Skip to main content
⌂
Alhidaaya.com homepage
slogan image
  • Log in

left sidebar menu

  • Qur-aan
  • Hadiyth
  • Sunnah
  • Tawhiyd
  • Aqiydah
  • Manhaj
  • Shirki & Kufru
  • Bid-'ah (Uzushi)
  • Salaf Wa Ummah
  • Firaq-Makundi
  • Fiqh-Ibaadah
  • Duaa-Adhkaar
  • Fataawa Za Ulamaa
  • Kauli Za Salaf
  • Akhlaaq-Aadaab
  • Raqaaiq
  • Familia-Jamii
  • Maswali-Majibu
  • Chemsha Bongo
  • Vitabu
  • Mapishi

16-Malaika: Mbawa Za Malaika

Malaika

Alhidaaya.com

16:  Mbawa Za Malaika

 

Allaah Ta’aalaa Anasema:

"الْحَمْدُ لِلَّـهِ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚ يَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ"

“AlhamduliLLahi (Himdi Anastahiki Allaah), Muanzilishi wa mbingu na ardhi, Mwenye Kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbili-mbili, tatu-tatu na nne-nne. Huzidisha katika uumbaji Atakavyo.  Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu”.  [Faatwir: 01]

Ibn Kathiyr amesema:  “Kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wengine tatu tatu, wengine nne nne, na wengine zaidi ya hapo.   Huzitumia kuruka haraka ili kwenda kufikisha yale waliyotumwa na Allaah kuyafikisha au kuyafanya, au kutekeleza jukumu lolote walilokalifishwa”.

‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (Radhwiya Allaah ‘anhu) amesema kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona Jibriyl akiwa na mbawa mia sita”.

Toka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu), Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"إِذَا قَضَى اللَّهُ فِي السَّمَاءِ أَمْرًا ضَرَبَتِ الْمَلاَئِكَةُ بِأَجْنِحَتِهَا خُضْعَانًا لِقَوْلِهِ كَأَنَّهُ سِلْسِلَةٌ عَلَى صَفْوَانٍ فَإِذَا فُزِّعَ عَنْ قُلُوبِهِمْ قَالُوا مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ قَالُوا الْحَقَّ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ"

“Allaah Anapopitisha amri mbinguni, Malaika Hupiga mbawa zao kwa ajili ya kulitii Neno Lake ambalo ni kama sauti ya mnyororo (unaoburutwa) juu ya mwamba.  Na fazaiko linapoondoka nyoyoni mwao huuliza:  Nini Amesema Mola wenu?  (Malaika wabebao ‘Arshi) hujibu:  Ni haki, Naye Ni Mwenye ‘Uluwa,  Mkubwa wa dhati, vitendo na sifa”.  [Hadiyth Swahiyh.  Al-Bukhaariy (4800)]

Kwa haya, tunapata kujua kwamba kuna Malaika wenye mbawa mbili mbili, wenye tatu tatu, wenye nne nne na wenye zaidi ya hapo.  Jibriyl pekee ameelezewa kuwa anazo mia sita, na wengineo kama wabebao ‘Arshi, Miykaaiyl na Israafiyl hakuna ajuaye isipokuwa Allaah Pekee.


Book traversal links for Malaika

  • ‹ 15-Malaika: Je, Tunaweza Kuwaona Malaika Katika Umbile Lao Halisi?
  • Up
  • 17-Malaika: Je, Malaika Wana Sifa Ya Uzuri Wa Sura Na Umbo? ›
moon-icon

Mafunzo Katika Miezi Ya Hijri Ya Kutekeleza Na Ya Kujiepusha

  • Muharram
    image
    مُحَرَّمْ
  • Swafar
    image
    صَفَرْ
  • Rabiy’u Al-Awwal
    Rabiy’u Al-Awwal
    رَبيعُ الْأَوًّلْ
  • Rabiy'u Al-Aakhir
    Rabiy'u Al-Aakhir
    رَبيعُ الآخِرْ
  • Jumaadaa Al-Uwlaa
    image
    جُمَادَى الْأُوْلَى
  • Jumaadaa Al-Aakhirah
    image
    جُمَادَى الْآخِرَة
  • Rajab
    image
    رَجَبْ
  • Sha'baan
    Shabaan
    شَعْبَانْ
  • Ramadhwaan
    iocn
    رَمَضَانْ
  • Shawwaal
    image
    شَوّالْ
  • Dhul-Qa’dah
    image
    ذُو الْقَعْدَةْ
  • Dhul-Hijjah
    icon
    ذُو الحِجَّةْ
Alhidaaya.com homepage
  • Kuhusu Alhidaaya
  • Maoni Yako-Wasiliana Na sisi (Contact Us)
  • Tovuti Muhimu

© 2026 Alhidaaya.com All rights reserved.