Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy11 - Kitabu Cha Nikaah

ومن كتاب النكاح

1-Mlangoباب الحث على التزويجMlango Wa Kuhimiza Kuoa

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْج، عَنْ أَبِي الْمُغَلِّسِ، عَنْ أَبِي نَجِيحٍ، قَال: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ قَدَرَ عَلَى أًنّ يَنْكِح، فَلَمْ يَنْكِحْ، فَلَيْسَ مِنَّا"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abul-Mughallis, kutoka kwa Abuw Najiyh, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwenye kuweza kuoa, kisha asioe, basi huyo si katika sisi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1383
Hadiyth
2210

2-Mlangoباب من كان عنده طول فليتزوجMlango Wa Aliye Na Uwezo, Basi Na Aoe

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ عُمَارَة، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، قَال: قَالَ عَبْدُ اللَّه: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَبَابًا لَيْسَ لَنَا شَيْءٌ، فَقَال: "يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمُ الْبَاءَة، فَلْيَتَزَوَّجْ فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ، فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّ الصَّوْمَ لَهُ وِجَاءٌ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa 'Umaarah, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) tukiwa vijana, hatuna kitu chochote. Akasema: "Enyi kongamano la vijana! Atakayeweza miongoni mwenu gharama za ndoa, basi aoe; kwani hakika hilo ni zuri zaidi katika kuinamisha macho, na ni hifadhi zaidi kwa tupu. Na asiyeweza, basi ni juu yake kufunga Swawm, kwani hakika Swawm ni kinga kwake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1383
Hadiyth
2211

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَة، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: لَقِيَهُ عُثْمَانُ وَأَنَا مَعَهُ، فَقَالَ لَهُ: أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ هَلْ لَكَ فِي جَارِيَةٍ بِكْرٍ تُذَكِّرُك؟، فَقَالَ: لَئِنْ قُلْتَ: ذَاكَ فَقَدْ سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمْ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَلْيَصُمْ فَإِنَّ الصَّوْمَ لَهُ وِجَاءٌ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: 'Uthmaan (رضي الله عنه) alikutana naye nami nikiwa pamoja naye, akamwambia: Abaa 'Abdir-Rahmaan, je, una haja ya msichana bikra atakayekukumbusha (yaliyopita)? Akasema: Ikiwa umesema hivyo, basi kwa hakika nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Enyi kongamano la vijana! Atakayeweza miongoni mwenu gharama za ndoa, basi aoe; kwani hakika hilo ni zuri zaidi katika kuinamisha macho, na ni hifadhi zaidi kwa tupu. Na asiyeweza, basi afunge Swawm, kwani hakika Swawm ni kinga kwake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1384
Hadiyth
2212

3-Mlangoباب في النهي عن التبتلMlango Wa Kuhusu Katazo La At-Tabattul (Kujitenga
Na Wanawake Kwa Ajili Ya Ibaada)

أَخْبَرَنَا أَبُو الْيَمَانِ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ، أَنَّهُ سَمِعَ سَعْدَ بْنَ أَبِي وَقَّاصٍ، يَقُولُ: "لَقَدْ رَدَّ ذَلِكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى عُثْمَانَ، وَلَوْ أَجَازَ لَهُ التَّبَتُّلَ، لَاخْتَصَيْنَا"

Ametukhabarisha Abul-Yamaan, ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib, kwamba alimsikia Sa'd bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه) akisema: "Kwa hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkatalia 'Uthmaan [bin Madhw'uwn] (رضي الله عنه) hilo; na lau angemruhusu At-Tabattul (kujitenga na wanawake kwa ajili ya ibaada), tungejihasi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1385
Hadiyth
2213

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ مَسْعَدَةَ، حَدَّثَنَا الْأَشْعَثُ بْنُ عَبْدِ الْمَلِكِ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَعْدِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ التَّبَتُّلِ"

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Hammaad bin Mas'adah, ametusimulia Al-Ash'ath bin 'Abdil-Malik, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Sa'd bin Hishaam, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza At-Tabattul (kujitenga na wanawake kwa ajili ya ibaada)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1385
Hadiyth
2214

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ بُكَيْرٍ، حَدَّثَنِي ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، قَالَ: لَمَّا كَانَ مِنْ أَمْرِ عُثْمَانَ بْنِ مَظْعُونٍ الَّذِي كَانَ مِنْ تَرْكِ النِّسَاءِ، بَعَثَ إِلَيْهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَا عُثْمَانُ إِنِّي لَمْ أُومَرْ بِالرَّهْبَانِيَّةِ أَرَغِبْتَ عَنْ سُنَّتِي؟"، قَالَ: لَا، يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: "إِنَّ مِنْ سُنَّتِي أَنْ أُصَلِّي، وَأَنَام، وَأَصُومَ، وَأَطْعَمَ، وَأَنْكِحَ، وَأُطَلِّقَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي، فَلَيْسَ مِنِّي يَا عُثْمَانُ، إِنَّ لِأَهْلِكَ عَلَيْكَ حَقًّا، وَلِنَفْسِكَ عَلَيْكَ حَقًّا". قَالَ سَعْدٌ: فَوَاللَّهِ لَقَدْ كَانَ أَجْمَعَ رِجَالٌ مِنَ الْمُسْلِمِينَ عَلَى أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِنْ هُوَ أَقَرَّ عُثْمَانَ عَلَى مَا هُوَ عَلَيْهِ أَنْ نَخْتَصِيَ فَنَتَبَتَّلَ

Ametusimulia Muhammad bin Yaziyd Al-Hizaamiy, ametusimulia Yuwnus bin Bukayr, amenisimulia Ibn Is-haaq, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Sa'd bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه), amesema: Lilipotokea lile jambo la 'Uthmaan bin Madhw'uwn (رضي الله عنه) la kuwaacha wanawake, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtumia (mjumbe), akasema: "Yaa 'Uthmaan, hakika mimi sikuamrishwa uruhubani (maisha ya utawa). Je, umeichukia Sunnah yangu?" Akasema: Hapana, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Hakika miongoni mwa Sunnah yangu ni kwamba ninaswali na ninalala, ninafunga Swawm na ninakula, ninaoa na ninataliki. Basi atakayeichukia Sunnah yangu, si katika mimi. Yaa 'Uthmaan, hakika ahli yako wana haki juu yako, na nafsi yako ina haki juu yako." Sa'd (رضي الله عنه) amesema: Basi Wa-Allaahi, kwa hakika wanaume kadhaa miongoni mwa Waislamu walikuwa wameazimia kwamba, ikiwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) atamkubalia 'Uthmaan (رضي الله عنه) (kubaki) katika hali aliyokuwa nayo, tujihasi na tujitenge na wanawake (kwa ajili ya ibaada).

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1386
Hadiyth
2215

4-Mlangoباب تنكح المرأة على أربعMlango Wa Mwanamke Huolewa Kwa Sababu Nne

حَدَّثَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "تُنْكَحُ النِّسَاءُ لِأَرْبَعٍ: لِلدِّينِ، وَالْجَمَالِ، وَالْمَالِ، وَالْحَسَبِ، فَعَلَيْكَ بِذَاتِ الدِّينِ تَرِبَتْ يَدَاك".

Ametusimulia Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametupa khabari Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Wanawake huolewa kwa (sababu) nne: kwa dini, na uzuri, na mali, na heshima ya nasaba. Basi shikamana na mwenye dini; mikono yako ijae udongo!"

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1387
Hadiyth
2216

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ، عَنْ جَابِرٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم، بِهَذَا الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa bin Abiy Rabaah, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1388
Hadiyth
2217

5-Mlangoباب الرخصة في النظر إلى المرأة عند الخطبةMlango Wa Ruhusa Ya Kumtazama Mwanamke Wakati Wa Kuposa

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَاصِمٍ الْأَحْوَلِ، عَنْ بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْمُزَنِي، عَنْ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ أَنَّهُ خَطَبَ امْرَأَةً مِنَ الْأَنْصَارِ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اذْهَبْ، فَانْظُرْ إِلَيْهَا، فَإِنَّهُ أَجْدَرُ أَنْ يُؤْدَمَ بَيْنَكُمَا"

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Aaswim Al-Ahwal, kutoka kwa Bakr bin 'Abdi-Allaah Al-Muzaniy, kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه), kwamba alimposa mwanamke miongoni mwa Answaar (رضي الله عنهم). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Nenda ukamtazame, kwani hilo linastahiki zaidi kudumisha mapatano (na mapenzi) baina yenu wawili."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1389
Hadiyth
2218

6-Mlangoباب إذا تزوج الرجل ما يقال لهMlango Wa Mtu Anapooa, Huambiwa Nini

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ الْعَبْدِيُّ الْبَصْرِيُّ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ الْحَسَنِ، قَالَ: سَمِعْتُهُ يَقُولُ: قَدِمَ عَقِيلُ بْنُ أَبِي طَالِبٍ الْبَصْرَةَ، فَتَزَوَّجَ امْرَأَةً مِنْ بَنِي جُشَمٍ، فَقَالُوا لَهُ: بِالرِّفَاءِ وَالْبَنِينَ، فَقَالَ: لَا تَقُولُوا ذَلِكَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَانَا عَنْ ذَلِكَ، وَأَمَرَنَا أَنْ نَقُولَ: "بَارَكَ اللهُ لَكَ، وَبَارَكَ عَلَيْكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr Al-'Abdiy Al-Baswriy, ametukhabarisha Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: Nilimsikia akisema: 'Aqiyl bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه) aliwasili Al-Baswrah, akaoa mwanamke wa Banuw Jusham. Wakamwambia: (Iwe) kwa maelewano na (kupata) watoto wa kiume! Akasema: Msiseme hivyo; hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitukataza hilo, na akatuamrisha tuseme:

بَارَكَ اللهُ لَكَ، وَبَارَكَ عَلَيْكَ

Allaah Akubariki na Abariki juu yako.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1389
Hadiyth
2219

حَدَّثَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ، عَنْ سُهَيْلٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ كَانَ إِذَا رَفَّأَ لِإِنْسَانٍ، قَالَ: "بَارَكَ اللَّهُ لَكَ، وَبَارَكَ عَلَيْكَ، وَجَمَعَ بَيْنَكُمَا فِي خَيْرٍ"

Ametusimulia Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz, kutoka kwa Suhayl, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alikuwa anapompongeza mtu (aliyeoa), husema:

بَارَكَ اللَّهُ لَكَ، وَبَارَكَ عَلَيْكَ، وَجَمَعَ بَيْنَكُمَا فِي خَيْرٍ

Allaah Akubariki na Abariki juu yako, na Awajumuishe katika kheri.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1390
Hadiyth
2220

7-Mlangoباب النهي عن خطبة الرجل على خطبة أخيهMlango Wa Katazo La Mtu Kuposa Juu Ya Posa Ya Nduguye

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سُهَيْلِ بْنِ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَّهُ نَهَى عَنْ أَنْ يَخْطُبَ الرَّجُلُ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Suhayl bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba: "Alikataza mtu kuposa juu ya posa ya nduguye."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1392
Hadiyth
2221

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، قَالَ: حَدَّثَنِي نَافِعٌ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا يَخْطُبْ أَحَدُكُمْ عَلَى خِطْبَةِ أَخِيهِ وَلَا يَبِيعُ عَلَى بَيْعِ أَخِيهِ حَتَّى يَأْذَنَ لَهُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, amesema: Amenisimulia Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu asipose juu ya posa ya nduguye, wala asiuze juu ya mauzo ya nduguye, mpaka ampe idhini."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1392
Hadiyth
2222

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ فَاطِمَةَ بِنْتِ قَيْسٍ: أَنَّهَا حَدَّثَتْهُ وَكَتَبَهُ مِنْهَا كِتَابًا أَنَّهَا كَانَتْ تَحْتَ رَجُلٍ مِنْ قُرَيْشٍ، مِنْ بَنِي مَخْزُومٍ، فَطَلَّقَهَا الْبَتَّةَ، فَأَرْسَلَتْ إِلَى أَهْلِهِ تَبْتَغِي مِنْهُمُ النَّفَقَةَ، فَقَالُوا: لَيْسَ لَكِ نَفَقَةٌ، فَبَلَغَ ذَلِكَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "لَيْسَ لَكِ نَفَقَةٌ، وَعَلَيْكِ الْعِدَّةُ، وَانْتَقِلِي إِلَى بَيْتِ أُمِّ شَرِيكٍ، وَلَا تُفَوِّتِينَا بِنَفْسِكِ"، ثُمَّ قَالَ: "إِنَّ أُمَّ شَرِيكٍ امْرَأَةٌ يَدْخُلُ عَلَيْهَا إِخْوَانُهَا مِنَ الْمُهَاجِرِينَ، وَلَكِنِ انْتَقِلِي إِلَى بَيْتِ ابْنِ أُمِّ مَكْتُومٍ فَإِنَّهُ رَجُلٌ أَعْمَى، إِنْ وَضَعْتِ ثِيَابَكِ لَمْ يَرَ شَيْئًا وَلَا تُفَوِّتِينَا بِنَفْسِكِ"، فَانْطَلَقَتْ إِلَى بَيْتِ ابْنِ أُمِّ مَكْتُومٍ فَلَمَّا حَلَّتْ، ذَكَرَتْ أَنَّ مُعَاوِيَةَ، وَأَبَا جَهْمٍ خَطَبَاهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَمَّا مُعَاوِيَةُ، فَرَجُلٌ لَا مَالَ لَهُ، وَأَمَّا أَبُو جَهْمٍ، فَلَا يَضَعُ عَصَاهُ عَنْ عَاتِقِهِ، فَأَيْنَ أَنْتِ مِنْ أُسَامَةَ؟" فَكَأَنَّ أَهْلَهَا كَرِهُوا ذَلِكَ، فَقَالَتْ: وَاللَّهِ لَا أَنْكِحُ إِلَّا الَّذِي قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَنَكَحَتْ أُسَامَةَ. قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو: قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ: يَا فَاطِمَةُ، اتَّقِي اللَّهَ، فَقَدْ عَلِمْتِ فِي أَيِّ شَيْءٍ كَانَ هَذَا، قَالَ: وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: {يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ وَاتَّقُوا اللَّهَ رَبَّكُمْ لا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلا يَخْرُجْنَ إِلا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ} وَالْفَاحِشَةُ أَنْ تَبْذُوَ عَلَى أَهْلِهَا، فَإِذَا فَعَلَتْ ذَلِكَ، فَقَدْ حَلَّ لَهُمْ أَنْ يُخْرِجُوهَا

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Faatwimah bint Qays (رضي الله عنها), kwamba yeye alimsimulia — naye aliiandika kutoka kwake maandishi —, kwamba alikuwa chini ya mtu mmoja wa Quraysh, wa Banuw Makhzuwm, akamtaliki talaka ya mwisho. Akatuma (mjumbe) kwa jamaa zake akitaka kutoka kwao matumizi; wakasema: Huna matumizi. Hilo likamfikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Huna matumizi, na juu yako ni eda. Na hamia nyumba ya Ummu Shariyk (رضي الله عنها), wala usijiamulie jambo la nafsi yako bila sisi." Kisha akasema: "Hakika Ummu Shariyk (رضي الله عنها) ni mwanamke ambaye ndugu zake miongoni mwa Muhaajiruwn (waliohajiri kwenda Madiynah) (رضي الله عنهم) huingia kwake. Lakini hamia nyumba ya Ibn Ummi Maktuwm (رضي الله عنه), kwani yeye ni mtu kipofu; ukivua nguo zako, hataona kitu. Wala usijiamulie jambo la nafsi yako bila sisi." Akaenda nyumbani kwa Ibn Ummi Maktuwm (رضي الله عنه). Alipotoka eda, alitaja kwamba Mu'aawiyah na Abuw Jahm (رضي الله عنهما) walimposa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ama Mu'aawiyah (رضي الله عنه), ni mtu asiye na mali; na ama Abuw Jahm (رضي الله عنه), haiweki fimbo yake kutoka begani mwake. Basi wewe uko wapi na Usaamah (رضي الله عنه)?" Ikawa kama kwamba jamaa zake walilichukia hilo. Akasema: Wa-Allaahi, sitaolewa isipokuwa na yule aliyemtaja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Basi akaolewa na Usaamah (رضي الله عنه). Muhammad bin 'Amr amesema: Muhammad bin Ibraahiym amesema: Yaa Faatwimah, mche Allaah! Kwani kwa hakika unajua hilo lilikuwa katika jambo gani. Akasema: Na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Allaah (تعالى) Amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ وَاتَّقُوا اللَّهَ رَبَّكُمْ لا تُخْرِجُوهُنَّ مِنْ بُيُوتِهِنَّ وَلا يَخْرُجْنَ إِلا أَنْ يَأْتِينَ بِفَاحِشَةٍ مُبَيِّنَةٍ

Ee Nabiy! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahaarah) zao, na hesabuni barabara eda, na mcheni Allaah Rabb wenu. Msiwatoe katika nyumba zao, na wala wao wasitoke isipokuwa wakileta uchafu ulio bayana [Atw-Twalaaq (65:1)]

Na uchafu (huo) ni kuwatolea maneno machafu watu wake (wa mume); akifanya hivyo, basi imewahalalikia kumtoa.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1392
Hadiyth
2223

8-Mlangoباب الحال التي يجوز للرجل أن يخطب فيهاMlango Wa Hali Ambayo Mtu Anaruhusiwa Kuposa Ndani Yake

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ يَعْنِي ابْنَ أَبِي هِنْدٍ، حَدَّثَنَا عَامِرٌ، حَدَّثَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ: "أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ تُنْكَحَ الْمَرْأَةُ عَلَى عَمَّتِهَا، وَالْعَمَّةُ عَلَى ابْنَةِ أَخِيهَا، أَوْ الْمَرْأَةُ عَلَى خَالَتِهَا، أَوْ الْخَالَةُ عَلَى بِنْتِ أُخْتِهَا، وَلَا تُنْكَحُ الصُّغْرَى عَلَى الْكُبْرَى، وَلَا الْكُبْرَى عَلَى الصُّغْرَى"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Daawuwd — yaani Ibn Abiy Hind —, ametusimulia 'Aamir, ametusimulia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه): "Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mwanamke kuolewa juu ya shangazi yake, na shangazi juu ya binti wa kaka yake, au mwanamke juu ya mama yake mdogo, au mama mdogo juu ya binti wa dada yake; wala asiolewe mdogo juu ya mkubwa, wala mkubwa juu ya mdogo."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1394
Hadiyth
2224

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: "أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُجْمَعَ بَيْنَ الْمَرْأَةِ وَعَمَّتِهَا وَالْمَرْأَةِ وَخَالَتِهَا"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه): "Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kukusanywa (katika ndoa) baina ya mwanamke na shangazi yake, na mwanamke na mama yake mdogo."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1394
Hadiyth
2225

9-Mlangoباب في النهي عن الشغارMlango Wa Kuhusu Katazo La Shighaar (Kubadilishana Wanawake
Katika Ndoa Bila Mahari)

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِع، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الشِّغَارِ". قَالَ مَالِكٌ: وَالشِّغَارُ: أَنْ يُزَوِّجَ الرَّجُلُ الْآخَرَ ابْنَتَهُ، عَلَى أَنْ يُزَوِّجَهُ الْآخَرُ ابْنَتَهُ بِغَيْرِ صَدَاقٍ، قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: تَرَى بَيْنَهُمَا نِكَاحًا؟. قَالَ: لَا يُعْجِبُنِي

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza Shighaar (kubadilishana wanawake katika ndoa bila mahari)." Maalik amesema: Na Shighaar ni mtu kumuoza mwingine binti yake, kwa sharti kwamba huyo mwingine naye amuoze binti yake bila mahari.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unaona kuwa kuna ndoa baina yao wawili? Akasema: Hainipendezi.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1395
Hadiyth
2226

10-Mlangoباب في نكاح الصالحين والصالحاتMlango Wa Kuhusu Kuwaozesha Wanaume Wema
Na Wanawake Wema

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ عُمَرَ بْنِ كَيْسَانَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ وَهْبِ بْنِ أَبِي مُغِيثٍ، حَدَّثَتْنِي أَسْمَاءُ بِنْتُ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَنْكِحُوا الصَّالِحِينَ وَالصَّالِحَاتِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: وَسَقَطَ عَلَيَّ مِنَ الْحَدِيثِ "فَمَا تَبِعَهُمْ بَعْدُ فَحَسَنٌ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibraahiym bin 'Umar bin Kaysaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Wahb bin Abiy Mughiyth, amenisimulia Asmaa bint Abiy Bakr (رضي الله عنها), kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Waozesheni wanaume wema na wanawake wema."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Na yamenipotea katika Hadiyth (maneno haya): "Basi kinachowafuata baada (ya hapo) ni kizuri."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1395
Hadiyth
2227

11-Mlangoباب النهي عن النكاح بغير وليMlango Wa Katazo La Ndoa Bila Walii

أَخْبَرَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا نِكَاحَ إِلَّا بِوَلِيٍّ"

Ametukhabarisha Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1396
Hadiyth
2228

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ حُجْرٍ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى، عِنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا نِكَاحَ إِلَّا بِوَلِيٍّ"

Ametusimulia 'Aliy bin Hujr, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakuna ndoa isipokuwa kwa walii."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1396
Hadiyth
2229

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَيُّمَا امْرَأَةٍ نُكِحَتْ بِغَيْرِ إِذْنِ وَلِيِّهَا، فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ، فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ، فَنِكَاحُهَا بَاطِلٌ، فَإِنْ اشْتَجَرُوا، قَالَ أَبُو عَاصِمٍ، وَقَالَ مَرَّةً: فَإِنْ تَشَاجَرُوا فَالسُّلْطَانُ وَلِيُّ مَنْ لَا وَلِيَّ لَهُ، فَإِنْ أَصَابَهَا، فَلَهَا الْمَهْرُ بِمَا اسْتَحَلَّ مِنْ فَرْجِهَا". قَالَ أَبُو عَاصِمٍ: أَمْلَاهُ عَلَيَّ سَنَةَ سِتٍّ وَأَرْبَعِينَ وَمِائَةٍ

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili, basi ndoa yake ni batili, basi ndoa yake ni batili. Na wakizozana — Abuw 'Aaswim amesema: Na alisema mara (nyingine): Na wakigombana — basi mtawala ni walii wa asiye na walii. Na (mume) akimwingilia, basi atapata mahari kwa sababu ya alichohalalisha katika tupu yake." Abuw 'Aaswim amesema: Aliniimlia (Hadiyth hii) mwaka wa mia moja na arobaini na sita.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1396
Hadiyth
2230

12-Mlangoباب في اليتيمة تزوجMlango Wa Kuhusu Msichana Yatima Anayeozeshwa

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ أَبِي إِسْحَاق، حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ بْنُ أَبِي مُوسَى، عَنْ أَبِي مُوسَى، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تُسْتَأْمَرُ الْيَتِيمَةُ فِي نَفْسِهَا، فَإِنْ سَكَتَتْ، فَقَدْ أَذِنَتْ، وَإِنْ أَبَتْ لَمْ تُكْرَهْ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Yuwnus bin Abiy Is-haaq, amenisimulia Abuw Burdah bin Abiy Muwsaa, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msichana yatima atakwe shauri kuhusu nafsi yake; akinyamaza, basi ametoa idhini, na akikataa, hatalazimishwa."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1397
Hadiyth
2231

13-Mlangoباب في استئمار البكر والثيبMlango Wa Kuhusu Kutakwa Shauri
Kwa Bikra Na Aliyewahi Kuolewa

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنِي يَحْيَى، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تُنْكَحُ الثَّيِّبُ حَتَّى تُسْتَأْمَرَ، وَلَا تُنْكَحُ الْبِكْرُ حَتَّى تُسْتَأْذَنَ، وَإِذْنُهَا الصُّمُوتُ".

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amenisimulia Yahyaa, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Asiolewe aliyewahi kuolewa mpaka atakwe shauri, wala asiolewe bikra mpaka atakwe idhini; na idhini yake ni kunyamaza."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1398
Hadiyth
2232

أَخْبَرَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ: أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ حَدَّثَهُ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، بِهَذَا الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Wahb bin Jariyr, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Abuw Salamah, kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) alimsimulia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1398
Hadiyth
2233

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْفَضْلِ، عَنْ نَافِعِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْأَيِّمُ أَحَقُّ بِنَفْسِهَا مِنْ وَلِيِّهَا، وَالْبِكْرُ تُسْتَأْذَنُ فِي نَفْسِهَا وَإِذْنُهَا صُمَاتُهَا"

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Al-Fadhwl, kutoka kwa Naafi' bin Jubayr bin Mutw'im, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanamke asiye na mume (aliyewahi kuolewa) ana haki zaidi juu ya nafsi yake kuliko walii wake; na bikra atakwe idhini kuhusu nafsi yake, na idhini yake ni kunyamaza kwake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1398
Hadiyth
2234

حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنِي مَالِكٌ أَوَّلُ شَيْءٍ سَأَلْتُهُ عَنْهُ، قَالَ: حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْفَضْلِ، عَنْ نَافِعِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تُسْتَأْذَنُ الْبِكْرُ وَإِذْنُهَا صُمَاتُهَا"

Ametusimulia Is-haaq bin 'Iysaa, amenisimulia Maalik — (hilo lilikuwa) jambo la kwanza nililomuuliza —, amesema: Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Fadhwl, kutoka kwa Naafi' bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Bikra atakwe idhini, na idhini yake ni kunyamaza kwake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1399
Hadiyth
2235

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَوْهَبٍ، أَخْبَرَنَا نَافِعُ بْنُ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْأَيِّمُ أَمْلَكُ بِأَمْرِهَا مِنْ وَلِيِّهَا، وَالْبِكْرُ تُسْتَأْمَرُ فِي نَفْسِهَا، وَصَمْتُهَا إِقْرَارُهَا"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, amenisimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Mawhab, ametukhabarisha Naafi' bin Jubayr bin Mutw'im, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanamke asiye na mume (aliyewahi kuolewa) ana mamlaka zaidi juu ya jambo lake kuliko walii wake; na bikra atakwe shauri kuhusu nafsi yake, na kunyamaza kwake ndiko kukubali kwake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1399
Hadiyth
2236

14-Mlangoباب الثيب يزوجها أبوها وهي كارهةMlango Wa Aliyewahi Kuolewa Anayeozeshwa
Na Baba Yake Naye Hapendi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، أَنَّهُ سَمِعَ الْقَاسِمَ بْنَ مُحَمَّدٍ: أَنَّهُ سَمِعَ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ يَزِيدَ، وَمُجَمِّعَ بْنَ يَزِيدَ الْأَنْصَارِيَّيْنِ، حَدَّثَاهُ: أَنَّ رَجُلًا مِنْهُمْ مِنَ الْأَنْصَارِ يُدْعَى خِذَامًا أَنْكَحَ بِنْتًا لَهُ فَكَرِهَتْ نِكَاحَ أَبِيهَا، فَأَتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرَتْ ذَلِكَ لَهُ، فَرَدَّ عَنْهَا نِكَاحَ أَبِيهَا "، فَنَكَحَتْ أَبَا لُبَابَةَ بْنَ عَبْدِ الْمُنْذِرِ فَذَكَرَ يَحْيَى: أَنَّهُ بَلَغَهُ أَنَّهَا كَانَتْ ثَيِّبًا

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa bin Sa'iyd, kwamba alimsikia Al-Qaasim bin Muhammad, kwamba alimsikia 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd na Mujammi' bin Yaziyd, wote wawili Al-Answaariy, wakimsimulia kwamba mtu mmoja miongoni mwao, wa Answaar (رضي الله عنهم), aitwaye Khidhaam, alimuozesha binti yake; (binti) akaichukia ndoa aliyomuozesha baba yake. Akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akamtajia hilo; akamwondolea ndoa aliyomuozesha baba yake. Akaolewa na Abuw Lubaabah bin 'Abdil-Mundhir (رضي الله عنه). Na Yahyaa akataja kwamba ilimfikia (khabari) kwamba yeye alikuwa amekwisha olewa (kabla).

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1400
Hadiyth
2237

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، وُمُجَمِّعٍ ابْنَيْ يَزِيدَ ابْنِ جَارِيَةَ، أَنَّ خَنْسَاءَ بِنْتَ خِذَامٍ زَوَّجَهَا أَبُوهَا وَهِيَ ثَيِّبٌ، فَكَرِهَتْ ذَلِكَ، فَأَتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَرَدَّ نِكَاحَهَا"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan na Mujammi', wana wawili wa Yaziyd bin Jaariyah, kwamba Khansaa bint Khidhaam (رضي الله عنها) baba yake alimuozesha naye akiwa amekwisha olewa (kabla), akachukia hilo. Akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), "akaibatilisha ndoa yake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1400
Hadiyth
2238

15-Mlangoباب المرأة يزوجها الوليانMlango Wa Mwanamke Anayeozeshwa Na Mawalii Wawili

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا سَعِيدٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ أَوْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ، أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَيُّمَا امْرَأَةٍ زَوَّجَهَا وَلِيَّانِ لَهَا، فَهِيَ لِلْأَوَّلِ مِنْهُمَا، وَأَيُّمَا رَجُلٍ بَاعَ بَيْعًا مِنْ رَجُلَيْنِ، فَهُوَ لِلْأَوَّلِ مِنْهُمَا".

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه) au Samurah bin Jundub (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanamke yeyote ambaye mawalii wake wawili wamemuozesha, basi yeye ni wa (yule aliyeozeshwa na) wa kwanza kati yao wawili. Na mtu yeyote aliyeuza bidhaa kwa watu wawili, basi ni ya wa kwanza kati yao wawili."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1401
Hadiyth
2239

حَدَّثَنَا عَفَّان، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا قَتَادَةُ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَمُرَةَ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، بِنَحْوِهِ

Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Samurah (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa namna inayokaribiana nayo.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1402
Hadiyth
2240

16-Mlangoباب النهي عن متعة النساءMlango Wa Katazo La Mut'ah (Ndoa Ya Muda) Ya Wanawake

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيز، عَنِ الرَّبِيعِ بْنِ سَبْرَةَ: أَنَّ أَبَاهُ حَدَّثَهُ: أَنَّهُمْ سَارُوا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حِجَّةِ الْوَدَاعِ، فَقَالَ: "اسْتَمْتِعُوا مِنْ هَذِهِ النِّسَاءِ". وَالِاسْتِمْتَاعُ عِنْدَنَا: التَّزْوِيجُ، فَعَرَضْنَا ذَلِكَ عَلَى النِّسَاءِ، فَأَبَيْنَ أَنْ لَا يَضْرِبْنَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُنَّ أَجَلًا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "افْعَلُوا". فَخَرَجْتُ أَنَا وَابْنُ عَمٍّ لِي مَعَهُ بُرْدٌ، وَمَعِي بُرْدٌ، وَبُرْدُهُ أَجْوَدُ مِنْ بُرْدِي، وَأَنَا أَشَبُّ مِنْهُ، فَأَتَيْنَا عَلَى امْرَأَةٍ فَأَعْجَبَهَا شَبَابِي، وَأَعْجَبَهَا بُرْدُهُ، فَقَالَتْ: بُرْدٌ كَبُرْدٍ، وَكَانَ الْأَجَلُ بَيْنِي وَبَيْنَهَا عَشْرًا، فَبِتُّ عِنْدَهَا تِلْكَ اللَّيْلَةَ، ثُمَّ غَدَوْتُ، فَإِذَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمٌ بَيْنَ الرُّكْنِ وَالْبَابِ، فَقَالَ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنِّي قَدْ كُنْتُ أَذِنْتُ لَكُمْ فِي الِاسْتِمْتَاعِ مِنَ النِّسَاءِ، أَلَا وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَهُ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ، فَمَنْ كَانَ عِنْدَهُ مِنْهُنَّ شَيْءٌ، فَلْيُخَلِّ سَبِيلَهَا، وَلَا تَأْخُذُوا مِمَّا آتَيْتُمُوهُنَّ شَيْئًا"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz, kutoka kwa Ar-Rabiy' bin Sabrah, kwamba baba yake (رضي الله عنه) alimsimulia kwamba wao walisafiri pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika Hajj ya kuaga, akasema: "Jistareheni na wanawake hawa." Na kujistarehe (huko) kwetu ni kuoa. Tukaliweka hilo mbele ya wanawake, wakakataa (kukubali) bila wao kuweka muda baina yetu na wao. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Fanyeni." Nikatoka mimi na mtoto wa ami yangu; yeye alikuwa na joho, nami nilikuwa na joho; na joho lake lilikuwa bora zaidi kuliko joho langu, nami nilikuwa kijana zaidi kuliko yeye. Tukamfikia mwanamke mmoja; ujana wangu ukampendeza, na joho lake likampendeza. Akasema: Joho ni kama joho. Na muda baina yangu na yeye ukawa (siku) kumi. Nikalala kwake usiku ule, kisha nikaenda asubuhi; mara Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesimama baina ya Rukn (pembe ya Al-Ka'bah yenye Jiwe Jeusi) na mlango (wa Al-Ka'bah), akasema: "Enyi watu! Hakika mimi nilikuwa nimewapa idhini ya kujistarehe na wanawake. Tanabahini! Na hakika Allaah Ameiharamisha mpaka Siku ya Qiyaamah. Basi aliye na chochote kati yao, na amwachie njia yake; wala msichukue chochote katika kile mlichowapa."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1403
Hadiyth
2241

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ الرَّبِيعِ بْنِ سَبْرَةَ الْجُهَنِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نِكَاحِ الْمُتْعَةِ عَامَ الْفَتْحِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Ar-Rabiy' bin Sabrah Al-Juhaniy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza ndoa ya mut'ah (ndoa ya muda) mwaka wa Al-Fat-h (kufunguliwa Makkah)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1403
Hadiyth
2242

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ حَدَّثَنِي ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ الْحَسَنِ، وَعَبْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِيهِمَا، قَالَ: سَمِعْتُ عَلِيًّا، يَقُولُ لِابْنِ عَبَّاسٍ: "إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنِ الْمُتْعَةِ: مُتْعَةِ النِّسَاءِ، وَعَنْ لُحُومِ الْحُمُرِ الْأَهْلِيَّةِ عَامَ خَيْبَرَ"

Ametusimulia Muhammad, amenisimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Al-Hasan na 'Abdu-Allaah, kutoka kwa baba yao, amesema: Nilimsikia 'Aliy (رضي الله عنه) akimwambia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): "Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mut'ah (ndoa ya muda) — mut'ah ya wanawake —, na (alikataza) nyama za punda wa kufugwa, mwaka wa Khaybar."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1403
Hadiyth
2243

17-Mlangoباب في نكاح المحرمMlango Wa Kuhusu Kuoa Kwa Aliye Katika Ihraam

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ مُوسَى، عَنْ نُبَيْهِ بْنِ وَهْبٍ، عَنْ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ عُثْمَانَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْمُحْرِمُ لَا يَنْكِحُ وَلَا يُنْكِحُ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Ayyuwb bin Muwsaa, kutoka kwa Nubayh bin Wahb, kutoka kwa Abaan bin 'Uthmaan, kutoka kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Aliye katika Ihraam haoi wala haozeshi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1409
Hadiyth
2244

18-Mlangoباب كم كانت مهور أزواج النبي صلى الله عليه وسلم وبناتهMlango Wa Kiasi Gani Yalikuwa
Mahari Ya Wake Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Binti Zake

أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ هُوَ: ابْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ كَمْ كَانَ صَدَاقُ أَزْوَاجِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: "كَانَ صَدَاقُهُ لِأَزْوَاجِهِ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أُوقِيَّةً، وَنَشًّا"، وَقَالَتْ: أَتَدْرِي مَا النَّشُّ؟. قَالَ: قُلْتُ: لَا، قَالَتْ: "نِصْفُ أُوقِيَّةٍ، فَهَذَا صَدَاقُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِأَزْوَاجِهِ"

Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz — naye ni Ibn Muhammad —, kutoka kwa Yaziyd bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym, kutoka kwa Abuw Salamah, amesema: Nilimuuliza 'Aaishah (رضي الله عنها): Mahari ya wake wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) yalikuwa kiasi gani? Akasema: "Mahari yake kwa wake zake yalikuwa uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) kumi na mbili na nash." Na akasema: Je, unajua nash ni nini? Amesema: Nikasema: Hapana. Akasema: "Ni nusu ya uwqiyyah. Basi haya ndiyo mahari ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa wake zake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1410
Hadiyth
2245

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ مَنْصُورِ بْنِ زَاذَانَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي الْعَجْفَاءِ السُّلَمِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ يَخْطُبُ، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمّ قَالَ: "أَلَا لَا تُغَالُوا فِي صُدُقِ النِّسَاءِ، فَإِنَّهَا لَوْ كَانَتْ مَكْرُمَةً فِي الدُّنْيَا، أَوْ تَقْوَى عِنْدَ اللَّهِ، كَانَ أَوْلَاكُمْ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَا أَصْدَقَ امْرَأَةً مِنْ نِسَائِهِ، وَلَا أُصْدِقَتِ امْرَأَةٌ مِنْ بَنَاتِهِ فَوْقَ اثْنَتَيْ عَشْرَةَ أُوقِيَّةً، أَلَا وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيُغَالِي بِصَدَاقِ امْرَأَتِهِ حَتَّى يَبْقَى لَهَا فِي نَفْسِهِ عَدَاوَةٌ حَتَّى يَقُولَ: كَلِفْتُ لَكِ عَلَقَ الْقِرْبَةِ أَوْ عَرَقَ الْقِرْبَةِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Hushaym, kutoka kwa Manswuwr bin Zaadhaan, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Abul-'Ajfaa As-Sulamiy, amesema: Nilimsikia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) akikhutubia; akamhimidi Allaah na akamsifu, kisha akasema: "Tanabahi! Msipindukie mipaka katika mahari ya wanawake; kwani lau (kufanya hivyo) kungekuwa ni heshima duniani, au taqwa mbele ya Allaah, basi mwenye kustahiki zaidi kati yenu kwa hilo angekuwa ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Hakumpa mahari mwanamke yeyote katika wake zake, wala hakupewa mahari mwanamke yeyote katika binti zake, zaidi ya uwqiyyah (kipimo cha uzito wa dirhamu arobaini) kumi na mbili. Tanabahi! Na hakika mmoja wenu huzidisha mno mahari ya mkewe mpaka unabakia moyoni mwake uadui dhidi yake, hata husema: Nimejikalifisha kwa ajili yako hata kamba ya kiriba — au: jasho la kiriba."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1411
Hadiyth
2246

19-Mlangoباب ما يجوز أن يكون مهراMlango Wa Kinachojuzu Kuwa Mahari

حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ قَالَ: أَتَتِ امْرَأَةٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: إِنَّهَا وَهَبَتْ نَفْسَهَا لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا لِي فِي النِّسَاءِ مِنْ حَاجَةٍ"، فَقَالَ رَجُلٌ: زَوِّجْنِيهَا، فَقَالَ: "أَعْطِهَا ثَوْبًا"، فَقَالَ: لَا أَجِدُ، قَالَ: "أَعْطِهَا وَلَوْ خَاتَمًا مِنْ حَدِيدٍ"، قَالَ: فَاعْتَلَّ لَهُ، فَقَالَ: "مَا مَعَكَ مِنَ الْقُرْآنِ؟"، قَالَ: كَذَا وَكَذَا، قَالَ: "فَقَدْ زَوَّجْتُكَهَا عَلَى مَا مَعَكَ مِنَ الْقُرْآنِ"

Ametusimulia 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), amesema: Mwanamke mmoja alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema kwamba yeye amejitoa nafsi yake kwa Allaah na kwa Rasuli Wake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Sina haja na wanawake." Mtu mmoja akasema: Niozeshe yeye. Akasema: "Mpe nguo." Akasema: Sipati. Akasema: "Mpe hata pete ya chuma." Akasema: Akatoa udhuru (wa kutokuwa nayo). Akasema: "Una nini katika Qur-aan?" Akasema: Kadhaa na kadhaa. Akasema: "Basi nimekuozesha yeye kwa kile ulicho nacho katika Qur-aan."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1412
Hadiyth
2247

20-Mlangoباب في خطبة النكاحMlango Wa Kuhusu Khutbah (Hotuba) Ya Ndoa

حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، وَحَجَّاجٌ، قَالَا: حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: أَنْبَأَنَا أَبُو إِسْحَاق، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا عُبَيْدَةَ يُحَدِّثُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: عَلَّمَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خُطْبَةَ الْحَاجَةِ: "الْحَمْدُ لِلَّهِ أَوْ إِنَّ الْحَمْدَ لِلَّهِ نَحْمَدُهُ وَنَسْتَعِينُهُ وَنَسْتَغْفِرُهُ، وَنَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ شُرُورِ أَنْفُسِنَا، مَنْ يَهْدِهِ اللَّهُ، فَلَا مُضِلَّ لَهُ وَمَنْ يُضْلِلْ، فَلَا هَادِيَ لَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ"، ثُمَّ يَقْرَأُ ثَلَاثَ آيَاتٍ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلا تَمُوتُنَّ إِلا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ}، {يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالا كَثِيرًا وَنِسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالأَرْحَامَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا}، {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا} ثُمَّ يَتَكَلَّمُ بِحَاجَتِهِ

Ametusimulia Abul-Waliyd na Hajjaaj, wamesema: Ametusimulia Shu'bah, amesema: Ametupa khabari Abuw Is-haaq, amesema: Nilimsikia Abuw 'Ubaydah akihadithia kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitufundisha khutbah (hotuba) ya haja:

الْحَمْدُ لِلَّهِ أَوْ إِنَّ الْحَمْدَ لِلَّهِ نَحْمَدُهُ وَنَسْتَعِينُهُ وَنَسْتَغْفِرُهُ، وَنَعُوذُ بِاللَّهِ مِنْ شُرُورِ أَنْفُسِنَا، مَنْ يَهْدِهِ اللَّهُ، فَلَا مُضِلَّ لَهُ وَمَنْ يُضْلِلْ، فَلَا هَادِيَ لَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ

Himdi ni ya Allaah — au: Hakika Himdi ni ya Allaah —; tunamhimidi, na tunamtaka msaada, na tunamwomba Maghfirah, na tunajikinga kwa Allaah kutokana na shari za nafsi zetu. Ambaye Allaah Amemwongoza, basi hakuna wa kumpoteza; na ambaye Amempoteza, basi hakuna wa kumwongoza. Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na nashuhudia kwamba Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mja Wake na Rasuli Wake.

Kisha anasoma Aayah tatu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلا تَمُوتُنَّ إِلا وَأَنْتُمْ مُسْلِمُونَ

Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha na chungeni sana, angalieni msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu. [Aal-‘Imraan (3:102)]

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ وَاحِدَةٍ وَخَلَقَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَبَثَّ مِنْهُمَا رِجَالا كَثِيرًا وَنِسَاءً وَاتَّقُوا اللَّهَ الَّذِي تَسَاءَلُونَ بِهِ وَالأَرْحَامَ إِنَّ اللَّهَ كَانَ عَلَيْكُمْ رَقِيبًا

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu Ambaye Amekuumbeni kutokana na nafsi moja (Aadam) na Akaumba kutoka humo mke wake (Hawwaa) na Akaeneza kutoka hao wawili wanaume na wanawake wengi. Na mcheni Allaah Ambaye Kwake mnaombana (haki zenu kwa kuunga) undugu. Hakika Allaah daima Ni Mwenye Kuwachungeni. [An-Nisaa (4:1)]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَقُولُوا قَوْلا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ وَمَنْ يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

Enyi walioamini! Mcheni Allaah na semeni kauli nyofu ya haki. Atakutengenezeeni amali zenu, na Atakughufurieni madhambi yenu. Na anayemtii Allaah na Rasuli Wake, basi kwa yakini amefanikiwa mafanikio adhimu. [Al-Ahzaab (33:70-71)]

Kisha anaizungumza haja yake.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1413
Hadiyth
2248

21-Mlangoباب الشرط في النكاحMlango Wa Sharti Katika Ndoa

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ عَبْدِ الْحَمِيدِ بْنِ جَعْفَرٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ مَرْثَدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ أَحَقَّ الشُّرُوطِ أَنْ تُوفُوا بِهِ مَا اسْتَحْلَلْتُمْ بِهِ الْفُرُوجَ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa 'Abdul-Hamiyd bin Ja'far, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Marthad bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika masharti yanayostahiki zaidi kuyatimiza ni yale ambayo kwayo mmezihalalisha tupu (za wake zenu)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1413
Hadiyth
2249

22-Mlangoباب في الوليمةMlango Wa Kuhusu Karamu Ya Harusi

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَأَى عَلَى عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ صُفْرَةً، فَقَالَ: "مَا هَذِهِ الصُّفْرَةُ؟"، قَالَ: تَزَوَّجْتُ امْرَأَةً عَلَى وَزْنِ نَوَاةٍ مِنْ ذَهَبٍ، قَالَ: "بَارَكَ اللَّهُ لَكَ، أَوْلِمْ وَلَوْ بِشَاةٍ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliona juu ya 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf (رضي الله عنه) (alama ya) rangi ya manjano, akasema: "Ni nini rangi hii ya manjano?" Akasema: Nimeoa mwanamke kwa (mahari ya) uzito wa kokwa (ya tende) ya dhahabu. Akasema: "Allaah Akubarikie! Fanya karamu ya harusi, hata kwa mbuzi mmoja."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1414
Hadiyth
2250

23-Mlangoباب ما جاء في إجابة الوليمةMlango Wa Yaliyopokewa
Kuhusu Kuitikia (Mwaliko Wa) Karamu Ya Harusi

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا دُعِيَ أَحَدُكُمْ إِلَى وَلِيمَةٍ، فَلْيُجِبْ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: يَنْبَغِي أَنْ يُجِيبَ وَلَيْسَ الْأَكْلُ عَلَيْهِ بِوَاجِبٍ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu akialikwa kwenye karamu ya harusi, basi aitikie."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Inampasa aitikie, na kula si wajibu juu yake.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1415
Hadiyth
2251

24-Mlangoباب في العدل بين النساءMlango Wa Kuhusu Uadilifu Baina Ya Wake

حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ النَّضْرِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ بَشِيرِ بْنِ نَهِيكٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ كَانَتْ لَهُ امْرَأَتَانِ، فَمَالَ إِلَى إِحْدَاهُمَا، جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَشِقُّهُ مَائِلٌ"

Ametusimulia Abul-Waliyd, ametusimulia Hammaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa An-Nadhwr bin Anas, kutoka kwa Bashiyr bin Nahiyk, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwenye kuwa na wake wawili, akamwelemea mmoja wao, atakuja Siku ya Qiyaamah na upande wake mmoja umeinama."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1415
Hadiyth
2252

25-Mlangoباب في القسمة بين النساءMlango Wa Kuhusu Kugawa (Zamu) Baina Ya Wake

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَزِيدَ الْخَطْمِيِّ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقْسِمُ فَيَعْدِلُ وَيَقُولُ: "اللَّهُمَّ هَذَا قَسْمِي فِيمَا أَمْلِكُ، فَلَا تَلُمْنِي فِيمَا تَمْلِكُ وَلَا أَمْلِكُ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Aaswim, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Yaziyd Al-Khatwmiy, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akigawa (zamu baina ya wake zake) na akifanya uadilifu, na akisema:

اللَّهُمَّ هَذَا قَسْمِي فِيمَا أَمْلِكُ، فَلَا تَلُمْنِي فِيمَا تَمْلِكُ وَلَا أَمْلِكُ

Yaa Allaah! Huu ndio mgawanyo wangu katika ninachokimiliki; basi Usinilaumu katika Unachokimiliki na nisichokimiliki.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1416
Hadiyth
2253

26-Mlangoباب الرجل يكون عنده النسوةMlango Wa Mtu Anayekuwa Na Wake Kadhaa

أَخْبَرَنَا إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا ابْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ يُونُسَ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا سَافَرَ، أَقْرَعَ بَيْنَ نِسَائِهِ، فَأَيَّتُهُنَّ خَرَجَ سَهْمُهَا، خَرَجَ بِهَا مَعَهُ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl, ametusimulia Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Yuwnus bin Yaziyd, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaposafiri, hupiga kura baina ya wake zake; basi yeyote kati yao ambaye kura yake ilitoka, hutoka naye."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1417
Hadiyth
2254

27-Mlangoباب الإقامة عند الثيب والبكر إذا بنى بهماMlango Wa Kukaa Kwa Aliyekwisha Olewa
Na Kwa Bikra Anapoingia Nao (Katika Ndoa)

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لِلْبِكْرِ سَبْعٌ، وَلِلثَّيِّبِ ثَلَاثٌ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Bikra ana (haki ya siku) saba, na aliyekwisha olewa (siku) tatu."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1417
Hadiyth
2255

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْحَارِثِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَمَّا تَزَوَّجَ أُمَّ سَلَمَةَ، أَقَامَ عِنْدَهَا ثَلَاثًا، وَقَالَ: "إِنَّهُ لَيْسَ بِكِ عَلَى أَهْلِكِ هَوَانٌ، إِنْ شِئْتِ، سَبَّعْتُ لَكِ، وَإِنْ سَبَّعْتُ لَكِ، سَبَّعْتُ لِسَائِرِ نِسَائِي"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Muhammad bin Abiy Bakr, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Abiy Bakr bin 'Abdir-Rahmaan bin Al-Haarith bin Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ummu Salamah (رضي الله عنها), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipomuoa Ummu Salamah (رضي الله عنها), alikaa kwake (siku) tatu, na akasema: "Hakika wewe huna udhalili wowote mbele ya jamaa zako. Ukitaka, nitakaa kwako siku saba; na nikikaa kwako siku saba, nitakaa siku saba kwa wake zangu wengine wote."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1418
Hadiyth
2256

28-Mlangoباب بناء الرجل بأهله في شوالMlango Wa Mtu Kuingia Kwa Mkewe
Katika (Mwezi Wa) Shawwaal

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ أُمَيَّةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "تَزَوَّجَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي شَوَّالٍ، وَأُدْخِلْتُ عَلَيْهِ فِي شَوَّالٍ، فَأَيُّ نِسَائِهِ كَانَ أَحْظَى عِنْدَهُ مِنِّي؟" قَالَت: "وَكَانَتْ تَسْتَحِبُّ أَنْ تُدْخِلَ عَلَى النِّسَاءِ فِي شَوَّالٍ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Umayyah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Urwah, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinioa katika (mwezi wa) Shawwaal, na nikaingizwa kwake katika Shawwaal; basi ni yupi miongoni mwa wake zake aliyekuwa na bahati zaidi kwake kuliko mimi?" Amesema: "Na alikuwa akipenda wanawake waingizwe (kwa waume zao) katika Shawwaal."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1418
Hadiyth
2257

29-Mlangoباب القول عند الجماعMlango Wa Kauli (Ya Kusema) Wakati Wa Kujimai

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ كُرَيْبٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا يَمْنَعُ أَحَدَكُمْ أَنْ يَقُولَ حِينَ يُجَامِعُ أَهْلَهُ: بِسْمِ اللَّهِ، اللَّهُمَّ جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ، وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا"، فَإِنْ قَضَى اللَّهُ وَلَدًا، لَمْ يَضُرَّهُ الشَّيْطَانُ

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Kurayb, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ni nini kinachomzuia mmoja wenu kusema anapojimai na mkewe:

بِسْمِ اللَّهِ، اللَّهُمَّ جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ، وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

Kwa Jina la Allaah. Yaa Allaah! Tuepushe na shaytwaan, na Umuepushe shaytwaan na Utakachoturuzuku.

Basi Allaah Akikadiria mtoto, shaytwaan hatamdhuru."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1419
Hadiyth
2258

30-Mlangoباب النهي عن إتيان النساء في أعجازهنMlango Wa Katazo La Kuwaingilia Wanawake
Katika Tupu Zao Za Nyuma

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ الْوَلِيدِ بْنِ كَثِيرٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْحُصَيْنِ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عَمْرِو بْنِ قَيْسٍ الْخَطْمِيِّ، عَنْ هَرَمِيِّ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ خُزَيْمَةَ بْنَ ثَابِتٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِنَّ اللَّهَ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ، لَا تَأْتُوا النِّسَاءَ فِي أَعْجَازِهِنَّ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Al-Waliyd bin Kathiyr, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin Al-Huswayn, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Amr bin Qays Al-Khatwmiy, kutoka kwa Harmiy bin 'Abdi-Allaah, amesema: Nilimsikia Khuzaymah bin Thaabit (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika Allaah Haoni haya kwa haki: msiwaingilie wanawake katika tupu zao za nyuma."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1420
Hadiyth
2259

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ: أَنَّ الْيَهُودَ، قَالُوا لِلْمُسْلِمِينَ: "مَنْ أَتَى امْرَأَتَهُ وَهِيَ مُدْبِرَةٌ، جَاءَ وَلَدُهُ أَحْوَلَ. فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ}"

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Muhammad bin Al-Munkadir, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), kwamba Mayahudi waliwaambia Waislamu: "Atakayemwingilia mkewe naye amempa mgongo, mtoto wake atakuja akiwa na makengeza." Basi Allaah (تعالى) Akateremsha:

نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ

Wake zenu ni konde kwenu. Basi ziendeeni konde zenu (panapotoka kizazi) vyovyote mpendavyo [Al-Baqarah (2:223)]

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1420
Hadiyth
2260

31-Mlangoباب الرجل يرى المرأة فيخاف على نفسهMlango Wa Mtu Anayemuona Mwanamke, Akaikhofia Nafsi Yake

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، أَخْبَرَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ حَلَّامٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: رَأَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ امْرَأَةً فَأَعْجَبَتْهُ، فَأَتَى سَوْدَةَ وَهِيَ تَصْنَعُ طِيبًا، وَعِنْدَهَا نِسَاءٌ، فَأَخْلَيْنَهُ، فَقَضَى حَاجَتَهُ، ثُمَّ قَالَ: "أَيُّمَا رَجُلٍ رَأَى امْرَأَةً تُعْجِبُهُ، فَلْيَقُمْ إِلَى أَهْلِهِ، فَإِنَّ مَعَهَا مِثْلَ الَّذِي مَعَهَا"

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametukhabarisha Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Hallaam, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimuona mwanamke, akampendeza. Akamwendea Sawdah (رضي الله عنها), naye alikuwa akitengeneza manukato, na kwake walikuwepo wanawake; wakampisha faragha, akakidhi haja yake. Kisha akasema: "Mwanamume yeyote atakayemuona mwanamke anayempendeza, basi aende kwa mkewe; kwani yeye (mkewe) ana mfano wa kile alicho nacho (yule mwanamke)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1421
Hadiyth
2261

32-Mlangoباب في تزويج الأبكارMlango Wa Kuhusu Kuoa Mabikra

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُطِيعٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَنْبَأَنَا سَيَّارٌ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، حَدَّثَنَا جَابِرُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: كُنَّا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ فَلَمَّا قَفَلْنَا تَعَجَّلْتُ، فَلَحِقَنِي رَاكِبٌ، قَالَ: فَالْتَفَتُّ، فَإِذَا أَنَا بِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ لِي: "مَا أَعْجَلَكَ يَا جَابِرُ؟" قَالَ: إِنِّي حَدِيثُ عَهْدٍ بِعُرْسٍ، قَالَ: "أَفَبِكْرًا تَزَوَّجْتَهَا أَمْ ثَيِّبًا؟" قَالَ: قُلْتُ: بَلْ ثَيِّبًا، قَالَ: "فَهَلَّا بِكْرًا تُلَاعِبُهَا وَتُلَاعِبُكَ؟" قَالَ: ثُمَّ قَالَ لِي: "إِذَا قَدِمْتَ فَالْكَيْسَ الْكَيْسَ"، قَالَ: فَلَمَّا قَدِمْنَا، ذَهَبْنَا نَدْخُلُ، قَالَ: "أَمْهِلُوا حَتَّى نَدْخُلَ لَيْلًا، أَيْ: عِشَاءً لِكَيْ تَمْتَشِطَ الشَّعِثَةُ، وَتَسْتَحِدَّ الْمُغِيبَةُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Mutwiy', ametusimulia Hushaym, ametupa khabari Sayyaar, kutoka kwa Ash-Sha'biy, ametusimulia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: Tulikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) safarini. Tuliporudi, niliharakisha; akanifikia mpandaji mmoja. Akasema: Nikageuka, mara (nikamuona) ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akaniambia: "Ni nini kinachokuharakisha, yaa Jaabir?" Akasema: Hakika mimi nina muda mfupi tangu nifunge harusi. Akasema: "Je, umemuoa bikra au aliyekwisha olewa?" Akasema: Nikasema: Bali aliyekwisha olewa. Akasema: "Kwa nini (hukuoa) bikra, ukacheza naye na yeye akacheza nawe?" Akasema: Kisha akaniambia: "Utakapofika, basi (shika) busara, busara!" Akasema: Tulipofika, tukaenda kuingia (majumbani). Akasema: "Ngojeni mpaka tuingie usiku — yaani: wakati wa 'Ishaa — ili mwanamke aliyetimka nywele azichane, na yule ambaye mumewe hakuwepo ajinyoe (nywele za siri)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1422
Hadiyth
2262

33-Mlangoباب في الغيلةMlango Wa Kuhusu Ghiylah (Kumwingilia Mke Anayenyonyesha)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ نَوْفَلٍ الْأَسَدِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَة، عَنْ جُدَامَةَ بِنْتِ وَهْبٍ الْأَسَدِيَّةِ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ أَنْهَى عَنِ الْغِيلَةِ حَتَّى ذَكَرْتُ أَنَّ فَارِسَ، وَالرُّومَ يَصْنَعُونَ ذَلِكَ فَلَا يَضُرُّ أَوْلَادَهُمْ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: الْغِيلَةُ: أَنْ يُجَامِعَهَا وَهِيَ تُرْضِعُ

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Nawfal Al-Asadiy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Judaamah bint Wahb Al-Asadiyyah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kwa hakika nilikusudia kukataza ghiylah (kumwingilia mke anayenyonyesha), mpaka nikakumbuka kwamba Wafursi na Warumi wanafanya hivyo, na haiwadhuru watoto wao."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ghiylah ni (mume) kumwingilia (mkewe) naye ananyonyesha.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1423
Hadiyth
2263

34-Mlangoباب في النهي عن ضرب النساءMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuwapiga Wanawake

حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "مَا ضَرَبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَادِمًا قَطُّ، وَلَا ضَرَبَ بِيَدِهِ شَيْئًا إِلَّا أَنْ يُجَاهِدَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ عز وجل"

Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakupata kumpiga mtumishi kamwe, wala hakupiga kitu kwa mkono wake, isipokuwa awe anapigana jihaad katika Njia ya Allaah (عز وجل)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1424
Hadiyth
2264

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ إِيَاسِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي ذُبَابِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَضْرِبُوا إِمَاءَ اللَّهِ"، فَجَاءَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: قَدْ ذَئِرْنَ عَلَى أَزْوَاجِهِنَّ، فَرَخَّصَ لَهُمْ، فِي ضَرْبِهِنَّ، فَأَطَافَ بِآلِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَقَدْ طَافَ بِآلِ مُحَمَّدٍ نِسَاءٌ كَثِيرٌ يَشْكُونَ أَزْوَاجَهُنَّ لَيْسَ أُولَئِكَ بِخِيَارِكُمْ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Iyaas bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Dhubaab (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiwapige wajakazi wa Allaah." 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: (Wanawake) wamewathubutia waume zao (kwa kuwaasi). Akawaruhusu kuwapiga. Wanawake wengi wakazizunguka ahli za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakiwashtaki waume zao. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Kwa hakika wanawake wengi wamezizunguka ahli za Muhammad wakiwashtaki waume zao; hao (waume) si walio bora miongoni mwenu."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1424
Hadiyth
2265

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ زَمَعَةَ، قَالَ: خَطَبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ النَّاسَ يَوْمًا وَوَعَظَهُمْ فِي النِّسَاءِ، فَقَالَ: "مَا بَالُ الرَّجُلِ يَجْلِدُ امْرَأَتَهُ جَلْدَ الْعَبْدِ، وَلَعَلَّهُ يُضَاجِعُهَا فِي آخِرِ يَوْمِهِ؟!"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Zam'ah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwakhutubia watu siku moja, na akawapa mawaidha kuhusu wanawake, akasema: "Ana nini mtu anayemchapa mkewe kama anavyochapwa mtumwa, na huenda akalala naye mwishoni mwa siku yake?!"

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1425
Hadiyth
2266

35-Mlangoباب مداراة الرجل أهلهMlango Wa Mtu Kumvumilia Mkewe Kwa Upole

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، حَدَّثَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ أَبِي الْعَلَاءِ، عَنْ نُعَيْمِ بْنِ قَعْنَبٍ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ الْمَرْأَةَ خُلِقَتْ مِنْ ضِلَعٍ، فَإِنْ تُقِمْهَا، كَسَرْتَهَا، فَدَارِهَا، فَإِنَّ فِيهَا أَوَدًا وَبُلْغَةً"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia 'Abdul-Waarith, ametusimulia Al-Jurayriy, kutoka kwa Abul-'Alaa, kutoka kwa Nu'aym bin Qa'nab, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mwanamke ameumbwa kutokana na ubavu; ukimnyoosha, utamvunja. Basi mvumilie kwa upole; kwani ndani yake kuna upindaji, na (pia) kuna kinachotosha (kuishi naye)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1425
Hadiyth
2267

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّمَا الْمَرْأَةُ كَالضِّلَعِ: إِنْ تُقِمْهَا، تَكْسِرْهَا، وَإِنْ تَسْتَمْتِعْ بِهَا، تَسْتَمْتِعْ وَفِيهَا عِوَجٌ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mwanamke ni kama ubavu: ukimnyoosha, utamvunja; na ukistarehe naye, utastarehe naye huku ndani yake kuna upindaji."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1425
Hadiyth
2268

36-Mlangoباب في العزلMlango Wa Kuhusu 'Azl (Kumwaga Nje)

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ الْهَاشِمِيُّ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَة، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: سَأَلَ رَجُلٌ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْعَزْلِ، فَقَالَ: "أَوَ تَفْعَلُونَ ذَلِكَ؟ فَلَا عَلَيْكُمْ أَنْ لَا تَفْعَلُوا، فَإِنَّهُ لَيْسَ مِنْ نَسَمَةٍ قَضَى اللَّهُ تَعَالَى أَنْ تَكُونَ إِلَّا كَانَتْ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Daawuwd Al-Haashimiy, kutoka kwa Ibraahiym bin Sa'd, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu 'azl (kumwaga nje), akasema: "Je, nyinyi mnafanya hivyo? Si juu yenu kutofanya (hivyo); kwani hakika hakuna nafsi ambayo Allaah (تعالى) Ameikadiria iwepo, isipokuwa itakuwepo."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1426
Hadiyth
2269

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ بِشْرٍ يَرُدُّ الْحَدِيثَ إِلَى أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّه، الرَّجُلُ تَكُونُ لَهُ الْجَارِيَةُ فَيُصِيبُ مِنْهَا، وَيَكْرَهُ أَنْ تَحْمِلَ، أَفَيَعْزِلُ عَنْهَا؟ وَتَكُونُ عِنْدَهُ الْمَرْأَةُ تُرْضِعُ فَيُصِيبُ مِنْهَا وَيَكْرَهُ أَنْ تَحْمِلَ. أَفَيَعْزِلُ عَنْهَا؟ قَالَ: "لَا عَلَيْكُمْ أَنْ لَا تَفْعَلُوا، فَإِنَّمَا هُوَ الْقَدَرُ". قَالَ ابْنُ عَوْنٍ: فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِلْحَسَنِ، فَقَالَ: وَاللَّهِ لَكَأَنَّ هَذَا زَجْرٌا، وَاللَّهِ لَكَأَنَّ هَذَا زَجْرًا!!

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Bishr, akiirudisha Hadiyth kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Tulisema: Yaa Rasula-Allaah, mtu anakuwa na mjakazi, akajimai naye, naye anachukia ashike mimba; je, afanye 'azl (kumwaga nje) kwake? Na anakuwa na mke anayenyonyesha, akajimai naye, naye anachukia ashike mimba; je, afanye 'azl kwake? Akasema: "Si juu yenu kutofanya (hivyo); kwani hakika hilo ni Qadar (Majaaliwa ya Allaah)." Ibn 'Awn amesema: Nikamtajia hilo Al-Hasan, akasema: Wa-Allaahi, ni kama kwamba hili ni karipio! Wa-Allaahi, ni kama kwamba hili ni karipio!

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1427
Hadiyth
2270

37-Mlangoباب في الغيرةMlango Wa Kuhusu Ghayrah (Wivu)

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ شَقِيقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَيْسَ أَحَدٌ أَغْيَرَ مِنَ اللَّهِ، لِذَلِكَ حَرَّمَ الْفَوَاحِشَ وَلَيْسَ أَحَدٌ أَحَبَّ إِلَيْهِ الْمَدْحُ مِنَ اللَّهِ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Shaqiyq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna yeyote mwenye Ghayrah (Wivu) zaidi kuliko Allaah; kwa sababu hiyo Ameharamisha machafu. Na hakuna yeyote anayependa zaidi kusifiwa kuliko Allaah."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1428
Hadiyth
2271

أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي كَثِيرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنِي ابْنُ جَابِرِ بْنِ عَتِيكٍ، حَدَّثَنِي أَبِي، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مِنَ الْغَيْرَةِ مَا يُحِبُّ اللَّه، وَمِنْهَا مَا يُبْغِضُ اللَّهُ: فَالْغَيْرَةُ الَّتِي يُحِبُّ اللَّه: الْغَيْرَةُ فِي الرِّيبَةِ، وَالْغَيْرَةُ الَّتِي يُبْغِضُ اللَّه، الْغَيْرَةُ فِي غَيْرِ رِيبَةٍ"

Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym, amenisimulia Ibn Jaabir bin 'Atiyk, amenisimulia baba yangu [Jaabir bin 'Atiyk (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Katika ghayrah (wivu) kuna Anayoipenda Allaah, na katika hiyo kuna Anayoichukia Allaah. Basi ghayrah Anayoipenda Allaah ni ghayrah katika (jambo la) shaka; na ghayrah Anayoichukia Allaah ni ghayrah katika (jambo) lisilo na shaka."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1428
Hadiyth
2272

حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ وَرَّادٍ مَوْلَى الْمُغِيرَةِ، عَنِ الْمُغِيرَةِ، قَالَ: بَلَغَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّ سَعْدَ بْنَ عُبَادَةَ، يَقُولُ: لَوْ وَجَدْتُ مَعَهَا رَجُلًا لَضَرَبْتُهَا بِالسَّيْفِ غَيْرَ مُصْفَحٍ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَتَعْجَبُونَ مِنْ غَيْرَةِ سَعْدٍ؟ أَنَا أَغَيْرُ مِنْ سَعْدٍ وَاللَّهُ أَغَيْرُ مِنِّي، وَلِذَلِكَ حَرَّمَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ وَلَا شَخْصَ أَغَيْرُ مِنَ اللَّهِ، وَلَا أَحَبُّ إِلَيْهِ مِنَ الْمَعَاذِيرِ، وَلِذَلِكَ بَعَثَ النَّبِيِّينَ مُبَشِّرِينَ وَمُنْذِرِينَ وَلَا شَخْصَ أَحَبُّ إِلَيْهِ الْمَدْحُ مِنَ اللَّه، وَلِذَلِكَ وَعَدَ الْجَنَّةَ"

Ametusimulia Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Warraad mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Mughiyrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Al-Mughiyrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifikiwa (na khabari) kwamba Sa'd bin 'Ubaadah (رضي الله عنه) anasema: Lau ningemkuta mwanamume pamoja naye (mke wangu), ningempiga yeye (mke) kwa upanga, bila (kutumia) ubapa wake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, mnastaajabu ghayrah (wivu) ya Sa'd (رضي الله عنه)? Mimi nina ghayrah zaidi kuliko Sa'd (رضي الله عنه), na Allaah Ana Ghayrah (Wivu) zaidi kuliko mimi; na kwa sababu hiyo Ameharamisha machafu ya wazi na ya siri. Na hakuna yeyote mwenye Ghayrah zaidi kuliko Allaah, na wala hakuna yeyote anayependa zaidi udhuru kuliko Allaah; na kwa sababu hiyo Amewatuma Manabii (عليهم السلام) wakiwa wabashiriaji na waonyaji. Na hakuna yeyote anayependa zaidi kusifiwa kuliko Allaah; na kwa sababu hiyo Ameahidi Jannah (Pepo)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1428
Hadiyth
2273

38-Mlangoباب في حق الزوج على المرأةMlango Wa Kuhusu Haki Ya Mume Juu Ya Mke

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَنْبَأَنَا قَتَادَةُ، عَنْ زُرَارَةَ بْنِ أَوْفَى الْعَامِرِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِذَا بَاتَتِ الْمَرْأَةُ هَاجِرَةً لِفِرَاشِ زَوْجِهَا، لَعَنَتْهَا الْمَلَائِكَةُ حَتَّى تَرْجِعَ"

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, ametupa khabari Qataadah, kutoka kwa Zuraarah bin Awfaa Al-'Aamiriy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwanamke akilala usiku amehama kitanda cha mumewe, Malaika (عليهم السلام) humlaani mpaka arudi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1429
Hadiyth
2274

39-Mlangoباب في اللعانMlango Wa Kuhusu Li'aan (Kulaaniana Baina Ya Mume Na Mke)

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ: أَنَّ عُوَيْمِرًا الْعَجْلَانِيَّ، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّه، أَرَأَيْتَ رَجُلًا وَجَدَ مَعَ امْرَأَتِهِ رَجُلًا، أَيَقْتُلُهُ فَيَقْتُلُونَهُ، أَمْ كَيْفَ يَفْعَلُ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "قَدْ أَنْزَلَ اللَّه فِيكَ وَفِي صَاحِبَتِكَ، فَاذْهَبْ فَأْتِ بِهَا". قَالَ سَهْلٌ: فَتَلَاعَنَا، وَأَنَا مَعَ النَّاسِ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَمَّا فَرَغَا مِنْ تَلَاعُنِهِمَا، قَالَ: كَذَبْتُ عَلَيْهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنْ أَمْسَكْتُهَا، فَطَلَّقَهَا ثَلَاثًا قَبْلَ أَنْ يَأْمُرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. قَالَ ابْنُ شِهَابٍ: وَكَانَتْ تِلْكَ بَعْدُ سُنَّةَ الْمُتَلَاعِنَيْنِ.

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), kwamba 'Uwaymir Al-'Ajlaaniy (رضي الله عنه) alisema: Yaa Rasula-Allaah, waonaje mtu aliyemkuta mwanamume pamoja na mkewe; je, amuue, nao wamuue (kwa kisasi), au afanye vipi? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Kwa hakika Allaah Ameteremsha (Wahyi) kuhusu wewe na kuhusu mwenzako (mkeo); basi nenda umlete." Sahl (رضي الله عنه) amesema: Wakafanya Li'aan (kulaaniana baina ya mume na mke), nami nikiwa pamoja na watu kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Walipomaliza Li'aan yao, akasema: Nitakuwa nimemsingizia uongo, yaa Rasula-Allaah, nikimbakisha. Akamtaliki talaka tatu kabla Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hajamwamrisha. Ibn Shihaab amesema: Na hiyo ikawa baadaye ndiyo Sunnah ya wanaolaaniana.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1430
Hadiyth
2275

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ، أَنَّ عُوَيْمِرًا أَتَى عَاصِمَ بْنَ عَدِيّ، وَكَانَ سَيِّدَ بَنِي عَجْلَانَ، فَذَكَرَ نَحْوَهُ، وَلَمْ يَذْكُرْ "طَلَّقَهَا ثَلَاثًا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), kwamba 'Uwaymir (رضي الله عنه) alimwendea 'Aaswim bin 'Adiyy (رضي الله عنه) — naye alikuwa bwana (kiongozi) wa Banuw 'Ajlaan —, akataja kwa namna yake (Hadiyth iliyotangulia), wala hakutaja: "Akamtaliki talaka tatu."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1431
Hadiyth
2276

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ بْنُ أَبِي سُلَيْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ، يَقُولُ: "سُئِلْتُ عَنِ الْمُتَلَاعِنَيْنِ فِي إِمَارَةِ مُصْعَبِ بْنِ الزُّبَيْرِ: أَيُفَرَّقُ بَيْنَهُمَا؟ فَمَا دَرَيْتُ مَا أَقُولُ، قَالَ: فَقُمْتُ حَتَّى أَتَيْتُ مَنْزِلَ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، فَقُلْتُ لِلْغُلَامِ: اسْتَأْذِنْ لِي عَلَيْهِ، فَقَالَ: إِنَّهُ قَائِلٌ لَا تَسْتَطِيعُ أَنْ تَدْخُلَ عَلَيْهِ، قَالَ: فَسَمِعَ ابْنُ عُمَرَ صَوْتِي، فَقَالَ: ابْنُ جُبَيْرٍ؟، فَقُلْتُ: نَعَمْ، فَقَالَ: ادْخُلْ، فَمَا جَاءَ بِكَ هَذِهِ السَّاعَةَ إِلَّا حَاجَةٌ، قَالَ: فَدَخَلْتُ عَلَيْهِ فَوَجَدْتُهُ وَهُوَ مُفْتَرِشٌ بَرْذَعَةَ رَحْلِهِ، مُتَوَسِّدٌ مِرْفَقَةُ أَوْ قَالَ: نُمْرُقَةً، شَكَّ عَبْدُ اللَّهِ حَشْوُهَا لِيفٌ، فَقُلْتُ: يَا أَبَا عَبْدِ الرَّحْمَنِ: الْمُتَلَاعِنَانِ، أَيُفَرَّقُ بَيْنَهُمَا؟. قَالَ: سُبْحَانَ اللَّهِ، نَعَمْ، إِنَّ أَوَّلَ مَنْ سَأَلَ عَنْ ذَلِكَ فُلَانٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْكَ، أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ أَحَدَنَا رَأَى امْرَأَتَهُ عَلَى فَاحِشَةٍ كَيْفَ يَصْنَعُ؟ إِنْ سَكَتَ، سَكَتَ عَلَى أَمْرٍ عَظِيمٍ، وَإِنْ تَكَلَّمَ فَمِثْلُ ذَلِكَ؟، قَالَ: فَسَكَتَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَمْ يُجِبْهُ، فَقَامَ لِحَاجَتِهِ، فَلَمَّا كَانَ بَعْدَ ذَلِكَ، أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ الَّذِي سَأَلْتُكَ عَنْهُ قَدْ ابْتُلِيتُ بِهِ، قَالَ: فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى هَؤُلَاءِ الْآيَاتِ الَّتِي فِي سُورَةِ النُّورِ: {وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ شُهَدَاءُ إِلا أَنْفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَةَ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَنْ تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّهِ عَلَيْهَا إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ} حَتَّى خَتَمَ هَؤُلَاءِ الْآيَاتِ، قَالَ: فَدَعَا الرَّجُلَ، فَتَلَاهُنَّ عَلَيْهِ، وَذَكَّرَهُ بِاللَّهِ، وَأَخْبَرَهُ أَنَّ عَذَابَ الدُّنْيَا أَهْوَنُ مِنْ عَذَابِ الْآخِرَةِ، فَقَالَ: مَا كَذَبْتُ عَلَيْهَا، . ثُمَّ دَعَا الْمَرَأَةَ فَوَعَظَهَا وَذَكَّرَهَا، وَأَخْبَرَهَا أَنَّ عَذَابَ الدُّنْيَا أَهْوَنُ مِنْ عَذَابِ الْآخِرَةِ، فَقَالَتْ: وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ إِنَّهُ لَكَاذِبٌ، فَدَعَا الرَّجُلَ فَشَهِدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنْ الصَّادِقِينَ، وَالْخَامِسَةَ أَنَّ لَعْنَةَ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ، ثُمَّ أُتِيَ بِالْمَرْأَةِ فَشَهِدَتْ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّهِ عَلَيْهَا إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ، ثُمَّ فَرَّقَ بَيْنَهُمَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari 'Abdul-Malik bin Abiy Sulaymaan, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin Jubayr akisema: Niliulizwa kuhusu wanaolaaniana katika uongozi wa Mus'ab bin Az-Zubayr: Je, watenganishwe? Sikujua niseme nini. Akasema: Nikainuka mpaka nikafika nyumbani kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), nikamwambia mtumishi: Niombee idhini ya kuingia kwake. Akasema: Hakika yeye amelala (usingizi wa) mchana; huwezi kuingia kwake. Akasema: Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akasikia sauti yangu, akasema: Ibn Jubayr? Nikasema: Ndiyo. Akasema: Ingia; hakuna kilichokuleta saa hii isipokuwa haja. Akasema: Nikaingia kwake, nikamkuta ametandika tandiko la (chini ya) kipando chake, ameweka kichwa juu ya mto — au alisema: mto mdogo; 'Abdu-Allaah ametia shaka —, uliojazwa nyuzi za mtende. Nikasema: Yaa Abaa 'Abdir-Rahmaan, wanaolaaniana, je, watenganishwe? Akasema: Subhaana-Allaah! Ndiyo. Hakika wa kwanza aliyeuliza kuhusu hilo ni fulani; alisema: Yaa Rasula-Allaah — Allaah Akuswalie —, waonaje lau mmoja wetu angemwona mkewe katika uchafu (wa zinaa), afanye vipi? Akinyamaza, amenyamaza juu ya jambo kubwa; na akizungumza, basi ni mfano wa hilo. Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akanyamaza, hakumjibu. Akasimama (kwenda) kwa haja yake. Ilipokuwa baada ya hapo, alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika lile nililokuuliza kuhusu hilo nimekwishajaribiwa nalo. Akasema: Allaah (تعالى) Akateremsha Aayah hizi zilizoko katika Suwrah An-Nuwr (24):

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُمْ شُهَدَاءُ إِلا أَنْفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ وَالْخَامِسَةُ أَنَّ لَعْنَةَ اللَّهِ عَلَيْهِ إِنْ كَانَ مِنَ الْكَاذِبِينَ وَيَدْرَأُ عَنْهَا الْعَذَابَ أَنْ تَشْهَدَ أَرْبَعَ شَهَادَاتٍ بِاللَّهِ إِنَّهُ لَمِنَ الْكَاذِبِينَ وَالْخَامِسَةَ أَنَّ غَضَبَ اللَّهِ عَلَيْهَا إِنْ كَانَ مِنَ الصَّادِقِينَ

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli. Na (kiapo) cha tano kwamba Laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo. Na itamwondokea (mke) adhabu atakapotoa ushahidi mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo. Na (kiapo) cha tano kwamba Ghadhabu ya Allaah iwe juu yake akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. [An-Nuwr (24:6-9)]

mpaka akazimaliza Aayah hizo. Akasema: Akamwita yule mwanamume, akamsomea (Aayah) hizo, na akamkumbusha Allaah, na akamkhabarisha kwamba adhabu ya duniani ni nyepesi zaidi kuliko adhabu ya Aakhirah. Akasema: Sikumsingizia uongo. Kisha akamwita yule mwanamke, akamwaidhi na akamkumbusha, na akamkhabarisha kwamba adhabu ya duniani ni nyepesi zaidi kuliko adhabu ya Aakhirah. Akasema: Naapa kwa Ambaye Amekutuma kwa haki, hakika yeye ni mwongo. Akamwita yule mwanamume, akashuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye ni miongoni mwa wakweli, na (kiapo) cha tano kwamba Laana ya Allaah iwe juu yake, akiwa ni miongoni mwa waongo. Kisha yule mwanamke akaletwa, akashuhudia mara nne kwa kiapo cha Allaah kwamba yeye (mumewe) ni miongoni mwa waongo, na (kiapo) cha tano kwamba Ghadhabu ya Allaah iwe juu yake, akiwa (mumewe) ni miongoni mwa wakweli. Kisha akawatenganisha.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1431
Hadiyth
2277

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنِي مَالِكٌ، قَالَ: سَمِعْتُ نَافِعًا، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، قَالَ: "فَرَّقَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَيْنَ الْمُتَلَاعِنَيْنِ، وَأَلْحَقَ الْوَلَدَ بِأُمِّهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, amenisimulia Maalik, amesema: Nilimsikia Naafi', kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwatenganisha wanaolaaniana, na akamnasibisha mtoto na mama yake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1432
Hadiyth
2278

40-Mlangoباب في العبد يتزوج بغير إذن من سيدهMlango Wa Kuhusu Mtumwa Anayeoa Bila Idhini Ya Bwana Wake

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَقِيلٍ، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرًا، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَيُّمَا عَبْدٍ تَزَوَّجَ بِغَيْرِ إِذْنِ مَوَالِيهِ أَوْ أَهْلِهِ، فَهُوَ عَاهِرٌ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Hasan bin Swaalih, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Muhammad bin 'Aqiyl, amesema: Nilimsikia Jaabir (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtumwa yeyote aliyeoa bila idhini ya mabwana zake au ahli zake, basi yeye ni mzinifu."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1433
Hadiyth
2279

حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا مِنْدَلٌ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ مُوسَى بْنِ عُقْبة، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَيُّمَا عَبْدٍ تَزَوَّجَ بِغَيْرِ إِذْنِ مَوَالِيهِ، فَهُوَ زَانٍ"

Ametusimulia Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Mindal, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mtumwa yeyote aliyeoa bila idhini ya mabwana zake, basi yeye ni mzinzi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1433
Hadiyth
2280

41-Mlangoباب الولد للفراشMlango Wa Mtoto Ni Wa Mwenye Kitanda

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ ابْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، يَرْفَعُهُ، قَالَ: "الْوَلَدُ لِلْفِرَاشِ، وَلِلْعَاهِرِ الْحَجَرُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Ibn Al-Musayyib, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), akiipandisha [hadi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)], amesema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda, na mzinifu ni kukosa (haki)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1436
Hadiyth
2281

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْوَلَدُ لِلْفِرَاشِ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1436
Hadiyth
2282

حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، أَخْبَرَنِي عُرْوَةُ، عَنْ عَائِشَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: كَانَ عُتْبَةُ بْنُ أَبِي وَقَّاصٍ عَهِدَ إِلَى أَخِيهِ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ: أَنْ يَقْبِضَ إِلَيْهِ ابْنَ وَلِيدَةِ زَمْعَةَ، فَقَالَ عُتْبَةُ: إِنَّهُ ابْنِي، فَلَمَّا قَدِمَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَمَنَ الْفَتْحِ، أَخَذَ سَعْدُ بْنُ أَبِي وَقَّاصٍ ابْنَ وَلِيدَةِ زَمْعَةَ، فَإِذَا هُوَ أَشْبَهُ النَّاسِ بِعُتْبَةَ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، فَقَالَ النَّبِيُّ: "هُوَ لَكَ يَا عَبْدُ بْنَ زَمْعَةَ مِنْ أَجْلِ أَنَّهُ وُلِدَ عَلَى فِرَاشِ أَبِيهِ"، وَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "احْتَجِبِي مِنْهُ يَا سَوْدَةُ بِنْتَ زَمْعَةَ مِمَّا رَأَى مِنْ شَبَهِهِ بِعُتْبَةَ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، وَسَوْدَةُ بِنْتُ زَمْعَةَ"

Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', ametusimulia Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenikhabarisha 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: 'Utbah bin Abiy Waqqaasw alikuwa amemuusia ndugu yake Sa'd bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه) kwamba amchukue kwake mtoto wa mjakazi wa Zam'ah. 'Utbah akasema: Hakika yeye ni mwanangu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuja zama za Ufunguzi (wa Makkah), Sa'd bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه) akamchukua mtoto wa mjakazi wa Zam'ah; mara ikawa yeye ndiye anayefanana zaidi na 'Utbah bin Abiy Waqqaasw kuliko watu wote. Nabiy akasema: "Yeye ni wako, Yaa 'Abd bin Zam'ah, kwa sababu amezaliwa juu ya kitanda cha baba yake." Na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Jisitiri naye, Yaa Sawdah bint Zam'ah" — kwa sababu ya kufanana kwake na 'Utbah bin Abiy Waqqaasw alikokuona —, na Sawdah bint Zam'ah (رضي الله عنها).

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1436
Hadiyth
2283

42-Mlangoباب من جحد ولده وهو يعرفهMlango Wa Aliyemkana Mtoto Wake Naye Anamjua

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُول حِينَ أُنْزِلَتْ آيَةُ الْمُلَاعَنَةِ: "أَيُّمَا امْرَأَةٍ أَدْخَلَتْ عَلَى قَوْمٍ نَسَبًا لَيْسَ مِنْهُمْ، فَلَيْسَتْ مِنَ اللَّهِ فِي شَيْءٍ، وَلَنْ يُدْخِلْهَا اللَّهُ جَنَّتَهُ، وَأَيُّمَا رَجُلٍ جَحَدَ وَلَدَهُ وَهُوَ يَنْظُرُ إِلَيْهِ، احْتَجَبَ اللَّهُ مِنْهُ وَفَضَحَهُ عَلَى رُءُوسِ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ". قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: قَالَ مُحَمَّدُ بْنُ كَعْبٍ الْقُرَظِيّ، وَسَعِيدٌ يُحَدِّثَهْ بِهِ، بِهَذَا: وَقَدْ بَلَغَنِي هَذَا الْحَدِيثُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yaziyd bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Yuwnus, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba yeye alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema, ilipoteremshwa Aayah ya Li'aan (kulaaniana baina ya mume na mke): "Mwanamke yeyote aliyewaingizia watu (mtoto wa) nasaba isiyokuwa yao, basi hana chochote kwa Allaah, na Allaah Hatamwingiza kamwe Jannah (Pepo) Yake. Na mwanamume yeyote aliyemkana mtoto wake naye anamtazama, Allaah Atajisitiri naye, na Atamfedhehesha mbele ya vichwa vya (viumbe) wa mwanzo na wa mwisho." 'Abdu-Allaah amesema: Muhammad bin Ka'b Al-Quradhwiy — na Sa'iyd alikuwa akimsimulia (Hadiyth) hiyo — alisema kuhusu hii: Na kwa hakika imenifikia Hadiyth hii kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1437
Hadiyth
2284

43-Mlangoباب الرجل يتزوج امرأة أبيهMlango Wa Mtu Anayemuoa Mke Wa Baba Yake

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ جَعْفَرٍ الرَّقِّيُّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ زَيْدٍ، عَنْ عَدِيِّ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ الْبَرَاءِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَقِيتُ عَمِّي وَمَعَهُ رَايَةٌ، فَقُلْتُ: أَيْنَ تُرِيدُ؟ قَالَ: "بَعَثَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى رَجُلٍ نَكَحَ امْرَأَةَ أَبِيهِ، فَأَمَرَنِي أَنْ أَضْرِبَ عُنُقَهُ وَآخُذَ مَالَهُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Ja'far Ar-Raqqiy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr, kutoka kwa Zayd, kutoka kwa 'Adiyy bin Thaabit, kutoka kwa Yaziyd bin Al-Baraa, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilikutana na ami yangu (رضي الله عنه) akiwa na bendera. Nikasema: Unakwenda wapi? Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amenituma kwa mtu aliyemuoa mke wa baba yake, akaniamrisha nimkate shingo yake na nichukue mali yake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1438
Hadiyth
2285

44-Mlangoباب قول الله تعالى لا يحل لك النساء من بعدMlango Wa Kauli Ya Allaah (تعالى) : «Si halali kwako
wanawake wengine baada ya hao» [Al-Ahzaab (33:52)]

حَدَّثَنِي مُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، قَالَ: حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي مُوسَى، عَنْ رَجُلٍ مِنَ الْأَنْصَارِ يُسَمَّى: زِيَادًا، قَالَ: قُلْتُ لِأُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ: أَرَأَيْتَ لَوْ أَنَّ أَزْوَاجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُتْنَ، كَانَ يَحِلُّ لَهُ أَنْ يَتَزَوَّجَ؟ قَالَ: "نَعَمْ، إِنَّمَا أَحَلَّ اللَّهُ لَهُ ضَرْبًا مِنَ النِّسَاءِ، وَوَصَفَ لَهُ صِفَةً"، فَقَالَ: "لَا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِنْ بَعْدُ، مِنْ بَعْدِ هَذِهِ الصِّفَةِ"

Amenisimulia Mu'allaa bin Asad, amesema: Ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa Muhammad bin Abiy Muwsaa, kutoka kwa mtu mmoja wa Answaar aitwaye Ziyaad, amesema: Nilimwambia Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه): Waonaje lau wake za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) wangefariki, je, ingekuwa halaal kwake kuoa? Akasema: "Ndiyo; hakika Allaah Amemhalalishia aina fulani tu ya wanawake, na Akamwelezea sifa (yao)." Akasema:

لَا يَحِلُّ لَكَ النِّسَاءُ مِنْ بَعْدُ

Si halali kwako wanawake wengine baada ya hao [Al-Ahzaab (33:52)]

(Yaani:) baada ya sifa hii.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1438
Hadiyth
2286

أَخْبَرَنَا الْمُعَلَّى، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "مَا تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى أَحَلَّ اللَّهُ لَهُ أَنْ يَتَزَوَّجَ مِنَ النِّسَاءِ مَا شَاءَ"

Ametukhabarisha Al-Mu'allaa, ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa 'Ubayd bin 'Umayr, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hakufariki mpaka Allaah Alipomhalalishia kuoa katika wanawake aliowataka."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1439
Hadiyth
2287

45-Mlangoباب في الأمة يجعل عتقها صداقهاMlango Wa Kuhusu Mjakazi
Ambaye Kuachwa Huru Kwake Kunafanywa
Kuwa Ndio Mahari Yake

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ الْحَبْحَابِ، عَنْ أَنَسٍ: "أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَعْتَقَ صَفِيَّةَ وَجَعَلَ عِتْقَهَا صَدَاقَهَا"

Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Shu'ayb bin Al-Habhaab, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه): "Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwacha huru Swafiyyah (رضي الله عنها), na akafanya kuachwa huru kwake kuwa ndio mahari yake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1439
Hadiyth
2288

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ: "أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَعْتَقَ صَفِيَّةَ وَتَزَوَّجَهَا وَجَعَلَ عِتْقَهَا صَدَاقَهَا"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه): "Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwacha huru Swafiyyah (رضي الله عنها), na akamuoa, na akafanya kuachwa huru kwake kuwa ndio mahari yake."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1439
Hadiyth
2289

46-Mlangoباب فضل من أعتق أمة ثم تزوجهاMlango Wa Fadhila Ya Aliyemwacha
Huru Mjakazi Kisha Akamuoa

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ صَالِحِ بْنِ صَالِحِ بْنِ حَيٍّ الْهَمْدَانِيِّ، قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ الشَّعْبِيِّ فَأَتَاهُ رَجُلٌ مِنْ أَهْلِ خُرَاسَانَ، فَقَالَ: يَا أَبَا عَمْرٍو، إِنَّ مَنْ قِبَلَنَا مِنْ أَهْلِ خُرَاسَانَ يَقُولُونَ فِي الرَّجُلِ: إِذَا أَعْتَقَ أَمَتَهُ ثُمَّ تَزَوَّجَهَا، فَهُوَ كَالرَّاكِبِ بَدَنَتَهُ؟ فَقَالَ الشَّعْبِيُّ: حَدَّثَنِي أَبُو بُرْدَةَ بْنُ أَبِي مُوسَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ثَلَاثَةٌ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُمْ مَرَّتَيْنِ: رَجُلٌ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمَنَ بِنَبِيِّهِ، ثُمَّ أَدْرَكَ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَآمَنَ بِهِ وَاتَّبَعَهُ، وَعَبْدٌ مَمْلُوكٌ أَدَّى حَقَّ اللَّهِ وَحَقَّ مَوَالِيهِ، فَلَهُ أَجْرَانِ، وَرَجُلٌ كَانَتْ لَهُ أَمَةٌ فَغَذَّاهَا، فَأَحْسَنَ غِذَاءَهَا، وَأَدَّبَهَا فَأَحْسَنَ تَأْدِيبَهَا فَأَعْتَقَهَا وَتَزَوَّجَهَا، فَلَهُ أَجْرَانِ". ثُمَّ قَالَ لِلرَّجُلِ: خُذْ هَذَا الْحَدِيثَ بِغَيْرِ شَيْءٍ، فَقَدْ كَانَ يُرْحَلُ فِيمَا دُونَ هَذَا إِلَى الْمَدِينَةِ، فَقَالَ هُشَيْمٌ: أَفَادُونِي بِالْبَصْرَةِ فَأَتَيْتُهُ فَسَأَلْتُهُ عَنْهُ.

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Hushaym, kutoka kwa Swaalih bin Swaalih bin Hayy Al-Hamdaaniy, amesema: Nilikuwa kwa Ash-Sha'biy; akamjia mtu mmoja miongoni mwa watu wa Khuraasaan, akasema: Yaa Abaa 'Amr, hakika walio upande wetu miongoni mwa watu wa Khuraasaan wanasema kuhusu mtu anayemwacha huru mjakazi wake kisha akamuoa, kwamba yeye ni kama mwenye kumpanda ngamia wake wa kuchinjwa (aliyemtoa kuwa Hadyi). Ash-Sha'biy akasema: Amenisimulia Abuw Burdah bin Abiy Muwsaa, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Watu watatu watapewa ujira wao mara mbili: Mtu miongoni mwa Watu wa Kitabu aliyemwamini Nabiy wake (عليه السلام), kisha akamdiriki Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akamwamini na akamfuata; na mtumwa anayemilikiwa aliyetekeleza haki ya Allaah na haki ya mabwana zake, basi yeye ana ujira mara mbili; na mtu aliyekuwa na mjakazi, akamlisha na akamlisha vizuri, na akamwadibu na akamwadibu vizuri, akamwacha huru na akamuoa, basi yeye ana ujira mara mbili." Kisha akamwambia yule mtu: Ichukue Hadiyth hii bila ya kitu chochote (bila malipo); kwani (mtu) alikuwa akisafiri hadi Madiynah kwa (ajili ya jambo) lililo duni kuliko hili. Hushaym akasema: Walinifaidisha (Hadiyth hii) huko Al-Baswrah, nikamwendea (Swaalih), nikamuuliza kuhusu (Hadiyth) hiyo.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1440
Hadiyth
2290

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ صَالِحِ بْنِ حَيٍّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، نَحْوَ هَذَا الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Swaalih bin Hayy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa namna ya Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1441
Hadiyth
2291

47-Mlangoباب الرجل يتزوج المرأة فيموت قبل أن يفرض لهاMlango Wa Mtu Anayemuoa Mwanamke, Kisha Akafariki
Kabla Ya Kumkadiria (Mahari)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، فِي رَجُلٍ تَزَوَّجَ امْرَأَةً وَلَمْ يَكُنْ فَرَضَ لَهَا شَيْئًا، وَلَمْ يَدْخُلْ بِهَا، وَمَاتَ عَنْهَا، قَالَ فِيهَا: لَهَا صَدَاقُ نِسَائِهَا، وَعَلَيْهَا الْعِدَّةُ، وَلَهَا الْمِيرَاثُ، قَالَ مَعْقِلٌ الْأَشْجَعِيُّ: "قَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بِرْوَعَ بِنْتِ وَاشِقٍ امْرَأَةٍ مِنْ بَنِي رُؤَاسٍ بِمِثْلِ مَا قَضَيْتَ". قَالَ: فَفَرِحَ بِذَلِكَ، قَالَ مُحَمَّدٌ، وَسُفْيَانُ: نَأْخُذُ بِهَذَا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kuhusu mtu aliyeoa mwanamke, naye hakuwa amemkadiria (mahari) chochote, wala hakuingiliana naye, na akafariki akamwacha; akasema kuhusu (mwanamke) huyo: Anastahiki mahari ya wanawake wenzake, na juu yake ni eda, na anastahiki mirathi. Ma'qil Al-Ashja'iy (رضي الله عنه) akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu kuhusu Barwa' bint Waashiq (رضي الله عنها) — mwanamke wa Banuw Ru-aas — mfano wa ulivyohukumu." (Msimulizi) akasema: Akafurahi kwa hilo. Muhammad na Sufyaan wamesema: Tunalichukua hili.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1441
Hadiyth
2292

48-Mlangoباب ما يحرم من الرضاعMlango Wa Yanayoharamishwa Kwa Kunyonya

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا رَوْحٌ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ عَمْرَةَ، عَنْ عَائِشَةَ: أَنَّهَا كَانَتْ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْتِ حَفْصَةَ، فَسَمِعَتْ صَوْتَ إِنْسَانٍ، قَالَتْ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، سَمِعْتُ صَوْتَ إِنْسَانٍ فِي بَيْتِكَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أُرَاهُ فُلَانًا لِعَمِّ حَفْصَةَ مِنَ الرَّضَاعَةِ"، قَالَتْ عَائِشَةُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَلَوْ كَانَ فُلَانٌ حَيًّا لِعَمِّهَا مِنَ الرَّضَاعَةِ دَخَلَ عَلَيَّ؟، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "نَعَمْ، يَحْرُمُ مِنَ الرَّضَاعَةِ مَا يَحْرُمُ مِنَ الْوِلَادَةِ"

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Rawh, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa 'Amrah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba yeye alikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyumba ya Hafswah (رضي الله عنها), akasikia sauti ya mtu. Amesema: Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, nimesikia sauti ya mtu katika nyumba yako. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Namdhania ni fulani" — (akimkusudia) ami ya Hafswah wa kunyonya. 'Aaishah (رضي الله عنها) akasema: Yaa Rasula-Allaah, na lau fulani — (akimkusudia) ami yake wa kunyonya — angekuwa hai, angeingia kwangu? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Ndiyo; huharamishwa kwa kunyonya yale yanayoharamishwa kwa uzazi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1442
Hadiyth
2293

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: أَخْبَرَتْنِي عَائِشَةُ: أَنَّ عَمَّهَا أَخَا أَبِي الْقُعَيْسِ جَاءَ يَسْتَأْذِنُ عَلَيْهَا بَعْدَمَا ضُرِبَ الْحِجَابُ، فَأَبَتْ أَنْ تَأْذَنَ لَهُ حَتَّى يَأْتِيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَسْتَأْذِنَهُ، فَلَمَّا جَاءَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَكَرَتْ ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَتْ: جَاءَ عَمِّي أَخُو أَبِي الْقُعَيْسِ فَرَدَدْتُهُ حَتَّى أَسْتَأْذِنَكَ، قَالَ: "أَوَ لَيْسَ بِعَمِّكِ؟"، قَالَتْ: إِنَّمَا أَرْضَعَتْنِيَ الْمَرْأَةُ وَلَمْ يُرْضِعْنِي الرَّجُلُ، فَقَالَ: "إِنَّهُ عَمُّكِ فَلْيَلِجْ عَلَيْكِ"، فَقَالَتْ: وَكَانَتْ عَائِشَةُ تَقُولُ: يَحْرُمُ مِنَ الرَّضَاعَةِ مَا يَحْرُمُ مِنَ الْوِلَادَةِ

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, amesema: Amenikhabarisha 'Aaishah (رضي الله عنها) kwamba ami yake (رضي الله عنه), ndugu wa Abul-Qu'ays, alikuja akiomba idhini ya kuingia kwake baada ya kuwekwa Hijaab (amri ya kujisitiri). Akakataa kumpa idhini mpaka Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aje, nimuombe idhini. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuja, alimtajia hilo; akasema: Alikuja ami yangu (رضي الله عنه), ndugu wa Abul-Qu'ays, nikamrudisha mpaka nikuombe idhini. Akasema: "Je, kwani yeye si ami yako?" Akasema: Hakika aliyeninyonyesha ni mwanamke, wala hakuninyonyesha mwanamume. Akasema: "Hakika yeye ni ami yako, basi na aingie kwako." Akasema: Na 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa akisema: Huharamishwa kwa kunyonya yale yanayoharamishwa kwa uzazi.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1442
Hadiyth
2294

أَخْبَرَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ مَالِكٍ، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دِينَارٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يَحْرُمُ مِنَ الرَّضَاعَةِ مَا يَحْرُمُ مِنَ الْوِلَادَةِ".

Ametukhabarisha Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Maalik, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Huharamishwa kwa kunyonya yale yanayoharamishwa kwa uzazi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1443
Hadiyth
2295

قَالَ مَالِكٌ: وَحَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَمْرَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، مِثْلَهُ

Maalik amesema: Na amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa 'Amrah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1443
Hadiyth
2296

49-Mlangoباب كم رضعة تحرمMlango Wa Ni Mara Ngapi Za Kunyonya Zinazoharamisha

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا تُحَرِّمُ الْمَصَّةُ وَالْمَصَّتَانِ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kufyonza mara moja wala mara mbili hakuharamishi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1444
Hadiyth
2297

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي الْخَلِيلِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ أُمِّ الْفَضْلِ: أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي قَدْ تَزَوَّجْتُ امْرَأَةً وَعِنْدِي أُخْرَى، فَزَعَمَتِ الْأُولَى أَنَّهَا أَرْضَعَتِ الْحُدْثَى، فَقَالَ: "لَا تُحَرِّمُ الْإِمْلَاجَةُ وَلَا الْإِمْلَاجَتَانِ"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abul-Khaliyl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Al-Haarith, kutoka kwa Ummul-Fadhwl (رضي الله عنها), kwamba mtu mmoja alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nimeoa mwanamke, na kwangu nina mwingine; yule wa kwanza akadai kwamba yeye alimnyonyesha yule mpya. Akasema: "Kunyonyeshwa mara moja wala mara mbili hakuharamishi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1444
Hadiyth
2298

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، أَنْبَأَنَا رَوْحٌ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، عَنْ عَمْرَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "نَزَلَ الْقُرْآنُ بِعَشْرِ رَضَعَاتٍ مَعْلُومَاتٍ يُحَرِّمْنَ، ثُمَّ نُسِخْنَ بِخَمْسٍ مَعْلُومَاتٍ، فَتُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُنَّ مِمَّا يُقْرَأُ مِنَ الْقُرْآنِ"

Ametukhabarisha Is-haaq, ametupa khabari Rawh, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Bakr, kutoka kwa 'Amrah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Qur-aan iliteremka kwa (kunyonya) mara kumi zinazojulikana, zinazoharamisha; kisha zikafutwa kwa (kunyonya) mara tano zinazojulikana. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafariki, nazo ni miongoni mwa yanayosomwa katika Qur-aan."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1444
Hadiyth
2299

50-Mlangoباب ما يذهب مذمة الرضاعMlango Wa Kinachoondoa
Haki Ya Kunyonyeshwa (Anayostahiki Mnyonyeshaji)

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدَةُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيه، عَنْ حَجَّاجِ بْنِ حَجَّاجٍ الْأَسْلَمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، أَنَّهُ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا يُذْهِبُ عَنِّي مَذَمَّةَ الرَّضَاعِ؟ قَالَ: "الْغُرَّةُ: الْعَبْدُ أَوِ الْأَمَةُ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia 'Abdah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Hajjaaj bin Hajjaaj Al-Aslamiy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba alisema: Yaa Rasula-Allaah, ni kitu gani kitakachoniondolea haki ya kunyonyeshwa (anayostahiki mnyonyeshaji)? Akasema: "Ghurrah (kitu bora kabisa): mtumwa au mjakazi."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1446
Hadiyth
2300

51-Mlangoباب شهادة المرأة الواحدة على الرضاعMlango Wa Ushahidi Wa Mwanamke Mmoja Juu Ya Kunyonyesha

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي عُقْبَةَ بْنُ الْحَارِثِ، ثُمّ قَالَ: لَمْ يُحَدِّثْنِيهِ وَلَكِنْ سَمِعْتُهُ يُحَدِّثُ الْقَوْمَ، قَالَ:" تَزَوَّجْتُ بِنْتَ أَبِي إِهَابٍ، فَجَاءَتْ أَمَةٌ سَوْدَاءُ، فَقَالَتْ: إِنِّي أَرْضَعْتُكُمَا، فَأَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لَهُ فَأَعْرَضَ عَنِّي. قَالَ أَبُو عَاصِمٍ: قَالَ فِي الثَّالِثَةِ أَوْ الرَّابِعَةِ. قَالَ: كَيْفَ وَقَدْ قِيلَ؟، وَنَهَاهُ عَنْهَا. قَالَ أَبُو عَاصِمٍ: وَقَالَ عَمْرُو بْنُ سَعِيدِ بْنِ أَبِي حُسَيْنٍ، عَنِ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ: " فَكَيْفَ وَقَدْ قِيلَ؟ " وَلَمْ يَقُلْ: نَهَاهُ عَنْهَا. قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: كَذَا عِنْدَنَا

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, amesema: Amenisimulia 'Uqbah bin Al-Haarith (رضي الله عنه), kisha akasema: Hakunisimulia (yeye mwenyewe), lakini nilimsikia akiwasimulia watu, amesema: Nilimuoa bint Abiy Ihaab. Akaja mjakazi mweusi, akasema: Hakika mimi niliwanyonyesha nyinyi wawili. Nikamwendea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), nikamtajia hilo, akanipa mgongo. Abuw 'Aaswim amesema: Alisema (hivyo) mara ya tatu au ya nne. Akasema: "Itakuwaje, na hali imekwishasemwa?" Na akamkataza (asiendelee) naye. Abuw 'Aaswim amesema: Na 'Amr bin Sa'iyd bin Abiy Husayn amesema, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah: "Basi itakuwaje, na hali imekwishasemwa?" Wala hakusema: Akamkataza naye.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Hivyo ndivyo ilivyo kwetu.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1446
Hadiyth
2301

52-Mlangoباب في رضاعة الكبيرMlango Wa Kuhusu Kunyonya Kwa Mtu Mzima

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَشْعَثَ بْنِ سُلَيْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَائِشَةَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا وَعِنْدَهَا رَجُلٌ فَتَغَيَّرَ وَجْهُهُ، وَكَأَنَّهُ كَرِهَ ذَلِكَ، فَقُلْتُ: إِنَّهُ أَخِي مِنَ الرَّضَاعَةِ، فَقَالَ: "انْظُرْنَ مَا إِخْوَانُكُنَّ فَإِنَّمَا الرَّضَاعَةُ مِنَ الْمَجَاعَةِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ash'ath bin Sulaym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia kwake na kwake kulikuwa na mtu; uso wake ukabadilika, na kama kwamba alichukia hilo. Nikasema: Hakika yeye ni ndugu yangu wa kunyonya. Akasema: "Angalieni ndugu zenu ni wa namna gani; kwani hakika kunyonya (kunakoharamisha) ni kule kunakotokana na njaa."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1447
Hadiyth
2302

أَخْبَرَنَا أَبُو الْيَمَانِ الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: جَاءَتْ سَهْلَةُ بِنْتُ سُهَيْلِ بْنِ عَمْرٍو وَكَانَتْ تَحْتَ أَبِي حُذَيْفَةَ بْنِ عُتْبَةَ بْنِ رَبِيعَةَ، رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: إِنَّ سَالِمًا مَوْلَى أَبِي حُذَيْفَةَ يَدْخُلُ عَلَيْنَا وَأَنَا فُضُلٌ وَإِنَّمَا نَرَاهُ وَلَدًا، وَكَانَ أَبُو حُذَيْفَةَ تَبَنَّاهُ كَمَا تَبَنَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَيْدًا، فَأَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى: {ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ} "فَأَمَرَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ ذَلِكَ أَنْ تُرْضِعَ سَالِمًا". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: هَذَا لِسَالِمٍ خَاصَّةً

Ametukhabarisha Abul-Yamaan Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Sahlah bint Suhayl bin 'Amr (رضي الله عنها) — naye alikuwa mke wa Abuw Hudhayfah bin 'Utbah bin Rabiy'ah (رضي الله عنه) — alimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika Saalim (رضي الله عنه), mwachwa huru wa Abuw Hudhayfah, huingia kwetu nami nikiwa nimevaa nguo moja (ya nyumbani), na hakika sisi tunamwona kuwa ni mtoto (wetu). Na Abuw Hudhayfah (رضي الله عنه) alikuwa amemfanya kuwa mwanawe (wa kupanga) kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyomfanya Zayd (رضي الله عنه) (kuwa mwanawe wa kupanga). Allaah (تعالى) Akateremsha:

ادْعُوهُمْ لآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِنْدَ اللَّهِ

Waiteni kwa (majina ya) baba zao. Huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Allaah [Al-Ahzaab (33:5)]

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwamrisha wakati huo amnyonyeshe Saalim (رضي الله عنه).

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Hili ni kwa Saalim (رضي الله عنه) peke yake.

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1448
Hadiyth
2303

53-Mlangoباب في النهي عن التحليلMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuhalalisha
(Aliyetalikiwa Talaka Tatu Kwa Mumewe Wa Kwanza)

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ الْهُزَيْلِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمُحِلَّ وَالْمُحَلَّلَ لَهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Qays, kutoka kwa Al-Huzayl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amemlaani Al-Muhill (mwenye kumuoa aliyetalikiwa talaka tatu ili amhalalishe kwa mumewe wa kwanza) na Al-Muhallal lahu (yule anayehalalishiwa)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1450
Hadiyth
2304

54-Mlangoباب في وجوب نفقة الرجل على أهلهMlango Wa Kuhusu Uwajibu Wa Mwanamume
Kuwapa Ahli Zake Matumizi

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، أَنَّ هِنْدًا أُمَّ مُعَاوِيَةَ امْرَأَةَ أَبِي سُفْيَانَ أَتَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ وَإِنَّهُ لَا يُعْطِينِي مَا يَكْفِينِي وَبَنِيَّ إِلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْهُ، وَهُوَ لَا يَعْلَمُ، فَهَلْ عَلَيَّ فِي ذَلِكَ جُنَاحٌ؟ فَقَالَ: "خُذِي مَا يَكْفِيكِ وَوَلَدَكِ بِالْمَعْرُوفِ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Hind (رضي الله عنها), mama yake Mu'aawiyah (رضي الله عنه), mke wa Abuw Sufyaan (رضي الله عنه), alimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika Abuw Sufyaan (رضي الله عنه) ni mtu bakhili, na hakika yeye hanipi kinachonitosheleza mimi na wanangu, isipokuwa kile nilichokichukua kutoka kwake, naye hajui. Je, kuna dhambi juu yangu katika hilo? Akasema: "Chukua kinachokutosheleza wewe na wanao kwa wema (kwa kiasi kinachokubalika)."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1450
Hadiyth
2305

55-Mlangoباب في حسن معاشرة النساءMlango Wa Kuhusu Kuishi Vizuri Na Wanawake

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "خَيْرُكُمْ خَيْرُكُمْ لِأَهْلِهِ، وَإِذَا مَاتَ صَاحِبُكُمْ، فَدَعُوهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mbora wenu ni mbora wenu kwa ahli zake; na anapofariki mwenzenu, basi mwacheni."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1451
Hadiyth
2306

56-Mlangoباب في تزويج الصغار إذا زوجهن آباؤهنMlango Wa Kuhusu Kuozwa Kwa Wasichana Wadogo
Ikiwa Baba Zao Ndio Waliowaoza

أَخْبَرَنَا إِسْمٰعِيلُ بْنُ خَلِيلٍ، أَنْبَأَنَا عَلِيُّ بْنُ مُسْهِرٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "تَزَوَّجَنِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَنَا بِنْتُ سِتِّ سِنِينَ، فَقَدِمْنَا الْمَدِينَةَ، فَنَزَلْنَا فِي بَنِي الْحَارِثِ بْنِ الْخَزْرَجِ فَوُعِكْتُ، فَتَمَرَّقَ رَأْسِي، فَأَوْفَى جُمَيْمَةً، فَأَتَتْنِي أُمُّ رُومَانَ وَإِنِّي لَفِي أُرْجُوحَةٍ وَمَعِي صَوَاحِبَاتٌ لِي، فَصَرَخَتْ بِي فَأَتَيْتُهَا وَمَا أَدْرِي مَا تُرِيدُ، فَأَخَذَتْ بِيَدِي حَتَّى أَوْقَفَتْنِي عَلَى بَابِ الدَّارِ، وَإِنِّي لَأَنْهَجُ حَتَّى سَكَنَ بَعْضُ نَفَسِي، ثُمَّ أَخَذَتْ شَيْئًا مِنْ مَاءٍ، فَمَسَحَتْ بِهِ وَجْهِي وَرَأْسِي، ثُمَّ أَدْخَلَتْنِي الدَّارَ، فَإِذَا نِسْوَةٌ مِنَ الْأَنْصَارِ فِي الْبَيْتِ، فَقُلْنَ: عَلَى الْخَيْرِ وَالْبَرَكَةِ، وَعَلَى خَيْرِ طَائِرٍ، فَأَسْلَمَتْنِي إِلَيْهِنَّ، فَأَصْلَحْنَ مِنْ شَأْنِي، فَلَمْ يَرُعْنِي إِلَّا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ضُحى، فَأَسْلَمَتْنِي إِلَيْهِ وَأَنَا يَوْمَئِذٍ ابْنَةُ تِسْعِ سِنِينَ"

Ametukhabarisha Ismaa'iyl bin Khaliyl, ametupa khabari 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alinifunga ndoa nikiwa binti wa miaka sita. Tukawasili Madiynah, tukafikia kwa Banuw Al-Haarith bin Al-Khazraj. Nikapatwa na homa, nywele za kichwa changu zikanyonyoka; kisha (nywele zangu) zikaota mpaka kufikia usawa wa mabega. Ummu Ruwmaan (رضي الله عنها) akanijia, nami niko juu ya bembea, na pamoja nami wako marafiki zangu. Akaniita kwa sauti, nikamwendea, na sijui anataka nini. Akanishika mkono mpaka akanisimamisha kwenye mlango wa nyumba, nami nikihema, mpaka sehemu ya pumzi yangu ikatulia. Kisha akachukua kiasi cha maji, akanipangusa nayo uso wangu na kichwa changu. Kisha akaniingiza ndani ya nyumba; mara kuna wanawake wa Answaar (رضي الله عنهن) ndani ya chumba, wakasema: (Umekuja) juu ya kheri na baraka, na juu ya bahati njema! Akanikabidhi kwao, wakanitengeneza (hali yangu). Na hakuna kilichonishtua isipokuwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) (aliyekuja) wakati wa Dhwuhaa (jua likiwa limepanda); akanikabidhi kwake, nami siku hiyo nikiwa binti wa miaka tisa."

Mjalada
3
Kitabu
11
Ukurasa
1451
Hadiyth
2307