Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy09 - Kitabu Cha Vinywaji

ومن كتاب الأشربة

1-Mlangoباب ما جاء في الخمرMlango Wa Yaliyopokewa Kuhusu Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: "أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَيْلَةَ أُسْرِيَ بِهِ بِإِيلْيَاءَ بِقَدَحَيْنِ مِنْ خَمْرٍ وَلَبَنٍ، فَنَظَرَ إِلَيْهِمَا ثُمَّ أَخَذَ اللَّبَنَ، فَقَالَ جِبْرَائِيلُ: الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي هَدَاكَ لِلْفِطْرَةِ، لَوْ أَخَذْتَ الْخَمْرَ، غَوَتْ أُمَّتُكَ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametusimulia Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib, kwamba alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), usiku aliopelekwa safari ya usiku, aliletewa huko Iyliyaa (Baytul-Maqdis) mabakuli mawili, (moja la) khamr (pombe) na (jingine la) maziwa. Akayatazama, kisha akachukua maziwa. Jibriyl (عليه السلام) akasema: "Himdi zote ni za Allaah Ambaye Amekuongoza kwenye Fitwrah (maumbile ya asili). Lau ungechukua khamr, Ummah wako ungepotea."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1325
Hadiyth
2133

2-Mlangoباب في تحريم الخمر كيف كانMlango Wa Kuhusu Jinsi Kulivyokuwa Kuharamishwa
Kwa Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا ثَابِتٌ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: كُنْتُ سَاقِيَ الْقَوْمِ فِي مَنْزِلِ أَبِي طَلْحَةَ، قَالَ: فَنَزَلَ تَحْرِيمُ الْخَمْرِ، قَالَ: فَأَمَرَ مُنَادِيًا فَنَادَى، فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ: اخْرُجْ فَانْظُرْ مَا هَذَا. قَالَ: فَخَرَجْتُ فَقُلْتُ: هَذَا مُنَادٍ يُنَادِي: "أَلَا إِنَّ الْخَمْرَ قَدْ حُرِّمَتْ". فَقَالَ لِيَ: اذْهَبْ فَأَهْرِقْهَا، قَالَ: فَجَرَتْ فِي سِكَكِ الْمَدِينَةِ. قَالَ: وَكَانَتْ خَمْرُهُمْ يَوْمَئِذٍ الْفَضِيخَ. فَقَالَ بَعْضُ الْقَوْمِ: قُتِلَ قَوْمٌ وَهِيَ فِي بُطُونِهِمْ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ عز وجل: {لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوْا وَآمَنُوا}، الْآيَةَ

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa mnyweshaji wa watu katika nyumba ya Abuw Twalhah (رضي الله عنه). Akasema: Kukateremka (hukmu ya) kuharamishwa khamr (pombe). Akasema: Akaamrisha mwitaji, naye akaita. Abuw Twalhah (رضي الله عنه) akasema: Toka nje uangalie ni nini hiki. Akasema: Nikatoka, nikasema: Huyu ni mwitaji anayeita: "Tanabahini! Hakika khamr imeharamishwa." Akaniambia: Nenda ukaimwage. Akasema: Ikatiririka katika njia za Madiynah. Akasema: Na khamr yao siku hiyo ilikuwa ni fadhwiykh (kinywaji cha tende changa zilizopondwa). Baadhi ya watu wakasema: Wameuawa watu na hali (khamr) imo matumboni mwao. Basi Allaah (عز وجل) Akateremsha:

لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا إِذَا مَا اتَّقَوْا وَآمَنُوا

Hakuna lawama juu ya wale walioamini na wakatenda mema katika vile walivyokula (kabla ya kuharamishwa) ikiwa watakuwa na taqwa na wakaamini [Al-Maaidah (5:93)]

mpaka mwisho wa Aayah.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1327
Hadiyth
2134

3-Mlangoباب في التشديد على شارب الخمرMlango Wa Kuhusu Onyo Kali Kwa Mnywaji Wa Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ شَرِبَ الْخَمْرَ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ لَمْ يَتُبْ مِنْهَا، حُرِمَهَا فِي الْآخِرَةِ فَلَمْ يُسْقَهَا"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayekunywa khamr (pombe) duniani, kisha asitubu kutokana nayo, ataharamishiwa (kuinywa) Aakhirah, wala hatanyweshwa."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1328
Hadiyth
2135

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي رَبِيعَةُ بْنُ يَزِيدَ عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الدَّيْلَمِيِّ، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ فِي حَائِطٍ لَهُ بِالطَّائِفِ، يُقَالُ لَهُ: الْوَهْطُ، فَإِذَا هُوَ مُخَاصِرٌ فَتًى مِنْ قُرَيْشٍ يُزَنُّ ذَلِكَ الْفَتَى بِشُرْبِ الْخَمْرِ، فَقُلْتُ: خِصَالٌ بَلَغَتْنِي عَنْكَ أَنَّكَ تُحَدِّثُ بِهَا، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: مَنْ شَرِبَ الْخَمْرَ شَرْبَةً، لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ صَبَاحًا، فَلَمَّا أَنْ سَمِعَ الْفَتَى يَذْكُرُ الْخَمْرَ، اخْتَلَجَ يَدَهُ مِنْ يَدِ عَبْدِ اللَّهِ، ثُمَّ وَلَّى. فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ: اللَّهُمَّ إِنِّي لَا أُحِلُّ لِأَحَدٍ أَنْ يَقُولَ عَلَيَّ مَا لَمْ أَقُلْ، وَإِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ شَرِبَ الْخَمْرَ شَرْبَةً، لَمْ تُقْبَلْ لَهُ صَلَاةٌ أَرْبَعِينَ صَبَاحًا، فَإِنْ تَابَ، تَابَ اللَّهُ عَلَيْهِ، فَلَا أَدْرِي فِي الثَّالِثَةِ أَمْ فِي الرَّابِعَةِ: كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يَسْقِيَهُ مِنْ رَدْغَةِ الْخَبَالِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: Amenisimulia Rabiy'ah bin Yaziyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ad-Daylamiy, amesema: Niliingia kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنهما) katika bustani yake (iliyozungushiwa ukuta) huko Atw-Twaaif, inayoitwa Al-Waht. Kumbe yeye anatembea ameshikana mkono na kijana mmoja wa Quraysh; kijana huyo alikuwa akituhumiwa kunywa khamr (pombe). Nikasema: Ni mambo yaliyonifikia kutoka kwako kwamba unayasimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Atakayekunywa khamr funda moja, haitakubaliwa kwake Swalaah asubuhi arubaini." Yule kijana alipomsikia akitaja khamr, aliuvuta mkono wake kutoka mkononi mwa 'Abdu-Allaah (رضي الله عنهما), kisha akageuka akaondoka. 'Abdu-Allaah (رضي الله عنهما) akasema:

اللَّهُمَّ إِنِّي لَا أُحِلُّ لِأَحَدٍ أَنْ يَقُولَ عَلَيَّ مَا لَمْ أَقُلْ

Yaa Allaah, hakika mimi simhalalishii yeyote kunisingizia nisiyoyasema.

Na hakika mimi nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayekunywa khamr funda moja, haitakubaliwa kwake Swalaah asubuhi arubaini. Na akitubu, Allaah Atapokea tawbah yake. — Sijui (alisema) katika (mara ya) tatu au katika (mara ya) nne: — Imekuwa haki juu ya Allaah Amnyweshe kutoka katika radghatul-khabaal (usaha na jasho la watu wa motoni) Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1328
Hadiyth
2136

4-Mlangoباب النهي عن القعود على مائدة يدار عليها الخمرMlango Wa Kukatazwa Kukaa Kwenye Meza Ya Chakula
Inayozungushwa Juu Yake Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ أَبِي جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا أَبُو الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ، فَلَا يَقْعُدْ عَلَى مَائِدَةٍ يُشْرَبُ عَلَيْهَا الْخَمْرُ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Al-Hasan bin Abiy Ja'far, ametusimulia Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho, basi asikae kwenye meza ya chakula inayonywewa juu yake khamr (pombe)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1329
Hadiyth
2137

5-Mlangoباب في مدمن الخمرMlango Wa Kuhusu Mwenye Kudumu Kunywa Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ الْبَصْرِيُّ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ جَابَانَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، ، قَالَ: "لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ وَلَدُ زِنْيَةٍ، وَلَا مَنَّانٌ، وَلَا عَاقٌّ، وَلَا مُدْمِنُ خَمْرٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr Al-Baswriy, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa Jaabaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hataingia Jannah (Peponi) mtoto wa zinaa, wala mwenye kusimbulia (anachokitoa), wala mwenye kuwaasi wazazi, wala mwenye kudumu kunywa khamr (pombe)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1330
Hadiyth
2138

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ الْحَجَّاجِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مَهْدِيٍّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ نُبَيْطِ بْنِ شَرِيطٍ، عَنْ جَابَانَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ عَاقٌّ، وَلَا مَنَّانٌ، وَلَا مُدْمِنُ خَمْرٍ"

Ametusimulia Ahmad bin Al-Hajjaaj, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Mahdiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa Nubaytw bin Shariytw, kutoka kwa Jaabaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hataingia Jannah (Peponi) mwenye kuwaasi wazazi, wala mwenye kusimbulia (anachokitoa), wala mwenye kudumu kunywa khamr (pombe)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1330
Hadiyth
2139

6-Mlangoباب ليس في الخمر شفاءMlango Wa Hakuna Ponyo Katika Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا سُهَلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا سِمَاكٌ، قَالَ: سَمِعْتُ عَلْقَمَةَ بْنَ وَائِلٍ يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِيهِ وَائِلٍ، أَنَّ سُوَيْدَ بْنَ طَارِقٍ سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ الْخَمْرِ، فَنَهَاهُ عَنْهَا أَنْ يَصْنَعَهَا، فَقَالَ: إِنَّهَا دَوَاءٌ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّهَا لَيْسَتْ دَوَاءً وَلَكِنَّهَا دَاءٌ"

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Simaak, amesema: Nilimsikia 'Alqamah bin Waail akisimulia kutoka kwa baba yake, Waail (رضي الله عنه), kwamba Suwayd bin Twaariq (رضي الله عنه) alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu khamr (pombe), naye akamkataza kuitengeneza. Akasema: Hakika hiyo ni dawa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika hiyo si dawa, lakini hiyo ni ugonjwa."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1331
Hadiyth
2140

7-Mlangoباب مما يكون الخمرMlango Wa Khamr (Pombe) Hutokana Na Nini

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا كَثِيرٍ يَقُولُ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "الْخَمْرُ مِنْ هَاتَيْنِ الشَّجَرَتَيْنِ: النَّخْلَةِ وَالْعِنَبِ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, amesema: Nilimsikia Abuw Kathiyr akisema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Khamr (pombe) hutokana na miti hii miwili: mtende na mzabibu."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1331
Hadiyth
2141

8-Mlangoباب ما قيل في المسكرMlango Wa Yaliyosemwa Kuhusu Kileo

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنْ الْبِتْعِ، قَالَ: "كُلُّ شَرَابٍ أَسْكَرَ حَرَامٌ"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu al-bit' (kinywaji kinachotengenezwa kwa asali), akasema: "Kila kinywaji kinacholevya ni haraam."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1332
Hadiyth
2142

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَا وَمُعَاذَ بْنَ جَبَلٍ إِلَى الْيَمَنِ، فَقَالَ: "اشْرَبُوا، وَلَا تَشْرَبُوا مُسْكِرًا، فَإِنَّ كُلَّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abuw Burdah bin Abiy Muwsaa, kutoka kwa baba yake [Abuw Muwsaa (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinituma mimi na Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) kwenda Yemen, akasema: "Kunyweni, wala msinywe kileo, kwani kila kileo ni haraam."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1332
Hadiyth
2143

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو أُسَامَةَ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ كَثِيرِ بْنِ سِنَانٍ، حَدَّثَنِي الضَّحَّاكُ بْنُ عُثْمَانَ، عَنْ بُكَيْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْأَشَجِّ، عَنْ عَامِرِ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ سَعْدٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَنْهَاكُمْ عَنْ قَلِيلِ مَا أَسْكَرَ كَثِيرُهُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametupa khabari Abuw Usaamah, ametusimulia Al-Waliyd bin Kathiyr bin Sinaan, amenisimulia Adh-Dhwahhaak bin 'Uthmaan, kutoka kwa Bukayr bin 'Abdi-Allaah bin Al-Ashajj, kutoka kwa 'Aamir bin Sa'd, kutoka kwa Sa'd (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Ninakukatazeni kidogo cha kile ambacho kingi chake kinalevya."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1333
Hadiyth
2144

حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ رَاشِدٍ، عَنْ أَبِي وَهْبٍ الْكَلَاعِيِّ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِنَّ أَوَّلَ مَا يُكْفَأُ قَالَ زَيْدٌ: يَعْنِي: فِي الْإِسْلَامَ كَمَا يُكْفَأُ الْإِنَاءُ يَعْنِي: الْخَمْرِ"، فَقِيلَ: كَيْفَ يَا رَسُولَ اللَّهِ وَقَدْ بَيَّنَ اللَّهُ فِيهَا مَا بَيَّنَ؟ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يُسَمُّونَهَا بِغَيْرِ اسْمِهَا فَيَسْتَحِلُّونَهَا"

Ametusimulia Zayd bin Yahyaa, ametusimulia Muhammad bin Raashid, kutoka kwa Abuw Wahb Al-Kalaa'iy, kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika kitu cha kwanza kitakachopinduliwa — Zayd amesema: yaani katika Islaam — kama kinavyopinduliwa chombo — yaani khamr (pombe)." Pakaulizwa: Vipi, yaa Rasula-Allaah, na hali Allaah Amekwisha kubainisha kuhusu hiyo Aliyoyabainisha? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Wataiita kwa jina lisilokuwa jina lake, kisha wataihalalisha."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1333
Hadiyth
2145

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، حَدَّثَنِي أَبُو وَهْبٍ، عَنْ مَكْحُولٍ، عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الْخُشَنِيِّ، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ بْنِ الْجَرَّاحِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَوَّلُ دِينِكُمْ نُبُوَّةٌ وَرَحْمَةٌ، ثُمَّ مُلْكٌ وَرَحْمَةٌ، ثُمَّ مُلْكٌ أَعْفَرُ، ثُمَّ مُلْكٌ وَجَبَرُوتٌ يُسْتَحَلُّ فِيهَا الْخَمْرُ وَالْحَرِيرُ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: سُئِلَ عَنْ أَعْفَرَ، فَقَالَ: يُشَبِّهِهُ بِالتُّرَابِ وَلَيْسَ فِيهِ خَيْرٌ

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, amenisimulia Abuw Wahb, kutoka kwa Mak-huwl, kutoka kwa Abuw Tha'labah Al-Khushaniy (رضي الله عنه), kutoka kwa Abuw 'Ubaydah bin Al-Jarraah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanzo wa Dini yenu ni Unabii na Rehma, kisha ufalme na Rehma, kisha ufalme a'far (wenye rangi ya vumbi), kisha ufalme na ujabari, ambao ndani yake itahalalishwa khamr (pombe) na hariri."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Aliulizwa kuhusu a'far, akasema: Anaufananisha na udongo, wala hamna kheri ndani yake.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1334
Hadiyth
2146

9-Mlangoباب النهي عن بيع الخمر وشرائهاMlango Wa Kukatazwa Kuuza Khamr (Pombe) Na Kuinunua

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا طُعْمَةُ، حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ بَيَانٍ التَّغْلِبِيُّ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: "مَنْ بَاعَ الْخَمْرَ، فَلْيُشَقِّصْ الْخَنَازِيرَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: إِنَّمَا هُوَ عُمَرُ بْنُ بَيَانٍ

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Tu'mah, ametusimulia 'Umar bin Bayaan At-Taghlibiy, kutoka kwa 'Urwah bin Al-Mughiyrah bin Shu'bah, kutoka kwa baba yake [Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه)], kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema: "Anayeuza khamr (pombe), basi na akate nguruwe vipande vipande (kama mchinjaji)."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Hakika yeye ni 'Umar bin Bayaan.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1334
Hadiyth
2147

حَدَّثَنَا يَعْلَى، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ الْقَعْقَاعِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ وَعْلَةَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ عَنْ بَيْعِ الْخَمْرِ، فَقَالَ: كَانَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَدِيقٌ مِنْ ثَقِيفٍ أَوْ مِنْ دَوْسٍ، فَلَقِيَهُ بِمَكَّةَ عَامَ الْفَتْحِ بِرَاوِيَةٍ مِنْ خَمْرٍ يُهْدِيهَا لَهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا فُلَانُ، أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَدْ حَرَّمَهَا؟" قَالَ: فَأَقْبَلَ الرَّجُلُ عَلَى غُلَامِهِ، فَقَالَ: اذْهَبْ فَبِعْهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "بِمَاذَا أَمَرْتَهُ يَا فُلَانُ؟" قَالَ: أَمَرْتُهُ بِبَيْعِهَا. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الَّذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا، حَرَّمَ بَيْعَهَا". فَأَمَرَ بِهَا فَأُكْفِئَتْ فِي الْبَطْحَاءِ

Ametusimulia Ya'laa, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Al-Qa'qaa' bin Hakiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Wa'lah, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu kuuza khamr (pombe). Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa na rafiki kutoka (kabila la) Thaqiyf au kutoka (kabila la) Daws. Akakutana naye Makkah mwaka wa Ufunguzi (wa Makkah) akiwa na kiriba kikubwa cha khamr anachompa zawadi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yaa fulani, je, hukujua kwamba Allaah (تعالى) Ameiharamisha?" Akasema: Yule mtu akamgeukia mtumishi wake, akasema: Nenda ukaiuze. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Umemwamrisha nini, yaa fulani?" Akasema: Nimemwamrisha aiuze. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika Ambaye Ameharamisha kuinywa, Ameharamisha kuiuza." Akaamrisha (imwagwe), ikamwagwa katika Al-Batwhaa (bonde la Makkah).

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1335
Hadiyth
2148

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرٍو يَعْنِي: ابْنَ دِينَارٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: بَلَغَ عُمَرَ أَنَّ سَمُرَةَ بَاعَ خَمْرًا، فَقَالَ: قَاتَلَ اللَّهُ سَمُرَةَ، أَمَا عَلِمَ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَعَنَ اللَّهُ الْيَهُودَ، حُرِّمَتْ عَلَيْهِمْ الشُّحُومُ فَجَمَلُوهَا، فَبَاعُوهَا". قَالَ سُفْيَانُ: جَمَلُوهَا: أَذَابُوهَا

Ametusimulia Muhammad bin Ahmad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr — yaani Ibn Diynaar —, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Ilimfikia 'Umar (رضي الله عنه) (khabari) kwamba Samurah (رضي الله عنه) ameuza khamr (pombe). Akasema: Allaah Amwangamize Samurah! Je, hakujua kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: "Allaah Awalaani Mayahudi; waliharamishiwa mafuta (ya wanyama), wakayayeyusha, kisha wakayauza." Sufyaan amesema: Jamaluwhaa maana yake: waliyayeyusha.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1336
Hadiyth
2150

10-Mlangoباب العقوبة في شرب الخمرMlango Wa Adhabu Ya Kunywa Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا عَاصِمُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا سَكِرَ، فَاجْلِدُوهُ، ثُمَّ إِذَا سَكِرَ، فَاجْلِدُوهُ، ثُمَّ إِذَا سَكِرَ، فَاجْلِدُوهُ، ثُمَّ إِذَا سَكِرَ، فَاضْرِبُوا عُنُقَهُ". يَعْنِي فِي الرَّابِعَةِ

Ametukhabarisha 'Aaswim bin 'Aliy, ametusimulia Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Al-Haarith bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Akilewa, mpigeni mijeledi; kisha akilewa, mpigeni mijeledi; kisha akilewa, mpigeni mijeledi; kisha akilewa, ikateni shingo yake" — yaani katika (mara ya) nne.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1336
Hadiyth
2151

11-Mlangoباب في التغليظ لمن شرب الخمرMlango Wa Kuhusu Onyo Zito Kwa Aliyekunywa Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَزْنِي الزَّانِي حِينَ يَزْنِي وَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَلَا يَسْرِقُ السَّارِقُ حِينَ يَسْرِقُ وَهُوَ مُؤْمِنٌ، وَلَا يَشْرَبُ الْخَمْرَ حِينَ يَشْرَبُهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mzinifu hazini wakati anapozini naye ni Muumini; wala mwizi haibi wakati anapoiba naye ni Muumini; wala (mtu) hanywi khamr (pombe) wakati anapoinywa naye ni Muumini."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1337
Hadiyth
2152

12-Mlangoباب فيما ينتبذ للنبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Kinywaji Kinachorowekwa
Kwa Ajili Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبِي سُلَيْمَانَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "كَانَ يُنْبَذُ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي السِّقَاءِ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ سِقَاءٌ، نُبِذَ لَهُ فِي تَوْرٍ مِنْ بِرَامٍ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Abiy Sulaymaan, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akirowekewa (kinywaji) katika kiriba; na ikiwa hakuna kiriba, alirowekewa katika chungu cha jiwe."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1337
Hadiyth
2153

13-Mlangoباب في النقيعMlango Wa Kuhusu Naqiy' (Kinywaji Cha Zabibu
Au Tende Zilizorowekwa Majini)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي عَمْرٍو السَّيْبَانِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الدَّيْلَمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّ أَبَاهُ أَوْ أَنَّ رَجُلًا مِنْهُمْ سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا قَدْ خَرَجْنَا مِنْ حَيْثُ عَلِمْتَ، وَنَزَلْنَا بَيْنَ ظَهْرَانَيْ مَنْ قَدْ عَلِمْتَ، فَمَنْ وَلِيُّنَا؟ قَالَ: "اللَّهُ وَرَسُولُهُ". قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا كُنَّا أَصْحَابَ كَرْمٍ وَخَمْرٍ، وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَ الْخَمْرَ، فَمَا نَصْنَعُ بِالْكَرْمِ؟ قَالَ: "اصْنَعُوهُ زَبِيبًا". قَالُوا: فَمَا نَصْنَعُ بِالزَّبِيبِ؟ قَالَ: "انْقَعُوا فِي الشِّنَانِ، انْقَعُوهُ عَلَى غَدَائِكُمْ، وَاشْرَبُوهُ عَلَى عَشَائِكُمْ، وَانْقَعُوهُ عَلَى عَشَائِكُمْ، وَاشْرَبُوهُ عَلَى غَدَائِكُمْ، فَإِنَّهُ إِذَا أَتَى عَلَيْهِ الْعَصْرَانِ، كَانَ خَلًّا قَبْلَ أَنْ يَكُونَ خَمْرًا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy 'Amr As-Saybaaniy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ad-Daylamiy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba baba yake, au kwamba mtu mmoja miongoni mwao, alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tumetoka mahali ulipopajua, na tumeshuka katikati ya (watu) uliowajua; basi ni nani walii wetu? Akasema: "Allaah na Rasuli Wake." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tulikuwa watu wa mizabibu na khamr (pombe), na hakika Allaah Ameharamisha khamr; basi tuifanye nini mizabibu? Akasema: "Ifanyeni zabibu kavu." Wakasema: Basi tuzifanye nini zabibu kavu? Akasema: "Rowekeni katika viriba vikukuu: zirowekeni (wakati wa) chakula chenu cha asubuhi, na mnywe (maji yake wakati wa) chakula chenu cha jioni; na zirowekeni (wakati wa) chakula chenu cha jioni, na mnywe (maji yake wakati wa) chakula chenu cha asubuhi. Kwani hakika (kinywaji) hicho kikipitiwa na nyakati mbili (asubuhi na jioni), kinakuwa siki kabla hakijawa khamr."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1338
Hadiyth
2154

14-Mlangoباب النهي عن نبيذ الجر، وما ينبذ فيهMlango Wa Kukatazwa Nabiydh (Kinywaji Cha Tende
Kilichoroweshwa) Ya Mitungi Ya Udongo, Na Vile
Vinavyorowekewa Ndani Yake

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي عَرُوبَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ عَزْرَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عُمَرَ عَنْ نَبِيذِ الْجَرِّ، فَقَالَ: "حَرَّمَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ". فَلَقِيتُ ابْنَ عَبَّاسٍ فَأَخْبَرْتُهُ بِقَوْلِ ابْنِ عُمَرَ، فَقَالَ: صَدَقَ أَبُو عَبْدِ الرَّحْمَنِ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy 'Aruwbah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa 'Azrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) kuhusu nabiydh (kinywaji cha tende kilichoroweshwa) ya mitungi ya udongo. Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliiharamisha." Nikakutana na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), nikamkhabarisha kauli ya Ibn 'Umar (رضي الله عنهما). Akasema: Amesema kweli Abuw 'Abdir-Rahmaan (رضي الله عنه).

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1339
Hadiyth
2155

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَنَسُ بْنُ مَالِكٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا تَنْتَبِذُوا فِي الدُّبَّاءِ وَالْمُزَفَّتِ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenisimulia Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiroweke (kinywaji) katika kibuyu na chombo kilichopakwa lami."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1340
Hadiyth
2156

أَخْبَرَنَا أَبُو زَيْدٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا الْحَكَمِ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ أَوْ سَمِعْتُهُ سُئِلَ عَنْ نَبِيذِ الْجَرِّ، فَقَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَبِيذِ الْجَرِّ وَالدُّبَّاءِ". وَسَأَلْتُ ابْنَ الزُّبَيْرِ، فَقَالَ مِثْلَ قَوْلِ ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: "مَنْ سَرَّهُ أَنْ يُحَرِّمَ مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ، أَوْ مَنْ كَانَ مُحَرِّمًا مَا حَرَّمَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ، فَلْيُحَرِّمْ النَّبِيذَ" قَالَ: وَحَدَّثَنِي أَخِي، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ الْجَرِّ وَالدُّبَّاءِ وَالْمُزَفَّتِ، وَعَنْ الْبُسْرِ وَالتَّمْرِ"

Ametukhabarisha Abuw Zayd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, amesema: Nilimsikia Abul-Hakam, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) — au nilimsikia akiulizwa — kuhusu nabiydh (kinywaji cha tende kilichoroweshwa) ya mitungi ya udongo. Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza nabiydh ya mitungi ya udongo na ya kibuyu." Na nilimuuliza Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما), akasema mfano wa kauli ya Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما). Akasema: Na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Anayefurahishwa kuharamisha alichokiharamisha Allaah na Rasuli Wake — au: anayeharamisha alichokiharamisha Allaah na Rasuli Wake —, basi na aiharamishe nabiydh." Akasema: Na amenisimulia ndugu yangu, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza mitungi ya udongo, na kibuyu, na chombo kilichopakwa lami, na (kuchanganya) busr (tende changa) na tende."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1340
Hadiyth
2157

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ، عَنْ فُضَيْلِ بْنِ زَيْدٍ الرَّقَاشِيِّ، أَنَّهُ أَتَى عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مُغَفَّلٍ، فَقَالَ: أَخْبِرْنِي بِمَا يَحْرُمُ عَلَيْنَا مِنْ الشَّرَابِ، فَقَالَ: الْخَمْرُ. قُلْتُ: هُوَ فِي الْقُرْآنِ؟ قَالَ: مَا أُحَدِّثُكَ إِلَّا مَا سَمِعْتُ مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَدَأَ بِالِاسْمِ أَوْ بِالرِّسَالَةِ، قَالَ: فَقَالَ: "نَهَى عَنْ الدُّبَّاءِ وَالْحَنْتَمِ وَالنَّقِيرِ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Thaabit bin Yaziyd, ametusimulia 'Aaswim, kutoka kwa Fudhwayl bin Zayd Ar-Raqaashiy, kwamba alimwendea 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), akasema: Nikhabarishe kuhusu kinachoharamishwa kwetu katika vinywaji. Akasema: Khamr (pombe). Nikasema: Je, (uharamu wake) uko katika Qur-aan? Akasema: Sikusimulii isipokuwa niliyomsikia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) — alianza kwa jina, au kwa (cheo cha) Ujumbe —, amesema: Akasema: "Alikataza kibuyu, na al-hantam (mitungi ya kijani), na gogo lililochongwa."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1341
Hadiyth
2158

15-Mlangoباب في النهي عن الخليطينMlango Wa Kuhusu Kukatazwa Al-Khaliytwayn
(Kuchanganya Aina Mbili Katika Kuroweka Kinywaji)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، وَسَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، وَاللَّفْظُ لِيَزِيدَ، قَالَا: أَنْبَأَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا تَنْتَبِذُوا الزَّهْوَ وَالرُّطَبَ جَمِيعًا، وَلَا تَنْتَبِذُوا الزَّبِيبَ وَالتَّمْرَ جَمِيعًا، وَانْتَبِذُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا عَلَى حِدَتِهِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn na Sa'iyd bin 'Aamir — na tamko ni la Yaziyd —, wamesema: Ametupa khabari Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, kutoka kwa baba yake [Abuw Qataadah (رضي الله عنه)], kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Msiroweke zahw (tende zilizoanza kuiva) na rutwab (tende mbivu) pamoja, wala msiroweke zabibu kavu na tende pamoja; na rowekeni kila kimoja katika hivyo peke yake."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1343
Hadiyth
2159

16-Mlangoباب في النهي أن يسمى العنب الكرمMlango Wa Kuhusu Kukatazwa Zabibu Kuitwa
Al-Karm (Jina Linalotokana Na Ukarimu)

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سِمَاكٍ، عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ وَائِلٍ، عَنْ أَبِيهِ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا تَقُولُوا: الْكَرْمَ، وَقُولُوا: الْعِنَبَ أَوْ الْحَبَلَةَ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa 'Alqamah bin Waail, kutoka kwa baba yake [Waail bin Hujr (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiseme: Al-Karm (jina linalotokana na ukarimu); na semeni: Al-'Inab (zabibu), au: Al-Habalah (mzabibu)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1343
Hadiyth
2160

17-Mlangoباب في النهي أن يجعل الخمر خلاMlango Wa Kuhusu Kukatazwa
Kuifanya Khamr (Pombe) Kuwa Siki

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ السُّدِّيِّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَبَّادٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: " كَانَ فِي حِجْرِ أَبِي طَلْحَةَ يَتَامَى، فَاشْتَرَى لَهُمْ خَمْرًا، فَلَمَّا نَزَلَ تَحْرِيمُ الْخَمْرِ، أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: أَجْعَلُهُ خَلًّا؟ قَالَ: " لَا "، فَأَهْرَاقَهُ

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa As-Suddiy, kutoka kwa Yahyaa bin 'Abbaad, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: "Abuw Twalhah (رضي الله عنه) alikuwa na mayatima chini ya malezi yake, akawanunulia khamr (pombe). Kuharamishwa kwa khamr kulipoteremka, alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akamtajia hilo, akasema: Je, niifanye siki? Akasema: 'Hapana.' Basi akaimwaga."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1344
Hadiyth
2161

18-Mlangoباب في سنة الشراب كيف هي؟Mlango Wa Kuhusu Sunnah Ya Kunywa, Ni Vipi?

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّهُ رَأَى رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَرِبَ لَبَنًا، وَعَنْ يَسَارِهِ أَبُو بَكْرٍ، وَعَنْ يَمِينِهِ رَجُلٌ أَعْرَابِيٌّ، فَأَعْطَى الْأَعْرَابِيَّ فَضْلَهُ، ثُمَّ قَالَ: "الْأَيْمَنَ فَالْأَيْمَنَ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, ametusimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba alimuona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akinywa maziwa, na kushotoni kwake (alikuwa) Abuw Bakr (رضي الله عنه), na kuliani kwake mtu mmoja bedui. Akampa yule bedui masazo yake, kisha akasema: "(Anaanza) wa kulia, kisha wa kulia."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1345
Hadiyth
2162

19-Mlangoباب في النهي عن الشرب من في السقاءMlango Wa Kuhusu Kukatazwa Kunywa
Kutoka Mdomoni Mwa Kiriba

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا قَتَادَةُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى أَنْ يُشْرَبَ مِنْ فِي السِّقَاءِ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Qataadah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kunywa kutoka mdomoni mwa kiriba."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1345
Hadiyth
2163

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يُشْرَبَ مِنْ فِي السِّقَاءِ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kunywa kutoka mdomoni mwa kiriba."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1345
Hadiyth
2164

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ ابْنِ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ اخْتِنَاثِ الْأَسْقِيَةِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kukunja (midomo ya) viriba (na kunywa kutoka humo)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1346
Hadiyth
2165

20-Mlangoباب في الشرب بثلاثة أنفاسMlango Wa Kuhusu Kunywa Kwa Pumzi Tatu

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَزْرَةُ بْنُ ثَابِتٍ، عَنْ ثُمَامَةَ، قَالَ: كَانَ أَنَسٌ يَتَنَفَّسُ فِي الْإِنَاءِ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلَاثًا، وَزَعَمَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "يَتَنَفَّسُ فِي الْإِنَاءِ مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلَاثًا"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Azrah bin Thaabit, kutoka kwa Thumaamah, amesema: Anas (رضي الله عنه) alikuwa akipumua katika chombo mara mbili au tatu, na akadai kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa "akipumua katika chombo mara mbili au tatu."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1347
Hadiyth
2166

21-Mlangoباب من شرب بنفس واحدMlango Wa Aliyekunywa Kwa Pumzi Moja

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، عَنْ مَالِكٍ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ حَبِيبٍ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي الْمُثَنَّى، قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ مَرْوَانَ فَجَاءَ أَبُو سَعِيدٍ فَقَالَ: قَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي لَا أَرْوَى مِنْ نَفَسٍ وَاحِدٍ؟ قَالَ: "فَأَبِنْ الْإِنَاءَ عَنْ فِيكَ، ثُمَّ تَنَفَّسْ". قَالَ: إِنِّي أَرَى الْقَذَاةَ؟ قَالَ: "أَهْرِقْهُ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, kutoka kwa Maalik, kutoka kwa Ayyuwb bin Habiyb Az-Zuhriy, kutoka kwa Abul-Muthannaa, amesema: Nilikuwa kwa Marwaan, akaja Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), akasema: Mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi sikati kiu kwa pumzi moja. Akasema: "Basi kiweke mbali chombo na mdomo wako, kisha pumua." Akasema: Hakika mimi naona kibanzi (ndani yake). Akasema: "Yamwage (yaliyomo)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1348
Hadiyth
2167

حَدَّثَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبِي، أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِذَا بَالَ أَحَدُكُمْ، فَلَا يَمَسَّ ذَكَرَهُ بِيَمِينِهِ، وَلَا يَسْتَنْجِي بِيَمِينِهِ، وَلَا يَتَنَفَّسْ فِي الْإِنَاءِ"

Ametusimulia Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, amesema: Amenisimulia baba yangu [Abuw Qataadah (رضي الله عنه)], kwamba alimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mmoja wenu anapokojoa, basi asiiguse dhakari yake kwa mkono wake wa kulia, wala asijisafishe (baada ya haja) kwa mkono wake wa kulia, wala asipumue katika chombo."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1348
Hadiyth
2168

22-Mlangoباب في الذي يكرع في النهرMlango Wa Kuhusu Anayekunywa
Kwa Mdomo Moja Kwa Moja Kutoka Mtoni

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا فُلَيْحُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْحَارِثِ الْأَنْصَارِيِّ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: أَتَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا مِنْ الْأَنْصَارِ يَعُودُهُ، وَجَدْوَلٌ يَجْرِي، فَقَالَ: "إِنْ كَانَ عِنْدَكُمْ مَاءٌ بَاتَ فِي الشَّنِّ، وَإِلَّا كَرَعْنَا"

Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, ametusimulia Fulayh bin Sulaymaan, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Haarith Al-Answaariy, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwendea mtu mmoja miongoni mwa Answaar (رضي الله عنهم) kumtembelea (katika ugonjwa wake), na kijito (cha maji) kilikuwa kikitiririka. Akasema: "Ikiwa mnayo maji yaliyolala usiku katika kiriba kikuukuu, (basi tunyweshe); la sivyo, tutakunywa kwa midomo yetu (moja kwa moja kutoka kijitoni)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1349
Hadiyth
2169

23-Mlangoباب في الشرب قائماMlango Wa Kuhusu Kunywa Ukiwa Umesimama

حَدَّثَنَا مَنْصُورُ بْنُ سَلَمَةَ الْخُزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ عَبْدِ الْكَرِيمِ، عَنْ الْبَرَاءِ ابْنِ ابْنَةِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ، عَنْ أُمِّ سُلَيْمٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "شَرِبَ مِنْ فَمِ قِرْبَةٍ قَائِمًا"

Ametusimulia Manswuwr bin Salamah Al-Khuzaa'iy, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa 'Abdul-Kariym, kutoka kwa Al-Baraa, mwana wa binti wa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Ummu Sulaym (رضي الله عنها), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikunywa kutoka mdomo wa kiriba akiwa amesimama."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1349
Hadiyth
2170

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا عِمْرَانُ بْنُ حُدَيْرٍ، عَنْ أَبِي الْبَزَرِيِّ: يَزِيدَ بْنِ عُطَارِدَ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "كُنَّا نَشْرَبُ وَنَحْنُ قِيَامٌ، وَنَأْكُلُ وَنَحْنُ نَسْعَى عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ".

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari 'Imraan bin Hudayr, kutoka kwa Abul-Bazariy Yaziyd bin 'Utwaarid, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Tulikuwa tukinywa hali tumesimama, na tukila hali tunatembea, katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1350
Hadiyth
2171

أَخْبَرَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، نَحْوَهُ

Ametukhabarisha Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), mfano wake.

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1350
Hadiyth
2172

24-Mlangoباب من كره الشرب قائماMlango Wa Aliyechukia Kunywa Ukiwa Umesimama

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ أَنَسٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ الشُّرْبِ قَائِمًا". قَالَ: وَسَأَلْتُهُ عَنْ الْأَكْلِ، قَالَ: "ذَاكَ أَخْبَثُ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kunywa ukiwa umesimama." (Qataadah) akasema: Nikamuuliza kuhusu kula, akasema: "Hilo ni ovu zaidi."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1351
Hadiyth
2173

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي زِيَادٍ الطَّحَّانِ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ لِرَجُلٍ رَآهُ يَشْرَبُ قَائِمًا: "قِئْ". قَالَ: لِمَ؟ قَالَ: "أَتُحِبُّ أَنْ تَشْرَبَ مَعَ الْهِرِّ؟" قَالَ: لَا، قَالَ: "فَقَدْ شَرِبَ مَعَكَ شَرٌّ مِنْهُ، الشَّيْطَانُ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abuw Ziyaad Atw-Twahhaan, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) (akisimulia) kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), (kwamba) alimwambia mtu mmoja aliyemuona akinywa akiwa amesimama: "Jitapishe." (Yule mtu) akasema: Kwa nini? Akasema: "Je, unapenda kunywa pamoja na paka?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi amekwishakunywa pamoja nawe aliye mbaya zaidi kuliko yeye: shaytwaan."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1351
Hadiyth
2174

25-Mlangoباب الشرب في المفضضMlango Wa Kunywa Katika Chombo Kilichopambwa Kwa Fedha

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا لَيْثُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ، أَنَّهَا أَخْبَرَتْهُ أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الَّذِي يَشْرَبُ فِي آنِيَةٍ مِنْ فِضَّةٍ، فَإِنَّمَا يُجَرْجِرُ فِي بَطْنِهِ نَارَ جَهَنَّمَ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Yuwnus, ametusimulia Layth bin Sa'd, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Zayd bin 'Abdi-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr, kutoka kwa Ummu Salamah (رضي الله عنها), kwamba yeye alimkhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Anayekunywa katika vyombo vya fedha, basi hakika anajimiminia tumboni mwake (kwa mvumo) moto wa Jahannam."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1352
Hadiyth
2175

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ حُذَيْفَةَ إِلَى الْمَدَائِنِ فَاسْتَسْقَى، فَأَتَاهُ دِهْقَانٌ بِإِنَاءٍ مِنْ فِضَّةٍ، فَرَمَى بِهِ وَجْهَهُ، فَقُلْنَا: اسْكُتُوا، فَإِنَّا إِنْ سَأَلْنَاهُ لَمْ يُحَدِّثْنَا، فَلَمَّا كَانَ بَعْدُ، قَالَ: أَتَدْرُونَ لِمَ رَمَيْتُهُ؟ قُلْنَا: لَا، قَالَ إِنِّي كُنْتُ نَهَيْتُهُ، وَذَكَرَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ نَهَى عَنْ الشُّرْبِ فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ، وَعَنْ لُبْسِ الْحَرِيرِ وَالدِّيبَاجِ، وَقَالَ: "هُمَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا، وَلَكُمْ فِي الْآخِرَةِ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Ibn 'Awn, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, amesema: Tulitoka pamoja na Hudhayfah (رضي الله عنه) kwenda Al-Madaain, akaomba kunyweshwa. Dihqaan (mkuu wa kijiji miongoni mwa Waajemi) akamletea chombo cha fedha, akamrushia nacho usoni mwake. Tukasema: Nyamazeni, kwani tukimuuliza hatatusimulia. Ilipokuwa baadaye, akasema: Je, mnajua kwa nini nilimrushia? Tukasema: Hapana. Akasema: Hakika mimi nilikuwa nimemkataza. Na akamtaja Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba alikataza kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha, na kuvaa hariri na diybaaj (hariri iliyonakshiwa), na akasema: "Hivyo viwili ni vyao (makafiri) duniani, na ni vyenu Aakhirah."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1352
Hadiyth
2176

26-Mlangoباب في تخمير الإناءMlango Wa Kuhusu Kufunika Chombo

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، حَدَّثَنِي جَابِرٌ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو حُمَيْدٍ السَّاعِدِيُّ، قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلَبَنٍ، فَقَالَ: "أَلَا خَمَّرْتَهُ وَلَوْ تَعْرِضُ عَلَيْهِ عُودًا؟"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, amenisimulia Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Amenisimulia Abuw Humayd As-Saa'idiy (رضي الله عنه), amesema: Nilimletea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) maziwa, akasema: "Kwa nini usiyafunike, japo kwa kuweka juu yake kijiti kwa upana?"

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1353
Hadiyth
2177

حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدٍ، عَنْ سُهَيْلٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "أَمَرَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِتَغْطِيَةِ الْوَضُوءِ، وَإِيكَاءِ السِّقَاءِ، وَإِكْفَاءِ الْإِنَاءِ"

Ametusimulia 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Suhayl, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha kufunika maji ya Wudhuu, na kufunga kiriba, na kukifudikiza chombo."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1354
Hadiyth
2178

27-Mlangoباب النهي عن النفخ في الشرابMlango Wa Kukatazwa Kupuliza Katika Kinywaji

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي الْمُثَنَّى الْجُهَنِيِّ، قَالَ: قَالَ مَرْوَانُ لِأَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيّ: هَلْ سَمِعْتَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَى عَنْ النَّفْخِ فِي الشَّرَابِ؟ قَالَ: "نَعَمْ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ayyuwb bin Habiyb, kutoka kwa Abul-Muthannaa Al-Juhaniy, amesema: Marwaan alimwambia Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه): Je, ulimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza kupuliza katika kinywaji? Akasema: "Ndiyo."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1354
Hadiyth
2179

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ ابْنِ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَبْدِ الْكَرِيمِ الْجَزَرِيِّ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ النَّفْخِ فِي الشَّرَابِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Abdul-Kariym Al-Jazariy, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza kupuliza katika kinywaji."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1354
Hadiyth
2180

28-Mlangoباب في ساقي القوم آخرهم شرباMlango Wa Kuhusu Mnyweshaji Wa Watu
Ndiye Wa Mwisho Wao Kunywa

حَدَّثَنَا عَفَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، وَسُلَيْمَانُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ رَبَاحٍ، عَنْ أَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "سَاقِي الْقَوْمِ آخِرُهُمْ شُرْبًا"

Ametusimulia 'Affaan bin Muslim, ametusimulia Hammaad bin Salamah na Sulaymaan bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Rabaah, kutoka kwa Abuw Qataadah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mnyweshaji wa watu ndiye wa mwisho wao kunywa."

Mjalada
2
Kitabu
9
Ukurasa
1355
Hadiyth
2181