Skip to main content

Sunan Ad-Daarimiy21 - Kitabu Cha Faraaidh (Mirathi)

ومن كتاب الفرائض

1-Mlangoباب: في تعليم الفرائضMlango Wa Kuhusu Kufundisha Faraaidh
(Ilimu Ya Mafungu Ya Mirathi)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا عَاصِمٌ، عَنْ مُوَرِّقٍ الْعِجْلِيِّ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: "تَعَلَّمُوا الْفَرَائِضَ وَاللَّحْنَ وَالسُّنَنَ كَمَا تَعَلَّمُونَ الْقُرْآنَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari 'Aaswim, kutoka kwa Muwarriq Al-'Ijliy, amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), na lugha (ya Kiarabu kwa usahihi wake), na Sunnah, kama mnavyojifunza Qur-aan."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2892

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "تَعَلَّمُوا الْفَرَائِضَ فَإِنَّهَا مِنْ دِينِكُمْ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), kwani hiyo ni katika Dini yenu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2893

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا يُوسُفُ الْمَاجِشُونُ، قَالَ: قَالَ ابْنُ شِهَابٍ: "لَوْ هَلَكَ عُثْمَانُ، وَزَيْدٌ فِي بَعْضِ الزَّمَانِ، لَهَلَكَ عِلْمُ الْفَرَائِضِ، لَقَدْ أَتَى عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ، وَمَا يَعْلَمُهَا غَيْرُهُمَا"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Yuwsuf Al-Maajishuwn, amesema: Ibn Shihaab amesema: "Lau 'Uthmaan na Zayd (رضي الله عنهما) wangefariki katika baadhi ya zama, ingeangamia ilimu ya Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi). Kwa yakini zilipita juu ya watu zama ambazo hakuna aliyekuwa akiijua isipokuwa wao wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2894

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ الْقَاسِمِ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ:" تَعَلَّمُوا الْقُرْآنَ وَالْفَرَائِضَ، فَإِنَّهُ يُوشِكُ أَنْ يَفْتَقِرَ الرَّجُلُ إِلَى عِلْمٍ كَانَ يَعْلَمُهُ، أَوْ يَبْقَى فِي قَوْمٍ لَا يَعْلَمُونَ

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa Al-Qaasim, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Jifunzeni Qur-aan na Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), kwani karibuni mtu atahitajia ilimu aliyokuwa akiijua, au atabakia kati ya watu wasiojua."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2895

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زِيَادُ بْنُ أَبِي مُسْلِمٍ، عَنْ أَبِي الْخَلِيلِ، قَالَ: قَالَ أَبُو مُوسَى: "مَنْ عَلِمَ الْقُرْآنَ وَلَمْ يَعْلَمْ الْفَرَائِضَ، فَإِنَّ مَثَلَهُ مَثَلُ الْبُرْنُسِ لَا وَجْهَ لَهُ، أَوْ: لَيْسَ لَهُ وَجْهٌ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Ziyaad bin Abiy Muslim, kutoka kwa Abul-Khaliyl, amesema: Abuw Muwsaa (رضي الله عنه) amesema: "Mwenye kuijua Qur-aan na asizijue Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), basi hakika mfano wake ni mfano wa burnus (kanzu yenye kofia) isiyo na uso — au: haina uso."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2896

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَال: قُلْتُ لِعَلْقَمَةَ: مَا أَدْرِي مَا أَسْأَلُكَ عَنْهُ؟ قَالَ: "أَمِتْ جِيرَانَكَ"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: Nilimwambia 'Alqamah: Sijui nikuulize kuhusu nini? Akasema: "Wafishe majirani zako (yaani: jifanye kuwa wamefariki, kisha uulize kuhusu mirathi yao)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2897

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ طَلْحَةَ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ الْوَلِيدِ الْهَمْدَانِيِّ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: "تَعَلَّمُوا الْفَرَائِضَ، وَالطَّلاقَ، وَالْحَجَّ، فَإِنَّهُ مِنْ دِينِكُمْ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Muhammad bin Twalhah, kutoka kwa Al-Qaasim bin Al-Waliyd Al-Hamdaaniy, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Jifunzeni Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), na Twalaaq (talaka), na Hajj, kwani hilo ni katika Dini yenu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2898

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ كَثِيرٍ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "كَانُوا يُرَغِّبُونَ فِي تَعْلِيمِ الْقُرْآنِ وَالْفَرَائِضِ وَالْمَنَاسِكِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Kathiyr, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Walikuwa wakihimiza kufundisha Qur-aan, na Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi), na ibaada za Hajj."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1885
Hadiyth
2899

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ أَبِي عُبَيْدَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ:" مَنْ قَرَأَ الْقُرْآنَ، فَلْيَتَعَلَّمْ الْفَرَائِضَ، فَإِنْ لَقِيَهُ أَعْرَابِيٌّ، قَالَ: يَا مُهَاجِرُ، أَتَقْرَأُ الْقُرْآنَ؟ فَإِنْ قَالَ: نَعَمْ، قَالَ: تَفْرِضُ؟ فَإِنْ قَالَ: نَعَمْ، فَهُوَ زِيَادَةٌ وَخَيْر، وَإِنْ قَالَ: لَا، قَالَ: فَمَا فَضْلُكَ عَلَيَّ يَا مُهَاجِرُ؟!

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Abuw 'Ubaydah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Mwenye kusoma Qur-aan, basi ajifunze Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi). Kwani akikutana naye Bedui, atasema: Yaa Muhaajir (mwenye kuhama), je, unasoma Qur-aan? Akisema: Ndiyo, atasema: Je, unajua kugawa Faraaidh? Akisema: Ndiyo, basi hilo ni ziada na kheri. Na akisema: Hapana, atasema: Basi una ubora gani juu yangu, yaa Muhaajir?!"

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1888
Hadiyth
2900

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا عُقْبَةُ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ، قَالَ: سَأَلْنَا مَسْرُوقًا: كَانَتْ عَائِشَةُ تُحْسِنُ الْفَرَائِضَ؟ قَالَ: "وَالَّذِي لَا إِلَهَ غَيْرُهُ، لَقَدْ رَأَيْتُ الْأَكَابِرَ مِنْ أَصْحَابِ مُحَمَّدٍ يَسْأَلُونَهَا عَنْ الْفَرَائِضِ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia 'Uqbah bin Khaalid, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, amesema: Tulimuuliza Masruwq: Je, 'Aaishah (رضي الله عنها) alikuwa akizijua vizuri Faraaidh (ilimu ya mafungu ya mirathi)? Akasema: "Naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki asiyekuwa Yeye, kwa yakini niliwaona wakubwa miongoni mwa Swahaba (رضي الله عنهم) wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wakimuuliza kuhusu Faraaidh."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1889
Hadiyth
2901

2-Mlangoباب: من ادعى إلى غير أبيهMlango Wa Mwenye Kujinasibisha Kwa Asiyekuwa Baba Yake

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ أَبِي عُثْمَانَ، عَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ، وَعَنْ أَبِي بَكْرَةَ قَالَ شُعْبَةُ: هَذَا أَوَّلُ مَنْ رَمَى بِسَهْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، وَهَذَا تَدَلَّى حِصْنِ الطَّائِفِ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم إِنَّهُمَا حَدَّثَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "مَنْ ادَّعَى إِلَى غَيْرِ أَبِيهِ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ غَيْرُ أَبِيهِ، فَالْجَنَّةُ عَلَيْهِ حَرَامٌ"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Abuw 'Uthmaan, kutoka kwa Sa'd bin Abiy Waqqaasw, na kutoka kwa Abuw Bakrah (رضي الله عنهما) — Shu'bah amesema: Huyu ni wa kwanza aliyerusha mshale katika Njia ya Allaah, na huyu alijiteremsha kutoka ngome ya At-Twaaif kwenda kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) —, kwamba wao wawili walisimulia: Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Atakayejinasibisha kwa asiyekuwa baba yake, ilhali anajua kwamba si baba yake, basi Jannah (Pepo) ni haraam juu yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1889
Hadiyth
2902

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنْ أَبِي بَكْرٍ الصِّدِّيقِ، قَالَ:" كُفْرٌ بِاللَّهِ ادِّعَاءٌ إِلَى نَسَبٍ لَا يُعْرَفُ، وَكُفْرٌ بِاللَّهِ تَبَرُّؤٌ مِنْ نَسَبٍ وَإِنْ دَقَّ.

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Murrah, kutoka kwa Abuw Ma'mar, kutoka kwa Abuw Bakr As-Swiddiyq (رضي الله عنه), amesema: "Ni kumkufuru Allaah kujinasibisha kwa nasaba isiyojulikana; na ni kumkufuru Allaah kujitenga na nasaba, hata ikiwa ni ndogo."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1890
Hadiyth
2903

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ زَكَرِيَّا أَبِي يَحْيَى، قَالَ: سَمِعْتُ أَبَا وَائِلٍ يُحَدِّثُ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، نَحْوًا مِنْهُ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Zakariyyaa Abuw Yahyaa, amesema: Nilimsikia Abuw Waail akisimulia kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) mfano wa hivyo.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1891
Hadiyth
2904

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا إِسْحَاق بْنُ مَنْصُورٍ السَّلُولِيُّ، عَنْ جَعْفَرٍ الْأَحْمَرِ، عَنْ السَّرِيِّ بْنِ إِسْمَاعِيل، عَنْ قَيْسِ بْنِ أَبِي حَازِمٍ، قَالَ: أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِأُبَايِعَهُ، فَجِئْتُ وَقَدْ قُبِض، وَأَبُو بَكْرٍ قَائِمٌ فِي مَقَامِهِ، فَأَطَالَ الثَّنَاءَ وَأَكْثَرَ الْبُكَاءَ، فَقَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ: "كُفْرٌ بِاللَّهِ انْتِفَاءٌ مِنْ نَسَبٍ وَإِنْ دَقَّ، وَادِّعَاءُ نَسَبٍ لَا يُعْرَفُ"

Ametusimulia Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Is-haaq bin Manswuwr As-Saluwliy, kutoka kwa Ja'far Al-Ahmar, kutoka kwa As-Sariyy bin Ismaa'iyl, kutoka kwa Qays bin Abiy Haazim, amesema: Nilimjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ili nimpe bay'ah (ahadi ya utiifu); nikafika naye amekwisha kufariki, na Abuw Bakr (رضي الله عنه) amesimama mahali pake. Akarefusha kusifu na akazidisha kulia; akasema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: "Ni kumkufuru Allaah kujikana nasaba, hata ikiwa ni ndogo; na kujinasibisha kwa nasaba isiyojulikana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1891
Hadiyth
2905

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْحَمِيدِ بْنُ بَهْرَامَ، عَنْ شَهْرِ بْنِ حَوْشَبٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:" أَيُّمَا رَجُلٍ ادَّعَى إِلَى غَيْرِ وَالِدِه، أَوْ تَوَلَّى غَيْرَ مَوَالِيهِ الَّذِينَ أَعْتَقُوهُ، فَإِنَّ عَلَيْهِ لَعْنَةَ اللَّه، وَالْمَلائِكَةِ، وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ إِلَى يَوْمِ الْقِيَامَة، لا يُقْبَلُ مِنْهُ صَرْفٌ وَلَا عَدْلٌ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia 'Abdul-Hamiyd bin Bahraam, kutoka kwa Shahr bin Hawshab, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtu yeyote aliyejinasibisha kwa asiyekuwa baba yake mzazi, au akajinasibisha kwa wasiokuwa mabwana zake waliomwacha huru, basi juu yake ni laana ya Allaah, na ya Malaika (عليهم السلام), na ya watu wote, mpaka Siku ya Qiyaamah; haikubaliwi kutoka kwake (ibaada ya) faradhi wala ya Sunnah."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1891
Hadiyth
2906

3-Mlangoباب: في زوج وأبوين وامرأة وأبوينMlango Wa Kuhusu Mume
Na Wazazi Wawili, Na Mke Na Wazazi Wawili

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: كَانَ عُمَرُ إِذَا سَلَكَ بِنَا طَرِيقًا وَجَدْنَاهُ سَهْلًا، وَإِنَّهُ قَالَ فِي زَوْجٍ وَأَبَوَيْنِ:" لِلزَّوْجِ النِّصْفُ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِيَ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: 'Umar (رضي الله عنه) alikuwa anapotupitisha njia, tunaikuta nyepesi. Na hakika yeye alisema kuhusu mume na wazazi wawili: "Mume ana nusu, na mama ana theluthi ya kilichobakia."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2907

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ الرِّشْكُ، قَالَ: سَأَلْتُ سَعِيدَ بْنَ الْمُسَيِّبِ عَنْ رَجُلٍ تَرَكَ امْرَأَتَهُ، وَأَبَوَيْهِ، فَقَالَ: "قَسَّمَهَا زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ مِنْ أَرْبَعَةٍ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Yaziyd Ar-Rishk, amesema: Nilimuuliza Sa'iyd bin Al-Musayyib kuhusu mtu aliyeacha (baada ya kufariki kwake) mkewe na wazazi wake wawili. Akasema: "Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) aliigawa kutoka (mafungu) manne."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2908

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ شُعْبَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ: أَنَّ عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ قَالَ فِي امْرَأَةٍ وَأَبَوَيْنِ: "لِلْمَرْأَةِ الرُّبُعُ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِيَ"

Ametusimulia Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Shu'bah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhallab, kwamba 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) alisema kuhusu mke na wazazi wawili: "Mke ana robo, na mama ana theluthi ya kilichobakia."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2909

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ أَيُّوبَ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَبِي الْمُهَلَّبِ، عَنْ عُثْمَانَ بْنِ عَفَّانَ أَنَّهُ قَالَ: "لِلْمَرْأَةِ الرُّبُعُ سَهْمٌ مِنْ أَرْبَعَةٍ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِيَ سَهْم، وَلِلأَبِّ سَهْمَانِ".

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kutoka kwa Abul-Muhallab, kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه), kwamba alisema: "Mke ana robo, fungu moja kati ya manne; na mama ana theluthi ya kilichobakia, fungu moja; na baba ana mafungu mawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2910

أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، عَنْ حَجَّاجٍ، عَنْ عُمَيْرِ بْنِ سَعِيدٍ: أَنَّهُ سَأَلَ الْحَارِثَ الْأَعْوَرَ عَنْ امْرَأَةٍ، وَأَبَوَيْنِ، فَقَالَ مِثْلَ قَوْلِ عُثْمَانَ

Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad, kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa 'Umayr bin Sa'iyd, kwamba alimuuliza Al-Haarith Al-A'war kuhusu mke na wazazi wawili; akasema mfano wa kauli ya 'Uthmaan (رضي الله عنه).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2911

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا هِشَامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، أَنَّهُ قَالَ فِي امْرَأَةٍ تَرَكَتْ زَوْجَهَا وَأَبَوَيْهَا: "لِلزَّوْجِ النِّصْفُ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِيَ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hishaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), kwamba alisema kuhusu mwanamke aliyeacha mumewe na wazazi wake wawili: "Mume ana nusu, na mama ana theluthi ya kilichobakia."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2912

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ ابْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ عَامِرٍ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ: فِي امْرَأَةٍ وَأَبَوَيْنِ، قَالَ: "مِنْ أَرْبَعَةٍ: لِلْمَرْأَةِ الرُّبُعُ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِي، وَمَا بَقِيَ فَلِلْأَبِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa 'Aamir Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kuhusu mke na wazazi wawili, amesema: "Kutoka (mafungu) manne: mke ana robo, na mama ana theluthi ya kilichobakia, na kilichobakia ni cha baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1892
Hadiyth
2913

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، وَمَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: كَانَ عُمَرُ إِذَا سَلَكَ بِنَا طَرِيقًا اتَّبَعْنَاهُ فِيهِ، وَجَدْنَاهُ سَهْلًا، وَإِنَّهُ" قَضَى فِي امْرَأَةٍ وَأَبَوَيْنِ مِنْ أَرْبَعَةٍ: فَأَعْطَى الْمَرْأَةَ الرُّبُع، وَالأُمَّ ثُلُثَ مَا بَقِيَ، وَالْأَبَ سَهْمَيْنِ.

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash na Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: 'Umar (رضي الله عنه) alikuwa anapotupitisha njia, tukamfuata ndani yake, tunaikuta nyepesi. Na hakika yeye "alihukumu kuhusu mke na wazazi wawili kutoka (mafungu) manne: akampa mke robo, na mama theluthi ya kilichobakia, na baba mafungu mawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1895
Hadiyth
2914

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ عَنْ عِيسَى، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ مِثْلَ ذَلِكَ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Iysaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) mfano wa hivyo.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2915

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الْمُسَيَّبِ بْنِ رَافِعٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: كَانَ يَقُولُ: "مَا كَانَ اللَّهُ لِيَرَانِي أَنْ أُفَضِّلَ أُمًّا عَلَى أَبٍ"

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Al-Musayyab bin Raafi', kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: Alikuwa akisema: "Allaah Hakuwa Mwenye Kuniona nikimfadhilisha mama juu ya baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2916

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ عِكْرِمَةَ، قَالَ: "أَرْسَلَ ابْنُ عَبَّاسٍ إِلَى زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ: أَتَجِدُ فِي كِتَابِ اللَّهِ لِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِي؟ فَقَالَ زَيْدٌ: إِنَّمَا أَنْتَ رَجُلٌ تَقُولُ بِرَأْيِكَ، وَأَنَا رَجُلٌ أَقُولُ بِرَأْيِي"

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa 'Ikrimah, amesema: "Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alimtumia (ujumbe) Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه): Je, unakuta katika Kitabu cha Allaah (kwamba) mama ana theluthi ya kilichobakia? Zayd (رضي الله عنه) akasema: Hakika wewe ni mtu unayesema kwa rai yako, nami ni mtu ninayesema kwa rai yangu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2917

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حَجَّاجٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، وَحَجَّاجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّهُمَا قَالَا فِي زَوْجٍ وَأَبَوَيْنِ: "لِلزَّوْجِ النِّصْفُ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ جَمِيعِ الْمَالِ، وَمَا بَقِيَ فَلِلْأَبِ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Hajjaaj, kutoka kwa Ash-Sha'biy; na Hajjaaj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kwamba wao wawili walisema kuhusu mume na wazazi wawili: "Mume ana nusu, na mama ana theluthi ya mali yote, na kilichobakia ni cha baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2918

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: "لِلْأُمِّ ثُلُثُ جَمِيعِ الْمَالِ فِي امْرَأَةٍ وَأَبَوَيْنِ، وَفِي زَوْجٍ وَأَبَوَيْنِ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametupa khabari Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Mama ana theluthi ya mali yote katika (mas-ala ya) mke na wazazi wawili, na katika (mas-ala ya) mume na wazazi wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2919

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الْفُضَيْلِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: خَالَفَ ابْنُ عَبَّاسٍ أَهْلَ الْقِبْلَةِ فِي امْرَأَةٍ وَأَبَوَيْنِ: "جَعَلَ لِلْأُمِّ الثُّلُثَ مِنْ جَمِيعِ الْمَالِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Al-Fudhwayl bin 'Amr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) aliwakhalifu watu wa Qiblah (Waislamu) kuhusu mke na wazazi wawili: "Alimfanyia mama theluthi ya mali yote."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1896
Hadiyth
2920

4-Mlangoباب: في ابنة وأختMlango Wa Kuhusu Binti Na Dada

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ الثَّوْرِيِّ، عَنْ أَشْعَثَ بْنِ أَبِي الشَّعْثَاءِ، عَنْ الْأَسْوَدِ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: "قَضَى مُعَاذُ بْنُ جَبَلٍ بِالْيَمَنِ فِي بِنْتٍ وَأُخْتٍ، فَأَعْطَى الْبِنْتَ النِّصْفَ، وَالْأُخْتَ النِّصْفَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan Ath-Thawriy, kutoka kwa Ash'ath bin Abish-Sha'thaa, kutoka kwa Al-Aswad bin Yaziyd, amesema: "Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) alihukumu huko Yemen kuhusu binti na dada: akampa binti nusu, na dada nusu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1898
Hadiyth
2921

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ الْأَسْوَدِ بْنِ يَزِيدَ: أَنَّ ابْنَ الزُّبَيْرِ كَانَ لَا يُوَرِّثُ الْأُخْتَ مِنْ الْأَبِ، وَالْأُمِّ مَعَ الْبِنْتِ حَتَّى حَدَّثَهُ الْأَسْوَدُ أَنَّ مُعَاذَ بْنَ جَبَلٍ جَعَلَ لِلْبِنْتِ النِّصْفَ، وَلِلْأُخْتِ النِّصْفَ "، فَقَالَ: أَنْتَ رَسُولِي إِلَى عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَة، فَأَخْبِرْهُ بِذَاكَ، وَكَانَ قَاضِيَهُ بِالْكُوفَةِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Al-Aswad bin Yaziyd, kwamba Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما) alikuwa hamrithishi dada wa baba na mama mmoja pamoja na binti, mpaka Al-Aswad alipomsimulia kwamba Mu'aadh bin Jabal (رضي الله عنه) "alimfanyia binti nusu, na dada nusu." Akasema: Wewe ni mjumbe wangu kwa 'Abdu-Allaah bin 'Utbah; mkhabarishe hilo. Naye alikuwa Qaadhi wake huko Al-Kuwfah.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1898
Hadiyth
2922

حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ عُمَرَ، قَالَ: سَأَلْتُ ابْنَ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ رَجُلٍ تَرَكَ بِنْتًا وَأُخْتًا؟ فَقَالَ: "لِابْنَتِهِ النِّصْف، وَلأُخْتِهِ مَا بَقِيَ" قَالَ: وَقَالَ: أَخْبَرَنِي أَبِي، عَنْ خَارِجَةَ بْنِ زَيْدٍ: أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ كَانَ "يَجْعَلُ الْأَخَوَاتِ مَعَ الْبَنَاتِ عَصَبَةً، لَا يَجْعَلُ لَهُنَّ إِلَّا مَا بَقِيَ"

Ametusimulia Bishr bin 'Umar, amesema: Nilimuuliza Ibn Abiz-Zinaad kuhusu mtu aliyeacha binti na dada. Akasema: "Binti yake ana nusu, na dada yake ana kilichobakia." Akasema: Na akasema: Amenikhabarisha baba yangu, kutoka kwa Khaarijah bin Zayd, kwamba Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) alikuwa "akiwafanya madada pamoja na mabinti kuwa 'asabah (warithi wanaochukua kilichobakia baada ya wenye mafungu), hawafanyii (fungu) ila kilichobakia."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1898
Hadiyth
2923

5-Mlangoباب: في المشركةMlango Wa Kuhusu Al-Musharrakah (Mirathi
Ambayo Ndugu Wa Baba Na Mama Hushirikishwa
Na Ndugu Wa Mama Katika Theluthi)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَنْصُورٍ، وَالْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: فِي زَوْجٍ، وَأُمٍّ، وَإِخْوَةٍ لِأَبٍ وَأُم، وَإِخْوَةٍ لِأُمٍّ، قَالَ: كَانَ عُمَر، وَعَبْدُ اللَّه، ِوَزَيْدٌ يُشَرِّكُونَ، وَقَالَ عُمَرُ: "لَمْ يَزِدْهُمْ الْأَبُ إِلَّا قُرْبًا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Manswuwr na Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kuhusu mume, na mama, na ndugu wa baba na mama mmoja, na ndugu wa mama mmoja, amesema: 'Umar, na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd], na Zayd (رضي الله عنهم) walikuwa wakishirikisha (ndugu wa baba na mama mmoja pamoja na ndugu wa mama mmoja katika theluthi). Na 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Baba hakuwazidishia ila ukaribu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1900
Hadiyth
2924

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ، عَنْ عَلِيٍّ: أَنَّهُ كَانَ "لَا يُشَرِّكُ"

Ametusimulia Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba yeye alikuwa "hashirikishi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1900
Hadiyth
2925

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ سُلَيْمَانَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِي مِجْلَزٍ: أَنَّ عُثْمَانَ كَانَ يُشَرِّك، وَعَلِيٌّ كَانَ لا يُشَرِّكُ "

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Sulaymaan At-Taymiy, kutoka kwa Abuw Mijlaz, kwamba 'Uthmaan (رضي الله عنه) alikuwa akishirikisha, na 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa hashirikishi.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1901
Hadiyth
2926

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ ذَكْوَانَ: "أَنَّ زَيْدًا كَانَ يُشَرِّكُ"

Ametusimulia Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Dhakwaan: "Kwamba Zayd (رضي الله عنه) alikuwa akishirikisha."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1901
Hadiyth
2927

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ عُمَيْرٍ، عَنْ شُرَيْح: " أَنَّهُ كَانَ يُشَرِّكُ

Ametusimulia Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin 'Umayr, kutoka kwa Shurayh: "Kwamba yeye alikuwa akishirikisha."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1901
Hadiyth
2928

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الْحَجَّاجِ، عَنْ عَبْدِ الْمَلِكِ بْنِ الْمُغِيرَةِ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ فَيْرُوزَ، عَنْ أَبِيه: أَنَّ عُمَرَ قَالَ فِي الْمُشَرَّكَة:" لَمْ يَزِدْهُمْ الْأَبُ إِلَّا قُرْبًا

Ametusimulia Muhammad bin Asw-Swalt, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Al-Hajjaaj, kutoka kwa 'Abdul-Malik bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Fayruwz, kutoka kwa baba yake, kwamba 'Umar (رضي الله عنه) alisema kuhusu Al-Musharrakah (mirathi ambayo ndugu wa baba na mama hushirikishwa na ndugu wa mama katika theluthi): "Baba hakuwazidishia ila ukaribu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1901
Hadiyth
2929

6-Mlangoباب: في ابني عم: أحدهما زوج والآخر أخ لأمMlango Wa Kuhusu Wana Wawili Wa Ami: Mmoja Wao
Ni Mume, Na Mwingine Ni Kaka Wa Mama Mmoja

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ الْأَعْوَرِ، قَالَ: أُتِيَ عَبْدُ اللَّهِ فِي فَرِيضَةِ بَنِي عَمٍّ، أَحَدُهُمْ أَخٌ لِأُمٍّ، فَقَالَ: الْمَالُ أَجْمَعُ لِأَخِيهِ لِأُمِّه، فَأَنْزَلَهُ بِحِسَابِ، أَوْ بِمَنْزِلَةِ الْأَخِ مِنْ الْأَبِ وَالْأُمِّ، فَلَمَّا قَدِمَ عَلِيٌّ، سَأَلْتُهُ عَنْهَا، وَأَخْبَرْتُهُ بِقَوْلِ عَبْدِ اللَّهِ، فَقَالَ: "يَرْحَمُهُ اللَّهُ، إِنْ كَانَ لَفَقِيهًا، أَمَّا أَنَا فَلَمْ أَكُنْ لِأَزِيدَهُ عَلَى مَا فَرَضَ اللَّهُ لَهُ: سَهْمٌ السُّدُسُ، ثُمَّ يُقَاسِمُهُمْ كَرَجُلٍ مِنْهُمْ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith Al-A'war, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) aliletewa (mas-ala ya) mirathi ya wana wa ami, mmoja wao ni kaka wa mama mmoja. Akasema: Mali yote ni ya kaka yake wa mama mmoja. Akamweka kwa hesabu — au: katika daraja — ya kaka wa baba na mama mmoja. Basi 'Aliy (رضي الله عنه) alipowasili, nilimuuliza kuhusu hilo, na nikamkhabarisha kauli ya 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه). Akasema: "Allaah Amrehemu! Hakika alikuwa ni Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh). Ama mimi, nisingemzidishia juu ya kile Alichomfaridhia Allaah: fungu la sudusi, kisha anagawana nao kama mtu mmoja miongoni mwao."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1902
Hadiyth
2930

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ، عَنْ عَلِي: أَنَّهُ أُتِيَ فِي ابْنَيْ عَمٍّ أَحَدُهُمَا أَخٌ لِأُمٍّ، فَقِيلَ لِعَلِيٍّ: إِنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ كَانَ يُعْطِيهِ الْمَالَ كُلَّهُ، فَقَالَ عَلِيٌّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: إِنْ كَانَ لَفَقِيهًا، وَلَوْ كُنْتُ أَنَا "أَعْطَيْتُهُ السُّدُسَ، وَمَا بَقِيَ كَانَ بَيْنَهُمْ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba aliletewa (mas-ala ya) wana wawili wa ami, mmoja wao ni kaka wa mama mmoja. 'Aliy (رضي الله عنه) akaambiwa: Hakika Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa akimpa mali yote. 'Aliy (رضي الله عنه) akasema: Hakika alikuwa ni Faqiyh (Mwanazuoni wa Fiqh); na lau ningekuwa mimi, "ningempa sudusi, na kilichobakia kingekuwa baina yao."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1903
Hadiyth
2931

7-Mlangoباب: في بنت وابنة ابن، وأخت لأب وأمMlango Wa Kuhusu Binti, Na Binti Wa Mwana, Na Dada Wa Baba
Na Mama Mmoja

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ الثَّوْرِيُّ، عَنْ أَبِي قَيْسٍ الْأَوْدِيِّ، عَنْ هُزَيْلِ بْنِ شُرَحْبِيلَ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى أَبِي مُوسَى الْأَشْعَرِيِّ، وَإِلَى سَلْمَانَ بْنِ رَبِيعَةَ فَسَأَلَهُمَا عَنْ بِنْتٍ، وَبِنْتِ ابْنٍ، وَأُخْتٍ لِأُمٍّ وَأَبٍ، فَقَالَا: لِلِابْنَةِ النِّصْفُ، وَمَا بَقِيَ فَلِلْأُخْتِ، وَأْتِ ابْنَ مَسْعُودٍ فَإِنَّهُ سَيُتَابِعُنَا، فَجَاءَ الرَّجُلُ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ، فَسَأَلَهُ عَنْ ذَلِكَ، فَقَالَ: لَقَدْ ضَلَلْتُ إِذًا، وَمَا أَنَا مِنْ الْمُهْتَدِينَ، وَإِنِّي أَقْضِي بِمَا "قَضَى بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: لِلِابْنَةِ النِّصْفُ، وَلِابْنَةِ الِابْنِ السُّدُسُ، وَمَا بَقِيَ فَلِلْأُخْتِ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan Ath-Thawriy, kutoka kwa Abuw Qays Al-Awdiy, kutoka kwa Huzayl bin Shurahbiyl, amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Abuw Muwsaa Al-Ash'ariy (رضي الله عنه) na kwa Salmaan bin Rabiy'ah, akawauliza kuhusu binti, na binti wa mwana, na dada wa mama na baba mmoja. Wakasema: Binti ana nusu, na kilichobakia ni cha dada; na mwendee Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), kwani yeye atatufuata (katika hilo). Yule mtu akaja kwa 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه), akamuuliza kuhusu hilo. Akasema: Kwa yakini nitakuwa nimepotoka, na hapo nami sitokuwa miongoni mwa waliohidika! Na hakika mimi ninahukumu kwa yale "aliyohukumu kwayo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): binti ana nusu, na binti wa mwana ana sudusi, na kilichobakia ni cha dada."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1903
Hadiyth
2932

8-Mlangoباب: في الإخوة والأخوات والولد، وولد الولدMlango Wa Kuhusu Kaka
Na Madada, Na Watoto, Na Watoto Wa Watoto

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ: أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ فِي أَخَوَاتٍ لِأَبٍ وَأُمٍّ، وَإِخْوَةٍ وَأَخَوَاتٍ لِأَبٍ: "لِلْأَخَوَاتِ لِلْأَبِ وَالْأُمِّ الثُّلُثَانِ، وَمَا بَقِيَ فَلِلذُّكُورِ دُونَ الْإِنَاثِ"، فَقَدِمَ مَسْرُوقٌ الْمَدِينَةَ، فَسَمِعَ قَوْلَ زَيْدٍ فِيهَا فَأَعْجَبَهُ، فَقَالَ لَهُ بَعْضُ أَصْحَابِهِ: أَتَتْرُكُ قَوْلَ عَبْدِ اللَّهِ؟ قَالَ: إِنِّي أَتَيْتُ الْمَدِينَةَ فَوَجَدْتُ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ مِنْ الرَّاسِخِينَ فِي الْعِلْمِ. قَالَ أَحْمَدُ: فَقُلْتُ لِأَبِي شِهَاب: وَكَيْفَ قَالَ زَيْدٌ فِيهَا؟ قَالَ: شَرَّكَ بَيْنَهُمْ

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Muslim, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kwamba alikuwa akisema kuhusu madada wa baba na mama mmoja, na kaka na madada wa baba mmoja: "Madada wa baba na mama mmoja wana theluthi mbili, na kilichobakia ni cha wa kiume, si wa kike." Kisha Masruwq akawasili Madiynah, akasikia kauli ya Zayd (رضي الله عنه) kuhusu hilo, ikampendeza. Baadhi ya wenzake wakamwambia: Je, unaiacha kauli ya 'Abdu-Allaah (رضي الله عنه)? Akasema: Hakika mimi nilikwenda Madiynah, nikamkuta Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) ni miongoni mwa wenye msingi madhubuti katika ilimu. Ahmad amesema: Nikamwambia Abuw Shihaab: Na Zayd (رضي الله عنه) alisema vipi kuhusu hilo? Akasema: Aliwashirikisha baina yao.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1904
Hadiyth
2933

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ عِيسَى بْنِ يُونُسَ، عَنْ إِسْمَاعِيل، قَالَ: ذَكَرْنَا عِنْدَ حَكِيمِ بْنِ جَابِر: أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ قَالَ فِي أَخَوَاتٍ لِأَبٍ وَأُمٍّ وَإِخْوَةٍ وَأَخَوَاتٍ لِأَبٍ: أَنَّهُ كَانَ يُعْطِي الْأَخَوَاتِ مِنْ الْأَبِ وَالْأُمِّ الثُّلُثَيْنِ، وَمَا بَقِيَ فَلِلذُّكُورِ دُونَ الْإِنَاثِ، فَقَالَ حَكِيمٌ: قَالَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ: "هَذَا مِنْ عَمَلِ الْجَاهِلِيَّةِ أَنْ يَرِثَ الرِّجَالُ دُونَ النِّسَاءِ إِنَّ إِخْوَتَهُنَّ قَدْ رُدُّوا عَلَيْهِنَّ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Ismaa'iyl, amesema: Tulitaja mbele ya Hakiym bin Jaabir kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alisema kuhusu madada wa baba na mama mmoja, na kaka na madada wa baba mmoja: kwamba yeye alikuwa akiwapa madada wa baba na mama mmoja theluthi mbili, na kilichobakia ni cha wa kiume, si wa kike. Hakiym akasema: Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) amesema: "Hili ni katika amali za Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam): kwamba wanaume warithi, si wanawake. Hakika kaka zao wamerudishwa juu yao."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1905
Hadiyth
2934

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مَعْبَدِ بْنِ خَالِدٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَائِشَةَ: " أَنَّهَا كَانَتْ تُشَرِّكُ بَيْنَ ابْنَتَيْنِ وَابْنَةِ ابْن، وَابْنِ ابْن: تُعْطِي الِابْنَتَيْنِ الثُّلُثَيْنِ، وَمَا بَقِيَ فَشَرَّكَتْهُمْ وَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ لَا يُشَرِّكُ، يُعْطِي الذُّكُورَ دُونَ الْإِنَاثِ، وَقَالَ:" الْأَخَوَاتُ بِمَنْزِلَةِ الْبَنَاتِ "

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ma'bad bin Khaalid, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها): "Kwamba yeye alikuwa akishirikisha baina ya mabinti wawili, na binti wa mwana, na mwana wa mwana: huwapa mabinti wawili theluthi mbili, na kilichobakia aliwashirikisha (ndani yake)." Na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) alikuwa hashirikishi: huwapa wa kiume, si wa kike. Na akasema: "Madada wako katika daraja ya mabinti."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1906
Hadiyth
2935

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي سَهْلٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ كَانَ يَقُولُ فِي بِنْتٍ وَبَنَاتِ ابْنٍ، وَابْنِ ابْنٍ: "إِنْ كَانَتِ الْمُقَاسَمَةُ بَيْنَهُمْ أَقَلَّ مِنْ السُّدُسِ، أَعْطَاهُمْ السُّدُسَ، وَإِنْ كَانَ أَكْثَرَ مِنَ السُّدُس، ِأَعْطَاهُمُ السُّدُسَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Sahl, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa akisema kuhusu binti, na mabinti wa mwana, na mwana wa mwana: "Ikiwa kugawana baina yao ni chini ya sudusi, aliwapa sudusi; na ikiwa ni zaidi ya sudusi, aliwapa sudusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1906
Hadiyth
2936

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ مَسْرُوقٍ: أَنَّهُ كَانَ يُشَرِّكُ فَقَالَ لَهُ عَلْقَمَةُ: هَلْ أَحَدٌ مِنْهُمْ أَثْبَتُ مِنْ عَبْدِ اللَّهِ؟ فَقَالَ: لَا، وَلَكِنِّي رَأَيْتُ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ، وَأَهْلَ الْمَدِينَةِ "يُشَرِّكُونَ فِي ابْنَتَيْنِ وَبِنْتِ ابْن، ٍوَابْنِ ابْن، وَأُخْتَيْنِ"

Ametusimulia Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Masruwq, kwamba alikuwa akishirikisha. 'Alqamah akamwambia: Je, yuko yeyote miongoni mwao aliye thabiti zaidi kuliko 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه)? Akasema: Hapana; lakini nimemuona Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) na watu wa Madiynah "wakishirikisha kuhusu mabinti wawili, na binti wa mwana, na mwana wa mwana, na madada wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1906
Hadiyth
2937

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سِيرِينَ، عَنْ شُرَيْحٍ: "فِي امْرَأَةٍ تَرَكَتْ زَوْجَهَا، وَأُمَّهَا، وَأُخْتَهَا لِأَبِيهَا وَأُمِّهَا، وَأُخْتَهَا لِأَبِيهَا، وَإِخْوَتَهَا لِأُمِّهَا، جَعَلَهَا مِنْ سِتَّةٍ، ثُمَّ رَفَعَهَا فَبَلَغَتْ عَشْرَةً، لِلزَّوْجِ النِّصْفُ ثَلَاثَةُ أَسْهُمٍ، وَلِلْأُخْتِ مِنْ الْأَبِ وَالْأُمِّ النِّصْفُ ثَلَاثَةُ أَسْهُمٍ، وَلِلْأُمِّ السُّدُسُ سَهْمٌ، وَلِلْإِخْوَةِ مِنْ الْأُمِّ الثُّلُثُ سَهْمَانِ، وَلِلْأُخْتِ مِنْ الْأَبِ سَهْمٌ تَكْمِلَةُ الثُّلُثَيْنِ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn, kutoka kwa Shurayh: "Kuhusu mwanamke aliyeacha mumewe, na mama yake, na dada yake wa baba na mama mmoja, na dada yake wa baba mmoja, na ndugu zake wa mama mmoja: aliifanya (mas-ala hiyo) kutoka (mafungu) sita, kisha akaiongeza ikafikia kumi: mume ana nusu, mafungu matatu; na dada wa baba na mama mmoja ana nusu, mafungu matatu; na mama ana sudusi, fungu moja; na ndugu wa mama mmoja wana theluthi, mafungu mawili; na dada wa baba mmoja ana fungu moja, kukamilisha theluthi mbili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1907
Hadiyth
2938

9-Mlangoباب: في المملوكين وأهل الكتابMlango Wa Kuhusu Watumwa Na Ahlul-Kitaab (Watu Wa Kitabu)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: أَنَّ عَلِيًّا، وَزَيْدًا كَانَا "لَا يَحْجُبَانِ بِالْكُفَّار، وَلا بِالْمَمْلُوكِينَ، وَلَا يُوَرِّثَانِهِمْ شَيْئًا" وَكَانَ عَبْدُ اللَّهِ "يَحْجُبُ بِالْكُفَّارِ وَبِالْمَمْلُوكِينَ، وَلَا يُوَرِّثُهُمْ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy: kwamba 'Aliy na Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنهما) walikuwa "hawawafanyi makafiri wala watumwa kuwa ni wenye kuzuia (mafungu ya warithi wengine), wala hawawarithishi chochote"; na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) alikuwa "akiwafanya makafiri na watumwa kuwa ni wenye kuzuia (mafungu ya warithi wengine), wala hawarithishi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1908
Hadiyth
2939

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: أَنَّ عَلِيًّا، وَزَيْدًا، قَالَا:" الْمَمْلُوكُونَ، وَأَهْلُ الْكِتَابِ لا يَحْجُبُونَ وَلا يَرِثُونَ وَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ:" يَحْجُبُونَ وَلَا يَرِثُونَ "

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym: kwamba 'Aliy na Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنهما) walisema: "Watumwa na Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu) hawazuii (mafungu ya warithi wengine), wala hawarithi." Na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) akasema: "Wanazuia, wala hawarithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1908
Hadiyth
2940

10-Mlangoباب: الجدMlango Wa Babu

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَخْبَرَنَا يَحْيَى، عَنْ سَعِيدٍ: أَنَّ عُمَرَ "كَانَ كَتَبَ مِيرَاثَ الْجَدِّ، حَتَّى إِذَا طُعِنَ دَعَا بِهِ فَمَحَاهُ، ثُمّ قَالَ: سَتَرَوْنَ رَأْيَكُمْ فِيهِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametukhabarisha Yahyaa, kutoka kwa Sa'iyd: kwamba 'Umar (رضي الله عنه) "alikuwa ameandika (hukmu ya) mirathi ya babu; mpaka alipochomwa (kisu), aliitisha (maandishi) hayo, akayafuta. Kisha akasema: Mtaona rai yenu kuhusu (jambo) hilo."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1909
Hadiyth
2941

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ، أنبأنا أَشْعَثُ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: قُلْتُ لِعَبِيدَةَ: حَدِّثْنِي عَنِ الْجَدِّ، فَقَالَ: "إِنِّي لَأَحْفَظُ فِي الْجَدِّ ثَمَانِينَ قَضِيَّةً مُخْتَلِفَةً"

Ametukhabarisha Yaziyd, ametupa khabari Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: Nilimwambia 'Abiydah: Nisimulie kuhusu babu. Akasema: "Hakika mimi nimehifadhi kuhusu babu maamuzi themanini yanayotofautiana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1909
Hadiyth
2942

أَخْبَرَنَا أَبُو غَسَّانَ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عَمْرٍو الْخَارِفِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: أَتَاهُ رَجُلٌ فَسَأَلَهُ عَنْ فَرِيضَة، فَقَالَ: "إِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهَا جَدٌّ، فَهَاتِهَا" حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَبِي إِسْحَقَ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ عَمْرٍو قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى عَلِيٍّ فَسَأَلَهُ عَنْ فَرِيضَةٍ، فَقَالَ: "إِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهَا جَدٌّ، فَهَاتِهَا"

Ametukhabarisha Abuw Ghassaan, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Ubayd bin 'Amr Al-Khaarifiy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alimjia akamuuliza kuhusu mas-ala ya mirathi. Akasema: "Ikiwa hakuna babu ndani yake, basi ilete." Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Ubayd bin 'Amr, amesema: Mtu mmoja alikuja kwa 'Aliy (رضي الله عنه) akamuuliza kuhusu mas-ala ya mirathi. Akasema: "Ikiwa hakuna babu ndani yake, basi ilete."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1909
Hadiyth
2943

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ أَيُّوبَ السَّخْتِيَانِيِّ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ رَجُلٍ مِنْ مُرَادٍ، ٍسَمِعَ عَلِيًّا، يَقُولُ:" مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَتَقَحَّمَ جَرَاثِيمَ جَهَنَّمَ، فَلْيَقْضِ بَيْنَ الْجَدِّ وَالْإِخْوَةِ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ayyuwb As-Sakhtiyaaniy, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa mtu mmoja wa (kabila la) Muraad, (kwamba) alimsikia 'Aliy (رضي الله عنه) akisema: "Anayefurahishwa na kujitosa katika vina vya Jahannam, basi na ahukumu kati ya babu na ndugu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1910
Hadiyth
2944

11-Mlangoباب: قول أبي بكر في الجدMlango Wa Kauli Ya Abuw Bakr (رضي الله عنه) Kuhusu Babu

أخبرنا مسلم بن إبراهيم، حدثنا وهيب، حدثنا خالد، عن أبي نضرة، عن أبي سعيد الخدري،

Ametukhabarisha Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Khaalid, kutoka kwa Abuw Nadhwrah, kutoka kwa Abuw Sa'iyd Al-Khudriy (رضي الله عنه),

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2945

وَعَنْ عِكْرِمَةَ: أَنَّ أَبَا بَكْرٍ الصِّدِّيقَ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا".

Na kutoka kwa 'Ikrimah: kwamba Abuw Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) "alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2946

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ سُلَيْمَانَ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ كُرْدُوسٍ، عَن أبِى بُرْدَةَ، عَنْ أَبِي مُوسَى: أنَّ أَبَا بَكْرٍ الصِّدِّيقِ جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Sulaymaan Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Kurduws, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه): kwamba Abuw Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2947

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى، عَنْ كُرْدُوسٍ، عَنْ أَبِي مُوسَى، أَنَّ أَبَا بَكْرٍ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Abuw Burdah bin Abiy Muwsaa, kutoka kwa Kurduws, kutoka kwa Abuw Muwsaa (رضي الله عنه), kwamba Abuw Bakr (رضي الله عنه) "alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2948

أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ مَرْوَانَ، عَنْ عُثْمَانَ: أَنَّ أَبَا بَكْرٍ كَانَ "يَجْعَلُ الْجَدَّ أَبًا"

Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa Abuw Burdah, kutoka kwa Marwaan, kutoka kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه): kwamba Abuw Bakr (رضي الله عنه) alikuwa "akimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2949

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، وَمُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عُثْمَانَ: أَنَّ أَبَا بَكْرٍ كَانَ "يَجْعَلُ الْجِدَّ أَبًا"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah na Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه): kwamba Abuw Bakr (رضي الله عنه) alikuwa "akimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1911
Hadiyth
2950

أَخْبَرَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، قَالَ: لَقِيتُ مَرْوَانَ بْنَ الْحَكَمِ بِالْمَدِينَةِ، فَقَالَ: يَا ابْنَ أَبِي مُوسَى، أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّ الْجَدَّ لَا يُنَزَّلُ فِيكُمْ مَنْزِلَةَ الْأَبِ، وَأَنْتَ لَا تُنْكِرُ؟ قَالَ: قُلْتُ: وَلَوْ كُنْتَ أَنْتَ لَمْ تُنْكِرْ، قَالَ مَرْوَانُ: فَأَنَا أَشْهَدُ عَلَى عُثْمَانَ بْنِ عَفَّانَ أَنَّهُ شَهِدَ عَلَى أَبِي بَكْرٍ أَنَّهُ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا، إِذَا لَمْ يَكُنْ دُونَهُ أَبٌ"

Ametukhabarisha Al-Aswad bin 'Aamir, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa Abuw Burdah, amesema: Nilikutana na Marwaan bin Al-Hakam huko Madiynah, akasema: Yaa Ibn Abiy Muwsaa, je, sikukhabarishwa kwamba babu hawekwi kwenu katika daraja ya baba, nawe hukatai? Akasema: Nikasema: Na lau ungekuwa ni wewe, usingekataa. Marwaan akasema: Basi mimi nashuhudia juu ya 'Uthmaan bin 'Affaan (رضي الله عنه) kwamba yeye alishuhudia juu ya Abuw Bakr (رضي الله عنه) kwamba "alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba, ikiwa hakuna baba aliye karibu zaidi kuliko yeye."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1912
Hadiyth
2951

حَدَّثَنَا الْأَسْوَدُ بْنُ عَامِرٍ، أَنْبَأَنَا شُعْبَةُ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ أَبِي نَضْرَةَ، وَعَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ أَبَا بَكْرٍ كَانَ "يَجْعَلُ الْجَدَّ أَبًا"

Ametusimulia Al-Aswad bin 'Aamir, ametupa khabari Shu'bah, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Abuw Nadhwrah; na kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): kwamba Abuw Bakr (رضي الله عنه) alikuwa "akimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1913
Hadiyth
2952

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: جَعَلَهُ الَّذِي قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَوْ كُنْتُ مُتَّخِذًا أَحَدًا خَلِيلًا، لَاتَّخَذْتُهُ خَلِيلًا، وَلَكِنْ أُخُوَّةُ الْإِسْلَامِ أَفْضَلُ، يَعْنِي أَبَا بَكْرٍ جَعَلَهُ أَبًا، يَعْنِي: الْجَدَّ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: Aliyemfanya (babu kuwa baba) ni yule ambaye Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alisema (kumhusu): "Lau ningemfanya mtu yeyote kuwa Khaliyl (kipenzi mwandani), ningemfanya yeye kuwa Khaliyl; lakini udugu wa Kiislamu ni bora zaidi." Yaani: Abuw Bakr (رضي الله عنه); alimfanya kuwa baba — yaani: babu.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1913
Hadiyth
2953

حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ، عَنْ ابْنِ الزُّبَيْر: أَنَّ أَبَا بَكْرٍ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا"

Ametusimulia Muslim, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa Ibn Abiy Mulaykah, kutoka kwa Ibn Az-Zubayr (رضي الله عنهما): kwamba Abuw Bakr (رضي الله عنه) "alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1913
Hadiyth
2954

حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: إِنَّ الْجَدَّ قَدْ مَضَتْ سُنَّتُهُ، وَإِنَّ أَبَا بَكْرٍ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا"، وَلَكِنَّ النَّاسَ تَخَيَّرُوا

Ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Hakika (hukmu ya) babu, Sunnah yake imekwishapita; na hakika Abuw Bakr (رضي الله عنه) alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba; lakini watu wamejichagulia (rai zao)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1913
Hadiyth
2955

12-Mlangoباب: في قول عمر في الجدMlango Wa Kuhusu Kauli Ya 'Umar (رضي الله عنه) Juu Ya Babu

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ:" إِنَّ أَوَّلَ جَدٍّ وَرِثَ فِي الْإِسْلَامِ عُمَرُ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Hakika babu wa kwanza kurithi katika Islaam ni 'Umar (رضي الله عنه)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1914
Hadiyth
2956

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ عَاصِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "إِنَّ أَوَّلَ جَدٍّ وَرِثَ فِي الْإِسْلَامِ عُمَر، فَأَخَذَ مَالَهُ، فَأَتَاهُ عَلِيٌّ، وَزَيْدٌ، فَقَالَا: لَيْسَ لَكَ ذَاكَ، إِنَّمَا أَنْتَ كَأَحَدِ الْأَخَوَيْنِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa 'Aaswim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Hakika babu wa kwanza kurithi katika Islaam ni 'Umar (رضي الله عنه); akachukua mali yake (yote). 'Aliy na Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنهما) wakamjia, wakasema: "Hilo si lako; hakika wewe ni kama mmoja wa ndugu wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1915
Hadiyth
2957

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ عِيسَى الْحَنَّاطِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: كَانَ عُمَرُ " يُقَاسِمُ بِالْجَدِّ مَعَ الْأَخِ وَالْأَخَوَيْنِ، فَإِذَا زَادُوا أَعْطَاهُ الثُّلُثَ، وَكَانَ يُعْطِيهِ مَعَ الْوَلَدِ السُّدُسَ

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa 'Iysaa Al-Hannaatw, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "'Umar (رضي الله عنه) alikuwa akimgawia babu (fungu sawa na ndugu) pamoja na ndugu mmoja na ndugu wawili; na (ndugu) wanapozidi, alimpa theluthi. Na alikuwa akimpa sudusi pamoja na mtoto."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1915
Hadiyth
2958

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا هِشَامُ بْنُ عُرْوَةَ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ مَرْوَانَ بْنِ الْحَكَمِ: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ لَمَّا طُعِنَ، اسْتَشَارَهُمْ فِي الْجَدِّ، فَقَالَ:" إِنِّي كُنْتُ رَأَيْتُ فِي الْجَدِّ رَأْيًا، فَإِنْ رَأَيْتُمْ أَنْ تَتَّبِعُوهُ، فَاتَّبِعُوهُ، فَقَالَ لَهُ عُثْمَانُ: إِنْ نَتَّبِعْ رَأْيَكَ فَإِنَّهُ رَشَدٌ، وَإِنْ نَتَّبِعْ رَأْيَ الشَّيْخِ، فَلَنِعْمَ ذُو الرَّأْيِ كَانَ

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Hishaam bin 'Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Marwaan bin Al-Hakam: kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) alipochomwa (kisu), aliwataka shauri kuhusu (mirathi ya) babu, akasema: "Hakika mimi nilikuwa nimeona rai (fulani) kuhusu babu; basi mkiona kuifuata, ifuateni." 'Uthmaan (رضي الله عنه) akamwambia: Tukifuata rai yako, basi hiyo ni uongofu; na tukifuata rai ya mzee (aliyekuwa kabla yako), basi hakika alikuwa mwenye rai bora kabisa!

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1915
Hadiyth
2959

13-Mlangoباب: قول علي في الجدMlango Wa Kauli Ya 'Aliy (رضي الله عنه) Kuhusu Babu

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: كَتَبَ ابْنُ عَبَّاسٍ إِلَى عَلِيّ وَابْنُ عَبَّاسٍ بِالْبَصْرَةِ: إِنِّي أُتِيتُ بِجَدٍّ وَسِتَّةِ إِخْوَةٍ، فَكَتَبَ إِلَيْهِ عَلِيٌّ:" أَنْ أَعْطِ الْجَدَّ سُدسا، وَلَا تُعْطِهِ أَحَدًا بَعْدَهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alimwandikia 'Aliy (رضي الله عنه) — na Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) alikuwa Al-Baswrah —: Hakika mimi nimeletewa (mas-ala ya mirathi ya) babu na ndugu sita. 'Aliy (رضي الله عنه) akamwandikia: "Mpe babu sudusi, wala usimpe (hiyo) yeyote baada yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1916
Hadiyth
2960

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ إِسْمَاعِيل، عَنْ الشَّعْبِيِّ فِي سِتَّةِ إِخْوَةٍ وَجَدٍّ، قَالَ:" أَعْطِ الْجَدَّ السُّدُسَ. قَالَ أَبُو مُحَمَّد: كَأَنَّهُ يَعْنِي: عَلِيًّا رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ الشَّعْبِيُّ يَرْوِيهِ عَنْ عَلِيٍّ رِضْوَانُ اللَّهِ عَلَيْهِ

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Ismaa'iyl, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kuhusu ndugu sita na babu, amesema: "Mpe babu sudusi."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Ni kama kwamba anamkusudia 'Aliy (رضوان الله عليه); Ash-Sha'biy anaipokea kutoka kwa 'Aliy (رضوان الله عليه).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1917
Hadiyth
2961

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلَمَةَ: أَنَّ عَلِيًّا كَانَ" يَجْعَلُ الْجَدَّ أَخًا مَتَى يَكُونَ سَادِسًا

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Salamah: kwamba 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa "akimfanya babu kuwa (ni sawa na) ndugu mpaka atakapokuwa wa sita."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1918
Hadiyth
2962

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ الْحَسَنِ: أَنَّ عَلِيًّا كَانَ" يُشَرِّكُ الْجَدَّ مَعَ الْإِخْوَةِ إِلَى السُّدُسِ

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan: kwamba 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa "akimshirikisha babu pamoja na ndugu mpaka sudusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1918
Hadiyth
2963

حَدَّثَنَا هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُرَّةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ سَلَمَةَ، قَالَ: كَانَ عَلِيٌّ " يُشَرِّكُ بَيْنَ الْجَدِّ وَالْإِخْوَةِ حَتَّى يَكُونَ سَادِسًا

Ametusimulia Haashim bin Al-Qaasim, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa 'Amr bin Murrah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Salamah, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa "akishirikisha kati ya babu na ndugu mpaka (babu) atakapokuwa wa sita."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1918
Hadiyth
2964

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: كَانَ عَلِيٌّ " يُشَرِّكُ الْجَدَّ إِلَى سِتَّةٍ مَعَ الْإِخْوَةِ، يُعْطِي كُلَّ صَاحِبِ فَرِيضَةٍ فَرِيضَتَهُ، وَلَا يُوَرِّثُ أَخًا لِأُمٍّ مَعَ جَدٍّ، وَلَا أُخْتًا لِأُمٍّ، وَلَا يَزِيدُ الْجَدَّ مَعَ الْوَلَدِ عَلَى السُّدُسِ، إِلَّا أَنْ يَكُونَ غَيْرُهُ، وَلَا يُقَاسِمُ بِأَخٍ لِأَبٍ مَعَ أَخٍ لِأَبٍ وَأُمٍّ، وَإِذَا كَانَتْ أُخْتٌ لِأَبٍ وَأُمٍّ، وَأَخٌ لِأَبٍ، أَعْطَى الْأُخْتَ النِّصْفَ، وَالنِّصْفَ الْآخَرَ بَيْنَ الْجَدِّ وَالْأَخِ نِصْفَيْنِ، وَإِذَا كَانُوا إِخْوَةً وَأَخَوَاتٍ، شَرَّكَهُمْ مَعَ الْجَدِّ إِلَى السُّدُسِ

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa "akimshirikisha babu pamoja na ndugu mpaka (wawe) sita; akimpa kila mwenye fungu (lililowekwa) fungu lake. Wala hamrithishi kaka wa mama mmoja pamoja na babu, wala dada wa mama mmoja. Wala hamzidishii babu, pamoja na mtoto, zaidi ya sudusi, isipokuwa awepo mwingine asiyekuwa yeye. Wala hamgawii (babu, kwa kumhesabu) kaka wa baba mmoja pamoja na kaka wa baba na mama mmoja. Na anapokuwepo dada wa baba na mama mmoja na kaka wa baba mmoja, humpa dada nusu, na nusu nyingine (huigawa) kati ya babu na kaka, nusu kwa nusu. Na wanapokuwa ni ndugu wa kiume na dada, huwashirikisha pamoja na babu mpaka sudusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1919
Hadiyth
2965

14-Mlangoباب: قول ابن عباس في الجدMlango Wa Kauli Ya Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) Kuhusu Babu

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، عَنْ سُفْيَانَ، عَنْ الْعَبْسِيِّ هُوَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ خَالِدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مَعْقِلٍ، قَالَ: سُئِلَ ابْنُ عَبَّاسٍ عَنْ الْجَد؟ فَقَالَ:" أَيُّ أَبٍ لَكَ أَكْبَر؟ فَقُلْتُ أَنَا: آدَمُ، قَالَ: أَلَمْ تَسْمَعْ إِلَى قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى: {يَا بَنِي آدَمَ}

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Al-'Absiy — naye ni 'Abdu-Allaah bin Khaalid —, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Ma'qil, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) aliulizwa kuhusu babu. Akasema: "Ni baba yako yupi aliye mkubwa zaidi?" Nikasema mimi: Aadam (عليه السلام). Akasema: Je, hukusikia Kauli ya Allaah (تعالى):

يَا بَنِي آدَمَ

Enyi wana wa Aadam! [Al-A’raaf (7:26)]

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1919
Hadiyth
2966

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ إِسْمَاعِيل بْنِ سُمَيْعٍ، عَنْ رَجُلٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ:" لَوَدِدْتُ أَنِّي وَالَّذِينَ يُخَالِفُونَنِي فِي الْجَدِّ تَلَاعَنَّا، أَيُّنَا أَسْوَأُ قَوْلًا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ismaa'iyl bin Sumay', kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Ningependa kwamba mimi na wale wanaonipinga kuhusu babu tuombeane laana, (ili ijulikane) ni yupi kati yetu mwenye kauli mbaya zaidi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1920
Hadiyth
2967

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّهُ "جَعَلَ الْجَدَّ أَبًا"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): kwamba yeye "alimfanya babu kuwa (ni sawa na) baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1920
Hadiyth
2968

15-Mlangoباب: قول ابن مسعود في الجدMlango Wa Kauli Ya Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) Kuhusu Babu

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق قَالَ: دَخَلْتُ عَلَى شُرَيْحٍ وَعِنْدَهُ عَامِرٌ، وَإِبْرَاهِيمُ، وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ فِي فَرِيضَةِ امْرَأَةٍ مِنَّا: الْعَالِيَةِ، تَرَكَتْ زَوْجَهَا، وَأُمَّهَا، وَأَخَاهَا لِأَبِيهَا، وَجَدَّهَا، فَقَالَ لِي: هَلْ مِنْ أُخْتٍ؟ قُلْتُ: لَا، قَالَ: لِلْبَعْلِ الشَّطْرُ وَلِلْأُمِّ الثُّلُثُ، قَالَ: فَجَهِدْتُ عَلَى أَنْ يُجِيبَنِي، فَلَمْ يُجِبْنِي إِلَّا بِذَلِكَ، فَقَالَ إِبْرَاهِيمُ، وَعَامِرٌ، وَعَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ: مَا جَاءَ أَحَدٌ بِفَرِيضَةٍ أَعْضَلَ مِنْ فَرِيضَةٍ جِئْتَ بِهَا، قَالَ: فَأَتَيْتُ عَبِيدَةَ السَّلْمَانِيَّ وَكَانَ يُقَال: لَيْسَ بِالْكُوفَةِ أَحَدٌ أَعْلَمَ بِفَرِيضَةٍ مِنْ عَبِيدَةَ، وَالْحَارِثِ الْأَعْوَرَ، وَكَانَ عَبِيدَةُ يَجْلِسُ فِي الْمَسْجِدِ، فَإِذَا وَرَدَتْ عَلَى شُرَيْحٍ فَرِيضَةٌ فِيهَا جَدٌّ، رَفَعَهُمْ إِلَى عَبِيدَةَ، فَفَرَضَ فَسَأَلْتُهُ، فَقَالَ: إِنْ شِئْتُمْ نَبَّأْتُكُمْ بِفَرِيضَةِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ فِي هَذَا:" جَعَلَ لِلزَّوْجِ ثَلَاثَةَ أَسْهُمٍ النِّصْفَ، وَلِلْأُمِّ ثُلُثُ مَا بَقِيَ، السُّدُسُ مِنْ رَأْسِ الْمَالِ، وَلِلْأَخِ سَهْمٌ، وَلِلْجَدِّ سَهْمٌ، قَالَ أَبُو إِسْحَاقَ: الْجَدُّ أَبُو الْأَبِ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuw Is-haaq, amesema: Niliingia kwa Shurayh, na kwake walikuwepo 'Aamir, na Ibraahiym, na 'Abdur-Rahmaan bin 'Abdi-Allaah, kuhusu mas-ala ya mirathi ya mwanamke mmoja wa kwetu — Al-'Aaliyah —: aliacha mume wake, na mama yake, na kaka yake wa baba mmoja, na babu yake. (Shurayh) akaniambia: Je, kuna dada yeyote? Nikasema: Hapana. Akasema: Mume (atapata) nusu, na mama theluthi. Akasema: Nikajitahidi ili anijibu (zaidi), lakini hakunijibu isipokuwa kwa hilo. Ibraahiym, na 'Aamir, na 'Abdur-Rahmaan bin 'Abdi-Allaah wakasema: Hajaleta mtu yeyote mas-ala ya mirathi tata zaidi kuliko mas-ala uliyoileta. Akasema: Nikamwendea 'Abiydah As-Salmaaniy — na ilikuwa ikisemwa: Hakuna yeyote Al-Kuwfah aliye mjuzi zaidi wa mas-ala ya mirathi kuliko 'Abiydah na Al-Haarith Al-A'war; na 'Abiydah alikuwa akikaa Msikitini, na Shurayh anapoletewa mas-ala ya mirathi yenye babu ndani yake, huwapeleka kwa 'Abiydah, naye huwagawia mafungu —, nikamuuliza. Akasema: Mkipenda, nitakukhabarisheni mgao wa 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) katika (mas-ala kama) hii: "Alimpa mume mafungu matatu — nusu —, na mama theluthi ya kilichobakia — sudusi ya rasilimali (mali yote) —, na ndugu fungu moja, na babu fungu moja." Abuw Is-haaq amesema: "Babu ni baba wa baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1921
Hadiyth
2969

16-Mlangoباب: قول زيد في الجدMlango Wa Kauli Ya Zayd [Bin Thaabit] (رضي الله عنه) Kuhusu Babu

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ الْحَسَنِ: أَنَّ زَيْدًا كَانَ "يُشَرِّكُ الْجَدَّ مَعَ الْإِخْوَةِ إِلَى الثُّلُثِ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan: kwamba Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنه) alikuwa "akimshirikisha babu pamoja na ndugu mpaka theluthi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1922
Hadiyth
2970

حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ: أَنَّهُ كَانَ "يُقَاسِمُ بِالْجَدِّ مَعَ الْإِخْوَةِ إِلَى الثُّلُثِ، ثُمَّ لَا يُنْقِصُهُ"

Ametusimulia 'Umar bin Hafsw bin Ghiyaath, ametusimulia baba yangu, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه): kwamba yeye alikuwa "akimgawia babu (fungu sawa na) ndugu mpaka theluthi, kisha hampunguzii (zaidi ya hapo)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1922
Hadiyth
2971

حدثنا سعيد بن المغيرة، عن عيسى بن يونس، عن إسماعيل، قال: قال عامر: «خذ من أمر الجد ما اجتمع الناس عليه» قال أبو محمد: "يعني: قول زيد"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa 'Iysaa bin Yuwnus, kutoka kwa Ismaa'iyl, amesema: 'Aamir amesema: "Chukua katika jambo la babu yale ambayo watu wamekubaliana juu yake."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: "Yaani: kauli ya Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنه)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1922
Hadiyth
2972

17-Mlangoباب: الأكدرية: زوج، وأخت لأب وأم، وجد، وأمMlango Wa Al-Akdariyyah (Mas-ala Ya Mirathi):
Mume, Dada Wa Baba Na Mama Mmoja, Babu, Na Mama

أَخْبَرَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ هَمَّامٍ، عَنْ قَتَادَةَ: أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ قَالَ فِي أُخْتٍ، وَأُمٍّ، ٍّوَزَوْجٍ، وَجَدٍّ، قَالَ:" جَعَلَهَا مِنْ سَبْعٍ وَعِشْرِينَ: لِلْأُمِّ سِتَّةٌ، وَلِلزَّوْجِ تِسْعَةٌ، وَلِلْجَدِّ ثَمَانِيَةٌ، وَلِلْأُخْتِ أَرْبَعَةٌ

Ametukhabarisha Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Hammaam, kutoka kwa Qataadah: kwamba Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) alisema kuhusu (mirathi ya) dada, na mama, na mume, na babu; amesema: "Aliifanya (mirathi hiyo) kutoka (mafungu) ishirini na saba: mama sita, na mume tisa, na babu manane, na dada manne."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1924
Hadiyth
2973

18-Mlangoباب: في الجداتMlango Wa Kuhusu Bibi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ:" إِنَّ أَوَّلَ جَدَّةٍ أُطْعِمَتْ فِي الْإِسْلَامِ سَهْمًا أَمُّ أَبٍ، وَابْنُهَا حَيٌّ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Hakika bibi wa kwanza aliyepewa fungu (la mirathi) kama riziki katika Islaam ni mama wa baba, na hali mwanawe yu hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1924
Hadiyth
2974

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: "أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَطْعَمَ جَدَّةً سُدُسًا"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): "kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimpa bibi sudusi kama riziki."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1924
Hadiyth
2975

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ مَيْسَرَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ: أَنَّ عُمَرَ "وَرَّثَ جَدَّةً مَعَ ابْنِهَا"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibraahiym bin Maysarah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib: kwamba 'Umar (رضي الله عنه) "alimrithisha bibi pamoja na mwanawe."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1925
Hadiyth
2976

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، أَخْبَرَنِي مَنْصُورُ بْنُ الْمُعْتَمِرِ، قَالَ: سَمِعْتُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "أَطْعَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثَلَاثَ جَدَّاتٍ سُدُسًا. قَالَ: قُلْتُ لِإِبْرَاهِيمَ: مَنْ هُنَّهْ؟ قَالَ: جَدَّتَاكَ مِنْ قِبَلِ أَبِيكَ، وَجَدَّتُكَ مِنْ قِبَلِ أُمِّكَ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Shu'bah, amenikhabarisha Manswuwr bin Al-Mu'tamir, amesema: Nilimsikia Ibraahiym akisema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliwapa bibi watatu sudusi kama riziki." Akasema: Nikamwambia Ibraahiym: Ni akina nani hao? Akasema: "Bibi zako wawili wa upande wa baba yako, na bibi yako wa upande wa mama yako."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1926
Hadiyth
2977

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: أَنْبَأَنِي الْحَسَنُ، قَالَ: "تَرِثُ الْجِدَّةُ وَابْنُهَا حَيٌّ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Yaziyd bin Ibraahiym, amesema: Amenipa khabari Al-Hasan, amesema: "Bibi hurithi na hali mwanawe yu hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1926
Hadiyth
2978

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ دَاوُدَ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "لَا تَرِثُ أُمُّ أَبِ الْأُمِّ، ابْنُهَا الَّذِي تُدْلِي بِهِ لَا يَرِثُ، فَكَيْفَ تَرِثُ هِيَ؟"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Mama wa baba wa mama harithi; mwanawe ambaye kupitia kwake anafungamana (na maiti) harithi, basi vipi atarithi yeye?"

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1927
Hadiyth
2979

أَخْبَرَنَا أَبُو مَعْمَرٍ، عَنْ إِسْمَاعِيلَ ابْنِ عُلَيَّةَ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ عَلْقَمَةَ، عَنْ حُمَيْدِ بْنِ هِلَالٍ، عَنْ أَبِي الدَّهْمَاءِ، عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ، قَالَ: "تَرِثُ الْجِدَّةُ وَابْنُهَا حَيٌّ"

Ametukhabarisha Abuw Ma'mar, kutoka kwa Ismaa'iyl Ibn 'Ulayyah, kutoka kwa Salamah bin 'Alqamah, kutoka kwa Humayd bin Hilaal, kutoka kwa Abud-Dahmaa, kutoka kwa 'Imraan bin Huswayn (رضي الله عنه), amesema: "Bibi hurithi na hali mwanawe yu hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1927
Hadiyth
2980

19-Mlangoباب: قول أبي بكر الصديق في الجداتMlango Wa Kauli Ya Abuw Bakr
Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه) Kuhusu Bibi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: جَاءَتْ إِلَى أَبِي بَكْرٍ جَدَّةٌ أُمُّ أَبٍ، أَوْ أُمُّ أُمٍّ، فَقَالَتْ: إِنَّ ابْنَ ابْنِي أَوْ ابْنَ ابْنَتِي تُوُفِّيَ، وَبَلَغَنِي أَنَّ لِي نَصِيبًا، فَمَا لِي؟ فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ: مَا سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ فِيهَا شَيْئًا، وَسَأَسْأَلُ النَّاسَ، فَلَمَّا صَلَّى الظُّهْرَ، فَقَالَ: أَيُّكُمْ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ فِي الْجَدَّةِ شَيْئًا؟ فَقَالَ الْمُغِيرَةُ بْنُ شُعْبَةَ: أَنَا، قَالَ: مَاذَا؟ قَالَ: أَعْطَاهَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سُدُسًا، قَالَ: أَيَعْلَمُ ذَاكَ أَحَدٌ غَيْرُكَ؟ فَقَالَ مُحَمَّدُ بْنُ مَسْلَمَةَ: صَدَقَ، فَأَعْطَاهَا أَبُو بَكْرٍ السُّدُسَ، فَجَاءَتْ إِلَى عُمَرَ مِثْلُهَا، فَقَال: مَا أَدْرِي، مَا سَمِعْتُ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا شَيْئًا، وَسَأَسْأَلُ النَّاسَ، فَحَدَّثُوهُ بِحَدِيثِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ، وَمُحَمَّدِ بْنِ مَسْلَمَةَ، فَقَالَ عُمَرُ: أَيُّكُمَا خَلَتْ بِهِ فَلَهَا السُّدُسُ، فَإِنْ اجْتَمَعْتُمَا، فَهُوَ بَيْنَكُمَا

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Bibi mmoja — mama wa baba, au mama wa mama — alikuja kwa Abuw Bakr (رضي الله عنه), akasema: Hakika mwana wa mwanangu, au mwana wa binti yangu, amefariki, na imenifikia kwamba mimi nina fungu; basi nina nini? Abuw Bakr (رضي الله عنه) akasema: Sikumsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema chochote kumhusu (bibi), nami nitawauliza watu. Alipomaliza kuswali Adhuhuri, akasema: Ni nani kati yenu aliyemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema chochote kuhusu bibi? Al-Mughiyrah bin Shu'bah (رضي الله عنه) akasema: Mimi. Akasema: Nini? Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alimpa sudusi." Akasema: Je, kuna yeyote asiyekuwa wewe anayelijua hilo? Muhammad bin Maslamah (رضي الله عنه) akasema: Amesema kweli. Abuw Bakr (رضي الله عنه) akampa sudusi. Kisha bibi mfano wake akaja kwa 'Umar (رضي الله عنه); akasema: Sijui; sikusikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) chochote kumhusu (bibi), nami nitawauliza watu. Wakamsimulia Hadiyth ya Al-Mughiyrah bin Shu'bah na Muhammad bin Maslamah (رضي الله عنهما). 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Yeyote kati yenu wawili atakayekuwa peke yake, basi yeye ana sudusi; na mkikusanyika, basi (sudusi) hiyo ni kati yenu wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1928
Hadiyth
2981

20-Mlangoباب: قول علي وزيد في الجداتMlango Wa Kauli Ya 'Aliy Na Zayd (رضي الله عنهما) Kuhusu Bibi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، وَزَيْدٍ قَالَا:" إِذَا كَانَتْ الْجَدَّاتُ سَوَاءً، وَرِثَ ثَلَاثُ جَدَّاتٍ جَدَّتَا أَبِيهِ أُمُّ أُمِّهِ، وَأُمُّ أَبِيهِ، وَجَدَّةُ أُمِّهِ، فَإِنْ كَانَتْ إِحَدَاهُنَّ أَقْرَب، فَالسَّهْمُ لِذَوِي الْقُرْبَى

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy na Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنهما), wamesema: "Bibi wanapokuwa sawa (katika daraja), hurithi bibi watatu: bibi wawili wa baba yake — mama wa mama yake, na mama wa baba yake —, na bibi wa mama yake. Na ikiwa mmoja wao yuko karibu zaidi, basi fungu ni la jamaa wa karibu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1929
Hadiyth
2982

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، وَزَيْدٍ: "أَنَّهُمَا كَانَا لَا يُوَرِّثَانِ الْجِدَّةَ أُمَّ الأَبِ مَعَ الأَبِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy na Zayd [bin Thaabit] (رضي الله عنهما): "kwamba wao wawili walikuwa hawamrithishi bibi — mama wa baba — pamoja na baba."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1929
Hadiyth
2983

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ: أَنَّ عُثْمَانَ كَانَ "لَا يُوَرِّثُ الْجَدَّةَ وَابْنُهَا حَيٌّ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy: kwamba 'Uthmaan (رضي الله عنه) alikuwa "hamrithishi bibi na hali mwanawe yu hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1929
Hadiyth
2984

21-Mlangoباب: قول ابن مسعود في الجداتMlango Wa Kauli Ya Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) Kuhusu Bibi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ ابْنِ مَسْعُودٍ، قَالَ: "إِنَّ الْجَدَّاتِ لَيْسَ لَهُنَّ مِيرَاثٌ، إِنَّمَا هِيَ طُعْمَةٌ أُطْعِمْنَهَا، وَالْجَدَّاتُ أَقْرَبُهُنَّ وَأَبْعَدُهُنَّ سَوَاءٌ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه), amesema: "Hakika bibi hawana mirathi; hakika hiyo ni riziki tu waliyopewa. Na bibi — aliye karibu kati yao na aliye mbali kati yao — ni sawa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1930
Hadiyth
2985

أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، أَنْبَأَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ الْمُغِيرَةِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "تَرِثُ الْجَدَّةُ وَابْنُهَا حَيٌّ"

Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametupa khabari Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Bibi hurithi na hali mwanawe yu hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1930
Hadiyth
2986

22-Mlangoباب: قول مسروق في الجداتMlango Wa Kauli Ya Masruwq Kuhusu Bibi

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "جِئْنَ أَرْبَعُ جَدَّاتٍ يَتَسَاوَقْنَ إِلَى مَسْرُوقٍ، فَأَلْغَى أُمَّ أَبِي الْأُمِّ، وَوَرَّثَ ثَلَاثًا: جَدَّتَيْ أَبِيهِ: أُمَّ أُمِّهِ، وَأُمَّ أَبِيهِ، وَجَدَّةَ أُمِّهِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Bibi wanne walikuja kwa Masruwq wakifuatana; akamwacha (asimrithishe) mama wa baba wa mama, na akawarithisha watatu: bibi wawili wa baba yake — mama wa mama yake, na mama wa baba yake —, na bibi wa mama yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1931
Hadiyth
2987

23-Mlangoباب: قول علي وعبد الله وزيد في الردMlango Wa Kauli Ya 'Aliy, 'Abdu-Allaah [Bin Mas'uwd]
Na Zayd [Bin Thaabit] (رضي الله عنهم)
Kuhusu Ar-Radd (Kurudishiwa Ziada Ya Mali Wenye Mafungu)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ فِي ابْنَةٍ، وَابْنَةِ ابْنٍ، قَالَ: "النِّصْفُ وَالسُّدُسُ، وَمَا بَقِيَ، فَرَدٌّ عَلَى الْبِنْتِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Shariyk, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), kuhusu binti na binti wa mwana, amesema: "Nusu na sudusi; na kilichobakia, kinarudishwa kwa binti."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1932
Hadiyth
2988

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّه: "أَنَّهُ أُتِيَ فِي إِخْوَةٍ لِأُمٍّ، وَأُمٍّ، فَأَعْطَى الْإِخْوَةَ مِنَ الْأُمِّ الثُّلُثَ، وَالْأُمَّ سَائِرَ الْمَالِ، وَقَالَ: الْأُمُّ عَصَبَةُ مَنْ لَا عَصَبَةَ لَهُ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Alqamah, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه): "kwamba yeye aliletewa (mas-ala ya mirathi ya) ndugu wa mama mmoja, na mama; akawapa ndugu wa mama mmoja theluthi, na mama mali iliyobakia, na akasema: Mama ni 'asabah (mrithi anayechukua kilichobakia) wa asiye na 'asabah."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1932
Hadiyth
2989

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: سَأَلْتُ الشَّعْبِيَّ عَنْ رَجُلٍ مَاتَ وَتَرَكَ ابْنَتَهُ، لَا يُعْلَمُ وَارِثٌ غَيْرُهَا، قَالَ: "لَهَا الْمَالُ كُلُّهُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa baba yake, amesema: Nilimuuliza Ash-Sha'biy kuhusu mtu aliyefariki akamwacha binti yake, hajulikani mrithi asiyekuwa yeye. Akasema: "Mali yote ni yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1933
Hadiyth
2990

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، أَنَّ ابْنَ مَسْعُودٍ كَانَ لَا يَرُدُّ عَلَى أَخٍ لِأُمٍّ مَعَ أُمٍّ، وَلا عَلَى جَدَّةٍ، إِذَا كَانَ مَعَهَا غَيْرُهَا مِمَّنْ لَهُ فَرِيضَةٌ، وَلَا عَلَى ابْنَةِ ابْنٍ، مَعَ ابْنَةِ الصُّلْبِ، وَلَا عَلَى امْرَأَةٍ وَزَوْج وَكَانَ عَلِيٌّ "يَرُدُّ عَلَى كُلِّ ذِي سَهْمٍ، إِلَّا الْمَرْأَةَ وَالزَّوْجَ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa harudishi (ziada) kwa kaka wa mama mmoja pamoja na mama; wala kwa bibi pindi akiwa pamoja naye mwingine miongoni mwa wenye fungu (lililowekwa); wala kwa binti wa mwana pamoja na binti wa kuzaa (wa maiti mwenyewe); wala kwa mke na mume. Na 'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa "akirudisha kwa kila mwenye fungu, isipokuwa mke na mume."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1933
Hadiyth
2991

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ: أَخْبَرَنِي مُحَمَّدُ بْنُ سَالِمٍ، عَنْ خَارِجَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِت: " أَنَّهُ أُتِيَ فِي ابْنَةٍ، أَوْ أُخْت، فَأَعْطَاهَا النِّصْفَ، وَجَعَلَ مَا بَقِيَ فِي بَيْتِ الْمَالِ وَقَالَ يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ: عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ خَارِجَةَ

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Sufyaan, amesema: Amenikhabarisha Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Khaarijah bin Zayd, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه): "kwamba yeye aliletewa (mas-ala ya mirathi ya) binti au dada, akampa nusu, na akakiweka kilichobakia katika Baytul-Maal (hazina ya mali ya Waislamu)." Na Yaziyd bin Haaruwn amesema: kutoka kwa Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Khaarijah.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1933
Hadiyth
2992

24-Mlangoباب: في ميراث ابن الملاعنةMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Mtoto Wa Mwanamke
Aliyelaaniana Na Mumewe

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ فِي ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ، قَالَ: "مِيرَاثُهُ لِأُمِّهِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Ma'shar, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe), amesema: "Mirathi yake ni ya mama yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1934
Hadiyth
2993

أَخْبَرَنَا مُعَاذُ بْنُ هَانِئٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ طَهْمَانَ، قَالَ: سَمِعْتُ رَجُلًا سَأَلَ عَطَاءَ بْنَ أَبِي رَبَاحٍ عَنْ وَلَدِ الْمُتَلَاعِنَيْنِ لِمَنْ مِيرَاثُهُ؟ قَالَ:" لِأُمِّهِ وَأَهْلِهَا

Ametukhabarisha Mu'aadh bin Haaniy, ametusimulia Ibraahiym bin Twahmaan, amesema: Nilimsikia mtu mmoja akimuuliza 'Atwaa bin Abiy Rabaah kuhusu mtoto wa wanandoa waliolaaniana: mirathi yake ni ya nani? Akasema: "Ni ya mama yake na jamaa zake (mama)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1934
Hadiyth
2994

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ أَبِي سَهْلٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ قَالَ: قَالَ عَلِيٌّ فِي ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ: "تَرَكَ أَخَاهُ لِأُمِّهِ، وَأُمَّهُ لِأَخِيهِ السُّدُسُ، وَلِأُمِّهِ الثُّلُثُ، ثُمَّ يُرَدُّ عَلَيْهِمَا، فَيَصِيرُ لِلْأَخِ الثُّلُثُ، وَلِلْأُمِّ الثُّلُثَانِ". وَقَالَ ابْنُ مَسْعُودٍ: لِأَخِيهِ السُّدُسُ، وَمَا بَقِيَ فَلِلْأُمِّ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Abuw Sahl, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: 'Aliy (رضي الله عنه) amesema kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe): "(Akifa) ameacha kaka yake wa mama mmoja, na mama yake: kaka yake atapata sudusi, na mama yake atapata theluthi; kisha (kilichobakia) kinarudishwa kwao wawili, hivyo kaka anakuwa na theluthi, na mama anakuwa na theluthi mbili." Na Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) amesema: "Kaka yake atapata sudusi, na kilichobakia ni cha mama."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1934
Hadiyth
2995

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ أَبِي سَهْلٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ فِي ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ: تَرَكَ ابْنَ أَخٍ وَجَدًّا، قَالَ: "الْمَالُ لِابْنِ الْأَخِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Abuw Sahl, kutoka kwa Ash-Sha'biy kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe), ameacha mtoto wa kaka na babu; amesema: "Mali ni ya mtoto wa kaka."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1934
Hadiyth
2996

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا سَالِمُ بْنُ نُوحٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَامِرٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ فِي مِيرَاثِ ابْنِ الْمُلَاعَنَة: "لِأُمِّهِ الثُّلُثُ، وَالثُّلُثَانِ لِبَيْتِ الْمَالِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Saalim bin Nuwh, kutoka kwa 'Umar bin 'Aamir, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) kuhusu mirathi ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe): "Mama yake atapata theluthi, na theluthi mbili ni za Baytul-Maal (hazina ya mali ya Waislamu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1934
Hadiyth
2997

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا سَالِمُ بْنُ نُوحٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَامِرٍ، عَنْ حَمَّادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "مِيرَاثُهُ لِأُمِّهِ تَعْقِلُ عَنْهُ عَصَبَةُ أُمِّهِ"، وَقَالَ قَتَادَةُ، عَنْ الْحَسَنِ: لِأُمِّهِ الثُّلُثُ، وَبَقِيَّةُ الْمَالِ لِعَصَبَةِ أُمِّهِ

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Saalim bin Nuwh, kutoka kwa 'Umar bin 'Aamir, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Mirathi yake ni ya mama yake; 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa mama yake ndio watakaobeba diyah (fidia ya damu) kwa niaba yake." Na Qataadah amesema, kutoka kwa Al-Hasan: Mama yake atapata theluthi, na mali iliyobakia ni ya 'asabah wa mama yake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1936
Hadiyth
2998

أَخْبَرَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، أَخْبَرَنَا قَتَادَةُ: أَنَّ عَلِيًّا، وَابْنَ مَسْعُودٍ قَالَا فِي وَلَدِ المُلَاعَنَةٍ تَرْكُ جَدَّتِهِ وَإِخْوَتِهِ لأُمِّهِ، قَالَ: "لِلْجَدَّةِ الثُّلُثُ، وَلِلْإِخْوَةِ الثُّلُثَانِ"، وَقَالَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ: لِلْجَدَّةِ السُّدُسُ، وَلِلْإِخْوَةِ لِلْأُمِّ الثُّلُثُ، وَمَا بَقِيَ فَلِبَيْتِ الْمَالِ

Ametukhabarisha Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, ametukhabarisha Qataadah: Kwamba 'Aliy na Ibn Mas'uwd (رضي الله عنهما) walisema kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe), ameacha bibi yake na ndugu zake wa mama mmoja; amesema: "Bibi atapata theluthi, na ndugu theluthi mbili." Na Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه) amesema: Bibi atapata sudusi, na ndugu wa mama mmoja theluthi, na kilichobakia ni cha Baytul-Maal (hazina ya mali ya Waislamu).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
2999

حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، أَنْبَأَنَا يُونُسُ، وَحُمَيدٌ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "تَرِثُهُ أُمُّهُ يَعْنِي: ابْنَ الْمُلَاعَنَةِ"

Ametusimulia Hajjaaj, ametusimulia Hammaad, ametupa khabari Yuwnus na Humayd, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Mama yake atamrithi — yaani: mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3000

أَخْبَرَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ: أَنَّ النَّخَعِيَّ، وَالشَّعْبِيّ، قَالَا: "تَرِثُهُ أُمُّهُ"

Ametukhabarisha Hajjaaj, ametusimulia Hammaad, ametusimulia Hajjaaj: Kwamba An-Nakha'iy na Ash-Sha'biy walisema: "Mama yake atamrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3001

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُبَيْدِ بْنِ عُمَيْرٍ، قَالَ: كَتَبْتُ إِلَى أَخٍ لِي مِنْ بَنِي زُرَيْقٍ أَسْأَلُهُ: لِمَنْ قَضَى النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ؟ فَكَتَبَ إِلَيَّ: " أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: قَضَى بِهِ لِأُمِّهِ هِيَ بِمَنْزِلَةِ أُمِّهِ وَأَبِيهِ. وقَالَ سُفْيَانُ: الْمَالُ كُلُّهُ لِلْأُمِّ هِيَ بِمَنْزِلَةِ أَبِيهِ وَأُمِّهِ

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Ubayd bin 'Umayr, amesema: Nilimwandikia ndugu yangu mmoja wa Banuw Zurayq nikimuuliza: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu (mirathi) ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) iwe ya nani? Akaniandikia: "Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu iwe ya mama yake; yeye (mama) yuko mahali pa mama yake na baba yake (mtoto huyo)." Na Sufyaan amesema: Mali yote ni ya mama; yeye yuko mahali pa baba yake na mama yake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3002

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ فِي ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ تَرَكَ أُمَّهُ وَعَصَبَةَ أُمِّهِ، قَالَ: "الثُّلُثُ لِأُمِّهِ، وَمَا بَقِيَ فَلِعَصَبَةِ أُمِّهِ"

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe), ameacha mama yake na 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa mama yake; amesema: "Theluthi ni ya mama yake, na kilichobakia ni cha 'asabah wa mama yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3003

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ ابْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عَلِيٍّ، وَعَبْدِ اللَّهِ فِي ابْنِ الْمُلاعَنَةِ، قَالا: "عَصَبَتُهُ عَصَبَةُ أُمِّهِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Aliy na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنهما) kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe), wamesema: "'Asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wake ni 'asabah wa mama yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3004

حَدَّثَنَا أَبُو الْوَلِيدِ الْحَلَبِيُّ مُوسَى بْنُ خَالِدٍ، حَدَّثَنَا مُعْتَمِرٌ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ الْحَسَنِ، أَنَّهُ كَانَ يَقُول: "مِيرَاثُ وَلَدِ الْمُلَاعَنَةِ لِأُمِّه، قُلْتُ: فَإِنْ كَانَ لَهُ أَخٌ مِنْ أُمِّه؟ قَالَ: لَهُ السُّدُسُ"

Ametusimulia Abul-Waliyd Al-Halabiy Muwsaa bin Khaalid, ametusimulia Mu'tamir, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba alikuwa akisema: "Mirathi ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) ni ya mama yake." Nikasema: Je, akiwa ana kaka wa mama mmoja? Akasema: "Atapata sudusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3005

حَدَّثَنَا أَبُو الْمُغِيرَةِ، حَدَّثَنَا الْأَوْزَاعِيُّ، حَدَّثَنَا الزُّهْرِيُّ، قَالَ: "وَلَدُ الْمُلَاعَنَةِ لِأُمِّه، تَرِثُ فَرِيضَتَهَا مِنْهُ، وَسَائِرُ ذَلِكَ فِي بَيْتِ الْمَالِ"

Ametusimulia Abul-Mughiyrah, ametusimulia Al-Awzaa'iy, ametusimulia Az-Zuhriy, amesema: "Mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) ni wa mama yake; (mama) atarithi fungu lake (lililowekwa) kutoka kwake, na kinachobakia katika hayo ni cha Baytul-Maal (hazina ya mali ya Waislamu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3006

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ مُوسَى بْنِ عُبَيْدَةَ، عَنْ نَافِعٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "إِذَا تَلَاعَنَا، فُرِّقَ بَيْنَهُمَا وَلَمْ يَجْتَمِعَا، وَدُعِيَ الْوَلَدُ لِأُمِّهِ، يُقَالُ: ابْنُ فُلَانَةَ، هِيَ عَصَبَتُهُ يَرِثُهَا وَتَرِثُهُ، وَمَنْ دَعَاهُ لِزِنْيَةٍ، جُلِدَ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Muwsaa bin 'Ubaydah, kutoka kwa Naafi', kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Wanapolaaniana (mume na mke), hutenganishwa baina yao wala hawakusanyiki (tena), na mtoto huitwa kwa (nasaba ya) mama yake — husemwa: Mwana wa fulani (mwanamke) —; yeye (mama) ndiye 'asabah (mrithi anayechukua kilichobakia) wake: (mtoto) anamrithi (mama), naye (mama) anamrithi (mtoto). Na atakayemwita (mtoto) kuwa ni wa zinaa, atapigwa mijeledi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3007

حَدَّثَنَا مُعَاذُ بْنُ هَانِئٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ طَهْمَانَ، حَدَّثَنَا الشَّيْبَانِيُّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ فِي وَلَدِ الْمُتَلَاعِنَيْنِ: "أَنَّهُ تَرِثُهُ عَصَبَةُ أُمِّهِ، وَهُمْ يَعْقِلُونَ عَنْهُ"

Ametusimulia Mu'aadh bin Haaniy, ametusimulia Ibraahiym bin Twahmaan, ametusimulia Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy kuhusu mtoto wa wanandoa waliolaaniana: "Kwamba 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa mama yake ndio watakaomrithi, nao ndio watakaobeba diyah (fidia ya damu) kwa niaba yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3008

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، أَنْبَأَنَا هَمَّامٌ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ عَزْرَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ جُبَيْرٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ فِي وَلَدِ الْمُلَاعَنَةِ هُوَ الَّذِي لَا أَبَ لَهُ "تَرِثُهُ أُمُّهُ وَإِخْوَتُهُ مِنْ أُمِّهِ، ِوَعَصَبَةُُ أُمِّهِ، فَإِنْ قَذَفَهُ قَاذِف، جُلِدَ قَاذِفُهُ"

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, ametupa khabari Hammaam, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa 'Azrah, kutoka kwa Sa'iyd bin Jubayr, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) kuhusu mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) — naye ndiye asiye na baba —: "Mama yake atamrithi, na ndugu zake wa mama mmoja, na 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa mama yake. Na mtu akimtuhumu (kuwa ni mtoto wa zinaa), mwenye kumtuhumu atapigwa mijeledi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1937
Hadiyth
3009

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَمْزَةَ، عَنْ النُّعْمَانِ، عَنْ مَكْحُولٍ: أَنَّهُ سُئِلَ عَنْ مِيرَاثِ وَلَدِ الْمُلَاعَنَةِ لِمَنْ هُوَ؟ قَالَ: جَعَلَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لِأُمِّهِ فِي سَبَبِهِ لِمَا لَقِيَتْ مِنْ الْبَلَاءِ، وَلِإِخْوَتِهِ مِنْ أُمِّهِ، وقَالَ مَكْحُول: فَإِنْ مَاتَتْ الْأُمُّ، وَتَرَكَتْ ابْنَهَا، ثُمَّ تُوُفِّيَ ابْنُهَا الَّذِي جُعِلَ لَهَا، كَانَ مِيرَاثُهُ لِإِخْوَتِهِ مِنْ أُمِّهِ كُلُّهُ، لِأَنَّهُ كَانَ لِأُمِّهِمْ وَجَدِّهِمْ، وَكَانَ لِأَبِيهَا السُّدُسُ مِنْ ابْنِ ابْنَتِهِ، وَلَيْسَ يَرِثُ الْجَدُّ إِلَّا فِي هَذِهِ الْمَنْزِلَةِ، لِأَنَّهُ إِنَّمَا هُوَ أَبُ الْأُمِّ، وَإِنَّمَا وَرِثَ الْإِخْوَةُ مِنْ الْأُمِّ أُمَّهُمْ، وَوَرِثَ الْجَدُّ ابْنَتَهُ لِأَنَّهُ جُعِلَ لَهَا، فَالْمَالُ الَّذِي لِلْوَلَدِ لِوَرَثَةِ الْأُمِّ وَهُوَ يُحْرِزُهُ الْجَدُّ وَحْدَهُ إِذَا لَمْ يَكُنْ غَيْرُهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-Mubaarak, ametusimulia Yahyaa bin Hamzah, kutoka kwa An-Nu'maan, kutoka kwa Makhuwl, kwamba aliulizwa kuhusu mirathi ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe): ni ya nani? Akasema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliifanya iwe ya mama yake kwa sababu yake (mtoto huyo), kwa yale aliyoyapata ya balaa, na ya ndugu zake wa mama mmoja." Na Makhuwl amesema: "Mama akifariki, na akamwacha mwanawe, kisha akafariki mwanawe huyo ambaye (mirathi yake) ilifanywa kuwa ya mama, mirathi yake yote itakuwa ya ndugu zake wa mama mmoja, kwa sababu ilikuwa ni ya mama yao na babu yao; na baba yake (mama) atapata sudusi kutoka (mirathi ya) mtoto wa binti yake. Na babu harithi isipokuwa katika hali hii, kwa sababu yeye ni baba wa mama tu. Na hakika ndugu wa mama mmoja wamemrithi mama yao, na babu amemrithi binti yake, kwa sababu (mirathi ya mtoto) ilifanywa kuwa ya mama; kwa hivyo mali iliyokuwa ya mtoto ni ya warithi wa mama, naye babu huichukua yote peke yake ikiwa hakuna mwingine."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1941
Hadiyth
3010

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْعَلَاءِ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ أَبِي بُكَيْرٍ، حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ طَهْمَانَ، عَنْ سِمَاكِ بْنِ حَرْبٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ: أَنَّ قَوْمًا اخْتَصَمُوا إِلَى عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ تَعَالَى عَنْه فِي وَلَدِ الْمُتَلَاعِنَيْنِ، فَجَاءَ عَصَبَةُ أَبِيهِ يَطْلُبُونَ مِيرَاثَه، فَقَالَ: "إِنَّ أَبَاهُ كَانَ تَبَرَّأَ مِنْهُ، فَلَيْسَ لَكُمْ مِنْ مِيرَاثِهِ شَيْءٌ، فَقَضَى بِمِيرَاثِهِ لِأُمِّهِ، وَجَعَلَهَا عَصَبَتَهُ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Al-'Alaa, ametusimulia Yahyaa bin Abiy Bukayr, ametusimulia Ibraahiym bin Twahmaan, kutoka kwa Simaak bin Harb, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما): Kwamba watu fulani walipelekeana kesi kwa 'Aliy (رضي الله تعالى عنه) kuhusu mtoto wa wanandoa waliolaaniana. 'Asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa baba yake wakaja wakidai mirathi yake. Akasema: "Hakika baba yake alikuwa amejitenga naye (amemkana); kwa hivyo hamna chochote katika mirathi yake." Akahukumu mirathi yake iwe ya mama yake, na akamfanya (mama) kuwa ndiye 'asabah wake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1942
Hadiyth
3011

25-Mlangoباب: في ميراث الخنثىMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Khunthaa
(Mwenye Viungo Vya Jinsia Zote Mbili)

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ عَبْدِ الْأَعْلَى: أَنَّهُ سَمِعَ مُحَمَّدَ بْنَ عَلِيٍّ يُحَدِّثُ، عَنْ عَلِيٍّ: فِي الرَّجُلِ يَكُونُ لَهُ مَا لِلرَّجُلِ وَمَا لِلْمَرْأَةِ مِنْ أَيِّهِمَا يُوَرَّثُ، فَقَالَ: "مِنْ أَيِّهِمَا بَالَ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa 'Abdul-A'laa: Kwamba alimsikia Muhammad bin 'Aliy akisimulia kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kuhusu mtu ambaye ana kile alichonacho mwanamume na kile alichonacho mwanamke: atarithishwa kwa (hukmu ya) kipi kati ya hivyo viwili? Akasema: "Kwa kile kati ya hivyo viwili anachokojolea."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1942
Hadiyth
3012

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ شِبَاكٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ فِي الْخُنْثَى، قَالَ: "يُوَرَّثُ مِنْ قِبَلِ مَبَالِهِ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia Hushaym, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Shibaak, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kuhusu khunthaa (mwenye viungo vya jinsia zote mbili), amesema: "Atarithishwa kwa upande wa mahali anapokojolea."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1943
Hadiyth
3013

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبُو هَانِئٍ، قَالَ: سُئِلَ عَامِرٌ عَنْ مَوْلُودٍ وُلِدَ، وَلَيْسَ بِذَكَرٍ، وَلَا أُنْثَى، لَيْسَ لَهُ مَا لِلذَّكَرِ، وَلَيْسَ لَهُ مَا لِلْأُنْثَى، يُخْرِجُ مِنْ سُرَّتِهِ كَهَيْئَةِ الْبَوْلِ وَالْغَائِطِ، سُئِلَ عَنْ مِيرَاثِهِ، فَقَالَ: "نِصْفُ حَظِّ الذَّكَرِ، وَنِصْفُ حَظِّ الْأُنْثَى"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Abuw Haaniy, amesema: 'Aamir aliulizwa kuhusu mtoto aliyezaliwa naye si mwanamume wala si mwanamke: hana kile alichonacho mwanamume, wala hana kile alichonacho mwanamke; anatoa kupitia kitovu chake (kitu) kama mfano wa mkojo na kinyesi. Aliulizwa kuhusu mirathi yake, akasema: "Nusu ya fungu la mwanamume, na nusu ya fungu la mwanamke."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1943
Hadiyth
3014

26-Mlangoباب: الكلالةMlango Wa Al-Kalaalah (Asiye Na Mzazi Wala Mtoto)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا عَاصِمٌ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: سُئِلَ أَبُو بَكْرٍ عَنْ الْكَلَالَةِ، فَقَالَ: "إِنِّي سَأَقُولُ فِيهَا بِرَأْيِي، فَإِنْ كَانَ صَوَابًا فَمِنْ اللَّهِ، وَإِنْ كَانَ خَطَأً فَمِنِّي، وَمِنَ الشَّيْطَانِ: أُرَاهُ مَا خَلَا الْوَالِدَ وَالْوَلَدِ"، َفَلَمَّا اسْتُخْلِفَ عُمَرُ، قَالَ: إِنِّي لَأَسْتَحْيِي اللَّهَ أَنْ أَرُدَّ شَيْئًا قَالَهُ أَبُو بَكْرٍ

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia 'Aaswim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: Abuw Bakr (رضي الله عنه) aliulizwa kuhusu al-kalaalah (asiye na mzazi wala mtoto). Akasema: "Hakika mimi nitasema kuhusu hilo kwa rai yangu; ikiwa ni sahihi, basi ni kutoka kwa Allaah, na ikiwa ni kosa, basi ni kutoka kwangu na kutoka kwa shaytwaan: naiona kuwa ni (warithi) wasiokuwa mzazi na mtoto." Basi 'Umar (رضي الله عنه) alipofanywa Khaliyfah, alisema: "Hakika mimi namuonea hayaa Allaah kurudisha kitu alichokisema Abuw Bakr (رضي الله عنه)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1944
Hadiyth
3015

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا سَعِيدٌ هُوَ ابْنُ أَبِي أَيُّوبَ، قَالَ: حَدَّثَنِي يَزِيدُ بْنُ أَبِي حَبِيبٍ، عَنْ مَرْثَدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْيَزَنِيِّ، عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ الْجُهَنِيِّ، أَنَّهُ قَالَ: "مَا أَعْضَلَ بِأَصْحَابِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ شَيْءٌ مَا أَعْضَلَتْ بِهِمْ الْكَلَالَةُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Sa'iyd — naye ni Ibn Abiy Ayyuwb —, amesema: Amenisimulia Yaziyd bin Abiy Habiyb, kutoka kwa Marthad bin 'Abdi-Allaah Al-Yazaniy, kutoka kwa 'Uqbah bin 'Aamir Al-Juhaniy (رضي الله عنه), kwamba alisema: "Hakuna kitu kilichowatatiza Swahaba (رضي الله عنهم) wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kama ilivyowatatiza al-kalaalah (asiye na mzazi wala mtoto)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1944
Hadiyth
3016

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ مُحَمَّدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "الْكَلَالَةُ مَا خَلَا الْوَالِدَ وَالْوَلَدَ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa Al-Hasan bin Muhammad, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Al-kalaalah (asiye na mzazi wala mtoto) ni (warithi) wasiokuwa mzazi na mtoto."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1944
Hadiyth
3017

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدٌ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يَعْلَى بْنِ عَطَاءٍ، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ سَعْدٍ: "أَنَّهُ كَانَ يَقْرَأُ هَذِهِ الْآيَةَ: {وَإِنْ كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلالَةً أَو امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ} قَالَ سَعْدٌ: لِأُمٍّ"

Ametukhabarisha Muhammad, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ya'laa bin 'Atwaa, kutoka kwa Al-Qaasim bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Sa'd [bin Abiy Waqqaasw] (رضي الله عنه): Kwamba alikuwa akiisoma Aayah hii:

وَإِنْ كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلالَةً أَو امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ

Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada [An-Nisaa (4:12)]

Sa'd (رضي الله عنه) amesema: (Kaka au dada) wa (upande wa) mama.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1944
Hadiyth
3018

27-Mlangoباب: في ميراث ذوي الأرحامMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Dhawil-Arhaam
(Jamaa Wa Uzazi Wasio Na Fungu Maalumu Wala Si 'Asabah)

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، حَدَّثَنَا أَبُو الْأَسْوَدِ مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ نَوْفَلٍ: أَنَّ عَاصِمَ بْنَ عُمَرَ بْنِ قَتَادَةَ الْأَنْصَارِيَّ أَخْبَرَهُ: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ "الْتَمَسَ مَنْ يَرِثُ ابْنَ الدَّحْدَاحَةِ، فَلَمْ يَجِدْ وَارِثًا، فَدَفَعَ مَالَ ابْنِ الدَّحْدَاحَةِ إِلَى أَخْوَالِ ابْنِ الدَّحْدَاحَةِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, ametusimulia Abul-Aswad Muhammad bin 'Abdir-Rahmaan bin Nawfal: Kwamba 'Aaswim bin 'Umar bin Qataadah Al-Answaariy alimkhabarisha: Kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) "alimtafuta anayemrithi Ibn Ad-Dahdaahah (رضي الله عنه), hakupata mrithi; akaipeleka mali ya Ibn Ad-Dahdaahah (رضي الله عنه) kwa wajomba wa Ibn Ad-Dahdaahah (رضي الله عنه)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1946
Hadiyth
3019

أَخْبَرَنَا أَبُو عَاصِمٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ مُسْلِمٍ، عَنْ طَاوُسٍ، عَنْ عَائِشَةَ، قَالَتْ: "اللَّهُ وَرَسُولُهُ مَوْلَى مَنْ لَا مَوْلَى لَهُ، وَالْخَالُ وَارِثُ مَنْ لَا وَارِثَ لَهُ"

Ametukhabarisha Abuw 'Aaswim, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Amr bin Muslim, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa 'Aaishah (رضي الله عنها), amesema: "Allaah na Rasuli Wake ni mawlaa (msimamizi) wa asiye na mawlaa, na mjomba ni mrithi wa asiye na mrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1946
Hadiyth
3020

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ فِرَاسٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ زِيَادٍ، قَالَ: "أُتِيَ عُمَرُ فِي عَمٍّ لِأُمٍّ، وَخَالَة، فَأَعْطَى الْعَمَّ لِلْأُمِّ الثُّلُثَيْنِ، وَأَعْطَى الْخَالَةَ الثُّلُثَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Firaas, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Ziyaad, amesema: "'Umar (رضي الله عنه) aliletewa (kesi ya mirathi ya) ami (kaka wa baba) wa mama mmoja na dada wa mama; akampa ami wa mama mmoja theluthi mbili, na akampa dada wa mama theluthi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1946
Hadiyth
3021

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ يُونُسَ، عَنِ الْحَسَنِ: أَنَّ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ "أَعْطَى الْخَالَةَ الثُّلُثَ، وَالْعَمَّةَ الثُّلُثَيْنِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan: Kwamba 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) "alimpa dada wa mama theluthi, na shangazi theluthi mbili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1947
Hadiyth
3022

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ عَمْرٍو، عَنْ غَالِبِ بْنِ عَبَّادٍ، عَنْ قَيْسِ بْنِ حَبْتَرٍ النَّهْشَلِيِّ، قَالَ: أُتِيَ عَبْدُ الْمَلِكِ بْنُ مَرْوَانَ فِي خَالَةٍ وَعَمَّةٍ، فَقَامَ شَيْخٌ، فَقَالَ: شَهِدْتُ عُمَرَ بْنَ الْخَطَّابِ "أَعْطَى الْخَالَةَ الثُّلُثَ، وَالْعَمَّةَ الثُّلُثَيْنِ"، قَالَ: فَهَمَّ أَنْ يَكْتُبَ بِهِ، ثُمَّ قَالَ: أَيْنَ زَيْدٌ عَنْ هَذَا

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Al-Hasan bin 'Amr, kutoka kwa Ghaalib bin 'Abbaad, kutoka kwa Qays bin Habtar An-Nahshaliy, amesema: 'Abdul-Malik bin Marwaan aliletewa (kesi ya mirathi ya) dada wa mama na shangazi. Mzee mmoja akasimama, akasema: Nilimshuhudia 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) "akimpa dada wa mama theluthi, na shangazi theluthi mbili." Akasema: Akakusudia kuliandika (liwe hukmu); kisha akasema: Zayd (رضي الله عنه) yuko wapi kuhusu hili?

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1948
Hadiyth
3023

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ مَسْرُوقٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ قَالَ: "الْخَالَةُ بِمَنْزِلَةِ الْأُمِّ، وَالْعَمَّةُ بِمَنْزِلَةِ الْأَبِ، وَبِنْتُ الْأَخِ بِمَنْزِلَةِ الْأَخِ، وَكُلُّ ذِي رَحِمٍ بِمَنْزِلَةِ رَحِمِهِ الَّتِي يُدْلِي بِهَا إِذَا لَمْ يَكُنْ وَارِثٌ ذُو قَرَابَةٍ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Masruwq, kutoka kwa 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), amesema: "Dada wa mama yuko katika daraja ya mama, na shangazi yuko katika daraja ya baba, na binti wa kaka yuko katika daraja ya kaka; na kila mwenye ujamaa wa uzazi yuko katika daraja ya jamaa wake ambaye kupitia kwake ameungana (na maiti), ikiwa hakuna mrithi mwenye ukaribu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1948
Hadiyth
3024

28-Mlangoباب: العصبةMlango Wa Al-'Asabah (Warithi Wanaochukua Kilichobakia
Baada Ya Wenye Mafungu)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا هِشَامٌ، عَنْ مُحَمَّدٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، قَالَ: حَدَّثَنِي الضَّحَّاكُ بْنُ قَيْسٍ: أَنَّ عُمَرَ قَضَى فِي أَهْلِ طَاعُونِ عَمَوَاسَ أَنَّهُمْ كَانُوا إِذَا كَانُوا مِنْ قِبَلِ الْأَبِ سَوَاءً، فَبَنُو الْأُمِّ أَحَقُّ، وَإِذَا كَانَ بَعْضُهُمْ أَقْرَبَ مِنْ بَعْضٍ بِأَبٍ، فَهُمْ أَحَقُّ بِالْمَالِ "

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Hishaam, kutoka kwa Muhammad, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Utbah, amesema: Amenisimulia Adhw-Dhwahhaak bin Qays (رضي الله عنه): "Kwamba 'Umar (رضي الله عنه) alihukumu kuhusu watu wa tauni ya 'Amawaas, kwamba wao, walipokuwa sawa upande wa baba, basi wana wa mama (mmoja) ndio wenye haki zaidi; na baadhi yao walipokuwa karibu zaidi kuliko wengine kwa baba, basi wao ndio wenye haki zaidi ya mali."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3025

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، حَدَّثَنِي أَبُو إِسْحَاق الشَّيْبَانِيُّ، عَنْ عُبَيْدِ بْنِ أَبِي الْجَعْدِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ شَدَّادِ بْنِ الْهَادِ، قَالَ: أُصِيبَ سَالِمٌ مَوْلَى أَبِي حُذَيْفَةَ يَوْمَ الْيَمَامَة، فَبَلَغَ مِيرَاثُهُ مِائَتَيْ دِرْهَمٍ، فَقَالَ عُمَرُ: "احْبِسُوهَا عَلَى أُمِّهِ حَتَّى تَأْتِيَ عَلَى آخِرِهَا"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, amenisimulia Abuw Is-haaq Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa 'Ubayd bin Abil-Ja'd, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Shaddaad bin Al-Haad, amesema: Saalim (رضي الله عنه) mawlaa (mwachwa huru) wa Abuw Hudhayfah (رضي الله عنه) aliuawa siku ya (vita vya) Al-Yamaamah, na mirathi yake ikafikia dirhamu mia mbili. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Zizuieni kwa ajili ya mama yake mpaka azitumie hadi mwisho wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3026

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الْحَارِثِ، عَنْ عَلِيٍّ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْإِخْوَةُ مِنْ الْأُمِّ يَتَوَارَثُونَ دُونَ بَنِي الْعَلَّاتِ، يَرِثُ الرَّجُلُ أَخَاهُ لِأَبِيهِ وَأُمِّهِ، دُونَ أَخِيهِ لِأَبِيهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa Al-Haarith, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Ndugu wa mama mmoja hurithiana, si wana wa wake wenza (ndugu wa baba mmoja); mtu humrithi kaka yake wa baba yake na mama yake, si kaka yake wa baba mmoja."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3027

حَدَّثَنَا سَهْلُ بْنُ حَمَّادٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ النُّعْمَانِ بْنِ سَالِمٍ، قَالَ: قُلْتُ لِابْنِ عُمَرَ: "أَرَأَيْتَ رَجُلًا تَرَكَ ابْنَ ابْنَتِهِ، أَيَرِثُهُ؟ قَالَ: لا"

Ametusimulia Sahl bin Hammaad, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa An-Nu'maan bin Saalim, amesema: Nilimwambia Ibn 'Umar (رضي الله عنهما): Unaonaje mtu aliyeacha mtoto wa binti yake, je, atamrithi? Akasema: "Hapana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3028

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا الْأَعْمَشُ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "الْأُمُّ عَصَبَةُ مَنْ لَا عَصَبَةَ لَهُ، وَالْأُخْتُ عَصَبَةُ مَنْ لَا عَصَبَةَ لَهُ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Mama ni 'asabah (mrithi anayechukua kilichobakia) wa asiye na 'asabah, na dada ni 'asabah wa asiye na 'asabah."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3029

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا ابْنُ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "أَلْحِقُوا الْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِي، فَهُوَ لِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Wapeni wenye mafungu (yaliyowekwa) mafungu yao; na kinachobakia ni cha mwanamume aliye karibu zaidi (kwa maiti)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1949
Hadiyth
3030

29-Mlangoباب: في ميراث أهل الشرك وأهل الإسلامMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Watu Wa Shirki Na Watu Wa Islaam

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى: أَنَّ سُلَيْمَانَ بْنَ يَسَارٍ أَخْبَرَهُ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْأَشْعَثِ: أَنَّ عَمَّةً لَهُ تُوُفِّيَتْ يَهُودِيَّةً بِالْيَمَنِ، فَذَكَرَ ذَلِكَ لِعُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ فَقَالَ: "يَرِثُهَا أَقْرَبُ النَّاسِ إِلَيْهَا مِنْ أَهْلِ دِينِهَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Yahyaa: Kwamba Sulaymaan bin Yasaar alimkhabarisha, kutoka kwa Muhammad bin Al-Ash'ath: Kwamba shangazi yake mmoja alifariki akiwa Myahudi huko Yemen. Akamtajia hilo 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه), akasema: "Atamrithi aliye karibu zaidi naye miongoni mwa watu wa dini yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1951
Hadiyth
3031

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ قَيْسِ بْنِ مُسْلِمٍ، عَنْ طَارِقِ بْنِ شِهَابٍ، قَالَ: مَاتَتْ عَمَّةُ الْأَشْعَثِ بْنِ قَيْسٍ وَهِيَ يَهُودِيَّة، فَأَتَى عُمَرَ بْنَ الْخَطَّاب، فَقَالَ: "أَهْلُ دِينِهَا يَرِثُونَهَا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Qays bin Muslim, kutoka kwa Twaariq bin Shihaab (رضي الله عنه), amesema: Shangazi wa Al-Ash'ath bin Qays (رضي الله عنه) alifariki naye ni Myahudi. Akamwendea 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه), akasema: "Watu wa dini yake ndio watakaomrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1951
Hadiyth
3032

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ حَمَّادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: "أَهْلُ الشِّرْكِ لَا نَرِثُهُمْ، وَلَا يَرِثُونَا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: "Watu wa shirki hatuwarithi, wala wao hawaturithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1951
Hadiyth
3033

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ عِيسَى الْحَنَّاطِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: "أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَأَبَا بَكْرٍ، وَعُمَرَ، قَالُوا: لَا يَتَوَارَثُ أَهْلُ دِينَيْنِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa 'Iysaa Al-Hannaatw, kutoka kwa Ash-Sha'biy: Kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), na Abuw Bakr na 'Umar (رضي الله عنهما), walisema: "Watu wa dini mbili hawarithiani."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1951
Hadiyth
3034

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عُمَرَ، قَالَ: "لَا يَتَوَارَثُ أَهْلُ مِلَّتَيْنِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه), amesema: "Watu wa mila mbili hawarithiani."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1951
Hadiyth
3035

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الْأَشْعَثِ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "لَا نَرِثُ أَهْلَ الْكِتَابِ وَلَا يَرِثُونَا، إِلَّا أَنْ يَمُوتَ لِلرَّجُلِ عَبْدُهُ أَوْ أَمَتُهُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Sisi hatuwarithi Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu: Mayahudi na Manaswara), wala wao hawaturithi, isipokuwa mtu akifiwa na mtumwa wake au mjakazi wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1953
Hadiyth
3036

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ الْأَشْعَثِ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا نَرِثُ أَهْلَ الْكِتَابِ وَلَا يَرِثُونَا، إِلَّا الرَّجُلُ يَرِثُ عَبْدَهُ، أَوْ أَمَتَهُ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Sisi hatuwarithi Ahlul-Kitaab (Watu wa Kitabu: Mayahudi na Manaswara), wala wao hawaturithi, isipokuwa mtu humrithi mtumwa wake au mjakazi wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1954
Hadiyth
3037

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ: " كَانَ مُعَاوِيَةُ يُوَرِّثُ الْمُسْلِمَ مِنْ الْكَافِرِ، وَلَا يُوَرِّثُ الْكَافِرَ مِنْ الْمُسْلِمِ، قَالَ: قَالَ مَسْرُوقٌ: وَمَا حَدَثَ فِي الْإِسْلَامِ قَضَاءٌ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْهُ، قِيلَ لِأَبِي مُحَمَّدٍ: تَقُولُ بِهَذَا؟ قَالَ: لا

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Masruwq, amesema: "Mu'aawiyah (رضي الله عنه) alikuwa akimrithisha Muislamu kutoka kwa kafiri, wala hamrithishi kafiri kutoka kwa Muislamu." Akasema: Masruwq amesema: "Na haujazuka katika Islaam uamuzi unaopendeza zaidi kwangu kuliko huo."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] aliulizwa: Je, wewe unasema hivi (unafuata kauli hii)? Akasema: Hapana.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1954
Hadiyth
3038

حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، عَنْ دَاوُدَ بْنِ أَبِي هِنْدٍ، عَنْ عَامِرٍ: أَنَّ الْمُعْزِلَةَ بِنْتَ الْحَارِثِ تُوُفِّيَتْ بِالْيَمَنِ وَهِيَ يَهُودِيَّةٌ، فَرَكِبَ الْأَشْعَثُ بْنُ قَيْسٍ، وَكَانَتْ عَمَّتَهُ، إِلَى عُمَرَ فِي مِيرَاثِهَا، فَقَالَ عُمَرُ: "لَيْسَ ذَاكَ لَكَ، يَرِثُهَا أَقْرَبُ النَّاسِ مِنْهَا مِنْ أَهْلِ دِينِهَا، لَا يَتَوَارَثُ مِلَّتَانِ"

Ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, kutoka kwa Daawuwd bin Abiy Hind, kutoka kwa 'Aamir: Kwamba Al-Mu'zilah bint Al-Haarith alifariki huko Yemen naye ni Myahudi. Al-Ash'ath bin Qays (رضي الله عنه) — naye (Al-Mu'zilah) alikuwa shangazi yake — akapanda (kipando chake) kwenda kwa 'Umar (رضي الله عنه) kuhusu mirathi yake. 'Umar (رضي الله عنه) akasema: "Hilo si lako; atamrithi aliye karibu zaidi naye miongoni mwa watu wa dini yake. Mila mbili hazirithiani."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1954
Hadiyth
3039

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا أَنَسُ بْنُ سِيرِينَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: "لَا يَتَوَارَثُ مِلَّتَانِ شَتَّى، وَلَا يَحْجُبُ مَنْ لَا يَرِثُ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Zayd, ametusimulia Anas bin Siyriyn, amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) amesema: "Mila mbili tofauti hazirithiani, wala asiyerithi hamzuilii (mrithi mwingine fungu lake)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1955
Hadiyth
3040

حَدَّثَنَا نَصْرُ بْنُ عَلِيٍّ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْأَعْلَى، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا يَرِثُ الْمُسْلِمُ الْكَافِرَ، وَلَا الْكَافِرُ الْمُسْلِمَ"

Ametusimulia Naswr bin 'Aliy, ametusimulia 'Abdul-A'laa, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Aliy bin Husayn, kutoka kwa 'Amr bin 'Uthmaan, kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Muislamu hamrithi kafiri, wala kafiri hamrithi Muislamu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1955
Hadiyth
3041

حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "إِذَا مَاتَ الْمَيِّتُ وَجَبَتْ الْحُقُوقُ لِأَهْلِهَا، وَلَمْ يَجْعَلْ لِمَنْ أَسْلَمَ أَوْ أُعْتِقَ قَبْلَ أَنْ يُقْسَمَ الْمِيرَاثُ شَيْئًا"

Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Ma'shar, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Maiti anapokufa, haki (za mirathi) huwa wajibu kwa wenye kuzistahiki; na hakumfanyia chochote aliyesilimu au aliyeachwa huru kabla ya mirathi kugawanywa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1955
Hadiyth
3042

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عِيسَى، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَرِثُ الْمُسْلِمُ الْكَافِرَ، وَلَا الْكَافِرُ الْمُسْلِمَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Iysaa, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Aliy bin Husayn, kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Muislamu hamrithi kafiri, wala kafiri hamrithi Muislamu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1956
Hadiyth
3043

حَدَّثَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ حُسَيْنٍ، عَنْ عَمْرِو بْنِ عُثْمَانَ، عَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "لَا يَرِثُ الْمُسْلِمُ الْكَافِرَ، وَلَا الْكَافِرُ الْمُسْلِمَ"

Ametusimulia 'Amr bin 'Awn, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Aliy bin Husayn, kutoka kwa 'Amr bin 'Uthmaan, kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رضي الله عنهما), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Muislamu hamrithi kafiri, wala kafiri hamrithi Muislamu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1956
Hadiyth
3044

30-Mlangoباب: المكاتبMlango Wa Mukaatab (Mtumwa Aliyeandikiana
Na Bwana Wake Kujikomboa Kwa Malipo)

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَيْسَ لِلْمُكَاتَبِ مِيرَاثٌ، مَا بَقِيَ عَلَيْهِ شَيْءٌ مِنْ مُكَاتَبَتِهِ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo) hana mirathi, maadamu kimebaki juu yake kitu chochote katika (malipo ya) mkataba wake (wa kujikomboa)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1956
Hadiyth
3045

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءٍ: "فِي رَجُلٍ لَهُ بَنُونَ قَدْ أَعْتَقَ مِنْ بَعْضِهِمْ النِّصْفَ، وَمِنْ بَعْضِهِمْ الثُّلُثَ، وَمِنْ بَعْضٍ الرُّبُعَ، قَالَ: لَا يَرِثُونَ حَتَّى يُعْتَقُوا"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa: "Kuhusu mtu mwenye wana, (ambao) amewaacha huru baadhi yao nusu, na baadhi yao theluthi, na baadhi robo; amesema: Hawarithi mpaka waachwe huru (kikamilifu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1957
Hadiyth
3046

حَدَّثَنَا عبد الله بن جعفر الرقي، وَسَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ حَمَّادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: "فِي رَجُلٍ اشْتَرَى ابْنَهُ فِي مَرَضِهِ، قَالَ: إِنْ خَرَجَ مِنْ الثُّلُثِ وَرِثَهُ، وَإِنْ وَقَعَتْ عَلَيْهِ السِّعَايَةُ لَمْ يَرِثْ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Ja'far Ar-Raqqiy na Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym: "Kuhusu mtu aliyemnunua mwanawe katika maradhi yake (ya kufa); amesema: Ikiwa (thamani yake) itatoka katika theluthi (ya mali), atamrithi; na ikiwa italazimika juu yake si'aayah (kujifanyia kazi ili alipe thamani iliyobaki ya uhuru wake), hatarithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1957
Hadiyth
3047

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "حَدُّ الْمُكَاتَبِ حَدُّ الْمَمْلُوكِ، حَتَّى يُعْتَقَ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah) ya mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo) ni hadd ya mtumwa, mpaka aachwe huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1957
Hadiyth
3048

31-Mlangoباب: الولاءMlango Wa Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "الْمَوْلَى أَخٌ فِي الدِّينِ وَنِعْمَةٌ، وَأَحَقُّ النَّاسِ بِمِيرَاثِهِ أَقْرَبُهُمْ مِنْ الْمُعْتِقِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Sa'iyd bin 'Abdir-Rahmaan, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mwachwa huru ni ndugu katika Dini na neema (ya bwana wake), na mwenye haki zaidi kati ya watu kwa mirathi yake ni aliye karibu zaidi miongoni mwao na aliyemwacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1958
Hadiyth
3049

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، حدثنا مَنْصُورٌ، عَنْ الْحَسَنِ، وَمُحَمَّدُ بْنُ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ فِي رَجُلٍ أَعْتَقَ مَمْلُوكًا، ثُمَّ مَاتَ الْمَوْلَى وَالْمَمْلُوكُ، وَتَرَكَ الْمُعْتِقُ أَبَاهُ وَابْنَهُ، قَالَا: "الْمَالُ لِلِابْنِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hushaym, ametusimulia Manswuwr, kutoka kwa Al-Hasan; na Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kuhusu mtu aliyemwacha huru mtumwa, kisha bwana (aliyeacha huru) na mtumwa (aliyeachwa huru) wakafa, na aliyeacha huru akaacha baba yake na mwanawe; (wote) wawili wamesema: "Mali ni ya mwana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1958
Hadiyth
3050

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبَّادٌ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَامِرٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ فِي رَجُلٍ تَرَكَ أَبَاهُ وَابْنَ ابْنِهِ، فَقَالَ: "الْوَلَاءُ لِابْنِ الِابْنِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abbaad, kutoka kwa 'Umar bin 'Aamir, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), kuhusu mtu aliyeacha baba yake na mwana wa mwanawe; akasema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa mwana wa mwana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1959
Hadiyth
3051

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا مُعَمَّرٌ، حَدَّثَنَا خُصَيْفٌ، عَنْ زِيَادِ بْنِ أَبِي مَرْيَمَ: أَنَّ امْرَأَةً أَعْتَقَتْ عَبْدًا لَهَا، ثُمَّ تُوُفِّيَتْ وَتَرَكَتْ ابْنَهَا وَأَخَاهَا، ثُمَّ تُوُفِّيَ مَوْلَاهَا، فَأَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ابْنُ الْمَرْأَةِ وَأَخُوهَا فِي مِيرَاثِهِ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "مِيرَاثُهُ لِابْنِ الْمَرْأَةِ، فَقَالَ أَخُوهَا: يَا رَسُولَ اللَّه، ِلَوْ أَنَّهُ جَرَّ جَرِيرَةً، عَلَى مَنْ كَانَتْ؟ قَالَ: عَلَيْكَ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Mu'ammar, ametusimulia Khuswayf, kutoka kwa Ziyaad bin Abiy Maryam: Kwamba mwanamke mmoja alimwacha huru mtumwa wake, kisha akafariki, na akaacha mwanawe na kaka yake; kisha mwachwa huru wake akafariki. Mwana wa yule mwanamke na kaka yake wakamjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kuhusu mirathi yake. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Mirathi yake ni ya mwana wa mwanamke." Kaka yake akasema: Yaa Rasula-Allaah, lau (mwachwa huru huyo) angefanya kosa (la jinai), (fidia yake) ingekuwa juu ya nani? Akasema: "Juu yako."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1959
Hadiyth
3052

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أَخْبَرَنَا مُغِيرَةُ، قَالَ: سَأَلْتُ إِبْرَاهِيمَ "عَنْ رَجُلٍ أَعْتَقَ مَمْلُوكًا لَهُ، فَمَاتَ وَمَاتَ الْمَوْلَى، وَتَرَكَ الْمُعْتِقُ أَبَاهُ وَابْنَهُ، فَقَالَ لِأَبِيهِ: كَذَا، وَمَا بَقِيَ فَلِابْنِهِ"

Ametusimulia Muhammad bin As-Swalt, ametusimulia Hushaym, ametukhabarisha Mughiyrah, amesema: Nilimuuliza Ibraahiym "kuhusu mtu aliyemwacha huru mtumwa wake, kisha (bwana) akafa, na mwachwa huru akafa, na aliyeacha huru akaacha baba yake na mwanawe. Akasema: Baba yake (apewe) kadhaa, na kinachobakia ni cha mwanawe."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1959
Hadiyth
3053

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الصَّلْتِ، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ شُعْبَةَ قَالَ: سَمِعْتُ الْحَكَمَ، وَحَمَّادًا، يَقُولَانِ: "هُوَ لِلِابْنِ"

Ametusimulia Muhammad bin As-Swalt, ametusimulia Hushaym, kutoka kwa Shu'bah, amesema: Nilimsikia Al-Hakam na Hammaad wakisema: "Ni (mirathi) ya mwana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1959
Hadiyth
3054

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الْحَسَن ": أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ " خَرَجَ إِلَى الْبَقِيعِ، فَرَأَى رَجُلًا يُبَاعُ، فَأَتَاهُ فَسَاوَمَ بِهِ، ثُمَّ تَرَكَهُ فَرَآهُ رَجُلٌ فَاشْتَرَاهُ فَأَعْتَقَهُ، ثُمَّ جَاءَ بِهِ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنِّي اشْتَرَيْتُ هَذَا فَأَعْتَقْتُهُ، فَمَا تَرَى فِيهِ؟ فَقَالَ: هُوَ أَخُوكَ وَمَوْلَاكَ، قَالَ: مَا تَرَى فِي صُحْبَتِهِ؟ فَقَالَ: إِنْ شَكَرَكَ فَهُوَ خَيْرٌ لَهُ وَشَرٌّ لَكَ، وَإِنْ كَفَرَكَ فَهُوَ خَيْرٌ لَكَ وَشَرٌّ لَهُ، قَالَ: مَا تَرَى فِي مَالِهِ؟ قَالَ: إِنْ مَاتَ وَلَمْ يَتْرُكْ عَصَبَةً فَأَنْتَ وَارِثُهُ "

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan: Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alitoka kwenda Al-Baqiy', akamwona mtu (mtumwa) anauzwa; akamwendea akapatana bei yake, kisha akamwacha. Mtu mmoja akamwona, akamnunua na akamwacha huru, kisha akamleta kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), akasema: Hakika mimi nimemnunua huyu na nimemwacha huru; basi unaonaje kuhusu yeye? Akasema: "Yeye ni ndugu yako na mwachwa huru wako." Akasema: Unaonaje kuhusu kusuhubiana naye? Akasema: "Akikushukuru, basi ni kheri kwake na shari kwako; na akikanusha (wema wako), basi ni kheri kwako na shari kwake." Akasema: Unaonaje kuhusu mali yake? Akasema: "Akifa na hakuacha 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba), basi wewe ndiye mrithi wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1960
Hadiyth
3055

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا أَشْعَثُ، عَنْ الْحَكَمِ، وَسَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ شَدَّادٍ: أَنَّ ابْنَةَ حَمْزَةَ أَعْتَقَتْ عَبْدًا لَهَا، فَمَاتَ وَتَرَكَ ابْنَتَهُ وَمَوْلَاتَهُ بِنْتَ حَمْزَةَ، "فَقَسَمَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِيرَاثَهُ بَيْنَ ابْنَتِهِ وَمَوْلَاتِهِ بِنْتِ حَمْزَةَ نِصْفَيْنِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Ash'ath, kutoka kwa Al-Hakam na Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Shaddaad: Kwamba binti ya Hamzah رضي الله عنه رضي الله عنها alimwacha huru mtumwa wake; (mtumwa huyo) akafa, na akaacha binti yake na bibi yake (aliyemwacha huru), binti ya Hamzah رضي الله عنه رضي الله عنها. "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akagawa mirathi yake baina ya binti yake na bibi yake (aliyemwacha huru), binti ya Hamzah رضي الله عنه رضي الله عنها, nusu kwa nusu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3056

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ شَمُوسَ الْكِنْدِيَّةِ، قَالَتْ: "قَاضَيْتُ إِلَى عَلِيٍّ فِي أَبٍ مَاتَ لَمْ يَدَعْ أَحَدًا غَيْرِي، وَمَوْلَاهُ، فَأَعْطَانِي النِّصْفَ، َوَأَعْطَى مَوْلَاهُ النِّصْفَ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Shamuws Al-Kindiyyah, amesema: "Nilipeleka kesi kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kuhusu baba (yangu) aliyefariki, hakuacha yeyote isipokuwa mimi na bwana wake (aliyemwacha huru). Akanipa nusu, na akampa bwana wake nusu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3057

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ ابْنِ أَبِي لَيْلَى، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ أَبِي الْكَنُودِ، عَنْ عَلِيٍّ: " أَنَّهُ أُتِيَ بِابْنَةٍ وَمَوْلًى، فَأَعْطَى الِابْنَةَ النِّصْفَ، وَالْمَوْلَى النِّصْفَ، قَالَ الْحَكَمُ: فَمَنْزِلِي هَذَا نَصِيبُ الْمَوْلَى الَّذِي وَرِثَهُ عَنْ مَوْلَاهُ

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Abul-Kanuwd, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه): "Kwamba aliletewa (kesi ya) binti na bwana (aliyemwacha huru maiti); akampa binti nusu, na bwana nusu." Al-Hakam amesema: Basi nyumba yangu hii ni fungu la bwana yule alilolirithi kutoka kwa mwachwa huru wake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3058

أَخْبَرَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، عَنْ ابْنِ إِدْرِيسَ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ مُدْلِجٍ: أَنَّهُ مَاتَ وَتَرَكَ ابْنَتَهُ وَمَوَالِيَهُ، فَأَعْطَى عَلِيٌّ ابْنَتَهُ النِّصْفَ وَمَوَالِيَهُ النِّصْفَ "

Ametukhabarisha Ibraahiym bin Muwsaa, kutoka kwa Ibn Idriys, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin Mudlij: Kwamba (mtu) alifariki, na akaacha binti yake na mabwana zake (waliomwacha huru); "'Aliy (رضي الله عنه) akampa binti yake nusu, na mabwana zake nusu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3059

حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ، عَنْ ابْنِ إِدْرِيسَ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ الشَّمُّوسِ: "أَنَّ أَبَاهَا مَاتَ، فَجَعَلَ عَلِيٌّ لَهَا النِّصْفَ وَلِمَوَالِيهِ النِّصْفَ"

Ametusimulia Ibraahiym, kutoka kwa Ibn Idriys, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ash-Shammuws: "Kwamba baba yake alifariki, 'Aliy (رضي الله عنه) akamfanyia (yeye) nusu, na mabwana zake (baba yake waliomwacha huru) nusu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3060

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا حَفْصُ بْنُ غِيَاثٍ، حَدَّثَنَا أَشْعَثُ، عَنْ جَهْمِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: أَنَّهُ "سُئِلَ عَنْ أُخْتَيْنِ اشْتَرَتْ إِحْدَاهُمَا أَبَاهَا فَأَعْتَقَتْهُ، ثُمَّ مَاتَ، قَالَ لَهُمَا: الثُّلُثَانِ فَرِيضَتُهُمَا فِي كِتَابِ اللَّهِ، وَمَا بَقِيَ فَلِلْمُعْتِقَةِ دُونَ الْأُخْرَى"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hafsw bin Ghiyaath, ametusimulia Ash'ath, kutoka kwa Jahm bin Diynaar, kutoka kwa Ibraahiym: Kwamba "aliulizwa kuhusu dada wawili, mmoja wao alimnunua baba yao akamwacha huru, kisha (baba) akafa. Akasema: (Dada) wawili wana theluthi mbili, (ndilo) fungu lao la faradhi katika Kitabu cha Allaah, na kinachobakia ni cha yule aliyemwacha huru, si yule mwingine."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1961
Hadiyth
3061

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، حَدَّثَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: "فِي امْرَأَةٍ أَعْتَقَتْ أَبَاهَا، فَمَاتَ الْأَبُ وَتَرَكَ أَرْبَعَ بَنَاتٍ هِيَ إِحْدَاهُنَّ، قَالَ: لَيْسَ عَلَيْهِ مِنَّةٌ، لَهُنَّ الثُّلُثَانِ، وَهِيَ مَعَهُنَّ"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Israaiyl, ametusimulia Al-Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy: "Kuhusu mwanamke aliyemwacha huru baba yake, kisha baba akafa na akaacha mabinti wanne, yeye akiwa mmoja wao; amesema: Hakuna juu yake (baba) fadhila (ya kuachwa huru inayompa yeye zaidi); wao wana theluthi mbili, naye yuko pamoja nao."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1964
Hadiyth
3062

32-Mlangoباب: فيمن أعطى ذوي الأرحام دون المواليMlango Wa Kuhusu Aliyewapa Dhawil-Arhaam
(Jamaa Wa Uzazi Wasio Na Fungu Maalumu Wala
Si 'Asabah) Badala Ya Mabwana Walioacha Huru

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ حَيَّانَ بْنِ سَلْمَانَ، قَالَ: كُنْتُ عِنْدَ سُوَيْدِ بْنِ غَفَلَةَ، فَجَاءَهُ رَجُلٌ، فَسَأَلَهُ عَنْ "فَرِيضَةِ رَجُلٍ تَرَكَ ابْنَتَهُ وَامْرَأَتَه، فَقَالَ: أَنَا أُنْبِئُكَ قَضَاءَ عَلِيٍّ، قَالَ: حَسْبِي قَضَاءُ عَلِيٍّ، قَالَ: قَضَى عَلِيٌّ لِامْرَأَتِهِ الثُّمُنَ، وَلِابْنَتِهِ النِّصْفَ، ثُمَّ رَدَّ الْبَقِيَّةَ عَلَى ابْنَتِهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Hayyaan bin Salmaan, amesema: Nilikuwa kwa Suwayd bin Ghafalah; mtu mmoja akamjia, akamuuliza kuhusu "mas-ala ya mirathi ya mtu aliyeacha binti yake na mke wake. Akasema: Nitakukhabarisha hukmu ya 'Aliy (رضي الله عنه). Akasema: Hukmu ya 'Aliy (رضي الله عنه) inanitosha. Akasema: 'Aliy (رضي الله عنه) aliamua mke wake apate thumni, na binti yake nusu, kisha akarudisha kilichobakia kwa binti yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1965
Hadiyth
3063

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ أَبِي الْهَيْثَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: أَنَّ مَوْلَاةً لِإِبْرَاهِيمَ تُوُفِّيَتْ وَتَرَكَتْ مَالًا، فَقُلْتُ لِإِبْرَاهِيمَ، فَقَالَ: "إِنَّ لَهَا ذَا قَرَابَةٍ"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Abul-Haytham, kutoka kwa Ibraahiym: Kwamba mwachwa huru wa kike wa Ibraahiym alifariki na akaacha mali. Nikamwambia Ibraahiym (kuhusu hilo); akasema: "Hakika yeye ana jamaa wa karibu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1965
Hadiyth
3064

33-Mlangoباب: الولاء للكبرMlango Wa Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru) Ni
Kwa Al-Kubr (Aliye Karibu Zaidi Kwa Nasaba Na Aliyeacha Huru)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا أَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عُمَرَ، وَعَلِيٍّ، وَزَيْدٍ، قَالَ: وَأَحْسَبُهُ قَدْ ذَكَرَ عَبْدَ اللَّهِ أَيْضًا: أَنَّهُمْ قَالُوا: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْرِ. يَعْنُونَ بِالْكُبْرِ: مَا كَانَ أَقْرَبَ بِأَبٍ أَوْ أُمٍّ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Umar, na 'Aliy, na Zayd (رضي الله عنهم) — amesema: Na nadhani alimtaja pia 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) —, kwamba wao walisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr. Wakimaanisha kwa al-kubr: aliye karibu zaidi (na aliyeacha huru) kwa (upande wa) baba au mama."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1966
Hadiyth
3065

حَدَّثَنَا يَزِيدُ، حَدَّثَنَا أَشْعَثُ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُتْبَةَ، قَالَ: "كَتَبَ إِلَيَّ عُمَرُ فِي شَأْنِ فُكَيْهَةَ بِنْتِ سَمْعَانَ أَنَّهَا مَاتَتْ وَتَرَكَتْ ابْنَ أَخِيهَا لِأَبِيهَا وَأُمِّهَا، وَابْنَ أَخِيهَا لِأَبِيهَا، فَكَتَبَ عُمَرُ: إِنَّ الْوَلَاءَ لِلْكُبْرِ"

Ametusimulia Yaziyd, ametusimulia Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin 'Utbah, amesema: "'Umar (رضي الله عنه) aliniandikia kuhusu jambo la Fukayhah bint Sam'aan, kwamba alifariki, na akaacha mwana wa kaka yake wa baba na mama mmoja, na mwana wa kaka yake wa baba mmoja. 'Umar (رضي الله عنه) akaandika: Hakika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1966
Hadiyth
3066

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: أَنَّ عَلِيًّا، وَزَيْدًا قَالَا: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْر". وَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ، وَشُرَيْحٌ: لِلْوَرَثَةِ

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy: Kwamba 'Aliy na Zayd (رضي الله عنهما) walisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)." Na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) na Shurayh walisema: Ni wa warithi.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1966
Hadiyth
3067

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنِ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "قَضَى عُمَر، وَعَبْدُ اللَّهِ، وَعَلِيٌّ، وَزَيْدٌ لِلْكُبْرِ بِالْوَلَاءِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "'Umar, na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd], na 'Aliy, na Zayd (رضي الله عنهم) waliamua walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) uwe kwa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1966
Hadiyth
3068

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، قَالَ: "تُوُفِّيَتْ فُكَيْهَةُ بِنْتُ سَمْعَانَ وَتَرَكَتْ ابْنَ أَخِيهَا لِأَبِيهَا، وَبَنِي بَنِي أَخِيهَا لِأَبِيهَا وَأُمِّهَا، فَوَرَّثَ عُمَرُ بَنِي أَخِيهَا لِأَبِيهَا"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, amesema: "Fukayhah bint Sam'aan alifariki, na akaacha mwana wa kaka yake wa baba mmoja, na wana wa wana wa kaka yake wa baba na mama mmoja; 'Umar (رضي الله عنه) akawarithisha wana wa kaka yake wa baba mmoja."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1966
Hadiyth
3069

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ السَّلَامِ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُمَرَ، وَعَلِيٍّ، وَزَيْدٍ: أَنَّهُمْ قَالُوا: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْرِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abdus-Salaam bin Harb, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Umar, na 'Aliy, na Zayd (رضي الله عنهم), kwamba wao walisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1967
Hadiyth
3070

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: " فِي أَخَوَيْنِ وَرِثَا مَوْلًى كَانَ أَعْتَقَهُ أَبُوهُمَا، فَمَاتَ أَحَدُهُمَا وَتَرَكَ وَلَدًا، قَالَ: كَانَ عَلِيٌّ، وَزَيْدٌ، وَعَبْدُ اللَّهِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ، يَقُولُونَ:" الْوَلاءُ لِلْكَبِر "

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym: "Kuhusu ndugu wawili waliomrithi mwachwa huru ambaye baba yao alikuwa amemwacha huru; kisha mmoja wao akafa na akaacha mtoto. Akasema: 'Aliy, na Zayd, na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنهم) walikuwa wakisema: Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1968
Hadiyth
3071

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، قَالَ: سَمِعْتُ مَطَرًا الْوَرَّاقَ، يَقُولُ: قَالَ عُمَرُ، وَعَلِيٌّ: "الْوَلاءُ لِلْكِبَرِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hammaad bin Zayd, amesema: Nilimsikia Matwar Al-Warraaq akisema: 'Umar na 'Aliy (رضي الله عنهما) wamesema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1968
Hadiyth
3072

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، عَنْ رَوْحٍ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، وَابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْرِ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, kutoka kwa Rawh, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa; na Ibn Jurayj, kutoka kwa Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, amesema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1969
Hadiyth
3073

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ بْنُ مُوسَى، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْرِ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah bin Muwsaa, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1969
Hadiyth
3074

34-Mlangoباب: في الرجل يوالي الرجلMlango Wa Kuhusu
Mtu Anayefunga Mapatano Ya Walaa (Haki Ya Urithi)
Na Mtu [Mwingine]

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، وَسُفْيَانُ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ الْحَسَنِ فِي الرَّجُلِ يُوَالِي الرَّجُلَ، قَالَا: "هُوَ بَيْنَ الْمُسْلِمِينَ". قَالَ سُفْيَانُ: وَكَذَلِكَ نَقُولُ

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa Ash-Sha'biy; na Sufyaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan, kuhusu mtu anayefunga mapatano ya walaa (haki ya urithi) na mtu (mwingine); (wote) wawili wamesema: "(Mirathi) yake ni baina ya Waislamu (wote)." Sufyaan amesema: Na hivyo ndivyo tunavyosema.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1969
Hadiyth
3075

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْعَزِيزِ بْنُ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَوْهَبٍ، قَالَ: سَمِعْتُ تَمِيمًا الدَّارِيَّ، يَقُولُ: سَأَلْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا السُّنَّةُ فِي الرَّجُلِ مِنْ أَهْلِ الْكُفْرِ يُسْلِمُ عَلَى يَدَيْ رَجُلٍ مِنْ الْمُسْلِمِينَ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "هُوَ أَوْلَى النَّاسِ بِمَحْيَاهُ وَمَمَاتِهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia 'Abdul-'Aziyz bin 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Mawhab, amesema: Nilimsikia Tamiym Ad-Daariy (رضي الله عنه) akisema: Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), nikasema: Yaa Rasula-Allaah, ni ipi Sunnah kuhusu mtu katika watu wa ukafiri anayesilimu mikononi mwa mtu miongoni mwa Waislamu? Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: "Yeye (aliyemsilimisha) ndiye mwenye haki zaidi kati ya watu kwake katika uhai wake na kufa kwake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1969
Hadiyth
3076

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: سُئِلَ عَنْ رَجُلٍ مِنْ أَهْلِ السَّوَادِ إِذَا أَسْلَمَ عَلَى يَدَيْ رَجُلٍ، قَالَ: "يَعْقِلُ عَنْهُ، وَيَرِثُهُ"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: (Ibraahiym) aliulizwa kuhusu mtu katika watu wa As-Sawaad (vijiji na mashamba ya 'Iraaq), anaposilimu mikononi mwa mtu; akasema: "(Mtu huyo) atamlipia diyah (fidia ya damu), na atamrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1969
Hadiyth
3077

35-Mlangoباب: من قال: إن المرأة ترث من دية زوجهاMlango Wa Waliosema: Hakika Mwanamke Anarithi
Katika Diyah (Fidia Ya Damu) Ya Mume Wake

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "تَرِثُ الْمَرْأَةُ مِنْ دِيَةِ زَوْجِهَا فِي الْعَمْدِ وَالْخَطَإِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mwanamke anarithi katika diyah (fidia ya damu) ya mume wake, katika (mauaji ya) kukusudia na ya makosa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1970
Hadiyth
3078

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "الدِّيَةُ عَلَى فَرَائِضِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Diyah (fidia ya damu) (hugawanywa) kwa mujibu wa Faraaidh (mafungu ya mirathi yaliyowekwa) za Allaah (عز وجل)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3079

حَدَّثَنَا مُسْلِمُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا أَيُّوبُ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ، قَالَ: "الدِّيَةُ سَبِيلُهَا سَبِيلُ الْمِيرَاثِ"

Ametusimulia Muslim bin Ibraahiym, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Ayyuwb, kutoka kwa Abuw Qilaabah, amesema: "Diyah (fidia ya damu), njia yake ni njia ya mirathi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3080

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حُمَيْدٍ، وَدَاوُدَ بْنِ أَبِي هِنْدٍ: عُمَرُ بْنُ عَبْدِ الْعَزِيزِ، كَتَبَ أَنْ: "يورث الإخوة من الأم من الدية"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Humayd na Daawuwd bin Abiy Hind: 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz aliandika: "Kwamba ndugu wa upande wa mama warithishwe katika diyah (fidia ya damu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3081

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، قَالَ: "الْعَقْلُ مِيرَاثٌ بَيْنَ وَرَثَةِ الْقَتِيلِ عَلَى كِتَابِ اللَّهِ وَفَرَائِضِهِ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, amesema: "Diyah (fidia ya damu) ni mirathi baina ya warithi wa aliyeuawa, kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah na Faraaidh (mafungu ya mirathi yaliyowekwa) Zake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3082

حَدَّثَنَا قَبِيصَةُ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَمْرِو بْنِ دِينَارٍ، عَنْ بَعْضِ وَلَدِ ابْنِ الْحَنَفِيَّةِ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: "لَقَدْ ظَلَمَ مَنْ لَمْ يُوَرِّثْ الْإِخْوَةَ مِنْ الْأُمِّ مِنْ الدِّيَةِ"

Ametusimulia Qabiyswah, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Amr bin Diynaar, kutoka kwa baadhi ya wana wa Ibn Al-Hanafiyyah, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Hakika amedhulumu yule asiyewarithisha ndugu wa upande wa mama katika diyah (fidia ya damu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3083

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو خَالِدٍ، أَنْبَأَنَا ابْنُ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عُمَرَ، وَعَلِيٍّ، وَزَيْدٍ، قَالُوا: "الدِّيَةُ تُورَثُ كَمَا يُورَثُ الْمَالُ خَطَؤُهُ وَعَمْدُهُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Khaalid, ametupa khabari Ibn Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Umar, na 'Aliy, na Zayd (رضي الله عنهم), wamesema: "Diyah (fidia ya damu) hurithiwa kama mali inavyorithiwa, (ikiwa ni ya mauaji ya) makosa yake na ya kukusudia kwake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1971
Hadiyth
3084

36-Mlangoباب: من قال: لا يورثMlango Wa Waliosema: Hawarithishwi
[Katika Diyah (Fidia Ya Damu)]

حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ: "كَانَ عَلِيٌّ لَا يُوَرِّثُ الْإِخْوَةَ مِنْ الْأُمِّ، وَلَا الزَّوْجَ، وَلَا الْمَرْأَةَ، مِنْ الدِّيَةِ شَيْئًا". قَالَ عَبْد اللَّهِ: بَعْضُهُمْ يُدْخِلُ بَيْنَ إِسْمَاعِيل، وَعَامِرٍ رَجُلًا

Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, ametusimulia Ismaa'iyl, kutoka kwa 'Aamir, amesema: "'Aliy (رضي الله عنه) alikuwa hawarithishi ndugu wa upande wa mama, wala mume, wala mke, chochote katika diyah (fidia ya damu)."

'Abdu-Allaah [Ad-Daarimiy] amesema: Baadhi yao huingiza mtu mmoja baina ya Ismaa'iyl na 'Aamir.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1973
Hadiyth
3085

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ زِيَادٍ الْأَعْلَمِ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "لَا تُوَرَّثُ الْإِخْوَةُ مِنْ الْأُمِّ مِنْ الدِّيَةِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ziyaad Al-A'lam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Ndugu wa upande wa mama hawarithishwi katika diyah (fidia ya damu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1973
Hadiyth
3086

37-Mlangoباب: ميراث الغرقىMlango Wa Mirathi Ya Waliozama Majini

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ خَارِجَةَ بْنِ زَيْدٍ، عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ، قَالَ: "كُلُّ قَوْمٍ مُتَوَارِثِينَ عَمِيَ مَوْتُهُمْ فِي هَدْمٍ، أَوْ غَرَقٍ، فَإِنَّهُمْ لَا يَتَوَارَثُونَ، يَرِثُهُمْ الْأَحْيَاءُ"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Ibn Abiz-Zinaad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Khaarijah bin Zayd, kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), amesema: "Kila watu wanaorithiana ambao kifo chao kimefichika (haijulikani nani alitangulia) katika kuporomokewa (na jengo) au kuzama, basi wao hawarithiani; huwarithi walio hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1974
Hadiyth
3087

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ زَيْدٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ عَتِيقٍ، قَالَ: قَرَأْتُ فِي بَعْضِ كُتُبِ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ فِي الْقَوْمِ يَقَعُ عَلَيْهِمْ الْبَيْتُ، لَا يُدْرَى أَيُّهُمَا مَاتَ قَبْلُ؟ قَالَ: "لَا يُوَرَّثُ الْأَمْوَاتُ بَعْضُهُمْ مِنْ بَعْضٍ، وَيُوَرَّثُ الْأَحْيَاءُ مِنْ الْأَمْوَاتِ"

Ametusimulia Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Hammaad bin Zayd, kutoka kwa Yahyaa bin 'Atiyq, amesema: Nilisoma katika baadhi ya barua za 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz kuhusu watu ambao nyumba inawaangukia, haijulikani yupi kati ya wawili wao alikufa kabla. Amesema: "Wafu hawarithishwi wao kwa wao, na walio hai hurithishwa kutoka kwa wafu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1974
Hadiyth
3088

حَدَّثَنَا نُعَيْمُ بْنُ حَمَّادٍ، عَنْ عَبْدِ الْعَزِيزِ بْنِ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا جَعْفَرٌ، عَنْ أَبِيهِ: أَنَّ أُمَّ كُلْثُومٍ، وَابْنَهَا زَيْدًا مَاتَا فِي يَوْمٍ وَاحِدٍ، فَالْتَقَتْ الصَّائِحَتَانِ فِي الطَّرِيقِ، فَلَمْ يَرِثْ كُلُّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِنْ صَاحِبِهِ، وَأَنَّ أَهْلَ الْحَرَّةِ لَمْ يَتَوَارَثُوا، وَأَنَّ أَهْلَ صِفِّينَ لَمْ يَتَوَارَثُوا "

Ametusimulia Nu'aym bin Hammaad, kutoka kwa 'Abdul-'Aziyz bin Muhammad, ametusimulia Ja'far, kutoka kwa baba yake: Kwamba Ummu Kulthuum (رضي الله عنها) na mwanawe Zayd walikufa siku moja; wanawake wawili waliokuwa wakitangaza vifo vyao kwa sauti wakakutana njiani; basi hakuna kati yao wawili aliyemrithi mwenzake. Na kwamba watu wa (tukio la) Al-Harrah hawakurithiana, na kwamba watu wa (vita vya) Swiffiyn hawakurithiana.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1974
Hadiyth
3089

أَخْبَرَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، أَنْبَأَنَا ابْنُ أَبِي لَيْلَى، عَنْ الشَّعْبِيِّ: "أَنَّ بَيْتًا فِي الشَّامِ وَقَعَ عَلَى قَوْمٍ، فَوَرَّثَ عُمَرُ بَعْضَهُمْ مِنْ بَعْضٍ"

Ametukhabarisha Ja'far bin 'Awn, ametupa khabari Ibn Abiy Laylaa, kutoka kwa Ash-Sha'biy: "Kwamba nyumba moja huko Shaam iliwaangukia watu, na 'Umar (رضي الله عنه) akawarithisha baadhi yao kutoka kwa wengine."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1974
Hadiyth
3090

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ حُرَيْسٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَلِيٍّ: "أَنَّهُ وَرَّثَ أَخَوَيْنِ قُتِلَا بِصِفِّينَ، أَحَدَهُمَا مِنْ الْآخَرِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Hurays, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه): "Kwamba aliwarithisha ndugu wawili waliouawa Swiffiyn, mmoja wao kutoka kwa mwingine."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1974
Hadiyth
3091

38-Mlangoباب: ميراث ذوي الأرحامMlango Wa Mirathi Ya Dhawil-Arhaam (Jamaa Wa Uzazi Wasio
Na Fungu Maalumu Wala Si 'Asabah)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْمُزَنِيِّ: "أَنَّ رَجُلًا هَلَكَ، وَتَرَكَ عَمَّتَهُ، وَخَالَتَهُ، فَأَعْطَى عُمَرُ الْعَمَّةَ نَصِيبَ الْأَخِ، وَأَعْطَى الْخَالَةَ نَصِيبَ الْأُخْتِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Humayd, kutoka kwa Bakr bin 'Abdi-Allaah Al-Muzaniy: "Kwamba mtu mmoja alikufa, na akaacha shangazi yake na dada wa mama yake; 'Umar (رضي الله عنه) akampa shangazi fungu la ndugu (yake wa kiume), na akampa dada wa mama fungu la dada (yake)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3092

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "مَنْ أَدْلَى بِرَحِمٍ، أُعْطِيَ بِرَحِمِهِ الَّتِي يُدْلِي بِهَا"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mwenye kujinasibisha (na maiti) kupitia jamaa wa uzazi, atapewa kwa (kiasi cha fungu la) jamaa yule wa uzazi anayejinasibisha kupitia kwake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3093

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، قَالَ: حَدَّثَنِي أَبُو إِسْحَاق الشَّيْبَانِيُّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: "فِي رَجُلٍ تَرَكَ عَمَّتَهُ، وَابْنَةَ أَخِيهِ، قَالَ: الْمَالُ لِابْنَةِ أَخِيهِ"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, amesema: Amenisimulia Abuw Is-haaq Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy: "Kuhusu mtu aliyeacha shangazi yake na binti wa kaka yake; amesema: Mali ni ya binti wa kaka yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3094

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ الْمُنْكَدِرِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْخَالُ وَارِثٌ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Muhammad bin Al-Munkadir, kutoka kwa Abuw Hurayrah (رضي الله عنه), kutoka kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), amesema: "Mjomba (kaka wa mama) ni mrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3095

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ عُبَيْدَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: أَنَّ عُمَرَ، وَعَبْدَ اللَّهِ رَأَيَا أَنْ يُوَرِّثَا خَالًا "

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa 'Ubaydah, kutoka kwa Ibraahiym: Kwamba 'Umar na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنهما) "waliona wamrithishe mjomba (kaka wa mama)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3096

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ سُلَيْمَانَ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ الشَّعْبِيِّ: فِي عَمَّةٍ، وَبِنْتِ أَخٍ، قَالَ: "الْمَالُ لِابْنَةِ الْأَخِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Sulaymaan Abuw Is-haaq, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kuhusu shangazi na binti wa kaka; amesema: "Mali ni ya binti wa kaka."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3097

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، أنبأنا حَسَنٌ، عَنْ سُلَيْمَانَ، عَنْ بَعْضِهِمْ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لِلْعَمَّةِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametupa khabari Hasan, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa baadhi yao, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "(Mali ni) ya shangazi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3098

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: فِي بِنْتِ أَخٍ، وَعَمَّةٍ، قَالَ: "أَعْطِي الْمَالَ لِابْنَةِ الْأَخِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kuhusu binti wa kaka na shangazi; amesema: "Ninampa binti wa kaka mali."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3099

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ: فِي رَجُلٍ تُوُفِّيَ وَلَيْسَ لَهُ وَارِثٌ إِلَّا ابْنَةُ أَخِيهِ وَخَالُهُ، قَالَ: "لِلْخَالِ نَصِيبُ أُخْتِهِ، وَلِابْنَةِ الْأَخِ نَصِيبُ أَبِيهَا"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Masruwq, kuhusu mtu aliyefariki, naye hana mrithi isipokuwa binti wa kaka yake na mjomba wake (kaka wa mama yake); amesema: "Mjomba (atapata) fungu la dada yake, na binti wa kaka (atapata) fungu la baba yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3100

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ عَامِرٍ، قَالَ: "كَانَ مَسْرُوقٌ يُنَزِّلُ الْعَمَّةَ بِمَنْزِلَةِ الْأَبِ، إِذَا لَمْ يَكُنْ أَبٌ، وَالْخَالَةَ بِمَنْزِلَةِ الْأُمِّ، إِذَا لَمْ تَكُنْ أُمٌّ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa 'Aamir, amesema: "Masruwq alikuwa akimweka shangazi katika daraja ya baba, ikiwa hakuna baba, na dada wa mama katika daraja ya mama, ikiwa hakuna mama."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1976
Hadiyth
3101

حَدَّثَنَا يَعْلَى، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ إِسْحَاق، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ حَبَّانَ نَسَبَهُ إِلَى جَدِّهِ، عَنْ عَمِّهْ وَاسِعِ بْنِ حَبَّانَ، قَالَ: تُوُفِّيَ ابْنُ الدَّحْدَاحَةِ، وَكَانَ أَتِيًّا، وَهُوَ الَّذِي لَا يُعْرَفُ لَهُ أَصْلٌ، فَكَانَ فِي بَنِي الْعَجْلَانِ، وَلَمْ يَتْرُكْ عَقِبًا، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ لِعَاصِمِ بْنِ عَدِيٍّ:" هَلْ تَعْلَمُونَ لَهُ فِيكُمْ نَسَبًا؟ قَالَ: مَا نَعْرِفُهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَدَعَا ابْنَ أُخْتِهِ، فَأَعْطَاهُ مِيرَاثَهُ

Ametusimulia Ya'laa, kutoka kwa Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa Muhammad bin Habbaan — amemnasibisha kwa babu yake —, kutoka kwa ami yake Waasi' bin Habbaan, amesema: Alifariki Ibn Ad-Dahdaahah (رضي الله عنه), naye alikuwa mgeni — naye ni yule ambaye haijulikani asili yake —, na alikuwa (akiishi) kwa Banuw Al-'Ajlaan, na hakuacha kizazi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia 'Aaswim bin 'Adiy (رضي الله عنه): "Je, mnamjua kuwa na nasaba yoyote kwenu?" Akasema: Hatumjui, yaa Rasula-Allaah. Akamwita mtoto wa dada yake, akampa mirathi yake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1979
Hadiyth
3102

حَدَّثَنَا عُمَرُ بْنُ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، حَدَّثَنَا أَبِي، عَنِ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُمَرَ: "أَنَّهُ أَعْطَى خَالًا الْمَالَ"

Ametusimulia 'Umar bin Hafsw bin Ghiyaath, ametusimulia baba yangu, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Umar (رضي الله عنه): "Kwamba alimpa mjomba (kaka wa mama) mali."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1980
Hadiyth
3103

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا أَبُو هَانِئٍ، قَالَ: سُئِلَ عَامِرٌ عَنْ امْرَأَةٍ أَوْ رَجُلٍ، تُوُفِّيَ وَتَرَكَ خَالَةً وَعَمَّةً، قَالَ: "لَيْسَ لَهُ وَارِثٌ وَلَا رَحِمٌ غَيْرُهُمَا"، فَقَالَ: كَانَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مَسْعُودٍ يُنَزِّلُ الْخَالَةَ بِمَنْزِلَةِ أُمِّهِ، وَيُنَزِّلُ الْعَمَّةَ بِمَنْزِلَةِ أَخِيهَا

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Abuw Haaniy, amesema: 'Aamir aliulizwa kuhusu mwanamke au mwanamume aliyefariki na akaacha dada wa mama na shangazi — (muulizaji) akasema: "Hana mrithi wala jamaa wa uzazi isipokuwa hao wawili" —; akasema: 'Abdu-Allaah bin Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa akimweka dada wa mama katika daraja ya mama yake (maiti), na akimweka shangazi katika daraja ya kaka yake (shangazi, yaani baba wa maiti).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1980
Hadiyth
3104

39-Mlangoباب: في الادعاء والإنكارMlango Wa Kuhusu Kudai Na Kukana

حَدَّثَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ عَمْرٍو، عَنِ الْحَسَنِ: فِي رَجُلٍ اعْتَرَفَ عِنْدَ مَوْتِهِ بِأَلْفِ دِرْهَمٍ لِرَجُلٍ، وَأَقَامَ آخَرُ بَيِّنَةً بِأَلْفِ دِرْهَمٍ، وَتَرَكَ الْمَيِّتُ أَلْفَ دِرْهَمٍ، فَقَالَ: "الْمَالُ بَيْنَهُمَا نِصْفَيْنِ، إِلَّا أَنْ يَكُونَ مُفْلِسًا، فَلَا يَجُوزُ إِقْرَارُهُ"

Ametusimulia Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa Al-Hasan, kuhusu mtu aliyekiri wakati wa kufa kwake (kwamba anadaiwa) dirham elfu moja na mtu mmoja, na mwingine akaleta ushahidi wa dirham elfu moja, na maiti akaacha dirham elfu moja; akasema: "Mali ni baina yao wawili nusu kwa nusu, isipokuwa awe amefilisika; hapo kukiri kwake hakufai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1981
Hadiyth
3105

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، قَالَ: قُلْتُ لِشَرِيكٍ: كَيْفَ ذَكَرْتَ فِي الْأَخَوَيْنِ يَدَّعِي أَحَدُهُمَا أَخًا؟ قَالَ: "يَدْخُلُ عَلَيْهِ فِي نَصِيبِهِ"، قُلْتُ: مَنْ ذَكَرَهُ؟ قَالَ: جَابِرٌ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عَلِيٍّ

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, amesema: Nilimwambia Shariyk: Ulitajaje kuhusu ndugu wawili ambao mmoja wao anadai (kuwa wana) ndugu (mwingine)? Akasema: "Anaingia (kushiriki) kwake katika sehemu yake." Nikasema: Ni nani aliyelitaja? Akasema: Jaabir, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1981
Hadiyth
3106

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ مُحَمَّدٍ الْمُحَارِبِيُّ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: فِي الْإِخْوَةِ يَدَّعِي بَعْضُهُمْ الْأَخَ، وَيُنْكِرُ الْآخَرُونَ، قَالَ:" يَدْخُلُ مَعَهُمْ بِمَنْزِلَةِ عَبْدٍ يَكُونُ بَيْنَ الْإِخْوَةِ، فَيَعْتِقَ أَحَدُهُمْ نَصِيبَهُ، قَالَ: وَكَانَ عَامِرٌ، وَالْحَكَمُ، وَأَصْحَابُهُمَا يَقُولُونَ: لَا يَدْخُلُ إِلَّا فِي نَصِيبِ الَّذِي اعْتَرَفَ بِهِ

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Muhammad Al-Muhaaribiy, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kuhusu ndugu ambao baadhi yao wanadai (kuwa wana) ndugu (mwingine), na wengine wanakana; amesema: "Anaingia pamoja nao kwa daraja ya mtumwa aliye (milki ya pamoja) baina ya ndugu, kisha mmoja wao akaacha huru sehemu yake." Amesema: Na 'Aamir, na Al-Hakam, na wenzao walikuwa wakisema: Haingii isipokuwa katika sehemu ya yule aliyemkiri.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1981
Hadiyth
3107

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ وَكِيعٍ، قَالَ: إِذَا كَانَا أَخَوَيْنِ، فَادَّعَى أَحَدُهُمَا أَخًا وَأَنْكَرَهُ الْآخَرُ؟ قَالَ: كَانَ ابْنُ أَبِي لَيْلَى، يَقُولُ: "هِيَ مِنْ سِتَّةٍ: لِلَّذِي لَمْ يَدَّعِ ثَلَاثَةٌ، وَلِلْمُدَّعِي سَهْمَانِ، وَلِلْمُدَّعَى سَهْمٌ"

Ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Wakiy', amesema: Wanapokuwa ndugu wawili, mmoja wao akadai (kuwa wana) ndugu (mwingine), na mwingine akamkana? Amesema: Ibn Abiy Laylaa alikuwa akisema: "Hiyo ni (mgawanyo) kutoka katika (mafungu) sita: yule asiyedai ana (mafungu) matatu, na mdai ana mafungu mawili, na anayedaiwa ana fungu moja."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3108

حَدَّثَنَا يُونُسُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ حَمَّادٍ: "فِي الرَّجُلِ يَكُونُ لَهُ ثَلَاثَةُ بَنِينَ، فَقَالَ: ثُلُثِي لِأَصْغَرِ بَنِيَّ، فَقَالَ الْأَوْسَطُ: أَنَا أُجِيزُ، وَقَالَ الْأَكْبَرُ: أَنَا لَا أُجِيزُ، قَالَ: هِيَ مِنْ تِسْعَةٍ يُخْرِجُ ثُلُثَهُ فَلَهُ سَهْمُهُ، وَسَهْمُ الَّذِي أَجَاز". وَقَالَ حَمَّادٌ: يَرُدُّ السَّهْمَ عَلَيْهِمْ جَمِيعًا، وَقَالَ عَامِرٌ: الَّذِي رَدَّ إِنَّمَا رَدَّ عَلَى نَفْسِهِ

Ametusimulia Yuwnus bin Muhammad, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Hammaad: "Kuhusu mtu mwenye watoto watatu wa kiume, akasema: Theluthi yangu ni ya mdogo zaidi wa wanangu. Wa kati akasema: Mimi naruhusu. Na mkubwa akasema: Mimi siruhusu. Amesema: Hiyo ni (mgawanyo) kutoka katika (mafungu) tisa; inatolewa theluthi yake, naye ana fungu lake na fungu la yule aliyeruhusu." Na Hammaad amesema: Fungu (hilo) linarudishwa kwao wote. Na 'Aamir amesema: Yule aliyerudisha, hakika amerudisha juu ya nafsi yake.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3109

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ آدَمَ، عَنْ شَرِيكٍ، عَنْ خَالِدٍ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ شُرَيْحٍ: فِي رَجُلٍ أَقَرَّ بِأَخٍ، قَالَ: "بَيِّنَتُهُ أَنَّهُ أَخُوهُ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia Yahyaa bin Aadam, kutoka kwa Shariyk, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Shurayh, kuhusu mtu aliyekiri (kuwa na) ndugu; amesema: "(Analazimika kuleta) ushahidi wake kwamba yeye ni ndugu yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3110

أَخْبَرَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ الْحَارِثِ الْعُكْلِيِّ: فِي رَجُلٍ أَقَرَّ عِنْدَ مَوْتِهِ بِأَلْفِ دِرْهَمٍ مُضَارَبَةً، وَأَلْفٍ دَيْنًا، وَلَمْ يَدَعْ إِلَّا أَلْفَ دِرْهَمٍ، قَالَ: "يُبْدَأُ بِالدَّيْنِ، فَإِنْ فَضَلَ فَضْلٌ كَانَ لِصَاحِبِ الْمُضَارَبَةِ"

Ametukhabarisha Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Al-Haarith Al-'Ukliy, kuhusu mtu aliyekiri wakati wa kufa kwake (kwamba ana) dirham elfu moja za mudhwaarabah (mtaji aliopewa kufanyia biashara, faida ikagawanywa baina yao), na elfu moja za deni, na hakuacha isipokuwa dirham elfu moja; amesema: "Huanzwa kwa deni; na ikibaki ziada, inakuwa ya mwenye mudhwaarabah."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3111

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: "فِي رَجُلٍ مَاتَ وَتَرَكَ ثَلَاثَ مِئَةِ دِرْهَمٍ، وَثَلَاثَةَ بَنِينَ، فَجَاءَ رَجُلٌ يَدَّعِي مِائَةَ دِرْهَمٍ عَلَى الْمَيِّتِ، فَأَقَرَّ لَهُ أَحَدُهُمْ، قَالَ: يَدْخُلُ عَلَيْهِمْ بِالْحِصَّةِ"، ثُمَّ قَالَ الشَّعْبِيُّ: مَا أُرَى أَنْ يَكُونَ مِيرَاثًا، حَتَّى يُقْضَى الدَّيْنُ

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa Ash-Sha'biy: "Kuhusu mtu aliyekufa akaacha dirham mia tatu na watoto watatu wa kiume; akaja mtu mmoja akidai dirham mia moja kwa maiti, na mmoja wao akamkiria. Amesema: Anaingia kwao kwa hisa (yake)." Kisha Ash-Sha'biy akasema: Sioni kwamba (mali hiyo) inakuwa mirathi mpaka deni lilipwe.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3112

حَدَّثَنَا أَبُو خَيْثَمَةَ مُصْعَبُ بْنُ سَعِيدٍ الْحَرَّانِيُّ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ الْأَشْعَثِ، عَنْ الْحَسَنِ: فِي رَجُلٍ هَلَكَ وَتَرَكَ ابْنَيْنِ، وَتَرَكَ أَلْفَيْ دِرْهَمٍ، فَاقْتَسَمَا الْأَلْفَيْ دِرْهَمٍ، وَغَابَ أَحَدُ الِابْنَيْنِ، فَجَاءَ رَجُلٌ، فَاسْتَحَقَّ عَلَى الْمَيِّتِ أَلْفَ دِرْهَمٍ، قَالَ: "يَأْخُذُ جَمِيعَ مَا فِي يَدِ الشَّاهِدِ، وَيُقَالُ لَهُ: اتَّبِعْ أَخَاكَ الْغَائِبَ، فَخُذْ نِصْفَ مَا فِي يَدِهِ"

Ametusimulia Abuw Khaythamah Musw'ab bin Sa'iyd Al-Harraaniy, ametusimulia Muhammad bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, kuhusu mtu aliyefariki akaacha watoto wawili wa kiume, na akaacha dirham elfu mbili; wakazigawana zile dirham elfu mbili, na mmoja wa wale watoto wawili akawa hayupo. Akaja mtu, akathibitisha haki juu ya maiti ya dirham elfu moja. Amesema: "Atachukua vyote vilivyo mkononi mwa aliyepo, na (aliyepo) ataambiwa: Mfuate ndugu yako asiyekuwepo, uchukue nusu ya kilicho mkononi mwake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3113

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ زِيَادٍ الْأَعْلَمِ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "إِذَا أَقَرَّ بَعْضُ الْوَرَثَةِ بِدَيْنٍ، فَهُوَ عَلَيْهِ بِحِصَّتِهِ"

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Ziyaad Al-A'lam, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Baadhi ya warithi wanapokiri deni, basi (deni hilo) liko juu yake kwa hisa yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1982
Hadiyth
3114

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ سَلَمَةَ، عَنْ أَبِي هَاشِمٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "إِذَا شَهِدَ اثْنَانِ مِنْ الْوَرَثَةِ بِدَيْنٍ، فَهُوَ مِنْ جَمِيعِ الْمَالِ إِذَا كَانُوا عُدُولًا"، وَقَالَ الشَّعْبِيُّ: عَلَيْهِمَا فِي نَصِيبِهِمَا

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Abuw Haashim, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Wawili miongoni mwa warithi wanaposhuhudia deni, basi (deni hilo) linatoka katika mali yote, ikiwa wao ni waadilifu." Na Ash-Sha'biy amesema: (Deni hilo) liko juu yao wawili katika sehemu yao.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1984
Hadiyth
3115

40-Mlangoباب: في ميراث المرتدMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Aliyeritadi

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ثَابِتُ بْنُ الْوَلِيدِ بْنِ جُمَيْعٍ، قَالَ: أَخْبَرَنِي أَبِي، عَنْ الْقَاسِمِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، قَالَ: كَانَ ابْنُ مَسْعُودٍ "يُوَرِّثُ أَهْلَ الْمُرْتَدِّ إِذَا قُتِلَ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Thaabit bin Al-Waliyd bin Jumay', amesema: Amenikhabarisha baba yangu, kutoka kwa Al-Qaasim bin 'Abdir-Rahmaan, amesema: Ibn Mas'uwd (رضي الله عنه) alikuwa "akiwarithisha jamaa wa aliyeritadi (mali yake) anapouawa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1985
Hadiyth
3116

حَدَّثَنَا الْحَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي عَمْرٍو الشَّيْبَانِيِّ: أَنَّ عَلِيَّ بْنَ أَبِي طَالِبٍ "جَعَلَ مِيرَاثَ الْمُرْتَدِّ لِوَرَثَتِهِ مِنَ الْمُسْلِمِينَ"

Ametusimulia Al-Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Abuw 'Amr Ash-Shaybaaniy, kwamba 'Aliy bin Abiy Twaalib (رضي الله عنه) "aliifanya mirathi ya aliyeritadi kuwa ni ya warithi wake miongoni mwa Waislamu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1985
Hadiyth
3117

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْحَجَّاجُ، عَنِ الْحَكَمِ: أَنَّ عَلِيًّا "قَضَى فِي مِيرَاثِ الْمُرْتَدِّ لِأَهْلِهِ مِنْ الْمُسْلِمِينَ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Hajjaaj, kutoka kwa Al-Hakam, kwamba 'Aliy (رضي الله عنه) "alihukumu kuhusu mirathi ya aliyeritadi kuwa ni ya jamaa zake miongoni mwa Waislamu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1985
Hadiyth
3118

41-Mlangoباب: ميراث القاتلMlango Wa Mirathi Ya Muuaji

حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ هُوَ ابْنُ عَمْرٍو، عَنْ عَبْدِ الْكَرِيمِ، عَنْ الْحَكَمِ، قَالَ:" إِذَا قَتَلَ الرَّجُلُ أَخَاهُ عَمْدًا، لَمْ يُوَرَّثْ مِنْ مِيرَاثِهِ، وَلَا مِنْ دِيَتِهِ، فَإِذَا قَتَلَهُ خَطَأً، وُرِّثَ مِنْ مِيرَاثِهِ، وَلَمْ يُوَرَّثْ مِنْ دِيَتِهِ. قَالَ: وَكَانَ عَطَاءٌ يَقُولُ ذَلِكَ

Ametusimulia Zakariyyaa bin 'Adiy, ametusimulia 'Ubaydu-Allaah — naye ni Ibn 'Amr —, kutoka kwa 'Abdul-Kariym, kutoka kwa Al-Hakam, amesema: "Mtu anapomuua ndugu yake kwa kukusudia, harithishwi katika mirathi yake wala katika diyah (fidia ya damu) yake; na anapomuua kwa makosa, anarithishwa katika mirathi yake, lakini harithishwi katika diyah yake." Amesema: Na 'Atwaa alikuwa akisema hivyo.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1986
Hadiyth
3119

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ خِلَاسٍ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: رَمَى رَجُلٌ أُمَّهُ بِحَجَرٍ فَقَتَلَهَا، فَطَلَبَ مِيرَاثَهُ مِنْ إِخْوَتِهِ، فَقَالَ لَهُ إِخْوَتُهُ: لَا مِيرَاثَ لَكَ، فَارْتَفَعُوا إِلَى عَلِيٍّ، "فَجَعَلَ عَلَيْهِ الدِّيَةَ، وَأَخْرَجَهُ مِنْ الْمِيرَاثِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Khilaas, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: Mtu mmoja alimtupia mama yake jiwe, akamuua. Akataka (sehemu ya) mirathi yake kutoka kwa ndugu zake. Ndugu zake wakamwambia: Huna mirathi. Wakapeleka (shauri lao) kwa 'Aliy (رضي الله عنه), "akamwajibisha diyah (fidia ya damu), na akamtoa katika mirathi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3120

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ الْحُرِّ، عَنْ الْحَكَمِ: أَنَّ الرَّجُلَ إِذَا قَتَلَ امْرَأَتَهُ خَطَأً، "أَنَّهُ يُمْنَعُ مِيرَاثَهُ مِنْ الْعَقْلِ وَغَيْرِهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Al-Hasan bin Al-Hurr, kutoka kwa Al-Hakam: Kwamba mtu anapomuua mkewe kwa makosa, "basi yeye huzuiliwa mirathi yake katika diyah (fidia ya damu) na kinginecho."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3121

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "لَا يَرِثُ الْقَاتِلُ مِنْ الْمَقْتُولِ شَيْئًا"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Mujaahid, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Muuaji hamrithi aliyeuawa chochote."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3122

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ قَتَادَةَ: "فِي رَجُلٍ قَذَفَ امْرَأَتَهُ، وَجَاءَ بِشُهُودٍ فَرُجِمَتْ؟ قَالَ: يَرِثُهَا"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Qataadah: "Kuhusu mtu aliyemtuhumu mkewe kwa zinaa, na akaleta mashahidi, akapigwa mawe (mpaka akafa)? Amesema: Anamrithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3123

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ حَمَّادٍ: "فِي رَجُلٍ جُلِدَ الْحَدَّ أَرَاهُ مَاتَ، شَكَّ أَبُو النُّعْمَانِ؟ قَالَ: يَتَوَارَثَانِ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Hammaad: "Kuhusu mtu aliyechapwa hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah) — naona (alisema): akafa; Abun-Nu'maan ametia shaka —? Amesema: Wanarithiana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3124

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: "الْقَاتِلُ لَا يَرِثُ، وَلَا يَحْجُبُ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Muhammad bin Saalim, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Muuaji harithi, wala hawazuilii (warithi wengine sehemu yao)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3125

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا حَسَنٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ أَبِي عَمْرٍو الْعَبْدِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، قَالَ: "لَا يُوَرَّثُ الْقَاتِلُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Hasan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Abuw 'Amr Al-'Abdiy, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), amesema: "Muuaji harithishwi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3126

حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا بْنُ عَدِيٍّ، حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، عَنْ مُطَرِّفٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "لَا يَرِثُ قَاتِلٌ خَطَأً، وَلَا عَمْدًا"

Ametusimulia Zakariyyaa bin 'Adiy, ametusimulia Abuw Bakr, kutoka kwa Mutwarrif, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Muuaji (aliyeua) kwa makosa harithi, wala (aliyeua) kwa kukusudia."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3127

أخبرنا محمد بن يوسف، عن سفيان، عن ليث، عن طاوس، عن ابن عباس، قال: «لا يرث القاتل»

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Muuaji harithi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1987
Hadiyth
3128

42-Mlangoباب: فرائض المجوسMlango Wa Faraaidh (Mirathi) Ya Majusi

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْأَعْلَى، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: "إِذَا اجْتَمَعَ نَسَبَانِ، وُرِّثَ بِأَكْبَرِهِمَا، يَعْنِي الْمَجُوسَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abdul-A'laa, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Nasaba mbili zinapokusanyika (kwa mtu mmoja), anarithishwa kwa iliyo kubwa zaidi kati ya hizo mbili; yaani: Majusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1990
Hadiyth
3129

حَدَّثَنَا حَجَّاجُ بْنُ مِنْهَالٍ، حَدَّثَنَا حَمَّادُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ أَبِي سُلَيْمَانَ، قَالَ: "يَرِثُ مِنْ الْجَانِبِ الَّذِي يَصْلُحُ، وَلَا يَرِثُ مِنْ الْجَانِبِ الَّذِي لَا يَصْلُحُ"

Ametusimulia Hajjaaj bin Minhaal, ametusimulia Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Hammaad bin Abiy Sulaymaan, amesema: "Anarithi kupitia upande unaofaa (kisheria), wala harithi kupitia upande usiofaa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1990
Hadiyth
3130

حَدَّثَنَا حَجَّاجٌ، حَدَّثَنَا حَمَّادٌ، عَنْ سُفْيَانَ الثَّوْرِيِّ، عَنْ رَجُلٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: أَنَّ عَلِيًّا، وَابْنَ مَسْعُودٍ، قَالَا فِي الْمَجُوسِ: "إِذَا أَسْلَمُوا، يَرِثُونَ مِنْ الْقَرَابَتَيْنِ جَمِيعًا"

Ametusimulia Hajjaaj, ametusimulia Hammaad, kutoka kwa Sufyaan Ath-Thawriy, kutoka kwa mtu mmoja, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kwamba 'Aliy na Ibn Mas'uwd (رضي الله عنهما) walisema kuhusu Majusi: "Wanaposilimu, wanarithi kupitia ujamaa wote wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1990
Hadiyth
3131

43-Mlangoباب: في ميراث الأسيرMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Mateka

أَخْبَرَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ فِي امْرَأَةِ الْأَسِيرِ: "أَنَّهَا تَرِثُهُ وَيَرِثُهَا"

Ametukhabarisha Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Ibn Abiz-Zinaad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz kuhusu mke wa mateka: "Kwamba yeye (mke) anamrithi (mumewe), na yeye (mume) anamrithi (mkewe)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1991
Hadiyth
3132

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ الْفَضْلِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنِي مَعْمَرٌ، عَنْ إِسْحَاق بْنِ رَاشِدٍ، عَنْ عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ فِي الْأَسِيرِ يُوصِي، قَالَ: "أُجيزُ لَهُ وَصِيَّتَهُ مَا دَامَ عَلَى دِينِهِ لَمْ يَتَغَيَّرْ عَنْ دِينِهِ"

Ametusimulia Muhammad bin Al-Fadhwl, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Al-Mubaarak, amenisimulia Ma'mar, kutoka kwa Is-haaq bin Raashid, kutoka kwa 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz kuhusu mateka anayeusia, amesema: "Ninamruhusia wasia wake madamu yuko juu ya Dini yake, hakubadilika kuiacha Dini yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1991
Hadiyth
3133

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ شُرَيْحٍ، قَالَ: "يُوَرَّثُ الْأَسِيرُ إِذَا كَانَ فِي أَيْدِي الْعَدُوِّ"

Ametukhabarisha Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa Shurayh, amesema: "Mateka anarithishwa anapokuwa mikononi mwa adui."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1991
Hadiyth
3134

حَدَّثَنَا مُحَمَّدٌ، قَالَ: حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، حَدَّثَنِي مَنْ سَمِعَ إِبْرَاهِيمَ، يَقُولُ: "يُوَرَّثُ الْأَسِيرُ"

Ametusimulia Muhammad, amesema: Ametusimulia Sufyaan, amenisimulia aliyemsikia Ibraahiym akisema: "Mateka anarithishwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1991
Hadiyth
3135

حَدَّثَنَا الْمُعَلَّى بْنُ أَسَدٍ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، عَنْ دَاوُدَ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ: أَنَّهُ كَانَ "لَا يُوَرِّثُ الْأَسِيرَ"

Ametusimulia Al-Mu'allaa bin Asad, ametusimulia Wuhayb, kutoka kwa Daawuwd, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib, kwamba yeye alikuwa "hamrithishi mateka."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1991
Hadiyth
3136

44-Mlangoباب: في ميراث الحميلMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Al-Hamiyl (Aliyeletwa
Kutoka Nchi Ya Ugenini, Akadaiwa Nasaba)

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: كَتَبَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ إِلَى شُرَيْحٍ: أَنْ "لَا يُوَرِّثَ الْحَمِيلَ إِلَّا بِبَيِّنَةٍ، وَإِنْ جَاءَتْ بِهِ فِي خِرَقِهَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Al-Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: 'Umar bin Al-Khatwtwaab (رضي الله عنه) alimwandikia Shurayh: Kwamba "asimrithishe al-hamiyl (aliyeletwa kutoka nchi ya ugenini, akadaiwa nasaba) isipokuwa kwa ushahidi, hata kama (mwanamke) amemleta katika vitambaa vyake (vya kumfunika mtoto mchanga)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3137

أَخْبَرَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "وَرِّثْ الْحَمِيلَ"

Ametukhabarisha 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mrithishe al-hamiyl (aliyeletwa kutoka nchi ya ugenini, akadaiwa nasaba)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3138

حَدَّثَنَا أَبُو سَعِيدٍ مِنْ بَنِي أُمَيَّةَ، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي مَرْيَمَ، عَنْ ضَمْرَةَ، وَالْفُضَيْلِ بْنِ فَضَالَةَ، وَابْنِ أَبِي عَوْفٍ، وراشد، وعطية، قَالُوا: "لَا يُوَرَّثُ الْحُمَلَاءُ"

Ametusimulia Abuw Sa'iyd, miongoni mwa Banuw Umayyah, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Abdi-Allaah bin Abiy Maryam, kutoka kwa Dhwamrah, na Al-Fudhwayl bin Fadhwaalah, na Ibn Abiy 'Awf, na Raashid, na 'Atwiyyah, wamesema: "Al-humalaa (wingi wa al-hamiyl: walioletwa kutoka nchi ya ugenini, wakadaiwa nasaba) hawarithishwi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3139

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، قَالَ: قَالَ ابْنُ الْمُبَارَكِ: حَدَّثَنَا ابْنُ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: ذُكِرَ عِنْدَهُ قَوْلُ مَنْ يَقُولُ فِي الْحَمِيلِ، فَأَنْكَرَ ذَلِكَ، وَقَالَ: "قَدْ تَوَارَثَ الْمُهَاجِرُونَ، وَالْأَنْصَارُ بِنَسَبِهِمْ الَّذِي كَانَ فِي الْجَاهِلِيَّةِ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, amesema: Ibn Al-Mubaarak amesema: Ametusimulia Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad, amesema: Ilitajwa mbele yake kauli ya anayesema (hivyo) kuhusu al-hamiyl (aliyeletwa kutoka nchi ya ugenini, akadaiwa nasaba), akalikana hilo, na akasema: "Muhaajiruwn (waliohajiri kwenda Madiynah) na Answaar (رضي الله عنهم) walirithiana kwa nasaba zao zilizokuwa katika Jaahiliyyah (zama za ujinga kabla ya Islaam)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3140

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، عَنْ ابْنِ إِدْرِيسَ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ الْحَسَنِ، وَابْنِ سِيرِينَ، قَالَا: "لَا يُوَرَّثُ الْحَمِيلُ إِلَّا بِبَيِّنَةٍ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, kutoka kwa Ibn Idriys, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa Al-Hasan na Ibn Siyriyn, wamesema: "Al-hamiyl (aliyeletwa kutoka nchi ya ugenini, akadaiwa nasaba) harithishwi isipokuwa kwa ushahidi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3141

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ حَمَّادٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَمْ يَكُنْ أَبُو بَكْرٍ، وَعُمَرُ، وَعُثْمَانُ يُوَرِّثُونَ الْحَمِيلَ"

Ametusimulia Abuw Bakr, ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Hammaad, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Abuw Bakr, na 'Umar, na 'Uthmaan (رضي الله عنهم) hawakuwa wakimrithisha al-hamiyl (aliyeletwa kutoka nchi ya ugenini, akadaiwa nasaba)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3142

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحِيمِ الْمُحَارِبِيُّ، عَنْ زَائِدَةَ، عَنْ أَشْعَثَ بْنِ أَبِي الشَّعْثَاءِ، قَالَ: "أَقَرَّتْ امْرَأَةٌ مِنْ مُحَارِبٍ جَلِيبَةٌ بِنَسَبِ أَخٍ لَهَا جَلِيبٍ، فَوَرَّثَهُ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ عُتْبَةَ مِنْ أُخْتِهِ"

Ametusimulia Abuw Bakr, ametusimulia 'Abdur-Rahiym Al-Muhaaribiy, kutoka kwa Zaaidah, kutoka kwa Ash'ath bin Abiy Ash-Sha'thaa, amesema: "Mwanamke mmoja wa (kabila la) Muhaarib, aliyeletwa kutoka ugenini, alikiri nasaba ya ndugu yake (wa kiume) aliyeletwa kutoka ugenini; na 'Abdu-Allaah bin 'Utbah akamrithisha (ndugu huyo) kutoka kwa dada yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1993
Hadiyth
3143

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ، عَنْ رَجُلٍ قَالَ عِنْدَ فِرَاقِ الدُّنْيَا: أَنَا مَوْلَى فُلَانٍ، قَالَ: "يُرَدُّ مِيرَاثَهُ لِمَنْ سَمَّى أَنَّهُ مَوْلَاهُ عِنْدَ فِرَاقِ الدُّنْيَا، إِلَّا أَنْ يَأْتُوا عَلَيْهِ بِبَيِّنَةٍ بِغَيْرِ ذَلِكَ يَرُدُّونَ بِهِ قَوْلَهُ، فَيُرَدُّ مِيرَاثُهُ إِلَى مَا قَامَتْ بِهِ الْبَيِّنَةُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab, kuhusu mtu aliyesema wakati wa kuiacha dunia: Mimi ni mawlaa (mwachwa huru) wa fulani; amesema: "Mirathi yake inarudishwa kwa yule aliyemtaja kuwa ndiye bwana wake (aliyemwacha huru) wakati wa kuiacha dunia, isipokuwa (watu) walete juu yake ushahidi wa kinyume cha hilo, wa kuirudisha kauli yake; hapo mirathi yake itarudishwa kwa yale ambayo ushahidi umesimama juu yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1995
Hadiyth
3144

45-Mlangoباب: في ميراث ولد الزناMlango Wa Kuhusu Mirathi Ya Mtoto Wa Zinaa

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ سَالِمٍ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، وَعَبْدِ اللَّهِ، قَالَا: "وَلَدُ الزِّنَا بِمَنْزِلَةِ ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Muhammad bin Saalim, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy na 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنهما), wamesema: "Mtoto wa zinaa ni kwa daraja ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1996
Hadiyth
3145

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زُهَيْرٌ، عَنْ الْحَسَنِ بْنِ الْحُرِّ، حَدَّثَنِي الْحَكَمُ: أَنَّ "وَلَدَ الزِّنَا لَا يَرِثُهُ الَّذِي يَدَّعِيهِ، وَلَا يَرِثُهُ الْمَوْلُودُ"

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym, ametusimulia Zuhayr, kutoka kwa Al-Hasan bin Al-Hurr, amenisimulia Al-Hakam: Kwamba "mtoto wa zinaa, hamrithi yule anayemdai (kuwa ni mwanawe), wala aliyezaliwa hamrithi (yeye)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1996
Hadiyth
3146

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا رَوْحٌ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ أَبِي حَفْصَةَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ حُسَيْنٍ أَنَّهُ كَانَ "لَا يُوَرِّثُ وَلَدَ الزِّنَا، وَإِنْ ادَّعَاهُ الرَّجُلُ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia Rawh, kutoka kwa Muhammad bin Abiy Hafswah, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa 'Aliy bin Husayn, kwamba yeye alikuwa "hamrithishi mtoto wa zinaa, hata kama mwanamume atamdai (kuwa ni mwanawe)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1996
Hadiyth
3147

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي بَكْرُ بْنُ مُضَرَ، عَنْ عَمْرٍو يَعْنِي ابْنَ الْحَارِثِ، عَنْ بُكَيْرٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ، قَالَ: "أَيُّمَا رَجُلٍ أَتَى إِلَى غُلَامٍ يَزْعُمُ أَنَّهُ ابْنٌ لَهُ، وَأَنَّهُ زَنَى بِأُمِّهِ، وَلَمْ يَدَّعِ ذَلِكَ الْغُلَامَ أَحَدٌ، فَهُوَ يَرِثُهُ". قَالَ بُكَيْرٌ: وَسَأَلْتُ عُرْوَةَ عَنْ ذَلِكَ، فَقَالَ مِثْلَ قَوْلِ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ وَقَالَ عُرْوَةُ: بَلَغَنَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: "الْوَلَدُ لِلْفِرَاشِ، وَلِلْعَاهِرِ الْحَجَرُ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Bakr bin Mudhwar, kutoka kwa 'Amr — yaani Ibn Al-Haarith —, kutoka kwa Bukayr, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, amesema: "Mwanamume yeyote aliyemjia mvulana akidai kwamba ni mwanawe, na kwamba alizini na mama yake, na hakuna yeyote aliyemdai mvulana huyo, basi yeye anamrithi." Bukayr amesema: Na nilimuuliza 'Urwah kuhusu hilo, akasema mfano wa kauli ya Sulaymaan bin Yasaar. Na 'Urwah amesema: Imetufikia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtoto ni wa mwenye kitanda, na mzinifu ni kukosa (haki)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1997
Hadiyth
3148

حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، عَنْ حَفْصِ بْنِ غِيَاثٍ، عَنْ عَمْرٍو، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "ابْنُ الْمُلَاعَنَةِ مِثْلُ وَلَدِ الزِّنَا، تَرِثُهُ أُمُّهُ، وَوَرَثَتُهُ، وَرَثَةُ أُمِّهِ"

Ametusimulia Ibraahiym bin Muwsaa, kutoka kwa Hafsw bin Ghiyaath, kutoka kwa 'Amr, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) ni mfano wa mtoto wa zinaa: mama yake anamrithi, na warithi wake ni warithi wa mama yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1997
Hadiyth
3149

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَا يُوَرَّثُ وَلَدُ الزِّنَا"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mtoto wa zinaa harithishwi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1998
Hadiyth
3150

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ الْمُغِيرَةِ، عَنْ ابْنِ الْمُبَارَكِ، عَنْ مَعْمَرٍ، أَوْ يُونُسَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ: فِي أَوْلَادِ الزِّنَا، قَالَ: "يَتَوَارَثُونَ مِنْ قِبَلِ الْأُمَّهَاتِ، وَإِنْ وَلَدَتْ تَوْأَمًا فَمَاتَ، وَرِثَ السُّدُسَ"

Ametusimulia Sa'iyd bin Al-Mughiyrah, kutoka kwa Ibn Al-Mubaarak, kutoka kwa Ma'mar, au Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kuhusu watoto wa zinaa, amesema: "Wanarithiana kupitia upande wa mama zao; na (mama) akizaa pacha, kisha (mmoja wao) akafa, (mwenzake) anarithi sudusi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1998
Hadiyth
3151

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، قَالَ: حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ شِبَاكٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَا يَرِثُ وَلَدُ الزِّنَا، إِنَّمَا يَرِثُ مَنْ لَمْ يُقَمْ عَلَى أَبِيهِ الْحَدُّ، أَوْ تُمْلَكْ أُمُّهُ بِنِكَاحٍ أَوْ شِرَاءٍ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, amesema: Ametusimulia Hushaym, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Shibaak, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mtoto wa zinaa harithi; hakika anarithi tu yule ambaye baba yake hakusimamishiwa hadd (adhabu iliyowekwa na Shariy'ah), au mama yake amemilikiwa kwa ndoa au kwa kununuliwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1998
Hadiyth
3152

حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ مُوسَى بْنِ مُحَمَّدٍ الْأَنْصَارِيِّ، عَنْ إِسْمَاعِيل، عَنْ الْحَسَنِ فِي الرَّجُلِ يَفْجُرُ بِالْمَرْأَةِ، ثُمَّ يَتَزَوَّجُهَا، قَالَ: "لَا بَأْسَ، إِلَّا أَنْ تَكُونَ حُبْلَى، فَإِنَّ الْوَلَدَ لَا يَلْحَقُهُ"

Ametusimulia Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Muwsaa bin Muhammad Al-Answaariy, kutoka kwa Ismaa'iyl, kutoka kwa Al-Hasan, kuhusu mtu anayezini na mwanamke, kisha akamuoa; amesema: "Hakuna ubaya, isipokuwa awe na mimba; kwani mtoto hanasibishwi kwake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1999
Hadiyth
3153

حَدَّثَنَا زَيْدُ بْنُ يَحْيَى، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ رَاشِدٍ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ مُوسَى، عَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ: أَنّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: قَضَى أَنَّ "كُلَّ مُسْتَلْحَقٍ اسْتُلْحِقَ بَعْدَ أَبِيهِ الَّذِي يُدْعَى لَهُ ادَّعَاهُ وَرَثَتُهُ بَعْدَهُ، فَقَضَى إِنْ كَانَ مِنْ أَمَةٍ يَمْلِكُهَا يَوْمَ يَطَؤُهَا، فَقَدْ لَحِقَ بِمَنْ اسْتَلْحَقَهُ، وَلَيْسَ لَهُ فِيمَا قُسِمَ قَبْلَهُ مِنْ الْمِيرَاثِ شَيْءٌ، وَمَا أَدْرَكَ مِنْ مِيرَاثٍ لَمْ يُقْسَمْ، فَلَهُ نَصِيبُهُ، وَلَا يَلْحَقُ إِذَا كَانَ الَّذِي يُدْعَى لَهُ أَنْكَرَهُ، وَإِنْ كَانَ مِنْ أَمَةٍ لَا يَمْلِكُهَا، أَوْ حُرَّةٍ عَاهَرَهَا، فَإِنَّهُ لَا يَلْحَقُ وَلَا يَرِثُ، وَإِنْ كَانَ الَّذِي يُدْعَى لَهُ هُوَ ادَّعَاهُ، فَهُوَ وَلَدُ زِنَا لِأَهْلِ أُمِّهِ مَنْ كَانُوا: حُرَّةً، أَوْ أَمَةً"

Ametusimulia Zayd bin Yahyaa, kutoka kwa Muhammad bin Raashid, kutoka kwa Sulaymaan bin Muwsaa, kutoka kwa 'Amr bin Shu'ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake ['Abdu-Allaah bin 'Amr (رضي الله عنهما)], kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alihukumu kwamba "kila mtoto anayenasibishwa, aliyenasibishwa baada ya (kufa) baba yake ambaye anadaiwa kwake — warithi wake wakamdai baada yake —, basi alihukumu: Ikiwa ni (mtoto) wa mjakazi aliyekuwa akimmiliki siku alipomwingilia, basi amekwisha nasibishwa kwa yule aliyemnasibisha, wala hana chochote katika mirathi iliyogawanywa kabla yake; na alichokiwahi katika mirathi ambayo haijagawanywa, basi ana sehemu yake. Wala hanasibishwi ikiwa yule anayedaiwa kwake alimkana. Na ikiwa ni (mtoto) wa mjakazi asiyemmiliki, au wa mwanamke huru aliyezini naye, basi yeye hanasibishwi wala harithi, hata kama yule anayedaiwa kwake ndiye aliyemdai; basi yeye ni mtoto wa zinaa, (ni) wa jamaa wa mama yake, vyovyote walivyo: (akiwa mama) huru au mjakazi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
1999
Hadiyth
3154

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، عَنْ الْحَسَنِ، عَنْ عُمَيْرِ بْنِ يَزِيدَ، قَالَ: سَأَلْتُ الشَّعْبِيَّ عَنْ مَمْلُوكٍ لِي وَلَدُ زِنًا، قَالَ: "لَا تَبِعْهُ، وَلَا تَأْكُلْ ثَمَنَهُ، وَاسْتَخْدِمْهُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, kutoka kwa Al-Hasan, kutoka kwa 'Umayr bin Yaziyd, amesema: Nilimuuliza Ash-Sha'biy kuhusu mtumwa wangu ambaye ni mtoto wa zinaa; akasema: "Usimuuze, wala usile thamani yake, na umtumikishe."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2000
Hadiyth
3155

حَدَّثَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ: سُئِلَ عَنْ وَلَدِ زِنَا يَمُوتُ، قَالَ:" إِنْ كَانَ ابْنَ عَرَبِيَّةٍ، وَرِثَتْ أُمُّهُ الثُّلُثَ، وَجُعِلَ بَقِيَّةُ مَالِهِ فِي بَيْتِ الْمَالِ، وَإِنْ كَانَ ابْنَ مَوْلَاةٍ، وَرِثَتْ أُمُّهُ الثُّلُثَ، وَوَرِثَ مَوَالِيهَا الَّذِينَ أَعْتَقُوهَا مَا بَقِيَ. قَالَ مَرْوَانُ: وَسَمِعْتُ مَالِكًا يَقُولُ ذَلِكَ

Ametusimulia Marwaan bin Muhammad, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Az-Zuhriy: Aliulizwa kuhusu mtoto wa zinaa anayekufa; akasema: "Ikiwa ni mtoto wa mwanamke wa Kiarabu, mama yake anarithi theluthi, na mali yake iliyobaki inawekwa katika Baytul-Maal (hazina ya Waislamu); na ikiwa ni mtoto wa mwanamke mwachwa huru, mama yake anarithi theluthi, na mabwana zake (mama), wale waliomwacha huru, wanarithi kilichobaki." Marwaan amesema: Na nilimsikia Maalik akisema hivyo.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2000
Hadiyth
3156

حَدَّثَنَا مَرْوَانُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا الْهَيْثَمُ بْنُ حُمَيْدٍ، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ الْحَارِثِ، حَدَّثَنِي عَمْرُو بْنُ شُعَيْبٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "قَضَى بِمِيرَاثِ ابْنِ الْمُلَاعَنَةِ لِأُمِّهِ كُلِّهِ، لِمَا لَقِيَتْ فِيهِ مِنْ الْعَنَاءِ"

Ametusimulia Marwaan bin Muhammad, ametusimulia Al-Haytham bin Humayd, kutoka kwa Al-'Alaa bin Al-Haarith, amenisimulia 'Amr bin Shu'ayb, kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) "alihukumu mirathi ya mtoto wa mwanamke aliyelaaniana (na mumewe) kuwa yote ni ya mama yake, kwa sababu ya mashaka aliyoyapata kwa ajili yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2000
Hadiyth
3157

حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل بْنُ أَبَانَ، عَنْ مُوسَى بْنِ مُحَمَّدٍ الْأَنْصَارِيِّ، قَالَ: حَدَّثَنِي الْحَارِثُ بْنُ حَصِيرَةَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَهْبٍ، عَنْ عَلِيٍّ: أَنَّهُ قَالَ فِي وَلَدِ الزِّنَا لِأَوْلِيَاءِ أُمِّهِ: "خُذُوهُ إِنَّكُمْ تَرِثُونَهُ وَتَعْقِلُونَهُ، وَلَا يَرِثُكُمْ"

Ametusimulia Ismaa'iyl bin Abaan, kutoka kwa Muwsaa bin Muhammad Al-Answaariy, amesema: Amenisimulia Al-Haarith bin Haswiyrah, kutoka kwa Zayd bin Wahb, kutoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه), kwamba alisema kuhusu mtoto wa zinaa, (akiwaambia) jamaa wa mama yake: "Mchukueni, kwani nyinyi mnamrithi, na mnambebea diyah (fidia ya damu), wala yeye hawarithi nyinyi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2001
Hadiyth
3158

46-Mlangoباب: ميراث السائبةMlango Wa Mirathi Ya As-Saaibah (Mtumwa Aliyeachiliwa
Huru Kabisa, Bwana Wake Akiacha Haki Ya Kumrithi)

أَخْبَرَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، وَعَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، قَالَا: حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ سَلَمَةَ بْنِ كُهَيْلٍ، عَنْ أَبِي عَمْرٍو الشَّيْبَانِيِّ، قَالَ: َقَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "السَّائِبَةُ يَضَعُ مَالَهُ حَيْثُ شَاءَ". قَالَ عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ: قَالَ شُعْبَةُ: لَمْ يَسْمَعْ هَذَا مِنْ سَلَمَةَ أَحَدٌ غَيْرِي

Ametukhabarisha Abuw Nu'aym na 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, wamesema: Ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Salamah bin Kuhayl, kutoka kwa Abuw 'Amr Ash-Shaybaaniy, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "As-saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi) anaiweka mali yake popote anapotaka." 'Abdu-Allaah bin Yaziyd amesema: Shu'bah amesema: Hakuna yeyote aliyesikia hili kutoka kwa Salamah isipokuwa mimi.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2002
Hadiyth
3159

أَخْبَرَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا حَاتِمُ بْنُ وَرْدَانَ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ الْحَسَنِ: سُئِلَ عَنْ مِيرَاثِ السَّائِبَةِ، فَقَالَ: "كُلُّ عَتِيقٍ سَائِبَةٌ"

Ametukhabarisha Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Haatim bin Wardaan, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan: Aliulizwa kuhusu mirathi ya as-saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi), akasema: "Kila mwachwa huru ni saaibah."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2002
Hadiyth
3160

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا سُلَيْمَانُ، عَنْ أَبِي عُثْمَانَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "الصَّدَقَةُ وَالسَّائِبَةُ لِيَوْمِهِمَا، أَوْ لِوَقْتِهِمَا"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Sulaymaan, kutoka kwa Abuw 'Uthmaan, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Swadaka na as-saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi) ni kwa siku yake — au: kwa wakati wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2002
Hadiyth
3161

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، قَالَ: سُئِلَ عَامِرٍ عَنْ الْمَمْلُوكِ يُعْتَقُ سَائِبَةً لِمَنْ وَلَاؤُهُ؟ قَالَ: "لِلَّذِي أَعْتَقَهُ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zakariyyaa, amesema: 'Aamir aliulizwa kuhusu mtumwa anayeachwa huru akiwa saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi): walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wake ni wa nani? Akasema: "Ni wa yule aliyemwacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2003
Hadiyth
3162

حَدَّثَنَا أَبُو حَاتِمٍ الْبَصْرِيُّ هُوَ رَوْحُ بْنُ أَسْلَمَ، حَدَّثَنَا بِشْرُ بْنُ الْمُفَضَّلِ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَمْرٍو، قَالَ: "مَاتَ مَوْلًى عَلَى عَهْدِ عُثْمَانَ لَيْسَ لَهُ وَالٍ، فَأَمَرَ بِمَالِهِ، فَأُدْخِلَ بَيْتَ الْمَالِ"

Ametusimulia Abuw Haatim Al-Baswriy — naye ni Rawh bin Aslam —, ametusimulia Bishr bin Al-Mufadhwdhwal, ametusimulia 'Abdur-Rahmaan bin Is-haaq, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr, amesema: "Mawlaa (mwachwa huru) mmoja alikufa katika zama za 'Uthmaan (رضي الله عنه), hana walii (wa kumrithi); akaamuru kuhusu mali yake, ikaingizwa katika Baytul-Maal (hazina ya Waislamu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2003
Hadiyth
3163

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا إِسْمَاعِيل، عَنْ عَامِرٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ: فِي رَجُلٍ مَاتَ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ مَوْلَى عَتَاقَةٍ، قَالَ: "مَالُهُ حَيْثُ أَوْصَى بِهِ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ أَوْصَى، فَهُوَ فِي بَيْتِ الْمَالِ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Ismaa'iyl, kutoka kwa 'Aamir, kutoka kwa Masruwq, kuhusu mtu aliyekufa naye hakuwa na bwana aliyemwacha huru; amesema: "Mali yake ni pale alipoiusia; na ikiwa hakuusia, basi iko katika Baytul-Maal (hazina ya Waislamu)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2003
Hadiyth
3164

حَدَّثَنَا أَبُو سَعِيدِ بْنُ عَمْرٍو، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ أَبِي مَرْيَمَ، عَنْ ضَمْرَةَ، وَرَاشِدِ بْنِ سَعْدٍ، وَغَيْرِهِمَا، قَالُوا فِيمَنْ أُعْتِقَ سَائِبَةً: "إِنَّ وَلَاءَهُ لِمَنْ أَعْتَقَهُ، إِنَّمَا سَيَّبَهُ مِنْ الرِّقِّ، وَلَمْ يُسَيِّبْهُ مِنْ الْوَلَاءِ"

Ametusimulia Abuw Sa'iyd bin 'Amr, kutoka kwa Abuw Bakr bin Abiy Maryam, kutoka kwa Dhwamrah, na Raashid bin Sa'd, na wengineo, wamesema kuhusu aliyeachwa huru akiwa saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi): "Hakika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wake ni wa yule aliyemwacha huru; hakika amemwachilia kutoka katika utumwa tu, wala hakumwachilia kutoka katika walaa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2004
Hadiyth
3165

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو دَاوُدَ، عَنْ شُعْبَةَ، قَالَ: أَخْبَرَنِي مَنْصُورٌ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، وَالشَّعْبِيِّ، قَالَا: "لَا بَأْسَ بِبَيْعِ وَلَاءِ السَّائِبَةِ وَهِبَتِهِ"

Ametusimulia Abuw Bakr bin Abiy Shaybah, ametusimulia Abuw Daawuwd, kutoka kwa Shu'bah, amesema: Amenikhabarisha Manswuwr, kutoka kwa Ibraahiym na Ash-Sha'biy, wamesema: "Hakuna ubaya kuuza walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wa saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi) na kuutoa zawadi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2004
Hadiyth
3166

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا الْمَسْعُودِيُّ، عَنْ الْقَاسِمِ، قَالَ: "أَعْتَقَ رَجُلٌ غُلَامًا سَائِبَةً، فَأَتَى عَبْدَ اللَّهِ، وَقَالَ: إِنِّي أَعْتَقْتُ غُلَامًا لِي سَائِبَةً، وَهَذِهِ تَرِكَتُهُ، قَالَ: هِيَ لَكَ، قَالَ: لَا حَاجَةَ لِي فِيهَا، قَالَ: فَضَعْهَا، فَإِنَّ هَاهُنَا وَارِثًا كَثِيرًا"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Al-Mas'uwdiy, kutoka kwa Al-Qaasim, amesema: "Mtu mmoja alimwacha huru mtumwa kijana akiwa saaibah (mtumwa aliyeachiliwa huru kabisa, bwana wake akiacha haki ya kumrithi); kisha akamjia 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه), na akasema: Hakika mimi nilimwacha huru mtumwa wangu kijana akiwa saaibah, na hii ni mali aliyoiacha. Akasema: Ni yako. Akasema: Sina haja nayo. Akasema: Basi iweke, kwani hapa kuna warithi wengi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2004
Hadiyth
3167

47-Mlangoباب: ميراث الصبيMlango Wa Mirathi Ya Mtoto Mchanga

أَخْبَرَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، أَنْبَأَنَا الْأَشْعَثُ، عَنْ أَبِي الزُّبَيْرِ، عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، قَالَ: "إِذَا اسْتَهَلَّ الصَّبِيُّ، وُرِّثَ وَصُلِّيَ عَلَيْهِ"

Ametukhabarisha Yaziyd bin Haaruwn, ametupa khabari Al-Ash'ath, kutoka kwa Abuz-Zubayr, kutoka kwa Jaabir bin 'Abdi-Allaah (رضي الله عنهما), amesema: "Mtoto mchanga anapolia (kwa sauti baada ya kuzaliwa), hurithishwa na huswaliwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2005
Hadiyth
3168

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ أَبِي إِسْحَاق، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "إِذَا اسْتَهَلَّ الصَّبِيُّ، وَرِثَ وَوُرِثَ وَصُلِّيَ عَلَيْهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Abuw Is-haaq, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Mtoto mchanga anapolia (kwa sauti baada ya kuzaliwa), hurithi, na hurithiwa, na huswaliwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2005
Hadiyth
3169

حَدَّثَنَا مَالِكُ بْنُ إِسْمَاعِيل، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ سِمَاكٍ، عَنْ عِكْرِمَةَ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "لَيْسَ مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا اسْتَهَلَّ، وَاسْتِهْلَالُهُ بِعَصْرِ الشَّيْطَانُ بَطْنَهُ، فَيَصِيحُ، إِلَّا عِيسَى ابْنَ مَرْيَمَ عَلَيْهِ السَّلَامُ"

Ametusimulia Maalik bin Ismaa'iyl, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa 'Ikrimah, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Hakuna mtoto anayezaliwa ila hulia (kwa sauti), na kulia kwake ni kwa shaytwaan kulibana tumbo lake, basi hupiga ukelele — isipokuwa 'Iysaa bin Maryam (عليه السلام)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2006
Hadiyth
3170

حَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ حَسَّانَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى هُوَ ابْنُ حَمْزَةَ، عَنْ زَيْدِ بْنِ وَاقِدٍ، عَنْ مَكْحُولٍ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: "لَا يَرِثُ الْمَوْلُودُ حَتَّى يَسْتَهِلَّ صَارِخًا، وَإِنْ وَقَعَ حَيًّا"

Ametusimulia Yahyaa bin Hassaan, ametusimulia Yahyaa — naye ni Ibn Hamzah —, kutoka kwa Zayd bin Waaqid, kutoka kwa Makhuwl, amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: "Mtoto aliyezaliwa harithi mpaka alie kwa kupiga ukelele, hata kama atazaliwa akiwa hai."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2007
Hadiyth
3171

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ إِسْحَاق، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ جَابِرٍ، قَالَ: "إِذَا اسْتَهَلَّ الْمَوْلُودُ، صُلِّيَ عَلَيْهِ وَوُرِثَ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia Muhammad bin Is-haaq, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه), amesema: "Mtoto aliyezaliwa anapolia (kwa sauti), huswaliwa na hurithiwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2007
Hadiyth
3172

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا مَعْنٌ، عَنْ ابْنِ أَبِي ذِئْبٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ: أَرَى "الْعُطَاسَ اسْتِهْلَالًا"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Muhammad, ametusimulia Ma'n, kutoka kwa Ibn Abiy Dhi'b, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: Ninaona "kupiga chafya (kwa mtoto mchanga) ni kulia (kunakothibitisha uhai wake)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2007
Hadiyth
3173

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا أَبُو عَوَانَةَ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "لَا يُوَرَّثُ الْمَوْلُودُ حَتَّى يَسْتَهِلَّ، وَلَا يُصَلَّى عَلَيْهِ حَتَّى يَسْتَهِلَّ، فَإِذَا اسْتَهَلَّ، صُلِّيَ عَلَيْهِ وَوُرِّثَ، وَكُمِّلَتْ الدِّيَةُ"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Abuw 'Awaanah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Mtoto aliyezaliwa harithishwi mpaka alie (kwa sauti), wala haswaliwi mpaka alie. Akilia, huswaliwa na hurithishwa, na diyah (fidia ya damu) yake hukamilishwa."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2007
Hadiyth
3174

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ صَالِحٍ، حَدَّثَنِي اللَّيْثُ، حَدَّثَنِي يُونُسُ، عَنْ ابْنِ شِهَابٍ: وَسَأَلْنَاهُ عَنْ السِّقْطِ، فَقَالَ: "لَا يُصَلَّى عَلَيْهِ، وَلَا يُصَلَّى عَلَى مَوْلُودٍ حَتَّى يَسْتَهِلَّ صَارِخًا"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Swaalih, amenisimulia Al-Layth, amenisimulia Yuwnus, kutoka kwa Ibn Shihaab: Na tulimuuliza kuhusu mimba iliyoharibika (mtoto aliyetoka kabla ya kutimia), akasema: "Haswaliwi; wala mtoto aliyezaliwa haswaliwi mpaka alie kwa kupiga ukelele."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2007
Hadiyth
3175

48-Mlangoباب: في ولاء المكاتبMlango Wa Kuhusu Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru) Wa Mukaatab (Mtumwa
Aliyeandikiana Na Bwana Wake Kujikomboa Kwa Malipo)

حَدَّثَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ قَتَادَةَ، قَالَ:" إِذَا ابْتَاعَ الْمُكَاتَبَانِ أَحَدُهُمَا الْآخَرَ: هَذَا هَذَا مِنْ سَيِّدِهِ، وَهَذَا هَذَا مِنْ سَيِّدِهِ، فَالْبَيْعُ لِلْأَوَّلِ. وَيَقُولُ أَهْلُ الْمَدِينَةِ: الْوَلَاءُ لِسَيِّدِ الْبَائِعِ، وَيَقُولُونَ: إِنَّمَا ابْتَاعَ هَذَا مَا عَلَى الْمُكَاتَبِ، فَالْوَلَاءُ لِلسَّيِّدِ

Ametusimulia Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Qataadah, amesema: "Mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo) wawili wanaponunuana, mmoja wao akamnunua mwingine — huyu akamnunua huyu kutoka kwa bwana wake, na huyu akamnunua huyu kutoka kwa bwana wake —, basi mauzo ni ya yule wa kwanza. Na watu wa Madiynah wanasema: Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa bwana wa muuzaji. Na wanasema: Hakika huyu amenunua tu kile kilichokuwa juu ya mukaatab (katika malipo ya kujikomboa kwake), kwa hiyo walaa ni wa bwana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2008
Hadiyth
3176

49-Mlangoباب: في الحر يتزوج الأمةMlango Wa Kuhusu Mtu Huru Anayemuoa Mjakazi

حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ هَارُونَ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ سَعِيدٍ، أَنَّ عُمَرَ، قَالَ:" أَيُّمَا حُرٍّ تَزَوَّجَ أَمَةً، فَقَدْ أَرَقَّ نِصْفَهُ، وَأَيُّمَا عَبْدٍ يَتَزَوَّجُ حُرَّةً، فَقَدْ أَعْتَقَ نِصْفَهُ، قَالَ أَبُو مُحَمَّد: يَعْنِي الْوَلَدَ

Ametusimulia Yaziyd bin Haaruwn, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Sa'iyd, kwamba 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Mtu huru yeyote aliyemuoa mjakazi, basi hakika ameifanya nusu yake kuwa mtumwa; na mtumwa yeyote anayemuoa mwanamke huru, basi hakika ameiacha huru nusu yake."

Abuw Muhammad [Ad-Daarimiy] amesema: Yaani: mtoto.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2009
Hadiyth
3177

50-Mlangoباب: ميراث الولاءMlango Wa Mirathi Ya Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru)

أَخْبَرَنَا أَحْمَدُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا أَبُو شِهَابٍ، عَنْ الشَّيْبَانِيِّ، عَنْ الشَّعْبِيِّ: فِي الْعَبْدِ يَتَزَوَّجُ الْمَرْأَةَ، ثُمَّ يُطَلِّقُهَا وَلَهُ مِنْهَا وَلَدٌ؟ قَالَ: "إِنْ كَانَتْ حُرَّةً، فَالنَّفَقَةُ عَلَى أُمِّهِ، وَإِنْ كَانَ عَبْدًا، يَعْنِي: الصَّبِيَّ، فَعَلَى مُوَالِيهِ"

Ametukhabarisha Ahmad bin 'Abdi-Allaah, ametusimulia Abuw Shihaab, kutoka kwa Ash-Shaybaaniy, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kuhusu mtumwa anayemuoa mwanamke, kisha akamtaliki, naye ana mtoto kutoka kwake? Akasema: "Ikiwa (mwanamke) ni huru, basi matumizi (ya mtoto) ni juu ya mama yake; na ikiwa ni mtumwa — yaani: mtoto mchanga —, basi (matumizi yake) ni juu ya mabwana zake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2009
Hadiyth
3178

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ. وحَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: أَنَّهُمَا قَالَا: "وَلَاؤُهُ لِمَنْ بَدَأَ بِالْعِتْقِ أَوَّلَ مَرَّةٍ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hushaym, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir; na ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, kwamba wao wawili walisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wake ni wa yule aliyeanza kumwacha huru mara ya kwanza."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2010
Hadiyth
3179

51-Mlangoباب: في العبد يكون بين رجلين فيعتق أحدهما نصيبهMlango Wa Kuhusu Mtumwa Anayemilikiwa
Na Watu Wawili, Kisha Mmoja Wao Akaacha Huru Fungu Lake

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا هُشَيْمٌ، أنبأنا يُونُسُ، عَنْ الْحَسَنِ. وحَدَّثَنَا جَرِيرٌ، عَنْ أَبَانَ بْنِ تَغْلِبَ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، أَنَّهُمَا قَالَا: "إِنْ ضَمِنَ، كَانَ الْوَلَاءُ لَهُ، وَإِنْ اسْتَسْعَى الْعَبْدُ، كَانَ الْوَلَاءُ بَيْنَهُمْ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Hushaym, ametupa khabari Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan; na ametusimulia Jariyr, kutoka kwa Abaan bin Taghlib, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym, kwamba wao wawili walisema: "Akidhamini (thamani ya fungu la mwenzake), walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) utakuwa wake; na mtumwa akitakiwa kufanya kazi ya kuchuma (ili ajilipie fungu lililobaki), walaa utakuwa baina yao."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2010
Hadiyth
3180

حَدَّثَنَا يَعْلَى، وَأَبُو نُعَيْمٍ، قَالَا: حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ: فِي عَبْدٍ بَيْنَ رَجُلَيْنِ أَعْتَقَ أَحَدُهُمَا نَصِيبَهُ، فَقَالَ: "يُتَمَّمُ عِتْقُهُ، فَإِنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ مَالٌ، اسْتُسْعِيَ الْعَبْدُ فِي النِّصْفِ بِقِيمَةِ عَدْلٍ، وَالْوَلَاءُ لِمَنْ أَعْتَقَ"

Ametusimulia Ya'laa na Abuw Nu'aym, wamesema: Ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir, kuhusu mtumwa anayemilikiwa na watu wawili, mmoja wao akaacha huru fungu lake, akasema: "Kuachwa huru kwake hukamilishwa (na huyo aliyeacha huru). Na ikiwa hana mali, mtumwa hutakiwa kufanya kazi ya kuchuma (ili ajilipie) nusu (iliyobaki) kwa thamani ya uadilifu; na walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa yule aliyeacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2011
Hadiyth
3181

حَدَّثَنَا هَارُونُ بْنُ مُعَاوِيَةَ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ الْمَعْمَرِيِّ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ ابْنِ طَاوُسٍ، عَنْ أَبِيهِ: فِي عَبْدٍ بَيْنَ رَجُلَيْنِ، أَعْتَقَ أَحَدَهُمَا نَصِيبَهُ وَأَمْسَكَهُ الْآخَرُ، قَالَ: "مِيرَاثُهُ بَيْنَهُمَا"

Ametusimulia Haaruwn bin Mu'aawiyah, kutoka kwa Abuw Sufyaan Al-Ma'mariy, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Ibn Twaawuws, kutoka kwa baba yake, kuhusu mtumwa anayemilikiwa na watu wawili, mmoja wao akaacha huru fungu lake, na mwingine akamshikilia (fungu lake), akasema: "Mirathi yake ni baina yao wawili."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2011
Hadiyth
3182

حَدَّثَنَا هَارُونُ، عَنْ أَبِي سُفْيَانَ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، قَالَ:" مِيرَاثُهُ لِلَّذِي أَمْسَكَهُ. وقال قَتَادَةُ: هُوَ لِلْمُعْتِقِ كُلُّهُ، وَثَمَنُهُ عَلَيْهِ، وَيَقُولُهُ أَهْلُ الْكُوفَةِ

Ametusimulia Haaruwn, kutoka kwa Abuw Sufyaan, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Az-Zuhriy, amesema: "Mirathi yake ni ya yule aliyemshikilia." Na Qataadah amesema: (Mirathi) yote ni ya aliyeacha huru, na thamani yake (ya fungu la mwenzake) ni juu yake. Na hivyo ndivyo wanavyosema watu wa Al-Kuwfah.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2012
Hadiyth
3183

52-Mlangoباب: ما للنساء من الولاءMlango Wa Yale Wanayostahiki Wanawake
Katika Walaa (Haki Ya Urithi Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru)

حَدَّثَنَا يَعْلَى بْنُ عُبَيْدٍ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءٍ: فِي الرَّجُلِ يَمُوتُ وَيَتْرُكُ مُكَاتَبًا، وَلَهُ بَنُونَ وَبَنَاتٌ، أَيَكُونُ لِلنِّسَاءِ مِنْ الْوَلَاءِ شَيْءٌ؟ قَالَ: "تَرِثُ النِّسَاءُ مِمَّا عَلَى ظَهْرِهِ مِنْ مُكَاتَبَتِهِ، وَيَكُونُ الْوَلَاءُ لِلرِّجَالِ دُونَ النِّسَاءِ، إِلَّا مَا كَاتَبْنَ، أَوْ أَعْتَقْنَ"

Ametusimulia Ya'laa bin 'Ubayd, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa, kuhusu mtu anayefariki na kuacha mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo), naye ana watoto wa kiume na wa kike: Je, wanawake wana chochote katika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru)? Akasema: "Wanawake hurithi katika kile kilichobaki juu ya mgongo wake (kama deni) katika malipo ya kujikomboa kwake; na walaa huwa wa wanaume pasipo wanawake, isipokuwa wale ambao wao (wanawake) wameandikiana nao (kujikomboa), au waliowaacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2012
Hadiyth
3184

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا شَرِيكٌ، عَنْ لَيْثٍ، عَنْ طَاوُسٍ، قَالَ: "لَا تَرِثُ النِّسَاءُ مِنْ الْوَلَاءِ إِلَّا مَا أَعْتَقْنَ، أَوْ أَعْتَقَ مَنْ أَعْتَقْنَ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Shariyk, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Twaawuws, amesema: "Wanawake hawarithi katika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) isipokuwa wale waliowaacha huru, au aliyeachwa huru na yule waliyemwacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2013
Hadiyth
3185

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا أَبُو سُفْيَانَ، عَنْ مَعْمَرٍ، عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ، قَالَ: "تُوُفِّيَ رَجُلٌ وَتَرَكَ مُكَاتَبًا، ثُمَّ مَاتَ الْمُكَاتَبُ وَتَرَكَ مَالًا، فَجَعَلَ ابْنُ الْمُسَيَّبِ، وَأَبُو سَلَمَةَ بْنُ عَبْدِ الرَّحْمَنِ مَا بَقِيَ مِنْ مُكَاتَبَتِهِ بَيْنَ بَنِي مَوْلَاهُ الرِّجَالُ وَالنِّسَاءُ عَلَى مِيرَاثِهِمْ، وَمَا فَضَلَ مِنْ الْمَالِ بَعْدَ كِتَابَتِهِ، فَلِلرِّجَالِ مِنْهُمْ مِنْ بَنِي مَوْلَاهُ، دُونَ النِّسَاءِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Abuw Sufyaan, kutoka kwa Ma'mar, kutoka kwa Yahyaa bin Abiy Kathiyr, amesema: "Mtu mmoja alifariki akaacha mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo); kisha mukaatab akafa akaacha mali. Ibn Al-Musayyib na Abuw Salamah bin 'Abdir-Rahmaan wakakifanya kilichobaki katika malipo ya kujikomboa kwake kuwa baina ya watoto wa bwana wake — wanaume na wanawake — kwa mujibu wa mirathi yao; na kilichozidi katika mali baada ya malipo ya kujikomboa kwake, ni cha wanaume miongoni mwao katika watoto wa bwana wake, pasipo wanawake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2013
Hadiyth
3186

أَخْبَرَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ السَّلَامِ بْنُ حَرْبٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، عَنْ عُمَرَ، وَعَلِيٍّ، وَزَيْدٍ، أَنَّهُمْ قَالُوا: "الْوَلَاءُ لِلْكُبْرِ، وَلَا يُوَرِّثُونَ النِّسَاءَ مِنْ الْوَلَاءِ إِلَّا مَا أَعْتَقْنَ، أَوْ كَاتَبْنَ"

Ametukhabarisha Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia 'Abdus-Salaam bin Harb, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, kutoka kwa 'Umar, na 'Aliy, na Zayd (رضي الله عنهم), kwamba wao walisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa al-kubr (aliye karibu zaidi kwa nasaba na aliyeacha huru); na hawawarithishi wanawake katika walaa isipokuwa wale waliowaacha huru, au walioandikiana nao (kujikomboa)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2013
Hadiyth
3187

حدثنا محمد بن عيسى، حدثنا إسماعيل بن إبراهيم، عن خالد، عن أبي قلابة،

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Ismaa'iyl bin Ibraahiym, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Abuw Qilaabah,

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2014
Hadiyth
3188

وحدثنا ابن وهب، عن يونس، عن الزهري، عن سعيد بن المسيب،

Na ametusimulia Ibn Wahb, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Sa'iyd bin Al-Musayyib,

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2014
Hadiyth
3189

وحَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي الزِّنَادِ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ سُلَيْمَانَ بْنِ يَسَارٍ: أَنَّهُمْ قَالُوا: "لَا تَرِثُ النِّسَاءُ مِنْ الْوَلَاءِ إِلَّا مَا أَعْتَقْنَ، أَوْ كَاتَبْنَ"

Na ametusimulia Ibn Abiz-Zinaad, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sulaymaan bin Yasaar, kwamba wao walisema: "Wanawake hawarithi katika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) isipokuwa wale waliowaacha huru, au walioandikiana nao (kujikomboa)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2015
Hadiyth
3190

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، عن مُعَاذٌ، عَنْ الْأَشْعَثِ، عَنْ الْحَسَنِ، قَالَ: "لَا تَرِثُ النِّسَاءُ مِنْ الْوَلَاءِ إِلَّا مَا أَعْتَقْنَ، أَوْ أَعْتَقَ مَنْ أَعْتَقْنَ، إِلَّا الْمُلَاعَنَةُ، فَإِنَّهَا تَرِثُ مَنْ أَعْتَقَ ابْنُهَا الَّذِي انْتَفَى مِنْهُ أَبُوهُ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, kutoka kwa Mu'aadh, kutoka kwa Al-Ash'ath, kutoka kwa Al-Hasan, amesema: "Wanawake hawarithi katika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) isipokuwa wale waliowaacha huru, au aliyeachwa huru na yule waliyemwacha huru; isipokuwa mwanamke aliyelaaniana na mumewe, kwani yeye hurithi aliyeachwa huru na mwanawe ambaye baba yake amemkana."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2015
Hadiyth
3191

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِيسَى، حَدَّثَنَا ابْنُ وَهْبٍ، عَنْ يُونُسَ، عَنْ الزُّهْرِيِّ، عَنْ سَالِمٍ، عَنْ أَبِيهِ: أَنَّهُ كَانَ "يَرِثُ مَوَالِيَ عُمَرَ دُونَ بَنَاتِ عُمَرَ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Iysaa, ametusimulia Ibn Wahb, kutoka kwa Yuwnus, kutoka kwa Az-Zuhriy, kutoka kwa Saalim, kutoka kwa baba yake [Ibn 'Umar (رضي الله عنهما)], kwamba yeye "alikuwa akiwarithi waachwa huru wa 'Umar (رضي الله عنه) pasipo mabinti wa 'Umar (رضي الله عنه)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2015
Hadiyth
3192

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَوْنٍ، عَنْ خَالِدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ، عَنْ خَالِدٍ الْحَذَّاءِ، عَنْ أَبِي قِلَابَةَ فِي امْرَأَةٍ مَاتَتْ، وَتَرَكَتْ بَنِيهَا، فَوَرِثُوهَا مَالًا وَمَوَالِيَ، ثُمَّ مَاتَ بَنُوهَا، قَالَ: "يَرْجِعُ الْوَلَاءُ إِلَى عَصَبَةِ الْمَرْأَةِ"

Ametukhabarisha 'Amr bin 'Awn, kutoka kwa Khaalid bin 'Abdi-Allaah, kutoka kwa Khaalid Al-Hadhdhaa, kutoka kwa Abuw Qilaabah, kuhusu mwanamke aliyefariki akawaacha wanawe (wa kiume), wakamrithi mali na waachwa huru, kisha wanawe wakafa; akasema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) hurudi kwa 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wa mwanamke."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2015
Hadiyth
3193

حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ، عَنْ إِسْرَائِيلَ، عَنْ مَنْصُورٍ، قَالَ: سَأَلْتُ إِبْرَاهِيمَ عَنْ رَجُلٍ كَاتَبَ عَبْدًا لَهُ، ثُمَّ مَاتَ وَتَرَكَ وَلَدًا رِجَالًا وَنِسَاءً، قَالَ: "لِلذُّكُورِ دُونَ الْإِنَاثِ"

Ametusimulia 'Ubaydu-Allaah, kutoka kwa Israaiyl, kutoka kwa Manswuwr, amesema: Nilimuuliza Ibraahiym kuhusu mtu aliyeandikiana na mtumwa wake (kujikomboa kwa malipo), kisha akafa akaacha watoto, wanaume na wanawake; akasema: "(Walaa) ni wa wanaume pasipo wanawake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2016
Hadiyth
3194

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، حَدَّثَنَا وُهَيْبٌ، حَدَّثَنَا يُونُسُ، عَنْ الْحَسَنِ، أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ فِي امْرَأَةٍ مَاتَتْ وَتَرَكَتْ مَوْلًى، قَالَ: "الْوَلَاءُ لِبَنِيهَا، فَإِذَا مَاتُوا، رَجَعَ إِلَى عَصَبَتِهَا"

Ametusimulia Abun-Nu'maan, ametusimulia Wuhayb, ametusimulia Yuwnus, kutoka kwa Al-Hasan, kwamba alikuwa akisema kuhusu mwanamke aliyefariki akaacha mwachwa huru, akasema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni wa wanawe (wa kiume); wakifa, hurudi kwa 'asabah (jamaa wa kiume wa upande wa baba) wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2016
Hadiyth
3195

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، أَخْبَرَنَا شُعْبَةُ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ قَالَ: "لَيْسَ لِلنِّسَاءِ مِنْ الْوَلَاءِ شَيْءٌ، إِلَّا مَا أَعْتَقَتْ هِيَ فيَ نَفْسِهَا"

Ametusimulia Sa'iyd bin 'Aamir, ametukhabarisha Shu'bah, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Wanawake hawana chochote katika walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru), isipokuwa yule ambaye yeye mwenyewe (mwanamke) amemwacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2016
Hadiyth
3196

حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ عَامِرٍ، عَنْ ابْنِ عَوْنٍ، عَنْ مُحَمَّدٍ، قَالَ: مَاتَ مَوْلًى لِعُمَرَ، فَسَأَلَ ابْنُ عُمَرَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ، فَقَالَ: هَلْ لِبَنَاتِ عُمَرَ مِنْ مِيرَاثِهِ شَيْءٌ؟ قَالَ: "مَا أَرَى لَهُنَّ شَيْئًا، وَإِنْ شِئْتَ أَنْ تُعْطِيَهُنَّ، أَعْطَيْتَهُنَّ"

Ametusimulia Sa'iyd bin 'Aamir, kutoka kwa Ibn 'Awn, kutoka kwa Muhammad, amesema: Mwachwa huru wa 'Umar (رضي الله عنه) alikufa; Ibn 'Umar (رضي الله عنهما) akamuuliza Zayd bin Thaabit (رضي الله عنه), akasema: Je, mabinti wa 'Umar (رضي الله عنه) wana chochote katika mirathi yake? Akasema: "Sioni kuwa wana chochote; na ukitaka kuwapa, wape."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2017
Hadiyth
3197

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، عَنْ هِشَامٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "يُحْرِزُ الْوَلَاءَ مَنْ يُحْرِزُ الْمِيرَاثَ"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Usaamah, kutoka kwa Hishaam, kutoka kwa baba yake, amesema: "Anayechukua walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni yule anayechukua mirathi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2017
Hadiyth
3198

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا أَبُو خَالِدٍ، حَدَّثَنَا يَحْيَى، عَنْ أَبِي بَكْرِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ: "أَنَّ امْرَأَةً مِنْ مُحَارِبٍ وَهَبَتْ وَلَاءَ عَبْدِهَا لِنَفْسِهِ، فَأَعْتَقَتْهُ، فَوَهَبَ وَلاءَ نَفْسِهِ لِعَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ، وَمَاتَتْ، فَخَاصَمَتِ الْمَوَالِيَ إِلَى عُثْمَانَ، فَدَعَا عُثْمَانُ الْبَيِّنَةَ عَلَى مَا قَالَ، قَالَ: فَأَتَى الْبَيِّنَةُ، فَقَالَ لَهُ عُثْمَانُ: اذْهَبْ، فَوَالِ مَنْ شِئْتَ". قَالَ أَبُو بَكْرٍ: فَوَالَى عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ عَمْرِو بْنِ حَزْمٍ

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Abuw Khaalid, ametusimulia Yahyaa, kutoka kwa Abuw Bakr bin 'Amr bin Hazm: "Kwamba mwanamke mmoja wa (kabila la) Muhaarib alimtunukia mtumwa wake walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wake mwenyewe, kisha akamwacha huru. Naye (huyo mtumwa) akamtunukia 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr bin Hazm walaa wa nafsi yake; na (yule mwanamke) akafa. Jamaa zake (wenye walaa) wakashtakiana kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه). 'Uthmaan (رضي الله عنه) akataka ushahidi juu ya aliyoyasema. Akasema: Akaleta ushahidi. 'Uthmaan (رضي الله عنه) akamwambia: Nenda, ukafanye walaa na yeyote umtakaye." Abuw Bakr amesema: Basi akafanya walaa na 'Abdur-Rahmaan bin 'Amr bin Hazm.

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2017
Hadiyth
3199

53-Mlangoباب: بيع الولاءMlango Wa Kuuza Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru)

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ دِينَارٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ، قَالَ: "نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ بَيْعِ الْوَلَاءِ، وَعَنْ هِبَتِهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما), amesema: "Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuuza walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru), na kuutoa zawadi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3200

حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ دِينَارٍ، عَنْ ابْنِ عُمَرَ: "أَنّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْ بَيْعِ الْوَلَاءِ، وَعَنْ هِبَتِهِ"

Ametusimulia Muslim, ametusimulia Shu'bah, ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Diynaar, kutoka kwa Ibn 'Umar (رضي الله عنهما): "Kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikataza kuuza walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru), na kuutoa zawadi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3201

حَدَّثَنَا يَعْلَى، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْمَلِكِ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: سَمِعْتُ ابْنَ عَبَّاسٍ، يَقُولُ: "لَا يُبَاعُ الْوَلَاءُ وَلَا يُوهَبُ، وَالْوَلَاءُ لِمَنْ أَعْتَقَ"

Ametusimulia Ya'laa, ametusimulia 'Abdul-Malik, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: Nilimsikia Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) akisema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) hauuzwi wala hautolewi zawadi; na walaa ni wa aliyeacha huru."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3202

حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ سَعِيدٍ، عَنْ أَبِي مَعْشَرٍ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عَبْدُ اللَّهِ: "الْوَلَاءُ لُحْمَةٌ كَلُحْمَةِ النَّسَبِ، لَا يُبَاعُ وَلَا يُوهَبُ"

Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Sa'iyd, kutoka kwa Abuw Ma'shar, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Abdu-Allaah [bin Mas'uwd] (رضي الله عنه) amesema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) ni fungamano kama fungamano la nasaba; hauuzwi wala hautolewi zawadi."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3203

حَدَّثَنَا مُسْلِم، حَدَّثَنَا هَمَّامٌ، حَدَّثَنَا قَتَادَةُ، عَنْ الْحَسَنِ، وَسَعِيدِ بْنِ الْمُسَيِّبِ: "أَنَّهُمَا كَرِهَا بَيْعَ الْوَلَاءِ"

Ametusimulia Muslim, ametusimulia Hammaam, ametusimulia Qataadah, kutoka kwa Al-Hasan na Sa'iyd bin Al-Musayyib: "Kwamba wao wawili walichukia kuuza walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3204

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ سَعِيدٍ، حَدَّثَنَا ابْنُ إِدْرِيسَ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، قَالَ: قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ: "لَا يُبَاعُ الْوَلَاءُ، أَيُؤْكَلُ بِرَقَبَةِ رَجُلٍ مَرَّتَيْنِ؟"

Ametusimulia 'Abdu-Allaah bin Sa'iyd, ametusimulia Ibn Idriys, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa, amesema: Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: "Walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) hauuzwi. Je, (mtu) atakula kwa shingo ya mtu mara mbili?"

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2018
Hadiyth
3205

54-Mlangoباب: في عول الفرائضMlango Wa Kuhusu 'Awl (Kuongezwa
Kwa Asili Ya Mgawanyo Wa Mirathi Mafungu Yanapozidi Mali)
Katika Faraaidh (Mafungu Ya Mirathi Yaliyowekwa)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنْ ابْنِ جُرَيْجٍ، عَنْ عَطَاءٍ، عَنْ ابْنِ عَبَّاسٍ، قَالَ: "الْفَرَائِضُ مِنْ سِتَّةٍ، لَا نُعِيلُهَا"

Ametusimulia Muhammad bin Yuwsuf, ametusimulia Sufyaan, kutoka kwa Ibn Jurayj, kutoka kwa 'Atwaa, kutoka kwa Ibn 'Abbaas (رضي الله عنهما), amesema: "Faraaidh (mafungu ya mirathi yaliyowekwa) ni kutokana na sita; hatuyafanyii 'awl (kuongezwa kwa asili ya mgawanyo wa mirathi mafungu yanapozidi mali)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2020
Hadiyth
3206

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عِمْرَانَ، عَنْ مُعَاوِيَةَ بْنِ مَيْسَرَةَ بْنِ شُرَيْحٍ، عَنْ شريح بْنِ الْحَارِثِ، قَالَ: "اخْتُصِمَ إِلَى شُرَيْحٍ فِي بِنْتَيْنِ، وَأَبَوَيْنِ، وَزَوْجٍ، فَقَضَى فِيهَا، فَأَقْبَلَ الزَّوْجُ يَشْكُوهُ فِي الْمَسْجِدِ، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ رَبَاحٍ فَأَخَذَهُ، وَبَعَثَ إِلَى شُرَيْحٍ، فَقَالَ: مَا تَقُولُ فِي هَذَا؟ قَالَ: هَذَا يَخَالُنِي امْرَءًا جَائِرًا، وَأَنَا إِخَالُهُ امْرَءًا فَاجِرًا، يُظْهِرُ الشَّكْوَى وَيَكْتُمُ قَضَاءً سَائِرًا، فَقَالَ لَهُ الرَّجُلُ: مَا تَقُولُ فِي بِنْتَيْنِ، وَأَبَوَيْنِ، وَزَوْجٍ؟ فَقَالَ: لِلزَّوْجِ الرُّبُعُ مِنْ جَمِيعِ الْمَالِ، وَلِلْأَبَوَيْنِ السُّدُسَانِ، وَمَا بَقِيَ فَلِلِابْنَتَيْنِ، فَلِأَيِّ شَيْءٍ نَقَصْتَنِي؟ قَالَ: لَيْسَ أَنَا نَقَصْتُكَ، اللَّهُ نَقَصَكَ، لِلِابْنَتَيْنِ الثُّلُثَانِ، وَلِلْأَبَوَيْنِ السُّدُسَانِ، وَلِلزَّوْجِ الرُّبُعُ، فَهِيَ مِنْ سَبْعَةٍ وَنِصْفٍ فَرِيضَةً، فَرِيضَتُكَ عَائِلَةٌ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Imraan, kutoka kwa Mu'aawiyah bin Maysarah bin Shurayh, kutoka kwa Shurayh bin Al-Haarith, amesema: Kesi ilipelekwa kwa Shurayh kuhusu mabinti wawili, na wazazi wawili, na mume; akahukumu kuhusu hilo. Mume akaja akimshtaki Msikitini. Akamtumia 'Abdu-Allaah bin Rabaah, akamkamata; na akatuma (mjumbe) kwa Shurayh, akasema: Unasemaje kuhusu huyu? Akasema: Huyu ananidhania kuwa mtu dhalimu, nami ninamdhania kuwa mtu muovu: anadhihirisha malalamiko na anaficha hukmu iliyoenea (inayojulikana kwa watu). Yule mtu akamwambia: Unasemaje kuhusu mabinti wawili, na wazazi wawili, na mume? Akasema: Mume ana robo ya mali yote, na wazazi wawili wana sudusi mbili, na kinachobaki ni cha mabinti wawili; basi kwa sababu gani umenipunguzia? Akasema: Si mimi niliyekupunguzia; Allaah Ndiye Aliyekupunguzia. Mabinti wawili wana theluthi mbili, na wazazi wawili wana sudusi mbili, na mume ana robo; basi hiyo ni (mirathi yenye mgawanyo wa) mafungu saba na nusu; mgawanyo wako ni wenye 'awl (kuongezwa kwa asili ya mgawanyo wa mirathi mafungu yanapozidi mali).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2020
Hadiyth
3207

55-Mlangoباب: جر الولاءMlango Wa Kuvuta Walaa (Haki Ya Urithi
Kwa Sababu Ya Kumwacha Huru)

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، عَنْ عَلِيٍّ، وَعُمَرَ، وَزَيْدٍ، قَالُوا: "الْوَالِدُ يَجُرُّ وَلَاءَ وَلَدِهِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, kutoka kwa 'Aliy, na 'Umar, na Zayd (رضي الله عنهم), wamesema: "Mzazi (baba) huvuta walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wa mtoto wake (kuuhamishia kwake)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2022
Hadiyth
3208

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ الشَّعْبِيِّ، قَالَ: "الْجَدُّ يَجُرُّ الْوَلَاءَ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ash-Sha'biy, amesema: "Babu huvuta walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2022
Hadiyth
3209

حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عُيَيْنَةَ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ مُسْهِرٍ، عَنْ أَشْعَثَ، عَنْ ابْنِ سِيرِينَ، عَنْ شُرَيْحٍ، قَالَ: "الْوَالِدُ يَجُرُّ وَلَاءَ وَلَدِهِ"

Ametusimulia Muhammad bin 'Uyaynah, kutoka kwa 'Aliy bin Mus-hir, kutoka kwa Ash'ath, kutoka kwa Ibn Siyriyn, kutoka kwa Shurayh, amesema: "Mzazi (baba) huvuta walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wa mtoto wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2022
Hadiyth
3210

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا زَكَرِيَّا، عَنْ عَامِرٍ: "فِي مَمْلُوكٍ تُوُفِّيَ وَلَهُ أَبٌ حُرٌّ، وَلَهُ بَنُونَ مِنْ امْرَأَةٍ حُرَّةٍ، لِمَنْ وَلَاءُ وَلَدِهِ؟ قَالَ: لِمَوَالِي الْجَدِّ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Zakariyyaa, kutoka kwa 'Aamir: "Kuhusu mtumwa aliyefariki, naye ana baba aliye huru, na ana watoto wa kiume kutoka kwa mwanamke huru: walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wa watoto wake ni wa nani? Akasema: Ni wa mabwana (walioacha huru) wa babu."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2022
Hadiyth
3211

حَدَّثَنَا أَبُو نُعَيْمٍ، حَدَّثَنَا إِسْرَائِيلُ، عَنْ مُغِيرَةَ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ: "فِي مُكَاتَبٍ مَاتَ وَقَدْ أَدَّى نِصْفَ مُكَاتَبَتِهِ، وَلَهُ وَلَدٌ مِنْ امْرَأَةٍ حُرَةٍ، قَالَ: مَا أُرَاهُ إِلَّا قَدْ جَرَّ وَلَاءَ وَلَدِهِ"

Ametusimulia Abuw Nu'aym, ametusimulia Israaiyl, kutoka kwa Mughiyrah, kutoka kwa Ibraahiym: "Kuhusu mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo) aliyekufa naye ameshalipa nusu ya malipo ya kujikomboa kwake, na ana mtoto kutoka kwa mwanamke huru, akasema: Sioni ila kwamba ameshavuta walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wa mtoto wake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2022
Hadiyth
3212

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ الْحَكَمِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: "كَانَ شُرَيْحٌ لَا يَرْجِعُ عَنْ قَضَاءٍ يَقْضِي بِهِ، فَحَدَّثَهُ الْأَسْوَدُ: أَنَّ عُمَرَ، قَالَ: إِذَا تَزَوَّجَ الْمَمْلُوكُ الْحُرَّةَ، فَوَلَدَتْ أَوْلَادًا أَحْرَارًا، ثُمَّ عُتِقَ بَعْدَ ذَلِكَ، رَجَعَ الْوَلَاءُ لِمَوَالِي أَبِيهِمْ"، فَأَخَذَ بِهِ شُرَيْحٌ

Ametusimulia Sulaymaan bin Harb, ametusimulia Shu'bah, kutoka kwa Al-Hakam, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: "Shurayh alikuwa harudi nyuma kutoka katika hukmu anayoihukumu. Al-Aswad akamsimulia kwamba 'Umar (رضي الله عنه) amesema: Mtumwa anapomuoa mwanamke huru, naye akazaa watoto walio huru, kisha (mtumwa huyo) akaachwa huru baada ya hapo, walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) hurudi kwa mabwana (walioacha huru) wa baba yao." Basi Shurayh akaichukua (kauli hiyo).

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2023
Hadiyth
3213

حَدَّثَنَا يَعْلَى، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عُمَر: "فِي الْمَمْلُوكِ يَكُونُ تَحْتَهُ الْحُرَّةُ، يُعْتَقُ الْوَلَدُ بِعِتْقِ أُمِّهِ، فَإِذَا عُتِقَ الْأَبُ، جَرَّ الْوَلَاءَ"

Ametusimulia Ya'laa, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema, kuhusu mtumwa ambaye ana mke aliye huru: "Mtoto huachwa huru kwa kuachwa huru kwa mama yake; na baba akiachwa huru, huvuta walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2024
Hadiyth
3214

حَدَّثَنَا مُسْلِمٌ، حَدَّثَنَا عَبْدُ الْوَارِثِ، عَنْ كَثِيرِ بْنِ شِنْظِيرٍ، عَنْ عَطَاءٍ: "فِي الْحُرَّةِ تَحْتَ الْعَبْدِ، قَالَ: أَمَّا مَا وَلَدَتْ مِنْهُ وَهُوَ عَبْدٌ، فَوَلَاؤُهُمْ لِأَهْلِ نِعْمَتِهَا، وَمَا وَلَدَتْ مِنْهُ وَهُوَ حُرٌّ، فَوَلَاؤُهُمْ لِأَهْلِ نِعْمَتِهِ"

Ametusimulia Muslim, ametusimulia 'Abdul-Waarith, kutoka kwa Kathiyr bin Shindhwiyr, kutoka kwa 'Atwaa: "Kuhusu mwanamke huru aliyeolewa na mtumwa, akasema: Ama wale aliowazaa kutoka kwake naye (baba) akiwa mtumwa, basi walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wao ni wa waliomfanyia (mama) neema (ya kumwacha huru); na wale aliowazaa kutoka kwake naye akiwa huru, basi walaa wao ni wa waliomfanyia (baba) neema (ya kumwacha huru)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2024
Hadiyth
3215

حَدَّثَنَا جَعْفَرُ بْنُ عَوْنٍ، عَنْ الْأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ، قَالَ: قَالَ عُمَرُ: "إِذَا كَانَتْ الْحُرَّةُ تَحْتَ الْمَمْلُوكِ، فَوَلَدَتْ لَهُ غُلَامًا، فَإِنَّهُ يُعْتَقُ بِعِتْقِ أُمِّهِ، وَوَلَاؤُهُ لِمَوَالِي أُمِّهِ، فَإِذَا أُعْتِقَ الْأَبُ، جَرَّ الْوَلَاءَ إِلَى مَوَالِي أَبِيهِ"

Ametusimulia Ja'far bin 'Awn, kutoka kwa Al-A'mash, kutoka kwa Ibraahiym, amesema: 'Umar (رضي الله عنه) amesema: "Mwanamke huru anapokuwa ameolewa na mtumwa, akamzalia mtoto wa kiume, basi (mtoto) huyo huachwa huru kwa kuachwa huru kwa mama yake, na walaa (haki ya urithi kwa sababu ya kumwacha huru) wake ni wa mabwana (walioacha huru) wa mama yake. Na baba akiachwa huru, huvuta walaa kwenda kwa mabwana (walioacha huru) wa baba yake."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2025
Hadiyth
3216

حَدَّثَنَا الْحَكَمُ بْنُ الْمُبَارَكِ، حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ سَلَمَةَ، عَنْ ابْنِ إِسْحَاق، عَنْ الْعَلَاءِ بْنِ عَبْدِ الرَّحْمَنِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: "كَانَتْ أُمِّي مَوْلَاةً لِلْحُرَقَةِ، وَكَانَ أَبِي يَعْقُوبُ مُكَاتَبًا لِمَالِكِ بْنِ أَوْسِ بْنِ الْحَدَثَانِ النَّصْرِيِّ، ثُمَّ إِنَّ أَبِي أَدَّى كِتَابَتَهُ، فَدَخَلَ الْحُرَقِيُّ عَلَى عُثْمَانَ، فَسَأَلَ لِي الْحَقَّ يَعْنِي: الْعَطَاءَ، وَعِنْدَهُ مَالِكُ بْنُ أَوْسٍ، فَقَالَ: ذَاكَ مَوْلَايَ، فَاخْتَصَمَا إِلَى عُثْمَانَ، فَقَضَى بِهِ لِلْحُرَقِيِّ"

Ametusimulia Al-Hakam bin Al-Mubaarak, ametusimulia Muhammad bin Salamah, kutoka kwa Ibn Is-haaq, kutoka kwa Al-'Alaa bin 'Abdir-Rahmaan, kutoka kwa baba yake, amesema: "Mama yangu alikuwa mwachwa huru wa (ukoo wa) Al-Huraqah, na baba yangu Ya'quwb alikuwa mukaatab (mtumwa aliyeandikiana na bwana wake kujikomboa kwa malipo) wa Maalik bin Aws bin Al-Hadathaan An-Naswriy. Kisha baba yangu akalipa malipo ya kujikomboa kwake. Al-Huraqiy akaingia kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه), akaniombea haki — yaani: posho (inayotolewa na watawala) —, na kwake alikuwepo Maalik bin Aws; akasema: Huyo ni mwachwa huru wangu. Wakashtakiana kwa 'Uthmaan (رضي الله عنه), akahukumu kuwa yeye ni wa Al-Huraqiy."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2025
Hadiyth
3217

56-Mlangoباب: الرجل يموت ولا يدع عصبةMlango Wa Mtu Anayekufa
Na Hakuacha 'Asabah (Jamaa Wa Kiume Wa Upande Wa Baba)

أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يَزِيدَ، حَدَّثَنَا حَيْوَةُ، أَخْبَرَنِي سَهْمُ بْنُ يَزِيدَ الْحَمْرَاوِيُّ: "أَنَّ رَجُلًا تُوُفِّيَ وَلَيْسَ لَهُ وَارِثٌ، فَكُتِبَ فِيهِ إِلَى عُمَرَ بْنِ عَبْدِ الْعَزِيزِ وَهُوَ خَلِيفَةٌ، فَكَتَبَ: أَنْ قَسِّمُوا مِيرَاثَهُ عَلَى مَنْ كَانَ يَأْخُذُ مَعَهُمْ الْعَطَاءَ، فَقُسِمَ مِيرَاثُهُ عَلَى مَنْ كَانَ يَأْخُذُ مَعَهُمْ الْعَطَاءَ فِي عِرَافَتِهِ"

Ametukhabarisha 'Abdu-Allaah bin Yaziyd, ametusimulia Haywah, amenikhabarisha Sahm bin Yaziyd Al-Hamraawiy: "Kwamba mtu mmoja alifariki naye hana mrithi. Pakaandikwa kuhusu yeye kwa 'Umar bin 'Abdil-'Aziyz — naye alikuwa Khaliyfah —, akaandika: Igaweni mirathi yake kwa wale waliokuwa wakichukua posho (inayotolewa na watawala) pamoja nao. Basi mirathi yake ikagawanywa kwa wale waliokuwa wakichukua posho pamoja nao katika kikundi chake (cha watu walio chini ya msimamizi mmoja)."

Mjalada
4
Kitabu
21
Ukurasa
2026
Hadiyth
3218