ومن كتاب الرقاق
1-Mlangoباب: من يرد الله به خيرا، يفقهه في الدينMlango Wa Atakayemtakia Allaah Kheri, Humfahamisha Dini
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ جَعْفَرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَعِيدِ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا، يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ"
Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Ja'far, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd bin Abiy Hind, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayemtakia Allaah kheri, Humfahamisha Dini."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1777
- Hadiyth
- 2748
2-Mlangoباب: ما جاء في الصحة والفراغMlango Wa Yaliyopokewa Kuhusu Afya Na Faragha
أَخْبَرَنَا الْمَكِّيُّ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ هُوَ: ابْنُ سَعِيدٍ، أَنَّهُ سَمِعَ أَبَاهُ يُحَدِّثُ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الصِّحَّةَ وَالْفَرَاغَ نِعْمَتَانِ مِنْ نِعَمِ اللَّهِ، مَغْبُونٌ فِيهِمَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ"
Ametukhabarisha Al-Makkiy bin Ibraahiym, ametusimulia 'Abdu-Allaah — naye ni Ibn Sa'iyd —, kwamba alimsikia baba yake akisimulia, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika afya na faragha ni Neema mbili miongoni mwa Neema za Allaah, ambazo wengi miongoni mwa watu wamepunjika ndani yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1777
- Hadiyth
- 2749
3-Mlangoباب: في حفظ السمعMlango Wa Kuhusu Kuhifadhi Kusikia
أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدٌ يَعْنِي: ابْنَ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنِ اسْتَمَعَ إِلَى حَدِيثِ قَوْمٍ وَهُمْ لَهُ كَارِهُونَ، صُبَّ فِي أُذُنِهِ الْآنُكُ"
Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid — yaani: Ibn 'Abdi-Allaah —, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayesikiliza mazungumzo ya watu, nao wanachukia (asikilize), atamiminiwa risasi iliyoyeyushwa ndani ya sikio lake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1779
- Hadiyth
- 2750
أَخْبَرَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ أَبِي الطُّفَيْلِ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تُتْبِعِ النَّظْرَةَ النَّظْرَةَ، فَإِنَّ الْأُولَى لَكَ، وَالْآخِرَةَ عَلَيْكَ"
Ametukhabarisha Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Muhammad bin Ibraahiym, kutoka kwa Salamah bin Abitw-Twufayl, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Usiufuatishe mtazamo (wa kwanza) kwa mtazamo (mwingine); kwani wa kwanza ni wako, na wa mwisho ni dhidi yako."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1779
- Hadiyth
- 2751
4-Mlangoباب: في حفظ اللسانMlango Wa Kuhusu Kuhifadhi Ulimi
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ يَعْلَى بْنِ عَطَاءٍ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ أَخْبِرْنِي بِعَمَلٍ فِي الْإِسْلَامِ لَا أَسْأَلُ عَنْهُ أَحَدًا. قَالَ: "اتَّقِ اللَّهَ، ثُمَّ اسْتَقِمْ". قَالَ: قُلْتُ: ثُمَّ أَيُّ شَيْءٍ؟. قَالَ: فَأَشَارَ إِلَى لِسَانِهِ
Ametukhabarisha Sa'iyd bin Ar-Rabiy', ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Ya'laa bin 'Atwaa, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin Sufyaan, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, nijulishe amali katika Islaam ambayo sitamuuliza yeyote kuhusu hiyo. Akasema: "Mche Allaah, kisha simama imara." Akasema: Nikasema: Kisha kitu gani? Akasema: Akaashiria ulimi wake.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1780
- Hadiyth
- 2752
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ يَعْنِي: ابْنَ إِسْمَاعِيل بْنِ مُجَمِّعٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي ابْنُ شِهَابٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مُعَاذٍ، عَنْ سُفْيَانَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ مُرْنِي بِأَمْرٍ أَعْتَصِمُ بِهِ. قَالَ: "قُلْ رَبِّيَ اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقِمْ". قَالَ: قُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ مَا أَكْثَرُ مَا تَخَوَّفُ عَلَيَّ؟. قَالَ: فَأَخَذَ نَبِيُّ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلِسَانِهِ ثُمَّ قَالَ: "هَذَا"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Ibraahiym — yaani: Ibn Ismaa'iyl bin Mujammi' —, amesema: Amenikhabarisha Ibn Shihaab, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Mu'aadh, kutoka kwa Sufyaan bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, niamrishe jambo nitakaloshikamana nalo. Akasema: "Sema: Rabb wangu ni Allaah, kisha simama imara." Akasema: Nikasema: Yaa Nabiyya-Allaah, ni kipi unachokikhofia zaidi juu yangu? Akasema: Nabiy wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akaushika ulimi wake, kisha akasema: "Huu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1780
- Hadiyth
- 2753
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ مِغْوَلٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُّ الْإِسْلَامِ أَفْضَلُ؟. قَالَ: "مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Maalik bin Mighwal, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Iliulizwa: Yaa Rasula-Allaah, Islaam ipi iliyo bora zaidi? Akasema: "(Ni ya) yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mkono wake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1781
- Hadiyth
- 2754
5-Mlangoباب: في الصمتMlango Wa Kuhusu Kunyamaza
أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُقْبَةَ، عَنْ يَزِيدَ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ الْحُبُلِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ صَمَتَ، نَجَا"
Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Uqbah, kutoka kwa Yaziyd bin 'Amr, kutoka kwa Abuw 'Abdir-Rahmaan Al-Hubuliy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr bin Al-'Aasw (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayenyamaza, ameokoka."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1781
- Hadiyth
- 2755
6-Mlangoباب: في الغيبةMlango Wa Kuhusu Ghiybah (Kusengenya)
أَخْبَرَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ الْعَلَاءِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قِيلَ لَهُ: مَا الْغِيبَةُ؟. قَالَ: "ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ". قِيلَ: وَإِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ؟. قَالَ: "فَإِنْ كَانَ فِيهِ، فَقَدْ اغْتَبْتَهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ، فَقَدْ بَهَتَّهُ"
Ametukhabarisha Nu'aym bin Hammaad, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, kutoka kwa Al-'Alaa, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba aliulizwa: Ni nini ghiybah (kusengenya)? Akasema: "Ni kumtaja kwako ndugu yako kwa jambo analolichukia." Ikasemwa: Na hata kama ndugu yangu yumo nalo ninalolisema? Akasema: "Ikiwa yumo nalo, basi umemsengenya; na ikiwa hayumo nalo, basi umemzulia uongo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1782
- Hadiyth
- 2756
7-Mlangoباب: في الكذبMlango Wa Kuhusu Uongo
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ إِدْرِيسَ الْأَوْدِيِّ، عَنْ أَبِي إِسْحَقَ، عَنْ أَبِي الْأَحْوَصِ: أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ يَرْفَعُ الْحَدِيثَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "إِنَّ شَرَّ الرَّوَايَا رَوَايَا الْكَذِبِ، وَلَا يَصْلُحُ مِنْ الْكَذِبِ جِدٌّ وَلَا هَزْلٌ. وَلَا يَعِدُ الرَّجُلُ ابْنَهُ ثُمَّ لَا يُنْجِزُ لَهُ: إِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ، وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ، وَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ، وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ، وَإِنَّهُ يُقَالُ لِلصَّادِقِ: صَدَقَ وَبَرَّ، وَيُقَالُ لِلْكَاذِبِ: كَذَبَ وَفَجَرَ. وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَصْدُقُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ صِدِّيقًا، وَيَكْذِبُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ كَذَّابًا". وَإِنَّهُ قَالَ: "لَنَا هَلْ أُنَبِّئُكُمْ مَا الْعَضْهُ؟ وَإِنَّ الْعَضْهَ: هِيَ النَّمِيمَةُ الَّتِي تُفْسِدُ بَيْنَ النَّاسِ"
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Idriys Al-Awdiy, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kwamba 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) — akiipandisha Hadiyth hadi kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) — amesema: "Hakika masimulizi maovu kabisa ni masimulizi ya uongo; na haifai katika uongo (kitu), si kwa dhati wala kwa mzaha; wala mtu asimuahidi mwanawe kisha asimtimizie. Hakika ukweli huongoza kwenye wema, na hakika wema huongoza kwenye Jannah (Pepo); na hakika uongo huongoza kwenye uovu, na hakika uovu huongoza kwenye moto. Na hakika mkweli huambiwa: Amesema kweli na amefanya wema; na muongo huambiwa: Amesema uongo na amefanya uovu. Na hakika mtu husema kweli mpaka huandikwa mbele ya Allaah kuwa mkweli kabisa, na husema uongo mpaka huandikwa mbele ya Allaah kuwa muongo kabisa." Na kwamba alituambia: "Je, niwajulishe ni nini al-'adhwh (uzushi mbaya)? Na hakika al-'adhwh ni kuchongea, kunakoharibu (mahusiano) baina ya watu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1783
- Hadiyth
- 2757
8-Mlangoباب: في حفظ اليدMlango Wa Kuhusu Kuhifadhi Mkono
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ عَمْرٍو، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Nilimsikia 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Muislamu ni yule ambaye Waislamu wamesalimika kutokana na ulimi wake na mkono wake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1785
- Hadiyth
- 2758
9-Mlangoباب: في أكل الطيبMlango Wa Kuhusu Kula Kilicho Kizuri
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْفُضَيْلُ بْنُ مَرْزُوقٍ، حَدَّثَنَا عَدِيُّ بْنُ ثَابِتٍ، عَنْ أَبِي حَازِمٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إِلَّا الطَّيِّبَ إِنَّ اللَّهَ أَمَرَ الْمُؤْمِنِينَ بِمَا أَمَرَ بِهِ الْمُرْسَلِينَ، قَالَ: {يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ}، وَقَالَ: {يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ}. قَالَ: ثُمَّ ذَكَرَ الرَّجُلَ يُطِيلُ السَّفَرَ أَشْعَثَ أَغْبَرَ يَمُدُّ يَدَيْهِ إِلَى السَّمَاءِ: يَا رَبِّ! يَا رَبِّ! وَمَطْعَمُهُ حَرَامٌ، وَمَلْبَسُهُ حَرَامٌ، وَمَشْرَبُهُ حَرَامٌ، وَغُذِّيَ بِالْحَرَامِ، فَأَنَّى يُسْتَجَابُ لِذَلِكَ؟"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Fudhwayl bin Marzuwq, ametusimulia 'Adiyy bin Thaabit, kutoka kwa Abuw Haazim, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Enyi watu! Hakika Allaah Ni Mzuri, Hakubali isipokuwa kizuri. Hakika Allaah Amewaamrisha Waumini yale Aliyowaamrisha Rusuli (عليهم السلام); Akasema":
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا إِنِّي بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
Enyi Rusuli! Kuleni katika vizuri na tendeni mema, hakika Mimi kwa yale myatendayo Ni Mjuzi. [Al-Muuminuwn (23:51)]
Na Akasema:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُلُوا مِنْ طَيِّبَاتِ مَا رَزَقْنَاكُمْ وَاشْكُرُوا لِلَّهِ إِنْ كُنْتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ
Enyi walioamini! Kuleni vizuri Tulivyokuruzukuni na mshukuruni Allaah mkiwa mnamwabudu Yeye Pekee. [Al-Baqarah (2:172)]
Akasema: "Kisha akamtaja mtu anayerefusha safari, mwenye nywele timtim na vumbi tupu, akinyoosha mikono yake mbinguni (akisema):
يَا رَبِّ! يَا رَبِّ
Yaa Rabbi! Yaa Rabbi!
Na hali chakula chake ni haraam, na mavazi yake ni haraam, na kinywaji chake ni haraam, na amelishwa kwa haraam; basi vipi ataitikiwa huyo?"
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1786
- Hadiyth
- 2759
10-Mlangoباب: ما يكفي من الدنياMlango Wa Kinachotosha Katika Dunia
حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ الْجُرَيْرِيِّ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَوَلَةَ، عَنْ بُرَيْدَةَ الْأَسْلَمِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَكْفِي أَحَدَكُمْ مِنَ الدُّنْيَا خَادِمٌ وَمَرْكَبٌ"
Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Al-Jurayriy, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mawalah, kutoka kwa Buraydah Al-Aslamiy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kinamtosha mmoja wenu katika dunia mtumishi na kipando."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1787
- Hadiyth
- 2760
11-Mlangoباب: في ذهاب الصالحينMlango Wa Kuhusu Kuondoka Kwa Swaalihina (Watu Wema)
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ مَنْصُورٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ بَيَانٍ هُوَ: ابْنُ بِشْرٍ الْأَحْمَسِيُّ، عَنْ قَيْسٍ، عَنْ مِرْدَاسٍ الْأَسْلَمِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَذْهَبُ الصَّالِحُونَ أَسْلَافًا وَيَبْقَى حُثَالَةٌ كَحُثَالَةِ الشَّعِيرِ"
Ametusimulia Sa'iyd bin Manswuwr, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Bayaan — naye ni Ibn Bishr Al-Ahmasiy —, kutoka kwa Qays, kutoka kwa Mirdaas Al-Aslamiy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Swaalihina (Watu wema) wataondoka mmoja baada ya mwingine, na watabakia takataka (za watu) kama takataka za shayiri."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1788
- Hadiyth
- 2761
12-Mlangoباب: في المحافظة على الصومMlango Wa Kuhusu Kuihifadhi Swawm
أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ عَمْرِو بْنِ أَبِي عَمْرٍو، عَنْ سَعِيدٍ الْمَقْبُرِيِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "كَمْ مِنْ صَائِمٍ لَيْسَ لَهُ مِنْ صِيَامِهِ إِلَّا الظَّمَأُ، وَكَمْ مِنْ قَائِمٍ لَيْسَ لَهُ مِنْ قِيَامِهِ إِلَّا السَّهَرُ"
Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiz-Zinaad, kutoka kwa 'Amr bin Abiy 'Amr, kutoka kwa Sa'iyd Al-Maqburiy, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Ni wangapi wenye kufunga Swawm ambao hawapati katika Swiyaam yao isipokuwa kiu; na ni wangapi wenye kusimama usiku (kuswali) ambao hawapati katika kisimamo chao isipokuwa kukesha."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1788
- Hadiyth
- 2762
13-Mlangoباب: في المحافظة على الصلاةMlango Wa Kuhusu Kuihifadhi Swalaah
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ: ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ، قَالَ: حَدَّثَنِي كَعْبُ بْنُ عَلْقَمَةَ، عَنْ عِيسَى بْنِ هِلَالٍ الصَّدَفِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ ذَكَرَ الصَّلَاةَ يَوْمًا، فَقَالَ: "مَنْ حَافَظَ عَلَيْهَا، كَانَتْ لَهُ نُورًا، وَبُرْهَانًا، وَنَجَاةً مِنَ النَّارِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، وَمَنْ لَمْ يُحَافِظْ عَلَيْهَا، لَمْ تَكُنْ لَهُ نُورًا، وَلَا نَجَاةً، وَلَا بُرْهَانًا، وَكَانَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مَعَ قَارُونَ، وَفِرْعَوْنَ، وَهَامَانَ، وَأُبَيِّ بْنِ خَلَفٍ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb —, amesema: Amenisimulia Ka'b bin 'Alqamah, kutoka kwa 'Iysaa bin Hilaal Asw-Swadafiy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba aliitaja Swalaah siku moja, akasema: "Atakayeihifadhi, itakuwa kwake nuru, na hoja, na uokovu kutokana na moto Siku ya Qiyaamah; na asiyeihifadhi, haitakuwa kwake nuru, wala uokovu, wala hoja; na Siku ya Qiyaamah atakuwa pamoja na Qaaruwn, na Fir'awn, na Haamaan, na Ubayy bin Khalaf."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1789
- Hadiyth
- 2763
14-Mlangoباب: في قيام الليلMlango Wa Kuhusu Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku)
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، قَالَ: حَدَّثَنِي ابْنُ عَجْلَانَ، عَنْ حُسَيْنِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَرْغَبُ فِي قِيَامِ اللَّيْلِ حَتَّى قَالَ: "وَلَوْ رَكْعَةً"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amesema: Amenisimulia Al-Layth, amesema: Amenisimulia Ibn 'Ajlaan, kutoka kwa Husayn bin 'Abdi-Allaah bin 'Ubaydi-Allaah bin 'Abbaas, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akihimiza Qiyaamul-Layl (Kisimamo Cha Usiku), mpaka akasema: "Hata kama ni Rakaa moja."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1789
- Hadiyth
- 2764
15-Mlangoباب: في الاستغفارMlango Wa Kuhusu Kuomba Maghfirah
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، حَدَّثَنَا أَبُو إِسْحَاق، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عَمْرٍو أَبِي الْمُغِيرَةِ، عَنْ حُذَيْفَةَ، قَالَ: كَانَ فِي لِسَانِي ذَرَبٌ عَلَى أَهْلِي، وَلَمْ يَكُنْ يَعْدُوهُمْ إِلَى غَيْرِهِمْ، فَسَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "أَيْنَ أَنْتَ مِنَ الِاسْتِغْفَارِ؟ إِنِّي لَأَسْتَغْفِرُ اللَّهَ كُلَّ يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ" قَالَ أَبُو إِسْحَاق: فَحَدَّثْتُ بِهِ أَبَا بُرْدَةَ، وَأَبَا بَكْرٍ ابْنَيْ أَبِي مُوسَى، قَالَا: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ كُلَّ يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Israaiyl, ametusimulia Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Ubayd bin 'Amr Abul-Mughiyrah, kutoka kwa Hudhayfah (رضي الله عنه), amesema: Kulikuwa katika ulimi wangu ukali dhidi ya watu wa nyumbani kwangu, wala haukuwa ukiwavuka kwenda kwa wengineo. Nikamuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: "Uko wapi wewe na kuomba Maghfirah? Hakika mimi namuomba Allaah Maghfirah kila siku mara mia." Abuw Is-haaq amesema: Nikawasimulia hilo Abuw Burdah na Abuw Bakr, wana wawili wa Abuw Muusaa (رضي الله عنه); wakasema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Namuomba Allaah Maghfirah kila siku mara mia: Namuomba Allaah Maghfirah na natubia Kwake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1790
- Hadiyth
- 2765
16-Mlangoباب: في تقوى اللهMlango Wa Kuhusu Kumcha Allaah
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ سَلْمِ بْنِ قُتَيْبَةَ، عَنْ سُهَيْلٍ الْقُطَعِيِّ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَرَأَ: {هُوَ أَهْلُ التَّقْوَى وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ}. قَالَ: "قَالَ رَبُّكُمْ: أَنَا أَهْلٌ أَنْ أُتَّقَى، فَمَنْ اتَّقَانِي فَأَنَا أَهْلٌ أَنْ أَغْفِرَ لَهُ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Al-Mubaarak, kutoka kwa Salm bin Qutaybah, kutoka kwa Suhayl Al-Qutwa'iy, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwamba alisoma:
هُوَ أَهْلُ التَّقْوَى وَأَهْلُ الْمَغْفِرَةِ
Yeye Ndiye Mstahiki wa Kuogopwa, na Mstahiki wa Kughufuria (madhambi) [Al-Muddath-thir (74:56)]
Akasema: "Rabb wenu Amesema: Mimi Ni Mstahiki wa Kuogopwa; basi atakayeniogopa, Mimi Ni Mstahiki wa Kumghufuria."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1791
- Hadiyth
- 2766
حَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ كَهْمَسِ بْنِ الْحَسَنِ، عَنْ أَبِي السَّلِيلِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنِّي لَأَعْلَمُ آيَةً لَوْ أَخَذَ بِهَا النَّاسُ لَكَفَتْهُمْ: {فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّهِ ذَلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا}"
Ametusimulia 'Uthmaan bin Muhammad, ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa Kahmas bin Al-Hasan, kutoka kwa Abus-Saliyl, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mimi naijua Aayah ambayo lau watu wangeishika, ingewatosha":
فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِنْكُمْ وَأَقِيمُوا الشَّهَادَةَ لِلَّهِ ذَلِكُمْ يُوعَظُ بِهِ مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ وَمَنْ يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجًا
Na watakapokaribia kufikia muda wao (wa eda), basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili waadilifu miongoni mwenu, na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Allaah. Hivyo ndivyo anavyowaidhiwa anayemwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na yeyote anayemcha Allaah, basi Atamfanyia njia ya kutoka (shidani). [Atw-Twalaaq (65:2)]
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1792
- Hadiyth
- 2767
17-Mlangoباب: في المحقراتMlango Wa Kuhusu Madhambi Yanayodharauliwa
أَخْبَرَنَا مَنْصُورُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ: ابْنُ مُسْلِمِ بْنِ بَانَكَ، عَنْ عَامِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الزُّبَيْرِ، عَنْ عَوْفِ بْنِ الْحَارِثِ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ لِي رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا عَائِشُ، إِيَّاكِ وَمُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ، فَإِنَّ لَهَا مِنَ اللَّهِ طَالِبًا"
Ametukhabarisha Manswuwr bin Salamah, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Muslim bin Baanak —, kutoka kwa 'Aamir bin 'Abdi-Allaah bin Az-Zubayr, kutoka kwa 'Awf bin Al-Haarith, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniambia: "Yaa 'Aaish, tahadhari na madhambi yanayodharauliwa, kwani hakika yana mwenye kuyafuatilia kutoka kwa Allaah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1792
- Hadiyth
- 2768
18-Mlangoباب: في التوبةMlango Wa Kuhusu Tawbah
حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ مَسْعَدَةَ الْبَاهِلِيُّ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "كُلُّ بَنِي آدَمَ خَطَّاءٌ، وَخَيْرُ الْخَطَّائِينَ التَّوَّابُونَ"
Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia 'Aliy bin Mas'adah Al-Baahiliy, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kila mwana wa Aadam (عليه السلام) ni mkosaji sana, na wabora wa wakosaji sana ni wenye kutubu sana."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1793
- Hadiyth
- 2769
19-Mlangoباب: لله أفرح بتوبة العبدMlango Wa Allaah Ana Furaha Zaidi Kwa Tawbah Ya Mja
أَخْبَرَنَا النَّضْرُ بْنُ شُمَيْلٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ النُّعْمَانِ هُوَ: ابْنُ بَشِيرٍ أَنَّهُ سَمِعَهُ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "سَافَرَ رَجُلٌ فِي أَرْضٍ تَنُوفَةٍ فَقَالَ: تَحْتَ شَجَرَةٍ وَمَعَهُ رَاحِلَتُهُ، عَلَيْهَا زَادُهُ وَطَعَامُهُ، فَاسْتَيْقَظَ وَقَدْ ذَهَبَتْ رَاحِلَتُهُ، فَعَلَا شَرَفًا، فَلَمْ يَرَ شَيْئًا، ثُمَّ عَلَا شَرَفًا، فَلَمْ يَرَ شَيْئًا، ثُمَّ عَلَا شَرَفًا فَلَمْ يَرَ شَيْئًا، قَالَ: فَالْتَفَتَ فَإِذَا هُوَ بِهَا تَجُرُّ خِطَامَهَا، فَمَا هُوَ بِأَشَدَّ فَرَحًا بِهَا مِنَ اللَّهِ بِتَوْبَةِ عَبْدِهِ إِذَا تَابَ إِلَيْهِ"
Ametukhabarisha An-Nadhwr bin Shumayl, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa An-Nu'maan — naye ni Ibn Bashiyr — (رضي الله عنهما), kwamba alimsikia akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu mmoja alisafiri katika ardhi ya jangwa tupu, akapumzika (usingizi wa) mchana chini ya mti, na pamoja naye kipando chake, juu yake kuna masurufu yake na chakula chake. Akaamka, na kumbe kipando chake kimeshaondoka. Akapanda mahali palipoinuka, asione kitu; kisha akapanda mahali palipoinuka, asione kitu; kisha akapanda mahali palipoinuka, asione kitu." Akasema: "Akageuka, na ghafla akakiona kinakokota hatamu yake. Basi yeye hana furaha zaidi kwa (kukipata) kipando hicho kuliko Allaah (Alivyo na furaha) kwa tawbah ya mja Wake anapotubu Kwake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1793
- Hadiyth
- 2770
20-Mlangoباب: في الأمل والأجلMlango Wa Kuhusu Matumaini Na Ajali
حَدَّثَنَا مُسَدَّدٌ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي يَعْلَى، عَنْ الرَّبِيعِ بْنِ خُثَيْمٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: خَطَّ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَطًّا مُرَبَّعًا، ثُمَّ خَطَّ وَسَطَهُ خَطًّا، ثُمَّ خَطَّ حَوْلَهُ خُطُوطًا، وَخَطَّ خَطًّا خَارِجًا مِنَ الْخَطِّ، فَقَالَ: "هَذَا الْإِنْسَانُ لِلْخَطِّ الْأَوْسَطِ وَهَذَا الْأَجَلُ مُحِيطٌ بِهِ، وَهَذِهِ الْأَعْرَاضُ لِلْخُطُوطِ فَإِذَا أَخْطَأَهُ وَاحِدٌ نَهَشَهُ الْآخَرُ، وَهَذَا الْأَمَلُ لِلْخَطِّ الْخَارِجِ"
Ametusimulia Musaddad, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Ya'laa, kutoka kwa Ar-Rabiy' bin Khuthaym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituchorea mstari wa mraba, kisha akachora mstari katikati yake, kisha akachora mistari kuuzunguka (mstari huo wa katikati), na akachora mstari unaotoka nje ya mstari (wa mraba). Akasema: "Huyu ni mwanaadam — kwa mstari wa katikati —, na hii ni ajali yake imemzunguka; na haya ni maafa — kwa ile mistari —: likimkosa moja, jingine humng'ata; na haya ni matumaini — kwa mstari ulio nje."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1795
- Hadiyth
- 2771
21-Mlangoباب: ما ذئبان جائعانMlango Wa Mbwa Mwitu Wawili Wenye Njaa
أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، عَنْ زَكَرِيَّا، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَعْدِ بْنِ زُرَارَةَ، عَنِ ابْنِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا ذِئْبَانِ جَائِعَانِ أُرْسِلَا فِي غَنَمٍ بِأَفْسَدَ لَهَا مِنْ حِرْصِ الْمَرْءِ عَلَى الْمَالِ وَالشَّرَفِ لِدِينِهِ"
Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, kutoka kwa Zakariyyaa, kutoka kwa Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Sa'd bin Zuraarah, kutoka kwa Ibn Ka'b bin Maalik, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mbwa mwitu wawili wenye njaa walioachiwa katika (kundi la) mbuzi na kondoo, hawaliharibu zaidi kuliko pupa ya mtu juu ya mali na utukufu (wa cheo) inavyoiharibu Dini yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1795
- Hadiyth
- 2772
22-Mlangoباب: في حسن الظن باللهMlango Wa Kuhusu Kumdhania Allaah Vizuri
أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ الْغَازِ، عَنْ حَيَّانَ أَبِي النَّضْرِ، عَنْ وَاثِلَةَ بْنِ الْأَسْقَعِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا عِنْدَ ظَنِّ عَبْدِي بِي، فَلْيَظُنَّ بِي مَا شَاءَ"
Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, ametusimulia Hishaam bin Al-Ghaaz, kutoka kwa Hayyaan Abun-Nadhwr, kutoka kwa Waathilah bin Al-Asqa' (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Allaah (تبارك وتعالى) Amesema: Mimi Niko kwenye dhana ya Mja Wangu juu Yangu; basi anidhanie apendavyo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1796
- Hadiyth
- 2773
23-Mlangoباب: وأنذر عشيرتك الأقربينMlango Wa «Na onya jamaa zako wa
karibu» [Ash-Shu’araa (26:214)]
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ، وَأَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَامَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ أَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى {وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ}، فَقَالَ: "يَا مَعْشَرَ قُرَيْشٍ، اشْتَرُوا أَنْفُسَكُمْ مِنَ اللَّهِ، لَا أُغْنِي عَنْكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، يَا بَنِي عَبْدِ مَنَافٍ، لَا أُغْنِي عَنْكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا. يَا عَبَّاسُ بْنَ عَبْدِ الْمُطَلِّبِ، لَا أُغْنِي عَنْكَ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، يَا صَفِيَّةُ عَمَّةَ رَسُولِ اللَّهِ لَا أُغْنِي عَنْكِ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا، يَا فَاطِمَةُ بِنْتَ مُحَمَّدٍ، سَلِينِي مَا شِئْتِ، لَا أُغْنِي عَنْكِ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا"
Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib na Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alisimama pale Allaah (تعالى) Alipoteremsha:
وَأَنْذِرْ عَشِيرَتَكَ الأَقْرَبِينَ
Na onya jamaa zako wa karibu. [Ash-Shu’araa (26:214)]
Akasema: "Enyi jamaa ya Quraysh! Zinunueni nafsi zenu kutoka kwa Allaah; sitakufaeni chochote mbele ya Allaah. Yaa Baniy 'Abdi Manaaf! Sitakufaeni chochote mbele ya Allaah. Yaa 'Abbaas bin 'Abdil-Muttwalib! Sitakufaa chochote mbele ya Allaah. Yaa Swafiyyah, shangazi wa Rasuli wa Allaah! Sitakufaa chochote mbele ya Allaah. Yaa Faatwimah bint Muhammad! Niombe utakacho; sitakufaa chochote mbele ya Allaah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1796
- Hadiyth
- 2774
24-Mlangoباب: لا ينجي أحدكم عملهMlango Wa Amali Ya Mmoja Wenu Haitamuokoa
أَخْبَرَنَا الْحَسَنُ بْنُ الرَّبِيعِ، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَحْوَصِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "قَارِبُوا وَسَدِّدُوا، وَاعْلَمُوا أَنَّ أَحَدًا مِنْكُمْ لَنْ يُنْجِيَهُ عَمَلُهُ". قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، وَلَا أَنْتَ. قَالَ: "وَلَا أَنَا إِلَّا أَنْ يَتَغَمَّدَنِيَ اللَّهُ بِرَحْمَةٍ مِنْهُ وَفَضْلٍ"
Ametukhabarisha Al-Hasan bin Ar-Rabiy', ametusimulia Abul-Ahwasw, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kurubieni (ukamilifu) na elekeeni usawa, na jueni kwamba yeyote miongoni mwenu, amali yake haitamuokoa." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, wala wewe? Akasema: "Wala mimi, isipokuwa Allaah Anifunike kwa Rehma kutoka Kwake na Fadhila."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1797
- Hadiyth
- 2775
25-Mlangoباب: ما منكم أحد إلا ومعه قرينه من الجنMlango Wa Hakuna Yeyote Miongoni Mwenu Isipokuwa Yuko
Pamoja Naye Mwenzake (Wa Kudumu) Kutoka Kwa Majini
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ سَالِمِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ إِلَّا وَمَعَهُ قَرِينُهُ مِنَ الْجِنِّ، وَقَرِينُهُ مِنَ الْمَلَائِكَةِ". قَالُوا: وَإِيَّاكَ؟. قَالَ: "نَعَمْ وَإِيَّايَ، وَلَكِنَّ اللَّهَ أَعَانَنِي عَلَيْهِ فَأَسْلَمَ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: مِنَ النَّاسِ مَنْ يَقُولُ: أَسْلَمَ: اسْتَسْلَمَ. يَقُولُ: ذَلَّ
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Saalim bin Abil-Ja'd, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna yeyote miongoni mwenu isipokuwa yuko pamoja naye mwenzake (wa kudumu) kutoka kwa majini, na mwenzake (wa kudumu) kutoka kwa Malaika (عليهم السلام)." Wakasema: Na wewe pia? Akasema: "Ndiyo, na mimi pia; lakini Allaah Amenisaidia dhidi yake, basi akasilimu."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Miongoni mwa watu wako wanaosema: aslama (akasilimu) maana yake ni: istaslama (akajisalimisha); anasema: akadhalilika (akanyenyekea).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1798
- Hadiyth
- 2776
26-Mlangoباب: لو تعلمون ما أعلمMlango Wa Lau Mngejua Ninayoyajua
حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُوسَى بْنِ أَنَسٍ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أَعْلَمُ، لَضَحِكْتُمْ قَلِيلًا، وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيرًا"،
Ametusimulia Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muwsaa bin Anas, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Lau mngejua ninayoyajua, mngecheka kidogo na mngelia sana."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1798
- Hadiyth
- 2777
حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِمِثْلِ هَذَا
Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa mfano wa hii.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1799
- Hadiyth
- 2778
27-Mlangoباب: في هوان الدنيا على الله تعالىMlango Wa Kuhusu Udhalili Wa Dunia Kwa Allaah (تعالى)
أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَزِّمِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّ بِسَخْلَةٍ جَرْبَاءَ قَدْ أَخْرَجَهَا أَهْلُهَا. قَالَ: "تُرَوْنَ هَذِهِ هَيِّنَةً عَلَى أَهْلِهَا؟". قَالُوا: نَعَمْ. قَالَ: "وَاللَّهِ لَلدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ هَذِهِ عَلَى أَهْلِهَا"
Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Abul-Muhazzim, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipita karibu na mwana-mbuzi mwenye upele, ambaye wenyewe walikuwa wamemtupa nje. Akasema: "Mnamuona huyu ni duni kwa wenyewe?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Wa-Allaahi, dunia ni duni zaidi kwa Allaah kuliko huyu alivyo duni kwa wenyewe."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1799
- Hadiyth
- 2779
28-Mlangoباب: أي الأعمال أفضلMlango Wa Amali Zipi Ni Bora Zaidi
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي الْمُرَاوِحِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: أَيُّ الْأَعْمَالِ أَفْضَلُ؟. قَالَ: "إِيمَانٌ بِاللَّهِ، وَجِهَادٌ فِي سَبِيلِ اللَّهِ"
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametusimulia Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abul-Muraawih, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Ni amali zipi zilizo bora zaidi? Akasema: "Imaan kwa Allaah, na jihaad katika Njia ya Allaah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1800
- Hadiyth
- 2780
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ يَحْيَى، عَنْ أَبِي جَعْفَرٍ: أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَفْضَلُ الْأَعْمَالِ عِنْدَ اللَّهِ إِيمَانٌ لَا شَكَّ فِيهِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: أَبُو جَعْفَرٍ: رَجُلٌ مِنَ الْأَنْصَارِ
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Yahyaa, kutoka kwa Abuw Ja'far, kwamba alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Amali bora zaidi mbele ya Allaah ni imaan isiyo na shaka ndani yake."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Abuw Ja'far ni mtu miongoni mwa Answaar.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1800
- Hadiyth
- 2781
29-Mlangoباب: لا يؤمن أحدكم حتى يحب لأخيه ما يحب لنفسهMlango Wa Haamini Mmoja Wenu
Mpaka Ampendee Ndugu Yake Anachokipenda Kwa Nafsi Yake
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يُحِبَّ لِأَخِيهِ مَا يُحِبُّ لِنَفْسِهِ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Haamini mmoja wenu mpaka ampendee ndugu yake anachokipenda kwa nafsi yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1801
- Hadiyth
- 2782
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، وَهَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، قَالَا: حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: "لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ، وَوَلَدِهِ، وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn na Haashim bin Al-Qaasim, wamesema: Ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Haamini mmoja wenu mpaka niwe ninapendwa zaidi kwake kuliko mzazi wake, na mwanawe, na watu wote."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1801
- Hadiyth
- 2783
30-Mlangoباب: أي المؤمنين خيرMlango Wa Ni Yupi Katika Waumini Aliye Bora
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ زَيْدِ بْنِ جُدْعَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ، عَنْ أَبِي بَكْرَةَ: أَنَّ رَجُلًا، قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيُّ النَّاسِ خَيْرٌ؟، قَالَ: "مَنْ طَالَ عُمُرُهُ، وَحَسُنَ عَمَلُهُ"، قَالَ: فَأَيُّ النَّاسِ شَرٌّ؟، قَالَ: "مَنْ طَالَ عُمُرُهُ، وَسَاءَ عَمَلُهُ"،
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa 'Aliy bin Zayd bin Jud'aan, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah, kutoka kwa Abuw Bakrah (رضي الله عنه), kwamba mtu mmoja alisema: Yaa Rasula-Allaah, ni watu gani walio bora? Akasema: "Ambaye umri wake umekuwa mrefu, na amali yake ikawa nzuri." Akasema: Basi ni watu gani walio waovu? Akasema: "Ambaye umri wake umekuwa mrefu, na amali yake ikawa mbaya."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1802
- Hadiyth
- 2784
حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ زَيْدٍ بِإِسْنَادِهِ، مِثْلَهُ
Ametusimulia Hajjaaj, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Aliy bin Zayd, kwa Isnaad (mlolongo wa wapokezi) yake, mfano wake.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1803
- Hadiyth
- 2785
31-Mlangoباب: في فضل آخر هذه الأمةMlango Wa Kuhusu Fadhila Ya Watu Wa Mwisho Wa Ummah Huu
أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، قَالَ: حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا أَسِيدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ خَالِدِ بْنِ دُرَيْكٍ، عَنْ ابْنِ مُحَيْرِيزٍ، قَالَ: قُلْتُ لِأَبِي جُمُعَةَ رَجُلٍ مِنَ الصَّحَابَةِ حَدِّثْنَا: حَدِيثًا سَمِعْتَهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: نَعَمْ أُحَدِّثُكَ حَدِيثًا جَيِّدًا: تَغَدَّيْنَا مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَمَعَنَا أَبُو عُبَيْدَةَ بْنُ الْجَرَّاحِ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَحَدٌ خَيْرٌ مِنَّا؟ أَسْلَمْنَا وَجَاهَدْنَا مَعَكَ؟، قَالَ: "نَعَمْ، قَوْمٌ يَكُونُونَ مِنْ بَعْدِكُمْ يُؤْمِنُونَ بِي وَلَمْ يَرَوْنِي"
Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, amesema: Ametusimulia Al-Awzaa'iy, ametusimulia Asiyd bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Khaalid bin Durayk, kutoka kwa Ibn Muhayriyz, amesema: Nilimwambia Abuw Jumu'ah (رضي الله عنه) — mtu mmoja miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) —: Tusimulie Hadiyth uliyoisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Ndiyo, nitakusimulia Hadiyth nzuri: Tulikula chakula cha mchana pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na pamoja nasi alikuwa Abuw 'Ubaydah bin Al-Jarraah (رضي الله عنه). Akasema: Yaa Rasula-Allaah, je, kuna yeyote aliye bora kuliko sisi? Tumesilimu na tumepigana jihaad pamoja nawe. Akasema: "Ndiyo; watu watakaokuwa baada yenu, wataniamini na hali hawakuniona."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1803
- Hadiyth
- 2786
32-Mlangoباب: في تعاهد القرآنMlango Wa Kuhusu Kuishughulikia Qur-aan
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَبْدِ الْمَجِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مَنْصُورٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "بِئْسَمَا لِأَحَدِكُمْ أَنْ يَقُولَ: نَسِيتُ آيَةَ كَيْتَ وَكَيْتَ، بَلْ هُوَ نُسِّيَ، فَاسْتَذْكِرُوا الْقُرْآنَ، فَإِنَّهُ أَسْرَعُ تَفَصِّيًا مِنْ صُدُورِ الرِّجَالِ مِنَ النَّعَمِ مِنْ عُقُلِهَا"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin 'Abdil-Majiyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Manswuwr, amesema: Nilimsikia Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Ni baya kiasi gani kwa mmoja wenu kusema: Nimesahau Aayah fulani na fulani! Bali yeye amesahaulishwa. Basi idurusuni Qur-aan; kwani hakika hiyo inaponyoka zaidi kutoka katika vifua vya watu kuliko mifugo (ngamia) kutoka katika kamba zao."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1804
- Hadiyth
- 2787
33-Mlangoباب: لا ينبغي لأحد أن يقول: أنا خير من يونس بن متىMlango Wa Haipasi Kwa Yeyote Kusema: Mimi
Ni Bora Kuliko Yuwnus Bin Mattaa (عليه السلام)
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعْيَمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَقُولَنَّ أَحَدُكُمْ: أَنَا خَيْرٌ مِنْ يُونُسَ بْنِ مَتَّى"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mmoja wenu asiseme kabisa: Mimi ni bora kuliko Yuwnus bin Mattaa (عليه السلام)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1805
- Hadiyth
- 2788
34-Mlangoباب: على كل مسلم صدقةMlango Wa Juu Ya Kila Muislamu Kuna Swadaka
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ جَعْفَرٍ الْمَدَائِنِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ صَدَقَةٌ"، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ أَوْ لَمْ يَفْعَلْ؟، قَالَ: "يَعْتَمِلُ بِيَدَيْهِ فَيَأْكُلُ مِنْهُ وَيَتَصَدَّقُ"، قَالُوا: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَفْعَلْ؟، قَالَ: "يُعِينُ ذَا الْحَاجَةِ الْمَلْهُوفَ"، قَالُوا: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَفْعَلْ؟، قَالَ: "يَأْمُرُ بِالْخَيْرِ"، قَالُوا: أَفَرَأَيْتَ إِنْ لَمْ يَفْعَلْ؟، قَالَ: "يُمْسِكُ عَنِ الشَّرِّ، فَإِنَّهَا لَهُ صَدَقَةٌ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Ja'far Al-Madaainiy, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Sa'iyd bin Abiy Burdah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Juu ya kila Muislamu kuna swadaka." Wakasema: Yaa Rasula-Allaah, je, ikiwa hakuweza au hakufanya? Akasema: "Afanye kazi kwa mikono yake miwili, ale katika (chumo) hilo na atoe swadaka." Wakasema: Unaonaje ikiwa hakufanya? Akasema: "Amsaidie mwenye haja aliyedhikika." Wakasema: Unaonaje ikiwa hakufanya? Akasema: "Aamrishe kheri." Wakasema: Unaonaje ikiwa hakufanya? Akasema: "Ajizuie na shari, kwani hiyo ni swadaka kwake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1806
- Hadiyth
- 2789
35-Mlangoباب: من راءى راءى الله بهMlango Wa Anayejionyesha, Allaah Atamwonyesha (Aibu Yake)
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو صَخْرٍ، أَنَّهُ سَمِعَ مَكْحُولًا يَقُولُ: حَدَّثَنِي أَبُو هِنْدٍ الدَّارِيُّ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَنْ قَامَ مَقَامَ رِيَاءٍ وَسُمْعَةٍ، رَاءَى اللَّهُ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَسَمَّعَ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, amesema: Amenisimulia Abuw Swakhr, kwamba alimsikia Makhuwl akisema: Amenisimulia Abuw Hind Ad-Daariy (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Atakayesimama kisimamo cha kujionyesha na cha kutaka kusikika, Allaah Atamwonyesha (aibu yake kwa watu) Siku ya Qiyaamah, na Atamsikilizisha (kwao)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1807
- Hadiyth
- 2790
36-Mlangoباب: مثل المؤمن كمثل الزرعMlango Wa Mfano Wa Muumini Ni Kama Mfano Wa Mmea
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ سَعْدِ بْنِ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ كَعْبٍ، عَنْ أَبِيهِ كَعْبِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَثَلُ الْمُؤْمِنِ مَثَلُ الْخَامَةِ مِنَ الزَّرْعِ تُفَيِّئُهَا الرِّيَاحُ: تُعَدِّلُهَا مَرَّةً، وَتُضْجِعُهَا أُخْرَى حَتَّى يَأْتِيَهُ الْمَوْتَ. وَمَثَلُ الْكَافِرِ كَمَثَلِ الْأَرْزَةِ الْمُجْذِيَةِ عَلَى أَصْلِهَا لَا يُصِيبُهَا شَيْءٌ حَتَّى يَكُونَ انْجِعَافُهَا مَرَّةً وَاحِدَةً". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: الْخَامَةُ: الضَّعِيفُ
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Sa'd bin Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Ka'b, kutoka kwa baba yake Ka'b bin Maalik (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mfano wa Muumini ni mfano wa khaamah (mche laini) wa mmea, pepo zinauyumbisha: mara unaunyoosha, na mara nyingine unaulaza, mpaka kifo kimjie. Na mfano wa kafiri ni kama mfano wa mti wa arzah (aina ya msonobari mgumu) uliosimama imara juu ya shina lake; hakuna kitu kinachousibu, mpaka kung'oka kwake kuwe ni mara moja."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Al-Khaamah: (mche) dhaifu.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1808
- Hadiyth
- 2791
37-Mlangoباب: الدنيا خضرة حلوةMlango Wa Dunia Ni Ya Kijani Kibichi, Tamu
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، وَعُرْوَةَ بْنِ الزُّبَيْرِ، أَنَّ حَكِيمَ بْنَ حِزَامٍ، قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ فَأَعْطَانِي، ثُمَّ سَأَلْتُهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَا حَكِيمُ، إِنَّ هَذَا الْمَالَ خَضِرٌ حُلْوٌ، فَمَنْ أَخَذَهُ بِسَخَاوَةِ نَفْسٍ، بُورِكَ لَهُ فِيهِ، وَمَنْ أَخَذَهُ بِإِشْرَافِ نَفْسٍ، لَمْ يُبَارَكْ لَهُ فِيهِ، وَكَانَ كَالَّذِي يَأْكُلُ وَلَا يَشْبَعُ، وَالْيَدُ الْعُلْيَا خَيْرٌ مِنَ الْيَدِ السُّفْلَى"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib na 'Urwah bin Az-Zubayr, kwamba Hakiym bin Hizaam (رضي الله عنه) amesema: Nilimuomba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akanipa; kisha nikamuomba, akanipa; kisha nikamuomba, akanipa; kisha nikamuomba. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yaa Hakiym, hakika mali hii ni ya kijani kibichi, tamu. Atakayeichukua kwa ukarimu wa nafsi, atabarikiwa ndani yake; na atakayeichukua kwa tamaa ya nafsi, hatabarikiwa ndani yake, na atakuwa kama anayekula wala hashibi. Na mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1809
- Hadiyth
- 2792
38-Mlangoباب: إن الله كره لكم قيل وقالMlango Wa Hakika Allaah Amekuchukieni
(Kueneza Maneno Ya): Imesemwa Na Amesema
حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو الرَّقِّيُّ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ وَرَّادٍ مَوْلَى الْمُغِيرَةِ، عَنِ الْمُغِيرَةِ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ وَأْدِ الْبَنَاتِ، وَعُقُوقِ الْأُمَّهَاتِ، وَعَنْ مَنْعٍ وَهَاتِ، وَعَنْ قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةِ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ الْمَالِ"
Ametusimulia Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin 'Amr Ar-Raqqiy, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Warraad mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Mughiyrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Al-Mughiyrah [bin Shu'bah] (رضي الله عنه), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amekataza kuwazika mabinti wakiwa hai, na kuwaasi mama, na (amekataza) kuzuia (haki iliyo juu yako) na (kudai kwa kusema): Nipe! Na (amekataza kueneza maneno ya): Imesemwa na amesema, na kuuliza maswali mengi, na kupoteza mali."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1810
- Hadiyth
- 2793
39-Mlangoباب: في الأئمة المضلينMlango Wa Kuhusu Viongozi Wapotoshaji
أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي أَسْمَاءَ، عَنْ ثَوْبَانَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّمَا أَخَافُ عَلَى أُمَّتِي الْأَئِمَّةَ الْمُضِلِّينَ"
Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abuw Asmaa, kutoka kwa Thawbaan (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika ninachokikhofia juu ya Ummah wangu ni viongozi wapotoshaji."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1811
- Hadiyth
- 2794
40-Mlangoباب: انصر أخاك ظالما أو مظلوماMlango Wa Mnusuru Ndugu Yako Akiwa Dhalimu
Au Akiwa Amedhulumiwa
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لِيَنْصُرِ الرَّجُلُ أَخَاهُ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا، فَإِنْ كَانَ ظَالِمًا، فَلْيَنْهَهُ، فَإِنَّهُ لَهُ نُصْرَةٌ، وَإِنْ كَانَ مَظْلُومًا، فَلْيَنْصُرْهُ"
Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu amnusuru ndugu yake akiwa dhalimu au akiwa amedhulumiwa. Ikiwa ni dhalimu, basi amkataze, kwani huko ndiko kumnusuru kwake; na ikiwa amedhulumiwa, basi amnusuru."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1812
- Hadiyth
- 2795
41-Mlangoباب: الدين النصيحةMlango Wa Dini Ni Nasaha
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ هِشَامِ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ أَسْلَمَ، وَنَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الدِّينُ النَّصِيحَةُ"، قَالَ: قُلْنَا: لِمَنْ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟، قَالَ: "لِلَّهِ، وَلِرَسُولِهِ، وَلِكِتَابِهِ، وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ"
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Hishaam bin Sa'd, kutoka kwa Zayd bin Aslam na Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituambia: "Dini ni nasaha." Akasema: Tukasema: Kwa nani, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Kwa Allaah, na kwa Rasuli Wake, na kwa Kitabu Chake, na kwa viongozi wa Waislamu, na kwa watu wao wa kawaida."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1812
- Hadiyth
- 2796
42-Mlangoباب: إن الإسلام بدأ غريباMlango Wa Hakika Islaam Ilianza Ikiwa Ngeni
حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي الْأَحْوَصِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: قَالَ لَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الْإِسْلَامَ بَدَأَ غَرِيبًا وَسَيَعُودُ غَرِيبًا أَظُنُّ حَفْصًا، قَالَ: فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ"، قِيلَ: وَمَنِ الْغُرَبَاءُ؟، قَالَ: "النُّزَّاعُ مِنَ الْقَبَائِلِ"
Ametusimulia Zakariyyaa bin 'Adiyy, ametusimulia Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abul-Ahwasw, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituambia: "Hakika Islaam ilianza ikiwa ngeni, na itarudi kuwa ngeni — nadhani Hafsw alisema: — basi Twuwbaa (furaha na kheri) ni kwa wageni." Pakasemwa: Na ni akina nani wageni? Akasema: "Waliojitenga (na kuhama) kutoka katika makabila (yao)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1813
- Hadiyth
- 2797
43-Mlangoباب: في حب لقاء اللهMlango Wa Kuhusu Kupenda Kukutana Na Allaah
أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ أَحَبَّ لِقَاءَ اللَّهِ أَحَبَّ اللَّهُ لِقَاءَهُ، وَمَنْ كَرِهَ لِقَاءَ اللَّهِ، كَرِهَ اللَّهُ لِقَاءَهُ". فَقَالَتْ عَائِشَةُ أَوْ بَعْضُ أَزْوَاجِهِ: إِنَّا لَنَكْرَهُ الْمَوْتَ. قَالَ: "لَيْسَ ذَلِكَ، وَلَكِنَّ الْمُؤْمِنَ إِذَا حَضَرَهُ الْمَوْتُ بُشِّرَ بِرِضْوَانِ اللَّهِ وَكَرَامَتِهِ، فَلَيْسَ شَيْءٌ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا أَمَامَهُ، فَأَحَبَّ لِقَاءَ اللَّهِ وَأَحَبَّ اللَّهُ لِقَاءَهُ، وَإِنَّ الْكَافِرَ إِذَا حَضَرَهُ الْمَوْتُ بُشِّرَ بِعَذَابِ اللَّهِ وَعُقُوبَتِهِ، فَلَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَهَ إِلَيْهِ مِمَّا أَمَامَهُ، فَكَرِهَ لِقَاءَ اللَّهِ، وَكَرِهَ اللَّهُ لِقَاءَهُ"
Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa 'Ubaadah bin Asw-Swaamit (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Anayependa kukutana na Allaah, Allaah Hupenda kukutana naye; na anayechukia kukutana na Allaah, Allaah Huchukia kukutana naye." 'Aaishah (رضي الله عنها) — au baadhi ya wake zake (رضي الله عنهن) — akasema: Hakika sisi tunachukia kifo. Akasema: "Si hivyo; lakini Muumini anapofikiwa na mauti, hubashiriwa Radhi za Allaah na Takrima Yake; basi hakuna kitu kinachopendeza zaidi kwake kuliko kilicho mbele yake; akapenda kukutana na Allaah, na Allaah Akapenda kukutana naye. Na hakika kafiri anapofikiwa na mauti, hubashiriwa Adhabu ya Allaah na Ikabu Yake; basi hakuna kitu kinachochukiza zaidi kwake kuliko kilicho mbele yake; akachukia kukutana na Allaah, na Allaah Akachukia kukutana naye."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1813
- Hadiyth
- 2798
44-Mlangoباب: في المتحابين في اللهMlango Wa Kuhusu Wanaopendana Kwa Ajili Ya Allaah
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَعْمَرٍ، عَنْ أَبِي الْحُبَابِ: سَعِيدِ بْنِ يَسَارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ تَعَالَى يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: أَيْنَ الْمُتَحَابُّونَ بِجَلَالِي؟ الْيَوْمَ أُظِلُّهُمْ فِي ظِلِّي يَوْمَ لَا ظِلَّ إِلَّا ظِلِّي"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Maalik, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Abdir-Rahmaan bin Ma'mar, kutoka kwa Abul-Hubaab Sa'iyd bin Yasaar, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah (تعالى) Atasema Siku ya Qiyaamah: Wako wapi wanaopendana kwa ajili ya Utukufu Wangu? Leo Nitawafunika katika Kivuli Changu, siku ambayo hakuna kivuli isipokuwa Kivuli Changu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1814
- Hadiyth
- 2799
45-Mlangoباب: لا يتمنى أحدكم الموتMlango Wa Mmoja Wenu Asitamani Kifo
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَخْبَرَنِي شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو عُبَيْدٍ مَوْلَى عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَوْفٍ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَا يَتَمَنَّ أَحَدُكُمْ الْمَوْتَ: إِمَّا مُحْسِنًا، فَلَعَلَّهُ أَنْ يَزْدَادَ، إِحْسَانًا، وَإِمَّا مُسِيئًا، فَلَعَلَّهُ أَنْ يَسْتَعْتِبَ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', amenikhabarisha Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Abuw 'Ubayd mawlaa (mwachwa huru) wa 'Abdur-Rahmaan bin 'Awf (رضي الله عنه), kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Mmoja wenu asitamani kifo: ama akiwa ni mtenda mema, basi huenda akazidisha mema; na ama akiwa ni mtenda maovu, basi huenda akarejea (kwa tawbah) kutafuta radhi (ya Allaah)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1815
- Hadiyth
- 2800
46-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «بعثت أنا والساعة كهاتين»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Nimetumwa Mimi Na Saa Kama Hivi Viwili"
حَدَّثَنَا وَهْبُ بْنُ جَرِيرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي التَّيَّاحِ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "بُعِثْتُ أَنَا وَالسَّاعَةَ كَهَاتَيْنِ" وَأَشَارَ وَهْبٌ بِالسَّبَّاحَةِ وَالْوُسْطَى
Ametusimulia Wahb bin Jariyr, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abut-Tayyaah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Nimetumwa mimi na Saa (Qiyaamah) kama hivi viwili." Na Wahb akaashiria kwa (kidole) cha shahaadah na cha kati.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1815
- Hadiyth
- 2801
47-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «أنتم آخر الأمم»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Nyinyi Ni Wa Mwisho Wa Ummah"
أَخْبَرَنَا النَّضْرُ بْنُ شُمَيْلٍ، حَدَّثَنَا بَهْزُ بْنُ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِنَّكُمْ وَفَّيْتُمْ سَبْعِينَ أُمَّةً أَنْتُمْ آخِرُهَا وَأَكْرَمُهَا عَلَى اللَّهِ"
Ametukhabarisha An-Nadhwr bin Shumayl, ametusimulia Bahz bin Hakiym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake [Mu'aawiyah bin Haydah (رضي الله عنه)], amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika nyinyi mmekamilisha Ummah sabini; nyinyi ndio wa mwisho wake, na wenye hadhi zaidi wao mbele ya Allaah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1816
- Hadiyth
- 2802
48-Mlangoباب: في فضل أهل بدرMlango Wa Kuhusu Fadhila Za Watu Wa Badr
حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَاصِمٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَيْنَ فُلَانٌ؟". فَغَمَزَهُ رَجُلٌ مِنْهُمْ، فَقَالَ: إِنَّهُ، وَإِنَّهُ!، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَلَيْسَ قَدْ شَهِدَ بَدْرًا؟"، قَالُوا: بَلَى. قَالَ: "فَلَعَلَّ اللَّهَ اطَّلَعَ عَلَى أَهْلِ بَدْرٍ، فَقَالَ: اعْمَلُوا مَا شِئْتُمْ، فَقَدْ غَفَرْتُ لَكُمْ"
Ametusimulia 'Amr bin 'Aaswim, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yuko wapi fulani?" Mtu mmoja miongoni mwao akamkonyeza (akimtia dosari), akasema: Hakika yeye (ni hivi), na hakika yeye (ni hivi)! Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, hakuhudhuria (vita vya) Badr?" Wakasema: Bila shaka. Akasema: "Basi huenda Allaah Amewaangalia watu wa Badr (رضي الله عنهم), Akasema: Fanyeni mtakavyo, kwani hakika Nimekwishakughufirieni."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1816
- Hadiyth
- 2803
49-Mlangoباب: النهي أن يقول: مطرنا بنوء كذا وكذاMlango Wa Katazo La Kusema: Tumenyeshewa Mvua
Kwa Sababu Ya Nyota Fulani Na Fulani
حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، قَالَ: أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ دِينَارٍ، عَنْ عَتَّابِ بْنِ حُنَيْنٍ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَوْ حَبَسَ اللَّهُ الْقَطْرَ عَنْ أُمَّتِي عَشْرَ سِنِينَ، ثُمَّ أَنْزَلَهُ، لَأَصْبَحَتْ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي بِهَا كَافِرِينَ يَقُولُونَ: هُوَ بِنَوْءِ مِجْدَحٍ". يقَالَ: الْمِجْدَحُ كَوْكَبٌ. يُقَالُ لَهُ: الدَّبَرَانُ
Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Hammaad bin Salamah, amesema: Ametukhabarisha 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa 'Attaab bin Hunayn, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Lau Allaah Angeuzuia mvua kwa Ummah wangu miaka kumi, kisha Akaiteremsha, lingepambaukiwa kundi miongoni mwa Ummah wangu wakiwa ni makafiri kwayo, wakisema: Hiyo ni kwa sababu ya nyota ya Mijdah." Inasemwa: Al-Mijdah ni nyota inayoitwa Ad-Dabaraan.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1817
- Hadiyth
- 2804
50-Mlangoباب: الحسنة بعشر أمثالهاMlango Wa Jema Moja Ni Kwa Mfano Wake Kumi
أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ وَاصِلٍ مَوْلَى أَبِي عُيَيْنَةَ، عَنْ بَشَّارِ بْنِ أَبِي سَيْفٍ، عَنْ الْوَلِيدِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ عِيَاضِ بْنِ غُطَيْفٍ، قَالَ: أَتَيْنَا أَبَا عُبَيْدَةَ بْنَ الْجَرَّاحِ نَعُودُهُ، فَقَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "الْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا"
Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Waaswil mawlaa (mwachwa huru) wa Abuw 'Uyaynah, kutoka kwa Bashshaar bin Abiy Sayf, kutoka kwa Al-Waliyd bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa 'Iyaadhw bin Ghutwayf, amesema: Tulimjia Abuw 'Ubaydah bin Al-Jarraah (رضي الله عنه) kumtembelea (katika ugonjwa wake). Akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Jema moja (hulipwa) kwa mfano wake kumi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1818
- Hadiyth
- 2805
51-Mlangoباب: ما قيل في ذي الوجهينMlango Wa Yaliyosemwa Kuhusu Mwenye Nyuso Mbili
أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الرُّكَيْنِ، عَنْ نُعَيْمِ بْنِ حَنْظَلَةَ، قَالَ شَرِيكٌ وَرُبَّمَا قَالَ: النُّعْمَانِ بْنِ حَنْظَلَةَ، عَنْ عَمَّارٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ كَانَ ذَا وَجْهَيْنِ فِي الدُّنْيَا، كَانَ لَهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لِسَانَانِ مِنْ نَارٍ"
Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Ar-Rukayn, kutoka kwa Nu'aym bin Handhwalah — Shariyk amesema: Na mara nyingine alisema: An-Nu'maan bin Handhwalah —, kutoka kwa 'Ammaar [bin Yaasir] (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Atakayekuwa mwenye nyuso mbili duniani, atakuwa na ndimi mbili za moto Siku ya Qiyaamah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1819
- Hadiyth
- 2806
52-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «أيما رجل لعنته أو سببته»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Mtu Yeyote Niliyemlaani Au Niliyemtukana"
حَدَّثَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَاحِدِ بْنُ زِيَادٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اللَّهُمَّ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ، فَأَيُّ الْمُسْلِمِينَ لَعَنْتُهُ، أَوْ شَتَمْتُهُ أَوْ جَلَدْتُهُ، فَاجْعَلْهَا لَهُ صَلَاةً وَرَحْمَةً وَقُرْبَةً تُقَرِّبُهُ بِهَا إِلَيْكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ"،
Ametusimulia Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia 'Abdul-Waahid bin Ziyaad, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
اللَّهُمَّ إِنَّمَا أَنَا بَشَرٌ، فَأَيُّ الْمُسْلِمِينَ لَعَنْتُهُ، أَوْ شَتَمْتُهُ أَوْ جَلَدْتُهُ، فَاجْعَلْهَا لَهُ صَلَاةً وَرَحْمَةً وَقُرْبَةً تُقَرِّبُهُ بِهَا إِلَيْكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ
Yaa Allaah, hakika mimi ni mwanaadam tu; basi Muislamu yeyote nitakayemlaani, au nitakayemtukana, au nitakayemchapa mijeledi, Lijaalie hilo kwake kuwa ni Swalaah (sifa njema kutoka Kwako juu yake), na Rehma, na ukurubisho Utakaomkurubisha nao Kwako Siku ya Qiyaamah.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1819
- Hadiyth
- 2807
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ نُمَيْرٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ جَابِرٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ.......... مِثْلَهُ، إِلَّا أَنَّ فِيهِ "زَكَاةً وَرَحْمَةً"
Ametusimulia Muhammad bin 'Abdi-Allaah bin Numayr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), mfano wake; isipokuwa ndani yake kuna: "utakaso na Rehma."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1820
- Hadiyth
- 2808
53-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «لو أن لي مثل أحد ذهبا»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Lau Ningekuwa Na Mfano Wa Uhud Kwa Dhahabu"
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، قَالَ: سَمِعْتُ سُوَيْدَ بْنَ الْحَارِثِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَا يَسُرُّنِي أَنَّ جَبَلَ أُحُدٍ لِي ذَهَبًا أَمُوتُ يَوْمَ أَمُوتُ عِنْدِي دِينَارٌ أَوْ نِصْفُ دِينَارٍ إِلَّا لِغَرِيمٍ"
Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, amesema: Nilimsikia Suwayd bin Al-Haarith, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hainifurahishi kwamba mlima wa Uhud uwe wangu (ukiwa) dhahabu, nife siku nitakayokufa nikiwa na dinari moja au nusu dinari, isipokuwa kwa ajili ya mdai (deni)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1820
- Hadiyth
- 2809
54-Mlangoباب: في الموبقاتMlango Wa Kuhusu Madhambi Yanayoangamiza
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْفَضْلِ، وَسُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا حَمَّادٌ هُوَ: ابْنُ زَيْدٍ، قَالَ: حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ هِلَالٍ، عَنْ عُبَادَةَ بْنِ قُرْطٍ، قَالَ: "إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ أُمُورًا هِيَ أَدَقُّ فِي أَعْيُنِكُمْ مِنَ الشَّعْرِ، كُنَّا نَعُدُّهَا عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ الْمُوبِقَاتِ". فَذُكِرَ لِمُحَمَّدٍ يَعْنِي: ابْنَ سِيرِينَ، فَقَالَ: صَدَقَ، فَأَرَى جَرَّ الْإِزَارِ مِنْ ذَلِكَ
Ametusimulia Muhammad bin Al-Fadhwl na Sulaymaan bin Harb, wamesema: Ametusimulia Hammaad — naye ni Ibn Zayd —, amesema: Ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa 'Ubaadah bin Qurtw (رضي الله عنه), amesema: "Hakika nyinyi mnafanya mambo ambayo machoni mwenu ni madogo zaidi kuliko unywele; tulikuwa tukiyahesabu katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuwa ni miongoni mwa madhambi yanayoangamiza." Hilo likatajwa kwa Muhammad — yaani: Ibn Siyriyn —, akasema: Amesema kweli; na naona kuburuta izari (nguo ya chini) ni miongoni mwa hayo.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1821
- Hadiyth
- 2810
55-Mlangoباب: الحمى من فيح جهنمMlango Wa Homa Inatokana Na Mvuke Wa Joto La Jahannam
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبَايَةَ بْنِ رِفَاعَةَ، عَنْ رَافِعِ بْنِ خَدِيجٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْحُمَّى مِنْ فَيْحِ جَهَنَّمَ أَوْ مِنْ فَوْرِ جَهَنَّمَ فَأَبْرِدُوهَا بِالْمَاءِ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abaayah bin Rifaa'ah, kutoka kwa Raafi' bin Khadiyj (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Homa inatokana na mvuke wa joto la Jahannam — au: kutokana na mchemko wa Jahannam —; basi ipozeni kwa maji."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1822
- Hadiyth
- 2811
56-Mlangoباب: المرض كفارةMlango Wa Ugonjwa Ni Kafara (Kifutio Cha Madhambi)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ مَرْثَدٍ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ مُخَيْمِرَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا مِنْ أَحَدٍ مِنَ الْمُسْلِمِينَ يُصَابُ بِبَلَاءٍ فِي جَسَدِهِ، إِلَّا أَمَرَ اللَّهُ الْحَفَظَةَ الَّذِينَ يَحْفَظُونَهُ، فَقَالَ: اكْتُبُوا لِعَبْدِي فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ مِثْلَ مَا كَانَ يَعْمَلُ مِنَ الْخَيْرِ، مَا كَانَ مَحْبُوسًا فِي وِثَاقِي"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Alqamah bin Marthad, kutoka kwa Al-Qaasim bin Mukhaymirah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna yeyote katika Waislamu anayesibiwa na balaa katika mwili wake, isipokuwa Allaah Huwaamrisha Malaika wahifadhi (عليهم السلام) ambao wanamhifadhi, Akasema: Mwandikieni Mja Wangu katika kila mchana na usiku mfano wa yale aliyokuwa akiyatenda katika kheri, maadamu yuko amezuiliwa katika Kifungo Changu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1823
- Hadiyth
- 2812
57-Mlangoباب: أجر المريضMlango Wa Ujira Wa Mgonjwa
أَخْبَرَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ الْحَارِثِ بْنِ سُوَيْدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يُوعَكُ، فَوَضَعْتُ يَدِي عَلَيْهِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّكَ لَتُوعَكُ وَعْكًا شَدِيدًا، فَقَالَ: "إِنِّي أُوعَكُ كَمَا يُوعَكُ رَجُلَانِ مِنْكُمْ"، قَالَ: قُلْتُ: ذَلِكَ بِأَنَّ لَكَ أَجْرَيْنِ؟، قَالَ: "أَجَلْ، وَمَا مِنْ مُسْلِمٍ يُصِيبُهُ أَذًى، مَرَضٌ فَمَا سِوَاهُ، إِلَّا حُطَّ عَنْهُ مِنْ سَيِّئَاتِهِ كَمَا تَحُطُّ الشَّجَرَةُ وَرَقَهَا"
Ametukhabarisha Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym At-Taymiy, kutoka kwa Al-Haarith bin Suwayd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Niliingia kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) naye akiwa na homa; nikaweka mkono wangu juu yake, nikasema: Yaa Rasula-Allaah, hakika wewe una homa kali mno. Akasema: "Hakika mimi napata homa kama wanavyopata homa watu wawili miongoni mwenu." Akasema: Nikasema: Hiyo ni kwa sababu una ujira mara mbili? Akasema: "Naam. Na hakuna Muislamu yeyote anayesibiwa na udhia — ugonjwa na kisichokuwa hicho —, isipokuwa hupukutishiwa maovu yake kama mti unavyopukutisha majani yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1824
- Hadiyth
- 2813
58-Mlangoباب: في فضل الصلاة على النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu
Fadhila Ya Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ جَعْفَرٍ الْمَدَنِيُّ، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلَاةً وَاحِدَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ عَشْرًا"
Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Ismaa'iyl bin Ja'far Al-Madaniy, kutoka kwa Al-'Alaa bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeniswalia Swalaah moja, Allaah Atamswalia mara kumi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1825
- Hadiyth
- 2814
حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ مَوْلَى الْحَسَنِ بْنِ عَلِيٍّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: جَاءَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَوْمًا وَهُوَ يُرَى الْبِشْرُ فِي وَجْهِهِ، فَقِيلَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا نَرَى فِي وَجْهِكَ بِشْرًا لَمْ نَكُنْ نَرَاهُ؟، قَالَ: " أَجَلْ، إِنَّ مَلَكًا أَتَانِي، فَقَالَ لِي: يَا مُحَمَّدُ إِنَّ رَبَّكَ يَقُولُ لَكَ: أَمَا يُرْضِيكَ أَنْ لَا يُصَلِّيَ عَلَيْكَ أَحَدٌ مِنْ أُمَّتِكَ، إِلَّا صَلَّيْتُ عَلَيْهِ عَشْرًا، وَلَا يُسَلِّمَ عَلَيْكَ، إِلَّا سَلَّمْتُ عَلَيْهِ عَشْرًا؟، قَالَ: قُلْتُ: " بَلَى "
Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Sulaymaan mawlaa (mwachwa huru) wa Al-Hasan bin 'Aliy (رضي الله عنهما), kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abiy Twalhah (رضي الله عنه), kutoka kwa baba yake [Abuw Twalhah (رضي الله عنه)], amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuja siku moja, na furaha ikionekana usoni mwake. Pakasemwa: Yaa Rasula-Allaah, hakika sisi tunaona usoni mwako furaha ambayo hatukuwa tukiiona? Akasema: "Naam. Hakika Malaika (عليه السلام) alinijia, akaniambia: Yaa Muhammad, hakika Rabb wako Anakuambia: Je, haikuridhishi kwamba hatakuswalia yeyote katika Ummah wako isipokuwa Nitamswalia mara kumi, wala hatakusalimia (yeyote) isipokuwa Nitamsalimia mara kumi?" Akasema: Nikasema: "Bila shaka."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1825
- Hadiyth
- 2815
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ زَاذَانَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ لِلَّهِ مَلَائِكَةً سَيَّاحِينَ فِي الْأَرْضِ يُبَلِّغُونِي عَنْ أُمَّتِي السَّلَامَ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin As-Saaib, kutoka kwa Zaadhaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Ana Malaika (عليهم السلام) wanaozunguka katika ardhi; wananifikishia Salaam kutoka kwa Ummah wangu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1825
- Hadiyth
- 2816
59-Mlangoباب: في أسماء النبي صلى الله عليه وسلمMlango Wa Kuhusu Majina Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَخْبَرَنَا شُعَيْبُ بْنُ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ جُبَيْرِ بْنِ مُطْعِمٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِنَّ لِي أَسْمَاءً: أَنَا مُحَمَّدٌ، وَأَنَا أَحْمَدُ، وَأَنَا الْمَاحِي الَّذِي يَمْحُو اللَّهُ بِيَ الْكُفْرَ، وَأَنَا الْحَاشِرُ الَّذِي يُحْشَرُ النَّاسُ عَلَى عَقِبِي، وَأَنَا الْعَاقِبُ، وَالْعَاقِبُ الَّذِي لَيْسَ بَعْدَهُ أَحَدٌ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametukhabarisha Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Muhammad bin Jubayr bin Mutw'im, kutoka kwa baba yake [Jubayr bin Mutw'im (رضي الله عنه)], amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika mimi nina majina: Mimi ni Muhammad, na mimi ni Ahmad, na mimi ni Al-Maahiy (Mfutaji) ambaye Allaah Anafuta kwangu ukafiri, na mimi ni Al-Haashir (Mkusanyaji) ambaye watu watakusanywa nyuma yangu, na mimi ni Al-'Aaqib (wa Mwisho); na Al-'Aaqib ni yule ambaye hakuna yeyote baada yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1826
- Hadiyth
- 2817
60-Mlangoباب: في السحتMlango Wa Kuhusu Suht (Chumo La Haraam)
أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُثْمَانَ بْنِ خُثَيْمٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ سَابِطٍ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يَا كَعْبُ بْنَ عُجْرَةَ، إِنَّهُ لَنْ يَدْخُلَ الْجَنَّةَ لَحْمٌ نَبَتَ مِنَ سُحْتٍ"
Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Uthmaan bin Khuthaym, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Saabitw, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Yaa Ka'b bin 'Ujrah, hakika haitaingia Jannah (Pepo) kamwe nyama iliyoota kutokana na suht (chumo la haraam)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1827
- Hadiyth
- 2818
61-Mlangoباب: المؤمن يؤجر في كل شيءMlango Wa Muumini Hulipwa Ujira Katika Kila Kitu
أَخْبَرَنَا أَبُو حَاتِمٍ الْبَصْرِيُّ هُوَ رَوْحُ بِنُ أَسْلَمَ الْبَصْرِيُّ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَنْبَأَنَا ثَابِتٌ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ صُهَيْبٍ، قَالَ: بَيْنَمَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَالِسٌ إِذْ ضَحِكَ، فَقَالَ: "أَلَا تَسْأَلُونِي مِمَّا أَضْحَكُ؟"، فَقَالُوا: مِمَّ تَضْحَكُ؟، قَالَ: "عَجَبًا مِنْ أَمْرِ الْمُؤْمِنِ كُلُّهُ لَهُ خَيْرٌ: إِنْ أَصَابَهُ مَا يُحِبُّ، حَمِدَ اللَّهَ عَلَيْهِ، فَكَانَ لَهُ خَيْرٌ، وَإِنْ أَصَابَهُ مَا يَكْرَهُ فَصَبَرَ، كَانَ لَهُ خَيْرٌ، وَلَيْسَ كُلُّ أَحَدٍ أَمْرُهُ لَهُ خَيْرٌ إِلَّا الْمُؤْمِنَ"
Ametukhabarisha Abuw Haatim Al-Baswriy — naye ni Rawh bin Aslam Al-Baswriy —, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametupa khabari Thaabit, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Abiy Laylaa, kutoka kwa Swuhayb (رضي الله عنه), amesema: Wakati Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa amekaa, ghafla akacheka, akasema: "Je, hamniulizi ni kwa nini ninacheka?" Wakasema: Unacheka kwa nini? Akasema: "Ajabu ya jambo la Muumini! Jambo lake lote ni kheri kwake: akipatwa na anachokipenda, humhimidi Allaah juu yake, ikawa ni kheri kwake; na akipatwa na anachokichukia, akasubiri, ikawa ni kheri kwake. Na si kila mtu jambo lake ni kheri kwake isipokuwa Muumini."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1827
- Hadiyth
- 2819
62-Mlangoباب: لو كان لابن آدم واديان من مالMlango Wa Lau Mwanaadam Angekuwa
Na Mabonde Mawili Ya Mali
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: كُنْتُ أَسْمَعُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَلَا أَدْرِي أَشَيْءٌ أُنْزِلَ عَلَيْهِ أَمْ شَيْءٌ يَقُولُهُ، وَهُوَ يَقُولُ: "لَوْ كَانَ، لِابْنِ آدَمَ وَادِيَانِ مِنْ مَالٍ لَابْتَغَى إِلَيْهِمَا ثَالِثًا، وَلَا يَمْلَأُ جَوْفَ ابْنِ آدَمَ إِلَّا التُّرَابُ، وَيَتُوبُ اللَّهُ عَلَى مَنْ تَابَ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Nilikuwa nikimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) — wala sijui kama ni kitu alichoteremshiwa au ni kitu anachokisema (yeye mwenyewe) —, naye akisema: "Lau mwanaadam angekuwa na mabonde mawili ya mali, angetafuta la tatu (la kuongeza) juu ya hayo mawili; na hakijazi tumbo la mwanaadam isipokuwa mchanga; na Allaah Humkubalia tawbah anayetubu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1828
- Hadiyth
- 2820
63-Mlangoباب: في النهي عن القصصMlango Wa Kuhusu Makatazo Ya Kusimulia Visa
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَقُصُّ إِلَّا أَمِيرٌ، أَوْ مَأْمُورٌ، أَوْ مُرَاءٍ". قُلْتُ لِعَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ: إِنَّا كُنَّا نَسْمَعُ مُتَكَلِّفٌ. فَقَالَ: هَذَا مَا سَمِعْتُ
Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Aamir, kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما)], amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hasimulii visa (mawaidha kwa watu) isipokuwa amiri, au aliyeamrishwa, au mwenye kujionyesha." Nikamwambia 'Amr bin Shu'ayb: Hakika sisi tulikuwa tukisikia: "Mwenye kujikalifisha." Akasema: Hili ndilo nililolisikia.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1828
- Hadiyth
- 2821
64-Mlangoباب: في الرخصة في القصصMlango Wa Kuhusu Ruhusa Ya Kusimulia Visa
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ مَيْسَرَةَ، قالَ: سَمِعْتُ كُرْدُوسًا وَكَانَ قَاصًّا، يَقُولُ: أَخْبَرَنِي رَجُلٌ مِنْ أَهْلِ بَدْرٍ، أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَأَنْ أَقْعُدَ فِي مِثْلِ هَذَا الْمَجْلِسِ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أُعْتِقَ أَرْبَعَ رِقَابٍ". قَالَ: قُلْتُ: أَنَا: أَيَّ مَجْلِسٍ يَعْنِي؟، قَالَ: كَانَ حِينَئِذٍ يَقُصُّ. قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: الرَّجُلُ مِنْ أَصْحَابِ بَدْرٍ هُوَ: عَلِيٌّ
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Bukayr, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Maysarah, amesema: Nilimsikia Kurduws — naye alikuwa msimulizi wa visa (mawaidha kwa watu) — akisema: Amenikhabarisha mtu mmoja miongoni mwa watu wa Badr (رضي الله عنه), kwamba alimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Kwa hakika kuketi katika kikao mfano wa hiki kunapendeza zaidi kwangu kuliko kuwaacha huru watumwa wanne." Akasema: Nikasema: Mimi (niliuliza): Anakusudia kikao gani? Akasema: Alikuwa wakati huo akisimulia visa.
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Mtu huyo miongoni mwa watu wa Badr ni: 'Aliy (رضي الله عنه).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1829
- Hadiyth
- 2822
65-Mlangoباب: لا يلدغ المؤمن من جحر مرتينMlango Wa Muumini Haumwi Kutoka Shimo Mara Mbili
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، قَالَ: حَدَّثَنَا عُقَيْلٌ، عَنِ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ: أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ أَخْبَرَهُ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amesema: Amenisimulia Al-Layth, amesema: Ametusimulia 'Uqayl, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: Amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) alimkhabarisha kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Muumini haumwi kutoka shimo moja mara mbili."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1830
- Hadiyth
- 2823
66-Mlangoباب: الشيطان يجري من ابن آدم مجرى الدمMlango Wa Shaytwaan Hupita
Ndani Ya Mwanaadam Kama Damu Inavyopita
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ مُجَالِدٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: وَرُبَّمَا سَكَتَ عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا تَدْخُلُوا عَلَى الْمُغِيبَاتِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَجْرِي مِنَ ابْنِ آدَمَ كَمَجْرَى الدَّمِ"، قَالُوا: وَمِنْكَ؟، قَالَ: "نَعَمْ، وَلَكِنَّ اللَّهَ أَعَانَنِي عَلَيْهِ فَأَسْلَمَ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Mujaalid, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) — amesema: Na huenda (mara nyingine) alinyamaza (bila kumtaja) Jaabir —, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msiwaingilie wanawake ambao waume zao hawapo, kwani shaytwaan hupita ndani ya mwanaadam kama damu inavyopita." Wakasema: Na kwako (pia)? Akasema: "Ndiyo, lakini Allaah Amenisaidia dhidi yake, basi akasilimu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1831
- Hadiyth
- 2824
67-Mlangoباب: في أشد الناس بلاءMlango Wa Kuhusu Watu Wenye Mitihani Mikali Zaidi
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ مُصْعَبِ بْنِ سَعْدٍ، عَنْ سَعْدٍ، قَالَ: سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ النَّاسِ أَشَدُّ بَلَاءَ؟، قَالَ: "الْأَنْبِيَاءُ، ثُمَّ الْأَمْثَلُ فَالْأَمْثَلُ، يُبْتَلَى الرَّجُلُ عَلَى حَسَبِ دِينِهِ، فَإِنْ كَانَ فِي دِينِهِ صَلَابَةٌ زِيدَ صَلَابَةً، وَإِنْ كَانَ فِي دِينِهِ رِقَّةٌ، خُفِّفَ عَنْهُ، وَلَا يَزَالُ الْبَلَاءُ بِالْعَبْدِ حَتَّى يَمْشِيَ عَلَى الْأَرْضِ مَا لَهُ خَطِيئَةٌ"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Musw'ab bin Sa'd, kutoka kwa Sa'd (رضي الله عنه), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa: Ni watu gani wenye mitihani mikali zaidi? Akasema: "Manabii (عليهم السلام), kisha walio bora zaidi, kisha walio bora zaidi (baada yao). Mtu hujaribiwa kwa kadiri ya Dini yake: ikiwa katika Dini yake kuna uthabiti, huzidishiwa ukali (wa mtihani); na ikiwa katika Dini yake kuna udhaifu, hupunguziwa. Na mtihani hauachi kumwandama mja mpaka atembee juu ya ardhi akiwa hana kosa lolote."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1831
- Hadiyth
- 2825
68-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «لا تطروني»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Msinisifu Kupita Kiasi"
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، حَدَّثَنَا مَالِكٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُبَيْدِ اللَّهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنْ عُمَرَ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا تُطْرُونِي كَمَا تُطْرِي النَّصَارَى عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ، وَلَكِنْ قُولُوا: عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ"
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametusimulia Maalik, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Msinisifu kupita kiasi kama Manaswara walivyomsifu kupita kiasi 'Iysaa bin Maryam (عليه السلام); lakini semeni: Mja wa Allaah na Rasuli Wake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1832
- Hadiyth
- 2826
69-Mlangoباب: إن لله مائة رحمةMlango Wa Hakika Allaah Ana Rehma Mia Moja
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "جَعَلَ اللَّهُ الرَّحْمَةَ مِائَةَ جُزْءٍ فَأَمْسَكَ عِنْدَهُ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ، وَأَنْزَلَ فِي الْأَرْضِ جُزْءًا وَاحِدًا، فَمِنْ ذَلِكَ الْجُزْءِ يَتَرَاحَمُ الْخَلْقُ، حَتَّى تَرْفَعَ الْفَرَسُ حَافِرَهَا عَنْ وَلَدِهَا خَشْيَةَ أَنْ تُصِيبَهُ"
Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Allaah Ameifanya Rehma kuwa sehemu mia moja; Akazuia Kwake sehemu tisini na tisa, na Akateremsha ardhini sehemu moja. Basi kutokana na sehemu hiyo viumbe huhurumiana, hata farasi huinua kwato yake mbali na mtoto wake kwa kuogopa isimpate."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1833
- Hadiyth
- 2827
70-Mlangoباب: من هم بحسنةMlango Wa Mwenye Kukusudia Jema
حَدَّثَنَا عَفَّانُ، حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، حَدَّثَنَا الْجَعْدُ أَبُو عُثْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا رَجَاءٍ الْعُطَارِدِيَّ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا يَرْوِيهِ عَنْ رَبِّهِ عز وجل قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ رَبَّكُمْ رَحِيمٌ: مَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كُتِبَتْ لَهُ حَسَنَةً، فَإِنْ عَمِلَهَا، كُتِبَتْ لَهُ عَشْرًا إِلَى سَبْعِمِائَةِ ضِعْفٍ إِلَى أَضْعَافٍ كَثِيرَةٍ، وَمَنْ هَمَّ بِسَيِّئَةٍ فَلَمْ يَعْمَلْهَا، كُتِبَتْ لَهُ حَسَنَةً، فَإِنْ عَمِلَهَا، كُتِبَتْ وَاحِدَةً، أَوْ يَمْحُوهَا. وَلَا يَهْلِكُ عَلَى اللَّهِ إِلَّا هَالِكٌ"
Ametusimulia 'Affaan, ametusimulia Ja'far bin Sulaymaan, ametusimulia Al-Ja'd Abuw 'Uthmaan, amesema: Nilimsikia Abuw Rajaa Al-'Utwaaridiy, amesema: Nilimsikia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), katika yale anayoyapokea kutoka kwa Rabb wake (عز وجل), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Rabb wenu Ni Mwenye Kurehemu: atakayekusudia jema kisha asilifanye, huandikiwa jema moja; na akilifanya, huandikiwa (mema) kumi mpaka mara mia saba mpaka mara nyingi zaidi. Na atakayekusudia ovu kisha asilifanye, huandikiwa jema moja; na akilifanya, huandikiwa (ovu) moja, au (Allaah) Analifuta. Na hataangamia kwa Allaah isipokuwa mwenye kuangamia."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1833
- Hadiyth
- 2828
71-Mlangoباب: المرء مع من أحبMlango Wa Mtu Yu Pamoja Na Anayempenda
أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ سُلَيْمَانَ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ الْمُغِيرَةِ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ هِلَالٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ الصَّامِتِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ: الرَّجُلُ يُحِبُّ الْقَوْمَ وَلَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَعْمَلَ مِثْلَ عَمَلِهِمْ؟، قَالَ: "أَنْتَ يَا أَبَا ذَرٍّ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ". قُلْتُ: فَإِنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ؟، قَالَ: "أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ"
Ametukhabarisha Sa'iyd bin Sulaymaan, kutoka kwa Sulaymaan bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Asw-Swaamit, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Nilisema: Yaa Rasula-Allaah, mtu anawapenda watu (fulani), lakini hawezi kufanya amali mfano wa amali zao? Akasema: "Wewe, yaa Abaa Dharr, uko pamoja na uliyempenda." Nikasema: Basi hakika mimi nampenda Allaah na Rasuli Wake? Akasema: "Wewe uko pamoja na uliyempenda."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1834
- Hadiyth
- 2829
72-Mlangoباب: إذا تقرب العبد إلى الله تعالىMlango Wa Mja Anapojikurubisha Kwa Allaah (تعالى)
أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا مَهْدِيٌّ، حَدَّثَنَا غَيْلَانُ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، عَنْ مَعْدِي كَرِبَ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَرْوِيهِ عَنْ رَبِّهِ، قَالَ: "يَا ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي، غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ فِيكَ. ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ إِنْ تَلْقَانِي بِقُرَابِ الْأَرْضِ خَطَايَا، لَقِيتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً بَعْدَ أَنْ لَا تُشْرِكَ بِي شَيْئًا، ابْنَ آدَمَ، إِنَّكَ إِنْ تُذْنِبْ حَتَّى يَبْلُغَ ذَنْبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ، ثُمَّ تَسْتَغْفِرُنِي أَغْفِرْ لَكَ وَلَا أُبَالِي"
Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Mahdiy, ametusimulia Ghaylaan, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, kutoka kwa Ma'diy Karib, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akipokea kutoka kwa Rabb wake, amesema: "Yaa mwanaadam! Hakika wewe, muda wote utakaoniomba na kunitarajia, Nitakughufuria juu ya yale yaliyokuwa kwako. Mwanaadam! Hakika wewe ukikutana Nami na makosa yanayokaribia kujaza ardhi, Nitakutana nawe na Maghfirah inayokaribia kuijaza, baada ya kuwa hukunishirikisha na chochote. Mwanaadam! Hakika wewe ukitenda dhambi mpaka dhambi yako ikafika mawingu ya mbingu, kisha ukaniomba Maghfirah, Nitakughufuria, wala Sijali."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1835
- Hadiyth
- 2830
73-Mlangoباب: في البر والإثمMlango Wa Kuhusu Wema Na Dhambi
أَخْبَرَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا صَفْوَانُ هُوَ: ابْنُ عَمْرٍو، قَالَ: حَدَّثَنِي يَحْيَى بْنُ جَابِرٍ الْقَاضِي، عَنِ النَّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ، قَالَ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الْبِرِّ وَالْإِثْمِ، فَقَالَ: "الْبِرُّ حُسْنُ الْخُلُقِ، وَالْإِثْمُ مَا حَاكَ فِي نَفْسِكَ وَكَرِهْتَ أَنْ يَعْلَمَهُ النَّاسُ".
Ametukhabarisha Abul-Mughiyrah, ametusimulia Swafwaan — naye ni Ibn 'Amr —, amesema: Amenisimulia Yahyaa bin Jaabir Al-Qaadhwiy, kutoka kwa An-Nawwaas bin Sam'aan (رضي الله عنه), amesema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu wema na dhambi. Akasema: "Wema ni tabia njema, na dhambi ni kile kinachokutatiza nafsini mwako, na ukachukia watu wakijue."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1836
- Hadiyth
- 2831
أَخْبَرَنَا إِسْحَاق بْنُ عِيسَى، عَنْ مَعْنِ بْنِ عِيسَى، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ صَالِحٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنِ النَّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ، قَالَ: سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ......... فَذَكَرَ بِنَحْوِهِ
Ametukhabarisha Is-haaq bin 'Iysaa, kutoka kwa Ma'n bin 'Iysaa, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Swaalih, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa An-Nawwaas bin Sam'aan (رضي الله عنه), amesema: Nilimuuliza Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) … akataja mfano wake.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1837
- Hadiyth
- 2832
74-Mlangoباب: في حسن الخلقMlango Wa Kuhusu Tabia Njema
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ حَبِيبِ بْنِ أَبِي ثَابِتٍ، عَنْ مَيْمُونِ بْنِ أَبِي شَبِيبٍ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اتَّقِ اللَّهَ حَيْثُمَا كُنْتَ، وَأَتْبِعْ السَّيِّئَةَ الْحَسَنَةَ تَمْحُهَا، وَخَالِقْ النَّاسَ بِخُلُقٍ حَسَنٍ"
Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Habiyb bin Abiy Thaabit, kutoka kwa Maymuwn bin Abiy Shabiyb, kutoka kwa Abuw Dharr (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mche Allaah popote ulipo, na liandamishe ovu kwa jema, litalifuta; na ishi na watu kwa tabia njema."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1837
- Hadiyth
- 2833
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ: ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ، قَالَ: حَدَّثَنِي مُحَمَّدُ بْنُ عَجْلَانَ، عَنْ الْقَعْقَاعِ بْنِ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَكْمَلُ الْمُؤْمِنِينَ إِيمَانًا أَحْسَنُهُمْ خُلُقًا"
Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb —, amesema: Amenisimulia Muhammad bin 'Ajlaan, kutoka kwa Al-Qa'qaa' bin Hakiym, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Waumini waliokamilika zaidi kwa imaan ni walio bora wao kwa tabia."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1838
- Hadiyth
- 2834
75-Mlangoباب: في الرفقMlango Wa Kuhusu Upole
حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ هُوَ ابْنُ سَلَمَةَ عَنْ يُونُسَ، وَحُمَيْدٍ، عَنِ الْحَسَنِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُغَفَّلٍ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ اللَّهَ رَفِيقٌ يُحِبُّ الرِّفْقَ، وَيُعْطِي عَلَيْهِ مَا لَا يُعْطِي عَلَى الْعُنْفِ"
Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad — naye ni Ibn Salamah —, kutoka kwa Yuwnus na Humayd, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mughaffal (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Ni Mpole, Anapenda upole, na Hutoa kwa upole yale Asiyoyatoa kwa ukali."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1840
- Hadiyth
- 2835
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ الْأَوْزَاعِيِّ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عُرْوَةَ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الرِّفْقَ فِي الْأَمْرِ كُلِّهِ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Al-Awzaa'iy, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Urwah, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika Allaah Anapenda upole katika jambo lote."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1841
- Hadiyth
- 2836
76-Mlangoباب: فيمن ذهب بصره فصبرMlango Wa Kuhusu Aliyepoteza Uoni Wake Akasubiri
أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ الْكَرْمَانِيُّ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَنْ أَذْهَبْتُ حَبِيبَتَيْهِ فَصَبَرَ وَاحْتَسَبَ، لَمْ أَرْضَ لَهُ بِثَوَابٍ دُونَ الْجَنَّةِ"
Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Muhammad Al-Karmaaniy, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ambaye Nimemuondoshea vipenzi vyake viwili (macho yake), akasubiri na akataraji malipo (Kwangu), Sitamridhia malipo yoyote yaliyo chini ya Jannah (Pepo)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1841
- Hadiyth
- 2837
77-Mlangoباب: في العدل بين الرعيةMlango Wa Kuhusu Uadilifu Baina Ya Raia
أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَشْهَبِ: جَعْفَرُ بْنُ حَيَّانَ، عَنِ الْحَسَنِ: أَنَّ عُبَيْدَ اللَّهِ بْنَ زِيَادٍ عَادَ مَعْقِلَ بْنَ يَسَارٍ فِي مَرَضِهِ الَّذِي مَاتَ فِيهِ، فَقَالَ لَهُ مَعْقِلٌ: إِنِّي مُحَدِّثُكَ بِحَدِيثٍ سَمِعْتُهُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَوْ عَلِمْتُ أَنَّ لِي حَيَاةً مَا حَدَّثْتُكَ، إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَّهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ، وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ"
Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Abul-Ash-hab Ja'far bin Hayyaan, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba 'Ubaydu-Allaah bin Ziyaad alimtembelea Ma'qil bin Yasaar (رضي الله عنه) katika ugonjwa wake ambao alifariki ndani yake. Ma'qil (رضي الله عنه) akamwambia: Hakika mimi nitakusimulia Hadiyth niliyoisikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم); lau ningejua kwamba nina uhai (zaidi), nisingekusimulia. Hakika mimi nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakuna mja yeyote ambaye Allaah Anamkabidhi uchungaji wa raia, akafa siku anayokufa naye ni mwenye kuwaghushi raia wake, isipokuwa Allaah Amemharamishia Jannah (Pepo)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1842
- Hadiyth
- 2838
78-Mlangoباب: في الطاعة ولزوم الجماعةMlango Wa Kuhusu Utiifu Na Kushikamana Na Jamaa
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا الْوَلِيدُ بْنُ مُسْلِمٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ بْنِ جَابِرٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي زُرَيْقُ بْنُ حَيَّانَ مَوْلَى بَنِي فَزَارَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ مُسْلِمَ بْنَ قَرَظَةَ الْأَشْجَعِيَّ يَقُولُ: سَمِعْتُ عَوْفَ بْنَ مَالِكٍ الْأَشْجَعِيَّ يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "خِيَارُ أَئِمَّتِكُمْ الَّذِينَ تُحِبُّونَهُمْ وَيُحِبُّونَكُمْ، وَتُصَلُّونَ عَلَيْهِمْ وَيُصَلُّونَ عَلَيْكُمْ، وَشِرَارُ أَئِمَّتِكُمْ، الَّذِينَ تُبْغِضُونَهُمْ وَيُبْغِضُونَكُمْ، وَتَلْعَنُونَهُمْ وَيَلْعَنُونَكُمْ". قُلْنَا: أَفَلَا نُنَابِذُهُمْ يَا رَسُولَ اللَّهِ عِنْدَ ذَلِكَ؟ قَالَ: "لَا، مَا أَقَامُوا فِيكُمْ الصَّلَاةَ، أَلَا مَنْ وُلِّيَ عَلَيْهِ وَالٍ فَرَآهُ يَأْتِي شَيْئًا مِنْ مَعْصِيَةِ اللَّهِ، فَلْيَكْرَهْ مَا يَأْتِي مِنْ مَعْصِيَةِ اللَّهِ، وَلَا يَنْزِعَنَّ يَدًا مِنْ طَاعَةٍ". قَالَ ابْنُ جَابِرٍ: فَقُلْتُ: آللَّهِ يَا أَبَا الْمِقْدَامِ! آللَّهِ، أَسَمِعْتَ هَذَا مِنْ مُسْلِمِ بْنِ قَرَظَةَ؟ فَاسْتَقْبَلَ الْقِبْلَةَ، وَجَثَا عَلَى رُكْبَتَيْهِ، فَقَالَ: آللَّهِ لَسَمِعْتُ هَذَا مِنْ مُسْلِمِ بْنِ قَرَظَةَ، يَقُولُ: سَمِعْتُ عَمِّي عَوْفَ بْنَ مَالِكٍ، يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُهُ
Ametusimulia Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Al-Waliyd bin Muslim, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd bin Jaabir, amesema: Amenikhabarisha Zurayq bin Hayyaan, mwachwa huru wa Banuw Fazaarah, kwamba alimsikia Muslim bin Qaradhwah Al-Ashja'iy akisema: Nilimsikia 'Awf bin Maalik Al-Ashja'iy (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Imaam wenu walio bora ni wale mnaowapenda nao wanakupendeni, na mnawaombea nao wanakuombeeni; na Imaam wenu walio waovu ni wale mnaowachukia nao wanakuchukieni, na mnawalaani nao wanakulaanini." Tukasema: Je, basi tusiwatupilie mbali (utiifu wao) wakati huo, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Hapana, maadamu wanasimamisha Swalaah kwenu. Tanabahini! Atakayetawaliwa na mtawala, akamuona anafanya kitu katika maasi ya Allaah, basi ayachukie maasi ya Allaah anayoyafanya, wala asiutoe kabisa mkono (wake) katika utiifu." Ibn Jaabir amesema: Nikasema: Naapa kwa Allaah, yaa Abal-Miqdaam! Naapa kwa Allaah, je, umeisikia hii kutoka kwa Muslim bin Qaradhwah? Akaielekea Qiblah, na akapiga magoti, akasema: Naapa kwa Allaah, kwa hakika nimeisikia hii kutoka kwa Muslim bin Qaradhwah, akisema: Nilimsikia ammi yangu 'Awf bin Maalik (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akiisema.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1843
- Hadiyth
- 2839
79-Mlangoباب: في نفخ الصورMlango Wa Kuhusu Kupulizwa Baragumu
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ سُلَيْمَانَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَسْلَمَ الْعِجْلِيِّ، عَنْ بِشْرِ بْنِ شَغَافٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: سُئِلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الصُّورِ، فَقَالَ: "قَرْنٌ يُنْفَخُ فِيهِ"
Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Sulaymaan At-Taymiy, kutoka kwa Aslam Al-'Ijliy, kutoka kwa Bishr bin Shaghaaf, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu baragumu. Akasema: "Ni pembe inayopulizwa ndani yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1844
- Hadiyth
- 2840
80-Mlangoباب: في شأن الساعة ونزول الرب تعالىMlango Wa Kuhusu Jambo La Saa Na Kushuka Kwa Rabb (تعالى)
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا سَلَمَةَ بْنَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "يَقْبِضُ اللَّهُ الْأَرْضَ وَيَطْوِي السَّمَاءَ بِيَمِينِهِ، ثُمَّ يَقُولُ: أَنَا الْمَلِكُ، أَيْنَ مُلُوكُ الْأَرْضِ؟"
Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', ametusimulia Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Nilimsikia Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Allaah Ataikamata ardhi, na Ataikunja mbingu kwa Mkono Wake wa Kulia, kisha Atasema: Mimi Ndiye Mfalme; wako wapi wafalme wa ardhi?"
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1844
- Hadiyth
- 2841
حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا الصَّعْقُ بْنُ حَزْنٍ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ الْحَكَمِ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ أَبِي وَائِلٍ، عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قِيلَ لَهُ: مَا الْمَقَامُ الْمَحْمُودُ؟، قَالَ: "ذَاكَ يَوْمٌ يَنْزِلُ اللَّهُ تَعَالَى عَلَى كُرْسِيِّهِ يَئِطُّ كَمَا يَئِطُّ الرَّحْلُ الْجَدِيدُ مِنْ تَضَايُقِهِ بِهِ، وَهُوَ كَسَعَةِ مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ، وَيُجَاءُ بِكُمْ حُفَاةً، عُرَاةً، غُرْلًا، فَيَكُونُ أَوَّلَ مَنْ يُكْسَى إِبْرَاهِيمُ، يَقُولُ اللَّهُ تَعَالَى: اكْسُوا خَلِيلِي، فَيُؤْتَى بِرَيْطَتَيْنِ بَيْضَاوَيْنِ مِنْ رِيَاطِ الْجَنَّةِ، ثُمَّ أُكْسَى عَلَى إِثْرِهِ، ثُمَّ أَقُومُ عَنْ يَمِينِ اللَّهِ مَقَامًا يَغْبِطُنِي الْأَوَّلُونَ وَالْآخِرُونَ"
Ametusimulia Muhammad bin Al-Fadhwl, ametusimulia Asw-Swa'q bin Hazn, kutoka kwa 'Aliy bin Al-Hakam, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Umayr, kutoka kwa Abuw Waail, kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: Aliambiwa: Ni nini cheo cha kuhimidiwa? Akasema: "Hiyo ni siku ambayo Allaah (تعالى) Atashuka juu ya Kursiyy (Kiti) Yake, nayo inatoa mlio kama unavyotoa mlio tandiko jipya (la ngamia) kutokana na kubanwa kwake na Yeye; nayo ni kama upana wa kilicho baina ya mbingu na ardhi. Na mtaletwa mkiwa pekupeku, uchi, wasiotahiriwa. Basi wa kwanza atakayevishwa (nguo) atakuwa ni Ibraahiym (عليه السلام); Allaah (تعالى) Atasema: Mvisheni Khaliyl (kipenzi mwandani) Wangu. Basi zitaletwa shuka mbili nyeupe miongoni mwa shuka za Jannah (Pepo); kisha nitavishwa mimi baada yake. Kisha nitasimama kuliani mwa Allaah kisimamo ambacho watanionea wivu mwema (bila husuda) wa mwanzo na wa mwisho."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1845
- Hadiyth
- 2842
81-Mlangoباب: النظر إلى الله تعالىMlango Wa Kumtazama Allaah (تعالى)
حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ: الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، عَنْ شُعَيْبِ بْنِ أَبِي حَمْزَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ الْمُسَيِّبِ، وَعَطَاءُ بْنُ يَزِيدَ اللَّيْثِيُّ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ أَخْبَرَهُمَا: أَنَّ النَّاسَ، قَالُوا لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: هَلْ نَرَى رَبَّنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ؟ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هَلْ تُمَارُونَ فِي رُؤْيَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ لَيْسَ دُونَهُ سَحَابٌ؟"، قَالُوا: لَا، يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: "فَهَلْ تُمَارُونَ فِي الشَّمْسِ لَيْسَ دُونَهَا سَحَابٌ؟"، قَالُوا: لَا، قَالَ: "فَإِنَّكُمْ تَرَوْنَهُ كَذَلِكَ"
Ametusimulia Abul-Yamaan Al-Hakam bin Naafi', kutoka kwa Shu'ayb bin Abiy Hamzah, kutoka kwa Az-Zuhriy, amenikhabarisha Sa'iyd bin Al-Musayyib na 'Atwaa bin Yaziyd Al-Laythiy, kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) aliwakhabarisha wawili hao kwamba watu walimwambia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Je, tutamwona Rabb wetu Siku ya Qiyaamah? Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Je, mnatiliana shaka katika kuuona mwezi usiku wa mwezi mpevu, pasipo mawingu mbele yake?" Wakasema: Hapana, yaa Rasula-Allaah. Akasema: "Basi je, mnatiliana shaka katika (kuliona) jua pasipo mawingu mbele yake?" Wakasema: Hapana. Akasema: "Basi hakika nyinyi mtamwona hivyo hivyo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1846
- Hadiyth
- 2843
82-Mlangoباب: في صفة الحشرMlango Wa Kuhusu Sifa Ya Kukusanywa
حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الطَّيَالِسِيُّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، قَالَ: حَدَّثَنَا الْمُغِيرَةُ بْنُ النُّعْمَانِ، قَالَ: سَمِعْتُ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ يُحَدِّثُ، عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: خَطَبَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: "يَا أَيُّهَا النَّاسُ، إِنَّكُمْ تُحْشَرُونَ إِلَى اللَّهِ تَعَالَى حُفَاةً عُرَاةً غُرْلًا، ثُمَّ قَرَأَ: {كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْدًا عَلَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ}"
Ametusimulia Abul-Waliyd Atw-Twayaalisiy, ametusimulia Shu'bah, amesema: Ametusimulia Al-Mughiyrah bin An-Nu'maan, amesema: Nilimsikia Sa'iyd bin Jubayr akisimulia kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikhutubu, akasema: "Enyi watu! Hakika nyinyi mtakusanywa kwa Allaah (تعالى) mkiwa pekupeku, uchi, wasiotahiriwa." Kisha akasoma:
كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْدًا عَلَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ
Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu Yetu. Hakika Sisi Ni Wenye Kufanya [Al-Anbiyaa (21:104)]
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1847
- Hadiyth
- 2844
83-Mlangoباب: في سجود المؤمنين يوم القيامةMlango Wa Kuhusu Kusujudu Kwa Waumini Siku Ya Qiyaamah
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الْبَزَّازُ، عَنْ يُونُسَ بْنِ بُكَيْرٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي ابْنُ إِسْحَاق، قَالَ: أَخْبَرَنِي سَعِيدُ بْنُ يَسَارٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِذَا جَمَعَ اللَّهُ الْعِبَادَ فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ، نَادَى مُنَادٍ: لِيَلْحَقْ كُلُّ قَوْمٍ بِمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ، فَيَلْحَقُ كُلُّ قَوْمٍ بِمَا كَانُوا يَعْبُدُونَ، وَيَبْقَى النَّاسُ عَلَى حَالِهِمْ، فَيَأْتِيهِمْ، فَيَقُولُ: مَا بَالُ النَّاسِ ذَهَبُوا وَأَنْتُمْ هَا هُنَا؟، فَيَقُولُونَ: نَنْتَظِرُ إِلَهَنَا، فَيَقُولُ: هَلْ تَعْرِفُونَهُ؟ فَيَقُولُونَ: إِذَا تَعَرَّفَ إِلَيْنَا، عَرَفْنَاهُ، فَيَكْشِفُ لَهُمْ عَنْ سَاقِهِ فَيَقَعُونَ سُجُودًا، فَذَلِكَ قَوْلُ اللَّهِ تَعَالَى: {يَوْمَ يُكْشَفُ عَنْ سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلا يَسْتَطِيعُونَ} يَبْقَى كُلُّ مُنَافِقٍ فَلَا يَسْتَطِيعُ أَنْ يَسْجُدَ، ثُمَّ يَقُودُهُمْ إِلَى الْجَنَّةِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Al-Bazzaaz, kutoka kwa Yuwnus bin Bukayr, amesema: Amenikhabarisha Ibn Is-haaq, amesema: Amenikhabarisha Sa'iyd bin Yasaar, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Allaah Atakapowakusanya waja katika uwanja mmoja, mwenye kunadi atanadi: Kila kaumu iungane na kile walichokuwa wakikiabudu. Basi kila kaumu itaungana na kile walichokuwa wakikiabudu, na watu watabakia katika hali yao. Atawajia, Aseme: Wana nini watu wameondoka nanyi mko hapa? Watasema: Tunamsubiri Mwabudiwa wetu. Atasema: Je, mnamjua? Watasema: Atakapojitambulisha kwetu, tutamjua. Basi Atawafunulia Muundi Wake, nao wataanguka wakisujudu. Basi hiyo ndiyo Kauli ya Allaah (تعالى):
يَوْمَ يُكْشَفُ عَنْ سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى السُّجُودِ فَلا يَسْتَطِيعُونَ
Siku utakapofunuliwa Muundi na wataitwa kusujudu lakini hawatoweza. [Al-Qalam (68:42)]
Atabakia kila mnafiki, hatoweza kusujudu. Kisha Atawaongoza kwenda Jannah (Pepo)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1848
- Hadiyth
- 2845
84-Mlangoباب: في الشفاعةMlango Wa Kuhusu Shafaa'ah (Uombezi)
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ زِيَادٍ، حَدَّثَنَا دُخَيْنٌ الْحَجْرِيُّ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "إِذَا جَمَعَ اللَّهُ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ فَقَضَى بَيْنَهُمْ وَفَرَغَ مِنَ الْقَضَاءِ، قَالَ الْمُؤْمِنُونَ: قَدْ قَضَى بَيْنَنَا رَبُّنَا، فَمَنْ يَشْفَعُ لَنَا إِلَى رَبِّنَا؟ فَيَقُولُونَ: انْطَلِقُوا إِلَى آدَمَ، فَإِنَّ اللَّهَ خَلَقَهُ بِيَدِهِ، وَكَلَّمَهُ، فَيَأْتُونَهُ، فَيَقُولُونَ: قُمْ فَاشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّنَا. فَيَقُولُ آدَمُ: عَلَيْكُمْ بِنُوحٍ، فَيَأْتُونَ نُوحًا، فَيَدُلُّهُمْ عَلَى إِبْرَاهِيمَ، فَيَأْتُونَ إِبْرَاهِيمَ، فَيَدُلُّهُمْ عَلَى مُوسَى، فَيَأْتُونَ مُوسَى، فَيَدُلُّهُمْ عَلَى عِيسَى، فَيَأْتُونَ عِيسَى، فَيَقُولُ: أَدُلُّكُمْ عَلَى النَّبِيِّ الْأُمِّيِّ. قَالَ: فَيَأْتُونِي فَيَأْذَنُ اللَّهُ عز وجل لِي أَنْ أَقُومَ إِلَيْهِ، فَيَثُورُ مَجْلِسِي أَطْيَبَ رِيحٍ شَمَّهَا أَحَدٌ قَطُّ، حَتَّى آتِيَ رَبِّي فَيُشَفِّعَنِي وَيَجْعَلَ لِي نُورًا مِنْ شَعْرِ رَأْسِي إِلَى ظُفْرِ قَدَمِي، فَيَقُولُ الْكَافِرُونَ عِنْدَ ذَلِكَ لِإِبْلِيسَ: قَدْ وَجَدَ الْمُؤْمِنُونَ مَنْ يَشْفَعُ لَهُمْ، فَقُمْ أَنْتَ فَاشْفَعْ لَنَا إِلَى رَبِّكَ، فَإِنَّكَ أَنْتَ أَضْلَلْتَنَا. قَالَ: فَيَقُومُ، فَيَثُورُ مَجْلِسُهُ أَنْتَنَ رِيحٍ شَمَّهَا أَحَدٌ قَطُّ، ثُمَّ يَعْظُمُ لِجَهَنَّمَ، فَيَقُولُ عِنْدَ ذَلِكَ: {وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدْتُكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ}" إِلَى آخِرِ الْآيَةِ
Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Ziyaad, ametusimulia Dukhayn Al-Hajriy, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniy (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Allaah Atakapowakusanya wa mwanzo na wa mwisho, Akahukumu baina yao na Akamaliza hukumu, Waumini watasema: Rabb wetu Amekwishahukumu baina yetu; basi nani atatuombea kwa Rabb wetu? Watasema: Nendeni kwa Aadam (عليه السلام), kwani Allaah Alimuumba kwa Mkono Wake, na Akamsemesha. Watamjia, waseme: Simama, utuombee kwa Rabb wetu. Aadam (عليه السلام) atasema: Shikamaneni na Nuwh (عليه السلام). Watamjia Nuwh (عليه السلام), naye atawaelekeza kwa Ibraahiym (عليه السلام). Watamjia Ibraahiym (عليه السلام), naye atawaelekeza kwa Muwsaa (عليه السلام). Watamjia Muwsaa (عليه السلام), naye atawaelekeza kwa 'Iysaa (عليه السلام). Watamjia 'Iysaa (عليه السلام), naye atasema: Nitakuelekezeni kwa Nabiy asiyejua kusoma wala kuandika (صلى الله عليه وآله وسلم). Akasema: Watanijia, na Allaah (عز وجل) Ataniruhusu nisimame Kwake. Kikao changu kitafukuta harufu nzuri kabisa ambayo hajapata kuinusa yeyote, mpaka nimfikie Rabb wangu, Anikubalie uombezi wangu, na Anijaalie nuru kuanzia nywele za kichwa changu mpaka ukucha wa mguu wangu. Hapo makafiri watamwambia Ibliys: Waumini wamepata wa kuwaombea; basi simama wewe utuombee kwa Rabb wako, kwani wewe ndiye uliyetupoteza. Akasema: Atasimama, na kikao chake kitafukuta harufu mbaya kabisa ambayo hajapata kuinusa yeyote. Kisha atakuwa mkubwa kwa ajili ya Jahannam, na atasema wakati huo:
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدْتُكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ
Na shaytwaan atasema litakapokidhiwa jambo: Hakika Allaah Alikuahidini ahadi ya haki (na Ameitimiza), nami nilikuahidini kisha nikakukhalifuni [Ibraahiym (14:22)]
" mpaka mwisho wa Aayah.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1849
- Hadiyth
- 2846
85-Mlangoباب: إن لكل نبي دعوةMlango Wa Hakika Kila Nabiy Ana Du'aa
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، أَنَّ أَبَا هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لِكُلِّ نَبِيٍّ دَعْوَةٌ، وَأُرِيدُ إِنْ شَاءَ اللَّهُ تَعَالَى أَنْ أَخْتَبِئَ دَعْوَتِي شَفَاعَةً لِأُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ"،
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenisimulia Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan, kwamba Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Kila Nabiy ana Du'aa; nami nataka — Akipenda Allaah (تعالى) — kuihifadhi Du'aa yangu iwe Shafaa'ah (uombezi) kwa Ummah wangu Siku ya Qiyaamah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1850
- Hadiyth
- 2847
حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي عَمْرُو بْنُ أَبِي سُفْيَانَ بْنِ أَسِيدِ بْنِ جَارِيَةَ مِثْلَ ذَلِكَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ
Ametusimulia Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha 'Amr bin Abiy Sufyaan bin Asiyd bin Jaariyah mfano wa hivyo, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1851
- Hadiyth
- 2848
86-Mlangoباب: «يدخل الجنة سبعون ألفا من أمتي بغير حساب»Mlango Wa "Wataingia Jannah (Pepo) Elfu Sabini
Katika Ummah Wangu Bila Ya Hesabu"
حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ زِيَادٍ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ يُحَدِّثُ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، أَنَّهُ قَالَ: "يَدْخُلُ الْجَنَّةَ سَبْعُونَ أَلْفًا مِنْ أُمَّتِي بِغَيْرِ حِسَابٍ". فَقَالَ عُكَّاشَةُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ ادْعُ اللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ، فَدَعَا، فَقَالَ آخَرُ: ادْعُ اللَّهَ لِي، فَقَالَ: "سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ"
Ametusimulia Abul-Waliyd, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Muhammad bin Ziyaad, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisimulia kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba alisema: "Wataingia Jannah (Pepo) elfu sabini katika Ummah wangu bila ya hesabu." 'Ukkaashah (رضي الله عنه) akasema: Yaa Rasula-Allaah, muombe Allaah Anijaalie kuwa miongoni mwao. Akamuombea. Mtu mwingine akasema: Niombee kwa Allaah (nami). Akasema: "'Ukkaashah (رضي الله عنه) amekutangulia kwayo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1851
- Hadiyth
- 2849
87-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم:
«يدخل الجنة بشفاعة رجل من أمتي سبعون ألفا»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
: "Wataingia Jannah (Pepo)
Kwa Shafaa'ah (Uombezi) Ya Mtu Mmoja
Katika Ummah Wangu Elfu Sabini"
أَخْبَرَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ خَالِدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ شَقِيقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي الْجَدْعَاءِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "لَيَدْخُلَنَّ الْجَنَّةَ بِشَفَاعَةِ رَجُلٍ مِنْ أُمَّتِي أَكْثَرُ مِنْ بَنِي تَمِيمٍ". قَالُوا: سِوَاكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟، قَالَ: "سِوَايَ"
Ametukhabarisha Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Shaqiyq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Abil-Jad'aa (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Hakika wataingia Jannah (Pepo) kwa Shafaa'ah (uombezi) ya mtu mmoja katika Ummah wangu (watu) wengi zaidi kuliko Banuw Tamiym." Wakasema: Asiyekuwa wewe, yaa Rasula-Allaah? Akasema: "Asiyekuwa mimi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1852
- Hadiyth
- 2850
88-Mlangoباب: قول الله تعالى: {يوم تبدل الأرض غير الأرض والسموات}Mlango Wa Kauli Ya Allaah (تعالى) : «Siku ardhi itakapobadilishwa
kuwa ardhi nyingine na mbingu pia» [Ibraahiym (14:48)]
حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا خَالِدٌ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ: قُلْتُ لِعَائِشَةَ: يَا أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، أَرَأَيْتِ قَوْلَ اللَّهِ تَعَالَى: {يَوْمَ تُبَدَّلُ الأَرْضُ غَيْرَ الأَرْضِ وَالسَّمَوَاتُ وَبَرَزُوا لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ} أَيْنَ النَّاسُ يَوْمَئِذٍ؟ قَالَتْ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ ذَلِكَ، فَقَالَ: "عَلَى الصِّرَاطِ"
Ametusimulia 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Khaalid, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Masruwq, amesema: Nilimwambia 'Aaishah (رضي الله عنها): Yaa Ummal-Muuminiyn, unaonaje Kauli ya Allaah (تعالى):
يَوْمَ تُبَدَّلُ الأَرْضُ غَيْرَ الأَرْضِ وَالسَّمَوَاتُ وَبَرَزُوا لِلَّهِ الْوَاحِدِ الْقَهَّارِ
Siku ardhi itakapobadilishwa kuwa ardhi nyingine na mbingu pia, na (viumbe wote) watahudhuria kwa Allaah Mmoja Pekee, Asiyepingika. [Ibraahiym (14:48)]
Watu watakuwa wapi siku hiyo? Akasema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu hilo, akasema: "Juu ya Asw-Swiraatw (daraja lililowekwa juu ya Jahannam)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1852
- Hadiyth
- 2851
89-Mlangoباب: في ورود النارMlango Wa Kuhusu Kuufikia Moto
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ السُّدِّيِّ، قَالَ: سَأَلْتُ مُرَّةَ عَنْ قَوْلِ اللَّهِ عز وجل: {وَإِنْ مِنْكُمْ إِلا وَارِدُهَا كَانَ عَلَى رَبِّكَ حَتْمًا مَقْضِيًّا} فَحَدَّثَنِي: أَنَّ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ مَسْعُودٍ حَدَّثَهُمْ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَرِدُ النَّاسُ النَّارَ ثُمَّ يَصْدُرُونَ عَنْهَا بِأَعْمَالِهِمْ، فَأَوَّلُهُمْ كَلَمْحِ الْبَرْقِ، ثُمَّ كَالرِّيحِ، ثُمَّ كَحُضْرِ الْفَرَسِ، ثُمَّ كَالرَّاكِبِ فِي رَحْلِهِ، ثُمَّ كَشَدِّ الرَّجُلِ، ثُمَّ كَمَشْيِهِ"
Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa As-Suddiy, amesema: Nilimuuliza Murrah kuhusu Kauli ya Allaah (عز وجل):
وَإِنْ مِنْكُمْ إِلا وَارِدُهَا كَانَ عَلَى رَبِّكَ حَتْمًا مَقْضِيًّا
Na hakuna yeyote miongoni mwenu, isipokuwa ni mwenye kuufikia (moto). Hiyo ni hukumu ya Rabb wako lazima itimizwe. [Maryam (19:71)]
Akanisimulia kwamba 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) aliwasimulia, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Watu wataufikia moto, kisha watatoka humo kwa (kadiri ya) amali zao: basi wa kwanza wao (atapita) kama mmweko wa umeme, kisha (mwingine) kama upepo, kisha kama mbio za farasi, kisha kama mpandaji juu ya kipando chake, kisha kama mbio za mtu, kisha kama mwendo wake (wa kawaida)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1853
- Hadiyth
- 2852
90-Mlangoباب: في ذبح الموتMlango Wa Kuhusu Kuchinjwa Kwa Mauti
أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يُؤْتَى بِالْمَوْتِ كَكَبْشٍ أَغْبَرَ، فَيُوقَفُ بَيْنَ الْجَنَّةِ وَالنَّارِ، فَيُقَالُ: يَا أَهْلَ الْجَنَّةِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، وَيُقَالُ: يَا أَهْلَ النَّارِ، فَيَشْرَئِبُّونَ وَيَنْظُرُونَ، وَيَرَوْنَ أَنْ قَدْ جَاءَ الْفَرَجُ، فَيُذْبَحُ وَيُقَالُ: خُلُودٌ لَا مَوْتَ"
Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mauti yataletwa kama kondoo dume mwenye rangi ya vumbi, yasimamishwe baina ya Jannah (Pepo) na moto. Kisha patasemwa: Enyi watu wa Jannah! Watanyoosha shingo zao na watatazama. Na patasemwa: Enyi watu wa motoni! Watanyoosha shingo zao na watatazama, na watadhani kwamba faraja imekuja. Kisha (mauti) yatachinjwa, na patasemwa: Ni kudumu milele, hakuna mauti."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1853
- Hadiyth
- 2853
91-Mlangoباب: في تحذير النارMlango Wa Kuhusu Kutahadharisha Na Moto
أَخْبَرَنَا عُثْمَانُ بْنُ عُمَرَ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سِمَاكٍ، عَنْ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَخْطُبُ، فَقَالَ: "أَنْذَرْتُكُمْ النَّارَ، أَنْذَرْتُكُمْ النَّارَ، أَنْذَرْتُكُمْ النَّارَ" فَمَا زَالَ يَقُولُهَا حَتَّى لَوْ كَانَ فِي مَقَامِي هَذَا، لَسَمِعَهُ أَهْلُ السُّوقِ، حَتَّى سَقَطَتْ خَمِيصَةٌ كَانَتْ عَلَيْهِ عِنْدَ رِجْلَيْهِ
Ametukhabarisha 'Uthmaan bin 'Umar, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa An-Nu'maan bin Bashiyr (رضي الله عنهما), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akikhutubu, akasema: "Nimekuonyeni moto! Nimekuonyeni moto! Nimekuonyeni moto!" Basi hakuacha kuyasema, kiasi kwamba lau angekuwa mahali hapa nilipo, watu wa sokoni wangemsikia; mpaka shuka lenye alama (la sufu) alilokuwa amelivaa likaanguka miguuni mwake.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1854
- Hadiyth
- 2854
92-Mlangoباب: فيمن قال: إذا مت فأحرقوني بالنارMlango Wa Kuhusu Aliyesema: Nikifa, Basi Nichomeni Kwa Moto
أَخْبَرَنَا النَّضْرُ بْنُ شُمَيْلٍ، قَالَ: أَخْبَرَنَا بَهْزُ بْنُ حَكِيمٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ، قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "كَانَ عَبْدٌ مِنْ عِبَادِ اللَّهِ، وَكَانَ لَا يَدِينُ لِلَّهِ دِينًا، وَإِنَّهُ لَبِثَ حَتَّى ذَهَبَ مِنْهُ عُمُرٌ وَبَقِيَ عُمُرٌ، فَعَلِمَ أَنَّهُ لَمْ يَبْتَئِرْ عِنْدَ اللَّهِ خَيْرًا، فَدَعَا بَنِيهِ، فَقَالَ: أَيُّ أَبٍ تَعْلَمُونِي؟ قَالُوا: خَيْرُهُ يَا أَبَانَا، قَالَ: فَإِنِّي لَا أَدَعُ عِنْدَ أَحَدٍ مِنْكُمْ مَالًا هُوَ مِنِّي إِلَّا أَخَذْتُهُ، أَوْ لَتَفْعَلُنَّ مَا آمُرُكُمْ، قَالَ: فَأَخَذَ مِنْهُمْ مِيثَاقًا وَرَبِّي، قَالَ: أَمَّا أَنَا إِذَا مُتُّ فَخُذُونِي فَأَحْرِقُونِي بِالنَّارِ حَتَّى إِذَا كُنْتُ حُمَمًا فَدُقُّونِي ثُمَّ اذْرُونِي فِي الرِّيحِ، قَالَ: فَفَعَلُوا ذَلِكَ بِهِ وَرَبِّ مُحَمَّدٍ حِينَ مَاتَ، فَجِيءَ بِهِ أَحْسَنَ مَا كَانَ قَطُّ، فَعُرِضَ عَلَى رَبِّهِ، فَقَالَ: مَا حَمَلَكَ عَلَى النَّارِ؟ قَالَ: خَشْيَتُكَ يَا رَبِّ، قَالَ: إِنِّي أَسْمَعُكَ لَرَاهِبًا، قَالَ: فَتِيبَ عَلَيْهِ". قَالَ أَبُو مُحَمَّدٍ: يَبْتَئِرُ، يَدَّخِرُ
Ametukhabarisha An-Nadhwr bin Shumayl, amesema: Ametukhabarisha Bahz bin Hakiym, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake (رضي الله عنه), amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Alikuwako mja mmoja miongoni mwa waja wa Allaah, naye hakuwa akishika Dini yoyote kwa ajili ya Allaah. Naye aliishi mpaka sehemu ya umri wake ikapita na sehemu ikabakia; akajua kwamba hakuweka akiba ya kheri yoyote kwa Allaah. Akawaita wanawe, akasema: Mnanijua kuwa ni baba wa namna gani? Wakasema: (Wewe ni) bora wao, yaa baba yetu. Akasema: Basi hakika mimi sitaiacha kwa yeyote miongoni mwenu mali iliyotoka kwangu isipokuwa nitaichukua, au mtafanya ninayokuamrisheni." Akasema: "Basi akachukua kutoka kwao ahadi nzito — naapa kwa Rabb wangu! — akasema: Ama mimi, nitakapokufa, basi nichukueni mnichome kwa moto, mpaka nitakapokuwa makaa, niponde-pondeni, kisha nipeperusheni katika upepo." Akasema: "Basi wakamfanyia hivyo — naapa kwa Rabb wa Muhammad — alipokufa. Akaletwa (mbele ya Allaah) katika hali nzuri kabisa kuliko alivyowahi kuwa, akahudhurishwa mbele ya Rabb wake. Akasema: Ni nini kilichokupelekea kwenye moto? Akasema: Ni kukukhofu Wewe, yaa Rabbi. Akasema: Hakika Mimi Nakusikia kuwa ni mwenye kukhofu (kweli)." Akasema: "Basi akapokelewa tawbah yake."
Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yabta-ir maana yake ni: yaddakhir (anaweka akiba).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1855
- Hadiyth
- 2855
93-Mlangoباب: دخلت امرأة النار في هرةMlango Wa Mwanamke Aliingia Motoni Kwa Sababu Ya Paka
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، أَنْبَأَنَا مَالِكٌ، عَنْ نَافِعٍ، عَنِ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "دَخَلَتِ امْرَأَةٌ النَّارَ فِي هِرَّةٍ، فَقِيلَ: لَا أَنْتِ أَطْعَمْتِيهَا وَسَقَيْتِيهَا، وَلَا أَنْتِ أَرْسَلْتِيهَا فَتَأْكُلَ مِنْ خَشَاشِ الْأَرْضِ"
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametupa khabari Maalik, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwanamke mmoja aliingia motoni kwa sababu ya paka. Akaambiwa: Wewe hukumlisha wala hukumnywesha, wala hukumwachia ale wadudu wa ardhini."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1856
- Hadiyth
- 2856
94-Mlangoباب: في شدة عذاب أهل النارMlango Wa Kuhusu Ukali Wa Adhabu Ya Watu Wa Motoni
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي أَيُّوبَ بْنِ مِقْلَاصٍ مَوْلَى أَبِي هُرَيْرَةَ، وَكُنْيَتُهُ: أَبُو يَحْيَى، قَالَ: سَمِعْتُ دَرَّاجًا: أَبَا السَّمْحِ، يَقُولُ: سَمِعْتُ أَبَا الْهَيْثَمِ، يَقُولُ: سَمِعْتُ أَبَا سَعِيدٍ الْخُدْرِيَّ، يَقُولُ: قَالَ: رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يُسَلَّطُ عَلَى الْكَافِرِ فِي قَبْرِهِ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ تِنِّينًا تَنْهَشُهُ وَتَلْدَغُهُ حَتَّى تَقُومَ السَّاعَةُ، وَلَوْ أَنَّ تِنِّينًا مِنْهَا نَفَخَ فِي الْأَرْضِ مَا أَنْبَتَتْ خَضْرَاءَ"
Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd bin Abiy Ayyuwb bin Miqlaasw, mwachwa huru wa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), na kunyah (jina la ubaba) yake ni Abuw Yahyaa, amesema: Nilimsikia Darraaj Abus-Samh akisema: Nilimsikia Abul-Haytham akisema: Nilimsikia Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Majoka tisini na tisa yatapewa mamlaka juu ya kafiri katika kaburi lake, yakimtafuna na kumuuma mpaka Saa (ya Qiyaamah) itakaposimama. Na lau joka moja kati yake lingepuliza katika ardhi, isingeotesha kitu kibichi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1857
- Hadiyth
- 2857
95-Mlangoباب: في أودية جهنمMlango Wa Kuhusu Mabonde Ya Jahannam
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَزْهَرُ بْنُ سِنَانٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ وَاسِعٍ، قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى بِلَالِ بْنِ أَبِي بُرْدَةَ، فَقُلْتُ: إِنَّ أَبَاكَ حَدَّثَنِي، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ فِي جَهَنَّمَ وَادِيًا يُقَالُ لَهُ: هَبْهَبُ، يَسْكُنُهُ كُلُّ جَبَّارٍ" فَإِيَّاكَ أَنْ تَكُونَ مِنْهُمْ
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Azhar bin Sinaan, kutoka kwa Muhammad bin Waasi', amesema: Niliingia kwa Bilaal bin Abiy Burdah, nikasema: Hakika baba yako alinisimulia kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika katika Jahannam kuna bonde linaloitwa Habhab; analikalia kila jabari." Basi jihadhari usiwe miongoni mwao.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1858
- Hadiyth
- 2858
96-Mlangoباب: ما يخرج الله من النار برحمتهMlango Wa Wale Ambao Allaah Atawatoa Motoni
Kwa Rehma Yake
أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ يَزِيدَ أَبِي مَسْلَمَةَ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَمَّا أَهْلُ النَّارِ الَّذِينَ هُمْ أَهْلُ النَّارِ، فَإِنَّهُمْ لَا يَمُوتُونَ فِي النَّارِ، وَأَمَّا نَاسٌ مِنَ النَّاسِ، فَإِنَّ النَّارَ تُصِيبُهُمْ عَلَى قَدْرِ ذُنُوبِهِمْ، فَيُحْرَقُونَ فِيهَا حَتَّى إِذَا صَارُوا فَحْمًا، أُذِنَ فِي الشَّفَاعَةِ فَيَخْرُجُونَ مِنَ النَّارِ ضَبَائِرَ ضَبَائِرَ، فَيُنْثَرُونَ عَلَى أَنْهَارِ الْجَنَّةِ. فَيُقَالُ لِأَهْلِ الْجَنَّةِ: أَفِيضُوا عَلَيْهِمْ مِنَ الْمَاءِ. قَالَ: فَيُفِيضُونَ عَلَيْهِمْ فَتَنْبُتُ لُحُومُهُمْ كَمَا تَنْبُتُ الْحِبَّةُ فِي حَمِيلِ السَّيْلِ"
Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Sa'iyd bin Yaziyd Abuw Maslamah, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ama watu wa motoni ambao wao ndio watu wake (hasa), hakika wao hawafi motoni. Na ama watu fulani miongoni mwa watu, hakika moto utawasibu kwa kadiri ya madhambi yao, watachomwa humo mpaka watakapokuwa makaa; (hapo) itatolewa idhini ya Shafaa'ah (uombezi), basi watatoka motoni makundi makundi, watatawanywa juu ya mito ya Jannah (Pepo). Kisha watu wa Jannah wataambiwa: Wamiminieni maji." Akasema: "Basi watawamiminia, na nyama zao zitaota kama inavyoota mbegu iliyoko katika takataka zinazobebwa na mafuriko."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1858
- Hadiyth
- 2859
97-Mlangoباب: في أبواب الجنةMlango Wa Kuhusu Milango Ya Jannah (Pepo)
حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ حُمَيْدٍ، حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ هِشَامٍ، عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ عُثْمَانَ الثَّقَفِيِّ، عَنْ أَبِي صَادِقٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ يَزِيدَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لِلْجَنَّةِ ثَمَانِيَةُ أَبْوَابٍ"
Ametusimulia Ahmad bin Humayd, ametusimulia Mu'aawiyah bin Hishaam, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa 'Uthmaan Ath-Thaqafiy, kutoka kwa Abuw Swaadiq, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Yaziyd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Jannah (Pepo) ina milango minane."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1859
- Hadiyth
- 2860
98-Mlangoباب: من يدخل الجنة لا يبأسMlango Wa Atakayeingia Jannah (Pepo) Hatapata Dhiki
حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي رَافِعٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ دَخَلَ الْجَنَّةَ يَنْعَمُ لَا يَبْؤُسُ: لَا تَبْلَى ثِيَابُهُ، وَلَا يَفْنَى شَبَابُهُ، وَلَهُ فِي الْجَنَّةِ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ"
Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Raafi', kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayeingia Jannah (Pepo) atakuwa katika neema, hatapata dhiki: nguo zake hazichakai, wala ujana wake haumaliziki; na atapata katika Jannah yale ambayo jicho halijapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala hayajapata kupita katika moyo wa mwanaadam."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1860
- Hadiyth
- 2861
99-Mlangoباب: لموضع سوط في الجنة خير من الدنيا وما فيهاMlango Wa Hakika Mahali Pa Mjeledi
Katika Jannah (Pepo) Ni Bora Kuliko Dunia
Na Vilivyomo Ndani Yake
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ فِي الْجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا فِيهَا، وَاقْرَؤُوا إِنْ شِئْتُمْ: {كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلا مَتَاعُ الْغُرُورِ}" الْآيَةَ
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika mahali pa mjeledi wa mmoja wenu katika Jannah (Pepo) ni bora kuliko dunia na vilivyomo ndani yake. Na someni mkipenda:
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فَمَنْ زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلا مَتَاعُ الْغُرُورِ
Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah, huyo kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu. [Aal-‘Imraan (3:185)]
mpaka mwisho wa Aayah."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1861
- Hadiyth
- 2862
100-Mlangoباب: في بناء الجنةMlango Wa Kuhusu Ujenzi Wa Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ سَعْدَانَ الْجُهَنِيِّ، عَنْ أَبِي مُجَاهِدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو مُدِلَّةَ: أَنَّهُ سَمِعَ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: قُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ: الْجَنَّةُ مَا بِنَاؤُهَا؟، قَالَ: "لَبِنَةٌ مِنْ ذَهَبٍ وَلَبِنَةٌ مِنْ فِضَّةٍ، مِلَاطُهَا الْمِسْكُ الْأَذْفَرُ، وَحَصْبَاؤُهَا الْيَاقُوتُ وَاللُّؤْلُؤُ، وَتُرَابُهَا الزَّعْفَرَانُ، مَنْ يَدْخُلْهَا يَخْلُدْ فِيهَا يَنْعَمُ لَا يَبْؤُسُ، لَا يَفْنَى شَبَابُهُمْ، وَلَا تَبْلَى ثِيَابُهُمْ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Sa'daan Al-Juhaniy, kutoka kwa Abuw Mujaahid, ametusimulia Abuw Mudillah kwamba alimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Tulisema: Yaa Rasula-Allaah, Jannah (Pepo), ujenzi wake ni wa nini? Akasema: "Tofali la dhahabu na tofali la fedha; chokaa chake ni miski yenye harufu kali; na changarawe zake ni yakuti na lulu; na udongo wake ni zafarani. Atakayeiingia atadumu humo milele, atakuwa katika neema, hatapata dhiki; ujana wao haumaliziki, wala nguo zao hazichakai."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1861
- Hadiyth
- 2863
101-Mlangoباب: في جنات الفردوسMlango Wa Kuhusu Jannaat Za Al-Firdaws
حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبُو قُدَامَةَ، عَنْ أَبِي عِمْرَانَ الْجَوْنِيِّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ قَيْسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "جَنَّاتُ الْفِرْدَوْسِ أَرْبَعٌ: ثِنْتَانِ مِنْ ذَهَبٍ: حِلْيَتُهُمَا وَآنِيَتُهُمَا، وَمَا فِيهِمَا، وَثِنْتَانِ مِنْ فِضَّةٍ: حِلْيَتُهُمَا وَآنِيَتُهُمَا وَمَا فِيهِمَا، وَلَيْسَ بَيْنَ الْقَوْمِ وَبَيْنَ أَنْ يَنْظُرُوا إِلَى رَبِّهِمْ إِلَّا رِدَاءُ الْكِبْرِيَاءِ عَلَى وَجْهِهِ فِي جَنَّاتِ عَدْنٍ، وَهَذِهِ الْأَنْهَارُ تَشْخُبُ مِنْ جَنَّاتِ عَدْنٍ فِي جَوْبَةٍ ثُمَّ تَصْعَدُ بَعْدُ أَنْهَارًا". قَالَ عَبْد اللَّهِ: جَوْبَةٌ: مَا يُجَابُ عَنْهُ الْأَرْضُ
Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Abuw Qudaamah, kutoka kwa Abuw 'Imraan Al-Jawniy, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdi-Allaah bin Qays, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Jannaat za Al-Firdaws ni nne: mbili ni za dhahabu — mapambo yake, vyombo vyake na vilivyomo ndani yake —, na mbili ni za fedha — mapambo yake, vyombo vyake na vilivyomo ndani yake. Na hakuna kilicho baina ya watu hao na baina ya kumtazama Rabb wao isipokuwa shuka ya Ukubwa iliyo juu ya Wajihi Wake katika Jannaat za 'Adn (kudumu milele). Na mito hii inabubujika kutoka Jannaat za 'Adn katika jawbah (uwanja ulio wazi), kisha inapanda baada ya hapo ikiwa mito."
'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Jawbah ni (mahali) ambapo ardhi imekatwa (kukawa wazi).
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1862
- Hadiyth
- 2864
102-Mlangoباب: في أول زمرة يدخلون الجنةMlango Wa Kuhusu Kundi La Kwanza Litakaloingia Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ أَوَّلَ زُمْرَةٍ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ مِنْ أُمَّتِي عَلَى صُورَةِ الْقَمَرِ لَيْلَةَ الْبَدْرِ، ثُمَّ الَّذِينَ يَلُونَهُمْ عَلَى أَحْسَنِ كَوْكَبٍ إِضَاءَةً فِي السَّمَاءِ". فَقَامَ عُكَّاشَةُ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، ادْعُ اللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ، فَقَالَ: "اللَّهُمَّ اجْعَلْهُ مِنْهُمْ". ثُمَّ قَامَ رَجُلٌ آخَرُ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، ادْعُ اللَّهَ أَنْ يَجْعَلَنِي مِنْهُمْ، فَقَالَ: "سَبَقَكَ بِهَا عُكَّاشَةُ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika kundi la kwanza litakaloingia Jannah (Pepo) katika Ummah wangu litakuwa kwa umbo la mwezi usiku wa mwezi mpevu; kisha wale wanaowafuatia (watakuwa) kama nyota yenye mwangaza mkali zaidi angani." 'Ukkaashah (رضي الله عنه) akasimama, akasema: Yaa Rasula-Allaah, muombe Allaah Anijaalie kuwa miongoni mwao. Akasema:
اللَّهُمَّ اجْعَلْهُ مِنْهُمْ
Yaa Allaah! Mjaalie awe miongoni mwao.
Kisha akasimama mtu mwingine, akasema: Yaa Rasula-Allaah, muombe Allaah Anijaalie kuwa miongoni mwao. Akasema: "'Ukkaashah (رضي الله عنه) amekutangulia kwayo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1863
- Hadiyth
- 2865
103-Mlangoباب: ما يقال لأهل الجنة إذا دخلوهاMlango Wa Yatakayoambiwa
Watu Wa Jannah (Pepo) Watakapoiingia
أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ بْنُ يَعِيشَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ آدَمَ، عَنْ حَمْزَةَ بْنِ حَبِيبٍ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْأَغَرِّ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، وَأَبِي سَعِيدٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {وَنُودُوا أَنْ تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ}، قَالَ: "نُودُوا: أَنْ صِحُّوا فَلَا تَسْقَمُوا، وَانْعَمُوا فَلَا تَبْأَسُوا، وَشِبُّوا فَلَا تَهْرَمُوا، وَاخْلُدُوا فَلَا تَمُوتُوا"
Ametukhabarisha 'Ubayd bin Ya'iysh, ametusimulia Yahyaa bin Aadam, kutoka kwa Hamzah bin Habiyb, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Agharr, kutoka kwa Abuw Hurayrah na Abuw Sa'iyd (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
وَنُودُوا أَنْ تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنْتُمْ تَعْمَلُونَ
Na wataitwa (kuambiwa): Hii ndiyo Jannah mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mnayatenda. [Al-A’raaf (7:43)]
Amesema: "Wataitwa (kuambiwa): Kuweni wazima, hamtaugua; na kuweni katika neema, hamtapata dhiki; na kuweni vijana, hamtazeeka; na dumuni milele, hamtakufa."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1864
- Hadiyth
- 2866
104-Mlangoباب: في أهل الجنة ونعيمهاMlango Wa Kuhusu Watu Wa Jannah (Pepo) Na Neema Zake
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ ثُمَامَةَ بْنِ عُقْبَةَ الْمُحَلِّمِيِّ، قَالَ: سَمِعْتُ زَيْدَ بْنَ أَرْقَمَ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ الرَّجُلَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ لَيُعْطَى قُوَّةَ مِائَةِ رَجُلٍ فِي الْأَكْلِ وَالشُّرْبِ وَالْجِمَاعِ، وَالشَّهْوَةِ"، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الْيَهُودِ: إِنَّ الَّذِي يَأْكُلُ وَيَشْرَبُ تَكُونُ مِنْهُ الْحَاجَةُ؟، َفَقَالَ: "يَفِيضُ مِنْ جِلْدِهِ عَرَقٌ، فَإِذَا بَطْنُهُ قَدْ ضَمَرَ"
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Thumaamah bin 'Uqbah Al-Muhallimiy, amesema: Nilimsikia Zayd bin Arqam (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mtu miongoni mwa watu wa Jannah (Pepo) atapewa nguvu za wanaume mia moja katika kula, kunywa, jimai na matamanio." Mtu mmoja miongoni mwa Mayahudi akasema: Hakika anayekula na kunywa hupatwa na haja (ya kujisaidia)? Akasema: "Jasho litabubujika kutoka katika ngozi yake, na ghafla tumbo lake limeshanywea."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1865
- Hadiyth
- 2867
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ الرِّفَاعِيُّ، حَدَّثَنَا مُعَاذٌ يَعْنِي: ابْنَ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَامِرٍ الْأَحْوَلِ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَهْلُ الْجَنَّةِ شَبَابٌ، جُرْدٌ، مُرْدٌ، كُحْلٌ، لَا تَبْلَى ثِيَابُهُمْ، وَلَا يَفْنَى شَبَابُهُمْ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd Ar-Rifaa'iy, ametusimulia Mu'aadh — yaani Ibn Hishaam —, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aamir Al-Ahwal, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Watu wa Jannah (Pepo) ni vijana, wasio na nywele mwilini, wasio na ndevu, wenye wanja machoni; nguo zao hazichakai, wala ujana wao haumaliziki."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1866
- Hadiyth
- 2868
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو الزُّبَيْرِ: أَنَّهُ سَمِعَ جَابِرًا قِيلَ لِأَبِي عَاصِمٍ: عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟. قَالَ: نَعَمْ "أَهْلُ الْجَنَّةِ لَا يَبُولُونَ، وَلَا يَمْتَخِطُونَ، وَلَا يَتَغَوَّطُونَ، وَيَكُونُ ذَلِكَ مِنْهُمْ جُشَاءً، يَأْكُلُونَ، وَيَشْرَبُونَ، وَيُلْهَمُونَ التَّسْبِيحَ وَالْحَمْدَ، كَمَا يُلْهَمُونَ النَّفَسَ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, amesema: Amenikhabarisha Abuz-Zubayr kwamba alimsikia Jaabir (رضي الله عنه) — Abuw 'Aaswim aliulizwa: (Ni) kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)? Akasema: Ndiyo —: "Watu wa Jannah (Pepo) hawakojoi, wala hawapengi kamasi, wala hawaendi haja kubwa; na hilo litakuwa kwao ni kucheuwa. Wanakula na wanakunywa, na wanatiwa ilhamu ya Tasbiyh (kumtakasa Allaah) na Himdi kama wanavyotiwa ilhamu ya kupumua."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1867
- Hadiyth
- 2869
105-Mlangoباب: ما أعد الله لعباده الصالحينMlango Wa Yale Aliyowaandalia Allaah Waja Wake Wema
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "يَقُولُ اللَّهُ عز وجل: أَعْدَدْتُ لِعِبَادِي الصَّالِحِينَ مَا لَا عَيْنٌ رَأَتْ وَلَا أُذُنٌ سَمِعَتْ، وَلَا خَطَرَ عَلَى قَلْبِ بَشَرٍ، وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: {فَلا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ}"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Allaah (عز وجل) Anasema: Nimewaandalia Waja Wangu wema yale ambayo jicho halijapata kuona, wala sikio halijapata kusikia, wala hayajapata kupita katika moyo wa mwanaadam. Na someni mkipenda:"
فَلا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَا أُخْفِيَ لَهُمْ مِنْ قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Basi nafsi yoyote haijui waliyofichiwa katika yanayoburudisha macho. Ni jazaa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [As-Sajdah (32:17)]
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1868
- Hadiyth
- 2870
106-Mlangoباب: في أدنى أهل الجنة منزلاMlango Wa Kuhusu Mwenye Daraja Ya Chini Kabisa
Katika Watu Wa Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ أَدْنَى أَهْلِ الْجَنَّةِ مَنْزِلًا مَنْ يَتَمَنَّى عَلَى اللَّهِ، فَيُقَالُ لَهُ: لَكَ ذَاكَ وَمِثْلُهُ مَعَهُ. إِلَّا أَنَّهُ يُلَقَّى سِوَى كَذَا وَكَذَا، فَيُقَالُ لَهُ: ذَاكَ لَكَ وَمِثْلُهُ مَعَهُ". قَالَ أَبُو سَعِيدٍ الْخُدْرِيُّ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "فَيُقَالُ لَهُ: ذَاكَ وَعَشْرَةُ أَمْثَالِهِ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika mwenye daraja ya chini kabisa katika watu wa Jannah (Pepo) ni yule atakayetamani (mambo) mbele ya Allaah, naye ataambiwa: Utapata hicho na mfano wake pamoja nacho. Isipokuwa kwamba atafundishwa (kutamani mengine) zaidi ya (hayo): kadha na kadha; naye ataambiwa: Hicho ni chako na mfano wake pamoja nacho." Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Ataambiwa: Hicho, na mfano wake mara kumi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1869
- Hadiyth
- 2871
107-Mlangoباب: في غرف الجنةMlango Wa Kuhusu Maghorofa Ya Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَبُو حَازِمٍ، عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ أَهْلَ الْجَنَّةِ لَيَتَرَاءَوْنَ أَهْلَ الْغُرَفِ كَمَا تَرَوْنَ الْكَوْكَبَ الدُّرِّيَّ فِي السَّمَاءِ".
Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Abuw Haazim, kutoka kwa Sahl bin Sa'd (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika watu wa Jannah (Pepo) watawaona watu wa maghorofa (ya juu) kama mnavyoiona nyota inayong'aa na kumeremeta angani."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1870
- Hadiyth
- 2872
قَالَ أَبُو حَازِمٍ: فَحَدَّثْتُ بِهَذَا الْحَدِيثِ النُّعْمَانَ بْنَ أَبِي عَيَّاشٍ، فَحَدَّثَنِي، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ: أَنَّهُ قَالَ: "الْكَوْكَبُ الدُّرِّيُّ فِي الْأُفُقِ الشَّرْقِيِّ وَالْغَرْبِيِّ"
Abuw Haazim amesema: Nikamsimulia Hadiyth hii An-Nu'maan bin Abiy 'Ayyaash, naye akanisimulia kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه) kwamba alisema: "Nyota inayong'aa na kumeremeta katika upeo wa mashariki na wa magharibi."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1870
- Hadiyth
- 2873
108-Mlangoباب: في صفة الحور العينMlango Wa Kuhusu Sifa Ya Huwrul-'Iyn (Wanawake Weupe
Wazuri Wa Jannah Wenye Macho Makubwa Ya Kupendeza)
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمِنْهَالِ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ الْقُرْدُوسِيُّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مَا فِي الْجَنَّةِ أَحَدٌ إِلَّا لَهُ زَوْجَتَانِ، إِنَّهُ لَيَرَى مُخَّ سَاقِهِمَا مِنْ وَرَاءِ سَبْعِينَ حُلَّةً، مَا فِيهَا مِنْ عَزَبٍ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Minhaal, ametusimulia Yaziyd bin Zuray', ametusimulia Hishaam Al-Qurduwsiy, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakuna yeyote katika Jannah (Pepo) isipokuwa ana wake wawili; hakika yeye anaona uboho wa miundi yao kutoka nyuma ya nguo sabini. Hakuna humo mseja (asiye na mke)."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1871
- Hadiyth
- 2874
109-Mlangoباب: في خيام الجنةMlango Wa Kuhusu Mahema Ya Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا أَبُو عِمْرَانَ الْجَوْنِيُّ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ قَيْسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْخَيْمَةُ دُرَّةٌ مُجَوَّفَةٌ، طُولُهَا فِي السَّمَاءِ سِتُّونَ مِيلًا، فِي كُلِّ زَاوِيَةٍ مِنْهَا أَهْلٌ لِلْمُؤْمِنِ لَا يَرَاهُمْ الْآخَرُونَ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Hammaam, ametusimulia Abuw 'Imraan Al-Jawniy, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdi-Allaah bin Qays, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hema ni lulu yenye uwazi ndani yake; urefu wake kwenda juu ni maili sitini. Katika kila pembe yake Muumini ana ahali ambao wengine hawawaoni."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1872
- Hadiyth
- 2875
110-Mlangoباب: في ولد أهل الجنةMlango Wa Kuhusu Mtoto Wa Watu Wa Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يَزِيدَ، وَالْقَوَارِيرِيُّ، عَنْ مُعَاذِ بْنِ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَامِرٍ الْأَحْوَلِ، عَنْ أَبِي الصِّدِّيقِ النَّاجِيِّ، عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ الْمُؤْمِنَ إِذَا اشْتَهَى الْوَلَدَ فِي الْجَنَّةِ، كَانَ حَمْلُهُ وَوَضْعُهُ وَسِنُّهُ فِي سَاعَةٍ كَمَا اشْتَهَى"
Ametukhabarisha Muhammad bin Yaziyd na Al-Qawaariyriy, kutoka kwa Mu'aadh bin Hishaam, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aamir Al-Ahwal, kutoka kwa Abus-Swiddiyq An-Naajiy, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika Muumini akitamani mtoto katika Jannah (Pepo), mimba yake, kuzaliwa kwake na kukua kwake (mpaka umri wake) kutakuwa katika saa moja, kama anavyotamani."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1872
- Hadiyth
- 2876
111-Mlangoباب: في صفوف أهل الجنةMlango Wa Kuhusu Safu Za Watu Wa Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، قَالَ: حَدَّثَنَا مُعَاوِيَةُ بْنُ هِشَامٍ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ عَلْقَمَةَ بْنِ مَرْثَدٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ بُرَيْدَةَ، قَالَ: أُرَاهُ عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "أَهْلُ الْجَنَّةِ عِشْرُونَ وَمِائَةُ صَفٍّ: ثَمَانُونَ مِنْهَا أُمَّتِي، وَأَرْبَعُونَ سَائِرُ النَّاسِ"
Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, amesema: Ametusimulia Mu'aawiyah bin Hishaam, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa 'Alqamah bin Marthad, kutoka kwa Sulaymaan bin Buraydah — amesema: Naona ni kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه) —, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Watu wa Jannah (Pepo) ni safu mia moja na ishirini: themanini kati yake ni Ummah wangu, na arubaini ni watu wengine wote."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1873
- Hadiyth
- 2877
112-Mlangoباب: في أنهار الجنةMlango Wa Kuhusu Mito Ya Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، قَالَ: أَنْبَأَنَا الْجُرَيْرِيُّ، عَنْ حَكِيمِ بْنِ مُعَاوِيَةَ، عَنْ أَبِيهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ فِي الْجَنَّةِ بَحْرَ اللَّبَنِ وَبَحْرَ الْعَسَلِ وَبَحْرَ الْخَمْرِ، ثُمَّ تَشَقَّقُ مِنْهُ الْأَنْهَارُ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, amesema: Ametupa khabari Al-Jurayriy, kutoka kwa Hakiym bin Mu'aawiyah, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika katika Jannah (Pepo) kuna bahari ya maziwa, na bahari ya asali, na bahari ya khamr (pombe); kisha mito itapasuka kutoka humo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1873
- Hadiyth
- 2878
113-Mlangoباب: في الكوثرMlango Wa Kuhusu Al-Kawthar (Mto Katika Jannah)
أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ عَطَاءِ بْنِ السَّائِبِ، عَنْ مُحَارِبِ بْنِ دِثَارٍ، قالَ: حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُمَرَ، قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ}، قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هُوَ نَهْرٌ فِي الْجَنَّةِ حَافَّتَاهُ مِنْ ذَهَبٍ، يَجْرِي عَلَى الدُّرِّ وَالْيَاقُوتِ، تُرْبَتُهُ أَطْيَبُ مِنْ رِيحِ الْمِسْكِ، وَطَعْمُهُ أَحْلَى مِنَ الْعَسَلِ، وَمَاؤُهُ أَشَدُّ بَيَاضًا مِنَ الثَّلْجِ"
Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, ametupa khabari Abuw 'Awaanah, kutoka kwa 'Atwaa bin As-Saaib, kutoka kwa Muhaarib bin Dithaar, amesema: Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: Ilipoteremka:
إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ
Hakika Sisi Tumekupa Al-Kawthar. [Al-Kawthar (108:1)]
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema: "Huo ni mto katika Jannah (Pepo); kingo zake mbili ni za dhahabu, unapita juu ya lulu na yakuti; udongo wake una harufu nzuri zaidi kuliko harufu ya miski, na ladha yake ni tamu zaidi kuliko asali, na maji yake ni meupe zaidi kuliko theluji."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1874
- Hadiyth
- 2879
114-Mlangoباب: في أشجار الجنةMlango Wa Kuhusu Miti Ya Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ فِي الْجَنَّةِ شَجَرَةً يَسِيرُ الرَّاكِبُ فِي ظِلِّهَا مِائَةَ عَامٍ لَا يَقْطَعُهَا، وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: {وَظِلٍّ مَمْدُودٍ}"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Muhammad bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika katika Jannah (Pepo) kuna mti ambao mpandaji (wa kipando) husafiri katika kivuli chake miaka mia bila kukimaliza. Na someni mkipenda:"
وَظِلٍّ مَمْدُودٍ
Na kivuli kilichotandazwa. [Al-Waaqi’ah (56:30)]
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1875
- Hadiyth
- 2880
أَخْبَرَنَا عَبْدُ الصَّمَدِ بْنُ عَبْدِ الْوَارِثِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ أَبِي الضَّحَّاكِ، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ فِي الْجَنَّةِ شَجَرَةً يَسِيرُ الرَّاكِبُ فِي ظِلِّهَا مِائَةَ عَامٍ لَا يَقْطَعُهَا، هِيَ شَجَرَةُ الْخُلْدِ"
Ametukhabarisha 'Abdusw-Swamad bin 'Abdil-Waarith, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Abudhw-Dhwahhaak, amesema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika katika Jannah (Pepo) kuna mti ambao mpandaji (wa kipando) husafiri katika kivuli chake miaka mia bila kukimaliza; huo ndio mti wa kudumu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1875
- Hadiyth
- 2881
115-Mlangoباب: في العجوةMlango Wa Kuhusu Al-'Ajwah (Aina Bora Ya Tende Za Madiynah)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا عَبَّادٌ هُوَ: ابْنُ مَنْصُورٍ، قَالَ: سَمِعْتُ شَهْرَ بْنَ حَوْشَبٍ، يَقُولُ: سَمِعْتُ أَبَا هُرَيْرَةَ، يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْعَجْوَةُ مِنَ الْجَنَّةِ، وَهِيَ شِفَاءٌ مِنَ السُّمِّ"
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari 'Abbaad — naye ni Ibn Manswuwr —, amesema: Nilimsikia Shahr bin Hawshab akisema: Nilimsikia Abuw Hurayrah (رضي الله عنه) akisema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Al-'ajwah (aina bora ya tende za Madiynah) inatoka Jannah (Pepo), nayo ni ponyo la sumu."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1876
- Hadiyth
- 2882
116-Mlangoباب: في سوق الجنةMlango Wa Kuhusu Soko La Jannah (Pepo)
أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "إِنَّ فِي الْجَنَّةِ لَسُوقًا". قَالُوا: وَمَا هِيَ، قَالَ: "كُثْبَانٌ مِنْ مِسْكٍ يَخْرُجُونَ إِلَيْهَا فَيَجْتَمِعُونَ فِيهَا، فَيَبْعَثُ اللَّهُ عَلَيْهِمْ رِيحًا فَتُدْخِلُهُمْ بُيُوتَهُمْ، فَيَقُولُ لَهُمْ أَهْلُوهُمْ: لَقَدْ ازْدَدْتُمْ بَعْدَنَا حُسْنًا، وَيَقُولُونَ لِأَهْلِيهِمْ مِثْلَ ذَلِكَ"،
Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Humayd, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Hakika katika Jannah (Pepo) kuna soko." Wakasema: Nalo ni nini? Akasema: "Ni vilima vya (mchanga wa) miski; wanatoka kuviendea na wanakusanyika humo; kisha Allaah Anawatumia upepo, ukawaingiza majumbani mwao. Ahli zao wanawaambia: Hakika mmeongezeka uzuri baada yetu. Nao wanawaambia ahli zao mfano wa hivyo."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1877
- Hadiyth
- 2883
حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَبْدِ الْجَبَّارِ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِنَحْوِهِ
Ametusimulia Sa'iyd bin 'Abdil-Jabbaar, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa namna inayokaribiana nayo.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1877
- Hadiyth
- 2884
117-Mlangoباب: حفت الجنة بالمكارهMlango Wa Jannah (Pepo) Imezungushiwa Yanayochukiza
أَخْبَرَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ثَابِتٍ، عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "حُفَّتْ الْجَنَّةُ بِالْمَكَارِهِ، وَحُفَّتْ النَّارُ بِالشَّهَوَاتِ"
Ametukhabarisha Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Jannah (Pepo) imezungushiwa yanayochukiza, na moto umezungushiwa matamanio."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1877
- Hadiyth
- 2885
118-Mlangoباب: في دخول الفقراء الجنة قبل الأغنياءMlango Wa Kuhusu Mafakiri Kuingia Jannah (Pepo)
Kabla Ya Matajiri
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي مُعَاوِيَةُ: أَنَّ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ جُبَيْرٍ حَدَّثَهُ، عَنْ أَبِيهِ جُبَيْرِ بْنِ نُفَيْرٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: بَيْنَا أَنَا قَاعِدٌ فِي الْمَسْجِدِ وَحَلْقَةٌ مِنْ فُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ قُعُودٌ إِذْ دَخَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَعَدَ إِلَيْهِمْ، فَقُمْتُ إِلَيْهِمْ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لَهُمْ: "لِيُبْشِرْ فُقَرَاءُ الْمُهَاجِرِينَ بِمَا يَسُرُّ وُجُوهَهُمْ، فَإِنَّهُمْ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ قَبْلَ الْأَغْنِيَاءِ بِأَرْبَعِينَ عَامًا". قَالَ: فَلَقَدْ رَأَيْتُ أَلْوَانَهُمْ أَسْفَرَتْ، قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عَمْرٍو: حَتَّى تَمَنَّيْتُ أَنْ أَكُونَ مَعَهُمْ
Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amesema: Amenisimulia Mu'aawiyah, kwamba 'Abdur-Rahmaan bin Jubayr alimsimulia, kutoka kwa baba yake Jubayr bin Nufayr, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما), amesema: Nilipokuwa nimekaa Msikitini, na duara (la watu) miongoni mwa mafakiri wa Muhaajiruwn (waliohajiri kwenda Madiynah) (رضي الله عنهم) wamekaa, mara Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akaingia, akakaa pamoja nao; nami nikainuka kwenda kwao. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawaambia: "Mafakiri wa Muhaajiruwn (رضي الله عنهم) wapewe bishara ya yale yatakayozifurahisha nyuso zao; kwani hakika wao wataingia Jannah kabla ya matajiri kwa miaka arobaini." Amesema: Hakika niliona rangi (za nyuso) zao zikinawiri. 'Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما) amesema: Mpaka nikatamani niwe pamoja nao.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1879
- Hadiyth
- 2886
119-Mlangoباب: في نفس جهنمMlango Wa Kuhusu Pumzi Ya Jahannam
أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ نَافِعٍ، أَنْبَأَنَا شُعَيْبٌ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبُو سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّهُ سَمِعَهُ يَقُولُ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "اشْتَكَتِ النَّارُ إِلَى رَبِّهَا، فَقَالَتْ: يَا رَبِّ أَكَلَ بَعْضِي بَعْضًا، فَأَذِنَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى لَهَا بِنَفَسَيْنِ: نَفَسٍ فِي الشِّتَاءِ، وَنَفَسٍ فِي الصَّيْفِ، فَهُوَ أَشَدُّ مَا تَجِدُونَ مِنَ الْحَرِّ، وَأَشَدُّ مَا تَجِدُونَ مِنَ الزَّمْهَرِيرِ".
Ametukhabarisha Al-Hakam bin Naafi', ametupa khabari Shu'ayb, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Amenikhabarisha Abuw Salamah, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba alimsikia akisema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Moto ulilalamika kwa Rabb wake, ukasema: Yaa Rabbi, baadhi yangu imekula baadhi nyingine. Allaah (تبارك وتعالى) Akauruhusu pumzi mbili: pumzi moja wakati wa baridi, na pumzi moja wakati wa joto. Basi hiyo ndiyo joto kali zaidi mnalolipata, na baridi kali zaidi mnayoipata."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1880
- Hadiyth
- 2887
أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَاصِمِ بْنِ بَهْدَلَةَ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، بِنَحْوِهِ
Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Aaswim bin Bahdalah, kutoka kwa Abuw Swaalih, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), kwa namna inayokaribiana nayo.
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1880
- Hadiyth
- 2888
120-Mlangoباب: في قول النبي صلى الله عليه وسلم: «ناركم هذه جزء من كذا جزءا»Mlango Wa Kuhusu Kauli Ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) :
«Moto Wenu Huu Ni Sehemu Moja Kati Ya Sehemu Kadhaa»
أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا الْهَجَرِيُّ، عَنْ أَبِي عِيَاضٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "إِنَّ نَارَكُمْ هَذِهِ جُزْءٌ مِنْ سَبْعِينَ جُزْءًا مِنْ نَارِ جَهَنَّمَ"
Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Al-Hajariy, kutoka kwa Abuw 'Iyaadhw, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Hakika moto wenu huu ni sehemu moja kati ya sehemu sabini za moto wa Jahannam."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1880
- Hadiyth
- 2889
121-Mlangoباب: في أهون أهل النار عذاباMlango Wa Kuhusu Mwenye Adhabu Nyepesi Kabisa
Katika Watu Wa Motoni
أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ عَجْلَانَ، عَنْ أَبِيه، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَهْوَنُ النَّاسِ عَذَابًا مَنْ لَهُ نَعْلَانِ يَغْلِي مِنْهُمَا دِمَاغُهُ"
Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn 'Ajlaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mwenye adhabu nyepesi kabisa katika watu ni yule mwenye viatu viwili ambavyo ubongo wake unachemka kwa sababu yake."
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1881
- Hadiyth
- 2890
122-Mlangoباب: قوله تعالى: {هل من مزيد}Mlango Wa Kauli Yake (تعالى) : «Je, kuna
ziada yoyote?» [Qaaf (50:30)]
أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ عَمَّارِ بْنِ أَبِي عَمَّارٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "يُلْقَى فِي النَّارِ أَهْلُهَا، وَتَقُولُ: هَلْ مِنْ مَزِيدٍ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ ثَلَاثًا، حَتَّى يَأْتِيَهَا رَبُّهَا تَعَالَى فَيَضَعَ قَدَمَهُ عَلَيْهَا فَتَنْزَوِي وَتَقُولُ: قَطْ قَطْ قَطْ"
Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa 'Ammaar bin Abiy 'Ammaar, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Watu wake hutupwa motoni, nao husema: Je, kuna ziada yoyote? Je, kuna ziada yoyote? — mara tatu — mpaka Rabb wake (تعالى) Aujie, Aweke Qadamu (Mguu) Yake juu yake, ukunjike, na useme: Inatosha! Inatosha! Inatosha!"
- Mjalada
- 3
- Kitabu
- 20
- Ukurasa
- 1882
- Hadiyth
- 2891