Kufanya Tendo La Ndoa Na Viumbe Visivyojulikana Usingizini

 

Kufanya Tendo La Ndoa Na Viumbe Visivyojulikana Usingizini

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Is it true that a person can have sex with unknown organisms while he/ she is fast asleep?  If yes what are those creatures and how do they do this?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Hakika jambo hilo linatendeka na viumbe hivyo ni majini. Navyo hufanya hayo ili kuwasumbua na kuwavuruga wanaadamu kwa sababu moja au nyengine.

 

Hivyo, tunakushauri kabla ya kulala uwe na wudhuu wako wa Swalaah na soma du’aa za kulala, Aayatul Kursiy, Qul Huwa Allaahu Ahad, na Al-Mu’awidhatayn (Qul A’udhu Bi-Rabbil Falaq na Qul A’udhu Bi Rabbin Naas) na upulize kwenye mikono yako na kujipaka sehemu ya mwili wako wote utakayoweza kuifikia. Pia ikiwa ndoto kama hizo zitakutokea, amka na chukua wudhuu na swali rakaa mbili na rejea kulala. In shaa Allaah hayo yataweza kukusaidia.

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Naingiliwa Kwa Kitendo Cha Ndoa Na Majini

 

Kuhusu Mashaytwaan Na Vipi Kujikinga Nao

 

Hupata Damu Baada Ya Kujimai Na Mume – Vipi Kujitibu Na Majini Wa Mahaba?

 

Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share