Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 04

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam - 04 

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

  Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 4 Linaloeleweka Vibaya

 

 

Uislaam unakubaliana zaidi na Waarabu tu kwa sababu:

 

  • Waislamu wengi ni Waarabu

 

  • Qur-aan ipo kwa Kiarabu

 

Jibu

 

Hoja ya mwanzo kuhusu suala hili linaloeleweka vibaya ipo mbali na ukweli. Waislamu walio zaidi ya bilioni moja duniani, basi kati ya asilimia 18 tu ni Waarabu. Nchi zilizo na idadi kubwa ya Waislamu duniani ni Indonesia. Nchi ya pili yenye idadi kubwa ya Waislamu ni Bangladesh. Sio nchi hata moja kati ya hizi ni ya Kiarabu.

 

Uislaam ni dini yenye kukua kwa kasi duniani (Encyclopedia Britannica). Ina wafuasi kwenye mabara yote yenye idadi kubwa ya watu, na pia inakubalika kwa Waarabu na wasio Waarabu. Waislamu hadi itakapofikia mwisho mwa karne, wanatarajiwa kuwa ni dini kubwa kabisa kati ya dini zenye wafuasi wachache largest religious minority nchini Marekani, wakiwashinda Mayahudi.

 

Lalamiko la ulimwengu la Uislaam kwa Waarabu na wasiokuwa Waarabu linafuatia ingawa Qur-aan ni ya Kiarabu. Allaah Anaelezea ndani ya Qur-aan kwamba njia hii ya maisha inayoitwa Uislaam ni ya watu wote, Anasema Allaah:

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٧﴾

 

Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa ni rahmah kwa walimwengu. [Al-Anbiyaa:107]

 

 

Pia Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٨﴾

 

Na Hatukukutuma (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) isipokuwa kwa watu wote uwe mbashiriaji na muonyaji, lakini watu wengi hawajui. [Sabaa: 28]

 

Juu ya hivyo, Allaah Hatumii kigezo cha rangi au lugha ya mama (mother tongue) kuwahukumu, wawe ni Waarabu au sio. Badala yake, ni kiwango cha kumtambua Allaah ndicho kigezo.

 

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴿١٣﴾

 

Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana namwanamme na mwanamke, na Tukakujaalieni mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Hujuraat: 13]

 

Uchaguzi wa Kiarabu kuwa ni lugha ya Qur-aan umeelezwa kiurahisi na kiuwazi Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa), Anasema Allaah:

 

وَلَوْ جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا أَعْجَمِيًّا لَّقَالُوا لَوْلَا فُصِّلَتْ آيَاتُهُ ۖ أَأَعْجَمِيٌّ وَعَرَبِيٌّ ۗ قُلْ هُوَ لِلَّذِينَ آمَنُوا هُدًى وَشِفَاءٌ ۖ وَالَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ فِي آذَانِهِمْ وَقْرٌ وَهُوَ عَلَيْهِمْ عَمًى ۚ أُولَـٰئِكَ يُنَادَوْنَ مِن مَّكَانٍ بَعِيدٍ﴿٤٤﴾

 

Na lau Tungeliifanya Qur-aan lugha isiyokuwa ya Kiarabu bila shaka wangelisema: Mbona hazikufasiliwa waziwazi Aayaat zake?  Ah! Ya lugha ya kigeni na hali (Nabiy) ni Mwarabu!? Sema: Hiyo ni kwa walioamini ni mwongozo na shifaa. Na wale wasioamini, wana uziwi masikioni mwao nayo ni upofu kwao. Hao wanaitwa kutoka mahali mbali. [Fusw-swilat:44]

 

Hata hivyo, ni muhimu pia kutilia mkazo kwamba Qur-aan ikiwa na uteremsho wa mtindo wa Kiarabu ni Neno sanifu la Allaah, lakini tafsiri yoyote sio (Qur-aan). Kila tafsiri kiusahihi inaitwa kuwa ni tafsiri na fafanuzi, kwani kila mfasiri anaingiza matashi/ upendeleo (bias) wake.

 

.../5

 

 

 

 

Share