Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy18 - Kitabu Cha Mauzo

ومن كتاب البيوع

1-Mlangoباب: في الحلال بين والحرام بينMlango Wa Kuhusu Halaal Iko Wazi Na Haraam Iko Wazi

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ النُّعْمَانَ بْنَ بَشِيرٍ، يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الْحَلَالُ بَيِّنٌ وَالْحَرَامُ بَيِّنٌ، وَبَيْنَهُمَا مُتَشَابِهَاتٌ، لَا يَعْلَمُهَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ فَمَنْ اتَّقَى الشُّبُهَاتِ، اسْتَبْرَأَ لِعِرْضِهِ وَدِينِهِ، وَمَنْ وَقَعَ فِي الشُّبُهَاتِ، وَقَعَ فِي الْحَرَامِ، كَالرَّاعِي يَرْعَى حَوْلَ الْحِمَى فَيُوشِكُ أَنْ يُوَاقِعَهُ، وَإِنَّ لِكُلِّ مَلِكٍ حِمًى، أَلَا وَإِنَّ حِمَى اللَّهِ مَحَارِمُهُ، أَلَا وَإِنَّ فِي الْجَسَدِ مُضْغَةً، إِذَا صَلَحَتْ، صَلَحَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، وَإِذَا فَسَدَتْ، فَسَدَ الْجَسَدُ كُلُّهُ، أَلَا وَهِيَ الْقَلْبُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Nilimsikia An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Halaal iko wazi na haraam iko wazi, na baina ya hayo mawili kuna mambo yenye kutatanisha ambayo watu wengi hawayajui. Basi atakayejiepusha na mambo yenye kutatanisha, ameitakasa heshima yake na Dini yake; na atakayetumbukia katika mambo yenye kutatanisha, atatumbukia katika haraam, kama mchungaji anayechunga pembezoni mwa himaa (eneo lililohifadhiwa lisichungwe), anakaribia kutumbukia ndani yake. Na hakika kila mfalme ana himaa. Tanabahini! Na hakika himaa ya Allaah ni mambo Aliyoyaharamisha. Tanabahini! Na hakika katika mwili kuna kipande cha nyama; kikitengemaa, mwili wote hutengemaa, na kikiharibika, mwili wote huharibika. Tanabahini! Nacho ni moyo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1647
Hadiyth
2573

2-Mlangoباب: دع ما يريبك إلى ما لا يريبكMlango Wa Acha Yanayokutia Shaka Uende
Kwa Yasiyokutia Shaka

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ بُرَيْدِ بْنِ أَبِي مَرْيَمَ، عَنْ أَبِي الْحَوْرَاءِ السَّعْدِيِّ، قَالَ: قُلْتُ لِلْحَسَنِ بْنِ عَلِيٍّ: مَا تَحْفَظُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟. قَالَ: سَأَلَهُ رَجُلٌ عَنْ مَسْأَلَةٍ لَا أَدْرِي مَا هِيَ، فَقَالَ: "دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لَا يَرِيبُكَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Burayd bin Abiy Maryam, kutoka kwa Abul-Hawraa As-Sa'diy, amesema: Nilimwambia Al-Hasan bin 'Aliy (رضي الله عنهما): Unahifadhi nini kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Mtu mmoja alimuuliza kuhusu suala moja ambalo sijui ni lipi, akasema: "Acha yanayokutia shaka, uende kwa yasiyokutia shaka."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1648
Hadiyth
2574

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ الزُّبَيْرِ أَبِي عَبْدِ السَّلَامِ، عَنْ أَيُّوبَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مِكْرَزٍ الْفِهْرِيِّ، عَنْ وَابِصَةَ بْنِ مَعْبَدٍ الْأَسَدِيِّ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ لِوَابِصَةَ: "جِئْتَ تَسْأَلُ عَنِ الْبِرِّ وَالْإِثْمِ؟". قَالَ: قُلْتُ: نَعَمْ. قَالَ: فَجَمَعَ أَصَابِعَهُ فَضَرَبَ بِهَا صَدْرَهُ، وَقَالَ: "اسْتَفْتِ نَفْسَكَ. اسْتَفْتِ قَلْبَكَ يَا وَابِصَةُ ثَلَاثًا الْبِرُّ مَا اطْمَأَنَّتْ إِلَيْهِ النَّفْسُ وَاطْمَأَنَّ إِلَيْهِ الْقَلْبُ، وَالْإِثْمُ مَا حَاكَ فِي النَّفْسِ وَتَرَدَّدَ فِي الصَّدْرِ، وَإِنْ أَفْتَاكَ النَّاسُ وَأَفْتَوْكَ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Az-Zubayr Abuw 'Abdis-Salaam, kutoka kwa Ayyuwb bin 'Abdi-Allaah bin Mikraz Al-Fihriy, kutoka kwa Waabiswah bin Ma'bad Al-Asadiy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwambia Waabiswah (رضي الله عنه): "Umekuja kuuliza kuhusu wema na dhambi?" Akasema: Nikasema: Ndiyo. Akasema: Akakusanya vidole vyake, akapiga kwavyo kifua chake, na akasema: "Iombe Fatwa nafsi yako. Uombe Fatwa moyo wako, yaa Waabiswah" — mara tatu —; "wema ni lile ambalo nafsi imetulia kwalo na moyo umetulia kwalo; na dhambi ni lile linalokereketa ndani ya nafsi na likasitasita kifuani, hata kama watu watakupa Fatwa na wakakupa Fatwa."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1649
Hadiyth
2575

3-Mlangoباب: في الربا الذي كان في الجاهليةMlango Wa Kuhusu Riba Iliyokuwa
Katika Jaahiliyyah (Zama Za Ujinga Kabla Ya Islaam)

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا عَلِيُّ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَبِي حُرَّةَ الرَّقَاشِيِّ، عَنْ عَمِّهِ، قَالَ: كُنْتُ آخِذًا بِزِمَامِ نَاقَةِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أَوْسَطِ أَيَّامِ التَّشْرِيقِ أَذُودُ النَّاسَ عَنْهُ، فَقَالَ: "أَلَا إِنَّ كُلَّ رِبًا فِي الْجَاهِلِيَّةِ مَوْضُوعٌ، أَلَا وَإِنَّ اللَّهَ قَدْ قَضَى أَنَّ أَوَّلَ رِبًا يُوضَعُ رِبَا عَبَّاسِ بْنِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، لَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari 'Aliy bin Zayd, kutoka kwa Abuw Hurrah Ar-Raqaashiy, kutoka kwa ammi yake (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa nimeshika hatamu ya ngamia jike wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katikati ya Siku za Tashriyq (siku tatu zinazofuata Siku ya Kuchinja), nikiwazuia watu wasimfikie. Akasema: "Tanabahini! Hakika kila riba (iliyokuwa) katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam) imefutwa. Tanabahini! Na hakika Allaah Amehukumu kwamba riba ya kwanza kufutwa ni riba ya 'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه). Ni zenu rasilimali zenu; msidhulumu na wala msidhulumiwe."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1649
Hadiyth
2576

4-Mlangoباب: في آكل الربا ومؤكلهMlango Wa Kuhusu Mlaji Wa Riba Na Mwenye Kumlisha

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي قَيْسٍ، عَنْ هُزَيْلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ آكِلَ الرِّبَا وَمُؤْكِلَهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Qays, kutoka kwa Huzayl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimlaani mlaji wa riba na mwenye kumlisha (riba)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1650
Hadiyth
2577

5-Mlangoباب: في التشديد في أكل الرباMlango Wa Kuhusu Kutia Mkazo Katika Kula Riba

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يُونُسَ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ سَعِيدٍ الْمَقْبُرِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَيَأْتِيَنَّ زَمَانٌ لَا يُبَالِي الْمَرْءُ بِمَا أَخَذَ الْمَالَ، بِحَلَالٍ أَمْ بِحَرَامٍ"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah bin Yuwnus, ametusimulia Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Sa'iyd Al-Maqburiy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika utakuja wakati ambao mtu hatajali ameichukua mali kwa njia gani: kwa halaal au kwa haraam."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1651
Hadiyth
2578

6-Mlangoباب: في الكسب وعمل الرجل بيدهMlango Wa Kuhusu Uchumaji Na Kazi Ya Mtu Kwa Mkono Wake

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُمَارَةَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ عَمَّتِهِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ أَحَقَّ مَا يَأْكُلُ الرَّجُلُ مِنْ أَطْيَبِ كَسْبِهِ، وَإِنَّ وَلَدَهُ مِنْ أَطْيَبِ كَسْبِهِ"

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Umaarah bin 'Umayr, kutoka kwa shangazi yake, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika kinachostahiki zaidi kuliwa na mtu ni (kile kinachotokana) na chumo lake lililo zuri kabisa; na hakika mwanawe ni katika chumo lake lililo zuri kabisa."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1651
Hadiyth
2579

7-Mlangoباب: في التجارMlango Wa Kuhusu Wafanyabiashara

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ هُوَ: ابْنُ عُثْمَانَ بْنِ خُثَيْمٍ عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ رِفَاعَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَى الْبَقِيعِ، فَقَالَ: "يَا مَعْشَرَ التُّجَّارِ!" حَتَّى إِذَا اشْرَأَبُّوا. قَالَ: "التُّجَّارُ يُحْشَرُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فُجَّارًا، إِلَّا مَنِ اتَّقَى اللَّهَ، وَبَرَّ، وَصَدَقَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: كَانَ أَبُو نُعَيْمٍ، يَقُولُ: عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ رِفَاعَةَ، وَإِنَّمَا هُوَ: إِسْمَاعِيل بْنُ عُبَيْدِ بْنِ رِفَاعَةَ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah — naye ni Ibn 'Uthmaan bin Khuthaym —, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Rifaa'ah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka kwenda Al-Baqiy', akasema: "Enyi jamii ya wafanyabiashara!" Mpaka walipoinua shingo zao (kumtazama), akasema: "Wafanyabiashara watafufuliwa Siku ya Qiyaamah wakiwa waovu, isipokuwa yule aliyemcha Allaah, na akatenda wema, na akasema kweli."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Abuw Nu'aym alikuwa akisema: 'Ubaydu-Allaah bin Rifaa'ah; na hakika yeye ni Ismaa'iyl bin 'Ubayd bin Rifaa'ah.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1652
Hadiyth
2580

8-Mlangoباب: في التاجر الصدوقMlango Wa Kuhusu Mfanyabiashara Mkweli

أَخْبَرَنَا قَبِيصَةُ، أَنْبَأَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "التَّاجِرُ الصَّدُوقُ الْأَمِينُ مَعَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ". قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: لَا عِلْمَ لِي بِهِ إِنَّ الْحَسَنَ سَمِعَ مِنْ أَبِي سَعِيدٍ، وَقَالَ: أَبُو حَمْزَةَ هَذَا، هُوَ صَاحِبُ إِبْرَاهِيمَ، وَهُوَ: مَيْمُونٌ الْأَعْوَرُ

Ametukhabarisha Qabiyswah, ametupa khabari Sufyaan, kutoka kwa Abuw Hamzah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mfanyabiashara mkweli sana, mwaminifu, (atakuwa) pamoja na Manabii (عليهم السلام), na Swiddiqiyna (wakweli kabisa), na Shuhadaa (Mashahidi)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Sina ilimu ya hilo kwamba Al-Hasan alisikia kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه). Na akasema: Abuw Hamzah huyu ndiye sahibu wa Ibraahiym [An-Nakha'iy], naye ni Maymuwn Al-A'war.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1653
Hadiyth
2581

9-Mlangoباب: في النصيحةMlango Wa Kuhusu Nasaha

حَدَّثَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل، عَنْ قَيْسٍ، عَنْ جَرِيرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "بَايَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى إِقَامِ الصَّلَاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، وَالنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ"

Ametusimulia Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Ismaa'iyl, kutoka kwa Qays, kutoka kwa Jariyr bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), amesema: "Nilimpa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) bay'ah (ahadi ya utiifu) juu ya kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kumnasihi kila Muislamu."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1654
Hadiyth
2582

10-Mlangoباب: في النهي عن الغشMlango Wa Kuhusu Katazo La Udanganyifu

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَقِيلٍ: يَحْيَى بْنُ الْمُتَوَكِّلِ، قَالَ: أَخْبَرَنِي الْقَاسِمُ بْنُ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ سَالِمٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ بِطَعَامٍ بِسُوقِ الْمَدِينَةِ فَأَعْجَبَهُ حُسْنُهُ، فَأَدْخَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَهُ فِي جَوْفِهِ، فَأَخْرَجَ شَيْئًا لَيْسَ كَالظَّاهِرِ فَأَفَّفَ لِصَاحِبِ الطَّعَامِ، ثُمَّ قَالَ: "لَا غِشَّ بَيْنَ الْمُسْلِمِينَ، مَنْ غَشَّنَا فَلَيْسَ مِنَّا"

Ametusimulia Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Abuw 'Aqiyl Yahyaa bin Al-Mutawakkil, amesema: Amenikhabarisha Al-Qaasim bin 'Ubaydi-Allaah, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipita kwenye chakula katika soko la Madiynah, uzuri wake ukampendeza. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingiza mkono wake ndani yake, akatoa kitu kisichokuwa kama (kile kilicho) juu. Akamwambia mwenye chakula: Uff! Kisha akasema: "Hakuna udanganyifu baina ya Waislamu. Atakayetudanganya, si katika sisi."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1655
Hadiyth
2583

11-Mlangoباب: في الغدرMlango Wa Kuhusu Usaliti

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سُلَيْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُقَالُ: هَذِهِ غَدْرَةُ فُلَانٍ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Sulaymaan, amesema: Nilimsikia Abuw Waail (akisimulia) kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Kila msaliti atakuwa na bendera Siku ya Qiyaamah; itasemwa: Huu ni usaliti wa fulani."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1656
Hadiyth
2584

12-Mlangoباب: في النهي عن الاحتكارMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuhodhi (Bidhaa)

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ مَعْمَرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نَافِعِ بْنِ نَضْلَةَ الْعَدَوِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا يَحْتَكِرُ إِلَّا خَاطِئٌ مَرَّتَيْنِ"

Ametusimulia Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Ma'mar bin 'Abdi-Allaah bin Naafi' bin Nadhwlah Al-'Adawiy (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hahodhi (bidhaa) isipokuwa mwenye dhambi" — mara mbili.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1656
Hadiyth
2585

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ زَيْدِ بْنِ جُدْعَانَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ عُمَرَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْجَالِبُ مَرْزُوقٌ، وَالْمُحْتَكِرُ مَلْعُونٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa 'Aliy bin Saalim, kutoka kwa 'Aliy bin Zayd bin Jud'aan, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwenye kuleta (bidhaa sokoni) huruzukiwa, na mwenye kuhodhi (bidhaa) amelaaniwa."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1657
Hadiyth
2586

13-Mlangoباب: في النهي عن أن يسعر في المسلمينMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuwapangia Waislamu Bei

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَخْبَرَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حُمَيْدٍ، وَثَابِتٍ، وَقَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: غَلَا السِّعْرُ عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ النَّاسُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ غَلَا السِّعْرُ فَسَعِّرْ لَنَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْخَالِقُ الْقَابِضُ الْبَاسِطُ الرَّازِقُ، الْمُسَعِّرُ، وَإِنِّي أَرْجُو أَنْ أَلْقَى رَبِّي وَلَيْسَ أَحَدٌ مِنْكُمْ يَطْلُبُنِي بِمَظْلَمَةٍ ظَلَمْتُهَا إِيَّاهُ بِدَمٍ وَلَا مَالٍ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametukhabarisha Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Humayd, na Thaabit, na Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Bei ilipanda katika zama za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم). Watu wakasema: Yaa Rasula-Allaah, bei imepanda, basi tupangie bei. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakika Allaah Ndiye Muumbaji, Mwenye Kukunja, Mwenye Kukunjua, Mwenye Kuruzuku, Mwenye Kupanga Bei. Na hakika mimi natumai kukutana na Rabb wangu na hali hakuna yeyote miongoni mwenu anayenidai dhulma niliyomdhulumu, katika damu wala mali."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1658
Hadiyth
2587

14-Mlangoباب: في السماحةMlango Wa Kuhusu Wepesi (Katika Kuamiliana)

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ يُونُسَ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا مَنْصُورُ بْنُ الْمُعْتَمِرِ، عَنْ رِبْعِيِّ بْنِ حِرَاشٍ: أَنَّ حُذَيْفَةَ حَدَّثَهُمْ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تَلَقَّتِ الْمَلَائِكَةُ رُوحَ رَجُلٍ مِمَّنْ قَبْلَكُمْ، فَقَالُوا: أَعَمِلْتَ مِنَ الْخَيْرِ شَيْئًا؟، فَقَالَ: لَا، قَالُوا: تَذَكَّرْ. قَالَ: كُنْتُ أُدَايِنُ النَّاسَ فَآمُرُ فِتْيَانِي أَنْ يُنْظِرُوا الْمُعْسِرَ، وَيَتَجَاوَزُوا عَنِ الْمُوسِرِ". قَالَ: "قَالَ اللَّهُ: تَجَاوَزُوا عَنْهُ"

Ametusimulia Ahmad bin Yuwnus, ametusimulia Zuhayr, ametusimulia Manswuwr bin Al-Mu'tamir, kutoka kwa Rib'iyy bin Hiraash, kwamba Hudhayfah (رضي الله عنه) aliwasimulia, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Malaika (عليهم السلام) waliipokea roho ya mtu mmoja miongoni mwa waliokuwa kabla yenu, wakasema: Je, ulitenda chochote katika kheri? Akasema: Hapana. Wakasema: Kumbuka. Akasema: Nilikuwa nikiwakopesha watu, nikiwaamrisha vijana wangu (watumishi) wampe muhula mwenye dhiki, na wamsamehe mwenye wasaa." Akasema: "Allaah Akasema: Msameheni."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1658
Hadiyth
2588

15-Mlangoباب: في البيعان بالخيار ما لم يتفرقاMlango Wa Kuhusu Wauzianaji Wawili
Wana Khiyari Madamu Hawajaachana

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ صَالِحٍ أَبِي الْخَلِيلِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ حِزَامٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْبَيِّعَانِ بِالْخِيَارِ مَا لَمْ يَتَفَرَّقَا فَإِنْ صَدَقَا وَبَيَّنَا، بُورِكَ لَهُمَا فِي بَيْعِهِمَا، وَإِنْ كَذَبَا وَكَتَمَا، مُحِقَ بَرَكَةُ بَيْعِهِمَا".

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Swaalih Abul-Khaliyl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Al-Haarith, kutoka kwa Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Wauzianaji wawili wana khiyari (hiari ya kuendeleza biashara au kuivunja) madamu hawajaachana. Wakisema kweli na wakabainisha, watabarikiwa katika biashara yao; na wakisema uongo na wakaficha, itafutwa baraka ya biashara yao."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1660
Hadiyth
2589

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، بِإِسْنَادِهِ مِثْلَهُ

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) yake, mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1660
Hadiyth
2590

16-Mlangoباب: إذا اختلف المتبايعانMlango Wa Wauzianaji Wawili Wanapotofautiana

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي لَيْلَى، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الْبَيِّعَانِ إِذَا اخْتَلَفَا وَالْبَيْعُ قَائِمٌ بِعَيْنِهِ، وَلَيْسَ بَيْنَهُمَا بَيِّنَةٌ، فَالْقَوْلُ مَا قَالَ الْبَائِعُ، أَوْ يَتَرَادَّانِ الْبَيْعَ"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Hushaym, ametusimulia Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa Al-Qaasim bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Wauzianaji wawili wanapotofautiana, na kilichouzwa kingalipo chenyewe, na hakuna ushahidi baina yao, basi kauli ni ile aliyoisema muuzaji, au warudishiane mauzo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1661
Hadiyth
2591

17-Mlangoباب: لا يبع على بيع أخيهMlango Wa Asiuze Juu Ya Mauzo Ya Nduguye

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ: ابْنُ إِسْحَقَ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ شِمَاسَةَ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا يَحِلُّ لِامْرِئٍ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ أَنْ يَبِيعَ عَلَى بَيْعِ أَخِيهِ حَتَّى يَتْرُكَهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Shimaasah, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Haihalaliki kwa mtu anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho kuuza juu ya mauzo ya nduguye mpaka (nduguye) ayaache."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1661
Hadiyth
2592

18-Mlangoباب: في الخيار والعهدةMlango Wa Kuhusu Khiyari
Na Dhamana (Ya Muuzaji Juu Ya Kasoro)

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا أَبَانُ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "عُهْدَةُ الرَّقِيقِ ثَلَاثَةُ أَيَّامٍ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Abaan bin Yaziyd, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dhamana (ya muuzaji juu ya kasoro) ya mtumwa ni siku tatu."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1661
Hadiyth
2593

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ هَمَّامٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عُهْدَةُ الرَّقِيقِ ثَلَاثَةُ أَيَّامٍ". فَفَسَّرَهُ قَتَادَةُ: إِنْ وَجَدَ فِي الثَّلَاثِ عَيْبًا رَدَّهُ بِغَيْرِ بَيِّنَةٍ، وَإِنْ وَجَدَهُ بَعْدَ ثَلَاثٍ، لَمْ يَرُدَّهُ إِلَّا بِبَيِّنَةٍ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Hammaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Dhamana (ya muuzaji juu ya kasoro) ya mtumwa ni siku tatu." Qataadah akaifasiri: "Akikuta kasoro ndani ya siku tatu, atamrudisha bila ushahidi; na akiikuta baada ya siku tatu, hatamrudisha isipokuwa kwa ushahidi."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1662
Hadiyth
2594

19-Mlangoباب: في المحفلاتMlango Wa Kuhusu Wanyama Waliozuiliwa Maziwa Kiwele

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمِنْهَالِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ هُوَ: ابْنُ حَسَّانَ عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنِ اشْتَرَى شَاةً مُصَرَّاةً أَوْ لَقْحَةً مُصَرَّاةً، فَهُوَ بِالْخِيَارِ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ، فَإِنْ رَدَّهَا، رَدَّ مَعَهَا صَاعًا مِنْ طَعَامٍ لَا سَمْرَاءَ"

Ametusimulia Muhammad bin Al-Minhaal, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Hishaam — naye ni Ibn Hassaan —, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenunua mbuzi aliyezuiliwa maziwa kiwele, au ngamia jike mwenye maziwa aliyezuiliwa maziwa kiwele, basi yeye ana khiyari (hiari ya kuendeleza biashara au kuivunja) kwa siku tatu. Akimrudisha, atarudisha pamoja naye pishi (Swaa') ya chakula, si ngano."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1662
Hadiyth
2595

20-Mlangoباب: في النهي عن بيع الغررMlango Wa Kuhusu Katazo La Biashara Ya Gharar
(Yenye Udanganyifu Na Isiyojulikana Matokeo Yake)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا يَحْيَى الْقَطَّانُ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْغَرَرِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Yahyaa Al-Qattwaan, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza biashara ya gharar (yenye udanganyifu na isiyojulikana matokeo yake)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1663
Hadiyth
2596

21-Mlangoباب: في النهي عن بيع الثمار حتى يبدو صلاحهاMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Matunda
Mpaka Kudhihiri Kuiva Kwake

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الثِّمَارِ حَتَّى يَبْدُوَ صَلَاحُهَا، نَهَى الْبَائِعَ وَالْمُشْتَرِيَ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuuza matunda mpaka kudhihiri kuiva kwake; alimkataza muuzaji na mnunuzi."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1664
Hadiyth
2597

22-Mlangoباب: في الجائحةMlango Wa Kuhusu Maafa (Yanayoangamiza Mazao)

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا ابْنُ جُرَيْجٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنِ ابْتَاعَ ثَمَرَةً فَأَصَابَتْهُ جَائِحَةٌ، فَلَا يَأْخُذَنَّ مِنْهُ شَيْئًا. بِمَ تَأْخُذُ مَالَ أَخِيكَ بِغَيْرِ حَقٍّ؟"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenunua matunda, kisha yakapatwa na maafa, basi (muuzaji) asichukue kutoka kwake chochote. Kwa sababu gani uchukue mali ya nduguyo bila haki?"

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1664
Hadiyth
2598

23-Mlangoباب: في المحاقلة والمزابنةMlango Wa Kuhusu Muhaaqalah (Kuuza Mimea Ya Nafaka
Iliyo Shambani Kwa Ngano) Na Muzaabanah (Kuuza
Matunda Ya Mitende Yaliyo Mtini Kwa Tende Kavu)

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرٍو وحَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْمُحَاقَلَةِ وَالْمُزَابَنَةِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: الْمُحَاقَلَةُ: بَيْعُ الزَّرْعِ بِالْبُرِّ. وَقَالُوا: كَذَلِكَ يَقُولُ ابْنُ الْمُسَيَّبِ

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Muhammad bin 'Amr; na ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza muhaaqalah (kuuza mimea ya nafaka iliyo shambani kwa ngano) na muzaabanah (kuuza matunda ya mitende yaliyo mtini kwa tende kavu)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Muhaaqalah ni kuuza mimea kwa ngano. Na wakasema: Hivyo ndivyo anavyosema Ibn Al-Musayyib.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1665
Hadiyth
2599

24-Mlangoباب: في العراياMlango Wa Kuhusu 'Araayaa (Kuuza Tende Mbichi Zilizo Mtini
Kwa Makadirio Yake Ya Tende Kavu, Ili Ziliwe
Na Watu Wa Nyumbani)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، قَالَ: "رَخَّصَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي بَيْعِ الْعَرَايَا بِالتَّمْرِ وَالرُّطَبِ، وَلَمْ يُرَخِّصْ فِي غَيْرِ ذَلِكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliruhusu kuuza 'araayaa (kuuza tende mbichi zilizo mtini kwa makadirio yake ya tende kavu, ili ziliwe na watu wa nyumbani) kwa tende kavu na kwa tende mbichi, na hakuruhusu katika (biashara) isiyokuwa hiyo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1665
Hadiyth
2600

25-Mlangoباب: في النهي عن بيع الطعام قبل القبضMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Chakula Kabla Ya Kukipokea

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنِ ابْتَاعَ طَعَامًا، فَلَا يَبِعْهُ حَتَّى يَقْبِضَهُ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayenunua chakula, basi asikiuze mpaka akipokee."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1666
Hadiyth
2601

26-Mlangoباب: في النهي عن شرطين في بيعMlango Wa Kuhusu Katazo La Masharti Mawili
Katika Mauzo Moja

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ حُسَيْنٍ الْمُعَلِّمِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ سَلَفٍ وَبَيْعٍ، وَعَنْ شَرْطَيْنِ فِي بَيْعٍ، وَعَنْ رِبْحِ مَا لَمْ يُضْمَنْ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Husayn Al-Mu'allim, kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما)], amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mkopo pamoja na mauzo, na masharti mawili katika mauzo moja, na faida ya kitu ambacho hakijaingia katika dhamana (ya muuzaji)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1667
Hadiyth
2602

27-Mlangoباب: فيمن باع عبدا وله مالMlango Wa Kuhusu Aliyeuza Mtumwa Naye Ana Mali

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، عَنْ ابْنِ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنِ اشْتَرَى عَبْدًا وَلَمْ يَشْتَرِطْ مَالَهُ، فَلَا شَيْءَ لَهُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, kutoka kwa Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake ['Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenunua mtumwa, na hakushurutisha (kupewa) mali yake, basi hana chochote (katika mali hiyo)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1667
Hadiyth
2603

28-Mlangoباب: في النهي عن المنابذة والملامسةMlango Wa Kuhusu Katazo La Munaabadhah
(Biashara Ya Kutupiana) Na Mulaamasah (Biashara Ya Kugusa)

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعَتَيْنِ، وَعَنْ لِبْسَتَيْنِ: عَنْ بَيْعِ الْمُنَابَذَةِ وَالْمُلَامَسَةِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: الْمُنَابَذَةُ: يَرْمِي هَذَا إِلَى ذَاكَ. وَيَرْمِي ذَاكَ إِلَى هذَا. قَالَ: كَانَ هَذَا فِي الْجَاهِلِيَّةِ

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Atwaa bin Yaziyd, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza biashara mbili, na mavazi mawili: (alikataza) biashara ya munaabadhah (biashara ya kutupiana) na mulaamasah (biashara ya kugusa)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Munaabadhah ni: huyu amtupie yule (bidhaa), na yule amtupie huyu. Akasema: Hii ilikuwa katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1668
Hadiyth
2604

29-Mlangoباب: في بيع الحصاةMlango Wa Kuhusu Biashara Ya Kijiwe

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْغَرَرِ، وَعَنْ بَيْعِ الْحَصَاةِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: إِذَا رَمَى بِحَصًا، وَجَبَ الْبَيْعُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza biashara ya gharar (yenye udanganyifu na isiyojulikana matokeo yake), na biashara ya kijiwe."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: (Ni kwamba) anaporusha kijiwe, mauzo yanalazimika.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1669
Hadiyth
2605

30-Mlangoباب: في النهي عن بيع الحيوان بالحيوانMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Mnyama Kwa Mnyama

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، وَجَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْحَيَوَانِ بِالْحَيَوَانِ نَسِيئَةً". ثُمَّ إِنَّ الْحَسَنَ نَسِيَ هَذَا الْحَدِيثَ، وَلَمْ يَقُلْ جَعْفَرٌ: ثُمَّ إِنَّ الْحَسَنَ نَسِيَ هَذَا الْحَدِيثَ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir na Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Samurah bin Jundub (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuuza mnyama kwa mnyama kwa kuchelewesha (malipo)." Kisha Al-Hasan akaisahau Hadiyth hii. Na Ja'far hakusema: Kisha Al-Hasan akaisahau Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1669
Hadiyth
2606

31-Mlangoباب: في الرخصة في استقراض الحيوانMlango Wa Kuhusu Ruhusa Ya Kukopa Mnyama

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَالِكٍ، قِرَاءَةً عَلَيْهِ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي رَافِعٍ: مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: اسْتَسْلَفَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَكْرًا، فَجَاءَتْ إِبِلٌ مِنْ إِبِلِ الصَّدَقَةِ. قَالَ أَبُو رَافِعٍ: فَأَمَرَنِي أَنْ أَقْضِيَ الرَّجُلَ بَكْرَهُ، فَقُلْتُ: لَمْ أَجِدْ فِي الْإِبِلِ إِلَّا جَمَلًا خِيَارًا رَبَاعِيًا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَعْطِهِ إِيَّاهُ، فَإِنَّ خَيْرَ النَّاسِ أَحْسَنُهُمْ قَضَاءً". قَالَ عَبْد اللَّهِ: هَذَا يُقَوِّي قَوْلَ مَنْ يَقُولُ: الْحَيَوَانُ بِالْحَيَوَانِ

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, kutoka kwa Maalik, kwa kusomewa yeye, kutoka kwa Zayd bin Aslam, kutoka kwa 'Atwaa bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Raafi' (رضي الله عنه) — mawlaa (mwachwa huru) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikopa ngamia mchanga (dume), kisha zikaja ngamia miongoni mwa ngamia za swadaka. Abuw Raafi' (رضي الله عنه) akasema: Akaniamrisha nimlipe yule mtu ngamia wake mchanga. Nikasema: Sikupata katika ngamia isipokuwa ngamia dume bora aliyetimiza miaka sita. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mpe huyo, kwani hakika bora ya watu ni aliye mzuri zaidi wao katika kulipa."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Hii inatia nguvu kauli ya anayesema: (Inafaa) mnyama kwa mnyama.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1670
Hadiyth
2607

32-Mlangoباب: في النهي عن تلقي البيوعMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuzipokea Bidhaa (Njiani
Kabla Ya Kufika Sokoni)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمِنْهَالِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ حَسَّانَ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَلَقَّوُا الْجَلَبَ، مَنَ تَلَقَّاهُ فَاشْتَرَى مِنْهُ شَيْئًا، فَهُوَ بِالْخِيَارِ إِذَا دَخَلَ السُّوقَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Minhaal, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Hishaam bin Hassaan, kutoka kwa Muhammad [bin Siyriyn], kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msizipokee bidhaa zinazoletwa (njiani). Atakayezipokea akanunua kutoka kwake chochote, basi yeye (mwenye bidhaa) ana khiyari (hiari ya kuendeleza biashara au kuivunja) atakapoingia sokoni."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1671
Hadiyth
2608

33-Mlangoباب: لا يبع على بيع أخيهMlango Wa Asiuze Juu Ya Mauzo Ya Nduguye

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَبِيعُ بَعْضُكُمْ عَلَى بَيْعِ بَعْضٍ، وَلَا تَلَقَّوُا السِّلَعَ حَتَّى يُهْبَطَ بِهَا الْأَسْوَاقَ، وَلَا تَنَاجَشُوا"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Asiuze baadhi yenu juu ya mauzo ya baadhi (mwingine); wala msizipokee bidhaa (njiani) mpaka zishushwe nazo masokoni; wala msifanyiane najsh (kupandisha bei kwa hila bila nia ya kununua)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1672
Hadiyth
2609

34-Mlangoباب: في النهي عن ثمن الكلبMlango Wa Kuhusu Katazo La Thamani Ya Mbwa

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، حَدَّثَنِي الزُّهْرِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنِ أَبِي مَسْعُودٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ثَمَنِ الْكَلْبِ، وَمَهْرِ الْبَغِيِّ، وَحُلْوَانِ الْكَاهِنِ"، قَالَ عَبْد اللَّهِ: حُلْوَانُ الْكَاهِنِ، مَا يُعْطَى عَلَى كَهَانَتِهِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, amenisimulia Az-Zuhriy, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abuw Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza thamani ya mbwa, na mahari ya mzinifu, na hulwaan (ujira) ya kuhani."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Hulwaan ya kuhani ni kile anachopewa kwa ukuhani wake.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1673
Hadiyth
2610

35-Mlangoباب: في النهي عن بيع الخمرMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Khamr (Pombe)

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ مُسْلِمٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: لَمَّا نَزَلَتِ الْآيَةُ فِي آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ فِي الرِّبَا، "خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَتَلَاهُنَّ عَلَى النَّاسِ، ثُمَّ حَرَّمَ التِّجَارَةَ فِي الْخَمْرِ"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Ilipoteremka Aayah iliyo mwishoni mwa Suwrah Al-Baqarah (2) kuhusu riba, "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka akazisoma kwa watu, kisha akaharamisha biashara ya khamr (pombe)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1673
Hadiyth
2611

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ أَبِي الضُّحَى، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: لَمَّا نَزَلَتِ الْآيَاتُ مِنْ أَوَاخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ، "خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَتَلَاهُنَّ عَلَى النَّاسِ، ثُمَّ نَهَى عَنِ التِّجَارَةِ فِي الْخَمْرِ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Abudh-Dhwuhaa, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Zilipoteremka Aayah za mwisho za Suwrah Al-Baqarah (2), "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka akazisoma kwa watu, kisha akakataza biashara ya khamr (pombe)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1673
Hadiyth
2612

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ: ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي يَزِيدَ، عَنْ الْقَعْقَاعِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ وَعْلَةَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ عَنْ جُلُودِ الْمَيْتَةِ، فَقَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "دِبَاغُهَا طَهُورُهَا" وَسَأَلْتُهُ عَنْ بَيْعِ الْخَمْرِ مِنْ أَهْلِ الذِّمَّةِ، فَقُلْتُ لَهُ: إِنَّ لَنَا أَعْنَابًا، وَإِنَّا نَتَّخِذُ مِنْهَا هَذِهِ الْخُمُورَ فَنَبِيعُهَا مِنْ أَهْلِ الذِّمَّةِ؟. قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: أَهْدَى رَجُلٌ مِنْ ثَقِيفٍ أَوْ دَوْسٍ لِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَاوِيَةً مِنْ خَمْرٍ فِي حَجَّةِ الْوَدَاعِ، فَقَالَ لَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَمَا عَلِمْتَ يَا أَبَا فُلَانٍ أَنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَهَا؟". قَالَ: لَا وَاللَّهِ. قَالَ: "فَإِنَّ اللَّهَ قَدْ حَرَّمَهَا". فَالْتَفَتَ إِلَى غُلَامِهِ، فَقَالَ: اخْرُجْ بِهَا إِلَى الْحَزْوَرَةِ فَبِعْهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَوَ مَا عَلِمْتَ يَا أَبَا فُلَانٍ، أَنَّ الَّذِي حَرَّمَ شُرْبَهَا، حَرَّمَ بَيْعَهَا؟". قَالَ: فَأَمَرَ بِهَا فَأُفْرِغَتْ فِي الْبَطْحَاءِ

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa Al-Qa'qaa' bin Hakiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Wa'lah, amesema: Nilimuuliza Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu ngozi za mizoga. Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kusindikwa kwake ndiko kutwaharishwa kwake." Na nikamuuliza kuhusu kuwauzia watu wa Dhimmah (ulinzi wa dola ya Kiislamu) khamr (pombe). Nikamwambia: Hakika sisi tuna mizabibu, na hakika sisi tunatengeneza kutokana nayo pombe hizi, kisha tunawauzia watu wa Dhimmah? Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akasema: Mtu mmoja wa (kabila la) Thaqiyf au Daws alimpa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) zawadi ya kiriba kikubwa cha khamr katika Hijjah ya kuaga. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Je, hukujua, yaa Abaa Fulaan, kwamba Allaah Ameiharamisha?" Akasema: Hapana, naapa kwa Allaah. Akasema: "Basi hakika Allaah Ameiharamisha." Akamgeukia kijana wake (mtumishi), akasema: Toka nayo uende Al-Hazwarah (mahali pa soko huko Makkah), ukaiuze. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, hukujua, yaa Abaa Fulaan, kwamba Aliyeharamisha kuinywa, Ameharamisha kuiuza?" Akasema: Akaamrisha (imwagwe), ikamwagwa katika Al-Batwhaa (bonde la Makkah).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1673
Hadiyth
2613

36-Mlangoباب: في النهي عن بيع الولاءMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Kuuza Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru Mtumwa)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْوَلَاءِ، وَعَنْ هِبَتِهِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: الْأَمْرُ عَلَى هَذَا، لَا يُبَاعُ وَلَا يُوهَبُ

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza kuuza walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru mtumwa), na kuutoa kuwa zawadi."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Jambo liko juu ya hili: (walaa) hauuzwi wala hautolewi kuwa zawadi.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1675
Hadiyth
2614

37-Mlangoباب: في بيع المدبرMlango Wa Kuhusu Kumuuza Mtumwa Aliyeachwa Huru
Baada Ya Kufa Kwa Bwana Wake

أَخْبَرَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ الْأَنْصَارِيَّ، قَالَ: أَعْتَقَ رَجُلٌ مِنَّا عَبْدًا لَهُ عَنْ دُبُرٍ. قَالَ: "فَدَعَا بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَبَاعَهُ". قَالَ جَابِرٌ: وَإِنَّمَا مَاتَ عَامَ أَوَّلَ. قِيلَ لعَبْدِ اللَّهِ: تَقُولُ بِهِ؟. قَالَ: قَوْمُ يَقُولُونَ

Ametukhabarisha Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, amesema: Nilimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah Al-Answaariy (رضي الله عنهما) akisema: Mtu mmoja miongoni mwetu alimwacha huru mtumwa wake (kwa sharti la kuwa huru) baada ya kufa kwake. Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwitisha (mtumwa huyo), akamuuza." Jaabir (رضي الله عنه) amesema: Na hakika (mtumwa huyo) alikufa mwaka uliopita tu.

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unasema hivyo? Akasema: Kuna watu wanaosema (hivyo).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1676
Hadiyth
2615

38-Mlangoباب: في بيع أمهات الأولادMlango Wa Kuhusu Kuwauza Wajakazi
Waliowazalia Mabwana Zao Watoto

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ حُسَيْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِذَا وَلَدَتْ أَمَةُ الرَّجُلِ مِنْهُ، فَهِيَ مُعْتَقَةٌ عَنْ دُبُرٍ مِنْهُ أَوْ بَعْدَهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Husayn bin 'Abdi-Allaah bin 'Ubaydi-Allaah bin 'Abbaas, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mjakazi wa mtu anapomzalia (mtoto), basi yeye ni mwenye kuachwa huru baada ya kufa kwake — au: baada yake."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1676
Hadiyth
2616

39-Mlangoباب: في صاع المدينة ومدهاMlango Wa Kuhusu Swaa' (Pishi) Ya Madiynah
Na Mudd (Kipimo Cha Viganja Viwili) Wake

أَخْبَرَنَا أَبُو مُحَمَّدٍ الْحَنَفِيُّ الْمَدَنِيُّ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمْ فِي مِكْيَالِهِمْ، وَبَارِكْ لَهُمْ فِي صَاعِهِمْ وَمُدِّهِمْ" يَعْنِي: الْمَدِينَةَ

Ametukhabarisha Abuw Muhammad Al-Hanafiy Al-Madaniy, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Is-haaq bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Twalhah, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:

اللَّهُمَّ بَارِكْ لَهُمْ فِي مِكْيَالِهِمْ، وَبَارِكْ لَهُمْ فِي صَاعِهِمْ وَمُدِّهِمْ

Yaa Allaah! Wabarikie katika kipimo chao, na Uwabarikie katika Swaa' yao na Mudd wao.

Yaani: (watu wa) Madiynah.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1677
Hadiyth
2617

40-Mlangoباب: في النهي عن بيع الطعام إلا مثلا بمثلMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Kuuza Chakula
Isipokuwa Kwa Kiasi Sawa Kwa Kiasi Sawa

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ بِلَالٍ، قَالَ: كَانَ عِنْدِي مُدُّ تَمْرٍ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَوَجَدْتُ أَطْيَبَ مِنْهُ صَاعًا بِصَاعَيْنِ، فَاشْتَرَيْتُ مِنْهُ، فَأَتَيْتُ بِهِ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "مِنْ أَيْنَ لَكَ هَذَا يَا بِلَالُ؟". قُلْتُ: اشْتَرَيْتُ صَاعًا بِصَاعَيْنِ. قَالَ: "رُدَّهُ وَرُدَّ عَلَيْنَا تَمْرَنَا"

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa Bilaal (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa na Mudd (kipimo cha viganja viwili) mmoja wa tende za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); nikapata (tende) bora kuliko hizo, Swaa' (pishi) moja kwa Swaa' mbili, nikanunua katika hizo. Nikamletea Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Umezipata wapi hizi, yaa Bilaal?" Nikasema: Nimenunua Swaa' moja kwa Swaa' mbili. Akasema: "Zirudishe, na uturudishie tende zetu."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1677
Hadiyth
2618

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ هُوَ: ابْنُ بِلَالٍ، عَنْ عَبْدِ الْمَجِيدِ بْنِ سُهَيْلِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّهُ سَمِعَ سَعِيدَ بْنَ الْمُسَيِّبِ يُحَدِّثُ أَنَّ أَبَا سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ وَأَبَا هُرَيْرَةَ حَدَّثَاهُ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ أَخَا بَنِي عَدِيٍّ الْأَنْصَارِيَّ فَاسْتَعْمَلَهُ عَلَى خَيْبَرَ، فَقَدِمَ بِتَمْرٍ جَنِيبٍ. قَالَ ابْنُ مَسْلَمَةَ: يَعْنِي: جَيِّدًا، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَكُلُّ تَمْرِ خَيْبَرَ هَكَذَا؟". قَالَ: لَا وَاللَّهِ يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا لَنَشْتَرِي الصَّاعَ بِالصَّاعَيْنِ مِنَ الْجَمْعِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَفْعَلُوا، وَلَكِنْ مِثْلًا بِمِثْلٍ، أَوْ بِيعُوا هَذَا، وَاشْتَرُوا بِثَمَنِهِ مِنْ هَذَا، وَكَذَلِكَ الْمِيزَانُ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Sulaymaan — naye ni Ibn Bilaal —, kutoka kwa 'Abdul-Majiyd bin Suhayl bin 'Abdir-Rahmaan, kwamba alimsikia Sa'iyd bin Al-Musayyib akisimulia kwamba Abuw Sa'iyd Al-Khudriy na Abuw Hurayrah (رضي الله عنهما) walimsimulia: Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimtuma ndugu wa Banuw 'Adiy, Al-Answaariy, akamfanya kuwa mtawala juu ya Khaybar. Akaja na tende za janiyb — Ibn Maslamah amesema: yaani: nzuri. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: "Je, tende zote za Khaybar ziko hivi?" Akasema: Hapana, Wa-Allaahi, yaa Rasula-Allaah; hakika sisi tunanunua Swaa' (pishi) moja kwa Swaa' mbili za tende za mchanganyiko. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Msifanye (hivyo); lakini (uzeni) kiasi sawa kwa kiasi sawa, au uzeni hizi, na nunueni kwa thamani yake katika hizi (nyingine). Na hivyo hivyo (kinachouzwa kwa) mizani."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1678
Hadiyth
2619

41-Mlangoباب: في النهي عن الصرفMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Swarf
(Kubadilishana Dhahabu Na Fedha)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ مَالِكِ بْنِ أَوْسِ بْنِ الْحَدَثَانِ النَّصْرِيِّ، عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رَضِي اللَّهُ عَنْهُ، قالَ: سمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الذَّهَبُ بِالذَّهَبِ هَاءَ وَهَاءَ، وَالْفِضَّةُ بِالْفِضَّةِ هَاءَ وَهَاءَ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ هَاءَ وَهَاءَ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ هَاءَ وَهَاءَ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ هَاءَ وَهَاءَ، وَلَا فَضْلَ بَيْنَهُمَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Maalik bin Aws bin Al-Hadathaan An-Naswriy, kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Dhahabu kwa dhahabu (iwe) papo kwa papo (chukua na utoe), na fedha kwa fedha papo kwa papo, na tende kwa tende papo kwa papo, na ngano kwa ngano papo kwa papo, na shayiri kwa shayiri papo kwa papo; na hakuna ziada baina ya viwili hivyo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1679
Hadiyth
2620

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدٌ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْأَشْعَثِ الصَّنْعَانِيِّ، قَالَ: قَامَ أنَاسٌ فِي إِمَارَةِ مُعَاوِيَةَ يَبِيعُونَ آنِيَةَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ إِلَى الْعَطَاءِ. فَقَامَ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ، فَقَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنْ بَيْعِ الذَّهَبِ بِالذَّهَبِ، وَالْفِضَّةِ بِالْفِضَّةِ، وَالْبُرِّ بِالْبُرِّ، وَالتَّمْرِ بِالتَّمْرِ، وَالشَّعِيرِ بِالشَّعِيرِ، وَالْمِلْحِ بِالْمِلْحِ إِلَّا مِثْلًا بِمِثْلٍ سَوَاءً بِسَوَاءٍ، فَمَنْ زَادَ أَوْ ازْدَادَ، فَقَدْ أَرْبَى"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Ash'ath Asw-Swan'aaniy, amesema: Watu fulani walisimama katika utawala wa Mu'aawiyah (رضي الله عنه), wakiuza vyombo vya dhahabu na fedha kwa (malipo ya) wakati wa kupokea posho. 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "amekataza kuuza dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, na ngano kwa ngano, na tende kwa tende, na shayiri kwa shayiri, na chumvi kwa chumvi, isipokuwa kiasi sawa kwa kiasi sawa, sawa kwa sawa. Basi atakayezidisha au akaomba kuzidishiwa, hakika amefanya riba."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1680
Hadiyth
2621

42-Mlangoباب: لا ربا إلا في النسيئةMlango Wa Hakuna Riba Isipokuwa Katika Kuahirisha (Malipo)

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي يَزِيدَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أُسَامَةُ بْنُ زَيْدٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّمَا الرِّبَا فِي الدَّيْنِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: مَعْنَاهُ: دِرْهَمٌ بِدِرْهَمَيْنِ

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Ubaydi-Allaah bin Abiy Yaziyd, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Amenikhabarisha Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika riba iko katika deni (tu)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Maana yake ni: dirhamu moja kwa dirhamu mbili.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1680
Hadiyth
2622

43-Mlangoباب: الرخصة في اقتضاء الورق من الذهبMlango Wa Ruhusa Ya Kulipwa Fedha Badala Ya Dhahabu

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: كُنْتُ أَبِيعُ الْإِبِلَ بِالْبَقِيعِ فَأَبِيعُ بِالدَّنَانِيرِ، وَآخُذُ الدَّرَاهِمَ، وَأَبِيعُ بِالدَّرَاهِمِ وَآخُذُ الدَّنَانِيرَ وَرُبَّمَا قَالَ: أَقْبِضُ فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، رُوَيْدَكَ أَسْأَلُكَ: إِنِّي أَبِيعُ الْإِبِلَ بِالْبَقِيعِ فَأَبِيعُ بِالدَّنَانِيرِ، وَآخُذُ الدَّرَاهِمَ، وَأَبِيعُ بِالدَّرَاهِمِ وَآخُذُ الدَّنَانِيرَ. قَالَ: "لَا بَأْسَ أَنْ تَأْخُذَ بِسِعْرِ يَوْمِكَ، مَا لَمْ تَفْتَرِقَا، وَبَيْنَكُمَا شَيْءٌ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Nilikuwa nikiuza ngamia huko Al-Baqiy' (eneo la Madiynah); nauza kwa dinari na nachukua dirhamu, na nauza kwa dirhamu na nachukua dinari — na huenda alisema: napokea. Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Yaa Rasula-Allaah, nipe nafasi nikuulize: Hakika mimi nauza ngamia huko Al-Baqiy'; nauza kwa dinari na nachukua dirhamu, na nauza kwa dirhamu na nachukua dinari. Akasema: "Hakuna ubaya kuchukua kwa bei ya siku yako, maadamu hamjaachana nanyi baina yenu kuna kitu (ambacho hakijakabidhiwa)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1681
Hadiyth
2623

44-Mlangoباب: في الرهنMlango Wa Kuhusu Rahani

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "تُوُفِّيَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَإِنَّ دِرْعَهُ لَمَرْهُونَةٌ عِنْدَ رَجُلٍ مِنَ الْيَهُودِ بِثَلَاثِينَ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alifariki na hakika deraya yake ilikuwa imewekwa rahani kwa mtu mmoja wa Mayahudi kwa Swaa' (pishi) thelathini za shayiri."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1681
Hadiyth
2624

45-Mlangoباب: في السلفMlango Wa Kuhusu Salaf (Kulipa Thamani Mapema
Kwa Bidhaa Itakayotolewa Baadaye)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ أَبِي نَجِيحٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ كَثِيرٍ، عَنْ أَبِي الْمِنْهَالِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ وَهُمْ يُسْلِفُونَ فِي الثِّمَارِ فِي سَنَتَيْنِ وَثَلَاثٍ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أسْلِّفُوا فِي الثِّمَارِ: فِي كَيْلٍ مَعْلُومٍ وَوَزْنٍ مَعْلُومٍ". وَقَدْ كَانَ سُفْيَانُ يَذْكُرُهُ زَمَانًا إِلَى أَجَلٍ مَعْلُومٍ، ثُمَّ شَكَّكَهُ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ كَثِيرٍ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Abiy Najiyh, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Kathiyr, kutoka kwa Abul-Minhaal, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja Madiynah nao wakifanya salaf (kulipa thamani mapema kwa bidhaa itakayotolewa baadaye) katika matunda kwa (muda wa) miaka miwili na mitatu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Fanyeni salaf katika matunda kwa kipimo kinachojulikana na uzito unaojulikana." Na Sufyaan alikuwa akiitaja kwa muda (akiongeza): "mpaka muda unaojulikana"; kisha 'Abdu-Allaah bin Kathiyr akamtia shaka (juu yake).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1682
Hadiyth
2625

46-Mlangoباب: في حسن القضاءMlango Wa Kuhusu Kulipa (Deni) Kwa Uzuri

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُحَارِبٍ، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرًا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "وَزَنَ لَهُ دَرَاهِمَ فَأَرْجَحَهَا"

Ametusimulia Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muhaarib, amesema: Nilimsikia Jaabir (رضي الله عنه) (akisema) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alimpimia dirhamu, akazizidisha uzito."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1683
Hadiyth
2626

47-Mlangoباب: الرجحان في الوزنMlango Wa Kuzidisha Katika Kupima Uzito

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ سُوَيْدِ بْنِ قَيْسٍ، قَالَ: جَلَبْتُ أَنَا وَمَخْرَمَةُ الْعَبْدِيُّ بَزًّا مِنَ الْبَحْرَيْنِ إِلَى مَكَّةَ، فَأَتَانَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَمْشِي، فَسَاوَمَنَا بِسَرَاوِيلَ أَوِ اشْتَرَى مِنَّا سَرَاوِيلَ وَثَمَّ وَزَّانٌ يَزِنُ بِالْأَجْرِ، فَقَالَ لِلْوَزَّانِ: "زِنْ وَأَرْجِحْ". فَلَمَّا ذَهَبَ يَمْشِي، قَالُوا: هَذَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa Suwayd bin Qays (رضي الله عنه), amesema: Mimi na Makhramah Al-'Abdiy (رضي الله عنه) tulileta vitambaa kutoka Al-Bahrayn kwenda Makkah. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatujia akitembea, akatupatanisha bei ya suruali — au: alinunua kwetu suruali —, na hapo palikuwa na mpimaji anayepima uzito kwa ujira. Akamwambia mpimaji: "Pima na uzidishe." Alipoondoka akitembea, (watu) wakasema: Huyu ni Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1684
Hadiyth
2627

48-Mlangoباب: في مطل الغني ظلمMlango Wa Kuhusu Kuchelewesha
Kwa Tajiri (Kulipa Deni) Ni Dhulma

حَدَّثَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: مَطْلُ الْغَنِيِّ ظُلْمٌ، وَإِذَا أُتْبِعَ أَحَدُكُمْ عَلَى مَلِيءٍ فَلْيَتْبَعْ "

Ametusimulia Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kuchelewesha (kulipa deni) kwa tajiri ni dhulma; na mmoja wenu anapohawilishiwa (deni lake) kwa tajiri, basi akubali kuhawilishwa."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1684
Hadiyth
2628

49-Mlangoباب: في إنظار المعسرMlango Wa Kuhusu Kumpa Muhula Mwenye Hali Ngumu

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا يُونُسُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ أَبِيهِ أَنَّهُ تَقَاضَى مِنَ ابْنِ أَبِي حَدْرَدٍ دَيْنًا كَانَ لَهُ عَلَيْهِ فِي الْمَسْجِدِ، فَارْتَفَعَتْ أَصْوَاتُهُمَا حَتَّى سَمِعَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ فِي بَيْتِهِ، فَخَرَجَ إِلَيْهِمَا، فَنَادَى: "يَا كَعْبُ". قَالَ: لَبَّيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ. فَقَالَ: "ضَعْ مِنْ دَيْنِكَ فَأَوْمَأَ إِلَيْهِ أَيْ الشَّطْرَ". قَالَ: قَدْ فَعَلْتُ. قَالَ: "قُمْ فَاقْضِهِ"

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ka'b, kutoka kwa baba yake [Ka'b bin Maalik (رضي الله عنه)], kwamba alimdai Ibn Abiy Hadrad (رضي الله عنه) deni alilokuwa nalo juu yake, Msikitini; sauti zao zikapanda mpaka Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akazisikia naye akiwa nyumbani kwake. Akatoka akawaendea, akaita: "Yaa Ka'b." Akasema: Nimekuitikia, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Punguza katika deni lako" — akamwashiria — yaani: nusu. Akasema: Nimefanya. Akasema: "Simama umlipe."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1685
Hadiyth
2629

50-Mlangoباب: فيمن أنظر معسراMlango Wa Kuhusu Aliyempa Muhula Mwenye Hali Ngumu

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زَائِدَةُ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ رِبْعِيٍّ، عَنْ أَبِي الْيَسَرِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ أَنْظَرَ مُعْسِرًا، أَوْ وَضَعَ عَنْهُ، أَظَلَّهُ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلُّهُ". قَالَ: فَبَزَقَ فِي صَحِيفَتِهِ، فَقَالَ: اذْهَبْ فَهِيَ لَكَ لِغَرِيمِهِ وَذَكَرَ أَنَّهُ كَانَ مُعْسِرًا

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zaaidah, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Rib'iyy, kutoka kwa Abul-Yasar (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayempa muhula mwenye hali ngumu, au akampunguzia (deni), Allaah Atamfunika kivuli katika Kivuli Chake siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa Kivuli Chake." Akasema: Akatemea mate katika karatasi yake (ya deni), akasema — kwa mdaiwa wake —: Nenda, hiyo ni yako. Na akataja kwamba (mdaiwa huyo) alikuwa mwenye hali ngumu.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1686
Hadiyth
2630

حَدَّثَنَا عَفَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو جَعْفَرٍ الْخَطْمِيُّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ كَعْبٍ الْقُرَظِيِّ، عَنْ أَبِي قَتَادَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ نَفَّسَ عَنْ غَرِيمِهِ أَوْ مَحَا عَنْهُ، كَانَ فِي ظِلِّ الْعَرْشِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"

Ametusimulia 'Affaan bin Muslim, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia Abuw Ja'far Al-Khatwmiy, kutoka kwa Muhammad bin Ka'b Al-Quradhwiy, kutoka kwa Abuw Qataadah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayempa nafasi mdaiwa wake, au akamfutia (deni), atakuwa katika kivuli cha 'Arsh (Kiti Cha Enzi) Siku ya Qiyaamah."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1686
Hadiyth
2631

51-Mlangoباب: في المفلس إذا وجد المتاع عندهMlango Wa Kuhusu Aliyefilisika
Inapokutwa Bidhaa (Ya Mtu) Kwake

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى: أَنَّ أَبَا بَكْرِ بْنَ مُحَمَّدٍ، أَخْبَرَهُ أَنَّهُ سَمِعَ عُمَرَ بْنَ عَبْدِ الْعَزِيزِ يُحَدِّثُ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا بَكْرِ بْنَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْحَارِثِ بْنِ هِشَامٍ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أَدْرَكَ مَالَهُ بِعَيْنِهِ عِنْدَ إِنْسَانٍ قَدْ أَفْلَسَ أَوْ عِنْدَ رَجُلٍ قَدْ أَفْلَسَ فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ مِنْ غَيْرِهِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Yahyaa, kwamba Abuw Bakr bin Muhammad alimkhabarisha kwamba alimsikia 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz akisimulia kwamba alimsikia Abuw Bakr bin 'Abdir-Rahmaan bin Al-Haarith bin Hishaam (akisema) kwamba alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeikuta mali yake yenyewe kwa mtu aliyefilisika — au: kwa mwanamume aliyefilisika —, basi yeye ana haki zaidi nayo kuliko mwingine."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1687
Hadiyth
2632

52-Mlangoباب: ما جاء في التشديد في الدينMlango Wa Yaliyopokewa Kuhusu Ukali (Wa Jambo La) Deni

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سَعْدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُمَرَ بْنِ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "نَفْسُ الْمُؤْمِنِ مُعَلَّقَةٌ مَا كَانَ عَلَيْهِ دَيْنٌ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Sa'd bin Ibraahiym, kutoka kwa 'Umar bin Abiy Salamah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Nafsi ya Muumini imetundikwa (imezuiliwa) maadamu ana deni juu yake."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1688
Hadiyth
2633

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ الرَّقَاشِيُّ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ مَعْدَانَ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ ثَوْبَانَ مَوْلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ فَارَقَ الرُّوحُ الْجَسَدَ وَهُوَ بَرِيءٌ مِنْ ثَلَاثٍ، دَخَلَ الْجَنَّةَ: مِنَ الْكِبْرِ، وَالْغُلُولِ، وَالدَّيْنِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Abdi-Allaah Ar-Raqaashiy, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa Ma'daan bin Abiy Twalhah, kutoka kwa Thawbaan (رضي الله عنه), mawlaa (mwachwa huru) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ambaye roho imeachana na mwili (wake) naye yuko mbali na mambo matatu, ataingia Jannah (Pepo): kiburi, na ghuluwl (khiyana katika ngawira), na deni."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1688
Hadiyth
2634

53-Mlangoباب: في الصلاة على من مات وعليه دينMlango Wa Kuhusu Kumswalia Aliyekufa Naye Ana Deni

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، وَأَبُو الْوَلِيدِ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَوْهَبٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي قَتَادَةَ، عَنْ أَبِيهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُتِيَ بِرَجُلٍ لِيُصَلِّيَ عَلَيْهِ، فَقَالَ: "صَلُّوا عَلَى صَاحِبِكُمْ فَإِنَّ عَلَيْهِ دَيْنًا". قَالَ أَبُو قَتَادَةَ: هُوَ عَلَيَّ يَا رَسُولَ اللَّهِ. قَالَ: "بِالْوَفَاءِ؟". قَالَ: "بِالْوَفَاءِ". قَالَ: فَصَلَّى عَلَيْهِ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir na Abul-Waliyd, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Abdi-Allaah bin Mawhab, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Qataadah, kutoka kwa baba yake [Abuw Qataadah (رضي الله عنه)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliletewa (jeneza la) mtu mmoja ili amswalie. Akasema: "Mswalieni mwenzenu; kwani hakika ana deni." Abuw Qataadah (رضي الله عنه) akasema: (Deni) hilo ni juu yangu, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Kwa kulilipa kikamilifu?" Akasema: "Kwa kulilipa kikamilifu." Akasema: Basi akamswalia.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1689
Hadiyth
2635

54-Mlangoباب: في الرخصة في الصلاة عليهMlango Wa Kuhusu Ruhusa Ya Kumswalia (Mwenye Deni)

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ مَا عَلَى الْأَرْضِ مُؤْمِنٌ إِلا وأَنَا أَوْلَى النَّاسِ بِهِ، فَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضَيَاعًا، فَلْأُدْعَ لَهُ، فَأَنَا مَوْلَاهُ، وَمَنْ تَرَكَ مَالًا، فَلِعَصَبَتِهِ مَنْ كَانَ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: ضَيَاعًا: يَعْنِي: عِيَالًا. وَقَالَ: فَلْأُدْعَ لَهُ، يَعْنِي: ادْعُونِي لَهُ أَقْضِ عَنْهُ

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuz-Zinaad, kutoka kwa Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko Mkononi Mwake, hakuna Muumini yeyote juu ya ardhi ila mimi ni mwenye haki zaidi kwake kuliko watu (wote). Basi atakayeacha deni au wategemezi (wasiojiweza), basi niitwe kwa ajili yake, kwani mimi ndiye walii wake; na atakayeacha mali, basi ni ya 'aswabah (warithi wa kiume wa upande wa baba) wake, yeyote yule awaye."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: «ضَيَاعًا» maana yake ni: wategemezi (wa familia). Na akasema: «فَلْأُدْعَ لَهُ» maana yake ni: Niiteni kwa ajili yake nimlipie.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1690
Hadiyth
2636

55-Mlangoباب: في الدائن معانMlango Wa Kuhusu Mwenye Deni Kusaidiwa (Na Allaah)

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ الْمُنْذِرِ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْمَاعِيل بْنِ أَبِي فُدَيْكٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ سُفْيَانَ مَوْلَى الْأَسْلَمِيِّينَ، عَنْ جَعْفَرِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جَعْفَرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ مَعَ الدَّائِنِ حَتَّى يُقْضَى دَيْنُهُ مَا لَمْ يَكُنْ فِيمَا يَكْرَهُ اللَّهُ". قَالَ: وَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ جَعْفَرٍ يَقُولُ لِخَازِنِهِ: اذْهَبْ فَخُذْ لِي بِدَيْنٍ، فَإِنِّي أَكْرَهُ أَنْ أَبِيتَ لَيْلَةً إِلا وَاللَّهُ مَعِي بَعْدَمَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Al-Mundhir Al-Hizaamiy, ametusimulia Muhammad bin Ismaa'iyl bin Abiy Fudayk, ametusimulia Sa'iyd bin Sufyaan, mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Aslamiyyiyn, kutoka kwa Ja'far bin Muhammad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ja'far (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Yuko pamoja na mwenye deni mpaka deni lake lilipwe, maadamu (deni hilo) halikuwa katika yale Anayoyachukia Allaah." Akasema: Na 'Abdu-Allaah bin Ja'far (رضي الله عنهما) alikuwa akimwambia mtunza hazina wake: Nenda ukanichukulie (kitu) kwa deni; kwani mimi nachukia kulala usiku mmoja ila Allaah Yuko pamoja nami, baada ya yale niliyoyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1690
Hadiyth
2637

56-Mlangoباب: في العارية مؤداةMlango Wa Kuhusu Kitu Cha Kuazima Kinarudishwa

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمِنْهَالِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي عَرُوبَةَ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدُبٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَلَى الْيَدِ مَا أَخَذَتْ حَتَّى تُؤَدِّيَهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Minhaal, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Sa'iyd bin Abiy 'Aruwbah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Samurah bin Jundub (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Juu ya mkono ni (dhamana ya) kile ulichokichukua mpaka ukirudishe."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1691
Hadiyth
2638

57-Mlangoباب: في أداء الأمانة واجتناب الخيانةMlango Wa Kuhusu Kutekeleza Amana Na Kujiepusha Na Khiyana

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا طَلْقُ بْنُ غَنَّامٍ، عَنْ شَرِيكٍ، وَقَيْسٍ، عَنْ أَبِي حَصِينٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَدِّ الْأَمَانَةَ إِلَى مَنِ ائْتَمَنَكَ، وَلَا تَخُنْ مَنْ خَانَكَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Twalq bin Ghannaam, kutoka kwa Shariyk na Qays, kutoka kwa Abuw Haswiyn, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Rudisha amana kwa aliyekuaminisha, wala usimfanyie khiyana aliyekufanyia khiyana."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1692
Hadiyth
2639

58-Mlangoباب: من كسر شيئا فعليه مثلهMlango Wa Aliyevunja Kitu, Basi
Juu Yake Ni (Kulipa) Mfano Wake

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: أَهْدَى بَعْضُ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهِ قَصْعَةً فِيهَا ثَرِيدٌ، وَهُوَ فِي بَيْتِ بَعْضِ أَزْوَاجِهِ، فَضَرَبَتْ الْقَصْعَةَ فَانْكَسَرَتْ، فَجَعَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَأْخُذُ الثَّرِيدَ فَيَرُدُّهُ فِي الصَّحْفَةِ وَهُوَ يَقُولُ: "كُلُوا غَارَتْ أُمُّكُمْ". ثُمَّ انْتَظَرَ حَتَّى جَاءَتْ قَصْعَةٌ صَحِيحَةٌ. فَأَخَذَهَا فَأَعْطَاهَا صَاحِبَةَ الْقَصْعَةِ الْمَكْسُورَةِ. قَالَ عَبْد اللَّهِ: نَقُولُ بِهَذَا

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Mmoja wa wake za Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم رضي الله عنها alimletea zawadi ya bakuli lenye thariyd (mkate uliovunjwa katika mchuzi), naye akiwa katika nyumba ya mmoja wa wake zake (رضي الله عنها). (Mke huyo) akalipiga bakuli, likavunjika. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaanza kuchukua ile thariyd na kuirudisha ndani ya bakuli huku akisema: "Kuleni; mama yenu ameona wivu." Kisha akasubiri mpaka likaletwa bakuli zima, akalichukua akampa mwenye lile bakuli lililovunjika.

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Sisi tunasema kwa (Hadiyth) hii.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1692
Hadiyth
2640

59-Mlangoباب: في اللقطةMlango Wa Kuhusu Luqatwah (Kitu Kilichookotwa)

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا. أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ الْوَلِيدِ بْنِ كَثِيرٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ شُعَيْبٍ، عَنْ عَمْرٍو وَعَاصِمٍ ابْنَيْ سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ رَبِيعَةَ الثَّقَفِيِّ: أَنَّ سُفْيَانَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ وَجَدَ عَيْبَةً فَأَتَى بِهَا عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ، فَقَالَ: "عَرِّفْهَا سَنَةً، فَإِنْ عُرِفَتْ، فَذَاكَ، وَإِلَّا فَهِيَ لَكَ، فَلَمْ تُعْرَفْ، فَلَقِيَهُ بِهَا فِي الْعَامِ الْمُقْبِلِ فِي الْمَوْسِمِ فَذَكَرَهَا لَهُ، فَقَالَ عُمَرُ: هِيَ لَكَ، فَإِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَنَا بِذَلِكَ". قَالَ: لَا حَاجَةَ لِي بِهَا. فَقَبَضَهَا عُمَرُ، فَجَعَلَهَا فِي بَيْتِ الْمَالِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Al-Waliyd bin Kathiyr, amesema: Amenisimulia 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa 'Amr na 'Aaswim, wana wawili wa Sufyaan bin 'Abdi-Allaah bin Rabiy'ah Ath-Thaqafiy, kwamba Sufyaan bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه) aliokota mkoba (wa kuwekea nguo), akampelekea 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضوان الله عليه). Akasema: "Utangaze mwaka mmoja; ukijulikana (mwenyewe), basi ni hivyo; la sivyo, ni wako." Haukujulikana. Akakutana naye pamoja nao mwaka uliofuata katika msimu (wa Hajj), akamtajia. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Ni wako; kwani Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituamrisha hivyo." Akasema: Sina haja nao. 'Umar (رضي الله عنه) akauchukua, akauweka katika Baytul-Maal (hazina ya mali ya Waislamu).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1693
Hadiyth
2641

60-Mlangoباب: في النهي عن لقطة الحاجMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya (Kuokota)
Luqatwah (Kitu Kilichookotwa) Ya Mwenye Kuhiji

أَخْبَرَنَا مُعَاذُ بْنُ هَانِئٍ مِنْ أَهْلِ الْبَصْرَةِ، حَدَّثَنَا حَرْبُ بْنُ شَدَّادٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا أَبُو سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ أَنَّهُ عَامَ فُتِحَتْ مَكَّةُ، قَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "إِنَّ اللَّهَ حَبَسَ عَنْ مَكَّةَ الْفِيلَ، وَسَلَّطَ عَلَيْهِمْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَالْمُؤْمِنِينَ، أَلَا وَإِنَّهَا لَمْ تَحِلَّ لِأَحَدٍ قَبْلِي وَلَا تَحِلُّ لِأَحَدٍ بَعْدِي، أَلَا وَإِنَّهَا سَاعَتِي هَذِهِ حَرَامٌ لَا يُخْتَلَى خَلَاهَا، وَلَا يُعْضَدُ شَجَرُهَا وَلَا تُلْتَقَطُ سَاقِطَتُهَا إِلَّا لِمُنْشِدٍ"

Ametukhabarisha Mu'aadh bin Haaniy, miongoni mwa watu wa Al-Baswrah, ametusimulia Harb bin Shaddaad, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Kathiyr, ametusimulia Abuw Salamah, ametusimulia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba mwaka ambao Makkah ilifunguliwa, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama, akasema: "Hakika Allaah Aliizuilia Makkah tembo, na Akawasalitisha juu yao Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na Waumini. Tanabahini! Na hakika (Makkah) haikuwa halaal kwa yeyote kabla yangu, wala haitakuwa halaal kwa yeyote baada yangu. Tanabahini! Na hakika hiyo, katika saa yangu hii, ni haraam: majani yake mabichi hayakatwi, wala miti yake haikatwi, wala kitu chake kilichoanguka hakiokotwi isipokuwa na mwenye kukitangaza."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1694
Hadiyth
2642

61-Mlangoباب: في الضالةMlango Wa Kuhusu Mnyama Aliyepotea

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الشِّخِّيرِ، عَنْ أَبِي مُسْلِمٍ، عَنِ الْجَارُودِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ضَالَّةُ الْمُسْلِمِ حَرَقُ النَّارِ"

Ametusimulia Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Yaziyd bin 'Abdi-Allaah bin Ash-Shikhkhiyr, kutoka kwa Abuw Muslim, kutoka kwa Al-Jaaruwd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mnyama aliyepotea wa Muislamu ni mwako wa moto."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1695
Hadiyth
2643

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ أَبِي الْعَلَاءِ، عَنْ أَبِي مُسْلِمٍ الْجَذَمِيِّ، عَنِ الْجَارُودِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ضَالَّةُ الْمُسْلِمِ حَرَقُ النَّارِ، ضَالَّةُ الْمُسْلِمِ حَرَقُ النَّارِ، ضَالَّةُ الْمُسْلِمِ حَرَقُ النَّارِ، لَا تَقْرَبَنَّهَا". قَالَ: فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، اللُّقَطَةُ نَجِدُهَا؟. قَالَ: "أَنْشِدْهَا، وَلَا تَكْتُمْ، وَلَا تُغَيِّبْ، وَإِنْ جَاءَ رَبُّهَا، فَادْفَعْهَا إِلَيْهِ، وَإِلَّا، فَمَالُ اللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Jurayriy, kutoka kwa Abul-'Alaa, kutoka kwa Abuw Muslim Al-Jadhamiy, kutoka kwa Al-Jaaruwd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mnyama aliyepotea wa Muislamu ni mwako wa moto; mnyama aliyepotea wa Muislamu ni mwako wa moto; mnyama aliyepotea wa Muislamu ni mwako wa moto; msimkaribie kabisa." Akasema: Mtu mmoja akasema: Yaa Rasula-Allaah, (vipi) luqatwah (kitu kilichookotwa) tunachokikuta? Akasema: "Kitangaze, wala usikifiche, wala usikitoweshe; na akija mwenyewe, basi mpe; la sivyo, basi ni mali ya Allaah, Anampa Amtakaye."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1695
Hadiyth
2644

62-Mlangoباب: فيمن اقتطع مال امرئ مسلم بيمينهMlango Wa Kuhusu Aliyekata (Akanyakua)
Mali Ya Mtu Muislamu Kwa Kiapo Chake

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ يَعْقُوبَ الْكُوفِيُّ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ جَعْفَرٍ، عَنْ الْعَلَاءِ، عَنْ مَعْبَدِ بْنِ كَعْبٍ السَّلَمِيِّ، عَنْ أَخِيهِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ أَبِي أُمَامَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنِ اقْتَطَعَ حَقَّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ بِيَمِينِهِ، فَقَدْ أَوْجَبَ اللَّهُ لَهُ النَّارَ، وَحَرَّمَ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ"، فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: وَإِنْ كَانَ شَيْئًا يَسِيرًا يَا رَسُولَ اللَّهِ؟. قَالَ: "وَإِنْ قَضِيبًا مِنْ أَرَاكٍ".

Ametukhabarisha Ahmad bin Ya'quwb Al-Kuwfiy, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Ja'far, kutoka kwa Al-'Alaa, kutoka kwa Ma'bad bin Ka'b As-Salamiy, kutoka kwa ndugu yake 'Abdu-Allaah bin Ka'b, kutoka kwa Abuw Umaamah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayekata haki ya mtu Muislamu kwa kiapo chake, basi Allaah Amemwajibishia moto, na Amemharamishia Jannah (Pepo)." Mtu mmoja akamwambia: Hata kama ni kitu kidogo, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Hata kama ni kijiti cha (mti wa) araak."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1696
Hadiyth
2645

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ الْوَلِيدِ بْنِ كَثِيرٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّهُ سَمِعَ أَخَاهُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ يُحَدِّثُ: أَنَّ أَبَا أُمَامَةَ الْحَارِثِيَّ حَدَّثَهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ......... فَذَكَرَ نَحْوَهُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Al-Waliyd bin Kathiyr, kutoka kwa Muhammad bin Ka'b bin Maalik, kwamba alimsikia ndugu yake 'Abdu-Allaah bin Ka'b bin Maalik akisimulia kwamba Abuw Umaamah Al-Haarithiy (رضي الله عنه) alimsimulia kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) … akataja mfano wake.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1697
Hadiyth
2646

63-Mlangoباب: في اليمين الكاذبةMlango Wa Kuhusu Kiapo Cha Uongo

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، وَحَجَّاجٌ، قَالَا: ثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: حَدَّثَنِي عَلِيُّ بْنُ مُدْرِكٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا زُرْعَةَ يُحَدِّثُ، عَنْ خَرَشَةَ بْنِ الْحُرِّ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "ثَلَاثَةٌ لَا يُكَلِّمُهُمْ اللَّهُ، وَلَا يَنْظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ"، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ مَنْ هُمْ خَابُوا وَخَسِرُوا؟ فَأَعَادَهَا، فَقُلْتُ: مَنْ هُمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟، فَقَالَ: "الْمُسْبِلُ، وَالْمَنَّانُ، وَالْمُنَفِّقُ سِلْعَتَهُ بِالْحَلِفِ كَاذِبًا"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd na Hajjaaj, wamesema: Ametusimulia Shu'bah, amesema: Amenisimulia 'Aliy bin Mudrik, amesema: Nilimsikia Abuw Zur'ah akisimulia, kutoka kwa Kharashah bin Al-Hurr, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Watu watatu, Allaah Hatowasemesha, wala Hatowatazama Siku ya Qiyaamah, wala Hatowatakasa, na watapata adhabu iumizayo." Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, ni akina nani hao? Wamepita patupu na wamekhasirika! Akayarudia (maneno hayo). Nikasema: Ni akina nani hao, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Anayeburuza (izari yake), na anayesimbulia (alichotoa), na anayeuza bidhaa yake kwa kiapo cha uongo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1698
Hadiyth
2647

64-Mlangoباب: من أخذ شبرا من الأرضMlango Wa Aliyechukua Shibiri Ya Ardhi

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، حَدَّثَنِي طَلْحَةُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَوْفٍ: أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ سَهْلٍ أَخْبَرَهُ أَنَّ سَعِيدَ بْنَ زَيْدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ ظَلَمَ مِنَ الْأَرْضِ شِبْرًا، فَإِنَّهُ يُطَوَّقُهُ مِنْ سَبْعِ أَرَضِينَ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenisimulia Twalhah bin 'Abdi-Allaah bin 'Awf, kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Sahl alimkhabarisha kwamba Sa'iyd bin Zayd (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayedhulumu shibiri ya ardhi, basi hakika atafungwa nayo shingoni (kama kongwa) kutoka ardhi saba."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1699
Hadiyth
2648

65-Mlangoباب: من أحيا أرضا ميتة فهي لهMlango Wa Aliyehuisha Ardhi Iliyokufa Basi Ni Yake

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ هِشَامِ بْنِ عُرْوَةَ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ رَافِعٍ: أَنَّ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ أَخْبَرَهُ: أَنَّ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ أَحْيَا أَرْضًا مَيْتَةً فَلَهُ فِيهَا أَجْرٌ وَمَا أَكَلَتِ الْعَافِيَةُ مِنْهَا، فَلَهُ فِيهَا صَدَقَةٌ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: الْعَافِيَةُ: الطَّيْرُ وَغَيْرُ ذَلِكَ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Hishaam bin 'Urwah, amesema: Amenikhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Raafi', kwamba Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) alimkhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayehuisha ardhi iliyokufa, basi atapata ndani yake ujira; na kile watakachokula al-'aafiyah (wanaotafuta riziki) kutoka humo, basi atapata ndani yake swadaka."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Al-'aafiyah ni ndege na wasiokuwa hao.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1700
Hadiyth
2649

66-Mlangoباب: في القطائعMlango Wa Kuhusu Ugawaji Wa Ardhi

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ الْحُمَيْدِيُّ، حَدَّثَنَا الْفَرَجُ بْنُ سَعِيدِ بْنِ عَلْقَمَةَ بْنِ سَعِيدِ بْنِ أَبْيَضَ بْنِ حَمَّالٍ السَّبَائِيُّ الْمَأْرِبِيُّ، حَدَّثَنِي عَمِّي ثَابِتُ بْنُ سَعِيدِ بْنِ أَبْيَضَ: أَنَّ أَبَاهُ سَعِيدَ بْنَ أَبْيَضَ حَدَّثَهُ، عَنْ أَبْيَضَ بْنِ حَمَّالٍ حَدَّثَهُ: أَنَّهُ اسْتَقْطَعَ الْمِلْحَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّذِي يُقَالُ لَهُ مِلْحُ سَدِّ مَأْرِبَ فَأَقْطَعَهُ، ثُمَّ إِنَّ الْأَقْرَعَ بْنَ حَابِسٍ التَّمِيمِيَّ. قَالَ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي قَدْ وَرَدْتُ الْمِلْحَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ، وَهُوَ بِأَرْضٍ لَيْسَ بِهَا مَاءٌ، وَمَنْ وَرَدَهُ، أَخَذَهُ، وَهُوَ مِثْلُ مَاءِ الْعِدِّ. فَاسْتَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْأَبْيَضَ فِي قَطِيعَتِهِ فِي الْمِلْحِ، فَقُلْتُ: قَدْ أَقَلْتُهُ عَلَى أَنْ تَجْعَلَهُ مِنِّي صَدَقَةً، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هُوَ مِنْكَ صَدَقَةٌ، وَهُوَ مِثْلُ مَاءِ الْعِدِّ، مَنْ وَرَدَهُ، أَخَذَهُ". قَالَ: وَقَطَعَ لَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَرْضًا وَنَخْلًا كَذَا بِالْجَوْفِ: جَوْفِ مُرَادٍ مَكَانَهُ حِينَ أَقَالَهُ مِنْهُ. قَالَ الْفَرَجُ: فَهُوَ عَلَى ذَلِكَ: مَنْ وَرَدَهُ، أَخَذَهُ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Az-Zubayr Al-Humaydiy, ametusimulia Al-Faraj bin Sa'iyd bin 'Alqamah bin Sa'iyd bin Abyadhw bin Hammaal As-Sabaaiy Al-Maaribiy, amenisimulia ami yangu Thaabit bin Sa'iyd bin Abyadhw, kwamba baba yake Sa'iyd bin Abyadhw alimsimulia, kutoka kwa Abyadhw bin Hammaal (رضي الله عنه) — alimsimulia —: Kwamba yeye alimwomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amgawie (machimbo ya) chumvi ambayo huitwa chumvi ya Bwawa la Maarib (mji wa Yemen), akamgawia. Kisha Al-Aqra' bin Haabis At-Tamiymiy (رضي الله عنه) akasema: Yaa Nabiyya-Allaah, hakika mimi nilikwenda kwenye (machimbo ya) chumvi hiyo katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam), nayo iko katika ardhi isiyokuwa na maji; na anayeiendea huichukua; nayo ni kama maji ya chemchemi yasiyokatika. Basi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwomba Al-Abyadhw (رضي الله عنه) amwachilie ugawaji wake wa (machimbo ya) chumvi. Nikasema: Nimekuachilia, kwa sharti kwamba uifanye kuwa swadaka kutoka kwangu. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hiyo ni swadaka kutoka kwako, nayo ni kama maji ya chemchemi yasiyokatika; anayeiendea huichukua." Akasema: Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamgawia ardhi na mitende (kiasi) kadhaa huko Al-Jawf: Jawf Muraad (bonde la kabila la Muraad), badala yake alipomwachilia (chumvi hiyo). Al-Faraj amesema: Basi (chumvi hiyo) iko hivyo: anayeiendea huichukua.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1700
Hadiyth
2650

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا غُنْدَرٌ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ وَائِلٍ، عَنْ أَبِيهِ "أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقْطَعَهُ أَرْضًا". قَالَ: فَأَرْسَلَ مَعِي مُعَاوِيَةَ. قَالَ: أَعْطِهَا إِيَّاهُ. قَالَ يَحْيَى: حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ بَشَّارٍ، حَدَّثَنَا غُنْدَرٌ، بِهَذَا الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Bashshaar, ametusimulia Ghundar, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa 'Alqamah bin Waail, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimgawia ardhi. Akasema [Waail (رضي الله عنه)]: (Rasuli) akamtuma Mu'aawiyah (رضي الله عنه) pamoja nami. Akasema (kumwambia Mu'aawiyah): "Mpe (ardhi) hiyo."

Yahyaa amesema: Ametusimulia Muhammad bin Bashshaar, ametusimulia Ghundar, kwa Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1702
Hadiyth
2651

67-Mlangoباب: في فضل الغرسMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Kupanda Miti

أَخْبَرَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ بْنُ زِيَادٍ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ الْأَعْمَشُ، حَدَّثَنَا أَبُو سُفْيَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، يَقُولُ: حَدَّثَتْنِي أُمُّ مُبَشِّرٍ امْرَأَةُ زَيْدِ بْنِ حَارِثَةَ، قَالَتْ: دَخَلَ عَلَيَّ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَائِطٍ لِي، فَقَالَ: "يَا أُمَّ مُبَشِّرٍ، أَمُسْلِمٌ غَرَسَ هَذَا، أَمْ كَافِرٌ؟". قُلْتُ: مُسْلِمٌ، فَقَالَ: "مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَغْرِسُ غَرْسًا فَيَأْكُلُ مِنْهُ إِنْسَانٌ، أَوْ دَابَّةٌ، أَوْ طَيْرٌ، إِلَّا كَانَتْ لَهُ صَدَقَةٌ"

Ametukhabarisha Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia 'Abdul-Waahid bin Ziyaad, ametusimulia Sulaymaan Al-A'mash, ametusimulia Abuw Sufyaan, amesema: Nilimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) akisema: Amenisimulia Ummu Mubashshir (رضي الله عنها), mke wa Zayd bin Haarithah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniingilia katika bustani yangu (iliyozungushiwa ukuta), akasema: "Yaa Umma Mubashshir, je, aliyepanda (mimea) hii ni Muislamu au ni kafiri?" Nikasema: Muislamu. Akasema: "Hakuna Muislamu yeyote anayepanda mmea, kisha akala kutokana nao binaadam, au mnyama, au ndege, isipokuwa (hilo) litakuwa ni swadaka kwake."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1703
Hadiyth
2652

68-Mlangoباب: في الحمىMlango Wa Kuhusu Himaa (Malisho Yaliyohifadhiwa)

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الزُّبَيْرِ، حَدَّثَنَا الْفَرَجُ بْنُ سَعِيدٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عَمِّي ثَابِتُ بْنُ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِيهِ سَعِيدٍ، عَنْ جَدِّهِ أَبْيَضَ بْنِ حَمَّالٍ: أَنَّهُ سَأَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ حِمَى الْأَرَاكِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا حِمَى فِي الْأَرَاكِ"، فَقَالَ: أَرَاكَةٌ فِي حِظَارِي؟، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا حِمَى فِي الْأَرَاكِ". قَالَ فَرَجٌ: يَعْنِي أَبْيَضُ: بِحِظَارِي: الْأَرْضَ الَّتِي فِيهَا الزَّرْعُ الْمُحَاطُ عَلَيْهَا

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Az-Zubayr, ametusimulia Al-Faraj bin Sa'iyd, amesema: Amenikhabarisha ami yangu Thaabit bin Sa'iyd, kutoka kwa baba yake Sa'iyd, kutoka kwa babu yake Abyadhw bin Hammaal (رضي الله عنه), kwamba alimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu himaa (malisho yaliyohifadhiwa) ya araak (mti wa miswaki). Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakuna himaa katika araak." Akasema: (Hata) mti wa araak ulio ndani ya uzio wangu? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Hakuna himaa katika araak." Faraj amesema: Anakusudia Abyadhw (رضي الله عنه) kwa «بِحِظَارِي» (ndani ya uzio wangu): ardhi ambayo ndani yake kuna mimea iliyozungushiwa uzio.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1704
Hadiyth
2653

69-Mlangoباب: في النهي عن بيع الماءMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Maji

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا ابْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ أَبِي الْمِنْهَالِ، قَالَ: سَمِعْتُ إِيَاسَ بْنَ عَبْدٍ الْمُزَنِيَّ وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: لَا تَبِيعُوا الْمَاءَ: فَإِنِّي سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "يَنْهَى عَنْ بَيْعِ الْمَاءِ". وَقَالَ عَمْرُو بْنُ دِينَارٍ: لَا نَدْرِي أَيَّ مَاءٍ. قَالَ: يَقُولُ: لَا أَدْرِي مَاءً جَارِيًا أَوِ الْمَاءَ الْمُسْتَقَى؟

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Ibn 'Uyaynah, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Abul-Minhaal, amesema: Nilimsikia Iyaas bin 'Abd Al-Muzaniy (رضي الله عنه) — naye alikuwa miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) — akisema: Msiuze maji, kwani hakika mimi nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akikataza kuuza maji. Na 'Amr bin Diynaar amesema: Hatujui ni maji gani. Amesema: Anasema: Sijui (kama ni) maji yanayotiririka au maji yanayotekwa?

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1704
Hadiyth
2654

70-Mlangoباب: في الذي لا يحل منعهMlango Wa Kuhusu Kile Ambacho Si Halaal Kukizuia

حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا كَهْمَسٌ، عَنْ سَيَّارٍ رَجُلٍ مِنْ فَزَارَةَ عَنْ أَبِيهِ، عَنْ بُهَيْسَةَ، عَنْ أَبِيهَا، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّهُ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَاسْتَأْذَنَهُ فَدَخَلَ بَيْنَهُ وَبَيْنَ قَمِيصِهِ وَقَدْ قَالَ عُثْمَانُ: فَالْتَزَمَهُ، فَقَالَ: مَا الشَّيْءُ الَّذِي لَا يَحِلُّ مَنْعُهُ؟، فَقَالَ: "الْمِلْحُ وَالْمَاءُ"، قَالَ: مَا الشَّيْءُ الَّذِي لَا يَحِلُّ مَنْعُهُ؟. قَالَ: "أَنْ تَفْعَلَ الْخَيْرَ خَيْرٌ لَكَ". قَالَ: مَا الشَّيْءُ الَّذِي لَا يَحِلُّ مَنْعُهُ؟. قَالَ: "إِنْ تَفْعَلْ الْخَيْرَ خَيْرٌ لَكَ" وَانْتَهَى إِلَى الْمِلْحِ وَالْمَاءِ. قِيلَ لِعَبْدِ اللَّهِ: تَقُولُ بِهِ؟ فَأَوْمَأَ بِرَأْسِهِ

Ametusimulia 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Kahmas, kutoka kwa Sayyaar — mtu mmoja wa (kabila la) Fazaarah —, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Buhaysah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Kwamba yeye alimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akamwomba idhini, akaingia baina yake na kanzu yake — na 'Uthmaan amesema: Akamkumbatia —, kisha akasema: Ni kitu gani ambacho si halaal kukizuia? Akasema: "Chumvi na maji." Akasema: Ni kitu gani ambacho si halaal kukizuia? Akasema: "Kufanya kheri ni bora kwako." Akasema: Ni kitu gani ambacho si halaal kukizuia? Akasema: "Kufanya kheri ni bora kwako." Na (jibu lake) likaishia kwenye chumvi na maji.

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unasema hivyo? Akaashiria kwa kichwa chake.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1705
Hadiyth
2655

71-Mlangoباب: إن النبي صلى الله عليه وسلم عامل خيبرMlango Wa Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Aliingia Mkataba Wa Kilimo Na Khaybar

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنِي نَافِعٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "عَامَلَ خَيْبَرَ بِشَطْرِ مَا يَخْرُجُ مِنْهَا مِنْ ثَمَرَةٍ أَوْ زَرْعٍ"

Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, amenisimulia Naafi', kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin 'Umar] (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliingia mkataba (wa kilimo) na (watu wa) Khaybar kwa nusu ya kinachotoka humo katika matunda au mazao (ya nafaka).

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1706
Hadiyth
2656

72-Mlangoباب: في النهي عن المخابرةMlango Wa Kuhusu Katazo La Mukhaabarah (Kukodisha Ardhi
Kwa Sehemu Ya Mazao Yake)

أَخْبَرَنَا أَبُو الْحَسَنِ، عَنْ زَكَرِيَّا بْنِ إِسْحَقَ، حَدَّثَنَا أَبُو الزُّبَيْرِ: أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرًا يَقُولُ: كُنَّا نُخَابِرُ قَبْلَ أَنْ يَنْهَانَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْخِبْرِ بَسَنَتَيْنِ أَوْ ثَلَاثٍ، عَلَى الثُّلُثِ، وَالشَّطْرِ، وَشَيْءٍ مِنْ تِبْنٍ، فَقَالَ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ كَانَتْ لَهُ أَرْضٌ فَلْيَحْرُثْهَا، فَإِنْ كَرِهَ أَنْ يَحْرُثَهَا، فَلْيَمْنَحْهَا أَخَاهُ، فَإِنْ كَرِهَ أَنْ يَمْنَحَهَا أَخَاهُ، فَلْيَدَعْهَا"

Ametukhabarisha Abul-Hasan, kutoka kwa Zakariyyaa bin Is-haaq, ametusimulia Abuz-Zubayr, kwamba alimsikia Jaabir (رضي الله عنه) akisema: Tulikuwa tukifanya mukhaabarah (kukodisha ardhi kwa sehemu ya mazao yake) — miaka miwili au mitatu kabla Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) hajatukataza al-khibr (mukhaabarah) — kwa theluthi, na nusu, na kitu katika makapi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatuambia: "Mwenye ardhi, basi aipande; na akichukia kuipanda, basi ampe nduguye (aitumie bure); na akichukia kumpa nduguye, basi aiache."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1707
Hadiyth
2657

73-Mlangoباب: في النهي عن المزارعة في الثلث والربعMlango Wa Kuhusu Katazo La Muzaara'ah (Kupanda
Kwa Ushirika Wa Mazao) Kwa Theluthi Na Robo

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَقَ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ السَّائِبِ، قَالَ: سَأَلْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مَعْقِلٍ عَنِ الْمُزَارَعَةِ، فَقَالَ: أَخْبَرَنِي ثَابِتُ بْنُ الضَّحَّاكِ الْأَنْصَارِيُّ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى عَنِ الْمُزَارَعَةِ". قَالَ لِعَبْدِ اللَّهِ: تَقُولُ بِهِ؟. قَالَ: لَا أَقُولُ بِالْأَوَّلِ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Abuw Is-haaq Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin As-Saaib, amesema: Nilimuuliza 'Abdu-Allaah bin Ma'qil kuhusu muzaara'ah (kupanda kwa ushirika wa mazao). Akasema: Amenikhabarisha Thaabit bin Adh-Dhwahhaak Al-Answaariy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza muzaara'ah.

(Mtu) alimwambia 'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy]: Je, unasema hivyo? Akasema: Sisemi kwa (hukmu) ya kwanza.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1708
Hadiyth
2658

74-Mlangoباب: في النهي عن بيع الأرض سنينMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuuza Ardhi Kwa Miaka

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْأَرْضِ الْبَيْضَاءِ سَنَتَيْنِ أَوُ ثَلَاثًا"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuuza (mazao ya) ardhi tupu kwa miaka miwili au mitatu.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1709
Hadiyth
2659

75-Mlangoباب: في الرخصة في كراء الأرض بالذهب والفضةMlango Wa Kuhusu Ruhusa Ya Kukodisha Ardhi
Kwa Dhahabu Na Fedha

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عِكْرِمَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْحَارِثِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَبِيبَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، قَالَ: كُنَّا نُكْرِي الْأَرْضَ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمَا عَلَى السَّوَاقِي مِنَ الزَّرْعِ، وَبِمَا سَعِدَ مِنَ الْمَاءِ مِنْهَا، "فَنَهَانَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَلِكَ، وَأَذِنَ لَنَا أَوْ قَالَ رَخَّصَ لَنَا فِي أَنْ نُكْرِيَهَا بِالذَّهَبِ وَالْوَرِقِ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ibraahiym bin Sa'd, kutoka kwa Muhammad bin 'Ikrimah bin 'Abdir-Rahmaan bin Al-Haarith bin Hishaam, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Abiy Labiybah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Sa'd bin Abiy Waqqaasw (رضي الله عنه), amesema: Tulikuwa tukikodisha ardhi katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa (mazao) yaliyo kwenye mifereji ya kumwagilia, na kwa yale yaliyonufaika na maji katika (ardhi) hiyo. Basi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akatukataza hilo, na akatupa idhini — au alisema: akaturuhusu — kwamba tuikodishe kwa dhahabu na fedha.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1709
Hadiyth
2660

76-Mlangoباب: في الخرصMlango Wa Kuhusu Kukadiria Mazao Kwa Makisio

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ خُبَيْبِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَسْعُودِ بْنِ نِيَارٍ الْأَنْصَارِيِّ، قَالَ: جَاءَ سَهْلُ بْنُ أَبِي حَثْمَةَ إِلَى مَجْلِسِنَا فَحَدَّثَ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِذَا خَرَصْتُمْ، فَخُذُوا وَدَعُوا، دَعُوا الثُّلُثَ، فَإِنْ لَمْ تَدَعُوا الثُّلُثَ، فَدَعُوا الرُّبُعَ"

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Khubayb bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Mas'uwd bin Niyaar Al-Answaariy, amesema: Sahl bin Abiy Hathmah (رضي الله عنه) alikuja katika kikao chetu, akasimulia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mnapokadiria (mazao kwa makisio), basi chukueni na muache; acheni theluthi; na msipoacha theluthi, basi acheni robo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1710
Hadiyth
2661

77-Mlangoباب: في النهي عن كسب الأمةMlango Wa Kuhusu Katazo La Mapato Ya Mjakazi

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جُحَادَةَ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ كَسْبِ الْإِمَاءِ"

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Muhammad bin Juhaadah, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mapato ya wajakazi.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1710
Hadiyth
2662

78-Mlangoباب: في النهي عن كسب الحجامMlango Wa Kuhusu Katazo La Mapato Ya Mwumikaji

أَخْبَرَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ قَارِظٍ: أَنَّ السَّائِبَ بْنَ يَزِيدَ حَدَّثَهُ: أَنَّ رَافِعَ بْنَ خَدِيجٍ حَدَّثَهُ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "كَسْبُ الْحَجَّامِ خَبِيثٌ، وَمَهْرُ الْبَغِيِّ خَبِيثٌ، وَثَمَنُ الْكَلْبِ خَبِيثٌ"

Ametukhabarisha Wahb bin Jariyr, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Ibraahiym bin 'Abdi-Allaah bin Qaaridhw, kwamba As-Saaib bin Yaziyd (رضي الله عنه) alimsimulia kwamba Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه) alimsimulia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mapato ya mwumikaji ni machafu, na mahari ya mwanamke mzinifu ni machafu, na thamani ya mbwa ni chafu."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1711
Hadiyth
2663

79-Mlangoباب: في الرخصة في كسب الحجامMlango Wa Kuhusu Ruhusa Ya Mapato Ya Mwumikaji

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا حُمَيْدٌ الطَّوِيلُ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "حَجَمَهُ أَبُو طَيْبَةَ وَأَمَرَ لَهُ بِصَاعَيْنِ مِنْ طَعَامٍ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Humayd Atw-Twawiyl, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Abuw Twaybah (رضي الله عنه) alimuumika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), naye (Rasuli) akaamrisha apewe pishi mbili za chakula.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1711
Hadiyth
2664

80-Mlangoباب: في النهي عن عسب الفحلMlango Wa Kuhusu Katazo La (Ujira Wa) Kupandisha Dume

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ فُضَيْلٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ثَمَنِ عَسْبِ الْفَحْلِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Ibn Fudhwayl, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza thamani ya kupandisha dume.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1712
Hadiyth
2665

أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا الْقَاسِمُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنْ الْمَهْرِيِّ، قَالَ: قَالَ أَبُو هُرَيْرَةَ "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ عَسْبِ الْفَحْلِ، وَأَجْرِ الْمُومِسَةِ"

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Al-Qaasim bin Al-Fadhwl, ametusimulia baba yangu, kutoka kwa Al-Mahriy, amesema: Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza (ujira wa) kupandisha dume, na ujira wa mwanamke mzinifu.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1712
Hadiyth
2666

81-Mlangoباب: فيمن باع دارا فلم يجعل ثمنها في مثلهاMlango Wa Kuhusu Aliyeuza Nyumba
Na Asiiweke Thamani Yake Katika Mfano Wake

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل هُوَ: ابْنُ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مُهَاجِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ الْمَلِكِ بْنَ عُمَيْرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَمْرَو بْنَ حُرَيْثٍ، عَنْ أَخِيهِ سَعِيدِ بْنِ حُرَيْثٍ وَكَانَتْ لَهُ صُحْبَةٌ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ بَاعَ مِنْكُمْ دَارًا أَوْ عَقَارًا، فَإِنَّهُ قَمِنٌ أَنْ لَا يُبَارَكَ لَهُ إِلَّا أَنْ يَجْعَلَهُ فِي مِثْلِهِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Ismaa'iyl — naye ni Ibn Ibraahiym bin Muhaajir —, amesema: Nilimsikia 'Abdul-Malik bin 'Umayr, amesema: Nilimsikia 'Amr bin Hurayth (رضي الله عنه), kutoka kwa ndugu yake Sa'iyd bin Hurayth (رضي الله عنه) — naye alikuwa Swahaba —, amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayeuza miongoni mwenu nyumba au ardhi, basi hakika yeye anastahiki kutobarikiwa (katika thamani yake), isipokuwa aiweke katika mfano wake."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1713
Hadiyth
2667

82-Mlangoباب: في حريم البئرMlango Wa Kuhusu Eneo Lililohifadhiwa La Kisima

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ إِبْرَاهِيمَ، أَنْبَأَنَا عَرْعَرَةُ بْنُ الْبِرِنْدِ السَّامِيُّ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنِ احْتَفَرَ بِئْرًا، فَلَيْسَ لِأَحَدٍ أَنْ يَحْفِرَ حَوْلَهُ أَرْبَعِينَ ذِرَاعًا عَطَنًا لِمَاشِيَتِهِ"

Ametukhabarisha Is-haaq bin Ibraahiym, ametupa khabari 'Ar'arah bin Al-Birind As-Saamiy, ametusimulia Ismaa'iyl bin Muslim, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayechimba kisima, basi hakuna yeyote mwenye haki ya kuchimba kukizunguka (umbali wa) dhiraa arobaini, (ziwe) mahali pa kupumzikia wanyama wake (baada ya kunywa)."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1714
Hadiyth
2668

83-Mlangoباب: في الشفعةMlango Wa Kuhusu Shuf'ah (Haki Ya Mshirika
Au Jirani Kutangulia Kununua)

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ جَابِرٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الشُّفْعَةِ إِذَا كَانَ طَرِيقُهُمَا وَاحِدًا؟. قَالَ: "يُنْظَرُ بِهَا، وَإِنْ كَانَ صَاحِبُهَا غَائِبًا"

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kuhusu shuf'ah (haki ya mshirika au jirani kutangulia kununua) ikiwa njia yao wawili ni moja? Akasema: "(Mwenye haki ya shuf'ah) atangojewa kwayo, hata kama mwenyewe hayupo."

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1714
Hadiyth
2669

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "قَضَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِالشُّفْعَةِ فِي كُلِّ شِرْكٍ لَمْ يُقْسَمْ: رَبْعَةٍ أَوْ حَائِطٍ لَا يَحِلُّ لَهُ أَنْ يَبِيعَ حَتَّى يُؤْذِنَ شَرِيكَهُ، فَإِنْ شَاءَ، أَخَذَ، وَإِنْ شَاءَ، تَرَكَ، فَإِنْ بَاعَ وَلَمْ يُؤْذِنْهُ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ". قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: تَقُولُ بِهَذَا؟. قَالَ: نَعَمْ

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Idriys, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu (kuwepo) shuf'ah (haki ya mshirika au jirani kutangulia kununua) katika kila (mali ya) ushirika ambayo haijagawanywa: nyumba au bustani (iliyozungushiwa ukuta). Si halaal kwake kuiuza mpaka amjulishe mshirika wake; akitaka, ataichukua, na akitaka, ataiacha. Na akiiuza bila kumjulisha, basi yeye (mshirika) ana haki zaidi nayo.

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, unasema kwa (kauli) hii? Akasema: Ndiyo.

Mjalada
3
Kitabu
18
Ukurasa
1715
Hadiyth
2670