Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy13 - Kitabu Cha Huduud (Adhabu Zilizowekwa Na Shariy'ah)

ومن كتاب الحدود

1-Mlangoباب رفع القلم عن ثلاثةMlango Wa Kuondolewa Kalamu Kwa Watu Watatu

أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ الْأَسْوَدِ، عَنْ عَائِشَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "رُفِعَ الْقَلَمُ عَنْ ثَلَاثَةٍ: عَنِ النَّائِمِ حَتَّى يَسْتَيْقِظَ، وَعَنِ الصَّغِيرِ حَتَّى يَحْتَلِمَ، وَعَنِ الْمَجْنُونِ حَتَّى يَعْقِلَ". وَقَدْ قَالَ حَمَّادٌ أَيْضًا: "وَعَنْ الْمَعْتُوهِ حَتَّى يَعْقِلَ"

Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Al-Aswad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kalamu (ya kuandika amali) imeondolewa kwa (watu) watatu: kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abaleghe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili." Na Hammaad amesema pia: "Na kwa punguani (mwenye upungufu wa akili) mpaka apate akili."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1477
Hadiyth
2342

2-Mlangoباب ما يحل به دم المسلمMlango Wa Yale
Ambayo Kwayo Damu Ya Muislamu Inakuwa Halaal

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ بْنِ سَهْلِ بْنِ حُنَيْفٍ، عَنْ عُثْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا يَحِلُّ دَمُ امْرِئٍ مُسْلِمٍ إِلَّا بِإِحْدَى ثَلَاثٍ: بِكُفْرٍ بَعْدَ إِيمَانٍ، أَوْ بِزِنًى بَعْدَ إِحْصَانٍ، أَوْ يَقْتُلُ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ فَيُقْتَلُ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Umaamah bin Sahl bin Hunayf, kutoka kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Si halaal damu ya mtu Muislamu isipokuwa kwa moja ya (mambo) matatu: kwa kufuru baada ya imaan, au kwa zinaa baada ya kuoa (au kuolewa), au aue nafsi bila (haki ya) nafsi, akauawa (kwa sababu hiyo)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1477
Hadiyth
2343

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُرَّةَ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَحِلُّ دَمُ رَجُلٍ يَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ إِلَّا أَحَدُ ثَلَاثَةِ نَفَرٍ: النَّفْسُ بِالنَّفْسِ، وَالثَّيِّبُ الزَّانِي، وَالتَّارِكُ لِدِينِهِ، الْمُفَارِقُ لِلْجَمَاعَةِ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Murrah, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Si halaal damu ya mtu anayeshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah, isipokuwa mmoja wa watu watatu: nafsi kwa nafsi, na thayyib (aliyekwisha kuoa au kuolewa) mzinifu, na mwenye kuiacha Dini yake, mwenye kujitenga na Jamaa'ah (ya Waislamu)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1478
Hadiyth
2344

3-Mlangoباب السارق توهب منه السرقة بعد ما سرقMlango Wa Mwizi Anayepewa Zawadi Ya Kitu Alichokiiba
Baada Ya Kuiba

أَخْبَرَنَا سَعْدُ بْنُ حَفْصٍ، حَدَّثَنَا شَيْبَانُ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: كَانَ صَفْوَانُ بْنُ أُمَيَّةَ نَائِمًا فِي الْمَسْجِدِ، فَأَتَاهُ رَجُلٌ وَهُوَ نَائِمٌ، فَاسْتَلَّ رِدَاءَهُ مِنْ تَحْتِ رَأْسِهِ، فتَنَبَّهَ بِهِ، فَلَحِقَهُ فَأَخَذَهُ فَانْطَلَقَ بِهِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، كُنْتُ نَائِمًا فِي الْمَسْجِدِ، فَأَتَانِي هَذَا فَاسْتَلَّ رِدَائِي مِنْ تَحْتِ رَأْسِي، فَلَحِقْتُهُ فَأَخَذْتُهُ، فَأَمَرَ بِقَطْعِهِ، فَقَالَ لَهُ صَفْوَانُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ رِدَائِي لَمْ يَبْلُغْ أَنْ يُقْطَعَ فِيهِ هَذَا؟ قَالَ: "فَهَلَّا، قَبْلَ أَنْ تَأْتِيَنِي بِهِ؟"

Ametukhabarisha Sa'd bin Hafsw, ametusimulia Shaybaan, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Swafwaan bin Umayyah (رضي الله عنه) alikuwa amelala Msikitini. Mtu mmoja akamjia naye amelala, akalichomoa joho lake kutoka chini ya kichwa chake. (Swafwaan) akazinduka kwa hilo, akamfuata akamkamata, akaenda naye kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Yaa Rasula-Allaah, nilikuwa nimelala Msikitini, akanijia huyu, akalichomoa joho langu kutoka chini ya kichwa changu; nikamfuata nikamkamata. (Nabiy) akaamrisha akatwe (mkono). Swafwaan (رضي الله عنه) akamwambia: Yaa Rasula-Allaah, hakika joho langu halijafikia (kiasi cha) kukatwa (mkono) huyu kwa sababu yake? Akasema: "Basi kwa nini (hukumsamehe) kabla hujaniletea?"

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1479
Hadiyth
2345

4-Mlangoباب ما تقطع فيه اليدMlango Wa Kile Ambacho Mkono Hukatwa Kwacho

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ الْهَاشِمِيُّ، أَنْبَأَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَمْرَةَ بِنْتِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَائِشَةَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "تُقْطَعُ الْيَدُ فِي رُبْعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا"

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Daawuwd Al-Haashimiy, ametupa khabari Ibraahiym bin Sa'd, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Amrah bint 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mkono hukatwa katika robo diynaar na zaidi."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1481
Hadiyth
2346

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَيُّوبَ، وَإِسْمَاعِيل بْنِ أُمَيَّةَ، وَعُبَيْدِ اللَّهِ، وَمُوسَى بْنِ عُقْبَة، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "قَطَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي مِجَنٍّ قِيمَتُهُ ثَلَاثَةُ دَرَاهِمَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ayyuwb, na Ismaa'iyl bin Umayyah, na 'Ubaydu-Allaah, na Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikata (mkono wa mwizi) katika ngao ambayo thamani yake ni dirham tatu."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1481
Hadiyth
2347

5-Mlangoباب الشفاعة في الحدود دون السلطانMlango Wa Uombezi Katika Huduud Kabla Ya Kumfikia Mtawala

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا اللَّيْثُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَائِشَةَ: أَنَّ قُرَيْشًا أَهَمَّهُمْ شَأْنُ الْمَرْأَةِ الْمَخْزُومِيَّةِ الَّتِي سَرَقَتْ، فَقَالُوا: مَنْ يُكَلِّمُ فِيهَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟، قَالُوا: وَمَنْ يَجْتَرِئُ عَلَيْهِ إِلَّا أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ حِبُّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَكَلَّمَهُ أُسَامَةُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَتَشْفَعُ فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللَّهِ؟" ثُمَّ قَامَ فَاخْتَطَبَ، فَقَالَ: "إِنَّمَا هَلَكَ الَّذِينَ قَبْلَكُمْ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا سَرَقَ فِيهُمُ الشَّرِيفُ، تَرَكُوهُ، وَإِذَا سَرَقَ فِيهِمُ الضَّعِيفُ، أَقَامُوا عَلَيْهِ الْحَدَّ، وَايْمُ اللَّهِ، لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ، لَقَطَعْتُ يَدَهَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Al-Layth, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Urwah bin Az-Zubayr, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), kwamba Quraysh walihangaishwa na jambo la mwanamke wa (ukoo wa) Makhzuwm aliyeiba. Wakasema: Nani atamzungumzia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu yeye? Wakasema: Na nani atathubutu kumwambia isipokuwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), kipenzi cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Usaamah (رضي الله عنه) akamzungumzia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, unaombea uombezi katika hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah) miongoni mwa Huduud za Allaah?" Kisha akasimama akakhutubu, akasema: "Hakika waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa kuwa walikuwa anapoiba kwao mtukufu, humwacha; na anapoiba kwao dhaifu, humsimamishia hadd. Na naapa kwa Allaah, lau Faatwimah bint Muhammad (رضي الله عنها) angeiba, ningeukata mkono wake."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1482
Hadiyth
2348

6-Mlangoباب المعترف بالسرقةMlango Wa Mwenye Kukiri Kuiba

أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَبِي الْمُنْذِرِ مَوْلَى أَبِي ذَرٍّ، عَنْ أَبِي أُمَيَّةَ الْمَخْزُومِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِسَارِقٍ اعْتَرَفَ اعْتِرَافًا، لَمْ يُوجَدْ مَعَهُ مَتَاعٌ، فَقَالَ: "مَا إِخَالُكَ سَرَقْتَ؟" قَالَ: بَلَى، قَالَ: "مَا إِخَالُكَ سَرَقْتَ؟" قَالَ: بَلَى، قَالَ: "فَاذْهَبُوا فَاقْطَعُوا يَدَهُ ثُمَّ جِيئُوا بِهِ" فَقَطَعُوا يَدَهُ، ثُمَّ جَاءُوا بِهِ، فَقَالَ: "اسْتَغْفِرِ اللَّهَ وَتُبْ إِلَيْهِ"، فَقَالَ: أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ، فَقَالَ: "اللَّهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ، اللَّهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Is-haaq bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Twalhah, kutoka kwa Abul-Mundhir, mwachwa huru wa Abuw Dharr (رضي الله عنه), kutoka kwa Abuw Umayyah Al-Makhzuwmiy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa mwizi aliyekiri kwa ukiri (wa wazi), na haikukutwa pamoja naye mali (aliyoiba). Akasema: "Sidhani kwamba umeiba!" Akasema: Bali (nimeiba). Akasema: "Sidhani kwamba umeiba!" Akasema: Bali (nimeiba). Akasema: "Basi nendeni mkaukate mkono wake, kisha mumlete." Wakaukata mkono wake, kisha wakamleta. Akasema: "Muombe Allaah Maghfirah na utubie Kwake." Akasema: Namuomba Allaah Maghfirah na natubia Kwake. Akasema:

اللَّهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ، اللَّهُمَّ تُبْ عَلَيْهِ

Yaa Allaah! Pokea tawbah yake. Yaa Allaah! Pokea tawbah yake.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1483
Hadiyth
2349

7-Mlangoباب ما لا يقطع فيه من الثمارMlango Wa Matunda Ambayo Mkono Haukatwi Kwa Kuyaiba

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا يَحْيَى هُوَ ابْنُ سَعِيدٍ، أَنَّ مُحَمَّدَ بْنَ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ أَخْبَرَهُ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا قَطْعَ فِي ثَمَرٍ وَلَا كَثَرٍ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Yahyaa — naye ni Ibn Sa'iyd —, kwamba Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan alimkhabarisha, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna kukatwa (mkono) katika matunda wala katika kathar (kiini cha mtende)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1485
Hadiyth
2350

حَدَّثَنَا الْحُسَيْنُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ رَجُلٍ مِنْ قَوْمِهِ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا قَطْعَ فِي ثَمَرٍ وَلَا كَثَرٍ"

Ametusimulia Al-Husayn bin Manswuwr, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa mtu mmoja wa watu wake, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakuna kukatwa (mkono) katika matunda wala katika kathar (kiini cha mtende)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1485
Hadiyth
2351

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا وَكِيعٌ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ عَمِّهِ وَاسِعِ بْنِ حَبَّانَ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا قَطْعَ فِي ثَمَرٍ وَلَا كَثَرٍ".

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Wakiy', kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa ami yake Waasi' bin Habbaan, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna kukatwa (mkono) katika matunda wala katika kathar (kiini cha mtende)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1485
Hadiyth
2352

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَحْوَهُ

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1485
Hadiyth
2353

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، وَالثَّقَفِيُّ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا قَطْعَ فِي ثَمَرٍ وَلَا كَثَرٍ". قَالَ: وَهُوَ شَحْمُ النَّخْلِ. وَالْكَثَرُ: الْجُمَّارُ

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Jariyr na Ath-Thaqafiy, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, amenikhabarisha Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna kukatwa (mkono) katika matunda wala katika kathar (kiini cha mtende)." Akasema: Nalo ni shahamu ya mtende. Na al-kathar ni al-jummaar (kiini cheupe kilicho juu ya shina la mtende).

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1486
Hadiyth
2354

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ يَحْيَى بْنِ حَبَّانَ، عَنْ أَبِي مَيْمُونٍ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا قَطْعَ فِي كَثَرٍ". قَالَ أَبُو مُحَمَّد: الْقَوْلُ مَا قَالَ أَبُو أُسَامَةَ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa Muhammad bin Yahyaa bin Habbaan, kutoka kwa Abuw Maymuwn, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna kukatwa (mkono) katika kathar (kiini cha mtende)."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Kauli (iliyo sahihi) ni ile aliyoisema Abuw Usaamah.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1487
Hadiyth
2355

8-Mlangoباب ما لا يقطع من السراقMlango Wa Wezi Wasiokatwa Mikono

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَنْبَأَنَا أَبُو الزُّبَيْرِ، قَالَ أَبُو الزُّبَيْرِ: قَالَ جَابِرٌ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَيْسَ عَلَى الْمُنْتَهِبِ، وَلَا عَلَى الْمُخْتَلِسِ، وَلَا عَلَى الْخَائِنِ قَطْعٌ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Ametupa khabari Abuz-Zubayr: Abuz-Zubayr amesema: Jaabir (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna (adhabu ya) kukatwa (mkono) juu ya mporaji (anayechukua mali kwa nguvu hadharani), wala juu ya mnyakuzi (anayenyakua mali kwa haraka akakimbia), wala juu ya mfanya khiyana (aliyeaminiwa mali akaifanyia khiyana)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1487
Hadiyth
2356

9-Mlangoباب في حد الخمرMlango Wa Kuhusu Adhabu Ya Hadd Ya Khamr (Pombe)

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، "أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِرَجُلٍ قَدْ شَرِبَ خَمْرًا فَضَرَبَهُ بِجَرِيدَتَيْنِ"، ثُمَّ فَعَلَ أَبُو بَكْرٍ مِثْلَ ذَلِكَ، فَلَمَّا كَانَ عُمَرُ: اسْتَشَارَ النَّاسَ، فَقَالَ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَوْفٍ: أَخَفُّ الْحُدُودِ: ثَمَانِينَ، قَالَ: فَفَعَلَ

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kwamba "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa mtu aliyekunywa khamr (pombe), akampiga kwa makuti mawili ya mtende." Kisha Abuw Bakr (رضي الله عنه) akafanya mfano wa hivyo. Ilipokuwa (zama za) 'Umar (رضي الله عنه), aliwataka shauri watu. 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf (رضي الله عنه) akasema: Iliyo nyepesi kabisa katika Huduud (adhabu zilizowekwa na Shariy'ah) ni themanini. Akasema: Akafanya (hivyo).

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1488
Hadiyth
2357

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ الْمُخْتَارِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ الدَّانَاجُ، حَدَّثَنَا حُضَيْنُ بْنُ الْمُنْذِرِ الرَّقَاشِيُّ، قَالَ: شَهِدْتُ عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ وَأُتِيَ بِالْوَلِيدِ بْنِ عُقْبَةَ، فَقَالَ عَلِيٌّ: "جَلَدَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَرْبَعِينَ، وَجَلَدَ أَبُو بَكْرٍ أَرْبَعِينَ، وَعُمَرُ ثَمَانِينَ، وَكُلٌّ سُنَّةٌ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametupa khabari 'Abdul-'Aziyz bin Al-Mukhtaar, ametusimulia 'Abdu-Allaah Ad-Daanaaj, ametusimulia Hudhwayn bin Al-Mundhir Ar-Raqaashiy, amesema: Nilikuwepo kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) alipoletewa Al-Waliyd bin 'Uqbah (رضي الله عنه). 'Aliy (رضي الله عنه) akasema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga mijeledi arubaini, na Abuw Bakr (رضي الله عنه) alipiga mijeledi arubaini, na 'Umar (رضي الله عنه) themanini; na kila moja ni Sunnah."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1488
Hadiyth
2358

10-Mlangoباب في شارب الخمر إذا أتي به الرابعةMlango Wa Kuhusu Mnywaji Khamr
(Pombe) Anapoletwa Mara Ya Nne

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ هُوَ ابْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُتْبَةَ بْنِ عُرْوَةَ بْنِ مَسْعُودٍ الثَّقَفِيُّ، عَنْ عَمْرِو بْنِ الشَّرِيدِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِذَا شَرِبَ أَحَدُكُمْ فَاضْرِبُوهُ، ثُمَّ إِنْ عَادَ، فَاضْرِبُوهُ، ثُمَّ إِنْ عَادَ، فَاضْرِبُوهُ، ثُمَّ إِنْ عَادَ الرَّابِعَةَ فَاقْتُلُوهُ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd — naye ni Ibn Zuray' —, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Utbah bin 'Urwah bin Mas'uwd Ath-Thaqafiy, kutoka kwa 'Amr bin Ash-Shariyd, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mmoja wenu akinywa (khamr), basi mpigeni; kisha akirudia, mpigeni; kisha akirudia, mpigeni; kisha akirudia mara ya nne, muueni."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1489
Hadiyth
2359

11-Mlangoباب التعزير في الذنوبMlango Wa Ta'ziyr (Adhabu Ya Kuadabisha) Katika Madhambi

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ، حَدَّثَنِي يَزِيدُ بْنُ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ بُكَيْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْأَشَجِّ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ هُوَ ابْنُ جَابِرٍ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ نِيَارٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا يَحِلُّ لِأَحَدٍ أَنْ يَضْرِبَ أَحَدًا فَوْقَ عَشْرَةِ أَسْوَاطٍ إِلَّا فِي حَدٍّ مِنْ حُدُودِ اللَّهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb —, amenisimulia Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Bukayr bin 'Abdi-Allaah bin Al-Ashajj, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan — naye ni Ibn Jaabir —, kutoka kwa Abuw Burdah bin Niyaar (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Si halaal kwa yeyote kumpiga yeyote zaidi ya mijeledi kumi, isipokuwa katika hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah) miongoni mwa Huduud za Allaah."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1490
Hadiyth
2360

12-Mlangoباب الاعتراف بالزناMlango Wa Kukiri Zinaa

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَنِي ابْنُ شِهَابٍ، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ جَابِرٍ: أَنَّ رَجُلًا مِنْ أَسْلَمَ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَحَدَّثَهُ أَنَّهُ زَنَى فَشَهِدَ عَلَى نَفْسِهِ أَنَّهُ زَنَى أَرْبَعًا، فَأَمَرَ بِرَجْمِهِ وَكَانَ قَدْ أُحْصِنَ "

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, ametusimulia Ibn Jurayj, amenikhabarisha Ibn Shihaab, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba mtu mmoja wa (kabila la) Aslam alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akamsimulia kwamba amezini, akajishuhudia nafsi yake mara nne kwamba amezini. Akaamrisha apigwe mawe, naye alikuwa amekwisha kuoa.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1491
Hadiyth
2361

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ سِمَاكٍ، أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرَ بْنَ سَمُرَةَ يَقُولُ: أُتِيَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَاعِزِ بْنِ مَالِكٍ رَجُلٍ قَصِيرٍ فِي إِزَارٍ مَا عَلَيْهِ رِدَاءٌ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُتَّكِئٌ عَلَى وِسَادَةٍ عَلَى يَسَارِهِ فَكَلَّمَهُ، فَمَا أَدْرِي مَا يُكَلِّمُهُ بِهِ، وَأَنَا بَعِيدٌ مِنْهُ، بَيْنِي وَبَيْنَهُ الْقَوْمُ، فَقَالَ: "اذْهَبُوا بِهِ فَارْجُمُوهُ"، ثُمَّ قَالَ: "رُدُّوهُ"، فَكَلَّمَهُ أَيْضًا وَأَنَا أَسْمَعُ غَيْرَ أَنَّ بَيْنِي وَبَيْنَهُ الْقَوْمُ، ثُمَّ قَالَ: "اذْهَبُوا بِهِ فَارْجُمُوهُ"، ثُمَّ قَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَخَطَبَ وَأَنَا أَسْمَعُهُ، ثُمَّ قَالَ: "كُلَّمَا نَفَرْنَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ، خَلَفَ أَحَدُهُمْ لَهُ نَبِيبٌ كَنَبِيبِ التَّيْسِ يَمْنَحُ إِحْدَاهُنَّ الْكُثْبَةَ مِنَ اللَّبَنِ؟ وَاللَّهِ لَا أَقْدِرُ عَلَى أَحَدٍ مِنْهُمْ، إِلَّا نَكَّلْتُ بِهِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Simaak, kwamba alimsikia Jaabir bin Samurah (رضي الله عنهما) akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه) — mtu mfupi, amevaa izari, hana joho juu yake —, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ameegemea mto upande wake wa kushoto. Akamsemesha; wala sijui alikuwa akimsemesha nini, nami nilikuwa mbali naye, baina yangu na yeye wapo watu. Akasema: "Mpelekeni mkampige mawe." Kisha akasema: "Mrudisheni." Akamsemesha tena, nami nikisikia, isipokuwa baina yangu na yeye wapo watu. Kisha akasema: "Mpelekeni mkampige mawe." Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasimama akakhutubu, nami nikimsikia; kisha akasema: "Je, kila tunapotoka kwenda katika njia ya Allaah, mmoja wao hubaki nyuma akiwa na sauti kama sauti ya beberu la mbuzi, akimpa mmoja wao (wanawake) maziwa kidogo? Wa-Allaahi, sitamweza yeyote miongoni mwao isipokuwa nitamwadhibu (adhabu ya) kuwa funzo (kwa wengine)."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1491
Hadiyth
2362

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، وَزَيْدِ بْنِ خَالِدٍ، وَشِبْلٍ، قَالُوا: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَنْشُدُكَ اللَّهَ إِلَّا قَضَيْتَ بَيْنَنَا بِكِتَابِ اللَّهِ، فَقَالَ خَصْمُهُ وَكَانَ أَفْقَهَ مِنْهُ: صَدَقَ، اقْضِ بَيْنَنَا بِكِتَابِ اللَّهِ، وَأْذَنْ لِي يَا رَسُولَ اللَّهِ أَنْ أَتَكَلَّمَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "قُلْ"، فَقَالَ: إِنَّ ابْنِي كَانَ عَسِيفًا عَلَى أَهْلِ هَذَا، فَزَنَى بِامْرَأَتِهِ، فَافْتَدَيْتُ مِنْهُ بِمِائَةِ شَاةٍ وَخَادِمٍ، وَإِنِّي سَأَلْتُ رِجَالًا مِنْ أَهْلِ الْعِلْمِ، فَأَخْبَرُونِي أَنَّ عَلَى ابْنِي جَلْدَ مِائَةٍ وَتَغْرِيبَ عَامٍ، وَأَنَّ عَلَى امْرَأَةِ هَذَا الرَّجْمَ، فَقَالَ: "وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَأَقْضِيَنَّ بَيْنَكُمَا بِكِتَابِ اللَّهِ: الْمِائَةُ شَاةٍ وَالْخَادِمُ رَدٌّ عَلَيْكَ، وَعَلَى ابْنِكَ جَلْدُ مِائَةٍ وَتَغْرِيبُ عَامٍ، وَيَا أُنَيْسُ اغْدُ عَلَى امْرَأَةِ هَذَا فَسَلْهَا، فَإِنْ اعْتَرَفَتْ، فَارْجُمْهَا"، فَاعْتَرَفَتْ، فَرَجَمَهَا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan bin 'Uyaynah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa Abuw Hurayrah na Zayd bin Khaalid (رضي الله عنهما), na Shibl, wamesema: Mtu mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Nakuapisha kwa Allaah, isipokuwa utuhukumu baina yetu kwa Kitabu cha Allaah. Mgomvi wake — naye alikuwa na ufahamu zaidi kuliko yeye — akasema: Amesema kweli; tuhukumu baina yetu kwa Kitabu cha Allaah, na uniruhusu, yaa Rasula-Allaah, nizungumze. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Sema." Akasema: Hakika mwanangu alikuwa 'asiyf (mfanyakazi wa kuajiriwa) kwa watu wa huyu, akazini na mke wake; nikamkomboa kutoka kwake kwa mbuzi mia moja na mtumishi. Na hakika mimi niliwauliza wanaume miongoni mwa wenye ilimu, wakanikhabarisha kwamba juu ya mwanangu ni mijeledi mia moja na kuhamishwa (mji) mwaka mmoja, na kwamba juu ya mke wa huyu ni kupigwa mawe. Akasema: "Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake! Kwa yakini nitahukumu baina yenu wawili kwa Kitabu cha Allaah: mbuzi mia moja na mtumishi ni marejesho kwako; na juu ya mwanao ni mijeledi mia moja na kuhamishwa (mji) mwaka mmoja. Na yaa Unays, nenda asubuhi kwa mke wa huyu umuulize; akikiri, mpige mawe." Akakiri, akampiga mawe.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1492
Hadiyth
2363

13-Mlangoباب المعترف يرجع عن اعترافهMlango Wa Mwenye Kukiri Anayerudi
Nyuma Katika Kukiri Kwake

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ ابْنُ إِسْحَاق بْنِ يَسَارٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيُّ، عَنْ أَبِي الْهَيْثَمِ بْنِ نَصْرِ بْنِ دَهْرٍ الْأَسْلَمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كُنْتُ فِيمَنْ رَجَمَهُ، قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: يَعْنِي مَاعِزَ بْنَ مَالِكٍ، فلَمَّا وَجَدَ مَسَّ الْحِجَارَةِ، جَزِعَ جَزَعًا شَدِيدًا، قَالَ: فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "فَهَلَّا تَرَكْتُمُوهُ؟"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq bin Yasaar —, ametusimulia Muhammad bin Ibraahiym At-Taymiy, kutoka kwa Abul-Haytham bin Naswr bin Dahr Al-Aslamiy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa miongoni mwa waliompiga mawe — Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yaani Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه) —. Alipohisi mguso wa mawe, alifazaika fazaa kubwa. Akasema: Tukamtajia hilo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: "Basi kwa nini hamkumwacha?"

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1493
Hadiyth
2364

14-Mlangoباب الحفر لمن يراد رجمهMlango Wa Kumchimbia Shimo Anayetakiwa Kupigwa Mawe

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي زَائِدَةَ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "انْطَلِقُوا بِمَاعِزِ بْنِ مَالِكٍ، فَارْجُمُوهُ". فَانْطَلَقْنَا بِهِ إِلَى بَقِيعِ الْغَرْقَدِ، فَوَاللَّهِ مَا أَوْثَقْنَاهُ وَلَا حَفَرْنَا لَهُ، وَلَكِنْ قَامَ فَرَمَيْنَاهُ بِالْعِظَامِ وَالْخَزَفِ وَالْجَنْدَلِ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Zaaidah, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mpelekeni Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه), mkampige mawe." Tukaenda naye mpaka Baqiy' Al-Gharqad. Wa-Allaahi, hatukumfunga wala hatukumchimbia shimo, lakini alisimama, tukampiga kwa mifupa, na vigae, na mawe makubwa.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1494
Hadiyth
2365

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا بَشِيرُ بْنُ الْمُهَاجِرِ، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَهُ رَجُلٌ يُقَالُ لَهُ مَاعِزُ بْنُ مَالِكٍ، فَاعْتَرَفَ عِنْدَهُ بِالزِّنَا، فَرَدَّهُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ جَاءَ الرَّابِعَةَ فَاعْتَرَفَ، "فَأَمَرَ بِهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَحُفِرَ لَهُ حُفْرَةٌ فَجُعِلَ فِيهَا إِلَى صَدْرِهِ، وَأَمَرَ النَّاسَ أَنْ يَرْجُمُوهُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Bashiyr bin Al-Muhaajir, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Buraydah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa nimeketi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); akamjia mtu mmoja aitwaye Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه), akakiri mbele yake zinaa. Akamrudisha mara tatu; kisha akaja mara ya nne, akakiri. "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha juu yake, akachimbiwa shimo, akawekwa ndani yake hadi kifuani mwake; na akawaamrisha watu wampige mawe."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1494
Hadiyth
2366

15-Mlangoباب في الحكم بين أهل الكتاب إذا تحاكموا إلى حكام المسلمينMlango Wa Kuhusu Kuhukumu Baina Ya Ahlul-Kitaab
(Watu Wa Kitabu) Wanapopeleka Mashtaka Yao
Kwa Mahakimu Wa Waislamu

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ عُقْبَةَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ: أَنَّ الْيَهُودَ جَاءُوا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِرَجُلٍ مِنْهُمْ وَامْرَأَةٍ قَدْ زَنَيَا، فَقَالَ: "كَيْفَ تَفْعَلُونَ بِمَنْ زَنَى مِنْكُمْ؟". قَالُوا: لَا نَجِدُ فِيهَا شَيْئًا، فَقَالَ لَهُمْ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَلَامٍ: كَذَبْتُمْ، فِي التَّوْرَاةِ الرَّجْمُ، فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ فَجَاءُوا بِالتَّوْرَاةِ، فَوَضَعَ مِدْرَاسُهَا الَّذِي يَدْرُسُهَا مِنْهُمْ كَفَّهُ عَلَى آيَةِ الرَّجْمِ، فَقَالَ: مَا هَذِهِ؟ فَلَمَّا رَأَوْا ذَلِكَ قَالُوا: هِيَ آيَةُ الرَّجْمِ، "فَأَمَرَ بِهِمَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ" فَرُجِمَا قَرِيبًا مِنْ حَيْثُ تُوضَعُ الْجَنَائِزُ عِنْدَ الْمَسْجِدِ. قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: فَرَأَيْتُ صَاحِبَهَا يَجْنَأُ عَلَيْهَا: يَقِيهَا الْحِجَارَةَ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zuhayr, ametusimulia Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Mayahudi walikuja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na mwanamume mmoja miongoni mwao na mwanamke waliokwisha kuzini. Akasema: "Mnafanya nini kwa aliyezini miongoni mwenu?" Wakasema: Hatukuti chochote kuhusu hilo. 'Abdu-Allaah bin Salaam (رضي الله عنه) akawaambia: Mmesema uongo! Katika Tawraat kuna (hukumu ya) kupiga mawe.

فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ

Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli [Aal-‘Imraan (3:93)]

Wakaileta Tawraat. Msomaji wake aliyekuwa akiisoma (Tawraat) miongoni mwao akaweka kiganja chake juu ya Aayah ya kupiga mawe. [Ibn Salaam (رضي الله عنه)] akasema: Ni nini hii? Walipoona hivyo, wakasema: Hiyo ni Aayah ya kupiga mawe. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha juu yao wawili, wakapigwa mawe karibu na mahali yanapowekwa majeneza, karibu na Msikiti. 'Abdu-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما) amesema: Nikamwona mwenzake (mwanamume) akiinama juu yake (mwanamke), akimkinga dhidi ya mawe.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1495
Hadiyth
2367

16-Mlangoباب في حد المحصنين بالزناMlango Wa Kuhusu Adhabu Ya Hadd Ya Waliokwisha Kuoa
Au Kuolewa Wanapozini

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى، بَعَثَ مُحَمَّدًا صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالْحَقِّ، وَأَنْزَلَ عَلَيْهِ الْكِتَابَ، وَكَانَ فِيمَا أَنْزَلَ آيَةُ الرَّجْمِ، فَقَرَأْنَاهَا وَوَعَيْنَاهَا وَعَقَلْنَاهَا، وَرَجَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَرَجَمْنَا بَعْدَهُ، فَأَخْشَى إِنْ طَالَ بِالنَّاسِ زَمَانٌ أَنْ يَقُولَ الْقَائِلُ: لَا نَجِدُ حَدَّ آيَةِ الرَّجْمِ فِي كِتَابِ اللَّهِ، وَالرَّجْمُ فِي كِتَابِ اللَّهِ حَقٌّ عَلَى مَنْ زَنَى مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ إِذَا أُحْصِنَّ، إِذَا قَامَتْ عَلَيْهِ الْبَيِّنَةُ، أَوْ كَانَ الْحَبَلُ أَوِ الِاعْتِرَافُ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Hakika Allaah (تعالى) Alimtuma Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki, na Akamteremshia Kitabu; na ikawa miongoni mwa Aliyoyateremsha ni Aayah ya kupiga mawe. Tuliisoma, tukaihifadhi na tukaifahamu. Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipiga mawe, nasi tukapiga mawe baada yake. Basi nahofia, muda ukirefuka juu ya watu, msemaji aseme: Hatuikuti hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah) ya Aayah ya kupiga mawe katika Kitabu cha Allaah. Na kupiga mawe katika Kitabu cha Allaah ni haki juu ya aliyezini miongoni mwa wanaume na wanawake wanapokuwa wamekwisha kuoa au kuolewa, ushahidi ukisimama juu yake, au ikawa mimba, au kukiri."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1496
Hadiyth
2368

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الرِّفَاعِيُّ، حَدَّثَنَا الْعَقَدِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ يُونُسَ بْنِ جُبَيْرٍ يُحَدِّثُ: عَنْ كَثِيرِ بْنِ الصَّلْتِ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، قَالَ: أَشْهَدُ لَسَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الشَّيْخُ وَالشَّيْخَةُ إِذَا زَنَيَا، فَارْجُمُوهُمَا الْبَتَّةَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Ar-Rifaa'iy, ametusimulia Al-'Aqadiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Yuwnus bin Jubayr, akisimulia kutoka kwa Kathiyr bin Asw-Swalt, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), amesema: Ninashuhudia kwamba hakika nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mzee mwanamume na mzee mwanamke wakizini, basi wapigeni mawe bila shaka yoyote."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1497
Hadiyth
2368

17-Mlangoباب الحامل إذا اعترفت بالزناMlango Wa Mwanamke Mjamzito Anapokiri Zinaa

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا بَشِيرُ بْنُ الْمُهَاجِرِ، حَدَّثَنِي عَبْدُ اللَّهِ بْنُ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كُنْتُ جَالِسًا عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَجَاءَتْهُ امْرَأَةٌ مِنْ بَنِي غَامِدٍ، فَقَالَتْ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي قَدْ زَنَيْتُ، وَإِنِّي أُرِيدُ أَنْ تُطَهِّرَنِي، فَقَالَ لَهَا: "ارْجِعِي". فَلَمَّا كَانَ مِنْ الْغَدِ، أَتَتْهُ أَيْضًا، فَاعْتَرَفَتْ عِنْدَهُ بِالزِّنَا، فَقَالَتْ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، طَهِّرْنِي، فَلَعَلَّكَ أَنْ تَرْدُدَنِي كَمَا رَدَدْتَ مَاعِزَ بْنَ مَالِكٍ، فَوَاللَّهِ إِنِّي لَحُبْلَى، فَقَالَ لَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ارْجِعِي، حَتَّى تَلِدِي". فَلَمَّا وَلَدَتْ، جَاءَتْ بِالصَّبِيِّ تَحْمِلُهُ فِي خِرْقَةٍ، فَقَالَتْ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ هَذَا قَدْ وَلَدْتُ، فَقَالَ: "فَاذْهَبِي فَأَرْضِعِيهِ، ثُمَّ افْطُمِيهِ". فَلَمَّا فَطَمَتْهُ، جَاءَتْ بِالصَّبِيِّ فِي يَدِهِ كِسْرَةُ خُبْزٍ، فَقَالَتْ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ، قَدْ فَطَمْتُهُ، فَأَمَرَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالصَّبِيِّ فَدُفِعَ إِلَى رَجُلٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ، وَأَمَرَ بِهَا فَحُفِرَ لَهَا حُفْرَةٌ، فَجُعِلَتْ فِيهَا إِلَى صَدْرِهَا، ثُمَّ أَمَرَ النَّاسَ أَنْ يَرْجُمُوهَا، فَأَقْبَلَ خَالِدُ بْنُ الْوَلِيدِ بِحَجَرٍ فَرَمَى رَأْسَهَا، فَتَلَطَّخَ الدَّمُ عَلَى وَجْنَةِ خَالِدِ بْنِ الْوَلِيدِ، فَسَبَّهَا، فَسَمِعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَبَّهُ إِيَّاهَا، فَقَالَ: "مَهْ يَا خَالِدُ، لَا تَسُبَّهَا، فَوَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَقَدْ تَابَتْ تَوْبَةً، لَوْ تَابَهَا صَاحِبُ مَكْسٍ، لَغُفِرَ لَهُ". فَأَمَرَ بِهَا فَصُلِّيَ عَلَيْهَا، وَدُفِنَتْ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Bashiyr bin Al-Muhaajir, amenisimulia 'Abdu-Allaah bin Buraydah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa nimeketi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); akamjia mwanamke mmoja wa Banuw Ghaamid, akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, hakika mimi nimezini, na hakika mimi nataka unitakase. Akamwambia: "Rudi." Ilipokuwa kesho yake, akamjia tena, akakiri mbele yake zinaa, akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, nitakase; huenda ukanirudisha kama ulivyomrudisha Maa'iz bin Maalik (رضي الله عنه). Wa-Allaahi, hakika mimi ni mjamzito. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Rudi mpaka uzae." Alipozaa, akaja na mtoto akimbeba katika kitambaa, akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, huyu nimekwisha kumzaa. Akasema: "Basi nenda ukamnyonyeshe, kisha umwachishe ziwa." Alipomwachisha ziwa, akaja na mtoto akiwa na kipande cha mkate mkononi mwake, akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, nimekwisha kumwachisha ziwa. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha kuhusu mtoto, akakabidhiwa mtu mmoja miongoni mwa Waislamu (رضي الله عنهم); na akaamrisha juu yake (mwanamke), akachimbiwa shimo, akawekwa ndani yake hadi kifuani mwake; kisha akawaamrisha watu wampige mawe. Khaalid bin Al-Waliyd (رضي الله عنه) akaja na jiwe, akampiga kichwa chake; damu ikarukia shavu la Khaalid bin Al-Waliyd (رضي الله عنه), akamtukana. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasikia matusi yake kwake, akasema: "Taratibu, yaa Khaalid! Usimtukane. Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, kwa hakika ametubu tawbah ambayo lau angeitubu mtozaji ushuru wa dhulma, angeghufuriwa." Akaamrisha juu yake, akaswaliwa, na akazikwa.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1497
Hadiyth
2369

حَدَّثَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ: أَنَّ امْرَأَةً مِنْ جُهَيْنَةَ أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهِيَ حُبْلَى مِنَ الزِّنَا، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي أَصَبْتُ حَدًّا فَأَقِمْهُ عَلَيَّ، فَدَعَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلِيَّهَا، فَقَالَ: "اذْهَبْ فَأَحْسِنْ إِلَيْهَا، فَإِذَا وَضَعَتْ حَمْلَهَا، فَأْتِنِي بِهَا". فَفَعَلَ، فَأَمَرَ بِهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَشُكَّتْ عَلَيْهَا ثِيَابُهَا ثُمَّ أَمَرَ بِهَا فَرُجِمَتْ ثُمَّ صَلَّى عَلَيْهَا، فَقَالَ عُمَرُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَتُصَلِّي عَلَيْهَا وَقَدْ زَنَتْ؟، فَقَالَ: "لَقَدْ تَابَتْ تَوْبَةً لَوْ قُسِمَتْ بَيْنَ سَبْعِينَ مِنْ أَهْلِ الْمَدِينَةِ لَوَسِعَتْهُمْ، وَهَلْ وَجَدْتَ أَفْضَلَ مِنْ أَنْ جَادَتْ بِنَفْسِهَا لِلَّهِ عز وجل"

Ametusimulia Wahb bin Jariyr, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhallab, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), kwamba mwanamke mmoja wa (kabila la) Juhaynah alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye ni mjamzito kutokana na zinaa, akasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi nimefanya (kosa la) hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah), basi nisimamishie. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita walii wake, akasema: "Nenda ukamfanyie wema; atakapozaa mimba yake, niletee." Akafanya (hivyo). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha juu yake, nguo zake zikafungwa vizuri juu yake; kisha akaamrisha juu yake, akapigwa mawe; kisha akamswalia. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: Yaa Rasula-Allaah, unamswalia naye amezini? Akasema: "Kwa hakika ametubu tawbah ambayo lau ingegawanywa baina ya watu sabini wa Madiynah, ingewatosheleza. Na je, umepata (jambo) bora zaidi kuliko kujitoa nafsi yake kwa ajili ya Allaah (عز وجل)?"

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1498
Hadiyth
2370

18-Mlangoباب في المماليك إذا زنوا يقيم سادتهم عليهم الحد دون السلطانMlango Wa Kuhusu Watumwa Wanapozini, Mabwana Zao
Huwasimamishia Hadd (Adhabu Iliyowekwa
Na Shariy'ah) Bila Ya Mtawala

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الْجُهَنِيِّ وَأَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُئِلَ عَنِ الْأَمَةِ تَزْنِي وَلَمْ تُحْصَنْ، فَقَالَ: "إِنْ زَنَتْ، فَاجْلِدُوهَا، ثُمَّ إِنْ زَنَتْ فَاجْلِدُوهَا". قَالَ: فَمَا أَدْرِي فِي الثَّالِثَةِ أَوْ فِي الرَّابِعَةِ "فَبِيعُوهَا وَلَوْ بِضَفِيرٍ"

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah bin 'Utbah, kutoka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniy na Abuw Hurayrah (رضي الله عنهما): Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu mjakazi anayezini naye hajaolewa. Akasema: "Akizini, mpigeni mijeledi; kisha akizini, mpigeni mijeledi." Amesema: Basi sijui ni katika (mara ya) tatu au katika (mara ya) nne: "Basi muuzeni, hata kwa kamba iliyosokotwa."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1499
Hadiyth
2371

19-Mlangoباب في تفسير قول الله تعالى أو يجعل الله لهن سبيلاMlango Wa Kuhusu Tafsiyr Ya Kauli Ya Allaah (تعالى) :
«au Allaah Awajaalie njia (nyingine)» [An-Nisaa (4:15)]

أَخْبَرَنَا بِشْرُ بْنُ عُمَرَ الزَّهْرَانِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ حِطَّانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "خُذُوا عَنِّي خُذُوا عَنِّي. قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلًا: الْبِكْرُ بِالْبِكْرِ، وَالثَّيِّبُ بِالثَّيِّبِ: الْبِكْرُ جَلْدُ مِائَةٍ وَنَفْيُ سَنَةٍ، وَالثَّيِّبُ جَلْدُ مِائَةٍ وَالرَّجْمُ"،

Ametukhabarisha Bishr bin 'Umar Az-Zahraaniy, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Hittwaan bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Ubaadah bin As-Swaamit (رضي الله عنه): Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Chukueni kutoka kwangu! Chukueni kutoka kwangu! Allaah Amekwisha wajaalia njia (nyingine): Bikra (anayezini) na bikra, na thayyib (aliyekwisha oa au kuolewa) na thayyib: bikra ni mijeledi mia moja na kuhamishwa mwaka mmoja, na thayyib ni mijeledi mia moja na kupigwa mawe."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1500
Hadiyth
2372

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَخْبَرَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ حِطَّانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِنَحْوِهِ

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametukhabarisha Hushaym, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Hittwaan bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa 'Ubaadah bin As-Swaamit (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1500
Hadiyth
2373

20-Mlangoباب فيمن يقع على جارية امرأتهMlango Wa Kuhusu Anayemwingilia Mjakazi Wa Mkewe

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا أَبَانُ بْنُ يَزِيدَ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ: كَتَبَ إِلَيَّ خَالِدُ بْنُ عُرْفُطَةَ عَنْ حَبِيبِ بْنِ سَالِمٍ: أَنَّ غُلَامًا كَانَ يُنْبَزُ فُرْفُورًا، فَوَقَعَ عَلَى جَارِيَةِ امْرَأَتِهِ، فَرُفِعَ ذَلِكَ إِلَى النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، فَقَالَ: لَأَقْضِيَنَّ فِيهِ بِقَضَاءٍ شَافٍ: "إِنْ كَانَتْ أَحَلَّتْهَا لَهُ جَلَدْتُهُ مِائَةً، وَإِنْ كَانَتْ لَمْ تُحِلَّهَا لَهُ، رَجَمْتُهُ"، فَقِيلَ لَهَا: زَوْجُكِ!، فَقَالَتْ: إِنِّي قَدْ أَحْلَلْتُهَا لَهُ. فَضَرَبَهُ مِائَةً. قَالَ يَحْيَى: هُوَ مَرْفُوعٌ.

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hammaad, ametusimulia Abaan bin Yaziyd, kutoka kwa Qataadah, amesema: Khaalid bin 'Urfutwah aliniandikia, kutoka kwa Habiyb bin Saalim: Kwamba kijana mmoja aliyekuwa akipachikwa lakabu ya Furfuwr, alimwingilia mjakazi wa mkewe. Jambo hilo likapelekwa kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما), akasema: Hakika nitaamua kuhusu hilo kwa uamuzi wa kutosheleza: "Ikiwa (mkewe) alimhalalishia (mjakazi huyo), nitampiga mijeledi mia moja; na ikiwa hakumhalalishia, nitampiga mawe." (Mkewe) akaambiwa: Mumeo! Akasema: Hakika mimi nilikuwa nimemhalalishia. Akampiga (mijeledi) mia moja. Yahyaa amesema: Hiyo ni Marfuu' (iliyopandishwa).

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1501
Hadiyth
2374

حَدَّثَنَا صَدَقَةُ بْنُ الْفَضْلِ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عُرْفُطَةَ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ سَالِمٍ، عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَحْوَهُ

Ametusimulia Swadaqah bin Al-Fadhwl, ametupa khabari Muhammad bin Ja'far, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Khaalid bin 'Urfutwah, kutoka kwa Habiyb bin Saalim, kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1502
Hadiyth
2375

21-Mlangoباب الحد كفارة لمن أقيم عليهMlango Wa Hadd (Adhabu Iliyowekwa
Na Shariy'ah) Ni Kafara Kwa Aliyesimamishiwa

أَخْبَرَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ الدِّمَشْقِيُّ، حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنَكْدِرِ، عَنْ ابْنِ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أُقِيمَ عَلَيْهِ حَدٌّ، غُفِرَ لَهُ ذَلِكَ الذَّنْبُ"

Ametukhabarisha Marwaan bin Muhammad Ad-Dimashqiy, ametusimulia Ibn Wahb, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, kutoka kwa Muhammad bin Al-Munkadir, kutoka kwa Ibn Khuzaymah bin Thaabit, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayesimamishiwa hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah), ataghufuriwa dhambi hiyo."

Mjalada
3
Kitabu
13
Ukurasa
1502
Hadiyth
2376