Kauli Za Salaf: Taqwa-Ikhlaasw
Dunia Ni Pandikizo La Aakhirah Pandikiza Khayr Upate Mavuno Ya Kukuridhisha
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
“Aliye na akili anaposoma Qur-aan na kutafakari, hutambua thamani ya dunia kwamba si chochote na kwamba ni pandikizo la Aakhirah. Kwa hiyo, tazama umepandikiza nini humo kwa ajili ya Aakhirah yako; ikiwa umepandikiza khayr basi bashiria kwa mavuno ambayo yatakuridhisha. Lakini ikiwa ni kinyume, basi umekhasirika duniani na Aakhirah.”
[Sharh Riyaadhw Asw-Swaaihiyn (3/358)]