ومن كتاب الرؤيا
1-Mlangoباب في قوله تعالى {لهم البشرى في الحياة الدنيا}Mlango Wa Kuhusu Kauli Yake (تعالى) : «Watapata
bishara katika uhai wa dunia» [Yuwnus (10:64)]
أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا أَبَانُ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، قَوْلُ اللَّهِ: {لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا}، قَالَ: "سَأَلْتَنِي عَنْ شَيْءٍ مَا سَأَلَنِي عَنْهُ أَحَدٌ قَبْلَكَ أَوْ أَحَدٌ مِنْ أُمَّتِي، قَالَ: هِيَ الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ، يَرَاهَا الْمُسْلِمُ أَوْ تُرَى لَهُ"
Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Abaan, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Nabiyya-Allaah, Kauli ya Allaah:
لَهُمُ الْبُشْرَى فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
Watapata bishara katika uhai wa dunia [Yuwnus (10:64)]
Akasema: "Umeniuliza kuhusu jambo ambalo hakuna yeyote aliyeniuliza kuhusu hilo kabla yako, au yeyote katika Ummah wangu." Akasema: "Hiyo ni ndoto njema anayoiona Muislamu au anaonyeshwa (na mwingine)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1357
- Hadiyth
- 2182
2-Mlangoباب في رؤيا المسلم جزء من ستة وأربعين جزءا من النبوةMlango Wa Kuhusu Ndoto Ya Muislamu: Ni Sehemu Moja
Kati Ya Sehemu Arubaini Na Sita Za Unabii
أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "رُؤْيَا الْمُؤْمِنِ جُزْءٌ مِنْ سِتَّةٍ وَأَرْبَعِينَ جُزْءًا مِنْ النُّبُوَّةِ"
Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Ndoto ya Muumini ni sehemu moja kati ya sehemu arubaini na sita za Unabii."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1358
- Hadiyth
- 2183
3-Mlangoباب ذهبت النبوة وبقيت المبشراتMlango Wa Unabii Umeondoka, Na Zimebakia Bishara
حَدَّثَنَا هَارُونُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي يَزِيدَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ سِبَاعِ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ أُمِّ كُرْزٍ الْكَعْبِيَّةِ، قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "ذَهَبَتْ النُّبُوَّةُ وَبَقِيَتْ الْمُبَشِّرَاتُ"
Ametusimulia Haaruwn bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sibaa' bin Thaabit, kutoka kwa Ummu Kurz Al-Ka'biyyah (رضي الله عنها), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Unabii umeondoka, na zimebakia bishara."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1359
- Hadiyth
- 2184
4-Mlangoباب في رؤية النبي صلى الله عليه وسلم في المنامMlango Wa Kuhusu
Kumuona Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Usingizini
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي الْأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ رَآنِي فِي الْمَنَامِ، فَقَدْ رَآنِي، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ لَا يَتَمَثَّلُ مِثْلِي"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeniona usingizini, basi hakika ameniona; kwani shaytwaan hajifananishi na mfano wangu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1359
- Hadiyth
- 2185
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُصَفَّى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ الزُّبَيْدِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ رَآنِي فِي الْمَنَامِ، فَقَدْ رَأَى الْحَقَّ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Muswaffaa, ametusimulia Muhammad bin Harb, kutoka kwa Az-Zubaydiy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Qataadah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeniona usingizini, basi hakika ameiona haki."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1359
- Hadiyth
- 2186
5-Mlangoباب فيمن يرى رؤيا يكرههاMlango Wa Kuhusu Mwenye Kuona Ndoto Anayoichukia
أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ مِنْ اللَّهِ، وَالْحُلْمُ مِنْ الشَّيْطَانِ، فَإِذَا حَلَمَ أَحَدُكُمْ حُلْمًا يَخَافُهُ، فَلْيَبْصُقْ عَنْ شِمَالِهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، وَلْيَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْ الشَّيْطَانِ، فَإِنَّهَا لَا تَضُرُّهُ"
Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, kutoka kwa baba yake [Abuw Qataadah (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ndoto njema inatoka kwa Allaah, na ndoto mbaya inatoka kwa shaytwaan. Basi mmoja wenu akiota ndoto mbaya anayoiogopa, atemee upande wake wa kushoto mara tatu, na ajikinge kwa Allaah kutokana na shaytwaan; kwani hakika hiyo haitamdhuru."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1360
- Hadiyth
- 2187
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ رَبِّهِ بْنِ سَعِيدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا سَلَمَةَ بْنَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ يَقُولُ: إِنْ كُنْتُ لَأَرَى الرُّؤْيَا تُمْرِضُنِي، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِأَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: وَأَنَا إِنْ كُنْتُ لَأَرَى الرُّؤْيَا تُمْرِضُنِي حَتَّى سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الرُّؤْيَا الصَّالِحَةُ مِنْ اللَّهِ، فَإِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مَا يُحِبُّ، فَلْيَحْمَدْ اللَّهَ، وَلَا يُحَدِّثْ بِهَا إِلَّا مَنْ يُحِبُّ، وَإِذَا رَأَى مَا يَكْرَهُه، فَلْيَتْفُلْ عَنْ يَسَارِهِ ثَلَاثًا، وَلْيَتَعَوَّذْ بِاللَّهِ مِنْ شَرِّهَا، وَلَا يُحَدِّثْ بِهَا أَحَدًا، فَإِنَّهَا لَنْ تَضُرَّهُ"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Abdu Rabbih bin Sa'iyd, amesema: Nilimsikia Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan akisema: Hakika nilikuwa naona ndoto ikanitia ugonjwa. Nikamtajia hilo Abuw Qataadah (رضي الله عنه); akasema: Nami nilikuwa naona ndoto ikanitia ugonjwa, mpaka nilipomsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Ndoto njema inatoka kwa Allaah. Basi mmoja wenu akiona anachokipenda, amhimidi Allaah, wala asimsimulie (ndoto hiyo) isipokuwa yule anayempenda. Na akiona anachokichukia, atemee upande wake wa kushoto (mara) tatu, na ajikinge kwa Allaah kutokana na shari yake, wala asimsimulie yeyote; kwani hakika hiyo haitamdhuru kamwe."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1360
- Hadiyth
- 2188
6-Mlangoباب الرؤيا ثلاثMlango Wa Ndoto Ni Aina Tatu
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ مَخْلَدِ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الرُّؤْيَا ثَلَاثٌ: فَالرُّؤْيَا الْحَسَنَةُ بُشْرَى مِنْ اللَّهِ، وَالرُّؤْيَا تَحْزِينٌ مِنْ الشَّيْطَانِ، وَالرُّؤْيَا مِمَّا يُحَدِّثُ بِهِ الْإِنْسَانُ نَفْسَهُ، فَإِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مَا يَكْرَهُهُ، فَلَا يُحَدِّثْ بِهِ، وَلْيَقُمْ، وَلْيُصَلِّ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Makhlad bin Husayn, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ndoto ni (aina) tatu: ndoto nzuri ni bishara kutoka kwa Allaah; na ndoto (nyingine) ni ya kuhuzunisha kutoka kwa shaytwaan; na ndoto (nyingine) ni katika yale anayojisemea mtu nafsini mwake. Basi mmoja wenu akiona anachokichukia, asikisimulie, na asimame aswali."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1361
- Hadiyth
- 2189
7-Mlangoباب أصدق الناس رؤيا أصدقهم حديثاMlango Wa Mkweli Zaidi Wa Watu
Katika Ndoto Ni Mkweli Zaidi Wao Katika Mazungumzo
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، عَنْ مَخْلَدِ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا اقْتَرَبَ الزَّمَانُ، لَمْ تَكَدْ رُؤْيَا الْمُؤْمِنِ تَكْذِبُ، وَأَصْدَقُهُمْ رُؤْيَا أَصْدَقُهُمْ حَدِيثًا"
Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, kutoka kwa Makhlad bin Husayn, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Zama zitakapokaribiana, ndoto ya Muumini haitakaribia kuwa ya uongo. Na mkweli zaidi wao katika ndoto ni mkweli zaidi wao katika mazungumzo."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1362
- Hadiyth
- 2190
8-Mlangoباب النهي عن أن يتحلم الرجل رؤيا لم يرهاMlango Wa Kukatazwa Mtu Kudai Kuota Ndoto Ambayo Hakuiona
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ عَبْدِ الْأَعْلَى، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَلِيٍّ، يَرْفَعُ الْحَدِيثَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَذَبَ فِي حُلْمِهِ، كُلِّفَ عَقْدَ شَعِيرَتَيْنِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa 'Abdul-A'laa, kutoka kwa Abuw 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), anaipandisha Hadiyth mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): "Atakayesema uongo katika ndoto yake, atakalifishwa kufunga fundo (kuziunganisha) punje mbili za shayiri Siku ya Qiyaamah."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1362
- Hadiyth
- 2191
9-Mlangoباب أصدق الرؤيا بالأسحارMlango Wa Ndoto Ya Kweli Zaidi
Ni Ya Nyakati Za Kabla Ya Alfajiri
أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ وَهْبٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ دَرَّاجٍ أَبِي السَّمْحِ، عَنْ أَبِي الْهَيْثَمِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَصْدَقُ الرُّؤْيَا بِالْأَسْحَارِ"
Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Wahb, kutoka kwa 'Amr bin Al-Haarith, kutoka kwa Darraaj Abus-Samh, kutoka kwa Abul-Haytham, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ndoto ya kweli zaidi ni (ile ya) nyakati za kabla ya Alfajiri."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1363
- Hadiyth
- 2192
10-Mlangoباب كراهية أن يعبر الرؤيا إلا على عالم أو ناصحMlango Wa Kuchukiza Kufasiriwa Ndoto Isipokuwa
Kwa Mwenye Ilimu Au Mwenye Kunasihi
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "لَا تَقُصُّوا الرُّؤْيَا إِلَّا عَلَى عَالِمٍ، أَوْ نَاصِحٍ"
Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alikuwa akisema: "Msiisimulie ndoto isipokuwa kwa mwenye ilimu, au mwenye kunasihi."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1364
- Hadiyth
- 2193
11-Mlangoباب الرؤيا لا تقع ما لم تعبرMlango Wa Ndoto Haitokei Maadamu Haijafasiriwa
أَخْبَرَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ يَعْلَى بْنِ عَطَاءٍ، قَالَ: سَمِعْتُ وَكِيعَ بْنَ عُدُسٍ يُحَدِّثُ، عَنْ عَمِّهِ أَبِي رَزِينٍ الْعُقَيْلِيِّ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الرُّؤْيَا هِيَ عَلَى رِجْلِ طَائِرٍ مَا لَمْ يُحَدَّثْ بِهَا، فَإِذَا حُدِّثَ بِهَا، وَقَعَتْ"
Ametukhabarisha Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ya'laa bin 'Atwaa, amesema: Nilimsikia Wakiy' bin 'Udus akisimulia kutoka kwa ammi yake Abuw Raziyn Al-'Uqayliy (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Ndoto iko juu ya mguu wa ndege maadamu haijasimuliwa; inaposimuliwa, hutokea."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1364
- Hadiyth
- 2194
12-Mlangoباب في رؤية الرب تعالى في النومMlango Wa Kuhusu Kumuona Rabb (تعالى) Usingizini
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنِي الْوَلِيدُ بْنُ مُسَلْمِ، حَدَّثَنِي ابْنُ جَابِرٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ اللَّجْلَاجِ، وَسَأَلَهُ مَكْحُولٌ أَنْ يُحَدِّثَهُ قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ عَائِشٍ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "رَأَيْتُ رَبِّي فِي أَحْسَنِ صُورَةٍ، قَالَ: فِيمَ يَخْتَصِمُ الْمَلَأُ الْأَعْلَى؟ فَقُلْتُ: أَنْتَ أَعْلَمُ يَا رَبِّ، قَالَ: فَوَضَعَ كَفَّهُ بَيْنَ كَتِفَيَّ، فَوَجَدْتُ بَرْدَهَا بَيْنَ ثَدْيَيَّ، فَعَلِمْتُ مَا فِي السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ، وَتَلَا: {وَكَذَلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ}"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, amenisimulia Al-Waliyd bin Muslim, amenisimulia Ibn Jaabir, kutoka kwa Khaalid bin Al-Lajlaaj — na Makhuwl alikuwa amemuomba amsimulie —, amesema: Nilimsikia 'Abdur-Rahmaan bin 'Aaish akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Nilimuona Rabb wangu katika umbo zuri kabisa. Akasema: Wakuu watukufu (Malaika) wanakhasimiana kuhusu nini? Nikasema: Wewe Ndiye Mjuzi zaidi, yaa Rabbi." Akasema: "Basi Akaweka Kiganja Chake baina ya mabega yangu, nikahisi ubaridi wake baina ya chuchu zangu; nikajua yaliyomo mbinguni na ardhini." Na akasoma:
وَكَذَلِكَ نُرِي إِبْرَاهِيمَ مَلَكُوتَ السَّمَوَاتِ وَالأَرْضِ وَلِيَكُونَ مِنَ الْمُوقِنِينَ
Na hivyo ndivyo Tunavyomwonyesha Ibraahiym ufalme mkubwa wa mbingu na ardhi na ili awe miongoni mwa wenye yakini. [Al-An’aam (6:75)]
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1365
- Hadiyth
- 2195
أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ قُطْبَةَ، عَنْ يُوسُفَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "مَنْ رَأَى رَبَّهُ فِي الْمَنَامِ، دَخَلَ الْجَنَّةَ"
Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, kutoka kwa 'Abdul-Hamiyd bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Qutwbah, kutoka kwa Yuwsuf, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Atakayemuona Rabb wake usingizini, ataingia Jannah (Pepo)."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1372
- Hadiyth
- 2196
13-Mlangoباب في القمص، والبئر، واللبن، والعسل، والسمن، والتمر، وغير ذلك في النومMlango Wa Kuhusu Kanzu, Kisima, Maziwa, Asali, Samli, Tende
Na Mengineyo Katika Usingizi
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ هُوَ ابْنُ سَعْدٍ، عَنْ صَالِحِ بْنِ كَيْسَانَ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ بْنِ سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "بَيْنَا أَنَا نَائِمٌ، رَأَيْتُ النَّاسَ يُعْرَضُونَ عَلَيَّ وَعَلَيْهِمْ قُمُصٌ، مِنْهَا مَا يَبْلُغُ الثُّدِيَّ، وَمِنْهَا مَا يَبْلُغُ دُونَ ذَلِكَ، وَعُرِضَ عَلَيَّ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ وَعَلَيْهِ قَمِيصٌ يَجُرُّهُ"، فَقَالَ مَنْ حَوْلَهُ: فَمَاذَا تَأَوَّلْتَ ذَلِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: "الدِّينَ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, ametusimulia Ibraahiym — naye ni Ibn Sa'd —, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Abuw Umaamah bin Sahl bin Hunayf, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Nilipokuwa nimelala, niliwaona watu wakionyeshwa mbele yangu nao wamevaa kanzu; miongoni mwazo zipo zinazofika matitini, na miongoni mwazo zipo zinazofika chini ya hapo. Na akaonyeshwa mbele yangu 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) naye amevaa kanzu anaiburuta." Waliokuwa pembeni yake wakasema: Basi umelifasiri hilo kuwa ni nini, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Ni Dini."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1373
- Hadiyth
- 2197
أَخْبَرَنَا أَبُو عَلِيٍّ الْحَنَفِيُّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ هُوَ ابْنُ عُمَرَ، عَنْ نَافِعٍ: أَنَّ ابْنَ عُمَرَ، قَالَ: كُنْتُ فِي عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَا لِي مَبِيتٌ إِلَّا فِي مَسْجِدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَصْبَحَ يَأْتُونَهُ فَيَقُصُّونَ عَلَيْهِ الرُّؤْيَا، قَالَ: فَقُلْتُ: مَا لِي لَا أَرَى شَيْئًا؟ فَرَأَيْتُ كَأَنَّ النَّاسَ يُحْشَرُونَ فَيُرْمَى بِهِمْ عَلَى أَرْجُلِهِمْ فِي رَكِيٍّ فَأُخِذْتُ، فَلَمَّا دَنَا إِلَى الْبِئْرِ، قَالَ رَجُلٌ: خُذُوا بِهِ ذَاتَ الْيَمِينِ، فَلَمَّا اسْتَيْقَظْتُ، هَمَّتْنِي رُؤْيَايَ وَأَشْفَقْتُ مِنْهَا، فَسَأَلْتُ حَفْصَةَ عَنْهَا، فَقَالَتْ: نِعْمَ مَا رَأَيْتَ. فَقُلْتُ لَهَا: سَلِي النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَسَأَلَتْهُ، فَقَالَ: "نِعْمَ الرَّجُلُ عَبْدُ اللَّهِ، لَوْ كَانَ يُصَلِّي مِنْ اللَّيْلِ".
Ametukhabarisha Abuw 'Aliy Al-Hanafiy, ametusimulia 'Abdu-Allaah — naye ni Ibn 'Umar —, kutoka kwa Naafi', kwamba Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: Nilikuwa katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na sikuwa na mahali pa kulala isipokuwa katika Msikiti wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoamka asubuhi, (watu) humjia wakamsimulia ndoto. Akasema: Nikasema: Nina nini mimi, sioni chochote? Basi nikaona kana kwamba watu wanakusanywa, wanatupwa kwa miguu yao ndani ya kisima, nami nikachukuliwa. Ilipokaribia kisimani, mtu mmoja akasema: Mpelekeni upande wa kulia. Nilipoamka, ndoto yangu ilinishughulisha, na nikaiogopa. Nikamuuliza Hafswah (رضي الله عنها) kuhusu ndoto hiyo; akasema: Ni nzuri uliyoiona. Nikamwambia: Muulize Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Akamuuliza; akasema: "Ni mtu mzuri 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه), lau angekuwa akiswali (sehemu) ya usiku."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1374
- Hadiyth
- 2198
حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مُحَمَّدٍ الْفَزَارِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، بِهَذَا الْحَدِيثِ. قَالَ ابْنُ عُمَرَ: وَكُنْتُ إِذَا نِمْتُ، لَمْ أَقُمْ حَتَّى أُصْبِحَ. قَالَ نَافِعٌ: وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ يُصَلِّي اللَّيْلَ
Ametusimulia Muwsaa bin Khaalid, kutoka kwa Ibraahiym bin Muhammad Al-Fazaariy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwa Hadiyth hii. Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) amesema: Na nilikuwa ninapolala, sisimami (kuswali) mpaka asubuhi. Naafi' amesema: Na Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) alikuwa akiswali usiku.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1374
- Hadiyth
- 2199
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ حَمْزَةَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: "بَيْنَا أَنَا نَائِمٌ، إِذْ أُتِيتُ بِقَدَحٍ مِنْ لَبَنٍ فَشَرِبْتُ مِنْهُ، حَتَّى إِنِّي لَأَرَى الرِّيَّ فِي ظُفْرِي أَوْ قَالَ: فِي أَظْفَارِي، ثُمَّ نَاوَلْتُ فَضْلَهُ عُمَرَ"، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا أَوَّلْتَهُ؟ قَالَ: "الْعِلْمَ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Hamzah bin 'Abdi-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Nilipokuwa nimelala, ghafla nililetewa kikombe cha maziwa, nikanywa kutoka humo, mpaka hakika mimi naona ushibe (wa maziwa hayo) katika ukucha wangu — au alisema: katika kucha zangu —; kisha nikampa 'Umar (رضي الله عنه) mabaki yake." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, umeyafasiri kuwa ni nini? Akasema: "Ni ilimu."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1375
- Hadiyth
- 2200
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَخْبَرَنَا الْوَلِيدُ، حَدَّثَنَا ابْنُ جَابِرٍ، حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ قَيْسٍ، حَدَّثَنِي بَعْضُ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "اللَّبَنُ الْفِطْرَةُ، وَالسَّفِينَةُ نَجَاةٌ، وَالْجَمَلُ حُزْنٌ، وَالْخُضْرَةُ الْجَنَّةُ، وَالْمَرْأَةُ خَيْرٌ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametukhabarisha Al-Waliyd, ametusimulia Ibn Jaabir, amenisimulia Muhammad bin Qays, amenisimulia mmoja wa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Maziwa ni Fitwrah (maumbile ya asili), na jahazi ni kuokoka, na ngamia ni huzuni, na rangi ya kijani ni Jannah (Pepo), na mwanamke ni kheri."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1375
- Hadiyth
- 2201
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ هُوَ ابْنُ كَثِيرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ مِمَّا يَقُولُ لِأَصْحَابِهِ: "مَنْ رَأَى مِنْكُمْ رُؤْيَا، فَلْيَقُصَّهَا عَلَيَّ فَأَعْبُرَهَا لَهُ". قَالَ: فَجَاءَ رَجُلٌ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، رَأَيْتُ ظُلَّةً بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ تَنْطِفُ عَسَلًا وَسَمْنًا، وَرَأَيْتُ سَبَبًا وَاصِلًا مِنْ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ، وَرَأَيْتُ أُنَاسًا يَتَكَفَّفُونَ مِنْهَا، فَمُسْتَكْثِرٌ وَمُسْتَقِلٌّ، وَرَأَيْتُ سَبَبًا وَاصِلًا مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ، فَأَخَذْتَ بِهِ فَعَلَوْتَ، فَأَعْلَاكَ اللَّهُ، ثُمَّ أَخَذَ بِهِ الَّذِي بَعْدَكَ فَعَلَا، فَأَعْلَاهُ اللَّهُ، ثُمَّ أَخَذَهُ الَّذِي بَعْدَهُ فَعَلَا، فَأَعْلَاهُ اللَّهُ، ثُمَّ أَخَذَهُ الَّذِي بَعْدَهُ فَقُطِعَ بِهِ، ثُمَّ وُصِلَ فَاتَّصَلَ. فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، ائْذَنْ لِي فَأَعْبُرَهَا، فَقَالَ: اعْبُرْهَا. وَكَانَ أَعْبَرَ النَّاسِ لِلرُّؤْيَا بَعْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَمَّا الظُّلَّةُ فَالْإِسْلَامُ، وَأَمَّا الْعَسَلُ وَالسَّمْنُ فَالْقُرْآنُ: حَلَاوَةُ الْعَسَلِ وَلِينُ السَّمْنِ، وَأَمَّا الَّذِينَ يَتَكَفَّفُونَ مِنْهُ، فَمُسْتَكْثِرٌ وَمُسْتَقِلٌّ فَهُمْ حَمَلَةُ الْقُرْآنِ، وَأَمَّا السَّبَبُ الْوَاصِلُ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الأَرْضِ فَالْحَقُّ الَّذِي أَنْتَ عَلَيْهِ، تَأْخُذُ بِهِ فَيُعْليكَ اللهُ بِهِ، ثُمَّ يَأْخُذُ بِهِ رَجُلٌ مِنْ بَعْدِكَ فَيَعْلُو بِهِ، ثُمَّ يَأَخُذُ بِهِ رَجُلٌ آخَرُ فَيَعْلُو بِهِ، ثُمَّ يَأْخُذُ بِهِ رَجُلٌ آخَرُ فَيَنْقَطِعُ بِهِ، ثُمَّ يُوصَلُ لَهُ فَيَعْلُو بِهِ، فَأَخْبِرْني يَا رَسُولَ اللَّهِ بِأَبِي أَنْتَ أَصَبْتُ أَمْ أَخْطَأْتُ، فَقَالَ: "أَصَبْتَ وَأَخْطَأْتَ". فَقَالَ: فَمَا الَّذِي أَصَبْتُ وَمَا الَّذِي أَخْطَأْتُ؟ فَأَبَى أَنْ يُخْبِرَهُ
Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, ametusimulia Sulaymaan — naye ni Ibn Kathiyr —, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ilikuwa miongoni mwa aliyokuwa akiwaambia Swahaba wake (رضي الله عنهم): "Atakayeona ndoto miongoni mwenu, basi anisimulie, nami nitamfasiria." Akasema: Akaja mtu mmoja, akasema: Yaa Rasula-Allaah, nimeona wingu (lenye kivuli) baina ya mbingu na ardhi likidondosha asali na samli; na nimeona kamba iliyounganika kutoka mbinguni mpaka ardhini; na nimeona watu wakichota kwa viganja vyao kutoka humo: basi (yupo) anayechukua mengi na (yupo) anayechukua machache; na nimeona kamba iliyounganika kutoka mbinguni mpaka ardhini. Ukaishika ukapanda juu, na Allaah Akakupandisha juu; kisha akaishika aliye baada yako akapanda juu, na Allaah Akampandisha juu; kisha akaishika aliye baada yake akapanda juu, na Allaah Akampandisha juu; kisha akaishika aliye baada yake, ikakatika naye, kisha ikaungwa ikaungana. Abuw Bakr (رضي الله عنه) akasema: Yaa Rasula-Allaah, niruhusu niifasiri. Akasema: "Ifasiri." — Na yeye alikuwa ndiye mjuzi zaidi wa watu wa kufasiri ndoto baada ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —. Akasema: Ama wingu, ni Islaam; na ama asali na samli, ni Qur-aan: utamu wa asali na ulaini wa samli; na ama wale wanaochota kwa viganja vyao kutoka humo, basi anayechukua mengi na anayechukua machache, hao ni wabebaji wa Qur-aan; na ama kamba iliyounganika kutoka mbinguni mpaka ardhini, ni haki uliyo juu yake: unaishika, na Allaah Anakupandisha juu kwayo; kisha ataishika mtu baada yako, apande juu kwayo; kisha ataishika mtu mwingine, apande juu kwayo; kisha ataishika mtu mwingine, ikatike naye; kisha ataungiwa (kamba hiyo), apande juu kwayo. Basi nikhabarishe, yaa Rasula-Allaah — (nakufidia) kwa baba yangu — je, nimepatia au nimekosea? Akasema: "Umepatia na umekosea." Akasema: Basi ni kipi nilichopatia, na ni kipi nilichokosea? Akakataa kumkhabarisha.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1376
- Hadiyth
- 2202
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ مِهْرَانَ، حَدَّثَنَا مِسْكِينٌ الْحَرَّانِيُّ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ بُرْقَانَ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ الْأَصَمِّ، عَنْ الْعَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، فَقَالَ: رَأَيْتُ فِي الْمَنَامِ كَأَنَّ شَمْسًا أَوْ قَمَرًا شَكَّ أَبُو جَعْفَرٍ فِي الْأَرْضِ تُرْفَعُ إِلَى السَّمَاءِ بِأَشْطَانٍ شِدَادٍ، فَذَكَرَ ذَلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: "ذَاكَ وَفَاةُ ابْنُ أَخِيكَ يَعْنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَفْسَهُ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Mihraan, ametusimulia Miskiyn Al-Harraaniy, kutoka kwa Ja'far bin Burqaan, kutoka kwa Yaziyd bin Al-Aswamm, kutoka kwa Al-'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه), akasema: Niliona usingizini kana kwamba jua — au mwezi; Abuw Ja'far alitia shaka — lililo ardhini linainuliwa kwenda mbinguni kwa kamba ndefu zenye nguvu. Akamtajia hilo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); akasema: "Hiyo ni kufariki kwa mwana wa ndugu yako" — anakusudia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) nafsi yake.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1377
- Hadiyth
- 2203
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ بَرِيدَ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "رَأَيْتُ فِي رُؤْيَايَ هَذِهِ أَنِّي هَزَزْتُ سَيْفًا فَانْقَطَعَ صَدْرُهُ، فَإِذَا هُوَ مَا أُصِيبَ مِنْ الْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ أُحُدٍ، ثُمَّ هَزَزْتُهُ أُخْرَى فَعَادَ كَأَحْسَنِ مَا كَانَ، فَإِذَا هُوَ مَا جَاءَ اللَّهُ بِهِ مِنْ الْفَتْحِ وَاجْتِمَاعِ الْمُؤْمِنِينَ، وَرَأَيْتُ فِيهَا أَيْضًا بَقَرًا وَاللَّهِ خَيْرٌ، فَإِذَا هُوَ النَّفَرُ مِنْ الْمُؤْمِنِينَ يَوْمَ أُحُدٍ، وَإِذَا الْخَيْرُ مَا جَاءَ اللَّهُ بِهِ مِنْ الْخَيْرِ، وَثَوَابِ الصِّدْقِ الَّذِي آتَانَا بَعْدَ يَوْمِ بَدْرٍ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Burayd, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Niliona katika ndoto yangu hii kwamba nimeutikisa upanga, ukakatika sehemu yake ya juu; kumbe hiyo ni yale yaliyowapata Waumini siku ya (vita vya) Uhud. Kisha nikautikisa mara nyingine, ukarudi kuwa bora kama ulivyokuwa; kumbe hiyo ni yale Aliyoyaleta Allaah ya ushindi na kukusanyika kwa Waumini. Na niliona humo pia ng'ombe, na Allaah ni kheri; kumbe hao ni kundi la Waumini siku ya Uhud, na kumbe kheri ni ile kheri Aliyoileta Allaah, na thawabu za ukweli Alizotupa baada ya siku ya (vita vya) Badr."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1377
- Hadiyth
- 2204
أَخْبَرَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "رَأَيْتُ كَأَنِّي فِي دِرْعٍ حَصِينَةٍ، وَرَأَيْتُ بَقَرًا يُنْحَرُ، فَأَوَّلْتُ أَنَّ الدِّرْعَ الْمَدِينَةُ، وَأَنَّ الْبَقَرَ نَفَرٌ، وَاللَّهِ خَيْرٌ، وَلَوْ أَقَمْنَا بِالْمَدِينَةِ، فَإِذَا دَخَلُوا عَلَيْنَا، قَاتَلْنَاهُمْ". فَقَالُوا: وَاللَّهِ مَا دُخِلَتْ عَلَيْنَا فِي الْجَاهِلِيَّةِ أَفَتُدْخَلُ عَلَيْنَا فِي الْإِسْلَامِ؟ قَالَ: "فَشَأْنَكُمْ إِذًا". وَقَالَتْ الْأَنْصَارُ بَعْضُهَا لِبَعْضٍ: رَدَدْنَا عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأْيَهُ، فَجَاءُوا، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ شَأْنُكَ، فَقَالَ: "الْآنَ؟ إِنَّهُ لَيْسَ لِنَبِيٍّ إِذَا لَبِسَ لَأْمَتَهُ أَنْ يَضَعَهَا حَتَّى يُقَاتِلَ"
Ametukhabarisha Al-Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Niliona kana kwamba niko ndani ya deraya madhubuti, na niliona ng'ombe wakichinjwa. Nikafasiri kwamba deraya ni Madiynah, na kwamba ng'ombe ni kundi la watu, na Allaah ni kheri. Na lau tungebakia Madiynah, basi wakituingilia, tutapigana nao." Wakasema: Wa-Allaahi, (mji wetu) haukuingiliwa juu yetu katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam); je, utaingiliwa juu yetu katika Islaam? Akasema: "Basi (fanyeni) jambo lenu hapo." Na Answaar (رضي الله عنهم) wakaambiana wao kwa wao: Tumemrudishia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) rai yake. Wakaja, wakasema: Yaa Rasula-Allaah, (fanya) jambo lako. Akasema: "Sasa? Hakika haimfai Nabiy, akishavaa deraya yake, aivue mpaka apigane."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1378
- Hadiyth
- 2205
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: "أَكْرَهُ الْغُلَّ، وَأُحِبُّ الْقَيْدَ، الْقَيْدُ ثَبَاتٌ فِي الدِّينِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alikuwa akisema: "Nachukia pingu ya shingoni, na napenda pingu ya miguuni; pingu ya miguuni ni uthabiti katika Dini."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1379
- Hadiyth
- 2206
أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ الْهَاشِمِيُّ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ مُوسَى بْنِ عُقْبَةَ، عَنْ سَالِمِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "رَأَيْتُ فِي الْمَنَامِ امْرَأَةً سَوْدَاءَ ثَائِرَةَ الشَّعْرِ تَفِلَةً، أُخْرِجَتْ مِنْ الْمَدِينَةِ فَأُسْكِنَتْ مَهْيَعَةَ، فَأَوَّلْتُهَا وَبَاءَ الْمَدِينَةِ يَنْقُلُهَا اللَّهُ إِلَى مَهْيَعَةَ"
Ametukhabarisha Sulaymaan bin Daawuwd Al-Haashimiy, ametusimulia Ibn Abiz-Zinaad, kutoka kwa Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Saalim bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)], amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Niliona usingizini mwanamke mweusi, mwenye nywele timtimu, mwenye harufu mbaya, akitolewa Madiynah, kisha akawekwa Mahya'ah [Al-Juhfah]. Nikaifasiri (ndoto hiyo) kuwa ni maradhi ya mlipuko ya Madiynah, Allaah Anayahamishia Mahya'ah."
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1379
- Hadiyth
- 2207
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، حَدَّثَنَا عَبِيدَةُ بْنُ الْأَسْوَدِ، عَنْ مُجَالِدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ جَابِرٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ يَوْمًا مِنْ الْأَيَّامِ: "إِنِّي رَأَيْتُ فِي الْمَنَامِ أَنَّ رَجُلًا أَتَانِي بِكُتْلَةٍ مِنْ تَمْرٍ فَأَكَلْتُهَا، فَوَجَدْتُ فِيهَا نَوَاةً، فَآذَتْنِي حِينَ مَضَغْتُهَا، ثُمَّ أَعْطَانِي كُتْلَةً أُخْرَى، فَقُلْتُ: إِنَّ الَّذِي أَعْطَيْتَنِي وَجَدْتُ فِيهَا نَوَاةً آذَتْنِي فَأَكَلْتُهَا". فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: نَامَتْ عَيْنُكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَذِهِ السَّرِيَّةُ الَّتِي بَعَثْتَ بِهَا، غَنِمُوا مَرَّتَيْنِ كِلْتَاهُمَا وَجَدُوا رَجُلًا يَنْشُدُ ذِمَّتَكَ. فَقُلْتُ لِمُجَالِدٍ: مَا يَنْشُدُ ذِمَّتَكَ؟ قَالَ: يَقُولُ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Yahyaa bin 'Abdir-Rahmaan, ametusimulia 'Abiydah bin Al-Aswad, kutoka kwa Mujaalid, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisema siku moja miongoni mwa siku: "Hakika mimi niliona usingizini kwamba mtu mmoja amenijia na donge la tende, nikalila; nikakuta ndani yake kokwa, ikaniudhi nilipolitafuna. Kisha akanipa donge jingine; nikasema: Hakika lile ulilonipa nimekuta ndani yake kokwa iliyoniudhi; nikalila." Abuw Bakr (رضي الله عنه) akasema: Jicho lako lilale (kwa utulivu), yaa Rasula-Allaah. Hiki ni kikosi ulichokituma: wamepata ngawira mara mbili; mara zote mbili walimkuta mtu anayeomba ahadi ya ulinzi wako. Nikamwambia Mujaalid: Ni nini 'anayeomba ahadi ya ulinzi wako'? Akasema: Anasema: Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1380
- Hadiyth
- 2208
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ بْنُ يَعِيشَ، حَدَّثَنَا يُونُسُ هُوَ ابْنُ بُكَيْرٍ، أَخْبَرَنَا ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ عَطَاءٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ عَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: كَانَتْ امْرَأَةٌ مِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَهَا زَوْجٌ تَاجِرٌ يَخْتَلِفُ، فَكَانَتْ تَرَى رُؤْيَا كُلَّمَا غَابَ عَنْهَا زَوْجُهَا، وَقَلَّمَا يَغِيبُ إِلَّا تَرَكَهَا حَامِلًا، فَتَأْتِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَتَقُولُ: إِنَّ زَوْجِي خَرَجَ تَاجِرًا فَتَرَكَنِي حَامِلًا، فَرَأَيْتُ فِيمَا يَرَى النَّائِمُ: أَنَّ سَارِيَةَ بَيْتِي انْكَسَرَتْ، وَأَنِّي وَلَدْتُ غُلَامًا أَعْوَرَ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "خَيْرٌ، يَرْجِعُ زَوْجُكِ عَلَيْكِ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَعَالَى صَالِحًا، وَتَلِدِينَ غُلَامًا بَرًّا". فَكَانَتْ تَرَاهَا مَرَّتَيْنِ أَوْ ثَلَاثًا، كُلُّ ذَلِكَ تَأْتِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَيَقُولُ ذَلِكَ لَهَا فَيَرْجِعُ زَوْجُهَا، وَتَلِدُ غُلَامًا، فَجَاءَتْ يَوْمًا كَمَا كَانَتْ تَأْتِيهِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غَائِبٌ، وَقَدْ رَأَتْ تِلْكَ الرُّؤْيَا، فَقُلْتُ لَهَا: عَمَّ تَسْأَلِينَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَا أَمَةَ اللَّهِ؟ فَقَالَتْ: رُؤْيَا كُنْتُ أُرَاهَا، فَآتِي رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَسْأَلُهُ عَنْهَا فَيَقُولُ خَيْرًا، فَيَكُونُ كَمَا قَالَ. فَقُلْتُ: فَأَخْبِرِينِي مَا هِيَ. قَالَتْ: حَتَّى يَأْتِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَعْرِضَهَا عَلَيْهِ كَمَا كُنْتُ أَعْرِضُ. فَوَاللَّهِ مَا تَرَكْتُهَا حَتَّى أَخْبَرَتْنِي، فَقُلْتُ: وَاللَّهِ لَئِنْ صَدَقَتْ رُؤْيَاكِ، لَيَمُوتَنَّ زَوْجُكِ وَتَلِدِينَ غُلَامًا فَاجِرًا، فَقَعَدَتْ تَبْكِي، وَقَالَتْ مَا لِي حِينَ عَرَضْتُ عَلَيْكِ رُؤْيَايَ؟ فَدَخَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهِيَ تَبْكِي، فَقَالَ لَهَا: مَا لَهَا يَا عَائِشَةُ؟ فَأَخْبَرْتُهُ الْخَبَرَ وَمَا تَأَوَّلْتُ لَهَا. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَهْ يَا عَائِشَةُ، إِذَا عَبَرْتُمْ لِلْمُسْلِمِ الرُّؤْيَا، فَاعْبُرُوهَا عَلَى الْخَيْرِ، فَإِنَّ الرُّؤْيَا تَكُونُ عَلَى مَا يَعْبُرُهَا صَاحِبُهَا". فَمَاتَ وَاللَّهِ زَوْجُهَا، وَلَا أُرَاهَا إِلَّا وَلَدَتْ غُلَامًا فَاجِرًا
Ametukhabarisha 'Ubayd bin Ya'iysh, ametusimulia Yuwnus — naye ni Ibn Bukayr —, ametukhabarisha Ibn Is-haaq, kutoka kwa Muhammad bin 'Amr bin 'Atwaa, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Alikuwa mwanamke mmoja miongoni mwa watu wa Madiynah, ana mume mfanyabiashara anayesafiri (huku na huko). Basi alikuwa akiona ndoto kila mumewe anapokuwa hayupo; na ni nadra (mumewe) kusafiri isipokuwa humwacha akiwa mjamzito. Basi humjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), husema: Hakika mume wangu ametoka kwa biashara, akaniacha mjamzito; nikaona katika yale anayoyaona aliyelala kwamba nguzo ya nyumba yangu imevunjika, na kwamba nimezaa mtoto wa kiume mwenye chongo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ni kheri; mume wako atarejea kwako, Akipenda Allaah (تعالى), akiwa mwema, na utazaa mtoto wa kiume mwema." Basi alikuwa akiiona (ndoto hiyo) mara mbili au tatu; kila mara humjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), naye humwambia hivyo; basi mumewe hurejea, na huzaa mtoto wa kiume. Siku moja akaja kama alivyokuwa akimjia, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hayupo, naye ameiona ndoto ile. Nikamwambia: Unamuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu nini, yaa Amata-Allaah? Akasema: Ni ndoto niliyokuwa nikiiona, kisha namjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), namuuliza kuhusu ndoto hiyo, naye husema kheri, nayo huwa kama alivyosema. Nikasema: Basi nikhabarishe ni ipi. Akasema: (Sikukhabarishi) mpaka aje Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nimuonyeshe kama nilivyokuwa nikimuonyesha. Basi Wa-Allaahi, sikumwacha mpaka akanikhabarisha. Nikasema: Wa-Allaahi, ikiwa ndoto yako ni ya kweli, hakika mume wako atakufa, na utazaa mtoto wa kiume muovu. Akakaa akilia, na akasema: Nina nini mimi nilipokuonyesha ndoto yangu? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingia naye analia; akasema kuhusu yeye: "Ana nini, yaa 'Aaishah?" Nikamkhabarisha khabari, na yale niliyomfasiria. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Acha, yaa 'Aaishah! Mtakapomfasiria Muislamu ndoto, basi ifasirini kwa kheri; kwani hakika ndoto huwa kama anavyoifasiri mwenyewe." Basi Wa-Allaahi, mumewe alikufa; na sidhani isipokuwa kwamba alizaa mtoto wa kiume muovu.
- Mjalada
- 2
- Kitabu
- 10
- Ukurasa
- 1380
- Hadiyth
- 2209