Du'aa Gani Kuomba Unapokunywa Maji Ya Zamzam?

 

SWALI:

salam aleikum wa Rahmatullah wa Barakat
 
Fadhli ni ya Subhana Wataallah olajalia Ahli Al Hidaya ujuzi wa ku elimisha Umati Mohamad Salallah Aleih Wasalam.
 
Maombi yangu, ni ilimishwe "DUA" ya kuomba kabla ya kunywa maji ya zamzam wakati mtu yoko Haj
 
Jazakumallah kul khairWa Asalam aleikum wa Rahmatullah wa Barakat
 
JIBU:
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
 

Hakuna du'aa maalumu iliyopatikana kutoka katika Hadiyth Sahihi ya kuomba wakati wa kunywa maji ya zamzam. Baadhi ya du'aa zilizonukuliwa zimechambuliwa kwa dalili kuwa ni kutoka katika zile Hadiyth dhaifu. Iliyopatikana kuwa ni Swahiyh ni kwamba unaomba chochote utakacho mwenyewe wakati kunywa. Hii ni kutokana na dalili ifuatayo:

 

(( ماء زمزم لما شرب له)) صحيح ابن ماجه  

((Maji ya zamzam kwa (jambo liloombewa) wakati wa kunywa)) [Swahiyh Ibn Maajah na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy]  
 
Na Allah Anajua zaidi

 

Share