Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume
الطَّلَاقُ المُنَجَّزُ والمُضَافُ والمُعَلَّقُ
Talaka Inayopita Hapo Hapo Inapotolewa, Talaka Inayofungamanishwa Na Wakati, Na Talaka Inayofungamanishwa Na Jambo Fulani
01: Talaka Inayopita Hapo Hapo"الطَّلّاقُ المُنَجَّزُ" :
Ni talaka ambayo kwenye tamko lake hakuna sharti lolote aliloliweka mume, au akaifungamanisha na wakati ujao, bali anaikusudia ipite hapo hapo. Ni kama kumwambia mkewe: "Nimekuacha".
Hukmu Yake:
Talaka hii hupita, na huwa ni sababu ya mke na mume kuachana, na itafuatiwa moja kwa moja na athari za talaka. Mume akimwambia mkewe: "Nimekutaliki", basi anakuwa moja kwa moja ameachika, na ataanza eda yake ikiwa ni katika wenye kupata hedhi.