Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislam - 05

 

Masuala Kumi Yanayoeleweka Vibaya Katika Uislaam - 05

 

Imefasiriwa na: Naaswir Haamid

 

Alhidaaya.com

 

 

Suala Nambari 5 Linaloeleweka Vibaya

 

Uislaam unamkataa Yesu kwa sababu:

 

  • Yesu hakubaliki kuwa ni ‘mtoto wa Allaah’

 

Jibu:

 

Zote mbili; Qur-aan na Sunnah zinatufundisha kwa msisitizo na bila ya wasiwasi kwamba Allaah Anatambua tamko la Utatu kuwa ni uongo ulio mkubwa mno. Qur-aan inaeleza:

 

وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَـٰنُ وَلَدًا ﴿٨٨﴾ لَّقَدْ جِئْتُمْ شَيْئًا إِدًّا ﴿٨٩﴾ تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْهُ وَتَنشَقُّ الْأَرْضُ وَتَخِرُّ الْجِبَالُ هَدًّا ﴿٩٠﴾ أَن دَعَوْا لِلرَّحْمَـٰنِ وَلَدًا ﴿٩١﴾ إِن كُلُّ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ إِلَّا آتِي الرَّحْمَـٰنِ عَبْدًا ﴿٩٣﴾

 

Na wamesema: Ar-Rahmaan Amejifanyia mwana. Kwa yakini mmeleta jambo kuu ovu na la kuchukiza mno!  Zinakaribia mbingu zipasuke kwa (tamko) hilo, na ardhi kuraruka, na milima kuporomoka na kubomoka. Kwa kule kudai kuwa Ar-Rahmaan Ana mwana. Na wala haipasi kwa Ar-Rahmaan kujifanyia mwana. Hakuna yeyote yule aliyeko katika mbingu na ardhi isipokuwa atamfikia Ar-Rahmaan kuwa ni mja. [Maryam: 88-93]

 

Hata hivyo, suala hilo linaloeleweka vibaya haliendani na hoja zinazotolewa hapo juu kwamba Yesu (‘Iysaa ‘Alayhis-salaam) anakataliwa (moja kwa moja). Ni vyema kutanabahisha kwa kusema kwamba inakataliwa kumueleza Yesu (‘Iysaa ‘Alayhis-salaam) kama ni ‘mtoto wa Allaah’. Kwa kuwa ni Rasuli wa Allaah, Yesu anatunukiwa cheo chake cha heshima namna walivyopewa Rusuli wote, kama ambavyo Aayah ifuatayo inavyotamka (tafsiri):

 

قُولُوا آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَمَا أُوتِيَ النَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿١٣٦﴾

 

Semeni: Tumemwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na Al-Asbaatw na aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya mmoja yeyote miongoni nasi ni Waislamu (tunajisalimisha) Kwake. [Al-Baqarah: 136]

 

 

 

.../6

 

Share