Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy19 - Kitabu Cha Kuomba Idhini

ومن كتاب الاستئذان

1-Mlangoباب: الاستئذان ثلاثMlango Wa Kuomba Idhini Ni Mara Tatu

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا دَاوُدُ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ: أَنَّ أَبَا مُوسَى الْأَشْعَرِيَّ اسْتَأْذَنَ عَلَى عُمَرَ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَلَمْ يُؤْذَنْ لَهُ، فَرَجَعَ، فَقَالَ: مَا رَجَعَكَ؟ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِذَا اسْتَأْذَنَ الْمُسْتَأْذِنُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ: فَإِنْ أُذِنَ لَهُ وَإِلَّا، فَلْيَرْجِعْ"، فَقَالَ: لَتَأْتِيَنَّ بِمَنْ يَشْهَدُ مَعَكَ، أَوْ لَأَفْعَلَنَّ، وَلَأَفْعَلَنَّ. قَالَ أَبُو سَعِيدٍ: وَأَتَانَا وَأَنَا فِي قَوْمٍ مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي الْمَسْجِدِ، وَهُوَ فَزِعٌ مِنْ وَعِيدِ عُمَرَ إِيَّاهُ، فَقَامَ عَلَيْنَا، فَقَالَ: أَنْشُدُ اللَّهَ مِنْكُمْ رَجُلًا سَمِعَ ذَلِكَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا شَهِدَ لِي بِهِ. قَالَ: فَرَفَعْتُ رَأْسِي، فَقُلْتُ: أَخْبِرْهُ أَنِّي مَعَكَ عَلَى هَذَا. وَقَالَ ذَاكَ آخَرُونَ، فَسُرِّيَ عَنْ أَبِي مُوسَى

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Daawuwd, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه): Kwamba Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه) aliomba idhini (ya kuingia) kwa 'Umar (رضوان الله عليه) mara tatu, na hakupewa idhini, akarudi. ('Umar) akasema: Nini kilichokurudisha? Akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mwenye kuomba idhini akiomba idhini mara tatu: akipewa idhini (basi aingie); la sivyo, basi arudi." ('Umar) akasema: Ni lazima umlete atakayeshuhudia pamoja nawe, au nitafanya (jambo), na nitafanya (jambo)! Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه) amesema: Na (Abuw Muwsaa) akatujia nami nikiwa katika kundi la watu miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Msikitini, naye akiwa na khofu kutokana na kitisho cha 'Umar (رضي الله عنه) kwake. Akasimama mbele yetu, akasema: Namuapisha kwa Allaah mtu yeyote miongoni mwenu aliyesikia hilo kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), ila anishuhudie kwalo. Amesema: Nikainua kichwa changu, nikasema: Mkhabarishe kwamba mimi niko pamoja nawe juu ya hili. Na wengine pia wakasema hivyo; Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) akaondokewa na khofu yake.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1717
Hadiyth
2671

2-Mlangoباب: كيف الاستئذانMlango Wa Namna Ya Kuomba Idhini

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ، قَالَ: سَمِعْتُ جَابِرَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَضَرَبْتُ بَابَهُ، فَقَالَ: "مَنْ ذَا؟". فَقُلْتُ: أَنَا. فَقَالَ: "أَنَا؟ أَنَا؟!" فَكَرِهَ ذَاكَ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muhammad bin Al-Munkadir, amesema: Nilimsikia Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما) akisema: Nilimjia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikabisha mlango wake. Akasema: "Ni nani huyo?" Nikasema: Mimi. Akasema: "Mimi? Mimi?" Akalichukia hilo.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1718
Hadiyth
2672

3-Mlangoباب: في النهي أن يطرق الرجل أهله ليلاMlango Wa Kuhusu Katazo La Mtu
Kuwajia Ahli Zake Ghafla Usiku

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ: سَمِعْتُ مُحَارِبَ بْنَ دِثَارٍ يَذْكُرُ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنْ يَطْرُقَ الرَّجُلُ أَهْلَهُ لَيْلًا، أَوْ يُخَوِّنَهُمْ، أَوْ يَلْتَمِسَ عَثَرَاتِهِمْ". قَالَ سُفْيَانُ: قَوْلُهُ: أَوْ يُخَوِّنَهُمْ، أَوْ يَلْتَمِسَ عَثَرَاتِهِمْ، مَا أَدْرِي: شَيْءٌ. قَالَهُ مُحَارِبٌ: أَوْ شَيْءٌ هُوَ فِي الْحَدِيثِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, amesema: Nilimsikia Muhaarib bin Dithaar akitaja, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza mtu kuwajia ahli zake ghafla usiku, au kuwatuhumu khiyana, au kutafuta makosa yao." Sufyaan amesema: Kauli yake: 'au kuwatuhumu khiyana, au kutafuta makosa yao' — sijui: ni kitu alichokisema Muhaarib, au ni kitu kilichomo katika Hadiyth.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1719
Hadiyth
2673

4-Mlangoباب: في إفشاء السلامMlango Wa Kuhusu Kueneza Salaam

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ عَوْفٍ، عَنْ زُرَارَةَ بْنِ أَوْفَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلَامٍ، قَالَ: لَمَّا قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الْمَدِينَةَ، اسْتَشْرَفَهُ النَّاسُ، فَقَالُوا: قَدِمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ. قَالَ: فَخَرَجْتُ فِيمَنْ خَرَجَ، فَلَمَّا رَأَيْتُ وَجْهَهُ، عَرَفْتُ أَنَّ وَجْهَهُ لَيْسَ بِوَجْهِ كَذَّابٍ. فَكَانَ أَوَّلَ مَا سَمِعْتُهُ، يَقُولُ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، أَفْشُوا السَّلَامَ، وَأَطْعِمُوا الطَّعَامَ، وَصِلُوا الْأَرْحَامَ، وَصَلُّوا وَالنَّاسُ نِيَامٌ، تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ بِسَلَامٍ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa 'Awf, kutoka kwa Zuraarah bin Awfaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Salaam (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowasili Madiynah, watu walijitokeza kumtazama, wakasema: Amewasili Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Amesema: Nikatoka miongoni mwa waliotoka. Nilipouona uso wake, nilitambua kwamba uso wake si uso wa mwongo. Basi jambo la kwanza nililomsikia akisema lilikuwa: "Enyi watu! Enezeni Salaam, na lisheni chakula, na ungeni udugu wa jamaa wa damu, na swalini na hali watu wamelala; mtaingia Jannah (Peponi) kwa amani."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1720
Hadiyth
2674

5-Mlangoباب: في حق المسلم على المسلمMlango Wa Kuhusu Haki Ya Muislamu Juu Ya Muislamu

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لِلْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ سِتٌّ: يُسَلِّمُ عَلَيْهِ إِذَا لَقِيَهُ وَيُشَمِّتُهُ إِذَا عَطَسَ، وَيَعُودُهُ إِذَا مَرِضَ، وَيُجِيبُهُ إِذَا دَعَاهُ، وَيَشْهَدُهُ إِذَا تُوُفِّيَ، وَيُحِبُّ لَهُ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ، وَيَنْصَحُ لَهُ بِالْغَيْبِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Muislamu ana juu ya Muislamu (haki) sita: amsalimie anapokutana naye; na amwombee Rehma anapochemua; na amtembelee anapougua; na amwitikie anapomwita; na amhudhurie (jeneza lake) anapofariki; na ampendelee anachokipenda kwa ajili ya nafsi yake; na amtakie nasaha asipokuwepo."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1720
Hadiyth
2675

6-Mlangoباب: في تسليم الراكب على الماشيMlango Wa Kuhusu Mwenye Kipando Kumsalimia Anayetembea

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، أَخْبَرَنَا أَبُو هَانِئٍ الْخَوْلَانِيُّ: أَنَّ أَبَا عَلِيٍّ الْجَنْبِيَّ حَدَّثَهُ، عَنْ فَضَالَةَ بْنِ عُبَيْدٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى الْمَاشِي، وَالْقَائِمُ عَلَى الْقَاعِدِ، وَالْقَلِيلُ عَلَى الْكَثِيرِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, ametukhabarisha Abuw Haaniy Al-Khawlaaniy, kwamba Abuw 'Aliy Al-Janbiy alimsimulia, kutoka kwa Fadhwaalah bin 'Ubayd (رضي الله عنه), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwenye kipando amsalimie anayetembea, na aliyesimama amsalimie aliyeketi, na wachache wawasalimie wengi."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1721
Hadiyth
2676

7-Mlangoباب: في رد السلام على أهل الكتابMlango Wa Kuhusu Kuwarudishia
Salaam Ahlul-Kitaab (Watu Wa Kitabu)

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الْيَهُودَ إِذَا سَلَّمَ أَحَدُهُمْ، فَإِنَّمَا يَقُولُ: السَّامُ عَلَيْكَ. قُلْ: عَلَيْكَ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Mayahudi, anaposalimia mmoja wao, basi husema: 'Mauti yawe juu yako.' Basi sema: 'Juu yako.'"

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1721
Hadiyth
2677

8-Mlangoباب: في التسليم على الصبيانMlango Wa Kuhusu Kuwasalimia Watoto

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سَيَّارٍ، قَالَ: كُنْتُ أَمْشِي مَعَ ثَابِتٍ الْبُنَانِيِّ، فَمَرَّ بِصِبْيَانٍ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ، وَحَدَّثَ ثَابِتٌ أَنَّهُ كَانَ مَعَ أَنَسٍ فَمَرَّ بِصِبْيَانٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ، وَحَدَّثَ أَنَسٌ: "أَنَّهُ كَانَ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَمَرَّ بِصِبْيَانٍ، فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ"

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Sayyaar, amesema: Nilikuwa nikitembea pamoja na Thaabit Al-Bunaaniy, akawapita watoto, akawasalimia. Na Thaabit akasimulia kwamba yeye alikuwa pamoja na Anas (رضي الله عنه), akawapita watoto, akawasalimia. Na Anas (رضي الله عنه) akasimulia: "Kwamba yeye alikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akawapita watoto, akawasalimia."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1722
Hadiyth
2678

9-Mlangoباب: في التسليم على النساءMlango Wa Kuhusu Kuwasalimia Wanawake

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ ابْنِ أَبِي حُسَيْنٍ، حَدَّثَنِي شَهْرٌ، عَنْ أَسْمَاءَ بِنْتِ يَزِيدَ بْنِ السَّكَنِ إِحْدَى نِسَاءِ بَنِي عَبْدِ الْأَشْهَلِ "أَنَّهَا بَيْنَا هِيَ فِي نِسْوَةٍ مَرَّ عَلَيْهِنَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَسَلَّمَ عَلَيْهِنَّ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Ibn Abiy Husayn, amenisimulia Shahr, kutoka kwa Asmaa bint Yaziyd bin As-Sakan (رضي الله عنها) — mmoja wa wanawake wa Banuw 'Abdil-Ash-hal —, kwamba yeye alipokuwa katika kundi la wanawake, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwapita, "akawasalimia."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1723
Hadiyth
2679

10-Mlangoباب: إذا قرئ على الرجل السلام كيف يردMlango Wa Mtu Akifikishiwa Salaam, Airudishe Vipi

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ: أَنَّ عَائِشَةَ زَوْجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا عَائِشُ هَذَا جِبْرِيلُ يَقْرَأُ عَلَيْكِ السَّلَامَ". قَالَتْ: وَعَلَيْهِ السَّلَامُ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكاتُهُ. قَالَتْ: وَهُوَ يَرَى مَا لَا أَرَى

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenisimulia Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kwamba 'Aaishah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yaa 'Aaish! Huyu ni Jibriyl (عليه السلام), anakusomea Salaam." Akasema: Na juu yake iwe amani na Rehma ya Allaah na Baraka Zake. Akasema: Naye anaona nisiyoyaona.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1724
Hadiyth
2680

11-Mlangoباب: في رد السلامMlango Wa Kuhusu Kurudisha Salaam

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ هُوَ: ابْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ هِلَالٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الصَّامِتِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: صَلَّى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَتَيْتُهُ حِينَ قَضَى صَلَاتَهُ، فَكُنْتُ أَوَّلَ مَنْ حَيَّا بِتَحِيَّةِ الْإِسْلَامِ. قَالَ: "عَلَيْكَ السَّلَامُ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، مِمَّنْ أَنْتَ؟". قَالَ: قُلْتُ: مِنْ غِفَارٍ. قَالَ: فَأَهْوَى بِيَدِهِ. قُلْتُ فِي نَفْسِي: كَرِهَ أَنِّي انْتَمَيْتُ إِلَى غِفَارٍ

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Sulaymaan — naye ni Ibn Al-Mughiyrah —, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Asw-Swaamit, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliswali, nikamjia alipomaliza Swalaah yake; nikawa mtu wa kwanza kumsalimia kwa maamkizi ya Islaam. Akasema: "Juu yako iwe amani na Rehma ya Allaah. Wewe ni miongoni mwa (watu) gani?" Amesema: Nikasema: Ni wa (kabila la) Ghifaar. Amesema: Akaupeleka mkono wake. Nikasema moyoni mwangu: Amechukia kwamba nimejinasibisha na Ghifaar.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1725
Hadiyth
2681

12-Mlangoباب: في فضل التسليم وردهMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Kutoa Salaam Na Kuirudisha

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ عَوْفٍ، عَنْ أَبِي رَجَاءٍ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ، فَرَدَّ عَلَيْهِ وَقَالَ: "عَشْرٌ". ثُمَّ جَاءَ رَجُلٌ فَسَلَّمَ، فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، فَرَدَّ عَلَيْهِ، فَقَالَ: "عِشْرُونَ". ثُمَّ جَاءَ رَجُلٌ فَسَلَّمَ، فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، فَرَدَّ عَلَيْهِ وَقَالَ: "ثَلَاثُونَ"

Ametusimulia Muhammad bin Kathiyr, ametusimulia Ja'far bin Sulaymaan, kutoka kwa 'Awf, kutoka kwa Abuw Rajaa, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Amani iwe juu yenu. Akamrudishia (Salaam), na akasema: "Kumi." Kisha akaja mtu (mwingine), akasalimia, akasema: Amani iwe juu yenu na Rehma ya Allaah. Akamrudishia, akasema: "Ishirini." Kisha akaja mtu (mwingine), akasalimia, akasema: Amani iwe juu yenu na Rehma ya Allaah na Baraka Zake. Akamrudishia, na akasema: "Thelathini."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1726
Hadiyth
2682

13-Mlangoباب: إذا سلم على الرجل وهو يبولMlango Wa Mtu Akisalimiwa Naye Anakojoa

أَخْبَرَنَا إِسْحَاق، حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هِشَامٍ، حَدَّثَنِي أَبِي، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ الْحُضَيْنِ، عَنِ الْمُهَاجِرِ بْنِ قُنْفُذٍ: أَنَّهُ سَلَّمَ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَبُولُ، "فَلَمْ يَرُدَّ عَلَيْهِ السَّلَامَ حَتَّى تَوَضَّأَ، فَلَمَّا تَوَضَّأَ، رَدَّهُ عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Is-haaq, ametusimulia Mu'aadh bin Hishaam, amenisimulia baba yangu, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Al-Hudhwayn, kutoka kwa Al-Muhaajir bin Qunfudh (رضي الله عنه), kwamba yeye alimsalimia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akiwa anakojoa, "hakumrudishia Salaam mpaka alipotawadha; alipotawadha, akamrudishia."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1726
Hadiyth
2683

14-Mlangoباب: في النهي عن الدخول على النساءMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuingia Kwa Wanawake

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ بِسْطَامَ، حَدَّثَنَا لَيْثُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي الْخَيْرِ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَدْخُلُوا عَلَى النِّسَاءِ". قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِلَّا الْحَمْوُ. قَالَ: "الْحَمْوُ: الْمَوْتُ". قَالَ يَحْيَى: الْحَمْوُ: يَعْنِي قَرَابَةَ الزَّوْجِ

Ametukhabarisha Yahyaa bin Bistwaam, ametusimulia Layth bin Sa'd, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Abul-Khayr, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiingie kwa wanawake." Ikasemwa: Yaa Rasula-Allaah, isipokuwa shemeji? Akasema: "Shemeji ni mauti." Yahyaa amesema: Al-Hamwu (shemeji): yaani jamaa wa mume.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1727
Hadiyth
2684

15-Mlangoباب: في نظرة الفجأةMlango Wa Kuhusu Mtazamo Wa Ghafla

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، وَأَبُو نُعَيْمٍ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ عَمْرِو بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي زُرْعَةَ بْنِ عَمْرِو بْنِ جَرِيرٍ، عَنْ جَرِيرٍ، قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَظْرَةِ الْفَجْأَةِ، فَقَالَ: "اصْرِفْ بَصَرَكَ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf na Abuw Nu'aym, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa 'Amr bin Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Zur'ah bin 'Amr bin Jariyr, kutoka kwa Jariyr (رضي الله عنه), amesema: Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mtazamo wa ghafla, akasema: "Geuza macho yako."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1728
Hadiyth
2685

16-Mlangoباب: في ذيول النساءMlango Wa Kuhusu Pindo Za Nguo Za Wanawake

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ: ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ صَفِيَّةَ بِنْتِ أَبِي عُبَيْدٍ، عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ زَوْجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَيْلِ الْمَرْأَةِ، فَقَالَ: "شِبْرًا"، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِذَنْ تَبْدُوَ أَقْدَامُهُنَّ؟، قَالَ: "قَدْرَ ذِرَاعٍ لَا يَزِدْنَ عَلَيْهِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: النَّاسُ يَقُولُونَ: عَنْ نَافِعٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ

Ametukhabarisha Ahmad bin Khaalid, ametusimulia Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Swafiyyah bint Abiy 'Ubayd, kutoka kwa Ummu Salamah (رضي الله عنها), mke wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu pindo la (nguo ya) mwanamke, akasema: "Shibiri moja." Nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hapo nyayo zao zitaonekana? Akasema: "Kiasi cha dhiraa moja, wasizidishe juu yake."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Watu wanasema: kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1728
Hadiyth
2686

17-Mlangoباب: في كراهية إظهار الزينةMlango Wa Kuhusu Karaha Ya Kudhihirisha Mapambo

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنِي رِبْعِيُّ بْنُ حِرَاشٍ، عَنِ امْرَأَتِهِ، عَنْ أُخْتٍ لِحُذَيْفَةَ، قَالَتْ: خَطَبَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ، أَمَا لَكُنَّ فِي الْفِضَّةِ مَا تَحَلَّيْنَ بِهِ؟ أَمَا إِنَّهُ لَيْسَتْ مِنْكُنَّ امْرَأَةٌ تَحَلَّى الذَّهَبَ فَتُظْهِرَهُ، إِلَّا عُذِّبَتْ بِهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, amenisimulia Rib'iy bin Hiraash, kutoka kwa mkewe, kutoka kwa dada mmoja wa Hudhayfah رضي الله عنه رضي الله عنها, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituhutubia, akasema: "Yaa jamaa ya wanawake! Je, hamna katika fedha kitu cha kujipambia? Ama hakika, hakuna mwanamke yeyote miongoni mwenu anayejipamba kwa dhahabu akaidhihirisha, isipokuwa ataadhibiwa kwayo."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1729
Hadiyth
2687

18-Mlangoباب: في النهي عن الطيب إذا خرجتMlango Wa Kuhusu Katazo La Manukato
(Kwa Mwanamke) Anapotoka

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ثَابِتِ بْنِ عُمَارَةَ، عَنْ غُنَيْمِ بْنِ قَيْسٍ، عَنْ أَبِي مُوسَى: "أَيُّمَا امْرَأَةٍ اسْتَعْطَرَتْ، ثُمَّ خَرَجَتْ لِيُوجَدَ رِيحُهَا، فَهِيَ زَانِيَةٌ، وَكُلُّ عَيْنٍ زَانِيَةٌ". وَقَالَ أَبُو عَاصِمٍ: يَرْفَعُهُ بَعْضُ أَصْحَابِنَا

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Thaabit bin 'Umaarah, kutoka kwa Ghunaym bin Qays, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه): "Mwanamke yeyote aliyejitia manukato, kisha akatoka ili harufu yake inusiwe, basi yeye ni mzinifu; na kila jicho ni zinifu." Na Abuw 'Aaswim amesema: Baadhi ya wenzetu wanaipandisha [mpaka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)].

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1730
Hadiyth
2688

19-Mlangoباب: في الواصلة والمستوصلةMlango Wa Kuhusu Mwanamke Anayeunganisha Nywele
Na Anayeomba Kuunganishiwa

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "لَعَنَ اللَّهُ الْوَاشِمَاتِ، وَالْمُسْتَوْشِمَاتِ، وَالْمُتَنَمِّصَاتِ، وَالْمُتَفَلِّجَاتِ لِلْحُسْنِ الْمُغَيِّرَاتِ خَلْقَ اللَّهِ"، فَبَلَغَ ذَلِكَ امْرَأَةً مِنْ بَنِي أَسَدٍ يُقَالُ لَهَا: أُمُّ يَعْقُوبَ، فَجَاءَتْ فَقَالَتْ: بَلَغَنِي أَنَّكَ لَعَنْتَ كَيْتَ وَكَيْتَ؟، فَقَالَ: وَمَا لِي لَا أَلْعَنُ مَنْ لَعَنَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَهُوَ فِي كِتَابِ اللَّهِ؟، فَقَالَتْ: لَقَدْ قَرَأْتُ مَا بَيْنَ اللَّوْحَيْنِ، فَمَا وَجَدْتُ فِيهِ مَا تَقُولُ. قَالَ: لَئِنْ كُنْتِ قَرَأْتِيهِ، لَقَدْ وَجَدْتِيهِ، أَمَا قَرَأْتِ {مَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ}؟، فَقَالَتْ: بَلَى. قَالَ: فَإِنَّهُ قَدْ نَهَى عَنْهُ، فَقَالَتْ: فَإِنِّي أَرَى أَهْلَكَ يَفْعَلُونَهُ؟. قَالَ: فَادْخُلِي فَانْظُرِي. فَدَخَلَتْ فَنَظَرَتْ، فَلَمْ تَرَ مِنْ حَاجَتِهَا شَيْئًا، فَقَالَ: لَوْ كَانَتْ كَذَلِكَ مَا جَامَعْتُهَا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd (رضي الله عنه)], amesema: "Allaah Amewalaani wanawake wanaochora chale na wanaoomba kuchorwa, na wanaoomba kunyolewa nyusi, na wanaotanua mianya ya meno kwa ajili ya urembo, wanaobadilisha maumbile ya Allaah." Hilo likamfikia mwanamke mmoja wa Banuw Asad anayeitwa Ummu Ya'quwb. Akaja, akasema: Imenifikia kwamba wewe umewalaani kadhaa na kadhaa? Akasema: Na nina nini nisimlaani aliyelaaniwa na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na hali hilo limo katika Kitabu cha Allaah? Akasema: Hakika nimesoma yaliyomo baina ya majalada mawili (ya Qur-aan), lakini sikukuta ndani yake unayoyasema. Akasema: Kama ungekuwa umeisoma, basi ungeikuta. Je, hukusoma:

مَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

Na lolote analokupeni Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi jiepusheni. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah Ni Mkali wa Kuakibu. [Al-Hashr (59:7)]

Akasema: Ndiyo (nimesoma). Akasema: Basi hakika yeye amelikataza hilo. Akasema: Hakika mimi naona ahli zako wanalifanya? Akasema: Basi ingia, utazame. Akaingia, akatazama, na hakuona chochote katika alichokikusudia. Akasema: Lau angekuwa hivyo, nisingekaa naye.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1730
Hadiyth
2689

20-Mlangoباب: في النهي عن مكامعة الرجل الرجل، والمرأة المرأةMlango Wa Kuhusu Katazo La Mwanamume Kulala
Pamoja Na Mwanamume, Na Mwanamke Na Mwanamke

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ حُبَابٍ، حَدَّثَنِي يَحْيَى بْنُ أَيُّوبَ الْحَضْرَمِيُّ، أَخْبَرَنِي عَيَّاشُ بْنُ عَبَّاسٍ الْحِمْيَرِيُّ، عَنْ أَبِي الْحُصَيْنِ الْحَجْرِيِّ، عَنْ أَبِي عَامِرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا رَيْحَانَةَ صَاحِبَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "يَنْهَى عَنْ عَشْرِ خِصَالٍ: مُكَامَعَةِ الرَّجُلِ الرَّجُلَ فِي شِعَارٍ لَيْسَ بَيْنَهُمَا شَيْءٌ. وَمُكَامَعَةِ الْمَرْأَةِ الْمَرْأَةَ فِي شِعَارٍ وَاحِدٍ لَيْسَ بَيْنَهُمَا شَيْءٌ. وَالنَّتْفِ، وَالْوَشْمِ، وَالنُّهْبَةِ، وَرُكُوبِ النُّمُورِ، وَاتِّخَاذِ الدِّيبَاجِ هَا هُنَا عَلَى الْعَاتِقَيْنِ، وَفِي أَسْفَلِ الثِّيَابِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: أَبُو عَامِرٍ. شَيْخٌ لَهُمْ، وَالْمُكَامَعَةُ: الْمُضَاجَعَةُ

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Zayd bin Hubaab, amenisimulia Yahyaa bin Ayyuwb Al-Hadhwramiy, amenikhabarisha 'Ayyaash bin 'Abbaas Al-Himyariy, kutoka kwa Abul-Huswayn Al-Hajriy, kutoka kwa Abuw 'Aamir, amesema: Nilimsikia Abuw Rayhaanah (رضي الله عنه), sahibu wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikuwa akikataza mambo kumi: mukaama'ah (kulala pamoja) ya mwanamume na mwanamume katika shuka, bila ya kuwa na kitu baina yao; na mukaama'ah ya mwanamke na mwanamke katika shuka moja, bila ya kuwa na kitu baina yao; na kunyonyoa (nywele), na kuchora chale, na kunyang'anya (mali ya watu), na kupanda (juu ya ngozi za) chui, na kuweka diybaaj (hariri nzito iliyonakshiwa) hapa juu ya mabega mawili, na chini ya nguo."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Abuw 'Aamir ni shaykh (mwalimu) wao. Na al-mukaama'ah ni: al-mudhwaaja'ah (kulala pamoja ubavu kwa ubavu).

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1732
Hadiyth
2690

21-Mlangoباب: لعن المخنثين والمترجلاتMlango Wa Laana Ya Wanaume Wanaojifananisha
Na Wanawake, Na Wanawake Wanaojifananisha Na Wanaume

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، وَوَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا هِشَامٌ الدَّسْتَوَائِيُّ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَعَنَ الْمُخَنَّثِينَ مِنَ الرِّجَالِ، وَالْمُتَرَجِّلَاتِ مِنَ النِّسَاءِ، وَقَالَ: "أَخْرِجُوهُمْ مِنْ بُيُوتِكُمْ". قَالَ: فَأَخْرَجَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فُلَانًا، وَأَخْرَجَ عُمَرُ فُلَانًا أَوْ فُلَانَةً. قَالَ عَبْد اللَّهِ: فَأَشُكُّ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn na Wahb bin Jariyr, wamesema: Ametusimulia Hishaam Ad-Dastawaaiy, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake, na wanawake wanaojifananisha na wanaume, na akasema: "Watoeni katika nyumba zenu." Amesema: "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamtoa fulani, na 'Umar (رضي الله عنه) akamtoa fulani au fulani (mwanamke)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: "Nina shaka (katika hilo)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1733
Hadiyth
2691

22-Mlangoباب: في أن الفخذ عورةMlango Wa Kuhusu
Kwamba Paja Ni 'Awrah (Sehemu Ya Mwili Inayopasa Kusitiriwa)

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا مَالِكٌ، عَنْ أَبِي النَّضْرِ، عَنْ زُرْعَةَ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ الصُّفَّةِ، قَالَ: جَلَسَ عِنْدَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَفَخِذِي مُنْكَشِفَةٌ، فَقَالَ: "خَمِّرْ عَلَيْكَ، أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ الْفَخِذَ عَوْرَةٌ؟"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Maalik, kutoka kwa Abun-Nadhwr, kutoka kwa Zur'ah bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه) — naye alikuwa miongoni mwa watu wa Asw-Swuffah (Swahaba mafakiri walioishi katika kibaraza cha Msikiti wa Madiynah) —, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliketi kwetu na paja langu likiwa wazi. Akasema: "Jifunike; je, hujui kwamba paja ni 'awrah (sehemu ya mwili inayopasa kusitiriwa)?"

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1734
Hadiyth
2692

23-Mlangoباب: في النهي عن دخول المرأة الحمامMlango Wa Kuhusu Katazo La Mwanamke
Kuingia Hammaam (Bafu La Umma)

أَخْبَرَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، قَالَ: دَخَلَ عَلَى عَائِشَةَ نِسْوَةٌ مِنْ أَهْلِ حِمْصَ يَسْتَفْتِينَهَا، فَقَالَتْ: لَعَلَّكُنَّ مِنَ النِّسْوَةِ اللَّاتِي يَدْخُلْنَ الْحَمَّامَاتِ؟. قُلْنَ: نَعَمْ. قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَا مِنْ امْرَأَةٍ تَضَعُ ثِيَابَهَا فِي غَيْرِ بَيْتِ زَوْجِهَا، إِلَّا هَتَكَتْ مَا بَيْنَهَا وَبَيْنَ اللَّهِ عز وجل".

Ametukhabarisha Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, amesema: Wanawake kutoka kwa watu wa Himsw waliingia kwa 'Aaishah (رضي الله عنها) wakimwomba Fatwa (hukmu ya kisheria). Akasema: Huenda nyinyi ni miongoni mwa wanawake wanaoingia katika hammaam (mabafu ya umma)? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna mwanamke yeyote anayevua nguo zake mahali pasipokuwa nyumba ya mumewe, isipokuwa amerarua (sitara iliyo) baina yake na baina ya Allaah (عز وجل)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1735
Hadiyth
2693

قَالَ أَبُو مُحَمَّد: أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِي الْمَلِيحِ، عَنْ عَائِشَةَ، هَذَا الْحَدِيثَ

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Abul-Maliyh, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), Hadiyth hii.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1735
Hadiyth
2694

24-Mlangoباب: لا يقيمن أحدكم أخاه من مجلسهMlango Wa Asimwinue Yeyote Kati Yenu Nduguye
Kutoka Mahali Pake Pa Kuketi

أَخْبَرَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْمُفَضَّلِ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يُقِيمُ الرَّجُلُ يَعْنِي: أَخَاهُ مِنْ مَجْلِسِهِ، ثُمَّ يَقْعُدُ فِيهِ، وَلَكِنْ تَفَسَّحُوا وَتَوَسَّعُوا"

Ametukhabarisha Musaddad, ametusimulia Bishr bin Al-Mufadhwdhwal, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu asimwinue — yaani nduguye — kutoka mahali pake pa kuketi, kisha akaketi humo; lakini mpishane na mpanuliane nafasi."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1735
Hadiyth
2695

25-Mlangoباب: إذا قام من مجلسه ثم رجع إليه فهو أحق بهMlango Wa Akiinuka Kutoka Kikao Chake Kisha
Akarudi, Basi Yeye Ndiye Mwenye Haki Zaidi Nacho

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا سُهَيْلٌ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا قَامَ أَحَدُكُمْ أَوِ الرَّجُلُ مِنْ مَجْلِسِهِ ثُمَّ رَجَعَ إِلَيْهِ، فَهُوَ أَحَقُّ بِهِ"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zuhayr, ametusimulia Suhayl, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu — au mtu — akiinuka kutoka kikao chake kisha akarudi kwacho, basi yeye ndiye mwenye haki zaidi nacho."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1736
Hadiyth
2696

26-Mlangoباب: في النهي عن الجلوس في الطرقاتMlango Wa Kuhusu Katazo La Kuketi Njiani

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا أَبُو إِسْحَاق، عَنِ الْبَرَاءِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ بِنَاسٍ جُلُوسٍ مِنَ الْأَنْصَارِ، فَقَالَ: "إِنْ كُنْتُمْ لَا بُدَّ فَاعِلِينَ، فَاهْدُوا السَّبِيلَ، وَأَفْشُوا السَّلَامَ، وَأَعِينُوا الْمَظْلُومَ". قَالَ شُعْبَةُ: لَمْ يَسْمَعْ هَذَا الْحَدِيثَ أَبُو إِسْحَاق مِنَ الْبَرَاءِ

Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Baraa (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwapita watu miongoni mwa Answaar (رضي الله عنهم) waliokuwa wameketi, akasema: "Ikiwa hamna budi kufanya (hivyo), basi waongozeni (watu) njia, na enezeni Salaam, na msaidieni aliyedhulumiwa." Shu'bah amesema: Abuw Is-haaq hakuisikia Hadiyth hii kutoka kwa Al-Baraa (رضي الله عنه).

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1737
Hadiyth
2697

27-Mlangoباب: في وضع إحدى الرجلين على الأخرىMlango Wa Kuhusu Kuweka Mguu Mmoja Juu Ya Mwingine

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ أَحْمَدَ بْنِ أَبِي خَلَفٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ: سَمِعْتُ الزُّهْرِيَّ يُحَدِّثُ، عَنْ عَبَّادِ بْنِ تَمِيمٍ، عَنْ عَمِّهِ، قَالَ: رَأَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "مُسْتَلْقِيًا فِي الْمَسْجِدِ، وَاضِعًا إِحْدَى رِجْلَيْهِ عَلَى الْأُخْرَى"

Ametukhabarisha Muhammad bin Ahmad bin Abiy Khalaf, ametusimulia Sufyaan, amesema: Nilimsikia Az-Zuhriy akisimulia, kutoka kwa 'Abbaad bin Tamiym, kutoka kwa ami yake (رضي الله عنه), amesema: Nilimwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) "amelala chali Msikitini, ameweka mmoja wa miguu yake juu ya mwingine."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1738
Hadiyth
2698

28-Mlangoباب: لا يتناجى اثنان دون صاحبهماMlango Wa Wasinong'onezane Wawili Bila Ya Mwenzao

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا كُنْتُمْ ثَلَاثَةً، فَلَا يَتَنَاجَى اثْنَانِ دُونَ صَاحِبِهِمَا، فَإِنَّ ذَلِكَ يُحْزِنُهُ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd (رضي الله عنه)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mkiwa watatu, basi wasinong'onezane wawili bila ya mwenzao, kwani hakika hilo humhuzunisha."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1738
Hadiyth
2699

29-Mlangoباب: في كفارة المجلسMlango Wa Kuhusu Kafara Ya Kikao

حَدَّثَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ يَعْنِي: ابْنَ دِينَارٍ، عَنْ أَبِي هَاشِمٍ، عَنْ رُفَيْعٍ: أَبِي الْعَالِيَةِ، عَنْ أَبِي بَرْزَةَ الْأَسْلَمِيِّ، قَالَ: لَمَّا كَانَ بِأَخَرَةٍ، كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا جَلَسَ فِي الْمَجْلِسِ فَأَرَادَ أَنْ يَقُومَ، قَالَ: "سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ". فَقَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّكَ لَتَقُولُ الْآنَ كَلَامًا، مَا كُنْتَ تَقُولُهُ فِيمَا خَلَا، فَقَالَ: "هَذَا كَفَّارَةٌ لِمَا يَكُونُ فِي الْمَجَالِسِ"

Ametusimulia Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Hajjaaj — yaani Ibn Diynaar —, kutoka kwa Abuw Haashim, kutoka kwa Rufay' Abul-'Aaliyah, kutoka kwa Abuw Barzah Al-Aslamiy (رضي الله عنه), amesema: Ilipokuwa mwishoni (mwa umri wake), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoketi katika kikao, kisha akataka kusimama, husema:

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ

Utakasifu ni Wako Yaa Allaah, na Himdi ni Zako. Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Nakuomba Unighufurie na ninarejea Kwako kutubia.

Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika wewe sasa unasema maneno ambayo hukuwa ukiyasema katika (zama) zilizopita. Akasema: "Haya ni kafara kwa yale yanayotokea katika vikao."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1739
Hadiyth
2700

30-Mlangoباب: إذا عطس الرجل ما يقولMlango Wa Mtu Akichemua, Aseme Nini

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ أَخِيهِ عِيسَى، عَنْ أَبِيهِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ أَبِي أَيُّوبَ الْأَنْصَارِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْعَاطِسُ يَقُولُ: الْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ. وَيَقُولُ الَّذِي يُشَمِّتُهُ: يَرْحَمُكُمْ اللَّهُ، وَيَرُدُّ عَلَيْهِ: يَهْدِيكُمُ اللَّهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa ndugu yake 'Iysaa, kutoka kwa baba yake 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Abuw Ayyuwb Al-Answaariy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Mwenye kuchemua husema:

الْحَمْدُ لِلَّهِ عَلَى كُلِّ حَالٍ

Himdi Anastahiki Allaah kwa kila hali.

Na yule anayemwombea Rehma husema:

يَرْحَمُكُمْ اللَّهُ

Allaah Akurehemu.

Na (mwenye kuchemua) humrudishia:

يَهْدِيكُمُ اللَّهُ وَيُصْلِحُ بَالَكُمْ

Akuongoze Allaah na Akutengenezee mambo yako.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1739
Hadiyth
2701

31-Mlangoباب: إذا لم يحمد الله لم يشمتهMlango Wa (Mwenye Kuchemua)
Asipomhimidi Allaah, Asiombewe Rehma

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: عَطَسَ رَجُلَانِ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَشَمَّتَ أَحَدَهُمَا وَلَمْ يُشَمِّتْ الْآخَرَ، فَقِيلَ لَهُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، شَمَّتَّ هَذَا وَلَمْ تُشَمِّتْ الْآخَرَ؟، فَقَالَ: "إِنَّ هَذَا حَمِدَ اللَّهَ، وَإِنَّ هَذَا لَمْ يَحْمَدْ اللَّهَ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: سُلَيْمَانُ هُوَ: التَّيْمِيُّ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Watu wawili walichemua mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم); akamwombea Rehma mmoja wao, na hakumwombea mwingine. Akaambiwa: Yaa Rasula-Allaah, umemwombea huyu na hukumwombea mwingine? Akasema: "Hakika huyu amemhimidi Allaah, na huyu hakumhimidi Allaah."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Sulaymaan ni At-Taymiy.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1740
Hadiyth
2702

32-Mlangoباب: كم يشمت العاطسMlango Wa Mara Ngapi Anaombewa Rehma
Mwenye Kupiga Chafya

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا عِكْرِمَةُ هُوَ: ابْنُ عَمَّارٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي إِيَاسُ بْنُ سَلَمَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبِي، قَالَ: عَطَسَ رَجُلٌ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَرْحَمُكَ اللَّهُ". ثُمَّ عَطَسَ أُخْرَى، فَقَالَ: "الرَّجُلُ مَزْكُومٌ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia 'Ikrimah — naye ni Ibn 'Ammaar —, amesema: Amenisimulia Iyaas bin Salamah, amesema: Amenisimulia baba yangu [Salamah bin Al-Akwa' (رضي الله عنه)], amesema: Mtu mmoja alipiga chafya mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Allaah Akurehemu." Kisha akapiga chafya mara nyingine, akasema: "Mtu huyu ana mafua."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1741
Hadiyth
2703

33-Mlangoباب: في النهي عن التصاويرMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Picha

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَتْ عَائِشَةُ: "كَانَ لَنَا ثَوْبٌ فِيهِ تَصَاوِيرُ، فَجَعَلْتُهُ بَيْنَ يَدَيْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يُصَلِّي، فَنَهَانِي أَوْ قَالَتْ: فَكَرِهَهُ، قَالَتْ: فَجَعَلْتُهُ وَسَائِدَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Qaasim, kutoka kwa baba yake, amesema: 'Aaishah (رضي الله عنها) amesema: "Tulikuwa na nguo yenye picha, nikaiweka mbele ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akiswali; akanikataza — au alisema: akaichukia —." Akasema: "Basi nikaifanya mito."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1742
Hadiyth
2704

34-Mlangoباب: لا تدخل الملائكة بيتا فيه تصاويرMlango Wa Malaika (عليهم السلام) Hawaingii Nyumba
Ambayo Ndani Yake Mna Picha

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ بْنُ زِيَادٍ، حَدَّثَنَا عُمَارَةُ بْنُ الْقَعْقَاعِ، حَدَّثَنَا الْحَارِثُ الْعُكْلِيُّ، عَنْ أَبِي زُرْعَةَ بْنِ عَمْرِو بْنِ جَرِيرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نُجَيٍّ، عَنْ عَلِيٍّ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ الْمَلَكَ لَا يَدْخُلُ بَيْتًا فِيهِ كَلْبٌ، وَلَا صُورَةٌ، وَلَا جُنُبٌ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia 'Abdul-Waahid bin Ziyaad, ametusimulia 'Umaarah bin Al-Qa'qaa', ametusimulia Al-Haarith Al-'Ukliy, kutoka kwa Abuw Zur'ah bin 'Amr bin Jariyr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Nujayy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Malaika (عليه السلام) haingii nyumba ambayo ndani yake mna mbwa, wala picha, wala mwenye janaba."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1742
Hadiyth
2705

35-Mlangoباب: في النفقة على العيالMlango Wa Kuhusu Matumizi Kwa Ajili Ya Familia

حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: عَدِيُّ بْنُ ثَابِتٍ أَخْبَرَنِي، قالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ يَزِيدَ يُحَدِّثُ، عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ الْبَدْرِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ: "الْمُسْلِمُ إِذَا أَنَفْقَ نَفَقَةً عَلَى أَهْلِهِ وَهُوَ يَحْتَسِبُهَا، فَهِيَ لَهُ صَدَقَةٌ"

Ametusimulia Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, amesema: 'Adiyy bin Thaabit amenikhabarisha, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd (رضي الله عنه) akisimulia kutoka kwa Abuw Mas'uwd Al-Badriy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba amesema: "Muislamu anapotoa matumizi kwa ahli zake, naye akitarajia malipo yake (kwa Allaah), basi hayo ni swadaka kwake."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1743
Hadiyth
2706

36-Mlangoباب: في الدابة يركب عليها ثلاثةMlango Wa Kuhusu Mnyama Wa Kupanda Anayepandwa
Na Watu Watatu

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ يَزِيدَ، قَالَ: حَدَّثَنَا عَاصِمٌ الْأَحْوَلُ، عَنْ مُوَرِّقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ جَعْفَرٍ، قَالَ: "كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَفَلَ، تُلُقِّيَ بِي وَبِالْحَسَنِ أَوْ بِالْحُسَيْنِ، قَالَ: وَأُرَاهُ قَالَ: الْحَسَنَ فَحَمَلَنِي بَيْنَ يَدَيْهِ، وَالْحَسَنَ وَرَاءَهُ، حَتَّى قَدِمْنَا الْمَدِينَةَ وَنَحْنُ عَلَى الدَّابَّةِ الَّتِي عَلَيْهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Thaabit bin Yaziyd, amesema: Ametusimulia 'Aaswim Al-Ahwal, kutoka kwa Muwarriq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ja'far (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa "anaporejea (kutoka safarini), tulipelekwa kumlaki, mimi na Al-Hasan (رضي الله عنه) — au Al-Husayn (رضي الله عنه); amesema: Na nadhani alisema: Al-Hasan —. Akanibeba mbele yake, na Al-Hasan (رضي الله عنه) nyuma yake, mpaka tukaingia Madiynah, nasi tukiwa juu ya mnyama ambaye Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa juu yake."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1743
Hadiyth
2707

37-Mlangoباب: في صاحب الدابة أحق بصدرهاMlango Wa Kuhusu Mwenye Mnyama Wa Kupanda Ndiye
Mwenye Haki Zaidi Ya Sehemu Yake Ya Mbele

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ يَحْيَى بْنِ طَلْحَةَ، عَنْ الْمُسَيَّبِ بْنِ رَافِعٍ، وَمَعْبَدِ بْنِ خَالِدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَزِيدَ الْخَطْمِيِّ وَكَانَ أَمِيرًا عَلَى الْكُوفَةِ، قَالَ: أَتَيْنَا قَيْسَ بْنَ سَعْدِ بْنِ عُبَادَةَ فِي بَيْتِهِ، فَأَذَّنَ الْمُؤَذِّنِ لِلصَّلَاةِ، وَقُلْنَا لِقَيْسٍ: قُمْ فَصَلِّ لَنَا، فَقَالَ: لَمْ أَكُنْ لِأُصَلِّيَ بِقَوْمٍ لَسْتُ عَلَيْهِمْ بِأَمِيرٍ، فَقَالَ رَجُلٌ لَيْسَ بِدُونِهِ. يُقَالُ لَهُ: عَبْدُ اللَّهِ بْنُ حَنْظَلَةَ بْنِ الْغَسِيلِ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الرَّجُلُ أَحَقُّ بِصَدْرِ دَابَّتِهِ، وَصَدْرِ فِرَاشِهِ، وَأَنْ يَؤُمَّ فِي رَحْلِهِ"، فَقَالَ قَيْسُ بْنُ سَعْدٍ عِنْدَ ذَاكَ: يَا فُلَانُ لِمَوْلًى لَهُ: قُمْ فَصَلِّ لَهُمْ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Is-haaq bin Yahyaa bin Twalhah, kutoka kwa Al-Musayyab bin Raafi' na Ma'bad bin Khaalid, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Yaziyd Al-Khatwmiy (رضي الله عنه) — naye alikuwa amiri wa Al-Kuwfah —, amesema: Tulimwendea Qays bin Sa'd bin 'Ubaadah (رضي الله عنه) nyumbani kwake. Muadhini akaadhini kwa ajili ya Swalaah, nasi tukamwambia Qays (رضي الله عنه): Simama utuswalishe. Akasema: Sikuwa mwenye kuwaswalisha watu ambao mimi si amiri wao. Mtu mmoja ambaye si duni kuliko yeye (kwa daraja), anayeitwa 'Abdu-Allaah bin Handhwalah bin Al-Ghasiyl (رضي الله عنه), akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu ana haki zaidi ya sehemu ya mbele ya mnyama wake (wa kupanda), na sehemu ya mbele ya tandiko lake, na kuongoza (Swalaah) katika makazi yake." Qays bin Sa'd (رضي الله عنه) akasema wakati huo: Yaa fulani — (akimwambia) mawlaa (mwachwa huru) wake —: Simama uwaswalishe.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1744
Hadiyth
2708

38-Mlangoباب: ما جاء أن على كل ذروة بعير شيطاناMlango Wa Yaliyopokewa Kuhusu Kwamba
Juu Ya Kila Nundu Ya Ngamia Kuna Shaytwaan

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ حَمْزَةَ بْنِ عَمْرٍو الْأَسْلَمِيِّ، قَالَ: وَقَدْ صَحِبَ أَبُوهُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبِي يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَلَى ذِرْوَةِ كُلِّ بَعِيرٍ شَيْطَانٌ، فَإِذَا رَكِبْتُمُوهَا فَسَمُّوا اللَّهَ وَلَا تُقَصِّرُوا عَنْ حَاجَاتِكُمْ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Usaamah bin Zayd, kutoka kwa Muhammad bin Hamzah bin 'Amr Al-Aslamiy, amesema — na baba yake (رضي الله عنه) alikuwa amesuhubiana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, amesema: Nilimsikia baba yangu (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Juu ya nundu ya kila ngamia kuna shaytwaan; basi mnapowapanda, tajeni Jina la Allaah, wala msijizuie (kuwatumia) katika haja zenu."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1745
Hadiyth
2709

39-Mlangoباب: في النهي عن أن تتخذ الدواب كراسيMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Kuwafanya
Wanyama Wa Kupanda Kuwa Viti

أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا شَبَابَةُ بْنُ سَوَّارٍ، حَدَّثَنَا لَيْثُ بْنُ سَعْدٍ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ مُعَاذِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِيهِ وَكَانَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "ارْكَبُوا هَذِهِ الدَّوَابَّ سَالِمَةً، وَلَا تَتَّخِذُوهَا كَرَاسِيَّ".

Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Shabaabah bin Sawwaar, ametusimulia Layth bin Sa'd, kutoka kwa Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Sahl bin Mu'aadh bin Anas, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه) — naye alikuwa miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) —, kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Wapandeni wanyama hawa wakiwa salama, wala msiwafanye kuwa viti."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1745
Hadiyth
2710

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، عَنْ اللَّيْثِ، إِلَّا أَنَّهُ يُخَالِفُ شَبَابَةَ فِي شَيْءٍ

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, kutoka kwa Al-Layth, [mfano wake], isipokuwa yeye anatofautiana na Shabaabah katika kitu fulani.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1746
Hadiyth
2711

40-Mlangoباب: السفر قطعة من العذابMlango Wa Safari Ni Kipande Cha Adhabu

أَخْبَرَنَا خَالِدُ بْنُ مَخْلَدٍ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ سُمَيٍّ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "السَّفَرُ قِطْعَةٌ مِنْ الْعَذَابِ يَمْنَعُ أَحَدَكُمْ نَوْمَهُ وَطَعَامَهُ وَشَرَابَهُ، فَإِذَا قَضَى أَحَدُكُمْ نَهْمَتَهُ مِنْ وَجْهِهِ فَلْيُعَجِّلْ الرَّجْعَةَ إِلَى أَهْلِهِ"

Ametukhabarisha Khaalid bin Makhlad, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Sumayy, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Safari ni kipande cha adhabu: inamzuilia mmoja wenu usingizi wake, na chakula chake, na kinywaji chake. Basi mmoja wenu anapomaliza haja yake katika safari yake, na aharakishe kurejea kwa ahli zake."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1746
Hadiyth
2712

41-Mlangoباب: ما يقول إذا ودع رجلاMlango Wa Anayoyasema Anapomuaga Mtu

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي كَعْبٍ: أَبُو الْحَسَنِ الْعَبْدِيُّ، قَالَ: حَدَّثَنِي مُوسَى بْنُ مَيْسَرَةَ الْعَبْدِيُّ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ لَهُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُرِيدُ السَّفَرَ. فَقَالَ لَهُ: "مَتَى؟". قَالَ: غَدًا إِنْ شَاءَ اللَّهُ. قَالَ: فَأَتَاهُ، فَأَخَذَ بِيَدِهِ، فَقَالَ لَهُ: "فِي حِفْظِ اللَّهِ، وَفِي كَنَفِهِ، زَوَّدَكَ اللَّهُ التَّقْوَى، وَغَفَرَ لَكَ ذَنْبَكَ، وَوَجَّهَكَ لِلْخَيْرِ أَيْنَمَا تَوَخَّيْتَ أَوْ أَيْنَمَا تَوَجَّهْتَ". شَكَّ سَعِيدٌ فِي إِحْدَى الْكَلِمَتَيْنِ

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Sa'iyd bin Abiy Ka'b Abul-Hasan Al-'Abdiy, amesema: Amenisimulia Muwsaa bin Maysarah Al-'Abdiy, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akamwambia: Yaa Nabiyya-Allaah, hakika mimi nataka (kwenda) safari. Akamwambia: "Lini?" Akasema: Kesho, Akipenda Allaah. Akasema: Akamjia, akamshika mkono wake, akamwambia: "(Uwe) katika Hifadhi ya Allaah, na katika sitara Yake. Allaah Akupe taqwa kuwa masurufu (ya safari yako), na Akughufurie dhambi yako, na Akuelekeze kwenye kheri popote utakapokusudia — au: popote utakapoelekea." Sa'iyd alitia shaka katika moja ya maneno hayo mawili.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1747
Hadiyth
2713

42-Mlangoباب: في الدعاء إذا سافر وإذا قدمMlango Wa Kuhusu Du'aa Anaposafiri Na Anaporejea

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَخْبَرَنَا عَاصِمٌ هُوَ الْأَحْوَلُ، قَالَ: وَثَبَّتَنِي شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَرْجِسٍ، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا سَافَرَ، قَالَ: "اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ وَعْثَاءِ السَّفَرِ، وَكَآبَةِ الْمُنْقَلَبِ، وَالْحَوْرِ بَعْدَ الْكَوْرِ، وَدَعْوَةِ الْمَظْلُومِ، وَسُوءِ الْمَنْظَرِ فِي الْأَهْلِ وَالْمَالِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametukhabarisha 'Aaswim — naye ni Al-Ahwal —, amesema: Na Shu'bah alinithibitishia [Hadiyth hii], kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Sarjis (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaposafiri, husema:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ وَعْثَاءِ السَّفَرِ، وَكَآبَةِ الْمُنْقَلَبِ، وَالْحَوْرِ بَعْدَ الْكَوْرِ، وَدَعْوَةِ الْمَظْلُومِ، وَسُوءِ الْمَنْظَرِ فِي الْأَهْلِ وَالْمَالِ

Yaa Allaah! Hakika mimi najikinga Kwako kutokana na mashaka ya safari, na huzuni ya marejeo, na kupungua baada ya kuzidi, na Du'aa ya aliyedhulumiwa, na mandhari mbaya katika ahli na mali.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1748
Hadiyth
2714

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْبَارِقِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا سَافَرَ فَرَكِبَ رَاحِلَتَهُ، كَبَّرَ ثَلَاثًا وَيَقُولُ: "{سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ}. اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِي سَفَرِي هَذَا الْبِرَّ وَالتَّقْوَى، وَمِنْ الْعَمَلِ مَا تَرْضَى. اللَّهُمَّ هَوِّنْ عَلَيْنَا السَّفَرَ، وَاطْوِ لَنَا بُعْدَ الْأَرْضِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الصَّاحِبُ فِي السَّفَرِ، وَالْخَلِيفَةُ فِي الْأَهْلِ، اللَّهُمَّ اصْحَبْنَا فِي سَفَرِنَا، وَاخْلُفْنَا فِي أَهْلِنَا بِخَيْرٍ"

Ametusimulia Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa 'Aliy bin 'Abdi-Allaah Al-Baariqiy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaposafiri, akapanda kipando chake, humtukuza Allaah mara tatu, na husema:

سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ وَإِنَّا إِلَى رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ

Utakasifu ni wa (Allaah) Ambaye Ametutiishia haya, na tusingeliweza wenyewe kumdhibiti. Na hakika kwa Rabb wetu, bila shaka tutarejea. [Az-Zukhruf (43:13-14)]

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ فِي سَفَرِي هَذَا الْبِرَّ وَالتَّقْوَى، وَمِنْ الْعَمَلِ مَا تَرْضَى. اللَّهُمَّ هَوِّنْ عَلَيْنَا السَّفَرَ، وَاطْوِ لَنَا بُعْدَ الْأَرْضِ، اللَّهُمَّ أَنْتَ الصَّاحِبُ فِي السَّفَرِ، وَالْخَلِيفَةُ فِي الْأَهْلِ، اللَّهُمَّ اصْحَبْنَا فِي سَفَرِنَا، وَاخْلُفْنَا فِي أَهْلِنَا بِخَيْرٍ

Yaa Allaah! Hakika mimi nakuomba katika safari yangu hii wema na taqwa, na katika amali yale Unayoyaridhia. Yaa Allaah! Turahisishie safari, na Utufupishie umbali wa ardhi. Yaa Allaah! Wewe Ndiye Mwenzi katika safari, na Mshika nafasi (Mlinzi) kwa ahli. Yaa Allaah! Uwe Mwenzi wetu katika safari yetu, na Utushikie nafasi yetu kwa ahli zetu kwa kheri.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1749
Hadiyth
2715

43-Mlangoباب: ما يقول عند الصعود والهبوطMlango Wa Anayoyasema
Wakati Wa Kupanda (Mwinuko) Na Kushuka

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو زُبَيْدٍ، عَنْ حُصَيْنٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "كُنَّا إِذَا صَعِدْنَا، كَبَّرْنَا، وَإِذَا هَبَطْنَا، سَبَّحْنَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Zubayd, kutoka kwa Huswayn, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Tulikuwa tunapopanda (mwinuko), tunamtukuza Allaah; na tunaposhuka, tunamsabbih Allaah."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1750
Hadiyth
2716

44-Mlangoباب: في النهي عن الجرسMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Kengele

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِي الْجَرَّاحِ مَوْلَى أَمِّ حَبِيبَةَ، عَنْ أُمِّ حَبِيبَةَ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْعِيرُ الَّتِي فِيهَا الْجَرَسُ، لَا تَصْحَبُهَا الْمَلَائِكَة"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Abul-Jarraah mawlaa (mwachwa huru) wa Ummu Habiybah (رضي الله عنها), kutoka kwa Ummu Habiybah (رضي الله عنها), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Msafara (wa ngamia) ambao ndani yake mna kengele, Malaika (عليهم السلام) hawaandamani nao."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1751
Hadiyth
2717

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، حَدَّثَنَا سُهَيْلُ بْنُ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا تَصْحَبُ الْمَلَائِكَةُ رِفْقَةً فِيهَا كَلْبٌ، أَوْ جَرَسٌ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Zuhayr, ametusimulia Suhayl bin Abiy Swaalih, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Malaika (عليهم السلام) hawaandamani na kundi la wasafiri ambalo ndani yake mna mbwa au kengele."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1751
Hadiyth
2718

45-Mlangoباب: النهي عن لعن الدوابMlango Wa Makatazo Ya Kuwalaani Wanyama Wa Kupanda

أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ فِي سَفَرٍ، فَسَمِعَ لَعْنَةً، فَقَالَ: "مَا هَذَا؟". قَالُوا: فُلَانَةُ لَعَنَتْ رَاحِلَتَهَا. فَقَالَ: "ضَعُوا عَنْهَا فَإِنَّهَا مَلْعُونَةٌ". قَالَ: فَوَضَعُوا عَنْهَا. قَالَ عِمْرَانُ: كَأَنِّي أَنْظُرُ إِلَيْهَا نَاقَةً وَرْقَاءَ

Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhallab, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa safarini, akasikia laana. Akasema: "Ni nini hiki?" Wakasema: Fulani (mwanamke) amemlaani ngamia wake wa kupanda. Akasema: "Mteremsheni (mizigo yake), kwani yeye amelaaniwa." Amesema: Wakamteremshia (mizigo yake). 'Imraan (رضي الله عنه) amesema: Ni kama kwamba ninamtazama — ngamia jike mwenye rangi ya kijivu.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1751
Hadiyth
2719

46-Mlangoباب: لا تسافر المرأة إلا ومعها محرمMlango Wa Mwanamke Asisafiri Ila Akiwa
Pamoja Na Mahram (Ndugu Asiyeruhusiwa Kumuoa)

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تُسَافِرِ الْمَرْأَةُ سَفَرًا ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ فَصَاعِدًا إِلَّا وَمَعَهَا أَبُوهَا، أَوْ أَخُوهَا، أَوْ زَوْجُهَا، أَوْ ذُو مَحْرَمٍ مِنْهَا"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Sa'iyd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanamke asisafiri safari ya siku tatu na zaidi, ila akiwa pamoja na baba yake, au kaka yake, au mume wake, au mahram (ndugu asiyeruhusiwa kumuoa) wake."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1752
Hadiyth
2720

47-Mlangoباب: إن الواحد في السفر شيطانMlango Wa Hakika Mmoja (Peke Yake) Safarini Ni Shaytwaan

أَخْبَرَنَا الْهَيْثَمُ بْنُ جَمِيلٍ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ هُوَ: ابْنُ مُحَمَّدٍ الْعُمَرِيُّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْ يَعْلَمُ النَّاسُ مَا فِي الْوَحْدَةِ، لَمْ يَسْرِ رَاكِبٌ بِلَيْلٍ وَحْدَهُ أَبَدًا"

Ametukhabarisha Al-Haytham bin Jamiyl, ametusimulia 'Aaswim — naye ni Ibn Muhammad Al-'Umariy —, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Lau watu wangejua yaliyomo katika upweke, asingesafiri usiku mpanda (kipando) peke yake kamwe."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1753
Hadiyth
2721

48-Mlangoباب: ما يقول إذا نزل منزلاMlango Wa Anayoyasema Anaposhukia Mahali (Safarini)

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ إِسْحَاق، وَعَفَّانُ، قَالَا: حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَجْلانَ، عَنْ يَعْقُوبَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الْأَشَجِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ سَعْدِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ خَوْلَةَ بِنْتِ حَكِيمٍ، قَالَتْ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَوْ أَنَّ أَحَدَكُمْ إِذَا نَزَلَ مَنْزِلًا، قَالَ: أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ، لَمْ يَضُرَّهُ فِي ذَلِكَ الْمَنْزِلِ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْهُ"

Ametukhabarisha Ahmad bin Is-haaq na 'Affaan, wamesema: Ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Muhammad bin 'Ajlaan, kutoka kwa Ya'quwb bin 'Abdi-Allaah bin Al-Ashajj, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Sa'd bin Maalik (رضي الله عنه), kutoka kwa Khawlah bint Hakiym (رضي الله عنها), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Lau mmoja wenu anaposhukia mahali angesema:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

Najikinga kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia kutokana na shari ya Alivyoviumba,

hakuna kitu kingemdhuru mahali hapo mpaka aondoke hapo."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1753
Hadiyth
2722

49-Mlangoباب: في الركعتين إذا نزل منزلاMlango Wa Kuhusu Rakaa Mbili Anaposhukia Mahali

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ "إِذَا نَزَلَ مَنْزِلًا، لَمْ يَرْتَحِلْ مِنْهُ حَتَّى يُصَلِّيَ رَكْعَتَيْنِ، أَوْ يُوَدِّعَ الْمَنْزِلَ بِرَكْعَتَيْنِ". قَالَ عَبْد اللَّهِ: عُثْمَانُ بْنُ سَعْدٍ ضَعِيفٌ

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa 'Uthmaan bin Sa'd, kutoka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa "anaposhukia mahali, haondoki hapo mpaka aswali Rakaa mbili, au aage mahali hapo kwa Rakaa mbili."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: 'Uthmaan bin Sa'd ni Dhwa'iyf (Dhaifu).

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1755
Hadiyth
2723

50-Mlangoباب: ما يقول إذا قفل من السفرMlango Wa Anayoyasema Anaporejea Kutoka Safarini

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْبَارِقِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا رَجَعَ مِنْ سَفَرِهِ، قَالَ: "آيِبُونَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَائِبُونَ عَابِدُونَ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa 'Aliy bin 'Abdi-Allaah Al-Baariqiy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anaporejea kutoka safari yake, husema:

آيِبُونَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَائِبُونَ عَابِدُونَ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ

Tunarejea — Akipenda Allaah —, tukitubia, tukiabudu, tukimhimidi Rabb wetu.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1755
Hadiyth
2724

51-Mlangoباب: الدعاء عند النومMlango Wa Du'aa Wakati Wa Kulala

أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: حَدَّثَنَا أَبُو إِسْحَاق، قَالَ: سَمِعْتُ الْبَرَاءَ بْنَ عَازِبٍ، يَقُولُ: إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ رَجُلًا إِذَا أَخَذَ مَضْجَعَهُ أَنْ يَقُولَ: "اللَّهُمَّ أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ، وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ، وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ، لَا مَلْجَأَ وَلَا مَنْجَى مِنْكَ إِلَّا إِلَيْكَ، آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ، وَنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ، فَإِنْ مَاتَ، مَاتَ عَلَى الْفِطْرَةِ"

Ametukhabarisha Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, amesema: Ametusimulia Abuw Is-haaq, amesema: Nilimsikia Al-Baraa bin 'Aazib (رضي الله عنهما) akisema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimwamrisha mtu mmoja, anapochukua mahali pake pa kulala, aseme: "

اللَّهُمَّ أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ، وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ، وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ، وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ، رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ، لَا مَلْجَأَ وَلَا مَنْجَى مِنْكَ إِلَّا إِلَيْكَ، آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ، وَنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ

Yaa Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako, na nimeuelekeza uso wangu Kwako, na nimekuachia jambo langu, na nimeutegemeza mgongo wangu Kwako, kwa matumaini na kwa kuogopa Kwako. Hapana pa kukimbilia wala pa kuokokea kutoka Kwako isipokuwa Kwako. Nimekiamini Kitabu Chako Ulichokiteremsha, na Nabiy Wako Uliyemtuma.

Basi akifa, atakufa juu ya Fitwrah (maumbile ya asili)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1756
Hadiyth
2725

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي سَعِيدٍ الْمَقْبُرِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا أَوَى أَحَدُكُمْ إِلَى فِرَاشِهِ، فَلْيَنْفُضْ فِرَاشَهُ بِدَاخِلَةِ إِزَارِهِ، فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي مَا خَلَفَهُ فِيهِ، وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ بِكَ وَضَعْتُ جَنْبِي، وَبِكَ أَرْفَعُهُ، اللَّهُمَّ إِنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِي، فَاغْفِرْ لَهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا، فَاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Sa'iyd Al-Maqburiy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu anapokwenda kitandani mwake, basi akung'ute tandiko lake kwa upande wa ndani wa izari yake, kwani yeye hajui ni nini kilichokuja baada yake juu ya (tandiko) hilo. Na aseme:

اللَّهُمَّ بِكَ وَضَعْتُ جَنْبِي، وَبِكَ أَرْفَعُهُ، اللَّهُمَّ إِنْ أَمْسَكْتَ نَفْسِي، فَاغْفِرْ لَهَا، وَإِنْ أَرْسَلْتَهَا، فَاحْفَظْهَا بِمَا تَحْفَظُ بِهِ عِبَادَكَ الصَّالِحِينَ

Yaa Allaah! Kwa (Msaada) Wako nimeuweka ubavu wangu, na kwa (Msaada) Wako nitauinua. Yaa Allaah! Ukiizuilia nafsi yangu (Ukaifisha), basi Ighufurie; na Ukiiachilia, basi Ihifadhi kwa kile Unachowahifadhi nacho Swaalihina (Waja wema) Wako."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1756
Hadiyth
2726

52-Mlangoباب: في التسبيح عند النومMlango Wa Kuhusu Tasbiyh (Kusema: Subhaana-Allaah)
Wakati Wa Kulala

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْعَوَّامُ بْنُ حَوْشَبٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ مُرَّةَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: أَتَانَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَتَّى وَضَعَ قَدَمَهُ بَيْنِي وَبَيْنَ فَاطِمَةَ، فَعَلَّمَنَا مَا نَقُولُ إِذَا أَخَذْنَا مَضَاجِعَنَا: "ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ تَسْبِيحَةً، وَثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ تَحْمِيدَةً، وَأَرْبَعًا وَثَلَاثِينَ تَكْبِيرَةً". قَالَ عَلِيٌّ: فَمَا تَرَكْتُهَا بَعْدُ. فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: وَلَا لَيْلَةَ صِفِّينَ؟. قَالَ: وَلَا لَيْلَةَ صِفِّينَ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-'Awwaam bin Hawshab, amesema: Amenisimulia 'Amr bin Murrah, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alitujia mpaka akaweka mguu wake baina yangu na baina ya Faatwimah (رضي الله عنها), akatufundisha tunayoyasema tunapochukua mahali petu pa kulala: "Tasbiyh (kusema: Subhaana-Allaah) thelathini na tatu, na Tahmiyd (kusema: Al-Hamdu li-Allaah) thelathini na tatu, na Takbiyrah (kusema: Allaah Ni Mkubwa zaidi) thelathini na nne." 'Aliy (رضي الله عنه) amesema: "Sikuziacha baada ya hapo." Mtu mmoja akamwambia: Hata usiku wa (vita vya) Swiffiyn? Akasema: "Hata usiku wa Swiffiyn."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1757
Hadiyth
2727

53-Mlangoباب: ما يقول إذا انتبه من نومهMlango Wa Anayoyasema Anapoamka Kutoka Usingizini

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ رِبْعِيِّ بْنِ حِرَاشٍ، عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اسْتَيْقَظَ. قَالَ: "الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Rib'iy bin Hiraash, kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoamka, husema:

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَحْيَانَا بَعْدَ مَا أَمَاتَنَا، وَإِلَيْهِ النُّشُورُ

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametupa uhai baada ya kutufisha, na ni Kwake tu kufufuliwa.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1758
Hadiyth
2728

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْحِزَامِيُّ، حَدَّثَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، قَالَ: حَدَّثَنِي عُمَيْرُ بْنُ هَانِئٍ الْعَنْسِيُّ، قَالَ: حَدَّثَنِي جُنَادَةُ بْنُ أَبِي أُمَيَّةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ تَعَارَّ مِنَ اللَّيْلِ، فَقَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ". ثُمَّ قَالَ: "رَبِّ اغْفِرْ لِي أَوْ قَالَ: ثُمَّ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى تُقُبِّلَتْ صَلَاتُهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Al-Hizaamiy, ametusimulia Al-Waliyd bin Muslim, ametusimulia Al-Awzaa'iy, amesema: Amenisimulia 'Umayr bin Haaniy Al-'Ansiy, amesema: Amenisimulia Junaadah bin Abiy Umayyah, amesema: Amenisimulia 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayeamka usiku (akigeuka kitandani), akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, Hana mshirika; ni Wake ufalme, na ni Zake Himdi, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Utakasifu ni wa Allaah, na Himdi zote ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah Ni Mkubwa zaidi, na hapana uwezo wala nguvu ila kwa (msaada wa) Allaah.

Kisha akasema:

رَبِّ اغْفِرْ لِي

Rabb wangu! Nighufurie.

— au alisema: Kisha akaomba Du'aa —, atajibiwa. Na akiazimia, akatawadha, kisha akaswali, Swalaah yake itakubaliwa."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1758
Hadiyth
2729

54-Mlangoباب: ما يقول إذا أصبحMlango Wa Anayoyasema Anapoingia Asubuhi

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَصْبَحَ. قَالَ: "أَصْبَحْنَا عَلَى فِطْرَةِ الْإِسْلَامِ، وَكَلِمَةِ الْإِخْلَاصِ، وَدِينِ نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَمِلَّةِ أَبِينَا إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا مُسْلِمًا"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Abzaa, kutoka kwa baba yake ['Abdur-Rahmaan bin Abzaa (رضي الله عنه)], amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa anapoingia asubuhi, husema:

أَصْبَحْنَا عَلَى فِطْرَةِ الْإِسْلَامِ، وَكَلِمَةِ الْإِخْلَاصِ، وَدِينِ نَبِيِّنَا مُحَمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَمِلَّةِ أَبِينَا إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا مُسْلِمًا

Tumeingia asubuhi na maumbile ya Kiislamu, na neno la ikhlaasw (kumtakasia Allaah ibada), na Dini ya Nabiy wetu Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na mila (Dini) ya baba yetu Ibraahiym (عليه السلام) aliyejiengua na dini potofu akashika Dini ya haki, na hali ya kuwa Muislamu.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1760
Hadiyth
2730

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ يَعْلَى بْنِ عَطَاءٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ أَبُو بَكْرٍ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مُرْنِي بِشَيْءٍ أَقُولُهُ إِذَا أَصْبَحْتُ وَإِذَا أَمْسَيْتُ. قَالَ: "قُلْ: اللَّهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِي، وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطَانِ وَشِرْكِهِ". قَالَ: "قُلْهُ إِذَا أَصْبَحْتَ وَإِذَا أَمْسَيْتَ، وَإِذَا أَخَذْتَ مَضْجَعَكَ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Ya'laa bin 'Atwaa, kutoka kwa 'Amr bin 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Abuw Bakr (رضي الله عنه) amesema: Yaa Rasula-Allaah, niamrishe kitu nikiseme ninapoingia asubuhi na ninapoingia jioni. Akasema: "Sema:

اللَّهُمَّ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، عَالِمَ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ، رَبَّ كُلِّ شَيْءٍ وَمَلِيكَهُ، أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ نَفْسِي، وَمِنْ شَرِّ الشَّيْطَانِ وَشِرْكِهِ

Yaa Allaah! Mwanzilishi wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa ghaibu na dhahiri, Rabb wa kila kitu na Mfalme wake. Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nafsi yangu, na kutokana na shari ya shaytwaan na shirki yake."

Akasema: "Yaseme unapoingia asubuhi, na unapoingia jioni, na unapochukua mahali pako pa kulala."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1760
Hadiyth
2731

55-Mlangoباب: ما يقول إذا لبس ثوباMlango Wa Anayoyasema Anapovaa Nguo

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ الْمُقْرِئُ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ: ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي مَرْحُومٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ مُعَاذِ بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ لَبِسَ ثَوْبًا، فَقَالَ: الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَسَانِي هَذَا وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلَا قُوَّةٍ، غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd Al-Muqriu, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb —, kutoka kwa Abuw Marhuwm, kutoka kwa Sahl bin Mu'aadh bin Anas, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayevaa nguo, akasema:

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي كَسَانِي هَذَا وَرَزَقَنِيهِ مِنْ غَيْرِ حَوْلٍ مِنِّي وَلَا قُوَّةٍ

Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Amenivisha (nguo) hii, na Akaniruzuku pasina uwezo kutoka kwangu wala nguvu,

ataghufuriwa yaliyotangulia katika dhambi zake."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1761
Hadiyth
2732

56-Mlangoباب: ما يقول إذا دخل المسجد وإذا خرجMlango Wa Anayoyasema Anapoingia Msikitini Na Anapotoka

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْلَمَةَ، حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ يَعْنِي: ابْنَ بِلَالٍ، عَنْ رَبِيعَةَ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ أَوْ أَبِي أُسَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمْ الْمَسْجِدَ، فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ، فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Maslamah, ametusimulia Sulaymaan — yaani: Ibn Bilaal —, kutoka kwa Rabiy'ah, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Humayd au Abuw Usayd (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu anapoingia Msikitini, basi aseme:

اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ

Yaa Allaah, Nifungulie milango ya Rehma Zako.

Na anapotoka, basi aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ

Yaa Allaah, hakika mimi nakuomba katika Fadhila Zako."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1761
Hadiyth
2733

57-Mlangoباب: ما يقول إذا دخل السوقMlango Wa Anayoyasema Anapoingia Sokoni

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَزْهَرُ بْنُ سِنَانٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ وَاسِعٍ، قَالَ: قَدِمْتُ مَكَّةَ فَلَقِيتُ بِهَا أَخِي سَالِمَ بْنَ عَبْدِ اللَّهِ فَحَدَّثَنِي، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ دَخَلَ السُّوقَ، فَقَالَ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، يُحْيِي وَيُمِيتُ، وَهُوَ حَيٌّ لَا يَمُوتُ، بِيَدِهِ الْخَيْرُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، كَتَبَ اللَّهُ لَهُ أَلْفَ أَلْفِ حَسَنَةٍ، وَمَحَا عَنْهُ أَلْفَ أَلْفِ سَيِّئَةٍ، وَرَفَعَ لَهُ أَلْفَ أَلْفِ دَرَجَةٍ". قَالَ: فَقَدِمْتُ خُرَاسَانَ فَلَقِيتُ قُتَيْبَةَ بْنَ مُسْلِمٍ، فَقُلْتُ: إِنِّي أَتَيْتُكَ بِهَدِيَّةٍ، فَحَدَّثْتُهُ، فَكَانَ يَرْكَبُ فِي مَوْكِبِهِ فَيَأْتِي السُّوقَ، فَيَقُومُ، فَيَقُولُهَا ثُمَّ يَرْجِعُ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Azhar bin Sinaan, kutoka kwa Muhammad bin Waasi', amesema: Niliingia Makkah, nikakutana humo na ndugu yangu Saalim bin 'Abdi-Allaah, akanisimulia kutoka kwa baba yake ['Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما)], kutoka kwa babu yake ['Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه)], kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeingia sokoni, akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، يُحْيِي وَيُمِيتُ، وَهُوَ حَيٌّ لَا يَمُوتُ، بِيَدِهِ الْخَيْرُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, Hana mshirika; ni Wake ufalme, na ni Zake Himdi, Anahuisha na Anafisha, Naye ni Hai, Hafi; kheri imo Mkononi Mwake, Naye juu ya kila kitu ni Muweza,

Allaah Atamwandikia mema elfu elfu (milioni moja), na Atamfutia maovu elfu elfu, na Atamnyanyulia daraja elfu elfu." Amesema: Kisha nikaingia Khuraasaan, nikakutana na Qutaybah bin Muslim, nikasema: Hakika mimi nimekujia na zawadi. Nikamsimulia (Hadiyth hii). Basi akawa anapanda katika msafara wake, anakuja sokoni, anasimama, anayasema (maneno hayo), kisha anarudi.

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1762
Hadiyth
2734

58-Mlangoباب: تسموا باسمي، ولا تكتنوا بكنيتيMlango Wa Jiiteni Kwa Jina Langu, Wala Msijiite
Kwa Kunyah (Jina La Heshima: Baba Wa Fulani) Yangu

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "تَسَمُّوا بِاسْمِي وَلَا تَكْتَنُوا بِكُنْيَتِي"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Jiiteni kwa jina langu, wala msijiite kwa kunyah (jina la heshima: baba wa fulani) yangu."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1765
Hadiyth
2735

59-Mlangoباب: في حسن الأسماءMlango Wa Kuhusu Uzuri Wa Majina

حَدَّثَنَا عَفَّانُ بْنُ مُسْلِمٍ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَنْبَأَنَا دَاوُدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي زَكَرِيَّا الْخُزَاعِيِّ، عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّكُمْ تُدْعَوْنَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِأَسْمَائِكُمْ وَأَسْمَاءِ آبَائِكُمْ، فَأَحْسِنُوا أَسْمَاءَكُمْ"

Ametusimulia 'Affaan bin Muslim, ametusimulia Hushaym, ametupa khabari Daawuwd bin 'Amr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Zakariyyaa Al-Khuzaa'iy, kutoka kwa Abud-Dardaa (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika nyinyi mtaitwa Siku ya Qiyaamah kwa majina yenu na majina ya baba zenu; basi yafanyeni mazuri majina yenu."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1766
Hadiyth
2736

60-Mlangoباب: ما يستحب من الأسماءMlango Wa Yanayopendekezwa Katika Majina

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ كَثِيرٍ، أَنْبَأَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَحَبُّ الْأَسْمَاءِ إِلَى اللَّهِ: عَبْدُ اللَّهِ، وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Kathiyr, ametupa khabari 'Ubaydu-Allaah bin 'Umar, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Majina yanayopendwa zaidi na Allaah ni: 'Abdu-Allaah (Mja wa Allaah), na 'Abdur-Rahmaan (Mja wa Ar-Rahmaan)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1766
Hadiyth
2737

61-Mlangoباب: ما يكره من الأسماءMlango Wa Yanayochukiza Katika Majina

أَخْبَرَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ الرُّكَيْنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ سَمُرَةَ: أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ "نَهَى أَنْ نُسَمِّيَ أَرِقَّاءَنَا أَرْبَعَةَ أَسْمَاءٍ: أَفْلَحُ، وَنَافِعٌ، وَرَبَاحٌ، وَيَسَارٌ"

Ametukhabarisha Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa Ar-Rukayn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Samurah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alikataza tuwaite watumwa wetu majina manne: Aflah (mwenye kufaulu zaidi), na Naafi' (mwenye kunufaisha), na Rabaah (faida), na Yasaar (wepesi)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1767
Hadiyth
2738

62-Mlangoباب: في تغيير الأسماءMlango Wa Kuhusu Kubadilisha Majina

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ هُوَ: ابْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ: أَنَّ أُمَّ عَاصِمٍ كَانَ يُقَالُ لَهَا عَاصِيَةُ، "فَسَمَّاهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَمِيلَةَ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad — naye ni Ibn Salamah —, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), kwamba Ummu 'Aaswim (رضي الله عنها) alikuwa akiitwa 'Aaswiyah (mwasi), "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita Jamiylah (mzuri)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1768
Hadiyth
2739

حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا عَطَاءُ بْنُ أَبِي مَيْمُونَةَ، عَنْ أَبِي رَافِعٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قالَ: كَانَ اسْمُ زَيْنَبَ، بَرَّةَ، "فَسَمَّاهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَيْنَبَ"

Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa bin Sa'iyd, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia 'Atwaa bin Abiy Maymuwnah, kutoka kwa Abuw Raafi', kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Jina la Zaynab (رضي الله عنها) lilikuwa Barrah (mwema mno), "Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwita Zaynab."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1768
Hadiyth
2740

63-Mlangoباب: في النهي عن أن يقول: ما شاء الله وشاء فلانMlango Wa Kuhusu Katazo La Kusema: Alitakalo Allaah
Na Akataka Fulani

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ رِبْعِيِّ بْنِ حِرَاشٍ، عَنِ الطُّفَيْلِ أَخِي عَائِشَةَ، قَالَ: قَالَ رَجُلٌ مِنَ الْمُشْرِكِينَ لِرَجُلٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ: نِعْمَ الْقَوْمُ أَنْتُمْ لَوْلَا أَنَّكُمْ تَقُولُونَ: مَا شَاءَ اللَّهُ، وَشَاءَ مُحَمَّدٌ. فَسَمِعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "لَا تَقُولُوا: مَا شَاءَ اللَّهُ وَشَاءَ مُحَمَّدٌ، وَلَكِنْ، قُولُوا: مَا شَاءَ اللَّهُ، ثُمَّ شَاءَ مُحَمَّدٌ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Rib'iy bin Hiraash, kutoka kwa Atw-Twufayl (رضي الله عنه) — ndugu wa 'Aaishah (رضي الله عنها) —, amesema: Mtu mmoja miongoni mwa washirikina alimwambia mtu mmoja miongoni mwa Waislamu: Nyinyi ni watu wazuri mno, lau si kwamba mnasema: Alitakalo Allaah, na akataka Muhammad. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasikia, akasema: "Msiseme: Alitakalo Allaah na akataka Muhammad; lakini semeni: Alitakalo Allaah, kisha akataka Muhammad."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1769
Hadiyth
2741

64-Mlangoباب: لا يقال للعنب: الكرمMlango Wa Zabibu Kutoitwa Karm
(Neno Lenye Maana Ya Ukarimu)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدٌ هُوَ: ابْنُ إِسْحَاق، عَنْ صَالِحِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْأَعْرَجِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَقُولُوا لِحَائِطِ الْعِنَبِ الْكَرْمُ، إِنَّمَا الْكَرْمُ الرَّجُلُ الْمُسْلِمُ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad — naye ni Ibn Is-haaq —, kutoka kwa Swaalih bin Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan Al-A'raj, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiiite bustani ya mizabibu karm (neno lenye maana ya ukarimu); hakika karm ni mtu Muislamu."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1770
Hadiyth
2742

65-Mlangoباب: في المزاحMlango Wa Kuhusu Mzaha

حَدَّثَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدٍ، عَنِ أَنَسٍ، قَالَ: كَانَ غُلَامٌ يَسُوقُ بِأَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَا أَنْجَشَةُ، رُوَيْدًا سَوْقَكَ بِالْقَوَارِيرِ"

Ametusimulia Abuw 'Aaswim, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Ubayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Kijana mmoja alikuwa akiwaendesha (ngamia waliowabeba) wake wa Nabiy صلى الله عليه وآله وسلم رضي الله عنهن. (Nabiy) akasema: "Yaa Anjashah, punguza mwendo wako unapowaendesha vyombo vya kioo (yaani wanawake)."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1770
Hadiyth
2743

66-Mlangoباب: في الذي يكذب ليضحك به القومMlango Wa Kuhusu Anayesema Uongo Ili Awachekeshe Watu

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَخْبَرَنَا بَهْزُ بْنُ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "وَيْلٌ لِلَّذِي يُحَدِّثُ فَيَكْذِبُ لِيُضْحِكَ بِهِ الْقَوْمَ، وَيْلٌ لَهُ! وَيْلٌ لَهُ!"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametukhabarisha Bahz bin Hakiym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake [Mu'aawiyah bin Haydah (رضي الله عنه)], amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Ole wake yule anayezungumza akasema uongo ili awachekeshe watu kwa (maneno) hayo! Ole wake! Ole wake!"

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1771
Hadiyth
2744

67-Mlangoباب: في الشعرMlango Wa Kuhusu Ushairi

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبْدَةُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ يَعْقُوبَ بْنِ عُتْبَةَ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: صَدَّقَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُمَيَّةَ بْنَ أَبِي الصَّلْتِ فِي بَيْتَيْنِ مِنْ شِعْرِهِ، فَقَالَ: رَجُلٌ وَثَوْرٌ تَحْتَ رِجْلِ يَمِينِهِ وَالنَّسْرُ لِلْأُخْرَى وَلَيْثٌ مُرْصَدُ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "صَدَقَ". قَالَ: وَالشَّمْسُ تَطْلُعُ كُلَّ آخِرِ لَيْلَةٍ حَمْرَاءَ يُصْبِحُ لَوْنُهَا يَتَوَرَّدُ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "صَدَقَ". فَقَالَ قَائِلٌ: تَأْبَى فَمَا تَطْلُعُ لَنَا فِي رِسْلِهَا إِلَّا مُعَذَّبَةً وَإِلَّا تُجْلَدُ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "صَدَقَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abdah bin Sulaymaan, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Ya'quwb bin 'Utbah, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsadikisha Umayyah bin Abiy Asw-Swalt katika beti mbili za ushairi wake. (Umayyah) alisema: Mtu na fahali chini ya mguu wake wa kulia, na tai kwa (mguu) mwingine, na simba aliye tayari kuvizia. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Amesema kweli." Akasema: Na jua huchomoza mwishoni mwa kila usiku likiwa jekundu, rangi yake huwa ya waridi asubuhi. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Amesema kweli." Msemaji mmoja akasema: Linakataa (kuchomoza), halituchomozei kwa upole wake, isipokuwa likiwa linaadhibiwa, na isipokuwa likichapwa mijeledi. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Amesema kweli."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1772
Hadiyth
2745

68-Mlangoباب: في إن من الشعر حكمةMlango Wa Kuhusu: Hakika Katika Ushairi Kuna Hekima

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ زِيَادٍ هُوَ: ابْنُ سَعْدٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَنَّ ابْنَ شِهَابٍ، أَخْبَرَهُ عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ الْأَسْوَدِ بْنِ عَبْدِ يَغُوثَ، عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ مِنَ الشِّعْرِ حِكْمَةً"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ziyaad — naye ni Ibn Sa'd —, amesema: Amenikhabarisha kwamba Ibn Shihaab alimkhabarisha, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdir-Rahmaan bin Hishaam, kutoka kwa Marwaan bin Al-Hakam, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Al-Aswad bin 'Abdi Yaghuwth, kutoka kwa Ubayy bin Ka'b (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika katika ushairi kuna hekima."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1773
Hadiyth
2746

69-Mlangoباب: لأن يمتلئ جوف أحدكمMlango Wa Kujaa Tumbo La Mmoja Wenu [Usaha
Au Damu Ni Bora Kwake Kuliko Kujaa Mashairi]

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، حَدَّثَنَا حَنْظَلَةُ، عَنْ سَالِمٍ عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لَأَنْ يَمْتَلِئَ جَوْفُ أَحَدِكُمْ قَيْحًا أَوْ دَمًا خَيْرٌ لَهُ مِنْ أَنْ يَمْتَلِئَ شِعْرًا "

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, ametusimulia Handhwalah, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika tumbo la mmoja wenu kujaa usaha au damu ni bora kwake kuliko kujaa mashairi."

Mjalada
3
Kitabu
19
Ukurasa
1774
Hadiyth
2747