Skip to main content

Surah Ziloteremka Makkah Na Za Madiynah

Suwrah Ziloteremka Makkah Na Za Madiynah

Alhidaaya.com

SWALI:

Asalamu alaykum warahmatu LLwah wa barakatu. Mimi napenda kuuliza suali. Kuna suwrah ngapi zilizo teremka Makkah na surwrah ngapi zilizo teremshwa Madinaa? Naomba nifahamishwe. Ahsante

JIBU:

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu idadi ya Surah zilizoteremshwa Makkah na zile za Madiynah.

Hakika katika hili Wanachuoni wametofautiana na kupatikana kauli tatu. Nazo ni kama zifuatazo:

Kauli

Makkah

Madiynah

1. Ya kwanza

86

28

2. Ya pili

87

27

3. Ya tatu

88

26

Tofauti hizi zimetokana na baadhi ya Suwrah ambazo Wanachuoni wengine wameziona na kuziorodhesha kuwa zimeteremshwa Makkah na wengine kuwa ni za Madiynah.

Na Allaah Anajua zaidi