Skip to main content

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume 

الطَّلَاقُ المُنَجَّزُ والمُضَافُ والمُعَلَّقُ

Talaka Inayopita Hapo Hapo Inapotolewa, Talaka Inayofungamanishwa Na Wakati, Na Talaka Inayofungamanishwa Na Jambo Fulani 

Alhidaaya.com 

02: Talaka Iliyofungamanishwa Na Wakati "الطَّلَاقُ المضَافُ" 

Ni talaka iliyofungamanishwa na wakati ambapo mume anakusudia talaka ipite wakati ule aliouainisha.  Ni kama kumwambia mkewe:  "Nitakuwa nimekutaliki mwanzoni mwa mwezi ujao, au jioni ya leo". 

Hukmu Yake:

'Ulamaa wamekhitilafiana katika kauli tatu kuhusiana na talaka hii inayofungamanishwa na wakati ujao.

Kauli Ya Kwanza: 

Talaka inapita hapo hapo, lakini haipiti mpaka uwadie wakati ulioainishwa.  Ni kauli ya Abu 'Ubayd, Is-Haaq, Ash-Shaafi'iy, Ahmad na Daawuwd Adh-Dhwaahiriy.

Kauli Ya Pili: 

Talaka inapita moja kwa moja, haisubiri muda kuwadia. Ni kauli ya Ibn Al-Musayyib, Abu Haniyfah, Al-Layth na Maalik.

Kauli Ya Tatu:

Si yenye kupita hapo kwa hapo wala hata wakati ulioainishwa unapowadia.  Ni madhehebu ya Abu Muhammad bin Hazm.  Ametoa dalili zifuatazo za kuwavunja hoja wenye kukhitilafiana naye akisema:

1-  Haikuelezwa katika Qur-aan wala katika Hadiyth za Rasuli (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba talaka inapita kwa namna hii, bali Allaah Ta'aalaa Ametufundisha kuhusu talaka ya mwanamke aliyeingiliwa na yule ambaye hakuingiliwa.  Allaah Anasema: 

"وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ" 

"Na yeyote atakayevuka Mipaka ya Allaah, basi kwa yakini ameidhulumu nafsi yake". [At-Twalaaq: 01]

2-  Ndoa ya kupangiwa muda au wakati fulani ukiwadia haijuzu, na hivyo hivyo kwa upande wa talaka.