ومن كتاب الديات
1-Mlangoباب في قتل العمدMlango Wa Kuhusu Kuua Kwa Kukusudia
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ فُضَيْلٍ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ أَبِي الْعَوْجَاءِ السُّلَمِيِّ، عَنْ أَبِي شُرَيْحٍ الْخُزَاعِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ أُصِيبَ بِدَمٍ أَوْ خَبْلٍ وَالْخَبْلُ: الْجُرْحُ فَهُوَ بِالْخِيَارِ بَيْنَ إِحْدَى ثَلَاثٍ: فَإِنْ أَرَادَ الرَّابِعَةَ، فَخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ: بَيْنَ أَنْ يَقْتَصَّ أَوْ يَعْفُوَ، أَوْ يَأْخُذَ الْعَقْلَ فَإِنْ أَخَذَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا ثُمَّ عَدَا بَعْدَ ذَلِكَ، فَلَهُ النَّارُ خَالِدًا فِيهَا مُخَلَّدًا"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith bin Fudhwayl, kutoka kwa Sufyaan bin Abil-'Awjaa As-Sulamiy, kutoka kwa Abuw Shurayh Al-Khuzaa'iy (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayefikwa na (msiba wa) damu au khabl — na khabl ni jeraha —, basi yeye ana khiyari (ya kuchagua) moja kati ya mambo matatu — na akitaka la nne, basi mzuieni (kwa kumshika mikono yake) —: kati ya kulipiza kisasi, au kusamehe, au kuchukua diyah (fidia ya damu). Na akichukua chochote katika hayo, kisha akafanya uadui baada ya hapo, basi atapata moto, akidumu humo, amedumishwa (humo)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1517
- Hadiyth
- 2396
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ، وَكَانَ فِي كِتَابِهِ: "أَنَّ مَنْ اعْتَبَطَ مُؤْمِنًا قَتْلًا عَنْ بَيِّنَةٍ فَإِنَّهُ قَوَدُ يَدِهِ إِلَّا أَنْ يَرْضَى أَوْلِيَاءُ الْمَقْتُولِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: اعْتَبَطَ: قَتَلَ مِنْ غَيْرِ عِلَّةٍ
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen, na ilikuwa katika kitabu chake: "Kwamba atakayemuua Muumini bila ya hatia, (na ikathibiti) kwa ushahidi, basi hakika (malipo) yake ni qawad (kulipiza kisasi cha kuua) kwa (kosa la) mkono wake, isipokuwa wakiridhia mawalii wa aliyeuawa."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: I'tabatwa: ameua bila ya sababu yoyote.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1518
- Hadiyth
- 2397
2-Mlangoباب في القسامةMlango Wa Kuhusu Qasaamah (Viapo Khamsini
Katika Kesi Ya Mauaji Yasiyo Na Ushahidi)
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، حَدَّثَنَا بُشَيْرُ بْنُ يَسَارٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ أَبِي حَثْمَةَ، قَالَ: خَرَجَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَهْلٍ أَحَدُ بَنِي حَارِثَةَ إِلَى خَيْبَرَ مَعَ نَفَرٍ مِنْ قَوْمِهِ يُرِيدُونَ الْمِيرَةَ بِخَيْبَرَ، قَالَ: فَعُدِيَ عَلَى عَبْدِ اللَّهِ، فَقُتِلَ: فَتُلَّتْ عُنُقُهُ حَتَّى نُخَعَ ثُمَّ طُرِحَ فِي مَنْهَلٍ مِنْ مَنَاهِلِ خَيْبَرَ، فَاسْتُصْرِخَ عَلَيْهِ أَصْحَابُهُ، فَاسْتَخْرَجُوهُ فَغَيَّبُوهُ، ثُمَّ قَدِمُوا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ، فَتَقَدَّمَ أَخُوهُ عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ سَهْلٍ وَكَانَ ذَا قِدَمٍ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَابْنَا عَمِّهِ مَعَهُ: حُوَيِّصَةُ بْنُ مَسْعُودٍ وَمُحَيِّصَةُ، فَتَكَلَّمَ عَبْدُ الرَّحْمَنِ وَكَانَ أَحْدَثَهُمْ سِنًّا، وَهُوَ صَاحِبُ الدَّمِ وَذَا قَدَمٍ فِي الْقَوْمِ فَلَمَّا تَكَلَّمَ، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْكُبْرَ الْكُبْرَ". قَالَ: فَاسْتَأْخَرَ فَتَكَلَّمَ حُوَيِّصَةُ وَمُحَيِّصَةُ، ثُمَّ هُوَ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تُسَمُّونَ قَاتِلَكُمْ، ثُمَّ تَحْلِفُونَ عَلَيْهِ خَمْسِينَ يَمِينًا، ثُمَّ نُسَلِّمُهُ إِلَيْكُمْ". قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا كُنَّا لِنَحْلِفَ عَلَى مَا لَا نَعْلَمُ، مَا نَدْرِي مَنْ قَتَلَهُ، إِلَّا أَنَّ يَهُودَ عَدُوُّنَا، وَبَيْنَ أَظْهُرِهِمْ قُتِلَ. قَالَ: "فَيَحْلِفُونَ لَكُمْ بِاللَّهِ إِنَّهُمْ لَبُرَءَاءُ مِنْ دَمِ صَاحِبِكُمْ، ثُمَّ يَبْرَءُونَ مِنْهُ". قَالُوا: مَا كُنَّا لِنَقْبَلَ أَيْمَانَ يَهُودَ، مَا فِيهِمْ أَكْبَرُ مِنْ أَنْ يَحْلِفُوا عَلَى إِثْمٍ. قَالَ: فَوَدَاهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ عِنْدِهِ بِمِائَةِ نَاقَةٍ
Ametusimulia Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, ametusimulia Bushayr bin Yasaar, kutoka kwa Sahl bin Abiy Hathmah (رضي الله عنه), amesema: 'Abdu-Allaah bin Sahl (رضي الله عنه) — mmoja wa Banuw Haarithah — alitoka kwenda Khaybar pamoja na kikundi cha watu wa kaumu yake, wakitaka (kununua) chakula huko Khaybar. Akasema: 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه) akashambuliwa, akauawa: shingo yake ilisokotwa mpaka ikavunjika, kisha akatupwa katika kisima kimoja miongoni mwa visima vya Khaybar. Wenzake wakaitwa kwa ukelele (wa kuomba msaada) kwa ajili yake; wakamtoa (kisimani) na wakamzika. Kisha wakamjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) huko Madiynah. Nduguye, 'Abdur-Rahmaan bin Sahl (رضي الله عنه), akatangulia — naye alikuwa na utangulizi (katika Islaam) pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, na watoto wawili wa ami yake pamoja naye: Huwayyiswah bin Mas'uwd na Muhayyiswah (رضي الله عنهما). 'Abdur-Rahmaan (رضي الله عنه) akazungumza — naye alikuwa ndiye mdogo wao kwa umri, na yeye ndiye mwenye damu (ya aliyeuawa), na mwenye utangulizi katika kaumu. Alipozungumza, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mkubwa (kwanza)! Mkubwa (kwanza)!" Akasema: Akarudi nyuma; wakazungumza Huwayyiswah na Muhayyiswah (رضي الله عنهما), kisha yeye ['Abdur-Rahmaan (رضي الله عنه)]. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mtamtaja muuaji wenu, kisha mtaapa juu yake viapo khamsini, kisha tutamkabidhi kwenu." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, hatukuwa wenye kuapa juu ya tusiyoyajua; hatujui ni nani aliyemuua, isipokuwa kwamba Mayahudi ni adui yetu, na ameuawa kati yao. Akasema: "Basi watawaapia kwa Allaah kwamba hakika wao hawana hatia ya damu ya mwenzenu, kisha watakuwa wamejitoa (katika dhima) yake." Wakasema: Hatukuwa wenye kukubali viapo vya Mayahudi; hakuna yeyote miongoni mwao aliye mkubwa (kiasi cha kujiepusha) na kuapa juu ya dhambi. Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamlipia diyah (fidia ya damu) kutoka kwake (mwenyewe): ngamia jike mia moja.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1519
- Hadiyth
- 2398
3-Mlangoباب القود بين الرجال والنساءMlango Wa Qawad (Kulipiza Kisasi Cha Kuua)
Baina Ya Wanaume Na Wanawake
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ وَكَانَ فِي كِتَابِهِ: "أَنَّ الرَّجُلَ يُقْتَلُ بِالْمَرْأَةِ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen, na ilikuwa katika kitabu chake: "Kwamba mwanamume anauawa kwa (kumuua) mwanamke."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1520
- Hadiyth
- 2399
4-Mlangoباب كيف العمل في القودMlango Wa Namna Ya Kutekeleza
Qawad (Kulipiza Kisasi Cha Kuua)
أَخْبَرَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ أَنَسٍ: أَنَّ جَارِيَةً رُضَّ رَأْسُهَا بَيْنَ حَجَرَيْنِ، فَقِيلَ لَهَا: مَنْ فَعَلَ بِكِ هَذَا أَفُلَانٌ، أَفُلَانٌ؟ حَتَّى سُمِّيَ الْيَهُودِيُّ، فَأَوْمَأَتْ بِرَأْسِهَا، فَبُعِثَ إِلَيْهِ فَجِيءَ بِهِ، فَاعْتَرَفَ، "فَأَمَرَ بِهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَرُضَّ رَأْسُهُ بَيْنَ حَجَرَيْنِ"
Ametukhabarisha 'Affaan, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه): Kwamba msichana mmoja kichwa chake kilipondwa kati ya mawe mawili. Akaulizwa: Ni nani aliyekufanyia hivi? Je, ni fulani? Je, ni fulani? Mpaka akatajwa yule Myahudi; akaashiria kwa kichwa chake (kukubali). Akatumiwa (mtu), akaletwa, akakiri. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamrisha (afanyiwe hivyo); kichwa chake kikapondwa kati ya mawe mawili.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1521
- Hadiyth
- 2400
5-Mlangoباب لا يقتل مسلم بكافرMlango Wa Muislamu Hauawi Kwa Sababu Ya Kafiri
أَخْبَرَنَا إِسْحَاقُ، أَنْبَأَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ أَبِي جُحَيْفَةَ، قَالَ: قُلْتُ لِعَلِيٍّ: يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ، هَلْ عَلِمْتَ شَيْئًا مِنَ الْوَحْيِ إِلَّا مَا فِي كِتَابِ اللَّهِ تَعَالَى؟. قَالَ: "لَا وَالَّذِي فَلَقَ الْحَبَّةَ وَبَرَأَ النَّسَمَةَ، مَا أَعْلَمُهُ إِلَّا فَهْمًا يُعْطِيهِ اللَّهُ الرَّجُلَ فِي الْقُرْآنِ، وَمَا فِي الصَّحِيفَةِ". قُلْتُ: وَمَا فِي الصَّحِيفَةِ؟. قَالَ: "الْعَقْلُ، وَفِكَاكُ الْأَسِيرِ، وَلَا يُقْتَلُ مُسْلِمٌ بِمُشْرِكٍ"
Ametukhabarisha Is-haaq, ametupa khabari Jariyr, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Abuw Juhayfah (رضي الله عنه), amesema: Nilimwambia 'Aliy (رضي الله عنه): Yaa Amiyral-Muuminiyn, je, unajua chochote katika Wahyi isipokuwa kilichomo katika Kitabu cha Allaah (تعالى)? Akasema: "Hapana; naapa kwa Yule Aliyepasua punje na Akaumba nafsi! Sijui (kitu) isipokuwa ufahamu ambao Allaah Humpa mtu katika Qur-aan, na kilichomo katika swahiyfah (karatasi ya maandishi)." Nikasema: Na ni nini kilichomo katika swahiyfah? Akasema: "Diyah (fidia ya damu), na kumkomboa mateka, na kwamba Muislamu hauawi kwa sababu ya mshirikina."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1521
- Hadiyth
- 2401
6-Mlangoباب في القود بين الوالد والولدMlango Wa Kuhusu Qawad (Kulipiza
Kisasi Cha Kuua) Baina Ya Mzazi Na Mwana
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَونٍ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ مُسْلِمٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تُقَامُ الْحُدُودُ فِي الْمَسَاجِدِ، وَلَا يُقَادُ بِالْوَلَدِ الْوَالِدُ"
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Muslim, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Huduud (adhabu zilizowekwa na Shariy'ah) hazisimamishwi Misikitini, wala mzazi hauawi kwa kisasi cha (kumuua) mwanawe."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1522
- Hadiyth
- 2402
7-Mlangoباب في القود بين العبد وسيدهMlango Wa Kuhusu Qawad (Kulipiza
Kisasi Cha Kuua) Baina Ya Mtumwa Na Bwana Wake
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ قَتَلَ عَبْدَهُ قَتَلْنَاهُ، وَمَنْ جَدَعَهُ، جَدَعْنَاهُ". قَالَ: ثُمَّ نَسِيَ الْحَسَنُ هَذَا الْحَدِيثَ، وَكَانَ يَقُولُ: لَا يُقْتَلُ حُرٌّ بِعَبْدٍ
Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Samurah bin Jundub (رضي الله عنه): Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayemuua mtumwa wake, tutamuua; na atakayemkata (pua au sikio) mtumwa wake, tutamkata." Akasema: Kisha Al-Hasan akaisahau Hadiyth hii, na alikuwa akisema: Muungwana hauawi kwa (kumuua) mtumwa.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1522
- Hadiyth
- 2403
8-Mlangoباب لمن يعفو عن قاتلهMlango Wa Anayemsamehe Muuaji Wake
أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الْهَمْدَانِيُّ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ عَوْفٍ، عَنْ حَمْزَةَ أَبِي عُمَرَ، عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ وَائِلٍ الْحَضْرَمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ وَائِلِ بْنِ حُجْرٍ، قَالَ: شَهِدْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ أُتِيَ بِالرَّجُلِ الْقَاتِلِ يُقَادُ فِي نِسْعَةٍ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِوَلِيِّ الْمَقْتُولِ: "أَتَعْفُو؟". قَالَ: لَا. قَالَ: "فَتَأْخُذُ الدِّيَةَ؟". قَالَ: لَا. قَالَ: "فَتَقْتُلُهُ؟". قَالَ: نَعَمْ. قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّكَ إِنْ عَفَوْتَ عَنْهُ، فَإِنَّهُ يَبُوءُ بِإِثْمِكَ وَإِثْمِ صَاحِبِكَ". قَالَ: فَتَرَكَهُ، قَالَ: فَأَنَا رَأَيْتُهُ يَجُرُّ نِسْعَتَهُ، قَدْ عَفَا عَنْهُ
Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah Al-Hamdaaniy, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa 'Awf, kutoka kwa Hamzah Abuw 'Umar, kutoka kwa 'Alqamah bin Waail Al-Hadhwramiy, kutoka kwa baba yake, Waail bin Hujr (رضي الله عنه), amesema: Nilimshuhudia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipoletewa mtu muuaji akiongozwa kwa kamba ya ngozi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia walii wa aliyeuawa: "Je, utamsamehe?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi utachukua diyah (fidia ya damu)?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi utamuua?" Akasema: Ndiyo. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika wewe, ukimsamehe, basi yeye atarudi na dhambi yako na dhambi ya mwenzako." Akasema: Akamwacha. Akasema: Basi mimi nilimuona akiikokota kamba yake ya ngozi, (walii) amekwisha kumsamehe.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1524
- Hadiyth
- 2404
9-Mlangoباب التشديد في قتل النفس المسلمةMlango Wa Onyo Kali Kuhusu Kuua Nafsi Ya Muislamu
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ فِرَاسٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْكَبَائِرُ: الْإِشْرَاكُ بِاللَّهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ، وَقَتْلُ النَّفْسِ شُعْبَةُ الشَّاكُّ أَوْ الْيَمِينُ الْغَمُوسُ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Bashshaar, ametusimulia Muhammad bin Ja'far, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Firaas, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Madhambi makubwa ni: kumshirikisha Allaah, na kuwaasi wazazi wawili, na kuiua nafsi" — Shu'bah ndiye mwenye shaka — "au kiapo cha uongo cha kuzamisha (kinachomzamisha mwenyewe katika dhambi)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1525
- Hadiyth
- 2405
10-Mlangoباب التشديد على من قتل نفسهMlango Wa Onyo Kali Kwa Aliyejiua
حَدَّثَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ ثَابِتِ بْنِ الضَّحَّاكِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَعْنُ الْمُؤْمِنِ كَقَتْلِهِ، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِشَيْءٍ فِي الدُّنْيَا، عُذِّبَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"
Ametusimulia Wahb bin Jariyr, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Thaabit bin Adh-Dhwahhaak (رضي الله عنه): Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kumlaani Muumini ni kama kumuua; na atakayejiua kwa kitu chochote duniani, ataadhibiwa kwacho Siku ya Qiyaamah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1526
- Hadiyth
- 2406
حَدَّثَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِحَدِيدَةٍ فَحَدِيدَتُهُ فِي يَدِهِ يَتَوَجَّأُ بِهَا فِي بَطْنِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِسَمٍّ فَسُمُّهُ فِي يَدِهِ يَتَحَسَّاهُ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ تَرَدَّى مِنْ جَبَلٍ فَقَتَلَ نَفْسَهُ، فَهُوَ يَتَرَدَّى فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا"
Ametusimulia Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayejiua kwa chuma, basi chuma chake kitakuwa mkononi mwake akijichoma nacho tumboni mwake katika moto wa Jahannam, akidumu humo milele. Na atakayejiua kwa sumu, basi sumu yake itakuwa mkononi mwake akiigugumia katika moto wa Jahannam, akidumu humo milele. Na atakayejitupa kutoka mlimani akajiua, basi atakuwa akijitupa katika moto wa Jahannam, akidumu humo milele."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1526
- Hadiyth
- 2407
11-Mlangoباب كم الدية من الورق والذهبMlango Wa Diyah (Fidia Ya Damu) Ni Kiasi Gani
Kwa Fedha Na Dhahabu
حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هَانِئٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ دِينَارٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قالَ: قَتَلَ رَجُلٌ رَجُلًا عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "فَجَعَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دِيَتَهُ اثْنَيْ عَشَرَ أَلْفًا، فَهُوَ قَوْلُهُ: {يَحْلِفُونَ بِاللَّهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا وَمَا نَقَمُوا إِلا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ مِنْ فَضْلِهِ} بِأَخْذِهِمُ الدِّيَةَ"
Ametusimulia Mu'aadh bin Haaniy, ametusimulia Muhammad bin Muslim, ametusimulia 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Mtu mmoja alimuua mtu katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaifanya diyah (fidia ya damu) yake kuwa (dirham) elfu kumi na mbili. Na hiyo ndiyo Kauli Yake:
يَحْلِفُونَ بِاللَّهِ مَا قَالُوا وَلَقَدْ قَالُوا كَلِمَةَ الْكُفْرِ وَكَفَرُوا بَعْدَ إِسْلامِهِمْ وَهَمُّوا بِمَا لَمْ يَنَالُوا وَمَا نَقَمُوا إِلا أَنْ أَغْنَاهُمُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ مِنْ فَضْلِهِ
Wanaapa kwa Jina la Allaah kuwa hawakusema ilhali wamekwishasema neno la kufuru, na wakakufuru baada ya kusilimu kwao. Na wakaazimia yale ambayo hawakuweza kuyafikia. Na hawakuchukia isipokuwa kwa kuwa Allaah na Rasuli Wake Amewatajirisha kwa Fadhila Zake [At-Tawbah (9:74)]
(Yaani) kwa kuchukua kwao diyah.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1527
- Hadiyth
- 2408
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، قَالَ: حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ: "وَعَلَى أَهْلِ الذَّهَبِ أَلْفُ دِينَارٍ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amesema: Amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen: "Na juu ya wenye dhahabu ni dinari elfu moja."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1527
- Hadiyth
- 2409
12-Mlangoباب كم الدية من الإبلMlango Wa Diyah (Fidia Ya Damu) Ni Kiasi Gani Kwa Ngamia
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ: "بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ: مِنْ مُحَمَّدٍ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى شُرَحْبِيلَ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَالْحَارِثِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ، وَنُعَيْمِ بْنِ عَبْدِ كُلَالٍ قِيَلِ ذِي رُعَيْنٍ وَمُعَافِرَ، وَهَمَدَانَ فَكَانَ فِي كِتَابِهِ: وَإِنَّ فِي النَّفْسِ الدِّيَةَ: مِائَةٌ مِنَ الْإِبِلِ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen:
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
Kwa Jina la Allaah Ar-Rahmaan (Mwingi wa Rehma), Ar-Rahiym (Mwenye Kurehemu)
"Kutoka kwa Muhammad, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwenda kwa Shurahbiyl bin 'Abdi Kulaal, na Al-Haarith bin 'Abdi Kulaal, na Nu'aym bin 'Abdi Kulaal, qayl (mfalme) wa Dhiy Ru'ayn na Ma'aafir na Hamdaan." Na ilikuwa katika kitabu chake: "Na kwamba katika nafsi ni diyah (fidia ya damu): ngamia mia moja."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1530
- Hadiyth
- 2410
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ، وَكَانَ فِي كِتَابِهِ: "وَفِي الْأَنْفِ إِذَا أُوعِبَ جَدْعُهُ الدِّيَةُ، وَفِي اللِّسَانِ الدِّيَةُ، وَفِي الشَّفَتَيْنِ الدِّيَةُ، وَفِي الْبَيْضَتَيْنِ الدِّيَةُ، وَفِي الذَّكَرِ الدِّيَةُ، وَفِي الصُّلْبِ الدِّيَةُ، وَفِي الْعَيْنَيْنِ الدِّيَةُ، وَفِي الرِّجْلِ الْوَاحِدَةِ نِصْفُ الدِّيَةِ، وَفِي الْمَأْمُومَةِ ثُلُثُ الدِّيَةِ، وَفِي الْجَائِفَةِ ثُلُثُ الدِّيَةِ، وَفِي الْمُنَقِّلَةِ خَمْسَ عَشَرَةَ مِنَ الْإِبِلِ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen, na ilikuwa katika kitabu chake: "Na katika pua ikikatwa yote, diyah (fidia ya damu); na katika ulimi, diyah; na katika midomo miwili, diyah; na katika korodani mbili, diyah; na katika dhakari, diyah; na katika uti wa mgongo, diyah; na katika macho mawili, diyah; na katika mguu mmoja, nusu ya diyah; na katika ma'muwmah (jeraha la kichwa linalofikia utando wa ubongo), theluthi ya diyah; na katika jaaifah (jeraha linalopenya mpaka ndani ya tumbo au kifua), theluthi ya diyah; na katika munaqqilah (jeraha linalovunja mfupa na kuuhamisha mahali pake), ngamia kumi na watano."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1531
- Hadiyth
- 2411
13-Mlangoباب كيف العمل في أخذ دية الخطأMlango Wa Namna Ya Kuchukua Diyah
(Fidia Ya Damu) Ya Kuua Kwa Makosa
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنْ حَجَّاجٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ خِشْفِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "جَعَلَ الدِّيَةَ فِي الْخَطَإِ أَخْمَاسًا"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Mu'aawiyah, kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa Zayd bin Jubayr, kutoka kwa Khishf bin Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه): Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliifanya diyah (fidia ya damu) katika (kuua kwa) makosa kuwa mafungu matano (ya ngamia).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1532
- Hadiyth
- 2412
14-Mlangoباب القصاص بين العبيدMlango Wa Qiswaasw (Kulipiza Kisasi) Baina Ya Watumwa
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الرِّفَاعِيُّ، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ: "أَنَّ عَبْدًا لِأُنَاسٍ فُقَرَاءَ، قَطَعَ يَدَ غُلَامٍ لِأُنَاسٍ أَغْنِيَاءَ. فَأَتَى أَهْلُهُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّهُ لِأُنَاسٍ فُقَرَاءَ؟ فَلَمْ يَجْعَلْ عَلَيْهِ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْئًا"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Ar-Rifaa'iy, ametusimulia Mu'aadh bin Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه): Kwamba mtumwa wa watu mafakiri alikata mkono wa kijana (mtumwa) wa watu matajiri. Watu wake wakamjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), wakasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika yeye ni wa watu mafakiri. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakumuwekea (adhabu) yoyote.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1533
- Hadiyth
- 2413
15-Mlangoباب في دية الأصابعMlango Wa Kuhusu Diyah (Fidia Ya Damu) Ya Vidole
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ غَالِبٍ التَّمَّارِ، عَنْ مَسْرُوقِ بْنِ أَوْسٍ، عَنْ أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْأَصَابِعُ سَوَاءٌ"، قَالَ: فَقُلْتُ: عَشْرٌ عَشْرٌ؟، قَالَ: "نَعَمْ"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ghaalib At-Tammaar, kutoka kwa Masruwq bin Aws, kutoka kwa Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Vidole ni sawa." Akasema: Nikasema: (Ngamia) kumi kumi? Akasema: "Ndiyo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1533
- Hadiyth
- 2414
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "هَذَا وَهَذَا سَوَاء، وَقَالَ: بِخِنْصِرِهِ وَإِبْهَامِهِ"
Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hiki na hiki ni sawa." Na akaashiria kwa kidole chake kidogo na kidole chake gumba.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1533
- Hadiyth
- 2415
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، حَدَّثَنِي أَبُو بَكْرِ بْنُ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ: "وَفِي كُلِّ إِصْبَعٍ مِنْ أَصَابِعِ الْيَدِ وَالرِّجْلِ عَشْرٌ مِنَ الْإِبِلِ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, amenisimulia Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen: "Na katika kila kidole miongoni mwa vidole vya mkono na mguu, ngamia kumi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1533
- Hadiyth
- 2416
16-Mlangoباب في الموضحةMlango Wa Kuhusu Muwdhwihah (Jeraha Linalofunua Mfupa)
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدَةُ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ مَطَرٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: "قَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْمَوَاضِحِ خَمْسًا خَمْسًا مِنَ الْإِبِلِ"
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia 'Abdah, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Matwar, kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما)], amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamua katika mawaadhwih (majeraha yanayofunua mfupa), ngamia watano watano."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1535
- Hadiyth
- 2417
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ: "وَفِي كُلِّ إِصْبَعٍ مِنْ أَصَابِعِ الْيَدِ وَالرِّجْلِ عَشْرٌ مِنَ الْإِبِلِ، وَفِي الْمُوضِحَةِ خَمْسٌ مِنَ الْإِبِلِ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen: "Na katika kila kidole miongoni mwa vidole vya mkono na mguu, ngamia kumi; na katika muwdhwihah (jeraha linalofunua mfupa), ngamia watano."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1535
- Hadiyth
- 2418
17-Mlangoباب في دية الأسنانMlango Wa Kuhusu Diyah (Fidia Ya Damu) Ya Meno
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، أَنْبَأَنَا عَبْدَةُ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ مَطَرٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: "قَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْأَسْنَانِ خَمْسًا خَمْسًا مِنَ الْإِبِلِ"
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametupa khabari 'Abdah, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Matwar, kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما)], amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliamua katika meno, ngamia watano watano."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1536
- Hadiyth
- 2419
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ دَاوُدَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَتَبَ إِلَى أَهْلِ الْيَمَنِ: "وَفِي السِّنِّ خَمْسٌ مِنَ الْإِبِلِ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Muwsaa, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa Sulaymaan bin Daawuwd, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin Muhammad bin 'Amr bin Hazm, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Amr bin Hazm (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwaandikia watu wa Yemen: "Na katika jino, ngamia watano."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1536
- Hadiyth
- 2420
18-Mlangoباب فيمن عض يد رجل فانتزع المعضوض يدهMlango Wa Kuhusu Aliyeuma Mkono Wa Mtu, Kisha
Aliyeumwa Akauvuta Mkono Wake
حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: قَتَادَةُ أَخْبَرَنِي، قَالَ: سَمِعْتُ زُرَارَةَ بْنَ أَوْفَى، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ: أَنَّ رَجُلًا عَضَّ يَدَ رَجُلٍ، قَالَ: فَنَزَعَ يَدَهُ فَوَقَعَتْ ثَنِيَّتَاهُ، فَاخْتَصَمُوا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَعَضُّ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ كَمَا يَعَضُّ الْفَحْلُ؟ لَا دِيَةَ لَكَ"
Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, amesema: Qataadah amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia Zuraarah bin Awfaa (akisimulia) kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه): Kwamba mtu mmoja aliuma mkono wa mtu. Akasema: (Aliyeumwa) akauvuta mkono wake, meno mawili ya mbele (ya aliyeuma) yakaanguka. Wakashtakiana kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Mmoja wenu anamuuma nduguye kama anavyouma ngamia dume? Huna diyah (fidia ya damu)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1537
- Hadiyth
- 2421
19-Mlangoباب العجماء جرحها جبارMlango Wa Mnyama, Jeraha Lake Ni Jubaar (Halina Fidia)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْعَجْمَاءُ جُرْحُهَا جُبَارٌ، وَالْبِئْرُ جُبَارٌ، وَالْمَعْدِنُ جُبَارٌ، وَفِي الرِّكَازِ الْخُمُسُ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mnyama, jeraha lake ni jubaar (halina fidia); na kisima ni jubaar; na machimbo (ya madini) ni jubaar; na katika rikaaz (mali iliyozikwa ardhini tangu zama za kabla ya Islaam) kuna khumsi (sehemu ya tano)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1537
- Hadiyth
- 2422
أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَأَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "جُرْحُ الْعَجْمَاءِ جُبَارٌ، وَالْبِئْرُ جُبَارٌ، وَالْمَعْدِنُ جُبَارٌ، وَفِي الرِّكَازِ الْخُمُسُ"
Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Jeraha la mnyama ni jubaar (halina fidia); na kisima ni jubaar; na machimbo (ya madini) ni jubaar; na katika rikaaz (mali iliyozikwa ardhini tangu zama za kabla ya Islaam) kuna khumsi (sehemu ya tano)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1538
- Hadiyth
- 2423
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْمَعْدِنُ جُبَارٌ، وَالسَّائِمَةُ جُبَارٌ، وَالْبِئْرُ جُبَارٌ، وَفِي الرِّكَازِ الْخُمُسُ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Machimbo (ya madini) ni jubaar (halina fidia); na mnyama anayechunga malishoni ni jubaar; na kisima ni jubaar; na katika rikaaz (mali iliyozikwa ardhini tangu zama za kabla ya Islaam) kuna khumsi (sehemu ya tano)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1538
- Hadiyth
- 2424
20-Mlangoباب في دية الجنينMlango Wa Kuhusu Diyah (Fidia Ya Damu) Ya Kijusi
حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ نُضَيْلَةَ، عَنِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَنَّ امْرَأَتَيْنِ كَانَتَا تَحْتَ رَجُلٍ، فَتَغَايَرَتَا، فَضَرَبَتْ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَى بِعَمُودٍ، فَقَتَلَتْهَا وَمَا فِي بَطْنِهَا، فَاخْتَصَمَا إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَضَى فِيهِ غُرَّةً، وَجَعَلَهَا عَلَى عَاقِلَةِ الْمَرْأَةِ"
Ametusimulia Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Ubayd bin Nudhwaylah, kutoka kwa Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kwamba wanawake wawili walikuwa chini ya mume mmoja, wakaoneana wivu. Mmoja wao akampiga mwenzake kwa nguzo (ya hema), akamuua yeye na kilichokuwa tumboni mwake. Wakashtakiana kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akaamua humo ghurrah (fidia ya mimba iliyoharibika), na akaiweka juu ya 'aaqilah (jamaa wa kiume wa upande wa baba wanaobeba diyah) ya mwanamke (aliyeua).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1538
- Hadiyth
- 2425
حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ عَمْرٍو هُوَ: ابْنُ دِينَار، عَنْ طَاوُسٍ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ عُمَرَ نَشَدَ النَّاسَ قَضَاءَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْجَنِينِ فَقَامَ حَمَلُ بْنُ مَالِكِ بْنِ النَّابِغَةِ، فَقَالَ: كُنْتُ بَيْنَ امْرَأَتَيْنِ، فَضَرَبَتْ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَى بِمِسْطَحٍ، "فَقَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي جَنِينِهَا بِغُرَّةٍ، وَأَنْ تُقْتَلَ بِهَا"
Ametusimulia Abuw 'Aaswim, ametusimulia Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Amr — naye ni Ibn Diynaar —, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): Kwamba 'Umar (رضي الله عنه) aliwaomba watu kwa kusisitiza (wamtajie) uamuzi wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu kijusi. Hamal bin Maalik bin An-Naabighah (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Nilikuwa kati ya wanawake wawili (wake zangu); mmoja wao akampiga mwenzake kwa nguzo ya hema. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaamua kuhusu kijusi chake ghurrah (fidia ya mimba iliyoharibika), na kwamba (muuaji) auawe kwa ajili yake.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1539
- Hadiyth
- 2426
21-Mlangoباب دية الخطإ على من هيMlango Wa Diyah (Fidia Ya Damu) Ya Kuua
Kwa Makosa Iko Juu Ya Nani
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَأَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ امْرَأَتَيْنِ مِنْ هُذَيْلٍ اقْتَتَلَتَا، فَرَمَتْ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَى بِحَجَرٍ، فَقَتَلَتْهَا وَمَا فِي بَطْنِهَا، فَاخْتَصَمُوا فِي الدِّيَةِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَضَى: أَنَّ دِيَةَ جَنِينِهَا غُرَّةٌ: عَبْدٌ أَوْ وَلِيدَةٌ، وَقَضَى بِدِيَتِهَا عَلَى عَاقِلَتِهَا، وَرَثَتُهَا وَلَدُهَا وَمَنْ مَعَهَا، فَقَالَ حَمَلُ بْنُ النَّابِغَةِ الْهُذَلِيُّ: كَيْفَ أَغْرَمُ مَنْ لَا شَرِبَ وَلَا أَكَلَ، وَلَا نَطَقَ وَلَا اسْتَهَلّ، فَمِثْلُ ذَلِكَ يُطَلُّ؟، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّمَا هُوَ مِنْ إِخْوَانِ الْكُهَّانِ". مِنْ أَجْلِ سَجْعِهِ الَّذِي سَجَعَ
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه): Kwamba wanawake wawili wa Hudhayl walipigana; mmoja wao akamtupia mwingine jiwe, akamuua yeye na kilichokuwa tumboni mwake. Wakashtakiana kuhusu diyah (fidia ya damu) kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); akaamua kwamba diyah ya kijusi chake ni ghurrah (fidia ya mimba iliyoharibika): mtumwa mwanamume au mjakazi; na akaamua diyah ya mwanamke (aliyeuawa) iwe juu ya 'aaqilah (jamaa wa kiume wa upande wa baba wanaobeba diyah) yake (muuaji); na warithi wake ni watoto wake na walio pamoja naye. Hamal bin An-Naabighah Al-Hudhaliy (رضي الله عنه) akasema: Vipi nitozwe fidia kwa ambaye hakunywa wala hakula, wala hakutamka wala hakulia (alipozaliwa)? Mfano wa huyo hupotea bure (bila fidia). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika huyu ni miongoni mwa ndugu wa makuhani" — kwa sababu ya maneno ya mizani (saj') yake aliyoyatunga.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1539
- Hadiyth
- 2427
22-Mlangoباب الدية في شبه العمدMlango Wa Diyah (Fidia Ya Damu)
Katika Mauaji Yanayofanana Na Kukusudia
أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ رَبِيعَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "دِيَةُ قَتِيلِ الْخَطَإِ شِبْهِ الْعَمْدِ، وَمَا كَانَ بِالسَّوْطِ وَالْعَصَا مِنْهَا: أَرْبَعُونَ فِي بُطُونِهَا أَوْلَادُهَا"
Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Al-Qaasim bin Rabiy'ah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Diyah (fidia ya damu) ya aliyeuawa kwa makosa yanayofanana na kukusudia — na kile kilichokuwa kwa mjeledi na fimbo —, katika hiyo (diyah): arobaini (ni ngamia ambao) matumboni mwao mna watoto wao."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1540
- Hadiyth
- 2428
23-Mlangoباب من اطلع في دار قوم بغير إذنهمMlango Wa Mwenye Kuchungulia
Katika Nyumba Ya Watu Bila Ya Idhini Yao
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ، أَخْبَرَهُ أَنَّ رَجُلًا اطَّلَعَ فِي جُحْرٍ فِي حُجْرَةِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِدْرَى يُخَلِّلُ بِهَا رَأْسَهُ، فَرَآهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "لَوْ أَعْلَمُ أَنَّكَ تَنْظُرُنِي، لَطَعَنْتُ بِهَا فِي عَيْنَيْكَ". وَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّمَا جُعِلَ الْإِذْنُ مِنْ أَجْلِ النَّظَرِ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sahl bin Sa'd As-Saa'idiy (رضي الله عنه), alimkhabarisha kwamba mtu mmoja alichungulia katika tundu katika chumba cha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa na midraa (kitana cha kuchania nywele) akikipitisha katika nywele za kichwa chake. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwona, akasema: "Lau ningelijua kwamba unanitazama, ningelikuchoma nacho katika macho yako mawili." Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika (kuomba) idhini kumewekwa kwa ajili ya kutazama."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1541
- Hadiyth
- 2429
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ ابْنِ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ، قالَ: بَيْنَمَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حُجْرَةٍ وَمَعَهُ مِدْرى يَحُكُّ بِهِ رَأْسَهُ، اطَّلَعَ عَلَيْهِ رَجُلٌ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْ أَعْلَمُ أَنَّكَ تَنْظُرُ لَقُمْتُ حَتَّى أَطْعَنَ بِهِ عَيْنَيْكَ. إِنَّمَا جُعِلَ الْإِذْنُ مِنْ أَجْلِ النَّظَرِ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), amesema: Wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa katika chumba, naye akiwa na midraa (kitana cha kuchania nywele) akijikuna nacho kichwa chake, mtu mmoja alimchungulia. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Lau ningelijua kwamba unatazama, ningelisimama mpaka nikuchome nacho macho yako mawili. Hakika (kuomba) idhini kumewekwa kwa ajili ya kutazama."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1541
- Hadiyth
- 2430
24-Mlangoباب لا يقتل قرشي صبراMlango Wa Mquraysh Hatauawa Akiwa Amefungwa
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ زَكَرِيَّا، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُطِيعٍ، عَنْ مُطِيعٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ يَوْمَ فَتْحِ مَكَّةَ: "لَا يُقْتَلُ قُرَشِيٌّ صَبْرًا بَعْدَ هَذَا الْيَوْمِ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَةِ"،
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Zakariyyaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mutwiy', kutoka kwa Mutwiy' (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema siku ya Ufunguzi wa Makkah: "Hatauawa Mquraysh akiwa amefungwa baada ya siku hii mpaka Siku ya Qiyaamah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1542
- Hadiyth
- 2431
حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُطِيعٍ، سَمِعْتُ مُطِيعًا، يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ........ فَذَكَرَ نَحْوَهُ. قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: فَسَّرُوا ذَلِكَ: أَنْ لَا يُقْتَلَ قُرَشِيٌّ عَلَى الْكُفْرِ يَعْنِي: لَا يَكُونُ هَذَا أَنْ يَكْفُرَ قُرَشِيٌّ بَعْدَ ذَلِكَ الْيَوْمِ فَأَمَّا فِي الْقَوَدِ، فَيُقْتَلُ
Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir, amesema: 'Abdu-Allaah bin Mutwiy' amesema: Nilimsikia Mutwiy' (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) … Akataja mfano wake.
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Wameifasiri (kauli) hiyo kwamba: Hatauawa Mquraysh kwa sababu ya ukafiri; yaani: Haitakuwa hivi kwamba Mquraysh atakufuru baada ya siku hiyo. Ama katika qawad (kulipiza kisasi cha kuua), basi atauawa.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1542
- Hadiyth
- 2432
25-Mlangoباب لا يؤخذ أحد بجناية غيرهMlango Wa Mtu Hachukuliwi Hatua Kwa Jinai Ya Mwingine
أَخْبَرَنَا يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ يَعْنِي: ابْنَ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الْمَلِكِ بْنَ عُمَيْرٍ، حَدَّثَنِي إِيَادُ بْنُ لَقِيطٍ، عَنْ أَبِي رِمْثَةَ، قَالَ: قَدِمْتُ الْمَدِينَةَ وَمَعِيَ ابْنٌ لِي، وَلَمْ نَكُنْ رَأَيْنَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. فَأَتَيْتُهُ، فَخَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَعَلَيْهِ ثَوْبَانِ أَخْضَرَانِ. فَلَمَّا رَأَيْتُهُ عَرَفْتُهُ بِالصِّفَةِ، فَأَتَيْتُهُ، فَقَالَ: "مَنْ هَذَا الَّذِي مَعَكَ؟". قُلْتُ: ابْنِي وَرَبِّ الْكَعْبَةِ، فَقَالَ: "ابْنُكَ؟"، فَقُلْتُ: أَشْهَدُ بِهِ. قَالَ: "فَإِنَّ ابْنَكَ هَذَا لَا يَجْنِي عَلَيْكَ وَلَا تَجْنِي عَلَيْهِ"
Ametukhabarisha Yuwnus bin Muhammad, ametusimulia Jariyr — yaani: Ibn Haazim —, amesema: Nilimsikia 'Abdul-Malik bin 'Umayr, (akisema:) Amenisimulia Iyaad bin Laqiytw, kutoka kwa Abuw Rimthah (رضي الله عنه), amesema: Nilifika Madiynah nikiwa pamoja na mwanangu mmoja, na tulikuwa hatujapata kumwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Nikamwendea; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatoka naye amevaa nguo mbili za kijani. Nilipomwona, nilimtambua kwa sifa (zake). Nikamwendea, akasema: "Ni nani huyu aliye pamoja nawe?" Nikasema: Ni mwanangu, naapa kwa Rabb wa Al-Ka'bah. Akasema: "Mwanao?" Nikasema: Ninalishuhudia hilo. Akasema: "Basi hakika mwanao huyu hatakutendea jinai, wala wewe hutamtendea jinai (yaani wewe hutabebeshwa kosa lake, wala yeye hatabebeshwa kosa lako)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1542
- Hadiyth
- 2433
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ إِيَادٍ، حَدَّثَنَا إِيَادٌ، عَنْ أَبِي رِمْثَةَ، قَالَ: انْطَلَقْتُ مَعَ أَبِي نَحْوَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ لِأَبِي: "ابْنُكَ هَذَا؟"، فَقَالَ: إِي وَرَبِّ الْكَعْبَةِ. قَالَ: "حَقًّا؟". قَالَ: "حَقًّا أَشْهَدُ بِهِ". قَالَ: فَتَبَسَّمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ضَاحِكًا مِنْ ثَبَتِ شَبَهِي فِي أَبِي وَمِنْ حَلِفِ أَبِي عَلَي، فَقَالَ: "إِنَّ ابْنَكَ هَذَا لَا يَجْنِي عَلَيْكَ وَلَا تَجْنِي عَلَيْهِ". قَالَ: وَقَرَأَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {وَلا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى}
Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Iyaad, ametusimulia Iyaad, kutoka kwa Abuw Rimthah (رضي الله عنه), amesema: Nilikwenda pamoja na baba yangu kuelekea kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akamwambia baba yangu: "Huyu ni mwanao?" Akasema: Ndiyo, naapa kwa Rabb wa Al-Ka'bah. Akasema: "Kweli?" Akasema: "Kweli, ninalishuhudia hilo." Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatabasamu akicheka kutokana na kuthibiti kwa kufanana kwangu na baba yangu, na kutokana na kuapa kwa baba yangu juu yangu. Akasema: "Hakika mwanao huyu hatakutendea jinai, wala wewe hutamtendea jinai (yaani wewe hutabebeshwa kosa lake, wala yeye hatabebeshwa kosa lako)." Akasema: Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasoma:
وَلا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَى
Na wala habebi mbebaji, mzigo (wa dhambi) wa mwengine [Al-An’aam (6:164)]
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 15
- Ukurasa
- 1543
- Hadiyth
- 2434