Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

 

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

041-Asbaabun-Nuzuwl Fusw-Swilat Aayah 22

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ وَلَا جُلُودُكُمْ وَلَـٰكِن ظَنَنتُمْ أَنَّ اللَّـهَ لَا يَعْلَمُ كَثِيرًا مِّمَّا تَعْمَلُونَ﴿٢٢﴾

Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu, na wala ngozi zenu; lakini mlidhania kwamba Allaah Hajui mengi katika yale mnayoyatenda. [Fusswilat (41:22)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

حَدَّثَنَا الصَّلْتُ بْنُ مُحَمَّدٍ، حَدَّثَنَا يَزِيدُ بْنُ زُرَيْعٍ، عَنْ رَوْحِ بْنِ الْقَاسِمِ، عَنْ مَنْصُورٍ، عَنْ مُجَاهِدٍ، عَنْ أَبِي مَعْمَرٍ، عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ ((‏وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ، عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ‏))‏ الآيَةَ - كَانَ رَجُلاَنِ مِنْ قُرَيْشٍ وَخَتَنٌ لَهُمَا مِنْ ثَقِيفَ، أَوْ رَجُلاَنِ مِنْ ثَقِيفَ وَخَتَنٌ لَهُمَا مِنْ قُرَيْشٍ فِي بَيْتٍ فَقَالَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ أَتُرَوْنَ أَنَّ اللَّهَ يَسْمَعُ حَدِيثَنَا قَالَ بَعْضُهُمْ يَسْمَعُ بَعْضَهُ‏.‏ وَقَالَ بَعْضُهُمْ لَئِنْ كَانَ يَسْمَعُ بَعْضَهُ لَقَدْ يَسْمَعُ كُلَّهُ‏.‏ فَأُنْزِلَتْ ‏((‏وَمَا كُنْتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَنْ يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلاَ أَبْصَارُكُمْ‏))‏ الآية

Ametuhadithia Asw-Swalt bin Muhammad, ametuhadithia Yaziyd bin Zuray‘i, toka kwa Rawh bin Al-Qaasim, toka kwa Manswuwr, toka kwa Mujaahid, toka kwa Abu Mu’ammar, toka kwa Ibn Mas‘uwd amesema:

وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ

Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu. [Fusswilat (41:22)]

Maquraysh wawili pamoja na shemeji yao toka Thaqiyf –au watu wawili toka Thaqiyf na shemeji yao Mquraysh- walikuwa katika nyumba (wakizungumza yasiyomridhisha Allah). (Halafu) wakaulizana: Hivi mnadhani kwamba Allaah Anasikia mazungumzo yetu? Baadhi yao wakasema: Anasikia sehemu ya mazungumzo. Na wengine wakasema: Ikiwa Anasikia sehemu ya mazungumzo, basi kwa hakika Anayasikia yote. Na hapo ikateremshwa:

 

وَمَا كُنتُمْ تَسْتَتِرُونَ أَن يَشْهَدَ عَلَيْكُمْ سَمْعُكُمْ وَلَا أَبْصَارُكُمْ

Na hamkuwa mkijisitiri hata yasishuhudie masikio yenu, na wala macho yenu. [Fussilat: 41:22)]

[Al-Bukhaariy Mujallad 10 Uk. 182]

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

039-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zumar Aayah 67

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾

Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itatekwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa (Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa) kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39:67)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، حَدَّثَنَا الأعمش، عَنْ إِبْرَاهِيمَ عَنْ عَلْقَمَةَ، عَنْ عَبْدِ اللَّهِ، رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم مَنْ أَهْلِ الْكِتَابِ، فَقَالَ: يَا أَبَا الْقَاسِمِ، أُبَلِّغَكَ أَنَّ اللَّهَ [تَعَالَى] يَحْمِلُ الْخَلَائِقَ عَلَى إِصْبَعٍ، والسموات عَلَى إِصْبَعٍ، وَالْأَرْضِينَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالشَّجَرَ عَلَى إِصْبَعٍ، وَالثَّرَى عَلَى إِصْبَعٍ؟ قَالَ: فَضَحِكَ رَسُولُ اللَّهِ  صلى الله عليه وسلم حَتَّى بَدَتْ نَوَاجِذُهُ. قَالَ: وَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ((وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ)) إِلَى آخِرِ الْآيَةِ.

Ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, ametuhadithia Al-A’amash toka kwa Ibraahiym, toka kwa ‘Al-Qamah, toka kwa ‘Abdullaah amesema: Mtu katika Ahlul Kitaab (ambaye ni Myahudi) alikuja kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Abal Qaasim! Je umepata kujua kwamba Allaah (عز وجل) Atavibeba Viumbe juu ya Kidole (Chake Siku ya Qiyaamah), na mbingu juu ya Kidole, na ardhi juu ya Kidole, na miti juu ya Kidole. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akacheka mpaka magego yake ya mbele yakaonekana (kusadikisha na kufurahishwa na maneno hayo). Na hapo Allaa (عز وجل) Akateremsha:

 

وَمَا قَدَرُوا اللَّـهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّمَاوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿٦٧﴾

Na hawakumkadiria Allaah kama inavyostahiki kumkadiria; na hali ardhi yote itakamatwa Mkononi Mwake Siku ya Qiyaamah; na mbingu zitakunjwa Mkononi Mwake wa kulia. Subhaanahu wa Ta’aalaa! Utakasifu ni wa Allaah na Ametukuka kwa ‘Uluwa kutokana na yale yote wanayomshirikisha. [Az-Zumar (39:67)]

[Ahmad katika Mujallad wa 1 ukurasa wa 378]

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

039-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zumar Aayah 53

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى)

 

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu. [Az-Zumar (39:53)]

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حدَّثَنِي إِبْرَاهِيمُ بْنُ مُوسَى، أَخْبَرَنَا هِشَامُ بْنُ يُوسُفَ، أَنَّ ابْنَ جُرَيْجٍ، أَخْبَرَهُمْ قَالَ يَعْلَى إِنَّ سَعِيدَ بْنَ جُبَيْرٍ أَخْبَرَهُ عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ ـ رضى الله عنهما ـ أَنَّ نَاسًا، مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صلى الله عليه وسلم فَقَالُوا إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً‏.‏ فَنَزَلَ ‏ ((وَالَّذِينَ لاَ يَدْعُونَ مَعَ اللَّهِ إِلَهًا آخَرَ وَلاَ يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَلاَ يَزْنُونَ‏)) ‏ وَنَزَلَ ‏((‏قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لاَ تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ‏))

Amenihadithia Ibraahiym bin Muwsaa, ametueleza Hishaam bin Yuwsuf kwamba Ibn Jurayj amewaeleza, amesema Ya’alaa kuwa Sa’iyd bin Jubayr amemweleza toka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba watu katika washirikina walikuwa wameua na wameua watu wengi sana, na wamezini na wamezini na wanawake wengi sana. Wakamwendea Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) wakamwambia: Hakika haya uyasemayo na unayoyalingania ni mazuri sana, basi ungetueleza kama kuna kafara kwa hayo tuliyoyafanya. Na hapo ikateremka:

 

وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ 

Na wale ambao hawaombi pamoja na Allaah mwabudiwa mwengine na wala hawaui nafsi ambayo Allaah Ameiharamisha isipokuwa kwa haki, na wala hawazini. [Al-Furqaan (25:68)].

 

Na ikateremka pia:

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

039-Asbaabun-Nuzuwl Az-Zumar Aayah 23 - 26

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُّتَشَابِهًا مَّثَانِيَ تَقْشَعِرُّ مِنْهُ جُلُودُ الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُمْ ثُمَّ تَلِينُ جُلُودُهُمْ وَقُلُوبُهُمْ إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُدَى اللَّـهِ يَهْدِي بِهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُضْلِلِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِنْ هَادٍ ﴿٢٣﴾ أَفَمَن يَتَّقِي بِوَجْهِهِ سُوءَ الْعَذَابِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ وَقِيلَ لِلظَّالِمِينَ ذُوقُوا مَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ ﴿٢٤﴾ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٢٥﴾ فَأَذَاقَهُمُ اللَّـهُ الْخِزْيَ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ ﴿٢٦﴾

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa, Kitabu; zinazoshabihiana ibara zake, zenye kukaririwa kila mara, zinasisimua kwazo ngozi za wale wanaomkhofu Rabb wao, kisha zinalainisha ngozi zao na nyoyo zao katika kumdhukuru Allaah. Huo ndio mwongozo wa Allaah Humwongoza kwao Amtakaye. Na ambaye Allaah Amempotoa basi hana wa kumuongoa. Je, yule anayekinga kwa uso wake adhabu mbaya Siku ya Qiyaamah (ni sawa na atayesalimika nao?). Na madhalimu wataambiwa: Onjeni yale mliyokuwa mkiyachuma. Wamekadhibisha wale wa kabla yao, basi (Allaah) Akawaletea adhabu kutoka mahali wasipotambua. Allaah Akawaonjesha hizaya katika uhai wa dunia na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni kubwa zaidi, lau kama wangelikuwa wanajua. [Az-Zumar (39:23 - 26)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

  قال سعد بن أبي وقاص قال أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم : لو حَدَّثْتَنا ، فأنزل الله عز وجل  " اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ "

Sa-’ad bin Abiy Waqqaasw amesema: Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) walimwambia Rasuli (صلى الله عليه وآله وسلم): Tunatamani utuhadithie khabari, Allaah (عز وجل)  Akateremsha:

اللَّـهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ

Allaah Ameteremsha kauli nzuri kabisa. [Az-Zumar (39:23)]

 

فقالوا : لو قصصت علينا فنزل نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ 

 

Wakasema: Tuna hamu utusimulie kisa, ikateremka:

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa. [Yuwsuf (12:3)]

فقالوا : لو ذكَّرتنا فنزل أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ   

Wakasema: Tungependa utukumbushe, ikateremka:

ألَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَنْ تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّهِ

Je, haujafika wakati kwa walioamini kwamba zinyenyekee nyoyo zao kwa kumdhukuru Allaah. [Al-Hadiyd (57:16)]”

 

وعن ابن مسعود رضي الله عنه أن أصحاب رسول الله صلى الله عليه وسلم مَلُّوا ملة ، فقالوا له : حَدِّثْنا فنزلت .

Na toka kwa Ibn Mas‘uwd (رضي الله عنه)  kwamba Swahaba wa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  waliboeka sana, wakamwambia Rasuli: Tupashe khabari, na Aayah ikateremka.

 

Al-Qurtwubiy katika Tafsiyr yake ameandika: “Kauli Yake (سبحانه وتعالى):

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 036-Asbaabun-Nuzuwl Yaasiyn 77 - 83

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

أَوَلَمْ يَرَ الْإِنسَانُ أَنَّا خَلَقْنَاهُ مِن نُّطْفَةٍ فَإِذَا هُوَ خَصِيمٌ مُّبِينٌ ﴿٧٧﴾ وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَن يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ ﴿٧٨﴾ قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ ﴿٧٩﴾ الَّذِي جَعَلَ لَكُم مِّنَ الشَّجَرِ الْأَخْضَرِ نَارًا فَإِذَا أَنتُم مِّنْهُ تُوقِدُونَ ﴿٨٠﴾ أَوَلَيْسَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يَخْلُقَ مِثْلَهُم ۚ بَلَىٰ وَهُوَ الْخَلَّاقُ الْعَلِيمُ ﴿٨١﴾ إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٨٢﴾ فَسُبْحَانَ الَّذِي بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

Je, binaadamu haoni kwamba Sisi Tumemuumba kutokana na tone la manii, mara yeye ni mpinzai bayana? Na akatupigia mfano, akasahau kuumbwa kwake; akasema: Ni nani atakayehuisha mifupa hii na hali imeshaoza na kusagika na kuwa kama vumbi. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Ataihuisha Yule Aliyeianzisha mara ya kwanza; Naye ni Mjuzi wa kila kiumbe. Ambaye Amekujaalieni moto kutokana na miti ya kijani, kisha nyinyi mnauwasha. Je, kwani Yule Aliyeumba mbingu na ardhi (mnadhani) Hana uwezo wa kuumba mfano wao? Naam bila shaka (Anaweza)! Naye ni Mwingi wa kuumba Atakavyo, Mjuzi wa yote. Hakika amri Yake Anapotaka chochote hukiambia: Kun! (Kuwa), nacho huwa. Basi Subhaanah! Utakasifu ni wa Ambaye Mkononi Mwake kuna ufalme wa kila kitu, na Kwake mtarejeshwa. [Yaasiyn (36): 77 – 83]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

قَالَ اِبْن أَبِي حَاتِم حَدَّثَنَا حَدَّثَنَا عَلِيّ بْن الْحُسَيْن بْن الْجُنَيْد حَدَّثَنَا مُحَمَّد بْن الْعَلَاء حَدَّثَنَا عُثْمَان بْن سَعِيد الزَّيَّات عَنْ هُشَيْم عَنْ أَبِي بِشْر عَنْ سَعِيد بْن جُبَيْر عَنْ اِبْن عَبَّاس رَضِيَ اللَّه عَنْهُمَا قَالَ : إِنَّ الْعَاص بْن وَائِل أَخَذَ عَظْمًا مِنْ الْبَطْحَاء فَفَتَّهُ بِيَدِهِ ثُمَّ قَالَ لِرَسُولِ اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَيُحْيِي اللَّه هَذَا بَعْد مَا أَرَى ؟ فَقَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ " نَعَمْ يُمِيتك اللَّه ثُمَّ يُحْيِيك ثُمَّ يُدْخِلك جَهَنَّم " قَالَ فَنَزَلَتْ الْآيَات مِنْ آخِر يس

Ibnu Abiy Haatim amesema: Ametuhadithia ‘Aliy bin Al-Husayn bin Al-Junayd, ametuhadithia Muhammad bin Al-‘Ulaa, ametuhadithia ‘Uthmaan bin Sa’iyd  Az-Zayyaat, toka kwa Hashiym, toka kwa Abu Bishr, toka kwa Sa’iyd bin Jubayr, toka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaah ‘anhumaa) amesema: Al-‘Aaswiy bin Waail aliokota fupa toka Al-Batwhaa akalimeng’enya na kulipukutisha kwa mkono wake. Kisha akamwambia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Je, kweli Allaah Atalihuisha hili baada ya kuwa limebungulika hivi? Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: ((Na’am, Allaah Atakufisha wewe, kisha Atakufufua, halafu Atakuingiza Jahannam)). Akasema: Aayaat zikateremka mwisho wa Yaasiyn”.

[Ibnu Abiy Haatim kama ilivyo kwa Ibn Kathiyr katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 581

 

 

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 036-Asbaabun-Nuzuwl: Yaasiyn Aayah 12

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِنَّا نَحْنُ نُحْيِي الْمَوْتَىٰ وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ ۚ وَكُلَّ شَيْءٍ أَحْصَيْنَاهُ فِي إِمَامٍ مُّبِينٍ ﴿١٢﴾

Hakika Sisi Tunahuisha wafu, na Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao na kila kitu Tumekirekodi barabara katika daftari bayana. [Yaasiyn (36:12)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

قال الْحَافِظ أَبُو بَكْر الْبَزَّار حَدَّثَنَا عَبَّاد بْن زِيَاد السَّاجِيّ حَدَّثَنَا عُثْمَان بْن عُمَر حَدَّثَنَا شُعْبَة عَنْ سَعِيد الْجُرَيْرِيّ عَنْ أَبِي نَضْرَة عَنْ أَبِي سَعِيد رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : إِنَّ بَنِي سَلَمَة شَكَوْا إِلَى رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بُعْد مَنَازِلهمْ مِنْ الْمَسْجِد فَنَزَلَ: (( وَنَكْتُب مَا قَدَّمُوا وَآثَارهمْ ))

Al-Haafidh Abu Bakr Al-Bazzaar amesema: Ametuhadithia ‘Abbaad bin Ziyaad As-Saajiyy, ametuhadithia ‘Uthmaan bin ‘Umar, ametuhadithia Shu‘ubah toka kwa Al-Jariyriy toka kwa Abu Nadhwrah (naye ni Al-Mundhir bin Maalik) toka kwa Abu Sa’iyd (Radhwiya Allaah ‘anhu)  amesema: Banu Salamah walimlalamikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa nyumba zao ziko mbali na Msikiti. Na hapo ikateremka:

وَنَكْتُبُ مَا قَدَّمُوا وَآثَارَهُمْ 

Tunaandika yale waliyoyakadimisha na athari zao. [Yaasiyn (36:12)]”

[Ibn Kathiyr katika Mujallad wa 3 ukurasa wa 556]

 

Na pia,

 

Asbaabun-Nuzuwl

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 53

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَدْخُلُوا بُيُوتَ النَّبِيِّ إِلَّا أَن يُؤْذَنَ لَكُمْ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيْرَ نَاظِرِينَ إِنَاهُ وَلَـٰكِنْ إِذَا دُعِيتُمْ فَادْخُلُوا فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ يُؤْذِي النَّبِيَّ فَيَسْتَحْيِي مِنكُمْ ۖ وَاللَّـهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ ۚ وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِن وَرَاءِ حِجَابٍ ۚ ذَٰلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ ۚ وَمَا كَانَ لَكُمْ أَن تُؤْذُوا رَسُولَ اللَّـهِ وَلَا أَن تَنكِحُوا أَزْوَاجَهُ مِن بَعْدِهِ أَبَدًا ۚ إِنَّ ذَٰلِكُمْ كَانَ عِندَ اللَّـهِ عَظِيمًا ﴿٥٣﴾

Enyi walioamini! Msiingie nyumba za Nabiy isipokuwa mkipewa idhini ya kwenda kula si kungojea kiive. Lakini mtakapoitwa, basi ingieni, na mkimaliza kula, tawanyikeni, na wala msikae kujiliwaza kwa mazungumzo. Hakika hiyo ilikuwa inamuudhi Nabiy, naye anakustahini, lakini Allaah Hasitahi (kubainisha) haki. Na mnapowauliza wake zake haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Na haipasi kwenu kumuudhi Rasuli wa Allaah. Na wala kuwaoa wake zake baada yake abadani. Hakika jambo hilo mbele ya Allaah ni kubwa mno. [Al-Ahzaab (33:53)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا إِسْحَاقُ بْنُ مَنْصُورٍ، أَخْبَرَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ بَكْرٍ السَّهْمِيُّ، حَدَّثَنَا حُمَيْدٌ، عَنْ أَنَسٍ رضى الله عنه قَالَ أَوْلَمَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم حِينَ بَنَى بِزَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ فَأَشْبَعَ النَّاسَ خُبْزًا وَلَحْمًا ثُمَّ خَرَجَ إِلَى حُجَرِ أُمَّهَاتِ الْمُؤْمِنِينَ كَمَا كَانَ يَصْنَعُ صَبِيحَةَ بِنَائِهِ فَيُسَلِّمُ عَلَيْهِنَّ وَيَدْعُو لَهُنَّ وَيُسَلِّمْنَ عَلَيْهِ وَيَدْعُونَ لَهُ فَلَمَّا رَجَعَ إِلَى بَيْتِهِ رَأَى رَجُلَيْنِ جَرَى بِهِمَا الْحَدِيثُ، فَلَمَّا رَآهُمَا رَجَعَ عَنْ بَيْتِهِ، فَلَمَّا رَأَى الرَّجُلاَنِ نَبِيَّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم رَجَعَ عَنْ بَيْتِهِ وَثَبَا مُسْرِعَيْنِ، فَمَا أَدْرِي أَنَا أَخْبَرْتُهُ بِخُرُوجِهِمَا أَمْ أُخْبِرَ فَرَجَعَ حَتَّى دَخَلَ الْبَيْتَ، وَأَرْخَى السِّتْرَ بَيْنِي وَبَيْنَهُ وَأُنْزِلَتْ آيَةُ الْحِجَابِ

Ametuhadithia Is-haaq bin Mansuwr, ametueleza ‘Abdullaah bin Bakr As-Sahmiy, ametuhadithia Humayd toka kwa Anas (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   alifanya walima ya mikate na nyama, watu wakala wakashiba hadi kusaza wakati alipomwoa Zaynab bint Jahsh. Kisha akatoka kwenda kwenye nyumba za (Wakeze) Mama wa Waumini kama ilivyokuwa ada yake asubuhi ya kila baada ya sherehe ya harusi yake, akawasalimia na kuwaombea, na wao wakamsalimia na kumwombea. Aliporudi nyumbani kwake, aliwakuta watu wawili wamezama kwenye maongezi. Alipowaona, alirudi na hakuingia nyumbani. Watu wale wawili walipomwona Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amerudi na hakuingia nyumbani kwake, walinyanyuka haraka na kuondoka. Nami (Anas) sikumbuki kama ni mimi niliyemweleza kuwa washaondoka au alielezwa na mtu mwingine. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akarejea akaingia nyumbani na akateremsha pazia kati yangu na yeye, na Aayah ya hijaab ikateremshwa.

 

[Al-Bukhaariy Mujallad 10 ukurasa wa 149]

 

Na Ibnu Abiy Marmaa amesema: 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 51

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ ۚ ذَٰلِكَ أَدْنَىٰ أَن تَقَرَّ أَعْيُنُهُنَّ وَلَا يَحْزَنَّ وَيَرْضَيْنَ بِمَا آتَيْتَهُنَّ كُلُّهُنَّ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَلِيمًا حَلِيمًا ﴿٥١﴾

Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako. Hivyo ni karibu zaidi kupelekea kuburudika macho yao, na wala wasihuzunike, na waridhike kwa yale uliyowapa kila mmoja wao. Na Allaah Anajua yale yaliyomo nyoyoni mwao. Na Allaah daima ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu. Ahzaab (33:51)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا زَكَرِيَّاءُ بْنُ يَحْيَى، حَدَّثَنَا أَبُو أُسَامَةَ، قَالَ هِشَامٌ حَدَّثَنَا عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَائِشَةَ رضى الله عنها قَالَتْ: كُنْتُ أَغَارُ عَلَى اللاَّتِي وَهَبْنَ أَنْفُسَهُنَّ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَقُولُ أَتَهَبُ الْمَرْأَةُ نَفْسَهَا فَلَمَّا أَنْزَلَ اللَّهُ تَعَالَى ‏((‏تُرْجِئُ مَنْ تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَنْ تَشَاءُ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلاَ جُنَاحَ عَلَيْكَ‏))‏ قُلْتُ مَا أُرَى رَبَّكَ إِلاَّ يُسَارِعُ فِي هَوَاكَ‏.‏

Ametuhadithia Zakariyya bin Yahyaa, ametuhadithia Abu Usaamah akisema: Hishaam ametuhadithia toka kwa baba yake toka kwa ‘Aaishah (رضي الله عنها) kwamba amesema: Nilikuwa nawafanyia wivu wanawake ambao wanajitoa wenyewe kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   (ili awaoe bila mahari) nikisema (na kustaajabu): Mwanamke anajitoa mwenyewe hivi?! Na Allaah Ta’aalaa Alipoteremsha:

 

تُرْجِي مَن تَشَاءُ مِنْهُنَّ وَتُؤْوِي إِلَيْكَ مَن تَشَاءُ ۖ وَمَنِ ابْتَغَيْتَ مِمَّنْ عَزَلْتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيْكَ 

Umuakhirishe umtakaye miongoni mwao na umsogeze kwako umtakaye. Na ukimtaka katika uliyemtenga basi hakuna dhambi juu yako.

 

nilisema: Naona Rabb wako Hakawii kabisa katika kukidhi matashi yako (ya kuoa, kukuruhusu kupanga zamu za kulala kwa wakezo upendavyo mwenyewe na kukutanulia mambo yako uridhike)”.

 

[Al-Bukhaariy Mujallad wa 10 ukurasa wa 144]

 

Pia,

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 37

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَإِذْ تَقُولُ لِلَّذِي أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَأَنْعَمْتَ عَلَيْهِ أَمْسِكْ عَلَيْكَ زَوْجَكَ وَاتَّقِ اللَّـهَ وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّـهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ ۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيْدٌ مِّنْهَا وَطَرًا زَوَّجْنَاكَهَا لِكَيْ لَا يَكُونَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ حَرَجٌ فِي أَزْوَاجِ أَدْعِيَائِهِمْ إِذَا قَضَوْا مِنْهُنَّ وَطَرًا ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ مَفْعُولًا ﴿٣٧﴾ مَّا كَانَ عَلَى النَّبِيِّ مِنْ حَرَجٍ فِيمَا فَرَضَ اللَّـهُ لَهُ ۖ سُنَّةَ اللَّـهِ فِي الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلُ ۚ وَكَانَ أَمْرُ اللَّـهِ قَدَرًا مَّقْدُورًا ﴿٣٨﴾ الَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَالَاتِ اللَّـهِ وَيَخْشَوْنَهُ وَلَا يَخْشَوْنَ أَحَدًا إِلَّا اللَّـهَ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ حَسِيبًا ﴿٣٩﴾ مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ ۗ وَكَانَ اللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا ﴿٤٠﴾

Na pale ulipomwambia yule ambaye Allaah Amemneemesha nawe ukamneemesha: Mshikilie mkeo, na mche Allaah! Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua, na unakhofu watu, na hali Allaah Ana haki zaidi umkhofu. Basi Zayd alipomaliza haja kwake Tukakuozesha ili isiwe dhambi juu ya Waumini kuhusu (kuoa) wake wa watoto wao wa kupanga wanapomaliza haja kwao. Na Amri ya Allaah daima ni yenye kutekelezwa. Hakuna lawama yoyote juu ya Nabiy (kufanya) katika yale Aliyomfaridhishia Allaah, ni desturi ya Allaah kwa wale waliopita kabla. Na amri ya Allaah daima ni kudura iliyokwishakadiriwa vyema kabisa.  Wale wanaobalighisha ujumbe wa Allaah na wanamkhofu Yeye na wala hawamkhofu yeyote isipokuwa Allaah. Na Allaah Anatosheleza kuwa Mwenye kuhesabu. Hakuwa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Rasuli wa Allaah na ni mwisho wa Manabii. Na Allaah daima ni Mjuzi wa kila kitu. [Al-Ahzaab (33: 37, 40)]

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ عَبْدِ الرَّحِيمِ، حَدَّثَنَا مُعَلَّى بْنُ مَنْصُورٍ، عَنْ حَمَّادِ بْنِ زَيْدٍ، حَدَّثَنَا ثَابِتٌ، عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ ـ رضى الله عنه أَنَّ هَذِهِ، الآيَةَ ‏وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّهُ مُبْدِيهِ‏ نَزَلَتْ فِي شَأْنِ زَيْنَبَ ابْنَةِ جَحْشٍ وَزَيْدِ بْنِ حَارِثَةَ‏.‏

Ametuhadithia Muhammad bin ‘Abdir-Rahiym, ametuhadithia Mu‘allaa bin Mansuwr toka kwa Hammaad bin Zayd, ametuhadithia Thaabit toka kwa Anas bin Maalik (رضي الله عنه)  kwamba Aayah hii:

وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّـهُ مُبْدِيهِ

Na ukaficha katika nafsi yako ambayo Allaah Ametaka kuyafichua.

Iliteremka kuzungumzia suala la Zaynab bint Jahsh pamoja na Zayd bin Haaritha”.

 

[Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kumi ukurasa wa 124]

 

Na pia...

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

033-Asbaabun-Nuzuwl Al-Ahzaab Aayah 25

 

 

Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

وَرَدَّ اللَّـهُ الَّذِينَ كَفَرُوا بِغَيْظِهِمْ لَمْ يَنَالُوا خَيْرًا ۚ وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ قَوِيًّا عَزِيزًا ﴿٢٥﴾

Na Allaah Akawarudisha nyuma wale waliokufuru kwa ghaidhi zao hawakupata kheri yoyote. Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani. Na Allaah daima ni Mwenye nguvu zote, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika. [Al-Ahzaab (33:26)]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

أَخْبَرَنَا عَمْرُو بْنُ عَلِيٍّ، قَالَ حَدَّثَنَا يَحْيَى، قَالَ حَدَّثَنَا ابْنُ أَبِي ذِئْبٍ، قَالَ حَدَّثَنَا سَعِيدُ بْنُ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي سَعِيدٍ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ شَغَلَنَا الْمُشْرِكُونَ يَوْمَ الْخَنْدَقِ عَنْ صَلاَةِ الظُّهْرِ، حَتَّى غَرَبَتِ الشَّمْسُ وَذَلِكَ قَبْلَ أَنْ يَنْزِلَ فِي الْقِتَالِ مَا نَزَلَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏((‏وَكَفَى اللَّهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ))‏ فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِلاَلاً فَأَقَامَ لِصَلاَةِ الظُّهْرِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا لِوَقْتِهَا ثُمَّ أَقَامَ لِلْعَصْرِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا فِي وَقْتِهَا ثُمَّ أَذَّنَ لِلْمَغْرِبِ فَصَلاَّهَا كَمَا كَانَ يُصَلِّيهَا فِي وَقْتِهَا ‏.‏

Ametueleza ‘Amri bin ‘Aliy amesema, ametuhadithia Yahyaa amesema, ametuhadithia Ibn Ubayya Dhi-ib amesema, ametuhadithia Sa’iyd bin Abiy Sa’iyd toka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Sa’iyd toka kwa baba yake akisema: Washirikina walitushughulisha Siku ya Khandak tusiweze kuswali Swalaah ya Adhuhuri mpaka jua likachwa, na hiyo ilikuwa kabla ya Allaah (عز وجل)   kuteremsha (Aayah hii) kuhusiana na vita:

وَكَفَى اللَّـهُ الْمُؤْمِنِينَ الْقِتَالَ 

Na Allaah Amewatosheleza Waumini vitani.

 

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru Bilaal (aqimu), akaqimu kwa Swalaah ya Adhuhuri, (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم)  akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake. Kisha (Bilaal) akaqimu kwa Swalaah ya Al-‘Aswr, na (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake. Halafu akaadhini kwa Swalaah ya Maghrib, na (Rasuli wa Allaah صلى الله عليه وآله وسلم) akaiswali kama alivyokuwa anaiswali katika wakati wake.”

 

[An-Nasaaiy katika Mujallad wa 2 Uk wa 15, Wapokezi wa Hadiyth hii ni wapokezi wa As-Swahiyh, na Ibn Jariyr ameikhariji katika Mujallad wa 21 ukurasa wa 149]