Kauli Za Salaf: Taqwa-Ikhlaasw
Mambo Mawili Utakapoyatenda Utapata Khayr Ya Dunia Na Aakhirah
Imaam Salamah bin Diynaar (Rahimahu Allaah)
Imaam Salamah bin Diynaar (Rahimahu Allaah) amesema:
“Mambo mawili utakapoyatenda, utapata khayr ya dunia na Aakhirah:
Unakifanya kile unachokichukia… ikiwa Allaah Anakipenda
Unakiacha kile unachokipenda… ikiwa Allaah Anakichukia.”
[Al-Ma’rifatu Wat-Taariykh, mj. 1, uk. 381]