Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy14 - Kitabu Cha Nadhiri Na Viapo

ومن كتاب النذور والأيمان

1-Mlangoباب الوفاء بالنذرMlango Wa Kutimiza Nadhiri

أَخْبَرَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي بِشْرٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ امْرَأَةً نَذَرَتْ أَنْ تَحُجَّ فَمَاتَتْ، فَجَاءَ أَخُوهَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَسَأَلَهُ عَنْ ذَلِكَ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْ كَانَ عَلَيْهَا دَيْنٌ أَكُنْتَ قَاضِيَهُ؟". قَالَ: نَعَمْ. قَالَ: "فَاقْضُوا اللَّهَ، فَاللَّهُ أَحَقُّ بِالْوَفَاءِ"

Ametukhabarisha Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abuw Bishr, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba mwanamke mmoja aliweka nadhiri ya kuhiji, kisha akafariki. Kaka yake akaja kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akamuuliza kuhusu hilo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Lau angekuwa anadaiwa deni, je, ungelilipa?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Basi mlipeni Allaah; kwani Allaah Ana haki zaidi ya kutimiziwa."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1505
Hadiyth
2377

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا حَفْصٌ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، عَنْ عُمَرَ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي نَذَرْتُ نَذْرًا فِي الْجَاهِلِيَّةِ، ثُمَّ جَاءَ الْإِسْلَامُ؟ قَالَ: "فِ بِنَذْرِكَ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Hafsw, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi niliweka nadhiri katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam), kisha Islaam ikaja? Akasema: "Timiza nadhiri yako."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1505
Hadiyth
2378

2-Mlangoباب في كفارة النذرMlango Wa Kuhusu Kafara Ya Nadhiri

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ زَحْرٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الرُّعَيْنِيّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ، قالَ: نَذَرَتْ أُخْتِي أَنْ تَحُجَّ لِلَّهِ مَاشِيَةً غَيْرَ مُخْتَمِرَةٍ، فَذَكَرْتُ ذَلِكَ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "مُرْ أُخْتَكَ فَلْتَخْتَمِرْ، وَلْتَرْكَبْ، وَلْتَصُمْ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin Zahr, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Ar-Ru'ayniy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Maalik, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniy (رضي الله عنه), amesema: Dada yangu aliweka nadhiri ya kuhiji kwa ajili ya Allaah akiwa anatembea kwa miguu, bila ya kujifunika ushungi. Nikamtajia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hilo, akasema: "Mwamrishe dada yako ajifunike ushungi, na apande (kipando), na afunge Swawm siku tatu."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1506
Hadiyth
2379

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، أَخْبَرَنِي قَتَادَةُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ أُخْتَ عُقْبَةَ نَذَرَتْ أَنْ تَمْشِيَ إِلَى الْبَيْتِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ لَغَنِيٌّ عَنْ نَذْرِ أُخْتِكَ، لِتَرْكَبْ وَلْتُهْدِ هَدْيًا"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaam, amenikhabarisha Qataadah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba dada yake 'Uqbah (رضي الله عنه) aliweka nadhiri ya kutembea kwa miguu mpaka Al-Bayt (Al-Ka'bah). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika Allaah Hana haja na nadhiri ya dada yako; apande (kipando), na atoe Hadyu (mnyama wa kuchinjwa Haram)."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1506
Hadiyth
2380

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي عَمْرٍو، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَدْرَكَ شَيْخًا يَمْشِي بَيْنَ ابْنَيْهِ، فَقَالَ: "مَا شَأْنُ هَذَا الشَّيْخِ؟"، فَقَالَ ابْنَاهُ: نَذَرَ أَنْ يَمْشِيَ، فَقَالَ: "ارْكَبْ، فَإِنَّ اللَّهَ غَنِيٌّ عَنْكَ وَعَنْ نَذْرِكَ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa 'Amr bin Abiy 'Amr, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta mzee mmoja akitembea baina ya wanawe wawili, akasema: "Ana nini mzee huyu?" Wanawe wawili wakasema: Aliweka nadhiri ya kutembea kwa miguu. Akasema: "Panda (kipando), kwani hakika Allaah Hana haja nawe na nadhiri yako."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1507
Hadiyth
2381

3-Mlangoباب لا نذر في معصية اللهMlango Wa Hakuna Nadhiri Katika Kumuasi Allaah

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا وَفَاءَ لِنَذْرٍ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ، وَلَا فِيمَا لَا يَمْلِكُ ابْنُ آدَمَ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhallab, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna kutimiza nadhiri katika kumuasi Allaah, wala katika (kitu) asichokimiliki mwanaadam."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1508
Hadiyth
2382

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ طَلْحَةَ بْنِ عَبْدِ الْمَلِكِ الْأَيْلِيِّ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ نَذَرَ أَنْ يَطِيعَ اللَّهَ، فَلْيُطِعْهُ، وَمَنْ نَذَرَ أَنْ يَعْصِيَ اللَّهَ، فَلَا يَعْصِهِ"

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Twalhah bin 'Abdil-Malik Al-Ayliy, kutoka kwa Al-Qaasim bin Muhammad, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi amtii; na atakayeweka nadhiri ya kumuasi Allaah, basi asimuasi."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1508
Hadiyth
2383

4-Mlangoباب من نذر أن يصلي في بيت المقدس أيجزئه أن يصلي بمكةMlango Wa Aliyeweka Nadhiri Ya Kuswali
Katika Baytul-Maqdis, Je, Inamtosheleza Kuswali Makkah?

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ أَبِي بَقِيَّةَ الْمُعَلِّمِ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ: أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنِّي نَذَرْتُ إِنْ فَتَحَ اللَّهُ عَلَيْكَ أَنْ أُصَلِّيَ فِي بَيْتِ الْمَقْدِسِ؟ فَقَالَ: "صَلِّ هَا هُنَا". فَأَعَادَ عَلَيْهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَشَأْنُكَ إِذَنْ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Baqiyyah Al-Mu'allim, kutoka kwa 'Atwaa bin Abiy Rabaah, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), kwamba mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, hakika mimi niliweka nadhiri, ikiwa Allaah Atakupa ushindi (wa Makkah), niswali katika Baytul-Maqdis? Akasema: "Swali hapa." Akamrudia (jambo hilo) mara tatu. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Basi hapo ni shauri lako."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1509
Hadiyth
2384

5-Mlangoباب النهي عن النذرMlango Wa Makatazo Ya Kuweka Nadhiri

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُرَّةَ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ: "إِنَّ النَّذْرَ لَا يَرُدُّ شَيْئًا، وَإِنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنَ الْبَخِيلِ الشَّحِيحِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Murrah, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah amesema: "Hakika nadhiri hairudishi kitu; na hakika hutolewa kwayo (mali) kutoka kwa bakhili, mchoyo."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1509
Hadiyth
2385

6-Mlangoباب النهي عن أن يحلف بغير اللهMlango Wa Makatazo Ya Kuapa Kwa Asiyekuwa Allaah

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ أَنَسٍ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَدْرَكَ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ وَهُوَ يَسِيرُ فِي رَكْبٍ، وَهُوَ يَحْلِفُ بِأَبِيه، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ، فَمَنْ كَانَ حَالِفًا، فَلْيَحْلِفْ بِاللَّهِ، أَوْ لِيَصْمُتْ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik bin Anas, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimkuta 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) naye akienda katika msafara wa wapanda (ngamia), naye akiapa kwa baba yake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika Allaah Anakukatazeni kuapa kwa baba zenu. Basi atakayekuwa ni mwenye kuapa, aape kwa Allaah, au anyamaze."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1510
Hadiyth
2386

7-Mlangoباب في الاستثناء باليمينMlango Wa Kuhusu Istithnaa (Kukiambatanisha Kiapo
Na Matakwa Ya Allaah) Katika Kiapo

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنِ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ، ثُمَّ قَالَ: إِنْ شَاءَ اللَّهُ، فَقَدِ اسْتَثْنَى"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeapa kiapo, kisha akasema: Akipenda Allaah, basi kwa hakika amefanya istithnaa (kukiambatanisha kiapo na Matakwa ya Allaah)."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1511
Hadiyth
2387

أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ، ثُمَّ قَالَ: إِنْ شَاءَ اللَّهُ، فَهُوَ بِالْخِيَارِ: إِنْ شَاءَ فَعَلَ، وَإِنْ شَاءَ لَمْ يَفْعَلْ"

Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeapa kiapo, kisha akasema: Akipenda Allaah, basi yeye ana khiyari: akitaka atafanya, na akitaka hatafanya."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1511
Hadiyth
2388

8-Mlangoباب القسم يمينMlango Wa Kwamba Qasam (Kuapa) Ni Kiapo

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ لِأَبِي بَكْرٍ: "لَا تُقْسِمْ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: الْحَدِيثُ فِيهِ طُولٌ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Abuw Bakr (رضي الله عنه): "Usiape."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Hadiyth (hii) ina urefu.

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1512
Hadiyth
2389

9-Mlangoباب من حلف على يمين فرأى غيرها خيرا منهاMlango Wa Aliyeapa Kiapo Kisha
Akaona Kingine Ni Bora Kuliko Hicho

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو ابْنِ مُرَّةَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَجُلًا يُقَالُ لَهُ: عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو زَمَنَ الْجَمَاجِمِ يُحَدِّثُ، قَالَ: سَأَلَ رَجُلٌ عَدِيَّ بْنَ حَاتِمٍ، فَحَلَفَ أَنْ لَا يُعْطِيَهُ شَيْئًا، ثُمَّ قَالَ: لَوْلَا أَنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ حَلَفَ عَلَى يَمِينٍ، فَرَأَى غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا، فَلْيَأْتِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ، وَلْيُكَفِّرْ عَنْ يَمِينِهِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, amesema: Nilimsikia mtu mmoja anayeitwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr — zama za Al-Jamaajim (vita vya Dayr Al-Jamaajim, uasi wa Ibn Al-Ash'ath) — akisimulia, amesema: Mtu mmoja alimuomba 'Adiyy bin Haatim (رضي الله عنه) (kitu); ('Adiyy) akaapa kwamba hatampa kitu chochote. Kisha akasema: Lau si kwamba mimi nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayeapa kiapo, akaona kingine ni bora kuliko hicho, basi alifanye lile lililo bora, na atoe kafara ya kiapo chake."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1512
Hadiyth
2390

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، حَدَّثَنَا الْحَسَنُ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ سَمُرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ سَمُرَةَ، لَا تَسْأَلِ الْإِمَارَةَ فَإِنَّكَ إِنْ أُعْطِيتَهَا عَنْ مَسْأَلَةٍ، وُكِلْتَ إِلَيْهَا، وَإِنْ أُعْطِيتَهَا مِنْ غَيْرِ مَسْأَلَةٍ، أُعِنْتَ عَلَيْهَا. فَإِذَا حَلَفْتَ عَلَى يَمِينٍ فَرَأَيْتَ غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا، فَكَفِّرْ عَنْ يَمِينِكَ وَأْتِ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ".

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Fadhwl, ametusimulia Jariyr bin Haazim, ametusimulia Al-Hasan, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Samurah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yaa 'Abdar-Rahmaan bin Samurah, usiombe uongozi; kwani hakika wewe ukipewa kwa sababu ya kuuomba, utaachiwa uubebe peke yako; na ukipewa bila ya kuuomba, utasaidiwa juu yake. Basi utakapoapa kiapo, ukaona kingine ni bora kuliko hicho, toa kafara ya kiapo chako, na ulifanye lile lililo bora."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1513
Hadiyth
2391

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَمُرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: فَذَكَرَ نَحْوَ الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Samurah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: Akataja mfano wa Hadiyth hiyo.

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1513
Hadiyth
2392

10-Mlangoباب إذا كان على الرجل رقبة مؤمنةMlango Wa Mtu Anapokuwa
Na Wajibu Wa Kumwacha Huru Mtumwa Muumini

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنِ الشَّرِيدِ، قَالَ: أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: إِنَّ عَلَى أُمِّي رَقَبَةً، وَإِنَّ عِنْدِي جَارِيَةً سَوْدَاءَ نُوبِيَّةً، أَفَتُجْزِئُ عَنْهَا؟. قَالَ: "ادْعُ بِهَا"، فَقَالَ: "أَتَشْهَدِينَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ؟"، قَالَتْ: نَعَمْ. قَالَ: "أَعْتِقْهَا، فَإِنَّهَا مُؤْمِنَةٌ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Ash-Shariyd (رضي الله عنه), amesema: Nilimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Hakika mama yangu ana wajibu wa (kumwacha huru) mtumwa; na hakika mimi nina mjakazi mweusi wa (watu wa) Nuba; je, atamtosheleza (mama yangu)? Akasema: "Mwite." Akasema (kumwambia mjakazi): "Je, unashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah?" Akasema: Ndiyo. Akasema: "Mwache huru, kwani yeye ni muumini."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1514
Hadiyth
2393

11-Mlangoباب الرجل يحلف على الشيء وهو يوري على يمينهMlango Wa Mtu Anayeapa Juu Ya Jambo Naye Anatumia
Tawriyah (Kuficha Kusudio Lake) Katika Kiapo Chake

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَمِينُكَ عَلَى مَا يُصَدِّقُكَ بِهِ صَاحِبُكَ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Hushaym, ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kiapo chako ni kwa mujibu wa (maana) ambayo mwenzako anakusadikisha kwayo."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1514
Hadiyth
2394

12-Mlangoباب بأي أسماء الله حلفت لزمكMlango Wa Kwa Jina Lolote Miongoni Mwa Majina Ya Allaah
Utakaloapia, Kiapo Kinakulazimu

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مُوسَى بْنِ عُقْبَةَ، عَنْ سَالِمٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: كَانَتْ يَمِينُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي يَحْلِفُ بِهَا "لَا وَمُقَلِّبِ الْقُلُوبِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Muwsaa bin 'Uqbah, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Kiapo cha Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambacho alikuwa akiapia kilikuwa: "Hapana! Naapa kwa Mgeuzaji wa nyoyo."

Mjalada
3
Kitabu
14
Ukurasa
1515
Hadiyth
2395