Kaka Amefariki Ameacha Mke Mtoto Na Mama Na Ndugu

 

 

Kaka Amefariki Ameacha Mke Mtoto Na Mama Na Ndugu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Naomba kuuliza kuwa kaka yangu amefariki ameacha mke na mtoto mmoja na aiyefariki ameacha gari aina ya pickup tani 3 ila mpaka sasa gari yake ilianguka baada ya kifo chake kwa wiki 1, ndo tuko katika mipango ya kuitengeneza na likishatengenezwa tutaliuza kama milioni 4 ili tuanzae mipango ya kugawa urithi, swali langu ni hili katika kugawa urithi nani ambaye anaestahiki kupata ulithi zaidi, je na mke wake atagawia urithi? je na mama yetu pia anapata kiasi gani? nashukuru kama mtanijibu.

 

 

JIBU:

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam  zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Mama mzazi anarithi sudusi (1/6) ya mali iliyoachwa na aliyefariki kwa mujibu wa Qur-aan:

 

وَلِأَبَوَيْهِ لِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُ وَلَدٌ

na wazazi wake wawili kila mmoja wao atastahiki sudusi katika alichoacha ikiwa anaye mtoto[An-Nisaa 4: 11]

 

 

Mke aliyefiliwa na mumewe anapata thumuni (1/8) kwa mujibu wa mgao wa Qur-aan:

 

 وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم

Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi watastahiki thumni katika mlichoacha[An-Nisaa 4: 12]

 

Ndugu wa aliyefariki hawatakuwa ni wenye kurithi chochote kwa kuwepo kwa mtoto wa aliyefariki. Hivyo, kitachobakia atapatiwa mtoto.

 

Tufahamu kuwa mgao huu ni baada ya kulipiwa madeni aliyokuwa nayo aliyefariki, kutoa pesa za mazishi na kama ameacha wasiya. Ikiwa hilo gari umesema linatengenezwa, gharama hiyo itatolewa kutoka kwa pesa hizo lakini ikiwa mtasaidia itakuwa ni kheri na thawabu kutoka kwenu.

 

Tunawaomba muwe na subira na uvumilivu kwa kuondokewa na kipenzi chenu na alipwe mema nanyi pia.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

Share