Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ
Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume
الطَّلَاقُ
Talaka
16: Aina Za Talaka:
Kwa jinsi picha yake ilivyo, talaka inaweza kugawanywa katika aina mbalimbali.
1- Kwa upande wa tamko linalotumika, iko aina mbili:
(a) Talaka ya tamko wazi.
(b) Talaka ya tamko fumbo. Hili lishazungumzwa nyuma.
2- Kwa upande wa athari inayotokana nayo, iko aina mbili pia.
(a) Talaka rejea "طَلَاقٌ رَجْعِي".
(b) Talaka mtengano, utengano mdogo au mkubwa "طَلَاقٌ بَائِنٌ بَيْنُونَةٌ صُغْرَى أَوْ كُبْرَى"
3- Kwa upande wa sifa yake, iko vilevile aina mbili.
(a) Ya kisunnah "طَلَاقٌ سُنِّيٌّ"(ya kishari'ah).
(b) Ya kibid-'ah "طَلَاقٌ بِدْعِيٌّ" (iliyo kinyume na shari'ah).
4- Kwa upande wa wakati wa kutokea athari itokanayo kwayo, iko ya aina tatu:
(a) Inayopita hapo hapo inapotolewa. (Kwa mfano mume akimwambia mkewe: "Nimekutaliki", mke anakuwa hapo hapo ashaachika).
(b) Iliyofungamanishwa na sharti. (Ni kama mume kumwambia mkewe: "Ukifanya jambo fulani basi umeachika", ikiwa atafanya jambo hilo, basi anakuwa ameachika).
(c) Iliyotegemezwa na wakati ujao. (Ni kama mume kumwambia mkewe: "Nimekutaliki kesho").
Na hebu sasa tuangalie uchanganuzi wa aina zote hizi na hukumu za kila moja.