Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume
الطَّلَاقُ السُّنِّيُّ والبِدعِيُّ
Talaka Ya Kisunnah Na Kibid'ah
01: Talaka Ya Kisunnah Na Kibid'ah
Talaka ziko aina mbili kwa mujibu wa wasifu wake wa kisharia: Talaka ya kisunnah, na talaka ya kibid'ah.
Talaka ya kisunnah ni ile inayowafikiana na sunnah katika namna ya kuitoa, yaani kwa mujibu wa Alivyoamrisha Allaah Ta’aalaa na Rasuli Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam. Na makusudio hapa si kwamba talaka kwa namna hiyo ni talaka iliyo suniwa, kwani kama ilivyotangulia, tuliona kwamba talaka ina hukumu tano za kisharia.
Talaka ya kibid'ah ni ile inayokwenda kinyume na sunnah katika kuitoa, yaani inayokaidi Alivyoamrisha Allaah Ta’aalaa na Rasuli Wake (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam).