SWALI:
Nini maana ya (al.manhajusalafiya) na je ni kikundi ao ni dini mpya. Nifidisheni mungu akulipeni fiduniya wal akhera
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Manhaj ya Salafiyyah.
Haya ni maneno mawili ambayo si mageni kwani yanatumika
Hii si Dini mpya ambayo imekuja kwetu kwani Dini yetu ya Uislamu haibadiliki mpaka siku ya Qiyaamah. Kwa kuwa Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) ndio walioifahamu Dini hii ya Uislamu zaidi kuliko waliokuja baada
Na wanaofuata Manhaj hii wanajulikana zaidi kwa jina la Ahlus Sunnah wal Jamaa'ah au Salafi.
Kwa hiyo, hiki si kikundi wala Dini kando bali ni muongozo aliokuja nao Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ukafahamika na kufuatwa na Maswahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata hao kwa wema hadi Qiyamaah. Ni Muongozo wa Dini yetu hii ya Uislamu, ambao utakupatia ufanisi hapa duniani na kesho Aakhirah.
Na Allaah Anajua zaidi