَبًّا مَحْنُوذًا قَدِمَتْ بِهِ أُخْتُهَا حُفَيْدَةُ بِنْتُ الْحَارِثِ مِنْ نَجْدٍ، فَقَدَّمَتْ الضَّبَّ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ قَلَّمَا يُقَدِّمُ يَدَهُ لِطَعَامٍ حَتَّى يُحَدَّثَ بِهِ وَيُسَمَّى لَهُ، فَأَهْوَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ إِلَى الضَّبِّ، فَقَالَتْ امْرَأَةٌ مِنْ نِسْوَةِ الْحُضُورِ: أَخْبِرْنَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا قَدَّمْتُنَّ لَهُ. قُلْنَ: هَذَا الضَّبُّ، فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ، فَقَالَ خَالِدُ بْنُ الْوَلِيدِ: أَتُحَرِّمُ الضَّبَّ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: "لَا، وَلَكِنَّهُ لَمْ يَكُنْ بِأَرْضِ قَوْمِي، فَأَجِدُنِي أَعَافُهُ". قَالَ خَالِدٌ: فَاجْتَرَرْتُهُ فَأَكَلْتُهُ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْظُرُ، فَلَمْ يَنْهَنِي
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kwamba alisema: Amenikhabarisha Abuw Umaamah bin Sahl bin Hunayf Al-Answaariy kwamba 'Abdu-Allaah bin 'Abbaas (رضي الله عنهما) alimkhabarisha kwamba Khaalid bin Al-Waliyd (رضي الله عنه) — ambaye huitwa Upanga wa Allaah — alimkhabarisha kwamba yeye aliingia pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa Maymuwnah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) — naye ni dada wa mama yake (Khaalid), na dada wa mama yake Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) —, akakuta kwake dhwabb (mnyama wa jangwani anayefanana na kenge) aliyechomwa (kwa mawe ya moto), ambaye dada yake Hufaydah bint Al-Haarith (رضي الله عنها) alikuja naye kutoka Najd. Akamkaribishia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) dhwabb huyo; naye alikuwa mara chache sana kunyoosha mkono wake kwenye chakula mpaka aelezwe kuhusu (chakula) hicho na atajiwe jina lake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyoosha mkono wake kumwelekea dhwabb. Mwanamke mmoja miongoni mwa wanawake waliohudhuria akasema: Mkhabarisheni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kile mlichomkaribishia. (Wanawake) wakasema: Huyu ni dhwabb. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akauinua mkono wake. Khaalid bin Al-Waliyd (رضي الله عنه) akasema: Je, unamharamisha dhwabb, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Hapana, lakini hakuwa katika ardhi ya watu wangu, kwa hiyo najikuta ninamchukia." Khaalid (رضي الله عنه) amesema: Nikamvuta (kwangu) nikamla, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitazama, wala hakunikataza.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1282
- Hadiyth
- 2060
9-Mlangoباب في الصيد يبين منه العضوMlango Wa Kuhusu Windo Linalokatika Kiungo Chake
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ أَسْلَمَ، قَالَ عَبْدُ الرَّحْمَنِ: أَحْسَبُهُ عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي وَاقِدٍ اللَّيْثِيِّ، قَالَ: قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ، وَالنَّاسُ يَجُبُّونَ أَسْنِمَةَ الْإِبِلِ وَأَلْيَاتِ الْغَنَمِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا قُطِعَ مِنْ بَهِيمَةٍ وَهِيَ حَيَّةٌ، فَهُوَ مَيْتَةٌ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin 'Abdi-Allaah bin Diynaar, ametusimulia Zayd bin Aslam — 'Abdur-Rahmaan amesema: Nadhani ni kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar —, kutoka kwa Abuw Waaqid Al-Laythiy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifika Madiynah, na watu walikuwa wakikata nundu za ngamia na mikia ya mafuta ya mbuzi na kondoo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Kinachokatwa kutoka kwa mnyama naye akiwa hai, basi hicho ni nyamafu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 7
- Ukurasa
- 1284
- Hadiyth
- 2061