Skip to main content

08-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبة - Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji021-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Mtu Asile Huku Ameegemea

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

Alhidaaya.com

Adabu Za Kula

021-Mtu Asile Huku Ameegemea

5-  Mtu Asile Huku Ameegemea

Ni kwa Hadiyth ya Abu Juhayfah, amesema:  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

"أَمَّا أَنَا، فَلا آكُلُ مُتَّكِئًا"

“Mimi kwa upande wangu, sili huku nimeegemea kitu”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5398) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (64)].