Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

Asbaabun-Nuzuwl

 

Sababu Za Kuteremshwa

Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan

 

096-Suwrah Al-'Alaq Aayah 6 - 19

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Kauli za Allaah (سبحانه وتعالى):

 

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾

Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi.

أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾

Kwa kuwa amejiona amejitosheleza.

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾

Hakika kwa Rabb wako ni marejeo.

أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾

Je, umemuona yule anayekataza?

عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾

Mja pale anaposwali?

أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾

Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu?

أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾

Au ameamrisha kuhusu taqwa?

أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾

Je, unaonaje!  Kama amekadhibisha na akakengeuka?

أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ اللَّـهَ يَرَىٰ ﴿١٤﴾

Je, hajui kwamba hakika Allaah Anaona?

كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ ﴿١٥﴾

Laa hasha! Asipoacha, bila shaka Tutamburuta kwa nywele za paji la uso.

نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ ﴿١٦﴾

Paji la usio linalokadhibisha lenye hatia.

فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ ﴿١٧﴾

Basi na aite timu yake.

سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ ﴿١٨﴾

Nasi Tutawaita Az-Zabaaniyah Malaika wa adhabu.

كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَاسْجُدْ وَاقْتَرِب ۩﴿١٩﴾

Laa hasha! Usimtii; na sujudu na kurubia (kwa Allaah).  [Al-Alaq: 6-19]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

 

  عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ قَالَ أَبُو جَهْلٍ هَلْ يُعَفِّرُ مُحَمَّدٌ وَجْهَهُ بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ قَالَ فَقِيلَ نَعَمْ ‏.‏ فَقَالَ: وَاللاَّتِ وَالْعُزَّى لَئِنْ رَأَيْتُهُ يَفْعَلُ ذَلِكَ لأَطَأَنَّ عَلَى رَقَبَتِهِ أَوْ لأُعَفِّرَنَّ وَجْهَهُ فِي التُّرَابِ. قَالَ: فَأَتَى رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يُصَلِّي زَعَمَ لِيَطَأَ عَلَى رَقَبَتِهِ. قَالَ: فَمَا فَجِئَهُمْ مِنْهُ إِلاَّ وَهُوَ يَنْكِصُ عَلَى عَقِبَيْهِ وَيَتَّقِي بِيَدَيْهِ. قَالَ: فَقِيلَ لَهُ: مَا لَكَ؟  فَقَالَ: إِنَّ بَيْنِي وَبَيْنَهُ لَخَنْدَقًا مِنْ نَارٍ وَهَوْلاً وَأَجْنِحَةً ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: ((لَوْ دَنَا مِنِّي لاَخْتَطَفَتْهُ الْمَلاَئِكَةُ عُضْوًا عُضْوًا)) ‏.‏ قَالَ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ - (لاَ نَدْرِي فِي حَدِيثِ أَبِي هُرَيْرَةَ أَوْ شَىْءٌ بَلَغَهُ) ‏-‏ ((كَلاَّ إِنَّ الإِنْسَانَ لَيَطْغَى * أَنْ رَآهُ اسْتَغْنَى * إِنَّ إِلَى رَبِّكَ الرُّجْعَى * أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَى * عَبْدًا إِذَا صَلَّى * أَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ عَلَى الْهُدَى * أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَى * أَرَأَيْتَ إِنْ كَذَّبَ وَتَوَلَّى‏))‏   يَعْنِي أَبَا جَهْلٍ  ((أَلَمْ يَعْلَمْ بِأَنَّ اللَّهَ يَرَى * كَلاَّ لَئِنْ لَمْ يَنْتَهِ لَنَسْفَعًا بِالنَّاصِيَةِ * نَاصِيَةٍ كَاذِبَةٍ خَاطِئَةٍ * فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ * سَنَدْعُ الزَّبَانِيَةَ * كَلاَّ لاَ تُطِعْهُ‏))‏ زَادَ عُبَيْدُ اللَّهِ فِي حَدِيثِهِ قَالَ: وَأَمَرَهُ بِمَا أَمَرَهُ بِهِ ‏.‏ وَزَادَ ابْنُ عَبْدِ الأَعْلَى ((فَلْيَدْعُ نَادِيَهُ)) يَعْنِي قَوْمَهُ ‏.‏

Kutoka kwa Abuu Hurayrah amesema, siku moja Abuu Jahal aliuliza kama Muhammad ameutia vumbi uso wake mbele yenu?  Wakajibu: Ndio! Abuu Jahal akasema: Naapa kwa Al-Laatta na Al-‘Uzzaa nikimuona anafanya hivyo basi nitamkanyaga shingo lake au nitamsigina uso wake kwenye mchanga. (Abuu Hurayrah) Akasema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akafika akaswali na yule aliyeazimia kumsiga uso wake kwenye mchanga akawa ameanguka chini akiegemea mikono yake. Akaulizwa: Una nini Abuu Jahal? Akajibu: Baina yangu na Muhammad niliona khandaki la moto na kati yetu kuna Malaika mwenye mbawa. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akasema: “Lau angenisogelea basi Malaika yule angemkatakata na kumchania mbali viungo viungo. (Hatujui kama ni Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Hurayrah au yoyote iliyofikishwa kwake kutoka chanzo kingine) Akasema Allaah (عزّ وجلّ) Akateremsha:

 

كَلَّا إِنَّ الْإِنسَانَ لَيَطْغَىٰ ﴿٦﴾ أَن رَّآهُ اسْتَغْنَىٰ ﴿٧﴾ إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ الرُّجْعَىٰ ﴿٨﴾  أَرَأَيْتَ الَّذِي يَنْهَىٰ ﴿٩﴾  عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰ ﴿١٠﴾ أَرَأَيْتَ إِن كَانَ عَلَى الْهُدَىٰ ﴿١١﴾  أَوْ أَمَرَ بِالتَّقْوَىٰ ﴿١٢﴾ أَرَأَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ ﴿١٣﴾ 

Laa hasha! Hakika mwana Aadam bila shaka amepindukia mipaka kuasi. Kwa kuwa amejiona amejitosheleza. Hakika kwa Rabb wako ni marejeo. Je, umemuona yule anayekataza? Mja pale anaposwali? Je, umeona kama alikuwa katika Uongofu? Au ameamrisha kuhusu taqwa? Je, unaonaje!  Kama amekadhibisha na akakengeuka? [Al-‘Alaq: 6-13]

 

Yaani Abuu Jahal.

 

Na pia,...

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

 

Sababu Za Kuteremshwa

(Baadhi Ya Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Suwrah Al-Kawthar

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

108:Al-Kawthar:  

 

إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ ﴿١﴾

1. Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah).

 

فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ ﴿٢﴾

2. Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja kwa ajili Yake.

 

إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ ﴿٣﴾

3. Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila khayr).

 

عن عكرمة عن ابن عباس قال: قدم كعب بن الأشرف مكة فقالت له قريش: أنت سيدهم ألا ترى إلى هذا الصنبور المنبتر من قومه يزعم أنه خير منا ونحن أهل الحجيج وأهل السدانة وأهل السقاية، فقال: أنتم خير منه، قال: فنزلت ((إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الْأَبْتَرُ))

 

Kutoka kwa ‘Ikrimah kutoka kwa Ibn ‘Abbass amesema: Ka’b bin Ashraf alifika Makkah na Quraysh wakamwambia: “Wewe ni bwana wao je, huoni kuwa Swanbuwr hii iliyokatika kizazi chake kutoka kwa watu wake anadai kuwa yeye ni bora kuliko sisi na sisi ndio watu wenye kushughulikia mahujaji na watu wa As-Sadaanah na watu wa Siqaayah?” Akasema Ka’b: “Ninyi ni bora kuliko yeye”. Akasema: Ikateremka: “Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila khayr)” [Imepokewa na Al-Bazaar kwa Isnaad Swahiyh]

 

Hadityh hii imepokewa na Ibn Jurayj (3/330) kutoka katika njia ya Shaykh wake Muhammad bin Bashaar amehadithia Ibn Abi ‘Adiyy kutoka kwake. Na akazidisha ndani yake imeteremka juu yake: “Je, huoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wanakhiari upotofu na wanataka mpotee njia?...” [An-Nisaa 4: 44] mpaka kauli Yake: “Mwenye kunusuru”

 

Pia,

 

عَنْ أَنَسٍ، قَالَ: بَيْنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ذَاتَ يَوْمٍ بَيْنَ أَظْهُرِنَا إِذْ أَغْفَى إِغْفَاءَةً ثُمَّ رَفَعَ رَأْسَهُ مُتَبَسِّمًا فَقُلْنَا: مَا أَضْحَكَكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟  قَالَ: ((أُنْزِلَتْ عَلَىَّ آنِفًا سُورَةٌ ))‏. فَقَرَأَ: (( بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)).‏ ثُمَّ قَالَ: ((أَتَدْرُونَ مَا الْكَوْثَرُ؟)). فَقُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ.‏ قَالَ: ((فَإِنَّهُ نَهْرٌ وَعَدَنِيهِ رَبِّي عَزَّ وَجَلَّ عَلَيْهِ خَيْرٌ كَثِيرٌ هُوَ حَوْضٌ تَرِدُ عَلَيْهِ أُمَّتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ آنِيَتُهُ عَدَدُ النُّجُومِ فَيُخْتَلَجُ الْعَبْدُ مِنْهُمْ فَأَقُولُ رَبِّ إِنَّهُ مِنْ أُمَّتِي‏.‏ فَيَقُولُ مَا تَدْرِي مَا أَحْدَثَتْ بَعْدَكَ))‏.‏ زَادَ ابْنُ حُجْرٍ فِي حَدِيثِهِ بَيْنَ أَظْهُرِنَا فِي الْمَسْجِدِ‏.‏ وَقَالَ:‏ ((مَا أَحْدَثَ بَعْدَكَ))‏.

 

Amesimulia Anas (رضي الله عنه): Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pamoja nasi akawa amepitiwa na lepe la usingizi kisha akanyanyua kichwa chake juu huku akitabasamu, tukasema: Ni kitu gani kimekufurahisha ee Rasuli wa Allaah? Akasema: “Imeniteremkia sasa hivi Suwrah: (Akaisoma Suwrah Al-Kawthar).

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ *

Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) Al-Kawthar (Mto katika Jannah). Basi swali kwa ajili ya Rabb wako na chinja.  Hakika mbaya wako, yeye ndiye atakayekatiliwa mbali (kizazi na kila kheri).”  [Al-Kawthar: (108)]  

 

Kisha akasema: “Je, mnajua ni nini Al-Kawthar?” Tukajibu: Allaah na Rasuli Wake Ndio Wajuao zaidi. Akasema: “Huo ni mto ambao Allaah (عزّ وجلّ) Ameniahidi. Una kheri nyingi sana, nao una hodhi lake ambalo Ummah wangu watakusudia kulifikia Siku ya Qiyaamah. Vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Mja miongoni mwao atatolewa mbali atengwe. Nitasema: Ee Rabb! Hakika yeye ni katika Ummah wangu!  Allaah Atasema: Hujui nini alizusha baada yako!”

 

Ibn Hujri amezidisha katika Hadiyth yake: Alikuwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amekaa kitako pamoja nasi Msikitini. Na (Allaah) Atasema: “Hujui walichokizusha baada yako!” [Muslim – Kitaab Asw-Swalaah - Mlango wa hoja anayesema kuwa Al-Basmalah ni Aayah katika kila mwanzo wa Suwrah isipokuwa Suwrah Al-Baraa (At-Tawbah)] 

 

 

 

 

Pia,

 

بينما ذاتَ يومٍ بينَ أظهرِنا يريدُ النَّبيَّ صلَّى اللَّهُ عليهِ وسلَّمَ إذ أغفى إغفاءةً ثمَّ رفعَ رأسهُ متبسِّمًا فقلنا لهُ: ما أضحكَكَ يا رسولَ اللَّهِ؟  قالَ: نزلت عليَّ آنفًا سورةٌ: ((بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ)) ثمَّ قالَ: ((هل تدرونَ ما الكوثرُ؟)) قلنا اللَّهُ ورسولُهُ أعلم قالَ: ((فإنَّهُ نهرٌ وعدنيهِ ربِّي في الجنَّةِ آنيتُهُ أكثرُ من عددِ الكواكبِ ترِدُهُ عليَّ أمَّتي فيختلِجُ العبدُ منهم فأقولُ يا ربِّ إنَّهُ من أمَّتي فيقولُ لي إنَّكَ لا تدري ما أحدثَ بعدَكَظ)).

Siku moja tulikuwa pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  na akapitiwa na usingizi mara akanyanyua kichwa chake huku akitabasamu. Tukamuuliza ni nini kinachokuchekesha ee Rasuli wa Allaah?” Akajibu: “Hivi imeniteremkia: 

 

((بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ * إِنَّا أَعْطَيْنَاكَ الْكَوْثَرَ * فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ * إِنَّ شَانِئَكَ هُوَ الأَبْتَرُ))

 

[Al-Kawthar: 108].

 

Kisha akauliza, Je, mnajua nini Al-Kawthar? Tukasema Allaah na Rasuli Wake ndio wanaojua.” Akasema: “Ni mto wa wa Jannah ambao Allaah Ameniahidi, na vyombo vyake (au bilauri) ni idadi ya nyota. Na  Ummah wangu watanifikia (katika hodhi) lakini  mtu atotelewa hapo na kutengwa, kisha nitasema, Ee Rabb wangu huyo ni katika Ummah wangu! Na hapo Ataniambi: Hakika wewe hujui alichokizua baada yako.” [Mpokeaji ni Anas bin Maalik, katika Swahiyh An-Nasaaiy cha Imaam Al-Albaaniy (uk. 903) hitimisho la hukumu ya mwenye kuzua. Angalia Swahiyh sharh ya Hadiyth namba (21618)]

 

Pia,

 

Amepokea Muslim, Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy kutoka kwa Anas [Muslim: (1/300), Abuu Daawuwd: (5/110) na An-Nasaaiy katika Al-Kubraa (6/533) na tamko ni la Muslim amesema: “Wakati Rasuli wa Allaah yuko mbele yetu Msikitini, ghafla alisinzia usinziaji wa mara moja kisha akanyanyua kichwa chake hali ya kuwa anatabasamu tukasema: Ni jambo gani ambalo linakuchekesha ee Rasuli wa Allaah?” Akasema: “Kwa hakika imeteremshwa kwangu punde Suwrah….” (akasoma Suwrah ya Al-Kawthar).

 

 

Asbaabun-Nuzuwl

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

012-Suwrah Yuwsuf Aayah 1-3

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿٢﴾

Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan kwa (lugha ya) Kiarabu ili muifahamu.

 

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua. [Yuwsuf: 1-3]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

 عن مصعب بن سعد عن أبيه سعد بن أبي وقاص في قول الله عز وجل: ((نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ)) الآية. قال: أنزل الله القرآن على رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم فتلاه عليهم زمانا، فقالوا: يا رسول الله لو قصصت علينا فأنزل الله ((الر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ)) إلى قوله ((نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ)) الآية. فتلاها رسول الله صلى الله عليه وعلى آله وسلم زمانا، فقالوا: يا رسول الله لو حدثتنا فأنزل الله تعالى ((اللَّهُ نَزَّلَ أَحْسَنَ الْحَدِيثِ كِتَابًا مُتَشَابِهًا))  أخرجه ابن حبان في صحيحه  والحاكم  وقال صحيح الإسناد  

 

Kutoka kwa Musw-‘ab  kutoka kwa baba yake Sa’ad bin Abiy Waqqaasw kuhusu kauli ya Allaah (عز وجل):

نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ وَإِن كُنتَ مِن قَبْلِهِ لَمِنَ الْغَافِلِينَ ﴿٣﴾

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. Na japokuwa kabla yake ulikuwa miongoni mwa wasiojua

Kwamba Qur-aan imeteremshwa kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akawasomea kwa kipindi kirefu. Kisha watu (wakatamani ziyada) wakasema: Ee Rasuli wa Allaah, ungelitusimulia: Allaah (سبحانه وتعالى) Akateremsha:

الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ ﴿١﴾

Alif Laam Raa. Hizo ni Aayaat za Kitabu kinachobainisha.

 

mpaka Kauli Yake:

 

Endelea ....