Sambusa Za Viazi

Sambusa Za Viazi

Vipimo

Viazi - 4

Vitunguu nyasi vilokatwakatwa - 3 miche

Kitunguu maji kilokatwakatwa - 1

Chumvi - 1 kijiko cha chai

Bizari ya pilau nzima ( jeera) - 1 kijiko cha chai

Mafuta - Nusu kilo

Manda za tayari - 10 - 20                                

Yai - 1 au 2

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

  1. Menya viazi, vioshe vikate slesi kisha  vikatekate vipande vidogo vidogo.

 

  1. Chemsha maji kidogo ukiwa umeyatia chumvi , kisha vimimine viazi ndani ya maji yawache paka uwone tena yachemka kwa mara ya pili acha kwa dakika 10 - 15, kisha ondoa jikoni. 
  2. Mimina katika chujio uchuje maji . 
  3. Roweka bizari kwenye maji kwa muda wa dakika 20 hivi. 
  4. Chukua bakuli kubwa lenye nafasi mimina viazi, vtunguu nyasi na maji,   chumvi, mafuta vijiko 2 – 3 vya supu, na bizari. Changanya vizuri. 
  5. Tandaza manda mezani au kwenye kibao fanya mkunjo wa sambusa kisha paka yai kwa brashi, kunja upate pembe moja . Tazama picha.

     

  1. Jaza viazi sehemu ulokunja kisha funga sambusa.

             

 

 

 

  1. Tia mafuta katika karai, yakipata moto, tia sambusa ziikaange hadi zigeuke rangi ya dhahabu.   
  2. Zitoe na zichuje mafuta tayari kuliwa kwa Sosi Ya Ukwaju  au  Chatine Ya Mtindi Na Nanaa

 

 

 

 

 

Share